Kwanini karama ya Mungu ni uzima wa milele?
Ukikaa chini ukajaribu kutafakari kwa umakini hili Neno UZIMA WA MILELE, utashangaa sana, wakati mwingine utajiuliza hili jambo linawezekanaje kanaje, na ukilitafari sana utaona kama akili yako inafika sehemu inagota. Eti unaishi tu siku zote bila kuwa na kikomo, unaishi leo, miaka mia inapita bado unaendelea tu kuishi.
Miaka elfu inapita bado unaendelea kuishi, miaka milioni moja inapita bado unaendelea kuishi, miaka bilioni moja inapita bado unaendelea kuishi. Miaka trilioni moja inapita ndio bado hata maisha hayajaanza…unaendelea tu, miaka kuadrilioni moja (ambayo ni sawasawa na miaka trilioni elfu moja), inapita bado unaendelea kuishi, miaka kuintilioni moja inapita ndio bado hata hakuna dalili ya kufika mwisho, miaka seksitilioni moja, wewe bado unaendelea tu kuishi. Miaka oktilioni na nonilioni, na desilioni na anidesilioni inapita, hapo bado utaendelea tu,..miaka dodesilioni, na tradesilioni na kuatuordesilioni na kuindesilioni na seksidesilioni bado tu safari inaendelea ukiwa bado kama kijana mdogo tu, n.k. n.k. tukiziandika namba zote hapa tunaweza kujaza ukurasa mzima na bado zisitoshe….
Embu jaribu kufikiria hayo ni maisha marefu kiasi gani, leo hii tu ikipita miaka 20 au 30 unaona kama ilikuwa ni zamani sana, na tena unaiita enzi hizo, sasa hapo bado haijatapita miaka milioni moja sijui hiyo utaiitaje labda utaaita kama ile ya historia zama za mawe za kwanza, pengine hata kumbukumbu zake utakuwa umezipoteza..
Sasa Mungu asiyekuwa na mwisho ametuahidia zawadi hiyo kuu bure, Hata tusingepewa zawadi nyingine hiyo tu ya Uzima wa Milele ingetutosha. Ni zawadi kubwa sana isiyoelezeka.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni UZIMA WA MILELE katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Na kumbuka pia Mungu asiye na mipaka, miaka hiyo yote hatutakuwa tunaishi tu kama watu wasiokuwa na mwelekeo “idle”. Au unaishi tu bila maaana yoyote hapana! vinginevyo umilele utakuwa wa ku-boa.
Badala yake kila siku, kila wakati kutakuwa na matukio yake na mambo yake mazuri mapya, yaani tutayafurahia maisha kila iitawapo leo, kwasababu kila siku itakuwa na mambo yake, kutakuwa hakuna magonjwa, kutakuwa hakuna kuzeeka, kutakuwa hakuna shida, kutakuwa hakuna mahangaiko, wala kupigwa na jua hakutakuwepo, wala ulemavu hautakuwepo, wala uchungu, wala kuudhiwa, wala kuumizwa, wala kudaiwa. Siku zote tutaishi katika raha isiyo na kifani, tukiushangaa utukufu wa Mungu na kumwabudu yeye katika raha isiyoelezeka.
Mungu kashaipigia mahesabu kila siku moja ya umilele hivyo analijua tukio ambalo litatokea siku Fulani ya mwaka Fulani wa bilioni moja huko mbeleni kwamba wewe utakuwa unafanya kitu Fulani na Yule kitu fulani,..Huyo ndio YEHOVA..hatuishi kumshangaa kwa matendo yake ya ajabu.
Isaya 55:8 “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”.
Kauli hiyo ya Mungu inatuthibitishia kuwa mipango ya Mungu aliyotuandalia sisi, hatuwezi kuidhania au kuifikiria ipasavyo hata kwa chembe ndogo sana. Kwasababu ipo mbali sana na upeo wetu wa kufikiri, na ndio maana ni jukumu letu kuhakikisha sisi sote hatuukosi huo uzima wa milele.. Kwasababu hapa ni kama tunaandaliwa tu kwa ajili ya kuishi maisha halisi, hapa duniani hatuna maisha, miaka 70 au 80 sio maisha. Bali tunaandaliwa tu kwa ajili ya kuishi kule ambako Mungu alitukusudia tuishi, tunatengenezwa tu ili tuweze kustahimili huo umilele unaokuja huko mbeleni..
Hivyo tukiwa tunayatafakari hayo kila siku tutapata nguvu ya kutokujali ni nini tunapoteza sasa tukiwa hapa duniani, kwa ajili ya maisha yetu ya umilele ya baadaye…hatutojali tunapoteza fursa ngapi za biashara kwa ajili ya kuhudhuria maombi, hatutojali tunapoteza hiki au kile kwa kwenda ibadani, kwa kujifunza Neno la Mungu…Hatutojali ni mambo mangapi ya kidunia yanatupita, sisi tunatazama maisha ya milele Mungu aliyotuandalia…
Hata mithali ya kidunia inasema, “usiache mbachao kwa msala upitao”. Ikiwa na maana tusiopoteze uzima wetu wa milele kwa vitu vya kidunia vinavyopita, ambavyo mwisho wake ni hapa tu..Itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima, kisha tupate hasara ya nafsi zetu.? Kwasababu mshahara wa dhambi ni mauti…lakini karama ya Mungu ni uzima wa milele.
Lakini uzima wa milele huu kuupata ni bure, nao unakuja kwa kumwamini tu YESU KRISTO, pale unapotubu kwa kudhamiria kwa dhati kutoka moyoni mwako kwamba kuanzia leo unaacha dhambi zako zote..Unafanya maamuzi ya kuacha pombe, kuacha uasherati, kucha uvaaji mbaya, kuacha rushwa, kuacha wizi n.k. Na vitu vyote ulivyokuwa unaviona vinakufaidisha sana vya kidunia unaviacha vyote unavihesabia kama ni mavi. Kama Mtume Paulo alivyovihesabia.
Wafilipi 3.7 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.
8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama MAVI ili nipate Kristo”
Na baada ya kutubu na kuyahesabia mambo yote uliyokuwa unayafanya machafu kama MAVI. Hatu inayofuata ni kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamwisha katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako sawasawa na Matendo 2:38,.Kisha Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu..Hivyo Hatua hizo zote zikikamilika juu yako basi na wewe utakuwa umefanyika kuwa mwana wa Mungu na yeye mwenyewe atakupa karama hii ya uzima wa milele bure..
Kumbuka …Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”…Na sio katika Ulimwengu.
Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
UFUNUO: Mlango wa 1
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
Litania ya bikira Maria mtakatifu ni nini?, Je Maria ni Malkia wa Malaika, Malkia wa mitume na malkia wa wakristo?.
Maana ya “LITANIA” ni Mfululizo wa sala ambayo maneno yake ni ya kujirudia rudia, ambayo yanahusisha upande mmoja kuitikia. (Mkusanyiko unaitikia). Mtindo huu wa sala unatumika sana na Kanisa Katoliki.
Kabla ya kuitafakari kama ni sala ya kimaandiko au la..Ni muhimu kufahamu kuwa lengo la ujumbe huu..sio kumshutumu mtu, wala kumhukumu, wala lengo sio kujifanya kuwa upande mmoja unajua zaidi ya mwingine..Lengo kuu ni kujifunza Maandiko, huku tukionyana na kusahihishana kasoro zetu kwa kutumia Biblia. Kama tulivyoagizwa katika Wakolosai 3:16.
Sasa tukirudi kwenye sala hiyo hapo juu..Tunaweza tukahoji mambo machache muhimu..
Je! Ni kweli Maria Mtakatifu? na ni mama mwenye Ubikira?..
Si kweli kwasababu Maria Baada ya kumzaa Bwana hakuendelea kuwa Bikira..na pia alipokufa, alizikwa na huko alipo sio bikira, yupo katika roho ambapo yeye naye anasubiri ufufuo ambao utakaokuja katika siku ile ya unyakuo,..ambapo atavaa mwili wa utukufu kama watakatifu wengine na kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Hivyo hawezi kuombwa kwa lolote wala haelewi kinachoendelea duniani.
Kadhalika Maria sio Malkia wa wakristo wala Malkia wa Malaika. Kwasababu Malaika hawana Malkia,..Na hakuna mahali popote katika maandiko matakatifu panasema hivyo..Isipokuwa wapagani ndio walikuwa wanaabudu kiumbe wanachokiita wao malkia wa mbinguni. Lakini katika maandiko hakuna sehemu yoyote inayoonesha kuwa kulikuwa au kutakuwepo na malkia wa malaika. Hivyo ni dhahiri kuwa kama sala hii haipo katika Biblia basi ni lazima itakuwa imetungwa tu na watu fulani ambao nia yao ni kupoteza wengine.
Hivyo sala hii sio sala ya kimaandiko bali ya kibinadamu, ambayo ndani yake upo mpango mkubwa sana wa Ibilisi..kuwafanya watu waabudu sanamu na vitu visivyokuwepo..
Ndugu kama unataka kusali, Bwana Yesu mwenyewe alitufundisha sala..Nayo ni hii..
Luka 11:1 “Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu]”
Ingekuwa Maria anastahili kuombwa Bwana Yesu angewafundisha wanafunzi wake hapo juu wamwombe Maria..Lakini unaona hajafanya hivyo..Ikimaanisha kuwa sala inastahili kwenda kwa Baba yetu wa Mbinguni basi.
Kama ulikuwa unasali sala hiyo ya “litania ya bikira Maria” na hukujua kuwa ni sala ya uongo, na leo umejua. Usifanye hivyo tena, ni machukizo mbele za Mungu..Ni ibada za sanamu ambazo Mungu amezikataza mara nyingi katika Biblia..Mpe leo Yesu Kristo maisha yako naye atakupa tumaini na moyo mpya wa sala..
Mada Nyinginezo:
JINSI YA KUJIWEKA KARIBU NA MUNGU.
Hakuna kitu kinachomtamaisha Mungu kama kujiweka karibu na sisi, tunalithitisha hilo katika maandiko haya “Yakobo 4:5 Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?” Unaona? lakini kwa bahati mbaya sisi ndio hatujui kanuni ya jinsi ya kujiweka karibu na Mungu..Na ndio maana tukiendelea mbele kidogo maandiko yanasema:..
Yakobo 4:8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi…
Unaona biblia inatupa ufahamu mwepesi wa namna ya sisi kuwa karibu na Mungu, nao ni kwa kumkaribia tu.. Watu wengi wanadhani wanaweza kuwa karibu na Mungu, au Mungu kuwa rafiki yao wa karibu wakiwa katika hali zao zile zile za kale, na mienendo ile ile wanayoiendea kila siku, na huku hawataki kuonyesha jitihada za kumkaribia Mungu, ndio hapo mwisho wa siku wanaona kama vile Mungu hana faida yoyote maishani mwao, au wanaona kama vile amekufa hayupo, au hawasikii, au hawajali…yote hiyo ni kwasababu hawajajua namna ya kumkaribia Mungu..
Tukiendelea kusoma ule ule mstari unasema…
Yakobo 4:8 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.
Unaona anatoa kanuni kadha wa kadha hapo ya kwanza na ya msingi ni:
Ukiwa mwenye dhambi, yaani kwa ufupi ukiwa hujaokoka, kamwe hutakaa umkaribie Mungu kwa namna yoyote ile, haijalishi, unatoa zaka kiasi gani, haijalishi unasaidia yatima kiasi gani, haijalishi, unahudhuria ibadani kiasi, maadamu upo nje ya Kristo, tayari wewe upo mbali sana na Mungu. Hivyo hatua ya kwanza na ya msingi ya Mungu kukuribia ni kutubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi zako zote, kumwambia Bwana Yesu akusamehe dhambi zote ulizomkosea, kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi Kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38, kisha kupokea Roho Mtakatifu. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeshakamilisha hatua ya kwanza ya kumkaribia Mungu..
Wapo watu baada ya kumpa Kristo maisha yao, bado wanayatamani mambo yale yale waliyoyaacha kule nyuma, sasa watu kama hao Mungu hawezi kuwakaribia kwasababu mioyo yao inakuwa imegawanyika, nusu kwa Mungu, nusu kwenye dunia..Ikiwa umedhamiria kweli kumfuata Kristo mfuate kwa kumaanisha kweli kweli, acha kila kitu mfuate, na hiyo inakuja kwa kujikana nafsi yako na kujitwika msalaba wako na kumfuata, unakuwa tayari kukubali kuchekwa, au kudharauliwa, au kutukanwa au kufanyiwa jambo lolote baya kwa ajili ya imani yako bila kutetereka..Na Mungu akishaona moyo wako upo thabiti kwake, hapo ndipo na yeye anaongeza hatua yake nyingine ya kukukaribia.
Tena anaendelea kusema.. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu…Hii haimaanishi kuwa ujifanye kuwa mtu wa huzuni kila saa, kama vile mfiwa hapana, bali unaugua kwa kuchukia dhambi, unaomboleza kwa mabaya yanayofanyika, sio unafurahia kuona ubaya, au dhambi zikifanyika, Na kwa kawaida kuugua pamoja na maombolezo kunazaa pia na kuombea wengine, na kuliombea kanisa lote kwa ujumla..na kuwashuhudia wengine habari njema..Sio pale tunapokuwa wakristo ndio basi tena, maadamu sisi tumeshaokolewa hayo mengine hayatuhusu…Tukiwa watu wa namna hiyo basi vilevile tufahamu kuwa Mungu naye atakuwa mbali na sisi lakini kama tukiwa tunahuzunika na kuomboleza kwa ajili yetu sisi na kwa wengine ili waokolewe, na kuchukua hatua stahiki basi tufahamu kuwa Mungu hapo atakuwa tena karibu zaidi na sisi, kwasababu tunaichukua ile huzuni yake tunaifanya ya kwetu..Mungu hafurahii maovu, wala hapendi mtu hata mmoja apotee.
Kwa namna ya kawaida hakuna mtu asiyempenda mtu mnyenyekevu, Vivyo hivyo na kwa Mungu tukiwa watu wanyenyekevu watu wa kujishusha mbele zake, watu tunaoungama makosa yetu, basi tutamvuta kwa haraka sana aje karibu sana na sisi kama ilivyokuwa kwa Daudi..Lakini tukijiona sisi kila kitu tunajua, hatutaki kuambiwa chochote, hata kama ni kweli, tunajiona tunajua biblia sana, dini zetu na madhehebu yetu yanatutosheleza kama vile mafarisayo na waandishi walivyokuwa, kwa kiburi chao walimkosa Mungu, walidhani wapo karibu na YEHOVA kumbe walikuwa hatua mia mbali na yeye.
Faida kubwa ni kuambukizwa ule utukufu wake, kama tu vile pale unapokaa karibu na mtu aliyejipulizia marashi makali kwa muda mrefu akiondoka ile harufu bado itabakia katika mwili wako..Vivyo hivyo na kwa Mungu ikiwa umezifuata hizo hatua zote basi ule utukufu wa Mungu unaingia ndani yako, kama vile Musa alivyokaa uweponi mwa Mungu kwa siku zile 40 kule mlimani, aliposhuka uso wake uling’aa kama vile wa malaika..Ni kwasababu alikuwa karibu sana na Mungu…Lakini sisi hatung’ai uso wa mwilini bali uso wa rohoni..
Matokeo yake ni kuwa jambo lolote tutakalomwomba Mungu tutatendewa…
Yohana 15:7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Vilevile wewe utakuwa ni wa kwanza kuzipokea zile siri za ndani kabisa za Mungu, kwasababu wewe ni bibi-arusi wa Kristo, na sikuzote bibia-arusi ndiye anayejua siri ya Bwana arusi, halikadhalika hakuna jambo lolote au adui yoyote atakayekushida kwasababu muda wote unaonekana kama miale ya moto duniani..Vilevile Mungu anakufanya kuwa chombo chake kiteule cha kuwachunga kondoo wake wengine.
Hizo ndio faida zake kuu. Kwanini tusitamani kuwa karibu naye? Tufanye bidii sote tufike hapo. Amen.
Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
NITAFUNGUAJE MILANGO ILIYOFUNGWA MBELE YANGU?
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
SWALI: Tukisoma Kutoka 34:1-5 Tunaona Musa anaambiwa atengeneze mbao mbili za mawe mfano wa zile za awali. Sasa swali ni kwanini ziwe mbili na sio moja au Zaidi? Na ni kwanini ziwe mbao za mawe. Je kuna ufunuo wowote kuhusu hilo?
Sababu kuu ya Mungu kuzichonga kwenye mawe na si penginepo ni kuonyesha uthabiti na ubora wa sheria zake., kumbuka kitu chochote kinachochongwa katika mwamba ni tofauti na kile kinachochorwa katika karatasi au kinachochongwa katika ubao..Mwamba wakati wote ni mgumu hivyo hata kile kinachochonga kitahitaji jitihada Zaidi katika kuchongwa, Japo inatumia nguvu zaidi na gharama lakini faida yake mwisho wa siku inakuwa ni kubwa, nayo ni UBORA..tofauti na kile kinachochorwa katika katarati ambapo kifuto kikipita kidogo tu maandishi yale yanafutika na kazi yote inakuwa bure, au kile kinachochorwa katika mbao ambacho nacho pia moto kidogo tu ukipita kazi yote inateketea na kumbukumbu lote kufutika….Lakini mwamba hata moto ukipita, ndio kwanza inazidi kuwa imara Zaidi, Na ndio maana utaona baada ya pale zile mbao mbili za mawe zilidumu kwa maelfu ya miaka mbeleni..
Kufunua kuwa upo ubao ulio mgumu Zaidi ya mwamba, ambapo Mungu aliuweka tayari huko mbeleni kuandika amri zake zisizoweza kufutika milele..na ubao huo si mwingine Zaidi ya moyo wa mwanadamu, huo ni bora Zaidi ya mwamba wowote duniani…Mungu akishaandika sheria zake ndani ya mwaminio, haziwezi kufutika tena milele, wala kupotea, kama ilivyokuwa katika agano la kale watu walikuwa wakizisahau sahau mpaka wakumbushwe vilevile vibao vile vilikuja kupotea baadaye na wala kumbukumbu lake halijulikana lilipo mpaka leo…
Yeremia 31:31 ‘’Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena’’.
Waebrania 10:16 ‘’Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo’’,
Unaona huo ndio ubora wa agano jipya..Sheria ile inaandikwa juu ya vibao vya mioyo yetu kwa sisi tulioamini isiyoweza kuharibiwa au kufutwa na mtu yeyote milele.. Hivyo kama wewe upo nje ya Kristo, mlango wa neema bado upo wazi, lakini hautakuwa wazi hivyo milele..Mkaribishe leo ndani ya maisha yako, kwa kutubu na kuacha dhambi zote, kisha baada ya hapo ataanza kukutengeneza na sheria yake ataiandika moyoni mwako, na wala dhambi haitakushinda milele, kwasababu sheria hiyo imechorwa ndani ya vilindi vya moyo wako asipoweza mtu wala shetani kuifikia na kuifuta…sheria hiyo itakulinda mpaka siku ile ya kwenda mbinguni katika Unyakuo.
Tubu dhambi zako sasa, nawe uufurahie wokovu, na neema ya bure ya BWANA YESU.
Fahamu kuwa zile amri kumi za Mungu ziliganyika katika mafungu makuu mawili, la kwanza ni Upendo kwa Mungu wetu, na la pili Ni upendo kwa jirani zetu kama nafsi zetu..Hakuna shaka zile nne za kwanza zilikuwa katika ubao mmoja unaojitegemea ambazo zinamuhusu Mungu, na zile sita za pili zilikuwa katika ubao wa pili ambazo zinatuhusu sisi, …
Na hiyo ndio mihili mikuu miwili hata katika agano jipya ambayo tunapaswa tutembee nayo, hizo ndizo mbawa zetu mbili tunapaswa turuke nazo kila siku, ya kwanza ni hiyo ya kumpenda Mungu, ambapo tukimpenda Mungu tutafanya yote anayotuagiza, na ya pili ndio hiyo tuwapende jirani zetu kama nafsi zetu tukiwapenda ndugu tutasitiri wingi wa dhambi, na kila tendo ovu dhidi ya majirani zetu na jamii kwa ujumla….Hatuwezi kuruka na mbawa mojawapo katika ya hizo, bali zote mbili zinakwenda pamoja..
Ubarikiwe sana..jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.
FIMBO YA HARUNI!
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Utauliza kuna nyimbo za wokovu?. Jibu ni Ndio! Uimbaji ni moja ya karama za Roho kama zilivyo karama nyingine, kama vile Uchungaji, Unabii, ualimu, uinjilisti n.k.
Na kama vile kulivyo na manabii wa uongo, na waalimu wa uongo na wainjilisti wa Uongo. Kadhalika pia kuna WAIMBAJI WA UONGO. Tabia zinazoonekana kwa manabii wa Uongo ndio zile zile zilizopo kwa waimbaji wa uongo.
Manabii Uongo wanapenda fedha. Na ndivyo ilivyo kwa waaimbaji wa Uongo. Nabii wa uongo hatahubiri wokovu hata siku moja. Bali atahubiri anavyojua yeye ilimradi tu, asiwaudhi watu ili wawe wepesi kufungua pochi zao na kumpatia chochote. Hawataweza kuvumilia kamwe kufanya kazi ya Mungu bila kupata malipo yoyote kutoka kwa waumini. Na wanajua kitu pekee kitakachomgeuza mtu na kuwa mkristo ni kumwambia kweli yote ya Biblia.
Waimbaji wa uongo nao ni hivyo hivyo. Kamwe hawataimba nyimbo za wokovu, za watu kutubia dhambi zao na maonyo ya siku za mwisho. Bali wataimba nyimbo za kuwafariji watu hata katika hali za dhambi walizopo. Lengo kuu na madhumuni ni ili wasiwaudhi mashabiki wao na hivyo wakakosa soko/fedha kwa nyimbo zao. Wanajua wakimhubiria mtu wokovu, mtu yule hatafikiria habari za kumpa yeye fedha. Bali atafikiria habari za kuyatakasa maisha yake. Mtu atatoka pale amechomwa moyo wake na mwenye moyo mzito, kitu ambacho wao hawakitaki. Kitawakoseshea mapato. Watakula nini??
Na Waimbaji wa uongo ni hivyo hivyo. Leo utaona mtindo fulani umetoka nao pia wamo. Tofauti yao na watu wasanii wa ulimwengu huu haipo. NI WASANII, Kuimba kwao ni SANAA na sio Injili. Malengo yao ni kuwa waimbaji maarufu duniani na sio kitu kingine. Lakini muhubiri wa kweli au mwimbaji wa kweli lengo lake sio kuwa maarufu duniani. Au sio kujulikana duniani kote bali ni kuhakikisha injili inajulikana na watu wote, inawafikia watu wote duniani. Watu watubu na kuokoka na kuacha dhambi na kumgeukia Kristo na kwenda mbinguni. Hiyo ndiyo raha ya mhubiri au mwimbaji wa kweli wa nyimbo za wokovu.
Na kama uimbaji ni moja ya karama za Roho Mtakatifu. Viwango vya Roho ni vile vile. Bwana Yesu alisema mtu yeyote akitaka kuwa mwanafunzi wangu.. “ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake anifuate. (Mathayo 16:24)”. Uanafunzi sio tu uchungaji, au uinjilisti au ualimu..bali ni pamoja na uimbaji.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.”
Umeijua Injili ya kweli. Lakini bado huimbi nyimbo za wokovu na badala yake unaimba tu nyimbo za kuwaburudisha watu. kiasi kwamba hata wakiwa bar! wanaona faraja tu kuipiga au kuisikiliza nyimbo yako. Fahamu kuwa kwako vitatakwa na vya ziada.
Na sifa nyingine ya mwisho ya Mwimbaji wa uongo, ni kufanya kazi kwa kutegemea malipo. Kwamfano utasikia mwimbaji fulani hataki kuimba mpaka ahakikishiwe kiwango fulani cha fedha. Akiahidiwa kiwango kidogo hasimami kuimba. Ukiona mwimbaji yupo hivyo basi fahamu kuwa ni mwimbaji wa uongo.
Ulishawahi kuona wapi, mchungaji anaalikwa kwenda kuhubiri kwa kuahidiwa kiwango fulani cha fedha?. Au mwinjilisti gani anakwenda kuhubiri huku tayari kashapambana na bei ya kupanda madhabahuni. Sasa kama wachungaji ambao karama zao zimewekwa wazi kwenye maandiko hawafanyi hivyo kwanini wewe unayejiita mwimbaji ufanye hivyo?. Huoni kama kutakuwa na kasoro kubwa sana kwako?.
Bwana atusaidie sana. Kama ulikuwa ni mmoja wapo wa wanaofanya hivyo, au wenye malengo ya kufanya hivyo. Na ulikuwa hujui kama ni makosa. Mlango wa kutubu bado upo wazi. Kutubu maana yake ni kugeuka kuacha kile ulichokuwa unakifanya kisicho sawa. Ukiamua tu kugeuka na kuamua kumwimbia Mungu NYIMBO ZA WOKOVU na sio NYIMBO ZA KUSAKA PESA. Bwana atakupokea, Kwasababu hizi ni siku za mwisho ambazo biblia imetabiri kuinuka kwa wimbi kubwa la manabii wa uongo, Ikijumuisha huko huko na waimbaji wa uongo na waalimu wa uongo na waachungaji wa uongo. Bwana akusaidie usiwe miongoni mwao, Bwana atusaidie tusiwe miongoni mwao.
Maran atha!jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Je! katika biblia mstari huu una maana gani? ”Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza’’? (Mithali 11:1)? ..Hiyo mizani ya hadaa ni ipi?
JIBU: Katika maisha ya kawaida Bwana anataka tuwe na haki, katika mambo yetu tunayoyafanya kila siku iwe ni katika biashara zetu au kazi zetu…Unapouza kitu uza kulingana na thamani ya kitu chenyewe unachouza, usizidishe thamani ya kitu kile ili upate faida kubwa vile vile usipunguze kipimo cha kitu kile ili upate faida kubwa…
Kwa mfano kama wewe ni muuzaji wa mchele, na umenunua kilo moja kwa shilingi elfu mbili, na bei inayoziwa sokoni ni shilingi elfu na mia tano kwa wateja…Na unajua kabisa faida yako inapaswa iwe ni shilingi mia tano kwa kila kilo, au ikizidi sana mia 7.
Lakini wewe unakwenda kuuza kwa bei ya juu kuliko inavyotakiwa ili wewe upate faida kubwa bila kujali kuwa unamkandamiza yule unaye muuzia kisa tu anaouhitaji mkubwa wa kitu hicho..Labla tuseme unauuza mchele ule kwa shilingi elfu 4 kwa kilo moja..Hivyo kwa kufanya hivyo, Ni machukizo kwa Bwana. Hiyo ni mizani ya hadaa, hutendi haki.
Vilevile Bwana hapendezwi na kupunguza kipimo cha bidhaa ile kwa hila, kwamfano unapunguza kwa makusudi kiwango cha upimaji, aidha katika mizani yako ili usiuze kingi upate faida kubwa..Hilo nalo ni chukizo kwa Bwana…Hiyo nayo ni mizani ya hadaa, hutendi haki.
Vilevile katika kazi nyingine zote tunazozifanya iwe ni kwa Mungu, au mashuleni, au mahakamani, tunapaswa tuamue kwa haki bila kumpendelea mtu, kwa kutokujali fedha, au heshima, au cheo, au jinsia,..Bwana anapenda haki, na palipo na haki ndipo kiti chake cha enzi kilipo…..(Zaburi 97:2)
Zaburi 89: 14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
Na ndio maana biblia inasema .. Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. (Mathayo 5:48)
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TWEKA MPAKA VILINDINI.
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
UNYAKUO.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Nifanye nini ili niifungue milango iliyofungwa mbele yangu?
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Moja ya mada inayozungumzwa na wakristo wengi hususani wa kanisa hili la Mwisho ni juu ya namna ya kufungua milango iliyofungwa mbele yetu.
Na kwa haraka haraka wengi wetu tunatafuta njia za haraka haraka ilimradi tu, Milango iliyopo mbele yetu ifunguke. Ndio hapo utaona baadhi wanaenda kwa watumishi wawaombee, wengine watatafuta mahali panapouzwa Mafuta fulani, au maji fulani ya baraka au upako. Wengine watakwenda kutafuta kwa kuombewa nyota zao na kutabiriwa. Na mambo mengine mengi yanafanyika katikati ya wakristo. Na Bahati mbaya wengi baada ya kufanya hivyo hali inabakia kuwa vile vile. Ni kwanini?. Ni kwasababu hiyo sio njia au Namna Mungu aliyoiweka ya kufungua milango iliyofungwa mbele yetu.
Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.”
Kumjua Mungu maana yake ni kutafuta maarifa ya kujua ni nini Mungu anataka, Yakikosekana maarifa ya kumjua Mungu ni rahisi sana kuangamia.
Sasa leo kwa ufupi sana tutatumia biblia kujua namna yakufungua milango iliyopo mbele zetu. Na pia kumbuka kabla ya yote kuwa sio kila mlango uliofungwa mbele yako. Ni shetani kahusika! Hapana mingine ni Mungu mwenyewe kaifunga kwaajili ya makusudi yake. Na tunajua makusudi ya Mungu siku zote ni Mema. Hivyo tutazungumzia kwa ujumla namna ya kufungua milango yote (Iliyofungwa na Mungu au shetani)
Ufunuo 3:7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, KWA KUWA UNAZO NGUVU KIDOGO, NAWE UMELITUNZA NENO LANGU, WALA HUKULIKANA JINA LANGU”.
Kwanza tunaona hapo kumbe Kristo anaweza kufunga kitu na hakuna awezaye kukifungua..Na pia anauwezo wa kufungua na hakuna awezaye kuufunga. (Hiyo ni point ya kwanza ya kuweka akilini). Ili tufahamu kuwa sio kila mlango uliofungwa mbele yetu ni shetani kahusika. Hapana bali mengine ni Kristo mwenyewe ndiye aliyehusika.
Lakini tukiendelea na mstari wa 8 ndio tutapata majibu ya swali letu. “Tutafunguaje milango iliyofungwa mbele yetu?”.
Bwana Yesu mwenye ufunguo wa mambo yote anaanza kwa kusema…Nayajua matendo yako!. Ikifunua kuwa mlango kufunguliwa au kufungwa unahusiana na “Matendo ya Mtu”..Anaendelea na kusema “nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, KWA KUWA UNAZO NGUVU KIDOGO, NAWE UMELITUNZA NENO LANGU, WALA HUKULIKANA JINA LANGU”
Umeona sababu za huyu mtu kufunguliwa mlango?. Sababu zipo tatu.
Ya kwanza Kwa kuwa anazo nguvu kidogo. Ya pili Kwa kuwa amelitunza Neno lake. Na ya tatu Hakulikana jina lake.
Kristo hajabadilika sababu zile zile alizozitumia kale ndizo anazozitumia leo kufungua milango iliyofungwa mbele yetu.
1 Yohana 2: 14 “….Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na Neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”. Kuliweka Neno la Mungu ndani yetu ndio NGUVU ZA ROHONI. Mtu asiye na Neno la Mungu ndani yake, nguvu zake za rohoni zipo chini sana. Na kumbuka kuliweka Neno moyoni sio kujua vifungu vingi vya Biblia, kwa kuikariri. Hapana bali kuliweka Neno la Mungu moyoni ni kuliishi Neno moja lililoandikwa katika biblia. Ni kuona matokeo ya lile Neno katika maisha yako.
Kwamfano biblia inaposema “wapendeni Adui zenu, waombeeni wanaowaudhi..Mathayo 5:44”. Kama mtu kaushika huo mstari kwa kuukariri na hautendei kazi hicho kilichoandikwa hapo. Mtu huyo hajalishika Neno la Mungu moyoni mwake, lakini kama anakitendea kazi kwa kuwaombea wengine huyo kaliweka moyoni Neno la Mungu.
Kulitunza ni tofauti kidogo na kuliishi. Kulitunza maana yake unalitenda lile Neno kila siku katika maisha. Sio leo unalitenda kesho unaliacha.
Maana yake ni kutoikana Imani. Kulikana jina la Mungu na kuikana Imani ni kitu kimoja. Kuikana Imani kunajumuisha kurudi nyuma kiimani. Petro alimkana Bwana Yesu maana yake alirudi nyuma kiimani. Kadhalika mtu anayerudi nyuma kiimani ni sababu tosha ya kujifungia milango ya Baraka mbele yake.
Ndugu hatupaswi kukimbilia maji ya Upako kupata kibali mbele yetu. Au kupata fursa Fulani mbele yetu. Njia pekee ya kupata fursa ya kitu Fulani ni kurekebisha MATENDO YETU na KULITUNZA NENO LA MUNGU maishani mwetu. Na ndipo hayo yote yaliyosalia uliyokuwa unamwomba Mungu yanafunguka.
Kama ulikuwa hujampa Kristo maisha yako, unageuka sasa kwa kudhamiria kuacha dhambi kabisa. Na humfuati kwasababu tu unataka fursa Fulani. Hapana bali kwasababu umejigundua wewe ni mwenye dhambi na unahitaji kubadilishwa. Na Kristo mwenyewe anapenda watu wanaotubu dhambi zao na kukiri kuwa ni wakosaji. Yeye anawapa msamaha bure wote wanaokimbilia kwake haijalishi wameasi kiasi gani. Na baada ya kupata msamaha huo ambao utaambatana na AMANI Fulani moyoni isiyokuwa ya kawaida. Moja kwa moja usikawie nenda kakamilishe wokovu wako kwa kubatizwa katika maji tele(Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu kulingana na (Matendo 2:38). Na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu ambaye atakuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko na kukusaidia kushinda dhambi ambazo ulikuwa huwezi kuzishinda kwa nguvu zako.
Hapo utakuwa umeokoka kwa kuzaliwa mara ya pili. Na utakuwa na tumaini la uzima wa milele. Na kwasababu umeupata kwanza ufalme wa Mungu na Haki yake. Na hizo fursa na milango iliyofungwa ambayo umekuwa ukiitabikia kwa muda mrefu itafunguka yenyewe pasipo stika wala chumvi.
Mada Nyinginezo:
DANIELI: Mlango wa 2
MIHURI SABA
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?
Nitamtambuaje bibi arusi wa kweli?
Shalom.
Ni vizuri tukafahamu kuwa katika ukristo yapo makundi matatu ya waaminio. Tukilielewa hilo itatusaidia sisi kujipima tupo katika kundi lipi. Na hatua zipi tuchukue ili tusimame katika upande salama.
Ni kundi la watu wanaojiita wakristo, hawa wanaweza wakawa wamezaliwa katika familia za kikristo au walioupokea ukristo kama dini yao mpya tu,. Au kama kitambulisho chao tu, Na kuwatambua hawa ni rahisi, huwa hawana habari na Mungu hata kidogo, kinachowatofautisha tu wao na ulimwengu ni hicho kitambulisho cha kikisto walichozaliwa nacho au walichokipokea basi.
Lakini mambo mengine yote yaliyosalia hayana tofuati na watu wengine wote wasiomjua Mungu, ukimuuliza Je! unajua kama unyakuo upo karibu atakwambia sifahamu unazungumzia nini. Ukimuuliza Je umeokoka atakwambia hiyo dini siijui..hana habari na ibada wala, wala kitu chochote cha ki-Mungu yupo tu, kama wapagani, lakini anajivunia ukristo wake. Na hawa wapo wengi sana.
Ni kundi la wakisto ambao wanaamini kila kitu, wanafahamu kila habari katika maandiko. Wanahudhuria ibadan, lakini ni vuguvugu, nusu kwa Mungu, nusu kwa shetani, Biblia inawafananisha hawa na wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika Mathayo 25..Na kwa jina lingine wanajulikana kama Masuria, hawana muunganiko rasmi na Kristo.
Hawa ndio siku ile watakapojigundua wameachwa katika unyakuo ndio watakaolia n kuomboleza, kwasababu nao pia walikuwa wanamtazamia Kristo lakini kwasababu ya kuwa vuguvugu, wataachwa..Na hawa pia wapo wengi katika kanisa.
Ni Wakristo ambao wamedhamiria kweli kuifuata njia ya Kristo. Ukristo sio dini yao, bali ni Imani yao. Hawa ndio wale wanawali werevu waliotwaa taa zao pamoja na mafuta ya ziada katika vyombo vyao vya pembeni..Na hawa ndio bibi arusi wa Kristo, ambao Kristo anawaandaa katika kila kipindi cha Kanisa..Na hawa ni wachache sana katika Kanisa.
Jambo la muhimu la kufahamu ni kuwa kati ya haya makundi matatu ya wanaojiita wakristo, ni kundi moja tu ndilo litakalonyakuliwa kwenda mbinguni..Nalo ndio hilo kundi la tatu. Bwana YESU leo hii hatafuti Masuria, wala watu walio baridi, bali anamwandaa bibi arusi wake haijalishi atakuwa ni mmoja au mia au elfu hilo halijalishi idadi yake ikishatimia haangalii ulimwengu mzima unafikiri vipi. Watanyakuliwa na kwenda mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo
Kama wengi wetu tunavyofahamu Ile habari ya Ibrahimu kwenda kumtafutia mwanawe Isaka mke katika nyumba ya baba yake. Ni habari inayofunua siri ya Kristo na bibi arusi wake jinsi atakavyompata katika siku za mwisho. Sasa tukisoma ile habari tunaona ulifika wakati Ibrahimu aliona mwanawe Isaka ameshakuwa mtu mzima. Na mama yake ameshafariki,hana mtu wa kumfariji, akaona ni vema akamtafutie mwanawe binti wa kuoa,..Ndipo akamtuma mtumwa wake alimwamini sana katika mali zake zote aliyeitwa Eliezeri afunge safari pamoja na Ngamia 10 watoke katika nchi ya Kaanani waende mpaka Mesopotamia nchi ya Baba yake,..asafiri umbali mrefu kusudi tu ampatie mwanawe mke aliye bora…
Na Ndivyo Mungu alivyofanya kwa mwanawe mpendwa YESU KRISTO, Hakumtafutia bibi Arusi wake safi kutoka katika kanisa la Israeli badala yake alikuja mbali kwa watu wa mataifa yaani mimi na wewe ili kututwaa tuwe pamoja naye katika kiti chake cha enzi..
Sasa Eliezeri akafunga safari mamia kwa mamia ya kilometa akiwa na ngamia zake 10 pengine alitumia wiki kadhaa au miezi kusafiri. Ndipo akafika karibu na nchi ile, nje kidogo na mji ambapo pana kisima cha maji ambapo mabinti wengi wa mji wanakitumia wakati wa jioni kuja kutweka maji. Kwa ajili ya shughuli za nyumbani.
Kama tunavyosoma habari ile, Eliezeri alimwomba Mungu ishara, akasema binti Yule nitakayemwomba maji ya kunywa katika mtungi wake, na kusema sitakupa tu wewe bali nitanyesha mpaka na ngamia zako basi huyo na awe mke wa mwana wa bwana wangu..Biblia inatuambia wakati wazo hilo bado lipo katika kichwa chake muda huo huo akatokea binti pale kisimani, kuchota maji tusome..
Mwanzo 24: 12 “Naye akasema, Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu.
13 Tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji,
14 basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu.
15 Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake.
16 Naye yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake, bikira, wala mwanamume hajamjua bado; akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.
17 Ndipo yule mtumishi akapiga mbio kwenda kumlaki, akasema, Tafadhali unipe maji kidogo katika mtungi wako ninywe.
18 Naye akasema, Unywe, bwana wangu, akafanya haraka, akatua mtungi wake mkononi mwake, akamnywesha.
19 Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa.
20 Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote”.
Ukiendelea kusoma utaona Yule mtu ndipo alipopata uhakika kuwa huyu binti ndiye Mungu aliyemkusudia kuwa bibi arusi wa Isaka. Ni rahisi kuona kama alimwomba Mungu ampe ishara nyepesi, lakini ile haikuwa ishara ndogo kama ukichunguza vizuri, kwa mazingira yale yaliyokuwepo.
Embu jaribu kufikiria Yule alikuwa ni mtoto wa kike, pili alikuwa na mtungi mmoja tu mdogo labda tuseme wa lita 10 ambayo ni sawa na ndoo moja ya maji. Na unaambiwa ngamia ni mnyama anayekunywa maji haraka sana zaidi ya wanyama wengi, ndani ya dakika tatu tu tayari kashamaliza lita 200 za maji..Hivyo ilihitajika mitungi/ndoo 20 za maji kukata kiu ya ngamia mmoja..Ukizingatia ngamia walikuwa 10 pale, hivyo kama ni kuwanyeshwa ngamia basi inakugharimu si chini ya ndoo 200, kushuka kisima na kupanda kuwashibisha ngamia wote..Hilo sio zoezi ndogo..
Kwa wakati ule ilikuwa ni rahisi sana kusaidiwa kunyeshwa kondoo zako 100 za maji na mbuzi zako lakini si ngamia. Tena ilikuwa inafanywa na wanaume si wanawake..Hivyo Eliezeri kumwomba Mungu ishara kama ile, alitambua kabisa kwa namna ya kawaida ni kama haiwezekani…Lakini msichana Rebeka hakujali hilo, kwa jinsi roho ya kujali ilivyokuwa imejaa ndani yake.
Alikwenda hivyo hivyo alishuka kisimani, akapanda mpaka mitungi yote mia mbili akaimaliza. Na Eliezeri hakufanya chochote, wala hakumsaidia bali alikuwa anamwangalia tu, labda kama atakata tamaa katikati ya safari, aseme sio huyo, asubirie mwingine kuja kuchota maji lakini Rebeka alichota maji ndoo zote labda 200 mpaka akamaliza..
Je! jiulize wewe binti wa kike unaweza ukafanya ukarimu kama huo kwa mtu usiyemjua ikiwa tu kumpisha mzee kwenye daladala ni shida itakuwaje kwa kazi kama hiyo?. Hata kwa kulipwa tu unaweza usifanya..Na kumbuka Rebeka alikuwa ni mzuri wa uso sana, kuwazidi wengi. Lakini hakujali hilo.Hapo ndipo Eliezeri akapata uthibitisho sasa kuwa huyu Rebeka ndio bibi arusi mwenyewe..Ukiendelea kusoma habari utaona hadi alipochuliwa na kuletwa Kaanani kwa mume wake Isaka.
Kumbuka Eliezeri anasimama kama kundi la watumishi wote wa Mungu ambao wametumwa ulimwenguni kote kuhubiri Injili. Kumtafutia Kristo bibi arusi safi wa kwenda naye mbinguni kwenye karamu ya mwana-kondoo.Kama Mtume Paulo anavyosema katika..
2Wakorintho 11: 2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi”.
Na watumishi wa Mungu pia wamepewa ishara ya kuwatambua bibi Arusi hao, na Ishara yenyewe ni kama ile ya Rebeka..Ndugu Tukijiona tunahubiriwa injili lakini tunaishia tu kwenye kile tunachoambiwa, labda tuseme tutubu au tubatizwe , halafu baada ya hapo basi, hatuonyeshi bidii zetu binafsi za kuthibitisha wito wetu kwa Mungu..Basi tujue kuwa sisi bado sio bibi arusi wa Kristo.
Kama Sisi wenyewe binafsi hatutaki kumtafuta Mungu wetu atufundishe zaidi. Hatutaki kuomba wenyewe bila ya kushurutishwa, tunangojea tu tufundishwe biblia jumapili kwa jumapili sisi hatuna muda na mambo hayo tunaendelea na shughuli zetu. Basi tujue sisi tutakuwa ni Masuria tu, wale wanawali wapumbavu, Unyakuo utakapopita tutabaki hapo..
Bibi arusi kama Rebeka haridhiki na hali ile ile aliyopo kwa muda mrefu, anafanya zaidi ya yale anayoelekezwa na kuambiwa. Soma habari ile ya wanawali 10 utaona wale werevu walijiongeza, kutafuta mafuta ya ziada kwa ajili ya TAA zao. Kwasababu walijua yale pekee hayawatoshi. Usitegemee kuhubiriwa tu peke yake.
Ndugu hizi ni siku za hatari, watakaonyakuliwa ni wachache sana, tuombe Mungu na vilevile tuongezee bidii zetu binafsi ili tustahili kuwa miongoni mwa bibi arusi wa Kweli wa Kristo.
Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
UNYAKUO.
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
Biblia inamaanisha nini kusema Yeye aliye na sikio, na asikie?
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
Tuingie kwa kupitia mlango ulio mwembamba. Shalom. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuyatafakari pamoja maandiko…Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo katika kitabu cha Luka..
Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu.
23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”
Moja ya sentensi zinazoogopesha ambazo Bwana Yesu alizizungumza ni hii..Nyingine ni ile ya Mathayo 12:31 anayosema…“ Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.”
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Sentensi hizi tatu alizozizungumza Bwana Yesu kama ukizitafakari kwa makini zinaogopesha sana..Sio za kuzichukulia kiwepesi wepesi kabisa.. Ni sentensi nzito sana. Na kama tunavyojua Bwana Yesu anachokisema siku zote ni lazima kije kutimia. Alimwambia Petro kabla Jogoo kuwika utanikana mara tatu…Na tunaona masaa machache tu mbeleni unabii huo ulitimia kama ulivyo. Kadhalika aliposema siku ile wengi watakuja na kumwambia Bwana Bwana hatukutoa pepo, hatukufanya unabii. Hatukufanya miujiza mingi kwa jina lako Ni kweli siku hiyo itafika na watakapokuja maelfu ya watu mbele zake na kusema hayo maneno hivyo hivyo.
Watakuwepo wahubiri wengi siku hiyo watakaosema maneno hayo mbele zake na Bwana atawakataa. Hivyo ni kujitahidi kuwa makini sana na kumwomba Bwana atusaidie siku zote hao watu wasiwe sisi. Kwasababu hakuna wa kusalimika hapo kama Neema yake haitahusika.
Lakini leo tutaitafakari sentensi hiyo ya kwanza ambayo alisema “Tujitahidi kuingia katika mlango ulio mwembamba”.
Luka 7:13 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Hapo kuna vitu viwili NJIA na MLANGO..Na anasema njia ni nyembamba, maana yake hiyo huwezi kupita kwa kifaa chochote kama gari au pikipiki. Wala hamwezi kupita ukiwa na mizigo, wala hawezi kupita mkiwa makundi. Ni mtu mmoja mmoja, kwasababu . Ulishawahi kupita kichochoroni na gari? Au na pikipiki?. Au ulishawahi kupita kichochoroni mkiwa mmeshikana mikono watu sita au 7 kwa pamoja?. Ni wazi kuwa hicho kitu hakiwezekani. Kwasababu njia ni nyembamba. Inahitajika apite mmoja mmoja. Na tena akiwa hana mizigo mizigo.
Kadhalika njia ya wokovu, ni habari ya mtu mmoja mmoja. Sio mtu na mke wake. Au mtu na baba yake. Inahitajika mtu kujikana nafsi peke yake na kuamua kumfuata Yesu. Na pia tunapomfuata Yesu yeye ni njia nyembamba hauendi na dini yako. Wala dhehebu lako litakalokusaidia kupita katika huo uchochoro. Unaweka dhehebu lako pembeni, dini yako pembeni. Unachukua msalaba wako unamfuata kama ulivyo.
Maana yake mwisho wa hiyo NJIA nyembamba ya uchochoro ulio mwembamba utakutana na mlango. Na huo mlango pia ni mwembamba vile vile kama hiyo NJIA. Hapo ndipo Bwana anatuambia tujitahidi. Uchochoro utapita bila gari, bila baiskeli, bila pikipiki lakini mlangoni je?.
Hapo Itakubidi upunguze hata mwili. Kwasababu pengine mwili wako ukiwa mkubwa sana unaweza ukakwama mlangoni. Hivyo ili uingie itahitajika hata upunguze baadhi ya viungo..Ndio maana Bwana Yesu alisema.
Kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate, Ni heri uingie katika ufalme wa mbinguni ukiwa kilema kuliko kuwa mzima na kuishia jehanamu.
Mathayo 5:30 “Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum”.
Hizo ndizo gharama! Na sio rahisi zina ugumu wake ndio maana Bwana hapo juu kasema TUJITAHIDI! Maana yake tufanye bidii kwa hali na mali tupite mlangoni. Tukitia Nia yeye katuahidi kutusaidia katika (Mathayo 19:26).
Je ni mali zako ndio zinazokukosesha na kukuzuia wewe kumtafuta Mungu? Ziweke pembeni kwa muda. Mtafute Kwanza Mungu na hizo zitakutafuata zenyewe baadaye. Je ni ndugu ndio wanaokuzuia kumgeukia Mungu na kufanya mapenzi yake?. Ikumbuke njia ile ni Nyembamba haiwezekani kupita makundi. Bwana Yesu alisema “apendaye Baba au mama kuliko mimi hanifai (Mathayo 10:37)”. Waambie ndugu zako kwa upendo, sasa umeokoka umeamua kumfuata Yesu kwa gharama zote.
Chochote kile kinachotuzuia kuingia katika ufalme wa Mbinguni sasa tunapaswa tujiepushe nacho, ili tukidhi vigezo vya kuingia katika huo mlango ulio mwembamba. Na hatupaswi kukawia kwasababu pale juu amesema. Utafika wakati mlango huo mwembamba utafungwa..Na watu watatamani kuingia watashindwa. Maisha ya ukristo ni Maisha ya mapambano, lakini Bwana akiwa upande wetu hakuna linaloshindikana. Tutashinda na Zaidi ya kushinda. Tukimfanya yeye kuwa tegemeo letu.
Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali share na wengine.
Mada Nyinginezo:
Biblia inamaana gani kusema;aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi?
Ipo Imani ya kwamba mtu anaweza kutoka nje ya mwili wake au kwa lugha nyingine inajulikana kama Astral projection. Ni kwamba mtu kwa mapenzi yake mwenyewe sio kwa kuhimizwa na nguvu nyingine tofauti na yake labda tuseme ya Mungu au shetani hapana, bali yeye mwenyewe anao uwezo wa kujiamulia kutoka nje ya mwili wake, na kusafiri na kwenda mbali, mahali popote anapotaka na kurudi.
Ni ukweli usiopingika kuwa imani hii siku za hivi karibuni imezidi kushamiri sana, wanasema kitendo hicho salama mtu yeyote anaweza kufanya hata akiwa tu chumbani kwake, kinachohitajika tu ni utulivu wa akili wa hali ya juu sana, yaani kuulazimisha ubongo ukae katika hali ya kutowaza kitu chochote kwa muda fulani, na kuhakikisha pia hakuna hofu yoyote moyoni.
Pia mwili uwe katika utulivu na hiyo inaweza ikafanyika aidha mtu akiwa amelala kitandani mwake chali, huku anaangalia juu. Au ameketi katika chumba chake chenye utulivu mkubwa sana, na kuweka kitu chochote mbele yake aidha mshumaa unaowaka, au akaweka mlio Fulani wa chini wa dansi , huku anapumua taratibu sana, na kukitazama bila kuhamisha mawazo yake mahali pengine popote. Hiyo inafanywa sana sana na dini za huko ASIA kama vile wahindu, na Wabuddha, kama ulishawahi kusikia kitu kinachoitwa YOGA, nayo ni njia mojawapo mafunzo ya kutoka nje ya mwili (Astral projection).
Wanasema mtu yeyote ambaye anaweza kufikia hatua hiyo basi atajiona kidogo kidogo roho yake inaachana na mwili wake. Na baadaye kabisa atatoka na kuuona mwili wake umeketi pale chini au umelala pale pale kitandani alipokuwa. Hivyo kuanzia hapo anaweza kutembea mahali popote anapoweza kwenda. Anaweza kuzunguka maeneo ya uwani, anaweza akapaa, anaweza kuenda sehemu ambazo hajawahi kufika kabisa..Na baadaye anaweza akarudi tena katika mwili wak,.
Wanasema kitendo hicho cha kutoka nje ya mwili(Astral projection) hakina madhara yoyote, kwanza ni kizuri kinamfanya mtu ajiamini, pili kinamfanya mtu aburudike. Na tatu kinamfanya mtu akue kiroho, na nne kinamfanya awe na afya njema..
Kwanza jambo la kwanza ambalo tunapaswa kufahamu ni kuwa ni kweli kabisa mtu anaweza akatoka nje ya mwili wake..Lakini sio kwa matakwa yake mwenyewe au kwa mapenzi yake mwenyewe..Sisi wanadamu Mungu alivyotuumba hakutupa uwezo huo, alituumba katika mwili, hivyo uwezo wa kuingia katika Roho na kwenda nje haiwezekani kama mtu hatawezeshwa na nguvu Fulani inayotoka rohoni. Na nguvu hiyo ni aidha inatoka kwa Mungu au kwa Shetani, basi hakuna hapo katikati.
Tunasoma katika maandiko Mtume Paulo anashuhudia na kusema alinyakuliwa na kupelewa hadi mbingu ya tatu(Sasa huko kunyakuliwa ndio kutoka nje ya mwili), akasema alipofika huko alionyeshwa mambo ambayo hayajuzu mwanadamu kuyanena..
2Wakorintho 12.:1 “Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.
2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);
4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.”
Unaona Maneno haya yanathibitisha kweli kuwa mwanadamu anaweza kutoka nje ya mwili wake, jambo hilo hilo linaonekana pia kwa mtume Yohana alipokuwa katika kile kisiwa cha Patmo, naye alikuwa katika Roho.
Na hata leo hii Mungu anaweza kutoa watu na huwa anawatoa katika mwili na kuwapeleka sehemu nyingine kuwaonyesha mambo ya rohoni, hilo linawezekana lakini haliji kwa jinsi mtu anavyotaka yeye. Bali kwa jinsi Mungu anavyotaka yeye, hata kama mtu huyo ni nabii kiasi gani, au anayo mahusiano gani na Mungu, hajiamulii mwenyewe sasa nataka nione maono. Au nataka niingie katika roho, ni Mungu mwenyewe ndio anayepanga na inakuja kwa wakati asioutegemea.
Ni kwamba, pale mtu anapotaka kujaribu kutafuta au kujiingiza katika maarifa ya rohoni kwa matakwa yake mwenyewe. Hapo ndipo shetani anapopata mlango kirahisi wa kumwingia mtu huyo na kumdanganya..Kama ulikuwa hujui hivyo ndivyo watu wanavyozama katika uchawi na ushirikina,..
Zipo shuhuda nyingi sana siwezi kukuelezea zote hapa, na kama wewe ni msomaji mzuri wa vitabu nakuomba usome kitabu hichi ambacho kilipata umaarufu mkubwa duniani, na kimewasaidia watu wengi sana ambao walikuwa wamezama katika vifungo vya namna hiyo vya shetani na kutoka kinavyomweleza dada mmoja aliyeingia katika uchawi na kuwa malkia wa kuzimu na baadaye kukombolewa na Kristo.
Na kufunua njia zote na milango yote ambayo shetani anayoitumia kuwavuta watu wengi kwake..Kitabu hicho kipo katika lugha ya kiingereza kinaitwa, HE CAME TO SET THE CAPTIVES FREE. Ikiwa utakihitaji utaniambia nikutumie kwa njia ya email kwa mfumo wa pdf Ukisome, moja ya mambo anayoeleza huko ni pamoja na kuwaonya watu wasifanye hivyo kabisa (Astral Projection).
Leo hii hata katika maeneo ya michezo na mazoezi (GYM). Wanafundishwa kufanya hivyo na kudai kuwa ni sehemu ya afya ya ubongo kufanya YOGA. Wanasema ukiweza kukaa katika hali hiyo bila kufikiria chochote au kuwaza chochote katika utulivu wa hali hiyo ya juu kwa muda mfupi tu hata wa nusu saa ni zaidi ya kupumzika kwa kulala usingizi. Nataka nikuambie usijaribu kufanya hivyo. Kwani shetani hapo ndipo anapopata upenyo kwa kupitia milango ya fahamu zako kukuteka na kukutoa katika mwili, na siku za mwanzoni utajiona kweli ni kama wewe unafanya lakini kumbe hujui tayari ni Pepo limekuchukua katika roho linakuzungusha. Unakuwa huna tofauti na mchawi anasafiri kwa ungo kutoka mji mmoja hadi mwingine kwa nusu saa.
Na kwa kuwa siku ya kwanza utapenda, kesho tena utataka ujaribu, na huko huko utakutana na mambo ya ajabu na nguvu za giza ambazo zitakupa maagizo zaidi ya kufanya ili uwe na uwezo huu au uwezo ule, na mwisho wa siku unajikuta umezama moja kwa moja katika uchawi wa hali ya juu.
Kwamwe usikae umfungulie shetani mlango kama huo ukadhani unajaribu tu. Ukifanya hivyo ndio umepotea moja kwa moja…Na waganga wa kienyeji nao wanatoaga hayo masharti.
Shetani sikuzote anajua wanadamu wanapenda maarifa Fulani zaidi wa hayo waliyowekewa, hivyo anakuja na kitu kipya kwasababu anajua wakisikia hivyo watavutiwa nacho, ndicho alichofanya pale Edeni kumwambia Hawa Ati hivi ndivyo Mungu alivyosema, ukila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya mtakufa?..Hakika hamtakufa kwasababu anajua siku mtakapokula MTAFUMBULIWA MACHO..
Vivyo hivyo leo hii anawaambia watu ukitoka nje ya mwili wako, basi utakuwa unajua kila kitu. Utakuwa unaweza kujiamrisha mwenyewe na kuongoza roho yako kwa jinsi unavyotaka..Lakini walioingia huko, wanahadhithia wanatamani kutoka lakini ni ngumu shetani kashawateka..
Hivyo epuka ujanja wa shetani. Mtu akikueleza habari hizo, tena mkemee. Dumu katika kulitafakari Neno la Mungu, na kuyatenda mapenzi yake, hiyo inatosha..Hizi ni nyakati za Hatari.
Mungu akubariki.
Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine.
Mada Nyinginezo: