AKETIYE MAHALI PA SIRI PAKE ALIYE JUU.

AKETIYE MAHALI PA SIRI PAKE ALIYE JUU.

Huu mstari una maana gani?

Zaburi 91:1 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi”.


Maandiko hayo yanatuonyesha kumbe Mungu anao uvuli wake.  Na uvuli huo hawakai watu wote  ilimradi tu,  bali wale tu wanaokaa katika mahali pake pa siri.

Sasa swali utajiuliza huko mahali pake pa siri  ni wapi?

Kuna madaraja ya kumfikia Mungu, yapo yanayofikiwa na wakristo wa kawaida tu, wale wanaomtafuta Mungu jumapili kwa jumapili, au mwezi kwa mwezi,  lakini pia yapo yanayofikiwa na wakristo waliojikana, na kudhamiria kumfuata Kristo katika Maisha yao.

Hao wanaojikana ndio wanaofikia mahali pa siri pa Mungu.

Wanafananisha na makuhani, ambao, katika ile hema ya kukutania, au hekalu la Mungu, ni wao tu walikuwa na uwezo wa kupaingia patakatifu, na kule patakatifu pa patakatifu, palipo na kile kiti cha rehema cha Mungu.Kumbuka si kila mwisraeli, alifika pale, si kila mtu anayejiona anamcha Mungu aliweza kufika pale, kwa mtu wa kawaida ukijitahidi sana, uliishia katika ule ua wa hema ya kukutanikia, lakini ndani, sehemu za siri za Mungu walioweza kuingia makuhani tu.

Vivyo hivyo katika agano jipya, Mungu anao sehemu yake ya siri, na ni watu baadhi tu wanaoweza kufika huko, Mfano hai katika biblia ni mwanamke kama ANA, yeye, aliweza kupafikia hapo..na ndio maana alikuwa miongoni mwa watu wachache sana waliofunuliwa mpango wa Mungu wa wokovu,yaani kuja kwake Yesu duniani..

Lakini hiyo yote ni kwasababu alikuwa ni mwanamke aliyeupoteza ubinti wake, autumie kwa Mungu hadi uzee wake, haundoki hekaluni, mchana na usiku akisali na kufunga.

Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.

37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.

38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”.

Mwingine, ni Simeoni, naye pia biblia inasema alikuwa ni mtu wa haki, na anaye mcha Mungu, tena Zaidi alikuwa anautazamia wokovu wa taifa lake Israeli, yaani wakati wayahudi wapo bize na mali na fedha, yeye alikuwa kama Danieli, akiomba na kutafuta Habari za kuja kwa masihi duniani.

Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako”,

Makundi ya watu kama hawa, huwa wanaonjeshwa kitu kingine tofauti na watu wa kawaida, huo ndio uvuli wake Mungu. Wanapewa mafunuo ya ndani sana, wanapewa ulinzi wa majeshi ya Malaika wengi,mfano Elisha, wanajaliwa haja za mioyo yao na Mungu. Kwasababu tayari wapo chini ya uvuli wake.

Je! Na sisi tunaweza kufikia mahali hapo?

Kama jibu ni ndio,

Basi hatuna budi, kufanana na makuhani wa Mungu kweli, wana wa Lawi, ambao wametengwa na dhambi na unajisi, Si tu kumkiri Kristo na kuendelea kuishi Maisha ya juu juu, bali tujikane na nafsi zetu pia kwake, yaani tuwe tayari kujitwika na misalaba yetu tumfate Kristo. Tukubali ulimwengu utupite na mambo yake yote.

Na kwa kufanya hivyo kwa neema zake, atatufikisha mahali pake pa siri.

Bwana atusaidie sote.

Amen.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?

Ni SIRI gani Paulo aliyokuwa anaimaanisha katika Waefeso 5:32?

Barazani pa Mungu ni wapi? Kama tunavyosoma katika Yeremia 23:18?

Bwana alimaanisha nini aliposema mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments