(Masomo maalumu kwa watumishi).
Jina la Mwokozi YESU KRISTO Lihimidiwe daima.
Je unajua namna yakujipima kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu na Kristo yu pamoja nawe?
Je unadhani ni ishara na miujiza ndio utambulisho pekee ya kwamba Kristo yu pamoja nawe?
Nataka nikuambie La!..Ishara na miujiza si uthibitisho wa kwanza wa Kristo kuwa pamoja nawe, kwasababu biblia inasema Yohana Mbatizaji hakufanya ishara hata moja lakini bado alikuwa mkuu kuliko manabii wote waliotangulia.
Yohana 10:41 “Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli”.
Na pia wapo watakaofanya ishara lakini atawakana kuwa hawajui…
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Umeona kumbe kufanya ishara au kutofanya si tija!..Si uthibitisho wa kwanza kuwa Kristo yu nawe!.
Sasa ni kipi kinachotupa uthibitsho kuwa tunatembea na YESU katika utumishi tunaoufanya?.
Jibu tutalipata katika maandiko yafuatayo..
Yohana 12:26 “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu”.
Hapo Bwana anasema mtu akitaka kumtumikia, yani kuwa mtumishi wake BASI AMFUATE!!… Na yeye alipo ndipo na mtumishi wake alipo, au kwa lugha nyepesi “Yeye yupo pamoja na wale waliomfuata”.
Sasa tunamfuata vipi YESU?.
Tusome tena maandiko yafuatayo..
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote AKITAKA KUNIFUATA, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote AKITAKA KUNIFUATA, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.
24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.
Kumbe ili tuwe watumishi wa kweli wa Mungu, ambao Kristo atakuwa nasi muda wote ni lazima TUJIKANE NAFSI KILA SIKU??.
Sasa swali ni je tumejikana nafsi zetu? au tunazipenda nafsi zetu na kuzishibisha kwa kila tunachokitaka.
Huwezi kumtumikia Mungu na huku hutaki kuacha mila, huwezi kumtumikia Mungu na huku unaupenda ulimwengu.Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu na huku hutaki kuacha mizaha, na wala dhambi.
Huwezi kumtumikia Mungu na bado unaishi na mke/mume asiye wako. Fahamu kuwa Kristo hayupo na wewe hata kama unaona ishara na miujiza katika maisha yako..hiyo ni kulingana na maneno ya Kristo mwenyewe.
Kanuni ya kutembea na Kristo, itabaki kuwa ile ile MILELE! Nayo ni KUJIKANA NAFSI, KUBEBA MSALABA NA KUMFUATA YEYE!. Kwasababu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele (Waebrania 13:8).
Na hiyo ni kwa faida yetu na si yake! (Ayubu 35:7).
Huenda umeshamwamini Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako!.. Hiyo ni nzuri sana, lakini bado haitoshi, ni lazima uongezee hapo “KUJIKANA NAFSI!”. Na baada ya kufanya hivyo pia ujiandae kwa dhiki kwaajili yake.
Jiandae kuchekwa, kudharaulika, kuonekana mshamba, mjinga na usiyejielewa. Usiogope maana hizo ndizo chapa zake Yesu, (Wagalatia 6:17), na wewe sio wa kwanza, zilianza kwa Kristo BWANA WETU NA AKAZISHINDA.
Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!.
Rudi nyumbani
Print this post
Yapo makazi ambayo si rafiki sana kwaajili ya uponyaji wa maisha yako!.
Kuna mahali/vijiji/mitaa ambayo ukikaa ni ngumu kupokea chochote kutoka kwa Mungu, isipokuwa Mungu mwenyewe amekuambia uishi hapo!. Lakini kama hakuna msukumo wowote wa KiMungu kuishi hapo, basi kuwa makini na mahali utakapopachagua!, kama ni mtaa, mji au kijiji.
Utauliza kwa namna gani?
Utakumbuka yule kipofu aliyepelekwa kwa Bwana ili aponywe!, biblia inasema “Bwana Yesu alimtoa nje ya kijiji kabla ya kumponya” na hata baada ya kumponya alimzuia asirudi kile kijiji alichokuwepo!.
Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23 Akamshika mkono yule kipofu, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? 24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. 25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. 26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, HATA KIJIJINI USIINGIE”
Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.
23 Akamshika mkono yule kipofu, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda.
25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.
26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, HATA KIJIJINI USIINGIE”
Umeona?..sababu ya Bwana kumtoa huyu kipofu nje ya kijiji si kwasababu ya ghasia ya watu!, hapana bali ni kutokana na hali ya kiroho ya mahali pale, maana yake mazingira ya kile kijiji yalikuwa ni magumu kwa yule mtu kupokea uponyaji! (Maana yake ukinzani uliokuwepo pale ulikuwa ni mkubwa sana), Ndio maana Bwana akamtoa kwanza nje ya kijiji kabla ya kumponya!
Hali kama hiyo inaendelea hata leo!, ipo mitaa ambayo ina vita vikali vya kiroho kuliko mingine, vipo vijiji vilivyo vizito kuliko vingine, na sisi kama wana wa Mungu ni lazima tuongozwe na roho mahali pa kwenda na mahali pa kuishi.
Aina ya vijiji/mitaa ifuatayo kuwa makini nayo!
1. Yenye watu wengi wasio na hofu ya Mungu.
Ukiona mtaa/kijiji hakuna hofu ya Mungu, maana yake watu wa mahali hapo ni watu wasiojali, na hata kuidharau injili, na kuipinga kazi ya Mungu, kuwa makini na huo mtaa au hicho kijiji. Kwasababu mitaa inayoikataa Injili mara nyingi inakuwa chini ya vifungo vya laana (Mathayo 10:14-15), na mwisho wake huwa inaharibiwa na Mungu aidha kwa mapigo ya magonjwa au majanga au hali za kiuchumi!.
2. Yenye kiwango kikubwa cha ushirikina na uasherati.
Uchawi na uasherati ni ibada kuu mbili za shetani. Mahali palipojaa kiwango kikubwa cha uasherati na ushirikina fahamu kuwa hiyo ni kambi ya adui asilimia zote. Kuwa makini na mahali hapo!. Kama Roho wa Bwana amekuongoza uishi, basi ishi hapo na utafanikiwa, maana ni mapenzi yake!..lakini kama sio, basi usiishi hapo, ili ubaki salama na familia yako!, (mara nyingi adui anatumia mitaa/vijiji kuharibu watoto au ndoa), hivyo kuwa makini!
Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake”
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
AINA ZA MAJINI, MAJINA YAO, KAZI ZAO, NA TIBA ZAKE.
Aina za dhambi
UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.
Kila mwanadamu, kuna aina Fulani ya mizigo anayo. Mizigo tunayoizungumzia hapa sio mizigo ile ya dhambi n.k. Hapana, bali ile ya kimajukumu. Kama vile utafutaji wa rizki, kodi, ada, elimu, ujenzi n.k. Hii ni mizigo ambayo inatufanya tusiwe katika hali Fulani ya utulivu.
Wakati mwingine haiepukiki, ni lazima tukumbane nayo. Lakini kosa linafanyika ni pale tunapotaka kuibeba mizigo hiyo yote ndani ya siku moja. Au tuyatatue matatizo yote kwa kipindi kifupi.
Ukiwa mtu wa namna hiyo hata ukiwa tajiri wa namna gani, Bado utaona maisha ni magumu, tena yenye shida na taabu isiyokuwa ya kawaida, na wengine wanaishia hadi kujinyonga kwa namna hii. Kwasababu gani? Kwasababu Mungu hajatuumbia tuibebe mizigo kwa namna hiyo? Leo tutaona ni kwa namna gani tunaweza kuibeba mizigo yote.
Kwamfano unapofikiria, changamoto za chakula cha mwaka mzima uzimalize leo, hivyo unafikiria ni wapi utapata pesa ya kununua mapipa 5 ya mahindi, wakati huo huo unafikiria ada za watoto za miaka 5 mbele itakuwaje, hivyo unahangaika uzipate nazo leo, tena wakati huo huo unafikiria uende katika mafunzo ya kujiongezea aina 7 za elimu, ambazo ungepaswa uzisomee kwa miaka 10, unataka uzimalize ndani ya miezi 3. Tena uanze kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanja vya watoto wako watano, ambapo ndio kwanza wananyonya, na wengine wapo tumboni.
Yaani kwa ufupi ufanye mambo yote chap-chap ndani ya kipindi hiki hiki kifupi. Ukweli ni kwamba kamwe hutakuwa na raha katika maisha yako. Utaona maisha ni mazito sana, hayabebeki, hata kama utakuwa unapata vingi kiasi gani. Kumbuka, Kusema hivi haimaanishi tusifikirie kuwekeza, hapana, lakini fikiria hivyo tayari kipo mkononi, lakini kama hakipo, usijijengee akili hiyo.
Hivyo Mungu ametusaidia kwa kutupa njia ya kuibeba mizigo hiyo yote. Nayo si nyingine zaidi ya ile ya “kuimega siku kwa siku”.
Luka 11:3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
Bwana ameivunja vunja mizigo yetu katika siku. Ametaka kukupa rizki ya siku, kesho usiwe na presha nayo sana, Bwana ataifungulia milango yake, amekupa ada ya muhula mmoja, shukuru, ile ya muhula wa pili ikifika atakupa, usiwe na wasiwasi wa ada ya miaka 3 mbele, atapata ugonjwa wa moyo. Acha hata kufikiria kodi ya miaka 2 mbele, ikiwa umejaliwa ya mwezi mmoja, shukuru. Hujua mwaka ujao utahama hapo, au Bwana atakufungulia milango ya Baraka zaidi ukanunua pako.
Jukumu lolote ulilonalo, embu livunje vunje kwenye vipindi vifupi, Kwasababu hujaumbiwa uibebe mizigo yote kwa wakati mmoja. Ukiitabikia sana “kesho yako” leo, ujue unajijengea mazingira ya stress.
Ni kwa faida yako mwenyewe., Lakini ukiwa mtu wa kushughulika na siku yako utashangaa tu mbeleni umeweza litatua hilo tatizo kubwa kirahisi, kwa njia mbalimbali Mungu atakazokufungulia, kwasababu ni hekima ya Mungu imetumika hapo si ya mwanadamu.
Mathayo 6:31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Shalom.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?
Fahamu Namna ya Kuomba.
Kupiga ramli ni nini katika biblia?
Watu wenye kuvunja maagano ndio watu wa namna gani? (Warumi 1:31)
Waebrania 4:14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu”
Kuungama maana yake ni kukiri kwa wazi jambo fulani mbele ya wote… Katika ukristo tunaungama kwa “kukiri kwa vinywa vyetu kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu, na kukiri kwa vinywa vyetu kuwa sisi ni wenye dhambi, na kutubu!”.. sawasawa na Warumi 10:10.
Warumi 10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.
Warumi 10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.
Biblia inazidi kutufundisha kuwa ni lazima TUYASHIKE MAUNGAMO YETU, maana yake tusikiri tu kwa vinywa na kusahau, bali yale tuliyoyakiri mbele za Mbingu na Nchi, hayo TUYAISHI siku zote za maisha yetu.
Sasa swali tunayashikaje/tunayaishije Maungamo yetu?.
Tusome 1Timotheo 6:12.
1Timotheo 6:12 “PIGA VITA VILE VIZURI VYA IMANI; SHIKA UZIMA ULE WA MILELE ULIOITIWA, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi 13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato”.
1Timotheo 6:12 “PIGA VITA VILE VIZURI VYA IMANI; SHIKA UZIMA ULE WA MILELE ULIOITIWA, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi
13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato”.
Kumbe tunayashika Maungamo yetu kwa kuvipiga vita vya Imani, na kushika ule uzima wa milele tulioitiwa!. Hebu tutazame moja baada ya lingine.
1.PIGA VITA VYA IMANI.
Vita vipo vingi, lakini kama wakristo tumeagizwa kupigana vita vya aina moja tu!, NAVYO NI VILE VYA IMANI!. Na vita hivyo hatupambani na wanadamu wenzetu, bali na roho za mapepo na falme zao katika ulimwengu wa roho…
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.
Kwa maelezo marefu kidogo kuhusiana na vita hivi vya Imani na jinsi ya kupambana fungua hapa >>> TUZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA.
2) SHIKA UZIMA WA MILELE.
Yohana 17:2 “kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 3 Na uzima wa milele ndio huu, WAKUJUE WEWE, MUNGU WA PEKEE WA KWELI, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA”.
Yohana 17:2 “kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
3 Na uzima wa milele ndio huu, WAKUJUE WEWE, MUNGU WA PEKEE WA KWELI, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA”.
Uzima wa milele maana yake ni “kumjua sana Mungu na Yesu Kristo aliyemtuma”… Hivyo tunavyodumu katika kutafuta kumjua Mungu na siri iliyopo ndani ya mwanae Yesu Kristo ndivyo uzima wa milele unavyozidi kudumu ndani yetu. Lakini tutakapopunguza kumtafuta Mungu, ndivyo ule uzima wa milele unavyozidi kufifia ndani yetu.
Je unayashika Maungamo yako?.
Bwana atusaidie.
Maran atha!
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
VITA DHIDI YA MAADUI
USIMPE NGUVU SHETANI.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Kuungama ni nini?
Jina Kuu la ukombozi wa roho zetu, (Jina la YESU KRISTO) lihimidiwe daima!
Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa vitabu vya biblia, tumekwisha kuvitazama vitabu kadhaa vya nyuma na leo tutavitazama vitabu vitatu vya mbele, ambavyo ni kitabu cha Yoeli, Amosi na Obadia. Hivyo ni vizuri kwanza kusoma vitabu hivi mwenyewe katika biblia, ndipo ukapitia uchambuzi huu, na kumbuka uchambuzi huu ni ufupisho tu!, na si wa kutegemea kama darasa kamili au ufunuo kamili wa vitabu hivi, hivyo ni muhimu sana kusoma biblia na kumruhusu Roho Mtakatifu afunue, ndipo masomo mengine yafuate juu yake.
Ikiwa bado hujavipitia vitabu vya awali, ni vizuri ukavipitia kwanza kabla ya vitabu hivi ili tuweze kwenda pamoja.
KITABU CHA YOELI:
Kitabu cha Yoeli, ni kitabu cha 29 katika orodha ya vitabu vya agano la kale, na kimeandikwa na Nabii Yoeli mwenyewe, mapema katika karne ya 8 kabla ya Kristo, kipindi cha Mfalme Uzia wa Yuda, na maana ya jina “Yoeli” ni “Yahwe ni Mungu”.
Kitabu cha Yoeli kina Milango (Sura) tatu tu!, na kila sura/mlango una ujumbe tofauti.
Yoeli: Mlango wa kwanza.
Katika mlango wa kwanza Nabii Yoeli, anaelezea madhara yaliyoletwa na Nzige, na parare, na madumadu waliotokea Israeli. Historia inaonyesha kipindi cha miaka kadhaa kabla ya Yoeli kuandika kitabu hiki, kulitokea Janga ambalo lililetwa na Mungu kutokana na maasi.
Na janga hilo lilikuwa la Kuzuka kwa Nzige, parare na madumadu ambao walikula mazao yote, na kutokusaza chochote, Uharibifu wa Nzige hao uliwashangaza wote, kwani walikula mazao yote.
Na baada ya pigo hilo, ndipo Mungu anampa Nabii Yoeli ujumbe wa kuwaambia watu wake, kwamba watafakari hayo yaliyotokea, na wapate akili, na kutubu,.. watafakari jinsi wadudu hao walivyoharibu mazao kiasi kwamba makundi yote ya watu waliathirika, mpaka makuhani pia waliadhirika kwani hakikupatikana hata cha kutoa katika nyumba ya Mungu, maana yake zile sadaka za unga zilizokuwa zinatolewa ndani ya hekalu hazikutolewa tena..(Yoeli1:9).
Yoeli 1:1 “Neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli. 2 Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu? 3 Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine. 4 Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu. 5 Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu. 6 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa. 7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe”.
Yoeli 1:1 “Neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli.
2 Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu?
3 Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.
4 Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.
5 Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
6 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa.
7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe”.
Kutokana na pigo hilo la Nzige, Mungu anawaita watu wake wote watubu!, ikiwemo makuhani, wafunge kwa kulia na kuomboleza, na tena wafunge katika saumu ya kweli (Yoeli 1:13-14).
Yoeli: Mlango wa 2.
Katika mlango wa Pili, Mungu analifananisha jeshi hilo la Nzige na jeshi atakalolinyanyua la watu ambao watavamia Israeli na kuharibu watu na vitu, kwa jinsi hiyo hiyo ya Nzige walivyoharibu mazao! Kwasababu ya maasi ya Israeli. Hivyo anazidi kuwaasa watubu!, kwa kupiga mbiu kwa watu wote, kwani jeshi hilo la watu ambao Bwana analifananisha na nzige litakapopita litapageuza Israeli jangwa (Yoeli 2:3), na Mungu atalipa uwezo wa kuharibu kwa uharibifu mkuu (Soma Yoeli 2:4-10).
Lakini katika Mstari wa 12, Bwana anarudia kutoa shauri la kutubu! Ili aiponye nchi kutokana na pigo la nzige, waliokula mazao, vile vile kwa pigo ambalo atakwenda kulipiga Taifa hilo kwa jeshi la watu wabaya atakaowatuma kuwadhuru.
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; 13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. 14 N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu? 15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; 16 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. 17 Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
14 N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?
15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;
16 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake.
17 Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Mstari wa 17-32: (Ahadi ya kuponywa miaka ya njaa)
Bwana anatoa ahadi ya marejesho ya chakula katika miaka iliyoliwa na parare na nzige (katika pigo la Nzige). endapo watatubu!
Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. 26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. 27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe”.
Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe”.
Lakini haiishii tu kutoa ahadi ya kuponya miaka iliyoliwa na Nzige, bali pia Bwana anatoa ahadi nyingine ya kipekee ya kuwabariki watu katika roho, (yaani kuwamwagia Roho wake Mtakatifu).
Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu”.
Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu”.
Mlango wa 3 wote unahusu ahadi ya Bwana ya kuwapigania Israeli dhidi ya majeshi yaliyowaonea, baada ya wao kutubu, na kumrudia yeye.
Sasa tukirudi katika biblia, tunasoma baada ya Nabii Yoeli kuondoka, Israeli hawakutubu kikamilifu, ijapokuwa walipigwa na janga hilo la Nzige, na parare na madumadu na tunutu..lakini waliendelea kuwa vile vile, mpaka Bwana alipotimiza neno lake hilo la kuleta jeshi la watu ambao wataharibu nchi mfano wa hao nzige waliotangulia, na jeshi halikuwa lingine Zaidi ya lile la Wakaldayo, ambalo Bwana Mungu aliliruhusu lifike Yuda na kuharibu hekalu na kuwaua wayahudi wengi na baadhi yao kuwachukua utumwani Babeli.
Na kule utumwani walikaa miaka 70, na baada ya ile miaka 70, Danieli alisimama kutubu kwa niaba yao baada ya kuujua unabii wa Yeremia kuhusu muda wao wa kukaa utumwani, na waliporejea Bwana aliwapa majuma 69 (ambayo ni miaka 483) ya kuujenga Yerusalemu kabla ya kutimiza ahadi yake ya kumwanga Roho Mtakatifu.
Na miaka hiyo ilipotimia Bwana aliachilia Roho wake mtakatifu sawasawa na ahadi yake aliyoiahidi, katika Yoeli 2:28, ambapo ilitimia ile siku ya Pentekoste (Matendo 2:17).
Matendo 2:14 “Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri”.
Matendo 2:14 “Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri”.
Na mpaka leo hii Roho Mtatifu yupo, na ndiye Muhuri wa Mungu juu ya mtu (Warumi 8:9, Waefeso 4:30, 2Wakorintho 1:22).
Kwa undani Zaidi kuhusiana na wadudu hawa (parare, nzige, madumadu na tunutu) na ujumbe gani wa ziada wamebeba kiroho, fungua hapa >>>Nzige, Parare, madumadu na tunutu ni wadudu gani? (Yoeli 2:25)?
KITABU CHA OBADIA:
Kitabu cha Obadia ni kitabu kilichoandikwa na Nabii Obadia mwenyewe, na kina Mlango mmoja tu!, hivyo kukifanya kuwa kitabu kifupi kuliko vitabu vyote vya agano la kale. Maana ya jina ‘Obadia’ ni “Mtumishi wa Bwana”.
Kitabu cha Obadia kinahusu Hukumu Mungu alioitangaza juu ya Taifa la Edomu (Nchi ya Edomu sasahivi ni maeneo ya kusini-magharibi mwa nchi ya Yordani).
Kwaasili Edomu ulikuwa ni urithi wa Esau aliyekuwa ndugu yake Yakobo! (Mwanzo 25:30 na Mwanzo 36:8)... Na tangu Esau na Yakobo wakiwa tumboni mwa mama yao, walikuwa wakipambana!.
Mwanzo 25:22 “Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. 23 Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo. 24 Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake”
Mwanzo 25:22 “Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.
23 Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.
24 Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake”
Kutokana na unabii huo wa Esau kupambana na Israeli, ulifika wakati kiburi cha wana wa Esau (Edomu) kilinyanyuka kwa kiwango kikubwa..kwani walijinyanyua mbele za Mungu na kufanya dhambi na vile vile kuwafanyia mabaya makubwa wana wa ndugu yao Yakobo (yani wana wa Israeli). Na hivyo Mungu kutamka hukumu juu yao kwa kinywa cha Nabii wake Obadia.
Obadia 1:1 “Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema,Haya,inukeni ninyi;Na tuinuke tupigane naye. 2 Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana. 3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? 4 Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana”.
Obadia 1:1 “Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema,Haya,inukeni ninyi;Na tuinuke tupigane naye.
2 Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana.
3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
4 Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana”.
Lakini mbali na hilo, historia inaonyesha kuwa kipindi Wakaldayo wameuhusuru Yerusalemu na baadaye kuivamia na kuharibu mali, wana wa Edomu walishirikiana na wakaldayo kushirikiana nao, na hata kuchukua mali nyingi za wana wa Israeli, sawasawa na unabii huo alioutoa Obadia miaka mingi kabla ya wana wa Israeli kuchukuliwa utumwani..
Obadia 1:11 “Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao”.
Hivyo kwa kosa hilo na mengine ambayo hayajatajwa katika biblia, Bwana Mungu alitangulia kuwaonya lakini hawakutubu, hivyo ulipofika wakati Edomu iliadhibiwa sawasawa na hukumu hiyo, lakini pia iliyopo sasa itakuja kuadhibiwa katika vita vya mwisho vya Ezekieli 38.
Maelezo kwa kina kuhusu Edomu fungua hapa >>>Edomu ni nchi gani kwasasa?
Na baada ya Bwana kuiadhibu Edomu, kutokana na mabaya waliyoifanyia Israeli, Bwana anatoa ahadi ya kuijenga Yerusalemu, baada ya ubaya wao kupita.
Obadia 1:18 “Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo”.
Ni nini tunajifunza katika kitabu hiki cha Obadia?..
Tunachoweza kujifunza kikubwa ni kwamba Mungu anatoa unabii unaokuja kama onyo!, ili yamkini mtu au Taifa lisije kuangukia katika hukumu ya Mungu, Watu wa Edomu walipewa unabii huu kama ushauri kwamba wakati wa msiba wa Israeli wasishirikiane na watu wakaldayo, na onyo hilo walipewa miaka mingi kabla ya Israeli kuja kuvamiwa na wakaldayo, lakini hawakutii unabii huo, na wakafanya waliyoyafanya na leo hii hawapo!.. Wanaoishi Edomu sasa si wana wa Esau bali wana wa Ishmaeli, ambao kulingana na unabii wa kibiblia watafutwa katika vile vita vya Ezekieli 38, na 39, kama walivyofutwa hawa wana wa Edomu.
Na sisi vile vile hatupaswi kutweza unabii (yaani kudharau unabii wa kibiblia). Unabii wa biblia unasema kuwa siku za mwisho watatokea watu wa dhihaka, watu wasiotii wazazi wao, wakaidi, wasiotaka kufanya suluhu, watukanani n.k (soma 2Timotheo 3:4), na kwamba watu wa namna hii hawataurithi ufalme wa Mungu.
Sasa unabii huu ni kweli utatimia, hivyo si wa kuutweza/kuupuzia..kwasababu ni kweli siku za mwisho, ambazo ndizo hizi hawa watu wametokea, hivyo hatupaswi kuwa miongoni mwa watakaotimiza unabii huo wa watakaodhihaki na kupotea, badala yake tutimize unabii wa watakaokolewa kwa kumfuata Mungu na kuitii Injili.
1Wathesalonike 5:20 “ msitweze unabii;”
Usikose mwendelezo..
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Vitabu vya Deuterokanoni ni vya kiMungu?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
Wafilipi 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Katika vifungu hivyo utaona neno “yoyote” limetumika sana. Ikiwa na maana yapo mengi, ya aina mbalimbali, ambayo hayajaandikwa hapo. Na hapo biblia inaegemea katika “yale yaliyo mema”.
Tukumbuke kuwa biblia haijaandika matendo yote mema mwanadamu anayopaswa kuyafanya. Kama ingekuwa hivyo basi kingekuwa ni kitabu kikubwa sana, ambacho hakuna mwanadamu yoyote angeweza kukimaliza kwa kukisoma. Lakini imetoa kama muhtasari tu, au mwongozo wa kufuata.
Kwamfano huwezi, kuona katika maandiko tunaagizwa ‘tuimbe kwaya kanisani’, lakini hayo ni moja na yenye kupendeza, au kuona tunaambiwa tuhubiri injili kwa njia ya maigizo. Lakini, tumebuni wenyewe na mwenye dhambi anapotizama filamu hizo, huwa inachangia katika kuwasogeza karibu kwa Kristo. Maadamu havitoki nje ya maudhui mema.
Au tunapotumia vipaza sauti, au tunaposambaza vipeperushi vya injili barabarani, huwezi ona agizo hilo, popote kwenye maandiko. Lakini ni moja ya yale yaliyo ya kweli.
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa yapo mambo mengi ambayo tunaweza kuyafanya, na Bwana hatuzuii kuyatafakari, ndio maana akamalizia kwa kusema ‘yatafakari hayo’. Maana yake tutafiti na tutumie njia zote, ambazo tunaona hatma yake itakuwa ni kuujenga ufalme wa Mungu, au kuufanya upendeze zaidi.
Angalia katika ujuzi wako, angalia katika elimu yako, ni kwa namna gani utafanya jambo la ki-Mungu lenye kukuletea sifa njema kwake. Utumishi wa Mungu sio pale madhabahuni tu kuhubiri, utumishi wa Mungu ni mpana. Hivyo Hapo hapo ulipo tafakari ni kwa namna gani utaujenga ufalme wa Mungu wako, na Bwana atakupa akili njema.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?
Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).
Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.
Jibu: Tusome,
Waebrania 8:13 “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”.
Neno “kuukuu” maana yake ni “kitu kilichochakaa/ kilichoisha muda wake”.. Hivyo hapo biblia inaposema kuwa Agano la kwanza amelifanya kuwa kuukuu tafsiri yake rahisi ni kwamba “Agano la kwanza yaani lile la kale amelifanya kuwa chakavu (lililoisha muda wake)/ lisilofaa tena”.
Lakini swali ni je!.. kupitia mstari huo inamaanisha kuwa Agano la kale litapotea kabisa na halitatumika?…kiasi kwamba halifai tena wala halitatumika?
Jibu ni la! Bwana Yesu alisema mwenyewe kuwa “hakuna yodi moja wala nukta moja ya torati itakayoondoka (soma Mathayo 5:18)”… Na Zaidi sana alisema hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza.
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.
Sasa swali linarudi pale pale kama hivyo ndivyo kwamba Bwana YESU hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza, na kwamba agano la kale bado litaendelea kuwepo, ni kwanini hapo katika Waebrania 8:13 biblia iseme kuwa litatoweka kabisa?. Je! Biblia inajichanganya??
Jibu ni La! biblia haijichanganyi bali tafakari zetu ndizo zinazojichanganya!.
Ili tuelewe vizuri tutafakari mfano ufuatao.
Kampuni moja limetoa aina Fulani la gari, na aina hiyo ya gari ikatumika kwa miaka kadhaa, lakini baada ya miaka 10 ikatoa toleo lingine jipya la aina ile ile ya gari, na hivyo kampuni hilo likaacha kuzalisha lile toleo la kwanza lililo dhaifu na kujikita katika uzalishaji wa toleo jipya.
Sasa ni wazi kuwa kwa jinsi miaka inavyozidi kwenda lile toleo la kwanza litaenda kupotea kabisa na kubaki hili la pili… kwa lugha nyepesi tunaweza kusema kuwa… “Kampuni lile limelifanya toleo la kwanza kuwa kuu, na hivyo lipo karibuni kutoweka kabisa”.
Lakini kwa kutoa toleo jipya haimaanishi kuwa limelipinga lile la kwanza, kwamba badala ya kuzalisha magari sasa linazalisha treni. Hapana! Bali kinyume chake limeliimarisha lile la kwanza, ikiwa na maana kuwa kama tairi za toleo la kwanza zilikuwa dhaifu, basi toleo la pili limeziongezea uimara, lakini gari ni lile lile, vile vile kama mwonekano wa toleo la kwanza ulikuwa si mzuri basi toleo la pili limeongeza uzuri wa kimwonekano lakini gari ni lile lile.
Na ndivyo katika habari ya agano jipya na lile la kale, Hakuna kilichoondolewa, na kuletwa kingine kipya, bali ni kile kile kilichokuwepo kimeimarishwa Zaidi, kuwa bora Zaidi, kuwa imara Zaidi, kuwa chenye uwezo Zaidi n.k
Kwamfano biblia inasema katika mojawapo ya amri katika agano la kale kuwa “usizini” ikaishia hapo… Sasa hii amri ilikuwa ni dhaifu, kwasababu inasema usizini tu!, mtu anaweza asizini kweli lakini moyoni mwake akalipuka tamaa..
Lakini sasa Bwana YESU aliye mjumbe wa agano jipya anakuja kuitimiliza amri hiyo kuwa “mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake”. Hata kabla ya kwenda kufanya kile kitendo.
Mathayo 5:27 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”
Mathayo 5:27 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”
Na vile vile katika amri ya “kuua” ni hivyo hivyo…(soma Mathayo 5:21-22).
Kwahiyo kwa lugha nyepesi ni kwamba Agano la pili ni toleo jipya la Agano la kwanza. Lakini mambo ni yale yale.
Sasa swali lingine.. Ni wakati gani ambapo agano la kale lilianza kuwa kuu kuu?
Jibu: Ni wakati wa kuja kwa Bwana Yesu kwa mara ya kwanza.
Kipindi Bwana Yesu alipokuja, yeye ndiye mwanzilishi wa agano jipya, na kuanzia huo wakati ndio agano la kale katika maarifa yake machanga lilipoanza kuisha muda wake, na mpaka leo hatulitumii tena, limetoweka! Na nguvu katika damu ya Yesu ndani ya agano jipya inatawala.
Ndio maana maarifa machanga ya agano la kale, mfano matumizi ya damu za wanyama kama sadaka za kafara zimebaki kutumiwa na watumishi wa shetani, na katika ukristo Damu ya Yesu ndio utimilifu wa Torati za kafara. Na yeyote anayetumia kafara za wanyama leo hii, awe anajiita mtumishi wa Mungu au mtu yeyote yule anafanya ibada za miungu.
Kwahiyo leo hii katika ukristo hatuna matambiko, wala kafara za wanyama, wala utakaso kupitia damu za wanyama, wala hatuishi kwa kujizuia kuua lakini mioyoni tuna hasira, au tamaa.. bali tunaishi kwa Roho mtakatifu na tunamuabudu Mungu katika roho na kweli.
Bwana atubariki.
MJUMBE WA AGANO.
Je! waliokufa kabla ya Bwana Yesu wataokolewaje?
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
SWALI: Nini maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
JIBU: Mstari huu unatuonyesha hatari ya kazi yoyote inayotendwa na mtu. Hapo ametumia mfano wa wanaochonga mawe. Wajenzi wa zamani walikwenda kuchonga mawe miambani kwa ajili ya ujenzi wa majengo yao, lakini wakiwa kule walikutana na hatari nyingi, aidha kuangukiwa na mawe hayo, na kuwaponda viungo vyao, vifaa vyao vya uchongaji kuwajeruhi.
Vilevile anatumia tena mfano wa wanaopasua miti, kwa ajili ya mbao za ujenzi, bado na wao pia wanakutana na hatari, aidha kuangukiwa na miti yenyewe, au shoka kuteleza na kumjeruhi mtu au yeye.
Kumbukumbu 19:5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai.
Ni sawa na mjenzi ambaye amezoea kupiga sana nyundo au kuwepo maeneo ya ujenzi muda wake mwingi, utaona upo wakati nyundo itateleza na kumponda kidole chake, au atakanyaga msumari n.k. Tofauti na kama angekuwa hajishughulishi na kazi hiyo yupo nyumbani tu.
Hii ni kufunua nini rohoni?
Kama wana wa Mungu tufahamu kuwa kazi yake ya kwenda kung’oa mapando ya mwovu, katika shamba la Bwana tutarajie kukutana na madhara yake, si wakati wote utakuwa ni mwepesi tu (yaani kuvuna), zipo nyakati tutakutana na kupigwa, au kudhalilishwa, au kufungwa na wakati mwingine hata kuuawa. (Mathayo 10:17-19)
Mtume Paulo alipokuwa katika ziara zake za kupanda ukristo Asia na Ulaya, alikutana na hatari nyingi, ikiwemo kupigwa mawe na watu wabaya, kufungwa, na kurushiwa vitisho mbalimbali. Wamishionari kama dr David Livingstone walioleta injili Afrika zamani walikutana na hatari za magonjwa kama malaria, na wanyama wakali.
Lakini katika yote, Bwana ameahidi, mafanikio makubwa, kuliko hatari zake. Hivyo hatupaswi kuogopa na kudhani kuwa kazi ya Mungu ni kazi ya kwenda kujichinja wakati wote. Hapana, zipo nyakati nyingi za raha, na mafanikio makubwa ya rohoni yasiyokuwa na ghasia yoyote, lakini Bwana hajatuficha pia hatari zake wakati mwingine. Ili tutakapokutana nazo tusihuzunike moyo na kukata tamaa, bali tuendelee na kazi.
Je! Umeokoka? Je! Umesamehewa dhambi zako? Kama ni la, ni nini kinachokusubirisha? Ukifa leo utakwenda wapi, kumbuka lipo ziwa la moto, kumbuka ipo hukumu kwa waovu. Tubu leo mgeukie Kristo akusafishe dhambi zako, Ukabatizwe katika jina la Yersu Kristo upokee ondoleo la dhambi. Hizi ni siku za mwisho, Kristo anakaribia kurudi.
Ikiwa upo tayari leo kufanya hivyo basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).
TUUTAFUTE UMOJA WA ROHO.
Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”. Kulingana na huu mstari je ni kweli fedha ni jawabu la kila kitu?.
Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.
Kulingana na huu mstari je ni kweli fedha ni jawabu la kila kitu?.
Jibu ni La! Fedha haitoi jawabu la mambo yote, kama ndio basi fedha ingeweza kununua uzima wa milele, hivyo kusingekuwa na haja ya Bwana Yesu kutoa uhai wake kwaajili ya uzima wa roho zetu.
Lakini biblia inatufundisha kuwa tumekombolewa kwa damu ya Yesu na si kwa fedha.
1 Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.
1 Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu
19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.
Vile vile fedha haiwezi kutibu kifo, wala kununua amani, kwasababu wapo watu wenye pesa nyingi lakini hawana amani n.k.
Lakini kama hivyo ndivyo kwamba fedha si jawabu la mambo yote, kwanini biblia iseme ni jawabu la mambo yote?.
Ili kupata jibu la swali hili ni vizuri tukausoma mstari huo kwa kutafakari kwa kina sehemu za kwanza za mstari huo na zile za mwisho.
Mstari huo unaanza kwa kusema.. “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko” na unaendelea kwa kusema… “Na divai huyafurahisha maisha”…na unamalizika kwa kusema “NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.
Sasa swali ni mambo gani hayo ambayo fedha inaleta majibu yake?.
Jibu: Ni mambo hayo yanayotajwa hapo juu, maana yake yahusuyo karamu hizo ziletazo kicheko zenye ulevi…. na si mambo mengine tofauti na hayo.
Na kweli mambo ya kidunia karibia yote jawabu lake ni fedha, maana yake ukiwa na fedha utaweza kuyafanya au kuyapata, na ukizikosa fedha pia unaweza kuyakosa.
Anasa zote za kidunia zinahitaji pesa, na wanaotaka anasa wanazitafuta pesa kwasababu hilo ndio jibu lake.
Lakini wana wa Mungu, hawaishi kwa fedha wala fedha si jawabu la mambo yao yote…bali Damu ya Yesu ndio jawabu la mambo yao yote.
Wana wa Mungu hata pasipo pesa wanaweza kuishi vizuri kabisa, na pia hawana tabia ya kupenda fedha, bali fedha yao ni Damu ya Yesu katika Roho Mtakatifu.
Je upo ndani ya agano la damu ya Yesu au Mungu wako ni fedha?.
Waebrania 13:5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa”
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?
Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.
Mtakatifu Rita, ambaye kwa kanisa katoliki anajulikana pia kama ‘mwombezi wa mambo yasiyowezekana’, na ‘mfanya miujiza’.
Ni mama aliyezaliwa mwaka 1381, katika mji unaitwa Kashia, taifa la Italy. Aliolewa akiwa na umri mdogo lakini baada ya mume wake na watoto wake wawili kufa aliamua kujiunga na utawa, ijapokuwa alipitia changamoto, kujiunga na jamii hiyo kwasababu tayari alikuwa ameshaolewa(sio bikira), lakini mwishoni alifanikiwa.
kulingana na kanisa katoliki maombi ya Rita yaliwaletea wengi majibu, lakini pia alitambulika kwa jeraha dogo kwenye kipaji cha uso wake, wakiamini kuwa ni alama ya ukristo, kufuatana na mateso ya Yesu msalabani, mahali alipowekewa taji ya miiba. Alikufa kati ya umri wa miaka 75-76.
Na ilipofika tarehe 24 May 1900, papa Leo XIII, Alimtangaza kuwa mtakatifu. Yaani ukitangazwa kuwa mtakatifu, unakidhi vigezo vya kuwa mwombezi wa walio hai.
Tangu huo wakati wakatoliki wengi duniani wamekuwa wakimfanyia novena, na litania. Na wengi wakishuhudia kuwa matatizo yao sugu, yakitatuliwa, hivyo imemfanya kuwa maarufu sana.
Lakini Je! Jambo hili ni kweli? Ni vema kufahamu kuwa katika maandiko matakatifu (BIBLIA), Hakuna mahali popote, tunafundishwa kuwa watakatifu waliokufa zamani au sasa wanaweza kutuombea. Zaidi sana wanakuwa hawaelewi neno lolote linaloendelea duniani, biblia inasema hivyo katika;
Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Umeona? Kwahiyo desturi hii, ya kupeleka maombi yetu kwa watakatifu watuombee, ni ya kipagani, Ni ibada za sanamu, ambayo asili yake ilianzia kwenye dini zinazoamini mizimu inaweza kuwasiliana nasi. Kusema hivi haimaanishi tunawapinga wakatoliki, au tunatangaza chuki hapana, bali tunasemezana ukweli ili tupone, kwasababu safari yetu ni moja sote tuurithi uzima wa milele, sisi tunasema ni wakristo.
Haijalishi utakuwa ulifanya novena ya Rita ikakuletea majibu kiasi gani, bado ni ibada ya sanamu, kumbuka pia shetani analeta majibu, si ajabu mambo hayo kutendeka, ili watu wapumbazike katika hayo.
2Wakorintho 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Mwombezi wetu ni mmoja tu naye ndiye YESU KRISTO (1Yohana 2:1). Lakini sio pamoja na Petro, au Paulo, au Eliya, au Mariamu, au Yusufu. Hao wote ni watakatifu ambao walihitaji ukombozi tu kama sisi, na wenyewe walituelekeza kumtazama Yesu Kristo, na sio wao.
Mtume Paulo alisema maneno haya;
1Wakorintho 1:13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
Hivyo hakuna haja ya kupeleka maombi yako kwa mtakatifu yoyote, na vilevile wale walio kule hawawezi kutuombea sisi pia. Halikadhalika wewe huwezi kumwombea mwenye dhambi aliyekufa, kwamba Bwana amtoe matesoni. Imani hiyo haipo pia katika biblia. Soma (Waebrania 9:27). Mafundisho ya watu kupitia toharani hayapo katika biblia.
Tujifunze kusoma biblia tutafunguka kwa mengi, mapokeo ya kidini sio Neno la Mungu. Hao wanaoabudu miti na mawe twaweza kuwacheka, lakini tukawa kama wale tu isipokuwa katika mfumo mwingine, tusipopenda kusoma biblia. Tukikataa kuwa wafuasi tu wa kidini tukapenda Neno la Mungu, Roho Mtakatifu atatusaidia kufunguka kwa mengi.
Hivyo ikiwa wewe ulikuwa ni mmojawapo wa wanaopeleka maombi kwa Rita wa kashia, au kwa mtakatifu mwingine yoyote acha sasa kufanya hivyo. Tubu dhambi ukabatizwe, upokee Roho Mtatakatifu ambaye atakuongoza na kukutia katika kweli yake yote(Yohana 16:13).
Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi waweza fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Mada Nyinginezo:
Novena ni nini? Na je ipo kibiblia?
Roho Mtakatifu ni nani?.
LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?
Kuomba katika roho ni kupi? na je nifanye nini ili niweze kuomba hivyo?
SISI TU MANUKATO YA KRISTO.
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.