Unyenyekevu ni nini?

Unyenyekevu ni nini?

Biblia inasema nini kuhusu unyenyekevu?

Unyenyekevu ni ile hali ya “kujishusha” na kuwa tayari “kutumika kwa utumishi ule usiostahili kutumika” bila kiburi wala majivuno.

Biblia inasema Mungu huwapinga wote wenye kiburi na wajikuzao lakini “wanyenyekevu” anawapa Neema.

Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU HUWAPINGA WAJIKUZAO, bali huwapa neema wanyenyekevu”.

1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI, LAKINI HUWAPA WANYENYEKEVU NEEMA”.

Na tena kitabu cha Mithali kinasema…

Mithali 3:33 “Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.

34 Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.”

Na zaidi ya yote, Injili ya Bwana Yesu ni kwa wote walio wanyenyekevu..

Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta NIWAHUBIRI WANYENYEKEVU HABARI NJEMA; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.

Maana yake ni kwamba “watu wajikwezao” na “wenye kiburi”.. Hawawezi kuipokea Habari njema ya Yesu, Neema ya Wokovu inakuwa haipo juu yao.

Na pia Bwana Yesu alitufundisha ni kwa namna gani tutakuwa wa kwanza, katika ufalme wa Mbinguni.. alisema tukitaka kuwa wa kwanza, basi hatuna budi kujinyenyekeza na kuwa wadogo kuliko wote, maana yake tuwe watumwa na watumishi kwa wengine.. tofauti na hekima ya dunia inavyosema au kufundisha kuwa mtu mkubwa ni Yule anayetumikiwa na mwenye kiburi.

Marko 10.42 “Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu,

44 na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.

45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

Hivyo biblia inatufundisha kuwa wanyenyekevu siku zote, yaani kuwa “wadogo”, sehemu nyingine Bwana Yesu anasema tunapaswa tujinyenyekeze na kuwa kama vitoto.

Mathayo 18:3 “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

4 Basi, YE YOTE AJINYENYEKESHAYE mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni”.

Unaweza kusoma pia, Mathayo 11:11, Waefeso 5:21, Zaburi 138:6, Mithali 11:2, na Mithali 18:12.

Hivyo na sisi hatuna budi kuwa wanyenyekevu siku zote, ili tukwezwe na tupate NEEMA zaidi, na sio tu kuwa wanyenyekevu kwa Mungu, bali pia kwa watu wengine wote, ikiwemo wazazi, wafanyakazi wenzetu na maboss zetu na kwa wenye mamlaka pia (Tito3:1).

Lakini tukiwa ni watu wa kiburi, au tukijiinua basi tutashushwa chini kama maandiko yanavyosema..

Luka 14:11 “Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Neema ni nini?

SALA YA ASUBUHI

ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Bwana Yesu amejulikana kwa majina mengi tofauti tofauti katika biblia, kuna sehemu katajwa kama Mwanakondoo (Yohana 1:29), sehemu nyingine kama nyota ya asubuhi, sehemu nyingine kama Mzao wa Daudi (ufunuo 22:16), sehemu nyingine kama Imanueli, sehemu nyingine kama Simba wa Yuda n.k.

Leo tutaangalia ni kwanini amejulikana kama Simba wa Yuda.

Bwana Yesu kama Simba wa Yuda ametajwa mara moja tu Katika biblia yote!. Na ametajwa hivyo ndani ya kitabu cha ufunuo.

Ufunuo wa Yohana 5:5 “Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba”.

Sasa ili tuelewe kwanini ni Simba?.

Hebu turudi tujikumbushe baraka za ambazo Yakobo aliwabarikia watoto wake wale 12.

Utaona kila mtoto alipewa maneno ya kinabii kwake yeye binafsi, na uzao wake wote utakaofuata baada yake..tunaweza kusoma baraka hizo katika kitabu cha Mwanzo 49.

Mwanzo 49:1 “Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.

2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,
Msikilizeni Israeli, baba yenu.

Sasa turuke mpaka mstari wa 8, tuone unabii wa Yuda mwana wa nne wa Yakobo..

8 Yuda, ndugu zako watakusifu,
Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.

9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?

10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.

Umeona hapo mstari wa 9 unasema “Yuda ni mwana Simba”..na tena anasema katika mstari wa 10… “Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda”.

Ikiwa na maana kuwa kuna mmoja atakayezaliwa katikati ya kabila la Yuda, ambaye atatawala kama Simba, na tena atakwa ni Mfalme. Na huyo si mwingine zaidi ya Bwana Yesu. Yakobo alimwona Bwana Yesu miaka mingi kabla ya kuja kwake ndani ya uzao wa mwanae Yuda, kama vile Balaamu alivyomwona Yesu ndani ya kusanyiko la Israeli..

Hesabu 24:17 “Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.

18 Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.

19 Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini”.

Ndio maana kwenye Ufunuo hapo anakuja kutajwa kama Simba wa kabila la Yuda.

Sasa kwanini awe simba na Dubu au Chui?

Ni kwasababu Simba ni jasiri, haogopi, tena ana nguvu na tena anajulikana kama Mfalme wa pori.

Na Bwana Yesu, maandiko yanasema atakuja kuitawala dunia kwa fimbo ya chuma,  hivyo kama vile simba alivyo mfalme wa pori, kadhalika na Bwana Yesu atakuja kutawala kama Simba baada ya unyakuo wa kanisa kupita.

Je umemwamini Yesu leo?.. Leo kaja kwetu kama Mwana-kondoo, mpole aendae machinjoni, tukikosa kwake tunaomba rehema na anatusamehewa kwasababu neema bado ipo.

Utafika wakati baada ya unyakuo wa kanisa kupita, kutakuwa hakuna tena rehema, huyu Yesu anayetuita sasa kwa sauti ya upole atageuka na kuwa Simba angurumaye..atawararua waovu wote katika ghadhabu ya Mungu mwenyezi, na katika vita vya Harmagedon na kuwatupa waovu wote katika ziwa la moto, mahali ambapo hakuna msamaha. Maandiko yanasema atakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya Mungu mwenyezi..

Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana”.

Na unyakuo wa kanisa ni siku yoyote kuanzia sasa hivi. Mlango wa rehema utakuwa umefungwa.

Swali ni je!, umempokea Yesu? na kuishi maisha ya utakatifu?.

Kama bado hujampokea, basi ni vyema ukafanya hivyo sasahivi, kabla nyakati hizo za hatari hazijafika.. tubu sasa na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina lake Yesu, upate ondoleo la dhambi (Matendo 2:38). Na Bwana atakurehemu na kukupa uzima wa milele.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)

Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda?

 Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?

TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Rudi nyumbani

Print this post

Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

Aina za Uongozi

Uongozi umegawanyika katika aina kuu tatu. 1) Uongozi wa Madhabahuni, 2) Uongozi wa kiserikali na 3) Uongozi wa kijamii.

          1. Uongozi wa Madhabahuni

Uongozi wa madhabahuni, ndio uongozi wa ngazi ya juu kuliko mwingine wowote ule. Uongozi huu ndio unahusisha Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu, mitume na Manabii. Watu hawa ndio Mungu kawachagua katika kulingoza kanisa lake (Waefeso 4:11), na katika uongozi wa kanisa, ni wanaume tu ndio waliopewa hiyo dhamana.. Maana yake, biblia haijaruhusu wanawake, kuwa wachungaji wala waalimu.

1Timotheo 2:11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye”.

               2. Uongozi wa Kiserikali.

Uongozi wa kiserikali ndio unahusisha, viongozi wote wa kimamlaka.. mfano, Raisi, Mawazili, wabunge, madiwani, wakuu wa mikoa, mameya, wenyekiti wa mitaa, na hata wajumbe.

Hawa maandiko yanasema pia ni watumishi wa Mungu, lakini katika utumishi wa mambo ya kimwili.

Warumi 13:1 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu”.

Na Mkristo yeyote Yule anaweza kushika mojawapo ya hizi nafasi, lakini Haiwezekani kutumika katika nafasi ya Uongozi wa madhabahuni na uongozi wa kiserikalini kwa wakati mmoja.. Haiwezekani kuwa Mchungaji na hapo hapo kuwa Raisi au mbunge.

Majukumu ya kiongozi wa Serikali kibiblia ni yapi?

  1. Kuwa Mwaminifu kwa Mungu aliyeruhusu uishike hiyo nafasi.

 mfano wa akina Shedraki, Meshaki na Abednego.. Ambao walikuwa ni mawaziri wa Mfalme Nebukadneza, siku walipoambiwa waisujudie sanamu ya Nebukadneza, walimheshimu Mungu zaidi ya mwanadamu, na hivyo Mungu akawaokoa na lile tanuru la Moto.

  1. Kuwa Mwaminifu kwa aliyekupa dhamana ya uongozi.

Kama umepewa dhamana hiyo na wananchi, basi kuwa mwaminifu kwao kwa kutekeleza yote uliyowaahidi kwa wakati, na kama umepewa dhamana hiyo kwa kuteuliwa na kiongozi aliye juu yako, basi kuwa mwaminifu katika hiyo nafasi kwa kutenda yale yote uliyoteuliwa kuyafanya, kwa uaminifu wote na utakatifu.. Mfano wa Danieli.

Danieli aliwekwa kuwa kama Waziri mkuu katika ufalme wa Uajemi, lakini siku zote alikuwa mwaminifu kwa mfalme, na wala hakuwahi kula rushwa kama maliwali wengine.

Danieli 6:1 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;

2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danielii alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.

3 Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.

4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.

         3. Uongozi wa kijamii

Mfano wa uongozi wa kijamii ni ule wa kifamilia, au kikabila.. Baba anaweza kuwa kiongozi wa familia, kadhalika mtu fulani anaweza kuwa kiongozi wa kabila fulani, mwanafunzi anaweza kuwa kiongozi wa wanafunzi wenzake (yaani kiranja) n.k

Majukumu ya kiongozi wa aina hii yanafanana na hayo ya uongozi wa kiserikali. Maana yake unahitaji UAMINIFU, kwa aliyekupa hiyo dhamana.

Hayo ndio mambo muhimu katika uongozi ya kuzingatia. Kumbuka tena jambo hili, siku zote “Uongozi ni dhamana”. Hivyo ukitaka ufanikiwe katika uongozi wa aina yeyote ile basi huna budi kuwa mwaminifu kwa aliyekupa hiyo dhamana, iwe ni Utumishi wa madhabahuni au wa kiserikali au kijamii, UAMINIFU NDIO SILAHA.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

YESU NI MFALME WA AINA GANI KWAKO? 

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

Konzi ni nini?(Mhubiri 4:6)

Rudi nyumbani

Print this post

Binadamu wa kwanza aliishi miaka mingapi?

Binadamu wa kwanza alikuwa ni “Adamu” na maandiko yanasema aliishi miaka 930.

Mwanzo 5:5 “ Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.

Adamu, hakuwa mtu aliyeishi miaka mingi kuliko wote. Maandiko yanarekodi kuwa Methusela ndiye aliyeishi miaka mingi zaidi, miaka 969 (Mwanzo 5:27).

Na mtu wa kwanza kuishi duniani, hakuwa “Nyani” kama Sayansi inavyosema, bali mtu wa kwanza alikuwa ni Adamu, ambaye aliumbwa na Mungu, na baadaye Hawa, na baada ya hapo, ndipo vizazi vya wanadamu vikatokea kupitia Adamu na Hawa.

Kwahiyo binadamu wa kwanza aliishi miaka mingapi?..Jibu: Aliishi miaka 930, na tangu Adamu mpaka sasa hivi karne hii ya 21, ni tofauti ya miaka takribani elfu sita (6,000), ambayo imegawanyika katika vipindi vitatu.

Kipindi cha kwanza ambacho kwa madirio ni miaka elfu mbili, ni tangu Adamu aumbwe mpaka Gharika ya Nuhu, na baada ya Gharika ya Nuhu mpaka kipindi cha kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni tofauti ya miaka mingine elfu mbili, na baada ya Bwana Yesu mapaka sasa ni miaka zaidi ya Elfu mbili mingine, hivyo Jumla ya miaka tangu Adamu mpaka sasa katika karne hii ya 21, ni miaka takribani elfu 6 na miaka kadhaa.

Lakini yote katika yote, Adamu mtu wa kwanza alikufa, ila yupo mwingine ambaye anajulikana kama Adamu wa pili, ambaye anadumu milele, alikufa akafufuka na sasa anaishi, na hafi tena, na huyo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo.

Huyo ndiye wa kumtegemea katika wakati huu wa sasa, kwasababu mamlaka yote ya mbinguni na duniani kakabidhiwa yeye, baada ya Adamu kuyapoteza pale Edeni.

Hivyo kila mtu amwaminiye Yesu, anapata ondoleo la dhambi, na ahadi ya uzima wa milele, na asiyemwamini atahukumiwa.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:

Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Rudi nyumbani

Print this post

JE NI LAANA KULELEWA NA BABA AU MAMA WA KAMBO?

Shalom, Jina la Bwana wetu, Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu.

Katika ulimwengu wa sasa, ukitaja mama wa kambo, au baba wa kambo, tayari picha ya kwanza inayotengenezeka kwenye vichwa vya wengi ni MATESO.

Lakini leo napenda tujifunze kitu kingine tofauti na hicho, ili tusije tukajikuta tunazuia baraka zetu pasipo sisi kujua.

Jambo la kwanza la kufahamu kabla hatujaingia kwenye kiini cha somo ni kwamba, popote pale unapojikuta upo, au umezaliwa, na kulelewa..jua Mungu kakuweka hapo kwa kusudi maalumu, ambalo ni la baraka.

Sasa turudi kwenye swali letu!. Je! Ni laana au mkosi, kuzaliwa au kulelewa na mama wa kambo au baba wa kambo?.

Tutalijibu swali hili, kwa kujifunza juu ya maisha mmoja katika biblia, na huyo si mwingine zaidi ya Bwana Yesu, Mkuu wa uzima..

Maandiko yanasema “tujifunze kwake”..Maana yake tumtazame yeye, tuyaangalie maisha yake, na tupate masomo (Mathayo 11:29).

Na leo tutapata somo lingine kutoka katika maisha yake.

Sasa wengi wetu hatujui kuwa Bwana wetu Yesu, alilelewa na Baba wa kambo katika mwili (Ni lugha ngumu kidogo hii, lakini ndivyo ilivyo).

Yusufu hakuwa Baba kamili wa Bwana Yesu. Mimba aliyoipata Mariamu haikumhusisha baba, ilikuwa ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu (soma Mathayo 1:18).

Baba wa Bwana Yesu, alikuwa ni Roho Mtakatifu.

Hivyo ni sahihi kabisa kusema, Yusufu alikuwa ni baba wa kambo wa Bwana Yesu.

Lakini ulishawahi kujiuliza ni kwanini Mungu aruhusu aishi na baba wa kambo?, kwani alishindwa kumfungulia Mariamu mlango, aishi mwenyewe tu na mtoto Yesu?.. Mungu angeweza kufanya hivyo, kwani yeye ni mweza wa kila kitu.

Angeweza kufungua mlango wa mali nyingi, kipindi Bwana Yesu anazaliwa na kumfanya Mariamu aishi maisha ya kifahari peke yake na mtoto Yesu, na pia angeweza kuzuia Yusufu asipose Mariamu kabisa..

Lakini hakufanya hivyo bali kinyume chake, baada tu ya Mariamu kuposwa ndipo mimba inaonekana..Na baada ya Yesu kuzaliwa, akaanza kubebwa na baba huyo huyo wa kambo, na hata wakati wa kazi ya ufundi, alifanya kazi ya baba huyo huyo wa kambo!.

Bwana aliruhusu maisha yake yawe hayo, ili kutufundisha na sisi kuwa si laana kuishi hayo maisha.

Sasa kulikuwa kuna nini kwa Yusufu, mpaka mkuu wa Uzima, Yesu Kristo apitie pale?

Yusufu alikuwa ni maskini kweli, hakuwa tajiri, lakini alikuwa amebeba ahadi ya kifalme, kumbuka Mungu alimwahidi Daudi, kwamba kupitia uzao wake atatokea Mfalme. Na Yusufu alikuwa ni wa Uzao wa Daudi.

Hivyo ili Bwana Yesu awe mfalme kupitia ahadi hiyo ya Daudi, ilikuwa hana budi azaliwe katika Hema ya Yusufu..angezaliwa pengine popote, ahadi hiyo ya Mungu isingetimia.

Mpaka hapo utakuwa umeanza kuona hata wewe ni kwasababu gani… umelelewa na huyo baba wa kambo Au mama wa kambo.

Haijalishi anakutesa kiasi gani, au ni maskini kiasi gani, lipo kusudi kwanini upo hapo, au umelelewa hapo, kuna baraka ambazo huwezi kuziona kwa macho!..

Kuzaliwa kwa Bwana kwenye lile zizi, chini ya Bwana Yusufu asiyekuwa na kitu, kulikuwa na maana kubwa.

Na wewe vile vile..tengeneza mambo yako vizuri sasahivi kwasaababu kuna baraka tele, mbele yako.

Ishi na Baba yako huyo vizuri, mheshimu, mbariki kwasababu ni Mungu ndiye aliyekuweka hapo, hujajiweka mwenyewe..na Mungu ndiye anayeijua mbele yetu..

Usianze kuharibu mambo kwa kunung’unika, unapopitia vikasoro vidogo vidogo, wewe tazama mbele, ongeza utii na heshima.

Kadhalika na kama wewe ni baba au ni mama na una watoto wa kambo, ishi nao vizuri, kwasababu nao pia wamebeba ahadi, ahadi hiyo isingeweza kukamilika pasipo wewe. Na mwisho utaona faida kubwa mbeleni.

Utasema vipi na mama wa kambo?

Musa alilelewa na Mama wa kambo, Binti Farao, hakujua atakuja kuwa nani..lakini maandiko yanasema, baadaye Mungu alikuja kumfanya Musa kuwa kama “mungu kwa Farao”.

Kutoka 7:1 “BWANA akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako”.

Alienda kwa binti Farao, ili kupata jina hilo MUSA, Jina hilo alipewa na “mama wa Kambo”…hakupewa na mama yake mzazi, wala halikuwa jina la kiyahudi..

Na cha ajabu ni kwamba, Mungu hakumbadilisha jina Musa…aliendelea nalo hilo hilo, Sauli alibadilishwa na kuwa Paulo, Yakobo alibadilishwa na kuwa Israeli, lakini Musa amebakia kuwa Musa mpaka leo…kumbe wito wake ulikamilishwa pia na mama wa kambo.

Hivyo tunachoweza kujifunza ni kuwa macho ya kiroho kuona mbele na si hapa tu..katika nafasi uliyopo kama unaishi na baba au mama wa kambo, mheshimu kama Baba yako na kama mama yako, unapoona shetani ananyayuka na kujaribu kuharibu uhusiano wenu.. basi ni wakati wa wewe nyanyuka na kuongeza maombi…usiende kusikiliza simulizi za kishetani zinazosimuliwa huko na huko katika mitandao na katika vijiwe kuhusu ubaya wamama au wababa wa kambo, utajizolea elimu zitakazoharibu maisha yako..Biblia ndio kitabu chetu na mwongozo wetu.

Kama Bwana Yesu aliishi na Baba wa kambo, na kufanya naye kazi moja na bado akawa mfalme, ni kitu gani kitakachokuzuia wewe kufikia baraka zako, kupitia huyo mzazi au mlezi ambaye si wako?.

Kadhalika na kama wewe ni mzazi, au mlezi wa mtoto ambaye si wako, usimkatae mtoto wa kambo, kwasababu hujui ana ahadi gani kupitia wewe.. Na Mungu amekuchagua wewe, kwasababu na wewe pia unabaraka juu yake.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba hakuna laana yoyote kuishi au kulelewa na Baba au mama wa kambo. Vile vile hakuna laana yoyote au mkosi, kulea mtoto wa kambo.

Bwana akubariki.

Ikiwa bado hujamwamini Bwana Yesu, ni vyema ukakata shauri sasa kwasababu siku tunazoishi hizi ni siku za mwisho.

Na Bwana Yesu alisema.. “Itatufaidia nini tupate ulimwengu mzima halafu tupate hasara ya nafsi zetu”

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Rudi nyumbani

Print this post

MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;

Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo, Mfalme wetu, Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Utakumbuka huduma ya Bwana wetu iligawanyika katika sehemu kuu tatu,

Ya kwanza, ilikuwa ni hapa duniani,

Ya pili ni Kuzimu

Na ya tatu ni mbinguni.

Lakini wengi wetu tunafahamu ile ya duniani na mbinguni, Lakini kwa sehemu ndogo sana tunaielewa ile ya kuzimu. Ni vema pia tukaifahamu hiyo ili tujue ni nini tutakutana nacho baada ya kifo.

Siku tukiifahamu kwa mapana, hatutaacha kumshukuru Bwana Yesu kwa kifo chake pale msalabani.

Kama tunavyosoma siku ile Bwana aliyokufa, kuna matukio kadha wa kadha yaliyotokea, mojawapo ni lile la pazia la hekalu kupasuka, lakini tukio lingine ambalo lilitokea la kustaajabisha sana, ni lile la kuonekana  kwa watu ulimwenguni ambao walikuwa tayari wameshakufa zamani. Na watu hao walikuwa ni watakatifu wa zamani.

Biblia inatuonyesha baada ya kufufuka kwao walianza kutembea tembea na kuingia mpaka mji mtakatifu  wa Mungu (Yerusalemu.)

Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.

51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;

52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;

53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.

Sasa swali unaweza kujiuliza ni kwanini uwe ni wakati ule na si mwingine, kwanini waonekane wanatoka makaburini, na kutembea tembea duniani, huku wakiwatokea watu? Kwanini iwe hivyo? Na hao watu sasahivi wapo wapi?

Hii ni kutuonyesha kuwa zamani mtu alipokufa, hakuwa huru hata kidogo, alikuwa anakwenda   moja kwa moja kaburini haijalishi ni mtakatifu au mwovu. Huko kaburini ndio sasa kuliganyika katika  sehemu ya waovu na wema.

Na kama tunavyojua sikuzote kaburi ni kama gereza, huwezi kwenda popote, au kufanya lolote, ndivyo ilivyokuwa kwa watu wote waliokuwa wanakufa zamani, walikuwa sehemu fulani tu, wamekaa wanasubiria siku moja masihi aje awaondoe huko.  (Waebrania 2:14-15)

Lakini Bwana Yesu alipokuja, alifanya kazi ya kuyapasua makaburi hayo yaliyokuwa yamewashikilia kwa nguvu ya dhambi kwa muda mrefu . Lakini biblia inatuonyesha hakupasua makaburi ya wote, bali ya wale watakatifu tu. Na matokeo yake  wakatoka huko, wakawa huru kama vile wanaishi tena duniani, na ndio maana wakawatokea wengi, wakatembea tembea huu na huko mpaka mji mtakatifu (Yerusalemu) n.k. kuonyesha ni jinsi gani wafu waliokufa katika Kristo walivyo huru, rohoni.

Hiyo ni kufunua kuwa, mtakatifu yeyote anayekufa leo, haendi tena kaburini kama watu wanavyodhani..ataliona tu kaburi kwa pale pembeni, lakini yeye hatakwenda huko kabisa bali ataondoka na kwenda kuendelea kuishi sehemu nyingine fulani iliyo nzuri sana, ijulikanayo kama Paradiso (peponi) Luka 23:43. Huko atakuwepo na Bwana Yesu mwenyewe, na watakatifu wengine, watakuwa ni kama tu vile hawajawahi kufa, wanaishi kama tunavyoishi hapa, isipokuwa tu huko ni kuzuri sana.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya,

Yohana 11:25b….Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

Yapo maisha baada ya kufa kwa mtakatifu.. , hawi kifungoni, anakuwa huru kule PEPONI (Paradiso), akimfurahia Kristo, huku akingojea siku ya Unyakuo ifike, aje kuuchukua mwili wake, aende mbinguni.

Lakini mtu anayekufa katika dhambi, ni moja kwa moja kaburini, kifungoni, kwenye giza nene, ndio kuzimu kwenyewe, maisha yake yanagotea pale anapokufa, hayawezi kuendelea kuishi, sio kwamba roho yake itakufa, hapana, bali ni kwamba hawezi kuwa na maisha, kama sisi tuliyonayo, au wale wale wengine waliyonayo.

Biblia inasema hivi, juu ya Bwana Yesu alipokwenda kuzimu;

1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;

20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.

Unaona watu wote wenye dhambi sasa wapo huko vifungoni, kwa maelezo marefu juu ya habari hiyo, tutumie ujumbe inbox tukutumie somo lake..

Lakini utajisikiaje wewe uliye dhambini, ukifa leo katika hali hiyo? Siku hiyo utatamani upate hata nuru kidogo hutaona, utatamani, utembee tembee huku na huko  kama wale wengine hutaweza, utatamani ule au unywe hutaweza, utakuwa katika jehanamu ya mateso daima, ukiteseka, kama Yule tajiri wa Lazaro, ambaye aliomba hata achovyewe maji kidogo kwenye ncha ya kidole cha Lazaro,akashindwa,(Luka 16:19-31) utakaa huku  huku ukingojea na wewe siku ile ya hukumu ifike, ufufuliwe, uhukumiwe kisha utupwe kwenye lile ziwa la moto milele na milele.

Ndugu, kumbuka kifo hakina hodi, vilevile Unyakuo pia hauna hodi, ni siku yoyote au wakati wowote, unaondoka hapa duniani, au Yesu anarudi, inasikitisha kusoma katika biblia kwamba “kuzimu hakishibi watu”. Ikiwa na maana Maelfu kwa maelfu wa watu wanaenda huko kila siku.

Tutawezaje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii. Aliyeshinda kaburi na mauti kwa ajili yetu, yupo hata sasa kutuokoa, Embu tufungue mioyo yetu, atupe wokovu huu bure. Atusamehe makosa yetu yote. Hata siku tukifa tuwe na uhakika kuwa kaburi sio sehemu yetu.

Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha uwe tayari kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kuukamilisha wokovu wako, Na Bwana atakupokea.

Ikiwa utahitaji msaada wa kumpokea Yesu, basi unaweza kuwasiliana nasi pia kwa namba hizi. +255693036618 / +255789001312

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

UNYAKUO.

Rudi nyumbani

Print this post

Bwana Yesu alikuwa kabila gani?

Je! Bwana Yesu alikuwa kabila gani, miongoni mwa kabila 12 za Israeli?.


Jinsi biblia inavyotafsiri makabila ni tofauti na ulimwengu sasa unavyotafsiri.

Kibiblia Kabila ni jamii ya watu wanaotoka katika mzizi wa familia moja, maana yake asili ya kizazi chao ni baba mmoja.

Kwamfano katika biblia tunaona Taifa moja la Israeli likiwa na kabila 12.

Lakini makabila hayo yote, asili yao ni mtu mmoja anayeitwa Yakobo, ambaye ndio lake Israeli. Huyu Israeli alioa wake wanne na kuzaa watoto 12.. hivyo majina ya hao watoto 12, ndio yakawa makabila 12.

Hivyo mwisraeli yoyote, ni lazima awe miongoni mwa hayo makabila 12.

Sasa tukirudi kwenye swali, Bwana Yesu alikuwa kabila gani?.

Jibu ni kwamba Bwana Yesu hakuwa miongoni mwa kabila za Israeli, kwasababu yeye hakuzaliwa na Baba wa kimwili.

Mimba aliyoipata Mariamu, ilikuwa ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu (Luka 1:35).

Hivyo Bwana hakuwa miongoni mwa kabila la Israeli, bali alikuwa ni uzao wa kimbinguni.

Lakini sasa, Yusufu ambaye ndiye aliyemposa Mariamu..(ambaye ndiye kama baba aliyekuwa mlezi wa Bwana Yesu katika utoto).

ndiye aliyekuwa wa kabila la YUDA. Hivyo kupitia yeye, ili ahadi ya Mungu ya kumketisha mmoja katika kiti chake cha enzi itimie..ndipo akampitisha Mfalme Yesu, katika mnyororo huo wa kabila hilo la Daudi, yaani Yuda.

Lakini Bwana yenyewe hakuwa wa kabila la Yuda.Bali kwasababu ya Yusufu, ndio akaitwa wa kabila la Yuda.

Ufunuo wa Yohana 5:5 “Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba”.

Huyo ni Yesu, anayezungumziwa hapo?.

Swali ni je! Umemwamini na kumpokea maishani mwako?..kama bado unasubiri nini?..

Hakuna wokovu kwa mwingine yeyote, isipokuwa kwa Yesu, mwamini leo na kisha tubu dhambi zako zote kwake, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu, upate ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:38).

Na Roho Mtakatifu atayabadilisha maisha yako, na kukuongoza.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda?

FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?

 Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?

Rudi nyumbani

Print this post

Je Bwana Yesu alioa mke?

Je Bwana Yesu alioa mke au kuwa na mahusiano na mwanamke yeyote?


Jibu: Bwana Yesu hakuoa wala kujihusisha na mahusano yoyote na mtu yeyote yule.
Alizaliwa na kuishi bila kuoa ili ayatende mapenzi ya Baba yake. Na zaidi ya yote hakuwahi kutenda dhambi hata moja, ikiwamo ya kutamani.

Yohana 8:46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”

Ipo mitazamo inayosema kuwa Bwana Yesu alikuwa katika mahusiano na Mariamu, Magdalena.

Mitazamo hiyo imetengenezwa na adui, ili kuwapotosha watu, na kuwafanya watu wamwone Bwana Yesu kama alikuwa mtu wa kawaida tu kama watu wengine. Hiyo imekuwa ni kawaida ya shetani siku zote, kujaribu kushusha vitu vya kiMungu hadhi, ili visivutie.

Lakini haisadii kwasababu kuna Roho Mtakatifu, ndiye anayeishawiahi mioyo, na si ushawishi wa maneno..Hivyo iwe kwa husuda au kwa haki, Kristo atahubiriwa na ataaminiwa tu, hakuna kitakachoweza kuzuia hilo..

Wafilipi 1:18 “Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi”.

Watu waliokusudiwa kumwamini mwokozi, watamwamini tu, na wote watakaomwamini, shetani hawezi kuwanyakua kutoka mikononi mwake.
Utukufu una yeye, Mkuu wa Uzima, Yesu Kristo, milele na milele.

washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)

KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?

Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?

WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

Rudi nyumbani

Print this post

Kuota mbwa kunamaanisha nini?

Mbwa ni mnyama anayeweza kuwakilisha vitu vitatu:

1) Mlinzi

2) Adui

3)Kitu najisi/Mchafu.

Inategemea hiyo ndoto imekuja katika mazingira gani..na pia kama imekuja katika mazingira ya kujirudia rudia au katika hali ya uzito wa kitofauti basi haipaswi kupuuzwa, inayo maana rohoni.

  1. Tukianzana namaana ya kwanza kama mlinzi:

Kama tunavyojua mbwa ni mlinzi. Na katika biblia watumishi wa Mungu pia wanafananishwa na mbwa walinzi.

 Vilevile watumishi  ambao hawasimami katika  nafasi zao kikamilifu za kuwalinda kondoo wa Mungu  wanafanishwa na mbwa walinzi wasioweza kubweka wala kung’ata.

Isaya 56:9-11

[9]Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni.
[10]Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.[11]Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.

Kwahiyo unapoota..mbwa mara kwa mara..pengine amesimama getini tu..au anafukuza kitu  au anafanya kitu fulani kwa ujasiri lakini hana shida na wewe.. hana mpango wa kukudhuru wewe..basi ni Mungu anakukumbusha kuwa uzidi kusisima vema katika nafasi yako kama mlinzi.

Lakini kama unaona mbwa huyo ni mwoga..anakimbizwa kimbizwa tu..anajificha ficha ujue huna nguvu rohoni..hivyo tengeneza mambo yako na Mungu ikiwa wewe ni mtumishi wa Mungu. Kwasababu Mungu anakuona kama mlinzi lakini bado hujakamilika katika kazi yako.

2) Maana ya pili ni kama Adui.

Kibiblia mbwa pia anawakilisha Adui.
Zaburi 22:16

“[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu”.

Zaburi 22:20 “Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa”.

Ukiota unakimbizwa na mbwa..au unashambuliwa nao. Au wanakutisha.au wanakuvizia kuchukua kitu chako..Ujue kuwa upo katika vita rohoni.
Ibilisi anataka kuiba kilicho chako.au kukuangamiza kabisa.. Hapo kama umeokoka huna budi kuwa mwombaji sana..mwambie Bwana akulinde na kukuhifadhli mbali na mashbulizi yote ya adui..pia zidisha kiwango chako cha kumtumikia Bwana ni ulinzi mkubwa sana.

Wafilipi 3:2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.
Lakini kama hujaokoka..fanya hima mapema sana umrudie Mungu wako. Vinginevyo upo hatarini kuangamia kabisa.

3) Maana ya tatu ni kitu najisi.

Kibiblia mbwa pia anawakilisha kitu najisi” au kichafu .Mbwa huwa hajali ni nini anakula anaweza rudia hata matapishi yake biblia inasema hivyo katika.. Mithali 26:11..

Ni wanyama wasiostahili heshima yoyote..

Mathayo 15:26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

Mbwa hajali ni yupi anakutana naye katika kupata watoto..anaweza kutanana hata na mama yake.
Hivyo kwa ujumla ni kwamba mbwa anawakilisha pia watu waovu..waliodhambini ambao hawajali maisha yao ya kiroho hata kidogo.

Kwahiyo kama unaota mara kwa mara mbwa ambao huelewi wapo kwa lengo gani..leo unamwona hivi kesho vile…ujue kuwa ndivyo Mungu akuonavyo.

Tubu dhambi zako mgeukie Mungu wako kama wewe ni mwenye dhambi..kumbuka katika hali kama hiyo uliyopo sasa ukifa ujue ni moja kwa moja kuzimu..biblia inasema hivyo kwa watu walio hivyo rohoni..

Ufunuo 22:15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Ikiwa upo tayari leo kumkaribisha Kristo ndani ya maisha yako akubadilishe basi fungua hapa kwa ajili ya kupokea mwongozo wa sala ya Toba..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?

Je! Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?.

Jibu: Kulingana na maandiko mtu wa kwanza kufa alikuwa ni HABILI, mwana wa ADAMU.

Mwanzo 4:8 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani].

Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua”.

Sababu ya Kaini kumuua Habili ndugu yake ilikuwa ni wivu. Kwani sadaka yake haikukubaliwa na Mungu lakini ya ndugu yake Mungu aliikubali kwasababu aliitoa katika vitu vilivyonona..na kutoka kwa wazaliwa wa kwanza.

Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.

4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;

5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde”.

Roho ya Habili, ipo peponi sasa, yaani paradiso sehemu ya watakatifu..akingoja ufufuo wa watakatifu, utakaotokea katika siku za mwisho, wakati parapanda ya mwisho itakapolia.

Na pia tunajifunza  tusiwe watu wasiomjali Bwana, kimatoleo kama Kaini, yeye alitoa tu ilimradi…lakini mwenzake alitoa katika vitu vilivyonona na katika wazao wa kwanza, pia tusiwe watu, wenye wivu kama Kaini.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.

MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

USIRUHUSU MUNGU AWEKE UADUI KATI YAKO NA WATU WAKO.

Rudi nyumbani

Print this post