Mtu akizaa watoto mia, lakini nafsi yake haikushiba mema;

Mtu akizaa watoto mia, lakini nafsi yake haikushiba mema;

SWALI: Naomba kujua Mstari huu unamaana gani?

Mhubiri 6:3 ‘Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;’


JIBU: Biblia inatuonyesha yapo makundi mawili ya watu   “Ambao wakiwa hapa duniani hawatapenda maisha yao hata kufa”

Kundi la kwanza:  Ni la watakatifu waliojikana nafsi, mfano wa hawa ni Ibrahimu ambaye ijapokuwa alikuwa ni tajiri, mwenye mali nyingi, lakini aliishi kama mpitaji hapa duniani, akaka katika mahema, akijua kuwa wenyewe wake ni kule mbinguni, hakufurahishwa na anasa zozote za ulimwengu huu kama Lutu.

Waebrania 11:9-10

[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Mfano wa hawa pia ni akina Musa, Yohana mbatizaji, pamoja na mitume na manabii wote tunaowasoma katika biblia..(Soma Waebrania 11:23-40 )

Hawa hawakuyafurahia maisha ya duniani, walijitesa nafsi zao, wasile raha yoyote ya duniani mpaka kufa kwao . Hivyo Wana heri kwasababu katika ulimwengu ujao walioungojea watatukuzwa sana na Kristo. Na sisi pia kama wana wa manabii na mitume tunapaswa tuwe kama hawa. Akili zetu na fikra zetu tuzielekeze katika ulimwengu ule na sio hapa.

Lakini kundi la Pili: Ndio kama hilo linalozungumziwa hapo..Ambalo pia linafanikishwa duniani, linapewa uzao mkubwa, watoto wengi, linajilimbikizia mali na heshima,…lakini halinufaiki na chochote katika vitu vyake, mpaka linakufa linakuwa bado halijaridhika. Huwenda linafanyakazi miaka yote usiku na mchana hadi uzeeni, na  kufanikiwa kuhifadhi fedha nyingi kwenye akaunti. Halafu linakufa bila kuonja chochote..tena linakosa maziko.

Sasa Mhubiri anasema ni heri mimba iliyoharibika..kuliko hao..kwasababu halijafaidi hapa duniani wala kule mbinguni halitaonja chochote..

Afadhali yule atuamiaye/ alaye akiba yake, hata kama hatakwenda popote lakini  jasho lake limemrudishia malipo kuliko hili, ambalo lilikuwa linasubiri siku moja lijifurahishe lakini hiyo siku haijafika.

Mstari huo unafanana na ule wa juu yake unaosema..

Mhubiri 6:2

[2]mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya.

Bwana atusaidie tuwe watu wa kujiwekea hazina mbinguni. Ikiwa umebarikiwa chochote ni vema ukiwekeze kwa Mungu, kubali kuwa kama mpitaji duniani, ili utajiri wako uwe ni kule na sio hapa. Bwana Yesu alisema hazina ya duniani hupotea, na haidumu lakini ile ya mbinguni hudumu milele.

 Kumbuka hazina inayozungumziwa hapa si ile ya kujitunzia akiba yako ya miezi mwili/mwaka mmoja mbele, kwa matumizi ya msingi hapana..lakini ni ile ya kujihakikishia maisha kana kwamba utaishi milele duniani, hiyo ndio inayozaa uchoyo, ubinafsi, na kutoridhika, na kuwa mtumwa wa mali  n.k. Hii, Ina hatari kubwa sana, sisi kama watakatifu kesho yetu yapaswa iwe mikononi mwa Mungu, sio katika akiba zetu, kama watu wa ulimwengu huu.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KAMA MHUBIRI USIWE MFANO WA DIOTREFE.

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.

KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe;

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments