Swali: Napenda kujua tunampendaje Bwana Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, kwa roho zetu zote, kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote kulingana na Marko 12:30.
Jibu: Tuanze kusoma kuanzia mstari wa 28..
Marko 12:28 “Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? 29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; 30 nawe mpende Bwana Mungu wako KWA MOYO WAKO WOTE, na KWA ROHO YAKO YOTE, na KWA AKILI ZAKO ZOTE, na KWA NGUVU ZAKO ZOTE. 31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi”.
Marko 12:28 “Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako KWA MOYO WAKO WOTE, na KWA ROHO YAKO YOTE, na KWA AKILI ZAKO ZOTE, na KWA NGUVU ZAKO ZOTE.
31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi”.
Awali ya yote ni vizuri tukajua tofauti ya “OMBI” na “AMRI”. Ombi ni kitu ambacho unaombwa ukifanye, na endapo usipokifanya basi huwezi kuhesabiwa makosa, kwasababu ni Ombi, (lina uchaguzi wa kukubali au kukataa) lakini AMRI ni kitu ambacho mtu unaamriwa kukifanya (iwe unapenda au hupendi, ni sharti ukifanye), na endapo usipokifanya basi inakuwa ni kosa!.
Sasa hapo Bwana Yesu aliposema kuwa “AMRI” ya kwanza ni kumpenda Bwana Mungu kwa moyo wote, roho yote, akili zote na nguvu zote, Hiyo Ni AMRI na si OMBI. Maana yake mtu yeyote asiyempenda Bwana Mungu wake kwa viwango hivyo, basi mtu huyo kavunja amri ya Kwanza na ataenda kuhukumiwa!.
Ndio maana Mtume Paulo kwa uweza wa Roho aliandika maneno haya..1Wakorintho 16:22 “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha”.
Maana yake kutompenda Bwana ni laana kubwa!.. kwasababu ni kuvunja amri ya kwanza.
Sasa tukirudi kwenye swali letu, Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo wote, roho zote, akili zote na nguvu zote?
1.KWA MOYO WOTE
Kufanya kitu kwa moyo maana yake ni kukifanya kitu kwa hiari.. pasipo kuwa na mambo au mawazo mengine ya kando kando, kama malalamiko, manung’uniko, majivuno, au pasipo kusukumwa sukumwa.
Kwahiyo maana ya kumpenda Mungu kwa Moyo wote, maana yake ni kumpenda Mungu pasipo masharti.. Maana yake kama unamtolea Mungu zaka, au sadaka basi unamtolea kwa kupenda wewe mwenyewe,na si kwasababu umeshurutishwa au kwasababu biblia inasema tumtolee…hapana bali unamtolea kana kwamba hakuna sheria yoyote iliyokuambia ufanye hivyo..
Vile vile kama unamtumikia, katika kuhubiri, kumwimbia, kusaidia wengine n.k basi unapaswa umtumikia kwa moyo, kana kwamba hakuna sheria iliyokuambia ufanye hivyo…
Luka 17:10 “Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya”
2. KWA ROHO YOTE
Roho siku zote ni chumba cha IBADA… Na mtu anayefanya ibada kwa Mungu maana yake anamwabudu Mungu, kwasababu neno lenyewe “Ibada” limetokana na Neno “kuabudu”..
Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba KATIKA ROHO NA KWELI. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”.
Ukimpenda Bwana kwa Roho yote, maana yake kila wakati utatafakari na kutafuta kumfanyia Mungu ibada iliyo kamilifu… hutafanya ibada iliyo nje na Kweli ya Mungu.. Kila siku utahakiki ibada unayoifanya kama ni katika roho na katika Kweli ya Mungu (Neno la Mungu), na utaifanya hivyo kwa bidii sana. Hutamchanganya Mungu na sanamu!, wala hutamchanganya Mungu na matambiko ya kimila, wala hutakuwa vuguvugu katika Imani yako…utajituma kufika ibadani siku zote, utajituma kuomba siku zote na mambo yote ya kiibada yatakuwa ni mambo ya kwanza katika maisha yako.
3. KWA NGUVU ZAKO ZOTE.
Wakati wa kuwa na NGUVU ni wakati wa “Ujana”.. Hiki ndicho kipindi ambacho watu wote wanapaswa watie bidii katika kumtafuta Mungu.
1Yohana 2:14b “… Nimewaandikia ninyi, vijana, KWA SABABU MNA NGUVU, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”.
Wakati wa ujana ni wakati ambao roho zetu zinakuwa na uwezo mkubwa wa kutunza maneno ya Mungu, kuliko wakati wa uzee.. Kiasi kwamba mtu anayeyasoma maandiko katika ujana ni rahisi maandiko yale kukaa ndani yake kwa muda mrefu na kuzaa matunda zaidi ya mtu mzima (mzee), jambo ambalo shetani analiogopa sana!.. Ndio maana hapo maandiko yanasema.. “Nimewaandikia ninyi, vijana, KWA SABABU MNA NGUVU, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, NANYI MMEMSHINDA YULE MWOVU”.
Vile vile katika kitabu cha Mhubiri 12:1 maandiko yanasema “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.
