Bwana Yesu alikuwa na maana gani aliposema “kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate”?
JIBU: Sentensi hiyo ina tafsiri mbili..Tafsiri ya kwanza ni ya rohoni, na pili ni ya mwilini…Tukianza na tafsiri ya rohoni ambayo inamaanisha viungo vyote vya rohoni. ..Kwamba kitu chochote kile ambacho ni kikwazo cha sisi kuingia mbinguni hicho ni sawa na kiungo, Umaarufu unaweza kuwa ni kiungo,.. marafiki wakati mwingine wanaweza kuwa ni kiungo (kwasababu wapo marafiki ambao ukikaa nao unaweza kuikosa mbingu, hivyo ni wakukata ili kuinusuru roho yako)..Shughuli ni kiungo (Zipo shughuli au kazi ambazo ukizifanya zitakukosesha mbingu haijalishi zimehalalishwa na nchi kiasi gani)..n.k
Tafsiri ya pili na ya muhimu inahusu viungo vya mwili. Mkono unaweza kukukosesha kuiona mbingu., kama mkono wako umezoea wizi., kila ukipita unatamani kudokoa, kama mkono wako umezoea kufanya masturbation, ..Kama imeshindikana kuamua kuacha kufanya hayo mambo kwa njia ya kawaida basi ni bora uukate huo mkono…ili usije ukakupeleka jehanamu ya moto… Kadhalika na ulimi wako kama unakusababisha kila dakika uzungumze mambo ya watu wengine vibaya, au uchonganishe au utukane ni heri ukaukata ili ujiokoe na ziwa la moto…
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana. 6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum. 7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu. 8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo”.
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo”.
Sasa hata mambo mawili yakiwekwa mbele yangu, nikaambiwa nichague moja,..kwamba ulimi wangu ukatwe niingie mbinguni au nibaki na ulimi wangu niingie Jehanamu…Ukweli ni kwamba nitachagua kukatwa ulimi ili niingie tu mbinguni Na kila mtu ni wazi atachagua hivyo hivyo.
Na viungo vingine vyote ni hivyo hivyo..kama vinatukosesha tumepewa ruhusa ya kuviondoa..sio dhambi! ..Kama tu tunaweza kuondoa figo iliyo na kansa mwilini, ili tu mwili wote usije ukafa…kwanini tushindwe kukata kiungo kimoja ambacho tusipokitoa kitatugharimu ziwa la moto?..Kama unaweza kufanyiwa operation ya kukatwa miguu ili ugonjwa usisambae mwili mzima au kukatwa ziwa ili tu kansa isikumalize mwili wote..kwanini tushindwe kuondoa hivyo hivyo kama vinakuwa sababu ya kutupeleka jehanamu…?
kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate.
Wengi wanapenda kulipooza hili Neno la Bwana Yesu na kusema kwamba “hakumaanisha viungo vya mwilini”..Alimaanisha viungo vya mwilini na vya rohoni..vyote viwili!!..Ni kweli tunavipenda viungo vyetu lakini kama vinakuwa ni vikwazo vya kwenda mbinguni hakuna namna..
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?
Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?
Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?
NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.
Je unaweza usisamehewe hapa duniani na kule ukasamehewa?
Rudi Nyumbani:
Print this post
heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
Shalom, Jina la Bwana YESU libarikiwe. Ni siku nyingine tena, Bwana ametupa pumzi yake ya uhai, hivyo hatuna budi kumshukuru kwa hili, haijalishi tu wagonjwa kiasi gani, au tunapitia katika magumu kiasi gani, maadamu tu! pumzi ipo basi tumsifu Mungu.
Leo tutaangazia ni Kwanini biblia mara kwa mara inatumia semi kama hizi: “heri leo”… “maana baadaye”…..
Hiyo inatuonyesha kuwa kile tunachopita leo hii, basi kinyume chake ndicho tutakachokipitia baadaye..Kuna kanuni fulani Mungu ameziweka katika vitu vya asili ambavyo tukivichunguza vizuri tutapata picha ya mambo yanayoendelea rohoni..Kwa mfano kuna wakati utaona muda mfupi kabla mvua kunyesha joto huwa linaongezeka kwa ghafla na kuwa kali sana pengine dakika tano au 10 hivi.. na baada ya hapo mvua kubwa inashuka yenye upepo na baridi…
Au wakati mwingine wa jioni jua linapokaribia kuzama, utagundua kuna nuru inaongezeka kiasi fulani kwa jinsi isivyo ya kawaida kisha baada ya dakika chache tu giza linakuja kuu.
Hiyo inatuonyesha kuwa kabla ya jambo fulani zuri au baya kutokea huwa kinatangulia kilicho kinyume chake..
Na ndivyo hata katika mambo ya Mungu, sikuzote Mungu kabla hajambariki mtoto wake yeyote ni lazima kwanza apitie hali fulani ya uhitaji au dhiki ili aweze kukimudu kile alichomwandalia kule mbeleni.Ndivyo alivyofanya kwa Yusufu ndivyo alivyofanya kwa wana wa Israeli kule jangwani, na ndivyo alivyofanya kwa Ayubu,..ndivyo alivyofanya kwa Nebukadneza, na ndivyo atakavyofanya kwa mtoto wake yeyote yule atakayemwita..
Na ndio maana Bwana Yesu alisema ikiwa unapitia huzuni sasa, kwa ajili ya Imani yako, hajalishi ni katika afya yako,au katika uchumi wako maadamu wewe ni mkristo, basi fahamu kuwa ipo faraja kubwa Mungu kaiweka hapo mbele kwa ajili yako ..Hivyo usiogope..afya tele ipo mbele yako, vicheko tele vipo mbele yako, chakula tele kipo mbele yako.
Mathayo 5:4 “Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika”
Luka 6:21 “Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka”
Luka 6:21 “Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba.
Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka”
Ukiona leo, unayo kiu ya kuyasikia maneno ya Mungu, na unatamani kumfahamu sana Mungu kwa viwango vya juu…Basi usiogope kuonekana umerukwa na akili sasa, au mtu wa itikadi kali…fahamu tu kuwa hapo mbeleni hiyo kiu haitakuwepo tena, na utamfahamu Mungu kwa viwango ambavyo si vya kawaida vya yeye anavyotaka umjue yeye, utazamishwa katika vilindi vya moyo wa Mungu, na kuonyeshwa mambo ambayo ni makubwa na magumu wanadamu wasiyoyajua..
Ukiona leo unachekwa na kudharauliwa na kuonekana kuwa wewe ni takataka kwasababu umeamua tu kumfuata Kristo basi ujue kuwa hapo mbeleni kuna kuheshimiwa na kuogopwa, na kutukuzwa kwa ajili ya Jina la YESU KRISTO.. Hiyo ndiyo kanuni..
Ukiona leo umeacha kila kitu, umekuwa tayari kupoteza hata kazi yako, au biashara yako, au mali zako, au elimu yako au hadhi yako kwa ajili ya Yesu au kwa ajili ya Injili ya Kristo isonge mbele,.. basi fahamu kuwa kupata mara 100 ya hivyo ulivyovipoteza ipo mbele yako..haijalishi itachukua miaka 5,10 au 20 au 50 lakini kabla haujafa Mungu atahakikisha amelitimiza hilo neno lake juu yako.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi? 28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. 29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”.
Vivyo hivyo tukiona sisi wakristo tumeupoteza ulimwengu wote.,kwa ajili kumtazama Kristo na ufalme wake wa milele, mpaka tunaonekana kama vile watu tusiostahili kuwepo katika ulimwengu huu, basi tujue kuwa,.. Huu huu ulimwengu tutaupata, maana biblia inasema dunia hii itarithiwa na wenye upole( watakatifu)..Na hiyo itatimia katika utawala wa miaka 1,000 unaokuja huko mbeleni.
Mathayo 5:5 “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi”.
heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka
Lakini kinyume chake pia ni kweli, ukiona sasa umeupata ulimwengu wote, basi ujue tayari umeshaupoteza,..Ukiona kila aina ya ouvu duniani unaokuja wewe ni wako, disko ni zako, uzinzi ni wako, ulevi ni wako, starehe zote ni zako, rushwa ni yako,… wizi ni wako, dhuluma ni zako, tamaa za ujanani ni zako, vimini na suruali ni zako, viduku, na milegezo ni yako..uzinzi ni wako, fashion ni zako…Basi ujue kuwa safari yako ni fupi hapo mbeleni, nyakati za shida zinakuongojea..
Mathayo 16:25 “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”..
Mathayo 16:25 “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”..
Unaona? Uamuzi ni wako,.. usifurahie kuwa unayo afya nzuri sasa na huku upo mbali na Kristo,.. usifurahie unayo elimu kubwa na huku yupo mbali.., unacho hichi aunacho kile, ni mrembo ni mzuri,..fahamu kuwa Mungu ameruhusu faraja yako ikujie sasa ili wakati wa wenzako kufarijiwa wewe uwe unalia na kusaga meno..
Zaburi 62:7 “Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele”
Kama wewe upo nje ya Kristo utajisikiaje usikie unyakuo umepita leo na wewe umebaki?., wakati wenzako wanafarijiwa milele mbinguni katika ile karamu ya mwana kondoo wewe upo hapa chini ukisubiri ziwa la moto wa milele. Ni majuto kiasi gani, ukikumbuka kuwa ulishahubiriwa injili mara nyingi na ukapashupaza shingo yako.
Embu leo sema Bwana Yesu usinipite, ninakukaribisha maishani mwangu tangu sasa. Sema hivyo ukimaanisha kabisa kutoka katika moyo wako kuwa kweli kuanzia leo umeamua kumfuata yeye..Ukiwa umepiga magoti yako mwombe akusafishe dhambi zako zote kwasababu hapo ulipo yupo ili kukusikia,.. tubu kabisa hata kwa machozi, na yeye hapo ulipo atakusamehe na kukupa amani ya ajabu ndani ya moyo wako..
Ukishaona hivyo, na amani imekuja ndani yako ujue amekusamehe,..unachopaswa kufanya usihangaike hangaike na huu ulimwengu bali haraka tafuta kanisa zuri la kiroho linalomuhubiri Kristo,.. uende pale, vilevile ukiwa hukubatizwa ipasavyo unapaswa ufanya haraka sana kutimiza agizo hilo muhimu Bwana Yesu alilotupa kwa kila mtu atakayeokoka, Kwamba wote tubatizwe katika ubatizo mmoja kwa jina lake..
Zipo batizo nyingi duniani ambazo si za kimaandiko lakini ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi (Yohana 3:23), na uwe ni KWA JINA LA YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38..
Baada ya hapo Roho Mtakatifu atakutia muhuri na atakuwa kiongozi wako milele kukuongoza na kukulinda mpaka ile siku ya Unyakuo itakapofika ikiwa bado utakuwa hai.
Bwana akulinde, Bwana akubariki.
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/maswali-na-majibu/
Kwanini awe Punda na si mnyama mwingine?
Karibu tujifunze Maandiko.
Tunaona kipindi kifupi kabla Bwana Yesu kuingia Yerusalemu aliwatuma wanafunzi wake wakamletee Mwana-punda ili alingie naye mjini..Ipo sababu kwanini alimtumia yule mtoto wa punda na si mama yake (Mathayo 21:4-5)..lakini leo hatutakwenda kuiangalia hiyo sababu..kama utapenda kufahamu ni kwanini hakumtumia Mama-punda bali mwanae…unaweza akatuambia inbox tukakutumia ujumbe wake…
Pamoja na hayo pia ipo sababu kubwa sana ni kwanini hakutumia mnyama mwingine yoyote kama vile Farasi au Ngamia kuingia naye Yerusalemu badala yake akatumia PUNDA, kwanini awe punda.. Na hali tunajua kuwa punda si mnyama wa heshima…Walau ingekuwa ni Farasi ingeleta heshima kidogo…lakini si punda?..Tofauti na wahubiri wengi waa leo hii ambao ukiota tu punda au ukifuga tu punda licha ya kumpanda ni rahisi kuambiwa una nyota ya punda!..(utaambiwa utakuwa mtumwa milele)…
Lakini haikuwa hivyo kwa Bwana wetu Yesu,..Yeye alimpanda huku akijua kuwa yeye ni mfalme anayesubiriwa mjini, na muda mfupi tu baadaye aliimbiwa na umati mkubwa kwa shangwe na vigelegele kwamba yeye ni Mfalme!!, Hosana juu mbinguni..watu walitandika mavazi yao chini na kukata matawi ya miti na kuyatandaza chini, Mfalme mkuu juu ya punda apite, na kumwimbia…Mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana!..Hivyo punda sio mnyama wa laana kama upotovu uliozagaa leo….
Hivyo kuna ufunuo hapo kwanini awe ni punda Bwana Yesu alimtumia na si mnyama mwingine..Na leo tutajifunza kwa ufupi siri hiyo, ambapo tukishaijua tutafahamu ni jinsi gani KRISTO alikuwa ni chombo ya muhimu sana kwetu.
Pamoja na tabia nyingine nyingi Punda alizonazo…lakini anayo tabia moja kuu ambayo imewazidi Wanyama karibia wote..Na tabia hiyo ni tabia ya KUHISI HATARI ILIYOPO MBELE, AU KUHISI KITU KINACHOKUJA MBELE…Chochote cha heri au cha shari kinachokuja mbeleni Punda ni mwepesi sana kukihisi…Jambo ambalo litamfanya aidha Agome kuendelea mbele au Aende huko anakokwenda kwa Furaha…. Jamii zote za Punda wanayo hiyo tabia, hata farasi anayo lakini si kwa kiwango alichonacho Punda…(kwasababu farasi naye ni jamii ya Punda).
Ayubu 39:19 “Je! Wewe ulimpa farasi uwezo wake? Au, ni wewe uliyemvika shingo yake manyoya yatetemayo? 20 Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige? Fahari ya mlio wake hutisha. 21 Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake; Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha. 22 Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai; Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga. …… 25 Kila ipigwapo baragumu yeye husema, AHA! NAYE HUSIKIA HARUFU YA VITA TOKA MBALI, Mshindo wa maakida, na makelele”.
Ayubu 39:19 “Je! Wewe ulimpa farasi uwezo wake? Au, ni wewe uliyemvika shingo yake manyoya yatetemayo?
20 Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige? Fahari ya mlio wake hutisha.
21 Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake; Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha.
22 Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai; Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga. ……
25 Kila ipigwapo baragumu yeye husema, AHA! NAYE HUSIKIA HARUFU YA VITA TOKA MBALI, Mshindo wa maakida, na makelele”.
Unaona! Farasi anauwezo wa kusikia harufu ya vita toka mbali..Kesho kutapiganwa vita farasi leo kashajua!! (Ni kipawa ambacho Mungu kawapa)..Sasa hisia za Punda ni kubwa kuliko za Farasi. Wafugaji wazoefu wa punda wanajua!..huwa punda akigoma kufanya kitu au kwenda mahali huwa hawamlazimishi..kwasababu wanaelewa hisia alizonazo punda..
Tunasoma mfano mmoja katika Biblia wa mtu anayeitwa Balaamu, huyu alitaka kwenda kuwalaani Israeli, jambo ambalo Mungu alimkataza kulifanya..lakini yeye akashupaza shingo,..wakati akiwa njiani anaelekea kwenda kuonana na mfalme Balaki kwa lengo la kuwalaani Israeli, akiwa amempanda punda wake…Njiani alikutana na Malaika ambaye alitaka kumwua lakini cha ajabu ni kwamba Balaamu hakumwona yule malaika lakini punda alimwona!..Japokuwa Balaamu alikuwa ni mtu wa kiroho sana aliyezoea kuona malaika lakini siku hiyo hakumwona…Punda alimsaidia kumwepushia ile ajali ya kuuawa. Mpaka alipofunguliwa macho na kuiona hatari iliyopo mbele yake..hivyo asingekuwa punda Balaamu angekufa..(Kasome Hesabu 22 yote). .
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2015, mwezi wa 10 tarehe 14..Tulikuwa tupo wawili tunapita mahali fulani huku tunazungumza habari za Mungu..Sehemu hiyo ilikuwa ni mbali kidogo na mji ni kama nusu Kijiji hivi…Ni sehemu ambayo ina wafugaji na wachungaji…Siku hiyo jua lilikuwa linawaka sana wakati tunatembea huku tunaongea..mbele yetu walitokea watu ambao walionekana wametoka porini kukusanya nyasi za ng’ombe hivyo wameziweka kwenye kigari ambacho mbele kilikuwa kinavutwa na punda watatu waliofungiwa nira. Binafsi sikuwahi kuona punda watatu wakiwa wamefungwa nira pamoja..Nimezoea kuona wawili tu…Na hata mwenzangu na yeye hakuwahi kuona hicho kitu…Basi wote kwa pamoja tukasema ngoja tusogee mbele kidogo tuona jinsi walivyozifunga hizo nira katikati ya hao punda watatu..
wale mabwana walikuwa wanawachapa waendelee kusogea mbele..maana ule mzigo ulikuwa ni mzito kidogo..Sasa wakati tunakazana kutazama zile nira katikati ya wale punda watatu, yule punda wa katikati akatoweka!. Wakabaki wawili tukaduwaa kidogo ni nini kinaendelea…Lakini wale mabwana wao ni hawakuona lolote…
tuligundua kuwa wale punda walikuwa na uwezo fulani ambao haukuwa wa kawaida..kwasababu mzigo ulikuwa mzito na viboko vingi lakini walitembea vizuri kama kawaida…Sasa kwa haraka haraka kama si mtu wa rohoni unaweza kuhisi umeona uchawi!!..lakini haukuwa uchawi, Roho Mtakatifu muda mfupi baada ya hilo tukio alizungumza na sisi kutufundisha jambo…
Tulichokiona kilikuwa ni ono!..Kwamba Bwana hata katikati ya Wanyama yupo kuwasaidia,..Na pia akatufundisha kuwa “walipo wawili au watatu yeye yupo katikati yao”..Ulikuwa ni uthibitisho tu kuwa Mungu yupo katikati yetu wakati tunazungumza habari zake… na wengine wakusanyikao katika Bwana yeye anakuwa katikati yao, mfano wa wale punda..Na wakati wale mabwana wanadhani wale punda wapo wawili tu…kumbe wale punda walikuwa wanamwona mwingine watatu akiwa katikati yao, akiwachukulia mizigo yao na maumivu yao… Haleluya!!, Hicho ndicho Roho Mtakatifu alichotufundisha siku hiyo.
Sasa tukirudi kwa kile kilichotokea wakati Bwana anaingia Yerusalemu…Unaweza kufikiri ni nini wale Punda walikiona mbele??..Farasi wangenusa vita lakini si WOKOVU uliokuwa unakwenda Yerusalemu..Ngamia wangenusa jangwa lakini Punda waliona wokovu…Waliona Amani, walimwona huyu tuliyembeba Anakwenda kuleta Ukombozi kwa viumbe vyote.
Hivyo wasingeweza kugoma..kama walivyogoma kwa Balaamu..Mbele ya Balaamu waliona kifo lakini mbele ya MASIHI YESU KRISTO WALIUONA WOKOVU!!! Haleluya. Waliona wokovu unaingia Yerusalemu, kipindi kifupi tu kijacho Roho Mtakatifu atashuka ndani ya watu kuanzia hapo Yerusalemu..waliona mabadiliko makubwa ya nyakati yanakwenda kuanza..Punda Waliona huyu atupandaye ataleta amani si tu kwa wanadamu bali hata kwa viumbe vyote..kwamba wakati utafika viumbe vyote vitawekwa huru kupitia huyu..Hivyo punda yule alitembea mbele kwenda Yerusalemu kwa furaha yote wala hakusimama njiani..
Warumi 8:19 “Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. 22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa”.
Warumi 8:19 “Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;
21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa”.
Ndugu kama Punda wameouona wokovu wewe kwanini usioune wokovu!..Punda walikubali kutumika wewe kwanini usikubali leo!..Punda waliupata ufunuo wa Yesu wewe kwanini hauuoni leo…Bado unaitumikia dunia ambayo mshahara wake ni mauti!!..bado mwasherati, mlevi, mzinzi, mla rushwa, msengenyaji, mwizi, mlawiti, mtoaji mimba, mvumishaji habari za uongo na mshirikina?..Utaficha wapi uso wako siku ile!..
Sasa lengo kuu sio kuwasifia punda, au kuwafanya kuwa viumbe wa kiungu!.. Kwamba wanastahili kuheshimiwa..au kutumika katika masuala ya utambuzi…Hapana! hakuna mnyama yoyote anayestahili kupewa heshima hiyo wala kuhusishwa na masuala ya Ibada…Lengo kuu ni kujifunza ni UTUKUFU ALIOUBEBA YESU KRISTO, Na kwamba kila kitu, ikiwemo viumbe vyote vimebeba ushuhuda wake…Kila mahali kwenye miti, miamba, bahari, mbingu, milima, sayari n.k kumeandikwa ushuhuda wa Yesu Kristo. Hivyo Yesu Kristo ni muhimu sana katika Maisha yetu.
Mathayo 11:28 ‘’Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi’’
Mathayo 11:28 ‘’Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi’’
Hivyo Kama hujamkabidhi Maisha yako…Mlango upo wazi sasa, ila hautakuwa hivyo siku zote…itafika wakati utafungwa na ukishafungwa itakuwa haiwezekani tena kuupata wokovu…Hivyo unachopaswa kufanya kama hujakoka ni hapo ulipo utubu dhambi zako zote bila kuacha hata moja…mwambie Bwana Yesu akusamehe na kwamba hutafanya tena hizo dhambi..na ukishatubu kwa kumaanisha kabisa, kuna msukumo wa ajabu utakuja ndani yako wa kukufanya utamani kumjua Mungu Zaidi…
Mkumbuke mtu yeyote ambaye hapo kwanza uliwahi kumwona ni mkristo wa kiroho, na matendo yake ni mazuri…kajiungamanishe naye huyo, na kuanzia hapo Roho Mtakatifu ataanza kutembea na wewe kukuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko…Pia katika hatua hizo zingatia kutafuta ubatizo haraka sana kama hukubatizwa..Ubatizo sahihi ni ule wa maji tele (Yohana 3:23),..na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, Na Roho Mtakatifu atafanya yaliyosalia ndani yako.
Kumbuka Yesu Kristo, ndiye NJIA, KWELI na UZIMA…Hakuna njia nyingine ya kuokolewa isipokuwa kwake yeye.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Maran atha!
KWANINI AWE NI PUNDA NA MWANA-PUNDA?
JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?
USISIKILIZE DHIHAKA ZA SHETANI, ZITAKUKWAMISHA.
TUMAINI NI NINI?
Bonde la kukata maneno ni nini?
Yoeli 3:14 “Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno. 15 Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. 16 Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli”.
Yoeli 3:14 “Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno.
15 Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza.
16 Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli”.
Biblia inatuambia kuna wakati unafika hapa mbele yetu ambao Mungu atayaleta mataifa yote katika bonde lijulikanalo kama bonde la kukata maneno, biblia imeliita pia kama Bonde la Yehoshafau ukisoma kuanzia mstari wa 12. Yehoshafua maana yake ni YEHOVA-ANAHUKUMU..Hivyo bonde hilo litakuwa ni bonde la Yehova kuya hukumu mataifa yote..
Unaweza ukajiuliza ni kwanini pia limeitwa bonde la kukata maneno.. Kwa lugha rahisi kukata maneno ni sawa na kusema kumaliza hoja, au malumbano,.. kwamfano mahali ambapo, pana malalamiko mengi labda tuseme katika Taifa fulani wananchi wake wanalamika kila siku miundo mbinu ni mibovu,..
wanashindwa kufanya shughuli zao za kimaendeleo, wanashindwa kusafiri, wanashindwa kwenda mashambani n.k.
sasa kama serikali italiona hilo na kuacha kuchukua hatua watu wake wataendelea kulalamika hivyo hivyo hata kwa karne na karne,.. sasa ili kukata maneno hayo, viongozi huwa wanachukua uamuzi wa lazima na wa haraka, aidha watalazimika kwenda kukopa pesa ili watimizie wananchi matakwa yao,.. au watatoa katika bajeti yao wahakikishe tu kuwa jambo hilo linafanyika haraka sana ili kukata maneno ya wananchi yasiendelee kuwasumbua..hivyo Kukata maneno ni kutoa suluhisho. (kwa kiingereza linaitwa Valley of decision).
Vivyo hivyo na kwa Mungu pia, leo hii yapo makundi makuu mawili ya watu yanayomlilia na kumpelekea tuhuma zao kila kila siku kundi la Kwanza ni lile linalomlilia Mungu na kumwambia ni lini Bwana utakomesha uovu juu ya nchi ili maasi yasiendelee?.
Ni lini utatulipizia kisasi juu ya maadui zetu na maadui zako? Ni lini ufalme wako utakuja duniani?…Ni lini Bwana…?
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Na kundi la pili ni lile linalodhihaki, na kusema, huyo Yesu mnayemngojea mbona harudi amekufa?., kundi linalolikufuru jina la Mungu bila hofu yoyote, kundi linalojiamulia kufanya maovu tu bila kujali kuwa yupo Mungu juu, kundi linalosema hakuna Mungu,.. kama yupo basi ajitokeze tumwone, akisimama hapo na kushusha moto mbinguni, ndipo tutamsujudia..mbona anajificha, anajifichia nini ikiwa yeye ni Mungu n.k..
Umeona? Makundi yote haya yanapeleka malalamiko yao..Sasa Bwana ameiandaa siku ambayo ATAKATA MANENO HAYA YOTE..Siku hiyo ndugu usitamani uwepo..Kwasababu kabla hajatenda tendo lolote atahakikisha kwanza mataifa yote yamekusanyika pamoja, kisha atayafanya yaelekeze uso wao pale Israeli.. na uwanja wa mapambano utakuwa katika lile bonde la Yehoshefau au bonde la kukata maneno..
Sasa wakati wameshajiweka tayari kwa vita biblia inatuambia ghafla, jua na mwezi vitatiwa giza, yaani kwa wale ambao watakuwa upande wa mchana kipindi hicho watalishuhudia jua likizama saa 7 mchana, na kuwa giza tororo duniani kote,. wala hata mwezi nao hautaonekana, wala hizi nyota, wala tochi, wala taa za barabarani haziwaka..duniani kote hakutakuwa na chanzo chochote cha mwanga kwa ufupi.
Amosi 8:9 “Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana”.
Kipindi hicho dunia itakuwa imeshaingiwa na hofu, wakiomboleza ni nini hiki kimetokea hapo ndipo wakatakapomwona Kristo akishuka na wingu kutoka juu pamoja na majeshi ya mbinguni..(watakatifu waliokuwa wamenyakuliwa), hapo ndipo Bwana atawaua kwa upanga utokao katika kinywa chake,.
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana. 17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; 18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. 19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake”.
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake”.
Katika kipindi hichi baada ya Kristo kuwaangamiza wale wote waliokuja kufanya vita kinyume chake ambao watakuwa ni mamilioni kwa mamilioni, hatua inayofuata ataketi na kuwahukumu wale waliosalia,.. huo ndio ule wakati wa kutenganishwa kondoo na mbuzi, mbuzi watatupwa katika lile ziwa la moto..Na hao wengine watapata neema ya kuingia katika ule utawala wa miaka 1000. Na kipindi hicho sio kwamba watu watakuwa ni wengi duniani hapana, biblia inasema watu wataadimika kuliko Dhahabu, (Soma Isaya 13:12), hivyo pengine ni watu 100 kati ya bilioni 7 waliopo duniani leo watakaosalimika, kama vile ilivyokuwa katika siku za Nuhu ilikuwa ni watu 7 kati ya mabilioni..Mungu hana wengi wape,..haangalii wingi wa watu wasiomwamini kama kigezo cha kuturehemu.
Na wakati huo sasa ndio Kristo atakapoitengeza tena hii dunia ndipo atakapotawala kama mfalme wa wafalme duniani, pamoja na wale watakatifu waliokwenda naye kwenye unyakuo na kurudi naye na wayahudi waliokuwa wamefichwa..Hao pekee ndio watakaofanana na malaika, watakaokuwa na miili ya umilele, lakini wengine watazaliana na kuongezeka mpaka mwisho wa ule utawala wa miaka 1000 utakapofika..
Hivyo unaweza ukaona ni jinsi gani hii dunia inavyoelekea pabaya, mambo hayo usidhani yatakuja kutokea miaka 800 mbeleni, tunaweza kuyashuhudia katika kizazi chetu hichi,.. kwani mataifa mengi tayari yameshaelekeza silaha zao Israeli kwa lengo la kuliondoa katika uso wa dunia unadhani ni kitu gani kimesalia..
Bonde la kukata maneno!! Lisiwe sehemu ya maisha yako.Mkaribishe Kristo maishani mwako leo ili akufanye kuwa kiumbe kipya, na kukuepusha na hukumu inayokuja..jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
CHUKIZO LA UHARIBIFU
SIKU YA HASIRA YA BWANA.
JUMA LA 70 LA DANIELI
ZIKUMBUKE SIKU ZIJAZO ZA GIZA, KWA MAANA ZITAKUWA NYINGI.
Dhambi inazaa kifo.
Jina la Yesu Kristo Mkuu wa Uzima.. libarikiwe!.
Yohana 8:33 “Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote”
Yohana 8:33 “Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote”
Mtu anayetenda kazi anafananishwa na Mfanyakazi…Na mfanyakazi anaweza akawa na cheo cha juu, au cha chini…Mara nyingi wale wenye vyeo vya chini sana wanaitwa watumwa…Watumwa wengi huwa wanapitia mateso..Mshahara wanaoupata haulingani na kazi wanazozifanya…Wanalazimika kumtumikia tu Bwana wao kwasababu hawana namna nyingine ya kujikwamua kimaisha.
Kadhalika Mtu atendaye dhambi!..Biblia inasema ni mtumwa wa dhambi..Na utumwa huo unafananishwa na utumwa wa wanyama…Kwamfano mnyama kama ng’ombe anaweza kutumikishwa kulima hekari hata 1,000 katika maisha yake yote, na kuzalisha maziwa lita elfu 5,000 katika maisha yake yote..lakini mshahara wake mwisho wa siku ni KISU SHINGONI MWAKE!. Na wala hakuna mtu anayejali kufa kwake…Na nyama yake itatumika kama kitoweo, na ngozi yake kwa kutengenezea viatu, na pembe zake kutengenezea mbiu na vifungo.
Kadhalika na utumwa wa dhambi ni hivyo hivyo…Dhambi inaweza kukutumikisha miaka yote na mwisho wa siku ikakuzawadia au kukulipa KIFO. Tena wakati mwingine kifo cha kikatili.
Warumi 6: 23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Ndugu mshahara wa dhambi ni mauti biblia haidanganyi!, …Usidanganywe na Tamaa za ulimwengu huu, “wanazoziita ustaarabu mpya”… zinazokuambia kuwa na boyfriend/girlfriend ni kwenda na wakati..zinazokuambia kujipamba uso na kujichubua na kuvaa wigi na hereni ni kujipenda!..zinazokuambia mpende akupendaye asiyekupenda mwache, na hivyo hata ukiwa na mke/mume msiyeelewana kidogo tu ni ruksa kumwacha na kutafuta mwingine!…
usidanganyike na Tamaa za anasa za ujanani zinazokuambia kwenda disko sio vibaya, zinazokuambia kunywa pombe yenye kidogo sio vibaya, zinazokuambia kuvaa vimini sio vibaya ni ujana tu!..utakapofikisha umri fulani ndipo utaanza kuvaa vizuri.
2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi”…
Yakobo 1:14 “ kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Yakobo 1:14 “ kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Ukitenda dhambi unajitengenezea mazingira ya kukutwa na kifo cha ghafla!….Sasa sio kwamba wote wanaokufa kwa ghafla wana dhambi!.. Hapana sio wote…Lakini idadi kubwa, Zaidi ya robo tatu ya vifo vinavyotoke leo hii duniani kote.. ni matokeo ya dhambi juu ya maisha ya watu Biblia inasema hivyo..(Soma Ezekieli 18:31, Ezekieli 33:11, Ezekieli. 18:20)
Uzinzi ni kifo!. Na kifo cha uzinzi na uasherati hakitokani tu na HIV au ugonjwa Fulani wa zinaa..kama wengi wanavyodhani….Wakati mwingine vifo vya ghafla visivyokuwa na chanzo au visivyoeleweka.. vinaweza kuwa ni matokeo ya dhambi ya uasherati juu ya maisha ya mtu..Mtu aliye mwasherati anaweza akafa tu hata kwa ajali sio lazima tu HIV..
Mshahara wa kushi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana ni kujitengenezea kifo,..kumwacha mkeo/mumeo na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine ni umejitengenezea kifo mwenyewe..(Kwasababu biblia inasema kifo ndicho kitakachowatenganisha sasa wewe umefanyika kifo katikati ya hiyo ndoa ndio maana umeitenganisha)… kutowaheshimu wazazi ni mauti!..mshahara wa rushwa, na wizi wa namna yoyote ile ni kifo,(na kifo sio tu cha kuchomwa moto! Kinaweza kuwa kingine hata ugonjwa Fulani tu! Ukakupata ghafla na kukuondoa)..mshahara wa kutoa mimba, kuua, kulawiti, kucheza kamari, kufanya uchawi, kuuabudu sanamu, usengenyaji,utukanaji n.k ni KIFO!..chaa kimwili na cha Kiroho..
Haijalishi hiyo dhambi ilikuwa inakunufaisha kiasi gani…Hata baadhi ya wanyama kama kuku wanaweza kunufaika kwa kulishwa vizuri na kupewa kila aina ya chakula ilikusudi kwamba wawe na nyama nyingi au watage sana…lakini pamoja na kunenepeshwa kwao kote..mshahara wao wa mwisho ni mauti!..Siku wasiyoitazamia na wasioitegemea msiba wao unawafika kwa ghafla..Ni idadi ndogo sana ya kuku wanaokufa kifo cha kawaida..
Unaweza ukawa unakula rushwa leo na ukafanikiwa, unaweza ukawa unaiba na unafanikiwa lakini fahamu kuwa kifo kinakuja mbele… Nataka nikuambie kifo ni kama usingizi ni kitu ambacho huwezi kukipangia wakati wa kukuvaa…kama vile unavyozama usingizini hujui dakika halisi uliyolala…utakapozinduka ndipo utakapojua kumbe muda ule ulipotelea usingizini..,Unaweza kujilaza kitandani na ukasema kabla ya kulala nitafanya hichi au kile..wakati unawaza hayo ghafla unajikuta umezinduka na hujafanya uliyokuwa unayasema..Na kifo ndio hivyo hivyo kinakuja kama usingizi, wakati unasema bado sitakufa nitatubu tu sasa kumbe tayari umeshaondoka na kujikuta tu umetokezea mahali pengine pa mateso yasiyoelezeka…
Mhubiri 8:8 “ Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; WALA HANA MAMLAKA JUU YA SIKU YA KUFA; Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea”.
Ikiwa hujampa Yesu Kristo maisha yako..na dhambi zinakutesa Kristo yupo sasa kukusaidia…
Kumbuka pia kuzimu ipo!..Mahali ambapo wenye dhambi wote watatupwa kama takataka na kupata mateso yasiyoelezeka… Mlango wa Neema sasa upo wazi..Na mpatanishi wetu sisi na Mungu yupo hai leo,.. Yesu Kristo anakuita utubu dhambi zako zote na akuoshe kwa damu yake na kukupa uzima wa Milele..na kukuokoa na ghadhabu ya Mungu itakayoikumba dunia kipindi sio kirefu tokea sasa..Na yeye Mungu hapendi sisi tuangamie, ndio maana akamtuma mwanawe mpendwa Yesu Kristo..Aje atuokoe sisi bure. Usipuuzie Neema hiyo, ipokee ikufanye kiumbe kipya maadamu unaishi.
Kumbuka tena, mshahara wa dhambi ni mauti. Na matokeo ya mauti itokanayo na dhambi ni kutupwa katika lile ziwa la moto..na chanzo cha dhambi ni Tamaa..
Maran atha. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.
UPAKO NI NINI?
KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.
UWE MWAMINIFU HATA KUFA.
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
Naomba kuuliza mtumishi ni Kwanini Yesu alisulubiwa na wezi wawili pale msalabani?
JIBU: Ni kweli Ilikuwa inajitosheleza kabisa Bwana wetu YESU kufa mwenyewe pale msalabani, lakini kulikuwa na sababu nyingine ya ziada Mungu kuruhusu Bwana wetu asulibiwe na wezi wengine wawili pamoja naye…
Awali ya yote tunapaswa tufahamu kuwa Bwana Yesu alikuja duniani kwa lengo la kutafuta kilichopotea, hiyo ndiyo iliyokuwa kazi yake kubwa.
Mathayo 18:11 [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.]
Hivyo kama Yesu alikuja kukiokoa kilichopotea, basi tufahamu kuwa alimaanisha kweli kweli kusema vile…, kiasi kwamba hata katika dakika ya mwisho ya uhai wa watu waovu Mungu alimweka katikati yao, atimize kusudi lake hilo la kuokoa.. Na ndio maana utaona aliwekwa katikati ya wale wezi wawili kabla ya kufa kwao..Kwasababu Mungu alitamani na wao pia waokolewe hata kama hawakupata neema ya kumsikia akifundisha katika masinagogi, au hekaluni au mijini au vijijini, bali hata hapo pia ipo fursa ya kuokolewa ikiwa watamwamini..
Hata sasa, Kristo hatimizi lengo la kuokoa kwa wale watu ambao pengine wanayo Maisha marefu ya kuishi,… hapana bali pia analitimiza lengo hilo kwa wale ambao anajua wapo katika dhambi nyingi na siku zao za kuishi hapa duniani zinakaribia kuisha, anachofanya huwa anajisogeza karibu sana na wao, kiasi kwamba wakati mwingine anajidhihirisha hata katika mateso wanayopitia ili tu wamwamini yeye waokolewe wasipotee..Kama vile alivyofanya kwa wale wezi wawili, alipitia katika mateso yao yale yale ya kusulibiwa ili tu wamsikilize..
Lakini sasa, cha ajabu ni kuwa katikati ya makundi haya mawili wapo wanaokubali na kugeuka haraka sana..lakini pia wapo ambao badala ya kukubali ndio wanakwenda mbali Zaidi na Mungu, badala ya kutubu ndio wanakufuru Zaidi..
Ndio hapo utasikia mtu anasema, sijui yule kahaba alijuaje juaje siku zake, wiki iliyopita tu, alikwenda kanisani akatubu leo hii tumesikia amepata ajali amekufa,… ukiona hivyo ujue alimtii Kristo katika saa zake za mwisho kama vile yule mwizi wa kwanza..
Mwingine utasikia anasema, alimfukuza mhubiri fulani nyumbani kwake juzi alipokuja kumletea vipeperushi vya injili, na leo hii kwa ghafla tu tumesikia kafa kwa stroke..Mwingine utasikia lisaa limoja lililopita alipokuwa hospitalini anaendelea tu vizuri, mwinjilisti mmoja alikuja akamuhubiria akakubali kutubu, na sasa hivi tunasikia amekufa…n.k. n.k shuhuda kama hizo utazisikia zipo nyingi…utagundua wapo wanaokufuru, wapo wanaotii..
Na ni mara nyingi wanaobahatika kupata hiyo fursa kusikia injili muda mfupi kabla ya kuondoka kwao ni wale ambao hawajawahi kusikia kabisa injili hapo kabla! Au waliisikia kwa juu juu tu, na hawakupata kujua zaidi ingawa walitamani….Hivyo Mungu anawaletea wokovu mpaka ile siku ya kufa kwao. Ili wasife kabla hawajampokea Yesu.
Lakini kwa wale ambao walishasikia na kupuuzia, inakuwa ni ngumu sana kupata hiyo nafasi,….Wakati Bwana Yesu anasulubiwa pale msalabani kulikuwepo na watu wengine mahali pengine wanakata roho..kulikuwepo na watu wengine mahali pengine labda wanachomwa moto kutokana na wizi wao..lakini hawakupata hiyo fursa ya kusogelewa na Bwana wakati wa kifo chao kama ya hawa wezi wawili waliosulubiwa pamoja na Bwana..
Hata mimi na wewe hatujui ni mangapi yapo mbele yetu, pengine tumebakisha wiki, au mwezi, au mwaka, lakini tunaona Kristo anatuhubiria injili kwa nguvu katika hali ya uzima tuliyonayo sasa, katika hali ya kufanikiwa tuliyopo sasa.. pengine kuliko hata alivyowahi kutuhubiria hapo nyuma, Tukiona hivyo tusianze kupuuzia, au kukejeli au kudharau Neno la Mungu, badala yake tukubali kutii na kugeuka haraka sana kama ilivyokuwa kwa yule mwizi wa kwanza,…tukichelewa chelewa, tujue kuwa tunajiweka wenyewe hatarini..Kwasababu katika dunia ya sasa hakuna mtu akifika kule atasema sikusikia injili..Karibi kila mtu kashasikia habari za Yesu…
Kama unaisikia injili sasa ukiwa mzima na unaidharau, mlango wa kutubu wakati wa kufa kwako unakuwa ni mwembamba sana. Ndio maana Biblia inasema saa ya wokovu ni SASA!..Sio kesho wala baadaye..SASA!!
Na Bwana Yesu hafanyi hivyo ili apate sababu ya kutuhukumu hapana badala yake ni ili atupe uzima wa milele na atuepushe na jehanamu..Hivyo kama wewe hujatubu bado na upo nje ya Kristo , muda ndio huu fanya hivyo sasa mpe Kristo Maisha yako, na yeye atakutengeneza na kukufanya kuwa kiumbe kipya..jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ubarikiwe.
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
NI KIPI MUNGU ANACHOKITAZAMA ZAIDI, MOYO AU MWILI?
MTUMAINIE YESU ASIYEISHA MATUKIO.
BUSTANI YA NEEMA.
Upako wa Roho Mtakatifu au kwa kiingereza (anointing of the Holy spirit). Ni neno lenye tafsiri pana kidogo. Linaloweza kumaanisha Nguvu au uwezo wa kipekee mtu anaoupekea kutoka kwa Roho Mtakatifu.. kumsaidia kufanya jambo Fulani kirahisi zaidi,. au kufanya jambo ambalo hapo mwanzo alikuwa hawezi kulifanya.
Kibiblia zamani, mtu kabla hajatawadhwa kuwa mfalme alikuwa anatiwa mafuta,.. kiashirio cha mafuta yaliyomwagwa ndani ya roho yake kama baraka kutoka kwa Mungu ya kumsaidia yeye kuwa mtawala..(2Wafalme 9:6)
Vilevile watumishi wa Mungu kama makuhani, na manabii, nao pia walikuwa wanatiwa mafuta,.. kabla ya kuanza kutumika katika kazi ya Mungu.(Kutoka 29:7, )
Lakini katika agano jipya, vipo pia vigezo vya kutiwa mafuta,.. na vigezo hivyo havitegemei kunyunyiziwa mafuta ya aina yoyote ndani ya mtu,.. Bali kinyume chake ni kwa kuyatenda maagizo ya Mungu..
Tunamwona mtu mmoja katika biblia ambaye Mungu alimtia mafuta(upako) mengi zaidi ya watu wote waliowahi kuishi chini ya jua.. na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO,.. yeye mafuta yale yote aliyotiwa yalikuja juu yake kwa sababu moja tu..nayo ni hii: alipenda haki, na kuchukia maasi.
Waebrania 1:8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele;. Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio. Unaona Kristo, alipenda haki na kuchukia maasi, na ndio maana alitiwa mafuta kushinda sisi wote.
Waebrania 1:8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele;. Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
Unaona Kristo, alipenda haki na kuchukia maasi, na ndio maana alitiwa mafuta kushinda sisi wote.
Vilevile na sisi tukiwa watu wa namna hiyo kama yeye wa kupenda haki na kuchukia maasi.. basi tuwe na uhakika kuwa Mungu naye atatutia mafuta mengi kupita kiasi katika maisha yetu na katika kumtumikia yeye..tutakuwa na upako wa kupita kiasi.
Tofauti na inavyodhaniwa na wengi leo hii, kwamba ukitaka upako,.. ni kwenda kufunga kuomba sana milimani, au kwenda kuwekewa mikono na mtumishi huyu au mtumishi Yule,.. hiyo sio sahihi..Ni vizuri tukifanya hivyo lakini huku nyuma tunafanya yampendezayo Mungu..Lakini kama hatufanya hayo na huku tunatafuta mafuta ya Roho Mtakatifu basi tuwe na uhakika kazi tunayoifanya ni bure..
Ni lazima kwanza tujazwe Roho, na Kujazwa Roho si kwa kunena kwa lugha,. bali ni kwa kulitii Neno la Mungu kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo,.. yaani kuwa watakatifu kama jina lake mwenyewe Roho Mtakatifu lilivyo..Ndipo hapo na yeye ataachilia mafuta yake(upako) ndani yetu.
Hivyo kama wewe bado huna Roho wa Mungu ndani yako, fahamu kuwa huwezi kufanya jambo lolote,.. huwezi kuyaelewa maandiko, huwezi kuishinda dhambi, wala huwezi kumtumikia Mungu..Vilevile huwezi kwenda mbinguni haijalishi unajitihada kiasi gani..
Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.
Lakini ikiwa utapenda Bwana akupe kipawa hicho, basi fahamu kuwa kipawa hicho ni bure,,, na wala hakiihitaji kutumia nguvu kukipata..Jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kutubu kwanza kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote,, kisha ukishatubu sasa na kusema kuanzia leo, mimi na ulimwengu basi, na kuanza kumtazama Kristo,. na kutaka kujifunza Neno lake kwa bidii..Mungu akishaona umegeuka na kuacha uliyokuwa unayafanya basi atakusamehe,. na AMANI YA AJABU itaingia ndani yako..Na yeye atasimama kukusaidia kwa namna ambayo hujawahi kuiona katika maisha yako.
Kisha bila kupoteza muda nenda katafute mahali utakapobatizwa katika ubatizo sahihi.. wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la YESU KRISTO,. sawasawa na (Matendo 2:38) ili uukamilishe wokovu wako, na kumruhusu Roho Mtakatifu kuingia ndani yako, na kuweka makao yake milele ndani yako..
Ukishafanya hivyo kwa moyo wa dhati bila kigugumizi, basi fahamu kuwa Roho wa Kristo ameshaingia ndani yako,. muda mfupi baadaye atakushushia vipawa vyake., kwa jinsi apendavyo yeye, aidha lugha, aidha maono, aidha ndoto, aidha uinjilisti,au unabii n.k.. Wewe tu mwenyewe utaona badiliko ndani yako siku baada ya siku..atakuwa anakufundisha na kukuongoza katika njia ya kweli yote, kwasababu yale mafuta yake tayari ameshayamwaga ndani yako.
1Yohana 2: 27 “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote., tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.
Hivyo atakufundisha, na kukupa upako halisi unaotoka kwake, na sio ule feki unaouzwa na manabii wa uongo katika chupa,. na vifungashio mabarabarani, upako unaotoka kuzimu, usioweza kuyageuza maisha yako.
Fanya hivyo, Na Bwana akusaidie katika kukamilisha hatua zote hizi.
Amen.
UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZAA MATUNDA.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
SIKU ILE NA SAA ILE.
Je! hizi roho saba za Mungu ni zipi? na je zinatofautiana na Roho Mtakatifu?
ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.
Kijito cha Utakaso, Ni kijito cha Damu ya Yesu, kidhihirishwacho kwa ubatizo wa maji mengi..Kama vile Maji ya farakano yalivyotumika katika Agano la kale kutakasa, katika Agano jipya yanatumika maji ya ubatizo.
Katika Agano la Kale, ilikuwa hata kugusa tu maiti, mtu tayari ameingia Unajisi, hivyo ilimpasa akafanye utakaso kwanza kabla ya kuingia katika kusanyiko la Bwana..
Hesabu 19:11 “Mtu agusaye maiti ye yote atakuwa najisi muda wa siku saba; 12 naye atajitakasa kwa yale maji siku ya tatu, na siku ya saba atakuwa safi; lakini kama hajitakasi siku ya tatu, ndipo na siku ya saba hatakuwa safi. 13 Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado”.
Hesabu 19:11 “Mtu agusaye maiti ye yote atakuwa najisi muda wa siku saba;
12 naye atajitakasa kwa yale maji siku ya tatu, na siku ya saba atakuwa safi; lakini kama hajitakasi siku ya tatu, ndipo na siku ya saba hatakuwa safi.
13 Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado”.
Na kulikuwa pia na sheria kali kwa mtu ambaye atakataa kujitakasa kwa kujiosha katika mji yaliyoamriwa. Ambayo ni maji ya farakano (Au maji ya Utakaso kwa jina lingine).
Hesabu 19:20 “Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa Bwana; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yu najisi”.
Katika Agano jipya, watu wote ambao hawajampa Yesu Kristo maisha yao, au kwa lugha rahisi HAWAJAOKOKA!..Hao ni watu najisi mbele za Mungu…Hivyo hawastahili hata kumwabudu Mungu katika hali walizopo, hawastahili hata kumsogelea Mungu wala kuuliza kitu chochote kutoka kwake..Watu wengi sana hawalijui hilo…
Ezekieli 14:3 “Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote? 4 Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake”
Ezekieli 14:3 “Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?
4 Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake”
Na wala hawawezi kumwomba Mungu wala kumtolea sadaka..kwasababu ni Najisi…
kumbu.23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”
Ni kitu gani kinachowafanya wawe Najisi?
Jibu Ni dhambi zilizomo ndani yao ndizo zimewafanya wawe NAJISI, machoni pa Mungu…Biblia inasema katika..
Marko 7:21 “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, 22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. 23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.
Marko 7:21 “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.
Unaona?..Dhambi ndizo zinazomtia mtu unajisi mbele za Mungu..Na Watu najisi hawawezi kumsogelea Mungu hata kidogo..Na watu najisi ni watu wote watendao dhambi, (yaani ambao hawajaokoka)...watu wote wenye chuki, wasengenyaji, waasherati, wezi, wavaaji vimini, suruali, nguo fupi na zilizo nusu uchu, wote wajipakao wanja, lipstick, na kuvaa wigi n.k...Mungu huwa anajificha uso wao wasimwone, maombi yao yanakuwa hayajibiwi…Kwakuwa ni Najisi mbele za Mungu.
Isaya 59:1″ Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. 3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”
Isaya 59:1″ Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”
Sasa watu wa Agano la kale walitakasika kwa kuoshwa kwenye maji…Lakini sisi watu wa Agano jipya wanatakasika kwa kuoshwa kwenye kijito cha Damu ya YESU. Kijulikanacho kama KIJITO CHA UTAKASO.
Katika kijito hicho cha utakaso, Mtu atazama na kuoshwa katika hicho na unajisi wake wote unaondoka..
Kwanza kwa kutubu: kutubu maana yake ni kukiri kwamba ulikuwa mkosaji na hivyo umeamua kugeuka na kuacha kufanya uliyokuwa unayafanya…Hicho kinafananishwa na kitendo cha kuvua nguo zako zote kabla ya kuingia kuoga kwenye kijito chochote kile.
Pili: Unajitosa kwenye kijito cha Utakaso..Kijito hicho ni Ubatizo wa Maji mengi ..Yaani baada tu ya kutubu, hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi… Kumbuka ubatizo sahihi sio wa kunyunyiziwa maji, au sio wa utotoni wala sio wa Baba, mwana na Roho Mtakatifu..Ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa mwili wote katika maji mengi sawasawa na Yohana 3:23.. na katika jina la YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38).
Kwa kuzama katika kijito hicho..Kwa nje utaonekana kama umezama kwenye maji ya ubatizo lakini katika Roho utaonekana umezama katika kijito cha damu ya YESU.. Kuzamishwa mwili wote katika maji mengi ni ishara inayoonesha umezamishwa roho yako katika kijito cha damu ya Yesu kiletacho utakaso…Na hivyo dhambi zako zote zitakuwa zimeondolewa kwa tendo hilo..Na hautahesabika kuwa najisi tena mbele za Mungu.
Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”
Je unastahili kumsogelea Mungu? au je wewe ni najisi?..Kama bado hujachovya kwenye hicho kijito cha utakaso unasubiri nini?..Tubu leo mwambie Bwana Yesu leo nakuja mbele zako, mimi ni mkosaji, naghairi mabaya yangu yote leo,..Naomba unisamehe dhambi zangu zote…..Nakuomba unipokee sawasawa na Neno lako lisemalo kwamba “wote wajao kwako hutawatupa nje kamwe”..Nakuomba unipe neema ya kukujua wewe siku zote za maisha yangu. Amen.
Ukiwa umeomba hivyo au hata zaidi ya hivyo..Basi fahamu ya kuwa Mungu si mwongo..Ameshakusamehe haijalishi dhambi zako zilikuwa ni nyingi kiasi gani..
Sasa hatua inayofuata ni ya MUHIMU SANA. Nenda katafute Ubatizo sahihi kwa hali na mali..Umejifunza hapo juu, maana ya kijito cha Utakaso..Kitafute hicho kwa hali na mali…Kama unafahamu mahali unaweza kupata huduma hiyo ya ubatizo fanya hivyo haraka, maana shetani hapendi kuona unakwenda mbinguni…Na kama hufahamu basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312 tutakuelekeza mahali karibu ni ulipo..ambapo unaweza kupata huduma hiyo.
Kumbuka Biblia inasema katika..1Wathesalonike 4:7 “Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso”.
Na tena Inasema…
Waebrania 10:10 “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu”.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
Nini maana ya kusali kwa kupayuka payuka?
WhatsApp
Mwananchi ni mtu aliye na uraia wa Nchi fulani.
Kwamfano mtu aliyezaliwa Taifa la Tanzania ni mwananchi wa Tanzania, Kadhalika lipo Taifa la kimbinguni..Na hilo yeyote anayezaliwa katika Taifa hilo anaitwa Mwananchi wa Taifa la Mbinguni..Na kila mwananchi analindwa na katiba.
Biblia inasema katika..
1Petro 2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, Taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema”.
1Petro 2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, Taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema”.
Huwezi kuzungumzia Taifa bila kuhusisha mwananchi wa hilo taifa. Palipo na Taifa ni lazima pawepo na wananchi..Na Taifa la Mbinguni lina wananchi wake.
Hebu tuzitafakari dondoo chache hizi muhimu, ili zitusaidie kuelewa ni namna gani ufalme wa Mbinguni unafanya kazi.
Hivyo tupo tayari sasa kujifunza juu ya upande wa Pili wa uraia wa MBINGUNI. Kumbuka mbingu ni Taifa kama tulivyosoma hapo juu..Kwahiyo hebu tutafakari pia dondoo chache zifuatazo ili tuelewe zaidi.
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 6.16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 6.18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 6.16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 6.18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
Hivyo Mwananchi yoyote wa Ufalme wa mbinguni hana budi Kuifahamu katiba kikweli kweli…Kama vile ilivyo jukumu la kila mwananchi kuifahamu katika ya nchi yake.
Madhara ya kutoifahamu biblia(Neno la Mungu) kwa Mwananchi wa Taifa la Mbinguni,.hayatofautiani sana na madhara ya mwananchi wa kawaida kutoifahamu katiba.
Mwananchi asiyeifahamu katiba, ni rahisi kufanya makosa na asijue kama anafanya makosa..Ni rahisi kwenda kulala na ndugu yake wa damu, na wakati hajui sheria ya nchi (katiba) inasema kwamba ni kosa mtu yeyote kulala na ndugu wake wa damu, hukumu yake ni kifungo cha maisha.
Kadhalika anaweza akagombana tu na ndugu yake na kwa hasira akaenda kumchomea nyumba yake, pasipo kujua katiba inasemaje kwa mtu anayepatikana kwa kosa la kuchoma nyumba..Kosa la kuchoma nyumba kulingana na sheria ya nchi yetu, hukumu yake ni kifungo cha maisha. Sasa mambo madogo tu kama hayo yanaweza kumsababishia akapoteza maisha yake yote kutumikia vifungo.
Vivyo hivyo mwananchi wa Taifa la mbinguni asipoielewa katiba ya mbinguni (yaani biblia) inasema nini, anaweza kujikuta anafanya mambo akidhani anampendeza Mungu kumbe anamchukiza Mungu pakubwa..na adhabu yake ikawa ni ziwa la moto milele..Mtu anaweza akawa ni mlevi akidhani ulevi si dhambi..anaweza akawa mwasherati akidhania uasherati sio dhambi..anaweza akawa mwabudu sanamu akidhani sio dhambi..n.k
Pia madhara mengine ya kutoijua katiba ni KUONEWA NA KUNYANYASWA. Mwananchi asiyeijua katiba ya nchi yake hata mtu akija tu anaweza kumtishia na kumnyima haki yake..lakini kama anaijua hawezi kubabaishwa kwasababu anaelewa vizuri sheria za nchi..Hivyo ni ngumu kupoteza haki yake..Vivyo hivyo Mwananchi wa Ufalme wa mbinguni asipoielewa vizuri biblia ni rahisi adui shetani kumnyang’anya haki yake. Utaona anapelekeshwa huku na huku, majaribu haya na yale..kuteswa huku na kule..Yote hayo ni kwasababu haijui biblia Neno la Mungu.
Na Dondoo ya mwisho kabisa ni kwamba kila mtu ili awe Mwananchi halali wa Taifa hilo ni lazima awe amezaliwa katika hilo Taifa (Huo ndio utambulisho wake wa kwanza),.. Vivyo hivyo katika Uraia wa ufalme wa mbinguni..Ni lazima mtu azaliwe katika ufalme huo.
Na mtu hazaliwi kwa damu na nyama, bali anazaliwa kwa Roho na kwa Maji ndipo ahesabike kuwa ni Mwananchi wa Taifa la Mbinguni.
Maana ya kuzaliwa kwa maji ni kubatizwa kwa maji mengi (Yohana 3:23) Na kwa Jina la Yesu (Matendo 2:38). Na maana ya kuzaliwa kwa Roho ni kupata ubatizo wa Roho Mtakatifu. Hatua hizo mbili ndio zinazokufanya uwe umezaliwa mara ya pili na kuwa Mwananchi wa ufalme wa Mbinguni.
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Je umezaliwa mara ya PILI?. Je wewe ni Mwananchi wa Taifa teule la kimbinguni..Je wewe ni mrithi?..Kumbuka FALME NA MATAIFA YA DUNIA YOTE YATAPITA…Lakini UFALME WA MBINGUNI UTADUMU MILELE..NA RAIA WAKE WATADUMU MILELE!!.
Yapo mengi ya kujifunza juu ya ufalme huu wa mbinguni tukilinganisha na ufalme wa duniani..lakini Muda usingetosha kuyaandika yote hayo, lakini kwa haya machache, yatatupa chachu ya kuzidi kuutafuta ufalme wa mbinguni kila siku kwa bidii.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAP
Tafadhali share na wengine.
INJILI NI NINI?
Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?
UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.
JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie katika Ufunuo 19:10 alikuwa ni nani, Je! ni Mwanadamu au Malaika?
Ufunuo 19: 10 “ Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii”.
Mtu anayetumika kama wewe huyo ni Mjoli wako. Mfanyakazi anayefanya kazi kama ya kwako huyo ni mjoli wako na wewe ni mjoli wake…Hivyo katika Mstari huo hapo juu Yohana alikuwa anataka kumsujudia yule aliyekuwa anazungumza naye,aliyekuwa anamwonyesha maono yale…Lakini akamzuia na kumwambia mimi ni mjoli wako (maana yake ninayafanya kazi kama ya kwako ya utumishi)..na pia wa ndugu zako (yaani wanadamu wenzake ambao ndio sisi tulio na ushuhuda wa Yesu).
Kwasababu Biblia inasema Malaika ni roho watumikao..wanaotuhudumia sisi(Soma Waebrania 1:3-14)..Kadhalika na sisi wanadamu tunaomtumikia Mungu ni Watumishi wa Mungu vile vile…tunaotumika katika Ufalme wa Mbinguni..Hivyo sisi pamoja na malaika ni Watumishi wa Mungu wa mbinguni…Kwahiyo sisi ni wajoli wa Malaika na Malaika vile vile ni wajoli wetu.
Kwahiyo tukirudi kwenye hilo swali linalouliza.. “aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?”…Jibu lake ni kwamba alikuwa ni MALAIKA. Kwasababu Yohana tangu mwanzo alikuwa haonyeshwi maono yale na mwanadamu yoyote…bali Malaika ambaye naye huyo Malaika aliyapokea maono hayo kutoka kwa Yesu Kristo mwenyewe. Hakuna mwanadamu yoyote aliyehusika hapo kwa namna moja au nyingine..
Ufunuo 1:1 “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma KWA MKONO WA MALAIKA akamwonyesha mtumwa wake Yohana”
Wapo watu wanakosa shabaha katika hilo kudhani kuwa Yule alikuwa ni mtakatifu Fulani aliyekufa zamani au aliyepaa pengine Musa au Eliya, au Nabii Fulani, kwamba ndiye aliyemwambia maneno hayo asimsujudie kwa kuwa yeye ni mjoli wake na wa ndugu zake walio na ushuhuda wa Yesu. Japo ambalo si la kimaandiko..Lakini sasa tunajua kuwa yule hakuwa mwanadamu bali ni Malaika wa mbinguni.
UFUNUO: Mlango wa 19
DANIELI: Mlango wa 1
ESTA: Mlango wa 1 & 2