JIBU: Jibu ni ndio.
Kosa alilolifanya Sulemani la kushawishiwa na wake zake kuwajengea madhabahu miungu, (1Wafalme 11:3:13) maandiko hayatuthibitishii kuwa lilikuwa ni endelevu, kana kwamba alimwacha Mungu moja kwa moja, hapana, au alitenda dhambi isiyosameheka kabisa hapana. Ni wazi kuwa Sulemani alitubu, kwa kosa lile, tunaposoma kitabu cha Mhubiri ambacho alikiandika katika uzee wake, kinatupa picha ya mambo mengi ambayo aliyatenda au aliyadhania kuwa ni sawa lakini mwisho wake akagundua ni ubatili ni sawa na kuufuata upepo. Na ndio maana mwisho kabisa akahitimisha, kuwa jumla ya yote yampasayo mtu ni kumcha Bwana na kuepukana na uovu. Kuonyesha kuwa Sulemani aligundua usahihi upo wapi, kabla hajafa.
Lakini pia asingetajwa katika vizazi vya ukoo wa Bwana Yesu kama angekuwa ni mmojawapo wa waliopotea. Hivyo hatuwezi kusema kuwa Sulemani alikwenda kuzimu, hata kama hakuna maandiko ya moja kwa moja yanayoonyesha mahali alipotubu.
Kikubwa tujifunze katika kosa alilolifanya. Maandiko yanasema kutii ni bora kuliko dhabihu. Kama Sulemani angetii agizo la Bwana la kutokuoa wanawake wa-kimataifa, hayo yote yasingemkuta. Lakini alidhani kwa hekima zake kuwa nyingi asingeweza kudanganyika. Ndio alikuwa mjanja mwanzoni katika ujana wake, lakini sekunde za mwisho za uzee wake shetani alimpiga mweleka. Zipo dhambi ambazo shetani anakuandalia uzitende baadaye, lakini maandalizi yake anayatengeneza sasa. Tii kila agizo la Mungu, hata kama ni dogo kiasi gani, hata kama litaonekana ni jepesi kulishinda kiasi gani sasa, wewe tii, kwasababu Mungu anaona mbele wewe unaona hapa. Simama katika Neno, sio katika mitazamo yako, ndipo utakapoweza kumshinda shetani, ikiwa wenye hekima kama hawa walinaswa katika tundu bovu wewe ni nani usinasike pindi unapolipuuzia Neno la Mungu linalokusemesha moyoni mwako uache hiyo tabia au hiyo dhambi?.
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?
Nchi ya Nodi ambayo Kaini alikimbilia ndio nchi gani kwasasa?(Mwanzo 4:16).
Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’? Mhubiri 3:11
JIBU:
Mhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Mwanadamu alivyoumbwa ni tofauti na wanyama au viumbe hai vingine. Kwani vyenyewe tangu vilipoumbwa mpaka sasa havibadiliki, wala haviendelei, kimaarifa, kiuelewa, au kiujuzi.. Lakini sisi wanadamu kila siku ndani yetu kuna kiu ya kujua zaidi na zaidi, kufahamu zaidi na zaidi, kutafuta zaidi na zaidi, kutokuridhika hata kama tumepata.. Na hiyo ndiyo inayotupelekea kupiga hatua mpya kila leo. Sasa hiyo hali isiyokoma ndani yetu ndio inayoitwa UMILELE.
Na Mungu ameiruhusu iwepo ndani ya mwanadamu, kuvumbua, mambo mapya, tangu zamani hata sasa, na anafanya bidii kutafuta akidhani labda atafikia ukomo anaoutazamia, lakini kila kunapokucha ndipo anapogundua kuwa bado sana kuyaelewa mambo ya Mungu. Wanadhani pengine kwa kugundua ndege, ndio itawafikisha mbinguni, lakini kumbe, ndio wanaona anga halina mwisho.
Maana yake ni kuwa, hata milele yote ya maisha, au ya maarifa, au ya uvumbuzi kamwe hatutakaa tummalize Mungu. Yatosha sisi kukaa katika pendo lake, kuyatenda mapenzi yake katika Kristo Yesu,. Lakini tusipoteze nguvu zetu kumtafiti Mungu, ni heri tutumie hizo kuutafiti utukufu wake ili tumwabudu kuliko kuzitafiti njia zake, au kanuni zake alizojibunia, tutapoteza muda.
Sulemani alisema..
Mhubiri 8:17 basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.
Dumu katika mapenzi yake Mungu, tunayojifunza kupitia biblia, kwani hilo ndio FUNGU letu tulilowekewa.
Ndio maana ya hilo Neno; Mhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na Kristo yupo mlangoni kurudi? Umejiandaaje? Tubu mgeukie Bwana akuponye.
Shalom.
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.
Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
SWALI: Biblia ilimaanisha nini iliposema Kaini ‘Akatoka mbele ya uso wa Bwana’. Kutoka kule kulimaanisha nini?
JIBU: Tunaona baada ya Kaini kumuua ndugu yake Habili kwa wivu, ambao ulizuka baada ya sadaka yake kukataliwa na ya ndugu yake kukubaliwa. Mungu alimsemesha, na kumweleza laana yake itakayompata baada ya pale. Lakini mwisho wa maneno yale, Tunaona Kaini anaonekana akitoka mbele ya uso wa Bwana. Maana yake ni nini?
Tusome.
Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. 13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. 16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni”
Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. 16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni”
Kutoka mbele ya uso wa Bwana hapo, sio Kuahirisha mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea baina yake yeye na Mungu hapana. Bali ni kumwacha Mungu moja kwa moja. Yaani kwa ufupi mkataba wake na Mungu aliumalizia pale. Hakuna cha dhabihu tena wala sadaka, wala kumwomba Mungu, wala kujihusisha na tendo lolote la kiibada. Akaanza kujishughulisha na mambo ya kidunia tu, na sayansi, na utafiti na uvumbuzi, na akafanikiwa sana katika bidii yake hiyo, yeye na uzao wake wote, wakawa watu hodari duniani, lakini waovu sana (Soma Mwanzo 4:20-22). Na hawa ndio waliopelekea gharika kuletwa duniani.
Tofauti na uzao wa Adamu kwa Sethi, wao waliendelea kuwepo mbele ya uso wa Bwana, wakitaka fadhili na rehema kwa Mungu daima,wakiliitia jina lake.
Mwanzo 4:25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana”.
Mpaka sasa makundi haya mawili yapo duniani. Lipo ambalo halina habari na Mungu,(Ambao ndio uzao wa Kaini rohoni) bali mambo ya kidunia tu, na limefanikiwa sana katika hayo, ni jepesi katika uvumbuzi na utafiti, lakini Mungu kwao ni kama historia za mababu wa kale, ni kama vile mashariki na magharibi zilivyo mbali. Lakini sisi hatupaswi kufanana wa watu hao. Bali kama Watoto wa Adamu kwa Sethi. Furaha yetu ipo katika Bwana. Tegemeo letu ni yeye, na nguvu zetu ni yeye, haijalishi tutakosa vyote au tutapata vyote. Yeye ndiye atakayekuwa urithi wetu milele.
Je! Wewe upo kundi lipi? Uthibitisho ni maisha yako ulipoyaelekeza.
Hizi ni nyakati za mwisho. Kristo anarudi. Tubu mgeukie Bwana, mtafute yeye.
Maran Atha.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Bustani ya Edeni ipo nchi gani?
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu. (Zab. 119:105).
Kuna tofauti ya Msamaha wa dhambi na Ondoleo la dhambi.
Mtu anapokukosea labda amekutukana au kukuibia na akikuomba msamaha unaweza kumsamahe (ukamwachilia kabisa moyoni mwako) lakini kumsamehe kwako hakumfanyi yeye kuacha ile tabia.. Maana yake ni kwamba kama ile tabia haitaondoka ndani ya huyo mtu basi ni wazi kuwa atarudia lile kosa siku nyingine. Atapumzika siku mbili au tatu na baadaye atarudia lile kosa. Sasa mtu kama huyu kapata msahama lakini si ondoleo la ile tabia.
Vile vile kwa Mungu tunaweza kupata msamaha wa makosa yetu na dhambi zetu, lakini kama hatutapata Ondoloe la dhambi hizo (Maana yake kama ule mzizi wa dhambi ndani yetu hautang’olewa) basi tutabaki vile vile, kila mara tutarudia makosa yale yale. Na mzizi wa dhambi ni lazima uondoke maishani mwetu kwasababu ndicho kitu kilichomleta Bwana Yesu duniani.
Bwana Yesu hakuja tu kuleta msamaha wa dhambi bali pia ondoleo la dhambi..Kwasababu msamaha wa dhambi ulikuwepo hata kabla ya Bwana Yesu kuja duniani, watu waliomba msamaha mbele za Mungu na wakasamehewa makosa yao, lakini Ondoleo la dhambi halikuwepo, Dhambi hazikuondolewa katika kumbukumbu za Mungu (zilifunikwa tu) na vile vile hazikuondolewa ndani ya mtu, bado watu waliendelea kurudia makosa yale yale, baada ya Bwana Yesu kuja watu ndipo wakapata ondoleo la dhambi, ndani yao (utumwa wa dhambi ukakoma kwa wale wote waliompokea).
Sasa tunapataje ondoleo la dhambi?.. kiasi kwamba dhambi haitupelekeshi tena wala kututawala?
Kwanza ni kwa kutubu mbele za Mungu, na kukiri kwamba sisi ni wakosaji, (hapa unatubia makosa yako yote ambayo umeyafanya kwa kujua, na kwa kutokujua mbele za Mungu, kwa tendo hilo Bwana atakusamehe ikiwa toba hiyo imetoka kweli ndani ya moyo na kwamba umekusudia kubadilika kabisa..)
Sasa hatua inayofuata ili Dhambi zako ziondolewe (ule mzizi wa dhambi ndani yako uondoke) baada ya kutubu ni wewe kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi… Hiki ni kipengele cha muhimu sana ambacho si cha kupuuzia hata kidogo..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU”
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU”
Ubatizo sahihi unakamilisha toba na hivyo mtu anayefanya hayo Mungu anampa zawadi ya Roho Mtakatifu pamoja na Ondoleo la dhambi, jambo ambalo ni muhimu sana.
Mtu huyu kama toba yake imetoka ndani ya moyo kabisa basi ule uzinzi uliokuwa unamsumbua mara kwa mara unakufa, anajikuta anaushinda uasherati na haurudii tena, kwasababu dhambi imeondolewa ndani yake, zile tabia zilizokuwa zinamwendesha mara kwa mara zinaondoka ndani yake kwasababu ule mzizi wa dhambi umeondolewa ndani yake n.k n.K
Na kumbuka ni muhimu sana kubatizwa ubatizo ulio sahihi, kwasababu si kila batizo zinaondoa dhambi.. nyingine utabatizwa lakini utabaki vile vile. Na ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 19:10)!.
Je unataka usiendelee kuwa mtumwa wa dhambi?.. Tumia kanuni hiyo ya Matendo 2:27-37. Na Mungu ni mwaminifu atafanya sawasawa na Neno lake.
Maran atha.
Ikiwa hujabatizwa bado na unahitaji msaada wa kupata ubatizo sahihi, basi waweza kuwasiliana nasi kwa namba zetu na tutakusaidia kwa hilo.
Shalom
AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.
NINI MAANA YA KUTUBU
Dameski ni wapi kwasasa?
BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Mafunzo maalumu kwa Wanawake.
Karibu tujifunze Biblia,
Je Bwana alishakufanyia muujiza wowote katika maisha yako?..Na ukaufurahia?.. Je baada ya hapo ulimfanyia nini Bwana?.. Je uliishia kushukuru tu na kuendelea na mambo yako? Au kuna lingine la ziada ulilifanya?, kama hukufanya chochote au hukujua nini cha kufanya basi leo fahamu yakupasayo kufanya!
Hebu tujifunze kwa baadhi ya wanawake katika biblia ambao hawakuwa Mitume, wala Waalimu, wala Maaskofu wala wachungaji lakini walikuwa wakimtumikia Bwana Yesu.. na kisha tutazame walikuwa wakimtumikia kwa namna gani?
Mathayo 27:55 “Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, HAO NDIO WALIOMFUATA YESU TOKA GALILAYA, NA KUMTUMIKIA. 56 Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo”.
Mathayo 27:55 “Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, HAO NDIO WALIOMFUATA YESU TOKA GALILAYA, NA KUMTUMIKIA.
56 Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo”.
Hawa wanawake walikuwa wakifuatana na Bwana Yesu kila mahali.. Lakini je! Walikuwa wanafuata naye kumtazama uso?, au kumsikiliza tu anayoyahubiri?..Jibu ni La! Biblia inatuambia walikuwa pia WAKIMTUMIKIA!!.. Sasa swali wakimtumikia kwa nini?..tusome mistari ifuatayo..
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, 2 NA WANAWAKE KADHA WA KADHA ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, WALIOKUWA WAKIMHUDUMIA KWA MALI ZAO”.
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2 NA WANAWAKE KADHA WA KADHA ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, WALIOKUWA WAKIMHUDUMIA KWA MALI ZAO”.
Umeona hapo?.. Walikuwa wakimhudumia kwa MALI ZAO!. Ikiwa na maana kuwa gharama kubwa za kuipeleka Injili zilikuwa zinabebwa na hawa WANAWAKE!.. hata ule mkoba ambao Yuda alikuwa anaushika, huenda sehemu kubwa ilijazwa na hawa wanawake!.
Na kwanini wanawake hawa walipata msukumo huo mkuu wa kumhudumia Bwana kwa mali zao?.. Jibu ni kwasababu walitendewa miujiza na Bwana, walitolewa pepo waliokuwa wanawatesa, waliponywa magonjwa yao yaliyokuwa yanawatesa, walipewa wokovu ndani yao ambao uliwapa Amani na tumaini la maisha..Hivyo wakaona si sawa kumtazama Yesu kwa uso tu na kumshukuru kwa maneno tu!, bali pia kwa vitendo.
Ndipo wakaona wavunje vibweta vyao ili Bwana akaende miji mingi Zaidi kuhubiri, wakaona watoe hazina zao ili wanafunzi wa Bwana wasipungukiwe wanapokwenda kuhubiri miji na miji. Na hivyo wakawa mashujaa wa Imani ambao mpaka leo tunawasoma.
Na sio hao tu, bali pia tunamwona na Mkwe wake Petro, (Mama yake mkewe) ambaye alikuwa anaumwa homa, biblia inasema baada ya Bwana kumponya, alinyanyuka na kuanza KUMTUMIKIA BWANA!.
Mathayo 8:14 “Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. 15 Akamgusa mkono, homa ikamwacha; NAYE AKAONDOKA, AKAWATUMIKIA”
Mathayo 8:14 “Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa.
15 Akamgusa mkono, homa ikamwacha; NAYE AKAONDOKA, AKAWATUMIKIA”
Je na wewe Mama unamtumikia nani?, Na wewe binti unamtumikia nani?…Je umemtumikia Bwana kwa kipi tangu alipokuponya?, tangu alipokufungua?, tangu alipokuinua?, tangu alipokupa wokovu bure?.. Je unamtumikia kwa maneno tu, au pia na vitendo?.
Ni kweli wewe sio Mchungaji, wala Mwalimu, wala Mhubiri, wewe ni kama tu Mariamu Magdalena, au Susana..basi fanya kama hao!.. Na kumbukumbu lako litadumu kama la hao wanawake lilivyodumu, Bwana atakuheshimu na kukuona wewe ni mtumishi wake kama tu walivyo Mitume kwasababu na wewe pia unamtumikia kwa mali zako.
Bwana akubariki.
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
WANNE WALIO WAONGO.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Swali: Katika kitabu cha Luka 5:1-7 tunaona kuwa Bwana Yesu aliwakuta Petro na Andrea ufukweni na akawaita, lakini tukirejea kwenye Yohana 1:35-42 tunasoma kuwa aliwaita wakati wapo kwa Yohana Mbatizaji?.. Je biblia inajichanganya?
Jibu: La! Biblia haijichanganyi hata kidogo, vinginevyo kitabu chote kitakuwa cha uongo!.. Lakini kwasababu ni kitabu cha kweli, basi kamwe hakiwezi kujichanganya!.
Kabla ya kuichambua mistari hiyo hebu tuisome kwanza..
Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti, 2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. 3 Akaingia katika chombo kimoja, NDICHO CHAKE SIMONI, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni. 4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. 5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, TUSIPATE KITU; LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU. 6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika”
Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,
2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.
3 Akaingia katika chombo kimoja, NDICHO CHAKE SIMONI, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, TUSIPATE KITU; LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika”
Hapa ni kweli Bwana aliwakuta Andrea na Petro baharini wakivua samaki.. Lakini katika kitabu cha Yohana tunasoma habari nyingine tofauti kidogo..
Yohana 1:35 “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40 ANDREA, NDUGUYE SIMONI PETRO, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41 HUYO AKAMWONA KWANZA SIMONI, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). 42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)”.
Yohana 1:35 “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.
36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!
37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.
38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
40 ANDREA, NDUGUYE SIMONI PETRO, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.
41 HUYO AKAMWONA KWANZA SIMONI, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)”.
Uhalisia ni kwamba Bwana Yesu alikutana na Adrea na Petro kwa mara ya kwanza kipindi wanatoka kwa Yohana Mbatizaji, lakini Bwana Yesu hakuwaambia wamfuate, (yaani wawe wanafunzi wake)!.. Lakini kwa tukio lile tayari walikuwa wameshafahamiana na Bwana.
Sasa tunapokuja katika tukio la kule baharini, ndipo Kristo anawaambia waache Nyavu zao wamfuate na yeye atawafanya kuwa wavuvi wa watu badala ya kuwa wavuvi wa samaki.
Kwahiyo katika tukio hili la pili ni wazi kuwa tayari Petro na Andrea walikuwa wanamjua Bwana, Ndio maana tunaona hata haikuwa ngumu kwa Petro kumkubalia Bwana akitumie chombo chake katika kuwafundisha makutano (Na Bwana anaonyesha kama kuwa na ujasiri wote katika kutumia chombo cha Petro na kumpa maagizo kana kwamba tayari wanajuana).. na ndio maana pia tunaona haikuwa ngumu kwa Petro kumwamini Bwana na kwenda kushusha nyavu kwa neon la Bwana.. kwasababu tayari alikuwa anamjua, walishakutana huko nyuma..
Kwahiyo hakuna mkanganyiko katika habari hizo, isipokuwa ni waandishi wawili wamenukuu matukio mawili tofauti.
Maran atha!
Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?
Je Bwana Yesu aliruhusu wanafunzi wake kubeba Fimbo au hakuwaruhusu? (Marko 6:8 na Mathayo 10:10).
Manyoyota ni neno lingine la “manyunyu”. Manyunyu ya mvua kwa lugha nyingine yanaitwa “manyoyota”
Ayubu 37:6 “Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na vivyo manyonyota ya mvua, Na hayo maji ya mvua yake kubwa”.
Baraka za Bwana zinafananishwa na manyunyu ya mvua..
Ezekieli 34:26 “Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya Baraka”
Tunapoenda katika njia zake Bwana atatunyeshea manyunyu ya Baraka.
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
IJUE HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUKUINUA KIMAISHA.
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote
Wakolosai 3:5 inamaana gani?
Kwanini mtu afanye miujiza na bado asiende mbinguni?
Neno “kuguguna” linapatikana mara moja tu katika kitabu cha Ayubu 30:3 na maana yake ni “kutafuna”
Ayubu 30: 2 “Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini? Watu ambao nguvu zao zimekoma. 3 Wamekonda kwa uhitaji na njaa; HUGUGUNA NCHI KAVU, penye giza la ukiwa na uharibifu”
Ayubu 30: 2 “Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini? Watu ambao nguvu zao zimekoma.
3 Wamekonda kwa uhitaji na njaa; HUGUGUNA NCHI KAVU, penye giza la ukiwa na uharibifu”
Hapa maandiko yanalizungumzia kundi la watu ambao ni maskini, wasio na nguvu, huguguna (hutafuna) riziki zao mahali pakame, penye giza na uharibifu.
Ufunuo kamili kwa mtu yule anayemtegemea mwanadamu.. Maandiko yanasema atakaa mahali pakame, katika nchi ya chumvi..
Yeremia 17:5 “ Bwana asema hivi, AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama FUKARA NYIKANI, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani PALIPO UKAME, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.”
Yeremia 17:5 “ Bwana asema hivi, AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6 Maana atakuwa kama FUKARA NYIKANI, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani PALIPO UKAME, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.”
Bwana atusaidie tumtegemee yeye siku zote, na kumfanya yeye kuwa kinga yetu.
Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)
RACA
HAMA KUTOKA GIZANI
Bwana alimaanisha nini kusema “kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”
Mapooza ni nini? Na je! Twawezaje kuepukana nayo?
Masomo maalumu kwa watumishi wa Mungu (Wahubiri).
Je umebeba ushuhuda gani katika injili yako?.
Tujifunze jambo kwa Yohana Mbatizaji..
Yohana 10:40 “Akaenda zake tena ng’ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. 41 Na watu wengi wakamwendea, wakasema, yohana kweli hakufanya ishara yo yote, LAKINI YOTE ALIYOYASEMA YOHANA KATIKA HABARI ZAKE HUYU YALIKUWA KWELI. 42 Nao wengi wakamwamini huko”.
Yohana 10:40 “Akaenda zake tena ng’ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
41 Na watu wengi wakamwendea, wakasema, yohana kweli hakufanya ishara yo yote, LAKINI YOTE ALIYOYASEMA YOHANA KATIKA HABARI ZAKE HUYU YALIKUWA KWELI.
42 Nao wengi wakamwamini huko”.
Hapo maandiko yanasema Yohana hakufanya ishara yoyote kama alivyofanya Musa katika hatua ya kuwahubiria ukombozi wana wa Israeli, au kama alivyofanya Eliya aliposhusha moto, au kama alivyofanya Eliya na manabii wengine..
Lakini Yohana yeye tunasona alibeba kitu kingine cha ziada.. Na kitu hicho ni “USHUHUDA WA KWELI WA YESU”. Na ndicho kilichomfanya aonekane mbele za Mungu kuwa mkuu kuliko manabii wote waliotangulia..
Mathayo 11:9 “Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na ALIYE MKUU ZAIDI YA NABII.…… 11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa WANAWAKE ALIYE MKUU KULIKO YOHANA MBATIZAJI; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye”.
Mathayo 11:9 “Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na ALIYE MKUU ZAIDI YA NABII.……
11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa WANAWAKE ALIYE MKUU KULIKO YOHANA MBATIZAJI; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye”.
Kwahiyo kumbe kinachojalisha si miujiza?, si ishara, si maajabu tunayoyatenda.. bali ni kile tunachokihubiri kumhusu Yesu?.. Je kina ukweli?.. na kama kina ukweli, je ni katika kiwango gani?
Yohana alianza kuhubiri habari za Toba na ondoleo la dhambi na kusema Ufalme wa Mungu umekaribia wamwamini yeye ajaye.
Mathayo 3:1 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, 2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Mathayo 3:1 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Injili ya namna hii ndiyo Bwana Yesu aliyoanza kuihubiri pia…
Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Umeona injili ya Yohana iliyovyofanana na ya Bwana?..Yohana aliuona ushuhuda wa Yesu na akauhubiri kabla hajaja, aliona hizi ni nyakati za kutubu na kumrudia Mungu, kwasababu ufalme wa Mungu umekaribia!!.. .
Vile vile hakuanza kuwaambia watu watubu halafu baadaye waendelee na dhambi zao, bali aliwaambia watubu na baada ya hapo wazae matunda yapatanayo na toba zao, wala wasijisifie dini, wala madhehebu.. Maana yake baada ya kutubia uzinzi ni lazima waishi maisha ya usafi baada ya hapo, kama umetubia ulevi ni lazima wauache ulevi, kama wametubia ukahaba ni lazima wauache ukahaba na vifaa vyote vya ukahaba, ikiwemo mavazi!..(hiyo ndio maana ya kuzaa matunda yapatanayo na toba).
Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8 Basi, TOENI MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA MAZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI”.
Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
8 Basi, TOENI MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA MAZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI”.
Injili ya namna hii ndiyo iliyobarikiwa na Bwana Yesu, na ndiyo iliyochaguliwa kuwa NJIA KWAAJILI YA BWANA!, Na ndiyo iliyomfanya Yohana awe mkuu kuliko manabii wote ingawa hakufanya muujiza wowote.
Je! Na wewe kama mtumishi wa Mungu unahubiri nini? Je unahubiri mambo ya ulimwengu huu au injili ya ufalme wa Mbinguni??.. Injili yako ni ya magari na majumba na pesa?..
Kumbuka Injili ya ufalme wa mbinguni ni ile ile haijabadilika ambayo ni “kutubu na kuzaa matunda yapatanayo na toba kwamaana ufalme wa mbinguni umekaribia” Huo ndio ushuhuda wa Yesu na ndio roho ya unabii.
Ufunuo 19:10b “….. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii”.
Vile vile usikimbilia kutafuta au kutengeneza miujiza, usitumie nguvu nyingi kutafuta maajabu… bali tafuta kwanza Ushuhuda wa Yesu, ukiupata huo utakuwa umepata muujiza mkubwa sana katika utumishi wako!.
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
WAKO WATATU WASHUHUDIAO MBINGUNI NA DUNIANI.
JE UMEKUFA PAMOJA NA NANI?
Wagalatia 6:1 ‘Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.
JIBU: Hapa biblia inatupa mwongozo sahihi wa jinsi ya kuwavuta upya ndugu ambao walianguka katika dhambi.
Tunafundishwa tuwarejeshe katika Roho ya upole, maana yake sio ya kulaumu au ya ukali. Kwamfano utakuta mtu karudi nyuma katika ulevi wake aliokuwa nao mwanzoni. hapo yakupasa utumie busara kumrejesha upya ili iwe rahisi tena mtu huyo kugeuka na kutubu, kuliko kutumia ukali mfano kumkaripia au vinginevyo. Ukitumia kauli za lawama au mashtumu, si rahisi kumvuta, kinyume chake zitamfanya achukie zaidi au akasirike.
Lakini pia sehemu ya pili anasema..ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
. Maana yake ni kwamba hata wewe mwenyewe Unaweza ukajaribiwa na shetani uwapo katika kazi hii ya kuwavuta wengine waliokengeuka katika wokovu. Kwamfano huyo mlevi anaweza akakutukana, halafu wewe ukakasirika, ukaanza kurejesha lugha za matusi kwake kwasababu ya hasira, hapo tayari umeshaanguka katika dhambi.
Baadhi ya watu wa Mungu wamejaribiwa na kuanguka katika uzinzi walipokuwa wanafanya huduma Kwa watu walio wa jinsia tofauti na wao. Wengine katika anasa waliposhirikiana na watu wa kidunia waliowashuhudia habari za Yesu.
Hivyo tunapaswa tujichunge nafsi zetu sana tuwapo katika kuipeleka habari njema kwa makundi ya watu tofauti tofauti. Kwasababu na sisi pia shetani anatuwinda. Lakini Tukiwa watu wa maombi na kuliishi Neno tutajilinda sana nafsi zetu na mitego hiyo ya shetani. Ndio maana ya hilo Neno ‘ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.
Mada Nyinginezo
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?
Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.
NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU
Rudi Nyumbani