Sehemu ya kwanza: LIA NA NYONYA.
Nakusalimu katika jina kuu lenye uweza la mwokozi wetu Yesu Kristo, sifa na heshima vina yeye milele na milele.
Haya ni Makala maalumu kwa waongofu wapya, ikiwa wewe umeokoka hivi karibuni, au una ndugu/mpendwa ambaye amempokea Bwana Yesu siku za karibuni basi Makala hizi ni muhimu sana kwako au kwa yule mwingine.
Tunaposema kuokoka, tunamaanisha Kuzaliwa mara ya pili. Na mtu anazaliwa mara ya pili, kwa kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu, na pia kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na kwa kupokea Roho Mtakatifu..Kwa kuzingatia hivyo vigezo, basi mtu huyo anakuwa ameshazaliwa mara ya pili.
Lakini sasa hilo peke yake halitoshi, wengi wanapotimiliza maagizo hayo wanajisahau na kudhani ndio tayari wameshatimilika, hakuna cha ziada.. Hawajui kuwa mtu unaweza ukawa kweli umezaliwa mara ya pili lakini ni kiumbe kilicho kufa.. Utajiuliza ni kwa namna gani inakuwa hivyo?
Mtu anayezaliwa mara ya pili katika roho anafananishwa na mtoto, anayezaliwa mara ya kwanza katika dunia. Kwa kawaida mtoto huyo, ni lazima aonyeshe tabia kuu mbili. Kabla hajaweza hata kuona, au kuzungumza, au kujitambua..Ni lazima
ALIE kwa sababu gani.. Mtoto anapotoka tumboni kwa mama yake, anakuwa kama kiumbe mfu, wanachofanya wakunga ni kumpiga kidogo, kumshutua ili atoe sauti, wakisikia analia basi wanatambua kuwa kiumbe kilichozaliwa ni hai, hivyo baada ya muda kidogo wanamsogeza katika hatua nyingine,
Ambayo ni kunyonyeshwa.
Cha kushangaza ni kwamba mtoto yule anaposogezwa katika nyonyo la mama yake, hakuna mtu yeyote anayemfundisha kunyonya, utaona ni yeye mwenyewe anajua wajibu wake, wa kula, ndio hapo utaona saa hiyo hiyo ataanza kufyonza maziwa kana kwamba alishawahi kufundishwa huko tumboni jukumu lake kabla hajafika duniani.
Sasa kiroho pia ndio ipo hivyo. Ikiwa wewe umezaliwa kweli mara ya pili, hizi ni hatua za awali kabisa ambazo utazionyesha. Na kupitia hizo sisi wengine tutathibitisha kweli wewe ni kiumbe kipya hai. Kwani ni lazima utoe kelele fulani rohoni.. Huwezi kutulia, ambao sisi tuliokomaa kiroho tutazitambua, japo wewe hutoweza kuzielewa katika hatua yako ya uchanga rohoni..
Sisi tutaona kuhangaika kwako kutaka msaada wa kumjua Mungu, Na sisi tukishalitambua hilo, basi tunakuwa na wajibu mkubwa sana wa kukusaidia, kukosegezea matiti (Neno la Mungu) unyonye..
Hebu tujifunze kisa cha Musa, pindi anazaliwa..Biblia inatuambia, alipozaliwa, mama yake alimficha ili Farao asimuue, lakini alipoona hali imekuwa mbaya, alimtengenezea kisafina kidogo, kisha, akamtupa mtoni.. Lakini mtoto yule alipokuwa katika kila kisafina, hakukaa kimya tu, bali alikuwa anapiga kilele, analia,sana na binti Farao aliposikia alikwenda kutazama na kufungua aone ni nini kipo ndani, akakaona katoto, wakakahurumia..Embu tusome kwa ufupi kisa hicho;
Kutoa 2:6 “Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, MTOTO YULE ANALIA. BASI AKAMHURUMIA, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. 7 Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? 8 Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. 10 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini”.
Kutoa 2:6 “Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, MTOTO YULE ANALIA. BASI AKAMHURUMIA, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. 7 Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
Kutoa 2:6 “Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, MTOTO YULE ANALIA. BASI AKAMHURUMIA, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.
7 Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
8 Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto.
9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha.
10 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini”.
Umeona? Mtoto yule angeangamia kama asingelia, lakini alipolia, akahurumiwa akatafutiwa msaada mapema wa kunyonyeshwa, na hatimaye akakua akaja kuwa Mkombozi wa Israeli, ndiye Musa tunayemsoma.
Ndugu/Dada uliyeokoka hivi karibuni, kutojishughulisha kwako na mambo ya Mungu, kunathibitisha kuwa wewe ni kiumbe mfu, kutoulizia kwako Habari ya ibada, kunatuambia kuwa wewe si kiumbe hai..Hupaswi kujificha, hupaswi kujiepusha na kiongozi wako wa kiimani..hupaswi kukaa mbali na wapendwa, hupaswi kupitisha siku nyingi hujulikani upo wapi, au maendeleo yako ya kiroho hayatambuliki.. kataa hiyo hali kwa nguvu zote..
Wewe tayari ni kiumbe kipya, yatamani sana maziwa ya roho.. Usisubiri kukumbushwa kumbushwa kuhudhuria mafundisho ya kuukulia wokovu, kama mtoto mchanga ambaye hafundishwi na mtu kunyonya ni wajibu wako kutafuta kufundishwa Neno la Mungu, kwa bidi zote..Sio wewe utafutwe.
1Petro 2:2 “Kama watoto wachanga wazaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili k hayo mpate kuukulia wokovu.
Hivyo anza sasa kubadilisha mwenendo wa Maisha yako.. Jifunze kuomba na wapendwa, jifunze, kusoma biblia mwenyewe kuanzia sasa, jifunze kuuliza maswali, jifunze kumshirikisha na kukuonyesha njia sahihi.
Wagalatia 6:6 “Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake up
Hivyo zingatia mambo hayo makuu mawili. Na Bwana akutie nguvu.
Shalom.
Sehemu ya pili itafuata…
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
:
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
UMEITIMIZA HAKI YOTE?
ILI TUONEKANE SAFI MBELE ZA MUNGU TUFANYE NINI?
Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Mstari huu una maana gani? Je, ni kweli waandishi waliweza kubadilisha baadhi ya maneno ya torati, Na hivyo inaifanya biblia isiamike hadi sasa?
Yeremia 8:8 “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
JIBU: Hii ni hoja inayotumiwa sana na wapinga-biblia, au wapinga-ukristo. Wakisimamia mstari huu, na kusema, unaona? Biblia ilichakachuliwa, zamani na waandishi wa kiyahudi kwa kuongeza baadhi ya maneno katika torati iliyoandikwa na mwenyezi Mungu,.. Kwahiyo hiyo inathibitisha kuwa biblia ni kitabu chenye kasoro..
Lakini je tukisoma vifungu hivyo, vinatuambia waliibadilisha torati?
Kabla ya kuendelea kusoma zaidi, embu tuitafakari tena hiyo kauli hapo mwishoni, anasema “kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo”. Ahaa Kumbe waandishi ndio wameifanya kuwa uongo..Lakini yenyewe kama yenyewe sio uongo.. Mfano nikikuambia, unanifanya kuwa mwongo mbele za ndugu zangu, haimaanishi kuwa mimi ni mwongo..maana yake ni kuwa, pengine ni kwasababu uliyawakilisha maneno yangu isivyopaswa, aidha kwa kuongeza chumvi au kupunguza, na kwasababu hiyo basi, mimi nikaonekana nimeongopa, lakini sivyo, mimi nilisema ukweli mwanzo, isipokuwa wewe ndio umeniwakilisha vibaya.
Ndivyo ilivyokuwa hapo, waandishi, ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kufundisha na kuwaelezea watu, walianza, kutoa tafsiri zisizo sawa za torati, na kuwafundisha watu na kuwaandikia, mfano Bwana Yesu alisema, waliipindua amri ya tano; inayosema waheshimu baba yako na mama yako, na kuwaambia watu, ikiwa kuna chochote umekiweka wakfu hupaswi kumsaidia mzazi wako, hata kama akiangamia kwa njaa ni sawa tu..Jambo ambalo Mungu hakuliagiza hata kidogo, ilikuwa ni wajibu wa kila mtu kumsaidia mzazi wake, awapo katika uhitaji (Soma Marko 7:7-13)
Umeona, sasa tukirudi kwenye ile habari ya mwanzo ili kuthibitisha hilo vizuri, ukiendelea kusoma vifungu vinavyofuata utaona Yeremia, anaeleza kwa undani jinsi kalamu za hao waandishi zilivyoweza kuipa torati tafsiri zisizo sahihi..
Yeremia 8:8 “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo. 9 Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana akili gani ndani yao? 10 Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; MAANA KILA MMOJA WAO, TANGU ALIYE MDOGO HATA ALIYE MKUBWA, NI MTAMANIFU; TANGU NABII HATA KUHANI, KILA MMOJA HUTENDA MAMBO YA UDANGANYIFU. 11 KWA MAANA WAMEIPONYA JERAHA YA BINTI YA WATU WANGU KWA JUU-JUU TU, WAKISEMA, AMANI, AMANI, WALA HAPANA AMANI. 12 Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana..
9 Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana akili gani ndani yao?
10 Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; MAANA KILA MMOJA WAO, TANGU ALIYE MDOGO HATA ALIYE MKUBWA, NI MTAMANIFU; TANGU NABII HATA KUHANI, KILA MMOJA HUTENDA MAMBO YA UDANGANYIFU.
11 KWA MAANA WAMEIPONYA JERAHA YA BINTI YA WATU WANGU KWA JUU-JUU TU, WAKISEMA, AMANI, AMANI, WALA HAPANA AMANI.
12 Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana..
Umeona hapo? Anasema, hao waandishi na makuhani, wanawatabiria watu amani, amani, na kuwaambia mnaishi sawasawa na torati ya Mungu inavyosema, hivyo hamwezi kupatwa na madhara, ili hali ndani yao wanatamani, ni waovu, waabudu masanamu, wanakula rushwa n.k..
Wakati torati inakataza vikali vitu hivyo, wenyewe wanawatumainisha watu, Mungu anawapenda, ndio hapo anasema, wanawaponya jeraha zao kwa juu juu tu, mwisho wa siku wanaadhibiwa, halafu wanasema Mungu ni mwongo.. Mbona anatupiga bila sababu!.
Je! Waandishi wa namna hii wapo hadi sasa?
Jambo hili lipo hadi sasa katika kanisa la Mungu, Siku hizi za mwisho makristo na manabii wengi sana wa uongo wametokea, nao wanawaponya watu wa Mungu juu juu tu, hawawaelezi ukweli, mpaka inafikia hatua Mungu anaonekana mwongo, hasikii wala hajibu.
Wanawaambia, utafanikiwa, utabarikiwa, kesho yako ni ya kung’ara kama jua, wanawaambia watoe sadaka nyingi, watumie maji ya upako, mafuta na chumvi, wakati mwingine wafunge mwaka mzima, Mungu atawabariki.. Lakini wanasahau kuwa hao watu wana mizigo ya dhambi, ndiyo inayowafanya wasijibiwe maombi yao.. Kama vile maandiko yanavyosema..
Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”.
Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”.
Hivyo hao watu wanataabika, januari mpaka disemba, lakini hawaona nuru yoyote, hawaona uzima wowote, ndio kwanza hali inakuwa mbaya, mwishoni wanakataa tamaa wanasema Mungu hajibu maombi, wanawageukia waganga wa kienyeji.
Ndugu, Neno la Mungu ni kweli kabisa, akisema atakuponya, atakuponya kweli, akisema atakubariki atakubariki kweli, lakini ni sharti ujue, anataka nini kwanza kwako ili hivyo vyote vikujie.. Anachotaka ni wewe uache dhambi, uache, rushwa, uache uzinzi, uache uongo, uache vimini, uache fashion za kidunia, anasa, uache ulevi, uwe mtakatifu. Ndipo hayo yote yatakapokujia..
Epuka injili zizisogusia dhambi katika maisha yako, ziepuke kama ukoma, hizo huwa zinakuja na maneno mazuri sana ya kushawishi na kufariji, lakini hazitakusaidia chochote, Mungu ni mtakatifu, kamwe hajibu maombi ya mwenye dhambi.
Je! Umeokoka? Kweli kweli kwa kumaanisha kumfuata Kristo? Kama la! Basi huu ndio wakati wako sasa kuanza upya na Kristo. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi, waweza tupigia kwa namba uzionaza hapo chini.
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
MAJIBU YA MASWALI YANAYOULIZWA NA WASIO WAKRISTO (Sehemu ya kwanza).
Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?
Yesu ni Mungu?, Na Kama ni Mungu kwanini alikufa?
Nini maana ya “Torati na manabii”?
Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?
Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Atukuzwe Yesu Kristo Bwana wetu milele na milele. Sifa na utukufu ni vyake yeye sikuzote..
Biblia inatuambia, mambo yote yaliyoandikwa katika agano la kale, yalikuwa ni kivuli cha agano jipya la rohoni. Hivyo maagizo mengi ya mwilini, unayoyasoma kule, yalikuwa ni muhtasari wa agano jipya lili bora Zaidi.
Ni sawa na mwanafunzi anayeanza chekechea, ukitaka kumfundisha Hesabu za KUJUMLISHA na KUTOA, huwezi moja kwa moja ukamwandikia 5-3=2. Ukadhani ataelewa, ni kweli kwa upande wako ni rahisi kwasababu tayari upeo wako ulishatanuka, lakini kwa mtoto, huna budi kutumia njia ya vitendo kwa mwanzoni..
Ndipo itabidi umwekee vijiti, au mawe, ahesabu kimoja mpaka cha tano, kisha aondoe hapo vitatu, ndipo vile viwili vinavyosalia, viwe jibu. Hivyo akilini mwake anajua hesabu ni vijiti na mawe, lakini kihalisia sio hivyo.. Atakapokomaa akili, ndipo atakuwa hana haja ya vijiti, au vidole, au mawe tena.
Vivyo hivyo katika biblia, agano la kale la mwilini lilikuwa ni hatua za awali za kulielewa agano lilibora la rohoni..(Waebrania 10:1, Wakolosai 2:16-17).
Sasa tukirudi katika kichwa cha somo letu. Tufanye nini ili tuonekane safi mbele za Mungu?.
Kumbuka, katika torati Mungu aliwaatenga Wanyama wote katika makundi mawili makuu.
Sasa ili mnyama aitwe safi, ilikuwa ni sharti, akidhi vigezo maalumu Mungu alivyovioanisha.. Na vigezo vyenyewe zipo vitatu ambavyo ni hivi;
Ikiwa na maana kama hatokidhi vigezo vyote vitatu, basi huyo mnyama ni najisi, haijalishi atakuwa na kimoja au viwili kati ya hivyo. Hakuruhusiwa, kuliwa, na wengine kufugwa au kuguswa mizoga yao.
Walawi 11:2 “Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
Walawi 11:2 “Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.
3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.
4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
Sio kwamba aliwaona wana sumu kali, au wana madhara wakiliwa, kama wengi wanavyodhani hapana, kwasababu wengi wao wanaliwa hadi sasa, na hakuna madhara yoyote yanayowapata bali alikuwa anatufundisha jambo la rohoni, ili tutakapoingia katika agano jipya tuelewe vema, Mungu anapozungumzia unajisi anamaanisha nini.
Kwamfano, anaposema,
Kucheua ni nini? Ni ile hali ya mnyama kuwa na uwezo wa kukirejesha tena kile chakula alichokimeza na kukitafuta tena, kwa kawaida Wanyama kama ng’ombe, twiga, ngamia, hawa wanakuwa na tumbo la ziada, ambalo linawasaidia kurejesha na kutafuna tena kile walichokila.
Hii inafunua nini sasa katika agano jipya?. Ukiwa si mtu wa kutafakari na kukitendea kazi kile unacholishwa (Neno la Mungu), wewe ni kusikia tu kilasiku, lakini hakuna tendo lolote la ziada unalolionyesha kwa kile ulichofundishwa, huzalishi chochote, mbele za Mungu ni kama mnyama najisi, asiyeweza kucheua, Na kamwe hutoweza kuingia mbinguni (patakatifu pa Mungu), siku ukifa. Mungu anataka tutendee kazi Neno lake, pia tujifunze kuzikumbuka Fadhili zake alizotutendea huko nyuma, tusiwe hasahaulifu. Usahaulifu ni tabia ya unajisi.
Hivyo jiangalie ndani yako je! Wewe ni mtu wa kulitendea kazi Neno la Mungu? Tangu uliopoanza kusikia ni mangapi umeyatendea kazi, Kama sio, basi bado hujawa safi.
2) Awe na Kwato:
Kucheua tu haitoshi, walikuwepo Wanyama wenye uwezo huo kama ngamia, lakini walikosa kwato.. yaani ni kama nyama tu imeshuka mpaka chini, ni sawa na kusema hawana kiatu.
Hivyo, ni dhaifu kwa upande mmoja, kwasababu wamekosa ulinzi miguuni, ukipita msumari mrefu, basi safari yao imekwisha, hawawezi kutembea kila mahali, penye miiba, hawawezi kuruka, kwasababu miguuni ni wadhaifu.
Tofauti na mnyama farasi,au swala, yeye ana kwato ndio maana ni mwepesi kutembea popote, ngombe anakwato, ndio maana anaweza kulima hata kwenye mashamba n.k.
Hii inatupa tafsiri gani rohoni?
Waefeso 6:14 “Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani”;
Waefeso 6:14 “Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani”;
Hapo anasema, ukiwa askari wa Kristo ni lazima ujifunze kusimama ukiwa umejifungia utayari miguuni.. utayari wa nini? Utayari wa kumtumikia Mungu kwa hali zote. Na je utayari huo unatokea wapi? Unatokea kwenye kuisikia injili ya Yesu Kristo, kwa kupitia hiyo tunapokea hamasa, na nguvu na uweza wa kumtumikia yeye.
Wanajeshi, kwa kawaida ni lazima wavae viatu vigumu miguuni waendapo vitani, ili kuwasaidia kukatisha katika mazingira yoyote magumu, vinginevyo wakienda peku peku, hawataweza kwenda mbali
Halikadhalika na wewe, ukiwa umejivika UTAYARI huo wa kumtumikia Bwana katika mazingira yoyote, rohoni unaonekana kama ni mnyama mwenye kwato. Unafaa kwa kazi,
3) Mwisho, kwato ziwe zimegawanyika.
Wapo Wanyama ambao walikuwa wanacheua, walikuwa wana kwato, lakini kwato zao zilikuwa hazijagawanyika mara mbili. Hapo bado walikuwa ni najisi.
Ni kwanini, Bwana alitaka kwato za mnyama zigawanyike mara mbili, ili waonekane safi? Ni siri gani ipo nyuma yake?
Kama tulivyotangulia, kuona kwato, Ni utayari tuupatao katika injili…
Lakini lazima tujifunze kuligawanya Neno la Mungu. Ndio maana biblia inayo agano la kale na jipya. Ili tuweze kuwa askari kamili ya Kristo, hatuna budi kufahamu kuweka injili ya Kristo kama atakavyo yeye, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu.
Kwa kukosa, kuelewa ufunuo uliokatika agano lake, ndio inayopelekea, watu kufundisha kuwa vyakula ni najisi kwasasa..
1 Timotheo 4 : 1-5
1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Wengine wanaona Ibrahimu, Daudi, wameoa wake wengi, anadhani ndio hata sasa ndivyo ilivyo, na Mungu anapendezwa navyo. Hawajui ni ufunuo gani ulikuwa nyuma yake.
Hivyo biblia inatutaka sana tujifunze kuligawanya vema Neno la Mungu. (2Timotheo 2:15).
Ni muhimu sana. Na hiyo inamuhitaji Roho Mtakatifu.
Hivyo kwa kukidhi vigezo hivi vitatu; 1) Kutendea kazi Neno la Mungu 2) Kumtumika kwa Bwana 3) Kuwa na maarifa ya Neno la Mungu. Basi utakuwa mnyama safi mbele za Mungu.
Na hivyo tutamkaribia Mungu.
Lumbwi ni nini katika biblia?
Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Bwana alimaanisha nini aliposema enendeni mkaihubiri injili kwa kila kiumbe?
Maji ya Farakano ni nini katika biblia?
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
Liwali ni mkuu wa mji au jimbo Fulani. (Gavana).
Kwamfano katika biblia tunaona, Pontio Pilato anatajwa kama Liwali wa Uyahudi sehemu ya kusini mwa Israeli,. Hivyo eneo lote la uyahudi yeye ndiye alikuwa kama mkuu wa majimbo hayo.
Mwingine ni Yusufu, biblia inasema, Farao alimweka kama Liwali wa nchi yote ya Misri.
Mwanzo 42:6 “Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake”.
Hivyo kazi yao haswaa ilikuwa ni sawa na ya wakuu wa mikoa wa sasa, au majimbo, ambapo kimsingi wanakuwa na mamlaka ya kuongoza shughuli zote za jimbo hilo kwa amri yao, wala hakuna chochote kinachoweza kufanyika bila idhini yao.
Hivi ni baadhi ya vifungu vya Zaida ambavyo utaweza kukutana na hilo neno;
Mathayo 27:1 “Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.
Mathayo 27:1 “Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.
Mathayo 28:14 “Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo”.
Mathayo 28:14 “Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo”.
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu”.
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu”.
Matendo 18:12, 23:24, 26:30
Ni nini twaweza zingatia kuhusu hawa maliwali?
Bwana Yesu alisema, katika utumishi wetu, utafika wakati, tutaitishwa mbele ya mabaraza ya wafalme, na maliwali, kushitakiwa.Hivyo tukijikuta katika mazingira kama hayo hatupaswi kuogopa, kwasababu Kristo ameahidi kuwa atakuwa na sisi katika mapito yetu yote.
Mathayo 10:18 “nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa”.19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.
Mathayo 10:18 “nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa”.
19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.
Je! Umeshamkabidhi Kristo Maisha yako?. Kama jibu ni hapana, na upo tayari kuokoka leo. Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya toba, >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Au tutafute kwa namba zetu hapo chini, kwa msaada huo.
+255693036618/+255789001312
Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?
Mharabu ni nani katika biblia?
Bawabu ni nani/nini?
Mapooza ni nini? Na je! Twawezaje kuepukana nayo?
Rudi Nyumbani
Akida ni mkuu wa majeshi ya zamani, hususani majeshi ya kirumi. Akida mmoja alikuwa anaongoza kikosi cha askari 100,. Maakida wengi walikuwa wanachaguliwa na watalawa wao wakuu moja kwa moja toka Rumi,wengine katika mabaraza, wengine kutoka kwa maliwali, na wengine moja kwa moja kwa kupandishwa vyeo, baada ya kutumika kwa muda mrefu (miaka 15-20), katika shughuli za kijeshi.
Kazi yao kubwa ilikuwa ni kusimama mstari wa mbele katika vita kuliongoza kundi lote jeshini, pia kutekeleza mauaji ya wahalifu, au washitakiwa, mfano wa hawa ni Yule akida aliye simamia mateso na mauji ya Bwana Yesu pale Kalvari
Marko 15:39 “Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.
Pia walikuwa wanafanya kazi ya kutoa mafunzo ya kijeshi, kugawa majukumu, kusimamia ujenzi wa ngome na kuta za ulinzi za taifa. Walifanya pia kazi ya kuwalinda wafungwa na kuwahakikishia ulinzi wao pindi wasafirishwapo, Mfano wa Hawa, soma .(Matendo 23:23, 24:23, )
Pamoja na hilo, maakida wengine walikuwa ni watu wakatili, na wapenda rushwa,
Lakini ni jambo gani Mungu anataka tujifunze nyuma ya watu hawa?
Ijapokuwa kazi hii, si kazi iliyoonekana kumrudishia Mungu utukufu, Lakini bado tunaona wapo maakida, kadha wa kadha katika biblia, waliompendeza Mungu katika utumishi wao, zaidi hata ya wayahudi wengi, waliokuwa wanajiona washika sheria na torati.
Kwamfano utaona Bwana Yesu alipokuwa katika ziara zake za kuhubiri na kufungua watu, alikutana na akida mmoja, ambaye aliustaajibisha sana moyo wake kwa imani aliyokuwa nayo, mpaka Bwana akasema hata katika Israeli,hakuna aliyekuwa na imani kubwa kama yake.
Mathayo 8:5 “Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, 6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. 7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. 8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli. 11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;”
Mathayo 8:5 “Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.
11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;”
Utaona pia, kulikuwa na akida mwingine, aliyeitwa Kornelio, huyo alikuwa anatoa sadaka nyingi sana, na kuwasaidia watu, mpaka siku moja malaika wa Bwana anamtokea na kumpa maagizo ya kufanya ili aupokee wokovu kamili.
Matendo 10:1 “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, 2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima”.
Matendo 10:1 “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima”.
Umeona? Ni nini Mungu anataka tujue?
Ni kwamba Mungu hatazami sana mahali unapotumika, lakini anatazama uaminifu wako, moyo wako, utakatifu wako, bidii yako kwake. Unaweza ukawa unafanya kazi serikalini, lakini ukamtumikia Mungu vema, kwa kukataa rushwa, na kutenda haki, na Mungu akapendezwa nawe..Mfano wa Danieli, Maadamu, upo mahali ambapo hapakinzani na sheria ya Mungu na taifa, usijisikie vibaya kutumika unachopaswa kufanya ni kumtumikia tu Mungu kwa uaminifu wote, kuangaza nuru yako ya wokovu kwa wale watu, na kumpenda yeye na kukataa njia zote mbaya zinazokinzana na Neno lake.
