BWANA ANAPOTUKASIRIKIA, ANA LENGO ZURI NA SISI.

BWANA ANAPOTUKASIRIKIA, ANA LENGO ZURI NA SISI.

BWANA ANAPOTUKASIRIKIA ANA LENGO ZURI NA SISI NDANI YA MOYO WAKE.

Marko 3:5 “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.

6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Neno la Mungu ndio chakula kitupacho uzima wa milele,. hivyo tunapochukua muda kulitafakari kila siku,. basi tunafanya jambo ambalo faida yake hatutaiona hapa peke yake, bali hata miaka miaka trilioni moja mbele.

Leo kwa neema za Mungu tutaangazia jambo moja kwa ufupi juu ya Hasira ya Kristo..Tukiyatafakari hayo maneno hapo juu tunaona kuna wakati Bwana alikwenda kwenye sinagogi na kukutana na mtu ambaye alikuwa na mkono uliopooza…

Lakini alipotaka kumponya, aligundua kuwa Mafarisayo na Maherodi walikuwa wanamzivia ili wamjaribu kama atamponya mkono wake siku ya sabato, ili wapate kumshitaki..Lakini yeye alipogundua hilo akakasirika sana, akatulia kwa muda akiwaangalia wale watu kwa hasira..kuanzia kushoto kwake mpaka kulia kwake, wale waliokuwa mbele yake, hadi wale waliokuwa nyuma yake… wote aliwaangalia kwa makusudi ili wauone uso wa Kristo ulivyojaa hasira..

Embu tafakari mfano na wewe ungekuwa upo na wale mafarisayo, ungemwonaje Kristo?..

Ni rahisi kusema huyu mtu kashaanza kutuchukia,. Au huyu mtu anakinyongo Fulani ndani yake kwa ajili yetu, lakini tunasoma biblia inasema, ndani ya moyo wake,. Alikuwa na huzuni kubwa kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao.. Alikuwa anawaonea huruma ndani ya moyo wake, alikuwa anawapenda upeo na hivyo hataki wapotee na ndio maana japokuwa uso wake ulikuwa umejaa hasira nyingi,.. Lakini moyoni mwake alikuwa unadondosha machozi mengi ya huzuni.. Hiyo ndio hasira ya kweli ya ki-Mungu.

Mungu anapokukemea kwa ajili ya dhambi zao, usidhani kuwa Mungu anakuchukia, au anakutesa, au ni mkatili,. uso wa Mungu unapogeuka kwako, usidhani kuwa Mungu hakupendi, lakini badala yake anafanya hivyo kwasababu anataka ugeuke usipotee, moyoni mwake anakuthamini kushinda wewe unavyodhani..(kumbuka tena Bwana anapotukasirikia ana lengo zuri na sisi)

Mungu anapokuambia, uzinzi unaofanya utakupeleka kuzimu, usidhani anakuchukia,. Anapokuambia, rushwa unayokula, ushirikina unaoufanya, matambiko na kafara unazozitoa, moja ya hizi siku utakwenda kuchomwa katika moto usiozimika,. Sio kwamba anakuchukia, anapokuadhibu kwa dhambi zako, na kumwona Mungu kwako kama ni mkatili mwenye uso wa hasira sikuzote kwako..Furahia ni kwasababu anakupenda, na anataka ubadilike..wakati mwingine anakunyang’anya hata baadhi ya vitu ulivyonavyo, au unamwomba hakupi hata kimoja,. Sio kwasababu hakujali, au hakuoni, hapana, Kaonyesha uso wa hasira nyingi kwako kwasababu njia zako ni mbaya..

Biblia inasema..

Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

Unaona hapo? Anasema “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi”..

Mungu akikupenda hata acha kuonyesha uso wa hasira kwako, hataacha kukuonya juu ya dhambi zako, kama vile leo hii anavyokuonya.. Anakueleza ukiendelea kuvaa nguo za nusu uchi utaishi jehanamu ya moto,. ukiendelea kutazama pornography utaishi jehanamu ya moto, ukiendelea kwenda disko utakufa siku moja na kushukia kuzimu…kwasababu anasema wote niwapendao! anawakemea.

Hivyo usishupaze shingo yako,. bali utubu leo hii, mgeukie Bwana wako, ili uugeuze uso wake wa hasira na kuwa wa furaha. Unachotakiwa kufanya ni kujisalimisha kwa Bwana, ukiwa na mzigo wa dhambi zako, na kumwambia, nisamehe nimekosa Mungu wangu na leo hii ninataka kuanza upya tena..Ninaacha hiki, ninaacha kile kwa kumaanisha kabisa..

Kisha ukishafanya hivyo, anza kuonyesha kweli kuwa umetubu.

kwa kuanza kujishughulisha na mambo ya Mungu na kukaa mbali na dhambi ulizokuwa unazifanya hapo kabla,. kama ni nguo za kizinzi unazichoma, kama ulikuwa unaishi na mke/mume ambaye si wako unamuacha.. kama ulikuwa unakwenda bar, unaacha, kama ulikuwa unatazama picha chafu mitandaoni unazifuta,.. kama ulikuwa unafanya uasherati na girlfriend au boyfriend hamjaona, unaacha, kisha unaanza kutafuta ndugu wa kikristo na kukaa nao,..

Sasa Mungu akishaiona Imani kama hiyo, na toba yako iliyoambatana na matendo kama hayo,. yeye mwenyewe kuanzia huo wakati anachukua jukumu la kukufanya kuwa mwana wake kweli kweli, atakupa uwezo wa ajabu wa kuweza kuyashinda hata yale ambayo ulikuwa huwezi kuyaacha..Na mwisho wa siku utajikuta umeshaimarika ndani ya Kristo kwa viwango vya juu sana.

Lakini pia kumbuka, mara baada ya kutubu kwako unapaswa ukabatizwe,. na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi (Yohana 3:23), na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38,.Ubatizo sahihi ni muhimu, fanya hivyo na hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili.

Kumbuka anasema wote niwapendao nawakemea au kwa lugha wote niwapendao niwaeleza ukweli..Hivyo umeusikia leo ukweli. Kubali na kugeuka.

Marko 3:5 “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao”

Ubarikiwe. Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

WOKOVU NI SASA

UPAKO NI NINI?

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Devis Julius administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments