Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo, Mfalme wetu, Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Utakumbuka huduma ya Bwana wetu iligawanyika katika sehemu kuu tatu,
Ya kwanza, ilikuwa ni hapa duniani,
Ya pili ni Kuzimu
Na ya tatu ni mbinguni.
Lakini wengi wetu tunafahamu ile ya duniani na mbinguni, Lakini kwa sehemu ndogo sana tunaielewa ile ya kuzimu. Ni vema pia tukaifahamu hiyo ili tujue ni nini tutakutana nacho baada ya kifo.
Siku tukiifahamu kwa mapana, hatutaacha kumshukuru Bwana Yesu kwa kifo chake pale msalabani.
Kama tunavyosoma siku ile Bwana aliyokufa, kuna matukio kadha wa kadha yaliyotokea, mojawapo ni lile la pazia la hekalu kupasuka, lakini tukio lingine ambalo lilitokea la kustaajabisha sana, ni lile la kuonekana kwa watu ulimwenguni ambao walikuwa tayari wameshakufa zamani. Na watu hao walikuwa ni watakatifu wa zamani.
Biblia inatuonyesha baada ya kufufuka kwao walianza kutembea tembea na kuingia mpaka mji mtakatifu wa Mungu (Yerusalemu.)
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.
Sasa swali unaweza kujiuliza ni kwanini uwe ni wakati ule na si mwingine, kwanini waonekane wanatoka makaburini, na kutembea tembea duniani, huku wakiwatokea watu? Kwanini iwe hivyo? Na hao watu sasahivi wapo wapi?
Hii ni kutuonyesha kuwa zamani mtu alipokufa, hakuwa huru hata kidogo, alikuwa anakwenda moja kwa moja kaburini haijalishi ni mtakatifu au mwovu. Huko kaburini ndio sasa kuliganyika katika sehemu ya waovu na wema.
Na kama tunavyojua sikuzote kaburi ni kama gereza, huwezi kwenda popote, au kufanya lolote, ndivyo ilivyokuwa kwa watu wote waliokuwa wanakufa zamani, walikuwa sehemu fulani tu, wamekaa wanasubiria siku moja masihi aje awaondoe huko. (Waebrania 2:14-15)
Lakini Bwana Yesu alipokuja, alifanya kazi ya kuyapasua makaburi hayo yaliyokuwa yamewashikilia kwa nguvu ya dhambi kwa muda mrefu . Lakini biblia inatuonyesha hakupasua makaburi ya wote, bali ya wale watakatifu tu. Na matokeo yake wakatoka huko, wakawa huru kama vile wanaishi tena duniani, na ndio maana wakawatokea wengi, wakatembea tembea huu na huko mpaka mji mtakatifu (Yerusalemu) n.k. kuonyesha ni jinsi gani wafu waliokufa katika Kristo walivyo huru, rohoni.
Hiyo ni kufunua kuwa, mtakatifu yeyote anayekufa leo, haendi tena kaburini kama watu wanavyodhani..ataliona tu kaburi kwa pale pembeni, lakini yeye hatakwenda huko kabisa bali ataondoka na kwenda kuendelea kuishi sehemu nyingine fulani iliyo nzuri sana, ijulikanayo kama Paradiso (peponi) Luka 23:43. Huko atakuwepo na Bwana Yesu mwenyewe, na watakatifu wengine, watakuwa ni kama tu vile hawajawahi kufa, wanaishi kama tunavyoishi hapa, isipokuwa tu huko ni kuzuri sana.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya,
Yohana 11:25b….Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Yapo maisha baada ya kufa kwa mtakatifu.. , hawi kifungoni, anakuwa huru kule PEPONI (Paradiso), akimfurahia Kristo, huku akingojea siku ya Unyakuo ifike, aje kuuchukua mwili wake, aende mbinguni.
Lakini mtu anayekufa katika dhambi, ni moja kwa moja kaburini, kifungoni, kwenye giza nene, ndio kuzimu kwenyewe, maisha yake yanagotea pale anapokufa, hayawezi kuendelea kuishi, sio kwamba roho yake itakufa, hapana, bali ni kwamba hawezi kuwa na maisha, kama sisi tuliyonayo, au wale wale wengine waliyonayo.
Biblia inasema hivi, juu ya Bwana Yesu alipokwenda kuzimu;
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
Unaona watu wote wenye dhambi sasa wapo huko vifungoni, kwa maelezo marefu juu ya habari hiyo, tutumie ujumbe inbox tukutumie somo lake..
Lakini utajisikiaje wewe uliye dhambini, ukifa leo katika hali hiyo? Siku hiyo utatamani upate hata nuru kidogo hutaona, utatamani, utembee tembee huku na huko kama wale wengine hutaweza, utatamani ule au unywe hutaweza, utakuwa katika jehanamu ya mateso daima, ukiteseka, kama Yule tajiri wa Lazaro, ambaye aliomba hata achovyewe maji kidogo kwenye ncha ya kidole cha Lazaro,akashindwa,(Luka 16:19-31) utakaa huku huku ukingojea na wewe siku ile ya hukumu ifike, ufufuliwe, uhukumiwe kisha utupwe kwenye lile ziwa la moto milele na milele.
Ndugu, kumbuka kifo hakina hodi, vilevile Unyakuo pia hauna hodi, ni siku yoyote au wakati wowote, unaondoka hapa duniani, au Yesu anarudi, inasikitisha kusoma katika biblia kwamba “kuzimu hakishibi watu”. Ikiwa na maana Maelfu kwa maelfu wa watu wanaenda huko kila siku.
Tutawezaje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii. Aliyeshinda kaburi na mauti kwa ajili yetu, yupo hata sasa kutuokoa, Embu tufungue mioyo yetu, atupe wokovu huu bure. Atusamehe makosa yetu yote. Hata siku tukifa tuwe na uhakika kuwa kaburi sio sehemu yetu.
Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha uwe tayari kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kuukamilisha wokovu wako, Na Bwana atakupokea.
Ikiwa utahitaji msaada wa kumpokea Yesu, basi unaweza kuwasiliana nasi pia kwa namba hizi. +255693036618 / +255789001312
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
UNYAKUO.
Rudi nyumbani
Print this post
Je! Bwana Yesu alikuwa kabila gani, miongoni mwa kabila 12 za Israeli?.
Jinsi biblia inavyotafsiri makabila ni tofauti na ulimwengu sasa unavyotafsiri.
Kibiblia Kabila ni jamii ya watu wanaotoka katika mzizi wa familia moja, maana yake asili ya kizazi chao ni baba mmoja.
Kwamfano katika biblia tunaona Taifa moja la Israeli likiwa na kabila 12.
Lakini makabila hayo yote, asili yao ni mtu mmoja anayeitwa Yakobo, ambaye ndio lake Israeli. Huyu Israeli alioa wake wanne na kuzaa watoto 12.. hivyo majina ya hao watoto 12, ndio yakawa makabila 12.
Hivyo mwisraeli yoyote, ni lazima awe miongoni mwa hayo makabila 12.
Sasa tukirudi kwenye swali, Bwana Yesu alikuwa kabila gani?.
Jibu ni kwamba Bwana Yesu hakuwa miongoni mwa kabila za Israeli, kwasababu yeye hakuzaliwa na Baba wa kimwili.
Mimba aliyoipata Mariamu, ilikuwa ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu (Luka 1:35).
Hivyo Bwana hakuwa miongoni mwa kabila la Israeli, bali alikuwa ni uzao wa kimbinguni.
Lakini sasa, Yusufu ambaye ndiye aliyemposa Mariamu..(ambaye ndiye kama baba aliyekuwa mlezi wa Bwana Yesu katika utoto).
ndiye aliyekuwa wa kabila la YUDA. Hivyo kupitia yeye, ili ahadi ya Mungu ya kumketisha mmoja katika kiti chake cha enzi itimie..ndipo akampitisha Mfalme Yesu, katika mnyororo huo wa kabila hilo la Daudi, yaani Yuda.
Lakini Bwana yenyewe hakuwa wa kabila la Yuda.Bali kwasababu ya Yusufu, ndio akaitwa wa kabila la Yuda.
Ufunuo wa Yohana 5:5 “Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba”.
Huyo ni Yesu, anayezungumziwa hapo?.
Swali ni je! Umemwamini na kumpokea maishani mwako?..kama bado unasubiri nini?..
Hakuna wokovu kwa mwingine yeyote, isipokuwa kwa Yesu, mwamini leo na kisha tubu dhambi zako zote kwake, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu, upate ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:38).
Na Roho Mtakatifu atayabadilisha maisha yako, na kukuongoza.
Maran atha!
Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda?
FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!
Je ni kweli Yuda hakuwa na dhambi kwa kumsaliti Bwana, kwasababu tayari ilikuwa imeshatabiriwa?
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?
Je Bwana Yesu alioa mke au kuwa na mahusiano na mwanamke yeyote?
Jibu: Bwana Yesu hakuoa wala kujihusisha na mahusano yoyote na mtu yeyote yule. Alizaliwa na kuishi bila kuoa ili ayatende mapenzi ya Baba yake. Na zaidi ya yote hakuwahi kutenda dhambi hata moja, ikiwamo ya kutamani.
Yohana 8:46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”
Ipo mitazamo inayosema kuwa Bwana Yesu alikuwa katika mahusiano na Mariamu, Magdalena.
Mitazamo hiyo imetengenezwa na adui, ili kuwapotosha watu, na kuwafanya watu wamwone Bwana Yesu kama alikuwa mtu wa kawaida tu kama watu wengine. Hiyo imekuwa ni kawaida ya shetani siku zote, kujaribu kushusha vitu vya kiMungu hadhi, ili visivutie.
Lakini haisadii kwasababu kuna Roho Mtakatifu, ndiye anayeishawiahi mioyo, na si ushawishi wa maneno..Hivyo iwe kwa husuda au kwa haki, Kristo atahubiriwa na ataaminiwa tu, hakuna kitakachoweza kuzuia hilo..
Wafilipi 1:18 “Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi”.
Watu waliokusudiwa kumwamini mwokozi, watamwamini tu, na wote watakaomwamini, shetani hawezi kuwanyakua kutoka mikononi mwake. Utukufu una yeye, Mkuu wa Uzima, Yesu Kristo, milele na milele.
washirikishe na wengine habari hizi njema,
Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?
Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?
WAOMBEENI WANAOWAUDHI.
Mbwa ni mnyama anayeweza kuwakilisha vitu vitatu:
1) Mlinzi
2) Adui
3)Kitu najisi/Mchafu.
Inategemea hiyo ndoto imekuja katika mazingira gani..na pia kama imekuja katika mazingira ya kujirudia rudia au katika hali ya uzito wa kitofauti basi haipaswi kupuuzwa, inayo maana rohoni.
Kama tunavyojua mbwa ni mlinzi. Na katika biblia watumishi wa Mungu pia wanafananishwa na mbwa walinzi.
Vilevile watumishi ambao hawasimami katika nafasi zao kikamilifu za kuwalinda kondoo wa Mungu wanafanishwa na mbwa walinzi wasioweza kubweka wala kung’ata.
Isaya 56:9-11
[9]Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni. [10]Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.[11]Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.
Kwahiyo unapoota..mbwa mara kwa mara..pengine amesimama getini tu..au anafukuza kitu au anafanya kitu fulani kwa ujasiri lakini hana shida na wewe.. hana mpango wa kukudhuru wewe..basi ni Mungu anakukumbusha kuwa uzidi kusisima vema katika nafasi yako kama mlinzi.
Lakini kama unaona mbwa huyo ni mwoga..anakimbizwa kimbizwa tu..anajificha ficha ujue huna nguvu rohoni..hivyo tengeneza mambo yako na Mungu ikiwa wewe ni mtumishi wa Mungu. Kwasababu Mungu anakuona kama mlinzi lakini bado hujakamilika katika kazi yako.
2) Maana ya pili ni kama Adui.
Kibiblia mbwa pia anawakilisha Adui. Zaburi 22:16
“[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu”.
Zaburi 22:20 “Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa”.
Ukiota unakimbizwa na mbwa..au unashambuliwa nao. Au wanakutisha.au wanakuvizia kuchukua kitu chako..Ujue kuwa upo katika vita rohoni. Ibilisi anataka kuiba kilicho chako.au kukuangamiza kabisa.. Hapo kama umeokoka huna budi kuwa mwombaji sana..mwambie Bwana akulinde na kukuhifadhli mbali na mashbulizi yote ya adui..pia zidisha kiwango chako cha kumtumikia Bwana ni ulinzi mkubwa sana.
Wafilipi 3:2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao. Lakini kama hujaokoka..fanya hima mapema sana umrudie Mungu wako. Vinginevyo upo hatarini kuangamia kabisa.
3) Maana ya tatu ni kitu najisi.
Kibiblia mbwa pia anawakilisha kitu najisi” au kichafu .Mbwa huwa hajali ni nini anakula anaweza rudia hata matapishi yake biblia inasema hivyo katika.. Mithali 26:11..
Ni wanyama wasiostahili heshima yoyote..
Mathayo 15:26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
Mbwa hajali ni yupi anakutana naye katika kupata watoto..anaweza kutanana hata na mama yake. Hivyo kwa ujumla ni kwamba mbwa anawakilisha pia watu waovu..waliodhambini ambao hawajali maisha yao ya kiroho hata kidogo.
Kwahiyo kama unaota mara kwa mara mbwa ambao huelewi wapo kwa lengo gani..leo unamwona hivi kesho vile…ujue kuwa ndivyo Mungu akuonavyo.
Tubu dhambi zako mgeukie Mungu wako kama wewe ni mwenye dhambi..kumbuka katika hali kama hiyo uliyopo sasa ukifa ujue ni moja kwa moja kuzimu..biblia inasema hivyo kwa watu walio hivyo rohoni..
Ufunuo 22:15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Ikiwa upo tayari leo kumkaribisha Kristo ndani ya maisha yako akubadilishe basi fungua hapa kwa ajili ya kupokea mwongozo wa sala ya Toba..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18
MTAWATUPIA MBWA NYAMA HIYO.
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
Je! Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?.
Jibu: Kulingana na maandiko mtu wa kwanza kufa alikuwa ni HABILI, mwana wa ADAMU.
Mwanzo 4:8 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua”.
Mwanzo 4:8 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani].
Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua”.
Sababu ya Kaini kumuua Habili ndugu yake ilikuwa ni wivu. Kwani sadaka yake haikukubaliwa na Mungu lakini ya ndugu yake Mungu aliikubali kwasababu aliitoa katika vitu vilivyonona..na kutoka kwa wazaliwa wa kwanza.
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde”.
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde”.
Roho ya Habili, ipo peponi sasa, yaani paradiso sehemu ya watakatifu..akingoja ufufuo wa watakatifu, utakaotokea katika siku za mwisho, wakati parapanda ya mwisho itakapolia.
Na pia tunajifunza tusiwe watu wasiomjali Bwana, kimatoleo kama Kaini, yeye alitoa tu ilimradi…lakini mwenzake alitoa katika vitu vilivyonona na katika wazao wa kwanza, pia tusiwe watu, wenye wivu kama Kaini.
SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.
MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
USIRUHUSU MUNGU AWEKE UADUI KATI YAKO NA WATU WAKO.
WhatsApp
Je! Ni kosa tu la kugeuza shingo na kutazama nyuma ndilo lililomgharimu mke wa Lutu maisha?.. Bila shaka Mungu asingeweza kumhukumu kwa kosa hilo, ni wazi kuwa kuna jambo lingine la ziada alilifanya..
Leo tutajifunza nini maana ya kugeuka nyuma, na mke wa Lutu aligeukaje nyuma hata ikamgharimu maisha yake..
Awali ya yote hebu tusome mstari ufuatao…
Luka 9:61 “Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. 62 Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, KISHA AKAANGALIA NYUMA, hafai kwa ufalme wa Mungu”.
Luka 9:61 “Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
62 Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, KISHA AKAANGALIA NYUMA, hafai kwa ufalme wa Mungu”.
Kwa mfano huo Bwana alitafsiri kuwa “kitendo cha kuamua kurudi nyuma baada ya kukusudia kumfuata yeye” ni sawa na “kutazama nyuma baada ya kudhamiria kwenda shambani”. Hivyo kutazama nyuma hapo, ni kumwacha Bwana Yesu kwa kitambo, kwenda kurekebisha mambo fulani kisha kumrudia.
Sasa mpaka kufikia hapo tutakuwa tumeshaanza kupata kuelewa nini maana ya mke wa Lutu kutazama nyuma.. Kwamba alimwacha Lutu na kurudi nyuma..
Lakini ili tulithibitishe hilo vizuri, hebu tusome tena maneno ya Bwana Yesu mahali pengine, ambapo aliieleza habari hiyo ya Mke wa Lutu vizuri zaidi..
Luka 17:28 “Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; 29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. 30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. 31 Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; NA KADHALIKA, ALIYE SHAMBANI ASIREJEE NYUMA. 32 MKUMBUKENI MKEWE LUTU”.
Luka 17:28 “Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
31 Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; NA KADHALIKA, ALIYE SHAMBANI ASIREJEE NYUMA.
32 MKUMBUKENI MKEWE LUTU”.
Hapo Bwana anaifananisha siku za kufunuliwa kwake na siku za Lutu, na anaelezea au anatoa ushauri jinsi ya kuokoka na ghadhabu ya Mungu kipindi itakapokaribia kumwagwa duniani kote, kama ilivyomwagwa katika miji ya Sodoma na Gomora.
Anasema siku hiyo “mtu aliye shambani asirejee nyuma”.. “maana akirudi huku atakutana na hatari itakayomgharimu maisha, hivyo abaki huko huko, au akimbie mbali zaidi”…na baada ya Bwana kusema maneno hayo anahitimisha kwa kusema “MKUMBUKENI MKEWE LUTU”.
Sasa jiulize kwanini aseme “Mkumbukeni mkewe Lutu”.. Maana yake kuna somo la kujifunza kutoka kwake, ili na sisi kipindi ghadhabu hiyo inakaribia kumwagwa duniani, tusiangamie kama yeye… Maana yake ni kwamba “mke wa Lutu alirejea nyuma”..aliangukia kwenye hilo kundi ambalo Bwana alisema, “aliye shambani asirejee nyuma”.. yeye alirejea nyuma na kukumbana na ghadhabu ya Mungu, ule moto na kiberiti na ile ardhi ya chumvi, ya Sodoma ambayo biblia inasema haiwezi kupandwa wala kumea, (Kumbukumbu 29:22-23), vikagandamana na mwili wake na kutengeneza umbile kama la mtu aliyesimama, kama nguzo, ambapo hata baada ya moto ule kuisha katika hiyo miji, na kila kitu kiteketea umbile lake lilibaki kama sanamu za kumbukumbu zinazotengenezwa na kuwekwa kwenye maingilio ya miji.
Hiyo yote ni kwasababu alirejea nyuma.. alianza kuitamani mikoba yake ya fedha aliyoiacha kule nyumbani.. Hakuwa na lengo la kurudi kuishi Sodoma, bali alivitamani vyombo vyake, mali zake, akazichukue na kisha aondoke nazo…ili huko aendako ziweze kumsaidia kuendesha maisha, lakini mambo yakabadilika, kabla ya kumaliza safari moto ulikuwa umeshamzunguka kila mahali.
Hiyo inatufundisha na sisi, tulioianza safari ya wokovu. Hii dunia tayari imeshatamkiwa hukumu, hakuna maombi yoyote yanayoweza kuifuta hukumu ya huu ulimwengu. Yaliyotamkwa na kuandikwa yatatimia kama yalivyo..
Hivyo kilichobaki kwetu ni sisi kuondoka na kujiokoa nafsi zetu, na katika safari yetu, hatupaswi kurejea nyuma..tunapaswa tukazane kuzidi kusonga mbele, kwasababu nyuma yetu, moto unazidi kusogea huku tuendako, hivyo tunakaza mwendo.
Kurejea nyuma ni kitendo cha kupiga hatua kabisa kuurudia ulimwengu.. ulikuwa umeshaushinda uzinzi lakini sasa umeurudia, ulikuwa umeshaishinda pombe na ulevi, na utukanaji, ulikuwa umeshaanza kumtumikia Mungu, lakini sasa umeacha, ulikuwa umeshaanza mambo yote ya ulimwengu, ikiwemo uvaaji mbaya, na kujipodoa..lakini sasa umerejea nyuma, umeanza kuyafanya hayo tena na ziaid ya hayo.. Bwana anakuambia.. “mkumbuke mkewe Lutu”..mkumbuke..mkumbuke..
Hakuna mtu mwingine yeyote Bwana aliyetuambia tumkumbuke katika biblia nzima… Ni huyu tu! Mke wa Lutu, ndiye aliyetuasa tumkumbuke…tusimsahau, maana yake tujifunze kwake.
Kama bado hujampokea Yesu maishani mwako mpokee leo, na kama tayari ulikuwa umeanza kurejea nyuma, basi ahirisha hiyo safari kabla hujafika mbali, kwasababu kuna wakati utatamani kumrudia Bwana lakini utashindwa, unyakuo wa kanisa upo karibu sana.
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
NI LIPI KATI YA MAKUNDI HAYA, WEWE UPO?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.
Kati ya yale makanisa 7 tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo, Kanisa la Thiatira, lilikuwa ni la tofauti sana, kwani lenyewe lilisifiwa sana na Bwana kwa jinsi lilivyokuwa linapanda viwango, siku baada ya siku, kiimani, kihuduma, pamoja na kiupendo, tofauti na makanisa mengine sita, hadi Bwana Yesu alilipongeza kwa kuliambia, matendo yake ya mwisho yamezidi yale ya kwanza..(Ufunuo 2:18-29)
Lakini pamoja na kuwa lilienda katika uaminifu huo, Shetani naye hakukaa nyuma. Bali alibuni njia ya kitofauti sana ya kuliangamiza, na njia yenyewe ndio hiyo ya kutumia MAFUMBO. Alibadili mbinu zake za kawaida, akawa anakuja tofauti na walivyotarajia. Na kwa njia hiyo alifanikiwa kulishusha kwa spidi kubwa kanisa lile, kwasababu baadhi yao walidhani kwamba wanaendelea vizuri na Mungu, kumbe wanamwabudu shetani moja kwa moja.
Leo kwa neema za Bwana tutajifunza baadhi ya FUMBO za shetani, wengi wetu hatuzijui ambazo anazitumia hata leo, na hizo zimewafanya watu wengi warudi nyuma, kama sio kuanguka kabisa kiroho.
Hizi ndio fumbo zake;
Wakati ule mtume Paulo anafika kwa mara ya kwanza, Mji huo wa THIATIRA, alikutana na kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo la utambuzi, na lilipomwona Paulo, lilimshuhudia Paulo ukweli, kwamba yeye ni mtumishi wa Mungu aliyejuu, na liliendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu tu, lengo lake likiwa ni kumpumbaza Paulo adhani ile ni roho ya Mungu ikimshuhudia, ili tu lisisumbuliwe kutenda kazi zake, Lakini mtume Paulo kwa kufunuliwa na Roho akatambua kuwa Yule sio Roho wa Mungu bali ni shetani, ndipo akalikemea likamtoka.
Mtendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. 17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. 18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. 19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;
Mtendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.
17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.
18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;
Hata leo, Shetani anawajia watu kwa namna hii, na wao bila kujua kumbe tayari wameshanaswa katika mitego yake. Ndugu si kila habari ya kweli inatoka kwa Mungu, Nabii kukueleza habari sahihi za maisha yako, hata ibilisi anaweza kufanya hivyo. Mpime kwa Neno la Mungu, na matunda anayoyatoa ndani yake. Hicho ndio kigezo. Usiridhishwe na maneno tu, ridhishwa na maisha nyuma ya hayo maneno.
2) Anataka tudhani kuwa hawezi kuwepo kanisani:
Hili hili kanisa la Thiatira, lilidhani hivyo, Mpaka Bwana Yesu alipolifumbua macho na kuliambia kuna mwanamke Yezebeli katikati yao, (Ambaye anawakilisha watumishi wa uongo waletao mafundisho mageni ndani ya kanisa), Anawafundisha njia potofu.
Ufunuo 2:18 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. 20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. 21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. 22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasio na mafundisho hayo, WASIOZIJUA FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine”.
Ufunuo 2:18 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasio na mafundisho hayo, WASIOZIJUA FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine”.
Hata leo, wapo watu wa Mungu wazuri, wanabidii kweli katika kumtafuta Mungu, lakini hawajui kuwa viongozi wao wanawakosesha kwa Mungu pasipo wao kujua, kwamfano, wambiwapo bikira Maria anaweza kuwa mpatanishi wako na Mungu, hayo ni machukizo, ufundishwapo mafundisho ya kutumia mafuta ya upako, chumvi, sabuni n.k. kana kwamba hivyo vitu vinatosha kumponya mtu, hizo ni ibada za sanamu. Lakini kwasababu unamwamini kiongozi wako kwamba hawezi kukosea, unamtii, ukidhani Mungu atakuridhia na wewe. Kuwa makini na kila fundisho geni unaloletewa na kiongozi wako.
3) Tudhani kuwa sikuzote anatisha na mwenye mapembe:
Wengi ukiwaambia shetani yupoje moja kwa moja, wanachowaza katika akili yao ni kitu cha kutisha chenye mapembe, na kichwa cha nyoka. Ni kweli hivyo vitu vinamwakilisha yeye. Lakini yeye hayupo hivyo, kumbuka, alikuwa ni malaika kama malaika wengine, na alipofukuzwa hakuondolewa chochote alichokuwa nacho, hata nguvu zake, bali alifukuzwa tu kwenye makao yake mbinguni.
Kwahiyo sasa alipo bado anatumia njia yake ya uzuri kuwadanganya watu wengi. Hii imewafanya watu wadhani shetani yupo katika vitu vichafu chafu, au vibaya baya, na shida na umaskini, vichaa, na wagonjwa.. Lakini Siku ile alimpofuata Bwana Yesu ili kumjaribu alikuja kama tajiri, mwenye milki zote za ulimwengu. Biblia inasema anaweza kujibadilisha kuwa malaika wa Nuru,
Kwahiyo usitazamie kuwa wakati wote atakufuata tu katika ndoto mbaya usiku au katika uchawi, au katika magonjwa. Wakati mwingine atakuja na amani feki, na utulivu, na utajiri. Ukadhani ni Mungu huyo kumbe ni shetani, anakutega ili kukuangamiza. Usikurupukie kila mafanikio mazuri, au fursa iliyopo mbele yako.
4) Tudhani kuwa hawezi kuzitetea njia za Mungu.
Tunaweza kudhani shetani hawezi, kujifanya anaisapoti kazi ya Mungu, au kuitetea, unafki huo anao. Wakati ule Bwana Yesu alipowaambia wanafunzi wake kuhusiana na mateso yake, utaona wakati huo huo shetani akamwingia Petro kujifanya, yeye ni mtetezi wa Bwana..
Mathayo 16:22 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.
Mathayo 16:22 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.
23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.
Ni kawaida yake, hata wakati akina Zerubabeli wanajenga hekalu la Bwana, maadui zao walijitokeza kwa kivuli cha kuwa wanataka kuwasaidia ujenzi, lakini walipofukuzwa ndio hapo wakaonyesha makucha yao, wao ni akina nani.(Ezra 4)
Shetani akishaona una kitu ndani yako cha ki-Mungu atakuja kwa njia ya msaada au utetezi, kuwa makini sana, na misaada unayoipokea katika utumishi wako au unachokifanya. Hakikisha unaifahamu na unaelewa kwa undani nyuma yake kuna roho gani. Vinginevyo utaingia katika matatizo makubwa sana.
5) Tudhani kuwa hawezi kukubali kushindwa.
Si kila wakati ibilisi atakuja kama mpingamizi, au mharibifu, hapana, lengo lake litakuwa ni hilo ndio, lakini atakuja kwa ujanja wa kujionyesha ameshindwa wewe una nguvu nyingi, atajiweka chini yako, ajifanye kuwa yeye siku zote ni mnyonge tu.. lakini kumbe ameshakuweza. Ndicho kilichomtokea Yoshua alipovuka Jordani, sababu mojawapo ya yeye kushindwa kuwaondoa wenyeji wote wa Kaanani ilikuwa ni hiyo, ya kumsikiliza shetani unyonge wake . Pale walipojifanya, wametokea nchi ya mbali, wanaomba sharti ya amani wasidhuriwe, kwasababu wamesikia ushujaa wao, kumbe ni watu wa karibu tu (Yoshua 9)
Leo hii mapepo yanaweza kukusifia sana, kujishusha, kusema wewe ni mkuu, unatisha,una upako, una nguvu, yakajifanya yanatetemeka mbele zako, ili tu uchukulie mambo rahisi rahisi, lakini kumbe tayari yanatenda kazi kwa nguvu ndani yenu bila kujua.. Usikisikilize kilio cha shetani. Ni mwongo.
6) Tudhani kuwa hajui mambo mengi.
Shetani anayotabia ya kujifanya mjinga, hajui kila kitu. Pale Edeni alimfuata mwanamke na kuanza kumwambia Ati, hivi ndivyo Mungu alivyosema, msile “matunda ya miti yote”?. Anajifanya kama hajui, ni matunda gani yaliyokatazwa, na ndio maana anasema “miti yote”. Anakusubiria utiririke, ndipo akunasie mahali fulani.
Hila hii anayo hata sasa, huyo kijana anakuja anajifanya hajui uzinzi ni nini..anataka taarifa kwako, umwambie kwa muhtasari, ndipo hapo akupeleke mpaka kwenye vilindi vya dhambi. Kila jambo baya, kabla ya kukuingiza, atataka wewe ndio umfundishe kwanza.
Kwahiyo hiki ni kipindi cha kuishi kwa umakini, tuzijue FUMBO ZA IBILISI. Ili asifanikiwe kutunasa popote pale. Tuzitambue fikra zake, tumpinge.
Swali ni je! Umeokoka? Je! Unaouhakika kuwa Kristo akirudi leo hii, utakwenda naye mbinguni? Kumbuka hizi ni siku za mwisho kweli kweli, siku yoyote unyakuo utapita, na ibilisi analijua hilo, na ndio maana anafanya kazi kwa nguvu nyingi sana kutafuta watu wa kuwameza.
Hivyo tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kumfuata Yesu. Ili akuweke huru.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza
Ni nani aliyemshawishi Daudi akawahesabu Israeli? Ni Mungu au shetani?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe.
Je unajua ni kwanini Bwana Yesu aliwaagiza Mitume wake pamoja na sisi wote kwamba tuende ulimwenguni kote tukawafanye watu wote kuwa WANAFUNZI na si WAKRISTO? (Mathayo 28:19).
Je! Unajua neno Ukristo mara ya kwanza lilizaliwa wapi?
Tusome Matendo 11:26..
Matendo 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na WANAFUNZI waliitwa WAKRISTO kwanza hapo Antiokia”.
Umeona hapo?..Maana yake kabla akina Petro, akina Yohana, na wengine wote waliomwamini Yesu kujulikana kama wakristo, walikuwa wanajulikana kama wanafunzi, hapo kabla.
Maana yake kuwa mkristo ni kuwa MWANAFUNZI WA YESU. Hili ni jambo la muhimu kujua sana.
Sasa swali tunakuwaje wanafunzi wa Bwana Yesu?..au watu wa kanisa la kwanza walikuwa wanafanyikaje kuwa wanafunzi?.
Bwana Yesu alitoa vigezo..Katika kitabu cha Luka..
Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”
Sasa tukirudi katika Matendo biblia inasema “Wanafunzi waliitwa wakisto kwa mara ya kwanza hapo Antiokia”..Maana yake mkristo yeyote ni mwanafunzi.
Kwa mantiki hiyo basi sentensi ya Bwana aliyoisema katika Luka 14:27 ni sahihi kabisa kuiweka hivi…
“Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa MKRISTO”.
Umeona hapo?..Hebu tosegee tena mbele kidogo..
Luka 14:26 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, 26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Luka 14:26 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Maana ya hiyo sentensi ni kwamba..
26 “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, HAWEZI KUWA MKRISTO”.
Kuchukia wazazi kunakozungumziwa hapo kuwachukia kwa chuki, bali kuchukia mawazo yao au mipango yao inayokinzana na mapenzi ya Mungu, kwamfano mzazi au ndugu anakuambia inakupasa urithi mikoba ya uchawi, au urithi chuki zake kwa mtu fulani, hapo Bwana anasema hatuna budi kuyachukia hayo mawazo na kuyakataa na kutoshirikiana nao hata kama watakutenga..hapo ni sawa na umewachukia ndugu zako, Kristo anakokuzungumzia..na ndio vigezo vya kuwa mwanafunzi yaani MKRISTO.
Tusogee tena mbele kidogo..
Bwana anasema..
Luka 14:33 “Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Kufuatia Matendo 11:26 inayosema kuwa Wanafunzi ndio wakristo..basi ni sahihi kabisa kuyaweka haya maneno ya Bwana katika hii Luka 14:33 hivi…
“Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, HAWEZI KUWA MKRISTO”.
Hiyo ikifunua kuwa kumbe miongoni mwa lile kundi lote lililokuwa linamfuata Bwana, wakristo walikuwa ni wachache sana..yaani ni wale wanafunzi wake tu, wa kike na wakiume, ambao walijikana nafsi na kujitwika misalaba yao na kumfuata Bwana Wengine wote hawakuwa wakristo.
Na maandiko yanasema Yesu ni yeye yule, jana na leo na hata milele. (Waebrania 13:8).
Ikiwa na maana kuwa kama vigezo vyake vya mtu kuwa mwanafunzi (yaani mkristo) vilikuwa ni kujikana nafsi na kubeba msalaba…basi vitakuwa ndio hivuo hivyo hata leo, kwasababu yeye ni yule yule habadiliki..
Waebrania 13:8 “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele”.
Je! Wewe ni MKRISTO?…Umejikana nafsi? Umeuchukia ulimwengu na kuuacha?..kama bado basi fahamu kuwa wewe si mkristo, haijalishi unasali katika dhehebu kubwa au umebatizwa, bado sio mkristo.
Kama bado unalewa, au unazini, au unavaa nguo za kubana na kuonyesha maungo yako, bado sio mkristo..
Amua leo kujikana nafsi na kuubeba msalaba wako, wacha dunia ikuone umechanganyikiwa lakini wewe unajua unayafanya mapenzi ya Baba yako aliye mbinguni..
Bwana Yesu alisema..“Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? ( Marko 8:36 ).
Itakufaidia nini uonekane wa kisasa halafu huendi mbinguni??
Bwana atupe macho ya kuona.
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?
Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?
Kibiriti tofauti na kinavyojulikana leo kwamba, ni kipande kidogo cha boksi kilichojaa chiti zinazotumika katika kuwashia moto. Lakini tafsiri halisi ya “kibiriti” au “kiberiti” sio hiyo. Kibiriti ni aina ya mawe, yanayopatikana duniani, yajulikanayo kwa jina hilo la kibiriti au Salfa..Kwa lugha ya kiingereza ni “Sulfur”.
Mawe haya kwa mwonekano yana rangi ya “manjano iliyofifia”..Tabia ya mawe haya ni kwamba yanawaka “kiwepesi” kama vile mafuta ya taa yanavyowaka kiwepesi yanapokutana na moto.. kadhalika na mawe haya ni myepesi kuwaka yanapokutana na moto.
Katika hali yake ya asili yanapokutana na moto kidogo tu! Yanaanza kuyeyuka taratibu taratibu na mwisho kuwa Uji mzito mweusi, kama tope!..ambao ni wa moto sana, usiozimika kirahisi, mfano wa Magma ya volkano. Lakini pia jiwe hilo hilo, likipelekwa kiwandani linaweza kuchanganywa na malighafi nyingine kutengeneza bidhaa nyingine zinazowaka kirahisi kama “Njiti za kiberiti” au “Unga wa risasi”. Lakini katika hali yake ya asili jiwe hilo la Salfa(kiberiti) likichomwa bila kuchanganywa na kitu kingine chochote, linayeyuka na kuwa tope zito la moto.
Lakini tukirudi kwenye biblia tunana sehemu kadhaa jiwe hili la Salfa(kiberiti) likitajwa.
Sehemu ya kwanza lilitajwa kipindi cha Sodoma na Gomora, wakati Bwana alipoiangamiza miji ile kwa moto. Biblia inasema moto na kibiriti vilishuka kutoka mbinguni.
Luka 17:28 “Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; 29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma KULINYESHA MOTO NA KIBIRITI kutoka mbinguni vikawaangamiza wote”.
29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma KULINYESHA MOTO NA KIBIRITI kutoka mbinguni vikawaangamiza wote”.
Kiberiti kinachozungumziwa hapo ni hayo mawe ya Salfa yaliyochanganyikana na moto, ambayo yalishuka kutoka juu..Na yaliposhuka moja kwa moja yakaanza kuyeyuka na kuwa TOPE ZITO JEUSI kama la volcano na kuchoma kila kitu.
Mpaka hapo utakuwa umeshaanza kuelewa kwanini Jehanamu ya moto, sehemu nyingine inafahamika kama ZIWA LA MOTO. Kwasababu huwezi kutaja neno ziwa bila kumaanisha “kimiminika” hivyo ziwa la moto maana yake ni “ni moto mwingi ulio katika mfumo wa kimiminika” mfano wa huo moto wa KIBIRITI (Salfa).
Ufunuo 21:7 “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Ufunuo 21:7 “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Utasoma tena neno hilo katika..
Ufunuo 14:9 “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; NAYE ATATESWA KWA MOTO NA KIBERITI mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
Ufunuo 14:9 “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; NAYE ATATESWA KWA MOTO NA KIBERITI mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
Na pia Ufunuo 19:30 inazungumzia jambo hilo hilo…
Ufunuo 19:20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ZIWA LA MOTO LIWAKALO KWA KIBERITI;
Na mwisho neno hilo limetajwa katika…
Ufunuo 20:10 “Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, AKATUPWA KATIKA ZIWA LA MOTO NA KIBERITI, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele”.
Sasa kwanini biblia imesema shetani na malaika zake WATATESWA katika Moto na Kiberiti, na SI WATACHOMWA TU!!.
Ni kwasababu Moto wa kiberiti ni tofauti na moto wa kawaida, moto wa kawaida wenyewe unaunguza tu! Na kuteketeza, lakini moto ulio katika mfumo wa kimiminika, tena kama uji uji huo ni unatesa.. Ndio maana kuungua kwa moto wa kawaida ni heri kuliko kuungua kwa vimiminika kama maji au uji..
Wanaofanya kazi za kuyeyusha Salfa(kibiriti) wanakuwa katika uangalifu mkubwa sana kwasababu wanasema moto ule ni mbaya kuliko moto mwingine wowote kwasababu “ule uji wake unapogusa mwili unakuwa unagandamana na ngozi” kwahiyo ili kuuondoa ni lazima ngozi ichubuke, na unakuwa na maumivu makali sana yanayotesa. Ndicho kilichowatokea watu wa Sodoma na Gomora, (walikufa kwa mateso na si kwa kuchomeka tu basi!.)
Na ndicho kitakachowakuta watu wote watakaotupwa katika lile ziwa la Moto.. watateswa katika ziwa la moto.
Swali ni je!, umempokea Yesu?.. Maandiko yanasema.. “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI.”
Je na wewe ni miongoni mwa wachukizao?, ni miongoni mwa wachawi, ni miongoni mwa wazinzi na waabudu sanamu?. Kama ndio!, basi tubu leo kwasababu Neema ya Kristo bado ipo, Ziwa la moto kaandaliwa shetani na malaika zake lakini si sisi!, lakini endapo tukiasi kama shetani alivyoasi basi na sisi tutaadhibiwa vile vile kama wao katika ziwa la moto.
Huko ni sehemu ya Mateso, moto ule ni kwa lengo la kutesa, na sio kuchoma tu!.
Bwana atusaidie tusifike huko, bali tuishi maisha ya kumpendeza yeye na kuyaishi maagizo yake.
(Moto na kiberiti, www.wingulamashahidi.org)
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
OLE WAKO KORAZINI NA BETHSAIDA.
YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.
Hili ni swali ambalo linaulizwa na wengi, hususani watu ambao walimwekea Mungu nadhiri huko nyuma lakini mwisho wa siku wamejikuta hawawezi kuzitoa.
Sasa kabla ya kwenda kuona kama msamaha upo au haupo, Jambo la kwanza unalopaswa kufahamu kuhusu nadhiri ni kwamba lile ni tendo la hiyari ambalo mtu anamwekea Mungu mwenyewe, na hapo ndipo Mungu anataka umakini sana kwasababu hakumlazimisha kufanya hivyo.
Biblia inasema ni heri, usiweke kabisa nadhiri kuliko kuiweka, halafu ukashindwa kuitoa,
Mhubiri 5: 4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri. 5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe”.
Mhubiri 5: 4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe”.
Unaona hapo? Mungu anasema yeye hawi radhi na wapumbavu. Ikiwa na maana kuwa nadhiri ambayo haitolewi kwa wakati, Ni haki ya Mungu kumwadhibu huyo mtu kwa jinsi atakavyo yeye.
Kwahiyo kabla hujatamka nadhiri yoyote kwa kinywa chako mbele za Mungu, hakikisha kwanza unaelewa unachokitamka, na una uwezo wa kukisimamia.Biblia inasema..
Mithali 20: 25 “Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu; Na baada ya kuweka nadhiri kuuliza-uliza habari”.
Sasa tukirudi kwenye kiini cha somo, Je! Kutotimiza nadhiri zako, Mungu hawezi kukusamehe?
Tukumbuke katika biblia ni dhambi moja tu isiyosameheka kwa Mungu, na dhambi yenyewe ni “Kumkufuru Roho Mtakatifu” Lakini hiyo haimaanishi kuwa adhabu za dhambi nyingine hazipo hapana.. Kuna dhambi ambazo Mungu atakusamehe bila adhabu, lakini pia zipo dhambi ambapo Mungu atakusamehe pamoja na adhabu. Kwa urefu wa somo hilo fungua hii link>>>>>> https://wingulamashahidi.org/2018/07/17/dhambi-ya-mauti/
Sasa ikiwa mtu hajamtimizia Mungu nadhiri zake, anaweza akatubu na pengine Mungu akamsamehe kabisa na mbinguni akaenda, lakini adhabu ya kosa lake, bado akaitumikia hapa hapa duniani, adhabu inaweza ikawa pengine hata kifo,n.k.
Lakini bado tukirudi katika biblia tunaona wapo watu ambao walihalifu nadhiri zao, lakini hawakuadhibiwa na Mungu, mmojawapo ni Daudi wakati ule anataka kwenda kumuua Nabali, aliapa kwa Mungu kwamba kama hatamuua Nabali na nyumba yake yote, basi Mungu amfanyie yeye hivyo . Lakini tunaona hakumuua Nabali alipofika katika nyumba ile, na Mungu vilevile hakumuua Daudi na nyumba yake kwa kutotimiza nadhiri zake. Hizo ndizo zinazojulikana kama nadhiri wa wapumbavu.
1Samweli 25: 22 “Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi”.
Sehemu nyingine, utaona ni wakati Sauli anapigana na wafilisti naye pia aliweka nadhiri kuwa mtu yeyote asionje chochote mpaka atakapomaliza kupigana na wafilisti na kuwashinda, atakayeonja atauawa lakini mwanae Yonathani, hakusikia agizo hilo, yeye akala, na Sauli alipopata taarifa akataka kumwangamiza, lakini Israeli wakamzuia, kwasababu yeye ndiye aliyeleta wokovu katika taifa. Na baada ya hapo hatuoni kama Mungu alimwangamiza Sauli kwa kuhalifu agizo lile.(Soma 1Samweli 14)
Lakini tunaona pia kulikuwa na mwamuzi mwingine aliyeitwa Yeftha, yeye alimwekea Mungu nadhiri kuwa atakaporudi kutoka vitani na ushindi, basi chochote kitakachotokea cha kwanza mbele yake, atamtolea Mungu kama sadaka ya kuteketezwa. Hakufikiria kwamba anaweza kutokea mtu mbele yake..
Lakini kweli Mungu alipomfanikisha katika vita, kitu cha kwanza kutokea mbele yake, hakikuwa ng’ombe, au mbuzi, bali binti yake wa pekee. Hivyo ikambidi aende kumchinja mwanawe na kumtoa kafara kwa Mungu, japo ambalo ni kinyume kabisa na maagizo ya Mungu, na ni machukizo. Yeftha Alikuwa na uwezo wa kuizuia nadhiri yake ya kipumbavu, kama alivyofanya Daudi au Sauli, lakini alitimiza nadhiri isiyokuwa na maana yoyote mbele za Mungu.
Hivyo, Mungu anaweza akaadhibu au asiadhibu, yote yapo katika uwezo wake mwenyewe..
Lakini katika yote, Mungu tangu zamani kwa hekima yake alishaona kuwa wapo watu wake, ambao watakuja kutamka nadhiri zao bila hata ya kufikiria, na ili kuwaepusha na adhabu, akampa maagizo Musa, juu ya nadhiri za wapumbavu kama hizo akasema..
Walawi 5:4 “au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo; 5 kisha itakuwa, hapo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo, ndipo atakapoliungama jambo hilo alilolikosa; 6 naye atamletea Bwana sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake”.
Walawi 5:4 “au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo;
5 kisha itakuwa, hapo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo, ndipo atakapoliungama jambo hilo alilolikosa;
6 naye atamletea Bwana sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake”.
Umeona?, Mtu kama huyo ambaye alitamka tu maneno bila kufikiri hatma yake itakuwaje mbeleni, pengine mwingine alisema mimi sitaoa au kuolewa maisha yangu yote, bila kupiga gharama zake. Mungu alimwambia Musa, mtu huyo atubu, kisha sio kutubu tu, bali aambatanishe na sadaka yake ya makosa kama vile atakavyoelekezwa na kuhani.
Hii ikiwa na maana, hata sasa wapo watu waliotamka nadhiri zako mbele za Mungu, lakini sasa wameshindwa kuzitoa, jambo la kwanza wanalopaswa kulifanya hapo ni kutubu kwa kumaanisha kabisa, sio kutubu kwa dakika mbili au tatu, hapana ni kulia kwa kumaanisha mbele za Mungu kwa kipindi fulani (ukikumbuka kuwa Mungu hawi radhi na wapumbavu, anaweza kukuondoa duniani kwa kosa hilo tu)..Kisha baadaye ukishamaliza maombi yako ya toba ya muda mrefu, andaa sehemu nono ya ulichonacho nacho (yaani sadaka), kisha kipeleke madhabahuni pa Mungu kwa ishara ya unyenyekevu kwa hofu nyingi.
Na baada ya hapo Mungu atakusamehe.
Shalom.
NADHIRI.
Fadhili ni nini? Nini maana ya “fadhili zake ni za milele” kibiblia?
Kwanini Paulo aungane na wale watu wanne wenye nadhiri?
Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?