Maana yake itafika kipindi (utakapokuwa mzee) utatamani Neno la Mungu likae na kudumu ndani yako lakini halitakaa na hivyo utakosa furaha, kwasababu Nguvu zako zitakuwa zimeisha.
Kwahiyo maana ya kumpenda Bwana kwa nguvu zote maana yake ni kumpenda BWANA katika ujana wako wote; unatumia muda mwingi katika kuomba maadamu unazo nguvu za mwili, vile vile unatumia muda mwingi katika kwenda kuhubiri maadamu unayo miguu yenye nguvu, pia unatumia muda mwingi katika kujifunza Neno la Mungu katika miaka ya ujana ambayo unazo nguvu katika roho za kuyatunza maneno ya Mungu.
Wengi wanasema nitamgeukia Mungu na kumtumikia nikiwa mzee.. kamwe usijaribu kuwaza hivyo!..biblia inasema kama unamkataa Mungu leo, utakapofikia uzee hutakuwa na Furaha wala Nguvu (Mhubiri 12:1).
Na pia Bwana Yesu alimwuliza Petro mara tatu, kama anampenda angali akiwa kijana..na akamwambia ukweli kuwa kama hatajishughulisha sasa katika kumtafuta yeye, na kumtumikia angali akiwa kijana, basi asitegemee ataweza akiwa mzee, kwasababu wakati wa uzee hatakuwa na hizo nguvu, bali atapelekwa huku na huko mahali asipopataka..
Yohana 21:15 “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, WEWE WANIPENDA KULIKO HAWA? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. 16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, WANIPENDA? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. 17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, WANIPENDA? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu. 18 Akasema, Amin, amin, nakuambia, WAKATI ULIPOKUWA KIJANA, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka
Yohana 21:15 “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, WEWE WANIPENDA KULIKO HAWA? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, WANIPENDA? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.
17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, WANIPENDA? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
18 Akasema, Amin, amin, nakuambia, WAKATI ULIPOKUWA KIJANA, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka
4. KWA AKILI ZAKO ZOTE.
Akili ni utashi wa kufanya mambo na kuyarahisisha yale yanayoonekana kuwa ni magumu… Kila mtu anazo akili za mwili alizojaliwa na Mungu, (Ingawa dhambi inaweza kumfanya mtu aonekane hana akili kabisa mbele za Mungu).
Hivyo kama umejiepusha na dhambi basi unazo akili, Hivyo katika hizo ulizopewa zitumie katika kumtumikia Mungu na kumtafuta.
Kwamfano katika dunia ya sasa, huwezi kusema utamtafuta Mungu halafu umkose, ikiwa umedhamiria kweli kumtafuta kwa akili zetu zote.. Yeye (Mungu) anasema tukimtafuta tutamwona (Yeremia 29:13).
Hebu tafakari Leo hii kuna simu nyingi feki kuliko orijino masokoni, lakini pamoja na kwamba feki ni nyingi mno kuliko orijino, lakini utaona kuna mtu anaitafuta orijino mpaka anaipata!.. Utaona anaulizia huku na huku, na kufanya uchunguzi huu na ule, mpaka anafikia kujua vimelea vya orijino na feki, na hatimaye anaipata iliyo orijino na kuiacha feki. (hapo ametumia akili zake zote kuitafuta simu orijino mpaka kaipata).
Lakini katika kumtafuta Mungu, utasikia mtu anakuambia “siku hizi manabii wa uongo wengi, sijui tumwamini yupi tumwache yupi” Hivyo anaamua tu!, kuacha kumtafuta Mungu, au kwenda kanisani..kwasababu tu manabii wa uongo wengi, au kwasababu tu, upotofu ni mwingi..
Mtu kama huyu hajaamua kutumia akili yake yote katika kumtafuta Mungu!! Ni mvivu wa akili.. kwasababu anao uwezo wa kutumia akili yake yote kutafuta simu orijino katikati ya feki, lakini si kuutafuta ukweli wa Mungu katikati ya uongo.
Lakini kama angeamua kutumia akili yake kidogo tu, na kuanza kuchambua hao wa uongo kupitia neno la Mungu, na kutafuta huku na huko, na kuulizia ulizia, na kutafiti tafiti, ni wazi kuwa siku moja angefika katika ukweli, na angewasaidia pia na wengine..
Lakini anadhani kwa yeye kutomtafuta Mungu siku ile atatoa udhuru mbele za Mungu, pasipo kujua kuwa anaivunja amri ya kwanza ya Mungu, ya kumpenda yeye kwa akili zote.
Ndugu Dada/Kaka.. Usipomtafuta Mungu sasa katika nyakati hizi, usipompenda kwa moyo wako wote na roho yako yote, na nguvu zako zote na akili zako zote, fahamu kuwa siku ya mwisho hutakuwa na udhuru, wala hakuna mwanadamu yoyote atakayekuwa na udhuru.
Bwana Yesu atusaidie tumpende yeye kwa vitu hivyo vinne kwa bidii sana.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
ILI TUONEKANE SAFI MBELE ZA MUNGU TUFANYE NINI?
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!
Rudi nyumbani
Print this post
Jibu: Tusome,
2 Wathesalonike 2:8 “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza KWA UFUNUO WA KUWAPO KWAKE”
Andiko hili linamhusu Mpinga Kristo ambaye maandiko yanasema katika siku ya mwisho Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kwa ufunuo wa kuwapo kwake (vitu hivyo viwili).
Sasa ufunuo wa kuwapo kwake unaozungumziwa hapo, sio ufunuo wa kuwepo kwa mpinga Kristo.. La! Bali sentensi hiyo inamaanisha kuwa mpinga-Kristo ataangamizwa kwa kule kudhihirishwa (au kufunuliwa) kwa Bwana Yesu katika utukufu wake, au kwa lugha nyingine rahisi ni kwamba ule Mwako wa utukufu Kristo atakaokuja nao, utamwangamiza mpinga Kristo. Hiyo ndio maana ya (ufunuo wa kuwapo kwake).
Sasa ni wakati gani ambapo Bwana Yesu atamwua kwa kinywa chake na kwa kufunuliwa kwake?.
Tusome Ufunuo 1:13-16
Ufunuo 1:13 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.12 NA MACHO YAKE YALIKUWA KAMA MWALI WA MOTO, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.15 NA UPANGA MKALI HUTOKA KINYWANJ MWAKE ILI AWAPIGE MATAIFA KWA HUO. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”.
Ufunuo 1:13 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 NA MACHO YAKE YALIKUWA KAMA MWALI WA MOTO, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 NA UPANGA MKALI HUTOKA KINYWANJ MWAKE ILI AWAPIGE MATAIFA KWA HUO. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”.
Umeona hapo?..
Kwa huo utukufu Bwana atakaokuja nao wa macho kama miali ya moto na upanga unaotoka katika kinywa chake (kwa mfano wa pumzi) hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kusimama mbele yake, akiwemo mpinga Kristo…kwasababu yeye (Bwana Yesu) ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
Je umeokoka?..kwa kutubu dhambi zako na kumaanisha kuziacha?. Kama bado unasubiri nini?..Huyu Yesu anayekuja leo kwako kwa sauti ya upole, fahamu kuwa hatakuwa hivyo siku zote..
Kuna wakati utafika atakuwa ni hakimu, na mhukumu, na atayapiga mataifa na kuyaadhibu.
Si jambo jema kuifikia hiyo siku, kwasababu ni siku ya hasira ya Mungu, ni heri tuyasalimishe maisha yetu kwake ili tuwe salama katika siku za mwisgo.
NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.
HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
USIISHIE TU KUPATA HAKI, BALI PATA NA WOKOVU.
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
Swali: Je kuna tofauti gani ya Mola na Mungu, na je sisi wakristo ni sahihi kutumia Jina Mola badala ya Mungu?
Jibu: Neno Mola, limeonekana mara kadhaa katika biblia…
Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, MOLA, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo”
Yuda 1:4 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake MOLA, na Bwana wetu Yesu Kristo”.
Ufunuo 6:10 “Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, EE MOLA, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi”.
Maana ya MOLA ni “Mungu-Mtawala”…
Neno ‘Mungu’ maana yake ni “Muumbaji”, yaani aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.. lakini jina Mola limeingia ndani zaidi, kumtaja Mungu kama Mtawala, Ni sawa na mtu anayesema “Mungu mwenyezi” badala ya “Mungu” au Mtu anayesema “Mungu mwenye Nguvu” badala ya “Mungu tu”. Mtu anayeomba kwa kumtaja Mungu pamoja na na sifa yake nyingine, hoja zake zinakuwa na Nguvu zaidi kuliko Yule anayetaja Mungu tu.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba, sisi wakristo ni sahihi kabisa kutumia neno Mola katika maombi yetu, kwasababu ni jina linaloelezea zaidi uweza wa Mungu, Ndio maana Wanafunzi walipokusanyika na kuomba baada ya Petro na Yohana kufunguliwa kutoka gerezani, maandiko yanasema pale walipokuwepo palitikiswa na wote wakajazwa Roho Mtakatifu na wakanena Neno la Mungu kwa ujasiri.
Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?………………..31 HATA WALIPOKWISHA KUMWOMBA MUNGU, MAHALI PALE WALIPOKUSANYIKA PAKATIKISWA, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”.
Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?………………..
31 HATA WALIPOKWISHA KUMWOMBA MUNGU, MAHALI PALE WALIPOKUSANYIKA PAKATIKISWA, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”.
Bwana Yesu akubariki.
MILANGO YA KUZIMU.
USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.
Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?
Mithali 17:12 “Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake”.
Mpumbavu kibiblia ni mtu yeyote ambaye amekataa sheria ya Mungu na Maarifa. Yaani kwa ufupi mtu asiyetaka kumjua Mungu wake ni mpumbavu. Mtu wa namna hii hatabiriki, kwasababu shetani ndiye anayekuwa bwana na kiongozi wa Maisha yake, sio Yesu..
Kwamfano Mithali 10:23 inasema..
“Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima”.
Sasa hapo biblia inaposema ni heri ukutane na dubu aliyenyang’wanya Watoto..inatupa picha jinsi gani mpumbavu alivyo hatari kuliko hata mnyama mkali dubu. Kwa kawaida dubu si mnyama mpole, na tena ukali wake unazidi pale anapokuwa na Watoto, lakini ukali huo unavuka mipaka pale anaponyang’anywa Watoto wake,Utakumbuka kile kisa cha Elisha kuwalaani wale vijana..biblia inasema arobaini na wawili kati yao waliraruliwa na dubu wawili tu jike.
Kutupa picha jinsi gani walivyohatari Wanyama hawa.. Lakini biblia inasema heri ukutane nao kuliko mpumbavu. Mfano wa wapumbavu katika biblia ni Herode, ambaye kwa wivu wake aliwaua watoto wote, waliokuwa Yerusalemu kipindi cha kuzaliwa kwa Bwana Yesu, kama hiyo haitoshi alimuua na Yohana mbatizaji, Pamoja na Yakobo mtume wake Bwana.
Wapumbavu ndio wale wale waandishi na mafarisayo, ambao walikuwa wanazunguka huku na huko , na kuwafanya watu kuwa waongofu wapya wa dini zao, na mwisho kuwafanya wana wa jehanamu mara mbili kuliko wao.(Mathayo 23:15).
Wapumbavu ndio manabii wa uongo walio sasa, ambao wanawatumainisha watu kuwa Mungu anawapenda wakiwa na mali au mafanikio, lakini hawakemei dhambi, na matokeo yake wengi wanakufa na kujikuta kuzimu, kwasababu walidanganywa na hila zao.
Vilevile Mpumbavu ndio mpinga-kristo atakaye kuja, ambaye ataundanganya ulimwengu mzima waipokee chapa yake, na hiyo itapelekea jopo kubwa sana la watu kufuatana naye kuzimu..Sasa biblia inasema ni heri ukutane na dubu aliyenyang’anywa Watoto wake, ambaye atakurarua tu mwili wako , baada ya hapo hawezi kukuathiri zaidi, lakini hawa, wanakurarua hadi na roho yako, kwa kukupeleka kuzimu.
Ndio maana Bwana alisema tujiepushe naosana..
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Soma NENO, dumu katika hilo, ndio salama yako nyakati hizi.. kwasababu tunaishi katika kipindi cha hatari sana. Ukiwa mvivu, utakwenda na maji yao.(Mathayo 24:24)
Bwana atusaidie..
Shalom.
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU.
Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 22:2
[2]Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.
JIBU: Pamoja na kwamba kutakuwa na kutokuelewana baina ya makundi haya ya watu..Maskini atamwonea wivu tajiri, na tajiri atamdharau maskini..Lakini katika hayo yote bado tu kila mmoja atamhitaji mwenzake…atakutana na mwenzake mahali fulani tu katika maisha..
Maskini atamfuata tajiri ampe kazi, vilevile tajiri atamtegemea maskini amwoshee gari lake, amfulie nguo zake, amlimie bustani yake.n.k Hivyo kila mahali uendapo makundi yote utayapata .. Na sababu tayari biblia imeshaitoa..”Kwamba Bwana ndiye aliyewaumba wote wawili”Akawaweka hapa duniani..wala mmoja hakumweka mawinguni, mwingine ardhini.
Hii ni kufunua kuwa tumewekwa kusaidiana, wala hakuna mtu anaweza kujikidhi yeye mwenyewe kwa kile alichonacho pasipo mwingine..zaidi sana yule ambaye unamwona hakufai ndiye atakayekufaa sana wakati fulani. Kwasababu ni Mungu ndiye aliyetuumba sote, mmoja hakuumbwa na shetani, na mwingine Mungu.
Hivyo hekima inatufundisha tukae kwa utulivu, tuthaminiane sisi kwa sisi
KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri.
Vyombo vya uzuri ni vipi vinavyotajwa katika biblia?
Swali: Katika 1Petro 2:13 Tumeambiwa tutii kila kitu tunachoamriwa na wafalme, lakini katika Matendo 5:29, tunaona Petro huyo huyo hawatii wenye mamlaka, anasema imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu..Je hapo panakaaje?
Jibu:Tusome
1 Petro 2:13 “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;14 ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema”
1 Petro 2:13 “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;
14 ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema”
Tusome tena…
Matendo 5:29 “Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”.
Ni kweli tumeamriwa kutii mambo yote, lakini si hata yale yasiyofaa. Kwamfano inatokea mkuu wa nchi au mwenye mamlaka anatoa amri ya watu kuabudu kitu fulani ambacho si Mungu wa mbingu na nchi (yaani Yehova).. Hapo hatuwezi kumtii, kwasababu kavuka mipaka, au mkuu anatoa amri hakuna kuhubiri injili, au kuomba au kufunga, hapo tumepewa ruhusa ya kutotii maagizo yake hayo.
Lakini mambo mengine, ambayo hayaathiri imani yetu, hayo hatuna budi kutii..
Kwamfano sheria imetolewa na wakuu wa nchi kuwa siku fulani itakuwa ni siku ya usafi nchi nzima, kwamba watu wote watoke wafanye usafi, hapo hatuna budi kutii, kwasababu jambo hilo haliathiri imani yetu, na zaidi sana litatuongezea ushuhuda mzuri katika jamii na linafaa kwa afya zetu. Na sheria nyingine zote mfano wa hizo, hatuna budi kuzitii.
Lakini ikitoka sheria ya kutukataza kumwabudu Mungu, au sheria ya kutulazimisha kufanya mabaya, sheria hiyo tumepewa ruhusa ya kuivunja, na tukawa hatujafanya dhambi, bali kinyume chake tukawa tumempendeza Mungu.
Ndio maana Petro ijapokuwa alilihubiri suala hilo la kuwatii wenye mamlaka, (Katika hiyo 1Petro 2:13) lakini ilipofika wakati hao wenye mamlaka walipowakataza wasihubiri habari njema za ufalme wa mbinguni… Petro na Yohana hawakukubaliana na hiyo sheria..ndipo wakasema imewapasa kumtii Mungu kuliko wanadamu, wakisaidiwa na Malaika wa Mungu.
Matendo ya Mitume 5:18 “wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.25 Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu.26 Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.27 Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”.
Matendo ya Mitume 5:18 “wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema
20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.
21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
25 Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu.
26 Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.
27 Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,
28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.
29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”.
Na sio tu kwa wafalme na wenye mamlaka, tuliopewa ruhusa ya kuvunja amri zao zilizozidi mipaka, bali hata katika familia..endapo Mume katoa sheria ya mke au watoto kuabudu miungu, hapo tumepewa ruhusa ya kutomtii mzazi huyo au mume kwa agizo hilo..Kwasababu ni agizo lililovuka mipaka..
Mathayo 10:37 “Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili”.
Lakini mume akitoa amri au sheria ambazo haziathiri imani zetu, hizo hatuna budi kuzitii, mfano mzazi anatoa amri ya kufanya shughuli fulani ya nyumbani iliyo halali hapo hatuna budi kutii hata kama hatutaki..
Kwahiyo kwa ufupi tumepewa amri ya kutii yote yaliyo mema lakini hatujapewa amri ya kutii mambo mabaya. Lakini yote hatuna budi kuyafanya kwa hekima.
Bwana atusaidie.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312.
JE NI KUTII AU KUPATA KWANZA MAARIFA?
KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13).
MIMI NI ALFA NA OMEGA.
SWALI: Je! maneno tunayoyasoma katika Mhubiri 7:24, yana maana gani?
[24]Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana, ni mtu yupi awezaye kuyatafuta?
JIBU: Hapo Kuna vitu viwili..
1) Yale yaliyo mbali.
2) Yale yaendayo chini sana.
Akimaanisha yaendayo mbali na upeo wa mwanadamu..na hayo si mengine zaidi ya mambo ya mbinguni, na kuzimu na ya maisha baada ya hapa..yatakuwa na mwonekano gani..picha yake halisi ipoje, miaka bilioni moja kutoka sasa watakatifu watakuwa wanafanya nini?..Hayo hakuna mtu anayeweza kuyavumbua isipokuwa Mungu tu peke yake.
Na yale yaendayo chini sana, maana yake ni yale yaliyositirika kama madini n.k. ambayo yenyewe yanapatikana chini sana. Hivyo vitu vilivyositirika/ siri za Mungu, ni mwanadamu gani anaweza kuzivumbua..
Kwamfano Siku ya unyakuo itakuwa lini, kabla ya uumbaji Mungu alikuwa anafanya nini, maji yanajaaje kwenye mawingu, yaliyo hewa tu, halafu baadaye yanamwagika chini kama mvua, mifupa unajiumbaje ndani ya tumbo la mama mjamzito, mapigo ya moyo yanadundishwa kwa nishati gani, mpaka hayachoki n.k Siri hizo anazo Mungu tu hakuna awezaye kuzivumbua..
Ayubu 11:7 inasema..
[7]Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?
Soma Kitabu cha Ayubu kuanzia sura ya 38-41, utaona Mungu anamuuliza mwanadamu maswali magumu ambayo mpaka sasa hakuna hata moja lililopatiwa jibu lake.
Hiyo ndio maana ya huo mstari;
Mhubiri 7:24
Yatosha sisi kumwamini yeye na kulitii Neno lake tu. Kwasababu hata tukijitahidi vipi kwa akili zetu kamwe hatutaweza kuzivumbua siri za ndani za Mungu wetu, isipokuwa yeye mwenyewe atufunulie.
Jina lake BWANA lihimidiwe. milele na milele. Amen.
Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.
MUME / MKE BORA KUTOKA KWA BWANA UTAMWONA UKIWA KATIKA MAZINGIRA GANI?
nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO
Nini maana ya ugonjwa wa kufisha? (Yeremia 17:9)
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze na kuyatafakari maandiko pamoja.
Leo napenda tujifunze juu ya lile tukio maarufu lililotokea siku ile ya Pentekoste, ambapo tunasoma Roho Mtakatifu alishuka juu ya Wanafunzi wa Bwana Yesu 11, pamoja na wanafunzi wengine wengi, jumla yao ni watu 120 (Matendo 1:15).
Ilipotimia siku ya Pentekoste tunasoma kuwa Watu wote walishukiwa na “Ndimi zilizogawanyikana kama ndimi za moto”.
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao”
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao”
Napenda tuyafakari hayo maneno kabla hatujaendelea mbele.
Neno la Kwanza ni “Ndimi”.. Ndimi ni wingi wa neno “ulimi”, Na mtu anapozungumzia Ulimi, anamaanisha “lugha”... Kwamfano tukitaafsiri neno “lugha mama” kwenda kwenye lugha ya kiingereza itakuwa ni “Mother tongue” na tafsiri ya “tongue” kwa Kiswahili ni “ulimi”.. Hivyo badala ya kusema “lugha mama” pia ni sahihi kusema “ulimi mama” (ni kitu kimoja).
Kwahiyo hapo biblia iliposema kuwa zilitokea “ndimi za moto” ilimaanisha kuwa ni “lugha za moto”.. Lakini haiishi hapo, biblia inaendelea kusema kuwa “zilikuwa ni ndimi zilizogawanyikana” maana yake ni kuwa zilikuwa ni “lugha zilizogawanyikana/tofautitofauti”.. kila mmoja alishukiwa na lugha yake tofauti na ya mwenzake.. Na lugha hizo hazikuwa za kimbinguni, bali za duniani kama vile Kiswahili, kiarabu, kihindi, kichina, kisukuma n.k
Matendo 2:4 “Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, 11 Wakrete na Waarabu; TUNAWASIKIA HAWA WAKISEMA KWA LUGHA ZETU MATENDO MAKUU YA MUNGU. 12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
Matendo 2:4 “Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.
6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?
8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,
11 Wakrete na Waarabu; TUNAWASIKIA HAWA WAKISEMA KWA LUGHA ZETU MATENDO MAKUU YA MUNGU.
12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
Mstari wa 11, biblia inasema… “TUNAWASIKIA HAWA WAKISEMA KWA LUGHA ZETU MATENDO MAKUU YA MUNGU”.
Kumbe Wanafunzi hawa waliojazwa Roho Mtakatifu, walikuwa wananena matendo makuu ya Mungu.. Kumbe walisikika wakiyatangaza matendo makuu ya Mungu, na si mambo mengine..
Sasa mfano wa matendo hayo ni yapi?
Ndio kama yale ya Mungu kupasua bahari na wana wa Israeli kupita salama, ndio kama yale ya Mana kushushwa kutoka mbinguni kwa miaka 40, ndio kama yale ya Bwana kuziangusha kuta za Yeriko, ndio kama yale ya Eliya kushusha moto n.k n.K (Hayo ndio matendo ambayo mitume walisikika wakiyatangaza kwa lugha nyingine)…Na watu waliposikia wakikumbushwa matendo makuu hayo ya Mungu, tena kwa lugha za ndani kabisa..mioyo yao iliwaka, kutaka kumrudia Mungu na kutaka kujua zaidi.
Hebu tengeneza picha unamwona mzungu aliyetoka Ulaya anazungumza lugha yako ya kikabila tena ile ya ndani kabisa, ambayo hata wewe pengine huipati vizuri, na ukizingatia yeye ni mgeni kabisa, na hajawahi kufika huko kijijini kwenu.. halafu maneno anayoyasema ni ya kumtukuza Mungu, kwa matendo makuu aliyoyafanya katika biblia.
Bila shaka utaduwaa na kushangaa!! Na kujiuliza maswali mengi, na jibu la mwisho utakalolipata ni kusema “huu ni muujiza” na zaidi sana hata kile mzungu huyo anachokisema kitakuja kwa uzito kwako, tofauti na kama angeongea kwa lugha yake ile ile ya kiingereza.
Ndicho kilichotokea siku ya Pentekoste, wanafunzi walisikika wakimtangaza Mungu kwa lugha mbalimbali, hivyo watu wakashangaa na kutenga muda kuwasikiliza, na siku hiyo wakaongezeka waongofu elfu 3.
Na sisi hatuna budi wakati mwingine, tuzungumze kwa lugha nyingine.. Kuzungumza kwa lugha nyingine si lazima kuwe kwa lugha ambayo huijui!, hapana! Hata kwa lugha yako hiyo hiyo lakini Bwana aibadilishe itoke kwa namna nyingine, ambayo italeta mageuzi kwa wale watakaokusikiliza.
Na si lazima kuwe kunena tu, bali hata KUIMBA, Bwana akabadilishe lugha na sauti yako iwe na uvuvio wa Roho ambao utawabadilisha watu wasikiao, na si katika kuimba tu, bali hata katika KUOMBA!. Bwana akabadili lugha yako, na kuwa lugha nyingine kusudi maombi yakolee munyu, mbele zake.
1Wakorintho 14:15 “Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia”.
Na si katika kuomba, na kuimba tu, bali hata katika MAISHA YETU YA KAWAIDA YA MAZUNGUMZO. Lugha zetu zinapaswa zibadilishwe.
Tukiwa watu wa lugha mbaya, maandiko yanasema tunaziharibu tabia zetu njema !(1Wakorintho 15:33). Na lugha mbaya ndizo zinazotukosesha kibali, lakini kauli mbaya huuwasha moto (Yakobo 3:6).
Siku ya leo ni siku ya kuomba BWANA AIBADILISHE LUGHA YAKO..Na kuwa lugha nyingine ya kuwafaa watu na kufaa mbele za Mungu.
Ikiwa bado hujaokoka, Bwana Yesu hawezi kuibadilisha lugha yako.. lakini leo hii ukiamua kumpokea Yesu maishani mwako kwa kumaanisha kabisa kwa dhati, basi Bwana atakupa lugha mpya.. Na hivyo utakuwa mtu mwingine wa kuzaa matunda siku zote..
Basi ikiwa umeshampokea Yesu, au leo hii umeshafanya maamuzi ya kumpokea Yesu na kutubu dhambi zako, basi pata muda jitenge binafsi mahali pa utulivu, na kisha piga magoti kwa utulivu na uombe na mwombe Bwana akupe kipawa hicho cha lugha mpya, naye ni mwaminifu atakupa, na tangu siku hiyo utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako..
Bwana akubariki.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
NYAKATI AMBAZO NI LAZIMA TUKUTANE NAZO TU.
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ni wasaa mwingine tena Bwana ametupa neema ya kuutafuta uso wake. Karibu tujifunze Neno la Mungu.
Lipo funzo kubwa sana Bwana anatufundisha nyuma ya wale malaika wake wawili aliowatuma sodoma kwa ajili ya kuuangamiza ule mji. Habari tunaifahamu, hakuna haja ya kulitazama tukio lote, lakini tutatazama huduma yao ya mwisho ambayo waliifanya kwa familia ya Lutu.. Hiyo itatufanya na sisi leo hii tuwe makini sana na hii neema ya Mungu tuliyopewa kwa kitambo.
Malaika wale walipomwambia Lutu atoke sodoma, maandiko yanasema, Lutu akawa ‘anakawia kawia’,..Hata baada ya “kuhimizwa sana” bado akawa anakawia kawia..hapo ndipo ikabidi wale malaika wachukue jukumu wenyewe la kuwatoa kwa nguvu sodoma, kana kwamba ndio wao wenye shida. Tusome;
Mwanzo 19:15 Hata alfajiri ndipo malaika WAKAMHIMIZA LUTU, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. 16 AKAKAWIA-KAWIA; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana ALIVYOMHURUMIA, wakamtoa wakamweka nje ya mji..
Biblia inatuambia Kwa jinsi Mungu ‘alivyomhurumia’ Lutu na familia yake, ikampelekea amtoe kwa nguvu kama katoto kanacholazimishwa kupelekwa shuleni kwa kubembelezwa.. Hivyo waliendelea kuvutwa kwa umbali mrefu kidogo.. Lutu na mke wake wakashikwa na malaika mmoja, halikadhalika mabinti zake wawili wakashikwa na malaika mwingine.. Wakati wanatembea Walikuwa wanaweza kuangalia nyuma kama watakavyo na wasiambiwe kitu. Pengine walifika mahali wakawa wanasema tumechoka, wanabembelezwa watembee tu hivyo hivyo, wanafarijiwa, wanatiwa nguvu, Kwani jukumu la wao kuokolewa halikuwa katika uwezo wa mikono yao, bali wa wale malaika wawili.
Lakini hali hiyo haikuendelea sana… biblia inatuambia, walipofika nje tu kidogo ya mji..Wakaachwa, na kuambiwa zamu hii, sasa kipengele kilichobakia ni juu yao wenyewe..sisi tumemaliza kazi yetu.
Mwanzo 19:17 “Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea”.
Ndipo safari ya kukimbia, ikaanza..Lakini mkewe lutu, akidhani wakati huu ni kama ule wa mwanzo akageuka nyuma akidhani watakuwepo malaika tena wa kumshika mkono,na kumvuta vuta, na kumbembeleza bembeleza kama mwanzoni.. saa ile ile akageuka kuwa jiwe la chumvi.
Maana yake ni nini?
Saa tunayoishi ni wakati ambao sio tena kubembelezewa wokovu kama ilivyokuwa miaka ya kale.. Bali tunaishi ukingoni sana mwa neema ya wokovu. Wakati ambapo tunapaswa tujiokoe nafsi zetu na huu ulimwengu mbovu unaokaribia kuisha.. Pengine utasema umejuaje tupo katika zama hizo za kujiokoa nafsi zetu wenyewe, zama za kukimbia bila kuangalia nyuma, na sio za kuvutwa na Mungu? ,..Ni kutokana na kauli ya Bwana Yesu mwenyewe aliyoisema katika vifungu hivi;
Luka 17:32 “Mkumbukeni mkewe Lutu. 33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya”.
Maana yake ni kuwa hakuna kusubiria tena, Mungu akuambie hivi, au akuambie vile, au akufanyie hiki kwanza au kile.. Tayari alishasema na wewe kwamba usiangalie nyuma, kuna kuna kuwa jiwe la chumvi..jiokoe nafsi yako. Hivyo unapokuwa mkristo vuguvugu, unakapokuwa mkristo-jina, ujue upo hatarini sana wakati huu.. unyakuo ukipita leo au ukifa katika hali hiyo usidhani kwamba utakuwa na nafasi ya pili.
Mlango wa neema unakaribia kufungwa kwa watu wa mataifa, na hivi karibuni Yesu anarudi, dalili zote zinaonyesha huwenda kizazi tunachoishi tutayashuhudia yote. Sasa ya nini kuendelea kuufanyia mzaha wokovu,..Yanini kuendelea kuupenda ulimwengu? Ya nini kushikamana na mambo ya sodoma kama mke wa Lutu…
Usipoupokea wokovu wa kweli leo, ujue kesho itakuwa ngumu sana kwako, kuliko siku moja nyuma. Kwasababu neema ya Mungu haidumu milele kwa mwenye dhambi..litambue hilo!
