Shalom, Nini kinachokufanya umfuate Yesu au uende kanisani?..Je moyo wako ni mnyofu mbele za Mungu?
Katika biblia, Agano jipya tunamsoma Mchawi mmoja aliyeitwa Simoni, ambaye alikuwa akifanya uchawi, na kuwadanganya watu, mpaka watu wakaamini kuwa anatumiwa na Mungu kufanya ishara zile, na alijigamba kuwa yeye ni Mtu Mkubwa (wa Mungu)...mpaka mji wote ukadanganyika na kumwamini. Lakini huyu Simoni aliposikia injili aliamini na akabatizwa…Lakini Nia yake ya ndani haikuwa kugeuka na kuacha dhambi zake za uchawi bali kuongeza nguvu zake za kichawi..Yaani maana yake alimwamini Yesu, ili apate kuongeza nguvu za kufanya miujiza na si kwasababu anautaka wokovu.
Ndugu mpendwa kigezo cha mtu kumkiri Yesu au kubatizwa sio tiketi pekee ya kukubaliwa na Bwana Yesu. Linahitajika jambo lingine na ziada, nalo ni “badiliko la kweli la ndani”.
Huyu Simoni mara ya kwanza alikuwa ni mchawi ambaye alijifanya ni mtumishi wa Mungu, lakini baadaye alipoona ukristo umeingia mahali pale akaona sasa ameshapata vazi jipya la kufunika kazi yake hiyo ya uchawi.
Hebu soma kwa makini habari ifuatayo usiruke kipengele hata kimoja…
Matendo 8:9 “Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.
10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.
12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka
14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.
20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.
21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa MOYO WAKO SI MNYOFU MBELE ZA MUNGU.
22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
23 Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu”
Sasa watu wa namna hii wapo wengi katika kanisa. Hususani katika hizi siku za mwisho, ambapo kwa asili ni waganga wa kienyeji, wengine ni wachawi wana mapepo ya utambuzi na bado wanazipenda kazi zao za kuagua, zinawapatia faida nyingi..hivyo wanapouona ukristo wa kweli unahubiriwa wanaona kama ni vazi jipya na hivyo wanakwenda kubatizwa na kusimama mimbarani kuendelea na uaguzi wao, wengine sio wachawi lakini ni wanasiasa tu ambao wanaona wakifanya siasi kwa vazi la uanasiasa hawafikii kirahisi malengo yao, hivyo wanajigeuza na kuwa wakristo ili waendeleze siasa zao katika madhabahu ya Mungu.
Na sio tu kwenye eneo zima la utumishi, bali hata walio waumini, wapo wengine wengine wanakwenda tu kanisani kwasababu wanashida ya wachumba kwasababu wameambiwa wachumba wazuri watawapata kanisani, lakini mioyoni mwao hawana habari na Kristo. Wanakubali kubatizwa kuwasababu wamesikia kwa kufanya hivyo mambo yao ya kimaisha yataenda sawa, kama tu huyu Simoni mchawi.
Wengine wanakwenda tu kwasababu ni siku nyingi hawajaenda kanisani, hivyo wanataka angalau waende mara moja moja kwa mwezi au mwaka, lakini ndani ya mioyo yao hawana nia na Mungu wala hawana mpango wa kubadilisha mtindo wa Maisha yao na kufanyika kiumbe kipya kwasababu mioyo yao sio minyoofu mbele za Mungu.
Wengine wanakwenda kwa nia tu ya kuonyesha mavazi yao, kila wanaponunua vazi jipya, wanawaza ni wapi watakwenda kujionyesha?..wanagundua ni kanisani..Hivyo kanisa ni kama kioo chao,…wengine wanapenda tu kukusanyika kwenye jumuiya ya watu wengi hawapendi kukaa wenyewe wenyewe, wanapenda kwenda kusikiliza vichekesho na kupata burudani za nyimbo za kwaya..wengine wanapenda kufanyiwa uaguzi, akipitia vita kidogo, au hasara kidogo katika Maisha yake anakwenda kumtafuta mbaya wake kwa waganga wa kienyeji..sasa akipata kanisa ambalo linatoa huduma kama hizo ndipo anapokita mizizi hapo lakini yeye hana mpango na kumwondoa Adui mkubwa wa dhambi katika Maisha yake.
Sasa kundi lote hili ndio linalojumuisha “Manabii na Makristo wa uongo watakaotokea siku za mwisho”…Wengi wanafikiri Manabii wa uongo ni wale tu wanaosimama pale madhabahuni na kujiita manabii…hapana sio hao tu, hata wachungaji wasio na nia ya Kristo biblia inawaita manabii wa uongo, hata waalimu wanaopotosha biblia inawapa jina moja hilo hilo ambalo ni manabii wa uongo, hata waimbaji walio kinyume na Neno la Mung una wanaopotosha watu wa nyimbo zao na mavazi yao na Maisha yao..jina lao ni hilo hilo “manabii wa uongo au makristo wa uongo”..
Hali kadhalika hata Waumini ambao wanakwenda kanisani kwa nia ambayo sio ya Kristo mioyoni mwao jina lao ni hilo hilo “manabii wa uongo na makristo wa uongo” kwasababu wanawadanganya watu wa nje na waumini wenzao walio waaminifu kwamba wameokoka kumbe ndani hawana nia ya Kristo. Hivyo manabii wa uongo ni jina la ujumla..kuwafunua wale wote ambao wanajifanya wana uhusiano na Imani ya Kikristo na kumbe ndani yao ni maadui wa Msalaba.
Je na wewe upo kwenye kundi gani?..la makristo wa uongo au wa kweli?..Kama unakwenda kanisani kwasababu ya kutafuta majumba, mke au mali…wewe sio nabii wa uongo???…Je uasherati umeuacha?, je matusi umeyaacha, rushwa umeziacha, wizi umeuacha?, usengenyaji umeuacha?, kuishi na mwanamke/mwanamume ambaye humjafunga ndoa bado unaendelea kuishi naye?, ..kama bado hujaacha hayo yote kwanini unajiita mkristo?..huoni kama wewe utakuwa ni mkristo wa uongo?..uliyetabiriwa kutokea siku za mwisho?, ambao mtawadanganya wengi?..
Unatoa fedha nyingi kanisani ili upokee baraka kwenye kazi yako haramu ya uuzaji wa pombe..wewe una tofauti gani na huyu Simoni mchawi ambaye anataka kuwapa fedha wakina Petro ili na yeye awe na uwezo wa kuwawekea watu mikono washukiwe na nguvu za Mungu..Lakini wakina Petro walimwambia..
“20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.
21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa MOYO WAKO SI MNYOFU MBELE ZA MUNGU.”
Lakini pamoja na hayo, pengine ulifanya hayo yote pasipo kujua…ulikuwa unakwenda kanisani nusu uchi kwasababu hukupata kufahamu kuwa unafanya dhambi, ulikuwa unafanya biashara haramu na huku unakwenda kutafa baraka kwa kazi hiyo kanisani kwasababu ulikuwa hujui. Kristo anakupenda na bado unauwezo wa kutengeneza upya na kuwa kipenzi cha Mungu..Unachopaswa kufanya ni kutubu tu!..Toba ni kila mtu anatubu, haijalishi ni mchungaji, mwalimu, au Nabii..wote tunatubu..na Mungu anapendezwa na mtu mwenye kunyenyekea..
Hivyo tubia mambo hayo yote kama ulikuwa unayafanya..na kisha usiyafanye tena..Baada ya kutubu na kudhamiria kuanza Maisha mapya na Kristo, nenda katafute ubatizo sahihi mahali popote ili upate kukamilisha wokovu wako, kumbuka ubatizo ni muhimu, na ni lazima uwe wa Maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38).
Na moyo wako utakuwa mnyofu mbele za Bwana na utafanyika kuwa mwanafunzi wa kweli wa Yesu, na Roho Mtakatifu mwenyewe atakuongoza kufanya yaliyosalia.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?
