Bwana Yesu alisema sehemu fulani maneno haya ” walakini siku ile na saa ile”..akiwa na maana kuwa Kuna siku inayokuja huko mbeleni, yenye Tarehe yake na mwezi wake, na mwaka wake. Siku hiyo itaitwa tarehe Fulani ya Mwezi Fulani na mwaka Fulani.
Siku hiyo upande mmoja wa dunia utakuwa ni mchana na mwingine usiku, siku hiyo watu watakuwa wanapika, wengine wanafanya biashara, wengine wanajenga, wengine wapo katikati ya harusi, wengine watakuwa safarini, wengine watakuwa misibani, wengine mashuleni, Wengine watakuwa wamelala, wengine wapo kanisani, wengine watakuwa mahospitalini, wengine mahakamani, wengine wanacheza mpira, wengine wapo disko. Wengine bungeni, wengine magerezani,wengine wanapanga mipango na mikakati ya namna ya kuimarisha vipato vyao na kazi zao n.k…Siku hiyo ndio itakuwa mwisho wa utendaji kazi wa Roho Mtakatifu duniani kwa watu wa mataifa…siku hiyo utapita kitu kinachoitwa UNYAKUO.
Wakati watu wengi watakuwa hawaelewi chochote, kufumba na kufumbua baadhi ya watu watatoweka, wachache sana…Tetesi tetesi chache zitasikika huko na huko kwamba kuna baadhi ya watu wamepotea katika mazingira ya kutatanisha, lakini kutokana na kwamba dunia imelewa na kulemewa na mambo mengi, wengi watasema ni habari za kuzusha, kwani imezoeleka kusikika unyakuo umepita na unakuta hakuna lolote lililotokea. Watasema mwaka 2000 ilikuwa hivyo hivyo, walitabiri na hakuna kilichotokea…mwaka 2002 ikawa hivyo hivyo, wakasema unyao umepita na hakuna lolote, kadhalika mwaka 2012…Na leo tena uzushi mpya umezuka.
Wakati mamia na maelfu ya watu wanapuuzia habari hizo na kuona ni habari za uzushi, upande wa pili kutakuwa na uchungu na vilio kwa wale waliowashuhudia wenzao wakinyakuliwa mbele ya macho yao, wale waliokuwa wanalima pamoja ghafla jirani anatoweka mbele yake, wale ambao walikuwa wamelala na wenzao katika chumba kimoja ambacho kilifungwa na makomeo kwa ndani, na walipoamka kwa ghafla wakakuta hawapo, huku milango bado imefungwa vile vile kwa ndani, wale ambao walikuwa wapo ibadani pamoja kanisani na ghafla wenzao wamepotea, wale ambao wamemwona mtu Fulani kaketi mahali Fulani na kufumba na kufumbua katoweka. Hao ndio watakaoelewa uchungu wa kuachwa. Watalia sana na kuomboleza lakini haitasaidia.
Siku hiyo utakapoona mwanao hayupo, dada yako aliyekuwa ameokoka hayupo, mchungaji wako hayupo, na wewe umeachwa! Itakuwa ni uchungu kiasi gani?. Ukitazama ni masaa machache tu nyuma umetoka kupokea rushwa, ukitazama ni masaa machache tu nyuma umesikia mahubiri ya kukuonya na ulimwengu ukakataa. Ukitazama ni wiki chache tu nyuma uliota ndoto inayokuonya kwamba hizi ni siku za mwisho ukapuuzia. Masaa machache tu ulisikia mahali panazungumziwa habari za unyakuo.
Ukitazama ni siku chache tu nyuma ndio ulianza kupoa, utajisikiaje? Ukitafakari sasa wenzako wanafutwa machozi mbinguni na wewe umebaki ukingojea dhiki kuu na chapa ya mnyama na ziwa la moto milele?, ukitafakari ni disko ndio iliyokuponza, mke au mume unayeishi naye ndio aliyekuponza, binti/kijana unayetembea naye ndiye aliyekuponza, utafutaji mali uliopindukia ndio iliyokuponza, miziki ya kidunia, na tamaa ndivyo vilivyokuponza kuikosa mbingu, utakuwa katika huzuni kubwa kiasi gani.
Ndugu hiyo siku inafika, labda ni leo, au kesho au kesho kutwa hakuna aijuaye! Lakini ipo karibuni sana biblia inasema hivyo…
Mathayo 24:36 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; 41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu 43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.”
Mathayo 24:36 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu
43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.”
Kukesha kunakozungumziwa hapo na Bwana Yesu, sio kujizuia kulala usingizi wa mwilini wakati wa usiku hapana!…Bali maana yake kujizuia kulala usingizi wa rohoni…kwasababu duniani sasahivi ni giza! Ni Giza Nene kutokana na matendo ya giza yanayotendeka, Na sikuzote tabia ya giza ni kusababisha usingizi, siku zote usiku ndio watu wanalala! Sio mchana wakati wa Nuru, Kwahiyo giza lililopo duniani leo linasababisha usingizi mkali wa kiroho, na hivyo tunapaswa tuushinde huo usingizi na kukesha! Kwasababu Bwana atakapokuja hatawachukua watu waliolala bali walio macho!
Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza. 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Bado unaendelea na uasherati? Unaendelea na utoaji mimba? Unaendelea na uvaaji mbaya na ibada za sanamu? Tubu na kumgeukia mwokozi, kabla siku ile na saa ile haijafika. Kwasababu Bwana hapendi kumwona mtu yeyote aangamie, bali ni atubu, vilevile anataka watu wote waingie katika karamu ya mwana wake aliyowaandalia siku ile..Sasa Kwanini uikose?, tubu angali muda unao, na Bwana atakupokea na kukukaribisha katika ufalme wake.
Bwana akubariki! jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.
SADAKA YA MALIMBUKO.
HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
Rudi Nyumbani:
Print this post
Timazi ni nini?
Ni kifaa kidogo kilichokuwa kinatumika zamani katika Ujenzi na hata sasa bado kinaendelea kutumika…kifaa chenye umbo la PIA. Kinakuwa kimetengenezwa kwa chuma kizito kidogo. Na kinafungwa kamba, na kuwa katika hala ya kuning’inia. Na kinaning’inizwa kutokea juu ya ukuta kwenda chini.
Katika Biblia kifaa hichi kimetajwa mara kadhaa (Soma 2Wafalme 21:13, Isaya 28:19-17 na Zekaria 4:10,). Na kifaa hiki kimekuwa kikiwakilisha Upimwaji wa Taifa la Israeli. Bwana alipotaka kutumia lugha ya kupima kiwango cha maovu au wema, mara nyingi alitumia lugha ya kijenzi.
Ndio maana utaona Mfalme Nebkadneza baada ya kumchukiza Mungu aliambiwa “Amepimwa katika Mizani na kuonekana umepunguka” (Danieli 5:27). Kiuhalisia mtu hawezi kuwekwa kwenye mizani ya nafaka na kupimwa!..Hapana bali utaona hiyo ni lugha tu ya kuonesha kiwango cha maovu cha mtu huyo. Mfano mwingine tunaona kwa Nabii Amosi.
Amosi 7:6 “Bwana akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU. 7 Haya ndiyo aliyonionyesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake. 8 Bwana akaniambia, Amosii, unaona nini? Nikasema, Naona timazi. Ndipo Bwana akasema, Tazama, nitaweka timazi kati ya watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe”
Amosi 7:6 “Bwana akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.
7 Haya ndiyo aliyonionyesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake.
8 Bwana akaniambia, Amosii, unaona nini? Nikasema, Naona timazi. Ndipo Bwana akasema, Tazama, nitaweka timazi kati ya watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe”
Hata sasa Bwana ameshika TIMAZI juu ya mtu mmoja mmoja, na juu ya Ulimwengu kwa Ujumla..Anayapima matendo ya kila mtu, aangalie kama yamepunguka! au la!. Kama yanampendeza basi mtu huyo atapata rehema na thawabu kutoka kwa Mungu na kupendwa sana, lakini kama yamepunguka basi kuna hatari ya kuhukumiwa kama Mfalme Nebkadneza alivyohukumiwa.
Je matendo yako yanastahili hukumu au thawabu?. Jibu unalo. Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako. Mlango wa Neema upo wazi, fanya hima uingie, kabla siku muda wako wa kuishi duiniani haujaisha.
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.
KUACHA KUVUTA SIGARA.
KUOTA UPO UCHI.
KUOTA UNAPAA.
KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.
Biblia inasema katika Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.” Hivyo Neno la Mungu ni Taa!
Maisha ya Mtu aliyeokoka yanafananishwa na Mtu asafiriye (Waebrania 11:13 na 1Petro 2:11). Na safari mtu aliyeokoka asafiriyo ni safari ya USIKU na si Mchana.
Hatari ya Kwanza: ni kukutana na wanyama wakali: Wanyama wote wararuao na wadhuruo huwa wanatembea Usiku, wanyama kama chui, simba, fisi, mbweha pamoja na nyoka huwa wanatafuta mara nyingi mawindo yao wakati wa Usiku.
Na viumbe vyote vinavyotembea usiku vinafunua viumbe vya rohoni vilivyo viovu ambayo ni mapepo..Ndio maana wanaojihusisha na uchawi wanatumia viumbe kama popo, bundi, fisi, chui, nyoka na viumbe vyote vinavyotembea gizani kufanya shughuli zao.
Wakati wa Usiku ni rahisi kupungukiwa umakini kutokana na Usingizi, au giza. Siku zote giza linaleta usingizi, wanaosafiri na magari usiku ni rahisi kupata ajali kuliko wanaosafiri mchana.
Hivyo ili kuzuia hatari zote hizi Msafiri asafiriye usiku anahitaji kuiongeza umakini sana anapotembea usiku na pia anahitaji TAA ITAKAYOMWONGOZA NJIA YAKE. Hakuna namna yoyote anaweza kukwepa matumizi ya Taa. Awe anatembea kwa miguu au kwa Gari, Taa ni Lazima.
Na sisi wakristo tupo safarini. Dunia ndio NJIA yetu. Na dunia yote sasa ni giza Kutokana na matendo ya giza yanayoendelea ulimwenguni kote. Uzinzi ni matendo ya giza, ulevi ni matendo ya giza. Kadhalika uchawi, rushwa, utoaji mimba, ulawiti, uvutaji sigara. Mauaji, usagaji na uchafu wa kila aina..Mambo hayo yanakoleza giza lililopo ulimwenguni.
Na sisi hatuna budi kupita katikati ya hilo giza ili tutokezee ng’ambo ya pili, hakuna kuingia mbinguni pasipo kupitia duniani!. Kwasababu hiyo basi tunahitaji Mwanga katika hili giza Nene!. Na Mwanga si kingine bali ni NENO LA MUNGU, Lililovuviwa na Roho Mtakatifu.
Neno la Mungu linaposema Usizini, ni kwa faida yetu! Neno hilo ni mwanga wa njia zetu, maana yake tukizini tumeizimisha taa. Na hivyo ni rahisi kupotea. Na kushambuliwa na wanyama wakali. Kadhalika na maneno mengine yote ambayo Biblia imekataza kama rushwa, usengenyaji, chuki, wivu, hasira, faraka, uchungu, wizi, uuaji, ulevi n.k hayo yote ni matendo yanayozima taa zetu na hivyo kutuweka hatarini katika safari yetu.
Zaburi 119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”.
Hivyo ukitaka kuisafisha njia yako!. Utaisafisha tu kwa kulitii na kulifuata Neno la Mungu ambalo hilo ndilo Taa yetu.
Kumbuka Bwana Yesu anakuja, na wala hatakawia. Hivyo kama hujaoshwa dhambi zako kimbilia Kalvari haraka kabla mlango wa Neema haujafungwa. Na Bwana atakuokoa.
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
BARAGUMU NI NINI?
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
JE KUJIUA NI DHAMBI?
Wakatoliki wanaabudu sanamu?
Rudi Nyumbani
SWALI: Huyu Yeshuruni ni nani kwenye biblia?. Na kwanini alinenepa na kumdharau mwamba wa wokovu wake (Kumb.32:15)?.
JIBU: Yeshuruni ni jina lingine la Taifa la Israeli lililotumika katika biblia ya kiyahudi hususani katika mashahiri,..Neno hili linaonekana mara 4 katika biblia soma (Kumbukumbu 32:15, 33:26, 33:5 na Isaya 44:2).
Hivyo tukirudi pale kwenye Kumbukumbu 32:15-18
Inasema..
Kumbukumbu 32:15 “Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake 16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo. 17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa. 18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau,”
Kumbukumbu 32:15 “Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake
16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.
17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa.
18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau,”
Maneno hayo aliyazungumza Musa akiwa jangwani, kama unabii, kuonyesha jinsi Israeli watakavyokuja kumsahau Mungu wao huko mbeleni watakapofika katika nchi yenye maziwa na na asali, kwa kufanikiwa kwao, kwa nchi kuwazalia, kwa kutokuwa tena na jangwa, wala kula chakula cha aina moja, kwa kufanya biashara na kufanikiwa na kuwa matajiri, watamsahau Mungu wao aliyewatoa katika ile nchi ya Misri, watamsahau yule Mungu ambaye walikuwa wanamtumainia walipokuwa jangwani kwenye shida, watamdharau na kugeukia miungu mingine. Na unabii huo ulikuja kutimia vilevile kama Musa alivyotabiri katika shahiri lile walipofika nchi ya ahadi.
Hivyo ukikutana na Neno hilo Yeshuruni ni nani, basi ufahamu hilo ni jina lingine la Israeli.
Hata leo hii ni kawaida ya watu kumtafuta Mungu wakati wa shida, tu, lakini pale wanapofanikiwa, au pale ambapo hawana haja ya kitu chochote, wana afya, wana mali basi Mungu kwao si kimbilio tena,..wapo tayari hata kuutakana wokovu na kuona kama ni ushamba.Ndio maana Bwana Yesu alisema ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko Tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu..
Utajiri wa aina yoyote ile ni ukweli usiopingika kuwa ni kikwako kikubwa sana katika ufalme wa mbinguni, kama vile umaskini uliopindukia ulivyo. Haimaanishi kuwa tusiwe matajiri lakini tunapaswa tutumie hekima katika kumwomba Mungu atupe kile ambacho ni sawasawa na uwezo wetu, tusije tukanenepa na kuwanda kama Yeshuruni na kumsahau Mungu, kama Aguri bin yake alivyotushauri katika Mithali 30:9.
Mithali 30:8“…………Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. 9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.”
Mithali 30:8“…………Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.”
Ubarikiwe,jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?
Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
2Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”
2Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”
Saa ya Wokovu ni sasa na sio kesho! Leo ndio wakati uliokubalika, dakika hii ndio wakati uliokubalika wa kupoekea Wokovu, usiseme kesho! Kwasababu kesho huwa inajipangia yenyewe mambo yake. Jambo ambalo wengi hawalijui ni kwamba Siku ndiyo inayotengeneza matukio na sio mtu anayetengeneza matukio ya siku.
Utapanga kesho ufue na kuanika nguo zako, lakini hiyo kesho mvua ikanyesha kubwa hata ikakuzuia wewe kufua. Umepanga kesho usafiri lakini hali ya hewa ikakuzuia. Umepanga kesho usafiri kwenda mashariki lakini ghafla ukajikuta unakwenda kusini kwenye mazishi.
Hivyo kesho si ya kuitumainia kabisa kwasababu imejaa mambo ya kushtukiza. Biblia inasema..
Mithali 27:1 “Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja”.
Mathayo 6:34 “Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.
Hivyo hakuna Tarehe, wala Mwezi wala Mwaka uliopangwa kwa wokovu…SAA YA WOKOVU NI SASA! na WAKATI ULIOKUBALIKA NDIYO SASA, na SIKU YA WOKOVU NI SASA.
Je! Umeokoka? na kama Bado unasubiri nini? Unajitumainisha na ya kesho? je wewe una hekima kulika Mungu anayekuambia kuwa usijisiu kwa ajili ya kesho? Hivyo ni kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, na Roho Mtakatifu anaugua ndani yako sasa juu ya dhambi zako. Usikawie, hapo ulipo piga magoti, nyosha mikono yako juu!. Tubu kwa kumaanisha kabisa kuhitaji rehema kutoka kwa Bwana.
Bwana anakuona moyo wako naye atakuokoa sasa! kwasababu amesema mwenyewe saa ya wokovu ni sasa! Hivyo leo leo utakuwa umeokoka kama umedhamiria kutubu!
Sema Bwana Yesu!, ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi! naomba unisamehe dhambi zangu zote, Naahidi kutokuzifanya tena! Nisaidide Bwana. Niondoe kutoka katika mstari wa wanaokwenda Jehanamu niingize katika orodha ya wanaokwenda mbinguni. Nipe moyo safi leo! naomba Roho wako Mtakatifu aingie ndani yangu sasa! niwe Mtakatifu. Nakiri kwamba wewe ndiye Mwokozi wangu, na Bwana wangu na Mungu wangu, katika Jina la Yesu.
Kama umefuatiliza sala hiyo. Basi umeshaokoka sasa! katika saa hii hii, kwasababu yeye anasema “Wakati uliokubalika nalikusikia“. Hivyo ameshakusikia. Kwahiyo sasa Chukua hatua ya kiimani kutafuta kanisa la kiroho ambalo utaweza kubatizwa ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu kama hujabatizwa! Hiyo yote ni ili kuutia muhuri wokovu ambao umeshaupata moyoni mwako leo.
Kama utapata shida katika kutafuta kanisa, unaweza kuwasiliana nasi tutakusaidia kukuelekeza kanisa karibu na mahali ulipo ambapo utaweza kupata huduma hiyo ya ubatizo na ya kufanya ushirika na watu wenye Imani moja na wewe. Tutumie ujumbe mfupi kwa kupitia namba hizi 0789001312.
Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?
WhatsApp
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio mwanga wa njia zetu na taa ya miguu yetu. Zab 119:105..Leo tutajifunza kwa ufupi sana juu ya kulipa Zaka, Kimaandiko Zaka ni fungu la 10, yaani sehemu ya 10 ya mapato ya mtu anayatoa kwa Mungu. Kwahiyo zaka ni mojawapo ya aina ya sadaka.
Kabla hatujaenda kujifunza kuhusu umuhimu wa kulipa zaka, kama ina ulazima au la! Hebu tujifunze kidogo historia ya ZAKA.
Zaka kwa mara ya Kwanza ilianza kutolewa na mtu anayeitwa Ibrahimu, ambaye anajulikana kama Baba wa Imani.
Mwanzo 14:17 “Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. ABRAMU AKAMPA FUNGU LA KUMI LA VITU VYOTE”.
Mwanzo 14:17 “Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. ABRAMU AKAMPA FUNGU LA KUMI LA VITU VYOTE”.
Ibrahimu alimpa fungu la 10 huyu Melkizedeki, huyu Melkizedeki alikuwa ni Mungu aliyekuja katika Mwili wa kibinadamu… na pia anajulikana kama Kuhani Mkuu, mfano wa Mwana wa Mungu (Yesu Kristo) hana baba, wala mama, wala hana mwanzo wa siku wala mwisho wake. Kwahiyo alikuwa ni Mungu mwenyewe aliyekuja katika mwili wa kibinadamu.
Sasa wakati Abramu ametoka kumwokoa ndugu yake Lutu ambaye alikuwa ametekwa yeye pamoja na wanawe, njiani wakati anarudi akakutana na Huyu Melkizedeki, na huyu Melkizedeki alikuwa amebeba Divai na Mkate, akampatia Abramu na kwasababu Abramu alimpenda sana Mungu, hakuona vyema kupokea bure bila kutoa chochote…zaidi ya yote Mungu amemwonekania na kumfanikisha katikati ya maadui zake na kuwashinda! Hivyo ndani yake kuna kitu cha kipekee kikamgusa akaona si vyema kutomrudishia chochote Mungu wake, hivyo akaamua mwenyewe pasipo kuambiwa na mtu yeyote kumtolea Mungu wake sehemu ya 10 ya vitu vyake!!! O huo ni moyo wa namna gani? Kumbuka hakuambiwa hata na Mungu afanye vile, ni yeye mwenyewe tu kuna kitu ndani yake kilimfanya ajisikie vibaya endapo angemwona Mungu wake anaondoka mikono mitupu, na hicho si kingine zaidi ya Roho Mtakatifu.
Sasa wakati huo kulikuwa hakuna sheria yoyote, wala amri 10 na Mungu hakuingia Agano na Ibrahimu kuhusu zaka, Miaka kama 400 hivi baadaye ndipo wana wa Israeli, walikuja kupewa sheria na Mungu! Na miongoni mwa hizo sheria ilikuwa ni pamoja na kulipa zaka!, ilikuwa ni lazima kulipa zaka, mtu asipolipa zaka ilikuwa inahesabika kwake kuwa ni dhambi!, na mbele za Mungu ni kama mwizi (Malaki 3:8-9).
Lakini sasa hatuishi kwa sheria bali kwa Imani, na Imani tunayoizungumzia ni Imani ile ile ya kwanza kama ya Ibrahimu, yaani Imani ya kufanya mambo bila ya kusukumwa sukumwa, na Imani hiyo ndio kama hiyo ya Ibrahimu, ya kumtolea Mungu fungu la 10 pasipo masharti!..Ibrahimu alitoa pasipo masharti, wala sheria, wala torati kwasababu Torati hata bado ilikuwa haijaja, wala kulazimishwa, wala kusukumwa wala kuombwa, wala kumwuliza Mungu, wala kuhubiriwa na mtu yeyote bali alitoa kwa Imani na kwa moyo, akitafakari kwamba vyote vimetoka kwa Mungu, na Mungu ndiye mpaji wangu (Yehova-YIRE), hivyo kama yeye amenipa sehemu kubwa ya vitu hivi, basi mimi nitamrudishia walau sehemu ya 10 ya vitu alivyonipa. Na akajiwekea hiyo kuwa ndio sheria yake daima! Kila sehemu ya 10 anayopata anamrudishia Mungu.
Ndugu, Ibrahimu alikutana na Melkizedeki, na hata sasa huyu Melkizedeki yupo naye si mwingine bali ni Bwana wetu Yesu Kristo, maandiko yanalithibitisha hilo katika…
Waebrania 6:20 “alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki”.
Waebrania 7:1 “Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; 3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. 4 Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara”.
Waebrania 7:1 “Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
4 Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara”.
Waebrania 5:5 “Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 6 kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.
Waebrania 5:5 “Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
6 kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.
Umeona Kristo amefananishwa na Melkizedeki, na kama Melkizedeki alipewa sehemu ya 10 na Ibrahimu, kadhalika Kristo naye anastahili sehemu ya 10, kwasababu yeye ndiye Melkizedeki wa Agano letu, na kama Melkizedekia alivyompigania Ibrahimu ndivyo Kristo anavyotupigania sisi sasa hivi,
Na kama Ibrahimu alimpa Melkizedeki fungu la 10 pasipo masharti, wala pasipo torati, wala pasipo sheria yoyote, wala pasipo kuhubiriwa na mtu, wala pasipo kushauriwa na mtu, wala pasipo kusukumwa na mtu yeyote ndivyo hivyo hivyo leo hii tunapaswa tumtolee YESU KRISTO fungu la 10 pasipo sheria yoyote, wala pasipo masharti yoyote, wala pasipo mahubiri yoyote, wala pasipo kusukumwa na mtu..Linapaswa liwe ni jambo linalotoka moyoni kwamba tunatambua uwepo wa Yesu Kristo katika maisha yetu na hivyo tunamheshimu kwa kumtolea fungu la 10, yeye hana shida na fedha! Lakini anaitazama mioyo yetu!. Na Bwana Yesu mwenyewe aliruhusu hilo katika (Mathayo 23:23).
Ukiona mtu anapinga kulipa ZAKA!(Na huku ameshaujua ukweli) Na anapinga kumtolea Mungu, Huo ni uthibitisho kuwa hana ROHO MTAKATIFU ndani yake! Ni moja ya uthibitisho wa mtu aliyekosa Roho Mtakatifu ndani yake!..Kwasababu ni wazi kuwa hampendi Mungu, kwasababu hawezi kumshukuru kwa kutoa hata sehemu ya 10 ya mali zake na kumrudishia yeye, ingawa anavuta pumzi bure, anakanyaga ardhi ambayo sio yake bure, anakula chakula ambacho hajui kimetengenezwaje tengenezwaje! Hathamini hata Kristo aliyeotoa uhai kwa ajili yake bure..Kwa ufupi ni mtu asiye na shukrani.
Na mtu wa namna hiyo atawezaye kumshukuru Mungu kwa kutoa sehemu ya 10 ya maisha yake kuhubiri Injili?, atawezaje kutoa kutoa hata uhai wake kwaajili ya Injili?, au atawezaje kuifia Imani? Kama tu sehemu ya 10 ya fedha yake hawezi kuitoa?. Huyo Mtu atawezaje hata kuacha vyote na kumfuata Kristo kama tu sehemu ya 10 kutoa ni vita?..Atawezaje kumtolea Mungu katika vyote alivyonavyo kama Yule mwanamke aliyetoa senti mbili na Bwana akamsifia? Tafakari tu!
Hivyo ZAKA sio kitu cha kukwepa kabisa! Hakitolewi kwa sheria wala kwa torati, wala kwa imeandikwa wapi kwenye biblia, bali kwa moyo kama vile Ibrahimu!..Kama huna kazi yoyote inayokupatia kipato hapo upo huru!, lakini chochote unachokipata tofauti na kazi kitolee sehemu ya 10 katika hicho na kumrudishia Mungu, huna kazi lakini umepewa zawadi kiasi Fulani cha fedha kitolee sehemu ya 10, na utoe kwa moyo pasipo kulazimishwa, kwasababu Mungu sio mkusanyaji mapato! Anataka tumtolee kwa Moyo na kwa furaha, huku tukielewa umuhimu wa kumtolea yeye kama Ibrahimu alivyofanya.
Kitakachompeleka mtu kuzimu sio kitendo cha kukiuka kulipa zaka au kuzini, au kuiba, au kutukana hapana kitakachompeleka mtu kuzimu ni kumkosa Kristo moyoni mwako, akaaye kama Roho Mtakatifu, ambapo sasa matokeo ya kutokuwa na Roho Mtakatifu ndio hayo sasa atakuwa mwizi, mwasherati, mtukanaji, atakuwa ni mtu asiyekuwa na Moyo wa Utoaji kabisa, likija suala la utoaji ni vita, anakuwa hawezi kuwasaidia wengine, na pia hawezi kuchangia chochote katika ufalme wa mbinguni katika utoaji wake, pia anakuwa mtu asiyesamehe Kwasababu Mtu aliye na Roho Mtakatifu hawezi kufanya mojawapo ya hayo mambo kwasababu Roho Mtakatifu atakuwa anaugua ndani yake kuhusu dhambi na atakuwa anaugua pia kuhusu ni kwanini hamtolei Mungu, hivyo hawezi kukwepa kulipa zaka kama vile asivyoweza kukwepa kuwasaidia wengine au kusali.
Upo usemi unaosema kwamba, mimi ni mkamilifu katika kila kitu! Isipokuwa ni zaka tu ndio sitoi!
Bwana akubariki jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Kumbukumbu 22:8 “Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kando-kando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko”.
Bwana Yesu alisema, mtu yeyote anayeyasikia maneno yangu na kuyatenda anafananishwa na mtu aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba…(Mathayo 7:24), Hii ikiwa na maana kuwa kumbe Maisha ya kila mtu aliyeokoka ni sawa na nyumba inayoijenga yeye mwenyewe,..Hivyo kila mtu anapaswa awe makini anapoijenga nyumba yake sio tu pale anapoujenga msingi wake bali pia mpaka pale anapomalizia…
Kwamfano tutaona hapa Bwana Yesu alikuwa anasisitiza juu ya msingi, ambao ndio mwanzo wa ujenzi wa maisha ya mtu, kwamba ukitaka nyumba yako(Maisha yako) yasiwe kazi bure basi zingatia ni ardhi gani unayoijengea nyumba yako, kama ni mwamba (ambao ndio maneno ya Yesu Kristo yenyewe) basi fahamu kuwa msingi wako nyumba yako utakuwa salama na nyumba yako itasimama imara milele lakini kama ni nje ya Kristo basi ujue Maisha yako unayoyaishi sasa hivi ni kazi bure kwasababu yatafikia mwisho yatakoma na utakuwa umepata hasara kubwa..
Lakini Sio tu kufanikiwa kuijenga nyumba yako juu ya mwamba imara, unapaswa pia uzingatie umaliziaji wa nyumba yako ili iwe katika ujenzi bora na salama..Kama tunavyosoma hapo juu enzi za agano la kale Mungu alitoa amri kwa waisraeli wote, pindi tu wanapomaliza kujenga nyumba zao, hawapasi kuzifunika tu kwa sakafu au matofali na kuziacha hivyo hivyo bila uzio wowote kama ujenzi mwingi unavyofanyika sikuhizi wa kuweka mabati, hapana bali Mungu aliwapa maagizo wahakikishe kuwa wanaweka ukuta kando-kando ya dari zao, ulionyanyuka, kusudi kwamba ikitokea mtu amepanda kule, na akateleza bahati mbaya, basi ule ukuta ulio kando kando ya dari umzuie asianguke mpaka chini, tofauti na ujenzi mwingi wa sasa hivi ulivyo, mtu akiteleza kwenye bati basi moja kwa moja ni mpaka chini, na pengine kumsababishia majeraha ya kudumu au mauti kabisa. Angalau baadhi ya magorofa marefu yana uzio huo kule juu kabsia, ingawa si yote.
Hivyo nyumba zote, na majengo yote ya kiyahudi ndivyo yalivyojengwa enzi zile. Na kama mtu asipofanya hivyo na ikatokea mtu akaanguka darini kwake, basi damu ya huyo mtu, Mungu ataitaka juu ya huyo mwenye nyumba.
Kama tulivyoona mkristo kweli anaweza akawa ameanza vizuri katika ujenzi wake, ameokoka, amemwamini Yesu Kristo, amepokea uzima wa milele, lakini hazingatii kuchukua tahadhari katika nyumba yake anayoijenga, haweki kuta, hajiwekei mipaka ya njia zake, hajui kuwa wapo watu wanamwangalia, wapo watu wanayatambelea Maisha yake kila siku, wanapanda mpaka juu ya dari lake, mahali ambao anadhania watu hawawezi kufika,Sasa kwa kutolijua hilo wale watu wanapofika, na kukutana na kikwazo kidogo tu, pengine wanamwona ni mvaaji wa vimini, unatembea nusu uchi barabarani halafu unasema umeokoka, ni rahisi wao kuanguka, na kusema kama wokovu ndio huu, ni heri niendelee kuwa kahaba milele…Hajui kuwa ameshamkosesha yule mtu na damu yake itatakwa juu yake.
Unakwenda disko, unatukana , na bado unasema umeokoka, unacheza kamari, una-bet na huku bado unasema umeokoka, wale watu wanaokutazama, wakiona mapungufu kama hayo, umewasababishia wao kuanguka mara mbili Zaidi. Ni heri ungesema sijaokoka wasingekuwa na la kujikwaa, na hiyo yote ni kwasababu hujiwekei kuta za kuilinda nyumba isiwe ya lawana.
Unasikiliza miziki ya kidunia, muda huo huo unamwimbia Mungu, wale watu wanaokuzunguka watakuonaje? Watasema kuna wokovu kweli hapo? unakula rushwa, unaongea matusi hivyo vyote ni vikwazo, unawasengenya wengine, hatujui kuwa sisi ni barua inayosomwa na watu wote. Ujenzi wetu wa mwisho unapaswa uthaminiwe kama ulivyokuwa ule wa kwanza.
Vinginevyo tutajikuta tunakwenda kulaumiwa kwa kuwakosesha wengine,. Na adhabu ya kuwakosesha wengine ni kubwa Zaidi, Bwana Yesu alitoa mfano wake na kusema ni heri mtu wa namna hiyo angefungiwa jiwe la kusagia na kutupwa baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hao.
Hivyo kama tumedhamiria kweli kumfuata Kristo, basi kila siku tujiangalie, tujiwekee mipaka, tuhakikishe ndani yetu hakuna mahali popote pa kumkwaza asiye amini..kuvaa vizuri ni mipaka!, kutokushiriki usengenyaji ni mipaka, kutoshiriki mazungumzo ya mizaha na kujiheshimu ni mipaka…Bwana atusaidie sote katika hilo.
Ubarikiwe. Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
HAMJAFAHAMU BADO?
NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.
NGUVU YA UPOTEVU.
http://wanatai.wingulamashahidi.org/
Ni muhimu kujifunza nini maana ya kukua kiroho,Namna ya kukua kiroho, faida za kukua kiroho. Na pia ni vizuri kujifunza mbinu za kukua kiroho.
Roho ni Utu wa Ndani wa Mtu ule unaozungumziwa katika kitabu cha Waefeso 3:16. Na utu huu wa ndani unakuwa si kwa kimo, bali kwa MAARIFA.
Mtu aliyemchanga kiroho anakuwa ana maarifa machache sana yamhusuyo Mungu. Haijalishi ana elimu nyingine yoyote nyingi kiasi gani, au ana elimu ya kidunia kiasi gani. Hivyo kukua kiroho maana yake kuongezeka maarifa katika kumjua Mungu.
Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa hakuna mtu yeyote duniani ambaye ameshakuwa kiroho, na kufikia kiwango ambacho ndio mwisho. Hapana kila siku tunakuwa kiroho, haijalishi tuna maarifa kiasi gani kuhusu Mungu. Bado kila siku tunamsoma yeye kwasababu yeye hamaliziki.
Hivyo njia pekee ya kukua kiroho angalau kufikia kiwango fulani ambacho kitakupa ujasiri wa kuweza kuzidhibiti hila na mbinu za yule Adui. Ni kukaa chini kujifunza Neno la Mungu. Wengi wanaikwepa njia hii na kufikiri kuwa kuna njia nyingine ya mkato ya kukua kiroho, labda ya kuombewa, au kuwekewa mikono. Hakuna njia ya mkato zaidi ya hiyo ndugu!
Mbinu ya kukua kiroho inafananishwa sana na mbinu ya kukua kimaarifa shuleni, ili mwanafunzi afaulu vizuri njia pekee ni kusoma kwa bidii na kuzingaia yale waalimu wanayomfundisha..Kadhalika na sisi wakristo njia pekee ya kukua kiroho ni KULISOMA NENO KWA BIDII. Na kufuatilia kwa makini yale yanayofundishwa na watumishi wa Mungu walio wa kweli.
Na watumishi hao ni zile karama kuu tano, Mitume, Manabii, wainjilisti, waalimu na Wachungaji. Sio Mitume na Manabii na Waalimu unaowaona leo ambao Mungu wao ni tumbo kama biblia inavyosema..Bali Waalimu na wachungaji wanaofundisha kweli yote kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu. Hao ndio wa kuwafuatilia kwa makini, kama vile mwanafunzi amfuatiliavyo mwalimu darasani..
Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.
Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.
Faida za kukua kiroho tunazipata katika mstari wa 13 na wa 14 unaosema…”
13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”
Lengo la kukua kiroho hata tutakapofikia cheo cha kimo cha Kristo. Ni ili tusichukuliwe chukuliwe na kila upepo wa elimu, kwa ujanja wa watu..Kwamfano utasikia watu wanakwambia mti fulani unasababisha kifo kwa wanafamilia. Au utasikia usikae baharini saa saba mchana kuna majini. au utasikia leo kimezuka hichi kanisani watu wanalishwa majani, wengine nyoka. Wengine wataambiwa ili wafunguliwe na matatizo yao watoe pesa kiasi fulani. Ili wafanikiwe wanunue mafuta haya au yale ya upako n.k
Hayo yote ndio yanayoitwa “upepo wa elimu” ambayo huwezi kuyashinda kama ni mchanga kiroho. Hivyo unapokuwa kiroho hizi Elimu zinakuwa hazikupelekeshi..Kunakuwa hakuna elimu yoyote inayozuka inataayoweza kukuchukua kwasababu una Elimu ya kutosha kuhusu Neno la Mungu. Haleluya.
Hivyo hizo ndio mbinu za kukua kiroho. Kwanza Soma Neno kwa bidii binafsi. Pili Jifunze kutoka kwa Watumishi wa Mungu, ambapo unaweza kusikiliza mahubiri kwa njia za semina, mitandano, kwenye vitabu n.k.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.
JE! MUNGU NI NANI?
AMANI YA BWANA /AMANI YA MUNGU.
Utukufu wa Mungu ni nini?
Utukufu ni heshima fulani ya hali ya juu inayomfunika mtu au kitu. Wanadamu tuna utukufu wetu, Wanyama wanao utukufu wao kadhalika Mungu naye anao utukufu wake.
Sasa utukufu wa Mungu ni nini/ ni kitu gani?
Jibu: Utukufu wa Mungu ni UTAKATIFU! Ndio Heshima ya juu kabisa Mungu aliyo nayo..Yeye anatambulika kwa utakatifu wake, ambao ni ukamilifu, usafi na HAKI, Hilo ndilo vazi lake kuu, na kitambulisho chake na Heshima yake.
Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. 19 Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. 20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. 21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; 22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita;”
Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako.
18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako.
19 Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.
21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba;
22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita;”
Kutoka 34:5″ Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. 6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne”.
Kutoka 34:5″ Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana.
6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne”.
Hivyo huo ndio utukufu wa Mungu, (Utakatifu na Ukamilifu), yeye ni mwenye rehema, mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu na si mwepesi wa hasira kwa ufupi ni “UTAKATIFU”..
Lakini pia pamoja na kwamba ni mwenye Huruma lakini bado pia hachukuliani na uchafu ndio maana anasema hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia..Hatamwesabia mwasherati, mzinzi, mwongo, mlevi, muuaji, msengenyaji kuwa hana hatia.
Ikimaanisha kuwa Utukufu wake alionao wa UTAKATIFU NA UKAMILIFU, Anataka na sisi tuwe nao.
Walawi 11:45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
Je! Utukufu wa Mungu upo juu yako nawe pia?..Kumbuka utukufu wa Mungu ni utakatifu, na biblia inasema hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao…(Waebrania 12:14).
Kwahiyo matendo yote yasiyotokana na utakatifu ndio yanayoondoa utukufu juu ya mtu.
Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”
Na huo Mtu huwezi kuupata ukiwa nje ya Kristo, hivyo ni lazima UOKOKE! Kwa kutubu na kumaanisha kuacha dhambi, kisha ubatizwe katika ubatizo sahihi kwa maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu kwaajili ya ondoleo la dhambi sawasawa na Matendo 2:38, na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako,. Ambaye ndiye utukufu wa Mungu, atakayekusaidia kuwa Mtakatifu kama vile jina lake lilivyo na kukuongoza katika kweli yote ya Biblia.
Kumbuka anasema “basi mtakuwa watakatifu kwakuwa mimi Bwana ni Mtakatifu”
Bwana akuabariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
SAYUNI ni nini?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
Malimbuko maana yake “kitu cha kwanza kuja au kuzaliwa au zao la kwanza”, kwa lugha ya kiingereza “first fruits”…Katika Biblia agano la kale mtoto wa kwanza wa kiume kuzaliwa alikuwa ni malimbuko. Na huyo ni lazima awe malimbuko kwa Bwana.
Mwanzo 49:3 “Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu”.
Na sio tu watoto wa kwanza wa kiume, Bali hata wanyama wa kwanza na mazao ya kwanza ya nchi yote hayo yaliitwa malimbuko, na yalipaswa yatolewe pia kwa Bwana.
Mambo ya Walawi 23:9 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;”
Bwana alituoa maagizo kwa wana wa Israeli wote kutoa malimbuko katika mazao yao, yaani kupeleka sehemu ya kwanza ya mavuno yao nyumbani kwa Mungu, kuonesha shukrani zao mbele za Mungu kwa kupewa mazao..
Kama Bwana asingewapa mvua basi wasingepata hata hicho kidogo, kwahiyo “walimrudishia Bwana sehemu ya kwanza kabisa ya mazao yao”, kuonesha kuwa Mungu ni wa Kwanza na mengine yatafuata.
Jibu ni ndio! ilikuwa na Baraka nyingi, kwasababu siku zote kitu cha Kwanza kumtolea Mungu kina nguvu kuliko cha Pili. Nguo mpya ambayo haijavaliwa na mtu ina thamani zaidi, na heshima zaidi kuliko ile ya Mtumba.
Raisi wa kwanza wa nchi, huwa anayoheshima kubwa Zaidi kuliko maraisi wengine wanaofuata. Kadhalika sadaka ya kwanza kabisa inayofika mbele za Mungu ina nguvu kubwa zaidi kuliko zinazofuata..Na sadaka hiyo ni ya “malimbuko”.
Kadhalika sadaka ya malimbuko ndiyo inayobariki kazi yote inayofuata, mshahara wa malimbuko ndio unaobariki mishahara mingine yote inayofuata. Tutakuja kuona hapo chini kidogo, ni kwa namna gani Kristo aliitwa limbuko lao waliolala, ikasababisha baraka kwa wote watakaolala kama yeye.
Jibu ni ndio! Kama tunalipa sadaka za Zaka, Malimbuko nayo ni lazima..Na baraka zake ni zile zile…Kwamba cha kwanza ni bora kuliko cha pili, haijalishi cha pili kitakuwa na wingi gani..lakini cha kwanza ni cha kwanza tu.
Na pia Roho Mtakatifu ndani yetu anatushuhudia, kwamba hiyo kazi kama Mungu asingeibariki basi tusingepata chochote, kwahiyo tunamheshimu Mungu na kumwonyesha kuwa yeye kwetu ni wa KWANZA kwa vitendo! kwahiyo tunampa Malimbuko yetu.
Kama umeajiriwa au umejiajiri, Mshahara wa Kwanza unaoupata unaupeleka kwa Bwana. Usiogope kupungukiwa, wala usiwaze waze utapata vipi fedha, yeye aliyekupa hiyo kazi anajua zaidi kuliko wewe, anasema maua haifanyi kazi na bado hayasokoti yanazidi kupendeza tu. kitu ambacho hata Sulemani katika fahari yake, hajawahi kuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo!. Kama Mungu anayavisha maua ya kondeni vizuri hivyo je si zaidi sisi?. (Mathayo 6:28)…hivyo usiangalie mazingira yanayokuzunguka mtolee Bwana sehemu ya kwanza.
Kadhalika Faida ya kwanza ya Biashara yoyote iliyo halali uliyojiajiri ni hivyo hivyo, sehemu ya kwanza ya mazao yako ya shambani, kama umevuna debe 10 mpelekee Bwana, mifugo yako imezaa wazaliwa wa kwanza mpelekee Bwana, au ibadilishe katika fedha, uipeleke nyumbani kwa Bwana.
Kumbuka kama umeshatoa mzaliwa wa kwanza wa mfugo wako, hao wengine hupaswi kutoa kama malimbuko. Hao utatoa tu kama sadaka na kwa jinsi Bwana atakavyokujalia. Na kwa jinsi utakavyopenda wewe kutoa, haina masharti!
Kumbuka pia kama umeacha kazi fulani na kwenda kuanza nyingine, ambayo inazalisha kwa namna nyingine, na ina mkataba mwingine wa kukuingizia kipato, hapo ni lazima utoe tena limbuko kwa hiyo kazi mpya ulioanza. Kwa ulinzi wa kazi yako.
Mtu wa Kwanza kufufuliwa alikuwa ni Kristo! Lazaro alifufuliwa lakini alikufa tena…Hivyo ufufuo wake haukuwa na nguvu ya umilele, lakini Yesu alifufuliwa na hawezi kufa tena yupo mpaka leo, kwahiyo yeye ndiye mzaliwa wa kwanza wa walio kufa, (LIMBUKO).
Na kutokana na Mungu kumtoa kaburini na kumleta juu kama Limbuko, amesababisha hata sisi tuliomwamini tutakaofuata kufa kama yeye, nasi pia tupate hiyo ofa ya bure ya kufufuliwa katika siku ile! haleluya!
Hivyo kama sio Mungu kumtoa Yesu kuwa limbuko, baraka ya kufufuliwa sisi wengine tusingekuwa nayo.
1Wakorintho 15:20 “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja”.
1Wakorintho 15:20 “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.
21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.
22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja”.
Wakolosai 1:18 “Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote”.
Hiyo ndiyo faida ya “kutoa sadaka ya malimbuko”, Inakuwa inabariki mazao mengine yaliyosalia..Kama Bwana Yesu alivyotubariki sisi tutakaokufa katika yeye. Tunalotumaini la ufufuo, kwasababu yeye amefanyika kuwa mtangulizi wetu, Na wewe unalo tumaini la kufufuliwa kazi yako upya, au biashara yako, au kilimo chako endapo kitasuasua kama ulitoa limbuko(kama sadaka ya utangulizi)! siku ile ulipoianza hiyo kazi,
Lakini pamoja na hayo yote! haitakufaidia chochote, kama utatoa sadaka ya malimbuko na huku maisha yako yapo nje ya wokovu, huku bado ni mlevi, bado ni msengenyaji, bado ni mtukanaji, bado ni mfanyaji masturbation, na bado kahaba, bado mla rushwa..Mungu wetu hafanyi kazi ya ukusanyaji mapato kwetu,…Kwamba uwe mwovu au usiwe mwovu kodi ni lazima ulipe!.
Hapana Mungu wetu hayupo hivyo, yeye hakusanyi mapato kutoka kwetu kama wafanyavyo TRA kwasababu yeye ana kila kitu tayari, anataka tu! tujifunze kutoa kwa faida yetu wenyewe, kama yeye alivyo mtoaji, na hapendezwi na sadaka ya mtu mwovu, hivyo kama unatoa sadaka na bado mlevi, au kahaba..ni afadhali usitoe kabisa kwasababu ni machukizo mbele za Mungu. Hakuchukii wewe, bali unachotoa kinamchukiza, na anataka tufanye kilicho bora.
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.
Hivyo kama hujampa Kristo maisha yako umechelewa sana, ni afadhali ufanye hivyo sasa kabla mlango wa Neema haujafungwa, unachotakiwa kufanya ni kutubu kwa kukusudia kuacha kufanya dhambi tena!!, Unaamua kwa vitendo! kuacha ulevi, anasa, uvaaji mbaya, rushwa, na mambo yote machafu kisha unaenda kubatizwa tena! kwasababu kama ulibatizwa na umerudia machafu ya ulimwengu huu, kiasi hata cha kufanya uzinzi na uasherati unapaswa ukabatizwe tena katika maji tele, na kwa jina la Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kulingana na Matendo 2:38,
kisha baada ya kufanya hivyo Roho Mtakatatifu ataingia ndani yako, na kukupa uwezo wa kushinda dhambi kwa namna ya kipekee.
Baada ya kufanya hivyo, utakuwa umeokoka na kufanyika kuwa mwana wa Mungu, hivyo tafuta kusanyiko la kikristo linalomhubiri Kristo, na maneno yake ya kwenye biblia yenye vitabu 66 na sio vitabu 666, ujiunge hapo!, ili usizimike kiroho. Na Bwana mwenyewe atakusaidia kufanya yaliyosalia, kwasababu Neno lake ni mwanga wa njia zetu.
Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?