Paulo akijua kuwa anakaribia ukingoni kabisa mwa safari yake, hakujali taarifa yoyote mbaya iliyoletwa mbele yake, utaona yeye mwenyewe anasema, mji kwa mji Roho Mtakatifu alimshuhudia kuwa vifungo na dhiki nyingi vinamngojea kule Yerusalemu alipokusudia kwenda, lakini bado alisema, siachi kupiga mbio nimalize mwendo wangu.
Matendo20:23 “isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. 24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu”.
Matendo20:23 “isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.
24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu”.
Kama hilo halitoshi alipofika Kaisaria, karibu kidogo na Yerusalemu, Nabii mmoja aliyeitwa Agabo, alitokea na kumtolea unabii kwa uweza wa Roho Mtakatifu akisema, Paulo atakwenda kufungwa, na kupata dhiki, hivyo asiende, Yerusalemu.
Lakini hilo nalo halikumfanya Paulo, aache kwenda Yerusalemu, badala yake aliwaambia;
Matendo 21:13 “Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu”.
Unaona, alifikia hatua, mawazo yake yote yalikuwa ni kuimalizia kazi yake kwa kishindo, kiasi cha kutojali dhiki zozote atakazokumbana nazo mbele yake
Sasa usifikirie ni jambo rahisi kuchukua maamuzi hayo kama asingekuwa ni mtu anayefahamu ni nini anakitafuta.. Paulo alikuwa ni mtu mwenye malengo, ni mtu aliyekuwa anatazama vya mbali sana, alijua kupiga mbio huko kuna tuzo Fulani kubwa mbeleni, hivyo ni sharti aishindanie kwa nguvu ili asiikose.
1Wakorintho 9:24 “Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. 25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. 26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”
Unaona alijua sikuzote mkimbiaji ambaye anajua lengo la kukimbia kwake ni nini huwa hakimbii kwa kuubembeleza mwili, bali anakimbia huku mawazo yake yakuwa kweney tuzo iliyowekwa mbele yake, hilo ndilo linalomfanya asitembee tembee njiani, asikubali kuusikiliza mwili, kwamba umechoka, hivyo apunguze mwendo.
Hali kadhalika mkimbiaji mzuri kwa namna ya kawaida, anapokaribia mzunguko wake wa mwisho ndio huwa anaongeza mwendo Zaidi, na ndicho alichokifanya Paulo.
Embu tumtazame mtu mwingine wa mwisho ambaye safari yake sikuzote ilikuwa ni ya mwendo tu, mtu ambaye yeye hakujali kikwazo chochote alipokuwa anamalizia mwendo wake hapa duniani. Na huyo si mwingine Zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Biblia inatuambia wakati wa kupaa kwake ulipokaribia, “ALIUKAZA” uso wake kwenda Yerusalemu.
Luka 9:51 “Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; 52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. 53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu”.
Kuukaza uso maana yake, ni kutokuwa tayari kuambiwa chochote, au kushauriwa chochote au kukwamishwa na chochote mpaka utimize malengo yako uliyoyakusudia mbele yako. Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu, wakati ambapo anajua amebakiwa na kipindi kifupi sana, amalize mwendo wake pale Yerusalemu, huku akijua moyoni mwake kuwa Mateso makali anakwenda kukumbana nayo, kusulibiwa, yeye hakujali chochote, Zaidi ndio alilazimisha kwenda huko huko.
Yohana 10:7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. 8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
Je na sisi kipindi hichi cha kufunga majira, bado tunapiga mbio au tumepunguza mwendo wetu wa Imani ? Pengine tumeacha kukimbia kwasababu hatujajua malengo yetu ni nini? tunakumbana na milima mrefu, tunakata tamaa, lakini pia tunapaswa tujue jambo moja ili uitwe mlima ni lazima utakuwa na upande wa pili wa mteremko pia.
Ni heri maisha mafupi ya hapo duniani, tuyaishie kupanda mlima, lakini tutakapofika kule ng’ambo kwenye umilele tuyaishie kwenye mteremko,..
Hizi ndizo nyakati za kuzidisha mwendo, kutojali vitisho vyovyote vya kiimani, vitisho vya ndugu, au rafiki, au majirani, kwasababu kama unyakuo hautatukuta, basi pia siku zetu za kuishi duniani zinapungua siku baada ya siku.
Hivyo tupige mbio tukijua kuwa zipo tuzo mbele yetu zinatungojea, lakini tukiwa walegevu hatutazipata.
2Timotheo 2:5 “Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali”.
Shalom
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
NITAFANYA YERUSALEMU KUWA JIWE LA KUWALEMEA .
JINSI PAULO ALIVYOPAMBANA NA UJINGA WA ROHONI.
Nini maana ya neno ‘Kuabiri’ kama linavyotumika katika biblia?
Rudi nyumbani
Print this post
Sikuzote roho haiji hivi hivi tu, bila kuwa na chanzo Fulani, na chanzo hicho kinaweza kuwa mtu, au kitu au sehemu, Sasa pale yule mtu anapoondoka, huwa anaacha tabia yake Fulani inayoendelea na tabia hiyo ikishakita mizizi vizuri ndio inaitwa roho,..
Kwamfano kwenye biblia utamwona mwanamke anaitwa Yezebeli, huyu mwanamke alikuwa ni mchawi, na mzinzi, na tabia zake tunazijua vizuri kwenye biblia, jinsi alivyoiharibu Israeli na kuigeuzwa kuwa nchi ya kichawi. Lakini tunasoma mara baada ya kufa kwake, roho yake iliendelea kutembea duniani, na ndio maana miaka mingi baadaye utaona Bwana Yesu anamzungumzia tena habari zake kana kwamba bado yupo duniani, katika kitabu cha Ufunuo,
Ufunuo 2:19 “Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu”
Utamwona pia Eliya, pindi alipoondoka roho yake ilianza kutembea tena wakati baada ya wakati, Kumbuka hawi Eliya mwenyewe kama Eliya, Au Yezebeli kama Yezebeli, bali ile tabia ya rohoni iliyokuwa juu ya Eliya, ndiyo inayotembea juu ya watu kadha wa kadha, Roho hiyo ilikuja juu ya Elisha, baadaye Yohana Mbatizaji n.k. na itaendelea kutembea hadi wakati wa nyakati za mwisho kabisa.(Malaki 4:5)
Halikadhali Na Bwana wetu Yesu Kristo, yeye alitembea hapa duniani, kwa miaka 33 na nusu, lakini alipoondoka, hakuondoka hivi hii ilikuwa ni sharti aichalie Roho yake katikati yetu, na ndio Roho Mtakatifu tuliye naye sasa. Kiasi kwamba mtu akiyaamini maneno yote ya Bwana Yesu moja kwa moja anampokea Roho wake ambaye atamsaidia aishi maisha kama ya Yesu.
Sasa tukishaweka msingi kama huo, tuende moja kwa moja katika somo letu la leo ambalo linamzungumzia yule Elima mchawi aliyekutana na Paulo na Barnaba pindi walipokuwa wanahubiri injili huko Pafo, tusome.
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.12 Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana”`.
Huyu mtu alikuwa ni mchawi, na wakati huo huo ni nabii wa Uongo. Kazi yake na lengo lake, lilikuwa ni kuwafanya watu wasiiamini njia ya wokovu, pale tu wanapokutana na injili ya kweli ya msalaba. Ni mchawi aliyebobea kwenye kitendo cha kupinga tu, na kushawishi watu kuiacha imani, na ndio maana mtume Paulo alimwambia “Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?”
Kwa kazi yake hii, mpaka akawa ameshawafikia kabisa na watu wakubwa na wenye akili kama huyu Sergio Paulo, ikiwa na maana kuwa huku chini tayari alishaburuza.
Kama tunavyoona hapo, Paulo alipoanza kumuhubiria huyu liwali, yeye bila kupoteza muda alianza kuwabishia wakina Paulo, na kutoa hoja zake za uongo, na pengine kumwambia yule liwali hawa watu ni waongo, wapiga dili, hakuna kitu kuokoka hapa duniani, huyo Yesu aliibiwa hajafufuka, hawa ni wapotoshaji n.k.
Lakini Paulo kulijua hilo, akamkemea saa ile ile akawa kipofu kwa muda.
Sasa huyu mtu alishakufa lakini aliiacha roho yake hapa duniani, na roho hiyo inatembea kwa kasi sana, sasa hivi duniani imewavaa watu wengi, na wenyewe hawajijui kuwa wanafanyika kuwa wachawi, pasipo wao kujijua.
Kuna watu kazi yao ni kupinga tu kila habari ya Kristo, wakiona kila mtumishi wa Mungu anahubiri, au kushuhudia, wanasema ni nabii wa uongo, wanasema ni wazinzi, wakisikia injili ya kweli inahubiriwa wanasema anapotosha,
Sasa kibiblia watu kama hao ni wachawi, hawajijui tu kama wameshafikia hiyo hatua
Katika nyakati hizi za kumalizia ni kujiangalia sana, si kila wazo la kila mtu la kulisikiliza, au kulipokea haijalishi atakuwa ni ndugu yako, au rafiki yako, au mfanyakazi mwenzako.
Bwana Yesu alisema, angalieni jinsi msikiavyo (Luka 8:18)
Kaa mbali nao, ikiwa unaona kila wakati tu wanakosoa habari za Mungu au watumishi wa Mungu, hakuna kipengele hata kimoja watakisifia, kaa mbali nao, wanakuwekea tu moyo mgumu wa kutokuamini.
Ukikutana na watu kama hao ujue unaongea na wachawi, jiupushe nao. Leo hii duniani utakutana nao wengi sana akina Elimu, Bar Yesu. Wewe jikite katika kumtafuta Muumba wako kwa bidii, mpende Mungu wako, sikiliza na soma Neno la Mungu, achana na hao wanaoipuuzia, au kukejeli kila kitu cha ki Mungu kinachokatiza mbele yao.
Jiepushe nao.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.
KUMTUMIKIA MUNGU, KUNAWEZA KUWE KINYUME NA MATARIJIO YAKO.
SWALI: Mtumishi wa Mungu! Bwana asifiwe, naomba ufafanuzi kidogo juu ya andiko hili katika Isaya 6:1-10 Ni Nani aliyesema “Nitume Mimi”?je Ni isaya au!? Na kwanini Isaya pia alitakaswa kwa kaa la moto?
JIBU: Tusome baadhi ya vifungu hivyo;
Isaya 6: 5 “Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi. 6 Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu; 7 akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa. 8 Kisha nikaisikia SAUTI YA BWANA, AKISEMA, NIMTUME NANI, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, MIMI HAPA, NITUME MIMI. 9 Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. 10 Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa”.
Shalom, Unabii huo ulikuwa unamuhusu Nabii Isaya mwenyewe aliyekiandika kitabu hicho, tofauti na watu wengi wanavyodhani kuwa huyo ni Yesu ndiye aliyesema maneno hayo, nitume mimi.?
Hiyo yote ni baada ya Isaya kuijiona amesimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu mbinguni, na kwamba muda mfupi baadaye atahitajika kufanya mahojiano na Mungu. Hivyo kwa kulijua hilo kabla hata hajasema chochote, alijitambua hali yake ilivyo kuwa yeye ni mtu mwenye midomo michafu, akiwa na maana mwongo, msengenyaji, mtukanaji n.k. Jambo ambalo halikuwa kuwa midomoni mwa Yesu, tangu anazaliwa.
Hivyoo akaomba kwanza tiba, asafishwe kinywa chake, kabla ya kuzungumza na Mungu, ndipo hapo utaona huyo kerubi akichukua kaa la moto kutoka katika madhabahu ya Mungu kwa koleo.. Sasa zingatia hilo neno madhabahu, kaa lile halikutolewa sehemu nyingine yoyote Zaidi ya madhabahuni pa Mungu. Na pia hakupewa kipelekewa kitu kizuri mdomoni labda tuseme embe au ndizi, au tango kimponye badala yake alipelekewa kaa la moto.
Na kama tunavyofahamu moto kazi yake ni kuunguza, tena, mbaya Zaidi pale unapokutana na mdomo, jaribu kutengeza picha kaa jekundu linakuja kugusana na midomo yako, mshituko na maumivu utakayosikia hapo yatakuwa ya namna gani, ni heri ungelikanyaga kwasababu mguu kidogo ni mgumu, kuliko kukutana na ulimi.
Lakini ndiyo njia ambayo Mungu aliichagua kumponya Isaya na midomo yake michafu.
Hata leo hii, ili Mungu aweze kutuponya na midomo ya usengenyaji, uongo, fitina, kiburi, ya faraka, n.k. Ni lazima tukubali kaa la Mungu lipitishwe vinywani mwetu.
Na kaa hilo halitoki sehemu nyingine isipokuwa madhabahuni pa pake, ikiwa hatutaki kukemewa dhambi zetu, hatutaki kukaripiwa, hatutaki kuonywa kwa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu, hatutaki kuhubiriwa maneno magumu yanayochomo mioyo yetu, ili tubadilike, kamwe, tusitegemee kama usengenyaji utaondoka vinywani mwetu.
Kama tutapenda wakati wote injili ya kupiga adui zetu, na injili za mafanikio, hatutaki kukemewa dhambi zetu, na kuelezwa uhalisia wa ziwa la moto kamwe vinywa vyetu haziwezi kuponywa.
Hivyo tukubali kukaripiwa na Mungu, tukubali kukemewa na yeye, kwasababu kwa njia hiyo ndio kaichagua ili kutuponya sisi, hakuna short-cut, Mungu anatujua vizuri sisi wanadamu, wakati mwingine tutahitaji moto ili tuponywe.
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”
Bwana akubariki.
Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?
KWANINI MIMI?
Nini maana ya uvuvio?.
UFUNUO: Mlango wa 15
WhatsApp
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Ni wasaa mwingine tena ambao Mungu ametujalia kuufikia hivyo nakukaribisha tuyatafakari kwa pamoja maneno ya uzima ndugu yangu.
Biblia inatuambia kuwa Bwana Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu, aliwatokea baadhi ya watu, ambao idadi yao ilikuwa kama watu 500,(1Wakorintho 15:6) , Lakini ulishawahi kujiuliza ni kwanini iwe hivyo? Je hao watu 500 walikuwa na kitu gani cha ziada kuwashinda wengine wote mpaka watokewe wao tu?
Ni vizuri tukafahamu kuwa hii ni kawaida ya Kristo, kwamba kuna wakati ataonekana na watu wote, lakini pia upo wakati hataonekana na watu wote bali wachache tu aliowachagua, Na ndicho kilichotokea hapa, miaka yote 33 aliyoishi duniani, kila mtu angeweza kumtembelea kama angetaka, kila mtu angeweza kwenda kumtazama kama angetaka, lakini mara baada ya kufufuka kwake, hakuna mtu yeyote angeweza kumwona, isipokuwa Yule tu aliyejidhihirisha kwake.
Na ndio maana aliwaambia wayahudi maneno haya Yohana 7:34 “Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja”.
Sasa hawa watu 500 ambao walipata neema ya kumwona Yesu baada ya kufufuka kwake, hawakuwa ni watu tu ambao bahati imewaangukia, hawana habari na Yesu, au hawajawahi kumfuatilia au kumsikia,.. Hapana, biblia inatuambia walikuwa ni watu ambao waliambatana naye, tangu akiwa Galiliya mpaka Yerusalemu, yaani tangu ncha moja ya taifa la Israeli mpaka ncha nyingine ya Israeli.
Matendo 13:29 “Hata walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamtelemsha katika ule mti, wakamweka kaburini. 30 Lakini Mungu akamfufua katika wafu; 31 akaonekana siku nyingi na wale WALIOPANDA NAYE KUTOKA GALILAYA HATA YERUSALEMU, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu”.
Matendo 13:29 “Hata walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamtelemsha katika ule mti, wakamweka kaburini.
30 Lakini Mungu akamfufua katika wafu;
31 akaonekana siku nyingi na wale WALIOPANDA NAYE KUTOKA GALILAYA HATA YERUSALEMU, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu”.
Hawa ndio waliotokewa na Yesu mara ya pili, Ni watu ambao walitembea na Yesu, tangu zamani sana, ni watu ambao waliokuwa wanazungumzia habari zake, Mfano wake utaona ni wale watu wawili waliokuwa wanaelekea kile kijiji cha Emau baada ya kufufuka kwake(Luka 24:13)..
Hao ndio watu ambao Yesu aliona kuna umuhimu wote wa kuwatokea katika utukufu mwingine baadaye. Siku zote wale wanaomuheshimu Mungu, Mungu nao anawaheshimu, wanaomkaribia Mungu, Mungu naye anawakaribia wao.(Yakobo 4:8). Na mmojawapo kati ya hawa ndiye aliyefanywa mtume kuchukua nafasi ya Yuda.
Sasa kutokea kwake mara ya pili kwao, haikuwa maonyesho tu. Bali Kristo aliwapa karama nyingine ambayo iliwafanya kuwa tofauti kabisa na watu wengine. Na karama yenyewe ni kuwa MASHAHIDI WA YESU. Hao ndio waliochaguliwa na Mungu kuisambaza injili ya Kristo ulimwenguni kote, kwa nguvu za Roho wa Mungu zilizoachiliwa juu yao,
Matendo 10:40 “Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, 41 SI KWA WATU WOTE, BALI KWA MASHAHIDI WALIOKUWA WAMEKWISHA KUCHAGULIWA NA MUNGU, NDIO SISI, TULIOKULA NA KUNYWA PAMOJA NAYE BAADA YA KUFUFUKA KWAKE KUTOKA KWA WAFU. 42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu”.
Matendo 10:40 “Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika,
41 SI KWA WATU WOTE, BALI KWA MASHAHIDI WALIOKUWA WAMEKWISHA KUCHAGULIWA NA MUNGU, NDIO SISI, TULIOKULA NA KUNYWA PAMOJA NAYE BAADA YA KUFUFUKA KWAKE KUTOKA KWA WAFU.
42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu”.
Soma pia Matendo 2:31-32
Unaona Ikiwa leo hii, hatutaki kujibidiisha kumtafuta Yesu, hatutaki kujifunza Neno lake, hatutaki kusikia habari zake,tunaona kama zinatuchosha, na bado tunasema tumeokoka, tufahamu kuwa, zipo hatua ambazo kamwe hatutakaa tumfikie Yesu.
Tunakosa shabaha pale tunapodhani kumjua Yesu ni kuokoka tu, na kutoa pepo halafu basi. Hatujui kuwa YESU NDIO SIRI YA MUNGU mwenyewe.. ambao utimilifu wote wa Mungu unakaa kwa namna ya kimwili (Wakolosai 2:9). Kiasi kwamba tukifikia utimilifu wote wa kumjua yeye, basi hakuna kitu chochote hapa duniani tutakachoshindwa kufanya, au kukijua. Na shetani hapa ndipo anapopapiga vita, kwasababu anajua siku mtu akimfahamu Yesu ipasavyo basi habari yake ndio imeishia hapo.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.
Kwahiyo na sisi tuonyeshe bidii ya kutafuta kumjua yeye, nasi tufikie hatua ya kutufanywa na mashahidi wake kweli kweli , kama alivyofanya kwa mitume wake na wale wengine mwanzoni.
Lakini tukiridhika na Yesu wa kuokokea tu, vivyo hivyo na yeye atajifunua kwetu kama huyo, lakini tukionyesha bidii ya kumtafuta, na kutaka kujua njia zake, na yeye atajifunua kwetu katika nguvu za kufufuka kwake, tutamjua kwa mapana na marefu yake, kama alivyofanya kwa wale watu wachache sana (500). Tutakuwa watu wengine kabisa.
Tuanze kulipigia hatua na hili.
Mafundisho mengine:
KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
Mafundisho
Mataifa ni nini katika Biblia?
Mtume alituasa wakati huu wa mwisho ni wakati wa kutojishikamanisha sana na mambo ya mwilini, au ya ulimwenguni. Embu tutafakari kwa pamoja hivi vifungu hapa chini. Anasema.
1Wakorintho 7:29 “Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana; 30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu. 31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita. 32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; 33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe. 34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe. 35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”.
Unaweza kupata picha alikuwa analenga nini hapo? Ni kwamba hatutakiwi tuvutwe kwenye mambo ya ulimwengu sana, mpaka tukasahau kuwa tunahitaji kumtumikia pia Mungu, angali tukiwa hapa dunia ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho.
Hii inatokea pengine mkristo mmoja ameingia katika ndoa, anasahau kabisa mambo ya Mungu, anaanza kujitaabisha na masuala ya mumewe au mkewe ampendezeje, maombi ameacha, kujifunza neno hafanyi tena.. Sasa katika mazingira kama haya Paulo alisema ukiingia kwenye ndoa, na uwe kama hujaoa, au uwe kama hujaolewa, usilikuze sana jambo hilo, mpaka likakufanya ukawa mlegevu kwa Mungu, kwasababu muda tuliobakiwa nao ni mchache.
Kwani mambo ya kuoa au kuolewa ni ya hapa tu duniani, tukifika huko ng’ambo hayatakuwepo, hivyo si mambo ya kuyatilia mkazo sana, na kusahau mambo ya uzima wa milele mbinguni.
Mwingine amezama katika masomo, kiasi kwamba hata muda wa kuongea na Mungu wake anakosa kabisa..
Mwingine utakuta ameingia katika biashara, na kwa bahati nzuri Mungu amemfanikisha sana, matokeo yake ni kuwa anasahau kabisa mambo ya rohoni anajikita muda wote katika biashara zake, hatengi tena muda wa kusali, au kwenda ibadani, au wa kumfanyia Mungu kitu.
Biblia inatuambia,
31 “Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita”.
Ni kweli tupo katika huu ulimwengu, hatuna budi kuutumia kwa sehemu, lakini tumeaswa, tuwe kama vile hatuutumii, tuwe kama tumejiegesha tu, tusizame huko moja kwa moja, kiasi cha kutufanya tusahau kama sisi ni wapitaji, wenyeje wetu upo mbinguni.
Bali sisi tuishi kama wale mashujaa 300 wa Gideoni, ambao wenyewe, walipopelekwa mtoni kunywa maji, hawakunywa kama Ng’ombe kwa kupeleka midomo yao moja kwa moja kwenye maji, bali walikunywa kwa kuchota kwa mikono yao na kuyalamba kama mbwa midomoni,. Ikiwa na maana kuwa hata maadui zao wangeweza kuja wakati wanakunywa maji yao wasingeweza kuwaua kwa haraka kwasababu wangewaona tokea mbali , tofauti na wale wengine ambao midomo yao ilielekea kwenye maji moja kwa moja, hawaelewi kitu kingine.(Waamuzi 7:4-7)
Vivyo hivyo na sisi, tunaishi hapa duniani, lakini tunapaswa tuishi kwa kuchukulia kawaida kila kitu, ili tusimpe shetani nafasi ya kutuvuta katika mambo mengine, tusizame moja kwa moja kwenye ulimwengu, tunapaswa tupate na nafasi kwa Mungu, kama ni shule, kama ni biashara, kama ni kazi, kama ni ndoa, kama ni sherehe, kama ni jambo lolote lile, sio la kuliumizia kichwa chako sana, au kulisumbukia, au kuliwazia kupitiliza, au kulifurahia sana.
Tukifanya Hivyo biblia inatuambia tutapata muda pia kwa Bwana. Na matokeo yake, hata siku ile ikifika haitatujilia kwa ghafla kama vile mwizi usiku. Maana biblia inasema ndivyo itakavyoujilia ulimwengu mzima. Na hiyo yote ni kwasababu watakuwa buzy katika mambo ya mwilini wakati huo.
Luka 31: 34 “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima”.
Kwahiyo kila siku tulifahamu hili, kuwa sikumoja inapopita, ndivyo tunavyoikaribia ile siku Kuu ya Unyakuo. Hivyo ni wajibu wetu na sisi kuhakikisha ni kwa namna gani tunampendeza Mungu wetu katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho.
Wafilipi 4: 6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”.
Bwana akubariki sana.
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.
UFUNUO: Mlango wa 14
Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)
Kutabana ni nini? (Mika 5:12)
FAHAMU UWIANO MUNGU ANAOHITAJI KUUONA KWETU.
Kuna wakati unaweza kupitia mahali ukajikuta upo katika hali ambayo hujui sababu ni nini, haujui kosa lako ni lipi mpaka upokee mapigo mazito kama hayo. Unabakia kujiuliza maswali kwanini mimi?
Ayubu alipitia mazingira kama hayo, katika maisha yake yote alijitahidi sana kuwa mkamilifu na mwelekevu mbele za Mungu, hakuruhusu dhambi imtawale katika maisha yake yote, alikuwa ni mwombaji, na mkaribishaji mzuri wa wageni, hivyo Mungu akambariki sana.
Lakini ukafika wakati, akashangaa ghafla mambo yamebadilika, mifugo yake yote imeibiwa, mali zake zote zimepotea, kama hilo halitoshi akasikia watoto wake wote 10 wamekufa kwa ajali mbaya sana ndani ya siku moja.. Wakati yupo katikati ya msiba, ghafla tena anaanza kuugua kwa magonjwa ya ajabu, kiasi kwamba inambidi akae kwenye majivu muda wote, alikonda kiasi cha kuona mifupa tu.
Embu jiweke wewe katika hiyo nafasi, unadhani haitakuwa rahisi kumkufuru Mungu? Ni rahisi sana, na ndicho alichokifanya mke wa Ayubu. Lakini Ayubu hakumkufuru Mungu, yeye hakufikia hatua hiyo mbaya bali aliishia kusema KWANINI MIMI?
Kwanini mimi na si mtu mwingine,…Na hiyo kwanini mimi ilimpelekea mpaka kuanza kulaani, kila kitu kwenye maisha yake, akailaani mpaka siku ya kuzaliwa kwake, akaona kama vile yeye si mtu mwenye bahati, ni heri tu asingezaliwa duniani.
Ayubu 3:2 “Ayubu akajibu, na kusema; 3 Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba. 4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie. 5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe……… 11 Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni? 12 Mbona hayo magoti kunipokea? Au hayo maziwa, hata nikanyonya? 13 Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;”
Ayubu 3:2 “Ayubu akajibu, na kusema;
3 Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba.
4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie.
5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe………
11 Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni?
12 Mbona hayo magoti kunipokea? Au hayo maziwa, hata nikanyonya?
13 Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;”
Ayubu, kila kukicha alitamani afe.(Ayu 7:4)
Hiyo hali inawakumba watu wengi sasa hivi hususani pale wanapopitia matatizo fulani madogo au makubwa, aidha wanapofiwa na wazazi wao, au watoto wao, au wanapopoteza mali zao, au vitu vyao ya thamani, au wanapokumbana na magonjwa mazito yasiyotibika, kama vile kansa, kisukari, au ukimwi, wanajiuliza ni tatizo gani walilolifanya mpaka wayapate magonjwa hayo, mbona wanakula vizuri tu, mbona hawatendi dhambi, inakuwaje wakumbane na hizo shida kwenye miili yao.
Wengine, wanauliza kwanini mimi nizaliwe kipofu, nilimkosea nini Mungu, kwanini nizaliwe mfupi, kwanini niwe mlemavu, kwanini nina mapungufu haya n.k..
Sasa katika haya maswali , kwanini! kwanini! kwanini!.. Mungu naye alianza kumuuliza Ayubu maswali mengine ya ziada, ambayo alitaka na yeye ampe majibu yake. Ukisoma Ayubu 38 na kuendelea utaona maswali aliyoulizwa Ayubu ni yapi, ambayo tunajua yote alishindwa kuyatolea majibu yake..Kwamfano maswali haya aliulizwa;
Ayubu 38:28 “Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande? 29 Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa? 30 Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi. 31 Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni? 32 Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake? 33 Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia? 34 Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize? 35 Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa? 36 Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?”
Ayubu 38:28 “Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande?
29 Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?
30 Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi.
31 Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
32 Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?
33 Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?
34 Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize?
35 Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa?
36 Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?”
Akagundua kuwa kumbe ni mambo mengi sana huku duniani, Mungu hajatupa majibu yake, , lakini tunaendelea tu kuishi nayo, wala hatuumizi vichwa vyetu kutaka kuyajua, na maisha yanaendelea kama kawaida. Sasa kwanini tutake kutolea majibu kila hali tunayopitia.
Ayubu baada ya kulijua hilo, alikaa kimya. Akamwambia Mungu hakika nilikosea kuzungumza maneno yasiyofaa. Na baada ya Mungu kugundua kuwa Ayubu kalijua hilo, akaugeuza uteka wake akampa mara dufu zaidi ya vile alivyovipoteza. Na sisi pia, tuliookoka, mambo yanapogeuka na kuwa ndivyo sivyo, sio wakati wa kuanza kulaumu, kwanini iwe mimi na sio Yule,..Kumbuka kila mtu anayo mapito yake, sio kila tatizo utalipatia jawabu lake sasa hivi, pengine utakuja kujua mbeleni au usijue kabisa, kikubwa mshukuru Mungu, na usonge mbele. Wakati utafika jaribu hilo litaisha, usianze kuuliza maswali ambayo hujui majibu yake, utaishi kulaumu, Mtumaini Mungu.
Songa mbele kama mkristo uliyeokoka..Timiza wajibu wako wa kumwomba Mungu na kumshukuru, na kuishi maisha ya utakatifu, Upo wakati Mungu atakuondolea huo ugonjwa, au hilo tatizo, au hiyo shida.
Shalom.
HUDUMA YA (ELIFAZI, SOFARI, NA BILDADI).
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Maswali na Majibu
JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.
KWANINI KRISTO AFE?
Jibu: Tusome..
2Wakorintho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha”.
Kuhuisha maana yake ni “kutoa uzima/uhai”, Mungu pekee ndiye anayetoa uzima na kutupa sisi. Hivyo hapo iliposema andiko huua, bali Roho huhuisha Maana yake ni kwamba, maandiko bila ufunuo wa Roho yanaweza kuipoteza roho ya mtu na kuiua kabisa (aidha mtu huyo akafa kiroho au hata kimwili kabisa). Lakini yakitumiwa kwa uongozo wa Roho, yanampa mtu uzima, na hata kama alikuwa amekufa anaweza kufufuka tena.
Sasa tutazame ni kwa namna gani andiko linaweza kumuua mtu kimwili, na baadaye kiroho.
Walawi 24:19 “Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo; 20 jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo”.
Walawi 24:19 “Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo;
20 jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo”.
Kumbukumbu 19:21 “Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu”.
Hapo anasema UZIMA kwa UZIMA, maana yake ni kwamba, mtu aliyetoa uhai wa mwenzake kwa makusudi sharti na yeye uhai wake uondolewe, au kama kamvunja jino, na la kwake pia litaondolewa, kama kampiga na kumtoboa jicho, na la kwake pia litatobolewa.
Kwahiyo hili andiko na mengine mengi yakichukuliwa kama yalivyo yanaua. Na watu wengi walikuwa wanakufa kwa maandiko hayo, ilikuwa mwanamke akifumaniwa katika uzinzi, hukumu yake ilikuwa ni kifo cha kupigwa mawe mpaka afe.
Lakini Roho Mtakatifu alipokuja, aliliweka hilo sawa kwa kinywa cha Bwana wetu Yesu Kristo na kusema..
Mathayo 5: 38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino 39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. 40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. 41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. 42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo 43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Mathayo 5: 38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Mfano wa andiko linaloweza kumuua mtu kiroho ni hili…
1Timotheo 5:23 “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara”.
Andiko hili limewapofusha watu macho na kuwafanya wawe walevi, na wasiojali na shetani, amelipigilia msumari hili, lengo lake ni watu wafe bila kutubu ili waende jehanamu ya moto. Roho za wengi, zimekufa katika andiko hili.
Na andiko lingine ni hili.. Mhubiri 9:5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.
Andiko hili limeua watu wengi sana kiroho, na kuishia kuamini kwamba hakuna maisha baada ya kifo, na kwamba hakuna jehanamu wala kinachoendelea..Hivyo wengi kwa andiko hili, wameona ni bora kuishi maisha ya kujipenda hapa duniani, na ya kutokujali, kwasababu baada ya kifo hakuna kitakachoendelea, hata akifanya uasherati, hakuna kwenda kuhukumiwa..Hivyo wengi wamekufa na dhambi zao kwa andiko hili. www wingulamashahidi org
Bwana Yesu, Mkuu wa Uzima alisema…
Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. 30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Hapo Roho anasema kuna hukumu baada ya kifo.
Hivyo ni muhimu sana kumpata Roho Mtakatifu, wakati wa kulisoma Neno la Mungu, kwasababu bila yeye ni vigumu kulielewa Neno la Mungu na kila utakapolisoma ni rahisi kutoa tafsiri zako, na si za Roho Mtakatifu.
Kama bado hujampokea Yesu, huwezi kamwe kuyaelewa maandiko, yatakuwa ni magumu, na kila utakapoyasoma utakuwa unapata maana ambazo sio sahihi, lakini pale tu utakapoamua kufanya uamuzi wa kumpokea Yesu moyoni mwako, na ukadhamiria kutubu na kuziacha dhambi zote unazozifanya kwa wazi na kwa siri, na ukawa tayari kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa Jina la Yesu Kristo, siku hiyo hiyo Roho Mtakatifu ataanza kufanya kazi ndani yako na kuumba jambo jipya.
Bwana akubariki
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kuwatema farasi, maana yake ni nini?
Wapendwa nini maana ya hili andiko “Ushuhuda wa YESU ndio ROHO YA UNABII” (ufunuo 19:10)?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
Shalom, nakusalimu katika jina lipitalo majina yote la Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme YESU KRISTO, Mungu mkuu, Sifa na heshima, na utukufu ni vya kwake milele. Yeye ndiye mwokozi wetu, na huo ndio ukweli pekee uliodumu na utakaodumu duniani kwa wakati wote.
Tukisoma kile kitabu cha Matendo ya mitume 7:17 inasema..
“17 Basi wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu ulipokuwa unakaribia, wale watu wakazidi na kuongezeka sana huko Misri, 18 hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri, asiyemfahamu Yusufu. 19 Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi”.
“17 Basi wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu ulipokuwa unakaribia, wale watu wakazidi na kuongezeka sana huko Misri,
18 hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri, asiyemfahamu Yusufu.
19 Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi”.
Lipo jambo moja tunaweza kulitazama leo hii, biblia inatuambia wakati ile ahadi Mungu aliyomuahidia Ibrahimu kuwa siku moja uzao wake, utakwenda kuirithi nchi ya Kaanani aliyomuahidia, ulipokaribia, biblia inasema, kuna tukio lilifuata baada ya pale, na tukio lenyewe ni wana wa Israeli kuongezeka kwa kasi sana kule Misri.
Jambo ambalo liliwashtusha wamisri waseme ni nini kimewapata hawa watu mpaka wanazaliana kwa spidi kasi hivi, yaani pengine ndani ya miaka kumi tu , idadi imejizidisha mara 3 ukilinganisha na miaka mingine yote iliyopita huko nyuma, miaka mitatu tena mingine vivyo hivyo. Hilo liliwashtusha sana wamisri mpaka kuona tunazidiwa sasa tubuni njia mbadala..
Kutoka 1:7 “NA WANA WA ISRAELI WALIKUWA NA UZAZI SANA, NA KUONGEZEKA MNO, NA KUZIDI KUWA WENGI, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao. 8 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. 9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12 LAKINI KWA KADIRI YA WALIVYOWATESA NDIVYO WALIVYOONGEZEKA NA KUZIDI KUENEA. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli”.
Kutoka 1:7 “NA WANA WA ISRAELI WALIKUWA NA UZAZI SANA, NA KUONGEZEKA MNO, NA KUZIDI KUWA WENGI, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao. 8 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.
10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.
11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
12 LAKINI KWA KADIRI YA WALIVYOWATESA NDIVYO WALIVYOONGEZEKA NA KUZIDI KUENEA. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli”.
Umeona? Lakini biblia inatuambia kuongezeka kwao, hakukuwa bure tu bali kulikuwa na sababu, na sababu yenyewe ni kuwa ILE AHADI YA MUNGU ilikuwa inakaribia kwenda kutimizwa juu yao.
Nachotaka uone ni kuwa, sikuzote, ahadi ya Mungu inapokaribia kutimizwa, Mungu huwa anahimiza mambo fulani fulani yafanyike haraka sana ndani ya kipindi kifupi sana kisichoweza kudhaniwa. Wana wa Israeli pengine walikaa zaidi ya miaka 300, kule Misri na uongezekaji wao ulikuwa wa wastani tu, au wa kawaida sana, lakini walipokaribia karibia miaka 400 hapo, ndipo idadi ya watu ikaongezeka kwa ghafla sana.
Jambo hili linafunua nini kwa agano jipya?
Wengi wetu hatuijui vizuri historia ya ulimwengu, tunadhani mambo yalivyo sasahivi ndivyo yalivyokuwa miaka ya nyuma. Ndugu, fahamu karne ya 20 na ya 21, ndizo karne pekee ambazo zinawashangaza watu wengi sana ulimwenguni hususani wale wanaofuatilia habari za historia, tukisema karne ya 20 tunamanisha kuanzia mwaka wa 1901.
Mambo mengi sana yametimia yaliyokuwa yanazungumziwa na Bwana Yesu, pengine yalionekana kama ni uongo kwasababu hayakuwahi kutimia kwenye miaka yote ya huko nyuma. Lakini ilipotimia karne ya 20 yakaanza kuonekana, Jambo mojawapo ni kuchipuka tena kwa taifa la Israeli, ambalo linafananishwa na mtini. Pili, kutokea kwa vita vya dunia viwili, kulipuka kwa magonjwa yasiyohesabika, na yasiyotibika, hata mafua unayofahamu wewe, hayakuwepo miaka ya 1800, zote hizo zilizungumziwa katika Mathayo 24, Marko 13 na Luka 21
Na mbaya zaidi, kulipuka kwa wimbi la manabii wengi wa uongo duniani. Hili tumelishuhudia sana sana kwenye hii karne yetu ya 21, kote huko nyuma hakukuwahi kuwa hata na mtu aliyejiita nabii, lakini leo hii ni kitu cha kawaida sana..
Mambo mengine ni Kuongezeka kwa maasi, watu kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu, kuongezeka kwa teknolojia, smartphones, n..k ambapo kunatimiza ule unabii wa Danieli unaosema maarifa yataongezeka(Danieli 12:4)…
Hayo yote ni kwasababu ile ahadi ya Mungu ya kulinyakuwa kanisa lake inakaribia kutokea hivi karibuni, kwahiyo Mungu anazidisha spidi ya mambo yote yatokee haraka haraka. Na mambo yote yakishatimia ghafla, atatokea Kristo na kulinyakua kanisa lake.
Ni kitendo cha kufumba na kufumbua, hutaona mtu. Tupo ukingoni mwa wakati, Mungu anahimiza mambo yake haraka haraka sasa hivi, Si wakati wa kuwa kama mke wa Lutu, mguu mmoja nje, mwingine ndani, ni wakati wa kumfuata Yesu wewe, kama wewe.
Luka 17:32 “Mkumbukeni mkewe Lutu. 33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya. 34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]”
Luka 17:32 “Mkumbukeni mkewe Lutu.
33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.
34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]”
Swali ni Je, umezaliwa mara ya pili, Je, wewe bado ni rafiki wa dunia? Je bado unaishi maisha ya kuwapendeza marafiki na wazazi? Mkumbuke mke wa Lutu.
Ni vitu vipi hivyo viwili visivyoweza kubadilika? (Ebr 6:18)
Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
VIKAANGUKA MACHONI PAKE VITU KAMA MAGAMBA.
Wakati mwingine Mungu anatumia njia za dhahiri kabisa kufunua yale yanayoendelea rohoni. Kwamfano utaona wakati ule Yesu anakutana na yule kichaa, na kuyaamuru yale mapepo yamtoke, tukio lililofuata baada ya pale ni wale nguruwe kupelekwa moja kwa moja ziwani na yale mapepo na kuuliwa huko. Hiyo ni kufunua kuwa mapepo hayana malengo mengine zaidi ya kuua tu na kuangamiza, wala hakuna pepo zuri au jini zuri kama watu wa dini nyingine wanavyodhani, maadamu una pepo ndani yako, basi ujue lengo lao ni moja, kukuangamiza tu.
Na ndio maana utaona lile pepo ambalo wanafunzi wa Yesu walishindwa kulitoa, baba wa yule kijana alisema, mara nyingi linamtupa mwanangu kwenye maji..mara nyingine kwenye moto(Marko 9:22)..Fikiria wewe unadhani lengo lake lilikuwa ni nini kama sio kumwangamiza. Hivyo hata leo hii, ukiwa na pepo la uzinzi, ujue kuwa shabaha ni wewe ukutane na ukimwi, ufe kabla ya wakati wako, au hata ukumbane na mabalaa mengi mengi yasiyoeleweka,ili tu uondoke katika hali ya dhambi ujikute kuzimu.
Sasa, tukirudi katika habari ya mwanzo, tulisema Mungu huwa anaruhusu wakati mwingine mambo Fulani yaonekane kwa dhahiri ili kufunua hali halisi ya mtu ilivyo rohoni.
Sehemu nyingine tena utaona ni pale mtume Paulo, alipokutana na Yesu alipokuwa anaelekea Dameski kufanya kazi yake ya kuliharibu kanisa la Mungu, Na Bwana alipomtokea kama tunavyojua habari, ni kuwa nuru ya Yesu ilimwangazia pande zote, sasa kutokana na kuwa nuru ile ilikuwa kali, ilimfanya awe kipofu wa muda. Mpaka alipokwenda kuombewa na mtu mmoja aliyeitwa Anania baada ya siku tatu ndipo akaona tena.
Lakini baada ya kuombewa kwake, biblia inatuambia, vitu kama magamba vilidondoka machoni pake. Tusome.
Matendo 9:17 “Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18 MARA VIKAANGUKA MACHONI PAKE VITU KAMA MAGAMBA, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; 19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.
Matendo 9:17 “Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
18 MARA VIKAANGUKA MACHONI PAKE VITU KAMA MAGAMBA, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.
haya magamba yalikuwa kwenye macho ya Paulo sikuzote lakini hakuwahi kuyajua, mpaka siku anaombewa na kudondoka ndipo anajua kitu hicho kilikuwa
Hiyo ilikuwa inafunua hali halisi ya Paulo ilivyokuwa rohoni. Alikuwa amepofushwa kikweli kweli na shetani, kwa kuwekewa haya magamba ya adui, bila hata ya yeye maskini kujijua.
Sasa haya magamba ya adui yapoje?
Haya, hayana malengo ya kuziba kila mahali katika maisha ya mtu hapana, haya yapo mahususi kukuziba lile eneo linalohusiana na kumjua Mungu. Unaweza ukawa na elimu yako nzuri, unaweza ukawa na hata na fedha nyingi, lakini unaweza ukashindwa kuiona njia Ya wokovu wa Mungu.
Pengine utakuwa mwepesi hata katika kufanya mambo mengine yote, utakuwa mwepesi kuelewa hata kanuni nyingine za maisha ya kila siku, lakini utakosa wepesi wa kuifahamu njia ya wokovu.
Ukihubiriwa habari za msalaba, kwako zinakuwa kama ni habari za kishamba vile, hata ukielezwa habari za kuzimu hazikushtui tena, haijalishi utatolewa na shuhuda nyingi kiasi gani, kwako ni kawaida tu, na ndio maana unaendelea na ulevi wako na uzinzi wako badi leo hii, sasa ukiona upo katika hali hiyo basi ufahamu magamba hayo ya rohoni yameshawekwa kwenye macho yako pasipo wewe kujijua. Pengine ulichobakiwa nacho ni kuisifia tu dini yako.
Na hali hiyo inaweza kuwa mbaya kiasi kwamba ukawa hata unaupinga wokovu, na kufanya vita nao kama ilivyokuwa kwa Paulo…Lakini jiulize unadhani Paulo alikuwa amekusudiwa kuwa mtu wa namna ile, ? Jibu ni hapana, ndio maana baada ya kuondolewa magamba hayo, akaupenda wokovu kwa namna isiyo ya kawaida, akawa mhubiri nambari moja wa njia ya wokovu.
Hii ni kazi ambayo shetani anaifanya kila kukicha, watu wanapofushwa macho yao ya rohoni, wasimjue Mungu, au wasione umuhimu wa wokovu, angali wakiwa bado hapa duniani.
2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
Magamba haya ukiyaendekeza ndani ya maisha yako, madhara yake utakuja kuyaona baada ya kifo. Kwasababu siku utakapokufa moja kwa moja utajikuta kule kuzimu, Na wewe huko utakuwa katika majuto yasiyokoma, kama ya yule tajiri wa Lazaro(Luka 16:19-31)… Mahali ambapo aliomba sana ndugu zake wasifike huko..
Ndugu yangu watu wanaoshuka kuzimu kila siku idadi yake haihesabiki, na wote huko laiti tungeonyeshwa hali zao zilivyo, jinsi wanavyojuta, jinsi wanavyosema tulipofushwa kiasi gani mpaka tukaudharau msalaba, na leo tupo hapa, tusingeuchukulia wokovu wetu juu juu tu. Hivyo tubu dhambi zako, mgeukie Kristo, na yeye atakuokoa. Epuka magamba haya ya ibilisi.
Kwasababu siku hizi ni za mwisho, na Kristo yupo mlangoni kurudi.
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?
Contact
Paulo katika kazi yake ya utume, hakuwa tu na jukumu la kuwahubiriwa watu Kristo ili wamwamini, kisha wapokee ondoleo la dhambi halafu basi..Hapana, bali pia ni mtu ambaye alikuwa anatia bidii nyingi sana katika kuwajuza watu juu ya ukweli wote wa Mungu na siri nyingine zilizojificha katika maandiko tangu zamani.
Na ndio maana utaona alisema..
Waefeso 5:17 “KWA SABABU HIYO MSIWE WAJINGA, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.
Paulo alipiga vita ujinga ambao watu wanao kuhusu Mungu, kwasababu alijua ni jinsi gani unavyoweza kumgharimu mkristo kwa sehemu kubwa. Ujinga ni ile hali ya mtu kukosa maarifa ambayo kama angeyapata basi yangemsaidia kuishi au kutenda mambo fulani kwa ufanisi mahali alipo.. Kwamfano, mtu ukikosa kufahamu kuwa duniani kuna kitu kinachoitwa teknolojia, na kwamba ukitaka kuwasiliana na mtu aliye mbali utatumia kifaa kinachoitwa simu,
Sasa wewe hataki kusikia habari za simu, badala yake unataka tu kukaa maporini , kuwinda swala, kuna wakati utafika utahitaji kuwasiliana na ndugu zako wa mbali, hapo ndipo itakugharimu utumie miguu yako au punda kwenda kuwafuata na hiyo pengine itakuchukua mwezi mzima kwenda na kurudi, kiasi kwamba kama angepata maarifa ya simu, au vyombo vya moto basi kuwasiliana kwako au kusafiri kwako kungekuwa ni kurahisi sana na kwa haraka.
Vivyo hivyo na katika Ukristo, tunakosa maarifa mengi sana, na hiyo inapelekea pengine tunashindwa kuufurahia wokovu wetu , au kuona safari hii ni ngumu sana, au kushindwa kabisa kustahimili mengi. Siku zote Hatuwezi kumtumikia Mungu, juu ya kiwango cha ufunuo tulichonacho kuhusu yeye. Kiwango chako cha kumwelewa Mungu ndicho kitakachoeleza maisha ya wokovu unayoishi sasa.
Sasa Mtume Paulo ni mtu ambaye alikuwa anatamani kupata maarifa ya kutosha kuhusu ufalme wa mbinguni, na ndio maana siri nyingi zihusuzo kanisa, na Mungu tunazipata katika nyaraka zake.Na ndio maana sehemu nyingi utaona anasema Neno hili SITAKI MKOSE KUFAHAMU. Akiwa na maana hataki tuwe wajinga..
Embu tuangalie baadhi ya vitu ambavyo alitaka sisi tusikose kufahamu.
Anasema..
1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini”.
Ukiendelea kusoma pale utaona anaeleza jinsi siku ya unyakuo itakavyokuwa, kwamba utatangulia kwanza ufufuo wa wafu, hivyo wewe kama ni mkristo, ukiifahamu siri hiyo kwamba lipo tumaini la kufufuliwa na kuonana wa wapendwa wetu katika Imani waliotutoka, hatutakuwa na huzuni ya kupitiliza, kama watu wa kidunia walivyo, hatutakuwa wa kulalamika, na kulaumu laumu muda wote.
2) Kuhusu hukumu watakayokabidhiwa watakatifu.
1Wakorintho 6:2 “Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?”
Watakatifu watakaoshinda hawatahukumu tu ulimwengu, bali mpaka na malaika, Je ulishawahi kulifikiria hilo wewe utawahukumuje malaika? Fikiria tena hilo, uone ni mambo makubwa kiasi gani Mungu amewaandalia watu wake huko mbeleni.
3) Siri ya Yesu iliyojificha katika agano la Kale.
1Wakorintho 10:1 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.
1Wakorintho 10:1 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.
Paulo anatufunulia siri nyingine kuwa hatupaswi kusoma agano la kale kama historia Fulani tu, tunapaswa tujue ndani ya historia zile Kristo amejificha, na Hivyo tunapaswa tusomapo tumwone Kristo, kwasababu vyote vile vilimfunua yeye. Hivyo Paulo anatuasa tusiwe wajinga pia katika hilo, tusome mawazo yetu tukiyaelekeza kwa Kristo.
4) Kuhubiri injili kuna dhiki.
2Wakorintho 1:8 “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi”.
Wengi tunadhani katika kumtumikia Mungu ni mteremeko tu wakati wote, hapana, Bwana Yesu kiongozi wetu alipitia dhiki, mitume pia walipitia dhiki wakati mwingine, vivyo hivyo na wewe, unapaswa ulielewe hilo, ili kusudi kwamba litakapotokea, usije ukawa mjinga kwa kuacha kuifanya kazi ya Mungu, ukasema huyu ni shetani, kwani Mungu sikuzote haruhusu watu wake wapitie dhiki.
5) Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Anataka tufahamu kuwa hii miili tuliyopewa na dhamana, ni mali ya mwingine sio yetu, hivyo tuithamini kwasababu tukiiharibu kwa uzinzi, au pombe, au michoro, au chochote kile, tutaharibiwa na sisi. Hilo tusiwe wajinga, wengi wameuliwa na Mungu kwa njia hiyo.
6) Utumishi wa Madhabahuni.
1Wakorintho 9:13 “Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?”
Paulo hataki watu wawe wajinga pia kufahamu, watumishi wa Mungu wana haki ya kula vya madhabahuni, kwasababu ndivyo Mungu alivyoagiza na wala sio mwanadamu. Hivyo sio jambo la kujadiliana nalo au kushangaa utakapokutana nalo.
7) Karama za Rohoni.
1 Wakorintho 12:1 “Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu”.
Hapa yapo makundi mawili ya wakristo, lipo kundi ambalo haliamini kabisa, au haliruhusu karama za Mungu kutenda kazi katika kanisa la Kristo, wakisikia kuna mtu anakarama ya kuona maono wanasema ni shetani, wakiona kuna mtu ananena kwa lugha wanasema huyo sio Roho. Hivyo utakuta kanisa limebakiwa kuongozwa na wenyeviti na makatibu, na maaskofu- jina, na makasisi, basi, hakuna chochote cha Zaidi ya litrujia kufuatwa.
Kundi lingine, ni lile lisiloweza kumbanua karama za Roho, huduma za Roho, Utendaji kazi na Ujazo/Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Haya yote Mtume Paulo alitaka tusiwe wajinga, matokeo yake ni kuwa leo hii utakutana na watu wengi wenye karama huku wakiendelea na maisha yao ya kale wakidhani kuwa wana Roho Mtakatifu kumbe walishaachwa zamani, japokuwa karama zao zinaendelea kufanya kazi.
8) Mpango wa Mungu kwa mataifa.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”.
Hii ni siri kubwa ambayo tukiijua hatutaishi maisha ya patapotea kwenye ukristo wetu, siku tukifahamu kuwa Utimilifu wa mataifa utawasili, na kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea sisi hatutakuwa na neema tena ya kuupokea wokovu, bali itarudishwa tena Israeli kwa kipindi kifupi, ndipo tutakapoishi maisha ya umakini sana katika Ukristo wetu.
Wengi wetu tunadhani, tutaendelea tu hivi hivi mpaka Yesu atakaporudi, Ndugu, Wokovu utaishia kwa wayahudi sio sisi. Kwahiyo tukiwa wajinga tukidhani kuwa tutaendelea hivi hivi, tujue tupo katika hatari kubwa sana ya kuuokosa, Unyakuo. Bwana Yesu kuna wakati atasimama, na kuufunga mlango. Wakati huo utakuwa ni hapa hapa duniani, na sio mbinguni. Kwasababu Utimilifu wa mataifa utakuwa umewasili. Mungu atakuwa ameshamalizana na sisi, utakuwa ni wakati wa wayahudi tena.
Embu jiulize, Je, ikiwa neema hiyo inarudishwa kule Israeli, utampatia wapi tena Kristo, na wakati Roho Mtakatifu hayupo tena juu yako. Ikiwa leo hii, unamkataa unampinga, angali neema ipo, unadhani nafasi hiyo itakuwepo tena? Hivyo usiichezee hii neema ambayo ndio tunakaribia kumaliza nayo. Dalili zote zinaonyesha kuwa hatuna muda mrefu Unyakuo utapita. Wafu watafufuliwa, na sisi tutaungana nao kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
Hivyo tubu dhambi zako mgeukie Mungu.
MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
UTAWALA WA MIAKA 1000.
CHUKIZO LA UHARIBIFU