Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe,
Leo tutajifunza jinsi ya kuuvuta uwepo wa Roho Mtakatifu karibu nasi. Yapo mambo makuu matatu yanayovuta uwepo wa Mungu karibu nasi.
Hili ni jambo la kwanza linalohifadhi uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Tunapoingia kwenye maombi Roho Mtakatifu anazidi kusogea karibu nasi, anasogea kuomba pamoja na sisi (Warumi 8:26) na vile vile anasogea kuzungumza na sisi.
Kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka kipindi, Bwana Yesu anabatizwa katika mto Yordani na Yohana, utaona Roho Mtakatifu alishuka juu ya Bwana kwa mithili ya HUA (Yaani Njiwa).
Lakini katika tukio hilo kuna siri moja imejificha pale, ambayo ukisoma kwa haraka haraka unaweza usiigundue. Na siri yenyewe ni MAOMBI!. Utaona baada ya Bwana kutoka majini, na kusogea pembeni utaona alianza KUOMBA!, na wakati akiwa katika maombi, ndipo Mbingu zilipofunguka na Roho Mtakatifu kushuka juu yake.
Luka 3:21 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, NAYE ANAOMBA, mbingu zilifunuka; 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe”.
Luka 3:21 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, NAYE ANAOMBA, mbingu zilifunuka;
22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe”.
Umeona? Ni wakati alipokuwa anaomba ndipo Roho Mtakatifu alishuka juu yake, na sio wakati anabatizwa tu peke yake.
Vile vile utaona kipindi cha Pentekoste, Mitume na wanafunzi wengine wapolikuwa wamekusanyika mahali Pamoja katika ghorofa wakidumu katika kusali, na kule kule ndipo Roho Mtakatifu akashuka juu yao na kuwajaza nguvu (Soma Matendo 1:13-14, Matendo 2:1-2).
Na sehemu nyingine nyingi, utona kuwa Roho Mtakatifu alishuka wakati watu wakiwa kwenye maombi..
Matendo 4:31 “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri”.
Vile vile na sisi tukitaka kuuvuta uwepo wa Roho Mtakatifu hata tumuhisi ndani yetu, au katikati yetu basi hatupaswi kuyakwepa MAOMBI, kadhalika tukitaka tumsikie anataka nini kwetu au anasema nini, njia pekee ni Maombi!
Sasa inawezekana hujui namna ya kuomba, ni rahisi sana.. Kama utatamani kupata mwongozo wa namna ya kuomba basi tutumie ujumbe inbox, ili tuweze kukutumia somo linalohusu “Njia bora ya kuomba”
Hii ni njia nyingine ya Muhimu ya kuuvuta uwepo wa Roho Mtakatifu karibu nasi. Kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza na kututia katika Kweli yote (Yohana 6:13-14), na Kweli ni Neno la Mungu (Yohana 17:17). Hivyo tunapotenga muda wa kuishika biblia na kuisoma kwa lengo la kujifunza, basi Roho Mtakatifu anasogea karibu nasi sana. Ni lazima atusogelee kwasababu ndio kazi yake yeye kutufundisha na kutufunulia maandiko.
Tunaweza kujifunza kwa yule Mkushi aliyekuwa anarudi nchini kwao, ambapo njiani alijikuta anafungua kitabu cha Isaya 53, kilichokuwa kinazungumzia Habari za Masihi, Yesu lakini hakuwa na ufunuo wowote juu ya hilo, Ndipo Roho Mtakatifu akaingia kazini kujisogeza karibu naye ili amtie katika kweli yote!!..
Roho Mtakatifu akaanzaa kuzungumza kwanza na Filipo siku kadhaa kabla hata ya Mkushi huyo kufikiria kusoma hilo andiko, Roho Mtakatifu akaanza kutengeneza njia ya kumkaribia Mkushi huyo, akamwambie Filipo ashuke njia ya jangwa, na alipokutana na yule Mkushi yupo matatani haelewi maandiko, ndipo Roho Mtakatifu akaanza kuzungumza kupitia kinywa cha Filipo. Na hatimaye kumfunua macho yake na kumtia katika kweli yote.
Matendo 8:29 “Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi”.
Matendo 8:29 “Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.
30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?
31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.
36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?
37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]
38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.
39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi”.
Roho wa Yesu ni yule yule na tabia zake ni zile zile, tukitaka atukaribie, tumsikie, au tumwone basi ni lazima pia tuwe wasomaji wa Neno.
Agizo kuu ambalo Bwana alilotupatia ni kupeleka injili ulimwenguni kote.
Marko 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Marko 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Kwanini kuhubiri/kumshuhudia Yesu kunamsogeza Roho Mtakatifu karibu nasi?. Kwasababu kila tunapofika mahali na kushuhudia tunafanyika vyombo vya Roho Mtakatifu, Hivyo Roho Mtakatifu hana budi kila wakati kuwa nasi kwasababu wakati wote tunatumika kama vyombo vyake, hakuna wakati uwepo wake utakaa mbali na sisi!..
Mathayo 10:18 “nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. 19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. 20 KWA KUWA SI NINYI MSEMAO, BALI NI ROHO WA BABA YENU ASEMAYE NDANI YENU”.
Mathayo 10:18 “nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
20 KWA KUWA SI NINYI MSEMAO, BALI NI ROHO WA BABA YENU ASEMAYE NDANI YENU”.
Kwahiyo kama wakati wote tutakuwa katika hayo mazingira ya kumshuhudia Kristo, maana yake wakati wote, kinywa kitakachokuwa kinasema ndani yetu ni kinywa cha Roho Mtakatifu, hivyo uwepo wake utakuwa nasi muda wote!, lakini kama hatutakuwa katika mazingira yoyote ya kumshuhudia Kristo ni ngumu Roho Mtakatifu kuwa na sisi, kuzungumza kupitia vinywa vyetu, au kusema nasi!.
Je! Na wewe leo Umempokea Yesu?
Na kama ndio je! Wewe ni MWOMBAJI?..wewe ni MSOMAJI WA NENO?…wewe ni MSHUHUDIAJI?. Kama hufanyi hayo basi, uwepo wa Roho Mtakatifu utawezaje kuusikia?, vile vile sauti yake utaweza kuisikia?!.
Leo shetani kawafanya wakristo wengi wasiwe Waombaji?..utakuta mkristo mara ya mwisho kutenga angalau lisaa limoja kuomba yeye binafsi hata hakumbuki!, (yeye atakuwa anapenda kusikiliza na kusoma mahubiri tu!, na kuombewa lakini kuomba mwenyewe hataki/hawezi), Utakuta mkristo mara ya mwisho kusoma Neno binafsi ni muda mrefu sana, leo hata ukimuuliza mkristo biblia ina vitabu vingapi hajui, ukimpa biblia afungue kitabu cha Yeremia atapepesuka nusu saa hajui kilipo mpaka akaangalie kwenye index, hiyo ni kuonesha ni jinsi gani biblia ni kitabu-baki tu kwake!, na si kila kitu kwake!.
Leo hii ukimwuliza mkristo mara ya mwisho kuzungumza na mtu mwingine Habari za wokovu, au kumshuhudia Kristo, hana hiyo kumbukumbu!, lakini shuhuda za mipira, na za Maisha ya watu wengine zimejaa katika kinywa chake!..
Kumbuka Bwana anatamani yeye kuwa karibu na sisi kuliko sisi tunavyotamani yeye awe karibu nasi, hivyo ni wajibu wetu kuongeza bidii katika kuomba, kusoma Neno, kushuhudia Pamoja na kuishi Maisha matakatifu.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
Shekina ni nini? Na Je! Utukufu wa shekina unamaana gani?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
Rudi nyumbani
Print this post
Tusome,
Warumi 1:25 “Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina”.
Kiumbe ni kitu chochote chenye uhai kilichoumbwa na Mungu. Katika dunia viumbe hai ni Wanadamu, Wanyama na mimea.
Kwahiyo maandiko hapo yaliposema kuwa “wameibadili kweli ya Mungu kuwa uongo na kukisujudia kiumbe” inamaanisha ni kiumbe chochote kile, na si kimoja maalum!..kinaweza kuwa mtu au mti, au mnyama Fulani. Maeneo ya Korea kaskazini watu wanaabudu MTU kama Mungu, maeneo ya India watu wanaabudu Nyoka na Ng’ombe, Maeneo ya Marekani ya kusini na watu wanaabudu Chui na maeneo ya Afrika watu wanaabudu Miti n.k. Hawa wote wanaabudu viumbe vilivyoumbwa na Mungu, jambo ambalo ni machukizo makubwa mbele za Bwana.
Na mbaya zaidi wengi wanaofanya hivyo maandiko yanasema wanafanya hivyo kwa kujua kabisa! Kwamba vitu hivyo si Mungu, na dhamiri zao zikiwashuhudia, lakini hawataki kubadilika.
Warumi 1:20 “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina”.
Warumi 1:20 “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina”.
Je na wewe unaabudu watu? Kumfanya mtu tegemeo lako asilimia mia hakuna tofauti na kumwabudu!, kumwogopa mtu na kumfanya kinga yako kiasi kwamba hata anaweza kukuamulia siku ya kuabudu na ukatii huko hakuna tofauti na kumwabudu (Unakiabudu kiumbe), kumtumikia mtu mpaka unakosa muda wa kwenda kumfanyia Mungu wako ibada angalau hata mara moja kwa wiki, huyo mtu ni mungu wako.
Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. 7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. 8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda”.
Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda”.
Je Bwana ni tegemeo lako au viumbe?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?
Vitimvi ni mipango inayopangwa kwa siri na kikundi cha watu ili kufanya uasi juu ya mtu au watu.
Katika biblia Mitume wa Bwana Yesu walifanyiwa vitimvi vingi sana vya kuwaangamiza, mfano wa hao utaona ni Mtume Paulo..
Matendo 20:2 “Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani. 3 Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi KUMFANYIA VITIMVI, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia”.
Matendo 20:2 “Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.
3 Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi KUMFANYIA VITIMVI, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia”.
Na pia utaona kuna wakati Paulo alipokuwa amefungwa kule Yerusalemu, baadhi ya wayahudi kama 40 hivi walijifunga kiapo kwamba hawatakula wala kunywa hata watakapomwua Paulo (Matendo 23:12). Sasa mipango hiyo ndiyo inayoitwa vitimvi!
Matendo 23:27 “Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi, wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni Mrumi. 28 Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamtelemsha nikamweka mbele ya baraza; 29 nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa. 30 Hata nilipopewa habari kwamba PATAKUWA NA VITIMVI JUU YA MTU HUYU, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu”.
Matendo 23:27 “Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi, wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni Mrumi.
28 Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamtelemsha nikamweka mbele ya baraza;
29 nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
30 Hata nilipopewa habari kwamba PATAKUWA NA VITIMVI JUU YA MTU HUYU, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu”.
Na kama wakristo wa kanisa la kwanza walipitia Vitimvi, kutokana na Imani yao, kadhalika na wakristo wa kweli wa siku hizi za mwisho ni lazima wapitie vitimvi kama wa kanisa la kwanza, kwasababu Roho ni yule yule, Bwana na yule yule hajabadilika.
Ni lazima upitie maudhi kwaajili ya Imani yako, ni lazima upitie kuhuzunishwa, ni lazima upangiwe visa, ni lazima wakati mwingine utenge au uchukiwe au hata kupigwa na kufungwa!. Hizo ndizo chapa za Yesu ambazo tunazopaswa kuzichukua..
Wagalatia 6:17 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu”.
Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?
YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.
MWISHO WA MAVUNO, NI MWISHO WA DUNIA.
Kuhusuru ni nini kibiblia? (Luka 19:43)
Neno “Uchungu wa mauti” lina maana gani kibiblia?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia, chakula cha uzima wa roho zetu.
Maandiko yanasema kuwa tunaokolewa kwa Neema na si kwa matendo,
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Maana yake ni kwamba hakuna tunachoweza kukifanya sisi kwa matendo yetu, kikatufanya tuwe na haki ya kuokolewa, haijalishi tutajiona tunafanya mema kiasi gani, bado tuna mabaya mengi tunayoyafanya pasipo sisi kujijua. Mbwa anaweza kujiona yupo sawa katika njia zake zote, lakini wewe mwanadamu bado utamwona anazo kasoro nyingi. Na kwa Mungu wetu ni hivyo hivyo, kamwe hatuwezi kujisifu kwa matendo yetu kwake, haijalishi tutajiona ni wasafi kiasi gani, kwake yeye bado tutakuwa na kasoro nyingi tu!.
Lakini katika kasoro zetu hizo bado anatupa wokovu. Sasa kitendo hicho cha kupewa Wokovu bure! Pasipo matendo yetu ndicho kinachoitwa NEEMA!..
Lakini sasa hii NEEMA, ambayo inatupa wokovu bure pasipo matendo, inayo DARASA. Maana yake inafundisha!.. Kuna kitu inataka kutoka kwetu!. Ambapo ikikikosa hicho kitu kutoka kwetu basi na yenyewe inatukataa sisi.
Sasa kitu hicho ni kipi??
Tito 2:11 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 NAYO YATUFUNDISHA KUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA; TUPATE KUISHI KWA KIASI, NA HAKI, NA UTAUWA, KATIKA ULIMWENGU HUU WA SASA; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu”
Tito 2:11 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 NAYO YATUFUNDISHA KUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA; TUPATE KUISHI KWA KIASI, NA HAKI, NA UTAUWA, KATIKA ULIMWENGU HUU WA SASA;
13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu”
Umeona hapo mstari wa 12?. Kitu gani neema ya Mungu inatufundisha au inachotaka kutoka kwetu?.. inatutaka sisi KUUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA!!!. Hicho tu!.. Inatutaka sisi tuwe wanafunzi bora juu ya hilo!. Tukiweza kufanikiwa kujifunza jambo hilo basi Neema ya Mungu itakaa na sisi milele!..
Haitatazama kasoro nyingine ndogo ndogo tulizo nazo. Mbwa anayekubali mafunzo ya Bwana wake ya kutotoka nje kuzurura na anapokubali kuwa na nidhamu, Bwana wake atampenda, kasoro nyingine ndogo ndogo alizonazo atazifumbia macho!, lakini Mbwa anayekataa mafunzo machache ya Bwana wake, hataki kufundishika, ni mzururaji huko na kule, Bwana wake atamchukia na kumfukuza!.
Na neema ya Mungu ni hivyo hivyo, tukitii FUNZO lake hilo la KUUKATAA ULIMWENGU NA UBAYA WOTE!, Zile kasoro nyingine ndogo ndogo tulizonazo neema ya Mungu haitaziona, tutahesabika tu kuwa tumestahili mbele zake.
Wengi leo hawapendi kuishi Maisha ya kuukataa ulimwengu.. huku wakiamini au kuaminishwa kuwa “tunaokolewa kwa neema na si kwa matendo”..pasipo kujua NEEMA YA MUNGU, nayo kuna kitu inataka kutoka kwetu!
Ukitaka Neema ya Mungu ikae nawe ni lazima ukatae fashion za kiulimwengu.
Ukitaka Neema ya Mungu ikae nawe ni lazima ukatae anasa za kiulimwengu
Ukitaka Neema ya Mungu ikae nawe ni lazima ukatae kujichubua, kuvaa wigi, kuweka rasta, hereni, kupaka wanja, lipstick, kuvaa suruali kwa wanawake, kuvaa vimini na nguo za kubana.
Ukitaka Neema ya Mungu ikae nawe ni lazima ukatae ulevi, kusikiliza miziki ya kidunia, kujichua, kuzini kutukana, kuiba na mambo yote yanayofanana na hayo.
Usidanganyike kuwa NEEMA YA MUNGU, inakubaliana na UDUNIA!.. Neema ya Mungu na udunia ni vitu viwili tofauti!..
Je! Umeukataa ubaya?..umeukataa Udunia?
Kama bado, basi fahamu kuwa Neema ya Mungu inakufundisha hivyo leo. Tubu dhambi leo na mpokee Yesu, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo na Roho Mtakatifu atakuongoza katika kweli yote, na kukusaidia kulitii agizo hilo la Neema ya Mungu.
USIWE MSIKIAJI TU! BALI MTENDAJI.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
Neema ni nini?
Swali 1: Ni nani aliyemshawishi Daudi kuwahesabu Israeli ni Mungu au shetani?..Maana 2Samweli 24:1 inasema ni Mungu lakini 1Nyakati 21:1 inasema ni shetani.
Jibu: Ni shetani ndiye aliyemshawishi Daudi kwa ruhusa ya Mungu. Ayubu alijaribiwa na shetani kwa ruksa maalumu kutoka kwa Mungu. Hivyo ni sawa na kusema Mungu ndiye alimjaribu Ayubu..ni hivyo hivyo kwa Daudi pia.
Swali 02: Mungu anadanganya?maana Ezekieli 14:9 inasema anadanganya.
Jibu: Mungu hadanganyi shetani ndiye anayedanganya, mtu mwovu anapoikataa njia ya haki, Mungu anaweza kuruhusu shetani amwingie na kumdanganya, hivyo inaweza kutafsirika kwamba kadanganywa na Mungu lakini si Mungu bali ni shetani (Soma 1Wafalme 22:20-23).
Swali 03: Nabii aliyetabiriwa na Musa kuwa atatokea si Yesu bali ni nabii mwingine kutoka Arabia, Mohamedi (Kumbukumbu 18:15).
Jibu:
Kumbukumbu la Torati 18:15 “BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye”
Musa alikuwa mwisraeli na si Mwarabu kutoka Saudi Arabia, na ndugu zake hawakuwa waarabu bali wayahudi..Na Mohamedi hakuwa Mwisraeli bali Mwarabu.
Lakini Bwana Yesu alikuwa Myahudi na alizaliwa Israeli. Na zaidi ya yote alifanya miujiza zaidi haya ya Musa. Kwahiyo Bwana Yesu ndiye aliyetabiriwa pale na yeye ndiye Mwanzo na Mwisho hakuna mwingine. (Matendo 7:37).
Swali 04: Biblia inasema tukifika peponi tutapewa wake mara 100 ya tulionao sasa, mabikira.(Marko 10:30). Kwanini mnasema hakuna kuoa peponi?
Marko 10:28 “Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. 29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele”
Marko 10:28 “Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.
29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele”
Ndugu wake na ndugu waume, sio wake au waume au wachumba, bali ni ndugu wenye jinsia za kiume na za kike, na zaidi ya yote thawabu hizo ni katika ulimwengu huu huu, na sio peponi. Mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa.(Marko 12:25)
Swali 05: Yesu alisema “kila mtu atabeba msalaba wake” iweje yeye achukue dhambi za wengine?
Jibu: Alisema “Mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake anifuate”. Marko 8:34.
Kinyozi akikwambia “ukitaka kuja kwangu kunyoa beba viwembe vyako unifuate na pia uwe tayari kupata maumivu endapo ikitokea hitilafu”.. Je! Kwa kusema hivyo atakuwa amekataa kuchukua mzigo wako wa kukunyoa?.
Na wokovu wa Yesu ni hivyo hivyo, ukitaka kupona, sharti ukubali gharama za wokovu. Ukikwepa gharama utakufa na dhambi zako.(Yohana 8:24).
Swali 06: Paulo kamtabiri Mohamed kupaa mpaka mbingu ya tatu 2Wakorintho 12:2, Mohamed ndiye pekee aliyefika mbingu ya tatu, Yesu hakufika huko.
Jibu: Si Mohamed aliyenyakuliwa mpaka mbingu ya tatu bali ni Paulo mwenyewe. Na Paulo aliishia hiyo mbingu ya tatu tu! Na si zaidi, lakini Bwana Yesu alifika mpaka mbingu za mbingu..ambazo hakuna aliyefika hata mmoja.
Yohana 3:13 “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”.
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa…”
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa…”
Swali 07: Je Bwana Yesu alikuwa ni Mungu au Mwanadamu? Maana biblia inasema alikuwa ni mtu! (Matendo 2:23)
Jibu: Bwana Yesu alikuwa ni Mungu kamili katika mwili wa kibinadamu, kutimiza kusudi Fulani maalumu,
Ukivaa vazi la kiaskari na kwenda kutimiza majukumu yako ya kiaskari, utaitwa askari na vile vile utafungwa na sheria za kiaskari, lakini hiyo haikufanyi wewe usiendelee kuwa mkurugenzi katika kampuni lako uliloliacha huko nyumbani, Au haikufanyi wewe usiendelee kuwa kiongozi katika Mtaa wako au mji wako.
Na Mungu alipouvaa mwili wa kibinadamu ulioitwa Yesu, ilikuwa ni lazima aitwe mtu! kwa kitambo lakini hiyo bado bado haimfanyi asiendelee kuwa Mungu.
Tito 2:13 ”tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu”
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
KWANINI MITUME WAMUULIZE BWANA FARAGHANI?
Ni yupi aliyekuwa mkwe wa Musa kati ya Reueli na Yethro?
Kama Mungu ndiye kaumba kila kitu, je ni yeye huyo huyo ndiye aliyeumba dhambi pia?
Rudi Nyumbani
Tunguja ni aina ya mmea ambao haupatikani kirahisi, mmea huo una mizizi ambayo inakuwa na umbile kama la mtu.
Kutokana na maumbile hayo ya mizizi ya mmea huo, kufanana na maumbile ya mwili wa mwanadamu, watu wa zamani na hata wa sasa baadhi, huamini mmea huo unabeba nguvu fulani za kiungu.
Hivyo ulitumika na wachawi katika kazi za kichawi na wasio wachawi kwa matumizi mengine ya kiimani, kama leo watu wanavyotumia mti wa muarobaini kwa matumizi mbalimbali.
Katika biblia tunamsoma Raheli, ambaye wakati fulani aliamini mizizi ya mmea huo inaweza kumpatia mtoto siku za mbeleni.
Hivyo wakati fulani Rubeni mtoto wa dada yake alipokuwa shambani aliuona mmea huo (Mtunguja). Na kuuchimbua mizizi yake, na kwenda kumpatia mama yake (Lea).
Lakini Raheli (ambaye hakuwa na mtoto) alipoona kuwa Rubeni mtoto wa dada yake kamletea mama yake tunguja ambazo alikuwa anazihitaji sana, ili zimsaidie kupata mtoto, alikwenda kumwomba dada yake baadhi ya hizo, ili zimsaidie kupata uzao.
Lakini dada yake alikataa kumpa, lakini akamwambia kama anazitaka, basi amwuzie haki ya Yakobo kulala kwake siku hiyo badala ya kulala na Raheli.(Kwasababu ilikuwa ni zamu ya Yakobo kulala kwa Raheli siku hiyo na si kwa Lea). Yakobo alikuwa anaenda kwao kwa zamu.
Na kwasababu Raheli ana uchu wa kupata mtoto, akahamisha tumaini lake lote kwa Mungu na kulipeleka kwenye zile Tunguja, kwamba ndio zitamsaidia kupata mtoto.
Hivyo akauza haki yake ya kukutana na Yakobo siku hiyo, na kumpa dada yake, na yeye kuchukua zile tunguja.(Aliuza haki yake hiyo kama vile Esau alivyouza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo ndugu yake kwasababu ya chakula kimoja tu).
Na matokeo ya Raheli kufanya vile hayakuwa mazuri, kwani badala ya yeye kupata mtoto, dada yake akapata watoto wengine watatu zaidi.
Mwanzo 30:14 “Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao. 15 Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao. 16 Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule. 17 akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano. 18 Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari. 19 Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita. 20 Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni. 21 Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina”
Mwanzo 30:14 “Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.
15 Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao.
16 Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule.
17 akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano.
18 Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.
19 Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita.
20 Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.
21 Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina”
Hiyo inatufundisha nini?
Siku zote ahadi za Mungu ni thabiti, akisema au akiahidi basi atatimiza alichokisema.
Lakini uvumilivu unapotushinda na kuamua kutafuta njia nyingine mbadala ya kulazimisha kupata jambo ambalo tayari Mungu alishatuahidi na kutuambia tungoje, basi tunajipoteza wenyewe au ndio tunavyozidi kukikawisha kile kitu kufika.(www wingulamashahidi org).
Siku ile Yakobo alipotoka shambani pengine ndio ilikuwa siku ya Raheli kupata ujauzito, lakini shetani alimshawishi na kuhamisha imani yake kwenda kwenye mimea inayotumika na wapagani, na mwishowe Mungu akamsikia dada yake badala yake yeye, kama alivyomsikia Yakobo badala ya Esau, ikampelekea Raheli kusubiri tena miaka mingine mingi (na tunguja zake hizo hazimkusaidia chochote).
Mpaka Mungu alipomhurumia tena kupenda kumpa uzao (www.wingulamashahidi.org)
Hivyo na wewe dada/mama unayetafuta uzao sasa.. Bwana amekuahidi atakupa mwana, usianze kutanga tanga kwa waganga wa kienyeji, kuwa mvumilivu, subiri.. kwasababu kwa kutanga tanga, usidhani kwamba ndio utaharakisha uzao wako uje!..badala yake ndio utauchelewesha kabisa au hata kuupoteza.
Kadhalika na mambo mengine yote!, Ikiwemo mali na afya..hatuyapati kwa kufuata maagizo ya waganga wa kienyeji, au kupiga ramli, au kutambika Au tunguli..tutayapataa kwa sisi kuzishikilia ahadi za Mungu na kuziamini na kuziishi.
Bwana atubariki.
Maran atha!.
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.
YUKO WAPI MFALME WA WAYAHUDI?
SWALI: BWANA YESU asifiwe mtumishi, mistari hii inanichanganya nisielewe vizuri, Neno la Mungu linasema;
Hesabu 23:19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Hapa biblia inasema hasemi uongo Wala hajuti, lakini ukisoma tena hapa inasema
1 Samweli 15:11 Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.
Nashindwa kuutambua ukweli Ni upi?
JIBU: Ukweli ni kwamba Mungu HAJUTI..Isipokuwa kuna wakati anajiweka katika mazingira ya kibinadamu ili tuzielewe hisia zake vema.
Na ndio maana mahali pengine utaona anazionyesha kazi zake kama vile zinamapungufu fulani, hazijakamilika..mpaka anatumia neno SI VEMA huyu mtu aishi peke yake nitamfanyia msaidizi, kana kwamba hakuliona hilo tangu mwanzo, lakini ukisoma mwanzoni kabisa katika kitabu cha Mwanzo 1:27 inatuambia tayati alishamuumba mwanaume na mwanamke katika mawazo yake..lakini katika utekelezaji anajifanya kama kasahau, ndio hapo anakuja kumuumba mwanamke baadaye sana baada ya uumbaji wote kukamilika Mwanzo 2:8..
Hiyo ndio tabia ya Mungu. Anajiweka hivyo wakati mwingine ili kutufundisha sisi jambo.
Mara nyingine anajifanya kama hana mashauri bora ya kumzidi mwanadamu..utakumbuka kule jangwani Musa alimshauri Mungu aghahiri mawazo yake..lakini haimaanishi kuwa Mashauri yetu ni zaidi ya Mungu. Soma Kutoka 32:9-14
Halikadhalika hapa..anasema..yeye si mwanadamu hata ajute..ikiwa na maana mipango yake yote tayari alishaiona mwisho wake utakuwaje tangu mwanzo..kwamba huu utaishia katika uzuri au huu utaishia pabaya..kwamfano alipomuumba shetani, alijua kabisa ataasi, na atawapoteza malaika na wanadamu wengi..lakini akamuumba hivyo hivyo..
Hata sasa Mungu anajua kabisa mwisho wa kila mwanadamu na kila jambo..kwamfano katika habari hiyo ya Sauli..Mungu alijua atakuja kukengeuka huko mbeleni..lakini alimpa bado ufalme..
Na alipokuja kukengeuka kweli, ndio tunaona Mungu anamwambia Samweli najuta kwanini nimechagua Sauli awe mfalme..kuonyesha tu hisia zake juu ya Sauli ili sisi wanadamu tumuelewe. Lakini alifahamu kila kitu.
Halikadhalika hata sasa mambo kama hayo Mungu anayafanya rohoni, .Mungu kukusifia leo haimaanishi kuwa ndio tiketi ya mbinguni moja kwa moja…Mungu kukutia mafuta sasa na kuwaacha wengine, haimaanishi kuwa wewe ndio kipendwa cha Bwana, hata ukifanya dhambi atakusitiri tu siku ile kisa ni kuhani wake.
Ukweli ni kwamba wapo watu ambao wataishia kuwa manabii wa uongo, wengine wapinga-kristo, na jehanamu wataenda..lakini ushuhuda wa wito watakuambia ni Yesu mwenyewe alinitokea na kunituma..Akanipa na ishara za miujiza, lakini wanaishia motoni
Mathayo 7:21-23 [21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. [22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? [23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Swali ni je…umempa Kristo maisha yako na kusimama kweli kweli? Unahabari kuwa Karama pekee sio uthibitisho kuwa Mungu yupo na wewe? Wakati wowote anaweza kujutia na kughahiri huo wito wako, aliokupa kama unasua sua
Kama hujasimama imara, fanya hivyo sasa. Mgeukie muumba wako kwa kumaanisha kwasababu, kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi
Bwana akubariki.
Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)
THAWABU YA UAMINIFU.
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?
JE! NA SISI NI SHABA ILIAYO NA UPATU UVUMAO?
Nini maana ya kupiga Kite! Katika biblia.
Neno kupiga kite limeonekana mara kadhaa katika biblia.
Maana ya “kupiga Kite” ni kutoa pumzi nje, kuashiria aidha kushangazwa, kupata unafuu au kukata tamaa.
Kwamfano mwanafunzi aliyekuwa anasubiria matokeo ya mtihani alioufanya, na wakati anaangalia matokeo kwenye orodha na kuona amefaulu basi unaweza kuona anashusha pumzi. (Kitendo hicho cha kushusha pumzi, kana kwamba kapunguza presha ndani yake, kitendo hicho ndicho kinachoitwa kupiga Kite).
Au mtu aliyejaribu kufanya jambo fulani kwa muda mrefu, asifanikiwe na kuazimia kujaribu kwa mara moja ya mwisho, kama tumaini lake la mwisho, na wakati anangojea kupata tumaini zuri, ghafla yanakuja matokeo mabaya ya kuvunja moyo, mtu wa namna hiyo pia utaona anashusha pumzi, kuashiria kukata tamaa (kitendo hicho pia ni kupiga kite).
Limetumika neno “kupiga” na sio “kufanya”...kwasababu matendo hayo ya kuvuta pumzi au kutoa, yanatamkwa kwa kuanza na neno “kupiga”..kwamfano “kupiga miayo”, huwezi kusema “kufanya miayo”.
Katika biblia Neno hilo limeonekana mara kadhaa.
Maombolezo 1:11 “Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamaniko yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge”.
Pia,
Maombolezo 1:4 “Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu”.
Unaweza kusoma pia 9, utaona Neno hilo hilo.Unaweza kusoma pia Maombolezo 1:21, na Zaburi 90:9 , utaona Neno hilo hilo.
Je umemwamini Bwana Yesu?..kumbuka ulimwengu huu unapita na mambo yake yote, miaka yetu inapukutika kama kite, anaanza na matumaini inaishia na huzuni na kukata tamaa, lakini kama tukiwa ndani ya Yesu itaanza na huzuni lakini itaishia na furaha.
Zaburi 90:9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
TAFUTA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KWA HUDUMA MUNGU ALIYOIWEKA NDANI YAKO.
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
Podo ni kimfuko au kibegi kidogo aidha cha ngozi au malighafi nyingine, ambacho hutumika kubebea mishale.
Utalisoma Neno hilo katika vifungu hivi;
Mwanzo 27:1-3[1]Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.[2]Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.[3]Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
Soma pia Ayubu 39:23, Isaya 49:2, Yeremia 5:16
Lakini Hiyo inafunua nini rohoni? Sikuzote askari makini huwa habebi mchale mmoja anapokwenda vitani..atahitaji Furushi la mishale kujihakikishia ushindi wake dhidi ya adui zake. Na ndio hapo atahitaji podo la kuihifadhia hiyo mishale yake.
Ni kama mwanajeshi, hawezi kutegemea risasi moja kujihakikishia ushindi atakuwa na mkanda wa risasi, ili adui yake ajapo amshindilie vya kutosha..
Halikadhalika na sisi kama wakristo, hatuna budi kuwa na podo zetu zenye mishale mingi ya kumpiga yule adui.Hatumpigi shetani kwa maombi tu peke yake, vinginevyo tutakwama mahali.. tutampiga kwa mshale wa kuhibiri injili pia, kwa mshale wa kutenda matendo mema, kwa mshale wa kumtolea Mungu sadaka, kwa mshale wa kuwasaidia wenye uhitaji, kwa mshale wa utakatifu n.k.
Hapo ndipo tutakuwa tumezijaza podo zetu silaha.
Embu soma kwa makini vifungu hivi;
Zaburi 127:4-5[4]Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.[5]Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.
Nasi tujitahidi kujaza podo zetu silaha nyingi ili shetani asipate upenyo wa kutushambulia kirahisi.
Bwana akubariki
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?
Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).
KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.
Mjoli ni mfanyakazi-mwenza, Ni mtu unayefanya naye kazi moja inayofanana.. Kwamfano kama wewe ni mwalimu, ukakutana na mwalimu mwenzako huyo ni mjoli wako…Kama wewe ni mhubiri ukakutana na mhubiri mwenzako huyo ni mjoli wako, kama wewe ni mkulima ukakutana na mkulima mwenzako huyo ni mjoli wako..
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia..
Mathayo 18:23-35[23]Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.[24]Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talantaelfu kumi.[25]Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.[26]Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.[27]Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.[28]Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinarimia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.[29]Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.[30]Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.[31]Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.[32]Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;[33]nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?[34]Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.[35]Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Wafilipi 4:3[3]Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Soma pia..Wakolosai 1:7 ,4:7, Ufunuo 19:10, 22:9.
Vivyo hivyo na sisi watakatifu ulimwenguni kote tuliookolewa na Yesu Kristo, kila mmoja ni mjoli kwa mwenzake. Hivyo hatuna budi kupendana, kutumikiana, kusameheana.. Maadamu tupo katika shamba moja na kazi moja, tunapaswa kuujenga ufalme wa Mungu kwa nguvu zetu zote. Huku tukizingatia misingi ya Biblia, na sio ya kidhehebu au kidini
Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?
Makuruhi ni nini, kama tunavyosoma katika biblia?
JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.
EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.