MWEZI WA ABIBU/NISANI NI MWEZI GANI?

MWEZI WA ABIBU/NISANI NI MWEZI GANI?

Mwezi wa Abibu ni upi?


Huu ni mwezi wa kwanza kwa kalenda ya Kiyahudi. Ambao kwa kalenda yetu hii ya ki-gregory unaangukia katikati ya mwezi Machi, na Aprili, kutegemeana na mwaka wenyewe jinsi ulivyokuja.

Upo mwaka ambao mwezi huu wa Abibu unaanza katikati ya  mwezi wa tatu, na upo mwaka, unaanza mwanzoni mwa mwezi wa nne.

Mwezi huu ni mwezi muhimu sana kwa wayahudi, kwasababu ndio mwezi wa kumbukizi yao ya kutoka katika nchi ya Misri(Nchi ya Utumwa).

Kutoka 13:4 “Ninyi mwatoka leo katika mwezi wa Abibu”.

Ndani ya mwezi huu, Siku ya 14 walikuwa wanasheherekea sikukuu iliyojulikana kama sikukuu ya pasaka, Na kuanzia tarehe 15-21, walisheherekea sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu.

Kumbukumbu 16:1 “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako.

2 Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake”.

Mwenzi wa Abibu ulijulikana kwa jina lingine kama  mwezi Nisani.

Esta 3:7 “Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari”.

Soma pia. Nehemia 2:1

Sasa wayahudi kila wanapoiungia huu mwezi wa Abibu/Nisani, huwa wanakumbuka siku ya kutolewa kwao utumwani..

Lakini swali linakuja kwako wewe mkristo, Siku yako ya Nisani ni ipi?

Abibu/Nisani yetu ni pale tunapookoka, siku tunapoamua kuacha dhambi na kumfuata Kristo, na kwenda kubatizwa, basi kuanzia siku hiyo nasi pia tunakuwa tumejumuishwa katika kalenda ya ki-Mungu. Hivyo rohoni tunaonekana kuwa tumeshauanza mwezi wa Abibu/Nisani.

Na faida yake ni kuwa, kuanzia huo wakati unakuwa unaanza kutembea  katika mpango wa Mungu wa kimbinguni, wewe unakuwa sio mwana-haramu tena, Mungu anaanza kutenda kazi zake ndani ya maisha yako, kipindi kwa  kipindi, Na hilo utalishuhudia mwenyewe, kwa jinsi siku zitakavyokuwa zinakwenda. Utaona tofauti yako ya mwezi uliopita na mwezi huu, utaona tofauti yako ya  mwaka ule uliookoka, na ile mingine iliyopita nyuma.

Lakini kama upo katika dhambi, wewe bado kalenda ya ki-Mungu haijaanza kuhesabiwa kwako. Na hivyo Mungu anakuwa hana mpango wowote na wewe, unakuwa ni kama mwana haramu tu. Shetani atajiamulia kufanya lolote atakalo katika maisha yako, atakuharibia maono yako, atafanya chochote ajisikiacho na mwisho wa siku utapotea na kwenda kuzimu. Na kuishia katika majuto ya milele

Lakini ukitubu dhambi zako, leo na ukawa tayari kuanza maisha mpya na Kristo, basi ni uhakika kuwa utaanza kutembea katika huo mpango wa Mungu. Hivyo bila kupoteza muda Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki,

pia fungua vichwa vingine  vya masomo chini, upate mafundisho mengine ya rohoni.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

Israeli ipo bara gani?

ESTA: Mlango wa 8, 9 & 10. (SIKU KUU YA PURIMU)

 MAVUNO NI MENGI

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments