Kipaku ni kipele kidogo kinachochipuka kwenye ngozi ya mwanadamu au mnyama. Kipele hichi kinaweza kusababishwa na mabadiliko ya mazingira, au aleji au magonjwa mbalimbali.
Hivyo Neno hili katika biblia linaonekana sehemu nyingi, hususani pale unapotajwa ugonjwa wa ukoma. Kwani ugonjwa huo kabla huujakolea kwenye mwili, huwa unaanza kwanza kama kipeleke kidogo king’aacho kekundu (ndio hicho kipaku). Hivyo katika hatua za awali ilikuwa ni ngumu kukitambua kama ni cha ukoma au cha ugonjwa mwingine wa kawaida. Hivyo ili kuepusha maambukizi zaidi kwa wengine, Mgonjwa Yule alitengwa kwa muda wa siku saba.
Na baada ya siku saba, kuhani huja na kuangalia, kama kipaku kile kimeenea zaidi kwenye mwili na kuzama kwenye ngozi basi ulikuwa ni ugonjwa wa ukoma. Hivyo mtu huyo alitengwa daima, kama hakutakasika.
Walawi 13:1 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,2 Mtu atakapokuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king’aacho, nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmojawapo;3 na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na kwamba malaika yaliyo katika hilo pigo yamegeuka kuwa meupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na kuhani atamwangalia na kusema kuwa yu mwenye unajisi.4 Na hicho kipaku king’aacho, kwamba ni cheupe katika ngozi ya mwili wake, na kuonekana kwake si shimo la kuingia ndani kuliko ngozi, na malaika hayakugeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba huyo aliye na hilo pigo;5 kisha kuhani atamwangalia siku ya saba; naye akiona ya kuwa pigo limeshangaa, na pigo halikwendelea mbele katika ngozi yake, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba tena;6 kisha siku ya saba kuhani atamwangalia tena; na tazama, ikiwa hilo pigo limeanza kufifia, wala pigo halikwendelea mbele katika ngozi yake, ndipo kuhani atasema kuwa yu safi; ni kikoko; naye atazifua nguo zake, kisha atakuwa yu safi”.
Walawi 13:1 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2 Mtu atakapokuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king’aacho, nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmojawapo;
3 na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na kwamba malaika yaliyo katika hilo pigo yamegeuka kuwa meupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na kuhani atamwangalia na kusema kuwa yu mwenye unajisi.
4 Na hicho kipaku king’aacho, kwamba ni cheupe katika ngozi ya mwili wake, na kuonekana kwake si shimo la kuingia ndani kuliko ngozi, na malaika hayakugeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba huyo aliye na hilo pigo;
5 kisha kuhani atamwangalia siku ya saba; naye akiona ya kuwa pigo limeshangaa, na pigo halikwendelea mbele katika ngozi yake, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba tena;
6 kisha siku ya saba kuhani atamwangalia tena; na tazama, ikiwa hilo pigo limeanza kufifia, wala pigo halikwendelea mbele katika ngozi yake, ndipo kuhani atasema kuwa yu safi; ni kikoko; naye atazifua nguo zake, kisha atakuwa yu safi”.
Ni fundisho gani lipo nyuma ya pigo hili la ukoma?
Zamani za agano la kale ukoma uliwakilisha pigo kutoka kwa Mungu,. Na sikuzote Mungu kabla hajaleta mapigo hutanguliza kwanza ishara na dalili, Kama vile KIPAKU tu kidogo.. Lakini baada ya siku SABA, huenea mwili wote.
Kufunua nini?
Yesu alipokuwa duniani alisema tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia, akasema pia kabla ya ule mwisho wa dunia kufika ambapo Mungu ataleta mapigo makubwa sana juu ya ulimwengu huu wa dhambi..Zitatangulia kwanza dalili na ishara, ambazo yeye aliziita ‘mwanzo wa utungu’..Ndio haya matetemeko, majanga, magonjwa, tetesi za vita, n.k. tuliyoyana tangu enzi za Bwana hadi sasa, (Ndio kipaku chenyewe rohoni, ila ukoma wenyewe kuenea bado).
Lakini aliruhusu kipindi cha neema cha NYAKATI SABA kipite kwanza, ili watu watengeneze mambo yao, watubu dhambi zao, Bwana awaepushe na uharibifu huo. Ndio hii miaka 2000, sasa ambapo ndani yake nyakati saba za kanisa zinapita, na sisi watu wa kizazi hiki ndio tupo katika kanisa la mwisho kabisa la saba, lijulikanalo kama LAODIKIA (Ufunuo 3:14-22).
Hivyo ni kama dalili za ukoma tu, mwisho wa siku saba, uhakika unapatikana. Na ndivyo ilivyosasa, hivi karibuni Unyakuo utapita, Bwana atawaondoa kwanza watu wake ulimwenguni. Na baada ya hapo atatusha laana yake ya mwisho juu ya huu ulimwengu, ndio vile vitasa saba vinavyozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo 16.
Jiulize ndugu yangu, je huu ukoma ulioanza ndani yako, kama kipaku, je umeshaupatia tiba? Kumbuka tiba ni Bwana Yesu, usisubiri unyakuo ukupite, au ufe katika dhambi zako, mguekie Masihi akuoshe na kukusafisha.
Maandiko yanasema kipindi cha Elisha, kulikuwa na wakoma wengi, Israeli, lakini hakutumwa kwa mmojawapo wao, ila Naamani mtu wa shamu (Luka 4:27). Kwasababu gani? Kwasababu alikubali kutii maagizo aliyopewa na Elisha kwenda kujichovya mtoni mara saba..Leo hii watu hatutaki kusoma kitabu cha Ufunuo, ambapo ndani yake tutakutana na ujumbe wa makanisa saba na nyakati zao. Ambazo kwa kuzielewa hizo tutaweza kuepukana na ukoma huu wa rohoni ambao Mungu anawapiga watu sasa.. Badala yake tunapenda kusikia habari ya kutabiriwa, na mafanikio ya mwilini.. Hii ni hatari kwasababu tunaweza kujikuta tunaachwa katika unyakuo, kama sio kufa katika dhambi.
Bwana atusaidie tulipende Neno lake.
Maran Atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?
Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?
BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?
Je mke wa Musa alikuwa ni Mweusi?
Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?
Nini tofauti ya Majira na Wakati?
Rudi nyumbani
Print this post
Mambo yaleyale waliyokuwa wanayafanya wana wa Israeli walipokuwa jangwani, yanafanywa sasa na wana wa Mungu. Ni vizuri tukafahamu asili ya ile ndani jinsi ilivyoundwa, ili tuelewe kwa undani, inavyoundwa sasa mioyoni mwa watu.
Maandiko yanatuonyesha, hawakuwa na rasilimali zozote za kuitengeneza, vilevile hawakuwa na urahisi wowote wa kuifanyia karamu yake, kwasababu pale palikuwa ni jangwani, hakuna namna wataweza kupika vyakula vizuri, pamoja na kupata pombe za kuifurahisha ibada yao.
Lakini cha ajabu ni kuwa, japokuwa changamoto hizo zilikuwepo, lakini vyote hivyo vilipatikana, na mambo yakaenda vizuri kabisa bila shida. Ndama akatengenezwa tena sio wa mawe bali wa dhahabu, vilevile Vinywaji vilipatikana(pombe zote) pamoja na vyakula vya kila namna? Na disco la miziki na vinanda juu vikawekwa.
Kutoka 32:2 “Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. 3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. 4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. 5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana. 6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze”.
Utajiuliza vilipatikanaje?
Hii ni kuthibitisha kuwa nafsi ya mtu ikidhamiria kutafuta jambo Fulani, ni lazima itapata tu haijalishi mazingira iliyopo.
Ndicho walichokifanya hawa.. Walipohitaji dhahabu, wakakumbuka kuwa wake zao, wanazo kwenye masikio yao, wanazo kwenye shingo zao.. Hivyo wakazitumia hizo hizo na kuzikusanya, zikawa nyingi, mno, wakampa Haruni akaziyeyusha na matokeo yake ikatokea ndama kubwa iliyong’aa sana.
Biblia haijatuambia pombe na vyakula vizuri walivitolea wapi, lakini ni wazi kuwa, waliagiza watu, waende nje ya jangwa kununua vyakula hivyo na pombe, katika miji ya kandokando huwenda muasisi alikuwa ni Kora au mwingine.. Au pengine wakatoa baadhi ya hizo dhahabu wakanunua. Lakini kwa vyovyote vile, na kwa njia yoyote ile, shughuli ilikamilika.
karamu ilikuwepo, watu walikula, walikunywa walisaza..na zaidi sana Sanamu yenye utukufu ilitengenezwa. Akili hizo hawakuwahi hata sikumoja kuzielekeza kwa Mungu wao aliyewaokoa kwa gharama kubwa sana kutoka kwa watesi wao wamisri, hawakuwahi kufikiria kumfanyia Mungu karama ya shukrani kama hiyo wale na wanywe mbele ya Yehova kwa matendo makuu aliyowatendea..
Hata kufikiria kutengeneza kibanda kidogo tu cha udongo kwa ajili ya Mungu wao kukutana nao, kuliko Musa kupanda huko milimani, na kutoweka muda mrefu,hawakuwahi kufikiri hivyo, wanakuwa wepesi kuwaza kuunda miungu ya dhahabu ambayo haijawahi kuwasaidia kwa chochote..Unadhani Kwa namna hiyo wangeachaje kumtia Mungu wivu?
Mambo kama haya yanaendelea sasa miongoni mwa wakristo..
Tukisikia harusi Fulani inafungwa, tunakuwa wepesi kubuni kila namna ya kuifanya ipendeze, tunaweza kutoa hata michango ya milioni moja, na kutengeneza kamati nzuri za maandalizi, tunatoa mapendekezo haya au yale, mpaka inatokea na kuvutia, hata kama ilikuwa ni ya bajeti ndogo lakini itafanikiwa tu mwisho wa siku..Lakini kwa Mungu aliyetukomboa, aliyetufia msalabani, ambaye kila siku anatupigania usiku na mchana, anatupa pumzi yake bure, hatuna muda naye..Zaidi tunaitazama nyumba yake, au kazi yake, tunaona kabisa ipo katika hali ya unyonge, lakini tunapita tu,kama vipofu, tunasema Mungu mwenyewe atatenda..
Tukiangalia tulivyovichangia katika mambo yasiyo ya msingi ni vingi kuliko tulivyovipeleka kwa Mungu. Ndugu tukiwa watu wa namna hii hapo tuwe na uhakika kuwa tumeunda sanamu za ndama nyingi, na tunaziabudu bila kujua. Na zimemtia sana Mungu wetu wivu sana.
Kukitokea party, au birthday, au tafrija Fulani, ni wepesi sana kuutikia, lakini kwa Mungu ni mpaka tukumbushwe kumbushwe, tuvutwe vutwe.. Hii inasikitisha sana.
Embu hii Ndama ya dhabahu tuivunje.. Hii miungu tuiondoe ndani yetu, mioyo yetu itusute.. Tumpe Mungu kipaumbele cha kwanza, kwasababu yeye ndio anayestahili kuliko hao wengine. Tusiwaone wale ni wajinga sana kuliko sisi. Huwenda wale wanao unafuu mkubwa zaidi ya sisi ambao tumeshaona mifano lakini tunarudia mambo yaleyale.
Tumpende Mungu, tuuthamini na wokovu wake, tuithamini pia na kazi yake.
EFATHA.
Baali alikuwa nani?
Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?
Maashera na Maashtorethi ni nini?
Kusubu ni nini? Miungu ya kusubu ni ipi?
Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
Hesabu 11:6 “lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu”
Nakusalimu katika jina lenye uweza la YESU KRISTO mwokozi wetu. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema ya kuifikia hivyo, nakukaribisha tuyatafakari pamoja maneno yake.
Wana wa Israeli walipofika jangwani hawakujua kuwa watalishwa chakula cha aina moja tu, Mwanzoni waliifurahia ile mana, jinsi ilivyokuwa nzuri na tamu, lakini siku zilivyozidi kwenda, hamu ya mana ile ikaanza kupungua ndani yao, wakaanza kutamani na vyakula vingine..Walipoona asubuhi kifungua kinywa ni mana, mchana ni mana, chakula cha jioni ni mana.. wakasema haya mambo yataendelea mpaka lini?..wakaikinai, Wakaanza kufikiria ni wapi watapata chakula cha aina nyingine walau wabadili ladha. Ni wapi watapata nyama, watapata kuku, watapata pilau, na pizza, na Baga.
Hesabu 11:4 “Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? 5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; 6 lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. 7 Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola”
Wana wa Israeli wakasau kuwa vyakula hivyo ndivyo vilivyokuwa vinawaletea magonjwa makali kule Misri, ndivyo vilivyokuwa vinafubaza miili yao. Tofauti na mana, ambayo walipoila hawakuumwa, wala kudhoofika maandiko yanasema hivyo (Kumbukumbu 8:3-4), japokuwa kilikuwa ni chakula cha aina moja tu, lakini ni salama.. Wao wakaidharau.
Ndugu yangu Mana inafananishwa na “Neno la Mungu”. Tunapookoka, tujue kuwa tutapewa chakula cha aina moja tu, nacho ni Neno la Mungu [Hilo usiliondoe akilini].. tutaamka nalo, tutatembea nalo, tutalala nalo. Ndio chakula cha Roho zetu pekee, kitufaacho kwa wakati wote hakuna kingine..Hatutalishushia na jbo lingine lolote…Hatujapewa biblia, pamoja na kitabu cha saikolojia, kitufariji Hatujapewa biblia na vilabu vya mipira (FIFA) vituburudishe , tunalimeza hivyo hivyo, bila kugoshiwa.
Lakini kwasababu ya tamaa ya mambo ya ulimwengu na mengineyo. Inasikitisha kuona wakristo wengi tunavyolikinai Neno la Mungu kwa haraka sana.. Utakuta mwanzoni mwa wokovu wetu, tulikuwa tunapenda sana kusikiliza Neno, tupo tayari kushinda muda wote kusikiliza mahubiri na mafundisho, tulikuwa tupo tayari kusoma mstari baada ya mstari, , kitabu baada ya kitabu, kudumu muda mrefu kwenye Neno la Mungu.Tukielezwa habari za mambo mengine, tuliona kama ni takataka..
Lakini ulipofika wakati tumekula tumeshiba, tunaona sasa kama hivyo vingine vya nje vinatupita.. Tunapoona biblia ni ile ile, haina matoleo mapya, maagizo ni yaleyale, yanayotutaka tuwe watakatifu na wenye imani, na tujiepushe na mambo ya ulimwengu huu.. Tunaona kama ni habari zile zile za kale za kujitesa.
Ndio hapo utamwona Mkristo anapoa anaanza, kufuatilia na miziki ya kidunia, anaanza kuwa mshabiki wa mipira na thamthilia za kidunia, tena anazichambua kwa undani kama vile tu anavyochambua Biblia, ili tu aipe nafsi yake ladha nyingine..mwingine anachanganyia na miziki ya kidunia humo humo..Mpaka Neno la Mungu linakuwa sio chakula kikuu kwake, bali sehemu ya vyakula vyake. Kama wana wa Israeli walivyoifanya mana, kuwa sehemu mojawapo ya vyakula vyao..
Lakini viliwatokea puani, wakaanza kufa, na kupata mapigo mengi sana, kutoka kwa Mungu. (Soma Hesabu 11:33).
Ndugu tunapoamua kumfuata Kristo tusitegemee tutapewa chakula kingine zaidi ya NENO LAKE. Na kama tukilikinai mapema sana, hatutamaliza mwendo wetu salama. Si ajabu tunakutwa na majaribu mengi, na mapigo mengi, kwasababu tu ya tamaa ya mambo mengine zaidi ya Neno la Mungu.
Tukijifunza kuishi sawasawa na biblia,tuitegemee hiyo tu, hata kama tutakosa vingi, hatutafaidi na vingi vya ulimwengu huu, lakini roho zetu na nafsi zetu zipo salama. Hivyo tujifunze, kukifurahia chakula hiki hiki kimoja, Mungu anatambua kuwa hatutadhoofika, kinyume chake ndio tutaimarika na kubarikiwa.
Tuache kutanga tanga na tamaa..Tii kile biblia inasema, vingine tuwaachie mataifa, Ili tuweze kufanikiwa na kuishi maisha mema katika hii dunia Mungu aliyotuweka, ndani yake.
Kumbuka shetani alilijua hilo, ndio maana alipomjaribu Bwana kule jangwani, kwa kumletea vyakula vyake vya vigeni, wakati ananjaa. Yesu alimwambia, imeandikwa mtu hataishi kwa mkate bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mathayo 4:1-4).
Akamfukuza, na wewe usimvulie shetani na mambo yake maovu.
Bwana atusaidie.
Ubarikiwe daima.
Biblia ni nini?
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Ni nani atakayeigeuza mioyo ya watoto iwaelekee mababa?
Wale mamajusi walikuwa ni wakina nani?
SWALI: Naomba kujua Mstari huu unamaana gani?
Mhubiri 6:3 ‘Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;’
JIBU: Biblia inatuonyesha yapo makundi mawili ya watu “Ambao wakiwa hapa duniani hawatapenda maisha yao hata kufa”
Kundi la kwanza: Ni la watakatifu waliojikana nafsi, mfano wa hawa ni Ibrahimu ambaye ijapokuwa alikuwa ni tajiri, mwenye mali nyingi, lakini aliishi kama mpitaji hapa duniani, akaka katika mahema, akijua kuwa wenyewe wake ni kule mbinguni, hakufurahishwa na anasa zozote za ulimwengu huu kama Lutu.
Waebrania 11:9-10
[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Mfano wa hawa pia ni akina Musa, Yohana mbatizaji, pamoja na mitume na manabii wote tunaowasoma katika biblia..(Soma Waebrania 11:23-40 )
Hawa hawakuyafurahia maisha ya duniani, walijitesa nafsi zao, wasile raha yoyote ya duniani mpaka kufa kwao . Hivyo Wana heri kwasababu katika ulimwengu ujao walioungojea watatukuzwa sana na Kristo. Na sisi pia kama wana wa manabii na mitume tunapaswa tuwe kama hawa. Akili zetu na fikra zetu tuzielekeze katika ulimwengu ule na sio hapa.
Lakini kundi la Pili: Ndio kama hilo linalozungumziwa hapo..Ambalo pia linafanikishwa duniani, linapewa uzao mkubwa, watoto wengi, linajilimbikizia mali na heshima,…lakini halinufaiki na chochote katika vitu vyake, mpaka linakufa linakuwa bado halijaridhika. Huwenda linafanyakazi miaka yote usiku na mchana hadi uzeeni, na kufanikiwa kuhifadhi fedha nyingi kwenye akaunti. Halafu linakufa bila kuonja chochote..tena linakosa maziko.
Sasa Mhubiri anasema ni heri mimba iliyoharibika..kuliko hao..kwasababu halijafaidi hapa duniani wala kule mbinguni halitaonja chochote..
Afadhali yule atuamiaye/ alaye akiba yake, hata kama hatakwenda popote lakini jasho lake limemrudishia malipo kuliko hili, ambalo lilikuwa linasubiri siku moja lijifurahishe lakini hiyo siku haijafika.
Mstari huo unafanana na ule wa juu yake unaosema..
Mhubiri 6:2
[2]mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya.
Bwana atusaidie tuwe watu wa kujiwekea hazina mbinguni. Ikiwa umebarikiwa chochote ni vema ukiwekeze kwa Mungu, kubali kuwa kama mpitaji duniani, ili utajiri wako uwe ni kule na sio hapa. Bwana Yesu alisema hazina ya duniani hupotea, na haidumu lakini ile ya mbinguni hudumu milele.
Kumbuka hazina inayozungumziwa hapa si ile ya kujitunzia akiba yako ya miezi mwili/mwaka mmoja mbele, kwa matumizi ya msingi hapana..lakini ni ile ya kujihakikishia maisha kana kwamba utaishi milele duniani, hiyo ndio inayozaa uchoyo, ubinafsi, na kutoridhika, na kuwa mtumwa wa mali n.k. Hii, Ina hatari kubwa sana, sisi kama watakatifu kesho yetu yapaswa iwe mikononi mwa Mungu, sio katika akiba zetu, kama watu wa ulimwengu huu.
Shalom.
KAMA MHUBIRI USIWE MFANO WA DIOTREFE.
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe;
SWALI: Bumbuazi la moyo ni nini? Kama tunavyosoma katika
Kumbukumbu 28:28 “BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
JIBU: Pale mtu anapopatwa na mshangao, unaomfanya ashindwe kuongea neno hata moja, au anapopigwa na butwaa..hapo tunasema mtu huyo amepigwa na bumbuazi..
Kwamfano bumbuazi linaweza likaja pale unapopishana na ajali Fulani mbaya ambayo ingekusababishia kifo, mfano labda unanusurika kugongwa na Lori la mchanga,kwa kawaida hali kama hiyo inaweza ikakufanya uwe nusu mwendawazimu hujui la kutenda muda huo, hilo ndio linaloitwa bumbuazi..
Sasa linapokuja bumbuazi la moyo, maana yake unakuwa kama mtu asiyeweza kufikiri lolote, rohoni, mtu aliyeachwa njia panda, uliyechanganyikiwa, huna ueleweko, hujielewi ni wapi unapaswa usimame..
Hiyo ndio mojawapo ya laana ambayo Mungu aliitoa kwa watu wote ambao wanaicha sheria yake, na maagizo yake..Alisema..
Kumbukumbu la Torati 28:15, 27-29
[15]Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata….[27]BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.[28]BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na KWA BUMBUAZI LA MOYONI;[29]utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
[15]Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata….
[27]BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
[28]BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na KWA BUMBUAZI LA MOYONI;
[29]utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
Hali hii ni mbaya, kwasababu inakufanya usiwe na uwezo wowote wa kuchanganua mambo ya rohoni. Unakuwa upo upo tu, huoni mbele, wala huelewi kinachoendelea.
Watu waliopigwa na bumbuazi hili huwa hawajali injili inayohubiriwa kwao hata kama ni kali namna gani, hata kama ukiwaambia Bwana asema “kesho” utakufa..Wataishia kukucheka tu.
Mfano wa hawa ndio wale wakwe zake Lutu, ambao alipokwenda kuwaambia juu ya uharibifu ambao Mungu anauleta juu ya Sodoma na Gomora..alionekana kama anacheza tu machoni pao.
Mwanzo 19: 14 ‘Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze’.
Leo hii, usiwaangalie wanadamu wanaodhihaki injili, wanaosema huyo Yesu mnayemsubiria miaka 2000 sasa yuko wapi..usiwaangalie hao…wengine tayari Mungu kashawapiga bumbuazi hili la moyo..
Ikiwa wewe unashuhudiwa ndani kwamba wakati umefika wa kumwamini Yesu na kujitwika msalaba wako na kumfuata, ni heri ufanye hivyo, bila kujali umati wa watu…okoa nafsi yako kama Lutu. Kwasababu mapigo kama haya Mungu anaendelea kuyaachilia kwa kasi sana kwa watu wanaokaidi amri zake.
Ithamini neema ya Kristo inayougua ndani ya moyo wako leo hii…kwasababu hiyo haitadumu milele, na wengi wameshaipoteza, kwa kutoitii sauti ya Kristo.
Nini maana ya “wazimu” katika biblia?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
Je! kuna madhara kuchukiwa na kila mtu kwasababu huna mali?. Kama biblia inavyosema katika Mithali 14:20?
Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
MITHALI AU METHALI ZA BIBLIA
Mego ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Mithali 17:1)
SWALI: Mstari huu unamaana gani?
Mithali 18:9 “Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu”.
JIBU: Mharabu ni neno linalomaanisha “Mharibifu”.. Hivyo hapo anaposema yeye aliye mvivu katika kazi yake ni ndugu yake aliye mharabu. Anaonyesha ni jinsi gani uvivu katika kazi, unavyokwenda sambamba na uharibifu wa vitu/mambo. Kama mtu na ndugu yake.
Kwamfano, mtu anayefanyakazi chini ya ubora, labda tuseme mkandarasi wa daraja, .. Kwasababu, hawi makini na kazi yake, atajenga daraja bovu, sasa licha ya kwamba atapoteza pesa nyingi za watu waliompa hiyo kazi, lakini pia anaweka maisha ya wengi hatarini, siku likikorongoka wengi watapoteza maisha. Sasa huyu hana tofauti na mharibifu, au Yule muuaji.
Watu wengi wamesababishiwa matatizo ya kiafya, kwasababu wamekula vyakula vilivyotengenezwa chini ya ubora. Mtu mvivu hutafuta njia ya mkato, ili kufikia malengo yake, na hiyo ndiyo inayopelekea kusababisha madhara kwa wengine..
Hata katika kazi ya Mungu, watu wengi wakiona jambo walilolitarajia linakawia au linapatikana kwa ugumu, huanza kutafuta njia za mkato kwa kutunga mafundisho ya uongo, na kutumia njia ambazo Mungu hajaziruhusu, lengo ni ili wawapate watu wengi kiharaka. Hatuwezi kusubiri, kwa kuomba na kujifunza kwa kipindi kirefu, mpaka tutakapokomaa, badala yake tunaruka madarasa ya Mungu, tunaona njia ya jangwani itatuchosha, haina faida, hatupati chochote, wacha tuifuate njia ya kora .. Matokeo yake tunafanya kazi ya Mungu chini ya ubora, tunawapotosha wengine, kwa elimu na injili gheni.
Maandiko yametutahadharisha sana katika kuitenda kazi ya Mungu, yanasema.
Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu..”
Tukiitwa kumtumikia Mungu, katika nafasi yoyote, iwe ni uchungaji, uimbaji, utume, ushemaji n.k. tukubali na gharama zake. Kwamba “tumeaminiwa uwakili” kama alivyosema mtume Paulo, tukijua kuwa siku ya hukumu tutaona hesabu ya utumishi wetu (1Wakorintho 9:16-17). Hivyo tuwe makini katika hilo, tusije tukawa waharibifu, kwa uvivu wetu.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mharabu ni nani katika biblia?
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?
Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?
Nini maana ya “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;?
Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 18:8 “Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo”.
JIBU: Mchongezi kibiblia ni mtu anayesambaza habari mbaya za wengine, au msengenyaji, na mlalamikiaji wa wengine. Jambo ambalo Mungu kalionya tangu zamani, hata kipindi wana wa Israeli wakiwa jangwani.
Walawi 19:16a “Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi;..”
Usengenyaji ni dhambi iliyostahili adhabu kali ya ukoma, kama yaliyomkuta Miriamu alivyofanya kwa Musa. Kwasababu hapo maandiko yanaeleza kuanza kwake ni kama kitoweo, yaani ni kama chakula kizuri sana kinachovutia mdomoni mwa anayekisikia.. Lakini madhara yake ni kwamba kinashuka mpaka pande za ndani za tumbo, ikiwa na maana kuwa huingia ndani kabisa ya moyo wa msikiaji, na kuzaa maumivu makali, Ni heri kingekuwa kinaishia pale mdomoni.
Ni jambo la kuwa nalo makini sana katika kanisa, kwasababu wengi wameacha imani kwasababu ya maneno, wengine wamewekeana chuki kwasababu ya kupokea taarifa zao Fulani kutoka kwa wengine. Vita vya chini chini baina ya mshirika na mshirika, upendo umepoa kwasababu tu ya uchongezi.
Pale mtu anapokufuata na kukwambia.. “nimesikia Fulani na Fulani”…”Unahabari Yule amefanya hivi au vile”…Taarifa kama hizi ngumu kukataa kuzisikia, zinakuja kama kitoweo kizuri sana, kinachovutia kukisikia, lakini hutoa chuki na hasira na uchungu ndani. Kwa mtoaji anaweza kuona kaleta habari njema, lakini kwa mpokeaji, au atakayekuja kusikia baadaye huchimbua matatizo mengi sana.
Hivyo hatupaswi kuruhusu minong’ono yoyote katikati yetu, hata kama tutaona haina madhara yoyote makubwa. Ni kudhibiti huo mnyororo haraka sana, tukiona taarifa Fulani zinaletwa kwetu zenye maudhui ya masengenyo ni kuzipinga muda huo huo, ili tuepuke madhara zaidi. Roho Mtakatifu alilionya kanisa juu ya jambo hili, hususani kwa wanawake akasema;.
Tito 2:3 “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji..”
1Timotheo 5:13 “Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa”.
Soma 1Timotheo 3:11, 2Timotheo 3:1-3.
Kama mkristo, ni jambo la kujiepusha sana, kuulinda ulimi wako.
WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA lyrics na historia
LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
KUWA MWOMBOLEZAJI.
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
SWALI: Mimi nimeokoka lakini nakuwa na hasira nyingi sana, nifanyaje ili niweze kuzizuia hasira zangu?
JIBU: Hasira zipo za aina mbili,
Kuna hasira zenye malengo chanya, na kuna hasira zenye malengo hasi.
Hasira zenye malengo chanya, zinakuwa na shabaha ya kujenga na sio kubomoa, upendo na sio uadui. Mfano wa Hasira hizi ni kama alizokuwa nazo Bwana Yesu..
Marko 3: 1-5
‘1 Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena’.
‘1 Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;
2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.
3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.
4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.
5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena’.
Halikadhalika alizidhihirisha pale alipoingia Hekaluni na kupindua meza za wafanyabiashara (Marko 11:15-18). Hata sasa hasira kama hizi za ki-Mungu zinahitajika..Pale ambapo mzazi unamwona mtoto wako, anatukana watu, halafu hudhihirishi hasira yako, kwa kumwadhibu na kumkemea hapo humpendi. Mungu aliwakasirikia mara nyingi watoto wake (Wayahudi), na kuwapa adhabu nyingi ikiwemo kuwapeleka utumwani, na kuwaweka chini ya maadui zao, n.k. Lakini lengo lake likiwa ni kuwafanya wasipotee, sio awatese (Yeremia 29:11 )
Lakini ipo hasira ambayo haitokani na Mungu bali inazalika katika wivu, kushindwa, majivuno, uchoyo. ambayo inapelekea kuleta madhara, au visasi kwa wengine. Kwa ufupi haina zao lolote la huruma au upendo ndani yake.. Mfano wa hasira kama hizi ni ile aliyokuwa nayo Kaini kwa ndugu yake, alipoona sadaka ya mwenzake imekubaliwa yake haijakubaliwa, akakasirika na kumuua.
Ni ile aliyokuwa nayo Yule mwana mkubwa, katika habari ya mwanampotevu, baada ya kuona ndugu yake aliyepotea anafanyiwa karamu yeye hafanyiwi (Luka 15:28), Ni ile aliyokuwa nayo Yona juu ya mtango, baada kuona Mungu anawarehemu watu 120,000, hawaui (Yona 4:9-11). Ndio ile iliyomfanya Simoni na Lawi kuwaua watu wasiokuwa na hatia kwa taarifa za kubakwa dada yao. Na ndio pia aliyokuwa nayo Sauli kwa Daudi.
Hasira hii, huzaa, mauaji, vinyongo na uchungu, masengenyo visasi n.k.
Lakini pia hasira hii inaweza ikazuka tu ghafla..kufuatana na asili ya dhambi ya kibinadamu.. Kwamfano, unapodharauliwa, unapopuuziwa, unapopigwa, unapoibiwa, unapodhulumiwa, unaposemwa vibaya, ghafla tu huzuka..panapofanyika kitu kinyume na ulivyotaka, unapotelekezwa, unaposalitiwa, unaponyimwa kitu, unapoelezwa ukweli n.k. Hasira hizi huwa zinawaka zenyewe katika mazingira kama haya..
Hivyo ni lazima ujue namna ya kupambana nazo, kwasababu maandiko yanasema..
Yakobo 1:20 “kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu”.
Sikuzote inakinzana na mpango wa Mungu. Hivyo uonapo hasira imekujia kutokana na mojawapo ya sababu hizo, huna budi kuishinda..
Hivyo hizi ni njia zitakazokusaidia kuishindana nayo.
Kujifunza kukaa kimya. Ni tiba madhubuti ya hasira.
Yakobo 1:19 “Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;”
Hapo anasema tusiwe wepesi wa “kusema wala kukasirika” mambo mawili, Maana yake ni kuwa Pale unapoudhiwa, ni rahisi, kurudisha majibu, aidha kwa “maneno au matendo”. Kama hutarudisha jibu la kipumbavu, basi utaonyesha kwa vitendo kama vile kurudisha rusha mkono, kusonya, kuguna, kuzira, kununa, kuzomea N.k
Haya ni mambo unapaswa ujitahidi kuyashinda. Ikitokea hii hali ndani yako, kaa kimya, adui wako wa kwanza awe ni hiyo hasira yako na sio aliyekukasirisha..Na baada ya muda itaondoka.
Bwana Yesu alisema..
Luka 6:36 “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa”.
Luka 6:36 “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa”.
Kuna kuudhiwa kweli kwenye msingi, ambapo unakuwa na sababu zote za kuwa na hasira ya kulipiza kisasi, kwamfano umeibiwa mali zako. Lakini biblia inatushauri tusiruhusu jua lichwe, bado uchungu huo upo mioyoni mwetu.
Waefeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka”;
Ikifika kesho yawaze ya siku hiyo. Yale ya jana yaache yapite.
Tunaposoma Neno maana yake tunaisoma tabia ya Kristo. Hivyo katika Neno utajifunza mambo mengi, ikiwemo uvumilivu, unyenyekevu, upendo, amani, kujitoa sadaka n.k. Ukiwa msomaji mkubwa sana utajijengea wigo wa kudhibiti hasira yako, kwamfano pale unaposoma maneno kama haya ya Bwana Yesu anayosema.
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Maombi hufukuza majaribu ya ibilisi, maombi hukuwekea wigo na mipaka rohoni. Maombi hukaribisha utukufu wa Mungu nafsini mwako. Hivyo unavyojifunza kudumu sana uweponi maana yake, uso wako unafanana na ule wa Mungu, kama vile Musa alivyokaa uweponi mwa Mungu muda mrefu siku 40, uso wake uling’aa kama malaika.
Halikadhalika ukiwa ni mtu wa maombi, ibada, mifungo, utabeba tabia za Kristo ndani yako, na hivyo utaweza kudhibiti hasira zako kiwepesi sana, lakini ukiwa ni mtu wa mwilini, hutaweza kushinda matendo ya mwili kama haya ya hasira.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
Kuliko kutazama vile vitendo 99 viovu ulivyofanyiwa, au vilivyokuudhi.. Jijengee tabia kutazama kimoja tu chema, kisha kitafakari hicho muda wote. Matokeo yake itakuwa ni kuishinda hasira. Kwamfano mzazi wako anaweza kukuudhi, ukasema kamwe sitakaa niongee naye. Lakini unasahau alishawahi kukunyonyesha katika matiti yake. Unapaswa ulifikirie hilo limoja wakati wote, bila kujali yale mengine mengi mabaya aliyokutendea. Ukifanya hivi utakuwa ni mtu wa kutokukasirika pia mapema. Lakini tukiwa ni wa kutazama tu sikuzote makosa, hasira haitaondoka.
Kibinadamu, ni ngumu sana kuona mapungufu yaliyopo ndani yako, lakini ni rahisi kuona yale yaliyo kwa wengine, Hivyo tukijifunza kupambana na hali zetu wenyewe, itatujengea unyenyekevu. Kwasababu zao mojawapo la hasira ni majivuno, kuona kwamba kila unachowaza wewe ndio bora kuliko kile.
Wafilipi 2:3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine”.
Wafilipi 2:3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine”.
Bwana Yesu alipokuwa anaudhiwa msalaba, aliwaona kama ni watu wasiojua wayatendayo, laiti wangejua wasingefanya vile. Kuna kuudhiwa, lakini anayekuudhi huwenda kasema kwa akili zake tu, lakini hakujua kinaweza kuleta madhara kwa mwingine,. Hivyo ni wajibu wako wewe ulipokeaye, kuwa na fikra hizo kama za Bwana, hutakuwa mtu wa kukasirika kiwepesi uonapo mambo hayajaenda kama utakavyo.
Hivyo kwa kuzingatia kanuni hizo basi utaweza kuishinda hali ya hasira kiwepesi. Bwana akubariki.
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
UFUNUO: Mlango wa 3 part 3
SIKU YA HASIRA YA BWANA.
Mithali 23:26 “Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. 27 Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba. 28 Naam, huotea kama mnyang’anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu”.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Kwa neema zake karibu tujifunze maneno ya uzima.
Hapo anaanza kwa kusema ‘mwanangu nipe moyo wako’..Halafu baada ya moyo anasema na “macho yako pia yapendezwe na njia zangu”…..Ni kwanini aseme hivyo? Ni kwasababu hapo ndipo kiini cha tatizo sugu la uzinzi kilipo.
Nataka tuone kwa jicho la ndani kwamba kahaba au Malaya anayezungumziwa hapa sio Yule unayekutana naye barabarani,akijiuza, bali ni Yule ambaye amesimama katika macho yako. .. Bwana Yesu alimjua kahaba huyu ndio maana akasema
Mathayo 5:28 “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”
Umeona, huyu anapitia machoni, kisha akishafunguliwa mlango anaingia moyoni mwako kuzini na wewe. Haonekani kwa macho ya kibinadamu, huyu hana gharama yoyote, hatoboi siri, wala hakuzungushi zungushi, wakati wowote ukimuhitaji yupo hapo mlangoni kwenye macho yako anataka kuingia.
Sasa akishapewa nafasi ya kutosha ndio hapo anapochukua umbile la mtu ili kujidhihirisha kwa nje tu. Ataonekana aidha kwa kumfuata wewe, au yeye kukufuata wewe..sio makahaba wote watakufuata.
Daudi hakufuatwa na mke wa Uria, bali ni yeye ndiye aliyemfuata, mwisho wa siku akatumbukia katika shimbo refu, akajitia unajisi mwenyewe(akajiongezea hila). Ni kwasababu gani? Ni kwasababu alimpa nafasi Yule aliyesimama mbele ya macho yake, alipomwona mwanamke anaoga, badala ayafiche macho yake akimbie mbali, aikatae hiyo hali isiingie moyoni mwake akairuhusu, ndipo kahaba huyo aliyechukua umbile la mke wa mtu akajidhihirisha kwa nje, akamfuata na kwenda kuzini naye.
Samsoni, hakufuatwa na Delila, isipokuwa alivutiwa katika macho yake, alipoona wanawake wa kifilisti ni warembo zaidi ya wakiyahudi,wana maumbile mazuri, wanavaa vizuri, akayatii macho yake..Na ndio hayo hayo yalikuja kupofuliwa baadaye, akatumbukia katika rima jembamba, akafa bado ni kijana.
Sulemani, hakujazuia macho yake, wala moyo wake, Ndio maana akajikusanyia wanawake wengi kwa jinsi alivyopenda, yeye mwenyewe kama alivyoandika katika kitabu cha mhubiri;
Mhubiri 2:10 “Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
Matokeo yake ikawa ni wao kumgeuza moyo. Na kumkosea Mungu, akaabudu miungu mingine, akawa ni miongoni mwa wenye hila(dosari), katika wanadamu.
Lakini Yusufu, hakuruhusu moyo wake na macho yake yashawishwe na huyu kahaba sugu, hata alipojaribiwa kwa nguvu alikimbia kabisa. Akajiepusha na anguko hilo.
Bwana Yesu alipokitazama kizazi kile, alikiona kama ni kizazi cha Uzinzi (Marko 8:38), sio kwasababu kila mtu alikuwa anazini tu ovyo ovyo huko barabarani, hapana, lakini aliwaona hawa makahaba wa siri wakizini nao mioyoni mwao,
Tusemeje sasahivi.?
Picha na video za ngono ambazo zimewaharibu watoto na vijana, vipindi vya tv, na tamthimilia na muvi ambazo zinabeba maudhui ya kizinzi ndani yake, vinaongoza matendo haya rohoni.
Kujichua, na mazungumzo mabaya maofisini, mashuleni, na vijiweni yanaongeza kwa kasi uasherati rohoni. Ni lazima tufahamu Ile kukutana na mvulana/msichana ni matokeo tu ya nje, ambayo hupaswi kujutiwa sana zaidi ya chanzo husika ambacho kinaanzia kwenye macho kisha baadaye moyoni.
Awali ya yote ni kwa kudhamiria kabisa kutubu dhambi zetu na kuuacha ulimwengu, kwa kumkaribisha Yesu mioyoni mwetu. Pili ni kwa kufanya agano na macho yetu, kama alivyofanya mtumishi wa Mungu Ayubu.
Ayubu 31:1 “Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana”?
Usifungue macho yako kushawishwa na kimelea chochote ambacho kinaweza kukusababishia tamaa moyoni mwako, pambana sana hapo, Ikiwa upo katika ndoa fungua tu kwa mkeo/mumeo..Ikiwa upo nje, usiruhusu kabisa.. weka mipaka na marafiki wa jinsia tofauti, acha kutazama muvi, au picha picha mitandaoni, acha mazungumzo mabaya, ukipishana na mwanamke amevaa kizinzi macho yako yasigeuke nyuma endelea mbele. Kwa kufanya hivyo utafanikiwa kumuua huyu kahaba atokeaye mbele ya macho yako.Na hawa wa nje watakufa wenyewe. Utaishi maisha ya ushindi sikuzote.
Bwana atuponye, Bwana atusaidie.
Mathayo 23:26 “Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi”
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.
Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
1Timotheo 5:22 “Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi”.
Hapa tunaona mtume Paulo, anampa Timotheo maagizo ya namna ya kuwa kiongozi bora (Askofu bora) wa makanisa la Mungu. Utaona anampa maagizo ya utaratibu wa kuwaandika wajane, kwamba ahakikishe wanaoandikwa ni wale walio wajane kweli kweli. (soma 1Timotheo 5:9-16).
Pia utaona anampa vigezo vya uongozi kwa viongozi wapya wa makanisa mapya, kwamba wanapaswa wawe wameshuhudiwa kuwa na sifa njema…ndipo awawekee Mikono!, lakini asiwe mwepesi wa kuwawekea mikono kwa haraka.
Na pia viongozi wa makanisa (yaani wachungaji, maaskofu na wote wanaosimama kama viongozi wa kanisa) basi wanapaswa wapewe heshima maradufu, maana yake Wakumbukwe katika riziki na mahitaji yao mara dufu zaidi ya wengine, kwasababu wanakesha kwaajili ya roho za watu, kuwaombea na kuwachunga na kufundisha.
1Timotheo 5:17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake”
1Timotheo 5:17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake”
Na zaidi sana asikubali Mashitaka ya Wazee kwa haraka, (Juu ya wachungaji, au mashemasi)..isipokuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.. kwamaana ibilisi anapenda kuwatumia watu kuzusha jambo Fulani la uongo juu ya kiongozi wa kanisa, lengo lake likiwa ni kuliharibu kundi hilo..
Kwahiyo hapa Mtume kwa uongozo wa Roho anamwonya Timotheo asiwe mwepesi kusikiliza au kuamini maneno yazungumzwayo au mashitaka yaletwayo dhidi ya viongozi wa makanisa.. Bali alichunguze jambo kwa makini mpaka atakapopata uthibitisho kamilifu kwa vinywa vya mashahidi wengi.
Lakini la mwisho kabisa Paulo anamwambia Timotheo kuwa ASIZISHIRIKI DHAMBI ZA WENGINE!.
1Timotheo 5:22 “Usimwekee mtu mikono kwa haraka, WALA USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE. UJILINDE NAFSI YAKO UWE SAFI”.
SASA NINI MAANA YA KUZISHIRIKI DHAMBI ZA WENGINE?
Kwanza ni muhimu kufahamu hao “wengine” wanaotajwa hapo ni akina nani?.. Wengine wanaotajwa hapo sio watu wa mataifa (yaani ambao hawajaokoka), la! Bali wengine wanaotajwa hapo ni “watu walio ndani ya Kanisa”. Watenda dhambi hawapo tu Bar!, au kwenye madanguro..bali wapo wengi pia kanisani.
Sasa Mtu wa kanisani anapofanya dhambi na wewe ukaiona na kuifanya kama hiyo hiyo? Maana yake na “wewe umeishiriki ile dhambi”, Kwamfano unapomwona mtu kaingia kanisani kavaa Nusu tupu, au kavaa nguzo zinazobana au zisizo na maadili, na wewe ukaona na ukamwiga, siku inayofuata na wewe ukavaa kama yeye..basi hapo kibiblia umeshiriki dhambi za huyo mwingine, hata kama kanisa zima linafanya mambo yasiyofaa sisi hatupaswi kushiriki dhambi zao, Kwasababu kuna madhara makubwa sana ya kushiriki dhambi za wengine.
Vile vile inawezekana wewe ni Mwimbaji ndani ya kanisa, lakini kuna waimbaji wenzako matendo yao ni ya giza, maandiko yanatuonya tusishiriki dhambi zao, maana yake tusiwe kama wao..
Vile vile wewe kama ni kiongozi (Mchungaji, askofu, shemasi)..halafu ukamwona kiongozi mwingine anafanya mambo yaliyo kinyume na maandiko, aidha ni mla rushwa, au ni mwizi, au mzinzi, au mlevi na anafanya mambo mengine mabaya na wewe ukaiga ule ubaya au ukaufumbia macho..kibiblia umeshiriki dhambi zake huyo kiongozi.
Na hapa Mtume Paulo anamwonya Timotheo kuwa ajihadhari asije akashiriki dhambi za wengine, ajilinde nafsi yake awe safi.
SASA MADHARA YA KUSHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE NI NINI?
Unaposhiriki dhambi za mwingine, maana yake MAPIGO nayo mnashiriki sawasawa, na LAANA pia mtashiriki sawasawa, maana yake kama Mungu amemkusudia kumwangamiza kabisa mtu huyo kutokana na tabia yake ya wizi anaoufanya kila siku ndani ya Nyumba ya Mungu, na wewe ukamwiga kwakufanya mara moja moja tu.. basi mtashiriki kiwango cha adhabu sawa.. Wewe unayeiba mara moja moja na Yule anayeiba kila siku wote kiwango chenu cha adhabu kitafanana, kwahiyo utajikuta wewe unayefanya kidogo mnapata adhabu sawa na Yule anayefanya sana.
Ndio maana Paulo anamwonya Timotheo asizishiriki dhambi za wengine, bali ajilinde nafsi yake awe safi.. Na sisi hatuna budi kuzilinda nafsi zetu ziwe safi.. Na tujiepushe na dhambi za wengine.
Maran atha!
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.
Bwana alimaanisha nini kusema “Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake”?
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).