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.29 Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu”.
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
29 Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu”.
Isikize sauti ya Mungu..ikuambiayo jiokoe nafsi yako, mkumbuke mke wa Lutu.
Nyakati zetu ni za hatari sana kuliko nyakati za kale.
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
USITAZAME NYUMA!
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Ni SIRI gani Paulo aliyokuwa anaimaanisha katika Waefeso 5:32?
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
Sefania 3:8 “Basi ningojeni, asema Bwana, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu”.
Majira yaliyopo mbele yetu, si rafiki kabisa ndugu yangu, bali ni majira ya vita. Fahamu kuwa hii dunia haitaisha katika amani..Vipo vita vikubwa na vibaya vinavyokuja mbele yetu… Hilo haliepukiki kwasababu biblia ilishatabiri. Na sasa zipo vita kuu mbili(2), ambazo zitapiganwa kinyume na Mungu kabla ya huu ulimwengu kuisha..
Tukisema ‘kinyume na Mungu’ Tunamaanisha kinyume na Israeli, kwasababu Mungu yupo katika taifa lake Israeli..Ndilo taifa pekee Mungu aliloliunda kwa lengo la kuyabariki mataifa na pia kwa lengo la kuyakomesha mataifa.
Vita ya kwanza itakuwa ni ile tunayoisoma katika kitabu cha Ezekieli 38&40, Hii itapiganwa kipindi kifupi sana kabla ya unyakuo, au kipindi kifupi sana baada ya unyakuo. Kwaufupi ni kwamba taifa hili la Urusi, ndilo litakalosimama kama kichwa cha vita hiyo, likiyaongoza na mataifa mengine machache ya kando kando ,lakini litapigwa na habari yao itakuwa imeishia hapo. Ikiwa utataka kupata maelezo zaidi kuhusiana na vita hii tutumie ujumbe inbox (+255693036618 / +255789001312), tukutumie somo lake.
Lakini vita nyingine, ni vita ijulikanayo kama vita ya Harmagedoni.. Hii haitakuwa tena ya mataifa machache tu..Hapana, bali itahusisha mataifa yote duniani. Yataungana, yakiwa na lengo moja la kuifuta Israeli katika uso wa dunia..Na sababu ambayo itapelekea ni kwamba Mungu ataitumia Israeli, kuyaudhi mataifa haya..aidha kwa kupitia manabii atakaowanyanyua, au kwa kupitia watawala watakaokuwepo. Na itapiganwa mwishoni kabisa mwa ulimwengu.
Zekaria 12:2 “Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.
3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake”.
Hata taifa lako unaloishi wewe litahusika wakati huo, watakuwa wamejiandaa na mabomu yao ya nyuklia na majeshi, ili kwenda kuisambaratisha nchi ile ndogo. Wakati huo Israeli wakiwa wanyonge, na wamezingirwa na majeshi, Ndipo Kristo mkombozi wao atakapotokea mawinguni. Na atashuka katika ule mlima wa Mizeituni, na kuanzia hapo, atafanya vita ya kuyateketeza mataifa yote ulimwenguni..halitasalia hata moja litakalokosa kunywa kikombe hicho cha ghadhabu ya Mungu.
Pitia kwa utulivu maandiko haya;
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake”.
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake”.
Pitia tena hili andiko, uone Kristo atakavyoshuka juu ya mlima wa mizeituni na kuanza maangamizi kwa watu waovu.
Zekaria 14:2 “Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.3 Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.
Zekaria 14:2 “Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.
3 Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.
4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.
Hapa ndipo utakapokuwa mwisho wa mataifa yote ulimwenguni.
Leo hii umeshaanza kuona ni jinsi gani, dunia inavyopata shida kwa taifa la Israeli?. Taifa hili kwasasa lina maadui wengi kuliko marafiki, limeshaonekana kama taifa asi la dunia. Na hapo Bwana hajalirudia taifa hili. Utafika wakati, hii neema itaisha kwetu sisi mataifa, ndipo watakapogeukiwa wao, na watatubu, kwa makosa waliyoyafanya ya kumsulubisha Bwana wao..
Soma..
Zekaria 12:9 “Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; NAO WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Ndugu, Wakati huu upo karibuni kutokea.. Je! Umejipangaje/Tumejipangaje? Neema ndio tunaiaga hivyo? Inawarudia wayahudi, ilipoanzia.. kama wewe unasubiri kila siku kupigiwa kelele za injili utubu..Fahamu kuwa zama hizo zimeshaisha..jicho la Mungu linaanza kurudi Israeli sasa.. Na siku sio nyingi, UNYAKUO, utapita, watakaobakia ndio watakaoshuhudia hayo yote. Lakini tuliokoka tutakuwa mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo.
Tubu leo mpe Yesu maisha yako, ukabatizwe katika ubatizo sahihi, na kupokea Roho Mtakatifu. Huu Ulimwengu si rafiki, yasalimishe maisha yako kwa Bwana.
Maran Atha.
WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZEA.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
HATARI! HATARI! HATARI!