Ni kwanini Bwana Yesu amefanyika kuwa ishara itakayonenewa?..Nini maana ya kunenewa?.
Luka 2:34 “Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa”.
Kunenewa kunakozungumziwa hapo sio “kenenewa vizuri” bali “kunenewa vibaya”.
Wana wa Israeli, walitegemea Masihi atazaliwa katika jumba la Kifalme, ataishi maisha ya kifahari, atakuwa mkuu na Mfalme ndani ya muda mfupi sana. Na atakuwa na fahari kuliko Sulemani, na zaidi ya yote atakuwa hafi, anadumu milele.
Ndicho walichokuwa wanategemea, kukiona kwa Masihi atakayekuja.
Lakini alipokuja Masihi mwenyewe (yaani Yesu) na kuona kwanza anazaliwa zizini na si kwenye jumba la kifalme kama walivyopanga, wakapata mashaka.
Walipomwona anakula na kunywa na watu maskini tena wenye dhambi mashaka yakaongezeka zaidi.
Lakini zaidi ya yote waliposikia kwamba eti atakufa na kufufuka, ndio kabisa wakasema huyu sie!.
Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. 33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa. 34 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?”.
Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa.
34 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?”.
Hivyo walikuwa wanazitafuta ishara kuu…katika vichwa vyao walikuwa wameshajiaminisha kuwa Masihi atakuwa kama Malaika-Mtu hawezi kufa, na atakuwa ameshika fimbo ya chuma kuyatiisha mataifa na wakati anazaliwa tu atakuwa tajiri.
Hivyo Ishara hiyo ya Ukuu uliopitiliza hawakuiona kwa Masihi, na kinyume chake masihi akaja kwa nyingine tofauti kabisa na ishara yenyewe ni ISHARA YA YONA.
Kikawaida hakuna mtu angependwa kufananishwa na Yona. Hakuna mtu anayevutiwa na tabia ya Yona, wala hakuna mtu anayetamani kuwa kama Yona, kwasababu ishara ya Yona sio nzuri.
Lakini Masihi aliichagua ishara hiyo badala ya ishara ya Ukuu na ufalme, Na kwa ishara hiyo ikawafanya watu kumnenea vibaya kama walivyomnenea nabii Yona.
Mathayo 12:38 “Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. 40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi”.
Mathayo 12:38 “Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.
39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi”.
Tukio la Yona kukaa tumboni kwa samaki siku tatu, leo hii linaonekana kama la kipumbavu, lakini pasipo ile ishara watu wa Ninawi wasingetubu!..wangedhani Yona kajizukia tu na kuanza kuhubiri habari zake, lakini waliposikia kuwa alikaa tumboni siku tatu bila kufa, wakatafakati alipataje pataje hewa akiwa kule tumboni muda wa siku tatu, alikaajekaaje bila kufa kule, wakaogopa, wakajua ule ni uweza wa Mungu.
Hivyo wakatubu kwa ishara hiyo, lakini endapo Yona angetoka moja kwa moja Israeli na kwenda Ninawi bila ishara yoyote, watu wa Ninawi wasingemsikiliza.
Na hata leo ni hivyo hivyo, Masihi alipenda kuchagua njia ya Mauti kama ishara kuu, ili sisi tuzidi kumwamini.
Hebu tafakari angekuja tu na kuishi na kisha kupaa bila kufa, tungeaminije kwamba mtu akifa anaweza kufufuka tena?. Hivyo ilibidi na yeye afe, azikwe na kisha afufuke ili sisi tuuone uweza wa kiungu uliopo ndani yake, na kupitia huo Umetufanya kumwamini yeye mara nyingi zaidi na vile vile kuleta mazao mengi zaidi kwake.
Yohana 12:23 “Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. 24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.
Yohana 12:23 “Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.
24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.
Swali ni je! Na wewe leo umemwamini Bwana kupitia Ishara hiyo Ya kufa na kufufuka kwake? Je unaineneaje hiyo ishara..unainenea vyema au vibaya?, Unamtazama Kristo kwa jicho gani leo?.
Unamtazamia Kristo yule wa kukupa majumba na magari ya kifahari, au unamtazamia yule aliyekufa kwaajili ya dhambi zako, yule anayekwambia utubu! Kristo wa kweli anasema hivi.
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. 35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. 36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? 37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”
Utatoa nini ili ujitoe kuzimu siku ile?, kwa uasherati unaoufanya?, Kwa ulevi unaoufanya, kwa wizi unaoufanya?..fedha hazitakutoa kuzimu siku ile, vile vile mzazi hatakutoa kuzimu, wala mpenzi, wala Raisi.
Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa. 10 Hatarudi tena nyumbani kwake Wala mahali pake hapatamjua tena”.
Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
10 Hatarudi tena nyumbani kwake Wala mahali pake hapatamjua tena”.
Mpokee leo Yesu akufanye kiumbe kipya, na ya kale yote yatakuwa yamepita, na atakufanya kuwa mpya.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
YONA: Mlango 1
YONA: Mlango wa 2
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
YONA: Mlango wa 4
MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Watu hawa ni miamba yenye hatari”. Hii miamba yenye hatari ni ipi?
JIBU: Tusome..
Yuda 1:12 “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa; 13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele”.
Yuda 1:12 “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;
13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele”.
Hapa ni mtu Yuda alikuwa anawalinganisha wachungaji na mitume wa uongo kama miamba yenye hatari.
Sasa miamba inayomaanishwa hapo, si hii miamba tuionayo nchi kavu, hapana, bali ni ile miamba ya habarini ambayo baadhi yao inatabia ya kuchomoza juu hadi karibu na usawa wa bahari. Miamba hii ni hatari sana kwa mabaharia, kwasababu huwa haionekani, lakini meli inapopita karibu nayo, inaichana, kama sio kuiharibu kabisa na matokeo yake, ni aidha meli kugotea palepale, au kuzama kabisa.
Kama mabaharia wasipokuwa waangalifu, kwa kupita njia zilezile walizozithibitisha ni rahisi sana kukutana na hii miamba na kuzipoteza meli zao moja kwa moja.
Sasa hapo anaposema “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu”;
Anamaanisha, wachungaji hawa, au watumishi hawa wa uongo ni ngumu kuwatambua, kama tu vile miamba hii hatari ilivyo ngumu kuiona habarini, pale ambapo Habari inaonekana shwari na tulivu yafaa kwa kusafiria kumbe ndipo ilipojifichia, halikadhalika, watumishi hawa wa uongo, mahali ambapo mpo katika karamu zenu za Upendo, yaani wakati ambapo mnamfurahia Mungu wenu, mnatangaza Habari njema, mkidhani kuwa wapo na nyie, kumbe ni mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo.
Mfano wa watu hawa alikuwa ni Yuda,alitembea na Bwana Pamoja na mitume wengine, lakini haikuwa rahisi kumgundua, hadi dakika ya mwisho, utaona alipokuwa katika mlo wa jioni, kama mpelelezi, hakuna aliyemtambua isipokuwa Bwana tu peke yake.
Mtume Paulo aliliona hilo hata wakati wa kuondoka kwake akasema..
Matendo 20:29 “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; 30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”.
Matendo 20:29 “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”.
Hadi sasa, inasikitisha kuona watumishi wa namna hii wapo wengi katika kanisa la Mungu, ,hawaoni shida kuwadanganya watu, wengine ni wachawi, wengine ni matapeli, wengine wapo kwa lengo la kuzivuruga tu kazi za Mungu, ili watu watusiishi Maisha matakatifu, hawawahurumii watu wanaotaka kumjua Mungu, lakini cha ajabu ukiwaangalia kwa nje, wanalitaja jina la Yesu, wanaongoza makanisa, wanashiriki katika kampeni zote za kidini.
Huu ni wakati wa kuwa makini sana, Ni wakati ambao wewe kama mkristo, kuondoa uvivu wa kusoma biblia, tunadanganywa kwasababu hatuna maarifa ya kutosha kuhusu Mungu wetu na utendaji kazi wake. Hatuwezi kumshinda shetani kwa maneno tu, au kwa kumkemea, tutamshinda shetani kwa lile Neno lililokaa ndani yetu kwa wingi, ndiyo silaha ambayo Bwana Yesu aliitumia kumshinda shetani pale alipokuwa anajaribiwa nay eye kule jangwani.
Vinginevyo tukiyaendesha Maisha yetu hivi hivi tu kwa jinsi tunavyotaka, tujiandae kukutana na hii miamba yenye hatari, isiyoonekana. Tukiwa wavivu kujifunza biblia, hakuna namna tutamkwepa shetani, hakuna namna.
Bwana atusaidie.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
Tusome,
1 Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.
Awali ya yote ni muhimu kufahamu maana ya neno “kusitiri” na vile vile ni muhimu kufahamu ni nani ambaye anayesitiriwa dhambi zake, je! ni yule anayependa au anayependwa?.
Neno “kusitiri” maana yake “kufunika au kuficha”..mtu aliyevaa nguo za kuufunika mwili wake wote, maana yake “kavaa nguo za kujisitiri mwili wake, ili asibakie kuwa tupu”. (Kauficha mwili wake).
Sasa tukirudi kwenye huo mstari wa kwenye 1Petro 4:8, maandiko yanasema upendano husitiri wingi wa dhambi.
Sasa dhambi zinazositiriwa/kufichwa si za yule anayependa bali yule anayependwa. Sasa zinasitiriwa kwa namna gani?
Neno la Mungu linasema katika kile kitabu cha 1Wakorintho 13:4-5.
1 Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; Mwisho kabisa anasema “UPENDO HAUHESABU MABAYA”.
1 Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; Mwisho kabisa anasema “UPENDO HAUHESABU MABAYA”.
Kutokuhesabu mabaya ndio “Kusitiri dhambi”.
Maana yake ni kwamba mtu mwenye upendo, maisha yake yote ni ya kusamehe tu na kutoweka kumbukumbu ya mambo mabaya anayofanyiwa.
Mathayo 18:21 “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini”.
Mfano mzuri wa Mmoja aliyeweza kusitiri wingi wa dhambi nyingi, ni Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe.
Kwa Upendo wake mwingi alijitoa nafsi yake sadaka ili sisi tupate kusitiriwa dhambi zetu. Kwake yeye tumepata ondoleo la dhambi. Tukiwa dhani yake hatuhukumiwi.
Mtume Paulo anazidi kuliweka wazi hilo katika kitabu cha Warumi.
Warumi 4:7 “Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao. 8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi”.
Warumi 4:7 “Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.
8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi”.
Je na wewe leo dhambi zako zimesitiriwa na kuondolewa kabisa?? Kumbuka dhambi zako haziwezi kuondolewa kama haupo ndani ya pendo la Kristo, kwasababu ni upendo tu ndio unaositiri wingi wa dhambi, maana yake kama haupo ndani upendo wa Kristo, basi hauna msamaha wa dhambi.
Sasa utauliza, unaingiaje katika pendo hilo na kupata msamaha?.
Unaingia katika pendo hilo kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa jina la Yesu Kristo na kumpokea Roho Mtakatifu.
Baada ya hapo dhambi zako zote zitaondolewa na kuwa mrithi wa ahadi za Mungu.
Na vile vile unapowahubiria wengine habari za Pendo la Kristo, na hata wao wakaingia katika pendo hilo, (kwa kutubu na kuacha dhambi)basi utakuwa umewasaidia dhambi zao kufunikwa na pia kuwaokoka na adhabu ya ziwa la moto, sawasawa na maandiko yafuatayo.
Yakobo 5:19 “Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;
20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Bwana atubariki sote.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
JE UPENDO WAKO UMEPOA?
UPENDO WA MUNGU.
UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;
Katika biblia ukiona neno “mwandamo wa mwezi”, au “mwezi mpya”, ujue ni neno lile lile moja linalomaanisha “siku ya kwanza ya mwezi”.
Katika agano la kale siku hii iliheshimiwa na kufanywa kama mojawapo ya siku takatifu, kama tu vile ilivyokuwa siku ya sabato, ambayo ni siku ya saba. Vivyo hivyo kila siku ya kwanza ya mwezi mpya, tarehe moja (kwa kalenda ya kiyahudi), ilikuwa ni takatifu kwao, na ni lazima watu wakamtolee Mungu sadaka za kuteketezwa, Sadaka za unga na vinywaji, Pamoja na kupiga tarumbeta juu ya sadaka hizo, (Hesabu 28:11-15), .Vilevile hukuruhusiwa kufanya shughuli yoyote au biashara yoyote(Nehemia 10:31-33)
Hesabu 28:11 “Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; 12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja;”
Hesabu 28:11 “Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;
12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja;”
Hesabu 10:10 “Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu”.
Lakini kuna wakati wayahudi, walizifanya sikukuu hizo kama mazoea tu, wakawa hawazitoi katika utakatifu, bali kama agizo tu la kidini na huku nyuma mioyo yao ipo mbali na Mungu, hivyo hiyo ikamfanya Mungu akasirishwe nao na hatimaye kuzitaa sikukuu zao hizo za mwandamo wa mwezi.
Isaya 1:13 “Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. 14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua”.
Isaya 1:13 “Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua”.
Neno hili utalisoma pia katika vifungu hivi;
Zaburi 81:3 “Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu”.
1Samweli 20:5 “Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hata siku ya tatu jioni.
Soma pia, 2Nyakati 2:4, 8:13, Ezra 3:5, Hosea 2:11.
Jibu ni la! Kama tu vile hatujapewa takwa la kuitunza sabato kama sheria , vivyo hivyo, na katika mwandamo wa mwezi mpya.
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; 17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo”.
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo”.
Ni kwamba tuthaminishe nyakati zetu mpya kwake. Wiki yako inapoisha na kuanza nyingine bila kumfanyia Mungu wako ibada, ni hatari kubwa sana, kama kwako ni jumapili, au jumamosi, ndio unamfanyia Mungu ibada, hakikisha unakutanika na wengine, kumwabudu Mungu wako, usiruhusu wiki yako ipite hivi hivi tu.
Halikadhalika, mwezi wako mpya unapoanza, usianze hivi hivi tu, bali chukua muda kwenda kumshukuru Mungu nyumbani kwake, ni muhimu sana. Ukiona wiki yako inapita hivi hivi tu, mwezi wako unapita hivi hivi tu, mwaka wako unapita hivi hivi tu, huna Habari na Mungu. Angalia Maisha yako ni lazima yatakuwa na kasoro Fulani tu.
Hivyo tujitahidi sana, tusiwe na mapengo pengo kwa Mungu wetu.
Bwana akubariki.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?
MWEZI WA ABIBU/NISANI NI MWEZI GANI?
WhatsApp
Huu mstari una maana gani?
Zaburi 91:1 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi”.
Maandiko hayo yanatuonyesha kumbe Mungu anao uvuli wake. Na uvuli huo hawakai watu wote ilimradi tu, bali wale tu wanaokaa katika mahali pake pa siri.
Sasa swali utajiuliza huko mahali pake pa siri ni wapi?
Kuna madaraja ya kumfikia Mungu, yapo yanayofikiwa na wakristo wa kawaida tu, wale wanaomtafuta Mungu jumapili kwa jumapili, au mwezi kwa mwezi, lakini pia yapo yanayofikiwa na wakristo waliojikana, na kudhamiria kumfuata Kristo katika Maisha yao.
Hao wanaojikana ndio wanaofikia mahali pa siri pa Mungu.
Wanafananisha na makuhani, ambao, katika ile hema ya kukutania, au hekalu la Mungu, ni wao tu walikuwa na uwezo wa kupaingia patakatifu, na kule patakatifu pa patakatifu, palipo na kile kiti cha rehema cha Mungu.Kumbuka si kila mwisraeli, alifika pale, si kila mtu anayejiona anamcha Mungu aliweza kufika pale, kwa mtu wa kawaida ukijitahidi sana, uliishia katika ule ua wa hema ya kukutanikia, lakini ndani, sehemu za siri za Mungu walioweza kuingia makuhani tu.
Vivyo hivyo katika agano jipya, Mungu anao sehemu yake ya siri, na ni watu baadhi tu wanaoweza kufika huko, Mfano hai katika biblia ni mwanamke kama ANA, yeye, aliweza kupafikia hapo..na ndio maana alikuwa miongoni mwa watu wachache sana waliofunuliwa mpango wa Mungu wa wokovu,yaani kuja kwake Yesu duniani..
Lakini hiyo yote ni kwasababu alikuwa ni mwanamke aliyeupoteza ubinti wake, autumie kwa Mungu hadi uzee wake, haundoki hekaluni, mchana na usiku akisali na kufunga.
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”.
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”.
Mwingine, ni Simeoni, naye pia biblia inasema alikuwa ni mtu wa haki, na anaye mcha Mungu, tena Zaidi alikuwa anautazamia wokovu wa taifa lake Israeli, yaani wakati wayahudi wapo bize na mali na fedha, yeye alikuwa kama Danieli, akiomba na kutafuta Habari za kuja kwa masihi duniani.
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, 29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; 30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako”,
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako”,
Makundi ya watu kama hawa, huwa wanaonjeshwa kitu kingine tofauti na watu wa kawaida, huo ndio uvuli wake Mungu. Wanapewa mafunuo ya ndani sana, wanapewa ulinzi wa majeshi ya Malaika wengi,mfano Elisha, wanajaliwa haja za mioyo yao na Mungu. Kwasababu tayari wapo chini ya uvuli wake.
Je! Na sisi tunaweza kufikia mahali hapo?
Kama jibu ni ndio,
Basi hatuna budi, kufanana na makuhani wa Mungu kweli, wana wa Lawi, ambao wametengwa na dhambi na unajisi, Si tu kumkiri Kristo na kuendelea kuishi Maisha ya juu juu, bali tujikane na nafsi zetu pia kwake, yaani tuwe tayari kujitwika na misalaba yetu tumfate Kristo. Tukubali ulimwengu utupite na mambo yake yote.
Na kwa kufanya hivyo kwa neema zake, atatufikisha mahali pake pa siri.
Bwana atusaidie sote.
Amen.
Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?
Ni SIRI gani Paulo aliyokuwa anaimaanisha katika Waefeso 5:32?
Barazani pa Mungu ni wapi? Kama tunavyosoma katika Yeremia 23:18?
Bwana alimaanisha nini aliposema mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu?
Neno Bushuti limeonekana mara moja tu katika biblia, na maana ya Neno hilo ni “Blanketi”.
Waamuzi 4:18 “Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti”.
Kipindi Sisera, Adui wa wayahudi anamkimbia Baraka, alifika kwenye nyumba ya mwanamke mmoja aliyeitwa Yaeli, na mwanamke huyu alimlaghai kwa hila na kumwua.
Kabla ya kumwua maandiko yanasema alimlaza na kumfunika kwa hilo Bushuti (yaani blanketi), na alipopata usingizi alimwua.
Habari hiyo kamili inapatikana katika mlango wa 4 wa kitabu hicho cha Waamuzi.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
THAWABU YA UAMINIFU.
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
LIFAHAMU SANA JAMBO HILI, ILI MUNGU AKUTUMIE.
Jeshi la Mbinguni wana wa Israeli waliloliabudu ni lipi?
HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE
Mithali 15:10a “Adhabu kali ina yeye aiachaye njia;..”.
Mapigo ya Mungu yanatofautiana na mtu na mtu.. Tofauti na tunavyodhani kuwa muuaji ndiye atakayeadhibiwa sana siku ile kuliko mtu aliyeuacha wokovu.
Jibu la la! Maandiko yanatuambia, “Adhabu kali ina yeye aiachaye njia”, hasemi tu ‘adhabu’ ina yeye aichaye njia, hapana, bali adhabu KALI..
Bwana Yesu alirudia , maneno hayo hayo tena katika
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. 48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na Zaidi”.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na Zaidi”.
Leo hii inasikitisha kuona kuwa watu wengi wanakiri kwa vinywa vyao kuwa wameokoka, lakini kimatendo wapo mbali na Kristo, hawa wote ni kundi la wakristo walioicha njia, au waliojua mapenzi ya Bwana wao lakini wasiyafanye, wanaojua kuwa kutazama pornography hakumpendezi Mungu, lakini wanatazama, kuishi na mume/mke ambaye si wako ni dhambi mbele za Mungu lakini wao bado wanaendelea kuishi nao, tena wanazaa nao,
Wanaojua, kabisa kuvaa nguo za nusu uchi, na kujichubua ni dhambi, lakini bado wanaendelea kufanya mambo kama hayo,. Wachungaji na watumishi wanaojua kabisa, uasherati ni kosa kubwa sana kwa watu kama hao, lakini sasa imeshakuwa desturi yao. Hao ndio Kristo anaowazungumzia kuwa watakuwa na adhabu kali sana kule kuzimu.
Ndugu yangu, mateso yaliyopo kule, usidiriki kuyapima kwa akili zako, ni mahali ambapo hata hao wanaoteswa huko hawatamani, kukuona mtu kama wewe umefika huko, ni mateso makali sana, yasiyoelezeka, soma (Luka 16:27-29).
Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya;
Marko 9:45 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; 48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.
Marko 9:45 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [
46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.
Ndugu,unaposikia injili halafu huitendei kazi, ujue kuwa inageuka na kuwa adhabu kwako, na kwa jinsi unavyoendelea kuisikia ndivyo unavyojiongezea mapigo. Yathamini Maisha yako ya rohoni, siku hizi ni za mwisho, Unyakuo ni wakati wowote, Bado hujui siku zako za kuishi hapa duniani zimebakia ngapi, sikuzote kifo huwa kinakuja ghafla tu, hakina hodi je! Mimi na wewe tumejiandaaje? Kwa injili zote hizi tulizozisikia?
Ni heri tuyasalimishe Maisha yetu kwa Bwana leo, atuokoe, na kutufungua, tumaanishe kabisa kumfuata yeye bila lawama yoyote, tuweke kando mambo ya ulimwengu yanayopita, tuutafute utakatifu kwa bidii, kwasababu pasipo huo kamwe mbingu hatutaiona (Waebrania 12:14),
Lakini Ikiwa utatamani kutubu leo, na kuanza Maisha yako upya na Bwana, katika kipindi hichi kifupi tulichobakiwa nacho, basi yeye yupo tayari kukusamehe.. Ukiiomba sala hii fupi ya TOBA, ukiisema kwa Imani, basi utapokea msamaha hapo hapo ulipo.. Hivyo kama upo tayari kuyasalimisha leo Maisha yako kwa Bwana.
Hapo ulipo unaweza kutafuta mahali pa utulivu peke yako, kisha piga magoti, nyosha mkono wako mmoja juu, kama ishara ya kuyasalimisha Maisha yako kwa Bwana. Kisha, ukishakuwa katika utulivu, sema maneno haya, kwa sauti:
BABA YANGU, NAJA MBELE ZAKO, NINAKIRI KUWA NIMEKUWA MWANA MWASI MBELE ZAKO KWA MUDA MREFU, KWA WINGI WA DHAMBI ZANGU, NIMESTAHILI ADHABU NA MAPIGO MAKALI KUTOKA KWAKO, NI KWELI BWANA NILIYAJUA MAPENZI YAKO LAKINI SIKUYATENDA. LAKINI LEO MIMI MWANAO (TAJA JINA LAKO) NIMEDHAMIRIA KUYAANZA MAISHA YANGU UPYA NA WEWE. NAOMBA UNISAMEHE BABA YANGU. KUANZIA LEO NINAACHA NJIA ZANGU MBAYA ZOTE, NINAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE, NINAUKATAA ULIMWENGU. NAOMBA DAMU YA MWANAO YESU KRISTO, UNISAFISHE NA KUNITAKASA KABISA. ASANTE BWANA YESU KWA KUNISAMEHE. KAMA ULIVYOSEMA KATIKA NENO LAKO, YEYOTE AJAYE KWANGU SITAMTUPA NJE KWAKE. NAMI NAAMINI UMENIPOKEA, NA KUNIFANYA KIUMBE KIPYA LEO. NAOMBA UNIPE UWEZO WA KUUSHINDA ULIMWENGU NA KUUISHIA WOKOVU SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU. ASANTE BWANA YESU KWA NEEMA YAKO, NA MSAMAHA WAKO. AMEN.
BABA YANGU, NAJA MBELE ZAKO, NINAKIRI KUWA NIMEKUWA MWANA MWASI MBELE ZAKO KWA MUDA MREFU, KWA WINGI WA DHAMBI ZANGU, NIMESTAHILI ADHABU NA MAPIGO MAKALI KUTOKA KWAKO, NI KWELI BWANA NILIYAJUA MAPENZI YAKO LAKINI SIKUYATENDA. LAKINI LEO MIMI MWANAO (TAJA JINA LAKO) NIMEDHAMIRIA KUYAANZA MAISHA YANGU UPYA NA WEWE. NAOMBA UNISAMEHE BABA YANGU.
KUANZIA LEO NINAACHA NJIA ZANGU MBAYA ZOTE, NINAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE, NINAUKATAA ULIMWENGU. NAOMBA DAMU YA MWANAO YESU KRISTO, UNISAFISHE NA KUNITAKASA KABISA.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNISAMEHE. KAMA ULIVYOSEMA KATIKA NENO LAKO, YEYOTE AJAYE KWANGU SITAMTUPA NJE KWAKE. NAMI NAAMINI UMENIPOKEA, NA KUNIFANYA KIUMBE KIPYA LEO. NAOMBA UNIPE UWEZO WA KUUSHINDA ULIMWENGU NA KUUISHIA WOKOVU SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU.
ASANTE BWANA YESU KWA NEEMA YAKO, NA MSAMAHA WAKO.
AMEN.
Basi ikiwa umeisema sala hiyo ya Imani, fahamu kuwa Mungu anatazama moyo wako, na sio sala tu. Yupo mwanamke ambaye alikuwa na dhambi nyingi, lakini kwa jinsi alivyomaanisha tu mbele za Yesu, kabla hata hajaomba msamaha au kujieleza chochote, muda huo huo Bwana alimwambia “umesamehewa dhambi zako”. Hiyo ni kuonyesha kuwa Toba hasaa haipo katika maneno matupu tu, bali katika moyo.(Luka 7:36-50)
Na wewe pia ikiwa toba yako, imeambatana na kuachana na huyo mume/mke wa mtu, imeambatana na kuacha kutazama picha za ngono mitandaoni milele, imeambatana na kuacha kuishi na huyo girlfriend/boyfriend ambaye hamjaona naye.. Ujue kuwa msamaha kutoka kwa Bwana umeshaupokea.
Hivyo, kuanzia leo, anza kuishi Maisha ya kuukulia wokovu, na kama hukubatizwa unapaswa ubatizwe, Ikiwa utahitaji msaada huo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi 0693036618/0789001312 tutakusaidia kwa neema za Bwana.
Bwana akubariki sana.
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?
Wale Nyoka waliowadhuru wana wa Israeli jangwani walikuwa wana maumbile ya moto au?. Maana maandiko yanasema walikuwa ni Nyoka wa moto, Na kama walikuwa wenye maumvile ya moto, waliwaumaje watu na walitokea wapi? Walishushwa au?
Jibu: Tusome,
Hesabu 21:6 “BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa”
Neno “moto” hapo halijatumika kuelezea maumbile (yaani miili) ya hao nyoka, kwamba wana miili iliyoundwa kwa malighafi ya moto, hapana!. Bali limetumika kuelezea “Rangi” ya hao Nyoka, kwamba wana rangi ya moto.
Rangi ya moto, inafananishwa na rangi ya “Shaba”. Mtu anaposema “sahani ile ni ya shaba” na anayesema “sahani ile ni ya moto” Ni kitu kimoja, wote wanamaanisha kitu kimoja.
Ndio maana baada ya pale utaona Musa anaagizwa atengeneze nyoka wa shaba, kuwakilisha rangi ya hao nyoka.
Hesabu 21:8 “Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. 9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi”.
Hesabu 21:8 “Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi”.
Nyoka hao wenye rangi ya moto, ni jamii ya Nyoka maarufu sana wenye sumu kali wanaopatikana jangwani, hadi leo wapo (Ni nyoka wa asili kabisa), maisha yao ni jangwani tu hawawezi kuishi mahali pengine, na huwa wanajificha chini ya mchanga, na kubakisha sehemu ndogo tu ya kichwa juu, hivyo si rahisi kuonekana. Na endapo mtu akipita na bahati mbaya akakanyaga mchanga mahali ambapo nyoka huyo kajificha, basi aling’atwa na hakukuwa na matibabu.
Hivyo kwa hitimisho, walikuwa ni nyoka wa asili, isipokuwa rangi yao ni ya Moto (au shaba).
Lakini pamoja na hayo kulikuwa na ufunuo mkubwa juu ya tukio hilo lililowatokea wana wa Israeli, na huyo nyoka wa shaba, mpaka akaitwa Nehushtani.
Kwa maelezo marefu juu ya Nehushtani, unaweza kufungua hapa>> NEHUSHTANI.
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
KUOTA NYOKA.
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
UZAO WA NYOKA.
SWALI: Huu mstari una maana gani ?
Mithali 20:12 [12]Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
JIBU: Utajiuliza ni kwanini haijasema “Sikio na jicho” Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili..badala yake inasema ..
Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
Hii ni kuweka msisitizo katika kazi zao jinsi zinavyojitegemea…sikio haliwezi kuona, wala jicho kusikia, kwasababu kila moja limeundiwa mfumo wake tofauti wa kipekee..Lakini kutokufanana kwao haviwafanyi viwe na miungu miwili tofauti..bali ni Mungu yule yule mmoja aliyeviumba vyote.
Hata sasa tunapaswa tutambue kuwa Mungu ni Mungu anayeumba vitu katika mionekano tofauti tofauti..mmoja atamfanya mchina mwingine mwafrika, sio kwamba kuna itilafu au mapungufu katika jamii fulani ndio maana ikawa hivyo hapana.. ndivyo Mungu alivyotaka watu wake wasiwe na mionekano na maumbile yanayofanana, amependa tu iwe hivyo
Vilevile katika Kanisa Mungu ameweka vipawa mbalimbali..mwingine mwinjilisti, mwingine mwalimu, mwingine mchungaji..hata katikati ya hao wainjilisti au manabii bado kawatofautisha wote wasifanane..
Kutokuhubiri kwa kufoka au kwa utulivu kama yule hakukufanyi wewe usiwe na karama ile..
1 Wakorintho 12:4-6 [4]Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. [5]Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. [6]Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Hivyo tuonapo tofauti hizi, ndani ya kanisa lake, au ulimwenguni tusinyoosheane vidole na kusema yule sio Mungu, maadamu tupo katika mstari ule ule wa imani, hatupaswi kushangaa sana au kulazimisha mambo yote yafanane..bali tukumbuke tu huu usemi..
Itambue nafasi yako, Mungu aliyokuchagulia, kisha isimamie hiyo kwa bidii kwasababu vyote ni kwa utukufu wake mwenyewe.
https://wingulamashahidi.org/wp-admin/post.php?post=18939&action=edit#
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
JE! NI DHAMBI KUIMBA WIMBO WA TAIFA?
SWALI: Naomba kuuliza kwamfano mimi ni mkristo mwenye uwezo wa kifedha, nikiombwa kuchangia ujenzi wa msikiti, Je! Ni halali kufanya hivyo?
JIBU: Tumeruhusiwa, kutoa misaada yoyote ile (Isiyokinzana na Neno la Mungu) kama tupendavyo kwa jinsi Bwana alivyotujalia bila kujali dini, Imani, jinsia au rangi, kabila n.k.. Kwamfano ukiombwa kujenga shule, au kutoa chakula, au kufadhili wazee wa Imani nyingine waruhusiwa kufanya hivyo, tena ni vema Zaidi, kwasababu unaonyesha upendo ule wa ki-Mungu kwao, ambao hautoki kwa sababu Fulani.
Lakini ikiwa ni mambo yanayokinzana na Neno la Mungu kama vile kusapoti ujenzi wa kiwanda cha pombe, au kusapoti madhabahu nyingine tofauti na ile ya YEHOVA, tunayemwabudu katika Kristo Yesu, hapo hatujaruhusiwa.
Kwasababu upo uhusiano mkubwa sana kati ya sadaka na madhabahu. Kumbuka kiroho Sadaka ni Ibada kamili.
Mathayo 6:21 “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako”.
Moyo wako hauwezi kuwepo katika kanisa la Kristo, na wakati huo huo uwepo katika msikiti, au katika hekalu la Buddha, au la Baniani ambao mungu wao ni ng’ombe,. Hapo utakachokuwa unakifanya ni uzinzi wa kiroho, unazini na miungu migeni, bila wewe mwenyewe kujijua.
Na biblia inasema Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu. Anatufananisha sisi na wake zake. Mungu hatazami tu pale tunapoisujudia au kuitumikia miungu migeni ndio achukizwe hapana, bali anatazama pia na sadaka zetu tuzitoazo.. Je tunazielekeza wapi? Kwake yeye, au kwa miungu migeni. Hapo tunapaswa tuwe makini sana.
Hivyo, kwa kuhitimisha ni kuwa, sisi kama wakristo, hatupaswi kuchangia ujenzi wa madhabahu za wasioamini. Ukiulizwa ni kwanini? Jibu lako ni kuwa IMANI YAKO HAIRUHUSU. Hivyo tu,
Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?
JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?
Maana Ya Maneno Katika Biblia.
Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)