Bumbuazi la moyo ni nini?(Kumbukumbu 28:28)

Bumbuazi la moyo ni nini?(Kumbukumbu 28:28)

SWALI: Bumbuazi la moyo ni nini? Kama tunavyosoma katika

Kumbukumbu 28:28 “BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;


JIBU: Pale mtu anapopatwa na mshangao, unaomfanya ashindwe kuongea neno hata moja, au anapopigwa na butwaa..hapo tunasema mtu huyo amepigwa na bumbuazi..

Kwamfano bumbuazi linaweza likaja pale unapopishana na ajali Fulani mbaya ambayo ingekusababishia kifo, mfano labda unanusurika  kugongwa na Lori la mchanga,kwa kawaida hali kama hiyo inaweza ikakufanya uwe nusu mwendawazimu hujui la kutenda muda huo, hilo ndio linaloitwa bumbuazi..

Sasa linapokuja bumbuazi la moyo, maana yake unakuwa kama mtu asiyeweza kufikiri lolote, rohoni, mtu aliyeachwa njia panda, uliyechanganyikiwa, huna ueleweko, hujielewi ni wapi unapaswa usimame..

Hiyo ndio mojawapo ya laana ambayo Mungu aliitoa kwa watu wote ambao wanaicha sheria yake, na maagizo yake..Alisema..

Kumbukumbu la Torati 28:15, 27-29

[15]Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata….

[27]BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.

[28]BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na KWA BUMBUAZI LA MOYONI;

[29]utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Hali hii ni mbaya, kwasababu inakufanya usiwe na uwezo wowote wa kuchanganua mambo ya rohoni. Unakuwa upo upo tu, huoni mbele, wala huelewi kinachoendelea.

Watu waliopigwa na bumbuazi hili huwa hawajali injili inayohubiriwa kwao hata kama ni kali namna gani, hata kama ukiwaambia Bwana asema “kesho” utakufa..Wataishia kukucheka tu.

Mfano wa hawa ndio wale wakwe zake Lutu, ambao alipokwenda kuwaambia juu ya uharibifu ambao Mungu anauleta juu ya Sodoma na Gomora..alionekana kama anacheza tu machoni pao.

Mwanzo 19: 14 ‘Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze’.

Leo hii, usiwaangalie wanadamu wanaodhihaki injili, wanaosema huyo Yesu mnayemsubiria miaka 2000 sasa yuko wapi..usiwaangalie hao…wengine tayari Mungu kashawapiga bumbuazi hili la moyo..

Ikiwa wewe unashuhudiwa ndani kwamba wakati umefika wa kumwamini Yesu na kujitwika msalaba wako na kumfuata, ni heri ufanye hivyo, bila kujali umati wa watu…okoa nafsi yako kama Lutu. Kwasababu mapigo kama haya Mungu anaendelea kuyaachilia kwa kasi sana kwa watu wanaokaidi amri zake.

Ithamini neema ya Kristo inayougua ndani ya moyo wako leo hii…kwasababu hiyo haitadumu milele, na wengi wameshaipoteza, kwa kutoitii sauti ya Kristo.

Maran Atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “wazimu” katika biblia?

KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?

Je! kuna madhara kuchukiwa na kila mtu kwasababu huna mali?. Kama biblia inavyosema katika Mithali 14:20?

Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)

Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)

MITHALI AU METHALI ZA BIBLIA

Mego ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Mithali 17:1)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Martha Fabian
Martha Fabian
1 year ago

Asanteni kwa ujumbe huu Mungu awabariki