Ulishawahi kujiuliza ni nini Mungu anafundisha wana wa Israeli nyuma ya agizo hili? Tunalolisoma katika Kumbukumbu 22:6
“Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; 7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.
Bwana aliwapa agizo, endapo mtu yeyote akipita, njiani au karibu na kichaka, kisha akakutana na kiota cha ndege koo kimelala pale karibuni, kinatekeka kirahisi, kiasi kwamba unaweza kuwachukua wote, bila nguvu yoyote.Basi hapo, walipewa sharti, wasiwe na tamaa ya kuwachukua wote, bali wamwache koo aende zake akaendeleze uzao, lakini wale makinda anaweza kuwachukua na kuwafanya wake. Hivyo kwa kitendo hicho tu, mtu anajiongezea siku za kuishi duniani.
Ufunuo wake ni upi Katika Ukristo na katika maisha?
1) Katika Maisha.
Ni mara ngapi tunaona watoto wa jamaa zetu, wamekuwa mayatima, au wazazi wao wapo katika hali ya kutojiweza kupitiliza, mpaka wanashindwa kuwamudu watoto wao, lakini sisi tunapita hatuna muda nao kisa tu sio sisi tuliowazaa . Tunawaona watoto wale wakiangamia pamoja na wazazi wao. Bwana anatushauri, tusifanye hivyo, ni heri tusiwajali wale wazazi, tuwaache, tusiwape kitu chochote, lakini wale watoto tuwahurumie, kwani tukifanya hivyo, Mungu atatubariki na kutuongezea siku za kuishi duniani.
Watu wengi tunadhani, kuwaheshimu tu wazazi, ndio tunapata siku nyingi za kuishi, lakini ukweli ni kwamba, ukiwajali pia watoto wa asiyejiweza, utajiongezea siku pia za kuishi duniani.
2) Katika ukristo.
Vilevile katika ukristo. Ipo mikusanyika mingi, Yapo makanisa mengi, zipo huduma nyingi, ambazo haziwaweki watu katika mstari wa wokovu wa kweli, viongozi wao ni vipofu, hivyo na wale wanaoongozwa pia watakuwa ni vipofu, na mwisho wa siku wote watatumbukia shimoni. Sasa ikiwa wewe ni mchungaji au mkristo, na unaona mwenzako mahali alipo anapotezwa..Usikae kimya, na kusema wale sio washirika wangu, au wale sio wa dhehebu langu, au wale sio wa dini yetu..Bali unapaswa kuwaeleza ukweli, uwavute katika mahali sahihi ili uokoe roho zao..
Yawezekana ikawa ni ngumu kumgeuza kiongozi, hivyo usihangaike naye sana ikiwa utashindwa kumfikia, lakini wale makinda hakikisha unawajuza njia sahihi. Hiyo itakuongezea siku zako za kuishi hapa duniani.
Katika siku hizi za mwisho, watu wengi wamewekwa sehemu za hatari, wengine wameaminishwa katika watu, wengine vitu, wengine katika dini, wengine taasisi..lakini Kristo hayupo kabisa mioyoni mwao. Hawamjui, hawalifahamu Neno, hawajui nyakati wanazoishi, dini walizopo ni za kipagani. Sasa hii ni hatari sana, tunapoona wakiendelea katika kudanganywa na viongozi wao ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao. Hivyo sisi tuwe wa kwanza kulihubiria hili kundi la Mungu, litoke huko lirudi kwenye Neno.
Bwana atusaidie shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KOIKOI ANGANI AJUA NYAKATI ZAKE ZILIZOAMRIWA.
Uzima wa milele ni nini?
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.
MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.
Thenashara ni nini? (Marko3:16)
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Naomba kufahamu vifungu hivi tunavyovisoma katika Isaya 24:18-20 vinamaana gani?
Isaya 24:18 “Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika. 19 Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana. 20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.”
JIBU: Mstari hiyo inatupa picha ya dunia ilivyosasa katika hali ya roho. Imefananishwa na mlevi ambaye amelewa sana, na hivyo hawezi kujimudu tena.
Kama tunavyofahamu, mlevi kabla ya kudondoka mtaroni na kulala hapo hapo, huwa unayumba yumba sana, anapepesuka sana, hatua moja mbele, kumi nyuma, kwenda kulia, kwenda kushoto, hiyo yote ni anatafuta uwiano lakini anaukosa kwasababu kichwa chote kimeshatiwa uzito, kila kitu kilichombele yake anakiona kama kimegeuzwa juu chini..
Hivyo kutembea kwake, hakuhusishi tena ubongo, bali uzoefu, na hatari zaidi pale atakapo jikwaa tu kidogo na kuanguka, basi safari yake inakuwa imeishia hapo, hawezi tena kunyanyuka, mpaka atakapolevu asubuhi.
Ndivyo dunia, ilivyo rohoni, nyakati hizi tulizopo, imelevywa sana kwa dhambi za wanadamu, na hivyo imepoteza muhimili wake, tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo, hatushangai sikuhizi kuona, majangwa mengi, ukame uliopitiliza, matetemeko makubwa ya ajabu, magonjwa ya kutisha kama Korona, Ebola kuzuka, mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo. Sasa haya yote hayajajizukia hivi hivi tu, bali ni kuleweshwa kwa dunia kwa dhambi zinazoendelea kuwa nyingi.
Ndugu yangu, tupo katika hatari kubwa; Hatari ya “hofu, mashimo, na mitego”, kama hayo maandiko yanavyosema, Ikiwa na maana kama tupo nje ya Kristo tujiandae, kukutana na mambo haya katika maisha yetu. Mtu ambaye hajaokoka, ni kwa neema za Mungu tu anaishi hadi sasa kwenye dunia hii inayowaya-waya kama machela.
Lakini kama tumeokolewa Bwana ameahidi kutuepusha nayo. Kwasababu unyakuo wa kanisa upo karibuni sana kutokea. Na baada ya hapo, ndipo huu ulimwengu utaanguka kabisa..
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Je! Unasubiri nini, usimkaribishe maishani mwako? Je! Unauhakika wa kesho? Vipi ikiwa utakufa leo, au Kristo amerudi ghafla sasa hivi utasema nini rafiki.. Kumbuka mipango yote ya mpinga-Kristo ipo tayari, injili imeshahubiriwa duniani kote, dakika tulizonazo ni za nyongeza tu, wakati wowote, parapanda italia, na hali halisi ilivyo tusidhani tuna miaka mingi mbele, muda umeisha kwelikweli, usipumbazwe na mambo ya ulimwengu ukadhani, Yesu harudi hivi karibuni. Ni kwasababu husomi biblia ndio maana unadhani hivyo. Injili ya sasa sio ya kubembelezwa tena, ni mtu mwenyewe kuona na kugeuka, na kuyasalimisha maisha yako. Sio wakati wa kutanga tanga, na maisha bali ni kumtafuta Mungu.
Bwana atusaidie.
Maranatha.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UNYAKUO.
MFALME ANAKUJA.
TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
Je! Bwana Yesu alikunywa kileo mpaka watu wakasema ni mlafi na mlevi? Kulingana na Mathayo 11:19?
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Ni siku nyingine tena yenye neema za Bwana.
Napenda leo tujifunze, ni nini kwanza Bwana anahitaji kuona kwetu kabla ya yeye kuachilia neema zake katika mambo tumwombayo au tuyatafutayo. Embu tusome habari hii kwa mara nyingine tena..
Luka 5:4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. 5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; 7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. 8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. 9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;”
Kumbe Bwana Aliona taabu ya Petro usiku ule ilivyokuwa, aliona kule kutafuta kwake usiku kuchwa pasipo mafanikio kulivyokuwa. Alipokuwa anatupa nyavu hapati, anajaribu tena hapati, anasogea sehemu nyingine avue ndio anakosa kabisa mpaka kunapambazuka, haambulii chochote..
Na ndio maana hatushangai jambo la kwanza Yesu alilomwambia Petro mara baada ya kuhubiri kwake, sio Petro twende shambani kwako nikakubariki, au twende tukahubiri injili, ..Hapana bali tweka vilindini ukavue samaki, nikabariki kwanza kwa kile ulichokuwa unakisumbukia kwa muda mrefu..
Hata sasa Kristo ni Yule Yule, kabla ya kutupigisha hatua yoyote kiroho..Hatuna budi kwanza tufanye kazi ya kuchosha usiku kucha, wakati mwingine bila mafanikio yoyote. Watu wengi wanataka Mungu atembee nao kwa viwango vya juu zaidi, lakini hawapo tayari kutaabika kwanza, hawapo tayari kutumika kwanza, katika utumishi wa Mungu kwa muda mrefu, tena ule ambao hauonyeshi matunda yoyote ya awali, lakini tunataka tulale, tuamke kesho tuwe kama Musa.
Huduma nyingi zimekufa kwa namna hii, pale wanapoona hakuna maendeleo au hatua zozote, mwishowe wanakata tamaa ya kumtumikia Mungu, wanavunjika moyo, wanaghahiri, wanakwenda kutafuta shughuli nyingine.
Ndugu, Hatuna budi kufahamu wakati mwingine ni desturi ya Mungu kutuacha kwanza, kwa kipindi Fulani, atupime uaminifu wetu, lakini pia atutengeneze, si kila wakati mambo yote yatakuja papo kwa papo kama wengi wanavyosema, yaweza kuchukua mwaka kama sio miaka, lakini tukivumilia, siku isiyokuwa na jina tutashangaa vile tulivyovitamani, tunavipata kwa urahisi sana, tena bila kusumbukia, wala kuchukua muda kama ilivyokuwa hapo mwanzo, Hatua kama hiyo ukishaifikia, ujue tayari Kristo ameshaona utumishi wako. Lakini lazima tufanye kazi ya kuchosha usiku kucha.
Waweza kusema, jambo kama hili alilifanya siku hiyo tu ya kwanza alipokutana na Petro, lakini utaona mwishoni kabisa mwa huduma yake kuwa nao, baada ya kufufuka kwake, mitume kwa mara nyingine tena walienda kuvua samaki, lakini usiku ule wote hawakupata kitu, ilipofika asubuhi wakamwona Yesu amesimama pwani, ndipo akawauliza wanangu mna kitoweo? Wakasema hapana, akawaambia watupe jarife upande wa kulia watapata (Yohana 21:1-13)
Na kweli samaki ambapo waliwasumbukia usiku kuchwa, wakawapata kwa dakika tano, tena sio kule vilindini bali pale pale pwani. Unataka Mungu aikuze huduma yako, tumika kwanza kwa Bwana, fanya uinjilisti sana, hata kama huoni mtu yeyote ameokoka leo au kesho, wakati wa Bwana ukifika, utaona maajabu. Lakini ukikata tamaa, ukasema sioni chochote, Kristo atasema hustahili kupokea neema.
Wewe ni mwimbaji wa Injili, imba sana, dumu kwa uaminifu kufanya mazoezi, tunga, jifunze kwa moyo wako wote, nyimbo za utakatifu, na kuponya,bila ulegevu, hata kama utaambiwa hujui kuimba,wewe imba sana, hata kama miaka 10 itapita bila kuona kazi yako inamponya mtu..endelea tu, wakati utafika wa Bwana kuachilia neema yake, ataibariki sauti yako, na kuwa msaada ya maelfu ya watu duniani. Sauti itakuwa ni ileile lakini itajazwa neema na nguvu.
Kuna wakati ambao Yesu alipowalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, waende ng’ambo, usiku ule bahari iliwachafukia, lakini maandiko yanatuambia Yesu aliwaona wakitaabika katika kuvuta makasia, lakini hakufanya chochote, mpaka usiku sana wa manane ndio akawafuata akiwa anatembea juu ya maji. Ndipo akawatulizia dhoruba yao. (Marko 6:45-52).. Katika habari ile utajiuliza ni kwanini Yesu awaache wataabike, muda wote ule bila kuchukua hatua..jibu ni kuwa alikuwa anawajengea ushuhuda. Nasi pia Kabla ya Yesu kuzimisha dhoruba katika maisha yetu, na kutupa amani daima, yatupasa tuwe wastahimilivu sasa katika majaribu mengi na shida kwa ajili ya jina lake.
Luka 6:21 “Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka”.
Jambo lolote la ki-Mungu unalopenda kulifanya, litende kwasababu Mungu anataka kuona kwanza kiu yako kwenye hilo jambo. Vilevile kama unataka Mungu akubariki, penda kutoa bila kutazamia malipo yoyote sasa, toa tu, hata kama ni kwa miaka, unaona unapata hasara tu, usikate tamaa, malipo yake utayaona wakati Fulani mbeleni, Bwana atakapoachilia neema zake.
Hii ni kanuni ya Ki-Mungu, aliitumia kwa, kwa Ibrahimu, Kwa Yusufu, kwa Musa, hata na kwetu pia anaitumia ikiwa tutakubali kwanza kufanya kazi ya kuchosha isiyokuwa na faida kwa muda mrefu.
Usikate tamaa, Bwana awe nawe.
Shalom
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
Je! Siku ilihesabiwaje kabla ya jua na mwezi kuumbwa?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
Sehemu ya 1
Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya”.
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima; Huu ni mfululizo wa makala, zinazochambua baadhi ya maneno au vifungu, ambavyo vimekuwa vigumu kwetu sisi kuvielewa kuhusiana na Mungu. Na hiyo imepelekea hadi baadhi ya watu wasimwamini kabisa Mungu na wengine kusema inakuwaje Mungu mwenye uwezo afanye vitendo kama hivi, au aruhusu mambo kama haya?
Hivyo katika makala hizi, tutaangazia uhalisia ya vifungu hivyo; Na tutapata amani katika hayo.
Kuna wakati Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno haya;
Yohana 13:7 “Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye”.
Ikiwa na maana kuna mambo ambayo Mungu anayafanya , kamwe hatutakaa tuyaelewe kwa sasa, bali baadaye sana. Na “Baadaye”, inaweza kumaanisha kipindi kirefu kijacho, au wakati wa baada ya haya maisha.
Hivyo basi, hakuna mwanadamu anayeweza kutolea majibu kila jambo analolisoma kuhusu Mungu, isipokuwa tu tunapapasa-pasaka, na kuelewa yale tuliojaliwa kuelewa na Roho Mtakatifu kwa sasa (Matendo 17:27).
Leo kwa sehemu tutaona, kwanini Mungu alisema maneno haya.
Sehemu: Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya”.
Swali linaloulizwa hapo, Je! Ni kweli Mungu aliwaumba wabaya ili kutimiza kusudi la ubaya?
Jibu ni ndio kama ilivyoandikwa.
Utauliza, ni kwanini sasa aseme yeye ni Mungu wa upendo, apendezwaye na haki? . Jibu ni lile lile, afanyalo leo hatutalijua, sasa lakini tutalijua vizuri baadaye. Na mawazo yake si mawazo yetu.
Ni vichache tu tunaweza kujua kwanini amewaumba watu wabaya kama ibilisi na mapepo yake, na waovu kama akina Kaini, kora, Belshaza? Ili wafanye mabaya duniani?
Majibu tuliyopewa kuyaelewa, ni ili kutimiza makusudi yake matatu makuu;
Kwamfano tunapoona hatma ya ibilisi na matendo yake maovu, hakuna hata mmoja anapendezwa na tabia kama zile, hivyo na sisi tutajilinda na dhambi ya uasi, kwa gharama zote, kwasababu tunajua mwisho wake utakuwa wapi. Hivyo yeye na watu wabaya wamekuwa funzo kubwa kwetu sisi, juu ya madhara ya dhambi.
Kama wasingekuwepo, tusingejua uzuri wa haki. Huwezi kujua sukari ni tamu kama hujawahi kuonja kitu kichungu, huwezi kujua hili ni joto kama hujawahi kuhisi baridi kabisa. Vilevile hatuwezi kujua Mungu ni wa upendo kama hatujakaa na watu wabaya, kama vile wauaji, wabinafsi n.k
Vilevile ameruhusu kwa lengo la kuadhibu, pale tumkoseapo Mungu. Anaruhusu watu kama akina Nebukadreza wa Babeli, kutuadhibu, kama wafilisti kwa Israeli walipomkosea Mungu. Hivyo wanasimama pia kama fimbo ya Mungu kwa watu wake kuwafunza.
Na vilevile kuwapa sababu zote hao watu wabaya kwanini wanastahili hukumu siku ile ya mwisho kwa matendo yao.
Pia sababu ya tatu ni ili kudhihirisha uweza wake mwingi. Mungu huwa anaruhusu wachawi kama Yane na Yambre washindane naye ili atoe maajabu yake yote, anaruhusu watu kama Farao wawe na mioyo migumu ili aonyeshe uweza wake mkuu wa uokozi, aliruhusu taifa lake Israeli lizungukwe na maadui zake aonyeshe jinsi anavyoweza kuokoa.
Soma hapa;
Warumi 9:17 “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu. 19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? 21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;”
Warumi 9:17 “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?
21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?
22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;”
Hivyo basi, hizi ni baadhi ya sababu, lakini zipo nyingine zaidi ya hizo ambazo tutakuja kuzifahamu baadaye.
Ni kutufundisha unyenyekevu, tukubali kufanyika watu wema, ili tusiwe vyombo vya ubaya, Kwasababu kila jambo unaloliona duniani, liwe baya liwe jema, lipo chini ya makusudi ya Mungu, hakuna linalotokea kwa bahati mbaya, na ndio maana mengi ya hayo bado hayajaondolewa yote. Lakini utafika wakati yataisha.
Kumbuka hatuna miaka 100 tu ya kumjua Mungu, bali tuna umilele mbeleni, Hivyo kwa kipindi hichi kifupi hatuweza kutoa habari zote za Mungu, na kumuuliza kwanini umeruhusu haya, au yale..tuwe watulivu.
Tupende mema tuwe salama, tumpe Kristo maisha yetu ili tusiwe vyombo vya ghadhabu kama Farao, bali vya heshima.
Bwana akubariki.
Mwendelezo unakuja..
JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?
KITABU CHA UZIMA
NGUVU YA UPOTEVU.
YESU NI NANI?
TOFAUTI YA MITUME, MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WAALIMU NI IPI?
HATARI! HATARI! HATARI!
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
Shalom…Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwe milele. Karibu tujifunze maneno yake ya uzima.
Lipo la kutafakarisha sana, katika ile habari ya yule mtu aliyesafiri, na kuwaita watumwa wake watatu na kumpa kila mmoja talanta ya Fedha wakafanyie biashara.
Kama tunavyoijua habari yule wa kwanza aliyepewa talanta tano, akaleta faida ya talanta nyingine tano, Vilevile yule aliyepewa talanta mbili akachuma nyingine mbili…lakini yule aliyepewa moja..maandiko yanatuambia hakuchuma chochote…
Na sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vile si nyingine zaidi ya “WOGA”…Tusome..
Mathayo 25:24-30
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;[25]basi NIKAOGOPA, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.[29]Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
[25]basi NIKAOGOPA, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
[29]Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Aliogopa nini?
Aliogopa atakapojaribu kuifanyia biashara ataipoteza…aliogopa kupata hasara..hivyo akaona ni heri aihifadhi tu..mahali fulani mpaka Bwana wake atakaporudi amrudishie kilicho chake wamalizane..
Aliogopa kuchekwa, na kudharauliwa, na kudhihakiwa, alijiona hawezi kuzalisha kile alichopewa, hana uzoefu na biashara..hakutaka kujitosa kama wale wenzake…ambao wao pia waliijua hatari ya biashara kwamba kuna kupata na kupoteza, lakini hawakutaka kuzipa kipaumbele… lakini yeye akasema sitaki kupata magonjwa ya moyo..wacha niihifadhi tu..kwani nini! , maadamu sijamtapeli..akirudi nitamrudishia kilicho chake.
Ndugu hii hali ipo kwa wakristo wengi hadi sasa..hawataki kupiga hatua moja mbele kuuzalia matunda wokovu wao kisa tu HOFU, ya kupata hasara..
Hasara ya nini?
Hasara ya ndugu kuwatenga, kama ndugu zao wakisikia kaokoka, wakiwatenga itakuwaje?
Hasara ya kuonekana wamerukwa na akili,..
Hasara ya marafiki kuwacheka, kuwaona ni washamba, wamepitwa na wakati..kwasababu wameacha mtindo fulani wa maisha.
Hasara ya kufukuzwa kazi, au kushushwa cheo kazini, kisa tu hawali rushwa tena.
Hasara ya kuachwa na mke/mume kisa tu wamejitwika msalaba wao na kuwafuata..
Hivyo hofu kama hizi na nyingine nyingi zimekuwa kigezo cha wakristo wengi kufukia talanta zao chini..wanasubiria tu siku ya kufa, Kristo aje na kuwauliza mmezalisha Nini kwenye Wokovu niliowapa siku ya kwanza…wenyewe waseme hakuna zaidi tu ya kuokoka..
Hii ni hatari kubwa sana…na jambo la kuhuzunisha..Ni lazima tujue “hakuna hatua moja mbele kama hakuna kujikana” Yesu aliye Bwana wetu alikubali kuchukiwa, kutengwa, kuonekana karukwa na akili, hadi kuuliwa, ili tu amzalie Mungu matunda yaliyo bora..(Yohana 7:5)
Marko 3:21
[21]Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.Na yeye mwenyewe akatuambia tusipojitosa kama yeye hatuwezi kuwa wanafunzi wake…
[21]Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
Na yeye mwenyewe akatuambia tusipojitosa kama yeye hatuwezi kuwa wanafunzi wake…
Luka 14:26-27
[26]Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.[27]Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
[26]Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
[27]Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Akasema pia..ili mbegu ya ngano iweze kuzaa na kuleta matunda mengi haina budi kuoza kwanza chini ya ardhi, ndipo baadaye ichipuke na kukukua na kuzaa..(Yohana 12:24)
Ni lazima tuonekane tumekufa kwanza ndipo tuzalishe talanta zetu..tuonekane tumepotea kwa ajili ya Kristo ndipo tupate karama zake, tukilikimbia hili, tujue hatutazalisha chochote, ukristo wetu utakuwa ni ule ule wa miaka nenda, miaka rudi.
Ndugu/dada umedhamiria kumfuata Yesu, embu acha udunia kwa moyo wako wote..acha vimini, acha marafiki wasiofaa, acha miziki, na tamaa za ujanani, mtafute Mungu kwa moyo wote, elekeza nguvu zako zote huko..Epuka kuwa mkristo-jina…yule wa kusema nimeokoka-nampenda Yesu, halafu maisha yako hayana ushuhuda hata chembe..
Maanisha sasa..kwasababu siku zinavyozidi kwenda, siku moja utakufa na utatolea hesabu wokovu uliopewa, ukauchezea kwa hofu za wanadamu na ulimwengu.
Bwana atusaidie..
Maran atha.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)
Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”
ANGALIA JINSI USIKIAVYO:
Yesu alifundisha kwa mifano. Je hiyo mifano maana yake nini?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO.
SWALI: Naomba nifahamishwe mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?
JIBU: Si kweli, Nguvu za giza huwa hazichagua, hali ya mtu ya kimaisha, zinawavaa matajiri vilevile vinawavaa maskini, zinawavaa wanaume, zinawavaa wanawake, zinawatesa watoto (Marko 9:21), vilevile zinawaathiri mpaka wanyama (Soma Mathayo 8:31 )..Kwasababu kazi ya shetani sikuzote ni kuuharibu mpango mzima wa Mungu kwa viumbe vyake vyote.
Hivyo usidanganyike kuwa matajiri hawawezi kuwa na mapepo, huwenda ni kwasababu wewe hujakutana na visa hivyo, lakini vipo vingi. Pia katika maandiko walikuwepo matajiri ambao walisumbuliwa na mapepo.
Soma..
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, 2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”
Umeona hapo, Hao wanawake wanaotajwa wote walikuwa ni matajiri, hakuna maskini, tukianzia na huyo Mariamu Magdalena, ambaye alitoa marhamu yake yenye thamani ya mamilioni ya pesa akammwagia Kristo miguuni pake, mpaka kwa Yoana mkewe Kuza, wakili wa Herode.
Mawakili kwa zamani ni sawa tu na mawaziri wakuu na wakuu wa majeshi sasahivi, hivyo huyu mke wa waziri mkuu alikuwa akimfuata Yesu, huwezi kusema ni maskini, alikuwa tajiri na wanawake wengine hapo wakitajwa walikuwa wakimuhudumia kwa mali zao.
Hivyo, hakuna mtu aliye na ofa kwa Mungu au kwa shetani, kwasababu ya hali yake ya kimaisha. Sote tunahitaji wokovu, tunahitaji msaada kwa Kristo sawasawa, tunahitaji kufunguliwa na yeye.
Tahadhari:
Epuka mahubiri yanayopigia kampeni utajiri, ambayo ndio yanayoendelea sikuhizi za mwisho kana kwamba ndio uhai wa mtu ulipo, yatakupoteza. Mkimbilie Kristo akupe uzima wa milele.
Efatha.
Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?
MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
Je! Unataka Roho Mtakatifu afanye kazi vizuri ndani yako?
Fuatilia somo hili.
Maandiko yanasema..
2Wakorintho 13:14 “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote”
Unaweza kujiuliza ni kwanini, ofisi hizo kuu tatu za Mungu, zitajwe na sifa zao? Na si zenyewe tu kama zilivyo, (yaani Mungu, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu).. Bali kila mmoja inaelezewa na sifa yake pembeni, yaani ‘Pendo’ la Mungu, na ‘Neema’ya Yesu Kristo, na ‘Ushirika’ wa Roho Mtakatifu? Kwanini iwe hivyo?
Ni kwasababu Mungu anataka tujue kwa ukaribu tabia kuu iliyotenda kazi katika kila ofisi,
Kwamfano Anaposema Pendo la Mungu…Maana yake ni kuwa Palipo na upendo, Mungu yupo, hivyo kazi zote za Mungu (Baba), zinadhihirika kwa upesi sana pale ambapo pana upendo kwasababu maandiko yanasema kuwa yeye ni upendo..
Ukitaka umuone Mungu kama baba yako, basi hauna budi kuwapenda watu kwa moyo.
1Yohana 4:16 “Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake”.
Usipopenda maana yake ni kuwa Mungu (kama Baba), kamwe hatakaa ajidhihirishe kwako.
1Yohana 4:20 “Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona”
Halikadhalika, maandiko yanasema.. “Neema ya Bwana Yesu Kristo, ikae nanyi nyote”. Ikiwa na maana kuwa Kristo yupo katika neema. Neema ni ile hali ya kutoa kitu ambacho mtu hajastahili kukipata. Kwamfano mtu anayefaulishwa, kwa kuhurumiwa na wakati hakusoma..Hiyo inatafsirika kama neema, ndicho Yesu alichokifanya sana akiwa duniani..
Kwanza aliacha enzi na mamlaka na uweza kule mbinguni, akaja duniani, ili kutupa sisi wokovu bure, bila kuusumbukia, akamwaga damu yake ili sisi tupate ondoleo la dhambi. Tukahesabiwa kuwa tumestahili uzima wa milele bure bila matendo. Kwaufupi Maisha yake yote yalikuwa yamejaa neema! neema! tu
Hivyo Kristo naye ili atembee na sisi, ni lazima nasi tuwe watu waliojaa neema kwa wengine.. Ndio maana akasema, ndugu yako akikukosa hata 7 mara 70, huna budi kumsamehe. Vilevile tujifunze kuachilia, na kutokuhukumu. Hivyo tukitaka tutembee kama Kristo duniani, basi tabia hii ni lazima tuwe nayo kwa wingi.
Lakini Pia maandiko yanasema..
‘Ushirika’ wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” ..
Maana yake ni kuwa utendaji kazi mkuu wa Roho Mtakatifu, upo katika ushirika.. Neno ushirika, limetokana na neno ushirikiano. Anachotaka kwanza ni ushirikiano wetu sisi na Mungu, lakini zaidi sana ushirikiano wetu sisi kwa sisi (tuliokoka).
Kanisa la sasa tunakosa kuona nguvu za Roho Mtakatifu kwasababu hatuna ushirikiano. Kila mmoja anatembea kivyake, kila mmoja ana nia yake, na matazamio yake binafsi. Hivyo basi Roho Mtakatifu anashindwa kufanya kazi kama anavyotaka. Tunamwita Roho Mtakatifu lakini haji kwasababu hatujui kuwa yeye yupo katika ushirikiano.
Siku ile ya Pentekoste, maandiko yanasema, kabla Roho Mtakatifu hajashuka, walikuwa kwanza mahali pamoja wote, wakidumu katika kusali.
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste WALIKUWAKO WOTE MAHALI PAMOJA. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste WALIKUWAKO WOTE MAHALI PAMOJA. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.
Hata baada ya pale, bado waliendelea kuwa wamoja, na kudumu katika nia moja.(Matendo 5:12)
Hivyo Roho Mtakatifu akatenda kazi sana miongoni mwa watu.
Hata sasa, ukitaka Roho Mtakatifu ajae kwa haraka sana ndani yako usiepuke, kuwepo katika ibada na wenzako, katika mikesha, katika maombi, katika ushirika wowote mwema, hapo Roho Mtakatifu yupo sana, kwasababu yeye kiini chake ni ushirika. Ukitaka aitumie vizuri karama yako, hakikisha unakuwepo miongoni mwa kanisa, ili idhihirike, kwasababu haiwezi kudhihirika mahali ambapo upo peke yako.
Kwasababu vipawa hivyo yeye mwenyewe anasema anavitoa kwa lengo la kuwakamilisha watakatifu, na kuujenga mwili wa Kristo (Waefeso 4:12), na si vinginevyo, Hivyo utaujengaje mwili wa Kristo endapo unajitenga na wenzako?
Kumbuka ofisi kuu, tuliyonayo sasa ni ya Roho Mtakatifu. Hivyo, tunamuhitaji sana ajae ndani yetu ili atuongoze katika kweli yote. Tukimzimisha, au tukimuhuzunisha, tutashindwa kumshinda shetani katika zama hizi za siku za mwisho.
Hivyo penda ushirika, penda umoja na watakatifu. Na Roho Mtakatifu atachukua nafasi yake juu yako.
Shalom.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
Roho Mtakatifu ni nani?.
MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU
Je! Unaweza kubatizwa na usipokee Roho Mtakatifu?. Na Je! Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono?
USINIONDOLEE ROHO WAKO MTAKATIFU.
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 20:10
[10]Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.
JIBU: Ni mstari unaolenga ubadhilifu katika biashara au maisha…kwamfano labda mtu ni muuzaji wa mchele..na kwenye duka lake anakuwa na mawe mawili ya mizani…moja la haki na lingine lenye uzito wa chini kidogo..hivyo akija mtu kumuuzia anampimia kwa lile jiwe la uzani wa chini, ili yeye abakiwe na kingi..
Au mwingine ni muuzaji wa mkaa, lile kopo la kipimo analibonda bonda ili lisichukue mkaa mwingi…sasa haya yote ni machukizo kwa Bwana..ndio hapo maandiko yanasema.. “Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA”.
Udanganyifu katika biashara ni tatizo sugu, na lipo katika nyanja mbalimbali pia kwamfano …utakuta mtu anauza maziwa ya ng’ombe, sasa ili apate faida kubwa zaidi anatia maji ili yawe mengi, kisha anauza…hayo ni machukizo..
Mwingine ni mama ntilie, ananunua sahani ndogo, au vikombe vidogo ili auze chai kidogo kwa bei ileile ya sikuzote apate faida kubwa.
Vilevile kuonyesha upendeleo kwa wengine ni machukizo kwa Mungu, kwasababu hivyo navyo ni vipimo mbalimbali. Labda ni muhuguzi, ambaye anawaongoza watu katika foleni ya kumwona daktari, anapokuja mtu wake wa karibu au mwenye pesa, anampitisha mlango wa nyuma, hamweki kwenye foleni.
Hivyo Bwana anatutaka tuwe watu wa usawa na wa haki. Kwasababu na yeye pia ni Mungu wa haki
shalom.
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.
VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.
Maana Ya Maneno Katika Biblia.
Tofauti kati ya kuhukumu na kulaumu ni ipi?
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
JINSI EDENI ILIVYOKUWA.
SWALI: Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema..
Wakolosai 2:5 “Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo”
Je! Kwasasa kauli hii inasimama katika mazingira gani?
JIBU: Katika mazingira ya kibinadamu kuna wakati inatokea, hutakuwa karibu na watakatifu wenzako kimwili, pengine kwasababu kadha wa kadha, lakini biblia bado inatoa tumaini kuwa hali hiyo ni kweli inaweza kuathiri mwili , lakini roho bado ikawa pale pale inashiriki neema na Baraka kana kwamba hukuondoka, lakini hiyo yote mpaka ifikiwe zipo taratibu zake..
Inahuzunisha kuona Neno hili linachukuliwa juu juu.. Utaona watu wanatoa udhuru zao, halafu mwishoni wanamalizia na hili Neno “Kimwili sipo nanyi, lakini nitakuwa nanyi kiroho” Wakidhani kuwa ni rahisi kiivyo.
Embu tuangalie Paulo aliyesema haya maneno kwa Wakolosai alichochewa na nini mpaka akapata ujasiri wa kusema vile..
Alilisisitiza hilo mwishoni kabisa mwa waraka wake akasema..
Wakolosai 4:18 Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi
Maana yake ni kuwa kama isingekuwa ni vifungo vile, kulikuwa hakuna udhuru wowote wa yeye kutokuwepo katika mwili na watakatifu. Lakini leo, watakatifu hawapo magerezani, wapo bize na kazi wanasema nimetingwa siwezi kuja kanisani, Hawapo nje ya mikoa au nchi, wapo mtaa wa pili lakini wanasema, kanisani ni mbali, nitakuwa nanyi kiroho. Hapo usijidanganye ndugu, hakuna muunganiko wowote ulio nao wa watakatifu wenzako..Upo nje ya kundi.
Anasema..
Wakolosai 1:9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni.
Japokuwa alikuwa vifungoni, lakini hakupotelea moja kwa moja huko, lakini alifanya bidii kila siku usiku na mchana, kuwaombea ndugu zake aliombali nao. Akiwaombea waimarike, wajazwe maarifa na hekima. Lakini ni mara ngapi, mpendwa mmoja akihama mkoa, au akisafiri nje ya kanisa, ndio anasahau kabisa kuliombea kanisa lake, Hapo Paulo aliliombea kwa Dua..Dua ni maombi ya kuzama ambayo yanaambatana na kufunga na kuomboleza kwa kipindi kirefu. Je na sisi tunafanya hivyo tuwapo mbali?
Na kwa kawaida mtu wa namna hii, atampenda Mungu hata na kwa matoleo yake, na dhabihu, kwa ajili ya kanisa lake. Kwasababu maandiko yanasema, hazina yako ilipo ndipo utakapokuwepo na moyo wako (Mathayo 6:21).
Wakolosai 4:7 Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; 8 ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu; 9 pamoja na Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu. Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.
Zaidi sana alikuwa anawaandikia nyaraka kama hizi, pamoja na kuwatumia za makanisa mengine wazisome, ili waimarike,(Wakolosai 4:16). Je! Na sisi tunaweza kuwa wafuatiliaji wa wapendwa wetu tuliowaacha nyuma? Au tutaliachia kanisa la kule lihusike lenyewe. Kwani wewe si haupo, ya nini tena, kuwaandikia waraka? Lakini Paulo hakuwa hivyo, alijitahidi kutumia karama yake hata kwa kuandika waraka, akiwa huko huko mbali lengo lake likiwa ni karama yake iifaidie kanisa.
.
Wakolosai 4:10-13,14
“Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni. 11 Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu. 12 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu…… 14 Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.”
“Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni. 11 Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu. 12 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu……
14 Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.”
Hakujificha, wala hakufanya mambo yake kwa siri, kanisa la Kolosai lilikuwa linafahamu kwa kina maendeleo ya kiroho ya Paulo, kwasababu Paulo mwenyewe alikuwa tayari kueleza wazi. Hakusubiri kufuatiliwa, lakini sasa kigezo cha watu kuwa mbali, ndio sababu ya kutokueleza maendeleo yao, wanapotea kabisa. Hapo hakuna muunganiko wowote.
Hivyo baadaya ya yeye kuyatimiza hayo ndipo sasa Roho Mtakatifu akamshuhudia aandike waraka ule kwamba japokuwa yupo nao mbali kimwili lakini kiroho yupo nao.
Hata sasa, mtu yeyote aliyembali na kanisa anayekidhi vigezo hivyo vyote, rohoni anakuwa hana tofauti na kama tu yupo pale. Hivyo wakibarikiwa wenzake na yeye atabarikiwa, wakipata neema na yeye atapata, Lakini kama atapoteza sifa hizo, haijalishi atatamka kwa maneno mazuri namna gani, hayupo kiroho na wenzake. Na hivyo hawezi shiriki chochote kitokacho kwa Mungu.
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)
Maongeo ni nini?(Wakolosai 2:19)
Uasherati wa Kiroho ni nini?
EPUKA MAKUNDI ILI UTAKATIFU WAKO UDUMU!.
KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.
KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU.
SWALI: Bwana Yesu asifiwe, naomba kufahamu tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri.
Ujasiri ni ile hali ya kuweza kukabiliana na tatizo au shida, au changamoto Fulani, (uwezo wa kuushinda woga).. Ujasiri unaweza kuonekana kwa kiumbe hai chochote cha Mungu, kwamfano unaweza kuonekana kwa mtu, vilevile unaweza kuonekana kwa Simba, au mbwa, au nyoka. Pia ni hali ambayo mtu/kiumbe kinaweza kuzaliwa nao, tofauti na imani,
Lakini Imani, inatokana na Neno ‘kuamini’.. Maana yake ni kwamba huzalika kwa kutegemea, kuamini kitu kingine (Haisimami yenyewe kama yenyewe)..Na kwa kupitia hicho ndio unapata sasa wa kutenda Neno ambalo mtu ulikuwa huwezi kulifanya. Kwamfano kwanini leo hii ukipishana na kuku barabarani hushtuki, lakini ukipishana na nyoka unaruka na kukimbia, au unachukua hatua ya kupambana naye? Ni kwasababu umeyaamini macho yako yaliyokupa taarifa kule kile ni kiumbe salama na kile ni hatari, lakini kama usingekuwa na macho matendo hayo yasingezalika. Hivyo ujasiri ni zao la imani, lakini imani haiwezi kuwa zao la ujasiri.
Na ndivyo ilivyo kwetu sisi, ili tuweze kupata IMANI timilifu. Hatuna budi tuwe na kitu cha uhakika cha kutegemea. Na hicho si kingine zaidi ya NENO LA MUNGU.. Hapo ndio mwisho wa mambo yote. Hilo ndio jicho letu la ndani tunalopaswa tulifufue, kwasababu ndio litatupa ujasiri wa kufanya mambo yote, na kutenda mambo yote yasiyowezekana kwa namna ya kibinadamu.
Na imani hii, haiji kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa kulisikia Neno la Mungu biblia inasema hivyo .
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.
Unaposoma Neno la Mungu, na kuona ndani yake, matendo makuu aliyoyofanya, ndipo unapopata Imani sasa na wewe ya kutenda au kusonga mbele, kwamfano, wewe ni tasa, unaposoma habari za Sara na Ibrahimu, na kuona katika uzee wa miaka 100 ndio wanapata watoto, hapo na wewe utapata nguvu ya kumwamini Mungu ukijua kuwa kama aliweza kufanya kwa Sara atafanya na kwako, kwasababu yeye ni Yule Yule jana na leo na hata milele. Lakini ikiwa huijui hii habari au huitafakari mara kwa mara, imani yako haiwezi kutokea, utabakia kusema mimi ndio basi, tena siwezi kuzaa.
Daudi alipokwenda kushindana na Goliati, alitafakari jinsi Mungu alivyomshindania, akiwa porini anachunga mbuzi na kondoo, jinsi alivyoweza kuua simba na dubu. Akamwesabia Mungu kuwa anaweza pia kumsaidia kwa Yule Goliati mtu wa miraba minne, na kweli ikawa hivyo.. Halikadhalika na wewe ili uweze kutenda mambo makubwa, kufungua mambo ambayo hayawezekani kwa akili za kibinadamu, unahitaji Imani, lakini si imani kwa wanadamu au kwa vitu au kwenye mali, bali imani kwa Mungu, ambalo ndio NENO LAKE.
Penda sana, kusoma Neno, kiwe ndio chakula chako asubuhi, mchana na jioni.
Biblia inasema..
Waebrania 11:24 “Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.30 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba.11.31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani.32 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
Waebrania 11:24 “Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;
25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;
26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.
29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.
30 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba.11.31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani.
32 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;
33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,
34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.
35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;
36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
Hiyo ndio tofauti kati ya imani na ujasiri.
KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.
ENZI NA MAMLAKA AMEZIFANYA KUWA MKOGO
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?
Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?
Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?
Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Maana yake nini?