Title 2021

AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.

Kufahamu huduma za Roho Mtakatifu wakati huu ni kugumu kwa wakristo, kama ilivyokuwa kufahamu huduma ya Yesu Kristo kwa wayahudi wakati ule. Wayahudi walimtazamia Kristo aje kama mfalme tu, Wakishikilia baadhi ya vifungu tu kama vile Isaya 9:6 na huku vingine wakiviacha nyuma. Hivyo pale alipokuja kama mwana-kondoo achinjwaye achukuaye dhambi za ulimwengu (sawasawa na Isaya 53) wakapoteza shabaha kabisa, na matokeo yake wakampinga wakasema huyu siye Masihi. Sisi tunafahamu masihi atakuja katika ukuu wa kifalme kama vile Daudi ili kutuokoa na maadui zetu.

Vivyo hivyo hata leo watu wengi wakisikia Roho Mtakatifu wanachojua ni kunena kwa lugha tu, halafu basi..Hawajui kazi nyingine za Roho Mtakatifu ni zipi katika kanisa, hawajui agenda yake ni ipi kwa wakati wetu huu tunaoishi sasa.

Leo tutatazama kazi ambazo Roho Mtakatifu anatarajia kuzitenda katika siku hizi za mwisho..

Ukisoma Ufunuo 1:4 inasema..

Ufunuo 1:4 “Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; NA ZITOKAZO KWA ROHO SABA WALIOKO MBELE YA KITI CHAKE CHA ENZI;”

Hapo utaona zikitajwa Roho saba za Mungu.. Sasa kiuhalisia Mungu hana roho saba, Mungu anayo Roho moja tu, ambaye ndiye Roho Mtakatifu. Lakini hapa tunaonyeshwa zikiwa saba, maana yake ni kuwa, Hizo ni SURA SABA, za Roho Mtakatifu, au HUDUMA /UTENDAJI KAZI saba wa Roho Mtakatifu.

Na utendaji kazi wake huu, ulianza kufanya kazi rasmi siku ile ya Pentekoste, na ukaendelea kutembea kwenye yale makanisa saba ambayo tunayasoma katika kitabu cha Ufunuo 2&3, kwa hizo Roho saba za Mungu..Ambapo tunajua kabisa kwa majira yakibiblia sisi tupo katika lile la mwisho la saba, lijulikanalo kama LAODIKIA.  Na kanisa hili kulingana na kalenda ya ki-Mungu lilianza mwaka wa 1906.

Mpaka hapo tunaweza kuona kabisa  kuwa sisi tunaongozwa na ile Roho ya Saba ya Mungu.

Sasa ni vizuri kujua jambo moja, kwa kawaida kitu cha kwanza na cha mwisho huwa vinakuwa na nguvu za kipekee na za kitofauti, msingi wa nyumba na finishing ya nyumba huwa vinatumia gharama kubwa sana.. Vilevile katika riadha mwanzo wa kukimbia na mwisho wa kukimbia huwa kunakuwa na ushindani sana, na ndio maana utaona wakimbiaji wengi wakikaribia kufika mwisho badala ya kupunguza mwendo utaona ndio wanaongeza nguvu zaidi.

Vivyo hivyo na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu  kwa haya makanisa saba, kanisa la kwanza na la mwisho Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa namna ya kipekee sana.. Alianza kwa nguvu nyingi sana na udhihirisho mwingi sana, wakati ule wa Pentekesto, kanisa la kwanza lilipoanza.. Na Vivyo hivyo atamaliza kwa nguvu nyingi na udhihirisho mwingi zaidi hata kuliko ule wa kwanza, kwa kanisa hili la mwisho la Laodikia.

Biblia inatuambia kipindi kile Mungu aliwatumia mitume wake, kufanya miujiza ya kupita kawaida, soma (Matendo 19:11). Na matokeo yake injili yao ikaenea ulimwenguni kote kwa kipindi kifupi sana. Miujiza kama ile iliyofanywa na mitume, mingi ya hiyo haikuwahi kutendeka kwa nyakati nyingine zilizofuata, kwasababu nyakati zilizofuata Roho Mtakatifu alitembea katika Uso mwingine na sio wa ishara na miujiza tena kama ilivyokuwa kwa kanisa la kwanza la mitume, hata zile karama za Roho nyingi hazikuonekana kwa hayo makanisa yaliyofuata. Soma historia ya kanisa utalithibitisha hilo.

Lakini tulipoingia katika kanisa hili la mwisho la Laodikia, ambalo lilianza mwaka wa 1906, Mungu alianza kuyarejesha tena yale ya mwanzo kama kipindi kile cha mitume. Karama za Roho zilianza kudhihirika kuonyesha kuwa Yule Roho wa SABA, ameanza kutenda kazi  katika uvuvio ule ule wa kama kanisa la kwanza. Na ndio maana utaona leo hii kutokana na udhihirisho wa karama za Mungu kuwa nyingi hata machafuko yamekithiri katika kanisa, manabii wa uongo wametokea humo humo, wengine wakigeuza karama za Mungu kuwa biashara na umaarufu.

Lakini ipo sehemu ya pili ambayo Roho Mtakatifu ameihifadhi kwa ajili ya WATUMISHI WAKE tu walio waaminifu. Na sehemu hiyo tunaweza kuisoma katika maandiko haya.

Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 TENA JUU YA WATUMISHI WENU, WANAUME KWA WANAWAKE, KATIKA SIKU ZILE, NITAMIMINA ROHO YANGU.

30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.

32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana”.

Ukisoma hapo kwa makini vifungu hivyo utaona sehemu ya kwanza katika unabii huo Mungu aliahidi kumwaga Roho wake, juu ya wote wenye mwili, ikiwa na maana kuwa WOTE, watakaomwamini yeye atawamwagia Roho wake bila kipimo, nao wataota ndoto, watatabiri, wataona maono..Lakini sehemu ya pili ya unabii huo, haimuhusu kila mtu. Bali itakuwa ni kwa watumishi wake tu.

Hao ndio amewaahidia, kuwamwagia Roho wake kwa kipimo cha kipekee sana na kupitia hao watakapokea nguvu za kitofauti sana, za kufanya miujiza isiyo ya kawaida.

Soma tena pale Anasema..

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.

Haya ndio Roho Mtakatifu amejiandaa kuyafanya katika nyakati hizi za kumalizia, tutaona ishara ambazo hazijawahi kurekodiwa katika historia ya dunia, mfano wa zile za Musa na Eliya. Zikifanywa na watumishi waaminifu wa Mungu. Na ishara hizi hazitakuwa kwa ajili ya maonyesho kama wanavyofanya manabii wa uongo ili kujichotea umaarufu na pesa, hapana, bali zitakuwa kwa lengo la kuyavuta yale mabaki ya Mungu yaliyosalia duniani kwa sasa ambayo yamechanganywa na ukengeufu wa dini zao uongo na makristo na manabii  wa uongo..

Zingatia, umwagiko huu hautamuhusu kila mtu, bali watumishi wa Mungu wa Kike na wa Kiume waliowaaminifu tu.

Je! Wewe na wewe upo ndani ya wokovu? Na kama upo je ni mtumishi wa Mungu mwaminifu?.

Kumbuka wakati huo upo karibuni sana kutokea. Hivyo tumika kwa Bwana wako kwa uaminifu, ili wakati huo yamkini kama ukikukuta uko hai, basi Mungu akufanye wewe kuwa sehemu ya hiyo huduma. Tumeitwa hapa duniani tumtumikie Mungu kwa uaminifu, kwa kadiri  ya karama alizotupa.

Tumtambue Roho Mtakatifu na mipango yake. Ili tuishi sawasawa na mapenzi yake hapa ulimwengu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi nyumbani

Print this post

Kujuzu ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 12:4?

Labda tuanzie kusoma kuanzia juu kidogo,

2Wakorintho 12:2 “ Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu

3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua

 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene”

Neno kujuzu maana yake ni “kutoruhusiwa”. Hivyo hapo Paulo alikuwa anaelezea maono aliyoyaona, kwamba alinyakuliwa mpaka mbingu ya tatu na kuambiwa maneno ambayo hakuruhusiwa kuyasema kwa watu.

Neno hilo pia tunalisoma katika kitabu cha Mwanzo..

Mwanzo 34: 7 “Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno LISILOJUZU kutendeka”

Hata katika imani yapo mambo ambayo hayajuzu kuyafanya..Kwa mkristo aliyeokoka, haijuzu kuupenda ulimwengu, haijuzu kuishi maisha ya dhambi na anasa, haijuzu kuwa mtukanaji, haijuzu kuwa mwizi na tapeli, haijuzu kuwa mzinzi na mwasherati, haijuzu kuwa mlevi, haijuzu kujifunga nira na watu wasioamini, na mambo mengi yote yanayofanana na hayo. Zaidi sana tunapaswa tujiweke katika hali ya usafi na utakatifu na kuchukua msalaba watu na kumfuata Yesu kila siku katika maisha yetu, kwasababu biblia inasema pasipo huo utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu.

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

KWANINI MIMI?

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

Rudi nyumbani

Print this post

Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).

 Ufunuo 21:8 “BALI WAOGA, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Mwoga ni mtu mwenye “hofu”. Na hofu inatokana na kutokuwa na uhakika wa jambo…Mtu anayekatiza mahali Fulani usiku, na hana uhakika kwamba ataimaliza hiyo njia anayoipita salama, kitakachomtawala baada ya hapo katika nafsi yake ni hofu na wala hakuna kingine, kadhalika mtu ambaye hana uhakika kwamba kesho atakula au atapata jambo Fulani, basi kinachofuata kwake ni kuingiwa na hofu vile vile mtu ambaye hana uhakika akifa atakwenda wapi, kitakachofuata kwake ni kuingiwa na hofu na mashaka… hata kama hajijui kama anayo hofu!, lakini tayari anayo.

Hivyo hofu inakuja kutokana na kukosa uhakika wa maisha,… na uhakika huo hauletwi na mwingine zaidi ya mmoja tu, ambaye ni YESU. Kwa kupitia yeye pekee ndiye anayetoa mashaka na hofu yote ndani ya mtu, anaondoa hofu ya maisha yake ya hapa duniani na ya maisha yanayokuja…kiasi kwamba mtu anakuwa hana hofu kabisa na maisha na vile vile hana hofu  ya mauti..

Waebrania 2:15  “awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa HOFU YA MAUTI walikuwa katika hali ya utumwa”.

Hivyo mtu aliye nje ya Kristo anayo hofu!.. hana uhakika kwamba kesho atakula!, hana uhakika kwamba mwezi ujao atakuwa salama, akisikia ugonjwa Fulani umezuka anaishiwa nguvu, akiumwa kidogo anapoteza tumaini lote, kila taarifa inayomjia kwake ni ya mshtuko tu!..kwaufupi kesho yake yote yamejaa mashaka!..

Na hiyo yote ni kwasababu yupo nje ya Kristo!.. na Kristo hayupo ndani yake!.. Kwasababu kama akizama kisawasawa hawezi kuwa na hofu yoyote ile!..anakuwa ni jasiri muda wote.

1Yohana 4:18  “Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo”.

Na kwasababu anakuwa hayupo ndani ya Kristo, basi ni lazima na mambo mengine maovu yatakuwa yanaambatana naye, kama ulevi, uashetari, uzinzi, usengenyaji, tama mbaya, kuupenda ulimwengu n.k … na hivyo hawezi kuurithi uzima wa milele, kwa tabia hizo.

Ufunuo 21: 7  “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

8  BALI WAOGA, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Je! Wewe ni mwoga?. Jipime kama una hofu ya kifo!, au una mashaka baada ya kifo utaenda wapi, basi! Kuna uwezekano bado hujakamilishwa katika pendo la Mungu.. Unamhitaji Kristo aingie katika maisha yako ili akupe uhakika wa uzima wa milele.. Uhakika huo utaitupa nje hofu yote.. hutaogopa kufa hata ukiambiwa leo ndio safari yako ya maisha imefika ukingoni, hata ukisikia kuna ugonjwa fulani hatari umezuka, hata ukisikia taarifa zozote za kuogopesha, wewe siku zote utabaki kuwa jasiri, zikija tufani, dhiki, tabu wewe unabaki yule Yule…huogopi ogopi.. Vile vile kama unaogopa wachawi, majini au kulogwa, bado Kristo hajaingia maishani mwako.

Marko 4.39  Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40  Akawaambia, MBONA MMEKUWA WAOGA? Hamna imani bado?

41  Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Nasi tukiwa ndani ya Yesu na Yesu akiwa ndani yetu, hofu yote inaondoka!..

 2Timotheo 1: 7 “ Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”.

Kumbuka tena WAOGA, wote hawataurithi uzima wa milele. (1Yohana 4:18).Hivyo woga pia ni kipimo tosha cha kujijua kama kweli tupo kwenye mstari wa Imani au la!.

Bwana atusaidie na kutubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

AOGOPACHO MTU ASIYE HAKI NDICHO KITAKACHOMJILIA.

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Kicho ni nini? (Waefeso 5:21, 2Samweli 23:3)

CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.

SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

JE! WEWE NI MFUNGWA WA BWANA?

Utumwa siyo neno zuri, lakini pia ni neno zuri. Watu wa dunia hii wanao watumwa,lakini pia Yesu Kristo anao watumwa wake. Ndio maana alisema maneno haya..

Mathayo 11:28 ”  Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”

Hapo hasemi kuwa tukishakwenda kwake ni kupumzishwa tu, basi na baada ya hapo hakuna kitakachoendelea..la! Hakusema hivyo, badala yake alisema “JITIENI NIRA YANGU” na tena anasema” mzigo wangu ni mwepesi “….Kumbe! Na yeye anayo nira!.. maana yake anatutoa kwenye utumwa mmoja na anataka kutuingiza kwenye utumwa mwingin!.. Tofauti ni kwamba nira yake yeye ni laini na pia mzigo wake ni mwepesi…

Lakini pamoja na hayo hasemi kwamba ” yeye atatutia nira yake,baada ya kutufungua hiyo nira ya adui ” badala yake anasema ” JITIENI NIRA YANGU ” huo ni kama “Ushauri” na siyo “amri”. Ingekuwa ni amri angesema ” njooni kwangu nami nitawapa pumziko na kuwatia nira yangu “..hapo ingeweza kuwa amri, lakini mpaka anasema sisi ndiyo tujitie nira yake… huo ni uchaguzi!!.. maana yake ukipenda kuwa huru sawa, au ukipenda kuichukua NIRA mpya ya YESU KRISTO ni vizuri zaidi…

Sasa kama hujui nira ni nini,..nira ni kifungo Fulani ambacho mnyama kama ng’ombe anavikwa shingoni, kama nyenzo ya kuvuta mzigo ulio nyuma yake..kadhalika na Kristo naye anayo nira ambayo anawafunga watu wake wale ambao kwa mapenzi yao wameamua kujitia katika UTUMWA WAKE. Na wanapofungwa Nira hiyo, wanageuka kuwa WAFUNGWA. Maana yake  wanakuwa ni wafungwa wa YESU kwa ajili ya Injili. Mfano wa hao ni Mtume Paulo 

Filemon 1:1 “Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemon mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi “

Waefeso 3:1 ” Kwasababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwaajili yenu ninyi Mataifa; 2 ikiwa mmesikia kwa habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu”

2Timotheo 1:8 ” Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi MFUNGWA WAKE, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwaajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu “

Wakolosai 4:3 ” Mkituombea na sisi pia,  kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo  kwaajili yake nimefungwa,

4 ili niidhihirihe, kama inipasavyo kunena”.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu KUFUNGWA kwa Paulo katika misitari ifuatayo (Filemon 1:9, Waefeso 4:1, Filemon 1:23).

Zifuatazo ni tabia za Wafungwa wa Kristo, kwa ajili ya Injili. 

Muda wote, masaa yote wapo katika mazingira ya kuifanya kazi ya Mungu.Mtume Paulo wa kwenye biblia na wengine baadhi, walijitoa katika Injili kiasi kwamba hawakuwa na muda wa kutafuta wake, akili zao zote zilikuwa katika kuifanya kazi ya Mungu, mambo ya ulimwengu huu waliyaona kama mavi (Wafilipi 3:8).

Hawaionei haya Injili.2Timotheo 1:8 ” Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake ,bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili,kwa kadiri ya nguvu ya Mungu. 

Wamejikana nafsi kweli kweli.Hakuna mtumwa yeyote anayekuwa na uhuru asilimia zote, muda wote utamkuta eneo la kazi..kitu kinachompa hofu kuliko yote ni kuipoteza kazi yake au kuiharibu, na kitu pekee kilichomuunganisha yeye na Bwana wake ni kazi yake hiyo aliyopewa, ya Injili. Huwezi kumkuta mtumwa aliye makini, muda wa kufanya kazi yupo anazurura!.. kadhalika wafungwa wa Yesu, kwaajili ya Injili hawazururi zururi katika huu ulimwengu, shughuli shughuli na anasa za ulimwengu huu, zinawapita! Na wala hawazitamani.. macho yao ni kuifanya kazi ya Bwana na kuimaliza.. kuhubiri  Injili kwao ni sharti! Sio ombi tena! 

1Wakorintho 9:16 ” Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili.17 maana nikitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili”.

Je wewe ni mfungwa wa Yesu?.. umejitia NIRA ya Bwana Yesu shingoni mwako?.. Au bado unayo nira ya adui shetani?.. Nira ya adui shetani ni ulevi unaoutumainia ambao unakufanya kuwa mtumwa wa pombe na singara!.. Nira ya shetani ni uzinzi na ukahaba unaoufanya ambao huwezi kuishi bila huo.. Nira ya adui shetani ni ushabiki wa mpira unaokufanya uwe mtumwa wa huo mpira.. Nira ya adui shetani ni tamaa zote za macho ambazo zimekufanya kuwa mtumwa..Nira hiyo huwezi kujivua mwenyewe, kwasababu aliyekufunga hukuwa na nia ya wewe kukuacha huru siku moja!

 Hivyo huwezi kujifungua, unamhitaji Yesu azivunje!… ndipo uwe huru!…  kwasababu kwa nguvu zako haiwezekani.. na baada ya kukufungua!, anakupa shauri la wewe kujitia nira yake!.. hapo siyo yeye anakufungua hiyo nira! Ni wewe ndio unayeamua kujifunga nira yake.. na kama ukitii na kukubali kumtumikia Yesu kwaajili ya Injili  yake, na kuwa mfungwa wake.. yeye alisema maneno haya..

Marko 10:28″ Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.

29 Yesu akasema, Amini,nawaambieni, Hakuna mtu aliyeach nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwaajili yangu,na kwaajili ya Injili,  30  ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, au ndugu wake, na mama, na   watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele “

Kumbuka kama bado hujampokea Yesu, basi fahamu kuwa bado unayo nira ya adui shetani mwako, na upo kwenye utumwa wa dhambi hata kama hujijui, Hivyo mgeukie leo Kristo akuweke huru,Yeye mwenyewe alisema ” Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli ( Yohana 8:36)”,

Hivyo tubu leo kwa kumaanisha kuacha dhambi zako zote unazozitenda kwa siri na kwa wazi, na kisha tafuta ubatizo sahihi, ubatizwe kwaajili ya ondoleo la dhambi zao, ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu ( Matendo 2:38), Na baada ya hapo amua kujitia Nira ya Kristo,  kwa kudhamiria kumtumikia yeye kwa gharama zozote zile, na Bwana mwenyewe atakufanya kuwa mtumwa wake.. na thawabu yako itakuwa kumbwa hapa duniani na utakapofika mbinguni. 

Bwana akubariki.

  +255693036618/ +255789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengin

Mada Nyinginezo:

 

                                                                                                             

 

 

 

 

 

 

Print this post

WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO.

Shalom. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Karibu tuyatafakari maneno mazuri ya uzima.

Ulishawahi kuutafakari vizuri huu mstari?

Isaya 35: 8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO”.

Sana sana hapo mwishoni anaposema “ wajapokuwa wajinga, hawatapotea”?…. Maana yake ni kuwa kuna uwezekano kweli wa kuwepo watu wa Mungu baadhi, wanaotembea katika wokovu, lakini kwa namna moja au nyingine wanaoujinga fulani ndani yao.

Na ujinga huo unaweza kusababishwa na aidha kutoyaelewa vizuri maandiko, au kushindwa kuulewa uweza wote wa Mungu, na njia zake, Lakini pamoja na kuwa watu hao watakuwepo, lakini biblia bado inasema, maadamu wapo katika NJIA KUU, njia ya uzima,NJIA YA UTAKATIFU, kamwe hawatapotea.

Leo hii sehemu nyingi utapita na kukutana na kundi la watu linasema, “kama ulokole ndio ule ni heri nibaki katika dhambi zangu”, walokole ni wavivu, wenyewe kazi yao ni kukaa muda wote kusali tu na kufunga makanisani hawana shughuli nyingine yoyote ya kufanya.. Utakutana na wengine wanasema, walokole kazi yao ni kujinyima tu, kupendeza hawapendezi, wapo rafu rafu, kama Mungu ndio hivyo heri nibakie katika  udunia wangu tu..

Ndugu, biblia inasema, hata kama wanachokifanya ni kutokana na ujinga wao.. Lakini maadamu wameupokea wokovu, wamekusudia kumfuata Mungu wao, kamwe hawatapotea, hata iweje, hilo ni hakikisho kutoka kwa Mungu. Hata wakiwa wamekataa kwenda shule, hata wakiwa wanalala maporini, hata wakiwa wanafunga mwaka mzima, hata wakiwa hawajui vizuri kusoma na kuandika, kamwe usitazamie watu kama hao watapotea..Hilo ondoa akilini.

Lakini kama wewe ni rafiki wa dunia. Unajiona njia zako ndio zipo sawa, unaona njia za watu wa kidunia ndio sahihi, jinsi wanavyoishi kwa raha, wanavyostawi, wanavyoruka ruka, wanavyopiga makeup, na kutembea uchi barabarani, na kuvaa milegezo, wewe ndio unapendezwa nao, nataka nikuambie hata kama utakuwa na akili vipi, mwisho wa siku utaishia pabaya tu. Kwasababu biblia inasema hivyo.

Mithali 14:12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”.

Wewe unayejiona, maisha ni anasa, na huku Kristo yupo mbali na wewe, mwisho wako utakuwa jehanamu, wewe unayejiona maisha ni kujiachia na kuzini, na kufanya kila aina ya dhambi kama unavyojisikia, yaani kwa ufupi unaupa moyo wako kila kitu unachopenda, na huku unaona wokovu ni mzigo mzito. Jiandae kukutana na mauti.

Umekuwa ukiwadhihaki wakristo, na kusema wale ni wajinga, wamerukwa na akili, Mungu gani wanayemuabudu anawafanya kuwa vile, wanaomba usiku na mchana, na hakuna muujiza wowote unaotendeka. Ndugu hata kama ni wajinga, lakini ufahamu kuwa ujinga wao wanaufanyia wakiwa katika gari ambalo lipo safarini.

Na wewe akili zako unazionyesha ukiwa nje ya gari. Hiyo ndio tofauti kati ya wewe na wao.. Hizo akili zitakusaidi nini ukifa leo, itakufaidia nini upate ulimwengu mzima, halafu unapata hasara ya nafsi yako?. Kama unadhani ni  wapumbavu, basi ingia ndani ya Kristo, na wewe uwepo ndani ya gari hilo salama, ndipo uutoe huo upumbavu ulio ndani yao. Lakini kama upo nje ya Kristo, ujue wewe ndio mjinga wa mwisho kabisa.

Haya maisha ni mafupi sana, nakushauri umpe Yesu maisha yako ndugu yangu. Leo unayo pumzi, lakini siku ya kesho hujui utakuwa wapi, hata kama utakuwepo kumbuka Maisha ni fumbo hakuna anayejua siku ya kuondoka kwake, hivyo yatupasa kila siku tujichunguze, Je! Bado tupo ndani ya gari la mbinguni au tulishashuka siku nyingi?

Bwana atusaidie sote.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengin

Mada Nyinginezo:

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

The King’s Highway — A Journey to God through Christ

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

KWANINI KRISTO AFE?

Rudi nyumbani

Print this post

Zunga ni nini? (Walawi 12:3, Kutoka 4:24)

Neno hilo utalisoma kwenye vifungu hivi katika biblia;

Walawi 12: 3 Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake.

Kutoka 4:24 “Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, Bwana akakutana naye akataka kumwua.

25 Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi”.

Zunga ni kipande cha govu kilicho mbele ya maumbile  ya mwanaume. Pale anapotahiriwa kipande hichi cha nyama ndicho kinachoondolewa. Hicho ndicho kinachojulikana kama Zunga.

Mungu alitoa maagizo kwa Ibrahimu na wazao wake wote, kuwa watahiriwe, kwa kukatwa zunga zao. Na kwamba hiyo ndio itakuwa dalili ya agano aliloingia nao, siku zote za maisha yao.

Mwanzo 17:9 “Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.

10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.

12 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako”.

Mwanzoni Ibrahimu wala wa Israeli hawakuelewa ufunuo wa Mungu kuwaambia wafanye vile. Lakini sisi tuliomwamini Kristo leo hii ndio tunaofahamu kuwa. Kumbe kila mwanadamu anazaliwa na zunga lake la asili(yaani dhambi ya asili) rohoni. Na kwamba linapaswa litoke, kwa kukatwa. Na linaondolewa kwa kumwamini tu Yesu Kristo, ambapo kunaambatana na kubatizwa katika ubatizo sahihi.

Wakolosai 2:11 “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.

12 Mkazikwa pamoja naye KATIKA UBATIZO; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”.

Unaona, usipotahiriwa moyo wako, wewe huna agano na Mungu. Hivyo kwasasa tohara yetu sio tena ya mwilini, bali rohoni, Na kila mmojawetu ni sharti awe nayo.

Wafilipi 3:3 “Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili”.

Swali ni Je! Umeokoka? Je! Umebatizwa ipasavyo?. Kumbuka ubatizo sahihi ni muhimu katika ukristo wako, na tohara yako ya rohoni kama tulivyosoma hapo juu. Yakamilishe maagizo yote ya Bwana Yesu, kwasababu hatuokoki kwa kukiri tu bali pia na kwa kubatizwa, na ubatizo ni sharti uwe wa kuzamishwa kwenye maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38, 8:16:, 10:48, 19:5

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! ULEVI NI DHAMBI?.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).

WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.

Vyombo vya uzuri ni vipi vinavyotajwa katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

MAVUNO YAMESHAKWISHA  SHAMBANI.

Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”.

Bwana Yesu asifiwe ndugu mpendwa..

Ukitaka kujua kuwa mambo yote sasa yameshakamilika, kinachongojewa ni UNYAKUO tu, angalia hali ya mavuno shambani mwa Bwana. Embu fananisha watu waliokuwa wanamjia Kristo kipindi cha mitume, na watu wanaookoka sasa  katika kipindi chetu hichi.

Kipindi kile injili ilipokwenda kuhuburiwa mahali kwa mara ya kwanza, mwitikio wa watu  wa kumgeukia Kristo ulikuwa ni wa kustaajabisha sana, utakumbuka baada ya Pentekoste tu, kanisa lilikuwa likijiongeza  kwa idadi ya maelfu, kwa injili ndogo sana. Na ndio maana kwa kipindi kifupi sana, ukristo ulienea ulimwenguni kote, na sio kuenea tu, badi kuhubiriwa (Wakolosai 1:6, 1Wathesalonike 1:8).Hiyo ni kuonyesha kuwa kweli ule ulikuwa ni wakati wa mavuno.

Lakini angalia sasa,  mambo ni tofauti hakuna mtu asiyeifahamu injili, au kuzijua habari za Kristo, wote tunazifahamu, lakini jiulize kwanini, watu hawataki kuokoka, kinyume chake ndio wanakwenda mbali kabisa na Ukristo..Hiyo ni kuonyesha kuwa mavuno yameshakwisha shambani, kilichobaki ni magugu tu.

Na hiyo imepelekea sasa injili kubadilika sio tena ya kuwavuta watu, bali ni ya ushuhuda. Unapoona, injili imekufikia hapo ulipo kitandani kwako ukiwa umeishika simu yako na kusoma, ujue hiyo sio ya kukuvuta wewe, hiyo ni ya ushuhuda tu, ukiona injili imekufikia hapo sebuleni kwako unapotazama tv na familia yako, injili inakufikia kwenye hivyo vipeperushi unavyovisoma huko mitaani. Unapewa biblia bure ya kwenye simu yako, mambo ambayo hata zamani hayakuwepo. Basi ujue hiyo sio injili ya kukuvuta tena kwa Kristo ndugu. Ni injili ya USHUHUDA Tu. Ili utakapokufa katika dhambi zako, usiwe na sababu ya kusema sikuwahi kusikia, au kuona, au kuambiwa.

Wewe jiulize tu, ni kwanini pamoja na mahubiri yote hayo uliyohubiriwa na kuyasikia siku zote za maisha yako, na bado huna badiliko lolote ndani yako. Unadhani ni jambo la kawaida? Hapana, kwa kawaida Neno moja tu lingetosha kukufanya uwe mtakatifu sawasawa na Waebrania 4:12.  Lakini hujageuka kwasababu  wewe sio Ngano bali ni gugu tu.

Kilichosalia sasa hivi ni Mungu anatazama walau kama yatakuwepo masalia salia machache ayaokoe. Lakini nataka nikuambie, moja ya hizi siku ambazo zinahesabika, tutashuhudia mabadiliko makubwa sana duniani. Tutashuhudia tendo kuu la Unyakuo wa kanisa.

Ndio yale maneno ambayo Bwana Yesu alisema, .(Mathayo 24:40-42) yatatimia hapo. Usiku huo wawili watakuwa wamelala mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wanasaga(ikimaanisha watakuwa katika biashara zao), mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa. Wale watakaoachwa, huku duniani kitakachokuwa kinaendelea ni vilio na kusaga meno. Wakijuta kwanini kipindi kile hawakuitii sauti ya Mungu, ilipokuwa inawavuta kwake kwa upole. Watalia na kuomboleza, kweli kweli, ndugu usiwe mmojawapo.

Lakini watakaokuwa wamenyakuliwa, moja kwa moja wataelekea mbinguni wakiwa na miili yao ya utukufu, katika ile karamu ya mwana-kondoo.  Kwenye raha isiyokuwa na kifani. Wakifutwa machozi kwa taabu zao walizokuwa wanapitia huku duniani kwa ajili ya Kristo.

Ndugu mambo haya unaweza kuona kama ni hadithi, au mambo yatakayotokea miaka elfu 5 mbeleni, usijidanganye. Yesu aliposema TUBUNI, kwa maana ufalme wa mbinguni UMEKARIBIA. Alikuwa hasemi uongo. Ni kweli ufalme wa mbinguni  ulikuwa umekaribia, jiulize  sisi wa sasa hivi tusemeje?.

Maanisha kugeuka, unaposikia injili kwa wakati huu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

UFUNUO: Mlango wa 14

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Je watu ambao hawajasikia kabisa injili watahukumiwa?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya kuoatama katika biblia?

Kuoatama ni lugha ya zamani, inayomaanisha “kwenda haja kubwa”

Kumbukumbu 23:13 “nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho;

 14 kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha”.

Wana wa Israeli walipewa maagizo na Mungu, waweke mazingira yao yanayowazunguka katika hali ya safi!.. Kwamba watu wasafishe mazingira ya maeneo wanayoishi, wasikae katika uchafu, mtu anapokwenda haja kubwa, angalau ahakikishe uchafu wake hauachi juu, bali aufukie.

Na hiyo ni kwasababu Bwana Mungu anapita katikati ya mazingira yao, ili kuwapigania..Hivyo apitapo na kuona au kukuta uchafu (mf. Kinyesi n.k), atageuka na kuwaacha!.

Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu haangalii roho tu, bali pia anaangalia pia Mwili na mazingira. Kama Mungu anaweza kuwaacha tu wana wa Israeli kwasababu ya kinyesi kilichozagaa juu ya ardhi, ataachaje kumwacha binti anayevaa nusu uchi?, ataachaje kumwacha binti anayevaa vimini au nguo zinazobana na kuchora maungo yake, ataachaje kumwacha kijana aliyejichora mwili wake?.

Ndugu, mahubiri ya kusema kwamba Mungu haangalii mwili anaangalia tu roho! Ni ya kutoka kuzimu!!, jihadhari nayo, ni ya adui shetani asilimia mia. Tunawajibu wa kujitunza miili yetu, kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na vile vile tunawajibu wa kujiweka safi katika mazingira pia ya nje, kwasababu Mungu wetu pia ni Mungu wa usafi na si uchafu. Kama anayatazama mazingira ya nje, na kutoa hukumu, hatashindwa kutazama mwili wako na kutoa hukumu.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)

Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?

]https://wingulamashahidi.org/2020/11/26/lango-limebadilika/

Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

Rudi nyumbani

Print this post

NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!

Katika ukristo ogopa sana ile kauli ya kusema “Huu si wakati”… “Bado kidogo”…. “Wakati wake utafika tu siku moja”… Ogopa sana kauli kama hizo, tena ziogope kuliko  ukoma.

Kwanini ninakuambia hivyo? Ni kwasababu wakati ambapo unafikiria majira yake bado, huo ndio wakati Kristo anatazamia kuona matunda kwako. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na asili. Hana tabia ya kutafuta matunda wakati wa msimu. Haongozwi na misimu.

Embu kitafakari vizuri kitendo alichokifanya siku ile alipokuwa anakwenda Yerusalemu kutokea Bethania, alipokutana na ule mtini njiani, alifanya nini!. Utaona alikwenda moja kwa moja na kutafuta matunda juu yake, Na alipokosa akaulaani na kunyauka saa ile ile , pasipo kujali kuwa ule haukuwa hata msimu wake wa kuzaa..

Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; MAANA SI WAKATI WA TINI.

14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”.

Hili ni jambo ambalo watu wengi hawalifahamu, wanapoangalia mazingira Fulani, wanaona kama vile wakati wake bado, pale mtu unapomuambia biblia inasema “saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubalika kuokoka ni leo (2Wakorintho 6:2 )” yeye atasema, ngoja kwanza, siku moja nitaokoka tu!, ngoja nimalize chuo, ngoja nioe kwanza, ngoja nipate kazi, ngoja nitoke kwanza kwa wazazi wangu..Ngoja nijenge nyumba yangu kwanza..

Huku akitazamia kweli siku moja akishavipata hivyo vitu  ndio atatulia afikirie sasa kumtumikia Mungu. Lakini hajui wakati amekaa akiungojea huo wakati  ufike Kristo anatokea ghafla kwenye maisha yake, kutafuta matunda, anayakosa, hatua inayofuata kwake ni KULAANIWA MILELE.

Maana yake ni kuwa kamwe asahau WOKOVU katika maisha yako, na ndio maana watu kama hao ambao wana tabia ya kusubiri, subiri, kujivuta vuta, mwisho wa siku unawakuta mpaka wanakufa hawajaokoka haijalishi kuwa wameshapata kila kitu. Sio kwamba kulikuwa na ugumu wowote. Hapana lakini kwasababu walishalaaniwa na Yesu tangu zamani, walipotazamiwa wamzalie Kristo matunda wakashindwa.

Hivyo ndugu, tambua kuwa jicho lako sio jicho la Yesu. Wewe unatazama misimu, Yesu hajui msimu. Wewe unatazama nyakati, Kristo hajui nyakati. Wakati wowote anataka ajapo akukute, ukiwa na matunda. Akukute unamzalia matunda ya Roho. Lakini ukiwa ni mtu wa kusubiria siku Fulani ifike ndio ufanye maamuzi. Upo katika hatari kubwa sana ya kulaaniwa.

Wana wa Israeli, kuna wakati nao pia walijibunia utaratibu kama huo, wakati ambapo Mungu alishawapa tamko la kwenda kumjengea nyumba, Lakini walipopokea vitisho kutoka kwa mfalme aliyefuata kwamba waache ujenzi, wao nao wakasikiliza sauti yake kweli wakaacha. Ukisoma pale utagundua kuwa Kilichofuata ni Mungu kuwalaani, akawapiga kwa umaskini na shida zisizokuwa za kawaida. Mpaka siku walipogundua kosa lao, na kwenda kumjengea tena Mungu nyumba, walijutia mawazo yao.

Hagai 1:2 “Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana.

3 Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,

4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika”?

Leo hii, mtu akishazuiwa na wazazi wake, au boss wake, au mume wake, basi hiyo ndio inakuwa tiketi ya yeye kuukimbia kabisa wokovu au utumishi wa Mungu, akijitetea kuwa pengine haukuwa wakati sahihi na ndio maana vikwazo kama hivyo vimetokea. Nataka nikuambie, ondoa hayo mawazo kuanzia leo, kwasababu hata kwa Yesu hayapo, utalaaniwa.

Upokee wokovu leo, tubu dhambi zako leo, kuwa tayari kubatizwa katika ubatizo sahihi  leo, anza kuishi maisha matakatifu yampendezayo Mungu, bila kujali mazingira, watu, hali, au msimu,..Na baada ya hapo yeye mwenyewe atakupokea na kukujalia kuzaa matunda wakati huu huu, unaoonekana kama haufai kwako.

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, wakati wa mavuno umekaribia sana, dalili zote zinaonyesha kizazi chetu tunachoishi kitashuhudia tukio halisi la kurudi kwa Bwana Yesu duniani mara ya pili, kulinyakua kanisa lake. Jiulize Ikiwa atarudi leo usiku utakuwa na lipi la kujitetea, ikiwa hukumpa maisha yako? Au ukifa leo utamweleza nini huko uendako kama Yesu si mwokozi wa maisha yako.

Usizifiche dhambi zako, ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako. Basi popote pale kama utahitaji msaada huo wasiliana nasi kwa namba hizo hapo chini, au tafuta kanisa la kiroho lililo karibu na wewe, wakusaidie kupokea wokovu.

Kisha hakikisha unatafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi, na kwa jina la YESU KRISTO (Zingatia sana hilo), kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

AINA TATU ZA WAKRISTO.

UFUNUO: Mlango wa 22

JE UNAYAFANYA MAPENZI YA MUNGU?

Mlima wa Mizeituni  unaumuhimu gani kwetu?

VAZI LA YESU HALIGAWANYWI.

Rudi nyumbani

Print this post

UKIOKOKA,HIZI FIKRA ZIKIJA NDANI YAKO, ZIKATAE.

Kuna silaha ambazo nataka ufahamu shetani anazozitumia kwa watu ambao wanakaribia kuokoka, au waliookoka lakini bado ni wachanga katika imani. Silaha hizo, zimewafanya watu wengi waishi katika hofu, na misongo mikubwa ya mawazo, mimi nikiwa mmojawapo kabla sijaokoka.

Nataka nikuambie mawazo haya yakikujia, yakatae kwa nguvu zako zote, kwasababu ni vita vya kifikra ambavyo shetani na majeshi yake ya mapepo wanavyoleta ili kukuangusha uiche imani, au usisonge mbele. Narudia tena usiruhusu hata kidogo mawazo hayo yakutawale;

     1)  Umemkufuru Roho Mtakatifu:

Hii ndiyo silaha ya ibilisi ya kwanza ; Anakuletea mawazo kuwa wewe huwezi kusamehewa, kwani dhambi yako ni ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Na anaweza kukurushia mpaka hayo mawazo ya namna hiyo ili ujione wewe tayari dhambi yako imeandikwa kwa kalamu ya chuma.

Nataka nikuambie, huo ni uongo tu, dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haiji hivyo. Na kamwe mtu aliyemkufuru Roho hata hofu na Mungu hana ndani yake, ni mfano wa mafarisayo na masadukayo ambao walikuwa wanazipinga kazi za Roho Mtakatifu wazi wazi na kuzishuhudia hadharani kuwa ni za mapepo wakati wanaujua kabisa ukweli kwamba na Roho Mtakatifu ndiye aliyekuwa anafanya kazi zile (Mathayo 12:24-32).

Sasa jiulize wewe ni lini ulishawahi kwenda kuzipinga kazi za Roho Mtakatifu huku ukajua kabisa ndio yeye, halafu ukatoa maneno ya kufuru  na kusema zile ni kazi ya mapepo..Ulishawahi kufanya jambo kama hilo mbele ya kadamnasi? Ni wazi kuwa hujawahi kufanya.. Sasa hayo mawazo ya wewe umemkufuru Roho Mtakatifu yametoka wapi kama sio kwa shetani?

Watu wengi, nimewasiliana nao, wamekuwa wakisumbuliwa na mawazo mkandamizo kama hayo, Lakini leo nataka nikuambie Usiogope, hiyo ni ishara kuwa Mungu yupo karibu na wewe sana, unachopaswa kujua ni kufahamu ile kweli, ili ikuweke huru kweli kweli.

   2) Bado hujaokoka: 

Unaweza ukawa umetubu kweli dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha, na ukabatizwa katika ubatizo sahihi, na baada ya hapo ukaanza kuishi maisha yanayompendeza Mungu, Lakini kipindi fulani kikapita shetani akakuletea mawazo kwamba bado hujaokoka, wanaookoka hawawi kama wewe. Mawazo kama haya, yakatae, Bwana Yesu alisema, “Hakuna mtu anayeweza kwenda kwake, kama Baba yake hajamvuta kwake (Yohana 6:44)” Hivyo mpaka wewe umefikia hatua ya kutubu, na kubatizwa na kuanza kuonyesha bidii ya kuishi sawasawa na mapenzi yake, haikuwa kwa akili zako, bali ni Yesu mwenyewe alikuvuta.

Hivyo songa mbele, zidi kujitakasa siku baada ya siku, mpaka kuufikia ukamilifu kwasababu Yesu yupo pamoja na wewe.

  3) Umeshachelewa:

Hili ni jambo lingine ambalo, limewadhoofisha wengi. Wanadhani elimu ya kidunia ni sawa na elimu ya ufalme wa mbinguni. Elimu ya kidunia, ukishakuwa mtu uzima na hujaenda shule, unaweza ukaonekana kama umeshachelewa. Duniani ukifikisha umri fulani hujaolewa, au hujapata kitu fulani umeshachelewa. Lakini kwa Mungu haiendi hivyo, maadamu pumzi ya uhai ipo ndani yako bado hujachelewa kumtumikia yeye.

Mungu anakutazama, ufanye vizuri isipokuwa tu uonyeshe bidii, ili ufanye vizuri kuliko hata wale ambao walikuwepo tangu zamani. Embu mkumbuke mtume Paulo, hakuwa miongoni mwa wale 12, wala siku ile ya Pentekoste hakuwepo. Lakini alikuja kufanya kazi kubwa kuliko wote waliomtangulia.

Ukumbuke pia ule mfano wa mwajiri na waajiriwa ambao Bwana Yesu aliutoa, akasema kulikuwa na wengine ambao walikutwa jioni kabisa hawana kazi yoyote, wakaambiwa waende shambani, na kule shambani walipomaliza shughuli yao, wakalipwa sawa sawa na wale wengine, ambao walikuwa tangu asubuhi shambani.(Mathayo 20:1-16). Na ndio maana Bwana Yesu akamalizia na kusema “wapo walio wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wale wa kwanza watakuwa wa mwisho”.

Vivyo hivyo na wewe, ikiwa umeitwa kwenye miaka ya 20, au 30 au 40 au 50 au 80. Hujachelewa  popote pale. Mtumikie Bwana kwa moyo wako wote na kwa uaminifu. Na thawabu yako inaweza kuwa kubwa kama tu ile ya mitume.

   4) Mungu hawezi kupendezwa na wewe:

Haya mawazo yanakuja hususani pale ambapo pengine hukutumiza wajibu wako fulani uliloambiwa na Mungu ufanye, au ulifanya dhambi fulani ambayo ilikuwa ni ya makusudi kabisa kwa Mungu, pengine ulivunja viapo vya ndoa yako ukaenda kuzini, au uliua mtu, au uliiba n.k..

Nataka nikuambie kama umetubu tayari kwa kumaanisha kutoka katika moyo wako. Basi usiruhusu tena hayo mawazo yawe ndani yako, kukutawala. Mrudie Mungu wako, mtumikie kwa bidii, kwani kumpendeza tena kunawezekana, na akawa rafiki yako, zaidi hata ya pale mwanzo kama utatii. Daudi alizini ni mke wa Uria, lakini alitubu, hata baada ya kuadhibiwa na Mungu, aliendelea kumtafuta Mungu wake, na mwisho wa siku bado akawa mtu ambaye ameupendeza moyo wa Mungu.

    5) Fulani ni bora kuliko wewe mbele za Mungu:

Haya ni mawazo mengine ya ibilisi, kukukandamizi tu usipige hatua, kwamba fulani ni zaidi yako wewe mbele za Mungu. Hilo jambo halipo, Mungu hana utaratibu huo wa kulinganisha watu.Yeye huwa anasimama katika utaratibu wake. Ni sawa na mwalimu anayesahihisha mitihani, hasahishi kwasababu fulani ni machachari kuliko wengine, hapana, bali kwasababu amejibu sawasawa na alichotaka.

Ndivyo ilivyo kwa Mungu, hana habari na sura ya mtu, ikiwa wewe utatembea katika njia zake, basi atakuwa rafiki kwako, wala hakulinganishi na mtu mwingine aliye juu yako au aliye chini yako, na Yule mwingine hamlinganishi na wewe, bali wote anawalinganisha na Neno lake, kila mmoja kivyake.

Hivyo na wewe tembea katika njia yako, na Mungu wako, acha kujilinganisha na fulani, jilinganishe na biblia. Vinginevyo shetani atakuletea mikandamizo ya mawazo ukashindwa kumtumikia Mungu kwa ufanisi, kwa kumwona fulani tayari ni mtiwa mafuta wa Bwana, wewe huwezi kumfikia yeye.

Mawazo kama hayo yakatae.

Kumbuka, kuingia katika wokovu ni kurahisi sana, lakini kudumu kunakuwa kugumu, na hiyo yote inasababishwa na shetani na mapepo yake, Na dawa ya shetani sio tu kuomba, bali pia kulijua NENO. Nikisema Neno, sio kukariri vifungu vya biblia hapana, bali kupata ufunuo wa Neno la Mungu katika maisha yako ya kila siku.

Bwana Yesu alimshinda shetani kwa Neno kule jangwani, vivyo hivyo na wewe. Mungu anaweza akawa ameshakupa uhuru, lakini kama hutakuwa na maarifa ya kutosha ya kuupigania uhuru wako, bado ibilisi atakusumbua hata kama umeokoka. Maombi ya kufunguliwa pekee hayawezi kukufanya kuwa huru.. Kama ni hivyo Bwana Yesu asingesema..Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32)Umeona kinachokamilisha uhuru wa mtu ni KWELI, na KWELI ni Neno la Mungu. (Yohana 17:17)

Hivyo jitahidi sana, uwe mtafakariji wa Neno. Ili ujue nafasi yako kwa Mungu ni ipi, wakati huu ni wakati wa vile VITA vikali ambavyo, Danieli alionyeshwa, katika (Danieli 10:1). Si vita tena vya kimwili, bali vita vya kifikra vinavyoletwa na ibilisi na mapepo yake.

Kama hujatubu, nafasi bado unayo. Tubu sasa mgeukie muumba wako, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, ikiwa hukufanya hivyo. Na baada ya hapo Mungu atakupa Roho wake Mtakatifu atakayekusaidi kuifahamu kweli yote ili uwe huru (Yohana 16:13).

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post