Naomba kujua kama Maji ya Zamzam yapo kibiblia na kama tunaweza kuyanunua na kutumia.
Jina kuu la Mwokozi wetu Yesu libarikiwe.
Maji ya Zamzam ni maji yanayoaminika kutoka katika kisima kimoja kilichopo Saudi Arabia kujulikanacho kwa jina hilo Zamzam.
Baadhi ya waarabu wanaamini kisima hicho ndicho kile kisima ambacho Hajiri aliyekuwa kijakazi wa Sara, mke wa Ibrahimua alioneshwa na yule malaika katika Mwanzo 21.
Mwanzo 21:17 “Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. 18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. 19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. 20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde. 21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Mwanzo 21:17 “Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Lakini je! Kuna ukweli katika hayo?
Jibu ni la! Hakuna ukweli katika hayo, Kisima Hajiri alichooneshwa na Malaika hakikuwepo katika nchi ya Saudia, bali katika jagwa la Parani, ambalo lipo maeneo karibia na jangwa la Sinai, mbali kabisa na Saudia.
Kadhalika biblia haijarekodi popote kuwa kisima hicho kilikuwa kinaitwa Zamzam, wala haijarekodi kuwa baada ya hapo maji yake yalikuwa ni matakatifu. Kilikuwa ni kisima tu kama kisima kingine ambacho Mungu alikitumia kumwokoa Ishmaeli pamoja na mamaye, hakikuwa cha kimiujiza, wala hakikubeba nguvu zozote za kiungu baada ya hapo.
Imekuwa ni kawaida watu kufanya ziara sehemu ambazo kulionekana uweza wa kiMungu.
Kwamfano utaona leo hii watu wanakwenda mlima Sinai, na kwenda kuadhimisha au kufanya ibada, mahali pale Musa alipoona kijiti kikiteketea, vile vile utaona wengine leo hii wanakwenda kuchukua maji ya mto Yordani, mahali ambapo Bwana Yesu alibatiziwa na Yohana Mbatizaji, wengine watachukua udogo kutoka Yerusalemu .nk. wakiamini kuwa vitu hivyo vina uungu wa kipekee na wakitofauti.
Pasipo kujua kuwa wamedanganyika, yule Adui shetani kawapofusha macho yao, wakifikiri wanamwabudu Mungu kupitia vitu hivyo kama wanamwabudu yeye.
Bwana Yesu alisema maneno haya.
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.
22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Umeona?. Nyakati hizi Mungu haabudiwi tena katika milima, wala katika udongo wala katika maji..bali anaabudiwa katika Roho na Kweli..
Hivyo mtu anayetumia kitu chochote kwa imani kuwa kinamsogeza kwa Mungu zaidi, au kinampatia uponyaji..basi mtu huyo kadanganyika na uongo wa adui.
Kama unapitia ugonjwa au tatizo, tumepewa jina la Yesu, ambalo hilo tukitamka mara moja tu kwa Imani, kazi zote za shetani zinavunjika.
Je! Umemwamini na kumpokea Yesu, wewe unayesoma ujumbe huu?. Kama bado unasubiri nini?..mpokee leo na akuoshe dhambi zako nawe utapata uzima wa milele.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
BIRIKA LA SILOAMU.
Je! Ni sahihi mtu kubatizwa kwenye maji ya KISIMANI?
Rudi nyumbani
Print this post
Maandiko yanasema, Neno la Mungu ni kama Upanga unaokata kuwili, (yaani una makali pande mbili,mfano wa sime). Na lina uwezo wa kuzigawanya Nafsi na Roho.
Mtu aliyejikana Nafsi yake, na kuyakataa mapenzi yake kwajili ya Mungu, maana yake ni kwamba Neno la Mungu kama Upanga limeingia ndani yake na kuitenganisha Roho yake na Nafsi yake, ndio maana mtu huyo haishi tena kwa nafsi yake, bali kwa roho yake tu, ambayo hiyo ndio inayotenda mapenzi ya Mungu!
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata KUZIGAWANYA NAFSI NA ROHO, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”.
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata KUZIGAWANYA NAFSI NA ROHO, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”.
Umeona?, hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kumtenga mtu na nafsi yake, isipokuwa Neno la Mungu tu!.. Hakuna mtu anayeweza kusema ameukataa ulimwengu, amejikana nafsi yake na huku upanga haujapita moyoni mwake.
Upanga wa Mungu yaani Neno lake, ndio unaoweza kututenga sisi na mambo ambayo tumeshindwa sisi kutengana nayo kwa nguvu zetu, huwezi kujitenga na hasira kama huu upanga hujapita ndani yako,kukutenga wewe na hiyo hasira, huwezi kujitenga na vinyongo na visasi kama huu upanga hujaingia ndani yako, kuna vitu unaweza kujitenga navyo, lakini kuna vingine vinahitaji upanga wa Roho (Neno la Mungu), ili vikuachie.. kwasababu vimejishonanisha na roho yako, au nafsi yako.
Ni lazima uruhusu upanga uingie ndani yako ili uweze kuvitenganisha vitu hivyo.
Sasa utaruhusu vipi huu upanga uingie ndani yako?
Maandiko yanasema Bwana Yesu ndiye Neno la Mungu,
Ufunuo 19:13 “Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi”.
Ufunuo 19:13 “Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi”.
Unaweza kusoma pia Yohana 1:1, utaliona jambo hilo hilo,
Hivyo kama Kristo ndiye NENO LA MUNGU, maana yake yeye ndiye UPANGA, ambapo anapoingia moyoni anatenganisha roho yako na nafsi yako, hakuna chochote kilichopo ndani yako kilichojificha asikijue, atayasafisha mawazo yako yote na kutenganisha uovu na wema ndani yako. Na kukuweka katika hali salama ya kuyatenda mapenzi ya Baba tu.
Kumbuka tena maandiko yanasema..
Hivyo kama tunataka kuwa wakamilifu, kama tunataka kuwa huru rohoni, kama tunataka kuyatenda mapenzi ya Mungu, BASI TUNAMHITAJI YESU SANA MIOYONI MWETU.
Wengi leo wanaye YESU katika biashara zao, wanaye Yesu katika watoto wao, wanaye Yesu katika viungo vyao, lakini hawana Yesu MIOYONI MWAO. Upanga umepita katika shughuli zao, upanga umepita katika biashara zao hata wameona shetani kawekwa mbali nao, kadhalikaupanga umepita katika miili yao hata wameona wametengwa mbali na magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua lakini UPANGA BADO HAUJAINGIA MIOYONI MWAO.
Mariamu aliyekuwa mamaye Yesu, ijapokuwa alikuwa na Yesu katika tumbo lake, lakini wakati ule bado alikuwa hajampata Yesu moyoni..Ndio maana Simoni, Yule nabii mzee alimwambia maneno haya..
Luka 2:34 “Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. 35 NAWE MWENYEWE, UPANGA UTAINGIA MOYONI MWAKO, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi”.
Luka 2:34 “Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
35 NAWE MWENYEWE, UPANGA UTAINGIA MOYONI MWAKO, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi”.
Kuna tofauti kubwa ya Yesu kuwepo tumboni mwa Mariamu na Yesu kuwepo moyoni mwa Mariamu..Ulifika wakati Mariamu alikuwa hana budi kumwamini Yesu kama mwokozi wake na Bwana wake, na si kama “mtoto wake”. Nafasi ya Mariamu kama mama wa Yesu, iliwahi kuisha mapema sana, kabla hata ya Bwana Yesu kusulubishwa, Mariamu alishaacha kitambo sana kumwona Bwana kama mwanawe, ilifika wakati alianza kumjua kama Bwana na Mwokozi, na kuyaamini maneno yake na kwenda kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. (Huo ni wakati ambapo upanga uliingia ndani yake na yeye pia).
Swali la kujiuliza ni je! Na wewe Upanga umeingia moyoni mwako?, au upo tu! Nje kwenye biashara yako?. Upanga ukiingia ndani yako kule kuupenda ulimwengu kunakufa, kule kujikana nafsi kunaingia ndani yako, kiasi kwamba hata ndugu wakuchukie, hata marafiki wajitenge nawe, hata ukose kila kitu lakini huwezi kuacha kuyafanya mapenzi ya Baba.
Dunia nzima inaweza kukuona umerukwa na akili, lakini wewe unajitambua unazo akili timamu katika Kristo. Mageuzi kama hayo katika maisha yako ndio uthibitisho kuwa Upanga umeingia ndani yako.
Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; LA! SIKUJA KULETA AMANI, BALI UPANGA. 35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. 37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. 39 MWENYE KUIONA NAFSI YAKE ATAIPOTEZA; NAYE MWENYE KUIPOTEZA NAFSI YAKE KWA AJILI YANGU ATAIONA.
Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; LA! SIKUJA KULETA AMANI, BALI UPANGA.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
39 MWENYE KUIONA NAFSI YAKE ATAIPOTEZA; NAYE MWENYE KUIPOTEZA NAFSI YAKE KWA AJILI YANGU ATAIONA.
Kama bado hujampokea Yesu maishani mwako, basi mtafute mtumishi yoyote wa Mungu wa kweli, na mweleze kuwa unahitaji kumpokea Yesu, atakusaidia katika kukuongoza sala ya kumpokea Yesu, au wasiliana nasi kwa namba hizi hapa chini.
NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.
Kwanini Bwana Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakanunue upanga?
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
KUNA NGUVU YA ZIADA KATIKA KULING’ANG’ANIA KUSUDI LA MUNGU.
Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?
SWALI: Nini maana ya huu mstari
Kumbukumbu 27: 24 “Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina”.
SWALI: Kulingana na sheria ya wayahudi, kosa lolotela kumdhuru mwenzako, liwe ni dogo au kubwa, lilipoonekana, adhabu yake ilitolewa palepale kulingana na kosa lenyewe.. kwamfano ukimng’oa mwenzako jino, na wewe pia uling’olewa la kwako, ukimtoa jicho, na lako pia linatolewa, ukiua na wewe pia uliuliwa,..hapo ndipo uovu ulipoweza kuondoka juu ya mtu.
Lakini kulikuwa na makosa mengine watu waliyafanya kwa siri, ambayo hayakuwa rahisi kugundulika kwa wazi, wanashangaa tu labda mtu kafa, wakidhani ni siku yake tu imefika, kumbe aliwekewa sumu siku nyingi ambayo ilikuwa inamuua kwa taratibu..
Sasa watu kama hawa, biblia inasema, wamelaaniwa, kwasababu wanawapiga wenzao kwa siri, wakidhani kuwa hata mbele za Mungu hawataonekana.
Mfano wa watu kama hawa katika biblia ni Yezebeli. Yeye alikwenda kumuua Nabothi Myezreeli, ili tu alipate shamba lake, akawaajiri watu wa kushuhudia uwongo waseme wamemsikia Nabothi amemtukana Mungu na mfalme, ili watu wampige mawe afe, na kweli akafanikiwa adhma yake, na watu hawakujua lolote.
Lakini Mungu alijua, ndipo akamtuma nabii Eliya kumtolea hukumu yake. Na kumwambia mbwa watamla maiti yake. Na kweli ndivyo ilivyokuja kuwa (1Wafalme 21).
Mwingine ni mfalme wa Daudi, yeye alimuua askari wake aliyeitwa Uria kwa siri akidhani kuwa Mungu hatamwona. Alichofanya ni kumwambia mkuu wake wa majeshi amweke, Uria mahali penye vita vikali, kisha wamuache mwenyewe, ili azidiwe na majeshi ya adui auliwe, na kweli, njama zake zilifanikiwa, lakini Mungu akamrudia Daudi na kumpa adhabu kali sana, na doa ambalo mpaka leo hii sisi tunalisoma (2Samweli 11).
Hata leo, watu wanawapiga wenzao kwa siri, kwa kuwawekea vikwazo mbalimbali, lakini kwa nje wanajifanya wapo Pamoja na wao kuwasaidia, tukiwa watu wa hivi Mungu atatulaani. Halikadhalika Wachawi wote wapo chini ya hii laana, kwasababu mchana wanacheka na wenzao kinafki, lakini usiku wanazunguka huku na huko kuwanga, na kuwasababishia wenzao madhara, na kuvuruga mipango ya watu wanaotaka kumtafuta Mungu.
Hivyo tuwe makini sana, ni heri uadhibiwe na mwanadamu, kuliko kuangukia katika laana za Mungu mwenyewe. Kwasababu yeye ndiye anayeichunguza mioyo ya watu. Ili tuweze kuishinda hii hali, hatuna budi kumaanisha kumfuata Kristo kweli kweli katika Maisha yetu. Hapo ndipo tutakapoweza kuishi Maisha ya upendo na wengine.
Bwana akubariki.
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?
MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!
Ni SIRI gani Paulo aliyokuwa anaimaanisha katika Waefeso 5:32?
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
Katika Agano la kale zilikuwepo aina za sadaka mbali mbali, ambazo Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wazitoe, ilikuwepo sadaka ya Amani, sadaka ya dhambi, sadaka ya kuinuliwa, kadhalika ilikuwepo sadaka ya kutikiswa na nyingine nyingi. Leo tutaitazama hii sadaka ya kutikiswa kwa ufupi na ujumbe wake katika roho.
Awali ya yote ikumbukwe kuwa makuhani peke yao ndio waliopewa dhamana na Mungu ya kutumika katika nyumba yake, na ndio waliopewa dhamana ya kufanya shughuli zote za kikuhani, ikiwemo kupokea sadaka kutoka kwa watu, walizomletea Bwana. Sadaka hizo zilikuwa za aina tofauti tofauti, zilikuwepo za wanyama, zilikuwepo za ndege kama njiwa, zilikuwepo pia za nafaka kama ngano, unga na nafaka nyingine.
Endapo Mtu akileta sadaka yake ya mnyama kama kondoo, basi alimleta kwa kuhani, kisha kuhani atamchinja Yule kondoo na kuichukua damu yako, ambayo hiyo ndiyo itakuwa kwaajili ya upatanisho wa Yule mtu, kisha viungo baadhi atavichoma juu ya madhabahu ndani ya Hema au hekalu mbele za Bwana, na sehemu ya nyama iliyobakia ambayo haijachomwa, Mungu aliruhusu Kuhani huyo iwe yake yeye na familia yake (Ndio mshahara wake). Makuhani walikuwepo wengi wanaofanya kazi hizo, na walikuwa wanafanya kazi hizo kwa zamu.
Na sadaka ya unga, ilikuwa ni hivyo hivyo, kiwango kidogo kilichomwa juu ya madhabahu mbele za Bwana na kiwango kilichobakia kilikuwa ni kwaajili ya Makuhani waliohudumu katika nyumba ya Bwana, Sadaka zote za dhambi na hatia ndio zilikuwa zinatolewa kwa utaratibu huo.
Sasa sadaka ya Kutikiswa ilikuwa ni tofauti kidogo, Kwani baada ya sadaka kupokelewa na Kuhani, kama ni Nafaka au Mnyama. Basi kuhani alichukua kwanza sehemu ndogo ya sadaka hiyo na kuinyanyua juu na kisha KUIPUNGA HEWANI MBELE ZA BWANA, kwa mfumo wa KUITIKISA TIKISA, Kisha baada ya hapo ataishusha chini, na kuendelea na hatua nyingine za kutekekeza baadhi ya viungo juu ya madhabahu, na sehemu iliyobakia ni riziki yao.
Sadaka ya kutikishwa ilihusisha aina zote za sadaka, yaani za Wanyama, ndege pamoja na Nafaka. Sasa sio kila sadaka wana wa Israeli walizokuwa wanazileta zilitikiswa namna hiyo mbele za Bwana, la! Bali ni baadhi tu!.
Walawi 7:28 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,29 Nena na wana wa Israeli uwaambie, Yeye asongezaye dhabihu yake ya sadaka za amani kwa Bwana, atamletea Bwana matoleo yake, kutoka katika ile dhabihu ya sadaka zake za amani;30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa SADAKA YA KUTIKISWA MBELE YA BWANA.31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu; lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na cha wanawe.32 Mguu wa nyuma wa upande wa kuume mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka katika hizo sadaka zenu za amani.33 Katika wana wa Haruni, huyo atakayeisongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake, yeye atapata mguu wa nyuma wa upande wa kuume kuwa sehemu yake.34 Kwa maana, HICHO KIDARI CHA KUTIKISWA, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.”.
Walawi 7:28 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
29 Nena na wana wa Israeli uwaambie, Yeye asongezaye dhabihu yake ya sadaka za amani kwa Bwana, atamletea Bwana matoleo yake, kutoka katika ile dhabihu ya sadaka zake za amani;
30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa SADAKA YA KUTIKISWA MBELE YA BWANA.
31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu; lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na cha wanawe.
32 Mguu wa nyuma wa upande wa kuume mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka katika hizo sadaka zenu za amani.
33 Katika wana wa Haruni, huyo atakayeisongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake, yeye atapata mguu wa nyuma wa upande wa kuume kuwa sehemu yake.
34 Kwa maana, HICHO KIDARI CHA KUTIKISWA, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.”.
Mistari mingine inayozungumziwa sadaka hiyo ya kutikiswa ni Kutoka 29:27,Walawi 8:27, Walawi 9:21, Walawi 10:14, Hesabu 6:20, Hesabu 8:11, na Hesabu 8:18.
Sadaka hiyo imebeba ujumbe gani kwetu?
Mungu aliruhusu baadhi za sadaka zitolewe kwa njia ya kawaida na nyingine zitolewe kwa njia hiyo ya kunyanyuliwa juu na kutikiswa tikiswa, (yaani kuipungia hewani)
Kutufundisha kuwa na sisi hatuna budi kuzitofautisha sadaka zetu, Sadaka ya kumshukuru Mungu kwa matendo aliyokufanyia mwaka mzima, au mwezi mzima, au jinsi alivyokuokoa na majaribu makuu haiwezi kuwa sawa na sadaka ya kawaida unayomtolea siku zote, Ya shukrani ni lazima iwe ya juu kidogo, na uitangaze mbele zake, kwasababu ya matendo makuu aliyokufanyia, ni lazima iambatane na kuinyanyua mikono yako juu na kumwimbia kwa kumshukuru, na kumtukuza, Sadaka ya namna hiyo inapendeza zaidi mbele za Mungu wetu..
Bwana atubariki.
Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?
Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?
Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
Shalom, karibu tujifunze na tujikumbushe wajibu wetu sisi kama watakatifu katika safari yetu ya Imani hapa duniani.
Kuna mambo ambayo tunaweza tukashindwa kumfanyia Mungu, tukadhani kuwa “Mungu anaelewa”, kumbe yanatafsirika kama Ni UDHURU mbele zake.
Tofauti na sisi tunavyoweza kutafsiri Neno udhuru. Kwamba ni kutoa sababu za uongo, ili tu kuepuka jukumu au wajibu Fulani, kwamfano, labda mtu kakuambia naomba ukanipakilie mzigo wangu kwenye gari pale stendi unitumie.. Sasa pengine wewe hutaki kwenda, ili kupindua hiyo safari, saa hiyo hiyo unaunda safari yako ya uongo na kumwambia, hapana sitaweza kwenda, kwani ninamgeni wangu natarajia baadaye, nikamchukue hotelini sijui atatoka muda gani..Lakini unajua kabisa, jambo kama hilo hukuwa na mpango nalo, huo ndio udhuru tunaoufahamu sisi.
Lakini kwa Mungu udhuru, ni kutoa sababu za kweli tena zenye maana na mashiko kabisa.. ambazo wakati mwingine ni kweli kabisa zinastahili kufanywa.. Ili kuelewa vizuri Embu tusome tena Habari hii kwa utulivu, naamini umeshaipitia mara kadhaa, lakini isome tena, na tena, uone ni nini Mungu analenga, na ujiangalie na wewe katika nafasi yako, Je! Mambo kama hayo yapo?,,Tusome..
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, 17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. 18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. 19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. 21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. 22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. 24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,
17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.
20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.
23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.
24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Embu zitafakari hizo sababu, uone kama hakuna hata moja isiyo na mashiko, ni kweli, sherehe tu, huwezi ifananisha na mke mpya..mwingine kanunua ng’ombe, wengi, hivyo ni lazima siku hiyo akawajaribu kwanza, vinginevyo wakiwa sio bora na siku imeshapita hawezi tena kuwarudisha,tayari ni hasara, mwingine kanunua shamba tayari, lakini bado hajaliona, hivyo ni lazima akalihakiki, kama ni lenyewe au kama ameuziwa dimbwi, na siku yenyewe ndio hiyo hiyo ya karamu aliyoalikwa hawezi kuacha kwenda?
Umeona, zote hizo zilikuwa ni sababu, lakini mwenye karamu anazitafsiri kama ni Udhuru. Kwasababu gani? Kwasababu wameyathamini mambo yao, Zaidi ya ile karamu yake kubwa.
Leo hii,watu wengi hata jumapili wameacha kwenda kanisani kabisa, wanasema, boss wangu hataki, wanazitetea kazi zao, ili wasifukuzwe..halafu kwenye vichwa vyao wanasema BWANA ANAELEWA!…Kama ingekuwa sio huyu boss wangu kunizuia, mimi nisingekosa kanisani hata siku moja..
Ndugu kwa Mungu huo ni udhuru..Kama unaweza kuitumikia kampuni yako, kwa siku 6 za wiki, hadi siku ya Mungu unaiiba, fahamu tu, Mungu hawezi kukuelewa, anautafsiri kama Udhuru. Haiwezekani wiki nzima, usijiwekee ratiba kwa Mungu wako ya kumwabudu yeye, hata siku moja.
Danieli hakuruhusu udhuru, hata alipokatazwa na mfalme wa dunia yote,(kumbuka Sio boss wa ka-kampuni fulani) kuabudu Mungu wake, na vitisho vyao vya kuwatupa katika tundu la simba wote watakaokaidi. kinyume chake Danieli ndio alifungua madirisha yake, akawa anamwabudu Mungu, wakati wengine, wanasema Mungu anaelewa, hali halisi ya sasa, tumekatazwa na mfalme, sisi ni nani tupinge..
Na walipomkamata na kumtupa katika tundu la Simba, Tunaona Mungu alikuwa naye..
Vivyo hivyo na akina Shedraka, Meshaki, na Abednego, walikataa udhuru wa Nebukadreza wa kuabudu sanamu, wakati wengine wanasema, Mungu anaelewa..wenyewe wakakataa kumvunjia Mungu heshima, ndipo walipotupwa katika tanuru la moto..Bwana aliwapigania na kuwaokoa.
