Jibu: Tusome,
Yohana 11:32 “ Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, 34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. 35 Yesu akalia machozi. 36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. 37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”
Yohana 11:32 “ Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame.
35 Yesu akalia machozi.
36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.
37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”
Ukisoma kwa makini habari hiyo utaona Bwana Yesu hakulia machozi kwa sabababu ya uchungu wa msiba, bali alilia kwasababu ya ugumu wa mioyo yao katika kumwamini Mungu.
Bwana hakuwa na uchungu na msiba kwasababu yeye ndiye ufufuo na uzima, alijua dakika chache mbeleni Lazaro atakuwa hai.
Lakini kitendo cha wale wafiwa walivyokuwa wanahuzunika, na kutokuamini kama Lazaro anaweza kuwa hai tena, na walivyokuwa wanalia kwa uchungu kama watu waliopoteza tumaini, kitendo hicho kilimuhuzunisha sana Bwana mpaka akalia machozi.
Amekaa nao mara nyingi, wamesikia akifufua wafu mara nyingi lakini bado walikuwa hawaaamini kama Mungu anaweza kumfanya akawa hai tena, ni jambo la kuhuzunisha sana..
Yohana 11:38 “Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje”.
Yohana 11:38 “Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje”.
Utaona pia mara kadhaa, Bwana alihuzunishwa na Mafarisayo..
Marko 3:1 “Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza; 2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. 3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. 5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, AKIONA HUZUNI KWA AJILI YA UGUMU WA MIOYO YAO, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. 6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”.
Marko 3:1 “Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;
2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.
3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.
4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.
5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, AKIONA HUZUNI KWA AJILI YA UGUMU WA MIOYO YAO, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”.
Na hata sasa Bwana analia machozi, kwasababu ya ugumu wa mioyo yetu, Hata sasa tunamhuzunisha Mungu kwa kutomwamini kwetu, na hata wakati mwingine tunapomjaribu.
Hivyo hatuna budi kuishi maisha ya Imani, ili tumpendeze Mungu.
Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza…”
Maran atha!.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UYATIE MACHOZI YANGU KATIKA CHUPA YAKO EE! BWANA.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
Rudi nyumbani
Print this post