Maombi(uombaji) ni nyenzo namba moja ya kumfikisha mtu uweponi mwa Mungu kwa haraka sana. Na kama tunavyofahamu sikuzote mtu yeyote aliyepo mbele za uso wa Yehova mwenyewe, uwezekano wa yeye kujibiwa mahitaji yake yote upo. Hivyo shetani kwa kulijua hilo hataki, mtu wakati wowote mtu afike huko hivyo anachofanya ni kumletea tu saikolojia za kipepo ili zimfanye asidhubutu kutaka kwenda kusali wakati wowote.
Na baadhi ya saikolojia hizo ni hizi:
Siku zote Kabla ya mtu hajafikiria tu kwenda kuomba, mawazo ya kwanza yanayomjia kichwani pake ni “nimechoka”..Ataanza kufikiria Nimekuwa kazini siku nzima, sijapata muda wa kupumzika, hata kidogo, hapa nilipo usingizi wenyewe umenikamata, najisikia homa homa, hivyo wacha leo nipumzike nitaomba siku nyingine..
Mwingine atasema nimefanya kazi ya Mungu siku nzima, tangu asubuhi hadi jioni hata sasa bado wapo watu wananitegemea nikawafundishe, nina mialiko mingi ya mikutano hivyo wiki hii nimechoka wacha nisiende kusali..
Lakini Bwana wetu Yesu Kristo yeye alikuwa anachoka kuliko hata sisi kwa utumishi mgumu kwa kuzunguka huko na kule, Utaona upo wakati baada ya kuwahubiriwa makutanao siku nzima mpaka imeshafika jioni badala awaage aende akapumzike kidogo, kinyume chake aliwalazimisha mitume wake watangulie mashuani, yeye akabaki nyuma kwenda kusali mlimani, alikaa kule masaa mengi, akisali, sio kwamba hakuwa amechoka hapana. Lakini alijua umuhimu wa maombi.
Mathayo 14:22 “Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
23 Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.
25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.”
Sisi pia, kwanini Neno “Nimechoka” linataka kuchukua nafasi ya maombi yetu?.Kwamwe tusikiendekeze hicho kigezo cha nimechoka kuchukua nafasi yetu ya maombi.
2. Sina Muda wa kuomba:
Neno lingine shetani analoliwekwa kwenye vichwa vya watu ni hili “sina muda wa kuomba”..kwani nimetingwa na mambo mengi, na shughuli nyingi nipo bize sana…Nimekutana na Watu wengi wakiniambia maneno haya, wanasema wanashindwa kwenda ibadani au kuomba kwasababu ya kukosa muda….Wapo pia watumishi wa Mungu wanaosema mimi nipo bize sana na huduma hivyo sina muda wa kuomba binafsi muda mrefu, ninamialiko mingi ya semina, sehemu mbali mbali..
Lakini nataka nikuambie pia tunaye Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ndiye kielelezo cha utumishi wetu, yeye alikuwa bize kuliko hata sisi, muda mwingine makutano walikuwa wanamsonga, muda wote wanataka awafundishe lakini biblia inatuambia..alijieupua, akaenda kutafuta mahali pa utulivu akaomba huko..
Luka 5:15 “Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.
16 Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba”.
Alifanya vile kwasababu alijua hata ile huduma aliyokuwa anaifanya ilihitaji maombi ili iweze kusimama, ni jambo la kushangaza kama tutasema sisi ni watumishi wa Mungu halafu tunakosa muda wa kuomba…Nasi pia tujiepue tupate muda wa kuomba binafsi.
Jambo lingine ni hili shetani analileta kichwani,.. mbona ninaweza kuyamudu tu Maisha yangu bila maombi?..Ni kweli utayamuda Maisha yako ya kidunia, lakini sio Maisha yako ya wokovu.
Utamudu kwenda disko, utamudu kuendelea kuwa mlevi, utamudu kuiba, utamudu kuwa mwasherati na utamudu kuwa bize na kazi zako kuliko hata hata kumtafuta Mungu na mambo mengine yanayofanana na hayo utayamudu kwasababu hayo yote hayahitaji maombi.
Lakini ukisema umeokoka halafu sio mwombaji, basi ujue hutaweza kuyashinda majaribu ya aina yoyote ile, Bwana Yesu mwenyewe alisema..Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni..Unadhani alikuwa anatania, unadhani shetani ataufurahia wokovu wako, ustarehe tu, halafu mwisho wa siku uende mbinguni?. Atakutafuta tu na kama wewe sio mwombaji basi huwezi kuchomoka,..na ndio maana taamaa za mwili unashindwa kuzitawala, kwasababu huombi, unashindwa kuwa na kiasi kwasababu muda wa maombi huna, hauuhisi uwepo wa Mungu maishani mwako, kwasababu wewe sio mwombaji..
Yakobo 4:1 “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa HAMWOMBI!”
Maombi ni Mafuta ya wokovu, kama vile gari lisivyoweza kwenda bila Petrol vivyo hivyo, wokovu wako hauwezi kupiga hatua yoyote bila kuwa maombi..
Saikolojia nyingine ya ki-shetani ni hii ya kudhani kuwa maombi yako hayawezi kujibiwa. Unaona kama ukiomba utapoteza muda bure,.Nataka nikuambie, Maombi yote yanasikiwa ikiwa utaomba sawasawa na mapenzi yake, lakini sio jambo la kufanya siku moja halafu basi Kesho unaendelea na mambo yako mengine, maombi ni sehemu ya Maisha ya mkristo ni mwendelezo, majibu ya maombi mengine yanakuja kwa kuomba tena na tena, leo, Kesho, Kesho kutwa n.k…lakini katika kuomba huko Bwana Yesu ametupa uhakika kuwa Ombi lolote la namna hiyo mwisho wa siku ni lazima lijibiwe tu..haliwezi kuachwa..
Luka 18:1 “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa”.
Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.
Mwisho, nataka nikuambie Wapo watu wanadhani wanaweza kuvumbua njia nyingine ya kuwasiliana na Mungu kirahisi au watapata suluhisho la matatizo yao Zaidi ya maombi..Fahamu kuwa Bwana wetu Yesu ameshatusaidia kufanya utafiti, sasa usitafute utafiti mwingine wa kwako wewe au wa kwangu mimi mbali na ule aliouthibitisha Yesu wa maombi..Yeye alikuwa hana dhambi hata moja, alikuwa ni mtakatifu sana, lakini katika utakatifu wake wote huo hakutupilia mbali suala la maombi alilifanya kama nyenzo ya yeye kufikia malengo yake, alifanya maombi kuwa sehemu ya Maisha yake..
Na wakati mwingine alikuwa anaomba kwa jasho na machozi mengi, na hata damu ilimtoka, akisihi mpaka akawa anasikilizwa…
Vinginevyo asingepokea kitu, Je mimi na wewe ambao si wakamilifu kama Bwana Yesu tunapaswaje?..tunaona raha gani kuishi Maisha ya kutokuomba halafu tunajiita bado ni wakristo..?
Waebrania 5:7 “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu”;
Hivyo tusitafute njia ya mkato..Kama tunataka tumwone Mungu akitembea katika Maisha yetu kwa ukaribu Zaidi na sisi, huu ndio wakati wa kuanza upya tena kwa nguvu za Maombi. Bwana alituambia walau saa moja kwa siku..Hivyo tujitahidi, tupambane, tushindane, tusiruhusu uongo wa shetani utuvurugie uombaji wetu, tusiruhusu, kukosa muda kutuvurugia ratiba yetu, tusiruhusu kutegemea nguvu zetu na akili zetu kutuharibia uombaji wetu..
Tuombe, tuombe, tuombe..
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
https://wingulamashahidi.org/mafundisho-ya-ndoa/
Urithi tulioahidiwa sisi wanadamu ni UZIMA WA MILELE. Na tumeahidiwa huo na Mungu wetu pale tu tunapomwamini Yesu Kristo. Mtu aliyemwamini YESU KRISTO, anakuwa ni mrithi wa Ahadi za Mungu zote pamoja na Maisha ya daima.…lakini wakati wa kupokea urithi bado unakuwa haujafika, ila katika roho ameshachaguliwa kuwa mrithi..kama tu vile mtoto anapoweza kuchaguliwa kuwa mrithi kabla hata ya wakati wa kurithishwa kufika..Ndivyo mtu aliyezaliwa mara ya pili anavyokuwa…Wakati utakapofika baada ya maisha haya kupita ndipo tutakapokabidhiwa vyote mikononi mwetu kama vile Bwana Yesu baada ya kumaliza kazi alivyokabidhiwa vyote na Baba…Mamlaka yote ya mbinguni na duniani alikabidhiwa.
Lakini habari ni kwamba urithi huu mtu anaweza kununua na kadhalika unaweza kuuuza..
Biblia inasema..
Marko 10:17 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.
19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.
20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.
21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate”.
Unaona hapo, ili uupate uzima wa milele hauna budi uuze baadhi ya mambo/vitu ulivyonavyo, na maana ya kuuza ni KUUTOA MOYO WAKO katika vitu ambavyo ulikuwa unaona vina maana katika maisha yako..Unatoa moyo wako kwenye fedha, unatoa moyo wako kwenye umaarufu, kwa kumaanisha kabisa sio kwa unafki, unatoa matumaini yako na moyo wako kwenye elimu yako, unatoa moyo wako kwenye anasa unazozifanya na dhambi na mambo yote ya kidunia, unakuwa kama ndio leo umeanza kuishi. Kiasi kwamba hakuna chochote cha nje tena kinachoweza kukusisimua au kilicho na nafasi kubwa katika moyo wako zaidi ya Yesu.
Kama Mtume Paulo alivyofanya…
Wafilipi 3:7 “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.
8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo”
Ukiingia gharama za namna hiyo za kuacha kila kitu kwaajili ya Kristo, hapo ni sawa umeuza kila kitu na kwenda kununua kitu cha thamani..Hivyo ufalme wa mbinguni una gharama, tena sio ndogo..kubwa sana..
Vivyo hivyo ufalme wa mbinguni UNAWEZA KUUZWA…Pamoja na kuwa unanunulika kwa gharama kubwa lakini pia unaweza kuuzwa..na unaweza kuuzwa hata kwa gharama ndogo sana….Hapa ni pale mtu aliyekuwa amepewa neema ya kumjua Kristo anapogeuka na kuidharau Neema ile na kuamua kuiacha na kurudia ulimwengu. Huyo nafasi yake inachukuliwa na mwingine, kama Yuda alivyouza nafasi yake kwa tabia yake ya WIZI, na kusababisha nafasi yake kupewa mwingine alyeitwa Mathiya.
Kadhalika Esau naye alivyouza nafasi yake ya urithi kwa chakula cha siku moja na kupewa Yakobo ndugu yake.
Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.
17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), IJAPOKUWA ALIITAFUTA SANA KWA MACHOZI”
Kama tunavyosoma hapo juu..Kuna wakati utafika kwa wale walioidharau Neema waliyopewa , wakati huo utakuwa ni wa majuto, na kilio na uchungu mwingi, watu watatamani kwa machozi warudishwe angalau dakika tano nyuma warekebishe makosa yao, lakini watakosa hiyo nafasi…watakapoona uasherati waliokuwa wanaufanya umewaponza wameikosa mbingu, ulevi waliokuwa wanajifurahisha nao kwa kitambo umewaponza, rushwa walizokuwa wanakula ziliwapofusha macho n.k..Wakati huo utakuwa ni wakati wa majonzi makubwa na majuto kama ya Yuda na Esau….Yuda baadaye alipokuja kujua makosa yake alilia mpaka kufikia kujinyonga kuona Maisha hayana maana tena…na Esau naye aliitafuta ile nafasi yake kwa machozi lakini hakuipata tena.
Bwana atusaidie tusiuze urithi wetu kwa vitu vichache vya dunia vinavyopita…badala yake tuutafute na kuununua kwa gharama zote. Ili siku ile tutakapoyaona yale ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia furaha yetu iwe timilifu.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
LIVUNJENI HEKALU HILI, NAMI KATIKA SIKU TATU NITALISIMAMISHA.
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
Unajua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea siku chache kabla ya Nuhu kuingia Safinani?…Mungu alimwambia Nuhu ingia wewe na mke wako na watoto wako na wanyama wote ndani ya safina..
Sasa kitendo tu cha Nuhu kuingia mule , muda huo huo Mungu aliufunga mlango. Lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa tendo la kufunga mlango halikumaanisha kuwa mvua itaanza kunyesha siku hiyo hiyo, hapana tunasoma mvua haikunyesha siku ile ile, bali ilisubiri muda wa siku saba, ndipo baadaye gharika ikashuka.. Mwanzo 7:13-17
Jambo tunaweza kuona hapo ni kuwa mlango wa wokovu ulikuwa umeshafungwa siku kadhaa nyuma kabla ya siku yenyewe ya maangamizi kufika..Pengine baadhi ya watu kuona jinsi mlango ule ulivyofungwa kwa namna isiyokuwa ya kawaida, walighahiri mawazo yao, wakamfuata Nuhu, wakamgongea mlango, wakimwambia Nuhu tufungulie tumegundua ni kweli hii dunia inakwenda kuangamizwa yote hivi karibuni hivyo na sisi tunataka kuzisalimisha roho zetu, tunakusihi utufungulie na sisi tuingie ndani…
Jibu la Nuhu, lilikuwa ni nini?, Mimi sikuufunga mlango, ni Mungu ndiye aliyeufunga na sijui katumia njia gani kuufunga kwasababu sioni hata komeo, wala kufuli pembeni, ni kama vile tumesakafiwa humu ndani, nitawasalidieje ndugu zangu..Ombeni, kwa Mungu labda atawasikia na kuwafungulia huu mlango kwasababu siku yenyewe ya maangamizi naona bado haijafika..
Pengine wale watu wachache waliokuwa pale nje, wakaanza kumlilia Mungu kwa machozi sana ili wafunguliwe mlango lakini hakukuwa na aliyejibu.. wengine walidhihaki na kuona Nuhu ndo kaamua kabisa kujisakafia ndani afie kule,..lakini wale wachache pengine wakaendelea kumsihi Nuhu kutafuta njia ya kuingia safinani.. Siku tano kabla ya gharika, wakaongezeka na wengine tena, nao pia wakawa wanamwambia Nuhu tufungulie ndugu zako, kwa maana kutokana na hali hii tunaoiona inavyoendelea sasa hivi, hii dunia siku chache sana inakwendwa kuangamizwa tufungulie Nuhu, tumetubu na ndio maana tumekuja kabla ya maangamizi yenyewe kufika tunakuomba utufungulie….Lakini Nuhu jibu lake lilikuwa ni lile lile sikuufunga mlango mimi..
Siku tatu kabla gharika, watu bado wanabisha hodi tu, wanatafuta upenyo mdogo lakini hawaoni, siku mbili kabla ya gharika, wanazidi kumsumbua Nuhu labda atafute kiupenyo cha mlango kwa huko ndani uvunje tuingie, lakini biblia inatuambia safina ile ilipigwa lami nje na ndani, hivyo hakukuwa na uwezekano wa kuivunja kiurahisi…
Mpaka ilipotimia siku ile ya gharika yenyewe kushuka,walikuwepo wengi sana pale nje ya safina wakimlilia Mungu, na kubisha hodi kwa bidii sana..lakini walikuwa tayari wameshachelewa..
Ndugu Biblia inatuambia wazi kama ilivyokuwa wote wakaangamia…hakuna aliyesalimika….Sasa biblia inatuambia kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu ndivyo itakavyokuja kuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu..Bwana Yesu alisema wazi kabisa..
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
Wengi tunadhani mambo hayo yatayokea baada ya kufa, jibu la ni La!, Hayo mambo yatakuwa ni hapa hapa duniani kipindi kifupi kabla ya unyakuo kupita…kuna watu watatamani sana waingizwe katika orodha ya watakaonyakuliwa lakini itakuwa ni ngumu tena..
Fahamu kuwa kitendo cha unyakuo sio kitendo cha kuotea tu, kwamba tunaishi ilimradi tu,halafu siku ile ikifika tutatoweka tu kwa bahati, hapana, Unyakuo unao HATUA zake..Na wale watakaonyakuliwa watajijua kabisa…jambo ambalo hawatajua ni siku yenyewe ya kuondoka, lakini watapewa uhakika huo wa kuondoka wakiwa bado wapo hapa hapa duniani kama vile ilivyokuwa kwa Eliya..
Sasa uhakika huo watautolea wapi?
Ukisoma kitabu cha ufunuo sura ya 10 yote utaona yapo mambo ambayo Yohana alionyeshwa akiwa katika kile kisiwa cha Patmo yahusuyo sauti za zile ngurumo saba, ambapo alipotaka kuziandika aliambiwa asubiri kwanza asiandike….Sasa hizo ni siri ambazo Mungu amezitunza kwa ajili ya bibi-arusi wake anayejiwekwa tayari leo hii kwa unyakuo.. Siri hizo hazijaandikwa mahali popote kwenye biblia..Lakini wakati huo utakapofika, Mungu atazihubiri duniani…Na hizo ndizo zitakazomvuta bibi-arusi ndani ya safina tayari kwa unyakuo siku yoyote..
Sasa wale ambao sio bibi-arusi wa Kristo,watakaposikia hizo jumbe zinahubiriwa, ndipo na wao watakaposhtuka ahaa!! Kwa mambo haya, ndio tunajua sasa unyakuo kweli ni siku yoyote..Hapo ndipo na wao watakapoanza shamra shamra za kumtafuta Mungu kwa kumaanisha, ndipo watakapoanza kubisha na kugonga kwa nguvu, wakitamani nao wahesabiwe..Siku hizo wataitafuta hiyo neema kwa bidii zote lakini hawataipata…
kwasababu mwana wa Adamu ameshasimama na kuufunga mlango…
Hao ndio wale wanawali wapumbavu, waliokwenda kutafuta mafuta na waliporudi wakakuta mlango umeshafunga..Ndivyo itavyokuja kuwa siku za hivi karibuni..(Soma Mathayo 25:1-12)
Nataka nikuambie ukishasikia tu ujumbe mwingine wa tofauti unapita duniani kote kwa nguvu nyingi za Mungu na udhihirisho mwingi, na kusikia mambo mageni masikioni mwako, yahusuyo safari ya kwenda nyumbani kwa Baba, kama bado wewe ni mkristo vuguvugu, basi ujue habari yako imeshakwisha mlango wa neema umekwisha fungwa..Ni heri kama utakuwa umesimama katika utakatifu na imani kwasababu hapo ndipo utakapopata uhakika wa kuondoka kwako hivi karibuni..Lakini kama wewe ni vuguvugu kwasababu hapa hatuzungumzii wale ambao ni baridi kwasababu wao hawataelewa chochote kitakachokuwa kinaendelea, tunamzungumzia wewe ambaye ni vuguvugu, habari yako siku hiyo itakuwa imekwisha..
Wewe ndio itakaoshuhudia wenzako wakienda mbinguni,..Utakuwa umelala na mume wako ambaye kila siku unamwona anajibidiisha kumtafuta Mungu na wewe utajikuta umeachwa, utakuwa unazungumza na mke wako na ghafla ataondoka, mwanao atakuwa amekwenda shule siku hiyo utashangaa harudi…Na ndio maana biblia inatuasa, TUJIWEKE TAYARI, kwa maana hatujui ni siku gani ajapo Bwana ..Hii dunia haina muda mrefu, Unyakuo si jambo la kulichukulia juu juu tu, ukiukosa ule, hali itakayokuwa inaendelea hapa duniani haielezeki, Bwana Yesu anavyosema utalia na kusaga meno alimaanisha kweli hivyo kwamba kusema hivyo kuwa kutakuwa na maombolezo ya ajabu kwa wale ambao watakuokosa unyakuo.
Bwana atutie nguvu katika safari yetu.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.
Kuota unaanguka chini maana yake ni nini?
Ndoto hii huwa inachukua maumbile tofautitofauti, wengine wanaota wanaanguka kutoka kwenye ghorofa refu sana, wengine kutoka kwenye mti mrefu, wengine kwenye shimo lisilokuwa na mwisho, wengine wanaota wanaanguka kutoka angani. Wengine wanaangukia kwenye maji n.k.
Maadamu kiini cha ndoto ni Kuanguka kutoka sehemu fulani, basi ujue ndoto hiyo ni tahadhari kubwa kwako kutoka kwa Mungu, kwani Biblia inasema..
Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;
18 YEYE HUIZUIA NAFSI YAKE ISIENDE SHIMONI, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake”;
Unaona huo mstari wa 15 unasema Mungu kumbe anaweza kuzungumza na mtu mara moja, katika ndoto na asipojali atazungumza naye hata mara mbili..ili tu amzuie nafsi yake isiende shimoni. Hivyo fahamu kuwa ndoto hiyo ni Mungu anazungumza na wewe kukuonya.
Ni vizuri kujua katika biblia inapozungumza kuanguka inamlenga ibilisi mwenyewe kwasababu yeye peke yake ndio anayetajwa akianguka kutoka mbinguni..Bwana Yesu alisema..
“…Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme(Luka 10:18)..
Sasa inaposema alimwona shetani akianguka inamaanisha kuwa hapo mwanzo alikuwa sehemu sahihi lakini kuna wakati ulifika alifanya mambo fulani yasiyofaa ndio yakamfanya atoke katika ile sehemu yake na aanguke chini kwa kasi sana kama umeme.. na hicho si kingine Zaidi ya dhambi ya uasi..
Hivyo tendo la kuanguka ni tendo linalofunua uasi.. Shetani alipoasi ndipo alipoanguka chini, Vivyo hivyo na mtu yeyote leo hii anapomuasi Mungu, ni ishara kuwa anaanguka kutoka katika uwepo wa Mungu na mwisho wake unaenda kuwa mbaya kama ulivyokuwa kwa shetani.
Kwahiyo ikiwa unaota unaanguka chini, tena mahali ambapo hufiki, basi ujue hiyo ni tahadhari kwako, kuwa unaanguka kutoka katika neema ya Mungu, mrudie Mungu wako kabla mlango wa neema haujafungwa.. Yaangalie Maisha yako, na matendo yako, unaona kabisa hayaendani na njia ya wokovu..unaona kabisa hata Kristo akirudi leo hii utaachwa kutokana na njia zako na mienendo yako.
Kwa kuwa Mungu anakupenda na anaona mwisho wako utakavyokuwa kama wa shetani, ndio maana anakuonyesha ndoto kama hiyo, anachotaka kwako ni utubu dhambi zako, umgeukie yeye. Ukitubu leo kwa kumaanisha atakuokoa, na kukusafisha kabisa..Anachohitaji kwako ni moyo wa kumaanisha, kabisa, Hivyo kama kweli umemaanisha kufanya hivyo leo basi ujue uamuzi unaoufanya ni mzuri..Usijiangalie wewe ni muislamu, au mkristo ikiwa Kristo hajaumbika ndani ya Maisha yako, haijalishi wewe ni nani, umepotea tu na hata ukifa leo huwezi kwenda mbinguni..
Hivyo kama unapenda Yesu leo awe mwokozi wako, na kiongozi wa Maisha yako basi
Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, hivyo usingojee Kesho, haitakuwa yako..
Sasa ukishajitenga sehemu yako mwenye, piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo,
Sasa Mungu akishaona umegeuka kabisa kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Ubarikiwe sana
Unaweza pia kujiunga na kundi letu la mafundisho Whatsapp, au kuwasiliana nasi kwa link hii
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
NIFANYE NINI ILI NILITIMIZE KUSUDI LA MUNGU.
NINI TUNAJIFUNZA KWA MWANA MPOTEVU NA NDUGUYE?
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Shalom. Jina kuu la Mwokozi wetu Yesu Kristo, libarikiwe.
Karibu tujifunze biblia.
Mathayo 3:5 “Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;
6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.
7 Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
8 Basi zaeni matunda yapasayo toba;
9 wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.
10 Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”
Soma tena mstari wa 7 “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? ”
Tunaweza kuiweka vizuri hiyo sentensi kwa namna hii “Enyi wazao wa nyoka ni nani aliyewadanganya(maana yake ni nani aliyewaonya) kwamba mtaiepuka hukumu inayokuja kwa njia hiyo mnayoitaka nyie?”..Njia gani?…Njia hiyo ya kuja kutaka kubatizwa na huku bado hamtaki kuacha dhambi zenu…Ni nani aliyewahubiria kuwa mtaikwepa hukumu kwa namna hiyo?…Maana yake mnafikiri kuwa kwa kuja kubatizwa tu hiyo inatosha kuikwepa hukumu itakayokuja….Mnajidanganya!…ZAENI MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!…Maana yake ni kwamba baada ya kutubu ishini kulingana na kutubu kwenu..Kama ulikuwa ni mwasherati, tubu na UACHE UASHERATI! Usiufanye tena, kama ulikuwa na kiburi tu na uache kuwa mwenye kiburi tena, kama ulikuwa mlevi unatubu na kuachana na ulevi wako, n.k..Huu ubatizo hautakuwa na msaada wowote kwenu kama mtakuja tu kubatizwa na huku bado hamjaacha matendo yenu mabaya. Huo ndio ujumbe Yohana Mbatizaji alikuwa anataka kuwapa wale Mafarisayo na Masadukayo.
Mafarisayo walisikia injili ya Yohana, wakaogopa, lakini wakasema aah ngoja tukabatizwe na sisi ili pengine tutaokoka huko mbeleni, lakini mioyoni mwao walikuwa hawana mpango wa kubadilika haka kidogo,..Walitaka kuugeuza ubatizo wa Yohana kama dini tu!..kama ni Liturujia mpya tu ya kufuata, kama katekisimo tu!..lakini walikuwa hawajui lengo kuu la ule ubatizo ni nini.. Lengo lake kuu lilikuwa ni kutubu na KUACHA DHAMBI!..sio kwenda kulowekwa kwenye maji na kurudi kuendelea na Maisha yako ya dhambi kama kawaida, na jina lako liwe limeshaandikwa mbinguni. Sio hivyo kabisa.
Vivyo hivyo na leo, ubatizo sio dini, na wala sio lebo ya kwamba Mungu anataka watu waliobatizwa ndio wawe wamepata tiketi ya kuingia mbinguni haijalishi wanaishije, yeye anataka tu watu wabatizwe.. hapana! Mungu anataka watu waliotubu na KUACHA DHAMBI. Hao ndio mbele za Mungu ubatizo wao una maana lakini kama mtu hujatubu kwa KUACHA DHAMBI, mtu huyo anamdhihaki Mungu.
Ukimuuliza mtu je umeokoka anakujibu, mimi nimebatizwa!..ukimuuliza tena je una uhakika wa kwenda mbinguni anakujibu ndio nilishabatizwa. Ubatizo hauna uhusiano wowote na kwenda mbinguni kama hujatubu kwa kuacha dhambi..Ndicho mafarisayo walichokuwa wanaenda kufanya kwa Yohana.
Umesema tu umetubu lakini bado unaendelea kuvuta sigara, bado unaendelea na uasherati, unaendelea na ulevi na ulawiti na usagaji, na pornography, halafu unasema umebatizwa au unakwenda KUTAFUTA UBATIZO, Ukidhani ndio unampendeza Mungu, na kwamba ndio utakwenda mbinguni..nataka nikuambie hapo unakwenda kujitafutia tu Laana badala ya Baraka.
Kutubu maana yake ni kugeuka na kuacha kile ulichokuwa unakifanya, na sio kusema tu mdomoni nimeacha na ilihali Maisha yako bado yapo vile vile. Ikiwa haupo tayari kuokoka, basi ni heri usiugize wokovu, wala usijiite hivyo, kwasababu ndivyo unavyomtia Mungu wivu kwa mienendo yako.
Watu wa Ninawi Mungu aliwasamehe kwasababu Aliona matendo yao kwamba wamegueka, wameacha mambo maovu waliyokuwa wanayafanya, hiyo ndiyo ikawafanya Waepukane na hukumu ile ambayo ilikuwa inawajia, na Mungu hakuona midomo yao kwamba wametubu kwa midomo ndipo awasamehe, hapana! bali matendo yao ndiyo yaliyosababisha wao kusamehewa.
Yona 3:10 “Mungu akaona MATENDO YAO, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende”
Hali kadhalika, usifanyike kuwa mzao wa nyoka, kwa kutafuta kutimiza maagizo ya Mungu na huku moyoni huna mpango wa kutenda mapenzi yake. Hizo ni tabia za Nyoka kibiblia. Mafarisayo wanamwendea Yohana kubatizwa na huku mioyoni mwao ni wale wale watu wenye viburi, wanaopenda utukufu, wenye wivu, wenye chuki, …maana japokuwa walikuwa wanamwendea Yohana kubatizwa lakini mioyoni mwao walikuwa wanamchukia n.k
Kama umeamua kumfuata Yesu leo, basi kubali pia kubeba na msalaba wako, kabla ya kwenda kubatizwa piga gharama kabisa kwamba unakwenda kuacha dhambi moja kwa moja, kwamba dunia ndio umeipa mgongo hivyo, msalaba mbele, ulimwengu umeuacha nyuma..Na kwa kufanya hivyo ndipo utaona nguvu za Mungu katika Maisha yako zikikusaidia na kukuongoza na ndivyo Mungu atakavyokukaribia Zaidi na kukupenda. Na kukubariki.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.
التنين القديم
لماذا الشيطان هو التنين القديم / التنين القديم؟
شالوم ، بنعمة إلهنا رأينا الشمس مرة أخرى اليوم. مرحبا بكم في دراسة كلمة الله التي هي غذاء لأرواحنا.
يقول الكتاب المقدس في ..
رؤيا يوحنا 20: 1 “ورأيت ملاكا ينزل من السماء ، وله مفتاح الحفرة القاع وسلسلة كبيرة في يده.
2 وأمسك التنين ، الذي عانى الشيطان والشيطان ، وقيده بألف سنة ، ”
يُعرف الشيطان باسم الثعبان القديم أو التنين القديم … وهذا يعني أنه عاش منذ فترة طويلة ، وقد عاش مثل التنين / الثعبان القديم منذ ذلك الحين … وإذا كنت تعرف أي شيء موجود منذ فترة طويلة ، فيجب أن يكون تجارب كافية عن الحياة ، على سبيل المثال ، يجب أن يعرف الرجل العجوز الكثير من الشباب. كبار السن هم أكثر دراية من المراهقين.
نظرًا لأنهم مروا بأشياء كثيرة في حياتهم وتعلموا الكثير ، فقد تعلموا من أخطائهم ومن أخطاء الآخرين … لذلك لا يمكن مقارنتهم مطلقًا بالأطفال حديثي الولادة أو المراهقين.
وبالمثل ، يُعرف الشيطان أيضًا باسم التنين القديم / التنين القديم …
هذا يعني أنه يعرف الكثير عن الإنسان … إنه موجود منذ عدن ، ويعرف آدم في وجهه وشكله وشخصيته التي لم ينسها ، ويعرف حواء أيضًا … إنه يعرف نوح ، وكان يشهد كيف دمر العالم عند الطوفان … كان ينظر … وما زال يتذكر صورة إبراهيم وسارة … يتذكر المكان الذي أزعجوه فيه في حياتهم. إنه يتذكر موسى … وما زال يعرف كل شخصيته ويعرف نقاط ضعفه. لديه وجه دانيال ونبوخذ نصر ، وإيليا ويتذكر سلوكهما … كما يعرف رئيس الحياة ، يسوع المسيح ، يتذكر جميع الأحداث من ولادته حتى أنه كان هناك في البرية لإغراءه ، وعندما توفي وقام ، يعرف قوته والقوة التي لديه الآن … إلخ
لذلك فإن الشيطان يعرف الناس جيدًا ، ويعرف الناس وسلوكهم ، ويعرف ما يحبه ، وما لا يعجبهم … لقد رأى كل الأجيال من آدم حتى الآن …
ما عليك سوى أن تسأل نفسك حتى الآن عن عمر 70 عامًا على الأرجح ، ومع ذلك يمكنك تصنيف سلوك بعض الأشخاص وبعض القبائل لدرجة أنك ربما تعرف سلوك شخص ما حتى لو لم يكن يتكلم كلمة واحدة .. يمكنك تجميعه / لها حتى قبل أن تذهب بعيدًا … الآن إذا كنت ممن تقل أعمارهم عن 60 عامًا تعرف بالفعل المجتمعات وعاداتها … إلى أي مدى تعتقد أن الشيطان سيعرف الناس؟ لأنه من عدن إلى هذا اليوم.
أريد أن أخبرك أنه يعرف البشر جيدًا … إنه يعرف مكان احتجاز الأطفال الأسرى ، كبارًا وصغارًا على حد سواء … لأن الرجل هو نفسه … لعدة أشخاص في الأجيال الماضية ونجح … إنه يعرف كيفية إسقاط الأطفال. عبيد الله … لأنه جرب في الماضي ونجح للآخرين بحيث يطبق نفس التجربة على الناس من جميع الأعمار. إنه (التنين القديم) يعرف كيفية إبعاد الناس عن الصلاة ، ويعرف كيف يؤثر عليهم ليس للبحث عن الله ، لأنه حاول بهذه الطريقة في الماضي ونجح. لديه خبرة كافية.
ما لم تحصل على حق في يسوع ، فلن تهزم الشيطان بأي شكل من الأشكال ، لديه معرفة أكثر منك وأنت ،
إذا كنت لا تريد الرب يسوع وأنك تستطيع أن تمنع نفسك من ارتكاب الزنا دون أن تكون في المسيح ، فأنا أريد أن أخبرك بالحقيقة أنك تضيع وقتك! في يوم من الأيام سوف ترتكبها … أشخاص مثلك حاولوا ذلك في الماضي وكان (الشيطان) قد قبض عليهم ، لذا فأنت لست أول من يفكر في ذلك أو يجربه.
مرة أخرى ، إذا قلت إن بإمكانك فعل أشياء جيدة أو بدون أن تكون في يسوع … أخت! لقد سعى الشيطان بالفعل إلى حل لأشخاص مثلك على الأرجح منذ أكثر من 2000 عام … قد تعتقد أنك أول من جرب ذلك ، لكن ربما يكون لدى الشيطان 10 ملايين قائمة من الأشخاص في الأجيال الماضية حاولوا أن يتصرفوا مثلك من السيد المسيح وقد تغلب عليهم جميعا.
لذلك أنت الذي ولدت هذه الأيام لا يمكنك أن تتفوق على حكمة الشخص الذي كان موجودا قبل سنوات عديدة … (ألا تعرف لماذا يسمى الشيطان إله هذا العالم؟ لأنه يعرف الشؤون الإنسانية أكثر من أي إنسان آخر).
لهذا أخبره الرب يسوع أنه يفكر دائمًا في ما يخص البشر وليس لله. لأنه لا يدرس الله بل يدرس الرجال وكيف يحكمه. اذهب واقرأ (متى 16:23).
لذلك سوف تسأل إذا كان الشيطان يعرف الكثير عن الشؤون الإنسانية ، فمن ذا الذي يستطيع الهروب؟ وتغلب عليه؟
الجواب هو هذا ؛ بالإضافة إلى كل عظمة الوعي الإنساني الذي لديه في حكمته ، هناك شخص أكبر منه سناً. هذا هو المعروف باسم قديم من الأيام.
دانيال 7:13 -14 “رأيت في رؤى ليلية ، واذا جاء واحد مثل ابن الإنسان مع غيوم السماء ، وجاء إلى قديم الأيام ، واقتادوه بالقرب منه.
١٤ وكان قد أُعطي له سلطانًا ومجدًا ومملكةً لكي تخدمه جميع الشعوب والأمم واللغات: سلطانه هو سلطان أبدي لا يموت ، ومملكته التي لا يجوز تدميرها ”
أبانا يعرفنا أكثر مما يعرفنا الشيطان. يتمتع الشيطان بالتجربة لإسقاطنا ، لكن الحكمة التي لدى الله لديها القدرة على معرفة أفكاره ونواياه وخططه ، وإسقاط أفكاره … كل ما يريد أن يفكر فيه ، نحن في المسيح بالفعل. لدينا القدرة على معرفة كل الفخاخ له. تخترقنا الحكمة الإلهية التي تعطينا القدرة على إدراك كل الأفكار الشيطانية والتغلب عليها.
لكن هذه الحكمة تُمنح فقط لأولئك الذين يؤمنون بابنه الحبيب ، يسوع المسيح.
لن يتمكن الآخرون خارج المسيح من هزيمة التنين القديم الذي هو الشيطان. سيتم توجيههم إلى الشيطان حيث يريدهم أن يذهبوا ، وهذا هو السبب في أن الشخص الذي لم ينقذ لن يكون له سلام ولن يتغلب أبدًا على الخطيئة أو إرادة العالم. هذا هو ما يفعله … في بعض الأحيان يخطط للقيام بهذا أو ذاك ، ولكن في النهاية ينتهي الأمر إلى أن يكون شيئًا آخر … لماذا؟ ذلك لأنه يريد أن يوجه نفسه ويعتقد أنه قادر على النجاح بقوته وعقله.
لذلك إذا لم يتم خلاصك ، ومع ذلك فإن الأمل في التغلب على التنين القديم لا يزال متاحًا حتى اليوم ، فإن حكمة الله الإلهية تريد أن تدخل فيك اليوم … لا تستمع إلى الشيطان الذي يخبرك في ذهنك الآن أنه لا يمكن إنقاذك أن لديك الكثير من الخطايا وأن الله لن يغفر لك … إنه يستخدم تكتيكاته القديمة فقط ، لذلك لا تستمع إليه … لكنك تنكره اليوم وتأكد من حرمانك من العمل … قرر اليوم أن تتوقف عن الخطيئة والتوبة والتوقف عن الذهاب إلى النوادي الليلية وتقرر إيقاف ثرثرة وتقرر إيقاف السكر. والزنا والرب أحبك … والحكمة الرائعة من قديم الأيام. (الرب) إلهنا ، سوف يأتي إليك ، قد يعرف ماكره وحيله ..
الأمثال 2: 6 “لأن الرب يعطي الحكمة: من فمه يأتي المعرفة والفهم.
7 وضع حكمة سليمة للأبرار: هو دجل لهؤلاء الذين يمشون منتصبين.
8 يحفظ طرق الدين ويحفظ طريق قديسيه.
9 حينئذ تفهم البر والحكم والعدالة. نعم ، كل طريق جيد.
10 عندما تدخل الحكمة الى قلبك وتكون المعرفة ممتعة لنفسك.
الرب يباركك.
يرجى مشاركتها مع الآخرين.
Nyimbo za Injili ni zipi?, waimbaji wanapaswa waitendeje huduma hiyo?..
Shalom. Karibu tuongeze maarifa kuhusu Neno la Mungu..Tukilijua Neno la Mungu vyema, tutayajua mapenzi ya Mungu na hivyo tutaishi kulingana na yeye anavyopenda na tutabarikiwa.
Moja ya karama ya muhimu sana katika Mwili wa Kristo ni karama ya uimbaji. Sasa ni wazi kuwa mtu yoyote anaweza kuimba, awe mwanamume au mwanamke..Lakini yupo ambaye akiimba nyimbo au akiimbisha basi kunaambatana na nguvu fulani za kipekee za Roho Mtakatifu. Sasa nguvu hizo sio za kuwafanya watu waanguke au walie..Hapana bali nguvu hizo ni zile zinazomfanya mtu apate badiliko fulani la rohoni, ageuke kutoka kuwa mwenye dhambi mpaka kuwa mtakatifu.
Mwimbaji huyu anapoimba au anapoimbisha, basi Roho yule yule anayeshuka juu ya watu wakati Mchungaji anahubiri ndio huyo huyo anayeshuka juu ya watu wakati anaimbisha.
Sasa huduma ya uimbaji sio huduma ya kutafuta fedha, kama vile huduma nyingine yoyote katika mwili wa Kristo isivyo ya lengo la kutafuta fedha wala umaarufu. Mchungaji au Mwalimu anapohubiri katika kanisa lake, na anapoalikwa mahali pengine au Taifa lingine kwenda kuihubiri Injili, hapaswi kwenda kule kwa lengo la kutafuta fedha. Biblia inasema tumepewa bure tutoe bure..Hivyo atakwenda kule alikoalikwa na atahubiri bure..Ndio wale waliomwalika watamgharimia nauli, pamoja na malazi na makazi kwa huo wakati, lakini hapaswi kwenda kwa lengo la kutafuta malipo/mshahara. Kama waliomwalika watakuwa na moyo mwingine na kusema hatutapenda mtumishi huyu aondoke mikono mitupu, hivyo kwa kuguswa kwao wakampatia chochote kile iwe fedha, au mali..hapo sio dhambi kupokea..lakini Mchungaji, au mwalimu au mtu yoyote yule hapaswi kuomba chochote, wala kuonyesha dalili ya kuwa mhitaji.
Mungu anajua kuwahudumia watu wake, haihitaji yeye kusaidiwa, hivyo aliposema…”Tumepewa bure tutoe bure alimaanisha kabisa”..kwamba kwa namna yoyote ile atawafungulia watumishi wake mlango wa kula na kunywa hata njia hiyo.
Vivyo hivyo na uimbaji wa nyimbo za injili. Mtu yeyote aliyepewa karama hiyo hapaswi kuwa kama wasanii wa nyimbo za ulimwengu ambao wapo kwa lengo la kutafuta fedha kwa sanaa zao hizo. Mtu mwenye karama ya uimbaji atafanya kazi ya Mungu bure pasipo malipo..akifika mahali kaalikwa kwenda kuongoza nyimbo za kumsifu Mungu na kumwabudu, hapaswi kutazamia malipo kwa namna yoyote ile. Anapaswa afanye kazi yake ya uimbaji kwa uaminifu kama ya mchungaji aliyealikwa…aimbe nyimbo za injili na kuhakikisha neema ya Mungu imeshuka juu ya watu, hiyo ndio inapaswa iwe furaha yake ya kwanza, na lengo lake kuu la kwenda pale.
Hali kadhalika hapaswi kubadilika kimavazi na kufanana na wasanii wa kidunia..Kazi ya Mungu sio ya kuonyesha uanamitindo…kwamba leo umevaa hiki, kesho unavaa kile, ili watu wakuone jinsi unavyojua kuvaa…Vaa nguo za heshima, kama ni mwanamke vaa gauni refu haijalishi ni la gharama au sio la gharama, lakini lazima liwe la kujisitiri, hupaswi kwenda kufanya huduma huku umevaa suruali, huku mgongo upo wazi, huku umejichubua uso, huku umeweka make up mfano wa Mwanamke Yezebeli wa kwenye biblia..hali kadhalika mwanaume hupaswi kwenda kufanya huduma huku umenyoa kidunia, huku umevaa nguo za kubana, huku umejipamba mpaka unakaribia kufanana na wanawake.
Ukifanya hivyo na kwenda kufanya huduma na mambo hayo machafu utakuwa bado hujaelewa nini maana ya kumtumikia Mungu, utakuwa unamdharau Mungu na madhabahu yake, na utakapoambiwa ukweli utaona kama unaonewa WIVU, hakuna wivu hapo unaoonewa, ni kwa faida yako binafsi..Unakwenda kuzitafutia laana badala ya baraka ndugu…..Unapoacha kusimama katika Neno la Mungu na kujilinganisha na wasanii wa kidunia, ni sawa na mchungaji aliyeacha majukumu yake madhabahuni na kujilinganisha na wanasiasa waliopo bungeni.
Ndugu yangu, uliyejaliwa karama ya uimbaji..Utumie kwa utukufu wa Mungu, kama wachungaji ambao wamealikwa kutembea dunia yote kuhubiri hawabweteki na kwanini wewe unabweteka na kujiharibia huduma yako kwa kuwaiga hao wasanii wa kidunia au hata baadhi ya wanaojiita wasanii wa injili ambao hawajaelewa maana ya kumtumikia Mungu?
Sasa utauliza je! Sitakiwi kabisa kwenda kurekodi nyimbo zangu studio?
Hapana unapaswa ukazirekodi kabisa tena kwa bidii nyingi, kwa uongozo thabiti wa Roho Mtakatifu, ili injili ienee kwa wengi, na kuwa msaada na baraka kwa wengi..Lakini katika hiyo usiigeuze kuwa ndio sehemu ya kupatia fedha na utajiri. Weka bei ya bidhaa hiyo ambayo inalingana na gharama ulizoingia, na faida kidogo kwaajili ya msingi wa kazi zitakazofuata kama hizo na si kwaajili ya kupata fedha, wala kwaajili ya kujiandaa kuwa msanii maarufu. Na hupaswi kukasirika unaposikia watu wanabarikiwa kwa nyimbo ulizoimba, au wanaziimba nyimbo zilizotungwa na wewe pasipo kukutaja wewe wala kukupa malipo…Hupaswi kukasirika, zaidi ya yote unapaswa ufurahi kwasababu injili ya Kristo inakwenda mbele.
Kwasababu hata wachungaji ndio hivyo hivyo, wanapotengeneza kitabu..na mafunuo waliyoyapata na kuyaandika ndani ya kile kitabu yatakwenda kufundishwa huko na huko, kila mahali na hata kumrudia yeye mwenyewe…na wala hawasemi wala kuchukia kwamba ule ufunuo ni wa kwao na kwamba wana hati miliki nao, mtu mwingine hapaswi kuhubiri bila idhini yao. Kama yupo Mtumishi wa namna hiyo, basi huyo naye bado hajaelewa nini maana ya kuwa mtumishi, kwasababu injili ya Kristo haihubiriwi kwa hati miliki. Lakini kama hujawahi kuona kwanini wewe muimbaji uchukie na kukwazika kuona mtu anaimba nyimbo uliyoiimba wewe bila hata kukutaja au kukutambua?.
Ukiona unasikia huo wivu basi fahamu kuwa bado kuna kasoro ndani yako, upo kutafuta umaarufu na faida kupitia kazi ya Mungu, na haupo kwa lengo la kuisambaza injili. Huna tofauti na Yuda Iskariote.
Hivyo zingatia hayo machache mtu wa Mungu, na Bwana atakusaidia, kama una huduma yoyote ndani yako ya kuhudumu kwa nyimbo za injili, tenga muda uilinganishe na huduma nyingine katika mwili wa Kristo jinsi zinavyofanya kazi, ili upate hekima na ufahamu jinsi ya kuitenda kazi ya Mungu katika shamba lake.
Bwaan akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Ukisoma ule waraka wa pili ambao Paulo alimwandikia Timotheo kuanzia ile sura ya tatu mstari wa 1-9, utaona jinsi Paulo alivyoanza kumweleza Timotheo juu ya mambo yatakayotokea siku za mwisho..Lakini alianza kwa kumwambia neno hili “siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari”.. Jiulize ni kwa nini alimwambia hivyo?. Alimwambia hivyo kwasababu aliona jinsi wimbi kubwa la watu wenye mfano wa utauwa (wanaonekana kama ni watu wa Mungu), lakini wakizikana nguvu zake, watakavyonyanyuka na kuwapoteza wengi.
Hao watu hawakuwepo wakati mwingine wowote isipokuwa tu watatokea katika siku za mwisho, yaani watu wanaoonekana ni watumishi wa Mungu, wanaoonekana wanawaongoza watu katika njia za kweli, lakini kumbe nyuma ya mgongo wanazikana nguvu za Mungu..
Sasa hizi nguvu za Mungu ni zipi?..
Biblia inatueleza “Neno la msalaba” ndio nguvu ya Mungu..
1Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu”.
Sehemu nyingine inaiita injili kama “uweza wa Mungu (POWER)” Warumi 1:16.
Unaona Injili inayolenga ukombozi wa msalaba, inayowafanya watu wautazame msalabani, watubu dhambi , wakapate msamaha na ondoleo la dhambi zao, hapo ndipo nguvu za Mungu zilipo..
Hakuna mahali popote biblia inasema nguvu za Mungu zipo katika mali, au biashara na majumba..Hayo hayawezi kumfanya mtu apate uzima wa milele…Sasa watu wa namna hii ndio watanyanyuka sana katikati ya kanisa la Mungu, ambao watakuwa wanajifanya ni wanatangaza habari za wokovu, kumbe wanahubiri mambo yao mengine, hawana habari na injili ya toba, wala hata haiwavutii, wala hawajali kwamba mtu wanayemchunga na kuchukua sadaka zake anaweza kufa leo na kwenda kuzimu kutokana na dhambi zake, hilo hawalijali wao wapo radhi kuwasisitizia tu mafanikio ya miili yao, lakini si roho zao.
Wengine wapo radhi, kuwakaririsha mapokeo ya dini zao, ili watu wawe tu wa kidini, wajue litrujia, wasome rozari, na sala zote za marehemu, lakini hao hao watu ukiwauliza je umeokoka, watakauambia mimi si mlokole, ukiwauliza, Je! Unajua kuwa kuna kitu kinachoitwa Unyakuo, watakauambia..sijui unazungumzia kitu gani!!..Sasa embu fikiria mtu wa namna hiyo mbinguni atakwendaje?..Lakini hayo yote ni kiongozi wake hajawahi kumwambia hayo mambo, ni kiongozi ambaye anao mfano wa utauwa lakini anazikana nguvu za Mungu..
Sasa Paulo aliwafananisha watu hawa na Yane na Yambre ambao walinyanyuka wakati wa Musa..Jinsi walivyokuwa wanapingana naye..
2Timotheo 3:8 “Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa Dhahiri”.
Sasa kama uwafahamu Yane na Yambre ni wakina nani…
Walikuwa ni wale wachawi wa Farao ambao Musa alipokuwa anafanya miujiza na wao walikuwa wanafanya ili tu kumpinga Musa.
Unaona? Jambo pekee ambalo lilikuwa linawatofautisha hawa wachawi wawili (Yane na Yambre) na Musa, halikuwa miujiza..hapana, hata wao kwa sehemu fulani walipewa kufanya miujiza, jambo pekee lililowatofautisha na Musa, ni UJUMBE waliobeba.. Musa alikuja na ishara lakini alikuwa na Ujumbe nyuma ya ishara zile..Nao ndio huu “Bwana asema hivi! Waache watu wangu huru,waende kunitumikia”..Lakini Yane na Yambre hawakuwa na ujumbe wowote isipokuwa kupinga tu, na kuwaburudisha na kuwatumainisha wamisri kwa miujiza yao,..Ni wana-mazingaombwe tu!..Mtu anayefanya mazingaumbwe siku zote hana ujumbe wowote kwa mazingaombwe yake, anafanya tu kuburudisha watu, na wala wakati mwingine anaweza asiongee kuanzia anaanza mazingaombwe yake mpaka anamaliza. Na wakina Yane walikuwa hivyo hivyo.
Musa alikuwa na ujumbe wa ukombozi, wa kuwatangazia watu uhuru watoke katika utumwa mgumu wa Farao, Ambao kwa sasa sisi tuliookolewa tunafananishwa na wana wa Israeli pale tunapomwamini Kristo, tunaokolewa kutoka katika utumwa wa dhambi wa Ibilisi.
Sasa ukiona, mtu anakujia na miujiza na ishara hizi au zile, lakini hana ujumbe wowote wa kukutoa Misri (kukutoa kwenye utumwa wa dhambi), Basi ujue kuwa unaongozwa na Yane na Yambre(wana mazingaombwe), watumishi wa shetani.. Haijalishi watashika biblia, haijilishi watakuombea upone kiasi gani, Yane na Yambre waliweza kuyafanya hayo yote, haijalishi watafanya miujiza mingi vipi, kama hawana ujumbe wa kukurudisha msalabani upate ukombozi wa roho yako, Ujue hao ni Yane na Yambre tu wanakuongoza…
Ndio hao sasa mtume Paulo anaowazungumzia kuwa “wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake”…..Hizi ndio nyakati zenyewe za hatari zinazozungumziwa hapo. Mahali popote unapoongozwa embu jipime nafsi yako, je tangu umekuwa hapo ni kitu gani kimeongezeka katika Maisha yako ya rohoni kwa ujumla, Je! Mahusiano yako na Mungu yameongezeka au yapo pale pale?, Kama sivyo basi ujue upo chini ya Yane na Yambre wa siku za mwisho.
Na kibaya Zaidi kama hujui, watu waliochangia kuufanya moyo wa Farao kuwa mgumu ni hawa wachawi wawili..Kama sio wao basi pengine Farao angeshatubu zamani..(Ingawa ni Mungu mwenyewe ndiye aliyeruhsu). Vivyo hivyo leo hutaki kumgeukia Kristo na kutaka kutubu dhambi zako na kutafuta utakatifu kwasababu tayari wapo akina Yane na Yambre wanaokupumbaza na miujiza, ukikumbushwa habari ya utakatifu na kwenda mbinguni, unasema nabii wetu/kiongozi wetu wa kidini mbona hajawahi kutufundisha hayo, na miujiza mbona inafanyika mingi tu..
Ndugu siku ukifa na kujikuta upo kuzimu, hutakuwa na la kujitetea, kwasababu biblia inatuambia..mtu akifa matendo yake yanafuatana naye (Ufunuo 14:13)..Haisema majumba yake, au magari yake, au bishara yake, au dhehebu lake, inasema matendo yake..Sasa kama nabii wako au mchungaji wako, anakutumaisha na mambo ya ulimwengu huu na wewe unaona raha, nataka nikuambie siku ile vyote pamoja na mali zako, pamoja na huyo kiongozi wako wa imani, aliyekuwa anakufundisha kujiwekea hazina duniani badala ya mbinguni, wote watakuaga pale makaburini, utakuwa umebakia wewe mwenyewe, utashangaa ni matendo yako tu yapo na wewe..hayo ndiyo yatakayoeleza hatma yako ni nini..
kwasababu biblia imeshatuonya jinsi ya kuendana na watu wa namna hii, hivyo ni wajibu wako wewe binafsi kutumia akili, kwa kuutafuta uhusiano wako binafsi na Mungu wako…Kuupima wokovu wako kama upo sawasawa au la, na kama haupo! Basi ndio ufanye bidii kumtafuta Kristo kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote, katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho, maadamu muda unao..
2Wakorintho 13:5 “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa”
Usisubiri ufe ndipo ujue kuwa ulikuwa kwenye njia isiyo sahihi, amka usingizi, anza kuyatengeneza Maisha yako.
Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza”.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo: