Bwana Yesu atukuzwe ndugu yangu. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima pamoja..
Tunaposoma biblia..tujue kuwa tunausoma ufahamu wa Mungu. Mtu asiyeitafakari biblia halafu anakimbilia kwenda kumtumikia Mungu.. Ajue kuwa anajiweka katika hatari kubwa sana ya kuangamizwa na Mungu.
Ni sawa na mtu anayekimbilia kufanya biashara ambayo hajaifanyia utafiti kujua changamoto zake.faida zake na hasara zake..
Leo tutatazama ni kwa namna gani.
Ndugu usipumbazwe hata kidogo kuona Mungu anasema nawe..anakuonyesha maono makubwa..anakusifia..anakutokea..anakutuma ukawahubirie watu injili.. Usipumbazwe kabisa na jambo hilo. Kama maagizo yaliyopo katika Neno lake huyatii..Kufa unaweza tu kufa.
Jambo kama hilo tutaliona kwa Musa. Kila mtu anafahamu kuwa alitokewa na Mungu mwenyewe katika mwali wa moto. Mungu akampa ishara kubwa..akamtuma aende Misri kwenda kuwaokoa mamilioni ya watu..Lakini cha ajabu tunashangaa Mungu alitaka kumuua njiani..
Yaani kama sio mke wake Sipora,kumsaidia habari ya Musa ingekuwa imeishia pale na maono yake na wito wake.
Kutoka 4:21-25
[21]BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao. [22]Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; [23]nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako. [24]Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, BWANA akakutana naye akataka kumwua. [25]Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi.
[21]BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao.
[22]Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;
[23]nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako.
[24]Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, BWANA akakutana naye akataka kumwua.
[25]Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi.
Sasa ni kwanini Mungu alitaka kumuua ni kwasababu alipuuzia maagizo ya msingi ya kuwatahiri watoto wake..Mambo ambayo Mungu alikuwa ameshawaagiza wana wa Israeli wote wafanye hivyo kulithibitisha agano lake..Lakini yeye hakuona umuhimu huo..kisa tu Mungu amemtokea..amemtuma kama nabii mkuu Misri..hivyo hakuna sababu ya kuhangaika na yale mengine..
Ni wangapi leo hii wamepatwa na kiburi cha kukataa maagizo ya Mungu kama vile ubatizo sahihi wa maji..kwa kisingizio kuwa Mungu anazungumza na wao..Mungu kawatokea..Mungu kawaagiza waende kutumika..ubatizo hauna maana yoyote ukishamkiri tu Kristo inatosha..Wewe si zaidi sana ya nabii Musa..Mungu hashindwi kukuua.
Unaweza kusema ni Musa tu peke yake yalimkuta haya..Yupo nabii mwingine huko mbeleni anaitwa Balaamu.. Yeye naye alitokewa na Mungu katika safari yake ya kwenda kuwalaani Israeli.
Mara ya kwanza Mungu akamuonya lakini hakusikia.. Akataka zaidi kufanya hivyo..baadaye Mungu akamruhusu na akamuhakikishia kuwa atakuwa pamoja naye..Lakini njiani Mungu alikuwa ameshamweka malaika wake tayari amuue. Kama si yule Punda kumsaidia habari yake ingekuwa naye imeisha pale…
Ni kwanini sasa iwe vile ni kwasababu alipuuzia maagizo ya awali ya Mungu “..amlaaniye Israeli na yeye atalaaniwa”(Mwanzo 12:3)..hivyo yeye akataka kulipindua hilo Neno kwa maono yake..au mitazamo yake mwenyewe. Akawa katika hatihati ya kufa..
Hesabu 22:12-13
[12]Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa. [13]Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi….
[12]Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.
[13]Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi….
Lakini baada ya kushurutishwa sana na wale wakuu wa Balaki..utaona alijifanya tena kwenda kumuuliza Mungu..hichi ndio kitu alichoambiwa mara ya pili
Hesabu 22:20-22
[20]Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi. [21]Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu. [22]Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa BWANA akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.
[20]Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.
[21]Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.
[22]Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa BWANA akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.
Ndugu..tuzifahamu tabia za Mungu..wapo watu wengi wameonyeshwa mambo makubwa sana katika wito wao. Lakini unashangaa hakuna hata moja limetimia..hadi siku anakufa..Ni kwanini?
Nikwasababu alikwenda pasipo kujua kanuni za Mungu. Tuishi kwa Neno la Mungu na sio kwa ndoto au sauti au maono. Haijalishi wito huo utakuwa mkubwa kiasi gani..hauwezi kuzidi Neno lake.. Neno linasema mwanamke hana nafasi ya kufundisha kanisani (palipo na mchanganyiko wa wanaume na wanawake) 1Timotheo 2:12..Lakini mwingine atasema Mungu kaniita kuwa Mchungaji..kanitokea kabisa na kunitia mafuta..
Mama kuwa makini..kasome biblia yako kwanza umwelewe Mungu ndipo ukatumike..
Hivyo ili tuwe salama.. kabla ya kuitii sauti yoyote ya nje..Tuitii kwanza Sauti ya Mungu iliyo katika Neno lake. Ndio hayo mengine yafuate.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp ya kila siku basi jiunge kwa kubofya hapa >>> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
JE UNAIFANYA KAZI YA MUNGU?
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Nini maana ya “wazimu” katika biblia?
JINSI PAULO ALIVYOPAMBANA NA UJINGA WA ROHONI.
PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya huu mstari..
Mithali 15:27
[27]Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
[27]Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe;
Bali achukiaye zawadi ataishi.
JIBU: Mstari huo ni mgumu kueleweka kidogo kwasababu kiswahili kilichotumika hapo ni kile cha zamani..
Ukiangalia tafsiri nyingine..mstari huo unamaana hii.. Atamaniye kupata vingi kwa njia isiyohalali huifadhaisha nyumba yake mwenyewe bali achukiaye rushwa ataishi.
Jambo ambalo ni kweli..kwamfano Mtu anayejiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya kwa tamaa tu ya kupata fedha nyingi..hajui kuwa mwisho wake ni kujibomoa yeye mwenyewe na pamoja nyumba yake yote.
Habakuki 2:9
[9]Ole wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kioto chake juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu!
Mwingine utakuta anatoa rushwa ili bidhaa zake zisilipishwe kodi..lakini hajui mwisho wake utakuwa mbaya siku moja.
Lakini kinyume chake biblia inasema atakayeyakwepa hayo yote ataishi..
Sikuzote tamaa ya za haraka haraka mwisho wake huwa ni mitegoni..
Mhubiri 4:6
[6]Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo.
[6]Heri konzi moja pamoja na utulivu,
Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;
na kujilisha upepo.
Pia kama utapenda uwe unafikiwa na masomo ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP basi bofya hapa ujiunge moja kwa moja >>>> WHATSAPP
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Maana ya huu mstari ni ipi? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.
UMEDI NA UAJEMI ZILITAWALAJE?
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
HUANGUA MAYAI YA FIRA, NA KUSUKA WAVU WA BUIBUI;
Ratili ni kipimo cha uzito kilichotumika enzi za kale..chenye uzito sawa na Gramu 500 hivi. Karibia na nusu kilo.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia..
Yohana 19:39
[39]Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia.
Pia..
Yohana 12:3
[3]Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.
Unaweza kupata picha Mariamu alibeba manukato yaliyokuwa na uzito wa karibia nusu kilo..na yote akammwagia Bwana Yesu..manukato ambayo ingetosha tu kuchukua kidogo na kumpaka lakini yeye aliyamimina kwake kama maji.
Kwasasa mafuta hayo kwa wingi wake ni thamani isiyo pungua milioni 6 kwa fedha za kitanzania..kufunua ni jinsi gani Mariamu alimthaminisha Yesu kuliko mtu mwingine yeyote au mfalme yeyote duniani..
Si ajabu kwanini matendo ya watu kama hawa tunayasoma hadi leo katika maandiko..Ni kutufundisha kuwa na sisi pia tukitoa vitu vyetu vya thamani nyingi sana kwa ajili ya Mungu..
Mungu naye ni lazima arudishe fadhila kwetu kwa kutupa kumbukumbu la daima..ndivyo alivyofanya kwa yule mwanamke pale watu walipomng’unikia kwa upotevu wote ule..Bwana alisema..
Marko 14:8-9
[8]Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko. [9]Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
[8]Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.
[9]Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Swali ni je na sisi tunaweza kumthamini Bwana kwa namna hiyo? Bwana atupe macho hayo.
Shalom.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)
Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima.
Ulishawahi kuutafakari kwa ukaribu huu mstari ambao Bwana Yesu aliusema katika..
Luka 16:12 “Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
Kauli hii ni kinyume na sisi tunavyoweza kuitafsiri. Kwa kawaida, ni sharti kwanza mtu atazame uaminifu wa kile cha kwako kwanza, ndipo ashawishike kukuongezea kilicho cha kwake. Ukienda kukopa Benki ni sharti waangalie mipango/ mikakati yako na matumizi yako kwa kile ambacho tayari umeshaanza kukifanya, ndipo wakupe mkopo wa kuongezea biashara yako.
Vinginevyo ukienda hoe hae, huna malengo au mipango, ni wazi kuwa hutaambulia chochote, kwasababu wanahofia kama tu hicho cha kwako kidogo kimekushinda kukitazama, ukiongezewa kikubwa utawezaje?
Kama cha kwako mwenyewe haukijali, utajali vipi vya wengine?. Kama unajiibia mwenyewe ofisini kwako, utayahurumiaje mashirika ya wengine uliyopewa uyasimamie..
Lakini kwa Mungu ni tofauti, ili akupe kitu chako mwenyewe, ni sharti kwanza ukijali cha mtu mwingine. Ni sharti kwanza uonyeshe uaminifu kile cha mwingine ulichowekewa dhamana.
Unataka Mungu akupe uchungaji wako, Atakuangalia Je ulishawahi kuwajali kondoo wa Mungu, katika hilo kanisa ulilowekwa chini yake sasa? Ulishawahi kuwahudumia kwa upendo kabisa na kuwajali kama Mungu anavyotaka, Kama hukuweza basi ni ngumu sana Mungu kukupa cha kwako.
Mtu anamwomba Mungu ampe watoto wa kulea, lakini watoto wa familia nyingine hawajali, wala hata hana mpango nao kisa tu hajawazaa yeye.. Mungu akishaona hivyo, anasema, hata akikupa wa kwako hutaweza kuwalea, ni heri tu ubaki hivyo hivyo ..
Leo watu wengi wanamwomba Mungu awape ofisi zao wenyewe, Je, pale ulipowekwa kama muajiriwa unatumika kwa uaminifu?.
Unataka Mungu akupe nyumba yako mwenyewe, Je! Umekuwa mwaminifu katika hiyo nyumba ya mwingine Mungu aliyokuweka chini yake? Unaijali, unaitunza, unaipa thamani kama vile ni ya kwako?
Chochote tunachokitaka kwa Mungu, tujue kuwa atatujaribu kwanza kwa kutuletea hicho hicho kutoka kwa wengine,aupime uaminifu wetu. Mungu alimpima Yusufu katika nyumba ya Potifa kama je! Atakuwa mwaminifu? Na alipouona uaminifu wake, ndipo akampa cha kwake, akawa waziri mkuu kule Misri.
Hata katika ufalme wa Mungu, hatutapewa miji yetu wenyewe tuimiliki kule kwenye mbingu mpya na nchi mpya kama hatutakuwa waaminifu hapa duniani, kwa utumishi Mungu aliotuwekea chini yake katika kanisa lake.
Ikiwa tunalegea legea, au tunavipuuzia vya Mungu, au tunafanya mambo ya aibu, tusahau kule kupewa chochote na Mungu wetu ili tumiliki.
Tafakari tena habari hii..
Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. 13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. 14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. 15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. 21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. 26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.
Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.
19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.
Hivyo tuwe waaminifu, mahali popote Mungu alipotuweka. Kwasababu hiyo ndio itakayofungua milango ya kuwepa vya kwetu wenyewe.
Bwana akubariki sana.
KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
YESU NI MFALME WA AINA GANI KWAKO?
KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.
Furaha kwa tafsiri ya kawaida, ni muhemko chanya wa kihisia unaotakana na aidha kuridhishwa na jambo fulani au kupata kitu fulani.
Kwa mfano katika biblia Wale mamajusi walipoina tena ile nyota ya Bwana kule Bethelehemu, walifurahi.
Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno”.
Utaona pia wale waliokwenda kaburini kwa Yesu,Na kukuta ameshafufuka, Biblia inasema walifurahi sana.
Mathayo 28:8 “Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari”.
Hata mbinguni malaika wanapoona mtu mmoja ametubu dhambi, huwa wanafurahi pia.
Luka 15:10 “Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”.
Kwahiyo utaona hapo furaha tunayoijua, huwa inazaliwa kutokana na kupatikana kwa kitu fulani kilichokuwa kinatarajiwa au jambo fulani.
Lakini furaha halisi ya ki-Mungu. Ni furaha inayozidi mipaka, , hata katika shida furaha hii ipo. Ni furaha ambayo huwezi kuielezea kwa upatikanaji tu, kama furaha nyingine, inazidi mipaka hiyo.. Kwa kifupi ni kuwa haiathiriwi na hali au mazingira.
Na furaha yenyewe inaletwa na KRISTO YESU mwenyewe.
Ikiwa na maana mtu anayempokea Kristo, kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Mungu anakuwa na jukumu la kumininia furaha hii kwa Roho Mtakatifu atakayempokea kipindi hicho.
Warumi 15:13 “Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu”.
1Nyakati 16:27 “Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake”. Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
1Nyakati 16:27 “Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake”.
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Luka 2:10 “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; 11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”.
Luka 2:10 “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”.
Yokobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”
Yokobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”
1Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.
Kwa muda wako pitia vifungu hivi
1Petro 1:8, Yohana 17:13
Na wewe ikiwa ni mmojawapo wa wale wanaotaka kuonja FURAHA hii ya Ki-Mungu ambayo si watu wote wanaweza kuonjeshwa utakuwa umefanya uamuzi wa busara sana. Kwasababu ni kwake tu peke yake ndipo Furaha inapopatikana, hakuna mwingine, Bwana anasema hivi;
Zaburi 5: 11 “Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia”.
Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
Unaona? Basi fungua leo moyo wako, Kristo aingie ndani yako, kukusamehe, na kukuwekea furaha idumuyo. Ikiwa Upo tayari leo kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.
Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?
Unyenyekevu ni nini?
Gombo ni nini?
Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.
WhatsApp
SWALI: Naomba kufahamu maana ya mstari huu”
[25]Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
[44]Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.
Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)
SIKU YA HOFU YANGU NITAKUTUMAINI WEWE.
AOGOPACHO MTU ASIYE HAKI NDICHO KITAKACHOMJILIA.
Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).
Je! Kucheza mpira au kushabikia mpira ni dhambi kulingana na maandiko?.
Bwana kutuumba miili yetu hii ili kuishughulisha, hajatuumbia ikae tu bila kujishughulisha..Na njia mojawapo ya kuishughulisha ni kwa kufanya mazoezi.
Na mazoezi hayo yanaweza kufanyika kwa njia ya kawaida au ya kucheza..Kwamfano watu wawili marafiki wanaweza kusimama na kushindana mbio, na mwisho wa mbio wakafurahi na kucheka, hatimaye wakawa wamecheza na hapo hapo kufanya mazoezi. Sasa kucheza kwa namna hiyo sio dhambi lakini tatizo linakuja mfumo unaochanganyikana na mchezo huo.
Kwamfano mchezo unapohusisha kuvaa kuilimwengu, au matusi, au miziki ya kiulimwengu, au mambo yoyote yasiyo na adabu mchezo huo ni dhambi, na sisi wakristo hatupaswi kuushiriko.
Kwamfano riadha za siku hizi ili wanawake au wanaume washiriki, hawana budi kubaki na nguo za ndani tu!..na sehemu nyingine yote ya mwili kubaki wazi.
Utakuta wanawake wanakimbia riadha wakiwa na chupi tu, na wanaume hivyo hivyo. Sasa michezo ya namna hiyo ni dhambi kushiriki kwa mkristo.
Na kama ni dhambi, basi na hata kuishabikia vile vile ni dhambi.
Kadhalika watu wawili wanaweza kitengeneza mpira wao na kisha kuipiga piga kwa miguu yao kujifurahisha..jambo hilo sio dhambi.
Lakini inapotokea mchezo huo unachanganyikana na mfumo fulani wa kishetani, tayari mchezo huo unakuwa ni najisi kwakristo, kwamfano utakuta mchezo fulani unadhaminiwa na shirika la pombe au la sigara, au la kubeti kiasi kwamba hata sare za mchezo huo ni nembo la mashirika hayo najisi.
Au utakuta michezo mingine ni lazima ihusishe miziki ya kidunia ambayo ni najisi kwa mkristo.
Hapo hatupaswi sisi kama wakristo kushiriki michezo hiyo, wala kuwa wafuasi wa hiyo michezo.
Hivyo kwaasili michezo sio mibaya, Hata Yakobo alicheza Mieleka na yule Malaika..
Lakini mieleka ya leo ni lazima ubakiwe na nguo za ndani tu!..Na tena siku hizi ni jinsia mbili tofauti zinapigana mieleka, kiasi kwamba huwezi kutazama mara mbili michezo hiyo imejaa matusi na ushetani.
Imefungamana na ushetani kiasi kwamba kitendo cha kuangalia tu tayari umenajisika..
Na siku zinavyozidi kwenda hiyo mifumo inazidi kuongezwa juu ya hiyo michezo na kuharibu kabisa maana ya michezo.
Huko mbeleni, riadha zitakuwa zinafanyika uchi wa mnyama kabisa, tofauti na leo ambapo ni nguo za ndani tu ndio zina sitiri. Kama tunataka kucheza (sisi kama wakristo), tunaweza kucheza sisi kwasisi bila kutumia mifumo hiyo ya kishetani.
Lakini pia biblia imetuonya kuwa na kiasi, maana yake sio kucheza mpaka unakuwa unafanana na watu wa kidunia.
Vile vile mambo yote tunapaswa kuyafanya kwa utukufu wa Mungu. Ukicheza na mtoto wako inaweza ikatosha, ukicheza na kaka yako inatosha, ukicheza na rafiki zako wawili au watatu inatosha, sio lazima tujichangange na harambee za watu wengi wa kiulimwengu, kushiriki nao michezo iliyojaa unajisi na mizaha.
Maran atha!
TUMEKUWA TAMASHA KWA DUNIA; KWA MALAIKA NA WANADAMU.
Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
JE! KUBET NI DHAMBI?
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Kabla ya kwenda katika maombi Awali ya yote ni vizuri ukafahamu kuwa mafanikio ya kiuchumi yanaweza kuletwa na vitu vikuu vitatu
Na kila mmoja anayo kanuni yake ya kuyafikia hayo mafanikio.
Kwamfano kwa mwanadamu, ili aweze kujikomboa kiuchumi, kanuni ni moja nayo ni “kuwa na bidii katika kufanya kazi”..haijalishi kazi hiyo itakuwa ni ya kuuza pipi, maadamu unatia bidii ndani yake, utafanikiwa kwasababu katika bidii hiyo, huko huko ndio unazalika ubunifu na mikakati, ya kupiga hatua, na kuwekeza,n.k. na mwisho wa siku utafanikiwa, Hata kama hatofikia utajiri ule, lakini mwisho wa siku utajikomboa kiuchumi, haijalishi atafanya hivyo kwa muda gani. Na hapo atakuwa tayari kashajikomboa kiuchumi.
Lakini kanuni za ibilisi ni tofauti na zile za kibinadamu. Pengine kwake si lazima ujishughulishe sana, lakini akakupa mafanikio tu, Kwasababu ndicho alichojaribu kufanya kwa Bwana Yesu, kwa kumwambia tu amsujudie ndipo atakapompa mali zote.
Mathayo 4:9 “akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.”
Unapokwenda kwa waganga watakupa mafanikio, lakini wakiwa na masharti yao kwamba ni lazima ufanye kitu fulani kwa shetani n.k..
Lakini tunaporudi kwa Mungu, napo pia kuna kanuni zake, za kufanikiwa. Ukienda nje ya hizo, na huku unahitaji mafanikio, au kukombolewa kiuchumi usijidanganye, unapoteza muda. Nenda tu kajibidiishe huko kama wanadamu wengine, utafanikiwa pia kwa njia hizo.
Lakini Kanuni za Mungu za kumkomboa mtu kiuchumi ni zipi?;
Kabla ya kuombewa ni lazima uwe mwana wake. Na mtu anakuwa mwana wake kwa kutubu dhambi zake zote, na kubatizwa, kisha kupokea Roho Mtakatifu. Na baada ya hapo kuanzia huo wakati na kuendelea kuishi maisha yampendezayo Mungu.
Biblia inasema..
Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”.
Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”.
Unaona? Ukishautafuta kwanza ufalme wake na haki yake, kuanzia huo wakati unakuwa tayari sasa, kushiriki Baraka zote kutoka kwa Mungu, kiwepesi pale unapomwomba.
Neno la Mungu linasema hivi..
2Wakorintho 8:9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”.
Na pia Yesu mwenyewe alisema..
Mathayo 19:28 “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. 29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele. 30 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza”.
Mathayo 19:28 “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
30 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza”.
Hivyo kabla ya kwenda kukuombea Baraka zako kutoka kwa Mungu.. ni sharti kwanza uwe tayari leo kumkabidhi Bwana Yesu maisha yako, kwa kumaanisha kabisa. Kama upo tayari basi hapo ulipo tafuta sehemu yenye utulivu, kisha piga magoti, kisha sema sala hii kwa imani, kwa kumaanisha kabisa, na Mungu atakuokoa siku ya leo.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa kwa sala hiyo fupi, amini kuwa Bwana Yesu ameshakusamehe, Na kuanzia sasa unakuwa tayari kushiriki, Baraka zote kutoka kwa Mungu.
Yeye mwenyewe alisema maneno haya;
Kumbukumbu: MLANGO 28
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. 10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. 11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. 12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. 13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya; 14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.
9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.
10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako.
11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.
13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
Baraka hizo zote, zitakufuata endapo utadumu tu katika WOKOVU.
Basi sasa, nitakuombea, ili milango hii ifunguke, katika maisha yako. Hapo ulipo Piga tena magoti, niombe kwa ajili yako. Fuatisha kwa sauti sala hii;
Baba Mwenyezi, Mungu wa milele, ahsante kwa kutupa zawadi ya kutuletea mkombozi duniani, Bwana wetu Yesu Kristo. Asante kwa kuwa alikuja kutukomboa kutoka katika dhambi zetu na laana zetu. Lakini hakuishia hapo tu, bali alitukomboa, mpaka na UCHUMI wetu.
Nami leo hii nimempokea na kumkiri kwa kumaanisha kabisa kumfuata tangu sasa hadi milele. Naomba Mungu wako zile Baraka zote ulizoziahidi katika Kumbukumbu la Torati 28:1-14, zinijilie juu yangu. Nami nikawe Baraka kwa jamii na kwa kanisa lako. Kuanzia sasa ikiwa kuna kazi zozote za ibilisi zilizotangulia nyuma yangu kunizuilia Baraka zangu, ninazikataa kwa jina la Yesu Kristo. Naiita Damu ya Yesu ikasafishe kapu langu, na mfuko wangu.
Asante Mungu wangu kwa kunikomboa.
Amen.
Basi, ikiwa umeyafuatilisha maombi hayo, ujue kuanzia sasa, Mungu atatembea na wewe katika uchumi wako, kwa kile unachokifanya, tenda mapenzi ya Mungu, utaona akikupigania. Lakini kumbuka Kama tulivyotangulia kusema, inahitaji Kutembea na Mungu ili akukamilishie ahadi hizo, sio tu kukiri kwa mdogo, unakwenda kuendelea na mambo yako..nikuambie ukweli tu, inahitaji maisha.
Mungu akubariki sana.
Ikiwa utahitaji msaada zaidi wa kumjua Mungu, au ubatizo, au unaswali lolote kuhusu biblia, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi Simu/Whatsapp: +255693036618 / +255789001312
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
TWEKA MPAKA VILINDINI.
NI YESU YUPI UMEMPOKEA?, NI ROHO IPI UMEIPOKEA? NA INJILI IPI UMEIPOKEA?
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Haya Mafungu ya biblia ambayo wazazi/walezi wanapaswa wayajue kuhusu watoto wao.
Zaburi 8:2a “Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu;..”
Mungu anaonyesha kuwa kupitia watoto wachanga, ambao unaweza kuwadharau hawajui kitu, hapo ndipo Mungu ameweka nguvu zake. Hivyo anza kumlea mtoto katika misingi ya kumcha Mungu tangu akiwa mdogo, kwasababu hapo ndipo Mungu anapoketi.
Na ndio maana biblia inasema..
Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Tabia ya kudharau watoto, au kuona kama umri wao wa kumjua Mungu bado, Yesu aliukemea sana, tunalithibitisha hilo katika..
Marko 10:13 “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.14 Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.16 Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia”.
Marko 10:13 “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.
14 Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.
16 Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia”.
Biblia inasema pia..
Zaburi 127:3 “Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu”.
Biblia bado inasisitiza wazazi, wasiwaudhi watoto wao, kwasababu zisizo na msingi, kisa tu wao ni watoto,
Waefeso 6:4 “Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Kwasababu malaika wao mbinguni wanawatazama uwatendeapo mabaya..
Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni”.
Zaidi pia Bwana Yesu anataka wazazi/walezi wajifunze kupitia watoto walionao, hivyo kwa kupitia wao tutapata kujua siri kubwa za ufalme wa mbinguni.
Mathayo 18 : 1-5
“1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.5 Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;”
“1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,
2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
5 Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;”
Lakini bado Mungu anasisitiza juu ya kuwarekebisha watoto, kwamba ni jukumu la kila mzazi/mlezi kumwadhibu mtoto wake, pale anapokosea . Hilo ni agizo la Mungu. Usipomwajibisha mtoto wako, Mungu atakuwajibisha wewe siku ile, kwa kutomtengeneza mwanao.
Mithali 22:15 “Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali”.
Mithali 23: 13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.
Mithali 23: 13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.
2) WAJIBU WA MTOTO.
Vilevile mzazi, unapaswa umfundishe mwanao wajibu wake kama mtoto, Sawasawa na Neno la Mungu linavyosema,
Na mojawapo ni kuwafundisha kukutii wewe.
Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.
Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.
Mithali 1:8 “Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako”.
Mithali 1:8 “Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako”.
Pia umfundishe kujua wajibu wake wa kumtafuta Mungu tangu akiwa mdogo..kwasababu kwa Mungu hakuna utoto.
Yeremia 1:6 “Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru”.
Yeremia 1:6 “Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru”.
Na mwisho Mkumbushe pia hata watoto watahukumiwa, na kuzimu wapo watoto ambao hawakuwajibika katika kuwatii wazazi wao, na kumcha Mungu.
Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.
Maran atha.
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo, Mfalme wetu, Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Utakumbuka huduma ya Bwana wetu iligawanyika katika sehemu kuu tatu,
Ya kwanza, ilikuwa ni hapa duniani,
Ya pili ni Kuzimu
Na ya tatu ni mbinguni.
Lakini wengi wetu tunafahamu ile ya duniani na mbinguni, Lakini kwa sehemu ndogo sana tunaielewa ile ya kuzimu. Ni vema pia tukaifahamu hiyo ili tujue ni nini tutakutana nacho baada ya kifo.
Siku tukiifahamu kwa mapana, hatutaacha kumshukuru Bwana Yesu kwa kifo chake pale msalabani.
Kama tunavyosoma siku ile Bwana aliyokufa, kuna matukio kadha wa kadha yaliyotokea, mojawapo ni lile la pazia la hekalu kupasuka, lakini tukio lingine ambalo lilitokea la kustaajabisha sana, ni lile la kuonekana kwa watu ulimwenguni ambao walikuwa tayari wameshakufa zamani. Na watu hao walikuwa ni watakatifu wa zamani.
Biblia inatuonyesha baada ya kufufuka kwao walianza kutembea tembea na kuingia mpaka mji mtakatifu wa Mungu (Yerusalemu.)
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.
Sasa swali unaweza kujiuliza ni kwanini uwe ni wakati ule na si mwingine, kwanini waonekane wanatoka makaburini, na kutembea tembea duniani, huku wakiwatokea watu? Kwanini iwe hivyo? Na hao watu sasahivi wapo wapi?
Hii ni kutuonyesha kuwa zamani mtu alipokufa, hakuwa huru hata kidogo, alikuwa anakwenda moja kwa moja kaburini haijalishi ni mtakatifu au mwovu. Huko kaburini ndio sasa kuliganyika katika sehemu ya waovu na wema.
Na kama tunavyojua sikuzote kaburi ni kama gereza, huwezi kwenda popote, au kufanya lolote, ndivyo ilivyokuwa kwa watu wote waliokuwa wanakufa zamani, walikuwa sehemu fulani tu, wamekaa wanasubiria siku moja masihi aje awaondoe huko. (Waebrania 2:14-15)
Lakini Bwana Yesu alipokuja, alifanya kazi ya kuyapasua makaburi hayo yaliyokuwa yamewashikilia kwa nguvu ya dhambi kwa muda mrefu . Lakini biblia inatuonyesha hakupasua makaburi ya wote, bali ya wale watakatifu tu. Na matokeo yake wakatoka huko, wakawa huru kama vile wanaishi tena duniani, na ndio maana wakawatokea wengi, wakatembea tembea huu na huko mpaka mji mtakatifu (Yerusalemu) n.k. kuonyesha ni jinsi gani wafu waliokufa katika Kristo walivyo huru, rohoni.
Hiyo ni kufunua kuwa, mtakatifu yeyote anayekufa leo, haendi tena kaburini kama watu wanavyodhani..ataliona tu kaburi kwa pale pembeni, lakini yeye hatakwenda huko kabisa bali ataondoka na kwenda kuendelea kuishi sehemu nyingine fulani iliyo nzuri sana, ijulikanayo kama Paradiso (peponi) Luka 23:43. Huko atakuwepo na Bwana Yesu mwenyewe, na watakatifu wengine, watakuwa ni kama tu vile hawajawahi kufa, wanaishi kama tunavyoishi hapa, isipokuwa tu huko ni kuzuri sana.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya,
Yohana 11:25b….Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Yapo maisha baada ya kufa kwa mtakatifu.. , hawi kifungoni, anakuwa huru kule PEPONI (Paradiso), akimfurahia Kristo, huku akingojea siku ya Unyakuo ifike, aje kuuchukua mwili wake, aende mbinguni.
Lakini mtu anayekufa katika dhambi, ni moja kwa moja kaburini, kifungoni, kwenye giza nene, ndio kuzimu kwenyewe, maisha yake yanagotea pale anapokufa, hayawezi kuendelea kuishi, sio kwamba roho yake itakufa, hapana, bali ni kwamba hawezi kuwa na maisha, kama sisi tuliyonayo, au wale wale wengine waliyonayo.
Biblia inasema hivi, juu ya Bwana Yesu alipokwenda kuzimu;
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
Unaona watu wote wenye dhambi sasa wapo huko vifungoni, kwa maelezo marefu juu ya habari hiyo, tutumie ujumbe inbox tukutumie somo lake..
Lakini utajisikiaje wewe uliye dhambini, ukifa leo katika hali hiyo? Siku hiyo utatamani upate hata nuru kidogo hutaona, utatamani, utembee tembee huku na huko kama wale wengine hutaweza, utatamani ule au unywe hutaweza, utakuwa katika jehanamu ya mateso daima, ukiteseka, kama Yule tajiri wa Lazaro, ambaye aliomba hata achovyewe maji kidogo kwenye ncha ya kidole cha Lazaro,akashindwa,(Luka 16:19-31) utakaa huku huku ukingojea na wewe siku ile ya hukumu ifike, ufufuliwe, uhukumiwe kisha utupwe kwenye lile ziwa la moto milele na milele.
Ndugu, kumbuka kifo hakina hodi, vilevile Unyakuo pia hauna hodi, ni siku yoyote au wakati wowote, unaondoka hapa duniani, au Yesu anarudi, inasikitisha kusoma katika biblia kwamba “kuzimu hakishibi watu”. Ikiwa na maana Maelfu kwa maelfu wa watu wanaenda huko kila siku.
Tutawezaje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii. Aliyeshinda kaburi na mauti kwa ajili yetu, yupo hata sasa kutuokoa, Embu tufungue mioyo yetu, atupe wokovu huu bure. Atusamehe makosa yetu yote. Hata siku tukifa tuwe na uhakika kuwa kaburi sio sehemu yetu.
Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha uwe tayari kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kuukamilisha wokovu wako, Na Bwana atakupokea.
Ikiwa utahitaji msaada wa kumpokea Yesu, basi unaweza kuwasiliana nasi pia kwa namba hizi. +255693036618 / +255789001312
UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
UNYAKUO.