Kuota mbwa kunamaanisha nini?

Kuota mbwa kunamaanisha nini?

Mbwa ni mnyama anayeweza kuwakilisha vitu vitatu:

1) Mlinzi

2) Adui

3)Kitu najisi/Mchafu.

Inategemea hiyo ndoto imekuja katika mazingira gani..na pia kama imekuja katika mazingira ya kujirudia rudia au katika hali ya uzito wa kitofauti basi haipaswi kupuuzwa, inayo maana rohoni.

  1. Tukianzana namaana ya kwanza kama mlinzi:

Kama tunavyojua mbwa ni mlinzi. Na katika biblia watumishi wa Mungu pia wanafananishwa na mbwa walinzi.

 Vilevile watumishi  ambao hawasimami katika  nafasi zao kikamilifu za kuwalinda kondoo wa Mungu  wanafanishwa na mbwa walinzi wasioweza kubweka wala kung’ata.

Isaya 56:9-11

[9]Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni.
[10]Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.[11]Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.

Kwahiyo unapoota..mbwa mara kwa mara..pengine amesimama getini tu..au anafukuza kitu  au anafanya kitu fulani kwa ujasiri lakini hana shida na wewe.. hana mpango wa kukudhuru wewe..basi ni Mungu anakukumbusha kuwa uzidi kusisima vema katika nafasi yako kama mlinzi.

Lakini kama unaona mbwa huyo ni mwoga..anakimbizwa kimbizwa tu..anajificha ficha ujue huna nguvu rohoni..hivyo tengeneza mambo yako na Mungu ikiwa wewe ni mtumishi wa Mungu. Kwasababu Mungu anakuona kama mlinzi lakini bado hujakamilika katika kazi yako.

2) Maana ya pili ni kama Adui.

Kibiblia mbwa pia anawakilisha Adui.
Zaburi 22:16

“[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu”.

Zaburi 22:20 “Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa”.

Ukiota unakimbizwa na mbwa..au unashambuliwa nao. Au wanakutisha.au wanakuvizia kuchukua kitu chako..Ujue kuwa upo katika vita rohoni.
Ibilisi anataka kuiba kilicho chako.au kukuangamiza kabisa.. Hapo kama umeokoka huna budi kuwa mwombaji sana..mwambie Bwana akulinde na kukuhifadhli mbali na mashbulizi yote ya adui..pia zidisha kiwango chako cha kumtumikia Bwana ni ulinzi mkubwa sana.

Wafilipi 3:2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.
Lakini kama hujaokoka..fanya hima mapema sana umrudie Mungu wako. Vinginevyo upo hatarini kuangamia kabisa.

3) Maana ya tatu ni kitu najisi.

Kibiblia mbwa pia anawakilisha kitu najisi” au kichafu .Mbwa huwa hajali ni nini anakula anaweza rudia hata matapishi yake biblia inasema hivyo katika.. Mithali 26:11..

Ni wanyama wasiostahili heshima yoyote..

Mathayo 15:26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

Mbwa hajali ni yupi anakutana naye katika kupata watoto..anaweza kutanana hata na mama yake.
Hivyo kwa ujumla ni kwamba mbwa anawakilisha pia watu waovu..waliodhambini ambao hawajali maisha yao ya kiroho hata kidogo.

Kwahiyo kama unaota mara kwa mara mbwa ambao huelewi wapo kwa lengo gani..leo unamwona hivi kesho vile…ujue kuwa ndivyo Mungu akuonavyo.

Tubu dhambi zako mgeukie Mungu wako kama wewe ni mwenye dhambi..kumbuka katika hali kama hiyo uliyopo sasa ukifa ujue ni moja kwa moja kuzimu..biblia inasema hivyo kwa watu walio hivyo rohoni..

Ufunuo 22:15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Ikiwa upo tayari leo kumkaribisha Kristo ndani ya maisha yako akubadilishe basi fungua hapa kwa ajili ya kupokea mwongozo wa sala ya Toba..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments