Baraka ni karama ya Mungu, na kila mmoja wetu aliyekombolewa na Yesu, ahadi hiyo ni yake. Baraka zimegawanyika mara mbili, zipo baraka za mwilini, na baraka za rohoni. Lakini kubwa zaidi ni zile za rohoni. Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyoeleza Baraka za Mungu. Lakini pia ikiwa utapenda kupata vifungu mbalimbali, pamoja na mafundisho mazuri ya Neno la Mungu, bofya link hii uweze kujiunga na kundi letu la Whatsapp>>> WHATSAPP GROUP
Wafilipi 4:19 “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”
Yakobo 1:17 “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka”.
Hesabu 6: 24 “Bwana akubarikie, na kukulinda; 25 Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; 26 Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani”
3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
2Wakorintho 9:8 “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;”
Kumbukumbu 28:2 “na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo”.
Waefeso 1:3 ” Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”
Mathayo 6:30 ” Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”
Malaki 3:10 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la”.
Zaburi 20:4 “Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote”.
Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa”.
Mithali 16:3 “Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika”
Yeremia 17:7 “Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake”
Pia Kwa wokovu/ maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU KIFO.
MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.
MISTARI YA BIBLIA YA UPONYAJI.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Rudi nyumbani
Print this post
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Huu ni mfululizo wa masomo maalumu kwa ajili ya wanawake: Ikiwa hukupata chambuzi nyingine za nyuma basi fungua link hii uweze kuzipitia >>> MAFUNDISHO KWA WANAWAKE
Mwanzo 34:1-3 Inasema..
“Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, AKATOKA KUWAONA BINTI ZA NCHI. 2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. 3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri”
Dina alikuwa ni binti wa Yakobo, aliyejitunza na kujiheshimu, alikaa chini ya Mama zake akifundishwa desturi za uzao wa Ibrahimu unavyopaswa uwe. Akafahamu kuwa uzao wao haupaswi kuchanganywa na uzao wa ukoo mwingine, Ili Baraka ya Ibrahimu aliyoahidiwa kwa uzao wake isiingiliwe na doa.
Lakini Tunaona, jambo moja alilolifanya Dina, ambalo pengine hakujua mwisho wake utampelekea pabaya. Na jambo lenyewe “ni yeye kutoka na kwenda kuonana na mabinti wa nchi”. Kama msichana alipoona mabinti wa mataifa mengine, wanaishi maisha ya kidunia, maisha ya anasa, maisha ya ukisasa. Na yeye naye akatamani kwenda kuunga urafiki nao, bila kujua mwisho wake utakuwaje.
Hivyo kidogo kidogo, akaanza kuchukuliwa na desturi za wanawake wa kidunia, akaanza kujichanganya, siku ya kwanza, siku ya pili, wiki ya kwanza wiki ya pili, mwezi wa kwanza, mwezi wa pili. Kidogo kidogo wale mabinti wa kidunia waanza kumfundisha tabia mbaya..Pengine wakaanza kumwambia “Mbona wewe ni mrembo, hadi sasa huna boyfriend”..Mbona una shepu zuri, embu vaa hizi nguo fupi uonekane na wanaume..Embu twende leo disco, tukakutane na vijana wenzetu, tule maisha, ujana maji ya moto..
Akawa anawasikiliza, na huko ndipo akakutana na huyo Shekemu, akamlaghai, kisha akambikiri..Taarifa zikawafikia ndugu zake, wakakasirika sana Simeoni na Lawi, hadi kufikia kitendo cha kwenda kuwaua watu wote wa huo ukoo. Kwasababu waliona tendo alilofanya Dina, ni chukizo kubwa sana kwa jamii yao. Kuuchafua uzao uliobarikiwa, kuvunja maagano ya Mungu.
Nini Bwana anataka mabinti na wanawake wajifunze?
Kabla ya kuanguka katika dhambi, ushawihi huwa unaanza kwanza kwa marafiki wanaokuzunguka. Angalia ni watu wa namna gani uliozoena nao, au uliounga urafiki nao, au unaokaa nao muda mrefu. Mabinti wengi waliookoka, hawajafundishwa kuvaa vibaya na wanaume wazinzi, bali na mabinti wenzao, hawajafundishwa kwenda disco au kunywa pombe na wanaume, bali mabinti wenzao. Hawajafundishwa kwenda kwa waganga na kaka zao, bali wanawake wenzao, hawajafundishwa kusengenya na jamii, bali ni wanawake wenzao wanaokutana nao masaluni na mabarazani.
Hawa ndio maadui wa kwanza. Dina hakutoka kwenda kumtafuta Shekemu, alitoka kuwatazama mabinti tu wa kidunia na huko huko wakamuunganishia Shekemu. Laiti angetulia nyumbani akakaa na wale wabinti wenzake wa ukoo mmoja hata kama ni washamba, angekuwa salama.
Wewe kama mwanamke usipende kuunga urafiki na wanawake ambao hawajaokoka, ambao hawana habari na Mambo ya ufalme wa mbinguni, upo chuo, upo shuleni, upo kazini, ni heri ubaki kivyako vyako, kuliko kujiingiza hatarini. Siku zote uangamivu unavyokuja huwa unaanzia mbali sana, hivyo kuwa makini, tafuta watu waliodhamiria kuishi maisha matakatifu, hao ndio wawe marafiki zako wa karibu, washauri wako, uige tabia zao, kataa kampani za kipepo, acha wakuone mshamba, lakini roho yako ipo salama, acha upitwe na fashion, acha upitwe na uzuri lakini jina lako lipo katika kitabu cha uzima.
Majira tunayoishi ni ya kung’ang’ania kwa nguvu wokovu tuliopewa, ni kuwa siriazi kweli kweli, kwasababu maelfu kwa maelfu ya watu wanaangamia, wanashindwa kumaliza mwendo wao salama hapa duniani wanaponzwa na marafiki, Unadhani na sisi tukiwa walegevu, tunadhiria kila kitu tu kinachokuja mbele yetu, tutawezaje kupona. Njia imesonga, mlango ni mwembamba, tunajiingiza kwa nguvu, isitoshe muda tuliobakiwa nao ni mchache. Hivyo hatupaswi kuwapa nafasi watu wakidunia katika maisha yetu.
Tujifunze kwa Dina. Tuwe salama. Kataa, kampani za kipepo!
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
MAFUNDISHO KWA WANAWAKE
FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!
MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.
Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?
Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)
Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?
Unaweza kushushwa chini, lakini simama usivunjike moyo.
2Wakorintho 4:8 “Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; 9 twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi”
Kwa kuwa bado tupo duniani, dhiki, mateso, manyanyaso hayaepukiki katika baadhi ya vipindi, Kiongozi wetu Yesu alituweka wazi, kwamba “duniani mnayo dhiki, lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu”(Yohana 16:33)
Utaudhiwa na mume/mke/baba/mtoto, kwasababu ya imani, utapigwa bila sababu, utatishiwa kufukuzwa kazi, utakuwa na mashaka pande zote, mwingine hujui kesho utaamkaje, ule nini, magonjwa hayana mwisho..Lakini katika yote, bado neema ya Mungu itatushika na kutusaidia, hatutasongwa kiasi hicho mpaka kuicha imani, hatutakata tamaa, hata turudi nyuma, Bwana atakuwa upande wetu.
Mambo hayo ni ya kitambo tu, hata kama tutauawa, bado tunao uzima wa milele, hata kama tutapoteza kila kitu bado mwenye vitu vyote yupo ndani yetu. Tutadhikika pande zote, tutasongwa kila mahali lakini hatutakata tamaa. Tukumbuke tu, Kila pito linasababu yake, lakini katika yote, tujue Bwana anatuwazia mawazo mema, tukishakwisha kukamilishwa tutatoka kama dhahabu.
Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno”.
Bado maandiko yanasema..
1Petro 1:6 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.
1Petro 1:6 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.
Bwana awe nawe.
Maombi yangu:
“Baba mwema, nakushukuru kwa neema ya wokovu uliyonipa, Najua kama sio wewe nisingefika hata hapa nilipo, nakuomba Mungu wangu unione katika dhiki zangu, uyaone machozi yangu, uniondoe katika mateso yangu. Lakini zaidi unipe nguvu ya kuweza kukabiliana na dhiki zote za ulimwenguni, nisirudi nyuma wala kukata tamaa. Nikutumikie wewe katika mazingira yote. Upendo wako usipunguke ndani yangu. Ninaomba nikiamini katika jina la Yesu Kristo. Amen”.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
UYATIE MACHOZI YANGU KATIKA CHUPA YAKO EE! BWANA.
Furaha ni nini?
Unyenyekevu ni nini?
JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini siku ile Bwana Yesu alipofufuka kutoka katika wafu, hakupotea na kutokea nje ya kaburi kisha kuendelea na safari yake ya kuwatokea mitume, na watu wengine lakini kinyume chake ilimpasa kwanza jiwe la kaburini liondolewe, ndipo atoke?
Kimsingi Bwana Yesu alipofufuka alikuwa na uwezo huo wa kupotea na kutokea, utakumbuka alifanya hivyo kwa watu zaidi ya 500, Tukiachia mbali siku ile mitume walipokuwa wamejifungia ndani kwa hofu ya wayahudi, Yesu aliwatokea na kuanza kuzungumza nao, wala hakuhitaji kuingia kwa kupitia mlangoni.
Lakini tukirudi kwenye kaburi, ilikuwa ni lazima apitie kwenye malango yake, na kama ni hivyo basi ni sharti pia jiwe liviringishwe ili atoke, na ndio maana malaika walitokea juu na kuifanya kazi hiyo (Mathayo 28:2).
Lakini sio wakati huo tu, utakumbuka pia kifo cha Lazaro, Bwana Yesu hakumfufua Lazaro hivi hivi tu, bali aliwaambia kwanza wale watu waliokuwa pale waliondoe jiwe kwanza ndipo shughuli za kufufua ziendelee. Hii ni kanuni ya kiroho ya Mungu, hakifufuliwi chochote bila kwanza kuondoa jiwe.
Yohana 11:39 “Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne…. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Yohana 11:39 “Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne….
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Na sisi pia, ili tumwone Yesu aliyefufuka na nguvu zake, ni lazima tuyaondoe mawe mioyoni mwetu. Tusitazamie Yesu atafanya lolote, au atatenda muujiza Fulani, hiyo haipo, atafufuka kweli lakini hatoweza kutoka mpaka tutakapoyaondoa mawe hayo makubwa mioyoni mwetu.
Mawe hayo ni yapi?
Ni ule ugumu wa mioyo yetu.
Kama tunavyofahamu sikuzote jiwe ni gumu, tofauti na nyama..si rahisi kuathiriwa na chochote, ukilipitisha kwenye moto litakuwa vilevile, ukilipitisha kwenye upepo haliwezi kukakamaa, ukilipitisha kwenye maji haliwezi kulowa, ukilipiga upanga, ndio kwanza upanga unaumia.
Wapo watu ambao wanasema wamemwamini Kristo, lakini hawapo tayari Kristo ayatengeneze maisha yao, bado mawe yamefunika mioyo yao, wanataka maisha yao ya sasa, na yale ya kale yasiwe na utofauti, lakini wakati huo huo wanasema wameokoka. Hawajui kuwa ukristo ni badiliko la maisha moja kwa moja.
Wakiambiwa, wasivae mavazi yampasayo mwanamume, wanaona ni unyanyasaji wa kijinsia, wakiambiwa, biblia inasema tusiipende dunia, kwasababu tukiipenda dunia, tunafanyika maadui wa Mungu( 1Yohana 2:15)…watakuambia hizo ni zama za kale, wakiambiwa kubeti ni dhambi, wanajifanya kama hawaoni, wao kila jambo linalogusa maisha yao ya dhambi, hupinga tu..
Hata waonyweje, hawataki kubadilika, Sasa, haya ndio mawe yanayomzonga Yesu asifufuke katika maisha ya watu wengi wanaosema wamempokea Yesu. Kamwe hawawezi kuona nguvu ya kufufuka kwa Yesu katika maisha yao, Watausikia tu upendo wa Yesu, lakini moyoni mwao kutakuwa kukame daima, wataisikia amani ya Kristo, lakini kiuhalisia wao hawajawahi kuionja mioyoni mwao. Yesu atabakia kuwa kama mtu Fulani mashuhuri aliyewahi kutokea zamani, kama tu wengine, lakini sio mwokozi, anayebadilisha maisha ya watu.
Ndugu yangu, jiachie kwa Bwana akuongoze kwa jinsi apendavyo yeye na sio kama upendavyo wewe, ndivyo utakavyouona wema wake, na nguvu zake maisha mwako. Ondoa jiwe hilo, mbele yako, liviringishe mbali, moyo wako uwe wazi ili Yesu atoke afanye kazi yake, na Bwana atayamalizia yaliyosalia sawasawa na ahadi yake katika;
Ezekieli 36:26 “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama”
Dunia ya sasa ni kujihadhari nayo sana, kwasababu, hata mpagani asiyemjua Mungu kabisa, ukimuuliza Je! Umempa Yesu maisha yako? Atasema ndio. Wokovu umepunguzwa na kufanywa kama staili tu, lakini sio geuko la maisha, Na ndicho shetani anachotaka kitokee kwako pia, ili kwamba usikae uone nguvu za Yesu aliyefufuka katika maisha yako.
Hivyo ikiwa wewe ni mkristo vuguvugu, embu kuanzia sasa, amua kujitwika msalaba wako na kumfuata Yesu, usiogope kuonekana mshamba, usiogope kuonekana umerukwa na akili, hata Bwana mwenyewe, alionekana hivyo, sasa kwanini wewe uogope, usiogope kutengwa na ndugu kisa umeamua kubadili mfumo wa maisha.. Ondoa jiwe hilo linalouzinga moyo wako.
Bwana akutie nguvu.
Ikiwa hujaokoka na upo tayari kuanza maisha mapya ndani ya Kristo kwa kumaanisha kabisa, kuukataa ulimwengu na mambo yake yote, Basi, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithibitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.
Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwabudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Ikiwa utahitaji msaada wa hayo yote, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
JIWE LILILO HAI.
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika.
Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.
YESU MPONYAJI.
Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).
URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?
SWALI: Mstari huu una maana gani?
Mithali 27:10 “Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali”
JIBU: Ni mstari unaolenga umuhimu wa marafiki wema katika maisha yetu. Hapo anaanza kwa kusema usimwache rafiki yako mwenyewe, lakini haishii tu kwa rafiki yako, anaendelea kusema pia hata rafiki wa baba yako. Kwasababu wanaweza wakawa msaada kwako wa karibu kuliko ndugu wakati mwingine.
Kauli hiyo haimaanishi kuwa ndugu hawana msaada, hapana, lakini kutegemea tu ndugu peke yake, na kuwapuuzia marafiki wema kwaweza kukukwamisha, kwamfano umezidiwa na ugonjwa chumbani kwako, na unahitaji huduma ya kwanza, hapo huwezi kumpigia simu ndugu yako aliye mkoa mwingine, au wilaya nyingine aje kukusaidia, ni wazi kuwa msaada wa kwanza utauhitaji kutoka kwa jirani yako.
Ndio maana ya huo mstari, usimwache rafiki yako mwenyewe, yaani usimpuuzie, wala usimpuuzie rafiki wa Baba yako hata kama sio rafiki yako. Marafiki wa ndugu zetu, mara nyingi hufanyika msaada mkubwa kwetu wakati mwingine, Hili ni jambo la kawaida katika jamii, mara nyingi tumeona marafiki wa wazazi, au wa ndugu zetu wakitumika kutusaidia kwa sehemu moja au nyingine.
Lakini tukiwa ndani ya Kristo, tunapata marafiki ambao ni zaidi hata ya ndugu, kwasababu wao, husukumwa na upendo wa Kristo ambao umezidi wote. Bwana ameahidi hivyo kwamba tukiacha vyote kwa ajili ya jina lake, basi hayo yote atatujalia (Marko 10:30).
Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na Yesu yupo mlangoni kurudi? Maisha yako yapo kwa nani. Kama upo nje ya Kristo ni heri ukatubu sasa, kwasababu mlango wa neema unakaribia kufungwa, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kama hukubatizwa, ili upate ondoleo la dhambi na upokee kipawa cha Roho Mtakatifu, ikiwa utahitaji msaada huo basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618 / +255789001312.
USIWE ADUI WA BWANA
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?
KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.
NDUGU,TUOMBEENI.
SWALI: Kwanini Biblia inakataza kula asali nyingi, nini maana ya mstari huu kiroho?
Mithali 25:16 “Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika”.
Pia sehemu nyingine inasema..
Mithali 25:27 Haifai kula asali nyingi mno; Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.
JIBU: Asali hufananishwa na Neno la Mungu,
Ezekieli 3:1 Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. 2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. 3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
Soma pia Ufunuo 10:10. Utalithibitisha hilo.
Na kila mmoja wetu anashauriwa alisome Neno la Mungu (alile) sana kwasababu ndio uzima wetu (Mathayo 4:4).
Mithali 24:13 Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo
Lakini katika maandiko hayo tunaona tena biblia inatuasa tusile nyingi mno kupita kiasi, ikaja kutuletea madhara..Sasa maana yake ni nini? Je! Tulipende Neno la Mungu kwa kiasi au la?
Jibu ni kwamba hapo haimaanishi tulisome/ tujifunze neno la Mungu kwa kiasi hapana.. Bali analenga katika Suala la NIA zetu.. Ni kawaida yetu sisi watoto wa Mungu, kuwa na NIA inayopitiliza hususani pale tunapolifahamu sana Neno la Mungu.
Kwamfano, tunaposoma juu ya neema ya Mungu iliyokuwa inatembea juu ya Eliya, Kisha tunaposoma kitabu cha Malaki4:4-5, kwamba ahadi imetolewa kuwa Roho ya Elia itarudi tena katika siku za mwisho. Baadhi ya watu wanajiweka katika nafasi hizo, na wanaamini kuwa Mungu anakwenda kuwaandaa kwa roho hiyo ili waje kuionya dunia kwa mapigo na ishara kama za kwake.
Au Musa kafunga siku 40 bila kunywa wala kula, akaongeza na nyingine 40 na yeye bila uongozi wa Roho Mtakatifu anasema na mimi lazima nifunge hivyo.
Wapo wengine wanasema na mimi nisipotokewa na Yesu kama Paulo alivyotokewa kule Dameski, bado sitakwenda kuhubiri injili, hivyo wanasubiriwa kwa miaka watokewe wapewe maagizo, kwa kufunga na kuomba. Sasa Hali kama hizi zina hatari kwasababu mwisho wa siku zinamfanya asiwe mtu wa matunda kwa kungojea jambo ambalo huwenda Mungu hajalikusudia katika maisha yao, kwasababu amenia makuu kuliko kipimo kile alichopimiwa na Mungu.
Mtume Paulo aliyasisitiza sana makanisa juu ya jambo hilo akasema..
Warumi 12:16b “.. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili
Na hapa pia anasema..
1Wakorintho 7:17 “Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote. 18 Je! Mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe. 19 Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu. 20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. 21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. 22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.
Ikiwa Bwana kakupa kipimo cha ushemasi, tembea katika hicho kwa uaminifu usilazimishe uwe nabii wa mataifa yote kama Yeremia. Bwana amekuokoa, tumika katika kipimo hicho hicho, ikiwa itampendeza kukunyanyua juu zaidi, basi atafanya kwa wakati wake, lakini kwasasa tujishughulishe na mambo manyonge,
Lakini si hayo tu, wakati mwingine katika kufahamu sana maandiko, hupelekea tabia za majivuno, kujiona unafahamu, kukataa kushauriwa kunazalika ndani ya mtu. Hivyo hupelekea kujifungia mwenyewe milango ya Mungu kuendelea kusema naye. Hivyo ili kuepuka kuitapika asali iliyo nzuri na njema, ni vizuri haya yote tukajiepusha nayo, tunapojifunza kwa bidii Neno la Mungu kila siku.
Tule asali kwa kadiri ya kututosha tusije tukashiba tukaitapika, kwa kukosa shabaha ya maandiko.
Maran Atha.
Shalom.
NJAA IPO?, USIACHE KULA ASALI.
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
Wewe umemwaga damu nyingi,
Kuna wakati Daudi aliingiwa na wazo la kumjengea Mungu nyumba, hivyo wazo hilo likawa jema sana machoni pa Mungu, likamfurahisha sana Bwana mpaka akamwahidia Baraka tele katika ufalme wake..Lakini tunasoma Mungu alimzuia Daudi asiijenge hiyo nyumba, bali mwana wake Sulemani ndiye aje kuijenga, sio kwamba Mungu alikuwa hatamani Daudi aijenge, hapana Mungu alimpenda sana, na alikuwa kipenzi chake, lakini kulikuwa na kikwazo kilichomkwamisha..
Embu tusome…
1 Nyakati 22:7-8 [7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu. [8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
1 Nyakati 22:7-8
[7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.
[8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
Sababu yenyewe Mungu ameitoa hapo kwamba Daudi “amemwaga Damu za watu wengi”..Daudi hakujua kuuwa kwakwe watu sio jambo ambalo lilikuwa linavutia machoni pa Bwana, japokuwa Mungu alikuwa pamoja naye wakati wote, hakujua kuwa kuua kule kulikuwa kunapeleka harufu mbaya mbele za Mungu aliye mtakatifu na msafi.
Hivyo wakati anapeleka ombi lake la kumjengea hekalu, Mungu akamkataza kwasababu alimuona ananuka damu za watu wengi, Na sikuzote Mungu hawezi kuruhusu mikono yenye damu, kushiriki katika kujenga vitu vitakatifu.
Ni nini Bwana anataka tujifunze.
Sisi kama wakristo, zipo dhambi au makosa ambayo tunayazoelea kuyafanya mara kwa mara, lakini hatujui kuwa tunamkosea Mungu, wakati mwingine tunapumbazika, kuona rehema na fadhili zake zinatufuata kila mahali, lakini ndani ya mioyo yetu tunamwaga damu kila kukicha kama Daudi.
Kwamfano, katika agano jipya, hatuui kwa Upanga au kwa mkuki, maandiko yanasema..
1Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
Kitendo tu cha kuwa na chuki, na jirani yako, au ndugu yako, kumbe rohoni unatafsirika kama mwuaji, hivyo chuki hizo zinavyoendelea na kuzidi wakati baada ya wakati, zinavyozidishwa kwa watu wengine kadha wa kadha, ndivyo mtu huyo anavyoonekana anamwaga damu nyingi.
Na madhara yake utakuja kuyaona mbeleni, wakati ambapo unamwomba Mungu kibali cha kutenda jambo Fulani jema kwa ajili yake, anakuzuia, unataka Mungu atembee na wewe katika viwango Fulani vya juu, anakuzuia, kwasababu umeendekeza makosa au dhambi hizo kwa muda mrefu.
Hivyo, tunapaswa, kila inapoitwa leo, tuangalie ni wapi tumezoelea kupafanya ambapo hapampendezi Mungu, kisha tuache mara moja, ili isije kutuletea madhara mbeleni, Kama ni katika usengenyaji, tuache mara moja, kama ni katika uongo, rushwa, udhuru, wivu, manung’uniko tuache mara moja.
Bwana atusaidie
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
EPUKA KUCHELEWA IBADA.
NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
KIFAHAMU KIGEZO CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 25:23 Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
JIBU: Maandiko yanasema Upepo wa kusi huleta mvua, hapo hasemi ‘upepo’ huleta mvua hapana bali anasema ‘Upepo wa kusi’, Maana yake ni kuwa kila aina ya upepo hubeba tabia yake, kwa mfano upepo wa Kaskazi, hauleti mvua, bali unaleta joto. Vivyo hivyo na pepo nyingine zote, hubeba tabia zao.
Hii ni kufunua nini?
Na sisi wanadamu huwa tunavumisha pepo zetu..Na ndio maana utasikia Neno “UVUMI” wa jambo Fulani, na taarifa hizo husambazwa kwa maneno ya vinywa vyetu, Hivyo kila jambo unalolitoa na kulipeleka kwa mtu mwingine au kwa jamii, huo ni upepo, na ni lazima uwe makini nao sana, kwasababu mwisho wa siku ni lazima ulete faida au madhara.
Na ndio maana hapo katika sehemu ya pili ya mstari huo anasema.. “Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu”. Kusingizia ni neno linalojumuisha usengenyaji, au mtu anayechukua taarifa zisizo za kweli na kuzipeleka kwa mwingine, Watu kama hawa, mwisho wa siku watavuna ghadhabu tu, au kuchukiwa, au kusababishiwa madhara na wale waliotolewa taarifa zao. Kwasababu kila uvumi unamatokeo yake.
Lakini tukiwa watu wa kupeleka habari njema, watu wa kuhubiri habari za Kristo, Maana yake ni kuwa Upepo tunaovumisha ni wa heri sikuzote, hivyo tufahamu kuwa mwisho wake utakuwa ni mzuri, utatuletea neema badala ya ghadhabu, kupendwa badala ya kuchukiwa, kusaidiwa badala ya kufukuzwa.
Hivyo tuwe makini na taarifa, au maneno yanayotoka katika vinywa vyetu, biblia inasema..
1 Petro 2:1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
Epuka masengenyo, na kuwazungumzia wengine vibaya.
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
JIPE NAFASI KATI YA TAARIFA UNAYOIPOKEA NA MAAMUZI UNAYOYATOA.
IEPUKE GHADHABU YA MUNGU.
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
Kwanini mtu afanye miujiza na bado asiende mbinguni?
Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.
SWALI: Naomba nieleweshwe maana ya huu mstari
Mithali 24:27
[27]Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.
JIBU: Zamani enzi za biblia, kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa watu wengi kama ilivyo sasa katika baadhi ya jamii.
Hivyo ilikuwa ni ajabu mtu kutumia rasilimali zake katika kununua au kujenga vitu visivyo na umuhimu sana, kama vile nyumba, nguo za kifahari, magari ya farasi n.k.angali shambani kwake hajajiwekeza vya kutosha.
Watu walikuwa wanakusanya kwanza chakula cha kutosha kujihakikishia shibe kwa miezi au miaka kadhaa, ndipo baada ya hapo hufikiria kutumia hazina zao katika kujenga, au kujiendeleza..lakini hawakujiendeleza kabla ya kuhakikisha mashamba yao yamewanufaisha..
Na ndio hapo Sulemani utaona anatoa ushauri ule ule..
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba tengeneza kwanza mambo yako uwe imara ndipo yale mengine ya ziada yafuate baadaye.
Ni kawaida ya mwanadamu kupenda, vitu vizuri kwanza kabla hajavitaabikia..
Alikuwepo Gehazi, mtumwa wa Elisha, yeye aliona kusubiri wakati wa Mungu ni kujichelewesha, kutumika kama mtumwa asiye na faida ni kupoteza muda, hivyo, zile zawadi zenye thamani nyingi zilizoletwa na Naamani, na Elisha kuzikataa, yeye akamwona kama alikuwa hapendi mema..lakini Elisha alimwambia maneno haya..
2 Wafalme 5:26
[26]Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi?
Alimuuliza Je huu ndio wakati? ..kumbe kulikuwa na wakati lakini haukuwa ule..
Watu wanataka kula vitu vya Bwana lakini hawataki kutengeneza kwanza kazi zao huko mashambani, hawana muda wa kuifikiria kazi ya Mungu, hawana muda na kuhubiri injili ya kweli,wanachokifiria ni matumbo, na kwamba watapata faida gani..
1 Timotheo 6:5-6
[5]… huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. [6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
[5]… huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
[6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
.Vilevile hata katika maisha ya kawaida, hekima hizi zinamafunzo, mtu atataka anunue simu ya milioni 2, lakini hana shughuli yoyote ya kumwingizia kipato, badala aitumie kama mtaji, kisha kile akipatacho kama faida ndio atumie kununua hayo mengine..
Bwana atusaidie, katika kuyapangalia maisha yetu ya rohoni na mwilini
TENGENEZA NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13).
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Nini maana ya Ukuta uliopakwa chokaa (Matendo23:3)?
Uchaga ni nini? (Luka 12:24)
Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha maovu, na maisha ya kale ya dhambi, wakati huo huo Mungu anakusamehe dhambi zako kabisa kabisa. Lakini hutasikia, hisia Fulani, au badiliko Fulani la wakati huo huo, kwani fikra zako za dhambi za zale bado zitaendelea kuzunguka kwenye akili yako. Hivyo wengi wakishaona hivi wanadhani kuwa Mungu hajawasamehe, na hivyo wanaendelea kubaki katika mashaka, au kurudia rudia kumlilia Mungu awasamehe.
Na hapa shetani ndipo anapata nafasi ya kuwatesa, na kuwakandamiza, wengine wanajikuta kila siku wanaomba Toba Mungu nisikie unisamehe!, Mungu nisikie unisamehe!, kumbe tayari Mungu alishawasamehe tangu siku ile ya kwanza walipomaanisha kweli kweli kugeuka na kukataa kurudia dhambi zao.
Ndugu, fahamu hata kama wewe utakuwa na kumbukumbu la nyuma la dhambi zako, lakini kwa Mungu ni tofauti, yeye akisamehe anasahau kabisa.
Waebrania 8:12 “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena”.
Unapokwenda mbele za Mungu, lazima uamini kwa moyo wako wote umeshasamehewa, vita vya kimawazo vinavyoanza kuja tangu huo wakati, huna budi kuvishinda, kwa kuvipinga, ukisikia moyoni mwako unaambiwa, aah! Wewe dhambi zako ni nyingi, ile dhambi ulishamkufuru Roho Mtakatifu, pinga, kataa sema mimi nimeshasamehewa kwa damu ya Yesu Kristo.
Kisha unavyozidi kufanya hivyo baada ya kipindi Fulani utaona amani ya Mungu imekuvaa.
Lakini pia ni lazima ukumbuke kuwa yapo mambo yanayochangia pia kusamehewa dhambi zetu, na yenyewe ni sisi kuwasamehe waliotukosea kama wapo.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 6:14 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”.Hivyo uombapo msamaha zingatia kuwa moyo wako ni mweupe kwa wengine.
Bwana akubariki
NINI MAANA YA KUTUBU
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).