Matendo 13:21 “ Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini. 22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, MTU ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU, ATAKAYEFANYA MAPENZI YANGU YOTE”.
Matendo 13:21 “ Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini.
22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, MTU ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU, ATAKAYEFANYA MAPENZI YANGU YOTE”.
Japo Daudi hakuwa mkamilifu kwa viwango kama vya watumishi wengine wa Mungu waliomtangulia au waliomfuata mfano wa Musa, Samweli, Eliya au Danieli, lakini biblia inamshuhudia kuwa ni mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu.(Daudi Aliupendeza moyo wa Mungu sana)..
Je! Alimpendezaje Mungu?
Embu tuangalie mambo baadhi yaliyomfanya Daudi awe vile, naamini yanaweza kutusaidia na sisi katika safari yetu ya kutafuta kumpendeza Mungu.
Jambo la kwanza: ni,Daudi alimwamini Mungu kwa moyo wake wote: Hakujali ukubwa wa tatizo lilolokuwa mbele yake, kwa jinsi tatizo lilivyoonekana kuwa kubwa ndivyo alivyomfanya Mungu wake kuwa mkubwa Zaidi ya hilo tatizo na hiyo ilimfanya asiogope chochote..
Zaburi 27:1 ‘Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?’ Wakati alipokuwa anapambana na Goliathi hakuogopa ukubwa wake na vitisho vyake ijapokuwa alikuwa hana silaha yoyote mkononi mwake lakini Daudi hakuogopa badala yake alimwambia maneno haya 1Samweli 17: 45 “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. 46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. 47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
Zaburi 27:1 ‘Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?’
Wakati alipokuwa anapambana na Goliathi hakuogopa ukubwa wake na vitisho vyake ijapokuwa alikuwa hana silaha yoyote mkononi mwake lakini Daudi hakuogopa badala yake alimwambia maneno haya
1Samweli 17: 45 “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
Nasi tujiulize, majaribu makubwa yanaposimama mbele yetu je ndio tunamkimbia Mungu au ndio tunamwamini Mungu, na kumuacha ili aonyeshe yeye uweza wake?. Kumbuka Daudi hakufanya hivyo sio tu kwa Goliathi bali katika matatizo mengi yote aliyowahi kukumbana nayo alisema pia nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti sitaogopa mabaya kwa maana Bwana yupo pamoja nami, Gongo lake na limbo yake vyanifariji.(Zaburi 23).
Zaburi 119:47 ‘Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda. 48 Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako’. Soma tena.. Zaburi 119:140 ‘Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda”.
Zaburi 119:47 ‘Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda.
48 Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako’.
Soma tena..
Zaburi 119:140 ‘Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda”.
Ukisoma sehemu nyingi katika Zaburi utaona Daudi akionyesha Upendo wake katika Neno la Mungu, na hiyo ilimfanya awe analitafakari sana, sio kulisoma tu kama gazeti hapana, bali alikuwa analitafakari sana mchana na usiku..
Na sisi je! Tunao moyo kama huo wa kulipenda Neno la Mungu, tunapoambiwa uzinzi ni dhambi, tunafurahia kusikia hivyo?, tunapoambiwa vimini ni dhambi tunafurahia kusikia hivyo?, tunapoambiwa usengenyaji ni dhambi Je tunazingatia kujirekebisha je, tunapoambiwa ulevi na uvutaji wa sigara ni dhambi tunasikiliza? tunalitafakari hilo usiku na mchanga..Kama ndio hivyo basi tujue kuwa tupo katika njia ya kuelekea kumpendeza Mungu..Daudi anasema hivi:
Zaburi ZABURI 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, NA SHERIA YAKE HUITAFAKARI MCHANA NA USIKU 3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”.
Zaburi ZABURI 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, NA SHERIA YAKE HUITAFAKARI MCHANA NA USIKU
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”.
Zaburi 119:140 ‘Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda’
Tatu: Daudi alikuwa ni mtu aliyekubali na kuyakiri makosa yake haraka sana, na kutubu. Alipozini na mke wa Uria, baada ya kuletewa habari hizo na nabii Nathani ukisoma 2 Samweli 12: 13 utaona hilo, saa ile ile Daudi alikiri kuwa kweli ametenda dhambi…Lakini sisi ni mara ngapi tunamficha Mungu dhambi zetu, hata kama uthibitisho wote unaonekana, tutajaribu kutengeneza mazingira na kusema ni kwasababu ya hiki au kile ndio maana nimetenda hivi au vile kama tu vile walivyofanya Adam na Hawa pale bustanini..
Ukisoma Zaburi 51, utaona jinsi Daudi alivyoungama dhambi zake zote..Vivyo hivyo na sisi Mungu atusaidie tuwe na moyo huo huo, wa kukiri makosa yetu na hivyo kutubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha.
Nne: Daudi alikuwa ni mtu wa kuustaajibu uweza wa Mungu, na hivyo hakuona aibu kuutangaza uweza huo kwa kila mtu:
Zaburi 119: 46 ‘Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu’.
Daudi alikuwa yupo radhi kumtukuza Mungu hadi nguo zinamtoka bila kujali yeye ni mfalme, (Daudi alicheza mpaka nguo zikaanguka)alimtukuza Mungu dunia nzima ilijua kuwa yeye kweli ni mtumishi wa Yehova. Ukisoma Zaburi sehemu kubwa utaona Daudi anavyoibiri kazi ya Mungu na uweza wake na utukufu wake duniani kote..
Mtume Paulo aliandika katika Warumi 1:16 ‘Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia’.
Hivyo na sisi Tunapaswa kuitangaza injili kwa nguvu zetu zote Mungu alizotupa, ili na sisi tumpendeze Mungu.
Bwana atusaidie sote katika hayo. Naamini tutachukua hatua nyingine katika kuyarekebisha hayo machache, Mungu akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine.
Mada Nyinginezo:
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.
Rudi Nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
1Wakorintho 13:8 “Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”…Nini maana ya ukiwapo unabii utabatilika?
JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu karama iliyo kuu kuliko zote ni upendo..(1Wakorintho 12:31)..Hii Ndio karama yenye nguvu kuliko karama nyingine zote (hakuna kitu chenye nguvu kuliko upendo)…Na karama hii ni tofauti na zile karama 9 ambazo mtu anakuwa na kipawa cha kipekee kutoka kwa Mungu, ambacho kinamtofautisha yeye na wengine katika kanisa…Karama ya Upendo ni karama ambayo Mungu anampa kila mtu pindi tu anapojiweka tayari kutaka kuwa na huo upendo.
Upendo unapokuwepo mahali hata unabii unakuwa hauna nguvu..Kwamfano Adamu na Hawa walipoasi tayari walikuwa wameshajitenga na uwepo wa Mungu milele, wao (pamoja na sisi wote maana wote tumetoka kwa Adamu)..kitendo tu cha kula lile tunda, basi mwanadamu alitoka katika nafasi ya kuwa mwana wa Mungu (kuishi milele) na kubakia kuwa tu kiumbe cha Mwenyezi Mungu tu!…. Muunganiko wa Mungu na mwanadamu ulikatikia pale Edeni kutokana na Adamu na Hawa kula lile tunda.
Lakini kutokana na Upendo Mungu aliotupendea alighairi mpango huo wa kumtenga mwanadamu milele na kumrudishia tena uzima wa Milele..
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.
Upendo umeutangua ule unabii wa sisi kutengwa na Mungu milele, ndio maana biblia inasema hapo juu “ukiwapo unabii utabatilika”..Upendo umebadilisha mawazo ya Mungu juu yetu moja moja…Tulikuwa tumetabiriwa kupotea milele, sasa kinyume chake kwasababu ya Upendo wake kwetu tumepokea Uzima wa Milele kupitia Yesu Kristo mwanawe.
Ndio maana Biblia inazidi kutuambia hata mambo yajayo (yaani Unabii) hayawezi kututenga sisi na upendo wa Mungu ulio katika Kristo, hata malaika, hata mbingu haziwezi kututenga sisi na Upendo wa Kristo kwetu..Tumependwa tumependwa! Hakuna kinachoweza kubadilisha hilo..
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. 35 NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?………. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?………. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Hivyo ni muhimu kulipata hili pendo la Kristo, ambalo linaweza kutangua hata unabii, upendo huo tukiupata tunaweza na sisi tukawapenda ndugu zetu hata kama wametufanyia mabaya kiasi gani, hata kama tulikuwa tumewatabiria kuwalipiza kisasi, upendo huo unayafuta hayo na kuwapenda ndugu pasipo masharti.
Vilevile unabii pia unatabia ya kuisha muda wake pale unapotimia, unao ukomo wake, lakini Upendo unaotoka kwa Mungu hauna mwisho, na sio Unabii tu peke yake wenye ukomo bali hata lugha, na maarifa yoyote ya kimbinguni au ya kiduniani vina ukomo haviwezi kuushinda upendo. Upendo una nguvu kuliko kitu kingine chote..Ndio maana amri iliyo kuu na kubwa kuliko zote ni UPENDO!
1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. 9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; 10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”.
1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”.
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?
SAYUNI ni nini?
Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
Rudi Nyumbani:
Kuna aina tatu za Imani zilizoonekana katikati ya kundi lililokuwa likumfuata Yesu waponywe.
Kundi la Kwanza: Ni lile lililohakikisha kuwa linamwona Yesu uso kwa uso, na kuzungumza naye, na kumwomba Bwana Yesu awaponye au kama mgonjwa wao hayupo hapo basi litahakikisha Bwana Yesu anaambata nao hadi makwao ili waombewe, Kundi hili linatabia ya kumwachia Yesu afanye shughuli zote.
Kundi hili ndio lililokuwa kubwa kushinda yote, na hata leo lipo na ni kubwa pia, hawa ndio wale watu ambao ni ili waponywe au wafanyiwe haja zao ni lazima wawatafute watumishi wa Mungu mahali popote walipo kwa gharama zozote zile, wapo radhi kwenda mpaka Nigeria, china bila kujali gharama za fedha wanazoingia ilimradi tu waonane na watumishi wa Mungu wawaombee.
Ni lile ambalo, lilipata ufunuo wa Zaidi wa kutambua uweza wa Yesu, Hivyo halikuhitaji mpaka Yesu afike nyumbani kwao ndipo waponywe. Mfano wa hili ni yule Akida aliyemfuata Yesu..
Tusome..
Mathayo 8:5 “Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, 6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. 7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. 8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. 10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli”.
Mathayo 8:5 “Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli”.
Unaona mtu huyu alitafakari kwa ukaribu sana akaangalia na kazi yake anayoifanya kila siku ya Uakida akasema moyoni mwake kama mimi nikitoa tu amri kwamba kitu fulani kifanyike , huwa kinatendeka haraka sana hata kama mimi sipo huko..Sasa si Zaidi huyu ambaye ni Masihi mwenyewe, mkuu wa ufalme wa mbinguni, anao uwezo pia wa kunitamkia tu uponyaji mahali nilipo na malaika zake wakalishughulika na hilo mara moja na mambo yote yakawa sawa..
Hivyo kwa ufunuo huo huo akamwambia Bwana huna haja ya wewe kuja nyumbani kwangu, ya nini kujichosha, wakati unalo jeshi la malaika chini yako?..SEMA NENO TU! Na mtumishi wangu atakuwa mzima..
Bwana alistaajabia sana, kwasababu kundi la watu wenye hiyo haikuiona kabisa, anasema hata katika Israeli nzima, ikiashiria kuwa watu wenye Imani ya namna hiyo iliyojaa ufunuo wa kumchukulia Yesu kama ni Zaidi ya wanavyomfikiria walikuwa nao wachache.
Watu wa namna hii pia leo wapo isipokuwa ni wachache sana, watu wenye Imani na YESU aliye ndani ya mioyo yao, watu ambao hawategemei watumishi wa Mungu kuwaombea, watu ambao hawahangaiki huku na kule kutafuta maombezi, Ni kwasababu wamepata ufunuo wa uweza wa nguvu za YESU, Mungu anapendezwa nao sana, hawa wakiwa na haja wanapiga magoti wenyewe wanamwomba YESU aliye ndani yao..Na mwisho wa siku wanapokea miujiza yao..Na kundi hili huwa ni rahisi Zaidi kupokea kuliko lile la kwanza.
Ni kundi ambalo halikuhitaji ruhusu yoyote ya YESU ili kupokea kitu kutoka kwake ..Halikuhitaji kumwita Yesu aje manyumbani kwao, wala halikuhitaji YESU awatamkie Neno lolote wala halikumuhitaji Yesu afahamu jambo lolote,..Lilifanya kimya kimya lakini matokeo yake yalikuwa ni makubwa na ya papo kwa papo..Mfano wa kundi hili tunaona ni yule mwanamke aliyetokwa na damu miaka 12, tusome:
Luka 8:43 “Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. 45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. 46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka. 47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara. 48 Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani”.
Luka 8:43 “Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.
46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.
47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.
48 Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani”.
Hapa ndipo Bwana Yesu anapotaka kila mmoja wetu afikie, mahali ambapo Yesu anakutafuta wewe, na sio wewe unamtafuta Yesu..kwamba tuwe na mamlaka kamili ya kuweza kutumia nguvu zake bila kipimo chochote. Na hatua hii ikikomaa vizuri ndani ya mtu ndio ile inakuja kuitwa IMANI TIMILIFU, (Wakorintho 13:2) ambayo mtu akiwa nayo anakuwa na uwezo wa kikiambia kitu hichi kwa jina la YESU ondoka nenda kule, nacho kikatii, Anao uwezo wa kuamrisha milima na kufanya jambo lolote kwa jinsi atakavyo yeye, hapo si kwamba anaomba kwa Mungu hapana, bali anafanya kwa amri yake mwenyewe kwa jina la Yesu nacho kinatokea..
Na njia pekee ya kufikia huko ni kuwa na maarifa ya kutosha, ya YESU KRISTO, tunahitaji kumjua sana Yesu KRISTO kwa mapana na marefu, kiasi kwamba ile Imani ya kufanya chochote kwa jina lake ijengeke yenyewe ndani yetu.
Bwana atujalie tufike huko, katika tumtafakari sana Bwana YESU, Mfalme wa Wafalme, kama ipasavyo ambaye biblia inatuambia “ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika”(Wakolosai 2:3).
Bwana akubariki sana, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Nifanyaje ili nijue kuwa uamuzi ninaokwenda kuchagua kufanya ni mapenzi ya Mungu?
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
JINA LA MUNGU NI LIPI?
Mpagani ni nani?
Jina la Mfalme Mkuu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze maneno yake ambayo ni mwanga wa njia zetu, na taa iongozayo miguu yetu (Zab. 119:105)
Leo tutajifunza kwa ufupi, umuhimu wa kutubu dhambi kabla ya kumaliza haya maisha, yapo mafundisho mengi yanayohubiri kuwepo kwa nafasi ya pili ya kusamehewa moto wa milele baada ya kufa…Miongoni mwa mafundisho hayo ni mafundisho ya kupitia Toharani. Lengo kuu la mafundisho haya ni kuwapa watu wanaoishi katika dhambi matumaini kwamba hata wakifa katika dhambi zao bado watakuwa na nafasi ya kutolewa kwenye mateso hayo ya milele na kuingia paradiso, na maombi ya watakatifu waliopo duniani yanaweza kupunguza mateso ya kule.
Haya ni moja ya mafundisho ya shetani yaliyobuniwa kuzimu kwa ujuzi wa hali ya juu yanayowapa watu matumaini na faraja za uongo…shetani anajua watu wanapenda faraja….Alijua Hawa anapenda faraja ndio maana uongo wa kwanza alioutumia ni uongo wa faraja…alimwambia Hawa kwamba “hakika hamtakufa” wakati Bwana alishawaambia wakila tu “watakufa”
Hivyo shetani ni Yule Yule aliyoyatumia Edeni kuwaangusha watu wa kwanza kuumbwa (Adamu na Hawa) ndio hayo hayo anayoyatumia kuwaangusha watu siku za mwisho (yaani mimi na wewe) hivyo tusipokuwa makini kidogo tu! Ni rahisi kwenda na maji!
Mahubiri ya Toharani yatawafanya watu wengi sana wajute siku ile, watakapokwenda huko na kugundua kuwa hakuna kitu kama hicho cha kupata nafasi ya pili. Walidanganywa!
Hebu chukua muda kutafakari kwa Makini sana mstari ufuatao ambao Bwana Yesu aliusema kisha useme mwenyewe kama kweli kutakuwa na nafasi ya pili..
Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.
Itafakari hiyo sentensi kwa makini, usiisome tu juu juu kwa mazoea, kwamba ulishawahi kuusoma huo mstari na hivyo huwezi kuurudia tena, hebu ingia ndani zaidi kuutafakari!…Bwana Yesu anasema msiposadiki kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu…Ikiwa na maana kuwa kuna tatizo “katika kufa ukiwa na dhambi”…Hiyo ndiyo maana yake!…Na madhara hayo ni baada ya kifo! Kwamba mtu akifa mifupa itakwenda kuchimbiwa kaburini, nguo zitachimbiwa, ardhini nyama ya mwili wake itachimbiwa na kuoza lakini dhambi zake alizonazo atavuka nazo upande wa pili…Na hivyo hiyo dhambi inapaswa ichujwe kabla ya kifo, iachwe hapa hapa duniani..kwasababu ukivuka nayo kule hakuna nafasi tena ya kuitua.
Ingekuwa hakuna tatizo katika kufa ukiwa na dhambi na kwamba kuna nafasi nyingine ya kuokoka ukiwa kule…Bwana Yesu asingesema hivyo…jiulize sana kwanini ahusishe “kifo” na “dhambi” maana yake ukishakufa na dhambi ndio basi tena…ndio maana alikuwa anakazana kuwaambia watubu kabla ya kufa! Kwasababu hakuna tena toba, wala injili baada ya kifo..kinachofuata baada ya hapo ni hukumu..
Ndugu Kama ulikuwa unaamini hivyo kwamba kuna nafasi ya pili ya kuokoka baada ya kifo, ambayo mafundisho haya yanafundishwa sana katika kanisa Katoliki au pengine ulisikia kwa mchungaji wako au kiongozi wako wa dini..fahamu kuwa ulidanganywa! Kama tu Hawa alivyodanganywa kwamba hatakufa!…Umesoma mwenyewe maneno ya Bwana Yesu hapo juu, jinsi alivyokuwa anakazana kuwafanya watu wamwamini kabla ya kufa… na wewe kama hutatubu leo na kumwamini Bwana Yesu utakufa katika dhambi zako..Na baada ya kifo ni hukumu!, kama ni mlevi, mwasherati, mtukanaji, mfanyaji masturbation, mtazamaji wa picha za uchafu, mlawiti, msagaji, msengenyaji, mtoaji mimba, mvaaji mavazi ya kikahaba n.k ukifa leo bila kutubu…utakwenda jehanamu! Hakuna nafasi ya pili…
Bwana anatuonya hapo juu! Kwamba tusipomwamini tutakufa katika dhambi zetu! Je! Na wewe unataka kufa katika dhambi zako? Kama sio basi ni vema ukakata shauri leo la kumgeukia Bwana Yesu, akusafishe dhambi zako na akuoshe kabisa…unachotakiwa kufanya ni kutii msukumo uliopo ndani yako unaokusukuma kuacha dhambi na kumgeukia mwokozi, ujumbe huu unaweza ukawa ni wa kwako kukubadilisha ..
Hivyo unautii huo wito kwa kuamua kwa dhati kwamba kuanzia leo mimi na dhambi basiii, disko ndio mwisho leo, kuchat chat ovyo katika mitandao kwenye vitu visivyo na maana ndio mwisho, kutukana ndio mwisho, kusikiliza miziki ya kidunia ndio mwisho, na unaifuta yote sasahivi bila kuacha wimbo hata mmoja, na unakata kila mnyororo, unasema mimi na uasherati basi, na wale wanawake au wanaume unaotembea nao sasa inatosha, unawapigia simu na kuwaeleza maamuzi yako, na unawaacha kabisa…na unachukua msalaba wako unamfuata Yesu wewe kama wewe..
Baada ya hapo ile nguvu ya Roho itakuvaa itakayokuwezesha kutokutamani hayo mambo tena…utakuwa hujilazimishi kujizua kutukana, au kuiba, au kuzini, n.k itakuwa ni kitu kinachotoka ndani chenyewe (kama vile usivyotumia nguvu yoyote kusukuma damu kwenye moyo wako)…na utaona amani Fulani ya ajabu imekuingia Ukiona hali kama hiyo imekuja ndani yako fahamu kuwa ni Roho Mtakatifu huyo..Lakini ukikaidi sauti yake na kuendelea na ulimwengu huu wa kitambo utakufa katika dhambi zako na hakutakuwa na nafasi ya pili tena huko uendako. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Bwana akubariki sana, Tafadhali share na wengine
Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
YONA: Mlango wa 3
WhatsApp
SWALI: BWANA YESU ASIFIWE SANA ndugu zangu..naswali naomba kujua BWANA alikuwa anamaana gani kusema haya maneno…Mathayo 5:13 ‘Ninyi ni chumvi ya dunia;lakini chumvi IKIWA IMEHARIBIKA ITATIWA NINI HATA IKOLEE?….’
JIBU: Bwana Yesu alitumia mfano wa chumvi kuonyesha jinsi watakatifu wanavyopaswa wawe waangalifu hapa duniani..Chumvi ni kama sukari, hata siku moja hujawahi kuweka sukari kwenye chai na ukakutana na kipande cha jiwe ndani yake, tofauti na vitu vingine kama vile mchele, au maharage ambavyo utakutana navyo sana, vivyo hivyo na chumvi nayo inapotengezwa, huwa inatengenezwa kwa umakini wa hali ya juu sana, kuhakikisha kuwa hakuna uchafu wowote unajipenyeza ndani ya chumvi ile..
Kwasababu wanafahamu chumvi ni tofauti na nafaka, ikiingia uchafu kidogo tu, basi haifai tena ni ya kutupa, ni kitu ambacho kisichoweza kuchambulika kama vile mchele, huwezi ukatoa punje moja moja ya chumvi uitenganishe na uchafu, hiyo haiwezekani, ikiingia uchafu kidogo tu, basi hiyo haifai tena, hata kamaa ukijaribu kuiweka katika mboga haiwezi kukolea kwa namna yoyote ile.
Vivyo hivyo na sisi tuliookoka, Bwana anasema ni chumvi, hatupaswi kutiwa unajisi na kitu chochote kichafu, kwasababu ulimwengu unatuangalia sisi kama viungo vya kipekee sana, na ndio maana hata leo ukisikia watu wawili wamefumaniwa katika uzinzi na mmojawapo ni mchungaji, utaona watu wote wanaacha kumfuatilia yule mwingine, na kuanza kufuatilia habari za yule mchungaji,..
ni kwasababu yeye alikuwa ni chumvi, lakini sasa ameshatiwa doa, unadhani mtu kama huyo hata kama akitubu kwa dhati kabisa, na Mungu kweli akamsamehe, Unadhani ile jamii inayomzunguza bado itamwelewa?, haiwezekani tena, utumishi wake ndio tayari umeshaharibika hivyo..
Na ndio maana Bwana anasema “chumvi ikiwa imeharibikaitatiwa nini hata ikolee?”, Wewe unasema umeokoka halafu bado unaonekana unatukana ovyo, utumishi wako utaaminikaje mbele za watu?, Unakwenda Disco, au muda wote wewe ni kusengenya watu, unadhani wale watu wanaokuzunguka watakuaminije hata kama utawapelekea habari za Mungu..
Waefeso 5:25 “……….kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”.
Waefeso 5:25 “……….kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”.
Hivyo hapo Bwana alikuwa anatuonya tuwe waangalifu, sisi ni chumvi, tuliotakaswa siku ile tulipookoka tusio na hila wala waa wala, kunyanzi lolote, na sio mchele ambao hata ukiingia uchafu unaweza kuchambulika.
Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/je-ni-vema-kwa-mkristo-kwenda-hospitali-au-kutumia-miti-shamba-anapougua/
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
Sasa hivi kuna madhehebu mengi duniani, na yanazidi kuongezeka kwa kasi. Madhehebu karibia yote yana Maaskofu na wachungaji…Na pia yana maaskofu wakuu…Ndio utasikia mahali fulani Askofu Mkuu wa kkkt anatajwa, askofu mkuu wa roman katoliki, askofu Mkuu wa fpct, Askofu Mkuu wa eagt, Askofu Mkuu wa Anglikana, Nabii Mkuu wa huduma fulani, Mwalimu Mkuu n.k
Vyeo hivi kwa Hekima ya kibinadamu havina tatizo lolote..kwasababu hata katika ngazi za uongozi wa nchi kunakuwa na Mkuu wa Nchi, na kisha wapo walio chini yake n.k Ili kuwepo na uongozi unaosimama na ulio katika utaratibu Mzuri ni lazima ngazi ziwepo, mmoja awe juu ya mwingine kiukuu.
Lakini tukirudi katika Hekima ya KiMungu, Jinsi uongozi wa KiMungu unavyojiongoza ni tofauti na wa kiulimwengu…Huwa inatumika Hekima nyingine tofauti kabisa na hekima ya ulimwengu huu.
Uongozi wa kiMungu hautumii ngazi za ukuu, kwamba mmoja anakuwa mkuu kwa mwingine bali unatumia kitu kinachoitwa KARAMA ZA ROHONI. Kumbuka ni za rohoni na si za mwilini…. Na karama hizi za rohoni hazina mtu aliye Mkuu kuliko mwingine au aliye Mkuu wa Mwingine. Ni kwanini? kwasababu vyote vina umuhimu sawa na vyote ni vikuu katika mwili wa Kristo.
Mtume Paulo alizilinganisha karama za rohoni na viungo vya Mwili, na kwa uwezo wa Roho akaonyesha kuwa viungo vyote ni vya muhimu na hakuna kilicho kikuu zaidi ya kingine kwasababu vyote vimeshikamana …Kiungo kilicho kikuu zaidi ya vingine vyote ni Kichwa tu! ambacho hicho Biblia ndio imesema ni KRISTO, lakini vilivyosalia vyote hakuna kilicho kikuu zaidi ya kingine.
Ni kwasababu ndio kiungo pekee kinachoongoza viungo vyote vya mwili, taarifa za kunyanyua mkono zinatoka kwenye kichwa (yaani ubongo), taarifa za kusogeza mguu zinatoka kwenye kichwa na sio kwenye mikono…Hivyo mkono hauwezi kuwa mkuu juu ya mguu…n.k
Kumbuka Laiti vipawa hivi visingekuwa ni vipawa vya rohoni, na kuwa vipawa vya mwilini, basi ingekuwa ni sawa kuwepo na Askofu Mkuu, au Mchungaji Mkuu au Nabii Mkuu, au Mwalimu Mkuu au kiongozi mkuu…lakini kwasababu sio vya mwilini hivyo sio sawa kuvigawanya na kusema kimoja ni kikuu kwa vingine mkono hauwezi ukauamrisha mguu utembee.. Kwahiyo Askofu anayejiita ni Mkuu kwa askofu mwenzake, anafanya jambo lililokinyume na maandiko….Huko ni kujikuza na kuchukua nafasi ya Kristo.
1Wakorintho 12:11 ‘lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. 12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo’…. 14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. 15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? 16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo? 17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? 18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. 19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. 22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;
1Wakorintho 12:11 ‘lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo’….
14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.
15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?
16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?
17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?
18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.
19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.
21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.
22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.
23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.
24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;
Hebu leo hii, mtu ambaye anajiita Askofu Mkuu, mwingine akosee tu kidogo na kumwita Askofu bila kuongezea hapo mbele neno ‘Mkuu’ uone atakavyowaka au kukasikira…Sasa hasira hizo za nini? kama kweli huyo hana nia ya kutafuta ukubwa?.
Ni Yesu Kristo peke yake, Nabii Mkuu ni Yesu Kristo peke yake, Mwalimu Mkuu ni Yesu Kristo peke yake, sisi tukijiita walimu, au wachungaji au maaskofu au manabii inatosha! zaidi ya hapo ni kinyume na maandiko!
Waebrania 13:20 “Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu”
Ubarikiwe.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
DANIELI: Mlango wa 1
DANIELI: Mlango wa 10
UMEPATANISHWA NA MAADUI ZAKO?
YUDA ISKARIOTE! MTUME ALIYECHAGULIWA NA BWANA YESU.
SWALI: Ukisoma Mathayo 12:32 “utaona anae mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa sasa na hata ule ulimwengu ujao.
Sasa sio ndio kusema, kama nimekufa nikiwa na baadhi ya makosa nitasamehewa ule ulimwengu ujao? Naomba kueleweshwa zaidi”.
JIBU: Mtu anaweza asisamehewe hapa duniani lakini kule aendako akasamehewa…kwamfano yule mnyanganyi aliyesulubiwa na Bwana Yesu pale msalabani, hakusamehewa adhabu ya kifo pale msalabani pengine alimwomba Mungu kimoyo moyo asife pale msalabani, lakini haikusaidia kufa alikufa……
lakini baada ya kufa alisamehewa adhabu ya moto wa milele..ingawa hakusamehewa adhabu ya kuchapwa na mijeledi na kusulubishwa…..lakini Bwana alimwambia atakuwa pamoja naye peponi siku ile kwasababu alitubu…
Mfano mwingine ni wafungwa, wapo wafungwa waliofungwa kutokana na makosa waliyoyafanya kihalali kabisa ambao wametubu na kulia Mungu awafungue kwenye vifungo hivyo…
Lakini Mungu hajawafungua kwenye vifungo vyao mpaka wanakufa..hao hawajasamehewa adhabu hapa duniani lakini wakifa watakwenda paradiso kwasababu walitubu.(Kundi lote hilo ndio kundi la watu ambao hawajasamehewa hapa lakini kule watasamehewa).
Vilevile ikiwa mtu alishaokoka halafu akaenda kufanya dhambi za makusudi, kwamfano ya uzinzi, baadaye akatubu, biblia inasema mtu kama huyo ni ngumu sana kusamehewa hapa, ni rahisi kukutana na adhabu ya mauti hata kama huko aendako atasamehewa. Hivyo ni kukaa mbali na dhambi..
1Wakorintho 5:1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. 3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. 4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.
1Wakorintho 5:1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.
2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.
3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.
4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;
5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.
Na pia inawezakana mtu asisamehewe hapa duniani na huko aendako pia asisamehewe..mfano mzuri ni Yule mnyanganyi wa pili aliyesulubiwa na Bwana Yesu pale msalabani, aliyemkufuru Bwana Yesu, Yule hakusamehewa hapa na kule hakusamehewa kwasababu hakutubu.
Lakini sio kama inavyotafsiriwa sasa na baadhi ya imani kwamba kuna uwezekano wa mtu aliyekufa bila kutubu akasamehewa huko anakokwenda kwa kupitia Toharani! hakuna kitu kama hicho mtu yeyote aliyekufa bila kutubu hakuna kusamehewa huko aendako. Atakwenda kuzimu kama maandiko yanavyosema, na hakuna maombi yoyote yatakayoweza kumtoa huko..
Kwahiyo ni heri kutokusamehewa hapa lakini huko uendako ukapata msamaha, na msamaha huo mtu anaupata kwa kutubu tu kabla ya kufa, na si njia nyingine yoyote.
Ubarikiwe.
MADA NYINGINEZO:
KUOTA UMEPOTEA.
INJILI NI NINI?
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
Shalom, mtu wa Mungu, Biblia inasema mtu hataishi kwa mkate tuu, bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Bwana, hivyo pale tunapojifunza Neno la Mungu kwa dhati tuwe na uhakika kuwa Roho zetu zinanenepa na hivyo kujiongezea siku za kuishi hapa duniani (1Wafalme 3:14)..
Tukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza tunaona jinsi Bwana alivyofanya kazi yake ya kuumba ulimwengu kwa siku 6, na ilipofika siku ya 7 aliacha kazi zake zote akastarehe, tena akaibariki siku hiyo kuonyesha kuwa kila kitu kimekamilika, Vile vile ukisoma sura ya pili utaona jinsi Bwana anavyompa Adamu maagizo ya kuishi katika bustani ile, akamletea na Wanyama wote awape majina, naye akafanya hivyo, basi Maisha ya Adamu na viumbe vyake vyote yakaendelea hivyo siku zinakuja siku zinakwenda..
Lakini kilipita kipindi Mungu akamtazama Adamu akasema neno hili “SI VEMA”..Tunasoma hilo katika..
Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”
Embu jaribu kufikiria mtu akisema Neno “si vema” anaashiria nini?, Ni wazi kuwa atakuwa ameona mapungufu, na hivyo anahitaji kufanya marekebisho fulani ili mambo yaende kama anavyotaka..
Ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu, japo alikuwa tayari ameshamuumba mwanamke katika mawazo yake tangu siku nyingi, ukisoma Mwanzo 1:27-28 utalithibitisha hilo, Mwanamke alikuwa tayari kashaumbwa kabla hata ya uumbaji wenyewe kuanza, lakini Mungu aliruhusu kwa makusudi kabisa asitokee katika uumbaji ule wa mwanzo alipokuwa anamuumba Adamu na viumbe vyake vyote, kana kwamba alisahau hivi, ili tu alitumie hili neno SI VEMA, kutufundisha sisi jambo..
Mwanamke alikuja kuumba baadaye kabisa, Maisha yameshaendelea edeni kwa kipindi fulani pengine cha mwaka 1 au 10 au 100 hatujui, lakini mwanamke siku alipokuja kuumbwa, uumbaji ulikuwa umeshamalizika siku nyingi sana huko nyuma.
Kwanini Mungu alifanya hivyo? ni kwasababu alikuwa anatufundisha kuwa yeye anapendezwa na marekebisho, embu jaribu kufikiria marekebisho yake yake jinsi yalivyo na manufaa makubwa kwetu sisi leo hii, jaribu kuwazi hii dunia mfano isingekuwa na wanawake tungeishije ishije huku duniani, mfano usingeupata upendo wa mama leo hii wewe ungekuwaje, usingeupata upendo wa dada leo hii wewe ungekuwaje, usingeuonja upendo wa mke leo hii wewe mwanamume ungekuwa mtu wa namna gani? N.k, hakuna mnyama yeyote au kiumbe chochote kingeweza kukupa faraja duniani kama sio mwanamke..
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa zawadi hii, lakini hiyo yote ni kutokana na marekebisho, kama Mungu angesema mimi nimeshamaliza uumbaji wangu, na siku ya 7 nimeshastarehe, hichi tunachokiona leo hii kisingekuwepo?.
Vivyo hivyo na sisi Mungu anatarajia tuwe tunafanya marekebisho katika ukristo wetu, katika huduma zetu za kuujenga ufalme wa mbinguni, tusione haya kusema SI VEMA…Mungu asiyeweza kukosea alisema hivyo wewe kwanini uone kila kitu kipo vyema?. Kwanini uridhike na ukristo ule ule ambao ulikuwa nao miaka 10 iliyopita, hadi leo unaendelea nao, na huku unaona kabisa unayo mapungufu mengi ndani yako ya kufanyiwa marekebisho?
Kazi ya Mungu inalala, miundo mbinu ya kanisa kila siku inaporomoka, kwanini usiseme SI VEMA hichi kiwe vile, au kile kiwe vile? Natoa mchango wangu wa fedha, au nguvu zangu kupakarabati hapa, au akili uzoefu wangu kufanikisha kile…Mungu anata tuwe hivyo..Unajuaje kuwa hicho unachokirekebisha kitakuwa na manufaa makubwa ya kuleta maelfu wa watu wa Kristo, kama vile mwanamke alivyo na manufaa makubwa sana leo hii kuleta roho nyingi za watu duniani?.
Ukiona umeokoka na muda mrefu upo vilevile, huongezi kiwango chako cha kusali huongezi kiwango chako cha kuwapelekea wengine injili, huongezi kiwango chako cha kufunga, basi ujue umeshatoka nje ya kusudi la Mungu alilotaka wewe uliendee…Tunapaswa tukue toka Imani, hadi Imani, toka utukufu hadi utukufu,..lakini tukiona kila kitu kipo sawa tu ndani yetu, tumeridhika basi tunajidanganya wenyewe.
Ni maombi yangu mimi na wewe, tutaanza kujifunza kusema SI VEMA, Na kuanzia leo kwa msaada wa Bwana tutahakikisha tunaboresha Maisha yetu ya rohoni pamoja na hudumu za kuipeleka injili.
Amen.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine, kama umeona pia SI VEMA, ushiriki baraka hizi peke yako.
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
JE KUJIUA NI DHAMBI?
Bwana Yesu alikuwa na wanafunzi wengi, lakini alikuwa na Mitume 12 tu! Matume hawa 12 wote walichaguliwa kwa ufunuo wa Roho, kwani tunasoma kwamba Bwana kabla ya kuwachagua mitume hao alikwenda kuomba kwanza, ndipo akafunuliwa majina ya mitume hao.
Lakini jambo la kushangaza kidogo ni kwamba miongoni mwa hao mitume 12, alikuwemo mtume mmoja wa Uongo, ambaye aliitwa Yuda Iskariote. Sasa swali linakuja? kwanini Roho Mtakatifu amchague Mtume wa Uongo katikati ya mitume wa ukweli?..Ukitafakari hilo kwa makini kama ni mtu wa kufikiri mambo litakuogopesha kidogo!..Roho Mtakatifu anawapaka mafuta mitume wa uongo na kuwatuma?..Maana Yuda naye alikuwa anatumwa kuhubiri na kutoa pepo kama mitume wengine wote..Na Bwana alimpenda tu kama alivyowapenda mitume wengine…Na bila shaka endapo watu wangemwuliza Bwana eti huyu Yuda naye ni mwanafunzi wako? Ni wazi kuwa angejibu ndio! Asingemkana kwasababu ni yeye ndiye aliyemchagua.
Na ni wazi kuwa mahali pa siri ambapo Bwana alikuwa anakaa, mahali ambapo haruhusu watu wengine kufika isipokuwa mitume wake tu angemruhusu Yuda..Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba upendeleo wote ambao Mitume wa kweli walikuwa wanaupata Yuda naye alishiriki.
Na cha ajabu ni kwamba Yuda Iskariote mwenyewe ambaye ni mtume wa Uongo, hakuna aliyekuwa anamjua kuwa ni mtume wa uongo, isipokuwa Bwana Yesu tu peke yake! Hata mitume wenzake walikuwa hawajui!..Ndio maana utaona wakati Bwana anawaambia mmoja wao atamsaliti…wale mitume 11, walishindwa hata kumhisi kuwa ni Yuda, walijihisi ni wao, kila mmoja alijidhania ni yeye!…ikionesha ni jinsi gani Yuda ilikuwa ni ngumu kumgundua.
Marko 14:18 “Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti. 19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?”
Marko 14:18 “Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti.
19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?”
Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie”.
Ni andiko gani hilo ili litimie? Ni hili:
Yohana 13:18 “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, ALIYEKULA CHAKULA CHANGU AMENIINULIA KISIGINO CHAKE”.
Unabii huo uliandikwa katika kitabu cha Zaburi 41: 9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”.
Yuda akamwinulia kisigino Bwana, akamsaliti kwa vipande 30 vya fedha…akasema
Mathayo 26:14 “Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani, 15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.”
Mathayo 26:14 “Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani,
15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.”
Na Mitume hawa wauongo wapo katika hizi siku za mwisho ili kutimiza hili andiko ! Kazi yao ni kumgeuzia Bwana kisigino na kumwuza kwa vipande vya fedha!..wanawafuata watu na kuwaambia mna shilingi ngapi niwapatie Maji ya Upako?….kama Yuda alivyofanya..badala ya kwenda kuwahubiria wakuu wa makuhani watubu dhambi zao, na kumwamini Yesu, yeye anakwenda kuwahubiria injili ya kuwauzia Yesu..Mfano dhahiri wa mitume na manabii wa uongo wa leo…wanawahubiria watu injili za kumwuza Yesu, una shilingi ngapi nikutolee pepo, una shilingi ngapi nikupe maji ya upako, unashilingi ngapi nije kufanya maombi ya ufumbuzi nyumbani kwako n.k?
Ndugu, epuka injii ya Yuda Iskariote, ya mafanikio kila kukicha? Jiangalie tangu umeanza kutumia hayo maji, mafuta ni nini umenufaika katika roho yako?..Kama umeona yamekusaidia kuacha dhambi, kuacha usengenyaji, kuacha rushwa, kuacha wizi, kuacha matusi, kusamehe, kuacha uasherati basi yatumie lakini kama umeyatumia na hali yako ya kiroho ipo vile vile basi fahamu kuwa Umeuziwa Bwana Yesu kama Yuda alivyowauzia mafarisayo…na wewe umemnunua kwa dhumuni la kwenda kumsaliti na kumsulibisha mara ya pili kutokana na dhambi zako.
Ikiwa hujampa Yesu Kristo maisha yako na unataka kufanya hivyo bado hujachelewa, hapo ulipo, tubu kwa kudhamiria kuacha dhambi zako zote na kisha tafuta mahali ukabatizwe kama hujabatizwa, kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa kuzama mwili wote na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, na baada ya hapo hakikisha unadumu katika kujifunza Neno la Mungu, katika kusali, na kufanya ushirika na wakristo wengine kanisani, kama tulivyoagizwa katika Matendo 2:42
Shalom! jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?
Kuota umepotea mjini, au kuota umepotea shuleni, au kuota umepotea msituni, au kuota umepotea njia panda au kuota umepotea katika riadha au kuota umepotea sehemu usiyoijua, kwa vyovyote vile maadamu ni ndoto ya kupotea basi fahamu kuwa ndoto za namna hii mara nyingi zinatokana na Mungu.
Na huwa zinakuja kwa makundi yote ya watu, (Yaani wale walio ndani ya Kristo na wale walio nje ya Kristo).
Zaburi 37: 18 Bwana anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele. 19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. 20 Bali WASIO HAKI WATAPOTEA, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Zaburi 37: 18 Bwana anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.
20 Bali WASIO HAKI WATAPOTEA, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Unaona wasio haki sikuzote huwa wanapotea, hivyo kuota umepotea ni ujumbe ambao Mungu anakuonyesha hali yako ilivyo rohoni, na kama vile huko ndotoni unavyojiona unahangaika huku na kule kutafuta njia sahihi ya kufika mahali unapotaka kufika na unashindwa, unateseka sana huku na kule, unaonyeshwa kuwa kuna wakati utafika utautafuta huo wokovu ulioupoteza na hautauona milele…na kibaya zaidi wakati huo utakuwa umeshachelewa.
Zaburi 1:6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.
Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha mambo kama hayo mapema ili utengeneze njia zako sasahivi, maadamu upo hai, maadamu imeitwa leo, Kesho inaweza isiwe yako, unaweza ukajiona upo sawa sasa katika Maisha yako, labda umejiendeleza, umefika mbali, una afya nzuri, umefanikiwa, unayo familia nzuri, lakini Mungu anakuambia umepotea, haijalishi upo katika mafanikio gani leo hii, Unachopasw kufanya ni ugeuke uombe msaada kwa Mungu naye atakuonyesha njia…na njia yenyewe ni YESU KRISTO.
Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.
Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. 11 [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea”.]
Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
11 [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea”.]
Kwahiyo ikiwa leo utakubali kutii na kumpa Maisha yako, basi atayaokoa na kukusamehe kabisa, ikiwa upo tayari sasa, hapo ulipo piga magoti kisha chukua dakika chache tafakari mambo yote maovu ulioyomfanyia Mungu, kisha kwa Imani, zungumza na Mungu, mwombe rehema,usimfiche chochote mwambie akusamehe maanisha kabisa kwasababu hapo ulipo anakusikia…Kisha ikiwa toba yako imetoka moyoni kwa dhati, na kwamba upo tayari kuacha yote ya nyuma uliyoyafanya basi fahamu kuwa Mungu amekusamehe, hivyo tu,
Ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38) Ili ukamilishe wokovu wako uwe milki halali ya YESU KRISTO, ndipo Mungu akumwagie kipawa chake cha Roho Mtakatifu. Hivyo zingatia hayo maagizo yote ni muhimu sana kuyafanya, ikiwa hufahamu vizuri ni wapi utapata ubatizo sahihi, basi wasiliana na sisi kwa namba hizi 0789001312 au 0654555788.Tutakusaidia kutafuta maeneo karibu na wewe.
Vile vile ikiwa wewe tayari ulishaokoka, na ndoto kama hizi, kuota umepotea shuleni, au kuota umepotea msituni, au kuota umepotea njia panda au kuota umepotea katika riadha au kuota umepotea sehemu usiyoijua zinakujia, basi fahamu kuwa Mungu anakukumbusha kuwa, unakaribia kuiacha njia ya wokovu, aidha kuna uamuzi unaokwenda kuufanya ambao utakupotezea ramani yako ya wokovu moja kwa moja, au umeshaanza kuifanya..au kuna dhambi unaitenda ambayo haimpendezi Mungu sasahivi,Hivyo kuwa makini sana.. Shika sana ulicho nacho asiye mwovu akalitwaa taji lako.
Ezekieli 44: 9 Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli. 10 Lakini Walawi waliofarakana nami, hapo Waisraeli walipopotea, waliopotea na kuvifuata vinyago vyao, watachukua uovu wao wenyewe.
Ezekieli 44: 9 Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.
10 Lakini Walawi waliofarakana nami, hapo Waisraeli walipopotea, waliopotea na kuvifuata vinyago vyao, watachukua uovu wao wenyewe.
Kwahiyo jitazame, kumbuka Bwana alipokutoa, usimwache yeye..Mungu anakuonya kwa njia hiyo kwasababu anakupenda..Hivyo ukiona unalolijfanya sasahivi linakutenga na Mungu kama linakushinda nguvu ya kulitawala basi liweke kando mtafute muumba wako kwanza kwa usalama wa roho yako na hayo mengine yawe baadaye kama yatakuwa na umuhimu.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NYOTA ZIPOTEAZO.
KUOTA UPO UCHI.
Kuota unafanya Mtihani.
KUOTA UNA MIMBA.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!