Jina la Bwana YESU KRISTO, aliye Mkuu wa mbingu na nchi libarikiwe.
Maandiko yanasema..
2 Wakorintho 5:6 “Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. 7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
2 Wakorintho 5:6 “Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.
7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
Leo tujifunze nini maana ya “tunaenenda kwa Imani na si kwa kuona”.
Wengi wetu tunadhani kuona kwa macho ndio njia pekee ya kulithibitisha jambo, lakini kiuhalisia kuona sio njia pekee ya kuthibitisha jambo, hata hivyo ni moja ya njia hafifu sana.
Kwa mfano macho hayawezi kupambanua ubwabwa wenye chumvi na ule usio na chumvi, maana yake huwezi kutazama ubwabwa na kujua ule umewekwa chumvi au la!. Macho yatapambanua tu aina ya chakula kilichopo mbele yako, kwamba ule ni ubwabwa na si ugali lakini hayawezi kufanya kitu kingine zaidi ya hicho.
Lakini ulimi unaweza kupambanua vyote, ubwabwa ukiwekwa kinywani ulimi unaweza kupambanua kuwa ule ni ubwabwa na si ugali, vile vile unaweza kupambanua kuwa ubwabwa ule umewekwa chumvi au la!.
Kwahiyo kuona si njia kamilifu ya kuthibitisha jambo.
Na katika mambo ya rohoni ni hivyo hivyo, maandiko yanasema “hatwenendi kwa kuona bali kwa Imani”.
Macho yetu hayana uwezo kamilifu wa kupambanua mambo ya rohoni. Ndio maana leo hii Bwana hajaruhusu tuujue uso wake, au tuwe tunamwona, ndipo tumthibitishe kwamba yupo, au tuweze kumsikia na kumwelewa.
Ni kwasababu hata tukimwona bado hatutamjua, kama vile macho yalivyo na uwezo wa kuona jambo lakini si kuonja jambo. Vivyo hivyo hata leo hii katika maisha haya tukimwona Bwana kwa macho, haitatusaidia sana, zaidi ya kumwona kwa Imani.
Leo hii watu wengi sana wanatafuta kumwona Bwana katika mwili, wengi wanafunga na kuomba Bwana Yesu awatokee kwa namna ya kimwili, wamwone na kuzungumza naye.
(Hata mimi nilishawahi kufanya hivyo, nilifunga na kuomba Bwana anitokee na kusema nami, niliendelea hivyo kwa muda mrefu mpaka Bwana aliponipa ufahamu, na kujua kuwa maombi niombayo sio ya kishujaa bali ni ya kitoto.
Kwamba sio ushujaa kutokewa na Bwana na kuzungumza naye bali ni utoto na uchanga..na wlaa.hakitaniongezea chochote kiroho. Tomaso alitafuta kumwona Bwana kwa namna ya mwili baada ya kufufuka kwake, lakini baada ya kutokewa alidhani atasifiwa na Bwana, lakini hakusifiwa.
Yohana 20:29 “Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona,wakasadiki”
Nataka nikuambie na wewe usijaribu kufanya hivyo (Ndio unaweza kufanya hivyo, na Bwana akakusikia na kujidhihirisha kwako kwa namna ya kimwili,na ukamwona na mkazungumza), lakini nataka nikuambie Tukio kama hilo kukutokea ni nadra sana kwasababu sio njia kamilifu ya Bwana alitoichagua kwa nyakati hizi.
Ni sawa sawa na mtu aje akuombe wewe mzungumze kwa njia ya barua za posta na si SIMU, kwamba yupo Morogoro halafu akitaka kukujulia hali au kukupa ujumbe fulani basi atumie aandike barua aipeleke posta na kuituma, kisha wewe uipokee na kumjibu kwa njia hiyo hiyo ya posta!.
Umeona? Ni jambo ambalo ni gumu kwako wewe kulifanya kwasababu ni teknolojia ya zamani na inayogharimu fedha na muda.
Kadhalika na njia ya Mungu kuzungumza nasi kimwili kwake ni teknolojia ya Zamani.
Ndio maana ni ngumu leo hii kututokea na kuzungumza nasi.
Bwana Yesu kukaa katika hali hiyo ya kutotutokea tokea kimwili ni yeye ndio kaichagua hiyo njia kwa faida yetu sisi, na si kwasababu sisi ni wenye dhambi ndio maana hatutokei tokei, wala si kwasababu hatuna maombi ya kutosha ndio maana hatutokei..hapana ni kwasababu teknolojia hiyo ni ya zamani kwake na haitufai sana sisi.
Bwana alisema..
Yohana 16:7 “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu”.
Umeona?.. hapo anasema mimi yanipasa niondoke ili msaidizi aje, na Si yeye aondoke kwasababu hatuombi au kwasababu sisi ni wenye dhambi.
Hakuna maombi yoyote ambayo yangeweza kumbakisha Bwana Yesu katika mwili hapa duniani.
Sasa swali “Tunaenendaje kwa Imani”?
Tunaenenda kwa Imani kwa kumpokea huyo Roho Mtakatifu, ambaye amemwagwa kwetu.
Tukimpata huyu hata Bwana Yesu asipotutokea kwa namna ya mwili katika maisha yetu yote, bado tutakuwa tumeyajua Yesu sana, tutakuwa tumemwelewa kwa undani wote kana kwamba yupo nasi katika mwili.
Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari”.
Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari”.
Leo hii wengi hawamtaki Roho Mtakatifu lakini wanamtaka Bwana Yesu katika mwili. Pasipo kujua kuwa Roho Mtakatifu ndio ukamilifu wote wa Bwana Yesu.
Na hawamtaki kwa matendo yao na si kwa midomo, ndio maana hawamwoni Yesu katika maisha yao, ndio maana hawamwelewi na ndio maana shetani anawasumbua sana.
Je na wewe umempata Roho Mtakatifu? Kama bado na unamtamani uwe naye basi usihofu! Kwasababu haihitaji utoe fedha ili umpate, wala haihitaji ufunge kwa maombi, wala haihitaji uende kwenye shule au chuo cha biblia, wala huhitaji mhubiri au mchungaji ndipo akupatie..
Unachokihitaji sasa ni kanuni ya jinsi ya kumpata, na kanuni hiyo ni rahisi, na ipo katika biblia tu! Na hakuna sehemu nyingine unaweza kuipata.
Na kanuni hiyo ni KUTUBU DHAMBI ZAKO KWA KUMAANISHA KUTOZIFANYA TENA, NA KUBATIZWA!!…Basi!!!
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Hapo mstari wa 39 hbiblia inasema… “Ahadi hiyo ni kwaajili YENU na watoto wenu”.. Maana yake ni kwaajili yako na wewe ndugu yangu!.
Sasa kama kanuni ni rahisi hivyo kwanini leo hii usitubu, na kwanini leo hii usibatizwe kwa jina la Yesu?
Bwana akupe kuchagua njia bora!
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
NI KWA NAMNA GANI ROHO HUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU?
KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.
Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
KUOTA NYOKA.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Shalom.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia..
Maandiko yanasema.
Waefeso 6:10 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake”.
Biblia inatufundisha kuwa mahodari katika Bwana na vile vile katika Uweza wa Nguvu zake.
Hapo kuna vitu viwili, 1). Kuwa Hodari katika Bwana. 2) Kuwa hodari katika uweza wa nguvu zake.
1) Kuwa hodari katika Bwana ni kupi?.
Kuwa Hodari katika Bwana ni katika kumtafuta yeye; yaani, kujituma katika kuutafuta uso wake.
Marko 12:30 “nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
2) Kuwa hodari katika uweza wa nguvu zake.
Kuwa hodari katika uweza wa nguvu zake ni kuwa na uwezo wa kuzitumia zile silaha za roho ambazo tunazisoma katika mistari inayofuata.
Tusome,
Waefeso 6:10 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu”.
Waefeso 6:10 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu”.
Biblia inatuasa tuwe hodari, tusiwe walegevu, kwasababu uweza wa Mungu unadhihirika katika uhodari wetu katika kuzitumia silaha hizo za roho.
Na silaha hizo ndio hizo zilizotajwa hapo ambazo ni Chepeo ya wokovu, Dirii ya Haki, Upanga wa Roho, Utayari miguuni, Kweli kiunoni na ngao ya Imani.
Askari ambaye si hodari ni yule ambaye anazo silaha lakini hana ujuzi au utaalamu wa kutosha wa kuzitumia.
Askari aliyeshika upanga halafu hana ujuzi wa kutosha namna ya kuutumia, adui akija atamdhuru pamoja na silaha yake.
Kadhalika na sisi tunapoushikilia upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu, na tukawa hatujui namna ya kulitumia inavyopaswa, adui yetu shetani anaweza kutudhuru kirahisi au kutupokonya upanga huo na kutudhuru nao.
Ndio maana utaona Bwana alipokuwa kule jangwani, shetani alipomjia kumjaribu kupitia Neno la Mungu, Bwana alikuwa ni hodari katika kulitumia Neno, hivyo alimjibu shetani kwa kumwambia “tena imeandikwa”.
Au kama Apolo alivyokuwa hodari katika maandiko.
Matendo 18:24 “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko”.
Hivyo biblia inatuasa tuwe na ujuzi wa kulitumia kihalali Neno la Mungu.
2 Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli”.
Je wewe ni hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake?.
Je umejivika silaha za wokovu, na kuweza kusimama, na kuzipinga hila za shetani.
1 Wakorintho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari”.
Bwana atubariki.
KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
JE! HAMPOTEI KWA SABABU HII?
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Rudi nyumbani
Ipo haki na ipo Haki yote.
Mathayo 3:13 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali”
Mathayo 3:13 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.
14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?
15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali”
Kuna maneno mawili hapo ambayo ningependa tuyatazame. 1) ITUPASAVYO 2) HAKI YOTE.
1) ITUPASAVYO.
Hapo Bwana hajasema, “Ndivyo inipasavyo kuitimiza haki yote” bali amesema “Ndivyo Itupasavyo”.. Maana yake hiyo haki haipaswi kutimizwa yeye peke yake tu, bali watu wote, na hao watu ni wale wote walio upande wake, ndio maana Bwana Yesu akasema Imet ujeupasa, maana yake yeye pamoja na wote watakaomfuata..ni lazima waitimize haki yote.
Sasa hiyo haki yote ni ipi?
2) HAKI YOTE.
Kama tulivyosema ipo haki na ipo haki Yote. Unapomwamini Bwana Yesu, hapo umeitimiza haki, unaposhiriki meza ya Bwana hapo umeitimiza haki, unapohubiri hapo umetimiza haki, unapoishi maisha ya utakatifu hapo umetimiza haki, lakini bado si haki yote. Haki yote inakamilika na wewe kukamilisha UBATIZO WA MAJI.
Bwana Yesu alikuwa mkamilifu, alikuwa tayari mtakatifu kiasi kwamba asingekuwa na haja ya kubatizwa. Lakini aliona asipobatizwa atakuwa hajaitimiza haki yote.
Sasa kama Bwana Yesu alibatizwa ili kuitimiza haki yote, mimi na wewe leo ni nani tusibatizwe! Au tuone ubatizo hauna maana?.
Kumbuka tena Bwana anasema Imetupasa!!..maana yake sio yeye peke yake tu! Bali yeye na sisi, wote imetupasa kuitimiza Haki ya Mungu.
Katika siku hizi za mwisho shetani anawazuia watu kwa nguvu wasiitimize haki yote, anataka waitimize Nusu haki tu!..kwasababu anajua mtu akiitimiza haki yote atakuwa amempoteza, na yeye bado anataka watu wengi zaidi, wapotee naye kwenye ziwa la moto.
Na kumbuka sio kila ubatizo ni ubatizo sahihi, shetani kashafika mpaka hatua ya kuupindisha ubatizo.
Ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na si kwa kunyunyiziwa, Bwana Yesu hakwenda kwa Yohana mbatizaji na kunyunyiziwa, maandiko yanasema “alipanda kutoka majini” na si “kutoka kwenye kikombe chenye maji”.
Marko 1:9 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. 10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake”
Marko 1:9 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.
10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake”
Yohana alibatiza katika maji mengi sehemu zote (Yohana 3:23).
Sasa swali ni hili: Kama nisipobatizwa kabisa au nikibatizwa kwa ubatizo usio sahihi, baada ya kuujua ukweli sitaokolewa!
Jibu rahisi ni NDIO! Hutakolewa siku ya mwisho, kwasababu umeijua Njia ya Haki na hujaifuata, watakaopata neema ni wale ambao hawakuwahi kusikia kabisa, ambao pengine wangesikia ukweli unaoupata au tunaoupata, wangebadilika haraka sana.
Swali ni je! UMEITIMIZA HAKI YOTE?.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
Uchungu wa mauti ni nini, kibiblia?
Matendo 2:23 “mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; 24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.
Matendo 2:23 “mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;
24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.
JIBU: Uchungu wa mauti, ni kufa bila kuwa na matumaini ya kufufuka, yaani kuoza na kupotea kabisa, ndicho kilichowakuta wanadamu wote, waliokufa, kabla ya Kristo walioza wakapotea kabisa, roho zao zikawa zipo ardhini tu, (makao ya wafu), Lakini Bwana wetu Yesu Kristo, yeye alipokufa, hakupotelea mavumbini, wala hakuoza, bali alifufuka siku ya tatu. Akawa mtu wa kwanza, aliyekufa akafufuka, kisha akapaa mbinguni, akiishi milele.
Na ndio maana hapo biblia inasema..
“ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao”.
Walipodhani, Kristo hawezi kufufuka, mpaka wakamwekea na muhuri na walinzi kwenye kaburi lake, hilo bado halikuwezekana, alifufuka tu. Kwasababu haiwezekani, uchungu wa mauti umshike Bwana.
Hata sasa sisi, sote, tuliomwamini, tunapokufa, uchungu wa mauti hautukamati, na ndio maana siku ile Bwana alipofufuka alifufuka na watakatifu wake akawapeleka peponi, (Mathayo 27:51-53), sisi kama watakatifu tunapokufa hatulali makaburini tena, wala hatuendi jehanamu, bali tunahamishwa na kupelekwa peponi,(sehemu nzuri sana ya raha) tukingojea siku ile kuu ya ukombozi wa miili yetu, ndipo tutakapoichukua miili yetu ardhini, na moja kwa moja tutakwenda mbinguni, Bwana wetu Yesu Kristo alipo.
Lakini kama bado upo nje ya Kristo, uchungu wa mauti, ni lazima ukupate tu, kwasababu ukifa utakwenda jehanamu huko chini, kuteswa, huku ukisubiria siku ile ya ufufuo uhukumiwe, kisha utupwe katika lile ziwa la moto. Ndugu Usichukulie rahisi rahisi kifo kama wewe ni mwenye dhambi, uchungu wa mauti hauelezeki, soma ile Habari ya Tajiri na Lazaro,(Luka 16:19-31) ndipo utapata picha halisi ni nini kinawakuta watu wote, wanaokufa sasa nje ya Kristo.
Je bado unaishi katika dhambi? Bado unaishi Maisha ya uvuguvugu, kumbuka, hakuna anayejua siku yake ya kuondoka hapa duniani, Ikiwa leo ndio siku yako, Jiulize Huko utakapokwenda utakuwa mgeni wa nani?
Majibu tunayo sote mioyoni mwetu.
Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”
DHAMBI YA MAUTI
Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?
KU WAPI, EWE MAUTI, KUSHINDA KWAKO?
Nini maana ya “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;?
Je! Ule Unabii wa mifupa mikavu una maana gani kwetu?
Ezekieli alionyeshwa maono,ambayo yalimshangaza sana, maono yenyewe yalihusu mifupa ya watu ambao walionekana kama walishakufa kipindi kirefu sana nyuma, na inavyoelekea yalikuwa ni mauaji ya halaiki, (watu wengi waliouawa kwa wakati mmoja).Kwasababu mifupa hiyo ilikuwa mingi sana katika bonde kavu.
Hivyo alipopitishwa kwenye bonde hilo, alisikia sauti ya Mungu ikimuuliza Ezekieli Je! Mifupa hii inaweza kuwa hai tena?, Ezekieli akajibu wewe Bwana wajua, yaani wewe ndiye unayejua kama yaweza kuwa hai tena au la.
Lakini kama tunavyosoma Habari muda huo huo aliambiwa aitabirie uhai, na alipofanya vile alishuhudia uumbaji wa Mungu kwa mara nyingine tena. Jinsi mifupa ilivyopata mishipa, mara nyama, mara uhai na kutembea na kuongea tena..
Tusome.
EZEKIELI: MLANGO 37
1 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; 2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. 3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. 4 Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. 5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. 6 Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 7 Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. 8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. 9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. 10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. 11 Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa. 12 Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. 13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. 14 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana.
1 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.
3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
4 Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana.
5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi.
6 Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
7 Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.
8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake.
9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi.
10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.
11 Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.
12 Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli.
13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu.
14 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana.
Hii ni mistari ya Faraja, kwasababu inaeleza ukuu wa Mungu, kwenye matumaini ambayo yalishakwisha potea. wana wa Israeli walipopelekewa unabii huu walipata nguvu mpya,kwasababu wakiwa Babeli walikuwa wameshapoteza matumaini ya kurudi katika taifa lao tena, kuishi na kumwabudu Mungu. Lakini Mungu akawaambia japokuwa mmekuwa kama mifupa mikavu iliyokauka, mimi nitawafufua tena na kuwarudisha katika nchi yenu, na kupanda na kujenga na kunitumikia tena.
Na kweli jambo hilo lilikuja kutokea vilevile, Bwana aliwarejesha tena katika taifa lao.
Hata sasa, unaweza ukawa umekufa, kwa namna nyingi, mpaka umekata tamaa ya kuishi au ya kuendelea mbele katika Imani, pengine afya yako imepoteza matumaini kabisa, labda unaugonjwa wa kiharusi huwezi kutembea umelala tu kitandani miaka mingi au una kansa hatua ya nne, umeambiwa na daktari una wiki chache tu za kuishi, au umeishi na virusi vya ukimwi kwa muda mrefu sasa, na kinga yako imeshuka sana, siku yoyote umeambiwa unaondoka, usiogope, Bwana anaweza kukurejesha ukawa mzima tena, kama zamani.
Ibrahimu alikuwa na matumaini hayo, na ndio maana hakuona shida kumtoa mwanaye kafara kwa ajili ya Bwana, mpaka Mungu akamuita baba wa Imani,
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, 19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano”.
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;
18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,
19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano”.
hivyo na wewe kuwa na Imani na Mungu wako, hakuna linalomshinda yeye.
Mwingine, unaweza ukawa hata chakula ni shida, hujui kesho utaamkaje, familia inakutegemea, kazi huna, umekuwa mifupa mikavu kwelikweli, kumbuka uwezo wa Mungu ni mkubwa sana. Anaweza kukufufua kutoka huko tena, na kukutajirisha.
Unachopaswa kufanya ni kutulia katika mapenzi yake. Yaani, kama hujaokoka basi OKOKA leo, na kama umeshaokoka, basi zidi kumwamini yeye, na hakika atakutengenezea njia pasipo na njia.
Ikiwa wewe ni mmojawapo wa mifupa hii mikavu, ningependa tusali Pamoja sala hii;
Basi magoti mahali ulipo kisha nyanyua mkono wako mmoja juu kisha sema sala hii kwa Imani na Bwana atakusaidi.
Baba yangu, Nimejua hakika wewe ni Mungu, wala hapana mwingine mwenye ishara kuu na za ajabu kama wewe. Nimesoma maneno yako, nami nimeamini, kuwa wewe MUNGU unaweza kurejesha uhai tena kwa watu waliokwisha kufa na kuoza na kubakia mifupa tu. Naomba Bwana wangu, unisamehe makosa yangu yote, niliyokukosea kwa kujua na kutokujua. Naomba Damu ya mwanao Yesu Kristo initakase kuanzia sasa, nami nakiri kuwa nitatembea katika maisha ya utakatifu, sikuzote za Maisha yangu. Naomba unisaidie tatizo langu hili (Taja tatizo lako, kama ni ugonjwa, shida, n.k. mwambie ), Unifufue upya, nisimame, nikutukuze, nikutumikie, nikuabudu Mungu wangu. Asante kwa kunisamehe, Asante kwa kunisaidia, asante kwa kuniweka huru.
Baba yangu, Nimejua hakika wewe ni Mungu, wala hapana mwingine mwenye ishara kuu na za ajabu kama wewe. Nimesoma maneno yako, nami nimeamini, kuwa wewe MUNGU unaweza kurejesha uhai tena kwa watu waliokwisha kufa na kuoza na kubakia mifupa tu. Naomba Bwana wangu, unisamehe makosa yangu yote, niliyokukosea kwa kujua na kutokujua. Naomba Damu ya mwanao Yesu Kristo initakase kuanzia sasa, nami nakiri kuwa nitatembea katika maisha ya utakatifu, sikuzote za Maisha yangu.
Naomba unisaidie tatizo langu hili (Taja tatizo lako, kama ni ugonjwa, shida, n.k. mwambie ), Unifufue upya, nisimame, nikutukuze, nikutumikie, nikuabudu Mungu wangu. Asante kwa kunisamehe, Asante kwa kunisaidia, asante kwa kuniweka huru.
Amen.
Irudie sala hiyo kwa mara nyingine tena, hadi usikie amani ndani ya moyo yako.
Na amini kuwa Bwana ameshaanza kutenda jambo katika Maisha yako,.
Ubarikiwe sana.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali./Ubatizo Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
Bwana Yesu asifiwe, nakukaribisha katika Makala zinazoeleza juu ya thawabu mbalimbali za Mungu, na vigezo ambavyo Mungu atavitumia kuzitoa thawabu hizo. Tumeshatazama vigezo vya thawabu kadha wa kadha huko nyuma, na sasa, tutaendelea na sehemu yetu ya tano (5)
5) Zipo thawabu za kumiliki miji mingi Zaidi katika ule ufalme wa Mungu.
Mungu ameahidi,kuwapa utawala mkubwa, wale watu ambao watatumika kwa uaminifu wakiwa hapa duniani.
Tuupitie mfano huu tutaelewa zaidi;
Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. 13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. 14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. 15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. 21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. 26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.
Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.
19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.
Mfano huo unajieleza wenyewe.. Ikiwa Bwana amekupa kiwango Fulani cha neema umtumikie hapa duniani, anatarajia kuona umekizalisha kwa wingi kwa jinsi uwezavyo. Mfano amekupa neema ya kufagia uwanja wa kanisa, anatarajia, kuona na vyoo pia, ni visafi, na madirisha na viti vinakaa katika hali ya usafi siku zote.
Kwasababu siku atakayokuja, atatazama, kama kile alichokupa mwanzo, na utawajibikaji wako je! vinaendana, lakini ikiwa utaona kazi ya kufagia kanisa, haina maana yoyote, ukaendelea na shughuli zako, atakuja kukuambia kama uliona uvivu kufagia basi si ungemwajiri mtu akusaidie kuifanya hiyo kazi umlipe, kuliko kuuacha uwanja wangu ukiwa na vichaka na matakataka namna ile? Unaona Kama tu alivyomwambia yule aliyepewa fungu moja, si ungeweka kwa watoa riba, ili nijapo nikute na faida yangu?. Ndivyo atakavyotuambia na sisi!
Lakini kama tutakuwa waaminifu wa kile alichotupa, tukazalisha na Zaidi ya pale, tujue kuwa, uaminifu wetu, utaamua umiliki wetu katika ufalme ule…Kama ni miji basi tutamiliki hiyo miji kulingana na uaminifu wetu sasa.
Hivyo hiyo inatupa hamasa, tuitende kazi ya Bwana bila kutoa visingizio, bila kudharau, tena tutende Zaidi ya pale kwa kadiri tuwezavyo, kwasababu hivyo hivyo vidogo ndivyo vitakavyopima utajiri wetu.
Bwana akubariki.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
WALIYATWAA MAVAZI YAKE, WAKAFANYA MAFUNGU MANNE,
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe;
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
UDHURU NI NINI KIBIBLIA?
Jibu: Hii ni moja ya hoja ambayo ni muhimu sana mkristo yeyote kuijua.
Ukweli ni kwamba shetani hawezi kuingia kwenye ufahamu wa mtu na kujua anachokifikiri au kukiwaza au kukipanga.
Huo uwezo hana, na hajawahi kuwa nao. Na sio yeye peke yake bali hata malaika hawana huo uwezo, wala wanadamu hawana huo uwezo.
Ni Mungu peke yake na mtu mwenyewe ndio wenye Nywila (password) ya kuingia ndani ya mawazo yako.
Maana yake ni kwamba kile unachokiwaza sasahivi ni wewe peke yako ndiye unayekijua na Mungu, shetani hakijui, wala malaika wala mwanadamu mwenzako.
Labda wewe ndio uamue kuwafunulia yaliyopo ndani yako.
Sasa swali hili; kama ni hivyo inakuwaje shetani anaonekana kama anajua mambo yetu hata yale ya siri?.
Jibu ni kwamba, anajua mambo yetu kwa kuzisoma fahamu zetu.
Hata wewe unaweza kumsoma mtu na kujua anachowaza kwa wakati huo, kama una utashi wa kutosha, lakini hiyo haijamaanisha kwamba umeingia katika ubongo wake na kuyaona mawazo yake kama Tv. Hapana!
Vivyo hivyo na shetani, ana uwezo mkubwa wa kumsoma mwanadamu na hata kujua anachowaza.. kwasababu amekabiliana na mwanadamu kwa miaka mingi, tangu Edeni anazijua tabia za wanadamu, hivyo ni rahisi pia kuyasoma mawazo yao lakini si kuingia ndani ya mawazo yao.
Kama vile wewe mtu mzima unavyoweza kuyasoma mawazo ya mtoto mdogo na kujua kila kitu anachokifikiri kwa wakati huo na shetani ni hivyo hivyo.
Lakini pamoja na kwamba shetani ana uwezo wa kuyasoma mawazo ya mtu, lakini bado anapata shida sana kuyasoma na kuwaelewa mawazo ya watu waliozaliwa mara ya pili kwa Roho.
Maandiko yanasema kuwa hali ya mtu aliyezaliwa mara ya pili ni kama upepo, haujulikani unapoanzia wala unapoishia.
Yohana 3:8 “Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho”.
shetani anapata wakati mgumu sana kuyasoma mawazo ya mtu aliyezaliwa mara ya pili.
Kwasababu atadhani yale majaribu aliyomjaribu nayo jana, yatamfanya leo asiendelee na wokovu, kinyume chake anashangaa ndio kwanza anasonga mbele.
Au anategemea vile vitisho alivyomtisha navyo jana usiku, vitamfanya leo sidhubutuu kuendelea kuhubiri, au kuendelea na shughuli zake za kawaida, kinyume chake anaona yule mtu anaendelea kuhubiri kwa raha au anaendelea na shughuli zake.
Anategemea ule uchumi alioutikisa jana, utamfanya huyu mtu leo awe katika dimbwi kubwa la mawazo na hata kukufuru kinyume chake anamwona hata hawazi.
Kila anachojaribu kukifanya ili kumtikisa mtu aliyezaliwa mara ya pili, anakutana na matokeo tofauti na anayoyategemea.
Mtu aliyezaliwa mara ya pili anakuwa hatabiriki katika upeo wa shetani na mapepo yake. Tofauti na mtu ambaye hajazaliwa mara ya pili ambapo akitishiwa na wachawi kidogo tu ndani ya nyumba yake, tayari kashatishika kiasi kwamba shetani na mapepo yake wanajua kesho huyo mtu hatalala tena kwenye hiyo nyumba..Na kweli kesho yake halali tena huko ndani.
Mtu na namna hiyo shetani anakuwa anaweza kumsoma kirahisi na vile vile anakuwa anampangia maisha.
Swali ni je! Mimi na wewe tumezaliwa mara ya pili kwa Roho?. Kama bado basi tufahamu kuwa maneno haya yafuatayo yanatuhusu.
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.
UKIOKOKA,HIZI FIKRA ZIKIJA NDANI YAKO, ZIKATAE.
YESU ANA KIU NA WEWE.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)
WhatsApp
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu katika kujifunza Neno la Bwana. Bado tupo katika mwendelezo wa thawabu mbalimbali za Mungu, na vigezo anavyovitumia kuzitoa. Hii sehemu ya 4.
4) Zipo thawabu kwa wanaowasadia maskini na wasiojiweza.
Bwana Yesu alimwambia yule Farisayo Tajiri aliyemwalika katika karamu yake maneno haya;
Luka 14:12 “Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. 13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, 14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki. 15 Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu”.
Luka 14:12 “Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,
14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
15 Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu”.
Ikiwa wewe ni mtakatifu Umeokoka, usisahau, kuwakumbuka watu wenye mahitaji, na wasiojiweza kwa kile Mungu alichokujalia, kwasababu kina thawabu yake kubwa mbinguni siku ile Bwana atakapowafufua wateule wake ili kuwapa thawabu.
Unapotoa msaada, au unapofanya sherehe, usiwaalike tu, watu wenye uwezo, bali tafuta na wengine wasio na kitu cha kukurudishia, tusiwaalike watu tu waliotuchangia, bali tuwaalike pia, na wasioweza kuchangia, kwasababu, tutakuwa tumejiwekea hazina nzuri mbinguni.. Mtume Paulo alikuwa na bidii kulifanya hilo, pale alipousiwa na mitume waliomtangalia. Alisema..
Wagalatia 2:9 “tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; 10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya”.
Wagalatia 2:9 “tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya”.
Unaona? Hivyo na sisi tuwaonapo maskini, na mayatima, na wenye mahitaji, basi tujue hapo ni mahali petu pa kujichumia thawabu zetu nyingi, tufanye bidi kuwasaidia. Kwasababu tukifika mbinguni, utajiri wetu, utapimwa kwa matendo kama haya, lakini kama kila tulichokuwa tunakipata, tunakula wenyewe, au na watu wenye uwezo kama sisi, tujue kuwa tunapunguza kiwango cha utajiri wetu mbinguni. Kutoa si mpaka tuwe na vingi, ukipata sh.100, inatosha, kuwaga 50, kwa maskini na nyingine ukatumia wewe.
Bwana atusaidie tulione hilo, tuanze sasa kuwakumbuka na watu wengine wenye uhitaji.
Usikose mwendelezo..
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 2)
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
Kristo atukuzwe! Kama dhambi ilikuja kupitia mtu mmoja (Adamu), na kila aliyezaliwa ameirithi, kwanini Neema iliyoletwa na Bwana Yesu hatujairithi, yaani wote wanaozaliwa wasiwe na dhambi?
Jibu: Ni kweli maandiko yanasema katika Warumi 5:12-21, Kwamba kwa kupitia mtu mmoja Adamu dhambi iliingia, na hivyo na sisi uzao wake wote tukaingia katika hali ya kukosa (yaani tukazaliwa huku tumerithi dhambi)..
Lakini swali ni je kwanini haipo hivyo kwa Bwana, kama yeye anafananishwa na Adamu wa pili, kwanini na sisi tusizaliwe hali tumeirithi hiyo neema bila kupitia hatua nyingine hizo za wokovu?.
Jibu ni kwamba, hatujairithi Neema kwa namna ya kimwili kwasababu Bwana Yesu hajatuzaa katika mwili kama Adamu alivyotuzaa sisi katika mwili.
Endapo Bwana angetuzaa upya watu wote katika mwili, kama vile Adamu alivyotuzaa kupitia Hawa, basi na sisi tungeirithi hiyo neema kwa njia ya mwili na kungekuwa hakuna haja ya kupitia hizo hatua za wokovu.
Lakini kwasababu Bwana hakuwa na mke, na wala hajazaa kwa namna ya mwili, kwasababu kama angekuja kwa njia hiyo ya kuzaa katika mwili basi wangezaliwa wanadamu wengine ambao ni uzao wa Bwana ulio mkamilifu kama Bwana, na hivyo sisi wengine ambao ni uzao wa Adamu ambao tumekwishazaliwa tayari tungekuwa bado tupo kwenye dhambi..na hapo kungekuwa hakuna wokovu.
Lakini ashukuriwe Mungu, Kristo hakuja kuleta uzao mwingine duniani bali kuukomboa ule ambao tayari upo, (yaani sisi tulio uzao wa Adamu).
Hivyo ni lazima Bwana aje na mpango mwingine wa kutuzaa katika roho na si katika mwili, ili tuwe uzao wake katika roho, na tuzirithi ahadi zake hizo katika roho..Ndio maana Bwana Yesu alisema hatuna budi kuzaliwa mara ya pili katika Roho.
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Umeona hapo?
Na tunazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho, yaani kwa Ubatizo wa maji na Kwa Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Maana yake ni kwamba mtu aliyebatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu (Matendo 2:38, Yohana 3:23), na akapokea Roho Mtakatifu anakuwa tayari amezaliwa mara ya pili, na hivyo ni mzao wa Bwana Yesu katika Roho. (Na tayari kapata ukombozi wa roho yake).
Ukombozi wa miili yetu utakuja siku ile ya unyakuo itakapofika (Waefeso 4:30), wakati parapanda itakapolia tutakapovikwa miili mipya ya utukufu isiyo na kasoro.
Swali ni je!. Mimi na wewe tumezaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho, kumbuka Bwana anasema mtu asiyezaliwa mara ya pili hawezi kuurithi uzima wa milele.
Maran atha!.
Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
JE! USIPOTIMIZA NADHIRI ZAKO ZOTE KWA BWANA. HAWEZI KUKUSAMEHE?
Shalom, huu ni mfululizo, wa Makala ambazo zinaeleza vigezo ambavyo Mungu, atavitumia kuwapa watu wake thawabu mbalimbali, au atakavyovitumia kuwakaribisha katika ufalme wake, hii ni sehemu ya tatu, ikiwa hukupitia sehemu zilizotangulia utatumia ujumbe inbox tukutumie chambuzi zake.
3) Biblia inatuonyesha kuna watu watu wataingizwa katika ufalme wa Mungu, bila kutambua sababu.
Inashangaza lipo kundi la watu ambalo litapewa neema ya kuungia ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo, bila lenyewe kutambua sababu mpaka litakapofunuliwa na Kristo mwenyewe siku ile.
Tunalisoma kundi hilo katika vifungu hivi.
Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Kundi hili, ni lile, lilowahifadhi, watumishi wa Kristo, wakiwa hapa duniani, wasijue kuwa walikuwa wanamtendea Kristo mwenyewe, hapa hazungumzii maskini, na omba omba, au mayatima hapana, wanaowahudumia hao wanayothawabu yao, ambayo tutaiona katika Makala inayofuata, bali wanaozungumziwa hapa ni watakatifu wa Bwana, ambao kutokana na maisha yao ya utumishi, walipitia kupungukiwa, kuumwa, kukosa chakula, nguo, makazi n.k. Sasa wapo ambao waliwaona na kuwahifadhi, wasijue kuwa wanamtendea Kristo mwenyewe.
Sasa siku ile itakapofika, hawa watumishi wa Bwana watasimama na kuwataja mbele ya Kristo, na kwasababu hiyo Kristo atawapa neema ya kuuingia ufalme wake. Sawasawa na ule mfano wakili dhalimu tunaousoma katika Luka 16:1-12.
Mtume Paulo aliwaombea rehema ndugu wa mtu mmoja aliyeitwa Onesiforo, kwa jinsi walivyomtunza na kumuhudumia kwa mahitaji mbalimbali alipokuwa anahubiri.
2Timotheo 1:16 “Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu; 17 bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata. 18 Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana”.
2Timotheo 1:16 “Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;
17 bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata.
18 Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana”.
Vivyo hivyo, na wale ambao, wanawaona watu wanaomtafuta Mungu, ni kama mizigo kwao, wanawadhihaki, wanawatukana, wanawafukuza, hata wakiomba maji wanawaona ni wavivu. Watu ambao wanaposikia watumishi wa kweli wa Mungu ni kama kero kwa kwao, Watu kama hawa upo wakati Kristo naye atawakana.
Inatufundisha nini?, tukisema tunampenda Kristo, tunamaanisha kuwa tunawapenda na wale wampendao, kama unawachukia watakatifu, utampendaje Kristo?. Hivyo, wapo watu ambao Kristo atawakaribisha kwa namna hii,. Vilevile wapo watu ambao Kristo atawafukuza kwa namna hii. Kwasababu hawakumkaribisha Kristo kwao.
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.