Tumetazama, wapo watu ambapo siku ile ya hukumu, watalipwa thawabu sawa na wale ambao wameteseke Maisha yao yote katika kumtumikia Mungu. Na kigezo chenyewe kwanini Mungu afanye hivyo, tumeshakiona katika maandiko, ikiwa hujapata uchambuzi wake, tutumie ujumbe, inbox tukutumie..
Tutaendelea, na vigezo cha pili cha thawabu, za Mungu. Hichi tunakisoma katika Mathayo 24:44-51
2) Kwamba wapo watu watawekwa juu ya kazi yote ya Mungu, mbinguni.
Unaweza kujiuliza, Je! Inamaana kuna watu ambao hawatawekwa, juu ya kazi za Mungu siku ile? Jibu ni ndio, twende moja kwa moja katika Habari hii, tuone ni kigezo gani, Kristo anakitumia, katika kutoa thawabu kama hiyo.
Mathayo 24:44 “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. 45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mathayo 24:44 “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.
47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;
49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;
50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Katika Habari hiyo, tunaona, mtu mmoja Tajiri aliondoka bila kutoa taarifa ya lini atarudi, lakini akamwacha mtumwa wake mmoja awe mwangalizi wa watu wake, ahakikishe anawahudumia, pasipo kusimamiwa. Lakini anasema kama mtumwa huyo atadhani kuwa Bwana wake atachelewa. akaanza kuwa mzembe, mara hawapi watu chakula, mara anawapiga, mara anaamrisha vibaya. Siku asiyodhani atakuja, na kumkata vipande vipande.
Lakini akimkuta yupo katika majukumu yake, basi ameahidi, kuwa atamweka juu vitu vyake vyote.
Leo hii kama wewe ni mtumishi wa Mungu, aidha mchungaji, nabii, mwalimu, mtume, mwimbaji, au unafanya kazi yoyote ile ya kuujenga ufalme wa Mungu..Fahamu kuwa Bwana anataka kukuona, wakati wote, muda wote, ukitumika kwa uaminifu katika hiyo kazi, ili siku atakapokujia ghafla (aidha kwa kifo au unyakuo ) akukute katika utumishi wako.
Lakini ukianza kuidharau kazi ya Mungu na kuigeuza kama vile biashara, hutaki kutumika mpaka ulipwe, hutaki kusimamia kundi lako kama mchungaji, unazini na washirika, hutaki kuwafundisha watu kama mwalimu, unaona uvivu wa kuwahubiria wengine Habari njema, kama mwinjilisti, unamgeuza Mungu kama mtu baki, unamtumikia tu pale unapojisikia, ukiwa huna mudi, unaendelea na mambo yako.
Ndugu, thawabu kama hii itakupita, Kazi ya Mungu inapasa iwe ni sehemu ya Maisha yako, ikiwa umeitwa kweli na Bwana, usiruhusu mapengo pengo yasiyokuwa na lazima yakusonge, mpaka kusudi lote liyeyuke ndani yako.
Lakini ukisimama katika nafasi yako, kama vile, huyu ambaye Bwana Yesu alimzungumzia hapo kwamba alimkuta anawapa watu wake chakula kwa wakati, aliahidi kumweka juu ya kazi yake yote.
Katika huo ufalme wa milele unaokuja huko, zitakuwepo kazi na majukumu, na hivyo, tangu sasa Bwana anatafuta watakaozisimamia kama viongozi kazi hizo za kimbinguni tukufu sana. Na watakaopewa nafasi hizo za kipekee ni wewe na mimi endapo tutakuwa tunagawa posho la Bwana kwa wakati.
Hivyo tuamke, kama tulikuwa tunalegea mahali, tuanze kuitenda kazi ya Bwana kwa bidii mpya.
Bwana akubariki.
Usikose mwendelezo..
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Rudi nyumbani
Print this post
Bwana Yesu asifiwe, katika Makala hizi, tutazama vigezo ambavyo Mungu atavitumia kutoa thawabu zake, tutakapofika kule ng’ambo, Hii itatusaidia kuzidisha hamasa zetu katika kumtumikia Mungu, kama vile mtume Paulo, alivyoliona hilo, mpaka akasema..
Wafilipi 3:14 “nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”.
Tutapitia baada ya vifungu, ambavyo vitatupa picha jinsi thawabu hizo Mungu atakavyozigawa; Kigezo cha thawabu ya kwanza tunakisoma katika Mathayo 20:1-16
Unaweza ukasema ni kwanini Mungu afanye hivyo? Embu tupitie Habari hii, tutapata majibu yote.
Mathayo 20 : 1-16
“1 Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. 2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. 3 Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; 4 na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. 5 Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. 6 Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? 7 Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu. 8 Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. 9 Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari. 10 Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari. 11 Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba, 12 wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa. 13 Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? 14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. 15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema? 16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho”.
“1 Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.
2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.
3 Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;
4 na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
5 Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.
6 Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
7 Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
8 Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza.
9 Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.
10 Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
11 Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba,
12 wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.
13 Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?
14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.
15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho”.
Lakini ni wakina nani hawa, ambao, watakuja kulipwa sawasawa na wale waliotaabika katika kazi ya Mungu kwa muda mrefu.
Ukitazama, utaona, wale wa mwisho, hawakuwa wanashughulika mahali popote hapo kabla.. Bali mwenye shamba alipowafuata na kuwauliza kwanini mmesimama hapa mchana kutwa wakasema “Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri”.. Hii ikiwa na maana kama wangebahatika kufuatwa na mwenye shamba tangu asubuhi nao pia wangefanya kazi kubwa tu kama wale wengine, lakini hakutokea mtu wa kuwaajiri mpaka jioni.
Ikifunua kuwa, kuna watu mpaka sasa bado hawajafikiwa na neema ya wokovu, na pengine umri umeenda, labda tuseme mpagani Fulani mwabudu ng’ombe, lakini akiwa na miaka 80, ndio anahubiriwa injili na kuokoka kwa kumaanisha, na baada ya hapo anakuwa tayari kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote, pengine akamtumikia Mungu kwa uaminifu kwa mwaka 1 tu akafa.
Au mwingine, neema imemkuta katika ujana wake, labda miaka 20 tu, lakini akatumika miaka 2 tu, alipofikisha miaka 22 akafariki.
Sasa watu kama hawa, kama walitumika kwa uaminifu kwa muda huo mfupi tu. Usishangae kuwakuta kule ng’ambo wamepewa thawabu sawa mitume. Ni kwanini? Ni kwasababu wakati neema inawafikia, na muda wao wa kutumika ulipokuja, waliandikiwa muda mchache sana. Hivyo kama wangekutwa tangu zamani ni wazi kuwa wangemtumikia Mungu kwa uaminifu.
Lakini,ikiwa wewe leo hii unaisikia neema, unaichezea, leo upo na Kristo, kesho upo na shetani, yaani hueleweki, usitazamie, Kristo atakupa thawabu yoyote, ikiwa utakufa leo katika hali kama hiyo, yaani umezaliwa katika familia ya kikristo, unajua kabisa misingi ya kiimani kwamba, pasipo wokovu huwezi kwenda popote, usitazamie, utalingana na yule mpagani au mtu wa dini nyingine ambaye kaokoa hivi karibuni, halafu akafa.
Bwana alisema wamwisho watakuwa wa kwanza, na kwanza watakuwa wamwisho. Ithamini neema uliyopewa , hizi ni siku za mwisho.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?
KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
AINA TATU ZA WAKRISTO.
Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”
Jibu: Tusome,
Yohana 11:32 “ Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, 34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. 35 Yesu akalia machozi. 36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. 37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”
Yohana 11:32 “ Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame.
35 Yesu akalia machozi.
36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.
37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”
Ukisoma kwa makini habari hiyo utaona Bwana Yesu hakulia machozi kwa sabababu ya uchungu wa msiba, bali alilia kwasababu ya ugumu wa mioyo yao katika kumwamini Mungu.
Bwana hakuwa na uchungu na msiba kwasababu yeye ndiye ufufuo na uzima, alijua dakika chache mbeleni Lazaro atakuwa hai.
Lakini kitendo cha wale wafiwa walivyokuwa wanahuzunika, na kutokuamini kama Lazaro anaweza kuwa hai tena, na walivyokuwa wanalia kwa uchungu kama watu waliopoteza tumaini, kitendo hicho kilimuhuzunisha sana Bwana mpaka akalia machozi.
Amekaa nao mara nyingi, wamesikia akifufua wafu mara nyingi lakini bado walikuwa hawaaamini kama Mungu anaweza kumfanya akawa hai tena, ni jambo la kuhuzunisha sana..
Yohana 11:38 “Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje”.
Yohana 11:38 “Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje”.
Utaona pia mara kadhaa, Bwana alihuzunishwa na Mafarisayo..
Marko 3:1 “Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza; 2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. 3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. 5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, AKIONA HUZUNI KWA AJILI YA UGUMU WA MIOYO YAO, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. 6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”.
Marko 3:1 “Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;
2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.
3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.
4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.
5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, AKIONA HUZUNI KWA AJILI YA UGUMU WA MIOYO YAO, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”.
Na hata sasa Bwana analia machozi, kwasababu ya ugumu wa mioyo yetu, Hata sasa tunamhuzunisha Mungu kwa kutomwamini kwetu, na hata wakati mwingine tunapomjaribu.
Hivyo hatuna budi kuishi maisha ya Imani, ili tumpendeze Mungu.
Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza…”
Maran atha!.
UYATIE MACHOZI YANGU KATIKA CHUPA YAKO EE! BWANA.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
WhatsApp
Unaweza ukajiuliza Je shetani anaweza kuwazuia watu wasihubiri injili?
Jibu ni ndio Tusome,
1 Wathesalonike 2:17 “Lakini ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu. 18 Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia”.
1 Wathesalonike 2:17 “Lakini ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu.
18 Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia”.
Kulingana na maneno hayo ya Mtume Paulo, ni wazi kuwa shetani anahusika pakubwa sana katika kuizuia injili.
Siku zote shetani ni adui wa injili hakuna mahali alishawahi kukubaliana na watu kuipeleka injili. Hataki injili ihubiriwe kwasababa anajua ni uweza wa Mungu uletao wokovu. (Warumi 1:16).
Na yeye hataki kamwe watu wapate wokovu, anataka wasiisikie injili ili wafe katika dhambi zao na wajikute katika hukumu kama yeye siku ile ya mwisho. Kwahivyo atafanya juu chini aizuie injili. Sasa swali anaizuiaje?.
Anaizuia kwa kunyanyua matukio ambayo yataikwamisha safari ya kwenda kuhubiri. Kwamfano akina Paulo labda walipanga kwenda huko Thesalonike lakini tarehe walizopanga kwenda hakukuwa na mashua za kuelekea huko au tufani zilianza kiasi kwamba haiwezekani kuanza safari kwa kipindi hicho.
Au wakati wameanza tu safari kufika maili kadhaa mbelen baharini ikachafuka, jahazi likavunjika, hivyo safari kuishia pale.
Au unakuta wamepanga safari vizuri tu inatokea wanapoteza nauli au wanaibiwa, hivyo safari inakuwa imeisha hapo. Au wamepanga safari, ghafla mmojawao anaugua n.k.
Hayo ndio mambo shetani anayoyafanya kuizuia injili, na zaidi ya yote Mtume Paulo mwenyewe aliyashuhudia hayo mambo wanayokutana nayo katika safari zao za kwenda kuhubiri.
2 Wakorintho 11:25 “Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; 26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; 27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi”.
2 Wakorintho 11:25 “Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;
26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;
27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi”.
Mambo hayo pia yaliwatokea wanafunzi wa Bwana Yesu walipokuwa wanavuka kwenda nchi ya Wagerasi, wakiwa katikati ya safari baharini, shetani alijaribu kuwazuia kwa kuwaletea tufani kubwa, shetani alitaka kuwazuia kwasababu aliona kuna watu wawili kule nga’ambo wenye pepo wanaishi makaburini, wanakwenda kufunguliwa, hivyo hilo jambo hawezi kuliruhusu, ndipo akawaletea tufani njiani, mpaka Bwana alipoamka na kuinyamazisha.(Mathayo 8:23-34).
Hivyo kilichomtokea Paulo na Wanafunzi wa Bwana Yesu kinaweza kumtokea mhubiri yeyote yule, haijalishi umeitwa kwa wito gani kamwe shetani hawezi kuruhusu wewe uhubiri injili kirahisi, ni lazima atakupinga tu.
Sasa swali kama hivyo ndivyo tunapaswa tufanyeje kila tunapotaka kwenda kuhibiri injili?.
Bwana Yesu alitupa dawa ya kuepukana na majaribu ya namna hiyo, na hiyo si nyingine zaidi ya kuomba kwa bidii. Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake mara kadhaa waombe ili wasije wakaingia majaribuni, kwasababu alijua silaha moja kubwa ya kudhoofisha vizuizi vya shetani ni kuomba, ndio maana ijapokuwa yeye mwenyewe alikuwa ni Mungu lakini alikuwa anakesha kuomba, ili kutufundisha sisi.
Na jukumu la kuomba sio tu la Mhubiri, au mchungaji, au Muinjilisti, au Mtume.
Jukumu la kuomba ni la kila mtu aliye mkristo, kila mtu anapaswa kuiombea ili injili iweze kupelekwa bila kizuizi chochote, unapotenga muda na kuiombea injili ya Bwana Yesu, hujui ni mchango gani mkubwa uliouchangia.. Kwa kuomba kwako huko unaharibu mipango ya shetani ya kumvunjia jahazi mhubiri fulani mahali fulani.
Kwa kufunga kwako kuiombea injili ya Bwana Yesu, umeharibu mipango ya wizi na magonjwa shetani aliyoipanga juu ya wahubiri fulani waliopanga kwenda kupeleka injili mahali fulani. Hivyo na wewe unakuwa ni mojawapo ya jeshi la Bwana katika kuipeleka injili mbele.
Lakini ukiacha tu na kusema.. Aaah mimi sio mhubiri, sio muinjilisti hiyo sio karama yangu, huombi, hufungi, huchangii, hufanyi chochote, basi fahamu kuwa unaupa nguvu ufalme wa giza.
Ndio maana Mtume Paulo baada ya kuwaandikia waraka hawa Wathesalonike kwamba ameshindwa kuja kwao shetani kamzuia, alimalizia na kuwaambia hao Wathesalonike kwamba WAMWOMBEE.
Wasikae tu wakasubiri, kwani vita ni vikali.
1 Wathesalonike 5:24 “Ndugu, tuombeeni”
Na zaidi ya yote katika waraka wake wa pili aliwakumbusha tena jambo hilo hilo..
2 Wathesalonike 3:1 “Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu ”.
Je na wewe unaiombea Injili ya Bwana Yesu?.
Bwana atubariki.
Ni madhara gani yatampata mtu yule anayetafsiri Neno isivyopaswa!
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Akiki ni aina ya madini inayokaribia kufanana kimwonekano na madini ya Marijani (Rubi). Kwa lugha ya kiingereza madini ya Akiki yanajulikana kama “Sardius”. (Tazama picha juu).
Na madini ya Yaspa ni aina nyingine ya madini, ambayo rangi yange ni ya kahawia (Tazama picha chini), mawe haya kwa kiingereza ndio yanayojulikana kama “JASPER”. Kimwonekano ni mawe mazuri kama yalivyo Akiki na Marijani.
Mawe haya (Akiki na Yaspi) yametajwa katika biblia kuwakilisha Utukufu wa Mungu.
Ufunuo 4:2 “Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; 3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la YASPI NA AKIKI, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. 4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu”.
Ufunuo 4:2 “Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;
3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la YASPI NA AKIKI, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.
4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu”.
Mwonekano wa Mungu ulikuwa ni Mithili ya Madini haya ya Yaspi na Akiki, kumbuka hapo biblia inasema ni “Mithili” na sio Mwonekano halisi. Biblia imetumia madini yetu ya kidunia yaliyo mazuri kuuelezea utukufu wa Mungu, lakini kiuhalisia Utukufu wa Mungu ni mkuu na mzuri kuliko mawe hayo, mwonekano wake hauwezi kulinganishwa na chochote. Lakini biblia imetumia mfano wa mawe hayo kuuwakilisha utukufu wa Mungu, ili tuweze kujua kuwa kwa Mungu kuna uzuri.
Vile vile tunasoma mji ule mpya ushukao mbinguni (Yerusalemu Mpya), umepambwa kwa mawe hayo mazuri (Akiki na Yaspi).
Ufunuo 21:17 “Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. 18 Na majenzi ya ule ukuta wake YALIKUWA YA YASPI, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa YASPI; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; WA SITA AKIKI; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.
Ufunuo 21:17 “Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.
18 Na majenzi ya ule ukuta wake YALIKUWA YA YASPI, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa YASPI; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
20 wa tano sardoniki; WA SITA AKIKI; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.
Maandiko yanasema pia shetani kabla ya kuasi, alikuwa amepambwa na kufunikwa na haya mawe ya thamani.
Ezekieli 28:13 “Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, AKIKI, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, NA YASPI, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.”
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Mbinguni ni kuzuri na si pa kukosa, tukose kila kitu katika haya maisha lakini tusiikose mbingu, kwasababu maandiko yanasema mambo tuliyoandaliwa huko jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.
Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?
ZUMARIDI NI MADINI GANI?
KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.
KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.
Ufisadi una maanisha nini katika biblia?
Zumaridi ni aina ya madini yenye rangi ya kijani,
Madini haya kimwonekano ni mazuri sana, Matumizi ya madini haya ni kama yale ya Marijani (Rubi) pamoja na Yakuti (Sapphire). Yote haya kazi yao ni moja ambayo ni kutengenezea vito vya thamani kama vile saa, pete na vitu vingine vya urembo.
Kimwonekani madini ya Zumaridi ni mazuri mno, na ni ya gharama kubwa, kama ilivyo Rubi na Yakuti.
Katika biblia madini haya ya Zumaridi yametajwa mara kadhaa.
Sehemu mojawapo na ya muhimu yalipotajwa ni katika kile kiti cha Enzi, ambapo ule upinde uliokizunguka Kile kiti cha Enzi, ulikuwa na mwonekano mithili ya madini hayo ya Zumaridi.
Ufunuo 4:3 “na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi”.
Mistari mingine inayozungumzia mawe hayo ni pamoja na Kutoka 28:18, Kutoka 39:11, Ezekieli 27:16, Ezekieli 28:13 na Ufunuo 21:19.
Biblia imetumia mawe haya kufunua uzuri uliopo katika Enzi yake, Enzi ya Mungu ni nzuri sana, mbinguni kuna makao mazuri sana tumeandaliwa, ni mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia. Hapo maandiko yanasema “upinde ulikizunguka mithili ya Zumaridi”..kumbe sio Zumaridi, bali mithili ya Zumaridi, maana yake ni kwamba uzuri wa mambo yaliyopo mbinguni, hauelezeki.
Biblia imetumia tu lulu na madini ya kidunia, kutusaidia angalau tulate picha, ya ni nini kilichopo kule.
Je unao uhakika wa kwenda mbinguni?.Kama hauna basi huna budi kuutafuta, kwasababu mbinguni si pa kukosa.
Maran atha!
YAKUTI NI MADINI GANI?
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?
Yakuti ni aina ya madini inayokaribiana kufanana sana na madini ya Rubi (yaani Marijani).
Madini ya Yakuti kwa lugha ya kiingereza ndio yanajulikana kama SAPPHIRE. Kazi yake ni kutengenezea vito bya thamani kama pete, saa za mkononi n.k, na thamani yake inakaribiana kufanana na ile ya madini ya Rubi, na yana muonekano mzuri sana.
Madini ya Yakuti yapo ya aina mbili, yapo Yakuti ya manjano na Yakuti ya Samawi (yaani blue).
Katika biblia Yakuti ya manjano imetajwa katika mistari kadhaa..
Ayubu 28:19 “Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi”.
Unaweza pia kusoma juu ya Yakuti hiyo ya manjano katika Kutoka 28:17, na Ezekieli 28:13.
Kadhalika unaweza kusoma juu ya Yakuti-Samawi katika mistari ifuatayo.. Kutoka 28:18, Kutoka 39:11 na Isaya 54:11.
Hivyo Kwaufupi madini haya kwenye biblia yametumika kuwakilisha vitu visafi na vitukufu, na vyenye heshima, kwamfano utaona kile kiti cha enzi cha Mungu, Nabii Ezekieli alichooneshwa kilikuwa ni mfano wa Yakuti-Samawi.
Ezekieli 10:1 “Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi”.
Halikadhalika katika ule mji Yerusalemu mpya, utakaoshuka kutoka mbinguni, maandiko yanasema utakuwa umepambwa kwa vito vya thamani, vya mfano Yakuti.
Ufunuo 21:19 “Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.
Ufunuo 21:19 “Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.
Kama vile tunavyoona madini ya Yakuti yalivyo mazuri, basi mbinguni kuna mazuri zaidi ya hayo tuliyoandaliwa, biblia imetaja tu Yakuti ili tuweze kuelewa na kutengeneza picha uzuri wa kule, lakini kiuhalisia vito vilivopo kule sio vya kidunia.
Mji ule Yerusalemu mpya ni mzuri sana, tujitahidi tuuingia,na tunauingia kwa kuishi maisha ya wokovu kwa uaminifu wote.
Ufunuo wa Yohana 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.
Risasi inayotajwa kwenye Ezekieli 27:12 ni ya namna gani?
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
Kuhusuru ni kuzinga kitu, pande zote kisiwe na upenyo wa kutoroka au kupita.
Mbinu hii yalitumia majeshi ya zamani katika vita..kabla ya kwenda kupigana na adui zao waliwazingira kwanza kuhakikisha hakuna upenyo wowote wa wao kutoka..na hiyo inaweza kuchukua hata miezi kadhaa.. Mpaka pale chakula kitakapoisha ndani..Sasa kwa hali kama hiyo maudui, wao wenyewe tu watalazimika aidha kuiomba amani..au watoke wapigane..na kwa kawaida huwezi pigana na adui yako ukiwa na njaa.. Utapigwa tu.
Neno hili utalisoma sehemu nyingi sana katika biblia..kwamfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo..
2 Wafalme 6:24-25
[24]Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. [25]Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
[24]Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria.
[25]Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
1 Samweli 23:8
[8]Basi Sauli akawaita watu wote waende vitani, ili waishukie Keila, na kumhusuru Daudi na watu wake.
1 Wafalme 8:37
[37]Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote;
Luka 19:43
[43]Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;
Soma pia Kumbukumbu 20:12, 19, 2Wafalme 24:11, Isaya 29:4
Ni picha gani tunaipata katika Roho?
Ndivyo anavyofanya shetani sasa katika roho..akitaka kuwaangusha watu hususani wale ambao anajua ni ngumu kuwaangusha..atakimbilia kuhusuru sehemu mbalimbali ambazo anajua wanazitegemea kuendeshea maisha yao, halafu baada ya hapo akishafanikiwa anamlazimisha ufanye dhambi fulani..
Labda anakunyima kazi..halafu anakuambia ukitaka hii kazi zini na mimi..ukiona hivyo usidhubutu..bali mpinge, kabisa kabisa..
Alipomwona Bwana Yesu anayo njaa kule jangwani..ndipo akamletea mkate..Lakini Bwana hakukubali ushawishi wake..akamwambia mtu hataishi kwa mkate, bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana.
Na wewe mwambie shetani hutaishi kwa hilo tu analoliwazia..bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana. Mungu atakupasulia mlango kwingine..
Maji ya Zamzam yapo kibiblia?
Mintarafu ni nini?
Wanefili walikuwa ni watu gani?
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.
KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.
Maandiko yanasema..
Mithali 13:12 “Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima”.
Ni kawaida siku zote kuugua pale unapokuwa katika hali ya kusubiria jambo kwa muda mrefu.
Mtu anayemngojea mwenzake aliyekawia kwa dakika 10, yule anayemngoja ataona kakawia kama lisaa hivi, ingawa ni dakika 10 tu zimepia.
Hiyo ni kwasababu, ya kile kinachotarajiwa kimekawia, moyo wa mtu huwa unaugua. Lakini maandiko yanazidi kusema kuwa mtu anapopata haja yake ni Mti wa Uzima. Sasa swali hapo ni kwanini mtu anapopata haja yake anafanishwa na mti wa Uzima.
Siku zote miti unafananishwa na watu.
Marko 8:24 “Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda”.
Pia Bwana sehemu nyingine alisema “mti hutambulika kwa matunda yake”..maana yake watu wanafananishwa na miti.
Luka 6:44 “kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. 45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”.
Luka 6:44 “kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”.
Maana yake ni kwamba, kama mtu ndani yake ni mwema, ni mtakatifu, ana uzima..Basi mtu huyo ni MTI WA UZIMA.
Matunda atakayoyatoa yatawapa wengine uzima.
Sasa ni kwa namna gani, mtu anayepata haja yake anafananishwa na mti wa uzima?.
Ni kwasababu ya ile furaha atakayoipata, itawafaidia wengi, ni kwasababu ya ile neema atakayoiachia baada ya pale.
Siku zote watazame watu waliofanikiwa kupata jambo fulani,waliokuwa wanalitafuta utaona wanakuwa wakarimu ghafla, utaona wanatoa maneno mazuri mdomoni mwao.
Mithali 15:4 “Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo”.
Lakini kinyume chake, mtu ambaye hajapata anachokitafuta anakuwa mkali. Huwezi kutegemea kupata chochote chema kutoka kwake, hiyo ni kwasababu bado hajakipata anachokitafuta.
Hivyo hizo ni hekima tu ambazo Sulemani aliziona na kuzitoa kwa watu.
Na sisi tunapompokea Yesu maishani, Roho Mtakatifu anatupa haja ya mioyo yetu, anakata kiu yote, hivyo tunajikuta nasi pia tunakuwa wazuri ghafla, tunatoa matunda ya Uzima, hivyo tunakuwa Mti wa Uzima kwa wengine.
Ndivyo maandiko yanavyosema..
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. 14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. 15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. 16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. 17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. 18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”.
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.
18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”.
Je na wewe ni Mti wa Uzima?, Kwa wengine?. Au ni mti wa Mauti?.
Ni HAJA moja tu maishani itakayokufanya uwe Mti wa uzima duniani. Na hiyo ni kumwamini Yesu na kupokea Roho Mtakatifu.
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Nini maana ya ‘Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu’ ?
HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
Kuna baadhi ya watu Mungu anawapanda katika kanisa, kwa namna ya kitofauti na kipekee sana..
Na pengine wenyewe hawalijui hilo..hivyo wanaishi maisha ya kimaficho ficho tu..au ya juu juu tu, kwa kisingizio kuwa wao si kama wengine.. wakidhani kuwa Kristo, amewaweka hapo bure, kwasababu hiyo..
Ulishawahi kuitafakari vizuri hii habari..
Luka 13:6-9 [6]Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. [7]Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? [8]Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; [9]nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.
Fikiria hilo ni shamba la Mizabibu..pengine ekari elfu moja, limeandaliwa mahususi kwa ajili ya kutoa zabibu za kibishara..lakini mwenye shamba tunaona bado katikati ya shamba hilo kubwa alipanda mti mwingine wa matunda ujulikanao kama “mtini”..
Kumbuka lengo lake halikuwa apate matunda ya biashara kutoka katika mti huo..bali pengine ya kula tu, na ndio maana mtini wenyewe ulikuwa ni mmoja tu. Lakini bado hakutaka ukae bila matunda..akaupa muda ili uzae..
Kuna watu Mungu kawapanda katika kanisa lake, ambao wanaweza kuonekana ni tofauti sana na watakatifu wengine pengine kilugha, labda hawajui kiswahili vizuri, au kimazingira, labda wapo mbali, au kinafasi, ni viongozi wakubwa n.k.na hivyo hawawezi moja kwa moja kutumika kama hawa wengine..kwa vikwazo hivyo.
Lakini wengi wa hawa huwa wanaishi maisha ya kujificha, wakidhani pengine sio sehemu ya kanisa la Kristo.
Nataka nikuambie, vyovyote vile ujionavyo..Kristo anatazamia matunda kutoka kwako. Anataka aone ukristo wako ukiangaza kwa wengine..anataka kuona unafanya kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni..anataka kuona shamba lake alilokuweka wewe ndani yake pamoja na hao wengine hulikalii bure…na wewe pia kwa nafasi yako uhakikishe unazaa matunda..
Hizi ni siku za mwisho ndugu yangu..Kristo anasema Naja upesi, na ujira wangu, upo mkononi mwangu kumlipa kila mtu..sawasawa na kazi yake ilivyo..
Ufunuo wa Yohana 22:12 [12]Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Utalipwa nini siku ile..ikiwa miaka nenda rudi, wewe ni msikiaji tu wa injili, miaka nenda rudi upo tu mafichoni, hutaki ijulikane..jiulize Ni nini umemfanyia Bwana basi..mpaka akupe ufalme siku ile?
Bwana atutie nguvu, tutambue kuwa sote tupo shambani mwake..na sio jukumu la askofu fulani au shemasi. Na kwamba Bwana atamvumilia mtakatifu yoyote katika shamba lake asiyemzalia matunda.
Tafadhali shea na wengine habari hizi njema,
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.