Kwa kufanya hivyo Basi Mungu atakutumia kutimiza kusudi lake, alilolikusudia juu yako, na watu wake, mfano wa Kornelio na Yule akida ambayo alidhubutu hata kuwajengea wayahudi sinagogi.
ORODHA YA WAFALME WA ISRAELI.
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.
Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
Uchaga ni nini? (Luka 12:24)
WhatsApp
Sifa ni kitendo cha kumshuhudia Mungu, au kuyasimulia matendo makuu ambayo ameyafanya au aliyonayo, na huwa inaambata na mguso wa ndani unaomfanya mtu arukeruke, acheze, afurahie, aimbe, ashangalie, apige kilele kwa nguvu, kwa hayo aliyoyaona kwa Mungu wake.
Kwamfano tunapoona jinsi, mbingu na nchi, jua na mwezi, na milima na bahari, vilivyoumbwa kwa uweza na ukuu wa ajabu, hapo tunapata sababu ya kumshuhudia Mungu, au kumtangaza kwa namna zote aidha kwa kumwimbia, kushangalia kwa sauti ya juu,
Au labda ulikuwa na shida Fulani labda ugonjwa, ukaponywa, au hitaji la kazi, nyumba, chakula ukapatiwa na yeye. Hapo ndipo unapopata sababu ya kuyatangaza maajabu yake, kwa kumwimbia kwa nguvu sana. Hizo ndio sifa.
Mungu anasema..
Zaburi 68:32 “Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo”.
Zaburi 117:1 “Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidin.
Zaburi 147:1 “Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu, Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri”.
Biblia inatuambia viumbe vyote na uumbaji wote, vinamsifu Mungu. Kwanini na sisi tusimwimbie yeye sifa zetu?. Embu tazama pumzi uliyopewa bure, embu tazama mapigo ya moyo yanayodundishwa ndani yako bila tozo lolote, embu tafakari jua unaloangaziwa na Yehova. Kwanini usimsifu yeye?
Bwana anaketi juu ya sifa.. (Zaburi 22:3), Na yeye pekee ndiye anayestahili kuabudiwa.
Hivyo wote wamsifuo kwa Roho na Kweli, yeye yupo juu yao. Katika sifa kuta za Yeriko zilianguka, , \vifungo vya Gereza vililegezwa Paulo na Sila walipokuwa gerezani, katika sifa maadui waliuliwa bila vita yoyote kipindi cha Mfalme Yehoshafati. Nasi pia tukiwa watu wa sifa, ni maombi tosha ya kutuweka huru na kutufungua.
Bwana atupe macho ya kuliona hilo.
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
Mwana haramu ni nani kibiblia? (Kumbukumbu 23:2).
Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)
BARAGUMU NI NINI?
Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?
Ulafi ni nini kibiblia?
Ukienda kuomba kazi yoyote halali, kikawaida huwezi kupewa majibu ya papo kwa papo na kuambiwa anza kazi leo, bila ya kutaka kwanza taarifa Fulani kutoka kwako, hata kama ni ile ndogo ya kufagia, vipo vigezo vitaambatanishwa tu na kazi hiyo, aidha utaulizwa umri wako, au hali yako ya kiafya, au fani uliyonayo, au jinsia yako, au elimu yako n.k. Lakini ikiwa hujasoma vigezo vyao, halafu ukapeleka maombi yako kienyeji, Ni wazi kuwa barua yako itatupwa kapuni.
Vivyo hivyo na kwa Mungu, tunapopeleka maombi yetu, ni sharti tujue vigezo vya kujibiwa, vinginevyo, tutabakia kumlaumu Mungu, mbona tulifunga, na kukesha lakini hujasikia maombi yetu.
Hivi ndio vigezo vikuu vya maombi yetu kujibiwa na Mungu
Hili ndio jambo la kwanza na la msingi; Dhambi ndiyo inayomdhoofisha Mungu, na kumdumaza kwenye eneo la kujibiwa maombi yetu.
Isaya 59:1 “”Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”.
Isaya 59:1 “”Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”.
Hakikisha unakaa mbali na mambo yote yanayomchukiza Mungu, yaliyo ndani yako, mfano uzinzi, ulevi, uongo, rushwa, wivu, matusi n.k.
Kuomba vizuri, sio kupangalia maneno katika uombaji, hapana, bali kuomba jambo linalotimiza mapenzi ya Mungu.
Yakobo 4:2 “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.
Yakobo 4:2 “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.
Jiulize unachokiomba je kina lengo gani, ni ili umkomoe yule adui yako?, au ili ukaongezee mtaji wa ile biashara yako ya bar?, au ili uonekane mwanamke wa kisasa mfano wa Yezebeli? Kama sivyo ni Ili nini?..Fahamu kuwa Mungu anachunguza mioyo. Hakikisha unachokiomba ni kwa utukufu wa Mungu. Vinginevyo hutapokea chochote.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mawazo yako yanapaswa yamwelekee Mungu, na sio Mungu Pamoja na wanadamu. Ukilijua hilo, basi hutaona sababu ya kujionyesha kwa watu ili wakupe utukufu.
Ukweli ni kwamba yapo maombi utahitaji kuonyesha bidii kwa Mungu ili uyapate, na sio kuomba dakika 5 halafu basi, hapo unaweza usipokee chochote, bali yakupasa kung’ang’ana mbele za Mungu ndipo yaje kutokea.
Yakobo 5:16 “… Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. 17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
Yakobo 5:16 “… Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
Hivyo ongeza misuli yako ya maombi. Hata ya masafa marefu na mikesha.
Yakupasa ujifunze uvumilivu. Uvumilivu ni muhimu sana ikiwa hujajibiwa leo, haimaanishi kuwa Mungu hajakusikia, bali omba tena kesho, na kesho kutwa, kwasababu ipo sababu kwanini hujakipata kwa muda huo.
Luka 18 : 1-8
18:1 “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. 2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. 3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. 4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, 5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. 6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. 7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? 8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani”?
18:1 “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani”?
Ni jambo dogo, lakini linamatokeo makubwa sana rohoni. Sio kwamba Mungu anahaja na fedha zetu hapana, lakini umtoleapo unaonyesha upendo wako kwake. Ukipeleka maombi yako kwake, jijengee utaratibu pia wa kuambatanisha na sadaka, kwa kile ulichojaliwa, ikiwa ni senti mbili, au milioni 10, mpelekee Bwana. Wengi waliotenda hivi walifanikiwa.
Malaki 3:10 “”Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la”.
Hivyo kwa kuzingatia, mambo hayo sita, basi ni hakika Mungu atakujibu maombi yako. Na utamfurahia yeye.
Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?
Namna ya kuomba
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tena tuyatafakari maneno matukufu ya mola wetu. Leo napenda tuutafakari huu mstari kwa ukaribu sana, kwasababu una maana kubwa nyuma yake huwenda tofauti na vile tunavyoufahamu.
Biblia inasema..
Mithali 23:29 “Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? 30 NI WALE WAKAAO SANA KWENYE MVINYO; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika”.
Mithali 23:29 “Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
30 NI WALE WAKAAO SANA KWENYE MVINYO; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika”.
Mwandishi anaeleza matokeo, ya mtu kufikiwa na hayo mambo yote sita(6) mabaya kwa mpigo ni nini.. Yaani Yowe, ole, ugomvi, mguno, jeraha zisizo na sababu, na macho mekundu.. ni nini..
> Anaposema Yowe, sote tunafahamu, mpaka mtu apige yowe, ni matokeo ya kakumbwa na jambo baya sana, ambalo linamfanya ahitaji msaada wa haraka sana, pengine labda anafukuzwa auawe, au anapigwa vikali , au amekumbwa na taarifa za kushtusha sana..Hivyo kwa kawaida hakuna yowe inayotokana na mema.
> Vilevile anaposema ni nani aliaye ole..Tunafahamu ole ni baada ya kutahadharishwa kwa mabaya. Lakini mpaka mtu analia ole, “kusema ole wangu mimi,” ni mtu ambaye tayari ameshakumbwa na mabaya hayo,aidha vifungo, magonjwa, taabu, mateso n.k.
> Halikadhalika anaposema, ni nani mwenye mguno; Anamaanisha mtu mwenye malalamiko, mwenye maneno yasiyofaa, au kueleweka, mtukanaji, mtu wa kashfa. Jambo hili nalo haliji kutoka katika mema.
> Vilevile aliye na jeraha zisizo na sababu, ni mtu aliyejiingiza katika matatizo ambayo hakustahili au hakupaswa kukumbwa nayo. Pengine amrukwa na akili, au uzembe uliopitiliza usio wa kibinadamu.
> Anaposema tena ni “nani mwenye ugomvi”..Yaani mtu anayezua ugomvi, malumbano, yasiyo na maana au sababu, kufoka, na ukorofi.
> Na pia mwenye macho mekundu, .Yaani macho yaliyolegezwa na pombe.
Sasa ukisoma kwa makini, vyote hivyo sita (6), haviji hivi hivi kwa wanywaji pombe kidogo, wanaweza wakafikia kiwango Fulani..Lakini mpaka tabia hizo zitokee kwa mlevi ni lazima awe ni mtu wa “KUKAA SANA KWENYE MVINYO” kama maandiko yanavyosema..Walevi waliopitiliza, ndio huwa wanaanguka mitaroni na kujiumiza miza wenyewe ovyo bila sababu, ndio wenye macho yaliyolegea mpaka kuwa mekundu, ndio wanaopiga piga makelele njiani na majumbani, ndio wanaopata hasara ya mali zao, na kupiga mayowe, anayetapika ovyo n.k… Hii hali mpaka afikie mtu, ni lazima atukuwa mule mlevi wa kishinda kilabuni usiku kucha.
Ni kutuonyesha jinsi kitu chenye ulevi kinapotumiwa kwa muda mrefu na sanaa, kinavyoweza kuleta matokeo yakubwa Zaidi..
Lakini biblia inatuambia kuwa ipo DIVAI MPYA. Ambayo sisi wakristo, tunakunywa na katika hiyo, tunalewa. Lakini kanuni ni ileile hatutaweza kulewa vema na kutoa matokeo yake, kama hatutakaa sana katika kuinywa..
Na divai yenyewe si mwingine Zaidi ya ROHO MTAKATIFU.
Siku ile ya Pentekoste mitume walipojazwa Roho Mtakatifu, walionekana kama walevi, waliolewa kwa mvinyo mpya..Kumbe hawakujua kuwa alikuwa ni Roho Mtakatifu kawafanya vile. Kuonyesha kuwa Roho naye huwa anawalewesha watu wake pia katika roho.
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto”.
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.
14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto”.
Na matokeo ya kuleweshwa kisawasawa na Roho Mtakatifu, ni kutoa matunda yake.. ambayo tunayasoma katika, Wagalatia 5:22 na pia kufanya kazi kama za mitume, walizofanya baada ya kupokea Roho..
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Hivyo hatuwezi kuwa na Upendo, kama hatutakaa sana uweponi mwa Mungu tulewe mema yake kisawasawa, hatutakaa tufikie furaha timilifu, kama tutakuwa tunamtafuta Mungu jumapili kwa jumapili, na sio muda wote.. Hatutakaa tuwe na kiasi, na upole na amani, kama hatujibidiishi, kuutafuta uso wa Mungu, kwa wakati mrefu. Hatuwezi kuzidhihirisha karama za Roho kama hatutampa muda wa kutosha mioyoni mwetu.
Tukae sana kwenye mvinyo wetu (Roho Mtakatifu), ili tumzalie Bwana matunda ya haki.
Hivyo, tukiwa na bidii katika Mungu, kusali, kufunga, kutafakari sana, maneno ya Mungu Pamoja na wapendwa wenzetu, Kidogo kidogo tunakuwa walevi, na kwa jinsi tunavyozidisha ndivyo tutakavyoyatoa hayo matunda ya Roho kirahisi sana ndani yetu.
Hivyo sote kwa Pamoja tuanze kuzidisha bidi zetu kwa Bwana. Ili Bwana naye apate nafasi ya kutuponya
Ikiwa hujaokoka, kumbuka kuwa hizi ni siku za mwisho, siku yoyote Yesu anarudi kulinyakua kanisa lake. Kumbuka injili iliyobakia sasa sio ya kubembelezewa wokovu, ni wewe mwenyewe kuona hali halisi na kujiokoa nafsi yako. Ikiwa upo tayari kutubu leo na kumpa Yesu Maisha yako, basi utakuwa umefanya uamuzi wa busara, katika dakika hizi za majeruhi tulizopo.
Hivyo kama utapenda kupata msaada huo. Basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi, ili tuweze kuomba na wewe na pia kukuongoza sala ya Toba (Bure). >>> +255693036618/ +255789001312 .
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Kwanini Bwana Yesu alisema “Msimwamkie mtu njiani”?
Roho Mtakatifu ni nani?
Bwana alimaanisha nini kusema “kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”
Je! Bwana Yesu alikunywa kileo mpaka watu wakasema ni mlafi na mlevi? Kulingana na Mathayo 11:19?
Mapooza ni kitu/vitu/mambo yote yasiyoweza kuzalisha chochote, au kufikia kilele chake cha kutoa matunda kamili.
Neno mapooza limetokana na neno kupooza. Kwamfano tunaposema mtu amepooza mkono, maana yake ni kwamba anao mkono lakini hana uwezo wa kufanya kazi ya mkono, yaana unakuwa kama vile umekufa tu lakini upo.
Nazi zote zinazotoka katika mti wa mnazi, si zote zinafaa kama kiungo, bali nyingine ni koroma, Sasa hizo koroma ndio mapooza yenyewe, japo kwa nje zinaonekana ni nazi.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia;
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 6 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake”.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
6 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake”.
Katika habari hii ni Mungu anaifananisha ile siku ya Bwana, na kama mtini upukutishavyo mapooza yake. Yaani kama vile tunavyofahamu miti ya matunda, huwa si matunda yote yanakomaa wakati wa mavuno, bali kuna mengine huwa yanaendelea kubaki katika miti, hadi wakati wa msimu wa upepo mkali wa upukutishaji unapovuma ndipo yanapoondoka hayo yaliyosalia (ambayo ndio mapooza)..Hivyo siku ya Bwana ndivyo itakavyokuwa wakati ambapo Mungu anaiondoa mbingu, hakuna nyota hata moja itakayobakia juu.
Utalisoma pia, katika ile Habari ya Elisha..
2Wafalme 2:19 “Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. 20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. 21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. 22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
2Wafalme 2:19 “Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.
20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea.
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
Maana yake ni kwamba yale maji waliyokuwa wanayanywa au wanayatumia kwa mimea yalikuwa si mazuri yanazaa mapooza, yaani vitu vyake havistawi au kuleta matunda, mimba za wanawake zilikuwa zinatoka, mboga mboga zilizokuwa zinanyeshewa zilikuwa hazikuwi, ipasavyo, wala miti haikuivisha matunda yake,
Hivyo Elisha alipoagizwa na Mungu kutia chumvi katika yale maji, wakati ule ule yakaponywa. Hivyo kukawa hakuzaliwi mapooza tena katika ile nchi.
Utalisoma pia Neno hilo katika Ayubu 15:32.
Jibu ni ndio, kwamfano, wewe ni mwanamke halafu, kila unaposhika mimba, kabla hujajifungua inatoka, huwenda kuna mapooza nyuma yake.
Au unafanya shughuli Fulani, ambayo kwa muda mrefu sana, haijakuletea mafanikio yoyote, hayo pia ni mapooza,
Au unalihangaikia jambo lolote lile jema, lakini kwa muda mrefu, unaona kama kuna dalili njema zinaonekana lakini mwishoni linakufa. Ujue pia mapooza yapo hapo.
Una karama ya muda mrefu lakini haina matunda yoyote katika ufalme wa Mungu,
Je suluhisho ni nini?
Yapo mambo mawili makuu ya kuyafanya.. Hususani hili la kwanza, ukilipuuzia hili ukakimbilia hilo la pili, ufahamu kuwa hali yako haitaweza kuwa na mabadiliko.
Kama vile Elisha, alivyoagizwa akatie chumvi ndani ya yale maji yaliyozaa mapooza, vivyo hivyo na wewe, huna budi kukubali kuwatiwa chumvi ili mapooza yaondoke ndani yako..
Hapa hatuzungumzii chumvi za upako, tunazungumzia Neno la Mungu. Mungu kumuagiza Elisha atie chumvi sio kwamba alikuwa anatuonyesha kuwa kuna upako ndani ya chumvi hapana, bali alikuwa anatoa taswira ya kufahamu chumvi ni nini katika ulimwengu wa roho, na sisi tunatiwaje chumvi..
Marko 9:47 “Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; 48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 49 Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”.
Marko 9:47 “Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
49 Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”.
Tafakari vema, jiulize, kwanini baada ya kutoa maagizo makali kama hayo, mwishoni akamalizia kwa kusema.. kila mtu atatiwa chumvi kwa moto..
Maana yake ni kuwa ili utiwe chumvi, huwezi epuka moto.. ili Maisha yako yaponywe, huwezi epuka kukata baadhi ya viungo vyako vinavyokukosea..
Viungo hivi ndio kama vipi..
Hivyo hiyo ndio njia ya kwanza yenye matokeo.. Kataa kwa nguvu zote, kuacha watu/vitu/mambo ambayo yanakufanya usiwe safi mbele za Mungu.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba unapaswa uokoke kwa kumaanisha kabisa kumfuata Yesu Kristo. Hakikisha umejitwika msalaba wako. Hii ndio njia kuu ya kuondoa mapooza yoyote ndani yako.
Hivyo nitaomba Pamoja na wewe.. Kisha kwa Imani Bwana atakufungua, wewe ambaye, tayari umeshampokea Yesu na kumfuata, au wewe ambaye unaahidi tangu sasa utafanya hivyo..
Hapo ulipo elekeza mawazo yako palipo na mapooza..kisha sema sala hii kwa sauti na kwa Imani, na kuanzia leo utaona mabadiliko yanakuja katika eneo hilo hilo unaloliombea..
PIGA MAGOTI, kisha sema maneno haya kwa sauti.
Mungu wangu, hakika nifahamu kuwa pasipo wewe mimi siwezi kuzalisha chochote, nami kama mwanao nakuja mbele zako, nikiomba msamaha unisamehe dhambi zangu zote, nilizokukosea, katika Maisha yako tangu nazaliwa. Nikakiri Yesu kuwa wewe ni Bwana na mwokozi na kiongozi wa Maisha yangu, wala Zaidi yako hakuna mwingine awezaye kuokoa. Tangu sasa naomba unifanye kiumbe kipya, na jina langu uliandike katika kitabu cha uzima, unipe uwezo wa kufanyika mwana wako kweli kweli, nami nimekubali tangu sasa kutiwa chumvi kwa maneno yako Bwana Yesu. Nakubali kuacha mambo/watu/vitu vyote viovu visivyokupendeza wewe bila kujali vitanigharimu kiasi gani.Najua wewe ni mwaminifu na utanisaidia, sawasawa na Neno lako ..Naomba Bwana unione tena katika hii shida yangu na uniponye (Taja eneo lako la mapooza). Asante Bwana Yesu kwa kuniponya.Naombi nikimaini. Amen.
Basi kama umeifuatisha hiyo sala ya Imani.. Fahamu kuwa Bwana ameshaanza kufanya muujiza katika hilo eneo lako la maishaa..Hivyo zingatia sasa kudhihirisha Imani yako kwa matendo kwa kujiepusha na mambo yote maovu yasiyompendeza Mungu, tangu leo, ishi maisha ya kujikana nafsi, mfuate Bwana Yesu. Hizi ni siku za mwisho, zidisha ukaribu wako kwa Bwana.
Amen.
UKIOKOKA,HIZI FIKRA ZIKIJA NDANI YAKO, ZIKATAE.
Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?
Sadaka ya kinywaji ilikuwaje? Na inawakilisha nini?
USIWE MSIKIAJI TU! BALI MTENDAJI.
Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).
AKAJIFUNGA VAZI LAKE, AKAJITUPA BAHARINI.
Nini maana ya “wazimu” katika biblia?
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Kabla ya kuwafahamu wana wa Asafu, ni vizuri kumfahamu Asafu mwenyewe alikuwa ni nani.
Asafu alikuwa ni mmoja wa walawi ambao, mfalme Daudi alimuweka kama kiongozi wa mbele wa sifa, atakayesimama mbele ya sanduku la Mungu daima kumsifu Mungu. (Soma 1Nyakati 6:31-32, 39).
1 NYAKATI: MLANGO 16
1 Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana. 3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. 4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli; 5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
1 Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.
2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana.
3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.
4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;
5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
Kulingana na maandiko, biblia inasema huyu Asafu hakuwa tu mwimbaji, bali Mwonaji pia,
2Nyakati 29:30 “Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie Bwana sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu”.
Baadaye, uzao wake uliendeleza nyayo zake, na wote wakawa waimbaji katika hekalu la Mungu lililokuja kujengwa baadaye, na hata baada ya ule uhamisho wa Babeli, waliporudi bado waliweza kuwekwa katika kazi hiyo hiyo ya Sifa..
Soma, Ezra 2:41 “Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane”.,
Pia Nehemia 7:44
Halikadhalika kuna baadhi ya Zaburi zilijulikana kama Zaburi za Asafu,Ambazo ni Zaburi 50 na ya 73-83. (Baadhi ya tafsiri zinaonyesha hivyo). Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu alimtumia yeye na uzao wake kwa njia ya uimbaji, kutoa nabii ambazo zinatusaidia hadi sasa.
Lakini kwasasa wana wa Asafu ni akina nani? Na tunapata funzo gani?
Wana wa Asafu ni watu wote wanaotumikia madhabahuni pa Bwana katika huduma ya kumsifu na kumwimbia Mungu. Watu hawa wanatenda kazi kubwa inayompendeza Mungu na kwa kupitia wao, Mungu huwa anapitisha, jumbe zake nyingi, na nabii nyingi zinazookoa na kuponya watu kama ilivyokuwa kwa wana wa Asafu, hii ikiwa na maana, kwamba wakitumika vema katika kazi yao, basi ni utumishi mkubwa sana, hata Zaidi ya huduma nyingine zote.
Lakini, watu hawa walijua kanuni ya kumwimbia Mungu, walimwimbia Mungu katika “uzuri wa utakatifu”, sawasawa 1Nyakati 16:29. Tofauti na sasa, waimbaji wengi, wamekuwa wasanii, wanageuza uimbaji wa injili kuwa Sanaa na sio wito na huduma ya Kristo Yesu.
Wanasahau kuwa huduma yao ndio ya kwanza kabisa inayomkaribia Mungu Zaidi ya nyingine zote,..Huduma ya Maserafi na Makerubi malaika watakatifu wasimamao mbele ya Mungu daima
Lakini kinyuma chake, Mwimbaji wa injili, utamkuta anakata mauno, anavaa vimini, anapamba uso kama Yezebeli, anaimba kwa staili za wasanii wa kidunia.. Twategemea vipi Mungu atasema au atawaponya, au atawafungua na watu wake kupitia uimbaji huo?, Haiwezekani..Inasikitisha kuona, kanisa la sasa, kundi kubwa la watu walioharibikiwa linatoka kwa wanakwaya na waimbaji.
Kumbuka Sababu iliyowafanya wana wa Israeli,wapelekwe utumwani haikuwa tu kuabudu maashera hapana, ilikuwa pia ni hiyo ya unafki katika kumwimbia.
Amosi 6:5 “ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi;”
Bwana anatuonya vikali, na sisi pia atatuadhibu vikali kama tutakuwa na tabia kama za wao, anataka anapoimbiwa aimbiwe katika “uzuri wa utakatifu” (1Nyakati 16:29)..Maana yake ni kwamba wewe mwongoza sifa, wewe mwimbaji, wewe mpiga kinanda,wewe mpiga gitaa, uwe kielelezo kuanzia mavazi yako, usemi, hadi tabia, mbele za watu. Utakatifu ndio uwe leseni yako, ya kumwimbia Mungu.
Kama utashindwa utakatifu, ni heri uache tu, ukafanye kazi nyingine, kwasababu utakuwa unajizombea laana badala ya baraka.
Mahali Mungu anasifiwa na kuabudiwa ni kuwa makini sana.. wengine walipoteza Maisha walipojaribu kuvuruga utaratibu pindi Mungu anapokuwa anasifiwa (Soma 2Samweli 6:1-11 ), Vivyo hivyo na wewe mwimbishaji kanisani, usipokuwa siriazi na huduma yako, uwezekano wa kukutwa na hayo upo mkubwa sana.
Bwana anataka sote tuwe wana wa Asafu, ili atutumie kumtukuza yeye, Pamoja na kuzungumza na watu wake, ili aziponye roho za watu..
MAOMBI YA YABESI.
NI KITU GANI TUNAJIFUNZA KWA RISPA, BINTI AYA?
SOMO no.02 (BINTI WA YEFTHA).
Gongo na Fimbo ni nini? Na vinawezaje kumfariji mtu? (Zaburi 23:4).
Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri.