Luka 11:24 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, 25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka. 26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.
Luka 11:24 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.
Ukitafakari vifungu hivyo, utagundua tabia kadha wa kadha za mapepo;
Ni adui wa maji; Sasa ni lazima ujue sehemu isiyokuwa na maji ni ipi kiroho? Ni moyo mkavu, usiokuwa na chemchemi ibubujikayo maji ya uzima ndani yake, yaani Roho Mtakatifu..
Yohana 4:14 “walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele”.
Mtu yeyote asiyekuwa na Kristo ndani yake, tayari kwa namna moja au nyingine ndani yake kuna mapepo, kwasababu ni kukame. Kwa urefu wa habari hiyo , tutumie ujumbe inbox tukutumie somo lake;
Ndio maana ukisoma hapo anasema, likirudi na kukuta nyumba yake imefagiliwa, linakwenda kutafuta mengine saba yaliyo maovu kuliko yeye.
Jiulize linakwenda kutafutia wapi,? Hiyo ni kuonyesha kuwa yapo mahali fulani yanangojea kuitwa, na kwanini lisitafute limoja tu, bali saba? Ni kuonyesha kuwa yapo mengi, na kwanini lisitafute la saizi yake, bali yenye nguvu kuliko yeye. Ni kuonyesha kuwa na yenyewe huwa yanafanya uchaguzi, ni nani wa kukaa nao. Hiyo yote ni kujihakikishia ulinzi wake ili atakaporudi asibugudhiwe kwa lolote.
Kulithibitisha hilo, Soma ile habari ya Mariamu Magdalena, ambaye Bwana Yesu alimponya kwa kuyatoa mapepo saba ndani yake; Kuonyesha kuwa hapo kabla alikuwa ni mtu vuguvugu, yaani Mungu kidogo shetani kidogo, ndio maana yakamuingia yote yale kwa mpigo.
Marko 16:9 “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba”.
Kuwa makini sana, unaposhiriki ibada yoyote ya Ki-Mungu, na ilihali maisha yako ni ya kipepo (yaani ya dhambi). Unazini, unalewa, unakwenda kwa waganga, unafanya anasa n.k. na wakati huo huo unakwenda kanisani kushiriki meza ya Bwana au kumwabudu Mungu, na kutoa sadaka.
Watu wengi leo hii hawajijui kuwa wanajiongezea tu idadi kubwa ya mapepo, kwasababu ibada yoyote uifanyayo kwa Mungu ni adui wa mapepo, hivyo yanapoona hali fulani ya hatari katika nyumba zao imetokea, Ni lazima yajihakikishie ulinzi kwa kuyaalika mengine saba yenye nguvu kuliko yenyewe.
Ndio hapo hali yako ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ya mwanzo. Unakwenda kanisani, Neno limekuchoma, uache uasherati, badala uache mambo hayo, unatoka kuendeleza tabia hizo, ujue kuwa utakuwa mzinzi mbaya kuliko hata ulivyokuwa pale mwanzo.
Ni heri ukatubu dhambi zako leo, Na kumfuata Bwana Yesu kwa kumaanisha kweli kweli, ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu, biblia inasema hivyo, kwasababu shetani anajua kuwa muda wake ni mchache, hivyo anafanya kazi kwa bidii sana akishirikiana na mapepo yake, kuwaangusha watu.
Ndio maana siku hizi za mwisho hushangai kuona, maovu yamekithiri duniani, hata aibu tena hamna, hizo zote ni kazi za mapepo wachafu, ambazo zimewavaa na kuwaendesha.
Hata wewe au mimi, tukiwa ni watu vuguvugu, hatueleweki tupo upande upi, tujue kuwa tupo kwenye hatari kubwa sana ya kuwa na mapepo wengi. Hivyo kwa haya machache ikiwa unataka, Kristo aanze na wewe upya katika maisha yako, na ayafukuze haya mapepo moja kwa moja.
Basi fuatisha sala hii;
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Na kufukuza mapepo yote, yaliyokuwa yameweka mzizi ndani yako.
Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
NUNUA MAJI YA UZIMA.
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.
Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?
Rudi nyumbani
SWALI: Bwana alimaanisha nini katika mstari huu;
Amosi 6:5 “ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi”
Je! alimkosa Daudi, kwa namna alivyokuwa anamsifu?
JIBU: Jibu ni la! Mstari huo haumaanishi kuwa Mungu anachukizwa na watu wanaomsifu kwa ala, na vyombo vingi vya muziki, hapana, kinyume chake anasisitiza sana tufanye hivyo, tena hiyo pia ilikuwa ni sababu nyingine iliyomfanya Mungu ampende Daudi..
Daudi kwa uvuvio wa Roho aliandika maneno haya;
Zaburi 150:3 “Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; 4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; 5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”.
Zaburi 150:3 “Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”.
Umeona? Kuonyesha kuwa Mungu anapendezwa sana na kufisiwa kwa ala na midundo mbalimbali ya miziki.
Lakini sasa kwanini kwenye mstari huyo wa Amosi, anaonekana kama anawakemea watu wanaofanya hivyo?
Kumbuka hapo, anasema ninyi “mnaoimba nyimbo za upuzi”. Ikiwa na maana, wanachokiimba hakimtukuzi Mungu, kinamfano wa ki-Mungu lakini ni cha kidunia, na pia hawamuiimbi Mungu katika Roho na Kweli, yaani, matendo yao, yapo mbali na Mungu halafu wanajifanya wanamwimbia yeye katika ustadi wa ala mbalimbali..
Ndicho walichokifanya wana Israeli hicho kipindi, walikuwa wanafanya maasi mengi, lakini wanajifanya wanajua kumtukuza Mungu kwa nguvu kama Daudi..Matokeo yake, Mungu akawazira kwa sifa zao za kinafki, akawapa adhabu ya kuchukuliwa utumwani Babeli..
Ukisoma mistari ya mbele kidogo Bwana anasema;
Amosi 6:8 “Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema Bwana, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake. 9 Hata itakuwa, wakisalia wanaume kumi katika nyumba moja, watakufa”.
Amosi 6:8 “Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema Bwana, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.
9 Hata itakuwa, wakisalia wanaume kumi katika nyumba moja, watakufa”.
Umeona, mfano wa Kanisa la Kristo lililopo sasa.
Tuna vyombo vingi vya kisasa vya kumsifu Mungu, tuna magitaa, tuna maspika yenye nguvu, tuna mapiano, vinanda vya kisasa, matarumbeta n.k. jambo ambalo ni zuri kumsifu Mungu kwa namna hiyo. Lakini angalia kinachoimbwa sasa, na staili za uchezaji, ni ‘upuuzi’ sawasawa na maneno ya Bwana. Huwezi tofautisha nyimbo ya ki-Mungu na nyimbo za wasanii wa kidunia.
Na hata kama tutaimba maneno ya kumsifu Mungu, lakini angalia matendo yetu nyuma ya pazia, yapo mbali kabisa na wokovu na utakatifu.
Hivyo unabii huo unatuhusu sisi, tunapaswa tujirekebishe, ili Bwana asituzire kwa kutupa adhabu kama alivyowapa wana wa Israeli kwa kuwapeleka utumwani Babeli.
Biblia inasema tumwabudu Mungu katika uzuri wa utakatifu, Na Sio katika vinywa tu, na midundo, Ili tupokee baraka alizozikusudia katika kufanya hivyo.
1Nyakati 16:29 “Mpeni Bwana utukufu wa jina lake;…. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu”;
Shalom.
Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)
Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)
Zaburi maana yake nini, katika Biblia?
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
Maana inayojulikana ya Unafiki ni ile hali ya kutoa maneno, au kuonyesha hisia au vitendo kwa nje tu, ambavyo kiuhalisia ndani ya mtu huyo havipo.
Kwamfano mtu anaweza kuwa anakuchukia, lakini kwa nje akawa anaonyesha kama kukujali na kukuchekea. Huo ndio unafiki.
Pengine unaweza ukawa unafahamu aina hiyo moja ya unafiki, lakini Leo tutaona aina mbalimbali za unafiki ambazo zinazungumziwa kwenye biblia, na namna gani ya kuzikwepa, kwasababu moja ya dhambi ambazo zinamchukiza Mungu sana ni unafiki, na inawapeleka watu wengi kuzimu pasipo wao kujua.
Hilo Bwana Yesu aliliweka wazi kabisa akasema..
Luka 12:54 Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo. 55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo. 56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?
Luka 12:54 Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.
55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.
56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?
Ikiwa Geografia ipo kichwani, kanuni za fizikia umezitunza mpaka unafahamu ni kwanini jani linaanguka chini na haliendi juu, unajua ukiumwa unaweza kwenda kutumia mwarobaini ukapona..Lakini unashindwa kujua kwa Mungu yupo, au hizi ni siku za mwisho. Ukweli ni kwamba Mungu anakuona kama ni mnafiki, na mwisho ukifika hatahangaika kukupa neema ya kumtambua bali utaishia kupotea kwasababu anajua wewe unajiweza, lakini hutaki tu.
Bwana alisema;
Mathayo 7:3 “Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako”.
Mathayo 7:3 “Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako”.
Hali hii inakufanya, uwaone wengine wote ni wakosaji, au hawastahili, na matokeo yake Mungu anakuona na kukuhukumu vilevile kama unavyowahukumu wao, Soma habari ya Yule farisayo aliyejihesabia haki zaidi ya mtoza ushuri( Luka 18:9-14) utalithibitisha hilo. Hivyo, hatuna budi, kujiuhubiria kwanza sisi, ndio tuende na kwa wengine.
Alisema:
Mathayo 6:1 “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.
Mathayo 6:1 “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.
Mathayo 23:13 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.”
Hii inawahusu sana sana viongozi wa dini, kwamfano pengine wanajua ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa katika maji mengi, lakini hawawafundishi kondoo wao hilo, wanajua, hizi ni siku za mwisho na Yesu yupo mlangoni kurudi, kwamba watu waache dhambi wamgeukie Mungu, kinyume chake wanawahubiria mafanikio tu miaka yote, ili tu wapate fedha. Huo Bwana anauona kama ni unafiki, mbaya sana, na adhabu yake ni ziwa la moto.
Mathayo 23:27 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. 28 Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi”.
Mathayo 23:27 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.
28 Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi”.
Hili bado lipo kwa viongozi wa imani, unakuwa askofu au mchungaji, unavaa kanzu nyeupe, unaitwa baba, lakini unafumaniwa na skendo za uzinzi, unakunywa pombe kichini chini, unapenda mambo ya ulimwenguni. Kwa Bwana ni heri tujionyeshe kuwa sisi ni wakosaji, kuliko kujificha nyuma ya kivuli cha utakatifu ni hatari sana.
Soma Mathayo 24:45-51, utaona anazungumzia habari ya Yule mtumwa mwaminifu, ambaye alifanya vyote alivyoagizwa na Bwana wake bila udhuru, lakini mwingine, akajisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia akaanza kuwapiga wafanyakazi wake. Bwana Yesu anasema atakaporudi, atamweka fungu lake pamoja na wanafiki. Epuka udhuru na uvivu katika kumtumikia Mungu.
Mathayo 24:50 “bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mathayo 24:50 “bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Kwamfano kuhimiza sana utoaji wa sadaka, ambao kimsingi Bwana mwenyewe alisema tufanye hivyo, lakini pale inapokuwa imezidi kila ibada ni sadaka tu, sadaka tu, mpaka ya mchicha, na tunasahau mambo makuu kama Utakatifu, kumcha Mungu na upendo. Huo ni unafiki mkubwa kwa Bwana..
Mathayo 23:23 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. 24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”.
Mathayo 23:23 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”.
Bwana atusaidie tujiepusha na hizo aina saba (7) za unafiki, kwasababu zitatupelekea jehanamu ikiwa zipo ndani yetu.
Lakini swali ni Je! Tunazikwepaje? Jibu ni kwa kumaanisha kumfuata Yesu kwa mioyo yetu yetu. Kwa jinsi tunavyomkaribia yeye ndivyo anavyotukaribia na sisi, kutusaidia kuwa kama yeye. Hivyo tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kutoka katika moyo wako, kisha nenda kabatizwe ikiwa hukufanya hivyo, kumbuka ubatizo sahihi ni kwa jina la YESU KRISTO sawasawa (Matendo 2:38). Kisha Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu, ikiwa utapenda upate msaada huo wa wokovu, basi wasiliana nasi kwa namba zinazoonekana chini;
Bwana akubariki.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
MAMA UNALILIA NINI?
YESU ANA KIU NA WEWE.
NGAZI 7 AMBAZO MKRISTO NI LAZIMA AZIPANDE KUUFIKIA UKAMILIFU.
Upole ni kitendo cha kutokuonyesha madhara, kwa mtu au kiumbe kingine, huwa unaambatana na utulivu . Upole unakuwa na maana Zaidi pale ambapo unaouwezo wa kuleta madhara kwa kiumbe kingine lakini hutumii uwezo huo, kumdhuru, Kwamfano ni kitu gani kinachomtofautisha nyoka na ng’ombe.
Nyoka ni kiumbe kidogo, dhaifu, hakina miguu, wala mikono, tofauti na ng’ombe, ambaye ni mkubwa, mzito, na mwenye pembe kiasi kwamba ukiwekwa naye katika mapambano ni rahisi kuuliwa naye. Lakini kwanini wewe itakuwa ni rahisi kumkimbilia ng’ombe na sio nyoka?.
Ni kwasababu ng’ombe ni mpole, si rahisi kutumia uweza wake wa pembe, na nguvu zake kukudhuru . Lakini ukimkaribia tu nyoka muda huo huo, atakuuma na utakufa.
Vivyo hivyo na katika wanadamu. Wapo ambao ni wapole lakini wapo ambao si wapole.
Katika biblia ipo mifano ya watu wawili ambao walishuhudiwa kuwa ni wapole. Wa kwanza ni Bwana wetu Yesu Kristo. Na wa pili ni Musa.
YESU KRISTO:
Bwana Yesu mwenyewe alisema.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Alikuwa ni mpole mfano wa mwanakondoo. Na kwasababu ya upole huo, ilimpelekea mpaka Roho Mtakatifu kushuka juu yake kipekee sana kama HUWA (Njiwa). Kumbuka sikuzote njiwa hatui sehemu isiyo na utulivu, wala hawezi kutua juu ya mnyama mkali kama vile mbwa mwitu, Bali anatua juu ya mnyama mpole kama vile kondoo, na ndio maana Bwana Yesu alitambulika kama mwanakondoo wa Mungu.
Hatushangai ni kwanini Mungu alimtukuza namna ile, kwanini leo hii watu wote wanamkimbilia Kristo, ni kwasababu alikuwa mpole sana rohoni. Sio kwamba alikuwa mnyonge, hawezi kuangamiza, au kuharibu watu, kumbuka Anaitwa pia “Simba wa Yuda”, Tunajua tabia za simba sio upole. Lakini yeye alikuja katika upole.. Hiyo ndio sifa kuu ya mtu mpole.
MUSA:
Mtu mwingine tunamsoma katika biblia aliitwa Musa. Utajiuliza ni kitu gani cha kipekee alichokuwa nacho Musa, mpaka kikamfanya awe karibu sana na Mungu kwa namna ile?
Ni kwasababu ya Upole wake, Tunasoma;
Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”.
Musa aliwazidi watu wote waliokuwa duniani kwa upole. Na hiyo ikamfanya awe karibu sana na Mungu, kuliko wanadamu wote walioishi duniani wakati huo.
Hata sasa, kanuni ya Mungu ni hiyo hiyo, Tukitaka tumkaribie Bwana sana, hatuna budi kuwa Wapole.
Tunakuwaje wapole?
Kwanza ni Kwa kujishusha: Unapokubali kuonekana wewe ni dhaifu, ni hatua nzuri sana ya kuelekea upole, Lakini unapotaka kujiona wewe ni Hodari wa mambo yote, ni ngumu kuwa mpole. Usipokubali kuchungwa, , ujue kuwa utabikia kuwa mbuzi sikuzote na si mwanakondoo
Pili Kwa kuzizuia hasira zetu: Hatuna budi, kuwa watu wa kuvizuia sana vinywa vyetu. Hasira huwa ndio chimbuko la ugomvi na vita. Hivyo ukiweza kudhibiti hasira zako hata kama utaudhiwa kiasi gani, hujibu, basi upole taratibu utaanza kujengeka ndani yako.
Tatu Kwa kusoma Neno na kuomba: Hii ni tiba kubwa sana, ukitaka ujue hesabu soma kitabu cha hisabati, halikadhalika ukitaka uwe na upole, usikwepe biblia. Kwasababu hiyo ndio itakukumbusha, misingi ya kuwa mpole kama Kristo alivyokuwa. Vilevile kusali, kunaukaribisha uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako, na hatimaye utafikia kiwango hicho.
Bwana atusaidie sana.
Furaha ni nini?
TUMAINI NI NINI?
Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?
Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Bwana Yesu asifiwe..
Ulishawahi kujiuliza kulikuwa na umuhimu gani, biblia kueleza tafsiri ya jina la mwanafunzi huyu aliyeitwa Tabitha?. Ukishaona mahali Fulani tafsiri ya jina la mtu inatolewa basi ujue kuna jambo Mungu anataka tujifunze, kwa huyo.
Mfano wa mtu mwingine kama Tabitha alikuwa ni Petro, Ukisoma Yohana 1:42, Bwana Yesu anafunua tafsiri ya jina lake.
Yohana 1:42 “Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).”
Unaona, kulikuwa na sababu ya Bwana kueleza tafsiri ya lile jina kwamba ni Jiwe/mwamba , ikiwa na maana kuwa zipo tabia, ambazo alikuwa nazo, au atakuja kuzionyesha zinazomwakilisha JIWE KUU mwenyewe ambaye ni Yesu Kristo..
Jambo hilo utalithibitisha mbeleni kidogo, katika Ufunuo alioupata kutoka kwa Mungu, kuhusiana na Bwana wetu Yesu Kristo, tusome;
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.
Umeona akiwa anamaanisha kuwa juu ya mwamba(yaani Ufunuo alioupata kuhusiana na Yesu ni nani), ndio Bwana Yesu atalijengea kanisa lake hapo. Kwahiyo utaona kutolewa tafsiri ya jina lake tangu kule mwanzoni ni kwasababu ya matendo au funuo alizokuwa anazipata kuhusiana na Yesu Kristo, kama msingi wa Kanisa.
Sasa tukirudi kwa Tabitha naye, tafsiri ya jina lake linatolewa, kwamba ni PAA.
Paa, ni aina ya swala. Mwanzoni nilitafakari sana kwanini aitwe swala, asiitwe labda simba, au au kifaru, au dubu, majina yenye sifa, lakini badala yake anaitwa swala.
Je swala anatabia gani nzuri?
Swala ni mnyama ambaye ni mwepesi sana, miguu yake ipo haraka mno, na ni mwepesi wa kurudia juu, kiasi kwamba akikimbia, katika nyasi ndefu au uwanda tambarare, hata simba hawezi kumkamata, mnyama pekee pirini ambaye anaweza kumkimbiza swala (Paa). Ni duma tu peke yake, tena kumpata kwake ni kwa shida sana.
Hivyo hiyo inamfanya, awe salama muda mwingi, akiwa porini.
Katika biblia mashujaa wa Bwana vitani walifananishwa na Paa, Kwamfano mmoja wa mashujaa wakuu wa Daudi aliyeitwa Asaheli alisifika kuwa mwepesi wa miguu kama swala hawa..
2Samweli 2:18 “Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu”.
“Kulungu, Paa, na Ayala” ni jamii hiyo hiyo moja ya Swala.
Soma pia,
1Nyakati 12:8 “Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;
Soma tena;
2Samweli 22:34 “Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. 35 Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba”.
2Samweli 22:34 “Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35 Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba”.
Wimbo 8:14 “Ukimbie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya manukato”.
Sasa mpaka hapo utapata picha ni kwanini Tabitha, aliitwa Paa, ni kwasababu miguu yake ilikuwa ni mepesi katika kutenda matendo mema. Mpaka akasifika katika mji mzima wa Lida, jinsi gani alikuwa tayari kwenda kuwashonea mitume nguo, na kanzu, Pamoja na watakatifu wengine,bila kuombwa wala kuulizwa, Jinsi gani alivyokuwa mwepesi wa kumtolea Mungu. Bila kusukumwa sukumwa, au kukumbushwa kumbushwa, yeye mwenyewe kama swala, alikimbia kutekeleza majukumu yake ya kiutumishi, Zaidi ya watu wote waliokuwa katika ule mji wa Lida.
Hatimaye akafa, lakini watu walimwona kama hastahili kuondoka mapema, watu waliliona pengo lake lilivyo kubwa, hadi wakati ule Petro, alipokwenda katika mji huo, kulikuwa na maiti nyingi lakini hakuitwa kwa mojawapo ya maiti hizo bali ya Dorkasi tu;
Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. 39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi”.
38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.
39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi”.
Hii ni kutufundisha kuwa, ili Mungu awe naye mwepesi kama Swala kutuhudumia, basi na sisi tuonyeshe wepesi wetu kwake. Je sisi nasi ni wepesi wa kutenda matendo mema kama Tabitha? Je tu wepesi kutoa mali zetu na vitu vyetu kwa ajili ya utumishi wa Bwana? Au tu wabinafsi, au mpaka tukumbushwe, au mpaka tulazimishwe, au mpaka tuvutwe vutwe?
Wakati mwingine kwanini, majibu ya maombi yetu yanachelewa?, Ni kwasababu sisi wenyewe sio wepesi kwa Bwana, tunamfanya yeye naye awe mzito.
Tuifanya miguu yetu mepesi, ili wakati wa haja zetu Bwana naye awe mwepesi kutusaidia, kama alivyofanya kwa Dorkasi.
Habakuki 3:19 “YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka”.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
hMada Nyinginezo:
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?
Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?
MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.
USIPUNGUZE KUTUMBUIZA!
Ahimidiwe Bwana wetu Yesu Kristo, utukufu na heshima vina yeye milele na milele.Amen
Wakati fulani mfalme wa Israeli aliyeitwa Yehoashi alimfuata Elisha ili kumjulia hali kabla hajafa.
Kama tunavyosoma habari ile Elisha alimwambia achukue mshale kisha aurushe upande wa mashariki kupitia dirishani. Na alipofanya vile Elisha alimwambia huo ni mshale wa ushindi dhidi ya maadui zake washami..
Hivyo mfalme alipoona vile jinsi alivyopewa maagizo mepesi na yenye uhalisia wa ushindi kwa tendo la kutupa mishale, hakuwa na shaka yoyote kusikia pengine Elisha atampa maagizo mengine kama hayo, ya kurusha mishale mingine mingi Zaidi ili kuwapiga maadui zake walio karibu naye.
Lakini mambo yalikuwa ni kinyume na mtazamo wake kwani Elisha alimwagiza apige mishale yake ardhini badala ya kuirusha juu, kama alivyofanya hapo kwanza, tendo hilo likaweka ukakasi kwake “kutupa mishale ardhini”!? pengine alidhani ni mishale inayomrudia yeye.
Tusome..
2 Wafalme 13:14-19
[14]Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake! [15]Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale. [16]Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme. [17]Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza. [18]Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha. [19]Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.
[14]Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
[15]Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale.
[16]Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.
[17]Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.
[18]Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha.
[19]Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.
Umeona, hakujua kuwa ile ya kupiga chini ndio mishale ya ushindi, kinyume chake akawa na hofu matokeo yake akapiga michache tu (yaani mitatu)..
Ni jambo la kawaida hata leo, Mungu anawaagiza watakatifu wake warushe mishale mingi mahali ambapo ni kinyume na matarajio yao..lakini mashaka yanawaingia, wanaona kama wanafanyakazi bure, na kupoteza nguvu.
Ndugu yangu vita vya kiroho ukivitazama kwa jicho la mwilini ni rahisi sana kukata tamaa, kwasababu unaweza ukajiona kama unapoteza tu nguvu zako na muda..kama vile kupiga mishale chini..
Unapokuwa katika maombi, usitazamie kuona badiliko lolote la nje labda mbingu imekuwa ya blue, au usikie mapanga yakipigwa na malaika katika anga la kwanza hapana..zaidi sana utaona ni kama siku nyingine tu ya kawaida, umeomba bure, umeuchosha mwili bure. Lakini katika roho umeangusha ngome nyingi sana za ibilisi, tena na kwa jinsi unavyozidi kudumu zaidi na zaidi katika kuomba ndivyo unavyomfukuza shetani mbali nawe kabisa kabisa .
Hivyo hupaswi kukata tamaa au kuacha kuomba kwasababu hiyo mishale ya ardhini ndio yenye mapigo ya Mungu kuliko ile ya juu.
Unaposhea Neno la Mungu na wengine mtandaoni unaweza usione Matokeo yoyote ya kile unachokifanya, lakini wewe endelea Shea sana kwasababu hiyo ndio mishale ya ushindi unayoidharau wewe.
Unapohubiri mitaani au masokoni, unaweza ukaona kama unawapigia tu watu makelele, au watu hawakusikilizi, lakini hiyo ndio mishale ya ushindi katika vita vyako.
Njia za Mungu sio njia zetu. Wewe utarusha juu, yeye atataka urushe chini..huwezi kumpangia kanuni ya vita.
Hivyo tufanyapo jambo lolote la ki-Mungu tusipime-pime sana au kuchunguza-chunguza sana kwa jicho la nje, kwasababu ukifanya hivyo itakuwa ni rahisi kukata tamaa…bali tufanye kile alichotuagiza kwa bidii kana kwamba tunapoteza nguvu zetu bure, na matokeo yake tutakuja kuyaona baadaye katika ulimwengu wa roho.
Ongeza michale yako ya chini.
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?
Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?
WhatsApp
Kigao ni aina ya silaha inayofanana na ngao,
Inachokitofautisha kigao na ngao ni kwamba kigao ni kidogo na chepesi, rahisi kubebeka, na huwa kinafungwa mkononi, lakini ngao huwa ni kubwa na nzito kidogo.
Mara nyingi katika vita vikubwa vya zamani, askari walikuwa wanakwenda vitani na ngao kubwa kwasababu vita vile, vilikuwa ni vya wengi, na mishale, mingi ilirushwa kutoka kila mahali, hivyo palihitajika kifaa kikubwa kidogo cha kujilinda, hapo ndipo ngao ilibebwa.
Lakini katika hali ya kawaida si kila mahali askari walitembea na ngao kubwa, hivyo walibeba vigao vyepesi na umuhimu wake ulikuwa ni pale, walipojikuta katika vita vya mtu na mtu, vya kurushiana mapanga, hapo kigao kilikutumika, kupangua mapanga na sio ngao, kwasababu ngao ni nzito, mahususi kwa kuzuia mishale ya mbali, lakini kwa vita vya mtu na mtu ni ngumu, kidogo ilihitaji kifaa chepesi..Ndio hicho kilichojulikana kama kigao.
Tazama picha juu..
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia;
Zaburi 35:1 “Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. 2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie”.
Zaburi 35:1 “Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.
2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie”.
Zaburi 91:3 “Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. 4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. 5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana”,
Zaburi 91:3 “Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana”,
1Wafalme 10:17, 2Nyakati 9:16
Je! Kigao kinafunua nini kwa agano jipya?
Sisi kama watakatifu Bwana anatushauri, tuvae silaha zote za haki ili tuweze kuzipinga hila za shetani (Waefeso 6:11). Na moja ya silaha hizo zilizozungumziwa hapo ni Ngao., Ikimaanisha na kigao.
Ambayo biblia inasema, ndio IMANI. Hivyo Imani yetu inapaswa isimame katika vita vikubwa, na katika vita vidogo, katika mapambano makubwa na katika mapambano madogo, tushike NGAO NA KIGAO.
Yeremia 46:3 “Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana”.
Mara nyingi tunadhani shetani atatuangusha kwa mamilioni ya majeshi ya mapepo atakayotutumia.. Lakini, anaweza kutumia askari wake mmoja wa giza akatuondolea Imani yetu kwa Bwana kabisa, akaturudisha nyuma.
Hivyo ni kuwa makini, tuwe na Ngao Pamoja na vigao vyetu rohoni. Imani yetu ithibitike kotekote. Kwasababu Imani ni kitu cha msingi sana kukilinda. Na hiyo tumeambiwa tuishindanie kwasababu tumekabidhiwa tu MARA MOJA tukiipoteza basi kuipata tena ni ngumu..
Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.
Ndugu kama umeokoka, shikilia wokovu kwa nguvu zote, usirudishwe nyuma na mwanadamu mmoja au majeshi ya maadui. Simama imara na Bwana atakusaidia.
Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi
Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?
MJUMBE WA AGANO.
Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?
SWALI: Kulingana na Hesabu 9:11 Je! kuna sikukuu za pasaka mbili kwa mwaka?
Hesabu 9:11 “mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;”
JIBU: Mungu aliwaagiza wana wa Israeli kila tarehe kumi na nne (4) ya mwezi wao wa kwanza, itakuwa ni sikukuu ya pasaka kwao, ambayo wataila kama kumbukumbu la siku ambayo Mungu aliwatoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa.
Hivyo kila inapokaribia tarehe hiyo ya mwezi wa kwanza wayahudi wote walijitakasa na kukusanyika pamoja ili kuila pasaka hiyo..Na ilikuwa ni sheria na lazima.
Lakini tunaona hapo katika kitabu cha Hesabu kuna mwezi mwingine ambao ni wa pili, tarehe kama hiyo hiyo ya 14, wayahudi walikuwa wanakusanyika tena waile pasaka..
Swali ni Je kulikuwa na pasaka nyingine ya pili?
Jibu ni ndio Mungu aliruhusu iwepo pasaka nyingine ndogo.. Na ni kwanini aliruhusu, ni kwasababu kulikuwa na watu ambao kipindi cha sikukuu ya kwanza hawakuweza kufika kwa wakati kutokana na umbali wa safari…na wengine walikuwa wamenajisika kwa kushika maiti, ambayo iliwagharimu muda wa siku saba mpaka wawe safi(Hesabu 19:11)..Na sheria ilikuwa hauruhusiwi kwa namna yoyote kuingia katika kusanyiko lolote la watakatifu mpaka utakapokuwa safi kabisa.
Kwahiyo kulikuwa na kundi kubwa la watu ambao walishindwa kuila sikukuu hiyo ya pasaka kwa kwasababu hizo zilizoorodheshwa.
Hivyo kwa makundi kama haya ya watu, walipewa nafasi yao ya kipekee na Mungu ili kusudi kwamba sikukuu hii isiwapite kabisa katika mwaka huo.
Hesabu 9:10-12 [10]Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA; [11]mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; [12]wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.
Hesabu 9:10-12
[10]Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA;
[11]mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;
[12]wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.
Hiyo ndio sababu ya kuwepo kwa sikukuu nyingine ndogo ya pasaka..iliyofanyika mwezi mmoja baadaye.
Lakini Je hadi sasa tunayo maagizo kama haya ya kuzishika sikukuu za pasaka?
Katika agano jipya hatusheherekei tena sikukuu za pasaka kwa jinsi ya mwili, bali kwa jinsi ya Roho tukikumbuka kuwa pasaka wetu Yesu Kristo tayari alishachinjwa zamani..
Hivyo wakati wote tupo katika pasaka yake.
Lakini leo hii wengine wanaifananisha siku hii na siku ya Valentino (Valentine’s day)..yaana siku ya wapendanao duniani kama wanavyosema ambayo huwa inaadhimishwa kila tarehe 14 mwezi wa 2 duniani kote..Jambo ambalo halihusiani kabisa na Sikukuu hii ya Bwana.
Kwanza mwezi wa pili wa kiyahudi sio sawa na mwezi wetu wa pili wa kalenda ya Gregory..
Pili Upendo uliotangazwa na Valentino.Hauhusiani kabisa na Upendo uliotangazwa na Yehova Mungu wetu katika maandiko yake matakatifu.
Hivyo hatupaswi kuyalinganisha mambo ya kimbinguni na sherehe za kidunia. Sisi kama wakristo hatusheherekei Valentine’s day. Ni sikukuu ya kipagani. Tunaisheherekea pasaka ya Bwana kila siku katika Roho.
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
UNYAKUO.
Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu, utukufu na ukuu vina yeye milele na milele amina.
Huu ni mwendelezo wa mafundisho ya wana-ndoa.
Ustawi bora wa ndoa, hautegemei tu, mume au mke kutimiza wajibu wao wa mwilini,. Hiyo ni sehemu moja wapo, lakini pia ipo nyingine ambayo ni ya muhimu sana, na shetani pia anaifahamu, na kuipiga vita sana, na wewe kama mwanandoa, ukikosa jicho hilo la rohoni kulitambua, yapo mambo mengi sana mazuri utayakosa katika maisha yako ya ndoa.
Kama vile mafanikio ya mtoto yanavyochangiwa na kuwaheshimu na kuwasikiliza wazazi wake. Vivyo hivyo mafanikio bora ya ndoa yanategemea sana, utii na heshima, na kuwasikiliza wakwe zako. Leo tutaona kibiblia ni kwa namna gani hili jambo lilivyo na nguvu nyingi sana katika ustawi mzuri wa ndoa.
MAMA-MKWE.
Ikiwa wewe ni binti uliyeolewa, fahamu kuwa baraka zako za kimaisha, hazipo tena kwa mama yako mzazi, bali zipo kwa mama-mkwe wako.
Vilevile ikiwa wewe ni kijana uliyeoa, fahamu pia, ubora na ustawi mzuri wa boma lako, hautegemei tena, wazazi wako, bali Baba-mkwe wako.
Ni ngumu kupokea, na ndio hapa, vita vinapokuwepo, lakini ndivyo Mungu alivyopenda iwe.
Ukisoma kitabu cha Ruthu kinaeleza kwa marefu, jinsi mama-mkwe alivyokuwa msingi wa Ruthu kufanikiwa na kupendwa na Mungu, kiasi kwamba hadi leo hii, tunakisoma kitabu hiki, ni kwasababu ya siri aliyoitambua kwa mkwe wake Naomi, utasoma, wakati Ruthu amefiwa na mume wake, hakutaka kuachana na mkwe wake, na kwenda kuolewa tena kwao, lakini alienda naye mpaka nchi ya ugenini, akakubali kuwa kama kijakazi wake, akakubali kuwa kama bibi mjane, japokuwa alikuwa kijana, lakini hakuachana naye hata kwa nukta moja, wakati mke-mwenza Orpa karudi kwao kuolewa, tena yeye hakumwacha mkwe wake Naomi kama tunavyosoma Habari, Lakini mwisho wa siku tunajua ni nini alikutana nacho Ruthu..Badala ya unyonge, ikiwa furaha. Hadi kupewa neema ya uzao wa Bwana Yesu kupitia kwake, angali hakuwa hata mwanamke wa kiyahudi bali wa kimataifa.
Kwa maelezo marefu juu ya Habari hiyo fungua link hii, >> https://wingulamashahidi.org/2020/02/19/ewe-mke-heshima-yako-ipo-kwa-wakwe-zako/
Au nitumie msg inbox nikutumie somo lake kwa urefu..
Hiyo ni kuonyesha kuwa mwanamke yeyote uliyeolewa, hatua kubwa za mafanikio yako, ipo kwa mkwe-wako. Shusha kiburi chako, jinyenyekeze, utamwona Bwana, hata kama ni mbaya bado, lipo zuri utalipata tu kwake ambalo ndio litakuwa chanzo cha kupanda juu kwako.
BABA-MKWE
Lakini leo nataka tuone pia baraka zilizo kwa Baba-Mkwe. Na hii hasaa inamuhusu mwanamume. Kamwe usimdharau baba wa mke wako, hata kama atakuwa ni mnyomge kiasi gani, lipo zuri moja tu atakuwa nalo, ambalo huwezi kulipata mahali pengine popote isipokuwa kwake, ambalo litakufaa sana.
Embu mtafakari Musa, alikuwa ni mtu aliyezungumza na Mungu uso kwa uso, akitaka jambo lolote kutoka kwa Mungu alikwenda moja kwa moja kuzungumza naye, Mungu alimpa Musa idadi kubwa ya watu, ili awachunge, lakini katika kuwachunga kule, kulikuwa hakuna utaratibu maalumu, watu walikuwa wanaenda tu, hivyo hivyo,kwa foleni kama vile hospitalini, na wakati wote huo, Mungu hakuwahi kuzungumza na Musa juu ya jambo hilo.
Sio kwamba alikuwa halioni, alikuwa analiona, lakini ni utaratibu wa Mungu, si kila jambo atakuagiza ufanye au atazungumza na wewe moja kwa moja, haijalishi wewe ni nani.. Hata wakati wote Mungu alipokuwa anazungumza na wana wa Israeli, hata siku moja hakuwahi kuwaambia mbona mnaniweka katika mahema yenye giza aliwaacha tu hivyo hivyo,.Lakini utaona miaka mingi sana baadaye Daudi aliligundua hilo, akasema nitamjengea Mungu nyumba. Na Mungu alipoona Daudi kawaza vile akapendezwa naye sana akambariki.(2Samweli 7)
Ndivyo ilivyokuwa kwa Musa, Kusanyiko lote, hakuweza kulimudu, hakuweza kulichunga ipasavyo, lakini Mungu alikuwa anazungumza naye kila siku, lakini sio kwa Habari hizo. Ndipo siku moja Baba-mkwe wake (yaani baba wa mke wake), alipomtembelea kule jangwani, akaona jambo ambalo, Musa wala Israeli hawakuliona. Tusome;
Kutoka 18:14 “Mkwewe Musa alipoyaona yote aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata jioni? 15 Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu; 16 wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake. 17 Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema. 18 Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. 19 Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao; 20 nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya. 21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; 22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. 23 Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani. 24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. 25 Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi. 26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe. 27 Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe”.
Kutoka 18:14 “Mkwewe Musa alipoyaona yote aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata jioni?
15 Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu;
16 wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake.
17 Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema.
18 Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako.
19 Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;
20 nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya.
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;
22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.
23 Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.
24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia.
25 Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi.
26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe.
27 Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe”.
Umeona? Alichokifanya Musa, kilileta matokeo makubwa sana kwake na kwa wale aliowachunga. Hata sasa, wewe ni Baba, una familia ndogo au kubwa, usimdharau mkwe wako, kama yupo hai, kaa naye, msikilize kwa makini, hata kama atakuwa mjinga, usione shida kumwomba ushari wa kindoa, lipo moja litakusaidia kwa ustawi bora wa familia yako. Halikadhalika na mwanamke pia, shikamana na mama-mkwe wako.
Hizo ni kanuni za kiroho, zizingatie kwa afya ya maisha yako ya kindoa.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
MAFUNDISHO YA NDOA.
NDOA NI NINI?
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
Kibiblia Kitanga ni sehemu ya mwisho wa mkono wa Mtu, au mnyama..kwa jina lingine ni kiganja.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi.
Danieli 5:24-25 [24]Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. [25]Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.
Huu ni ule wakati mfalme Belshaza wa Babeli alipokuwa ameketi nankufanyia anasa vyombo vitakatifu vya Mungu pamoja na makahaba wake..ndipo hapo hapo kiganja cha mkono kikatokea na kuanza kuandika ukutani maneno hayo, mene mene tekeli na peresi.
Utalisoma Neno hilo pia katika vifungu hivi.
Mambo ya Walawi 14:26-27 [26]kisha kuhani atamimina sehemu ya hayo mafuta katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto; [27]kisha kuhani atanyunyiza baadhi ya hayo mafuta yaliyo katika mkono wake wa kushoto, kwa kidole chake cha mkono wa kuume mara saba mbele za BWANA;
Mambo ya Walawi 11:27 [27]Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.
Isaya 49:16 [16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.
Soma pia; ( 2Wafalme 9:35, Danieli 10:10,
Lakini Je nini tunaweza kujifunza kila tutazamapo kitanga/ vitanga vyetu.?
Ukiwa mwovu..kumbuka kuwa siku moja kitanga cha Mungu kitakuandikia hukumu kama kilivyomwandikia Belshaza mfalme wa Babeli..kama wewe ni mfanyaji wa anasa, ni mzinzi, ni mlevi, ni mchawi, unaabudu sanamu..Bwana atakuadhibu kwa hukumu mbaya sana. Ya mene, mene, tekeli na Peresi.
Ukifikia hii hatua basi habari yako inakuwa imeishia hapo hapo.
Lakini ikiwa wewe unampenda Mungu na kumcha yeye, na kuyafanya maagizo yake..Vilevile ameahidi atakuandika katika vitanga vyake…ikiwa na maana mtu akiandika jambo katika kiganja chake lengo lake ni ili asikusahau, si ndio?..Ndivyo ilivyo kwa Mungu, kwa watu wake wampendao..amewaandika katika viganja vyake kamwe hawezi kuwasahau.
Isaya 49:14-16 [14]Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. [15]Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. [16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.
Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)
Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”