Kuna baadhi ya watu Mungu anawapanda katika kanisa, kwa namna ya kitofauti na kipekee sana..
Na pengine wenyewe hawalijui hilo..hivyo wanaishi maisha ya kimaficho ficho tu..au ya juu juu tu, kwa kisingizio kuwa wao si kama wengine.. wakidhani kuwa Kristo, amewaweka hapo bure, kwasababu hiyo..
Ulishawahi kuitafakari vizuri hii habari..
Luka 13:6-9 [6]Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. [7]Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? [8]Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; [9]nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.
Fikiria hilo ni shamba la Mizabibu..pengine ekari elfu moja, limeandaliwa mahususi kwa ajili ya kutoa zabibu za kibishara..lakini mwenye shamba tunaona bado katikati ya shamba hilo kubwa alipanda mti mwingine wa matunda ujulikanao kama “mtini”..
Kumbuka lengo lake halikuwa apate matunda ya biashara kutoka katika mti huo..bali pengine ya kula tu, na ndio maana mtini wenyewe ulikuwa ni mmoja tu. Lakini bado hakutaka ukae bila matunda..akaupa muda ili uzae..
Kuna watu Mungu kawapanda katika kanisa lake, ambao wanaweza kuonekana ni tofauti sana na watakatifu wengine pengine kilugha, labda hawajui kiswahili vizuri, au kimazingira, labda wapo mbali, au kinafasi, ni viongozi wakubwa n.k.na hivyo hawawezi moja kwa moja kutumika kama hawa wengine..kwa vikwazo hivyo.
Lakini wengi wa hawa huwa wanaishi maisha ya kujificha, wakidhani pengine sio sehemu ya kanisa la Kristo.
Nataka nikuambie, vyovyote vile ujionavyo..Kristo anatazamia matunda kutoka kwako. Anataka aone ukristo wako ukiangaza kwa wengine..anataka kuona unafanya kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni..anataka kuona shamba lake alilokuweka wewe ndani yake pamoja na hao wengine hulikalii bure…na wewe pia kwa nafasi yako uhakikishe unazaa matunda..
Hizi ni siku za mwisho ndugu yangu..Kristo anasema Naja upesi, na ujira wangu, upo mkononi mwangu kumlipa kila mtu..sawasawa na kazi yake ilivyo..
Ufunuo wa Yohana 22:12 [12]Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Utalipwa nini siku ile..ikiwa miaka nenda rudi, wewe ni msikiaji tu wa injili, miaka nenda rudi upo tu mafichoni, hutaki ijulikane..jiulize Ni nini umemfanyia Bwana basi..mpaka akupe ufalme siku ile?
Bwana atutie nguvu, tutambue kuwa sote tupo shambani mwake..na sio jukumu la askofu fulani au shemasi. Na kwamba Bwana atamvumilia mtakatifu yoyote katika shamba lake asiyemzalia matunda.
Tafadhali shea na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
AINA TATU ZA WAKRISTO.
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya huu mstari
Kumbukumbu 27: 24 “Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina”.
SWALI: Kulingana na sheria ya wayahudi, kosa lolotela kumdhuru mwenzako, liwe ni dogo au kubwa, lilipoonekana, adhabu yake ilitolewa palepale kulingana na kosa lenyewe.. kwamfano ukimng’oa mwenzako jino, na wewe pia uling’olewa la kwako, ukimtoa jicho, na lako pia linatolewa, ukiua na wewe pia uliuliwa,..hapo ndipo uovu ulipoweza kuondoka juu ya mtu.
Lakini kulikuwa na makosa mengine watu waliyafanya kwa siri, ambayo hayakuwa rahisi kugundulika kwa wazi, wanashangaa tu labda mtu kafa, wakidhani ni siku yake tu imefika, kumbe aliwekewa sumu siku nyingi ambayo ilikuwa inamuua kwa taratibu..
Sasa watu kama hawa, biblia inasema, wamelaaniwa, kwasababu wanawapiga wenzao kwa siri, wakidhani kuwa hata mbele za Mungu hawataonekana.
Mfano wa watu kama hawa katika biblia ni Yezebeli. Yeye alikwenda kumuua Nabothi Myezreeli, ili tu alipate shamba lake, akawaajiri watu wa kushuhudia uwongo waseme wamemsikia Nabothi amemtukana Mungu na mfalme, ili watu wampige mawe afe, na kweli akafanikiwa adhma yake, na watu hawakujua lolote.
Lakini Mungu alijua, ndipo akamtuma nabii Eliya kumtolea hukumu yake. Na kumwambia mbwa watamla maiti yake. Na kweli ndivyo ilivyokuja kuwa (1Wafalme 21).
Mwingine ni mfalme wa Daudi, yeye alimuua askari wake aliyeitwa Uria kwa siri akidhani kuwa Mungu hatamwona. Alichofanya ni kumwambia mkuu wake wa majeshi amweke, Uria mahali penye vita vikali, kisha wamuache mwenyewe, ili azidiwe na majeshi ya adui auliwe, na kweli, njama zake zilifanikiwa, lakini Mungu akamrudia Daudi na kumpa adhabu kali sana, na doa ambalo mpaka leo hii sisi tunalisoma (2Samweli 11).
Hata leo, watu wanawapiga wenzao kwa siri, kwa kuwawekea vikwazo mbalimbali, lakini kwa nje wanajifanya wapo Pamoja na wao kuwasaidia, tukiwa watu wa hivi Mungu atatulaani. Halikadhalika Wachawi wote wapo chini ya hii laana, kwasababu mchana wanacheka na wenzao kinafki, lakini usiku wanazunguka huku na huko kuwanga, na kuwasababishia wenzao madhara, na kuvuruga mipango ya watu wanaotaka kumtafuta Mungu.
Hivyo tuwe makini sana, ni heri uadhibiwe na mwanadamu, kuliko kuangukia katika laana za Mungu mwenyewe. Kwasababu yeye ndiye anayeichunguza mioyo ya watu. Ili tuweze kuishinda hii hali, hatuna budi kumaanisha kumfuata Kristo kweli kweli katika Maisha yetu. Hapo ndipo tutakapoweza kuishi Maisha ya upendo na wengine.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?
MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!
Ni SIRI gani Paulo aliyokuwa anaimaanisha katika Waefeso 5:32?
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
WhatsApp
Shalom, karibu tujifunze na tujikumbushe wajibu wetu sisi kama watakatifu katika safari yetu ya Imani hapa duniani.
Kuna mambo ambayo tunaweza tukashindwa kumfanyia Mungu, tukadhani kuwa “Mungu anaelewa”, kumbe yanatafsirika kama Ni UDHURU mbele zake.
Tofauti na sisi tunavyoweza kutafsiri Neno udhuru. Kwamba ni kutoa sababu za uongo, ili tu kuepuka jukumu au wajibu Fulani, kwamfano, labda mtu kakuambia naomba ukanipakilie mzigo wangu kwenye gari pale stendi unitumie.. Sasa pengine wewe hutaki kwenda, ili kupindua hiyo safari, saa hiyo hiyo unaunda safari yako ya uongo na kumwambia, hapana sitaweza kwenda, kwani ninamgeni wangu natarajia baadaye, nikamchukue hotelini sijui atatoka muda gani..Lakini unajua kabisa, jambo kama hilo hukuwa na mpango nalo, huo ndio udhuru tunaoufahamu sisi.
Lakini kwa Mungu udhuru, ni kutoa sababu za kweli tena zenye maana na mashiko kabisa.. ambazo wakati mwingine ni kweli kabisa zinastahili kufanywa.. Ili kuelewa vizuri Embu tusome tena Habari hii kwa utulivu, naamini umeshaipitia mara kadhaa, lakini isome tena, na tena, uone ni nini Mungu analenga, na ujiangalie na wewe katika nafasi yako, Je! Mambo kama hayo yapo?,,Tusome..
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, 17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. 18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. 19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. 21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. 22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. 24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,
17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.
20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.
23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.
24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Embu zitafakari hizo sababu, uone kama hakuna hata moja isiyo na mashiko, ni kweli, sherehe tu, huwezi ifananisha na mke mpya..mwingine kanunua ng’ombe, wengi, hivyo ni lazima siku hiyo akawajaribu kwanza, vinginevyo wakiwa sio bora na siku imeshapita hawezi tena kuwarudisha,tayari ni hasara, mwingine kanunua shamba tayari, lakini bado hajaliona, hivyo ni lazima akalihakiki, kama ni lenyewe au kama ameuziwa dimbwi, na siku yenyewe ndio hiyo hiyo ya karamu aliyoalikwa hawezi kuacha kwenda?
Umeona, zote hizo zilikuwa ni sababu, lakini mwenye karamu anazitafsiri kama ni Udhuru. Kwasababu gani? Kwasababu wameyathamini mambo yao, Zaidi ya ile karamu yake kubwa.
Leo hii,watu wengi hata jumapili wameacha kwenda kanisani kabisa, wanasema, boss wangu hataki, wanazitetea kazi zao, ili wasifukuzwe..halafu kwenye vichwa vyao wanasema BWANA ANAELEWA!…Kama ingekuwa sio huyu boss wangu kunizuia, mimi nisingekosa kanisani hata siku moja..
Ndugu kwa Mungu huo ni udhuru..Kama unaweza kuitumikia kampuni yako, kwa siku 6 za wiki, hadi siku ya Mungu unaiiba, fahamu tu, Mungu hawezi kukuelewa, anautafsiri kama Udhuru. Haiwezekani wiki nzima, usijiwekee ratiba kwa Mungu wako ya kumwabudu yeye, hata siku moja.
Danieli hakuruhusu udhuru, hata alipokatazwa na mfalme wa dunia yote,(kumbuka Sio boss wa ka-kampuni fulani) kuabudu Mungu wake, na vitisho vyao vya kuwatupa katika tundu la simba wote watakaokaidi. kinyume chake Danieli ndio alifungua madirisha yake, akawa anamwabudu Mungu, wakati wengine, wanasema Mungu anaelewa, hali halisi ya sasa, tumekatazwa na mfalme, sisi ni nani tupinge..
Na walipomkamata na kumtupa katika tundu la Simba, Tunaona Mungu alikuwa naye..
Vivyo hivyo na akina Shedraka, Meshaki, na Abednego, walikataa udhuru wa Nebukadreza wa kuabudu sanamu, wakati wengine wanasema, Mungu anaelewa..wenyewe wakakataa kumvunjia Mungu heshima, ndipo walipotupwa katika tanuru la moto..Bwana aliwapigania na kuwaokoa.
Lakini ikiwa sisi kila jambo tutazama, hali zetu, tusijidanganye kuwa Mungu anaelewa! Hizo zote ni udhuru. Usiruhusu kazi ile muda wa Mungu wako, usiruhusu, familia, mihangaiko, mali zitafune muda wa Mungu wako. Wengine wanasema jumapili ndio faida ninapata, ndugu ziache hizo faida zipite, Ni nani kakuambia Mungu hatakupa hizo siku nyingine? epuka udhuru..
Na ndio maana mwishoni kabisa mwa ile Habari, Bwana anasema…
“Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.
Watu wanaotanguliza mambo yao mbele Zaidi ya Mungu katika kipindi hichi cha siku za mwisho, kwenye Unyakuo, kwenye karamu ya mwanakondoo mbinguni hawataenda. Swali je! Na wewe ni mtu wa udhuru kwa Bwana? Jibu unalo.
Maran atha.
Maswali na Majibu
UFUNUO: Mlango wa 19
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
SWALI: Kulingana na Danieli 7:14 inatabiri kuwa Ufalme wa Bwana Yesu utakuwa ni wa milele, Lakini tukirudi katika 1Wakorintho 15:24 anasema mwishoni atampa Baba yake ufalme wake,
Je hapo inamaana gani , Bwana Yesu ataurejesha ufalme kwa Baba yake au?
JIBU: Tusome vifungu vyote..
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
Pia..
1Wakoritho 15:24 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
1Wakoritho 15:24 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
Ni vema tukumbuke kuwa Mungu na Yesu, sio watu wawili tofauti, wenye falme mbili tofauti.. Hapana, “SIRI ya uungu” ni kubwa sana, kama vile mtume Paulo alivyoandika katika 1Timotheo 3:16, Ikiwa na maana mtu usipofumbuliwa macho na kuielewa sehemu ya siri hii, anaweza kudhani Bwana Yesu na Baba yake, ni watu wawili tofauti kabisa…
Ukweli ni kwamba, ufalme Yesu, ndio ufalme wa Baba yake, na Ufalme wa Baba yake ndio ufalme wa Yesu, hivyo akimrudishia Baba ufalme, hakufanyi badiliko lolote, kwasababu yeye na Baba ni kitu kimoja. Ni kama anavyopenda tu yeye mwenyewe atawalie katika ofisi ipi!! Je ya Baba au ya Mwana.. hivyo tu..
Kwahiyo Ufalme huo, kwasasa unatawala rohoni, lakini utadhihirika rasmi, tunapoingia katika ule utawala wa miaka1000, ambapo Mungu (Ndani ya Kristo), atatawala kwa miaka hiyo elfu mpaka atakapohakikisha kila kitu kiovu kimefikia mwisho wake, Kisha baada ya hapo, atatawala sasa kama Baba (Yehova), milele na milele.
Na ndio maana ufalme wake ni wa milele na milele na milele.. Ambao hauwezi kuhasika na kwenda kwa adui, au kwa Malaika yoyote, au kwa kiumbe chochote, utabaki kwake milele na milele na milele. Utukufu na shukrani vimrudie yeye daima.
Amen.
YESU NI NANI?
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
DANIELI: Mlango wa 11
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
UNYAKUO.
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze Neno la Mungu ili tupate maarifa sahihi ya kuishi hapa duniani.
Na leo tutaona mazingira ambayo ukikaa katika hayo basi Mungu atakujalia umwone mke/mume sahihi aliyekuchagulia toka mbali.
Tofauti na mazingira ya kiulimwengu ambayo yenyewe ili yakupe mke/mume wa kidunia ni sharti uwe katika mazingira ya kidunia..yaani uvae vimini, ujitembeze na suruali barabarani, unyoe viduku, uishi kama wasanii wa kidunia, uwepo disco na kwenye party party kila wakati n.k. ili uonekane.
Ukikaa katika mazingira kama hayo hakika dunia itakupatia unachokitafuta..
Lakini leo tutajifunza mazingira ya ki-Mungu… Ili Mungu akuonyeshe mke/mume sahihi tokea mbali je! Ukae katika mazingira gani.?
Tutamtazama Isaka mtoto wa Ibrahimu. Kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka mpaka wakati mama yake anakufa hakuwa na mke bado.
Lakini siku moja Baba yake alipoona ni wakati sasa wa Isaka kuwa na mke alimtuma Kijakazi wake mmoja kwenda kumtafutia mke kutoka katika nchi ya mbali nchi sana ya baba zake. ..kwani hakutaka kumpatia mke kutoka katika miji ile waliyokuwepo.
Kuonyesha kuwa haijalishi utazungukwa na vijana wengi wazuri mahali ulipo, hiyo bado haikufanyi udhani mke/mume Mungu aliyekuchagulia ni lazima atoke hapo.
Sasa utaona mara baada ya yule kijakazi kutumwa kwenda kumtafutia Isaka mke na kumpata alipokuwa anarudi..Huku nyuma kuna tabia na desturi ambayo Isaka alikuwa nayo ambayo nataka leo tuione kwasababu hapa ndipo kiini cha somo letu kilipo.. Tusome..
Mwanzo 24:62-66
[62]Basi Isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana alikaa katika nchi ya kusini. [63]Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja. [64]Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia. [65]Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika. [66]Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyoyatenda.
Rudia tena Mstari wa 62 unasema…
‘Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni’.
Unaona, Pindi tu alipotoa mguu wake na kwenda kondeni kutafakari..alipojijengea desturi ya kwenda maporini mbali na makazi ya watu ili tu kupata utulivu na Mungu wake, kuutafakari ukuu wake na uweza wake na maajabu yake na ahadi zake..huko huko Mke wake alitokea..na akamwona tokea mbali..
Pengine yeye alidhani mjini alikoondoka ndipo wake wanapotokea lakini..alishangaa kule kule kondeni kwa mbali sana ngamia wanakuja wamembeba bibi arusi wake..
Hiyo ni kuonyesha Isaka haukuwa na hulka kama za vijana wengine walizokuwa nazo..alipendelea zaidi kumtafakari Mungu kuliko kuzurura zurura huko na huko.
Matokeo yake akampata Rebeka, mwanamke ambaye tunamsoma mpaka leo, licha ya kuwa alikuwa ni mwanamke anayemcha Mungu lakini bado alikuwa ni mzuri sana wa uso..Mwanzo 26:6-7
Ndugu, ikiwa unamuhitaji mke mzuri na anaye mcha Mungu basi kuwa kama Isaka..lakini ikiwa unamuhitaji Yezebeli basi ishi mfano wa hao vijana wa kidunia wanavyoishi leo hii..
Na hili pia lipo kwa upande wa pili wa mabinti..ikiwa unataka uolewe na mwanamume ilimradi tu mwanamume basi jiweke kama hao mabinti wa kidunia wanavyojiweka wanaotembea nusu uchi barabarani na kujipambapamba kama vile Yezebeli ili waonekane wanavutia.. Utampata unayemtafuta.
Lakini kinyume chake ni kuwa ukitulia katika kusudi la Mungu..unatumia muda mrefu kwa Mungu wako kuliko kutanga tanga..unamtakafakari tu yeye..nakwambia Mungu utakuongoza kwa Isaka wako tokea mbali..kama vile Rebeka alivyomwona Isaka akimfuta kutokea mbali..
Uhitaji kujionyesha onyesha ovyo..kwasababu anayekuletea mke/mume ni Mungu, si mwanadamu..wewe kaa katika kumtakafakari yeye maisha yako yote.
Kuoa utaoa, kuolewa utaolewa tu!..ukiishi maisha yanayopendeza Mungu si uongo utakutendea tu.
Daudi alisema..
Zaburi 37:25 [25]Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
Mungu hawezi kuacha kumpa mteule wake kitu kilicho chema, na kizuri.. Hawezi kuruhusu mke/mume pasua kichwa atokee mbele ya njia yake, mtu anayemcha yeye. Hilo haliwezekani..
Hivyo kama bado hujaokoka. Tubu leo anza maisha yako upya na Bwana Yesu kwa kumaanisha kabisa..Toba ya kweli inaambatana na kuucha ulimwenguni, mkatae shetani na kazi zake zote na vimini vyake vyote, na suruali zote na viduku vyote..kamtafakari Mungu huko makondeni, hata kama utaonekana mshamba..
Ishi maisha ya kumlingana Bwana..Na bila shaka wakati utafika atamtuma malaika wake kwenda kukuletea mwenzi sahihi..Kama Ibrahimu alivyomtuma kijakazi wake, kumletea Isaka Rebeka.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?
Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?
SWALI: Nini maana ya huu mstari,
Mithali 31:6 “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. 7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake”.
Mithali 31:6 “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake”.
Je tunaruhusiwa kunywa pombe, tunapokuwa katika shida?
JIBU: Kumbuka agano la kale lilikuwa ni agano la mwilini, hivyo walitafuta kila mbinu za mwilini ili kutatua matatizo ya mtu, kwamfano utaona ilikuwa ili kutatua tatizo la zinaa na migororo katika ndoa, waliruhusiwa kutoa talaka, au kuoa wake wengi. Lakini jambo kama hili haukuwa mpango wa Mungu tangu mwanzo.
Mathayo 19:7 “Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? 8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.
Mathayo 19:7 “Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.
Na ndio maana utaona, japokuwa waliruhusiwa kufanya hivyo, lakini bado tatizo la uzinzi halikutatuliwa lote, kwamfano Daudi alikuwa na wake wengi, pamoja na Masuria wengi, lakini bado hakuacha kwenda kutafuta wake za watu, na kuzini nao (Mke wa Uria). 2Samweli 11&12..Kwasababu kiu ya uzinzi haizimwi kwa kuoa wake wengi.
Vivyo hivyo, Na katika masuala ya kuondoa huzuni, au uchungu moyoni, walikuwa na desturi, kwamba mtu aliye katika hali hiyo, mfano kama kafiwa na watoto wake wote, au mke n.k. kama vile Ayubu Walikuwa wanawapa pombe, wanywe kwa kipindi hicho iwasahaulishe matatizo yao. Lakini hilo halikufanikiwa kwa wakati wote, kwasababu pombe ikiisha tu kichwani, huzuni yake inarudia tena pale pale..kwasababu kiu ya huzuni haiwezi kukatwa kwa pombe..Mungu aliruhusu tu iwe hivyo kwa muda, kwasababu ya mazingira waliyokuwa nayo kwa wakati ule, lakini halikuwa kusudi lake tangu mwanzo.
Na ndio maana sasa katika wakati wa agano jipya Mungu alileta suluhisho la moja kwa moja la mambo yote rohoni na suluhisho lenyewe ni ROHO MTAKATIFU.
Bwana Yesu alisema..
Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”
Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”
Roho Mtakatifu akishaingia ndani ya mtu, anafanya kazi ambayo pombe imeshindwa, madawa ya kulevya yameshindwa, anamwondolea mtu hofu yote, uchungu wote, tamaa yote, wasiwasi wote na mashaka yote, na kiu yote ya uovu milele. Na ndio maana mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu vizuri huwa anaonekana kama mlevi, mtu asiyejali ni nini anakipitia saa hiyo..Kama tunavyoona siku ile ya Pentekoste.
Matendo 2:15 “Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto”.
Matendo 2:15 “Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto”.
Hivyo, sisi hatuna ruhusu ya kunywa pombe, kwasababu ndani ya pombe, biblia inasema upo UZINZI, na matendo mabaya, lakini katika Roho Mtakatifu upo uhuru. Ukinywa pombe unatenda dhambi.
Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”
Kwahiyo mstari huo hauhalalishi ulevi, kama tu vile uoaji wa wake wengi usivyokuwa halali sasa, japokuwa uliruhusiwa katika agano la kale.
Tutambue ujumbe wa saa tunayoishi.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
JE! ULEVI NI DHAMBI?.
Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?
Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?
USIJITUMAINISHE JUU YA SIRA YAKO ANGALI UPO KATIKA DHAMBI.
Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)
SWALI:Tunasema Yesu karejesha kila kitu Adamu alichopoteza pale Edeni, Lakini kiuhalisia mbona hajarejesha kila kila kitu, mbona tunaona kifo bado kipo, mbona waovu ndio wanaotawala dunia, mbona magonjwa na ajali vinakithiri duniani?
JIBU: Ni kweli kabisa Bwana wetu Yesu Kristo, amekabidhiwa umiliki wa vitu vyote, Kuanzia juu mbinguni, mpaka huku duniani, vyote vipo chini yake. Na kazi kuu aliyokuja kuifanya ni kuvirejesha vyote vilivyoharibiwa na adui, katika nafasi yake, na hata Zaidi yah apo.
Mathayo 11: 27a Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu;..
Soma pia,
Waefeso 1:20 “…. akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote”.
Waefeso 1:20 “…. akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote”.
Basi kama ni hivyo, utauliza ni kwanini basi, hatuoni mamlaka yake yote yakitimia ulimwenguni?
Jambo ambalo watu wengi hawajui ni kuwa, Huduma ya Bwana wetu Yesu Kristo haijaishia pale tu alipopaa kwenda mbinguni..bali aliondoka kwa muda tu, akaahidi kurudi, Na ndio maana ujio wake,aliugawanya mara mbili, ambapo mara ya kwanza alikuja kwa lengo la kuokoa roho za watu na mauti, ndipo hapo akalazimika kufa msalabani, ili damu ipatikane kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Hivyo kipindi chote hicho hakuhangaika, na mambo yoyote ya mwilini, au ya kiutawala, au ya kijeografia japokuwa alikuwa amekabidhishwa vyote.
Lakini ujio wake wa pili, hautakuwa tena kama ule wa kwanza, wenye lengo la wokovu wa roho za watu..Hapana, bali atakuja mahususi kwa lengo la kuukomboa huu ulimwengu na mifumo yake yote mibovu, Hapo ndipo atakapokuja kama mtawala, yaani MFALME WA WAFALME na BWANA WA MABWANA. Katika ule utawala wa miaka 1000 (Ufunuo 19:16)
Sasa atakapokuja katika awamu hii,
1) jambo la kwanza atakalofanya ataleta Amani duniani. Kutimiza lile andiko kwamba siku ile Mbwa-mwitu atalala Pamoja na mwana-kondoo, mtoto anyonyaje atacheka kwenye tundu la nyoka. (Isaya 11:5-9, 65:25)
2) Pili atadhibiti uchungu; Watu hawatazaa t tena kwa uchungu (Isaya 65:23)
3) Tatu atabidhibiti, magonjwa na maajali: Hilo ndilo litakalowafanya watu waweze kuishi miaka mingi hata karibia na 1000. (Isaya 65:20). Biblia inasema kipindi hicho, mtu atayekufa na miaka mia ataitwa mtoto mchanga.
4) Nne atadhibiti uharibifu: Yaani Hutajenga, akakaa mwingine, wala hutapanda akala mwingine..(Isaya 65:22)
5) Tano atadhibiti dhambi: Kumbuka wakati huo shetani atakuwa amefungiwa, na mtu yeyote atakayeonyesha dalili za uvunjifu wa amani, fimbo ya chuma, itamlalia.(Ufunuo 12:5)
6) Na mwisho kabisa atamalizana na MAUTI, huyu ndiye adui wa mwisho.
Kiasi kwamba hakutakuwa na kifo tena ulimwenguni, wala machozi, wala maombolezo.
Hapo ndipo atakamporejeshea Baba mamlaka yote. Na kazi yake itakuwa imekwisha ya ukombozi. Na ndio hapo tutaingia katika ile mbingu mpya na nchi mpya, ambayo Jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.
1Wakorintho 15:24 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 ADUI WA MWISHO ATAKAYEBATILISHWA NI MAUTI”.
1Wakorintho 15:24 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
26 ADUI WA MWISHO ATAKAYEBATILISHWA NI MAUTI”.
Hivyo, kwa kipindi hichi tulichopewa hapa katikati, tangu siku alipopaa hadi sasa, ni kuhakikisha kila mmoja, anaupokeo huo ukombozi wa roho yake, kwa gharama yoyote ile. Na hiyo inakuja tu kwa kumwamini Yesu Kristo, na kumpokea Roho wake.
Lakini kama mtu atakutwa katika hali ya dhambi hadi siku anayorudi mara ya pili, ajue kuwa hakuna neema tena ya ukombozi juu yake kwasababu Kristo ameshabadili ofisi. Wakati huo, atawaangamiza waovu wote kwa kuwaua kwa pumzi yake (Ufunuo 19:21). Kisha kwenda kuwatupa katika ziwa la moto.
Hivyo, uovu unaouna leo hii duniani ni wa kitambo tu, vita unavyoviona, uchungu, magonjwa na vifo, vyote vina muda mfupi. Hivi karibu Bwana anarudi, kuja kutawala na sisi kwa muda wa miaka 1000. Ndani ya hichi kipindi kila kitu kitarejeshwa katika hali yake.
Na ndio maana huna sababu ya kukimbizana na huu ulimwengu mbovu, ambao tumezungukwa na hatari ya kila namna, ndugu jiwekee hazina mbinguni, kwenye huo ulimwengu ujao wa amani unaokuja.
Lakini kwa bahati mbaya si wote watapokea neema hii ya kutawala na Kristo. Ikiwa utakufa leo katika hali yako ya dhambi. Utabakia huko huko makaburini hadi siku ile ya ufufuo, kisha uhukumiwe na kutupwa motoni.
Je! Bado unaendelea katika dhambi zako? Bado unaichezea tu hii neema? Kisa Kristo ni mpole sasa kwako unadhani atakuvumilia hivyo katika hali yako ya dhambi milele ? Ndugu yangu. Bwana Yesu Kristo ni mkuu kuliko unavyoweza kufikiri, utalithibitisha hilo, siku ile atakaporudi mara ya pili. Ambapo biblia inasema kila kinywa kitakiri, na kila goti litapigwa. Na mataifa watamwombolezea.
Heri ukampa Yesu Kristo Maisha yako angali bado una muda mchache, hivi karibuni Parapanda italia, Na Kristo atabadili ofisi yake.
Maran Atha.
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Kwanini Mungu aliwaita Adamu na Hawa jina moja?
TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
SWALI; Naomba kuuliza katika ufunuo 21:27 kwamba hakitaingia kilicho kinyonge hili neno kinyonge linamaanisha nini? Je ni watu dhaifu mfano vilema?
Ufunuo wa Yohana 21:27 [27]Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
JIBU: “Kinyonge” kinachozungumziwa hapo si mtu mlemavu, kama ingekuwa hivyo Bwana Yesu asingesema..kiungo chako kimoja kikikukosea king’oe ni heri uingie mbinguni mlemavu kuliko kuwa viungo vyako vyote na kuishia kuzimu.(Mathayo 5:29-30)
Lakini kinyonge kinachozungumziwa hapo ni kipi?
Kitu kinyonge sikuzote ni kitu kisichokuwa na nguvu ya kustahimili mtikisiko fulani aidha mapigano,ugonjwa,Dhoruba, mateso n.k.
Vivyo hivyo katika roho mtu asiyekuwa na nguvu ya kuushinda ulimwengu huyo ni sawa na mnyonge. Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..
Mathayo 11:12[12]Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Utajiuliza ni kwanini Bwana arejee siku za Yohana mbatizaji, na sio siku za labda, Isaya, au Musa, au Samweli? Bali Yohana Mbatizaji?
Alisema hivyo, ili kutupa picha na sisi tunapaswa tuishi Maisha ya kuukana ulimwengu, mfano wa Yohana mbatizaji..Ambaye biblia inasema Maisha yake yote, aliishi majangwani mbali na ulimwengu, na matokeo yake akawa akiongezeka nguvu rohoni kila siku (Luka 1:80).
Hivyo na sisi tunapaswa tuushinde ulimwengu, ili tuweza kuuteka ufalme wa Mungu, ikiwa uzinzi utatushinda, ikiwa anasa na tamaa za ujanani zitatushinda, basi sisi ni wanyonge, na hivyo, kamwe hatutakaa tuuingie ule mji mpya wa Yerusalemu, utakaoshuka kutoka mbinguni. Kwasababu watakaoingia kule ni watakatifu tu walioushinda ulimwengu, na si vinginevyo.
Huu si wakati wa kuikumbatia dhambi..na kusema kwamba mimi siwezi kuushinda ulimwengu, ni wajibu wako kushindana mpaka ushinde…hupaswi kuwa mnyonge. Kumbuka wewe ukishindwa haimaanishi kuwa mwingine kashindwa.
Lakini tutawezaje kufikia hapo?
Tutafika kwa njia moja tu nayo ni kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi, na kujitwika misalaba yetu na kumfuata Yesu kwa gharama zozote zile.
Shalom.
MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.
KWANINI MIMI?
Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
Tofauti na desturi za mataifa mengi ya sasa zilivyo, kwamba mtu akitaka kuapa, huwa anashika kitabu Fulani cha dini kama vile biblia, au anaweka mkono wako kifuani ndipo anatamka kiapo chake..Zamani kulingana na desturi wa wayahudi ilikuwa ni mtu anaweka mkono wake, chini ya paja la anayemwapisha.
Pajani kibiblia ni sehemu ambayo ipo karibu sana na viungo vya uzazi.. Sehemu nyeti, ambapo hapawezi kufikiwa kama jambo lililopangwa halihitaji umakini sana. Ni sawa na leo watu wanavyotumia biblia mahakamani kuapa, ni kitabu nyeti sana, kiasi kwamba mpaka kimetumiwa hiko ni kuonyesha umakini wa kile unachotakiwa kukifanya.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa Ibrahimu, na Yakobo. Kwamfano Ibrahimu alipotaka mwanawe Isaka apatiwe mke kutoka katika nyumba ya Ndugu yake, aliyekuwa mbali sana, alimwita mtumwa wake, akamwapisha kwamba akamletee binti sawasawa na alivyomwagiza, Hivyo ili kuthibitisha kuwa mtumwa wake atayatekeleza yale aliyoagizwa, akachukua mkono wake, na kuulia katika paja lake, kuonyesha pia kwamba yupo tayari kutii kila agizo lililoamriwa juu yake.
Mwanzo 24:2 “Ibrahimu akamwambia mtumishi wake, mzee wa nyumba yake, aliyetawala vitu vyake vyote, Tafadhali uutie mkono wako chini ya paja langu, 3 nami nitakuapisha kwa Bwana, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;”… 9 Yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la Ibrahimu bwana wake, akamwapia katika neno hilo. 10 Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Mwanzo 24:2 “Ibrahimu akamwambia mtumishi wake, mzee wa nyumba yake, aliyetawala vitu vyake vyote, Tafadhali uutie mkono wako chini ya paja langu, 3 nami nitakuapisha kwa Bwana, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;”…
9 Yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la Ibrahimu bwana wake, akamwapia katika neno hilo. 10 Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Jambo kama hilo tunaliona pia kwa Yakobo, siku ile alipokaribia kufa, alimwita Yusufu na kumwambia, aweke mkono wake chini ya paja lake, ali amwapie, kwamba hatamzika kule Misri bali, katika nchi ya Baba yake.
Mwanzo 47:29 “Siku za kufa kwake Israeli zikakaribia; akamwita mwanawe Yusufu, akamwambia, Kama nimeona kibali machoni pako, weka mkono wako chini ya paja langu, ukanifanyie rehema na kweli; nakusihi usinizike katika Misri. 30 Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema. 31 Akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda”.
Mwanzo 47:29 “Siku za kufa kwake Israeli zikakaribia; akamwita mwanawe Yusufu, akamwambia, Kama nimeona kibali machoni pako, weka mkono wako chini ya paja langu, ukanifanyie rehema na kweli; nakusihi usinizike katika Misri.
30 Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema.
31 Akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda”.
Lakini sisi katika agano jipya, hatujapewa ruhusa ya kuapa bali Bwana Yesu alisema, maneno yetu yawe Ndio, ndio.. Au Sio,..sio..Na si zaidi. (Mathayo 5:33-37). Hakuna sababu ya kuapa, kwasababu hatuna mamlaka ya kutangua au kuthibitisha chochote katika maisha yetu kana kwamba vipo chini ya uwezo wetu.Sisi si Mungu.
Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?
Je Bwana Yesu alikuwa na mchoro (tattoo) katika paja lake? (Ufunuo 19:16).
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?
Kibiblia Kizazi ni kundi la watu linalozuka ghafla lenye tabia zinazofanana, linaweza kuzuka aidha kutokana na mabadiliko ya nyakati, au mabadiliko ya mazingira. Kwamfano, Wana wa Israeli walipokuwa Misri, chini ya Yusufu, waliishi kwa raha sana, Lakini Yusufu alipokufa pamoja na Yule Farao, kilinyanyuka kizazi kingine kisichokumbuka wema wa Yusufu, na hapo ndipo utumwa mgumu ulipoanza.
Vilevile, Wana wa Israeli walipofika katika nchi yao ya Ahadi, mwanzoni waliishi maisha ya kumcha Mungu sana, lakini wakati ulipopita mrefu kilinyanyuka kizazi kingine kisichomjali Yehova, hapo ndipo Israeli ilipoanza kuingia katika matatizo mengi sana.(Waamuzi 2:10)
Na katika hichi kipindi cha Siku za mwisho, tunapaswa tuwe makini sana, Zipo tabia ambazo utaziona kwa watu wengi sana, lakini kiuhalisia hazikuwepo huko nyuma. Hivyo ni vizuri ukafahamu aina ya vizazi vilivyopo duniani sasa hivi kulingana na biblia ili ujue wewe upo wapi na jinsi gani unapaswa ujiupeshe navyo.
Mathayo 12:39 “Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona”.
Ni kizazi cha watu kinachozuka kinapenda tu usherati na uzinzi kuliko kitu kingine chochote ulimwenguni. Leo hii tazama mawazo ya vijana wengi yalivyo, sikiliza mazungumzo yao, mambo wanayoyafanya kwa siri,vitu wanavyotazama mitandaoni, video za ngono, ni jambo la kawaida kwao, na kibaya zaidi sio tu vijana, hadi wazee na watoto wamo katika kundi hili. Jambo ambalo hapo zamani halikuwepo. Hiyo ni kuthibitisha kuwa ni hiki ni kizazi kingine kimezuka, ambacho ni hatari sana.
Marko 8:38 “Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika KIZAZI HIKI CHA UZINZI na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu”.
Ndugu, jiupeshe, na mkondo huu, si lazima uishe kama ulimwengu unavyotaka, kizazi hiki kimeshahukumiwa na Mungu.
Kipo kizazi cha Nyoka.
Mathayo 3:7 “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8 Basi zaeni matunda yapasayo toba; 9 wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto”. 10 Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Mathayo 3:7 “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
8 Basi zaeni matunda yapasayo toba;
9 wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto”.
10 Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Soma pia..Mathayo 12:34
Nyoka, alikuwa mwerevu sana kuliko wanyama wote mwituni, lakini alikubali kuwa chombo teule cha shetani. Uzao wake, ndio uliendelea mpaka kwa Kaini, na ndio maana watu wale walikuwa hodari sana , wagunduzi na wavumbuzi wakubwa, lakini waovu waliopindukia (Mwanzo 6:4). Ni watu ambao walikuwa hawana muda na Mungu, lakini kwa upande wa pili uzao wa Mungu, ulikuwa ni mnyenyekevu unaomtafuta Mungu usiku na mchana, vilevile na usio na masumbufu mengi ambao ulipitia kwa Sethi. (Mwanzo 4:26).
Inafunua hadi sasa, kwamba kizazi hiki kipo, Angalia dunia ya sasa, imestaarabika kuliko ile ya zamani, watu wanaelimu kubwa sana, wanagundua mambo makubwa sana, wamekwenda mpaka mwezini, lakini ukiwagusia habari za Mungu, wanakuambia hayo ni mawazo yako tu, hakuna Mungu,dini imetengenezwa na watu, wamejikita katika mambo ya mwilini, tu, elimu, utajiri, uvumbuzi basi, Mungu hayupo.
Ndugu, ikiwa na wewe upo katika jopo hili la watu, jiangue haraka sana, hichi ni kizazi, ambacho kipo ulimwenguni sasa.
Mithali 30:11 “Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao”.
Kuporomoka kwa maadili na nidhamu unakokuona leo, hakukuwepo huko nyuma. Leo utasikia mtoto anajibizana na mzazi wake, mwingine anampiga, mwingine anamzungumzia vibaya, wengine wametengeneza mpaka uadui na wazazi wao.. Kesi hizi ni nyingi sana sikuhizi..Wewe kama mtoto, wewe kama kijana, kuwa makini sana, kizazi hiki kimezuka ulimwenguni sasa. Unapoona, wenzako hawawaheshimu wazazi wao, na wewe usiwe mmojawapo.
Katika agano la kale mtu aliyejaribu kuonyesha utomvu wa nidhani kwa mzazi wake, sheria yake ilikuwa ni kifo. Jitathmini unawatii wazazi wako, Unawapenda?, unawabariki? Unawanenea mema? Unawaombea?.. Hata kama mzazi anakuudhi, huna ruhusu ya kurudisha baya kwa baya kwake. Vinginevyo upo chini ya laana ya kizazi hiki.
Mithali 30:12 “Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao”.
Hili kundi ni kubwa sana, Mtamuhubiria mtu na kumwambia pasipo kumwamini Kristo, huwezi kuokolewa, yeye atakuambia, mimi naamini matendo yangu ni safi, ninaamini Mungu hiyo inatosha, siwezi kuhukumiwa. Atakuwa radhi, kujihesabia haki, hata kama ni mzinzi, au mlevi..Haoni hatia yoyote kwa anayoyafanya. Yeye anachoamini ni kuwa Mungu hawezi kumchoma motoni milele,.Nimeshakutana na watu wa namna hii wengi sana. Wanaodhani kuwa kwa kile wanachokiamini, ndio tiketi ya Mungu kuwaokoa siku ile.
Ndugu kama upo katika hili kundi jiepushe nalo, Ikiwa bado hujaokoka, mkimbilie Yesu, yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kukusafisha dhambi zako, na sio kile unachokiamini.
Mithali 30:13 “Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana”.
Wapo watu ambao, kujishusha hakupo ndani yao. Wanajiona kuwa hakuna chochote kinachoweza kuwa msaada kwao, Mungu si kitu kwao, kwanini wakaombe, kwanini waende ibadani. Wapo radhi hata kuutukana wokovu, au kazi ya Mungu. Wanatumaini, mali zao, au ujuzi wao.
Kama tabia hizo zimeanza kuonekana ndani yako, geuka upesi.
Mithali 30:14 “Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu”.
Utu umeondoka duniani, Yupo radhi kufanya biashara haramu, bila kujali kinaleta madhara mangapi kwa jamii, anauza madawa ya kulevya, anauza bidhaa zilizoisha ubora, wanadhulumu haki za wajane na mayatima kwa faida zao wenyewe. Anaua, ili apate mali, n.k.
Tunayoyaona, hayakuwepo zamani, tusiwe watu wenye tamaa ya mali.
Lakini pamoja na kuwepo kwa vizazi hivi vyote, vya watu waovu.. Biblia inasema pia, kitakuwepo kizazi cha watu wenye adili, wanaomcha Mungu, wanaotenda mapenzi yake.
Zaburi 112:1 “Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake. 2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa”.
Zaburi 112:1 “Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.
2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa”.
Na ndio maana unaona pia wapo watakatifu wa Mungu leo duniani. Hawa ndio Bwana anaowatazama, na siku moja itafika Kristo atawahamisha kutoka katika huu ulimwengu kwa tukio la UNYAKUO na kuwapeleka mbinguni. Swali ni je wewe upo katika kizazi kipi?
Matendo 2:40 “Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.
Jibu unalo moyoni mwako.
Kumbuka Unyakuo upo karibu sana, dalili zote zimeshatimia, huna haja ya kuendelea kutangatanga na huu ulimwengu tena. Mgeukie Kristo akuokoe, ili uwe mmojawapo wa kizazi cha watu waadilifu.
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp yanayotumwa kila siku basi bofya hapa >>> WHATSAPP
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KWENDA?
FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.
Marago ni nini? ( Waamuzi 10:18)
Rushwa inapofushaje macho?