ROHO ANENA WAZIWAZI

ROHO ANENA WAZIWAZI

Shalom..Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Neno la Mungu linasema katika…

1 Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”

Maana ya kunena waziwazi ni kwamba…“ananena pasipo maficho yoyote wala pasipo siri yoyote”..yapo mambo ambayo Roho Mtakatifu akiyanena yanahitaji ufunuo mpana kutoka kwake..kwamfano utaona katika kitabu cha ufunuo sehemu kadha wa kadha, anasema “yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”. Au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema “yeye mwenye akili na aweze kuyajua haya yanayozungumzwa maana yake ni nini”..kwamaana inahitajika ufunuo kuyajua.

Kwamfano tunaweza kujifunza mfano mmoja, ambapo Roho hajanena waziwazi.

Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.

28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.

29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”

Hapo Roho kanena..lakini si wazi..kwasababu atakayesoma hajaambiwa nyota ya asubuhi hapo ni nini, wala hajaambiwa hao mataifa atakaowachunga ni wakina nani…maana yake mambo hayo yote yanahitaji ufunuo wa Roho kuyaelewa…hayajanenwa waziwazi..

Lakini katika hiyo 1Timotheo 4 biblia inasema Roho anena waziwazi..kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo….na mafundisho ya mashetani..

Hapo anasema wakizisikiliza roho zidanganyazo…na si wakizitazama au wakiziabudu..bali wakizisikiliza..maana yake hizo roho zinazungumza na zipo nyingi.

Sasa hizo zinazungumzaje?

Roho hizi zinazungumza kwa njia kuu mbili.

1. Katika nafsi ya mtu
2. Kupitia watumishi wa shetani, ambao wamevaa mavazi ya kondoo.

1. Katika nafsi ya mtu ni pale mtu anaposikia sauti au msukumo wa kwenda kufanya jambo lililo kinyume na mapenzi ya Mungu.. Kwamfano kama mtu atasikia sauti ikimwambia akatoe mimba, au akaue, au akaibe, akaabudu sanamu au akafanye uasherat, ukavae nguo za nusu uchi, ukapake lipatick, ukavae suruali kwa mwanamke, ukaende kwa waganga, ukaachane na mke wako/mume wako wa ndoa..n.k.kama akiisikiliza hiyo sauti na kwenda kufanya mojawapo ya hayo tayari atakuwa kasikiliza roho hiyo idanganyayo.

2. Vile vile kama atamsikia mtu au mhubiri akimshawishi kufanya mojawapo ya mambo hayo hapo juu tayari, na kwenda kufanya kama alivyosikia kutoka kwa huyo mtu au mhubiri, tayari atakuwa ameisikiliza roho hiyo na imeshamdanganya, aidha kwa kujua au kwa kutokujua..kupitia huyo mhubiri.

Hivyo Roho anatuambia waziwazi kuwa nyakati za mwisho ambazo ndizo hizi watu wengi sana watakuwa wanazisikiliza hizi roho..na si wachache bali ni wengi..Hivyo ni wajibu wetu kuwa macho,na kuwa makini sana ili tisiwe miongoni mwa hao “wengi”…ndio maana ametuambia waziwazi ili tujue hali halisi, na tuweze kujilinda.

Huu ni wakati wa kuzichunguza sana roho..niliwahi kukutana na mtu akaniambia ameokoka na anaamini sana sauti yoyote inayomjia ndani yake ni ya roho mtakatifu..Nikamuuliza anatumia nini kuipima hiyo sauti.. akasema anatumia hisia tu…hivyo hawezikudanganyika.
Ndugu hata uwe mhubiri mkubwa kiasi gani, hata uwe unanena kwa lugha, hata uwe unatabiri, au unaona maono, hata uwe kila siku unatembelewa malaika..roho za yule adui yetu shetani hazichunguzwi kwa ujuzi au utaalamu au uzoefu fulani au kwa hisia..hapana!! bali zinachunguzwa kwa Neno la Mungu tu..

Maana yake ni kwamba hata kama nimeokoka sio kila sauti inayokuja ndani yangu ni ya kuiamini, bali ni lazima ipimwe na neno la Mungu..kama inakubaliana na Neno hiyo ni sauti kutoka kwa Mungu..lakini kama inapingana na Neno, haijalishi imekuja kwa nguvu kiasi gani, au umekuja na amani kiasi gani, au imekuja na hisia nzuri kiasi gani…hiyo si ya kuifuata ni sauti kutoka kwa yule adui. Biblia inasema..

2 Wakorintho 11:14 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru”.

Na neno la Mungu tunalijua kwa kusoma biblia kwa bidii sana…hiyo ndiyo silaha.
Kumbuka tena usisahau neno hili… Roho anena waziwazi, kuwa nyakati za mwisho wengi watajitenga na Imani, na kusikiliza roho zidanganyazo… ni maombi yangu kuwa mimi na wewe hatutakuwa miongoni mwa hao “wengi”.

Kama hujampokea Yesu mpaka sasa, kwasababu fulani fulani, unazozijua wewe, fahamu kuwa umeshasikiliza roho hizo na zimekudanganya…Hivyo fungua leo macho yako na mgeukie Kristo uanze upya, naye atakupokea na kukusaidia kwasababu anatamani wewe uwe na uzima kuliko wewe unavyotamani.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

MAFUNDISHO YA MASHETANI

JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
bahati miremba
bahati miremba
1 year ago

Asante sana kwa mafundisho naweza penda nipate mafundisho kwa njia ya email : http://www.bahatimiremba@gmail.com