SWALI: Je! mstari huu unaelewekaje? Mithali 9:17 “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”
JIBU: Mstari huo unamfunua mtu mwenye asili ya dhambi, jinsi vitu vilivyo kinyume na mapenzi ya Mungu vinavyoweza kupendeza mbele yake zaidi ya vile ambavyo ni sahihi kwake kuvifanya.
Kwamfano katika habari hiyo ukianzia vifungu vya juu utaona vinamweleza mwanamke kahaba, anavyowateka watu kuzini naye. Na mtu mjinga ataona ni sahihi kwenda kwake, lakini mwisho wake ni mbaya. Watu wengi wanaacha ndoa zao nakwenda kuzini nje! Kwasababu wanaona kile wanachokipata huko nje, kina uzuri kuliko kile walichokizoea ndani, wengine wanafanya uasherati, kwasababu wanaona wakingojea mpaka wakati wa ndoa, watakosa mambo mengi. Hao ndio wanaotembea katika usemi huo “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”
Wengine wanaona wakitumia njia ya udanganyifu, ndio zitawafikisha katika malengo yao kwa haraka, kuliko njia za halali, hivyo hujiingiza katika wizi, na magendo.
Lakini ukizidi kusoma mstari unaofuata anasema..
. Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.
Maana yake ni kuwa wote wafanyao mambo kama hayo, mwisho wao unakuwa ni kifo, na kuishia kuzimu kabisa. Dumu katika ndoa yako, kataa vya wengine, epuka mambo ya sirini. Yusufu hakukubali kuzini na mke wa boss wake. Lakini Daudi alidanganyika akazini na mke wa kijakazi wake, matokeo yake yakawa na yeye kunajisiwa wake zake vilevile, mtoto wake kufa, na ufalme wake kutikiswa na mwana wake mwenyewe aliyeitwa Absalomu, lakini zaidi sana kupoteza furaha ya wokovu kwa miaka mingi sana. Daudi alijutia makosa yake kwa muda mrefu sana.
Hivyo usipumbazwe na vivutio vyovyote vya dhambi vitakugharimu sana.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
Jicho ni nini (Yakobo 3:11)
NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Je ni lazima nibadili jina baada ya kuokoka, na kama ni hivyo ni mazingira gani yaliyo sahihi kufanya hivyo?
JIBU: Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo.
Unapookoka, ni vema kufahamu Kristo akishakukomboa umekombolewa kweli kweli, Huwezi kukosa mbingu kwasababu ya jina lako, hata kama lina maana mbaya, kwasababu wapo watu waliokuwa na majina mabaya, mmojawapo ni Yabesi ambaye jina lake lilimaanisha “huzuni”, kwasababu alizaliwa katika kipindi cha huzuni, na wazazi wake wakamwita hivyo lakini alimlingana na Mungu na Mungu akambariki na kumtukuza sana (1Nyakati 4:9-10).Lakini walikuwepo pia watu wenye majina mazuri mmojawapo Yuda, lakini tabia zake hazikuendana na jina lake.
Hivyo ikiwa jina lako si zuri sana, na huoni shida kuendelea nalo, huwezi kumkosa Mungu kwasababu ya hilo. Lakini pia, yapo mazingira ambayo, inampasa mkristo abadili jina endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo. Na mazingira yenyewe ni kama haya;
Kwahiyo hivyo ndio vigezo vya mtu kusukumwa abadili jina. Lakini usibadili kwasababu ya shinikizo la mtu, ikiwa huoni kikwazo chochote kuitwa jina hilo lako. Kwasababu wokovu wako, hauwezi kuzuiwa na jina. Hilo ulifahamu.
Bwana akubariki.
JINA LAKO NI LA NANI?
MAANA YA MAJINA NA TAFSIRI ZAKE.
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.
Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.
KWA WINGI WA WASHAURI HUJA WOKOVU.
UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;
SWALI: Nini maana ya Zaburi 125:3 “ Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu”.
JIBU: Mstari huo unatuonyesha jinsi Mungu anavyowatenga watu wake na adhabu ambazo zinawahusu waovu. Kwamba kamwe fimbo ya adhabu haiwezi kuwahusu watu wa Mungu, Ndio maana ya hilo neno ‘Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki;.. Ni mfano tu wa wana wa Israeli wakati ule walipokuwa Misri, Mungu aliwatenga na wamisri na kuwaweka kule Gosheni, na mpigo yote yalipokuja hayakuwakuta wana wa Israeli, bali wamisri tu. Hata baadaye alipotaka kuliadhibu taifa zima, bado aliwaficha watu wake ndani ya nyumba, na Yule malaika aliyeshushwa kuwauwa watu, hakupita katika nyumba zao. Kuonyesha kuwa fimbo za makosa Mungu hana desturi ya kuzijumuisha na watu wake, isipokuwa tu wamekataa wenyewe. Ndivyo ilivyokuwa kwa Nuhu, na Lutu.
Na anafanya hivyo kwasababu gani? Ndio hapo anasema ili “Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu”. Kwamba anawataadharisha watu wake wasidiriki kufanya makosa kama hayo hayo ya waovu kwasababu na wenyewe adhabu inaweza kuwakuta vilevile. Na kweli ndivyo ilivyokuwa kwa wana wa Israeli baadaye, walimwacha Mungu wakaanza kuitumikia miungu, na matokeo yake Mungu akawarudisha tena utumwani, na miji yao kubomolewa.
Hivyo, ni kutuonya kuwa sisi tuliokoka, kamwe tusijichanganye na maovu kwasababu adhabu ya makosa yaweza kutupata na sisi pia, kwasababu Mungu hatazami uso wa mwanadamu, bali ulekevu wako kwake.
Kwa maana nyingine ya mistari mbalimbali ya biblia tembelea website yetu hii >>> www.wingulamashahidi.org.
Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)
Miimo ni nini na kizingiti ni nini?
Tirshatha ni nini? (Ezra 2:63)
Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
Je Bwana Yesu aliruhusu wanafunzi wake kubeba Fimbo au hakuwaruhusu? (Marko 6:8 na Mathayo 10:10).
Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?
UTARATIBU WA KUTOA FUNGU LA 10 UPOJE?.
SWALI: Dhabibu za roho ni zipi, zinazotajwa kwenye maandiko haya?
1Petro 2:5 “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo”.
Dhabihu ni sadaka za kuteketezwa zilizokuwa zinatolewa katika agano la kale. Hizi zilikuwa na lengo la kufanya upatanisho wa makosa ya watu, kwamfano alipochinjwa mwanakondoo, au ng’ombe au mbuzi, au njiwa (Walawi 1:3-16) na kuteketezwa kisha ule moshi wake ukapanda juu basi huo ndio unakuwa uthibitisho wa sadaka yake kukubaliwa. Na mtu huyo makosa yake yanakuwa yamefunikwa kwa muda.
Hivyo katika agano jipya pia tunayo dhabihu yetu, ambayo kwa kupitia hiyo tunapokea upatanisho wa makosa yetu, na dhabihu yenyewe ni YESU KRISTO mwokozi wetu ambaye yeye kama mwanakondoo alichinjwa kwa ajili yetu ili sisi tupokee ondoleo la dhambi, hivyo yoyote ambaye yupo sasa ndani ya Kristo Yesu tayari ameshamtolea Mungu dhabihu ya upatanisho wake.
Lakini tunapokuwa ndani ya Kristo, hatuna budi kuonyesha kuwa tumekombolewa na yeye, kwa matendo yetu. Hivyo ni lazima tutaonyesha tabia kama za mtu anayekwenda kutoa dhabihu mbele za Bwana, na sio kama za mtu aliyejiamulia tu. Na tabia zenyewe ndio hizo zinazojulikana kama dhabihu za roho ambazo sisi tunazitoa.
Zifuatazo ndio dhabihu za roho zenyewe.
1) Shukrani
Zaburi 50:14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
Zaburi 50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
Ukiwa mtu wa shukrani kwa Mungu, Ni kuonyesha kuwa umetambua kazi ya msalaba ndani yako. Na shukrani hizi ni lazima ziwe katika Sifa za kinywa chako, pamoja na matoleo kwa kile Mungu anachokubariki. Ni muhimu sana wewe kama mkristo kuwa mtu na namna hii. Wote waliokwenda kutoa sadaka za namna hii mioyo yao ilijaa shukrani kwa Mungu wao, hawakwenda hivi hivi tu.
2) Moyo uliopondeka
Zaburi 51:16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. 17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Moyo uliopondeka ni moyo wa toba, wa majuto ya dhambi, ambao unakufanya utaabike moyoni mwako kwasababu ya makosa yaliyotendeka, na hivyo unakufanya uwe mnyenyekevu sana mbele za Mungu.
Mtu mwenye moyo huu, mbele za Mungu anaonekana kama amejitambua yeye ni mkosaji, na hivyo Yesu amefanyika upatanisho kwa ajili yake, tofauti na mtu ambaye mambo yote kwake ni sawa, hata baada ya kuona kosa bado anaukaza moyo wake, kujifanya kama hana hatia yoyote mbele za Mungu. Yatupasa wakati wote tuwe watu wa kujinyenyekeza mbele za Mungu. Watu wa kutaka rehema zake.
3) Kuitoa miili yetu;
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Unapoutunza mwili wako mbali na mambo ya kidunia, kisha ukaufanya utumike kwa ajili ya kazi ya Mungu, hapo ni sawa na unamtolea Mungu dhabihu yenye kupendeza, yaani unaenda mbele za Mungu na badiliko, unasema msalaba mbele, udunia nyuma. Lakini ukiwa unavaa ovyo ovyo, unazini, unatumia mikorogo, unajichora mwili wako, unakunywa pombe, unavuta sigara, unatoa mimba, hapo hufanyi ibada yoyote mbele za Mungu. Kwasababu lazima ufahamu kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Wakorintho 3:16).
Hivyo, wewe ambaye umeokoka, zangatia mambo hayo matatu, SHUKRANI, MOYO ULIOPONDEKA, NA KUUTOA MWILI WAKO. Wokovu wako utakuwa na maana sana mbele za Mungu.
Je! Umeshaokoka?. Kama bado wasubiri nini? Unatambua kuwa haya ni majira ya siku za mwisho, na Kristo amekaribia kurudi?. Dalili zote zimeshatimia, Embu tubu sasa mgeukie Kristo akuokoe uwe upande salama. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi waweza fungua hapa kwa ajili ya mwongozo was ala hiyo.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Dhabihu ni nini?
KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU.
Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?
Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?
Mnanaa, Bizari na Jira ni viungo gani? (Mathayo 23:23)
Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).
Kwanini samaki wasio na mapezi na magamba hawakuruhusiwa kuliwa?
SWALI: Nini maana ya Neno hili; Mithali 22:29 “Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo”.
JIBU: Neno la Mungu linatuonyesha kuwa ‘bidii’ humkweza mtu. Na bidii inayozungumziwa kibiblia ni zaidi ile inayodhaniwa kufanya tu kazi sana kwa muda mrefu, hapana, bali ni pamoja na kutumia ujuzi wako wote na ufanisi ili kutimiza kusudi ulilowekewa ndani ya muda. Watu wa namna hii mara nyingi huwa wanateka macho ya watu wenye vyeo au wakuu wa nchi.
Kwamfano Wafanyakazi wanaoonyesha ufanisi katika utendaji kazi, na kutimiza malengo ya shirika lao ndani ya wakati waliowekewa, huwa wanapendwa na ma-boss wao, na mara nyingi hupandishwa vyeo kama sio kupewa zawadi. Wagunduzi wa mipango ambayo inaleta mabadiliko chanya kwenye jamii, huwa wanaalikwa na viongozi wakubwa na maraisi kupongezwa na wakati mwingine kufanywa washauri wao.
Vivyo hivyo kiroho pia, ili tupate kibali kwa aliye Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana, zaidi ya wakuu wote duniani (yaani YESU KRISTO), hatuna budi kuwa na bidii katika kumtumikia yeye, na kuyafanya mapenzi yake.
Anasema,..
Kumbukumbu 28:1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, KWA BIDII, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
Umeona? Tusipokuwa walegevu, Bwana atatunyanyua juu sana tena sana kwasababu ni ahadi yake na haiwezi kutanguka..
Warumi 12:11 ‘kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;’
Hivyo, hakikisha, kile ulichopewa na Bwana unakitendea kazi, zaidi sana angalia ni kwa namna gani utakiweka ili kilete matokeo mazuri katika ufalme wa Bwana, usikifanye bila maarifa, hakikisha unatumia vyote yaani; nguvu zake zote, akili zako zote, roho yako yote, na moyo wako wote kwa pamoja bila kusahau kimoja wapo, ndani ya muda huu mchache uliopewa na Mungu hapa duniani. Na hakika kitakapochipuka kama Bwana alivyokusudia, Bwana atakutukuza sana.
Lakini ikiwa upo nje ya Kristo, tambua kuwa bado huwezi kumtumikia Bwana, na hata ukifa sasa ni moja kwa moja unaenda katika jehanamu ya moto. Kwanini usiyapange upya maisha yako leo kwa kufanya uamuzi wa busara wa kumkabidhi Kristo maisha yako?
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa sala.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?
TULITAFUTE KWA BIDII TUNDA LA ROHO.
HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kufundisha kanisani au kwenye semina.
Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kufundisha kanisani au katika ibada. Zifuatazo ni dondoo chache zitakazoweza kukusaidia katika kuandaa Somo ambalo litakuwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu.
1. Tafuta sehemu ya utulivu.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa: Tafuta eneo lisilo na kelele, wala usumbufu, hakikisha husumbuliwi na mtu au simu. Hiyo inaweza kuwa katika chumba cha utulivu au mahali ambao hauwezi kusumbuliwa, Huo ni mlango wa kwanza unaouvuta uwepo wa Mungu karibu nawe, kwasababu maandiko yanasema Mungu wetu si Mungu wa machafuko (1Wakorintho 14:33) na pia ni Mungu anayezungumza katika mazingira tulivu.
1Wafalme 19:12 “na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu”.
Hivyo kabla ya kuanza kufikiri kuandaa somo au hubiri, jitenge na mazingira yote yatakayokuondolea utulivu, kwasababu ukikaa katika hayo mazingira hutamsikia Mungu, Hivyo zima simu kwa muda na pia kaa peke yako kwenye utulivu.
2. Kuwa na Kalamu na Karatasi.
Hii ni hatua ya pili: Andaa kalamu na karatasi kwasababu kabla ya kwenda kuwafundisha wengine, Roho Mtakatifu atakufundisha wewe kwanza.
Warumi 2:21 “basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe”
Kwahiyo wewe ni mwanafunzi wa kwanza wa Roho Mtakatifu kabla ya kwenda kuwafundisha wengine, na Mwanafunzi bora ni sharti awe na kalamu na karatasi kwa lengo la kuyarekodi yale anayojifunza.
Usipokuwa na sehemu ya kurekodi yale utakayoenda kujifunza itakuwa ni ngumu hata kuyashika..
3. Fungua kwa Maombi.
Omba utakaso kwaajili ya nafsi yako, Omba uwepo wa Mungu ushuke mahali hapo, omba utakaso wa eneo ulilopo, omba roho ya ufunuo ishuke juu yako, kemea nguvu za giza na zinazoshindana na azimio lako hilo (Tumia muda kidogo kuomba kwa kumaanisha).
4. Anza kusoma biblia na kutafakari
Baada ya maombi, anza kusoma biblia huku ukiruhusu akili yako itafakari. Wengi wakifika hii hatua wanafungua tu biblia na kutafuta mistari wanayoifahamu au watakayokutana nayo kwanza, pasipo kuruhusu tafakari katika fahamu zao.
Siri moja ya Roho Mtakatifu ni kwamba anazungumza na sisi pale tunapotafakari na si pale tunapoziba tafakari zetu. Unapokuwa katika kutafakari ndipo Roho Mtakatifu naye anaungana na tafakari zako pasipo kujua na ghafla unajikuta unafunguka akili na kujikuta unapokea vitu vipya, ambavyo ulikuwa huvijui, vitu hivyo vipya ambavyo ulikuwa huvijui vinavyokubaliana na Neno la Mungu ndio sauti ya Roho Mtakatifu, hivyo andiko hivyo ulivyovipokea kwasababu ndio vitakuwa sehemu ya somo lako ambalo Roho Mtakatifu anataka ujifunze wewe kwanza kisha ukawafundishe na wengine.
5. Omba tena
Hii ni hatua ya mwisho, baada ya kusoma na kutafakari kwa muda mrefu, na kupokea Funuo nyingi. Omba maombi ya mwisho ya kushukuru, kisha funga daftari lako.
Darasa lijalo tutajifunza jinsi ya kusimama na kufundisha kile ulichofundishwa na Roho Mtakatifu. Kwani ni muhimu pia kujua jinsi ya kufundisha ili usije ukajikuta unamzimisha Roho. (Kanuni ya kufundisha kwa matokeo yaliyokusudiwa ni rahisi sana, usikose darasa lijalo).
Maran atha
JE! UPO KATIKA MAJI YA UTULIVU?
NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?
Wanikolai ni watu gani? Katika biblia?
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
Guruguru na Goromoe ni wanyama gani? (Walawi 11:30)
Mstari mfupi zaidi kwenye biblia ni upi? na umebeba ujumbe gani?
Mistari inatofautiana urefu kulingana na lugha na lugha.. Mstari unaoonekana mfupi katika lugha ya moja unapotafsiriwa katika lugha nyingine unaweza kuwa mrefu kuliko mistari mingine.
Kwamfano katika lugha ya kiingereza, mstari ulio mfupi kuliko yote unapatikana katika kitabu cha Yohana 11:35 unaosema kwa kiingereza “Jesus wept” Lakini tukiurudisha kwenye lugha Kiswahili unasomeka kama “Yesu akalia machozi”, Hivyo kuufanya mstari huo kutokuwa mfupi kuliko mingine katika lugha yetu.
Sasa mstari mfupi kuliko yote kwenye lugha ya Kiswahili ni upi? (Katika agano jipya).
Ni mstari unaopatikana katika kitabu cha 1Wathesalonike 5:20 unaosema “msitweze unabii”.
Huo ndio mstari mfupi kuliko yote, katika biblia ya Kiswahili, ( Agano jipya) Na ndio ujumbe mfupi kuliko yote aliouchagua Roho Mtakatifu kwa watu wanaozungumza lugha ya Kiswahili, kwamba “tusitweze unabii”, au kwa lugha rahisi “Tusidharau wala kupuuzia unabii”.
Na unabii unaozungumziwa hapo kwamba tusiudharau/ tusiutweze sio nabii zinazosikika sasahivi za wanaojiita manabii au wanaojulikana kama manabii, hapana! Bali Nabii zilizoandikwa kwenye biblia, mfano wa Nabii hizo ni zile Bwana Yesu alizozitaja katika Mathayo 24, zinazohusiana na kurudi kwake kwamba Nyakati kutatokea vita, njaa, manabii wa uongo, Tauni, matetemeko, upendo wa wengi kupoa n.k Hizo ndio nabii ambazo hatupaswi kuzipuuzia, kwa maana ni kweli zitatimia.
Kuzidi kufahamu kwa kina Zaidi maana ya kutotweza unabii fungua hapa >>Msitweze unabii
Je umempokea Yesu?.. Je unajua kwamba kizazi tunachoishi ni kizazi ambacho kina uwezekano wa kushuhudia ujio wa pili wa Yesu dhahiri??
Maran atha!.
Nini maana ya ELOHIMU?
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
NI YESU YUPI UMEMPOKEA?, NI ROHO IPI UMEIPOKEA? NA INJILI IPI UMEIPOKEA?
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema tutoapo unabii tutoe kwa kadiri ya imani?(Warumi 12:6)
JIBU: Neno hilo utalipata katika vifungu hivi;
Warumi 12:5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
Warumi 12:5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
Andiko hili linatuonyesha kuwa kila mmoja wetu amepewa KIPIMO cha neema, na hicho kipimo, kwa lugha nyingine ndio kinaitwa ‘Imani’ kama ilivyotumika hapo. Maana yake ni kuwa ikiwa ni nabii, basi kuna tofauti ya viwango vya kinabii, kwamfano wapo wengine wanapewa taarifa za watu tu, wapo wengine wanapewa za nyakati zijazo, wapo wengine za mataifa, wapo wengine wanapewa taarifa dhahiri kabisa za moja kwa moja, na wapo wengine kwa njia za mafumbo n.k.. Vyote hivi vinajulikana kama ndio vipimo vya imani.
Lakini sasa ikiwa mtu hajajaliwa kuona jambo Fulani, kisha akalazimishia alione,ili tu aonekane yeye ni mwonaji wa mambo yote, maana yake mtu huyo ni kuwa amevuka kiwango cha imani alichopimiwa na Mungu.
Na hivyo ataishia kutoa taarifa za uongo ambazo Mungu hajazisema. Kwamfano mtu ataona maono, kisha asiyaelewe, hata baada ya kuomba hajayaelewa, lakini kwasababu hataki kushirikisha wenye karama za Hekima na Maarifa na upambanuzi, atataka yeye ndio atafsiri alichoonyeshwa, hivyo anatumia akili zake, na matokeo yake inakuwa ni upotoshaji badala ya ujengaji.
Vivyo hivyo na katika karama nyingine. Utakutana na mtu sio mwalimu, hajajaliwa karama hiyo, lakini kwasababu na yeye anataka kujionyesha ni mjuaji anafahamu yote, ataanza kufundisha, na hatimaye kuwapotosha watu kwa mafundisho yake dhaifu.
Mitume japokuwa walijaliwa wingi wa karama na vipawa vya Roho lakini hawakuwa hivyo. Paulo anasema..
2Wakorintho 10:12 “Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili. 13 Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu. 14 Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo;
2Wakorintho 10:12 “Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.
13 Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu.
14 Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo;
Palepale ulipofikishwa na Bwana dumu hapo hapo, ikiwa Bwana atakuongezea neema basi itathibitika, lakini usijiongezee chochote, zaidi ya kile ulichopimiwa. Na hatari sana
Waefeso 4:7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
UPO UMUHIMU MKUBWA WA KUMTOLEA BWANA!
USIJISIFIE KARAMA KWA UONGO.
Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;
KUWA WEWE.
Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?
Swali: Ni hofu gani inazungumziwa katika Zaburi 4:4?
Jibu: Turejee,
Zaburi 4:4 “Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia, 5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana”.
Zaburi 4:4 “Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia,
5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana”.
Hapa maandiko yanasema “Mwe na hofu WALA msitende dhambi” haisemi “Mwe na hofu ILA msitende dhambi” Kana kwamba hiyo hofu ikizidi sana italeta madhara, hapana bali kinyume chake, inapaswa iwepo nyingi.
Sasa swali ni hofu gani hiyo inayozungumziwa hapo?
Hofu inayozungumziwa hapo si hofu ya kumwogopa mwanadamu, au kumhofu shetani, La! Bali ni hofu ya kumwogopa Mungu (Hofu ya Mungu), ambayo Daudi aliitaja pia katika Zaburi 36:1
Zaburi 36:1 “Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, HAKUNA HOFU YA MUNGU mbele ya macho yake”
Hofu ya Mungu ni ile hali ya mtu kuogopa kuyaasi maneno ya Mungu, hivyo mtu huyo anakuwa anajiweka katika hali ya kujitenga na dhambi siku zote za maisha yake yote. Lakini mtu asiye na hofu ya Mungu anaweza kufanya anayojisikia pasipo kujali kuwa anayoyafanya yanamchukiza Mungu.
Mfano wa watu ambao biblia imewataja hawakuwa na hofu ya Mungu, ni watu wa nchi ya Gerari, ile Ibrahimu aliyoikimbilia.
Mwanzo 20:9 “Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka. 10 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili? 11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini HAPANA HOFU YA MUNGU MAHALI HAPA, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”
Mwanzo 20:9 “Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.
10 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?
11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini HAPANA HOFU YA MUNGU MAHALI HAPA, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”
Na dunia tunayoishi sasa (mimi na wewe) ni Zaidi ya miji ya Gerari, ni Zaidi ya Sodoma na Gomora, Hofu ya Mungu haipo tena. Na biblia inaonya “tuwe na hofu”, na wala tusitende dhambi.
Je! hofu ya Mungu ipo ndani yako?.. kama hofu ya Mungu ipo ndani yako utaogopa kutenda mabaya, hivyo huwezi kuendelea na ulevi unaoufanya, huwezi kuendelea na rushwa unazokula, huwezi kuendelea na uasherani na uzinzi, huwezi kuendelea la mauaji na kutokusamehe.. ni lazima utajitenga na hayo yote, kwasababu hofu ya Mungu ipo ndani yako.
Bwana atusaidie.
Maran atha!
SIKU YA HOFU YANGU NITAKUTUMAINI WEWE.
BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.
Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).
YESU KATIKA USINGIZI WAKE.
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
SWALI: mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.(Mathayo 23:15)
Mathayo 23:15
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.
JIBU: Bwana Yesu anaanza Kwa kueleza bidii ya mafarisayo, kwamba ni hodari wa kuieneza dini zao kiasi cha kufanya umisheni wa kuzunguka hata sehemu za mbali nje ya taifa lao ili kuwafundisha watu mapokeo Yao. Lakini Bwana hawakemei Kwa bidii Yao hiyo ya kuzunguka huku na huko, Bali anawakemea Kwa Imani yanayoisambaza Kwa watu, ambayo ni potofu.
Imani ya kinafki, inayoacha kufundisha mambo ya adili kama (Imani katika Mungu, Upendo, kuja Kwa mwokozi duniani), Bali katika zaka na michango kama ndio tiketi ya kukubaliwa na Mungu (Mathayo 23:23)..
Na matokeo yake ni kwamba wale wanaogeuzwa Huwa wanakuwa na kiu ya dhati ya kusimama. Hivyo Kwa kuwa wanafundishwa uongo, basi wanafanyika kuwa Wana wa udanganyifu mara mbili zaidi ya Hao wenyewe.
Ndio hapo utamwona mtu kama Paulo, alipogeuzwa akawa chini ya elimu ya mafarisayo, lakini matokeo yake yalizidi hata wakufunzi wake wakina Gamalieli, alianza kuwauwa na kuwaburuta wakristo, na ndio ulivyokuwa Kwa watoto wao wote..walikuwa wabaya zaidi Yao, Wana wa jehanamu mara mbili zaidi ya wao.
Hata Leo angalia matokeo ya dini, madhehebu na Imani za uongo. Utagundua kuwa wale wafuasi wao ndio wanaokuwa wabaya zaidi ya wale viongozi,
Na ndio maana akawaambia hukumu Yao itakuwa kubwa zaidi ya wengine (Mathayo 23:14)
Nini maana ya “wanawake saba watamshika mtu mume mmoja”
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
Kuzimu kuna nini?
NI NANI ATAKAYEWAPA ILIYO YENU WENYEWE?
Jehanamu ni nini?
MJUE SANA YESU KRISTO.
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.