Noeli kwa lugha ya kilatini ni neno linalomaanisha, “siku ya kuzaliwa” , lakini linalenga mahususi siku ya kuzaliwa kwa mfalme wa ulimwengu duniani (yaani Yesu Kristo). Na kwa lugha ya kifaransa neno hili linaweza kumaanisha aidha “habari njema” au “msimu wa Krisimasi” kwa ujumla.
Pengine Neno hili umeshawahi kulisikia sana likiitwa kwa jina la watu, au likitajwa katika nyimbo moja maarufu ijulikanayo kama “Noeli ya kwanza”;
Hivyo kwa maneno mafupi, hili ni neno linalomaanisha kusheherekea au kutangazwa kwa habari njema za kuzaliwa kwa Bwana Yesu duniani. Popote unapolisikia likitajwa basi ujue hizo ni habari za kuzaliwa kwa Yesu au msimu wote wa sikukuu ya Krisimasi kwa ujumla, Disemba 25
Kumbuka Neno hili halipo mahali popote katika biblia, Utalisikia sana sana katika madhebehu makongwe kama vile Katoliki, Anglikana na Lutheran.
Lakini Je ni takwa sisi wakristo kusheherekea Noeli /Krisimasi? Je! Ni kweli Yesu alizaliwa Disemba 25?.. Ili kufahamu fungua hapa >> KRISIMASI NI NINI?
Bwana akubariki.
Tazama maana nyingine ya maneno ya kibiblia chini;
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SIFONGO NA SIKI NI NINI?
Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?
Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
Rudi nyumbani:
Print this post
Ukiona unahubiriwa juu ya hukumu ya Mungu, au juu ya habari ya siku za mwisho halafu unachukia au unakwazika, lakini wakati huo huo ukiambiwa habari za mafanikio na mema ndio unafurahia, basi fahamu kuwa upo karibu sana kupotea.
Kwasababu kitengo hicho ndicho kitengo-mama cha shetani kuwadanganyia watu, Embu fikiria pale Edeni Mungu hakuwaficha chochote bali aliwaeleza Adamu na hawa madhara ya dhambi, akawaambia mkila matunda la ujuzi wa mema na mabaya hakika MTAKUFA..
Lakini shetani akaibuka na mahubiri yake laini, kinyume na yale Mungu aliyowaangiza, na kuwaambia hakika HAMTAKUFA,…Unaona? Hawa aliposikia habari za mema zimekuja, habari za mafanikio, habari za uzima wakati wote, habari za kuwa juu tu, haijalishi kuwa utamkasirisha Mungu kiasi gani, haijalishi kuwa utazini kiasi gani, atatoa mimba nyingi namna gani, maadamu ni ya kutakiwa mema, basi akayachukua tu na kuyadharau yale ya Mungu, akayashilia yale ya shetani akayaamini kwelikweli kuwa hatakufa, bali ataishi naye atayasimulia matendo ya Bwana.
Ndugu yangu hizi ni siku za mwisho, ambazo biblia ilizitabiri kuwa kutatokea wimbi kubwa la manabii wa uongo, ambao kimsingi kazi yao kubwa itakuwa ni hiyo..kuwahubiria watu maneno laini, haijalishi watakuwa hawajaokoka, au la, hilo haliwahusu, kazi yao ni kuwatabiria mafanikio tu na uzima, na mema, lakini madhara ya dhambi hawataambiwa.. Kama alivyofanya shetani kwa Hawa pale Edeni.
Isaya 30:9 “Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana; 10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, TUAMBIENI MANENO LAINI, HUBIRINI MANENO YADANGANYAYO;
Isaya 30:9 “Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;
10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, TUAMBIENI MANENO LAINI, HUBIRINI MANENO YADANGANYAYO;
Kwa hawa manabii, na waalimu wa uongo kamwe hutasikia Neno ‘ukizini hakika utakufa’, na kwenda jehanamu, huwezi kusikia maneno kama hayo, kwasababu shetani anataka wewe uendelee kubakia hivyo hivyo katika ujinga, ili ufe ghafla ujikute kuzimu uanze kujuta kwanini sikufahamu haya yote.
Angalia shida tunazozipitia duniani leo hii, ni kwasababu ya wazazi wetu kusikiliza injili laini za shetani, Inasikitisha kuona pale mtu unapoambiwa kuhusu dhambi zako, unaona kama vile unahukumiwa. Mama yetu Hawa aliona kama Mungu anamtamkia mabaya, akafanya makosa yale..Na sisi vivyo hivyo tukipuuzia injili ya kuambiwa ukweli, injili za kukemewa dhambi, injili za ziwa la moto. Tujue kuwa tunajiandaa kwa majuto ya milele.
Mara nyingi wana wa Israeli waliingia katika makosa kama haya mpaka wakapelekwa utumwani Babeli kwasababu ya kuwasikiliza manabii wa uongo waliokuwa wanawatabiria amani tu muda wote, bila kushughulika na dhambi zao, ambazo ndio kiini cha matatizo yao.
Soma vifungu hivi;
Ezekieli 13:16 “yaani, manabii wa Israeli, watabirio habari za Yerusalemu, na kuona maono ya amani katika habari zake; wala hapana amani, asema Bwana MUNGU”.
Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani”.
Unaona yaliyokuwa yanaendelea kale ndiyo yanayoendelea sasa.
Leo swali linakuja kwako, Je unaufungaje mwaka wako?, mwaka huu wa 2020 ndio unapita, unakuja mwingine mpya wa 2021, kumbuka kwa jinsi miaka inavyosogea ndivyo tunavyoyakaribia mambo mawili makuu mbele yetu, la kwanza Ni Unyakuo. Na la pili ni Kifo chako. Maelfu ya watu kila sekunde wanakufa duniani, vilevile na wewe hujui siku yako itakuwa ni lini, pengine ni kesho, au mwanzoni mwa mwaka ujao, Jiulize ukifa leo ghafla huko utakapokwenda utakuwa ni upande gani?
Vilevile jiulize ikiwa unyakuo utapita leo usiku halafu ukaachwa, utakuwa kwenye hali ya namna gani..Kumbuka ni siku kama hizi ndizo Bwana atakazorudi, watu watakuwa wakila na kunywa, wakipanda na kujenga, wakisherehekea, ndipo huo mwisho utakapokuja..Jiulize utakuwa wapi wakati huo ukikujia kwa ghafla.
Ukijifunza kuyatafakari hayo, hutaishi maisha ya ilimradi tu hapa duniani, bali utajiangalia sana mwenendo wako, ili siku ile isije ikakunasa kama mtego.
Hivyo, tubu dhambi zako mgeukie Muumba wako, usikubali uanze mwaka mpya na viporo vya dhambi vya mwaka huu, mgeukie Yesu Kristo leo hii, akusafishe dhambi zako.
Ikiwa upo tayari kutubu sasa, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako. Mahali popote ulipo, tafuta sehemu ya utulivu, piga magoti, kisha kwa kumaanisha kabisa kutoka katika moyo wako sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE, NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE, NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Basi kwa sala hiyo fupi, Mungu ameshakusamehe, kilichobakia kwako ni kubatizwa, ikiwa hukubatizwa, na kudumu katika neema na utakatifu siku zote za maisha yako.
Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya kiroho, basi tutafute kwa namba hizi +255693036618
Mungu akubariki.
UNYAKUO.
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
KUMTUMIKIA MUNGU, KUNAWEZA KUWE KINYUME NA MATARIJIO YAKO.
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
Rudi nyumbani
Shalom.
Karibu tujifunze maneno ya uzima,
Biblia inatuambia, Bwana wetu Yesu alijaribiwa sawa sawa na sisi, katika mambo yote, lakini hakutenda dhambi wala kutetereka katika imani, Sio kwamba alikuwa mgumu sana kuliko sisi, hapana, yeye mwenyewe alisema..
Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.
Bwana anajua kabisa siku unapokuwa mkristo, si wakati wote mambo yatakuwa mteremko kama wengi wanavyodhani, utakutana na majira mengi tofauti tofauti, ya kucheka, mengine ya kulia, ya kuwa mpweke, mengine ya kuchangamka, ya kupata, ya kupoteza, ya kupungukiwa, ya kujaliwa, ya kuugua, ya kuwa na afya n.k. yote hayo ni majira, lakini sote tunajua hali inakuwa mbaya zaidi pale tunapopitia katika hali za majaribu. Au kujaribiwa. Hivyo ni vizuri kujua kuwa tunapopitia majira kama hayo tunapaswa tufanye nini.
Embu leo tuangalie, ni nini kilikuwa kinaendelea katika mazingira ya kujaribiwa kwa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani.
Marko 1:12 “Mara Roho akamtoa aende nyikani. 13 Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia”.
Marko 1:12 “Mara Roho akamtoa aende nyikani.
13 Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia”.
Kama tunavyosoma hapo, katika kujaribiwa na shetani, vipo vitu viwili viliambatana naye. Cha kwanza ni wanyama wa mwituni. Akiwa jangwani alikutana na wanyama ambao hajazoea kukutana nao katika maisha ya kawaida, sehemu moja aliposogea alikutana na mbweha, mbele kidogo pengine alikutana na simba wenye njaa, siku tatu tena mbeleni tena alikutana na dubu, kila siku usiku anawaona chui wanakatiza, kwasababu yupo nyikani, wanyama wa nyikani kukutana nao, litakuwa ni jambo la kawaida.
Inafunua nini, wakati wa majaribu usishangae kukutana na mbwa mwitu wakali mbele yako, ambao pengine hapo nyuma hukuwahi kuwaona.., unapitia ugonjwa fulani mbaya, pengine unatarajia kuona faraja katika huo, kinyume chake ndio unaona watu wakikukimbia, wengine wanakusema vibaya, Umekuwa mkristo, ukitazamia familia yako ndio ikufurahie, kinyume chake ndio inakutenga na kukurushia maneno, wengine hawakudhara., Unakataa rushwa kazini, maboss wako ndio wana kuundia visa ufukuzwe kazi n.k.. Mambo kama hayo utakutana nayo kwa namna moja au nyingine.
Lakini pia tunaona Bwana Yesu katikati ya majaribu yale, lilikuwepo kundi lingine lisiloonekana ambalo lilikiwa likimuhudumia, na hao sio wengine zaidi ya malaika watakatifu.. Hapo ndipo kiini chetu cha somo kilipo..Ni faraja iliyoje. Wakati ambapo macho yake yanaona maadui waliomzunguka, lakini roho yake ilikuwa inawaona malaika wa Mungu wamemzunguka wakimuhudumia..kuhakikisha hadhuriki na maadui wake, kuhakikisha hafu, kuhakikisha analivuka lile jaribu haijalishi kuwa yupo katika wakati mgumu kiasi gani, kuhakikisha anapata faraja ya kweli kutoka kwa Mungu.
Hapa ndipo wengi wetu tunaposhindwa kupaona, na matokeo yake majaribu yanatuzidi nguvu mpaka kuiacha imani, au kurudi nyuma. Hilo ndio lililokuwa linataka kumtokea Yule mtumishi wa Elisha, siku ile walipozungukwa na majeshi ya maadui zao, jambo ambalo lilimpelekea aogope sana na kupaniki, na kulia.. Alipoanza kufikiria jinsi atakavyokwenda kukatwa vipande pande, au jinsi atakavyoondolewa kichwa chake, hilo lilimfanya atamani hata ardhi ipasuke saa ile ile , azame.
Lakini jicho la Elisha lilikuwa linaona mbali zaidi, lilikuwa linaona upande wa pili yupo nani, lilikuwa linaona jeshi la mbinguni lililokuwa pamoja naye, pindi anapopitia majira ya majaribu kama hayo, Ndipo baadaye akamwomba Mungu, amfungue macho yule kijana, akafunguliwa na kuona idadi isiyohesabika ya malaika wa Mungu wakiwa karibu yao wamewazunguka, kwa lengo la kuwahudumia.
2Wafalme 6:15 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? 16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. 17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.
2Wafalme 6:15 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?
16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.
Hizo ndio siri zilizowafanya manabii wote wa kale, kuyashinda majaribu mazito, kwasababu waliacha kuwaangalia maadui zao, wakaliangalia jeshi la Mungu mwenyezi lililo pamoja nao. Vile vile utaona wakati ule walipomkamata Danieli na kwenda kumtupa katika lile tundu la Simba, Danieli hakupeleka mawazo yake sana kwa wale simba, bali alimuawaza Mungu wa majeshi, akijua kuwa jeshi alilonalo la malaika watakatifu la kumuhudumia yeye ni kubwa sana. Na ndipo alipotupwa tu mule tunduni, wale simba hawakumdhuru, Na baadaye mfalme alipomuuliza ni nini?, Danieli akamwambia maneno haya
Danieli 6:22 “Mungu wangu AMEMTUMA MALAIKA WAKE, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno”.
Hivyo na wewe pia fahamu kuwa, katikati ya majaribu, wapo malaika wa Mungu kukuhudumia usipatwe na dhara lolote, katikati ya shida zako, mateso yako na magonjwa upo muujiza wa Mungu mkononi mwa malaika zake. Hivyo usiwe na hofu, wala wasiwasi wala uoga.
Subiri tu, utaona mambo ya ajabu. Ni vile tu, Mungu huwa si kila jambo atatufumbua macho yetu tuone, lakini kama angetaka iwe hivyo uone kila kitu, usingekaa uogope jaribu lolote lililo mbele yako. Hivyo tulia,utahudumiwa kwa namna ya kimbinguni, ondoa tu woga,mtazame Mungu. Acha kufikiria juu ya mateso na dhiki, mfikirie Mungu hilo tu. Utaona kazi za malaika wa Mungu wazi wazi mbele ya macho yako.
Shalom
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
NAWE UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.
KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
Kuabiri maana yake ni kupanga safari, husasani ile ya majini, Neno hilo ndilo lililozaa neno abiria, ikiwa na maana wale wanaosafiri.
Utalisoma sana sana katika zile ziara za mtume Paulo, na ile safari yake ya kuelekea Rumi kama mfungwa.
Vifuatavyo ni vifungu ambavyo utakutana na neno hilo.
Matendo 20:13 “Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni,TUKAABIRI kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu”.
Hapo mtume Paulo anamaanisha walipotangulia kwenda merikebuni walipanga safari ya majini ya kwenda Aso.
Matendo 21:1 “Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na KUABIRI, tukafika Kosi kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara”,
Hapo Paulo anamaanisha , walipokwisha kujitenga nao wakapanga safari majini ya kuelekea Kosi.
Vifungu vingine ni hivi;
Matendo 27:1 “Basi ilipoamriwa TUABIRI hata Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto. 2 Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi”.
Matendo 27:1 “Basi ilipoamriwa TUABIRI hata Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.
2 Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi”.
Matendo 28:10 “nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; BASI TULIPOABIRI wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo. 11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha”.
Matendo 28:10 “nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; BASI TULIPOABIRI wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.
11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha”.
Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.
Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?
Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
Shekina ni nini? Na Je! Utukufu wa shekina unamaana gani?
Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, Biblia inatuambia Neno lake ni kama fedha iliyosafishwa motoni mara saba,(Zab 12:6) ikiwa na maana kuwa Neno lile lile moja linaweza kuwa na mafunuo saba. Hivyo hatuchoki wala hatuachi kujifunza Neno lake kila inapoitwa leo. Na ndio maana biblia ni kitabu pekee kilichobaki duniani ambacho hakijawahi kupitwa na wakati.
Kuna jambo la muhimu sana, naamini tunaweza kujifunza kwa wale watu watatu waliopewa talanta na Bwana wao kwenda kuzizalisha. Tukisoma pale tunaona yule wa kwanza alipewa talanta 5, na kuwa uaminifu akafanikiwa kuzalisha nyingine tano, na yule wa pili alipewa talanta 2 na kwa uaminifu naye pia akaweza kuzalisha talanta nyingine mbili, Lakini yule wa tatu, ambaye hakuzalisha chochote, kuna maneno aliyazungumza, ambayo yalifichua siri ya Bwana wake, jinsi alivyokuwa na hiyo ndio ikawa sababu kubwa ya yeye kutokwenda kuzalisha chochote.
Embu tusoma habari yake, kwa ufupi, na mbeleni kuna jambo geni ambalo Mungu atatufundisha leo.
Mathayo 25:24 “Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, BWANA, NALITAMBUA YA KUWA WEWE U MTU MGUMU, WAVUNA USIPOPANDA, WAKUSANYA USIPOTAWANYA; 25 BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO KATIKA ARDHI; TAZAMA, UNAYO ILIYO YAKO. 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mathayo 25:24 “Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, BWANA, NALITAMBUA YA KUWA WEWE U MTU MGUMU, WAVUNA USIPOPANDA, WAKUSANYA USIPOTAWANYA;
25 BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO KATIKA ARDHI; TAZAMA, UNAYO ILIYO YAKO.
26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Sasa turudie tena huo mstari wa 24 anasema, nalitambua ya kuwa wewe ni mtu Mgumu.. Jiulize swali unadhani alikuwa anamsingizia Bwana wake kumwita mtu Mgumu? Hakuwa anamsingizia hata kidogo,alikuwa anazungumza kwa alichokiona kwa Bwana wake, ambaye alikuwa anamtumikia tangu siku nyingi…Tena akazidi kuendelea kumwambia, wewe huwa unavuna usipopanda, na unakusanya usipotawanya..Jiulize unadhani pia hapa alikuwa anamsingizia? Jibu ni la, nataka tusisimamie upande mmoja, embu tuangalie hoja za huyu mtumwa zilikuwa ni nini.
Kwa kauli zake ni kwamba alimwona huyu Bwana wake, ni mtu ambaye si mwepesi kuelewa, hususani pale wanapokuwa kazini na mambo hayakuenda sawa siku hiyo, hata aelezejwe, ni mgumu sana kuelewa, akiambiwa kulikuwa na shida hii, ndio maana fedha haijapatikana ya kutosha, ni ngumu kuelewa, na ndio maana anasema Ninajua kuwa wewe ni mtu Mgumu.
Vilevile kulingana na maelezo yake, huyu Bwana wake ni mtu ambaye, anatarajia kupata vingi kutoka kwa wafanyakazi wake, licha ya kwamba, hawekezi vya kutosha, ni bwana ambaye hatimizi sana wajibu wake, kama tajiri, bali kazi yote anawaachia wafanyakazi wake,watumike na mwisho wa siku anataka mapato mengi kutoka kwao. Na ndio maaana akawa na ujasiri wa kumwambia Unavuna usipopanda..Yaani unatarajia upate mengi, mahali ambapo hujawekeza kwa vingi.
Sasa Kwa kauli zake hizi mbili, pengine ndio ikampelekea asikitendee kazi kile alichopewa na badala yake akakifukia chini
Lakini wakati yeye anafikiria hivyo, wakati yeye anaona Bwana wake hawajali wafanyakazi, huku nyuma wenzake wanaona hakuna haja ya kumfikiria Bwana wao vibaya, wakaenda kuvifanyia kazi vile walivyopewa. Hata kama kazi ilikuwa ni ngumu isiyo na vitendea kazi vingi lakini wao waliendelea kufanya hivyo hivyo tu.
Lakini huyu mmoja akasema mimi nitamuhifadhia fedha yake akirudi nimpe, nisipate lawama, kwasababu huyu boss wangu ninamjua , naweza kumzalishia kimoja tu, hapa, akaja kunikaripia ni kwanini sikumletea vingi, hivyo wacha nimwekee kilicho chake.akirudi akikute, niepukane na lawama.
Lakini kama tunavyosoma Bwana wake alipokuja na kumkuta hana faida yoyote alimwita mtumwa mbaya na mlegevu.. Kwanini asingeichukua na kuiweka kwa watoa riba, mahali ambapo hapana hatari ya kupata hasara, mpaka akaamua kwenda kuichimbia chini iozee huko.. ?
Mnyang’anyeni kile alichopewa wapewe wale wengine. Na akatupwe katika giza la nje. Ndiko kutakakokuwa na kilio na kusaga meno
Ndugu, mfano huu unatuhusu sisi, yaani mimi na wewe. Kazi ya Mungu leo hii tunaweza kuiona ni ngumu ya kuchosha, kinyume na matarajio yetu, mpaka inawapelekea wengine kusema mpaka Mungu anipatie kwanza gari na nyumba ndio nitakwenda kumtumikia, mwingine anasema mpaka Mungu anipe fedha za kutosha ya kujenga kanisa ndio nitaanza kumtumikia kwasababu kazi ni yake na si yangu.
Ndugu yangu kama tunavisubiria tuvipate kwanza hivyo ndio tuanze ndo tumfanyie Mungu kitu tutasubiri sana, Kama tunangojea tuwezeshwe kwa vitu fulani vingi ndio tuseme leo tunajitoa kwa Mungu, hapo tusijidanganye, huo wakati hautafika. Kile ulichopewa na Mungu anzana nacho, na mbele ya safari Mungu atakufanikisha.
Wengine wanasema ngoja nipate pesa kidogo ya kuweza kumudu maisha yangu ndio nitaanza kumtolea Mungu, sadaka zangu. Kama mawazo yako yapo hivyo, ujue hicho kipindi kamwe hakitakaa kikufikie, utasubiri, utangoja, utamlilia Mungu akupe, kamwe hatakupa..Utoaji unaanzana na kile kimoja ulicho nacho, unakwenda kumtolea Mungu, Kama Mungu kakubariki kwa elfu mbili unamtolea elfu moja, hivyo hivyo, lakini ukisubiria upate vingi ndio upeleke kwa Mungu, sahau hilo jambo.
Ndivyo Kristo anavyofanya kazi hivyo, unaweza kumwona ni Bwana mgumu kweli, ambaye hawekezi vya kutosha kwanza kwa wafanya kazi wake, anawaacha wafanye kazi katika umaskini ..lakini hiyo ndio tabia yake. Unapaswa uielewe tu usonge mbele.
Leo hii utaona kama umetelekezwa lakini faida yake siku moja utaiona, utatateseka, lakini thawabu yake ni kubwa kulinganisha na mateso yako ya leo. Embu tafakari wale aliowapa talanta tano aliwalipa nini baadaye, utaona aliwaambia wakatawale miji mitano, na wale wa mbili akawaambia wakatawale miji miwili. Unaona, faida kidogo tu inampelekea Bwana kukupa miji. Hivyo Mungu anayosababu kwanini atake umtumikie au umtolee katika hali hiyo uliyopo. Zipo thawabu nono zinatusubiria huko mbinguni
Hivyo na sisi tusianze kusema kazi ya Mungu ni ngumu, au kumtolea Mungu ni kugumu. Tufanye tu. Tusiwe watumwa walegevu na wabaya wenye sababu nyingi zisizojenga.
Bali tuwe kama wale wawili wa kwanza. Ili Kristo atakapouona uaminifu wetu, ndio atuongeze, na kutupa vingi zaidi kwa majira yake.
THAWABU ZA SIRI, ZA WATAKATIFU MBINGUNI.
USIISHI BILA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KABISA..
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)
KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).
Swali: Mtume Paulo anasema katika 1Timotheo 4:3, kwamba “wakiwazuia watu wasioe”. Alikuwa ana maana gani hasa?.
Jibu: Tusome
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”.
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”.
Ni kweli nyakati za Mwisho biblia imetabiri watu watajitenga na imani na “kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani”.. Na pia “watawazuia watu wasioe”
Ukisoma hapo kwa makini utaona ni anasema “watawazuia watu wasioe” na sio “watawakataza”.. Kuwakataza ni tofauti na kuwazuia. Sasa Bwana Yesu alisema maneno haya..
Luka 11:52 “Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.”
Maana yake ni kwamba mtu anayegeuza maarifa ya Ufalme wa mbinguni, au anayeyapotosha, na kwenda kuwapotosha wengine, ni sawa na amewazuia watu hao kuingia katika ufalme wa mbinguni, kwasababu ameuondoa mlango wa maarifa.
Kwamfano mtu anayepotosha maarifa ya jinsi ya kuoa kibiblia na kumfanya yule mtu asioe kabisa au aoe kimakosa, hapo amemzuia mtu huyo kuoa.
Sasa Utauliza hilo jambo lipo leo?.. Mbona leo tunaona makanisani watu wanahubiriwa waje wapokee wachumba?..hatusikii watu wakizuiliwa kuoa?
Ndio jambo hilo lipo kwa sana, na limeenea duniani kote. Watu wengi sana wamezuiliwa kuoa/kuolewa pasipo wao wenyewe kujijua ingawa wapo katika mahusiano, au kile kinachoitwa ndoa. Kwasababu roho hii inatenda kazi kwa siri sana.
Kwamfano makanisa yanayofungisha ndoa za jinsia moja, na kuzibariki, na kusema ni ndoa takatifu. Watu wa namna hiyo, wanawazuia watu kuoa, kwasababu hiyo ndoa ya jinsia moja waliyoifungisha sio ndoa, bali ni kitu kingine. Hivyo mtu ataendelea kubaki katika hiyo ndoa ya kishetani akijua tayari kaoa, au kaolewa, kwasababu tu mchungaji wake kaidhinisha.. kumbe yupo katika laana, kwa kuzuiliwa kuoa/kuolewa inavyopaswa..
Pia leo hii kuna kundi kubwa la wanaume ambao hawajaoa (maana yake hawajafunga ndoa ya kikristo) lakini wanaishi na wanawake na kuzaa nao watoto na bado wanajiita wakristo, na wanahudhuria kanisani, wala hawaambiwi chochote katika kusanyiko walilopo, zaidi wanawekewa mikono na kubarikiwa ndoa yao hiyo batili, hawaambiwi chochote pengine kwasababu ni wachangiaji wakubwa hapo katika hilo kusanyiko. Hawa nao wamezuiliwa kuoa (yaani wamefungiwa mlango wa maarifa na viongozi wao wa dini). Kwasababu viongozi wao hao wanajua kabisa waasherati hawataurithi uzima wa milele lakini bado hawawafundishi au kuwakumbusha watu wanaowaongoza. Ambapo wangepaswa wawaambie na kuwakemea watubu, na wakafunge ndoa watoke katika hayo maisha ya uasherati wanayoishi.
Katika kanisa la kwanza, watu wa namna hiyo (wanaoishi pamoja huku hawajaoana) walikuwa wanatengwa kabisa, mpaka watakapotubu (na hiyo ni kwa faida ya roho zao)..lakini leo hii wanabarikiwa, jambo ambalo linahuzunisha sana.
Kadhalika yapo makanisa yanayofungisha ndoa za watu walioachana..Utakuta mwanamke kaachana na mumewe bila sababu yeyote, na kaenda kutafuta mwingine na anampeleka kanisani, kufungisha ndoa nyingine ya pili, na viongozi wengi pasipo kumhoji wala kufuatilia historia ya yule mtu kabla ya kuifungisha hiyo ndoa, wanafungisha hivyo hivyo tu, (ili pengine wasije wakamkwaza yule mshirika kipofu, kwasababu pengine ndiye mchangiaji mkubwa pale) bila kujua wamemzuia kuoa inavyopaswa kimaandiko yule mtu anayeoa, (wamemfungia mlango wa maarifa), na kumfanya aishi maisha ya uzinzi maisha yake yote.
Kwasababu huyo anayekwenda kumuuoa tayari ni mke wa mtu, hivyo anakwenda kufanya uzinzi..lakini kwasababu anaona hata mchungaji kakubaliana na hilo, na yeye dhamira yake inampa kibali kuoa kitu kilichoachwa, kwasababu mchungaji wake kakubali.. (Huyu naye kazuiliwa kuoa pasipo yeye kujijua)..Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo.
Luka 16:18 “Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini”.
Pia yapo makusanyiko yanayofundisha na kufungisha ndoa za mitara (yaani za wake wengi). Utakuta kijana amefikia umri wa kuoa, na kwa dhamira njema anatafuta mtu wa kuoa, lakini anambiwa na kiongozi kwamba ni ruksa kuoa hata wake wawili, hivyo anakwenda kuoa wanawake wawili, na bila kujua kuwa alichofungishwa sio ndoa bali ni kitu kingine, na bila kujua kuwa tayari kashazuiliwa kuoa, kama maandiko yanavyosema.
Na pia watu wote wanaoishi na magirlfriend au maboyfriend na wanafanya uasherati, na wanahudhuria kusanyiko au kanisa ambalo viongozi wao hawawaambii ukweli, au basi wamezuiliwa kuoa, na pia kama wanaujua ukweli lakini hawataki kuoana lakini wanaendelea kudumu katika uasherati wao, hawa wamejizuia wenyewe kuoa/kuolewa, hivyo wasipotubu watahukumiwa, (Biblia inasema hivyo)
Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.
Hivyo hii roho inafanya kazi kwa nguvu sana nyakati hizi za Mwisho, na inawachukua wengi. Ni kwanamna gani mtu anaweza kujihadhari nayo?..Ni kwa kufanya mambo yafuatayo.
1. Kwanza kwa kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, nguvu zako zote na akili zako zote.
Ukimpenda Mungu kwa viwango hivyo, itakufanya umtafute Mungu kwa bidii sana, itakufanya usiku na mchana utafute kulijua Neno lake kwa kulisoma na kulitafakari hiyo itakusaidia kujaa maarifa ya kutosha kumhusu Mungu, na hivyo kukufanya usiwe rahisi kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho ya uongo, mfano wa hayo ya ndoa za mitara, au za jinsia moja au za kuachana. Kwasababu utakuwa unalijua neno vizuri, hivyo hata mtu akija kukuambia Sulemani alioa wake wengi hivyo na wewe unaweza kuoa wake wengi, uwe unajua andiko la kuweza kuiangusha hiyo roho. Lakini kama Neno la Mungu halipo kwa wingi ndani yako, utahubiriwa mafundisho ya uongo nawe utaamini na kupotea. Na kujikuta upo kwenye mahusiano kumbe mbele za Mungu unazini na umeshazuiliwa kuoa kitambo sana.
2. Kwa kusali na kuomba kwa bidii.
Hizo ni silaha mbili kuu ambazo katika hizo ni ngumu kuchukuliwa na adui kwa vyovyote vile.
Bwana atubariki sote na kutusaidia.
Kama hujampokea Yesu, kumbuka siku zinaenda, na ile siku inazidi kukaribia, jiulize akirudi leo utakuwa wapi?
Marana atha.
Uchaji ni nini kama tunavyosoma katika 1Timotheo 2:10?
JE NI LAZIMA KUBADILISHA JINA BAADA YA KUOKOKA?
MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
Ukoma enzi za biblia ni ugonjwa uliojulikana kama pigo kuu kutoka kwa Mungu, kutokana na dhambi ambazo mtu alizozitenda.
Mtu aliyegundulika kuwa ana ukoma ilikuwa anatengwa na jamii nzima ya Israeli. Anapelekwa mahali ambapo wakoma wenzake walipo, mbali kidogo na makazi ya kawaida ya watu na haruhusiwi kuja kujichanganya na watu wengine asije akawaambukiza wale wasio na ugonjwa huo. Hata familia yake mwenyewe hakuruhusiwa kuisogelea, aliendelea kukaa huko huko, mbali kwa kipindi chote ambacho Mungu atamponya, na kama ikitokea hata ponywa basi maisha yake yote atakuwa ametengwa. Walawi 13.
Lakini ukoma haukuwa tu katika mwili bali ulikuwa pia katika nyumba. Utajiuliza nyumba nazo zilipigwa na ukoma na Mungu? Jibu ni ndio biblia inatuambia hivyo;
Wana wa Israeli walipokuwa jangwani Mungu aliwaagiza, akawaambia watakapoifikia hiyo nchi ya ahadi, na kukutana na nyumba ambayo Mungu kaipiga kwa ukoma, wasiikae, wasubiri kwanza kwa muda wa siku saba, kisha kuhani atakwenda kuingalia, na akiona ukoma ule, umeisha ndipo watakaporuhusiwa kukaa, lakini kama bado upo itakarabatiwa pale palipoathirika, na hapo watasubiri tena, kuangalia, ikiwa umeisha basi watu wataruhusiwa kuingia, lakini kama bado, kinyume chake ugonjwa ndio umezidi tu kutapakaa nyumba nzima..Basi nyumba hiyo yote ilikuwa inabomolewa na kila kitu chake kilikwenda kutupwa nje ya mji.
Walawi 14:33 “Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 34 Hapo mtakapoingia nchi ya Kanaani, ambayo nawapa kuwa ni milki yenu, nami nitakapolitia pigo la ukoma katika nyumba ya nchi hiyo ya milki yenu; 35 ndipo mwenye nyumba hiyo atakwenda na kumwambia kuhani, akisema, Naona mimi ya kwamba pana kama pigo katika nyumba yangu; 36 ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, mbele ya kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili kwamba vyote vilivyomo nyumbani visiwekwe kuwa unajisi; kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aitazame; 37 naye ataliangalia hilo pigo, na tazama, likiwa pigo limo ndani ya kuta za nyumba, nalo lina mashimo-mashimo, rangi ya majani, au mekundu, na kuonekana kuingia ndani kuliko huo ukuta; 38 ndipo kuhani atatoka katika nyumba hiyo mpaka mlangoni pa nyumba, na kuifunga hiyo nyumba muda wa siku saba; 39 siku ya saba kuhani atakwenda tena, naye ataangalia; na tazama, likiwa pigo limeenea katika kuta za nyumba; 40 ndipo kuhani atawaambia wayatoe hayo mawe, yaliyo na pigo, na kuyatupa mahali penye uchafu nje ya mji; 41 naye atafanya kwamba hiyo nyumba ikwanguwe ndani pande zote, na chokaa watakayokwangua wataimwaga nje ya mji mahali palipo na uchafu; 42 kisha watatwaa mawe mengine, na kuyatia mahali pa mawe hayo; naye atatwaa chokaa nyingine, na kuipaka chokaa hiyo nyumba. 43 Na kama hilo pigo likirudi tena, na kutokea ndani ya nyumba, baada ya yeye kuyatoa hayo mawe, na baada ya kuikwangua nyumba, na baada ya kupakwa chokaa, 44 ndipo kuhani ataingia ndani na kuangalia, na tazama, likiwa pigo limeenea ndani ya hiyo nyumba, ni ukoma unaokula hiyo nyumba; ni katika unajisi. 45 Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hata mahali palipo na uchafu.
Walawi 14:33 “Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
34 Hapo mtakapoingia nchi ya Kanaani, ambayo nawapa kuwa ni milki yenu, nami nitakapolitia pigo la ukoma katika nyumba ya nchi hiyo ya milki yenu;
35 ndipo mwenye nyumba hiyo atakwenda na kumwambia kuhani, akisema, Naona mimi ya kwamba pana kama pigo katika nyumba yangu;
36 ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, mbele ya kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili kwamba vyote vilivyomo nyumbani visiwekwe kuwa unajisi; kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aitazame;
37 naye ataliangalia hilo pigo, na tazama, likiwa pigo limo ndani ya kuta za nyumba, nalo lina mashimo-mashimo, rangi ya majani, au mekundu, na kuonekana kuingia ndani kuliko huo ukuta;
38 ndipo kuhani atatoka katika nyumba hiyo mpaka mlangoni pa nyumba, na kuifunga hiyo nyumba muda wa siku saba;
39 siku ya saba kuhani atakwenda tena, naye ataangalia; na tazama, likiwa pigo limeenea katika kuta za nyumba;
40 ndipo kuhani atawaambia wayatoe hayo mawe, yaliyo na pigo, na kuyatupa mahali penye uchafu nje ya mji;
41 naye atafanya kwamba hiyo nyumba ikwanguwe ndani pande zote, na chokaa watakayokwangua wataimwaga nje ya mji mahali palipo na uchafu;
42 kisha watatwaa mawe mengine, na kuyatia mahali pa mawe hayo; naye atatwaa chokaa nyingine, na kuipaka chokaa hiyo nyumba.
43 Na kama hilo pigo likirudi tena, na kutokea ndani ya nyumba, baada ya yeye kuyatoa hayo mawe, na baada ya kuikwangua nyumba, na baada ya kupakwa chokaa,
44 ndipo kuhani ataingia ndani na kuangalia, na tazama, likiwa pigo limeenea ndani ya hiyo nyumba, ni ukoma unaokula hiyo nyumba; ni katika unajisi.
45 Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hata mahali palipo na uchafu.
Sasa ni kwanini Mungu aitazame mpaka nyumba na kuipiga kwa ukoma? Kwa wakati ule zipo nyumba ambazo zilijengwa katika damu, nyingine katika dhuluma, nyingine rushwa, wizi, nyingine uzinzi n.k. Sasa nyumba kama hizi, Mungu hakuruhusu watoto wake, wazikae na ndio maana akazipiga kwa ukoma.
Hiyo inatufundisha nini sisi wa agano jipya?
Biblia inatuambia miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, ni nyumba za Mungu. Sasa pale anapotaka kushuka halafu anakutana na vimelea vya ukoma wa kiroho, tunachokisubiria ni nini kama sio kuharibiwa? Anakuja na kukutana na ulevi, uzinzi, uvutaji sigara, ni nini mtu huyo anatarajia kama sio kuuliwa na Mungu.
Anapokuja na kukutana na ushirikina, fitina, utazamaji wa picha za ngono, anakutana na uvaaji wa suruali kwa mwanamke, na nguo za kikahaba, na uchubuaji ngozi, ni nini anakingojea hapo kama sio kuharibiwa?
Kuna watu wanasema Mungu haangalii mwili bali roho, nataka nikuambie mwili wako unathamani kubwa kwa kama tu vile roho yako ilivyo, na usipoangalia na kuutunza utapigwa tu na Mungu, Kama aliweza kuzipiga nyumba ambazo hazina uhai wowote zamani, atashindwaje kuupiga mwili wako ulio na uhai ndani yake.
1Wakorintho 3:17 “Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Kama vile nyumba inavyopewa siku saba za kuangaliwa maendeleo yake, kama ukoma utaondoka au utaendelea, vivyo hivyo, na wewe ambaye unaliharibu hekalu la Mungu, usipumbazike kuona mbona hakuna hatua yoyote Mungu anayoichukua juu yangu. Upo wakati Mungu atasema sasa inatosha, mtu huyu hana faida yoyote kwangu, nimwondoe, tu… Anaweza asikuue kimwili, lakini rohoni ukawa mfu aliyeoza anayesubiria tu kufa kwenda kuzimu.
Mungu anatazamia tumzalie matunda katika miili yetu, vinginevyo atatung’oa mara moja, kwasababu kukaa bila kumzalia matunda anatuona kama TUNAMHARIBIA TU NCHI YAKE.
Luka 13:7 “Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?”
Hivyo, tubu mrudie Mungu, hizi ni nyakati za kumalizia, Kristo yupo mlangoni kurudi. Ulimwengu haujawahi kukutimizia furaha ya roho yako. Ni Kristo tu peke yake ndiye anayeweza kukupumzisha na kukuponya.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
DANIELI: Mlango wa 12.
In biblical times, there was a special road known as “The King’s Highway”—a major route that connected Egypt to Syria, passing through Jordan. It was vital for commerce and travel, maintained with bridges over rivers and leveled ground over valleys. Those who traveled on it had a clear and reliable path, much safer and faster than wandering through rough terrain.
This historical road is mentioned in the Old Testament and was well-known in the ancient world. But more importantly, it holds spiritual significance for us today, especially in understanding our journey of faith.
1. The Historical King’s Highway in Scripture
When the Israelites were traveling to the Promised Land, they reached Edom and requested to pass through via this road:
“Please let us pass through your land. We will not pass through field or vineyard, or drink water from a well. We will go along the King’s Highway, we will not turn aside to the right hand or to the left until we have passed through your territory.”(Numbers 20:17)
But the Edomites refused:
“You shall not pass through, lest I come out with the sword against you.”(Numbers 20:18)
Later, the Israelites made the same request to the Amorites:
“Let me pass through your land. We will not turn aside into field or vineyard. We will not drink the water of a well. We will go by the King’s Highway until we have passed through your territory.”(Numbers 21:22)
Again, they were denied—and this time, war broke out. But Israel prevailed.
2. Theological Insight: Old Testament Shadows and New Testament Realities
The Apostle Paul teaches that the events in the Old Testament serve as examples or shadows for us today:
“Now these things happened to them as an example, but they were written down for our instruction…”(1 Corinthians 10:11)
So what does the King’s Highway symbolize?
It represents a direct, secure, and God-ordained path toward His promises. In the Old Testament, it was the best route to the Promised Land. In the New Testament, that “highway” is Jesus Christ—the only true way to the eternal Promised Land: Heaven.
3. Jesus Christ: The True and Living Way
Jesus made this bold declaration:
“I am the way, and the truth, and the life. No one comes to the Father except through me.”(John 14:6)
This statement is exclusive and absolute. There is no other spiritual road that leads to God—not through religion, good deeds, prophets, or spiritual leaders. Only faith in Jesus Christ, evidenced by obedience and love, leads us to the Father.
The Prophet Isaiah foresaw this Highway of Holiness:
“And a highway shall be there, and it shall be called the Way of Holiness; the unclean shall not pass over it… It shall belong to those who walk on the way; even if they are fools, they shall not go astray.”(Isaiah 35:8)
This prophecy finds fulfillment in Christ, who makes sinners holy by His grace and leads them safely to eternal life.
4. Perseverance on the Path
Just as Israel faced opposition from Edom and the Amorites, we too face challenges—spiritual warfare, temptation, rejection, suffering. But like them, we must remain determined to stay on the path God has prepared. Jesus warned:
“For the gate is narrow and the way is hard that leads to life, and those who find it are few.”(Matthew 7:14)
The road may be difficult, but it is sure—and it leads to eternal joy.
5. A Call to Commitment
Many people are walking on uncertain paths, hoping their good works, religion, or traditions will lead them to God. But without Christ, every other road leads to destruction.
“There is a way that seems right to a man, but its end is the way to death.”(Proverbs 14:12)
Jesus is the only road built by God Himself—leveled by grace, paved by truth, and secured by His blood. He is the King’s Highway from Earth to Heaven.
Choose the Right Road
If you’ve been walking on uncertain paths, turn to Jesus today. Trust Him, follow Him, and walk in His ways. The journey with Him may involve sacrifice, but it is the only road that guarantees arrival at God’s presence.
The Israelites pursued the King’s Highway even when opposed—because they knew it was worth it. So must we.
“Let us run with endurance the race that is set before us, looking to Jesus, the founder and perfecter of our faith.”(Hebrews 12:1–2)
Jesus is the way. Walk in Him. Live in Him. And you will reach the Father.
That is the truth that has stood firm throughout all generations.
May the Lord bless you as you walk the King’s Highway.
Neno hili linatwa mara nyingi sana katika biblia, sana sana mahali ambavyo vinatajwa vizazi vya wana wa Israeli.
Mbari, kwa jina lingine ni UKOO. Kwamfano unaweza kukutana na sehemu fulani inasema, “hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao”. Hapo inamaanisha kuwa “hao ndio wakuu wa ukoo wa baba zao”,
Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo;
1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni”.
1Nyakati 7:4 “Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi”.
1Nyakati 8:28 “Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu”.
1Nyakati 9:33 “Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku”.
1Nyakati 26:13 “Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao”.
Luka 1:26 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, WA MBARI YA DAUDI; na jina lake bikira huyo ni Mariamu”.
Luka 1:26 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, WA MBARI YA DAUDI; na jina lake bikira huyo ni Mariamu”.
Soma pia Nehemia 10:34, 11:13
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
WhatsApp
Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio cha kweli cha roho zetu.
Kawaida ya Mungu ni huwa hatoi agizo juu ya agizo. Yaani kwa mfano leo akikupa agizo fulani ulitelekeze, haundi agizo lingine juu yake kulibatilisha hilo la kwanza, Atafanya hivyo endapo tu lile la kwanza litakuwa limeisha muda wake.
Mara nyingi tunakuwa tukiacha yale maagizo ya kwanza ya Mungu, na hiyo inatupelekea aidha kukutana na hukumu yake, au kushindwa kutekeleza mipango yetu kwa wakati.
Kwamfano utakutana na nabii mmoja katika biblia enzi za wafalme, ambaye alipewa maagizo na Mungu ya kwenda kumtolea unabii Mfalme mwasi Yeroboamu, akaambiwa akishamaliza kazi yake asile wala asinywe chochote katika mji huo, wala asilale au kupumzika na njia atakayoipita asiirudie tena hiyo hiyo. Lakini huyu nabii alipomaliza kweli kazi ya huduma alianza safari ya kuondoka. Lakini akiwa njiani alikutana na nabii mwingine mzee, akamshurutisha, aende kulala nyumbani kwake. Lakini yeye akamwambia Bwana amenionya nisikae mahali popote kwenye mji huu.
Sasa yule nabii mzee alipoona kuwa kijana huyu hataki, akamtungia habari za uongo na kumwambia, Bwana ameniambia ameghahiri, mpango wake, hivyo anataka uje ule upumzike nyumbani kwangu. Na yule kijana pasipo kufikiria ni kwanini Mungu awe kigeugeu, saa hiyo hiyo akamwamini, kwasababu tu ni nabii mwenzake tena mzee, anauzoefu wa mambo ya kinabii, akaenda kukaa kwake. Kitu kilichomtokea hatuna haja ya kueleza, sote tunajua alikuja kuliwa na simba, kwa kuyaasi maagizo ya Mungu (Soma 1Wafalme 13)
Tunamwona Mtu mwingine anaitwa, Balaamu, naye pia mwanzoni Mungu alimuonya asiende kuwalaani Israeli, lakini baadaye akawa analazimisha mawazo yake kwa Mungu, kilichofuata ilikuwa ni Mungu kumwambia haya nenda nitakuwa pamoja nawe..kumbe hakujua tayari njia Mungu alikuwa ameshamuandalia malaika wake amuue, na kama sio yule punda kumsaidia habari yake tusingeisoma leo hii kwenye biblia (Soma Hesabu 22).
Hiyo yote ni kutozingatia agizo la kwanza Mungu alilokupa, Siku zote agizo linalokuja juu ya agizo lile la mwanzo huwa halitokani na Mungu.
Tukisoma tena habari nyingine maarufu katika biblia ile ya Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Babeli utumwani, baada ya kukaa kule miaka 70. Biblia inatuambia Mungu alimuamsha moyo mfalme Koreshi wa uajemi, ili atoe amri kuwa watu wote waondoke kwenye makoloni yake, waende Yerusalemu kumjengea Mungu nyumba, kufuatana na unabii uliotolewa na Yeremia zamani.
Tunaona baada ya hapo Mfalme aliwapa zawadi nyingi sana, Hivyo waliondoka kwa moyo mkunjufu wakijua kabisa Mungu kaitimiza ahadi yake ya kwenda kumjengea nyumba Yerusalemu. Lakini walipofika kule na kuanza kutia msingi wa nyumba ya Mungu, maadui zao wakaanza kunyanyuka hilo likawadhoofisha, na kama hiyo haitoshi wakaandika waraka wa uchongezi wakampelekea mfalme mwingine wa uajemi ambaye alikuja kutawala baada ya Koreshi, aliyeitwa Dario, mfalme alipousoma, akatoa amri nyingine, kuwa usiendelee ujenzi wowote Yerusalemu, wa nyumba ya Bwana. Na mtu yeyote atakayefanya vile ilikuwa ni kifo.
Wayahudi waliposikia, juu waraka huo mpya, wote wakavunjika moyo, wakaacha kuijenga nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa tayari katika hatua nzuri, Hivyo ikapelekea nyumba hiyo kubakia hivyo hivyo kwa muda wa miaka mingi sana..Kila mtu akarudi kuendelea na shughuli zake kila siku.
Wakasau kuwa ni Mungu ndiye aliyewapa maagizo kuwa wakamjengee nyumba yeye, hawakujiuliza sasa haya maagizo mengine yanatoka wapi?
Mpaka baadaye sana, tunaona manabii wawili yaani Hagai na Zekaria wanatokea, wanawatabiria na kuwauliza kwanini mnaacha kujenga nyumba ya Mungu, wakidai kuwa huu sio wakati wa kumjengea Mungu? Kwa muda wako soma kitabu chote cha Hagai utaona mambo hayo.
Unaona, walisikiliza sauti ya pili, wakaicha ile ya kwanza, na hiyo ikawapelekea kucheleweshwa kwa huduma yao waliyokuwa wameshaianza,.. Siku zote sauti ya pili ni ya shetani, na sio ya Mungu.
Vilevile katika agano jipya kuna agizo ambalo tayari Mungu alishatupa.
Marko 16:15-16 Inasema..
“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Hili ni agizo ambalo Kristo alishatoa kibali, kufanya.. Lakini dunia ya sasa shetani ameshaiingilia, kiasi kwamba, sehemu nyingine watu hawaruhusiwi kuhubiri kabisa, sheria za nchi zao zimekataza..Sasa wewe kama mkristo ukiogopa sheria ya wanadamu, ukasema pengine huu sio wakati wa kufanya hivyo, ujue kuwa utafanana na wana wa Israeli walipokuwa wanalijenga hekalu la pili, utasubiria wee, na kamwe hiyo siku ambayo unayoina itafaa haitafika, Mungu atakachofanya ni kukumbusha tu, uliacha agizo la kwanza.
Sio hilo tu yapo maagizo mengine madogo madogo, yanakubana kiasi kwamba yanakufanya ushindwe hata kuiendeleza kazi ya Mungu, mpaka uwe na hiki au kile, au ukamilishe hiki au kile..Hayo yote hatupaswi kuyazingatia sana, mengine yana agenda ya shetani nyuma yake kukumwisha tu, bali tuzingatie lile agizo kuu la mwanzo ambalo Kristo ametupa enendeni ulimwenguni kote.
Mwingine atasema familia yangu iko hvi au vile..hupaswi kuangalia hayo yote
Safari ya imani, si mteremko muda wote, kuna wakati itasumbuliwa na mambo mengi, lakini hatupaswi kuyaogopa kwasababu Mungu ameshaahidi atakuwa na sisi katika hayo yote. Kama tu vile alivyokuwa kwa mababa zetu katika mapito yao.
MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:
BWANA AYAGANGE NA MACHO YETU PIA.
Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.