Lakini ikiwa sisi kila jambo tutazama, hali zetu, tusijidanganye kuwa Mungu anaelewa! Hizo zote ni udhuru. Usiruhusu kazi ile muda wa Mungu wako, usiruhusu, familia, mihangaiko, mali zitafune muda wa Mungu wako. Wengine wanasema jumapili ndio faida ninapata, ndugu ziache hizo faida zipite, Ni nani kakuambia Mungu hatakupa hizo siku nyingine? epuka udhuru..
Na ndio maana mwishoni kabisa mwa ile Habari, Bwana anasema…
“Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.
Watu wanaotanguliza mambo yao mbele Zaidi ya Mungu katika kipindi hichi cha siku za mwisho, kwenye Unyakuo, kwenye karamu ya mwanakondoo mbinguni hawataenda. Swali je! Na wewe ni mtu wa udhuru kwa Bwana? Jibu unalo.
Maran atha.
Maswali na Majibu
UFUNUO: Mlango wa 19
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
WhatsApp
SWALI: Kulingana na Danieli 7:14 inatabiri kuwa Ufalme wa Bwana Yesu utakuwa ni wa milele, Lakini tukirudi katika 1Wakorintho 15:24 anasema mwishoni atampa Baba yake ufalme wake,
Je hapo inamaana gani , Bwana Yesu ataurejesha ufalme kwa Baba yake au?
JIBU: Tusome vifungu vyote..
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
Pia..
1Wakoritho 15:24 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
1Wakoritho 15:24 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
Ni vema tukumbuke kuwa Mungu na Yesu, sio watu wawili tofauti, wenye falme mbili tofauti.. Hapana, “SIRI ya uungu” ni kubwa sana, kama vile mtume Paulo alivyoandika katika 1Timotheo 3:16, Ikiwa na maana mtu usipofumbuliwa macho na kuielewa sehemu ya siri hii, anaweza kudhani Bwana Yesu na Baba yake, ni watu wawili tofauti kabisa…
Ukweli ni kwamba, ufalme Yesu, ndio ufalme wa Baba yake, na Ufalme wa Baba yake ndio ufalme wa Yesu, hivyo akimrudishia Baba ufalme, hakufanyi badiliko lolote, kwasababu yeye na Baba ni kitu kimoja. Ni kama anavyopenda tu yeye mwenyewe atawalie katika ofisi ipi!! Je ya Baba au ya Mwana.. hivyo tu..
Kwahiyo Ufalme huo, kwasasa unatawala rohoni, lakini utadhihirika rasmi, tunapoingia katika ule utawala wa miaka1000, ambapo Mungu (Ndani ya Kristo), atatawala kwa miaka hiyo elfu mpaka atakapohakikisha kila kitu kiovu kimefikia mwisho wake, Kisha baada ya hapo, atatawala sasa kama Baba (Yehova), milele na milele.
Na ndio maana ufalme wake ni wa milele na milele na milele.. Ambao hauwezi kuhasika na kwenda kwa adui, au kwa Malaika yoyote, au kwa kiumbe chochote, utabaki kwake milele na milele na milele. Utukufu na shukrani vimrudie yeye daima.
Amen.
YESU NI NANI?
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
DANIELI: Mlango wa 11
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
UNYAKUO.
Maneno hayo tunayasoma katika kile kitabu cha Mathayo 18:18,
Mathayo 18:18 “AMIN, NAWAAMBIENI, YO YOTE MTAKAYOYAFUNGA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGWA MBINGUNI; NA YO YOTE MTAKAYOYAFUNGUA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGULIWA MBINGUNI”
Sasa ili tuweze kuelewa vizuri tuanzie kusoma mistari ya juu kidogo, mstari wa 15
Mathayo 18:15 “Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18 AMIN, NAWAAMBIENI, YO YOTE MTAKAYOYAFUNGA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGWA MBINGUNI; NA YO YOTE MTAKAYOYAFUNGUA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGULIWA MBINGUNI ”.
Mathayo 18:15 “Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
18 AMIN, NAWAAMBIENI, YO YOTE MTAKAYOYAFUNGA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGWA MBINGUNI; NA YO YOTE MTAKAYOYAFUNGUA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGULIWA MBINGUNI ”.
Katika mazingira kama hayo Bwana alimaanisha kuwa, inapotokea mtu mmoja (aliyeokoka), kafanya kosa basi unapaswa ukamwonye ukiwa wewe na yeye peke yenu, akikusikia na kutubu basi utakuwa umemwokoa kutoka njia ya upotevu (yaani umempata), lakini kama hajakusikia wewe baada ya kumwonya kimaandiko, maandiko yanasema ukachukue watu wengine wawili au watatu urudie mmwonye tena kwa pamoja na kama hataki kusikia basi kanisa liambiwe na aonywe na wengi zaidi na kama pia hataki kusikia na kutubu kwa kosa lake hilo au makosa yake…, maandiko yameruhusu mtu huyo kuachwa kama alivyo.
Na madhara ya kuachwa na kanisa kama alivyo ni makubwa kwasababu hayaishii tu hapa duniani, bali hata mbinguni mtu huyo anakuwa ameachwa (ametengwa na uwepo wa Mungu)..Hakuna chochote atakachovuna katika roho baada ya hapo, mpaka yeye mwenyewe atakapotubu..
Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kuitii injili. Hususani tunapoisikia zaidi ya mara moja, pale inapotuonya, kwasababu tusipoitii, basi inageuka kwetu kuwa USHUHUDA, (yaani sababu ya kutuhukumu siku ile ya mwisho), na inakuwa inafungwa juu yetu, kwasababu tumeidharau, na inapofungwa juu yetu, maana yake imekuwa imetufungia na dhambi.
Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno haya..
Marko 6:10 “Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale. 11 Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, MTOKAPO HUKO, YAKUNG’UTENI MAVUMBI YALIYO CHINI YA MIGUU YENU, KUWA USHUHUDA KWAO. 12 Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu.”
Marko 6:10 “Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale.
11 Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, MTOKAPO HUKO, YAKUNG’UTENI MAVUMBI YALIYO CHINI YA MIGUU YENU, KUWA USHUHUDA KWAO.
12 Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu.”
Utaona pia katika kanisa la kwanza, sehemu nyingi mitume walipokuwa wakifika, na kuhubiri injili, wenyeji wa miji ile walipowakataa walikung’uta mavumbi na kuondoka kwenda miji mingine, maana yake ni kwamba tayari watu wa huo mji, mbingu zimefungwa juu yao, hakuna chochote cha kiroho watakachonufaika nacho baada ya hapo, (wanakuwa wamefungiwa dhambi sawasawa na Yohana 20:23) kwasababu wameidharau injili iliyoletwa kwao zaidi ya mara moja, ikiwataka watubu wamgeukie Mungu.
Matendo 13:50 “Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. 51 NAO WAKAWAKUNG’UTIA MAVUMBI YA MIGUU YAO, WAKAENDA IKONIO”.
Matendo 13:50 “Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
51 NAO WAKAWAKUNG’UTIA MAVUMBI YA MIGUU YAO, WAKAENDA IKONIO”.
Hivyo Kaka/Dada, usidharau maonyo yoteyote ya Mungu yanayoletwa kwako, unapoonywa na kanisa juu ya uzinzi wako, juu ya huyo mwanamke/mwanaume wa kizinzi unayeishi naye, unapaswa uogope!, na kugeuka na kutubu haraka..Maana siku ile kanisa litakaposema basi!, na mbinguni kutakuwa ni BASI!!..Ni Mungu ndio kaamua iwe hivyo, si mwanadamu, ni Mungu ndio kaamua kanisa lake liwe na hayo mamlaka na si mwanadamu.. Na ni kwanini kaamua iwe hivyo, ni kwasababu kama hutaweza kumsikiliza ndugu mwenzako anayekuonya, au kulisikiliza kanisa, basi hata Kristo akikutokea hutaweza kumsikiliza, ndio maana kanisa litakaposeama basi, basi hata mbinguni nako ni Basi!
kwahiyo ni jambo la kuogopa sana!.. kadhalika usiidharau injili inayoletwa kwako, kwasababu siku ikiondolewa kwako, na ile nguvu ya kumrudia Bwana inakuwa haipo tena juu yako, hivyo itii injili yake leo, kwasababu anakupenda na anatupenda sote, hataki tuangamie, sawasawa na ahadi zake.
Luka 10:10 “Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, 11 Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. 12 Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo 13 Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. 14 Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi. 15 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu. 16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma”.
Luka 10:10 “Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni,
11 Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.
12 Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo
13 Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.
14 Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi.
15 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma”.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
UFUNUO: Mlango wa 3 part 3
Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze Neno la Mungu ili tupate maarifa sahihi ya kuishi hapa duniani.
Na leo tutaona mazingira ambayo ukikaa katika hayo basi Mungu atakujalia umwone mke/mume sahihi aliyekuchagulia toka mbali.
Tofauti na mazingira ya kiulimwengu ambayo yenyewe ili yakupe mke/mume wa kidunia ni sharti uwe katika mazingira ya kidunia..yaani uvae vimini, ujitembeze na suruali barabarani, unyoe viduku, uishi kama wasanii wa kidunia, uwepo disco na kwenye party party kila wakati n.k. ili uonekane.
Ukikaa katika mazingira kama hayo hakika dunia itakupatia unachokitafuta..
Lakini leo tutajifunza mazingira ya ki-Mungu… Ili Mungu akuonyeshe mke/mume sahihi tokea mbali je! Ukae katika mazingira gani.?
Tutamtazama Isaka mtoto wa Ibrahimu. Kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka mpaka wakati mama yake anakufa hakuwa na mke bado.
Lakini siku moja Baba yake alipoona ni wakati sasa wa Isaka kuwa na mke alimtuma Kijakazi wake mmoja kwenda kumtafutia mke kutoka katika nchi ya mbali nchi sana ya baba zake. ..kwani hakutaka kumpatia mke kutoka katika miji ile waliyokuwepo.
Kuonyesha kuwa haijalishi utazungukwa na vijana wengi wazuri mahali ulipo, hiyo bado haikufanyi udhani mke/mume Mungu aliyekuchagulia ni lazima atoke hapo.
Sasa utaona mara baada ya yule kijakazi kutumwa kwenda kumtafutia Isaka mke na kumpata alipokuwa anarudi..Huku nyuma kuna tabia na desturi ambayo Isaka alikuwa nayo ambayo nataka leo tuione kwasababu hapa ndipo kiini cha somo letu kilipo.. Tusome..
Mwanzo 24:62-66
[62]Basi Isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana alikaa katika nchi ya kusini. [63]Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja. [64]Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia. [65]Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika. [66]Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyoyatenda.
Rudia tena Mstari wa 62 unasema…
‘Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni’.
Unaona, Pindi tu alipotoa mguu wake na kwenda kondeni kutafakari..alipojijengea desturi ya kwenda maporini mbali na makazi ya watu ili tu kupata utulivu na Mungu wake, kuutafakari ukuu wake na uweza wake na maajabu yake na ahadi zake..huko huko Mke wake alitokea..na akamwona tokea mbali..
Pengine yeye alidhani mjini alikoondoka ndipo wake wanapotokea lakini..alishangaa kule kule kondeni kwa mbali sana ngamia wanakuja wamembeba bibi arusi wake..
Hiyo ni kuonyesha Isaka haukuwa na hulka kama za vijana wengine walizokuwa nazo..alipendelea zaidi kumtafakari Mungu kuliko kuzurura zurura huko na huko.
Matokeo yake akampata Rebeka, mwanamke ambaye tunamsoma mpaka leo, licha ya kuwa alikuwa ni mwanamke anayemcha Mungu lakini bado alikuwa ni mzuri sana wa uso..Mwanzo 26:6-7
Ndugu, ikiwa unamuhitaji mke mzuri na anaye mcha Mungu basi kuwa kama Isaka..lakini ikiwa unamuhitaji Yezebeli basi ishi mfano wa hao vijana wa kidunia wanavyoishi leo hii..
Na hili pia lipo kwa upande wa pili wa mabinti..ikiwa unataka uolewe na mwanamume ilimradi tu mwanamume basi jiweke kama hao mabinti wa kidunia wanavyojiweka wanaotembea nusu uchi barabarani na kujipambapamba kama vile Yezebeli ili waonekane wanavutia.. Utampata unayemtafuta.
Lakini kinyume chake ni kuwa ukitulia katika kusudi la Mungu..unatumia muda mrefu kwa Mungu wako kuliko kutanga tanga..unamtakafakari tu yeye..nakwambia Mungu utakuongoza kwa Isaka wako tokea mbali..kama vile Rebeka alivyomwona Isaka akimfuta kutokea mbali..
Uhitaji kujionyesha onyesha ovyo..kwasababu anayekuletea mke/mume ni Mungu, si mwanadamu..wewe kaa katika kumtakafakari yeye maisha yako yote.
Kuoa utaoa, kuolewa utaolewa tu!..ukiishi maisha yanayopendeza Mungu si uongo utakutendea tu.
Daudi alisema..
Zaburi 37:25 [25]Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
Mungu hawezi kuacha kumpa mteule wake kitu kilicho chema, na kizuri.. Hawezi kuruhusu mke/mume pasua kichwa atokee mbele ya njia yake, mtu anayemcha yeye. Hilo haliwezekani..
Hivyo kama bado hujaokoka. Tubu leo anza maisha yako upya na Bwana Yesu kwa kumaanisha kabisa..Toba ya kweli inaambatana na kuucha ulimwenguni, mkatae shetani na kazi zake zote na vimini vyake vyote, na suruali zote na viduku vyote..kamtafakari Mungu huko makondeni, hata kama utaonekana mshamba..
Ishi maisha ya kumlingana Bwana..Na bila shaka wakati utafika atamtuma malaika wake kwenda kukuletea mwenzi sahihi..Kama Ibrahimu alivyomtuma kijakazi wake, kumletea Isaka Rebeka.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?
Tuwasome,
Walawi 11:13 “Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14 na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15 na kila kunguru kwa aina zake; 16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; 18 na mumbi, na mwari, na mderi; 19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo”.
Walawi 11:13 “Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu;
14 na mwewe, na kozi kwa aina zake,
15 na kila kunguru kwa aina zake;
16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;
17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa;
18 na mumbi, na mwari, na mderi;
19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo”.
Tai ni ndege maarufu anayejulikana kwa uwezo wake wa kuona mbali, na vile vile mwenye uwezo wa kuruka juu zaidi ya ndege wengine wote, Mvua inaponyesha na mawingu kutanda, Tai hupaa juu ya mawingu, na baadaye kushuka chini mvua inapoisha, tofauti na ndege wengine wote ambao mawingu yanapotanda tu!, wanakimbilia viota vyao kujisitiri.(Tazama picha chini).
Furukombe au kwa kiingereza “Vulture” ni aina nyingine ya ndege ambao kimwonekano wanakaribia kufanana na Tai, isipokuwa hawa wana midomo mirefu kidogo, na pia wanakula Mizoga ya wanyama waliokufa maporini (Tazama picha chini), rangi yao ni rangi ya kahawia.
Kipungu ni aina iyo hiyo ya Furukombe, isipokuwa kipungu ni mweusi, tabia zake ni kama za Furukombe wa kahawia, anakula mizoga, tofauti na Furukombe, kipungu yeye anapatikana nchi za ukanda wa baridi.(Tazama picha chini)
Mwewe ni jamii ya Tai, na ni ndege maarufu wenye rangi ya kahawia na wanapatikana na kuonekana sana maziringira wanayoishi wanadamu. Mwewe naye huruka juu sana, lakini si kama Tai, anapatikana sana sehemu za joto, na chakula chake kikuu ni ndege wengine wadogo wadogo, kama mashomoro pamoja na vifaranga vya kuku. (Tazama picha chini).
Kozi ni Mwewe mweusi, Huyu hana tofauti na Mwewe wa kahawia kitabia, kilichowatofautisha ni rangi tu!, na ukubwa. Kozi yeye kiumbile ni mdogo kuliko Mwewe, na mkia wake ni mfupi. (Tazama picha chini).
Kirukanjia ni aina ya “Bundi” wenye manyoya kama mapembe kwenye vichwa vyao, (Tazama picha chini).
Dudumizi ni aina ya ndege weupe wanaoishi kwenye fukwe za bahari, ambao wana miguu iliyofungamana kama bata, chakula chao kikubwa ni samaki. (Tazama picha chini).
Kipanga ni ndege anayekaribia kufanana sana na Mwewe, isipikuwa yeye kimwonekano ni mdogo, tabia za kipanga ni kama za mwewe, chakula chake ni kama cha mwewe,(yaani kula ndege wengine wadogo ikiwemo vifaranga vya kuku).
Mnandi ni aina ya ndege wanakaribia kufanana na Dudumizi, isipokuwa Mnandi wanaishi kando kando ya maziwa na mito, na chakula chao kikubwa ni samaki kama walivyo dudumizi, na kimwonekano ni wausi.
Mumbi ni bundi mweupe, (Tazama picha chini).
Mwari ni bundi wa jangwani. (Tazama picha chini).
Mderi ni jamii ya Mwewe wanaokula samaki. . (Tazama picha chini)
Korongo ni jamii ya ndege weupe wenye midomo mirefu na miguu mirefu iliyo membamba, wanaishi kando kando ya mito na mabwawa, chakula chao kikubwa ni samaki na nyoka. (Tazama picha chini).
Koikoi ni jamii ya ndege wadogo, wenye sifa ya kusafiri umbali mrefu >Kwa maelezo marefu juu ya ndege hawa koikoi na somo gani wamebeba kiroho fungua hapa>> Koi koi.
Hudi hudi ni aina ya ndege, wenye kichwa kilichochongoka na wenye rangi mbali mbali kwenye manyoa yao..
Hiyo ndiyo orodha ya ndege ambayo Bwana Mungu aliwakata wana wa Israeli wasiwale. Kulikuwepo na wanyama wengine kama Nguruwe, Sungura, ngamia na wengine baadhi, ambao pia wana wa Israeli hawakuruhusiwa kuwala..
Bwana Mungu alitumia tabia za wanyama hao kutaka kufundisha jambo fulani la kiroho, ambalo sisi watu wa agano jipya tumeweza kulielewa, hivyo kwasasa hakuna tena kilicho najisi, vyote vimetakaswa.
Sasa kuelewa ni somo gani lilikuwa nyuma ya viumbe hao, mpaka kufikia Bwana Mungu kuwakataza Israeli wasiwale, unaweza kufungua hapa >>> Je tunaruhisiwa kula nyama ya Nguruwe?
Lumbwi ni nini katika biblia?
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?
Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?
MAMA, TAZAMA, MWANAO.
Hema ya kukutania kama jina lake lilivyo, ni hema iliyotengenezwa mahususi kwaajili ya “kukutania”.
Katika biblia, Musa aliongozwa na Bwana Mungu kutengeneza Hema ndogo maalumu, ambayo kupitia hiyo, Mungu ataweza kukutana na watu wake na kuzungumza nao.
Hema hiyo Musa aliambiwa aitengeneze nje ya kambi, Na haikuwa ya kudumu, bali ya kuhama hama, kwasababu wana wa Israeli walikuwa bado wapo katika safari ya kwenda Kaanani, hivyo ilikuwa ni ya kutengenezwa na kuvunjwa. (Tazama picha juu).
Na mtu yeyote alipokuwa na jambo ambalo anataka kuuliza kwa Bwana, basi alimfuata Musa, na kisha Musa huingia ndani ya hiyo hema kusikia kutoka kwa Bwana.
Hapo awali ni Musa tu, ndiye aliyekuwa na ruhusa ya kuingia ndani ya Hema, baadaye Haruni naye alikuja kupata nafasi ya kuingia, baada ya sheria za kikuhani kuongezwa.
Na Ishara itakayoonesha kuwa Bwana ameshuka juu ya Hema hiyo tayari kuzungumza na watu wake, ni ile Nguzo ya wingu ambayo iliyokuwa inawaongoza wana wa Israeli mchana.
Nguzo hiyo iliposhuka na kukaa juu ya hema basi wana wa Israeli wote walijua Bwana ameshuka na kuna jambo au ujumbe anataka kuutoa. Nguzo hiyo kwa jina lingine iliitwa “utukufu wa Bwana”.
Hivyo uliposhuka huo utukufu basi Musa aliingia ndani ya hiyo hema kusikia Bwana anasema nini.
Mfano utaona wakati Haruni na Miriamu walipomnung’unikia Musa juu ya mke wake wakiMisri , jambo ambalo halikumpendeza Mungu…utaona “Utukufu wa Mungu”, yaani ile nguzo ya wingu ilionekana juu ya hema.
Hesabu 12:1 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. 2 Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao. 3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. 4 BWANA akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. 5 BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. 6 Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. 7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; 8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?. 9 Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake. 10 Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. 11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi”.
Hesabu 12:1 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.
2 Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao.
3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
4 BWANA akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.
5 BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
6 Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto.
7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?.
9 Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
10 Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi”.
Pia unaweza kusoma juu ya habari ya Dathani na Kora walipoinuka na kutaka wao ndio wawe viongozi wa mkutano badala ya Musa.
Hesabu 16:19 “ Kisha Kora akutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa BWANA ukatokea mbele ya mkutano wote. 20 Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. 22 Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? 23 BWANA akasema na Musa, na kumwambia, 24 Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu”.
Hesabu 16:19 “ Kisha Kora akutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa BWANA ukatokea mbele ya mkutano wote.
20 Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.
22 Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?
23 BWANA akasema na Musa, na kumwambia,
24 Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu”.
Mistari mingine inayozungumzia juu ya hema ya Bwana na utukufu wake huo ni pamoja na Kutoka 40:34, Walawi 1:1, na Hesabu 2:17.
Lakini je hiyo Hema ya kukutania sasa ni wapi?
Hema yetu ya kukutania sasa ni kwenye Neno la Mungu (Biblia), hapo ndipo tutakapoonana na Mungu, tutakaposikia kutoka kwa Mungu,tutakapopata maonyo na faraja. Hapo ndipo penye utukufu wa Mungu.
Hakuna mahali pengine tutakapopata kusikia Sauti ya Mungu, isipokuwa katika Neno lake.
Hivyo hatuna budi kujifunza biblia kila siku.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
MUNGU HATAZAMI MOTO WA KIGENI,KUWA MAKINI!
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?
Rudi nyumbani: