Title June 2021

Nini maana ya “Bwana Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa?”(Ufunuo 1:5)

 Bwana Yesu sio tu mzaliwa wa kwanza wa waliokufa bali pia ni mzaliwa wa kwanza wa wanadamu wote walio hai.

Kwanini ni mzaliwa wa kwanza wa walio hai pia?.

Ni Kwasababu wote walio hai, hawana budi kuzaliwa tena mara ya pili ili wahesabike kuwa wana wa Mungu (Yohana 3:6). Ndio maana Bwana Yesu anabaki kuwa mzaliwa wa kwanza wa wanadamu wote..kwasababu ni yeye pekee tu ndiye aliyezaliwa mkamilifu, hana haja ya kuzaliwa mara ya pili, lakini sisi wengine wote hatuna budi kuzaliwa mara ya pili…

Warumi 8:29  “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ILI YEYE AWE MZALIWA WA KWANZA MIONGONI MWA NDUGU WENGI”.

Na ni kwanini yeye pia ni Mzaliwa wa kwanza wa waliokufa!.

Kabla ya kujua ni kwanini yeye ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, ni vyema tukajua kwa kina maana ya kuzaliwa.. Kuzaliwa ni kitendo cha kutoka katika upeo mmoja kuingia katika upeo mwingine..Tunapozaliwa hapa ulimwenguni, ni kwamba tumetoka katika upeo mwingine tusioujua sana ulio juu, na kuja katika huu ulimwengu.. hapo tunasema tumezaliwa.. Kadhalika mtu anayetoka katika upeo mwingine ulio chini na kuja katika huu ulimwenguni, naye pia huyu kazaliwa!, kwasababu hakuwepo katika ulimwengu lakini sasa yupo!..kuzaliwa huko ndio tunakuita kufufuka!

Hivyo baada ya Kristo kufa, yeye pekee ndiye mtu wa kwanza kufufuka!. (kuzaliwa kutoka katika wafu)

Sasa utauliza kama yeye ni wa kwanza vipi wale watu waliofufuliwa na nabii Elisha kabla yake, na Eliya, au vipi kuhusu Lazaro ambaye Bwana mwenyewe alimfufua!..

Kumbuka hao wote ni kweli walifufuliwa lakini baadaye walikuja kufa tena!.. Lazaro ni kweli alifufuliwa lakini alikuja kufa tena!..na wengine wote ni hivyo hivyo.. Lakini Bwana Yesu alipofufuka hakufa tena, yupo hai milele na milele..Na baada yake yeye ndio wafu wote wanafuata kufufuliwa, ili wasife tena.. ambapo yeye  anabaki kuwa mzaliwa wa kwanza kutoka katika mauti..

Ndio maana biblia inasema..

Wakolosai 1:17 “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

18  Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, NI MZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.

19  Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;

20  na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni”.

Na tena inasema..

Yohana 1:5  “tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, MZALIWA WA KWANZA WA WALIOKUFA, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake”

Pia unaweza kusoma Waebrania 1:5, 1Wakorintho 15:20, na Wakolosai 1:15.. Inaelezea zaidi juu ya Kristo kama mzaliwa wa kwanza waliokufa.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Kristo ndiye Mzaliwa wa kwanza wa kila kitu.(Ni mwanzo na Mwisho) Na mzaliwa wa kwanza siku zote ndiye mrithi!..sisi wengine tuliozaliwa mara ya pili katika roho ni kama wadogo zake. (Yeye ndio wa kwanza, sisi tunafuata) .Hivyo na sisi tunapozaliwa mara ya pili, tunazirithi ahadi za Mungu pamoja na Kristo..

Lakini kama hatutazaliwa mara ya pili, hatutaweza kuwa warithi..

Sasa tunazaliwaje mara ya pili?

Tunazaliwa mara ya pili, kwa kumwamini Yesu kama mzaliwa wa kwanza wa vitu vyote, na kwamba yeye ndiye aliyakabidhiwa urithi wote wa ahadi za Mungu, kwasababu ndiye mzaliwa wa kwanza..

Na baada ya kujua hilo na kuamini hilo, basi hatua inayofuata ni kutubu dhambi zetu zote tunazozifanya kwa wazi au kwa siri, na kujinyenyekeza chini yake na kisha tunatafuta ubatizo sahihi, ambao ni ule wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo kulinga na (Matendo 2:38) na kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu ambao tutakuwa tumeupokea, huo unatufanya kuwa wakamilifu..Kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema katika Marko 16:16, kwamba aaminiye na kubatizwa ataokoka, na pia alifafanua vizuri kwa Farisayo Nikodemo maana ya kuzaliwa mara ya pili, kwamba ni kwa Maji na kwa Roho.. Maana yake kwa ubatizo wa maji na wa Roho Mtakatifu!.

Yohana 3:4  “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

6  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7  Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”

Na kumbuka kuzaliwa ni hatua ya kwanza tu!..huna budi kuukulia wokovu kwa kumtafuta Mungu kwa bidii, unapozidi kumtafuta Mungu, ndivyo unavyozidi kukua kiroho, na hatimaye unafikia utimilifu ule Mungu anaotaka wewe uufikie.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

MUNGU HAONI SHIDA KUMUHAKIKISHIA MWOVU ULINZI.

SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?

Habari za Esau na Yakobo zina mafunzo makubwa sana kwetu,. Unajua biblia inaposema mambo yote yaliyoandikwa katika agano la kale yalikuwa ni kwa ajili ya kutuonya sisi, ilimaanisha kweli (Soma 1Wakor 10:11). Hivyo tunapaswa tusome kwa umakini mkubwa sana kwasababu  hakuna jambo ambalo linaendelea sasa hivi duniani halijaandikwa kwenye biblia.

Ulishawahi kujiuliza ni kipindi cha siku ngapi, au wiki ngapi, au miaka mingapi kilipita, tangu ule wakati  Esau anauza haki yake  ya mzaliwa wa kwanza kwa mdogo wake, mpaka ule wakati Baba yao anawabariki. Unaweza kudhani ni kipindi kifupi sana wakiwa bado ni watoto, lakini sio.

Ni kweli wakati Esau anauza haki yake, walikuwa bado ni vijana wadogo, kulingana na hadithi za wayahudi, siku ile Esau alipomfuata ndugu yake ni kumuuzia haki yake kwa chakula cha dengu alipokuwa ana njaa inasadikika walikuwa na umri wa miaka 15.

 Lakini wakati ambao Baba yao sasa anakaribia kufa, walikuwa si watoto tena, bali watu wazima sana, Kulingana na hadithi hizo hizo za kiyahudi walikuwa ni wazee wa miaka 63, kwasababu wakati tu Esau anaoa wake wahiti alikuwa na umri 40, (Mwanzo 26:34)  na hapo bado sana baba yao kuwabariki kwahiyo zaidi ya miaka 48, Yakobo alikuwa anaipigania tu ile haki ya mzaliwa wa kwanza.

Lakini nataka leo tuone kwa undani ni kwanini, Mungu alimchukia Esau, kwa ile tabia yake kama tunavyoma katika maandiko.

Warumi 9:13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia”.

 Wengi tunadhani ni kwa kosa la kule tu kile chakula alichopewa na ndugu yake baada ya kutegewa mtego wakati alipokuwa na njaa.. Ukweli ni kwamba Mungu asingeweza kuchukizwa na Esau kirahisi hivyo, kwa kosa la njaa, bali alichukizwa na Esau kwa ile kauli yake aliyoitoa ambayo aliendelea kuisimamia katika maisha yake yote..

Na kauli yenyewe ndio ile tunayoisoma katika biblia..(Zingatia vifungu vilivyo katika herufi kubwa)

Mwanzo 25:29 “Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.

30 Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.

31 Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.

32 Esau akasema, TAZAMA, MIMI NI KARIBU KUFA, ITANIFAA NINI HAKI HII YA UZAZI?

33 Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

34 Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. HIVYO ESAU AKAIDHARAU HAKI YAKE YA MZALIWA WA KWANZA”.

Sasa zingatia hiyo  kauli ya Esau..”mimi ni karibu na kufa, itanifaa nini hii haki ya uzazi”.. Ni heri angesema, “Haya nitakupa” Lakini yeye alisema ninakaribia kufa, itanifaidia nini hiyo haki za uzazi, akiwa na maana hiyo haki kama haiwezi kumtatulia matatizo yake aliyokuwa anapitia kwa wakati ule, haina maana yoyote, ni ya kudharauliwa tu,

Na ndio maana ukindelea kusoma utaona biblia inasema.. tangu huo wakati Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza,..Unaona bado aliendelea kushikilia msimamo wake huo huo, kwa miaka zaidi ya 40, mpaka siku ile ya kubarikiwa  na baba yao ilipofika, alipogundua umuhimu wa  Baraka hizo alikuwa ameshachelewa, japo alitafuta kila namna ya kumpendeza baba yake lakini jambo hilo halikufanikiwa hata kidogo, biblia inatuambia, alilia kwa machozi mengi yasiyoelezeka. Soma

Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.

17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi”.

Ndugu, hii roho ya Esau mpaka leo inafanya kazi sana, tena sana , nimekutana na watu wengi, unapowahubiria injili, ambayo ni kwa faida yao wenyewe, jambo la kwanza watakalokuuliza, nikiokoka, Yesu atanipa pesa za kumudu maisha yangu leo?, ukimwambia zitakuja kwa wakati wake, atasema, Basi simtaki hana faida kwangu, mwingine utampa kipeperushi chenye habari za wokovu,atatazama halafu kidogo, halafu saa hiyo hiyo atakuambia nilidhani unanipa pesa, wewe unanipa makaratasi, anakitupa hapo hapo mbele yako,.. Sasa watu kama hawa hawana tofuati na Esau, ambaye alikuwa anaidharau  haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwasababu haikuweza kumtatulia matatizo yake ya wakati ule.

Ndugu usiutafute wokovu wa kutatuliwa shida zako za sasa, kamwe usifanya hivyo, Mungu atakuona wewe ni kama Esau tu. Vilevile kama na wewe ni mmojawapo, wa wanaoidharau injili, ipo siku utautafuta wokovu kwa machozi mengi na kulia na kusaga meno na hautaupata.. Siku hiyo utakapoona, wenzako hawapo tena duniani wameshanyakuliwa wameenda  mbinguni kwenye karamu ya mwana-kondoo, wanashangalia, kwa furaha isiyo na kifani, na wewe upo hapa duniani, huna lolote nakuambia siku hiyo utalia sana..Leo unacheka lakini hiyo siku  utalia sana,.

Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;

12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Mpaka sasa hakuna asiyejua kuwa unyakuo upo karibuni kutokea, tumebakiwa na siku chache sana pengine wiki, au miezi, lakini tujue kizazi chetu kimekidhi vigezo vyote vya kushuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa Yesu duniani. Swali ni je! Wewe umejiwekaje tayari leo? Je! Ni kama Yakobo ambaye usiku na mchana alikuwa anautafuta urithi usioharibika kwa hali na mali, au kama Esau aliyedharau Baraka za mbali kwa mafanikio, na pesa za muda tu.

Jibu unalo.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?

USIRUDI NYUMA KWA KUITUMAINIA HAKI YAKO.

UFUNUO: Mlango wa 15

kwanini Yakobo amefananishwa na mdudu?(Isa 42:14)

Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?

Rudi nyumbani

Print this post

KATIKA MLIMA WA BWANA ITAPATIKANA.

Jina la Bwana wetu Yesu, libarikiwe, karibu tujifunza biblia..

Mwanzo 22: 6 “ Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.

7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?

 8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.

9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.

 10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.

11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.

 13 Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.

14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana”.

Kabla ya kufika mlimani Isaka alimwuliza Baba yake “Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?”.. Lakini Ibrahimu hakuwa na jibu la uhakika!.. Akaishia tu kusema.. “Bwana atajipatia mwanakondoo”..lengo la Ibrahimu kusema vile ni kumfumba tu macho!, mwanae Isaka asijue kuwa yeye ndiye anayekwenda kuchinjwa..

Na walipofika katika mlima wa Bwana, Ibrahimu tayari akiwa ameshamfunga mwanawe kwaajili ya kumchinja, tunasoma… Malaika wa Bwana alimzuilia na kumfumbua macho amwone mwanakondoo  aliyekuwa amenaswa pembe zake kwenye kichaka kilichopo nyuma yake.

Kondoo yule haijulikani alitoka wapi, pengine alipotea wakati wachungaji walipokuwa wanachunga huko milimani, na kunaswa kwenye kichaka kimoja wapo katika huo mlima, mahali pale pale Ibrahimu alipofika..Hivyo kwa vyovyote vile ilivyokuwa, lakini mwisho wa siku tunaona, tayari Mungu alikuwa amemwandaa mwanakondoo yule kwaajili ya sadaka ya kuteketezwa..

Nanichotaka uone ni kuwa sadaka inayompendeza Bwana haipatikani chini, bali inapatikana juu katika Mlima wa Bwana… Ndio maana hapo katika mstari wa mwisho tunasoma…

“Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana”…

Kumbuka sio katika mlima mwingine wowote itapatikana, la! Bali katika MLIMA WA BWANA TU!..Ndio maana hapo anasema “kama watu wasemavyo”..maana yake watu walishafanya utafiti na kugundua kuwa Baraka za Mungu hazipatikani mahali pengine popote, au katika mlima mwingine wowote isipokuwa katika Mlima wa Bwana. Sasa tangu huo wakati wayahudi wakapaheshimu mahali hapo Ibrahimu alipomchinja huyo mwana kondoo, na mahali hapo ndipo pakajulikana kama Mlima wa Bwana tangu wakati huo, na ndipo hekalu la Mfalme Sulemani lilipojengewa.. Hivyo baraka zote walikuwa wanazipata kutoka katika nyumba ile ya Mungu, ambayo ilijengwa juu ya m lima wa huo wa Bwana, uliojulikana kama Mlima Moria..(ndipo mahali pa juu Bwana alipopachagua)

Lakini baada ya Bwana Yesu kuja, Mlima wa Bwana ulibadilika kutoka “kuonekana kwa macho” mpaka “kutokuonekana kwa macho”

Tusome,

Yohana 4:20 “Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

21 Yesu akamwambia, Mama, UNISADIKI, SAA INAKUJA AMBAYO HAMTAMWABUDU BABA KATIKA MLIMA HUU, WALA KULE YERUSALEMU.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

23 LAKINI SAA INAKUJA, NAYO SASA IPO, ambayo waabuduo halisi WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”.

Umepaona mlimani kwa Bwana leo?.. Si kule Yerusalemu, wala si katika mojawapo ya milima tunayopanda kwenda kuomba kila siku… bali ni katika Roho, na si katika Roho tu..bali katika Roho na kweli.

Unapompokea Yesu katika maisha yako, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuishi katika Neno la Mungu.. Hapo tayari upo mlimani kwa Bwana. Kwasababu umebatizwa katika Roho Mtakatifu na vile vile unaishi katika Kweli ya Neno la Mungu.

Je leo upo mlimani kwa Bwana au bado upo chini?.. Kumbuka Baraka za kweli za Mungu zipo mlimani..huna budi kumchukua mwanao mpendwa na kuanza safari ya kwenda naye mlimani…Njia ya mlimani ni msalaba wa Bwana Yesu.

Mwanao mpendwa ni nini leo hii?..je! ni kazi yako?, elimu yako?, fedha zako?, hazina yako? Ndugu zako?.. Zichukue leo na kwenda naye kwa Bwana mlimani..kuwa radhi kuvipoteza vyote kwaajili ya Bwana kama Ibrahimu, na nakuambia badala ya kufikiri utavipoteza hivyo, kinyume chake utavipata kama Ibrahimu…

Lakini unapomfuata kuwa tayari kupoteza kila kitu!..ili upate kila kitu..

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”

Na pia alisema…

Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake ?”

Hiyo ndio gharama ya kwenda mlimani kwa Bwana, ndio gharama ya kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli.

Kama hujampokea Yesu na unataka kufanya hivyo leo, basi hapo ulipo jitenge dakika chache kisha piga magoti na zungumza na Bwana, kiri wewe ni mwenye makosa, na mwombe Bwana akurehemu, na baada ya hapo, dhamiria kuacha mambo yote maovu uliyokuwa unayafanya kwa wazi na kwa siri, kama ulevi, wizi, chuki, utukanaji, tamaa mbaya, kujichua, uasherati, usengenyaji n.k. Na baada ya hapo..Na baada ya hapo tafuta ubatizo sahihi, ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu atakuongoza katika kuijua kweli yote. Hapo utakuwa umefika mlimani kwa Bwana, na yale yote ambayo ulikuwa unadhani umeyapoteza..Bwana atayarejesha upya katika usahihi Zaidi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Kwanini  vizazi vya ukoo wa Yesu vinajipinga katika Mathayo na Luka.

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?

Rudi nyumbani

Print this post

UKIOKOKA, JIANDAE KUPITISHWA USIPOPATAZAMIA.

Kama leo hii Mungu akikutoa katika utumwa wa dhambi (Yaani kuokoka), basi weka akilini kuwa unapopelekwa kutakuwa ni nje ya matarajio yako, na pengine pasiwe ni pa kuvutia kabisa katika macho yako. Ni vizuri tukafahamu njia za Mungu, ili pale tunapokutana nazo tusiwe ni watu wa  kulaumu, laumu, au kuuliza uliza ni kwanini hivi, kwanini vile?

Kipindi kila Mungu alipowatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, walitazamia kupitishwa  katika NJIA kuu ya mataifa yote, iliyojulikana kama  njia ya wafilisti. Njia hiyo ilikuwa ni ya haraka na ya chap chap, kiasi kwamba kama wangeipitia hiyo, ingewachukua wiki kadhaa tu wangeshafika Kaanani. Lakini Mungu alikuwa na sababu ya wao kutowapitisha njia ile..Tusome..

Kutoka 13:17 “Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;

18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha”.

Unaona wana wa Israeli walipitishwa katika njia ya gheni kabisa machoni pao, njia yenye ukingo wa mbeleni ya bahari, njia ya vichakani, isiyopitwa na watu, njia ya upweke..Mpaka biblia inatuambia hicho ndicho kilichomvutia Farao, kuwafuatilia tena ili wawateke nyara wawarudishe Misri. Lakini hawakujua kuwa Mungu yupo kule kuwatetea.

Kutoka 14:1 “Bwana akasema na Musa, akamwambia,

2 Waambie wana wa Israeli, kwamba warudi na kupiga kambi yao mbele ya Pi-hahirothi, kati ya Migdoli na bahari, kukabili Baal-sefoni; mtapanga mbele yake karibu na bahari.

3 Naye Farao atasema katika habari za wana wa Israeli, Wametatanishwa katika nchi, ile jangwa imewazuia wasitoke.

4 Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi wakafanya hivyo.

5 Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?

6 Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye;”

Hata sasa, wapo watu wanapookoka, na ghafla kuona mambo yanakwenda kinyume na matazamio yao, wanapolazimika kuishi staili nyingine ya maisha, wanageuka na kurudi nyuma na kuuacha wokovu. Na tena pale wanapoona, kuna ukigo mzito mbele yao na kwamba wakiendelea na njia hiyo ya wokovu watakwama ndio kabisa  wanakimbia kwa miguu yote miwili, na kusema huyu si Mungu.

Pengine mwingine atapitia shida kidogo, au dhiki kutoka kwa ndugu, au kupungukiwa, jambo ambalo ni kinyume na matarajio yake, wakati hapo mwanzo yeye alidhani akimpokea Kristo siku hiyo hiyo mambo yataanza kuwa safi, sasa anapoona kumetokea mitikisiko Fulani katika maisha, anamwacha Mungu anasema huyu sio Mungu.

Ndugu ikiwa kweli umetubu dhambi zako, na umejitikwa msalaba wako kumfuata Kristo, umesema mimi na ulimwengu ndio kwaheri, kamwe usitazame nyuma, pale unapoona mambo yanakuja kinyume na matarajio yako, wewe songa mbele. Ni Mungu ndiye kakusudia kukupitisha hapo, usianze kulaumu laumu au kunung’unika, na kusema kwanini mimi, maadamu Kristo yupo ndani ya moyo wako, songa mbele. Unapoona njia hiyo imekuwa ndefu sana, kama vile huielewi itaisha lini? Bado usiwe mwepesi wa kutazama nyuma. Wewe endelea mbele maadamu unamwona Kristo kila siku katika maisha yako. Kumbuka iliwachukua miaka 40 wana wa Israeli kuifikia Kaanani yao.

Nawe pia upo wakati Bwana aliouweka atakufikisha katika Kaanani yako ya hapa duniani na mbinguni. Ni wewe tu, kutambua kuwa njia za Mungu sio njia zetu. Jambo ambalo wengi wetu hatulijua pale tunaposema tumemfuata Kristo, na huku tunamtaka Mungu atatupitisha kwa njia ya wengi.

Kamwe tuondoe hayo mawazo. Yeye ana njia zake, na wanadamu wana njia zao. Hilo tulifahamu. Na pia tukumbuke mtoto yoyote wa Mungu, atapitishwa tu kwenye njia hizo, haijalishi ni mjanja, au hodari, au tajiri au maskini kiasi gani, ni lazima atakutana tu na njia hizi zisizoeleweka za Mungu, kwasababu madarasa ya Mungu hayarukwi. Na tabia ya hizi njia ni kuwa zinaambatana ni miujiza mingi ya Mungu, ikiwa na maana mtu anaweza kufikia mahali anaona amekwama, ghafla anashangaa amepitaje pitaje mazingira hayo, huo ndio uthitibisho kuwa yupo katika njia hiyo ya Mungu.

Lakini kama akistahimili, basi ajue, licha tu ya kuupokea uzima lakini mwisho wako atakuwa ni wa mafanikio na wa Baraka sana hapa duniani.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

MUNGU HATAZAMI MOTO WA KIGENI,KUWA MAKINI!

Rudi nyumbani

Print this post

MUNGU HATAZAMI MOTO WA KIGENI,KUWA MAKINI!

Zamani nilipokuwa mdogo nilijaribu kufanya zoezi ambalo lilikuwa ni hatarishi kwangu. Nilidhani, kila “balbu” ilihitaji kitu kinachoitwa “Umeme”tu  bila kujua ni umeme kiasi gani unahitajika ili uwake. Hivyo, siku hiyo nikachukua nyaya mbili, nikazichomeka moja kwa moja kwenye soketi, lengo langu ni zile nyaya nitakapozigusanisha  sasa na  balbu nione ikiwaka, nifurahie.

Lakini nilipozigusanisha tu zile waya na balbu, matokeo yalikuwa ni tofauti na nilivyotarajia. Balbu ile ilipasuka. Na kwa neema za Mungu tu vile vipande vilivyorukwa havikuniingia machoni, vinginevyo leo hii ningekuwa kipofu.

Shida ni nini? Nilidhani kilichohitajika ni umeme tu, ilimradi umeme. Na hiyo yote nikwasababu nilikurupukia kitu ambacho sijafahamu kanuni zake kwanza, Ni  kwanini watu wanaitanguliza ile holder kwanza kabla ya kuiunganisha na umeme..! sikuwa na muda wa kufuatilia.

Mambo kama hayo yanaendelea leo hii rohoni, Watu wanajaribu kumfanyia Mungu ibada bila kufahamu kanuni sahihi ambazo Mungu anataka zifuatwe. Na matokeo yake ndio hapo tunaishia kuona matokeo hasi kama sio kuadhibiwa  na Mungu kabisa..

Katika biblia tunaona kulikuwa na watoto wawili wa Haruni, ambao walijaribu kufanya zoezi kama hili. Wenyewe waliingia hemani pa Mungu, na kuvukiza uvumba kinyume na utaratibu wa Mungu, na Mungu akawaua saa ile ile kwa kuwashushia moto na kuwateketeza kabisa,. Biblia inatuambia kosa walilolifanya lilikuwa ni KUTUMIA MOTO WA KIGENI, kuvukiza uvumba.

Walawi 10:1 “Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza.

2 Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa mbele za Bwana.

3 Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo Bwana alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi”

Moto wa kigeni ulikuwa ni upi? Ni moto wowote ambao ulitoka nje ya madhabahu ya Mungu. Utakumbuka wakati ule makuhani walipotaka kufanya upatanisho wa makosa na dhambi za watu, walikuwa wanaagizwa wachinje wanyama, Sasa moto uliokuwa unawateketezea hao wanyama ndio ulikuwa unaitwa moto wa madhabahuni, moto huo wa makaa haukuzimwa mchana wala usiku, uliwaka daima.

Sasa huo ndio waliokuwa wanauchukua makuhani, na kwenda nao ndani ya hema, kisha wanaweka uvumba uliosagwa vizuri, juu yake na kuvukiza. Pale moshi na harufu ya uvumba ule unapopanda juu, basi Mungu alikuwa anawasemehe makosa yao, waliomkosea.

Sasa hawa wana wawili wa Haruni, wao walidharau kanuni hii ya Mungu, wakadhani kinachohitajika ni Moto ilimradi moto tu,.. Wakauacha moto wa madhabahuni,ambapo upo pale hemani daima, wakaenda chukua moto wanaoujua wao kutoka huko nje, hatujui pengine waliutolea kwenye majiko yao ya nyumbani, hatujui, wakauleta nyumbani mwa Mungu, kisha wakaweka uvumba juu yake, ili wamvukizie Mungu kwa kupitia huo. Kilichotokea ni kuuliwa badala ya kupewa rehema.

Tunapaswa tujue kuwa wakati wowote tunapomfanyia Mungu ibada ya aina yoyote ile, tujiulize je tumefuata taratibu zake? Tunapowasilisha maombi yetu kwake je, tupo ndani ya wokovu? Je na sisi ni watakatifu? Kama sio ni heri tuache tu, kwasababu maombi yanayowekwa juu ya moto wa madhabahuni ya Mungu ni yale watakatifu tu, na si ya wengine, biblia inasema hivyo katika.

Ufunuo 8:3 “Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na MAOMBI YA WATAKATIFU wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.

4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika”.

Unaona? Hivyo kama wewe si mtakatifu, na  unasema  mimi ninasali, ninashiriki meza ya Bwana, ninaimba kwaya,, ninatawadha watakatifu miguu, ninamtolea Mungu.. ujue kuwa unaweka moto mgeni madhabahuni pa Mungu. Na upo hatarini sana kupigwa kama sio kuuliwa kabisa.

Huu ni ule wakati ambao Mungu anataka waabuduo halisi, wa kumwabudu yeye katika Roho na kweli. Na sio katika uongo, kama waliofanya akina Anania na Safira wakafa.

Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli”.

Mungu hataki ukristo feki, ndugu yangu, anasema ukitaka kuwa moto kuwa moto, au uwe baridi kabisa, kuliko kuwa vuguvugu, unasema umeokoka na bado unaendelea kuvaa vimini, na suruali, unavaa milegezo, unajichubua ngozi yako, unakunywa pombe, unazini. Hayo mambo si ya wakati wake huu, ambao Mungu anataka aabudiwe katika Roho na Kweli. Na wala usiyajaribu kwa Mungu, kwasababu unaweza ukadhani unampendeza Mungu, kumbe ndio unajitafutia mapigo kama ilivyokuwa kwa Nadabu na Abihu.

Kama hujaokoka kwa kumaanisha, basi okoka leo, Yesu aingie maishani mwako, dhamiria kabisa kuacha matendo yako maovu unayoyafanya, kisha ukabatizwe kama hukubatizwa na yeye mwenyewe atakupokea na kukusamehe, na ibada yako itaipokea na kukubariki.

Bwana atupe macho ya kuona..

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.

Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?

Je watu ambao hawajasikia kabisa injili watahukumiwa?

Nini maana ya uvuvio?.

Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?

Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?

Rudi nyumbani

Print this post

AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.

Kufahamu huduma za Roho Mtakatifu wakati huu ni kugumu kwa wakristo, kama ilivyokuwa kufahamu huduma ya Yesu Kristo kwa wayahudi wakati ule. Wayahudi walimtazamia Kristo aje kama mfalme tu, Wakishikilia baadhi ya vifungu tu kama vile Isaya 9:6 na huku vingine wakiviacha nyuma. Hivyo pale alipokuja kama mwana-kondoo achinjwaye achukuaye dhambi za ulimwengu (sawasawa na Isaya 53) wakapoteza shabaha kabisa, na matokeo yake wakampinga wakasema huyu siye Masihi. Sisi tunafahamu masihi atakuja katika ukuu wa kifalme kama vile Daudi ili kutuokoa na maadui zetu.

Vivyo hivyo hata leo watu wengi wakisikia Roho Mtakatifu wanachojua ni kunena kwa lugha tu, halafu basi..Hawajui kazi nyingine za Roho Mtakatifu ni zipi katika kanisa, hawajui agenda yake ni ipi kwa wakati wetu huu tunaoishi sasa.

Leo tutatazama kazi ambazo Roho Mtakatifu anatarajia kuzitenda katika siku hizi za mwisho..

Ukisoma Ufunuo 1:4 inasema..

Ufunuo 1:4 “Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; NA ZITOKAZO KWA ROHO SABA WALIOKO MBELE YA KITI CHAKE CHA ENZI;”

Hapo utaona zikitajwa Roho saba za Mungu.. Sasa kiuhalisia Mungu hana roho saba, Mungu anayo Roho moja tu, ambaye ndiye Roho Mtakatifu. Lakini hapa tunaonyeshwa zikiwa saba, maana yake ni kuwa, Hizo ni SURA SABA, za Roho Mtakatifu, au HUDUMA /UTENDAJI KAZI saba wa Roho Mtakatifu.

Na utendaji kazi wake huu, ulianza kufanya kazi rasmi siku ile ya Pentekoste, na ukaendelea kutembea kwenye yale makanisa saba ambayo tunayasoma katika kitabu cha Ufunuo 2&3, kwa hizo Roho saba za Mungu..Ambapo tunajua kabisa kwa majira yakibiblia sisi tupo katika lile la mwisho la saba, lijulikanalo kama LAODIKIA.  Na kanisa hili kulingana na kalenda ya ki-Mungu lilianza mwaka wa 1906.

Mpaka hapo tunaweza kuona kabisa  kuwa sisi tunaongozwa na ile Roho ya Saba ya Mungu.

Sasa ni vizuri kujua jambo moja, kwa kawaida kitu cha kwanza na cha mwisho huwa vinakuwa na nguvu za kipekee na za kitofauti, msingi wa nyumba na finishing ya nyumba huwa vinatumia gharama kubwa sana.. Vilevile katika riadha mwanzo wa kukimbia na mwisho wa kukimbia huwa kunakuwa na ushindani sana, na ndio maana utaona wakimbiaji wengi wakikaribia kufika mwisho badala ya kupunguza mwendo utaona ndio wanaongeza nguvu zaidi.

Vivyo hivyo na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu  kwa haya makanisa saba, kanisa la kwanza na la mwisho Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa namna ya kipekee sana.. Alianza kwa nguvu nyingi sana na udhihirisho mwingi sana, wakati ule wa Pentekesto, kanisa la kwanza lilipoanza.. Na Vivyo hivyo atamaliza kwa nguvu nyingi na udhihirisho mwingi zaidi hata kuliko ule wa kwanza, kwa kanisa hili la mwisho la Laodikia.

Biblia inatuambia kipindi kile Mungu aliwatumia mitume wake, kufanya miujiza ya kupita kawaida, soma (Matendo 19:11). Na matokeo yake injili yao ikaenea ulimwenguni kote kwa kipindi kifupi sana. Miujiza kama ile iliyofanywa na mitume, mingi ya hiyo haikuwahi kutendeka kwa nyakati nyingine zilizofuata, kwasababu nyakati zilizofuata Roho Mtakatifu alitembea katika Uso mwingine na sio wa ishara na miujiza tena kama ilivyokuwa kwa kanisa la kwanza la mitume, hata zile karama za Roho nyingi hazikuonekana kwa hayo makanisa yaliyofuata. Soma historia ya kanisa utalithibitisha hilo.

Lakini tulipoingia katika kanisa hili la mwisho la Laodikia, ambalo lilianza mwaka wa 1906, Mungu alianza kuyarejesha tena yale ya mwanzo kama kipindi kile cha mitume. Karama za Roho zilianza kudhihirika kuonyesha kuwa Yule Roho wa SABA, ameanza kutenda kazi  katika uvuvio ule ule wa kama kanisa la kwanza. Na ndio maana utaona leo hii kutokana na udhihirisho wa karama za Mungu kuwa nyingi hata machafuko yamekithiri katika kanisa, manabii wa uongo wametokea humo humo, wengine wakigeuza karama za Mungu kuwa biashara na umaarufu.

Lakini ipo sehemu ya pili ambayo Roho Mtakatifu ameihifadhi kwa ajili ya WATUMISHI WAKE tu walio waaminifu. Na sehemu hiyo tunaweza kuisoma katika maandiko haya.

Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 TENA JUU YA WATUMISHI WENU, WANAUME KWA WANAWAKE, KATIKA SIKU ZILE, NITAMIMINA ROHO YANGU.

30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.

32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana”.

Ukisoma hapo kwa makini vifungu hivyo utaona sehemu ya kwanza katika unabii huo Mungu aliahidi kumwaga Roho wake, juu ya wote wenye mwili, ikiwa na maana kuwa WOTE, watakaomwamini yeye atawamwagia Roho wake bila kipimo, nao wataota ndoto, watatabiri, wataona maono..Lakini sehemu ya pili ya unabii huo, haimuhusu kila mtu. Bali itakuwa ni kwa watumishi wake tu.

Hao ndio amewaahidia, kuwamwagia Roho wake kwa kipimo cha kipekee sana na kupitia hao watakapokea nguvu za kitofauti sana, za kufanya miujiza isiyo ya kawaida.

Soma tena pale Anasema..

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.

Haya ndio Roho Mtakatifu amejiandaa kuyafanya katika nyakati hizi za kumalizia, tutaona ishara ambazo hazijawahi kurekodiwa katika historia ya dunia, mfano wa zile za Musa na Eliya. Zikifanywa na watumishi waaminifu wa Mungu. Na ishara hizi hazitakuwa kwa ajili ya maonyesho kama wanavyofanya manabii wa uongo ili kujichotea umaarufu na pesa, hapana, bali zitakuwa kwa lengo la kuyavuta yale mabaki ya Mungu yaliyosalia duniani kwa sasa ambayo yamechanganywa na ukengeufu wa dini zao uongo na makristo na manabii  wa uongo..

Zingatia, umwagiko huu hautamuhusu kila mtu, bali watumishi wa Mungu wa Kike na wa Kiume waliowaaminifu tu.

Je! Wewe na wewe upo ndani ya wokovu? Na kama upo je ni mtumishi wa Mungu mwaminifu?.

Kumbuka wakati huo upo karibuni sana kutokea. Hivyo tumika kwa Bwana wako kwa uaminifu, ili wakati huo yamkini kama ukikukuta uko hai, basi Mungu akufanye wewe kuwa sehemu ya hiyo huduma. Tumeitwa hapa duniani tumtumikie Mungu kwa uaminifu, kwa kadiri  ya karama alizotupa.

Tumtambue Roho Mtakatifu na mipango yake. Ili tuishi sawasawa na mapenzi yake hapa ulimwengu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi nyumbani

Print this post

Kujuzu ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 12:4?

Labda tuanzie kusoma kuanzia juu kidogo,

2Wakorintho 12:2 “ Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu

3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua

 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene”

Neno kujuzu maana yake ni “kutoruhusiwa”. Hivyo hapo Paulo alikuwa anaelezea maono aliyoyaona, kwamba alinyakuliwa mpaka mbingu ya tatu na kuambiwa maneno ambayo hakuruhusiwa kuyasema kwa watu.

Neno hilo pia tunalisoma katika kitabu cha Mwanzo..

Mwanzo 34: 7 “Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno LISILOJUZU kutendeka”

Hata katika imani yapo mambo ambayo hayajuzu kuyafanya..Kwa mkristo aliyeokoka, haijuzu kuupenda ulimwengu, haijuzu kuishi maisha ya dhambi na anasa, haijuzu kuwa mtukanaji, haijuzu kuwa mwizi na tapeli, haijuzu kuwa mzinzi na mwasherati, haijuzu kuwa mlevi, haijuzu kujifunga nira na watu wasioamini, na mambo mengi yote yanayofanana na hayo. Zaidi sana tunapaswa tujiweke katika hali ya usafi na utakatifu na kuchukua msalaba watu na kumfuata Yesu kila siku katika maisha yetu, kwasababu biblia inasema pasipo huo utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu.

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

KWANINI MIMI?

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

Rudi nyumbani

Print this post

Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).

 Ufunuo 21:8 “BALI WAOGA, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Mwoga ni mtu mwenye “hofu”. Na hofu inatokana na kutokuwa na uhakika wa jambo…Mtu anayekatiza mahali Fulani usiku, na hana uhakika kwamba ataimaliza hiyo njia anayoipita salama, kitakachomtawala baada ya hapo katika nafsi yake ni hofu na wala hakuna kingine, kadhalika mtu ambaye hana uhakika kwamba kesho atakula au atapata jambo Fulani, basi kinachofuata kwake ni kuingiwa na hofu vile vile mtu ambaye hana uhakika akifa atakwenda wapi, kitakachofuata kwake ni kuingiwa na hofu na mashaka… hata kama hajijui kama anayo hofu!, lakini tayari anayo.

Hivyo hofu inakuja kutokana na kukosa uhakika wa maisha,… na uhakika huo hauletwi na mwingine zaidi ya mmoja tu, ambaye ni YESU. Kwa kupitia yeye pekee ndiye anayetoa mashaka na hofu yote ndani ya mtu, anaondoa hofu ya maisha yake ya hapa duniani na ya maisha yanayokuja…kiasi kwamba mtu anakuwa hana hofu kabisa na maisha na vile vile hana hofu  ya mauti..

Waebrania 2:15  “awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa HOFU YA MAUTI walikuwa katika hali ya utumwa”.

Hivyo mtu aliye nje ya Kristo anayo hofu!.. hana uhakika kwamba kesho atakula!, hana uhakika kwamba mwezi ujao atakuwa salama, akisikia ugonjwa Fulani umezuka anaishiwa nguvu, akiumwa kidogo anapoteza tumaini lote, kila taarifa inayomjia kwake ni ya mshtuko tu!..kwaufupi kesho yake yote yamejaa mashaka!..

Na hiyo yote ni kwasababu yupo nje ya Kristo!.. na Kristo hayupo ndani yake!.. Kwasababu kama akizama kisawasawa hawezi kuwa na hofu yoyote ile!..anakuwa ni jasiri muda wote.

1Yohana 4:18  “Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo”.

Na kwasababu anakuwa hayupo ndani ya Kristo, basi ni lazima na mambo mengine maovu yatakuwa yanaambatana naye, kama ulevi, uashetari, uzinzi, usengenyaji, tama mbaya, kuupenda ulimwengu n.k … na hivyo hawezi kuurithi uzima wa milele, kwa tabia hizo.

Ufunuo 21: 7  “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

8  BALI WAOGA, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Je! Wewe ni mwoga?. Jipime kama una hofu ya kifo!, au una mashaka baada ya kifo utaenda wapi, basi! Kuna uwezekano bado hujakamilishwa katika pendo la Mungu.. Unamhitaji Kristo aingie katika maisha yako ili akupe uhakika wa uzima wa milele.. Uhakika huo utaitupa nje hofu yote.. hutaogopa kufa hata ukiambiwa leo ndio safari yako ya maisha imefika ukingoni, hata ukisikia kuna ugonjwa fulani hatari umezuka, hata ukisikia taarifa zozote za kuogopesha, wewe siku zote utabaki kuwa jasiri, zikija tufani, dhiki, tabu wewe unabaki yule Yule…huogopi ogopi.. Vile vile kama unaogopa wachawi, majini au kulogwa, bado Kristo hajaingia maishani mwako.

Marko 4.39  Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40  Akawaambia, MBONA MMEKUWA WAOGA? Hamna imani bado?

41  Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Nasi tukiwa ndani ya Yesu na Yesu akiwa ndani yetu, hofu yote inaondoka!..

 2Timotheo 1: 7 “ Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”.

Kumbuka tena WAOGA, wote hawataurithi uzima wa milele. (1Yohana 4:18).Hivyo woga pia ni kipimo tosha cha kujijua kama kweli tupo kwenye mstari wa Imani au la!.

Bwana atusaidie na kutubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Kicho ni nini? (Waefeso 5:21, 2Samweli 23:3)

CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Rudi nyumbani

Print this post

JE! WEWE NI MFUNGWA WA BWANA?

Utumwa sio neno zuri, lakini pia ni neno zuri. Watu wa dunia hii wanao watumwa, lakini pia Yesu Kristo anao watumwa wake. Ndio maana alisema maneno haya..

Mathayo 11:28  “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30  kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”

Hapo hasemi kuwa tukishakwenda kwake ni kupumzishwa tu, basi na baada ya hapo hakuna kinachoendelea…la! Hakusema hivyo, badala yake alisema “JITIENI NIRA YANGU” na tena anasema “mzigo wangu ni mwepesi”…. Kumbe! Na yeye anayo nira!..maana yake ametutoa kwenye utumwa mmoja na anataka kutuingiza kwenye utumwa mwingine!… Tofauti ni kwamba nira yake yeye ni laini na pia mzigo wake ni mwepesi…

Lakini pamoja na hayo hasemi kwamba “yeye atatutia nira yake, baada ya kutufungua hiyo nira ya adui” badala yake anasema “JITIENI NIRA YANGU” huo ni kama “ushauri” na sio “amri”. Ingekuwa ni amri angesema “njooni kwangu nami nitawapa pumziko na kuwatia nira yangu”..hapo ingeweza kuwa amri, lakini mpaka anasema sisi ndio tujitie nira yake… huo ni uchaguzi!!…maana yake ukipenda kuwa huru sawa, au ukipenda kuichukua NIRA mpya ya YESU KRISTO ni vizuri zaidi..

Sasa kama hujui nira ni nini,…nira ni kifungo Fulani ambacho mnyama kama ng’ombe anavikwa shingoni, kama nyenzo ya kuvuta mzigo ulio nyuma yake… kadhalika na Kristo naye anayo nira ambayo anawafunga watu wake wale ambao kwa mapenzi yao wameamua kujitia katika UTUMWA WAKE. Na wanapofungwa Nira hiyo, wanageuka kuwa WAFUNGWA. Maana yake wanakuwa ni wafungwa wa YESU kwaajili ya Injili. Mfano wa hao ni Mtume Paulo.

Filemoni 1:1  “Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi”

Waefeso 3:1  “Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; 2  ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu”

2Timotheo 1:8 “Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi MFUNGWA WAKE, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu”

Wakolosai 4: 3 “mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,

4  ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena”.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu KUFUNGWA kwa Paulo katika mistari ifuatayo. (Filemoni 1:9 , Waefeso 4:1, 2Timotheo 1:8,  Filemoni 1: 23 ).

Zifuatazo ni tabia za Wafungwa wa Kristo, kwaajili ya Injili.

  1. Muda wote, masaa yote wapo katika mazingira ya kuifanya kazi ya Mungu.

Mtume Paulo wa kwenye biblia na wengine baadhi, walijitoa katika Injili kiasi kwamba hawakuwa na muda wa kutafuta wake, akili zao zote zilikuwa katika kuifanya kazi ya Mungu. Mambo ya ulimwengu huu waliyaona kama mavi (Wafilipi 3:8).

  1. Hawaionei haya injili.

2Timotheo 1:8  “Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu”

  1. Wamejikana nafsi kweli kweli.

Wafungwa wote wa Kristo wanakuwa wamejikana nafsi kweli kweli, wapo tayari hata kufa kwaajili ya injili, wapo tayari kutukanwa, kuonekana wajinga na waliorukwa na akili kwaajili ya injili, wapo tayari kuacha hata kila kitu ilimradi tu, kutimiza kusudi la Bwana wao.

  1. Wamejitenga na Ulimwengu.

Hakuna mtumwa yeyote anayekuwa na uhuru asilimia zote, muda wote utamkuta eneo la kazi..kitu kinachompa hofu kuliko zote ni kuipoteza kazi yake au kuiharibu, na kitu pekee kilichomuunganisha yeye na Bwana wake ni kazi yake hiyo aliyopewa, ya Injili. Huwezi kumkuta mtumwa aliye makini, muda wa kufanya kazi yupo anazurura!..Kadhalika wafungwa wa Yesu, kwaajili ya injili hawazururi zururi katika huu ulimwengu, shughuli shunguli na anasa za ulimwengu huu, zinawapita! na wala hawazitamani.. Macho yao ni kuifanya kazi ya Bwana na kuimaliza… Kuhubiri injili kwao ni Sharti! Sio ombi tena!.

1Wakorintho 9:16  “Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!

17  Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili”.

Je wewe ni Mfungwa wa Yesu?.. Umejitia NIRA ya Bwana Yesu shingoni mwako?.. Au bado unayo nira ya adui shetani?..Nira ya adui shetani ni ulevi unaoutumainia ambao unakufanya kuwa mtumwa wa pombe na sigara!.. Nira ya shetani ni uzinzi na ukahaba unaoufanya ambao huwezi kuishi bila huo.. Nira ya adui shetani ni ushabiki wa mpira unaokufanya uwe mtumwa wa huo, Nira ya adui shetani ni tama zote za macho ambazo zimekufanya kuwa mtumwa… Nira hiyo huwezi kujivua mwenyewe, kwasababu aliyekufunga hakuwa na nia ya wewe kukuacha huru siku moja!

Hivyo huwezi kujifungua, unamhitaji Yesu azivunje!.. ndipo uwe huru!..kwasababu kwa nguvu zako haiwezekani.. na baada ya kukufungua!, anakupa shauri la wewe kujitia nira yake!.. hapo sio yeye anakufunga hiyo nira! Ni wewe ndio unayeamua kujifunga nira yake… na kama ukitii na kukubali kumtumikia Yesu kwaajili ya injili yake, na kuwa mfungwa wake..yeye alisema maneno haya…

Marko 10:28  “Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.

29  Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30  ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele”

  Kumbuka kama bado hujampokea Yesu, basi fahamu kuwa bado unayo nira ya shetani shingoni mwako, na upo kwenye utumwa wa dhambi hata kama hujijui, Hivyo mgeukie leo Kristo akuweke huru, Yeye mwenyewe alisema “Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli (Yohana 8:36)”.

Hivyo tubu leo kwa kumaanisha kuacha dhambi zako zote unazozitenda kwa siri na kwa wazi, na kisha tafuta ubatizo sahihi, ubatizwe kwaajili ya ondoleo la dhambi zako, ubatizo sahihi ni ule wa maji tele na kwa jina la Yesu (Matendo 2:38), na baada ya hapo amua kujitia Nira ya Kristo, kwa kudhamiria kumtumikia yeye kwa gharama zozote zile, na Bwana mwenyewe atakufanya mtumwa wake.. na thawabu yako itakuwa kubwa hapa duniani na utakapofika mbinguni.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Je watu ambao hawajasikia kabisa injili watahukumiwa?

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

UFUNUO: Mlango wa 14

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

Vyombo vya uzuri ni vipi vinavyotajwa katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO.

Shalom. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Karibu tuyatafakari maneno mazuri ya uzima.

Ulishawahi kuutafakari vizuri huu mstari?

Isaya 35: 8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO”.

Sana sana hapo mwishoni anaposema “ wajapokuwa wajinga, hawatapotea”?…. Maana yake ni kuwa kuna uwezekano kweli wa kuwepo watu wa Mungu baadhi, wanaotembea katika wokovu, lakini kwa namna moja au nyingine wanaoujinga fulani ndani yao.

Na ujinga huo unaweza kusababishwa na aidha kutoyaelewa vizuri maandiko, au kushindwa kuulewa uweza wote wa Mungu, na njia zake, Lakini pamoja na kuwa watu hao watakuwepo, lakini biblia bado inasema, maadamu wapo katika NJIA KUU, njia ya uzima,NJIA YA UTAKATIFU, kamwe hawatapotea.

Leo hii sehemu nyingi utapita na kukutana na kundi la watu linasema, “kama ulokole ndio ule ni heri nibaki katika dhambi zangu”, walokole ni wavivu, wenyewe kazi yao ni kukaa muda wote kusali tu na kufunga makanisani hawana shughuli nyingine yoyote ya kufanya.. Utakutana na wengine wanasema, walokole kazi yao ni kujinyima tu, kupendeza hawapendezi, wapo rafu rafu, kama Mungu ndio hivyo heri nibakie katika  udunia wangu tu..

Ndugu, biblia inasema, hata kama wanachokifanya ni kutokana na ujinga wao.. Lakini maadamu wameupokea wokovu, wamekusudia kumfuata Mungu wao, kamwe hawatapotea, hata iweje, hilo ni hakikisho kutoka kwa Mungu. Hata wakiwa wamekataa kwenda shule, hata wakiwa wanalala maporini, hata wakiwa wanafunga mwaka mzima, hata wakiwa hawajui vizuri kusoma na kuandika, kamwe usitazamie watu kama hao watapotea..Hilo ondoa akilini.

Lakini kama wewe ni rafiki wa dunia. Unajiona njia zako ndio zipo sawa, unaona njia za watu wa kidunia ndio sahihi, jinsi wanavyoishi kwa raha, wanavyostawi, wanavyoruka ruka, wanavyopiga makeup, na kutembea uchi barabarani, na kuvaa milegezo, wewe ndio unapendezwa nao, nataka nikuambie hata kama utakuwa na akili vipi, mwisho wa siku utaishia pabaya tu. Kwasababu biblia inasema hivyo.

Mithali 14:12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”.

Wewe unayejiona, maisha ni anasa, na huku Kristo yupo mbali na wewe, mwisho wako utakuwa jehanamu, wewe unayejiona maisha ni kujiachia na kuzini, na kufanya kila aina ya dhambi kama unavyojisikia, yaani kwa ufupi unaupa moyo wako kila kitu unachopenda, na huku unaona wokovu ni mzigo mzito. Jiandae kukutana na mauti.

Umekuwa ukiwadhihaki wakristo, na kusema wale ni wajinga, wamerukwa na akili, Mungu gani wanayemuabudu anawafanya kuwa vile, wanaomba usiku na mchana, na hakuna muujiza wowote unaotendeka. Ndugu hata kama ni wajinga, lakini ufahamu kuwa ujinga wao wanaufanyia wakiwa katika gari ambalo lipo safarini.

Na wewe akili zako unazionyesha ukiwa nje ya gari. Hiyo ndio tofauti kati ya wewe na wao.. Hizo akili zitakusaidi nini ukifa leo, itakufaidia nini upate ulimwengu mzima, halafu unapata hasara ya nafsi yako?. Kama unadhani ni  wapumbavu, basi ingia ndani ya Kristo, na wewe uwepo ndani ya gari hilo salama, ndipo uutoe huo upumbavu ulio ndani yao. Lakini kama upo nje ya Kristo, ujue wewe ndio mjinga wa mwisho kabisa.

Haya maisha ni mafupi sana, nakushauri umpe Yesu maisha yako ndugu yangu. Leo unayo pumzi, lakini siku ya kesho hujui utakuwa wapi, hata kama utakuwepo kumbuka Maisha ni fumbo hakuna anayejua siku ya kuondoka kwake, hivyo yatupasa kila siku tujichunguze, Je! Bado tupo ndani ya gari la mbinguni au tulishashuka siku nyingi?

Bwana atusaidie sote.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

KWANINI KRISTO AFE?

Rudi nyumbani

Print this post