In biblical times, there was a special road known as “The King’s Highway”—a major route that connected Egypt to Syria, passing through Jordan. It was vital for commerce and travel, maintained with bridges over rivers and leveled ground over valleys. Those who traveled on it had a clear and reliable path, much safer and faster than wandering through rough terrain.
This historical road is mentioned in the Old Testament and was well-known in the ancient world. But more importantly, it holds spiritual significance for us today, especially in understanding our journey of faith.
1. The Historical King’s Highway in Scripture
When the Israelites were traveling to the Promised Land, they reached Edom and requested to pass through via this road:
“Please let us pass through your land. We will not pass through field or vineyard, or drink water from a well. We will go along the King’s Highway, we will not turn aside to the right hand or to the left until we have passed through your territory.”(Numbers 20:17)
But the Edomites refused:
“You shall not pass through, lest I come out with the sword against you.”(Numbers 20:18)
Later, the Israelites made the same request to the Amorites:
“Let me pass through your land. We will not turn aside into field or vineyard. We will not drink the water of a well. We will go by the King’s Highway until we have passed through your territory.”(Numbers 21:22)
Again, they were denied—and this time, war broke out. But Israel prevailed.
2. Theological Insight: Old Testament Shadows and New Testament Realities
The Apostle Paul teaches that the events in the Old Testament serve as examples or shadows for us today:
“Now these things happened to them as an example, but they were written down for our instruction…”(1 Corinthians 10:11)
So what does the King’s Highway symbolize?
It represents a direct, secure, and God-ordained path toward His promises. In the Old Testament, it was the best route to the Promised Land. In the New Testament, that “highway” is Jesus Christ—the only true way to the eternal Promised Land: Heaven.
3. Jesus Christ: The True and Living Way
Jesus made this bold declaration:
“I am the way, and the truth, and the life. No one comes to the Father except through me.”(John 14:6)
This statement is exclusive and absolute. There is no other spiritual road that leads to God—not through religion, good deeds, prophets, or spiritual leaders. Only faith in Jesus Christ, evidenced by obedience and love, leads us to the Father.
The Prophet Isaiah foresaw this Highway of Holiness:
“And a highway shall be there, and it shall be called the Way of Holiness; the unclean shall not pass over it… It shall belong to those who walk on the way; even if they are fools, they shall not go astray.”(Isaiah 35:8)
This prophecy finds fulfillment in Christ, who makes sinners holy by His grace and leads them safely to eternal life.
4. Perseverance on the Path
Just as Israel faced opposition from Edom and the Amorites, we too face challenges—spiritual warfare, temptation, rejection, suffering. But like them, we must remain determined to stay on the path God has prepared. Jesus warned:
“For the gate is narrow and the way is hard that leads to life, and those who find it are few.”(Matthew 7:14)
The road may be difficult, but it is sure—and it leads to eternal joy.
5. A Call to Commitment
Many people are walking on uncertain paths, hoping their good works, religion, or traditions will lead them to God. But without Christ, every other road leads to destruction.
“There is a way that seems right to a man, but its end is the way to death.”(Proverbs 14:12)
Jesus is the only road built by God Himself—leveled by grace, paved by truth, and secured by His blood. He is the King’s Highway from Earth to Heaven.
Choose the Right Road
If you’ve been walking on uncertain paths, turn to Jesus today. Trust Him, follow Him, and walk in His ways. The journey with Him may involve sacrifice, but it is the only road that guarantees arrival at God’s presence.
The Israelites pursued the King’s Highway even when opposed—because they knew it was worth it. So must we.
“Let us run with endurance the race that is set before us, looking to Jesus, the founder and perfecter of our faith.”(Hebrews 12:1–2)
Jesus is the way. Walk in Him. Live in Him. And you will reach the Father.
That is the truth that has stood firm throughout all generations.
May the Lord bless you as you walk the King’s Highway.
Neno hili linatwa mara nyingi sana katika biblia, sana sana mahali ambavyo vinatajwa vizazi vya wana wa Israeli.
Mbari, kwa jina lingine ni UKOO. Kwamfano unaweza kukutana na sehemu fulani inasema, “hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao”. Hapo inamaanisha kuwa “hao ndio wakuu wa ukoo wa baba zao”,
Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo;
1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni”.
1Nyakati 7:4 “Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi”.
1Nyakati 8:28 “Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu”.
1Nyakati 9:33 “Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku”.
1Nyakati 26:13 “Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao”.
Luka 1:26 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, WA MBARI YA DAUDI; na jina lake bikira huyo ni Mariamu”.
Luka 1:26 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, WA MBARI YA DAUDI; na jina lake bikira huyo ni Mariamu”.
Soma pia Nehemia 10:34, 11:13
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
Rudi nyumbani:
WhatsApp
Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio cha kweli cha roho zetu.
Kawaida ya Mungu ni huwa hatoi agizo juu ya agizo. Yaani kwa mfano leo akikupa agizo fulani ulitelekeze, haundi agizo lingine juu yake kulibatilisha hilo la kwanza, Atafanya hivyo endapo tu lile la kwanza litakuwa limeisha muda wake.
Mara nyingi tunakuwa tukiacha yale maagizo ya kwanza ya Mungu, na hiyo inatupelekea aidha kukutana na hukumu yake, au kushindwa kutekeleza mipango yetu kwa wakati.
Kwamfano utakutana na nabii mmoja katika biblia enzi za wafalme, ambaye alipewa maagizo na Mungu ya kwenda kumtolea unabii Mfalme mwasi Yeroboamu, akaambiwa akishamaliza kazi yake asile wala asinywe chochote katika mji huo, wala asilale au kupumzika na njia atakayoipita asiirudie tena hiyo hiyo. Lakini huyu nabii alipomaliza kweli kazi ya huduma alianza safari ya kuondoka. Lakini akiwa njiani alikutana na nabii mwingine mzee, akamshurutisha, aende kulala nyumbani kwake. Lakini yeye akamwambia Bwana amenionya nisikae mahali popote kwenye mji huu.
Sasa yule nabii mzee alipoona kuwa kijana huyu hataki, akamtungia habari za uongo na kumwambia, Bwana ameniambia ameghahiri, mpango wake, hivyo anataka uje ule upumzike nyumbani kwangu. Na yule kijana pasipo kufikiria ni kwanini Mungu awe kigeugeu, saa hiyo hiyo akamwamini, kwasababu tu ni nabii mwenzake tena mzee, anauzoefu wa mambo ya kinabii, akaenda kukaa kwake. Kitu kilichomtokea hatuna haja ya kueleza, sote tunajua alikuja kuliwa na simba, kwa kuyaasi maagizo ya Mungu (Soma 1Wafalme 13)
Tunamwona Mtu mwingine anaitwa, Balaamu, naye pia mwanzoni Mungu alimuonya asiende kuwalaani Israeli, lakini baadaye akawa analazimisha mawazo yake kwa Mungu, kilichofuata ilikuwa ni Mungu kumwambia haya nenda nitakuwa pamoja nawe..kumbe hakujua tayari njia Mungu alikuwa ameshamuandalia malaika wake amuue, na kama sio yule punda kumsaidia habari yake tusingeisoma leo hii kwenye biblia (Soma Hesabu 22).
Hiyo yote ni kutozingatia agizo la kwanza Mungu alilokupa, Siku zote agizo linalokuja juu ya agizo lile la mwanzo huwa halitokani na Mungu.
Tukisoma tena habari nyingine maarufu katika biblia ile ya Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Babeli utumwani, baada ya kukaa kule miaka 70. Biblia inatuambia Mungu alimuamsha moyo mfalme Koreshi wa uajemi, ili atoe amri kuwa watu wote waondoke kwenye makoloni yake, waende Yerusalemu kumjengea Mungu nyumba, kufuatana na unabii uliotolewa na Yeremia zamani.
Tunaona baada ya hapo Mfalme aliwapa zawadi nyingi sana, Hivyo waliondoka kwa moyo mkunjufu wakijua kabisa Mungu kaitimiza ahadi yake ya kwenda kumjengea nyumba Yerusalemu. Lakini walipofika kule na kuanza kutia msingi wa nyumba ya Mungu, maadui zao wakaanza kunyanyuka hilo likawadhoofisha, na kama hiyo haitoshi wakaandika waraka wa uchongezi wakampelekea mfalme mwingine wa uajemi ambaye alikuja kutawala baada ya Koreshi, aliyeitwa Dario, mfalme alipousoma, akatoa amri nyingine, kuwa usiendelee ujenzi wowote Yerusalemu, wa nyumba ya Bwana. Na mtu yeyote atakayefanya vile ilikuwa ni kifo.
Wayahudi waliposikia, juu waraka huo mpya, wote wakavunjika moyo, wakaacha kuijenga nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa tayari katika hatua nzuri, Hivyo ikapelekea nyumba hiyo kubakia hivyo hivyo kwa muda wa miaka mingi sana..Kila mtu akarudi kuendelea na shughuli zake kila siku.
Wakasau kuwa ni Mungu ndiye aliyewapa maagizo kuwa wakamjengee nyumba yeye, hawakujiuliza sasa haya maagizo mengine yanatoka wapi?
Mpaka baadaye sana, tunaona manabii wawili yaani Hagai na Zekaria wanatokea, wanawatabiria na kuwauliza kwanini mnaacha kujenga nyumba ya Mungu, wakidai kuwa huu sio wakati wa kumjengea Mungu? Kwa muda wako soma kitabu chote cha Hagai utaona mambo hayo.
Unaona, walisikiliza sauti ya pili, wakaicha ile ya kwanza, na hiyo ikawapelekea kucheleweshwa kwa huduma yao waliyokuwa wameshaianza,.. Siku zote sauti ya pili ni ya shetani, na sio ya Mungu.
Vilevile katika agano jipya kuna agizo ambalo tayari Mungu alishatupa.
Marko 16:15-16 Inasema..
“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Hili ni agizo ambalo Kristo alishatoa kibali, kufanya.. Lakini dunia ya sasa shetani ameshaiingilia, kiasi kwamba, sehemu nyingine watu hawaruhusiwi kuhubiri kabisa, sheria za nchi zao zimekataza..Sasa wewe kama mkristo ukiogopa sheria ya wanadamu, ukasema pengine huu sio wakati wa kufanya hivyo, ujue kuwa utafanana na wana wa Israeli walipokuwa wanalijenga hekalu la pili, utasubiria wee, na kamwe hiyo siku ambayo unayoina itafaa haitafika, Mungu atakachofanya ni kukumbusha tu, uliacha agizo la kwanza.
Sio hilo tu yapo maagizo mengine madogo madogo, yanakubana kiasi kwamba yanakufanya ushindwe hata kuiendeleza kazi ya Mungu, mpaka uwe na hiki au kile, au ukamilishe hiki au kile..Hayo yote hatupaswi kuyazingatia sana, mengine yana agenda ya shetani nyuma yake kukumwisha tu, bali tuzingatie lile agizo kuu la mwanzo ambalo Kristo ametupa enendeni ulimwenguni kote.
Mwingine atasema familia yangu iko hvi au vile..hupaswi kuangalia hayo yote
Safari ya imani, si mteremko muda wote, kuna wakati itasumbuliwa na mambo mengi, lakini hatupaswi kuyaogopa kwasababu Mungu ameshaahidi atakuwa na sisi katika hayo yote. Kama tu vile alivyokuwa kwa mababa zetu katika mapito yao.
MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:
BWANA AYAGANGE NA MACHO YETU PIA.
Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
Rudi nyumbani
SWALI: Biblia inamaanisha nini inaposema “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?(Yuda 1:23)
JIBU: Maneno hayo utayasoma katika vifungu hivi;
Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka, 23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, MKILICHUKIA HATA VAZI LILILOTIWA UCHAFU NA MWILI. 24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu”;
Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka,
23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, MKILICHUKIA HATA VAZI LILILOTIWA UCHAFU NA MWILI.
24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu”;
Kama tunavyosoma vifungu hivyo, vinaeleza wajibu wa kila aliyeokoka katika kuwavuta wengine katika Imani. Mtume Yuda anaeleza yapo makundi mbalimbali ya watu waonaopaswa kuokolewa, lipo kundi la watu ambalo linapaswa lihurumiwe kwa hofu, yaani lichukuliwe katika uchanga, na utulivu, livutwe kwa upendo wa Mungu tokea mbali, kundi hili ni la watu wote ambao hawamjui Mungu, wanaoishi duniani leo hii. Walevi, wezi, wazinzi, waoabudu sanamu, n.k.
Lakini lipo kundi lingine linalopaswa kuokolewa kwa kunyakuliwa katika moto. Unajua mpaka mtu awe ndani ya moto, huhitaji kumbembeleza bembeleza, ili kumtoa, unachopaswa kufanya ni kumnyakua tu atoke kule kwa gharama zozote zile, kwasababu akiendelea kubaki kule muda si mrefu atakufa. wapo watu ambao unaona kabisa wanakwenda kuangamia kwa mienendo yao ya dhambi, wapo wengine unaona kabisa wapo katika dakika za mwisho wamalizie mwendo wao hapa duniani, na bado hawajaokoka, wapo watu ambao wameshakata tamaa kiasi cha kwamba kilichobakia kwao ni kujiua tu siku yoyote, wapo watu ambao wamefungwa katika minyororo na mateso ya ibilisi, wao wenyewe hawawezi tena kufanya chochote juu ya maisha yao , n.k. Sasa watu kama hawa wanapaswa waokolewe kwa nguvu ya ziada. Kwa kuwafungua na kuwaombea sana, na kuwafuatialia kwa ukaribu sana, na wengine kwa kuwahubiria injili ya Jehanamu ili wajue huko wanapoelekea ni wapi, waogope wageuke kabla kifo hakijawakuta..
Sasa katika kazi hiyo yote ya uokoaji, mwandishi anasema.. “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”. Yaani kujilinda nafsi zenu, na nyinyi msije mkachukuliwa katika dhambi zao. Na ndio maana hapo anatumia mfano wa vazi lililotiwa unajisi kwa uchafu. Katika agano la kale vazi lililotiwa unajisi ni vazi lililovaliwa na mtu mwenye ukoma. Ambalo lilikuwa ni rahisi kumuambikaza mtu mwingine ukoma huo endapo atalishika au kulivaa. Yaani kwa ufupi Nguo zote zilizokuwa zinatiwa unajisi wa aina yoyote ile, uwe ni ule unaotoka mwilini au vyovyote vile uliweza kumtia unajisi hata mtu mwingine asiyestahili endapo tu atazigusa au kuzivaa. (Walawi 21:11, Hesabu 6:6).
Yapo matendo ambayo, ni rahisi kutiwa na watu wengine unajisi kwayo, unapokwenda kumubuhiria mzinzi, hakikisha na wewe huna uzinzi ndani yako, unapokwenda kumuhubiria mlevi hakikisha na wewe vimelea vya ulevi havipo ndani yako, vivyo hivyo na kila mtu unayekwenda kumshuhudia. Unapaswa ujichunge wewe mwenyewe kwanza. Kwasababu shetani naye anatenda kazi.
Wagalatia 6:1” Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, UKIJIANGALIA NAFSI YAKO USIJE UKAJARIBIWA WEWE MWENYEWE”.
Hiyo ndio maana ya kulichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?
MAMA UNALILIA NINI?
Je mtu anayeua anabeba dhambi zote za yule aliyemuua?
Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?
Jibu: Tusome.
Danieli 9:21 “naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni”.
Kurushwa upesi kunakozungumziwa hapo ni “kuruka kwa haraka” au kwa lugha rahisi zaidi ni “kuruka/kupaa kwa spidi”. Ndege wa angani huruka kwa upesi..Kwa mfano ni rahisi kumsogelea ndege kama njiwa, na akikuona tu, mara ghafla utamwona kapiga mbawa na kupotelea kwenye ukingo wa anga. Hiyo ndiyo maana ya kuruka kwa upesi.
Na Biblia inasema hapo Danieli alimwona Malaika Gabrieli akirushwa kwa upesi na Mungu.. Maana yake alikuwa anamwona katika maono, akija kwa kasi, na akiondoka kwa kasi.
Kumbuka wapo malaika wenye mbawa na wasio na mbawa (maana yake wasioruka)..Gabrieli ni miongoni mwa malaika wenye mbawa, na wa kupeleka ujumbe kwa watu.
Ni kawaida kile kitu kinachopeleka ujumbe kwa haraka sana ni bora kuliko kile kinachopeleka kwa taratibu. Hivyo Gabrieli ni malaika mwenye sifa ya kupeleka ujumbe kwa haraka sana
Malaika Gabrieli ameonekana katika agano la kale na vile vile katika agano jipya. Katika agano la kale, ndio hichi kipindi cha Nabii Danieli alipotumwa ampe ujumbe juu ya mambo yanayokuja.
Na katika Agano jipya alionekana kipindi cha Kuhani Zakaria, Baba yake Yohana Mbatizaji, alipotumwa na Mungu ampe ujumbe kuhusu kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji ambaye atatangulia kumtengenezea Bwana njia (Soma Luka 1:19). Na pia kipindi kifupi baadaya akaja kuonekana tena kwa Bikira Mariamu kumpa ujumbe wa kubeba mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Unaweza kusoma Luka 1:26).
Na hata leo Malaika Gabrieli anatumwa kwa watu wengi duniani walio waaminifu kwa Mungu kuwapa jumbe mbalimbali.
Kama utapenda kujua zaidi kuhusu Malaika unaweza kufungua hapa >> Malaika
Je umempokea Kristo?. Yesu anarudi.
Maran atha!
Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?
MALAIKA WAPELELEZI WA HUKUMU WANAPITA SASA.
Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?
Leo tutajifunza jinsi gani matatizo yetu yanavyoweza kuweza kutupofusha hata tusiione miujiza yetu.
Kuna wakati Mungu, anakuwa ameshakwisha anza tayari kututendea miujiza, lakini kutokana na kuwa tunayapa sana matatizo yetu uzito mkubwa kuliko yanavyostahili, inatupelekea hata miujiza yenyewe tuiione kama si kitu pale inapoanza kuja.
Embu fikiria wakati Kristo alipokufa na kulazwa pale makaburini, tunaona kuna mambo mengi yalikuwa yanaendelea pale, lakini kikubwa ambacho tunaweza kujifunza leo ni lile tukio la Mariamu Magdalene. Yeye alipofika pale alianza kulia kwa uchungu, akifikiria miujiza yote aliyotendewa na Yesu tangu akiwa duniani, akifikiria jinsi alivyoishi maisha ya haki na upendo usiokuwa na unafiki, wala hakufanya kosa lolote, na leo hii, anaona wamemuua, tena afadhali ingekuwa wamemuua na kumsulubisha tu, na kumwacha, lakini safari hii wameuiba mpaka na mwili wake pia, hilo ndio lililomfanya alie sana kwa uchungu, kiasi cha kumfanya ashindwe kuondoka pale aendelee tu kulia,
Lakini biblia inatuambia muda si muda, akiwa amesimama pale anachungulia ndani ya kaburi ghafla aliwaona malaika wawili, wamekaa, mmoja kichwani pa mahali walipomlazia Yesu na mwingine, miguuni..Lakini wale malaika wawili wakamuuliza swali, Mama unalilia nini?
Yohana 20:11 “Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. 13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka”.
Yohana 20:11 “Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.
13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka”.
Fikiria, ule uchungu wa mawazo ulimfanya hata asahau kuwa wale ni malaika wa Mungu, Uchungu wa kuibiwa kwa Bwana kulimfanya hata asifikirie wale watu wawili wenye mavazi yaliyong’aa meupe wametokea wapi muda ule, na wanafanya nini pale..Yeye moja kwa moja anaanza kuzungumza nao kama vile, ni watu wa kawaida anaokutana nao barabarani siku zote.
Kama hilo halitoshi, wakati anaendelea kulia pal, nje, akamwona Tena mtu mwingine anatembea tembea karibu yake,(hakujua kama ndiye Yesu) ndipo Yesu akamuuliza swali lile lile aliloulizwa na wale malaika..Mama unalilia nini?..
Yohana 20:15 “Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu)”.
Yohana 20:15 “Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu)”.
Unaona, Yesu alipogeuka na kumshtua MARIAMU!!!..Ndipo akabutuka na kugundua kuwa Yule ni Yesu aliyesimama mbele yake. Kama asingeshtuliwa, bado angeendelea kukaa katika majonzi yake tu, analia lia ovyo wakati Yesu anazungumza na yeye.
Wakati mwingine matamanio yetu yanakuwa makubwa kupitiliza, mpaka yanatupofusha tunashindwa hata kuona miujiza ya Mungu, kama sio kumwona Mungu mwenyewe.
Jambo kama hili utaliona kwa Balaamu pia, wakati ule anataka kwenda kuwalaani Israeli, alipokuwa njiani, punda wake alifunguliwa kinywa na Mungu, na kuanza kuongea naye.. Sasa yeye kwasababu moyo wake wote tayari ulikuwa kule anapoelekea, kuwalaani Israeli, hata kuzungumza na Punda hakuona kama ni muujiza ule, badala yake akaanza kuzungumza naye kama anavyozungumza na mwanadamu mwenzake tu..Kama alivyofanya Mariamu.
Hesabu 22:28 “Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi? 29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi. 30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La! 31 Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi”.
Hesabu 22:28 “Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?
29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.
30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!
31 Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi”.
Umeona? Pengine na wewe umekuwa ukizitazama sana shida zako, kuliko kuutazama uweza wa Mungu. Pengine ipo miujiza mikubwa Mungu ameshaanza kukufanyia lakini huwezi kuiona kwasababu wakati wote ukienda kwa Mungu unatazama tu ukubwa wa shida zako, na sio uweza wa Mungu.
Unasahau kuwa ni Malaika wa Bwana wamesimama pale pale unapopalilia, unasahau kuwa ni Yesu mwenyewe mkuu wa Uzima, amesimama pembeni yako kuzungumza na wewe na wewe juu ya hilo tatizo lako, lakini wewe unalia tu.. Leo nakuambia tuliza moyo wako, usilie mahali ambapo tayari Mungu ameshakusikia, bali, mshukuru yeye, zungumza na yeye, utaona miujiza mingi ambayo tayari ameshaanza kukufanyia katika maisha yako.
Mungu akubariki.
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
YESU MPONYAJI.
NAWE UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.
Shalom,
Kuna kipindi mitume walimpelekea Bwana hitaji hili;
Luka 17:5 “… Tuongezee imani”.
Kwao pengine hili lilikuwa ni hitaji jepesi sana , lakini kwa upande wa Bwana halikuwa ombi la kuwajibu kwa sentensi mbili, au kwa kuwawekea mikono tu na kupokea, hapana, na ndio maana baada ya ulizo hilo, hakukuwa na jibu la moja kwa moja kutoka kwa Bwana.
Sehemu nyingine alipoona upungufu wa Imani yao Bwana Yesu aliwaambia , namna hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa “kufunga na kuomba”(Mathayo 17:21) Na sehemu nyingine biblia inasema, Imani huja kwa kukisikia Neno la Mungu(Warumi 10:17).. Ikiwa na maana kuwa kwa jinsi unavyosoma Neno la Mungu, na kuona uweza wa Mungu alioufanya, tangu enzi na enzi, sasa kwa jinsi unavyosoma sana na kusikia Neno lake, ndivyo imani yako inavyojengeka kwake, na hatimaye unakuwa na imani timilifu, hata ya kuweza kuamishi milima kwa jina lake.
Lakini katika yote hayo utagundua kuna kitu kimoja kinachoitwa BIDII ndani yake..Ikiwa na maana imani haiwezi kuja hivi hivi tu kwa kukaa, kama hutakuwa na bidii ya kuitafuta, haitakaa ije kwako kamwe, haiji kwa kuwekewa mikono, wala haiji kwa kuombewa,..
Sasa Imani ni nguzo mojawapo ya Ukristo, zipo nguzo nyingine mbili za Ukristo nazo ni Upendo na Tumaini. Lakini leo hatutazungumzia juu ya Tumaini, bali tutazungumzia juu ya Upendo, ambao ndio mkuu kuliko hata Imani au tumaini.
Upendo ni kilele cha Ukristo, Kwasababu biblia inasema Mungu mwenyewe ni Upendo.
Na Mkristo aliyekuwa sana kiroho, atatambulika kwa kiwango chake cha Upendo. Lakini wengi wetu tunadhani upendo ni kuonyesha tabasamu zuri kwa mtu, au kumsaidia mtu sana. Hivyo ni kweli ni vimelea vizuri vya Upendo, Lakini Upendo wa ki-Mungu unavuka hapo, na kwenda zaidi.
Embu tuvipitie baadhi ya vipengele vikuu,na mwishoni kabisa tutajifunza jinsi gani tutaupata huu Upendo mkamilifu.
1 Wakorintho 13
13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
Ukianzia kusoma ule mstari wa 4, utaona misingi inayoubeba upendo ikanza kuzungumziwa, anasema huvumilia. Jiulize je ndani yako ulishawahi kuvumilia mabaya mangapi pale ulipotendewa, je pale alipokuaibisha uliweza kutunza siri yake?, je, ulimsamehe pale alipokuaibisha, je ulivumilia yote hayo yote bila kuweka kinyongo, au kukomoa?
Anasema tena, Upendo hufadhili; Neno fadhili ni pana sana, ni zaidi ya kumfanyia mwenzako wema, ambao hauna malipo yoyote kwako. Anasema tena, hautakabari, haujivuni, huatafuti mambo yake mwenyewe, je maisha na namna hiyo yapo ndani yako? Wewe kama mkristo uliyeokoka?
Anasema Upendo haukosi kuwa na adabu, Je! Wewe wakati wote unayo adabu kwa watu wote?, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, yaani inafikia hatua hauoni mabaya bali mema tu mtu anayokufanyia, Je ulishawahi kuwa mtu wa namna hii? Ulishawahi kuwa mtu wa kustahimili mambo yote, au kuvumilia mambo yote, au ni baadhi tu ya mambo umeyaweza? Kama ni baadhi tu basi Upendo wa ki Mungu bado haujakamilika ndani yako. Haijalishi utajiona ni mwema kiasi gani.
Hivyo utoshe tu kusema kwa namna ya kibinadamu Pendo hili la Ki-Mungu, si rahisi kulipata kwa maneno tu, au kwa kuombewa au kwa kuwekewa mikono, , hauwezi kustahimili yote, yapo mengine ambayo yatakuudhi, upo wakati ambao utawahusudu wengine, upo wakati ambao, utahesabu mabaya tu n.k. Huo ndio ukweli.
Lakini sasa tufanyeje ili tuyashinde hayo yote?
Kanuni ni ile ile, kama ya IMANI, unapaswa uonyeshe bidii, katika kutekeleza hivyo vitu.
1Petro 4:8 “Zaidi ya yote IWENI NA JUHUDI NYINGI KATIKA KUPENDANA; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.
Inahitaji juhudi, mpaka ujijenge na kuwa tabia ndani yako, unapoona mwenzako amekutendea mabaya, unapaswa ujitahidi kwa nguvu zote, kuyaachilia yale mabaya anayokufanyia, na kujifunza kuyatafakari yale mazuri yake.. Ndio siku za mwanzoni mwanzoni, itakuwa ni ngumu lakini unavyojijengea utaratibu huo kwa nguvu, baadaye inageuka na kuwa ni tabia yako. Mpaka mwisho wa siku, hata jambo liwe ni gumu kiasi gani, utaona linatapita tu mbele yako kama upepo, bila kikusumbua hata kidogo .
Kumbuka tena vimelea hivyo vya upendo haviji hivi hivi tu, kwa kuombewa, au kusubiria, bali vinakuja kwa kuonyesha bidii, yaani kuvitendea kazi, mpaka ufikie hatua ya kutoona uchungu, au kutohusudu, kunahitaji kukataa usengenyaji kuanzia sasa, kukataa kusikiliza maneno ya watu mabarazani, pale wanapomzungumzia mtu mwingine kwa ubaya. Kunahitaji kujitoa kwa wengine, bila kujali unapata faida gani kwao..N.k.
Warumi 12:10 “Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; 11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;”
Warumi 12:10 “Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;”
Upendo ni kitu cha kujazilishwa, yaani kila siku unakiongezea nyama mpya, kimoja huzaa kingine, na kingine huzaa kingine, mpaka tunafikia vile viwango vya Upendo wa ki-Mungu
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, 6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, 7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. 8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo”.
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo”.
Hivyo mimi na wewe kuanzia leo tuanze kuyatendea kazi haya, tujazilishe upendo wetu, siku baada ya siku tuongeze kimelea kipya cha upendo, Kwasababu tujue kuwa kitu cha kwanza ambacho kitatusogeza kwa Mungu kwa urahisi na haraka si Imani au tumaini bali ni Upendo, kwasababu yeye mwenyewe ni Upendo, na ndio maana Paulo anasema, hata nijapokuwa na Imani timilifu ya kuamisha milima kama sina Upendo mimi si kitu. Maana yake ni kuwa, huwezi kumwona au kumjua Mungu ukiukosa huo,
1Yohana 4:8 “Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo”.
Hivyo jambo hili, na kuwa nalo siriazi, ni kulitendea kazi kwa bidii zote, kila wakati kila muda mpaka lijengeke na kuwa tabia yetu.
1Petro 1:22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo”.
UPENDO WA MUNGU.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?
TUSIWE WATU WA KUPUNGUKIWA AKILI.
Jibu: Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ambayo mtu anaiinua mbele za Mungu. Na ni sehemu ya sadaka iliyo ya heshima kuliko nyingine yoyote ile.
Kwamfano mtu anaweza kutoa sadaka ya kawaida ya kila siku, lakini isiwe iliyo kuu na ya heshima, lakini akatenga sadaka moja ambayo itakuwa ndio kaiheshimu kuliko zote.. ambayo atakwenda kuiinua mbele za Mungu, huku akiambatanisha na haja fulani, au shukrani fulani.
Hesabu 15:18 “Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi niwapelekayo, 19 ndipo itakapokuwa ya kwamba hapo mtakapokula katika chakula cha nchi hiyo, mtamsongezea Bwana sadaka ya kuinuliwa”.
Hesabu 15:18 “Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi niwapelekayo,
19 ndipo itakapokuwa ya kwamba hapo mtakapokula katika chakula cha nchi hiyo, mtamsongezea Bwana sadaka ya kuinuliwa”.
Mara nyingi sadaka hii ya kuinuliwa inakuwa ni ya “maandalizi”, sio tu ya kufikiri siku moja na kwenda kuitoa, na pia inakuwa ni ya kujitoa kweli kweli (maana yake ni ya kiwango kikubwa, au ya kugharimu), ikiwa sio ya kugharimu inakuwa haina tofauti na sadaka nyingine.
Kumbuka pia sadaka kama Zaka, na Malimbuko hizo sio sadaka za kuinuliwa, hizo ni sadaka ambazo ni za wajibu, na hazipo katika kundi hili la sadaka za kuinuliwa.
Kumbuka tena sadaka hii ni tofauti na sadaka nyingine, ni lazima iwe na heshima kuliko nyingine, ndio maana imeitwa Sadaka ya KUINULIWA, maana yake ni ya hadhi ya juu zaidi kuliko nyingine, “Umeiinua kuliko nyingine”. kwahiyo ni dhambi kumtolea Mungu sadaka kilema. Na kuiinua mbele za Mungu.
Ni dhambi kumpa Mungu sadaka ya shukrani shilingi elfu moja, na kuisongeza mbele zake na kusema nimemwinulia Bwana sadaka hii, (tena na kujiona umemtolea kikubwa mbele zake) na unatoka ukijisifu kwamba umemtolea Mungu… na wakati kakufanyia muujiza wa mamilioni. Hapo ni sawa na umeiinua sadaka ambayo haistahili kuinuliwa, hivyo ni dhambi, ni heri usingetoa kabisa.
Ni sawa na umemwahidi mtu unampelekea zawadi nzuri na kubwa sana, baada ya jambo zuri alilokufanyia na tena ukainadi zawadi hiyo na kuitukuza sana mbele zake..na mwisho wa siku unampelekea zawadi ya hadhi ya chini sana, kuliko ya alivyotarajia, na tena ukaifunga kwenye box zuri. Unadhani ni nini kitafuata?..Ni wazi kuwa yule mtu atachukia atasema ni heri usingempa hiyo zawadi au ni kama ulikuwa unataka kumpa basi ungemwambia tu kwamba utampa kitu fulani kidogo, ili ajue na kujiandaa kabisa kwamba kitakachokuja kinaweza kuwa kidogo. Lakini kwa jinsi ulivyoisifia na kuiinua zawadi hiyo, halafu anakuta ni kidogo sana, ataishia kuchukia.
Ndio hivyo hivyo, pia sadaka ya kuinuliwa..inapaswa iwe kubwa na iwe tofauti na sadaka nyingine..vinginevyo kama huwezi basi toa tu sadaka yako ya kawaida ya kila siku ila usiinyanyue sana mbele za Mungu.
Lakini kama Bwana kakufanyia muujiza mkubwa sana, na wewe ukasema nitamsogezea sadaka ambayo nitaiinua mbele zake, na ukamtolea sehemu kubwa sana na iliyokugharimu angalau sawasawa au karibia na kile alichokufanyia. Hapo sadaka hiyo inakuwa na nguvu mara nyingi zaidi kuliko sadaka nyingine yoyote ya kawaida. Na inaachilia matokeo haraka sana, ikiwemo kuinuliwa kwa huyo mtu. Na Mungu anawaheshimu wale wote wanaomtolea kwa moyo na kwa bidii.
Bwana atubariki na kutusaidia.
Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?
TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.
FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.
Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?
Kuota upo nchi nyingine.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;
Mithali 20:13 “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
Mithali 20:19 “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana”.
Mtu mwenye kitango kwa lugha ya sasa ambayo ni rahisi kueleweka na watu wengi ni mtu “MMBEA”. Yaani mtu ambaye hawezi kusitiri jambo, yupo tayari kukizungumza kila kitu anachokisikia au kukiona kwa watu wengine.
Kwamfano utakuta mtu labda kakaribishwa nyumbani kwa jirani yake au ndugu yake wa mbali, ili akae au aishi tu pale kwa muda, sasa katika kuishi kwake akaona mapungufu fulani fulani ndani ya nyumba ile, ambayo hata wenye nyumba wenyewe hawakuona vema, kuyatangaza, lakini utakuta yeye anatoka pale na kuanza kufichua siri za nyumba hiyo kwa watu wengine, bila hata kujali utu, wale wapo hivi, wapo vile, yule mwanaume kumbe yupo hivi au vile n.k… Sasa mtu kama huyo ni mtu mwenye kitango ambaye biblia imetuonya, tusishirikane naye.
Mwingine ataelezwa jambo la siri na rafiki yake pengine labda ugonjwa fulani usiotibika, na akaombwa sana asimwambie mtu yeyote iwe siri yake, lakini yeye anatoka pale, anaanza kutangaza mtaa mzima yule fulani ana hiki au kile, mpaka habari inamrudia yule mwenyewe muhusika. Sasa watu wa namna hiyo ni hatari sana, hatupaswi kushirikiana nao, kwasababu hata kwa namna ya kawaida ikiwa anaweza kufichua siri za watu wengine kwako, ni wazi kuwa hata za kwako ameshawahi kuzifichua kwa watu wengine. Hivyo ukishakutana na watu kama hawa usijaribu kuwaeleza mambo yako ya siri, wala usikubali kusikiliza wanachokuambia.
Mara nyingi tunaziharibu siku zetu mapema kabisa kunapopambazuka, kwa midomo yetu wenyewe, biblia inasema;
1Petro 3:10 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, NA KUONA SIKU NJEMA, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila”.
Ukitaka ufurahie maisha, jifunze,kuudhibiti ulimi wako, ukitaka siku yako ibarikiwe tangu asubuhi mpaka jioni, jifunze kuutawala mdomo wako, sio kila jambo unaloliona au unalolisikia ni la kutangaza kwa watu , jifunze kutunza siri za watu wengine, kwani kwa kufanya hivyo sio tu siku yako itakuwa ni nzuri, lakini pia utakuwa unampendeza Mungu, Kwasababu Mungu naye hachukui mambo yetu ya siri na kwenda kuyatangaza kwa watu ovyo ovyo, japokuwa anajua mambo yetu wote ya siri tunayoyafanya.
Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Bwana akubariki.
KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.
JIHADHARI NA DHAMBI YA WIVU/HUSUDA.
Vyombo vya uzuri ni vipi vinavyotajwa katika biblia?
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?
SWALI: Shalom mpendwa katika Bwana , swali langu lipo katika kutoka 33:5 BWANA alipomwambia Musa vueni “vyombo vyenu vya uzuri” ili nipate kujua nitakalowatenda . Nataka kujua aliposema hivyo alikuwa na maana gani?
JIBU: Tusome habari yenyewe tokea mstari wa kwanza, lipo jambo zaidi ya hilo la kujifunza;
Kutoka 33:1 “Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii; 2 nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi; 3 waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia. 4 Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza WALA HAPANA MTU ALIYEVAA VYOMBO VYAKE VYA UZURI. 5 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa VUENI VYOMBO VYENU VYA UZURI ili nipate kujua nitakalowatenda. 6 Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele”.
Kutoka 33:1 “Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;
2 nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
3 waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia.
4 Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza WALA HAPANA MTU ALIYEVAA VYOMBO VYAKE VYA UZURI.
5 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa VUENI VYOMBO VYENU VYA UZURI ili nipate kujua nitakalowatenda.
6 Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele”.
Vyombo vya uzuri,ni mapambo ya aina yote, ikiwemo mikufu, pete, hereni, vikuu, nguo za thamani n.k.. Wana wa Israeli baada ya kumkosea sana Mungu, kwa kutengeneza ndama wa dhahabu, Mungu alikusudia kuanzia huo wakati kuwaacha moja kwa moja asitembee nao tena, kinyume chake awape malaika wake wawe wanaenda badala yake, lakini sio yeye tena. Lakini wana wa Israeli waliposikia hivyo wakamlilia sana Mungu wasiachwe, ndipo watu wote wakavua vyombo vyao vya uzuri, yaani vitu vyao vya thamani, wakavaa nguo za maombolezo, wakamlilia sana Mungu na kutubu kwa uchungu mwingi ili tu wasiachwe.
Hiyo ilikuwa ni desturi ya Israeli tangu zamani, na hata mataifa mengine, inapofikia wakati wa kuomba toba, au kuomboleza, ni sharti uweke kando mavazi ya thamani, na mapambo yako, uvae nguo za magunia uomboleze.
Lakini ni nini, tunaweza kujifunza katika habari hiyo?
Wana wa Israeli walitamani waangukie mikononi mwa Mungu kuliko mikononi mwa malaika zake, Kwasababu walimjua Mungu ndio uzima wao, licha ya kuwa ni mwenye ghadhabu nyingi, lakini pia bado ni mwenye rehema nyingi. Ni sawa na kilichomtokea Daudi kipindi kile, alipoambiwa na Mungu achague adhabu mojawapo kati ya zile tatu, yaani njaa miaka mitatu, au akimbizwe na adui zake miezi mitatu, au Tauni iletwe siku tatu juu ya nchi,. Daudi akachagua kuangukia mikononi mwa Mungu, kwa ile Tauni siku ya tatu, kwasababu alijua, mioyo ya wanadamu sio kama wa Mungu, kuliko kukimbizwa na maadui zake, ni heri aadhibiwe na Mungu..Na kweli japokuwa Mungu aliwaua maelfu ya watu, lakini baadaye aliuzuia mkono wake, akarehemu.
Je! Na wewe umechagua kuangukia mikononi mwa nani? Mungu, au mwanadamu?.
Daudi alisema..
Zaburi 118:18 “Bwana ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife”.
Inasikitisha kuona kwamba watu wanakataa kuongozwa na Mungu, wanataka waongozwe na wanadamu, wanachukia kuadhibiwa na Mungu, wanataka wakaadhibiwe na wanadamu. Wana wa Israeli waliomboleza kusikia tu wanakwenda kuongozwa na malaika,ambao hata hawana shida yoyote, lakini waliona bado hakuna kiongozi mzuri na bora zaidi ya Bwana.
Ndugu yangu huna kimbilio lingine lililo salama kwako, zaidi ya Mungu.. Si hata malaika wake, si mwanadamu, au kiumbe kingine chochote, au kitu kingine chochote. Mkimbilie Bwana leo hii akuokoe, na ayasafishe maisha yako. Usizifiche dhambi zako mbele za Mungu, kwa hofu ya kwamba atayakemea matendo yako, ni kweli lazima ayakemee, na wakati mwingine akuadhibu, lakini adhabu zake ni dawa, na sio mauti. Hivyo chagua kuangukia mikononi mwake, uwe salama.
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”.
Maran Atha.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
AINA TATU ZA WAKRISTO.
Swali: Je Ni sahihi kwa Mkristo kupeleka kesi mahakamani?
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.