Category Archive Uncategorized @sw-tz

TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU

Nakusalimu katika jina tukufu sana la mwokozi wetu Yesu Kristo, Nakualika katika kuyatafakari maneno ya uzima.

Leo tutajifunza siri mojawapo iliyokuwa nyuma ya watu wa zamani, ambayo tukiitumia na sisi italeta mageuzi makubwa sana katika ulimwengu huu tunaoishi. Wengi wetu tunadhani watu wa leo wanayoakili zaidi ya kuwashinda wale, lakini ukweli ni kwamba yapo mambo mengi yalifanywa na watu wa kale, ambayo mpaka leo hatuwezi kuyafanya. Mfano mmojawapo ni yale mapiramidi yaliyopo Misri (ambayo yapo katika maajabu saba ya dunia), teknolojia iliyotumika pale, hadi sasa hakuna ujenzi unaoweza kuwa kama ule, ijapokuwa tunazo teknolojia kubwa na za kisasa.

Tukisoma katika maandiko tunaona, Jinsi Babeli ilivyoanza kujengwa na kusitawi. Lakini hilo halikuwa jambo zito, kwasababu miji mingi pia ilikuwa inajengwa. Jambo lililoipelekea Babeli kuwa tofauti na miji mingine ni pale watu walipotaka kuunda Mnara, ndani ya mji ule, lengo lao lilikuwa ni kufika MBINGUNI, ili wajipatie jina. Sasa wengi wetu tunaona kama walikuwa ni wajinga kuunda hiyo Projekti yao. Tunadhani walikuwa wanafanya jambo la masiara au walikuwa hawaelewi kitu wanachokifanya. Ni sawa na leo mtu akuambie ninaunda ndege, ambayo itanifikisha mbinguni, ni rahisi kusema amerukwa na akili. Lakini maandiko yanatuonyesha watu hawa, walikuwa wanajua wanachokifanya mpango huo wangeweza kufanikiwa kama Mungu asingeingilia kati. Embu tusome habari hiyo tuone jambo hilo;

Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.  2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 

3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.  4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 

5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.  6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA. 

7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.  8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.  9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.

Umeona hapo? Mungu hakusema hawa watu wamerukwa na akili, wanafanya kazi isiyokuwa na faida, bali alisema hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Maana yake ni kuwa watafanikiwa, Hivyo Mungu akaangalia NGUVU yao ya kufikia adhma yao ipo wapi? Akaona kuwa sio katika ile teknolojia, bali katika ule USEMI MMOJA waliokuwa nao.

Usemi maana yake ni NIA. Hawa watu waliingia maagano, wakapatana kwa moyo mmoja, kwamba kila mmoja atajitoa kwa akili, hali na mali, kuhakikisha Mnara huo unajengeka na kilele chake kinafika mbinguni, hata kama itawagharimu miaka 1000, lakini mwisho wa siku ni lazima wafike mbinguni. Lakini Mungu akaenda kuuchafua usemi wao wakawa hawaelewani baada ya pale, kwasababu walichokuwa wanakijenga ni kwa ajili ya JINA LAO na sio jina la MUNGU. Hivyo Usemi wao ukachafuliwa wakawa hawaelewani, mpaka na lugha zao zikageuzwa pia.

Ni nini Bwana anataka tuone hapo,

Ni nguvu ya USEMI MMOJA.

Na sisi kama kanisa la Kristo lililo hai. Nafasi yetu ya kuufikia utukufu WOTE wa Mungu ulio mbinguni tunao.

Kwasababu Tayari siku ile ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alirudisha USEMI HUU mmoja katikati yetu. Na ndio maana siku ile utaona watu walianza kunena kwa lugha za mataifa mengine magheni, kuonyesha kuwa Sasa Mungu anataka mataifa yote wakaribie waliunde taifa la Mungu haijalishi lugha zao, jinsia zao, rangi zao. Aliwakumbusha tukio lile la Babeli, kwamba sasa lianze kufanyika tena kwa jina la Bwana. Watu wale wakatii na siku ile ile kanisa likaanza. Mnara wa Mungu ukaanza kujengwa duniani.

Matendo 2:1  “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2  Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3  Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5  Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6  Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

7  Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8  Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9  Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia.

10  Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,.11  Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.

12  Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?

Na ndio maana hatushangai kwanini Kanisa la kwanza lilikuwa na mapinduzi makubwa sana. Kwa kipindi kifupi sana injili ilienea duniani kote, na walikuwa hawana vyuo vya biblia. Ni kwasababu walikuwa na USEMI mmoja.

Lakini leo kanisa limevunjika vunjika, shetani kalisarambaratisha, kachafua lugha yetu. Hata ndani ya kanisa moja kila mmoja anao usemi wake. Ijapokuwa wote mnaliamini Neno hilo hilo moja. Kwasababu gani, ni kwasababu tunatafuta utukufu wetu wenyewe na sio ule wa Mungu.

Ni kweli tutaunganishwa na Neno lakini tusipotaka kujishusha na kutii, ili tumwinue Kristo na sio sisi wenyewe, kamwe hatutaona utukufu wa Mungu kama vile inavyopaswa. Hatutaufikia moyo wa Mungu mbinguni, hatutaona udhihirisho wa wazi wa Miujiza mikubwa ya Mungu katika kanisa. Ni sharti tujikane nafsi zetu kila mmoja tumfuate Yesu , ili tuujenge mnara huu wa Bwana.

Luka 14:27  “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28  Maana ni nani katika ninyi, KAMA AKITAKA KUJENGA MNARA, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? 29  Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki”.

Tufahamu kuwa kanisa sio shirika la kijamii, sio huduma, wala sio chuo Fulani, bali ni udhihirisho wa Mungu duniani kupitia watu wake aliowakomboa. Hivyo ni lazima sisi kama viungo vya Kristo tujishikamanishe tuwe mwili mmoja Ili Kristo atende kazi zake duniani kama alivyokuwa anatenda zamani. Na hii inaanza na mtu mmoja mmoja, pale tunapodhamiria kuyatii maneno ya Kristo.

Bwana atujalie kuliona hilo.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?

Pentekoste ni nini?

NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?

USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.

Kibiriti ni kitu gani? kama kinavyozungumziwa kwenye maandiko?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Rudi nyumbani

Print this post

Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma? 

SWALI: Nini maana ya haya maneno Mungu aliyomwambia Ayubu kuhusiana na  tabia za Mbuni?

Ayubu 39:13 Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma?  14 Kwani yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi, Na kuyatia moto mchangani,  15 Na kusahau kwamba yumkini mguu kuyavunja, Au mnyama wa mwitu kuyakanyaga.  16 yeye huyafanyia ukali makinda yake, kana kwamba si yake; Ijapokuwa taabu yake ni ya bure, hana hofu;  17 Kwa sababu Mungu amemnyima akili, Wala hakumpa fahamu.  18 Wakati anapojiinua juu aende, Humdharau farasi na mwenye kumpanda. 


JIBU: Ukianzia kusoma mistari michache ya juu katika hiyo hiyo  sura  ya 39, Utaona Mungu anamweleza Ayubu baadhi ya wanyama ambao wanauwezo fulani mkubwa lakini hauwasidii kufanya mambo ya msingi, kwamfano mstari wa 5-8, anamtaja punda-milia, ni mnyama anayefanana na punda, ana nguvu na uwezo wa kukimbia zaidi hata ya punda, lakini je! Anamuuliza Ayubu unaweza kumkamata na kumfanya mtumwa wako akubebe mizigo? Au akulimie. Jibu ni la!

Mstari wa 9-12, anamtaja tena, Nyati, anamsifia nguvu zake, kwamba ni nyingi sana, lakini je utaweza kumfunga nira na kumwambia akulimie shamba lako kama ufanyavyo kwa ng’ombe? Jibu ni la kwasababu jambo hilo halipo ndani yake.

Na hapa kwenye mstari wa 13-18 Anamtaja tena Ndege mbuni na sifa zake. Anasema mabawa yake ni bora na mazuri, kiasi cha kuweza kuyatamia vema mayai ardhini zaidi ya ndege wengine wote duniani. Lakini kinyume chake ni kuwa mbuni ni ndege asiyejali mayai wala vifaranga vyake kuliko ndege wote unaowafahamu. Japokuwa anaouwezo mkubwa wa kuwashinda maadui zaidi ya ndege wote, lakini uwezo wake hautumii katika mambo yaliyo na faida. Mbuni anataga popote tu, hata kando ya njia,

hawezi kutafuta sehemu iliyo salama kama ndege wengine ambao huenda sehemu za maficho na kutaga huko ili watoto wao wawe salama pindi wazaliwapo lakini yeye hilo halijali, anataga popote apaonapo, matokeo yake ni aidha mayai yake kukanyagwa na wanyama wakubwa au kuibiwa na kenge au wanyama wengine wezi. Mbuni anaouwezo wa kutaga mpaka mayai 60 na kutamia yote yakatotolewa, lakini kwa tabia yake ya kutokujali anaweza kuambulia vifaranga viwili au vitatu tu. Anaweza kuyasahau mayai yake mchangani, jua au joto la mchangani likamsaidia kotolesha.

Na akishazaa, watoto wake awahudumii, kama wafanyavyo ndege wengine wadogo, ambao huakikisha wanazunguka huko na huko kutafuta vyakula vya watoto wao. Lakini bado maandiko haya yanaonyesha jinsi gani alivyomshapu kuliko hata farasi. Mwendo wa mbuni unauzidi mwendo wa farasi yoyote duniani. Kuonyesha jinsi alivyo mwepesi kujipigania lakini sio watoto wake.

Ni nini Mungu alikuwa anamwonyesha Ayubu ni kwamba, uwezo wa kufanya jambo Fulani sio tija ya mtu huyo kulitenda, kama Mungu hakumpa moyo huo. Wapo wenye mali nyingi, lakini hawana moyo wa kusaidia wanyonge, wapo wenye vipawa vizuri lakini hawezi kumwimbia Mungu. Nguvu zao ni bure hazina faida, wapo wenye uwezo wa kufundisha lakini hawewezi kujinyenyekeza chini ya makusudi ya Mungu watumiwe ili kuujenga ufalme wa Mungu, wanakuwa tu kama punda-milia wa nyikani.

Wapo wenye uwezo wa kulichunga kundi la Mungu lakini wanakuwa kama mbuni, nguvu zao, ukubwa wao hauwasaidii katika kujali kazi ya Mungu. Lakini Bwana akikupa moyo huo, basi utafanya hata kama utakuwa ni dhaifu, utafanya tu. Na hili ndio jambo ambalo tunapaswa tumwombe Bwana . ATUPE MOYO WA KUMTUMIKIA YEYE. Tusitazame kwamba mpaka tupate kitu Fulani ndio tuweze, mpaka tukasomee uchungaji ndio tuweze kuchunga, mpaka tupate pesa ndio tuweze kuisapoti kazi ya Mungu, Bwana atupe moyo huo tangu sasa wakati hatuna uwezo wowote. Kwani huo ndio utakaotusukuma kufanya makubwa.

Lakini pia yapo mambo matatu tunaweza kujifunza:

Jambo la kwanza ni sisi wenyewe, tusiwe kama mbuni ambao hatujali kuhudumia vinavyozalika ndani ya roho zetu. Kwa kutengeneza viota vyetu mahali salama,kinyume chake tunamwachia shetani azichukue mbegu zetu rohoni zinazopandwa, tunaziacha juu juu na matokeo yake ibilisi anakuja kuzila sawasawa tu na mfano wa mpanzi ambao Yesu aliutoa juu ya zile mbegu zilizoangukia njiani ndege wakazila. Ndivyo ilivyo maisha ya wengi, wanapolisikia Neno la Mungu badala walitunze na kulipalilia ndani yao  ili liwazalie matunda wao wanazembea tu, wanaishi kama wanavyotaka. Hivyo tunakuwa wapumbavu kama mbuni, kwa kutokuzalisha chochote.

Jambo la pili: Linahusu familia: Wazazi wasiowajali watoto wao, Ni wajibu kwa mzazi kuwatunza wanawe, kwa kuwahudumia kimwili na kiroho. Imekuwa rahisi leo hii wazazi kujali sana Elimu za watoto wao jambo ambalo ni zuri, lakini kuhusiana na maisha yao ya kiroho wamewaweka nyuma . Hiyo ni hatari kubwa sana, usipompa Mungu watoto wako awalee, shetani atakusaidia kuwaelea. Na matokeo yake utayaona baadaye watakapokuwa watu wazima. Kama mzazi jali sana maisha ya kiroho ya watoto wako, wapeleke Sunday school, wapeleke katika semina za watoto kanisani, wahubirie, wafundishe kuomba, kufunga, kuimba nyimbo za wokovu n.k.

Jambo la tatu: Ni kuhusu watumishi wa Mungu. Bwana hataki tuwe kama Mbuni katika eneo la kulichunga kundi lake. Tunachowaza ni kujijali sisi tu, lakini kuwafuatilia na kuwachunga kondoo wa Bwana tunaona uvivu. Tunasahau kuwa shetani huko nje! Anafanya kazi usiku na mchana kuwarudisha tena ulimwenguni. Hivyo ni angalizo kwetu sisi watumishi wa Mungu. Popote ulipo hakikisha unalilisha na kulichunga kundi la Mungu dhidi ya Yule mwovu. Tuwe na hekima za ‘chungu’

Bwana akubariki sana.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?

“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)

HUDUMA YA (ELIFAZI, SOFARI, NA BILDADI).

Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).

KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)

HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele. Nakualika Tena wakati huu tujifunze maneno ya uzima wa Roho zetu.

Wengi wetu tunavutiwa na maisha ya Yesu alipoanza huduma, tunafurahishwa na jinsi alivyokuwa anafanya miujiza mikubwa, alivyokuwa anahubiri kwenye miji na vijiji, alivyokuwa anaponya wagonjwa,kutoa Pepo na kufufua wafu n.k.

Lakini ni Wachache sana wanaweza kuyatafakari maisha ya Yesu kabla ya huduma. Na hayo ndio Yana umuhimu sana kwetu kuliko Yale aliyoyadhihirisha baadaye.

Maandiko yanasema Yesu alimpendeza Mungu kabla hata hajaanza huduma yoyote ya kuhubiri, kutoa Pepo, na kuokoa watu…alishampendeza Mungu kabla ya hayo yote, tunalithibitisha hilo katika kitabu Cha Mathayo 3 siku Ile anabatizwa na Yohana, 

Mathayo 3:16-17

[16]Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

[17]na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Umeona alishampendeza Mungu kabla hata ya utumishi wowote, kuanza..tofauti na Leo tunavyodhani kwamba ili tumpendeze Mungu, ni sharti tuwe wahubiri wakubwa, au tuwe na upako, au tuwe wachungaji..hiyo sio kanuni ya Mungu.

Hivyo ni lazima tujue Mungu alipendezwa na Yesu kwa kipi? Ni kitu gani alikuwa anafanya mpaka kimfanye akubaliwe na Mungu namna Ile?

JIBU lipo katika Maisha aliyokuwa anaishi Kwa ile miaka 30 kabla ya huduma. Na hapa ndipo tunapaswa tupaangalie sana. Na tujifunze ili na sisi tufanane naye.

Watu wengi wanaona kama maisha yake ya awali yalifichwa sana, zaidi ya Yale aliyoyatenda katika huduma. Ni kweli ukitazama Kwa jicho la nje sehemu kubwa ya injili imeandika juu ya huduma ya Yesu, yaani ile miaka mitatu na nusu ya mwisho ya maisha yake. Lakini ukweli ni kwamba maisha ya Yesu kabla ya huduma ndio yameandikwa kwa wingi zaidi kuliko Yale aliyoyafanya katika huduma.

Hivyo Kwa neema za Bwana tutaona  juu ya maisha yake yalikuwaje, tangu utotoni mpaka anakaribia kuanza huduma.

Sehemu ya kwanza tutaona Mahali ambapo maandiko yameeleza moja Kwa moja maisha yake yalivyokuwa. Na sehemu ya pili tutaona maandiko ambayo sio ya moja Kwa moja, lakini yalimwelezea Yesu maisha yake.

Tukianza na maandiko yanayoeleza moja Kwa moja juu ya maisha yake. Kama yafuatavyo;

1) YESU ALIISHI MAISHA YA KUMPENDEZA MUNGU PAMOJA NA WANADAMU.

Luka 2:52

[52]Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Maisha yake yote alikuwa ni mtu mwenye bidii sana kuhakikisha hafanyi jambo lolote ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Alikuwa yupo makini sana na hilo, lakini zaidi sana alihakikisha katika jamii hawi na harufu mbaya. Alizingatia kuwa na adabu na heshima Kwa Kila mtu aliyekutana naye.

Si ajabu watu walipomuona walimsifia sana, na kusema yule kijana anaheshima, yule kijana ni mtaratibu, natamani watoto wangu wangekuwa kama yule, hatumuoni kwenye kampani za wahuni, hatumuoni akiruka ruka na mabinti barabarani, hatumuoni akitembea Kwa majigambo barabarani, muda wote anatabasamu, hakasiriki haraka, anahekima kama za mtu mzima wakati bado ni kijana..

Yesu alipata sifa isiyo ya kawaida katika jamii, alipoishi duniani, hakuna mtu alimchukia Kwa Tabia zake, alijitoa kwelikweli kuishi kikamilifu katika jamii yake.

Na sisi pia hichi ndio kitu Mungu anataka kukiona katika maisha yetu tunapookoka kabla hata ya kufikiria kuwa wahubiri ,je  mtaani kwako unaonekanaje, shuleni kwako Tabia zako zikoje? Mwonekano wako unawavutiaje watu, ofisini kwako kauli zako na wanyakazi wenzako Zina mvuto gani mpaka watu wakuone wewe ni mtu Bora kuliko wengine wote?

2) YESU ALIKUWA MTIIFU

Luka 2:51

[51]Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.

Aliwatii wazazi wake, hakukuwa na kiburi ndani yake, Neno utiifu kwa Yesu lilikuwa ni kama pumzi kwenye mapafu. Alipoagizwa alifanya, alipotumwa alikwenda, maisha yake yalikuwa ni ya namna hiyo, ili kutunza hadhi yake aliyokuwa nayo ya kuwapendeza watu wote..

Na sisi je tunaweza tukawa watiifu Kwa wazazi wetu wa kimwili na wa kiroho? Tuwatii viongozi wetu wa kiroho hata kama tutakuwa tunafahamu jambo Fulani zaidi ya wao, maadamu Bwana katuweka chini Yao.Hatuna budi kufanana na Yesu. Bwana atusaidie juu ya hilo.

3) ALIPENDA KUKAA NYUMBANI MWA BABA YAKE

Hii ni sifa nyingine inayomwelezea Yesu Tabia yake.

Luka 2:41-49

[41]Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka.

[42]Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu;

[43]na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari.

[44]Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;

[45]na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.

[46]Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

[47]Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.

[48]Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.

[49]Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?

Akiwa kijana mdogo wa miaka 12, hakujali atakula nini, atalala wapi, ataoga wapi..alinogewa na ibada na mafundisho hekaluni akaona hata ule muda wa sikukuu hautoshi yeye kukata kiu yake Kwa Mungu, akaendelea kubaki palepale siku tatu, akiwa amefunga, yeye ni kujifunza tu, na kuyatafakari maneno ya Baba yake..

Wazazi wake hawakujua kuwa angekuwa na kiu Kali namna ile, lakini baada ya pale walimzoea, ikawa ndiyo desturi ya maisha yake yote.

Yesu alikuwa ni mtu asiye mtoro wa ibada, alikuwa anatumia majira yake mengi, kwenda kwenye masinagogi na kutafakari Neno la Mungu pamoja na viongozi wake wa kidini. Hakuwa mtu wa kujitenga Tenga, kama watu wanavyodhani.

Lakini pia alikuwa ni jemedari wa maombi kweli kweli na Dua.

Alikuwa anaomba sana Kwa bidii, Kwa kulia na machozi sana, na kwa kujimimina sana. Maandiko yanasema hivyo;

Waebrania 5:7

[7]Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

Na sisi je tunaweza tukaiga Tabia hii ya Bwana. Je! Furaha yetu ni kuwepo uweponi MWA Bwana muda mwingi au kuwepo katika anasa za Dunia? Au katika biashara zetu? Ni lazima Bwana apewe kipaumbele Cha kwanza.

4) YESU ALIISHI MAZINGIRA YA KUFANYA KAZI

Pamoja na kuwa alikuwa ni mtiwa mafuta wa Bwana ameandaliwa Kwa kusudi moja tu la kuwaokoa watu. Lakini kipindi anasubiri wakati wa Bwana, hakukaa hivi hivi tu, Mungu aliruhusu afanye kazi.

Marko 6:3

[3]Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.

Yesu hakuwa kama Yohana mbatizaji, Kukaa majangwani mbali na watu muda wote, lakini alikuwa ni mtu ambaye yupo katikati ya jamii, anayejulikana, anafahamika, alifanya kazi pamoja na baba yake ya useremala. 

Kwasasa tunaweza kusema alikuwa kariakoo akiuza vifaa vya majumbani na baba yake.

Lakini katika hayo yote aliishi maisha makamilifu ya kujichunga na kuwa na kiasi. 

Hii ni kutuonyesha kuwa unapookoka, uwapo popote pale iwe ni kazini, au kwenye biashara Yako, bado unaweza kumpendeza tu Mungu. Hivyo tusiruhusu kazi ziwe kisingizio cha sisi kutoishi maisha makamilifu. Yesu alikuwa ni mtu wa kujichanganya, lakini hakuruhusu dhambi iwe juu yake. Alipouza kabati hakukwepa kulipa Kodi, hakumuuzia mtu meza Kwa bei isiyoendana na thamani yake.  Hivyo ikampelekea Mungu ampende sana

Hayo ni maandiko ya moja Kwa moja yanayoeleza maisha ya Yesu yalivyokuwa.

Lakini maandiko mengine tunayapata wapi?

JIBU ni kuwa tunayapata katika kinywa Cha Yesu mwenyewe. Kwa kawaida mtu hawezi kusema maneno ambayo yeye hayaishi. Vinginevyo atakuwa ni mnafki, na Yesu yupo mbali sana na unafki, aliukemea sana, hata alipouona ndani ya mafarisayo na waandishi,walipowafundisha watu mambo ambayo wao hawayaishi.(Mathayo 23:1-5)

Hivyo ukitaka kufahamu Kwa kina maisha ya Yesu yalikuwaje sikikiza maagizo yote aliyokuwa anayatoa katika vitabu vyote vya injili.

Kwamfano. Mathayo soma sura yote ya 5-7 utaona maneno kadha wa kadha aliyokuwa anawafundisha makutano.

Anasema wapendeni adui zenu na kuwaombea(Mathayo 5:43-44): Yesu alikuwa anawaombea watu wote waliokuwa wanamchukia Kwa kumwonea wivu. Badala ya kuwatakia mapigo anawatakia maisha marefi, kuwaombea toba wageuzwe.

Anasema mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie la kushoto(Mathayo 5:38-40). Kuonyesha kuwa hakuwa mtu wa Shari, sikuzote alipotukanwa, au alipoaibishwa hakurudisha majibu, Bali alikubali kuaibishwa zaidi, ili aipushe malumbano zaidi.

Anasema amtazamaye mwanamke Kwa kumtamani amekwisha kuzini naye(Mathayo 5:28). Hakuwa na uvumilivu na macho yake, hakuwahi kuruhusu tamaa itawale maisha yake. Alijitenga na vichocheo vyote vya uzinzi, na mazungumzo yote yasiyofaa.

Alikuwa ni mtu wa kusamehe mara Saba sabini, hakuwa anawahukumu watu, au kuwalaumu(Mathayo 7:1-4)

Alikuwa si mtu wa kuruhusu hasira, aliona ukiwa hivyo adhabu Yako inakupasa ziwa la moto (Mathayo 5:21).

Bado alijishuhudia kuwa yeye ni mpole na mnyenyekevu (Mathayo 11:29), aliishi Kwa kujishusha, bila kumdharau yoyote, watu wote walikuwa na nafasi sawa kwake..

Na maandiko mengine mengi, aliyotuelekeza. Hivyo itoshe kusema maisha ya Yesu yaliyomfanya Mungu ampende kabla hata ya huduma ndiyo haya tunayoyasoma katika vitabu vya injili…

Hivyo ndugu Mimi na wewe yatupasa,. Tufikie hapo, acha kumuomba Mungu upako. Utakuja wenyewe tu endapo utampendeza Mungu kwanza kama Bwana Yesu, ukiwa unauhitaji. Penda mema chukia maasi..ndivyo Yesu alivyokuwa hapa duniani, hakuivumilia dhambi kwa namna yoyote, na matokeo yake Bwana akamtia nguvu kuliko mwanadamu yoyote aliyewahi kutokea hapa duniani.

Waebrania 1:9

[9]Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Bwana atusaidie sasa tuishi kama Kristo, ili baadaye tutende kama Kristo.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?

Kibiriti ni kitu gani? kama kinavyozungumziwa kwenye maandiko?

Nini maana ya Ukuta uliopakwa chokaa (Matendo23:3)?

FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

WITO WA MUNGU

Rudi nyumbani

Print this post

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

Zaburi 144:1 “Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno yake ya uzima. Leo tutaona namna ya kuomba maombi ya vita. Tukisema maombi ya vita tunamaanisha maombi ya kushindana na nguvu zote za Yule mwovu katika ulimwengu wa Roho, maombi ya kulegeza vifungo na nira, na minyororo, na kuangusha ngome pamoja na kuta za Yule mwovu zinazokinzana na sisi katika ulimwengu wa Roho, kupitia majeshi yake ya mapepo wabaya.

Ndugu ni lazima ufahamu, Kuna aina nyingi za maombi, kuna maombi ya shukrani, maombi ya mahitaji, maombi ya upatanisho n.k.. Yote haya yana wakati wake wa kuyatumia. Lakini pia yapo maombi ya Vita, ambayo ni lazima sana na ni muhimu kwa Mkristo kuyatumia.

Hivyo siku ya leo tutaona ni jinsi gani tunaweza kutumia maombi haya ili tuziangushe ngome za adui yetu ibilisi kiwepesi.

Baadhi ya watakatifu hawajui namna ya kuomba, wanafikiri pale unaposema shindwa shetani! Shindwa shetani! Kwa Saa tatu, au usiku kucha ndivyo wanavyomwangusha ibilisi. Uhalisia ni kwamba, hatumshindi ibilisi kwa maneno yetu kuwa mengi, Bali tunamshinda ibilisi kwa Neno la Mungu kukaa ndani yetu kwa wingi. Ambalo hilo litakusaidia kujua SILAHA unazopaswa uzitumie kumpiga nazo shetani. Bila kufahamu Silaha zako za kiroho, ni ngumu sana kumshinda shetani kimaombi. Kwasababu maombi yako yatakuwa ni ya juu juu, yasiyokuwa na nguvu za kiroho.

Bwana asipokufundisha kupigana vita, haijalishi maombi yako yatakuwa na maneno mengi kiasi gani, huwezi angusha ngome za adui. Hivyo penda sana kulisoma Neno la Mungu kwa kulitafakari kwasababu huko ndiko utakapojifunza kupigana vita vyako.

Kibiblia zipo silaha nyingi ambazo Mungu alizitumia kuwapigania watu wake, na Leo tutaziorodhesha chache, na tutaona jinsi tunavyoweza pia kuzitumia rohoni. Kwasababu kumbuka Neno la Mungu halijaandikwa kutupa stori  Fulani tu, tuifurahie halafu basi hapana, bali kila tendo, kila Neno linatafsiri kubwa sana rohoni.

Hivyo hizi ni baadhi ya silaha ambazo Mungu alizitumia kuwasaidia watu wake kupigana vita;

MVUA YA MAWE:

Mvua ya mawe

Mungu aliangusha mvua ya mawe kubwa sana, kwa wale watu wa Yerusalemu na wenzake walioungana kupigana na Yoshua kipindi kile wanaenda kuimiliki nchi yao, Utaona baadhi yao waliuliwa na Israeli, lakini wengi wa hao Mungu alimalizia kutoa hazina yake ya mvua kubwa ya mawe ikawaangamiza wengi sana kuliko hata wale waliouliwa na Yoshua.

Yoshua 10:11 “Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa katika kutelemkia Bethhoroni, ndipo Bwana alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao hata kufikilia Azeka, nao wakafa; hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa Israeli kwa upanga”

Jinsi ya kuomba: Bwana peleka, mawe yako ya barafu, katika madhabahu Zote za ibilisi, peleka mvua yako ya barafu katika vilinge vya kichawi, vinavyosimama kinyume na imani yangu. Haribu, bomoa, kila mbinu iliyoundwa dhidi yangu mimi (Taja maeneo yote ya maisha yako). Kama ulivyomshindia Yoshua nishindanie na mimi. [Hivyo Endelea kuita mvua hiyo na katika ulimwengu wa Roho, kwa jinsi unavyoiita kwa imani ndivyo inavyokuwa].

KIKOTO:

Yesu alipoingia hekaluni, alikutana na watu walioigeuza nyumba ya Mungu kuwa pango la wanyang’anyi. Ndipo akaunda kikoto kile, akapindua meza zote na kuwachapa wote waliofanya biashara pale, akawafukuza hekaluni kwa mamlaka yote, hekalu likawa safi kwa muda mfupi.

Yohana 2:15 “ Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16  akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”

Namna ya kuomba: Bwana naunda kikoto chako, napindua madhahabu zote za kipepo zilizoundwa moyoni mwangu na Yule adui, ninatawanyisha, ninasambaratisha, kila uovu, kila sanamu iliyopachikwa na Ibilisi (taja maeneo yote yanayohitaji maombi), kinyume na mapenzi ya Mungu. Ninavuruga kazi zote za ibilisi, kikoto cha Bwana kisafishe mwili wangu, kisafishe ibada yangu, kisafishe maisha yangu ya rohoni, kisafishe nyumba yangu, Naondosha uovu wa kila namna hata katika kazi yangu. [Sasa kwa jinsi unavyoomba kwa bidii na kurejea tukio hilo, ndivyo katika Roho Bwana anamnyuka shetani kwa namna ile ile. Ng’ang’ania hapo omba kwa imani kwa muda mrefu, kwasababu ndivyo ibilisi anavyodondoshwa].

KELELE ZA VITA:

kelele za vita

Bwana hutumia vitisho pia, kuwaondoa maadui, utakumbuka wakati Fulani wana wa Israeli, walizungukwa na maadui kwa muda mrefu. Hadi nchi ikaingiwa na njaa, watu wakaanza kulana ili waishi. Lakini jinsi Mungu alivyowaondoa maadui zao inashangaza. Kwasababu alifanya tu, kuwasikilizisha sauti za vita. Hivyo wale maadui waliposikia waliogopa sana wakawa wanakimbia kwa hofu kubwa sana huku wanaacha nyara zao nyuma. Baadaye Wayahudi kwenda wanashangaa hawawaoni maadui zao, wakijuliza ni nini kimetokea, mpaka waache na nyara, wakagundua kuwa ni Bwana ndiye aliyewatetea. Ndipo wakazichukua nyara kiwepesi na vita vikawa vimeisha kwa namna ile.

2Wafalme 7:6 “Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.  7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao”

Namna ya kuomba: Bwana peleka sauti zako za vita, katika ngome ya ibilisi, wafukuze waende mbali nami, hazina zote na vipawa vyote walivyoniibia katika roho na mwili ninavirejeza kwa Sauti yako ya vita. Watawanyike kwa njia saba. Vyote walivyoviiba navirejesha, fungua mipaka yangu, safisha hema yangu, adui atoweke kwa sauti za vita vya Bwana. [ Omba kwa kutaja maeneo yote ambayo unataka Bwana akutetee katika hayo].

UPOFU:

Wale malaika wa Bwana walioshuka Sodoma ili kuipeleleza, walikutana na wenyewe wa mji ule, ambao walitaka kulala nao. Hivyo malaika wale wakiwa nyumbani kwa Lutu. Maandiko yanaema waliwapiga upofu watu wale wasiweze kuiona nyumba mpaka asubuhi. Utakumbuka pia Paulo alipofika katika kile kisiwa kilichoitwa. Alishindana sana na Yule mchawi mpaka akamwomba Mungu ampige kwa upofu akawa kipofu kwa muda.

Mwanzo 19:10”Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.  11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango”.

Namna ya kuomba: Bwana piga upofu majeshi ya mapepo yote mabaya yaliyokuja kufanya vita kinyume changu mimi, wasione roho yangu, uufiche uhai wangu ndani yako, shusha kiwi na giza mbele yao. Wapapase, wasione huduma yangu, (taja mambo yako yote ambayo unatamani ibilisi asiyaone), waangamie na kuishia shimoni, watafute lakini wasione. [Hivyo Kwa jinsi unavyosimamia vifungu hivyo ndivyo unavyoshinda vita rohoni kiwepesi kwasababu mambo hayo yanatendeka kwelikweli].

JIWE LA MUNGU:

maombi ya vita jiwe la Yesu

Jiwe la Mungu ni Yesu. Yeye mwenyewe alijifananisha na jiwe hilo lililo zito sana na gumu. Akasema. Likimwangukia mtu linamsaga tikitiki, na yoyote atakayeliangukia atavunjika vunjika Kuonyesha ni jinsi gani lilivyo bora, ndio lile lililopiga sanamu ya Nebukadreza, na kuisaga kama unga, na kupotea kabisa(Danieli 2:34).

Mathayo 21:44  “Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki”.

Namna ya Kuomba: Yesu simama mwenyewe unitetee, kama jiwe lililo hai lenye nguvu na imara. Piga kila aina ya kuta nzito za ibilisi zinazozuia upenyo wangu. Nazibomoa kwa jiwe hili, ninalirusha katika kila Nyanja, impige ibilisi katika kipaji cha uso wake, aanguke kama Goliathi mbele ya Daudi. Wewe uliye jiwe piga kila ngome, ya mwovu lisage na kuharibu na kusagasaga, kazi zote za mwovu mbele yangu ziwe kama makapi mbele ya Upepo.[Lielekeze jiwe hili, liangushe kwelikweli kwa imani ndivyo itakavyokuwa katika ulimwengu wa roho]

Natumai mpaka hapo umeshapata mwangaza wa namna ya kulitumia Neno kuomba maombi haya ya vita, Kwasababu ya muda, hatuwezi toa maelezo ya silaha zote zilizo katika biblia, Hivyo hizi ni silaha nyingine ambazo zitumie, zikusaidie.

6) UPEPO WA KUSULISULI NA RADI:  Andiko la kusimamia (Zaburi 77:18). Omba Bwana avuruge, na kuichosha mikakati yote ya adui dhidi yako mfano wa kisulisuli kizungushacho makapi.

7) GHARIKA YA BWANA: Andiko la kusimamia (Mwanzo 6:17). Kama Bwana alivyoangamiza waovu wakati ule wa Nuhu kwa gharika Omba Bwana akafungue madirisha yake ya mbinguni, agharikishe majeshi ya kipepo yanayokufuatilia yakuangamize, yaangamie kama majeshi ya Farao katika bahari ya Shamu.

8) UPANGA WA BWANA: Andiko la kusimamia (Ufunuo 19:15). Omba ule upanga wa Bwana ukatao kuwili, ukate, na kuua mambo yote maovu ya adui yanayosimama mbele yako

9) KUTAWANYWA USEMI: Andiko la kusimamia (Mwanzo 11:7-9). Kama alivyouvuruga usemi wa wajenzi wa Babeli wasielewane, vivyo hivyo akaruge hila za ibilisi na mapepo yake zisipatane juu yako.

10) MOTO WA BWANA: Andiko la kusimamia (2Wafalme 1:10). Moto ukaunguze mapando yote, ya ibilisi, aliyoyapanda moyoni mwako,

11) NZIGE, PARARE, MADUMADU, TUNUTU: Andiko la kusimamia (Yoeli 2:25). Bwana akatume jeshi lake la waharibuo, wakatafune kazi zote za mwovu, wakalete hasara, warudishe nyuma, na kudhoofisha ufalme wote wa giza.

12) MAJIPU YA BWANA: Andiko la kusimamia (Kutoka 9:9). Bwana alete hali mbaya ya mateso, kwa wakuu wote wa giza wafanyao vita kinyume na wewe.

13) TETEMEKO: Andiko la kusimamia (1Samweli 14:15) . Bwana alete utisho na mashaka, na tetemeko kwa wakuu wa giza na mapepo yasimamo kinyume cha kazi ya Mungu.

14) UKAME (kiu na njaa): Andiko la kusimamia (Amosi 8:11). Bwana alete ukame wa kiroho, kwa majoka yote yanayosimama kutaka kumeza watu wa Mungu, yafe na kuteketea kwa kukosa mawindo ya watu.

15) RUNGU LA BWANA: Andiko la kusimamia (Yeremia 51:20).  Lipige na kuleta majeraha katika ufalme wa giza, liziraishe mapepo yote na vikaragosi vyake vyote vifanyavyo vita na wewe.

Zipo na silaha nyingine nyingi katika maandiko Hatuwezi kuziorodhesha zote, Hivyo kwa jinsi Neno la Mungu linavyokaa ndani yako, ndivyo utakavyoweza kuzivumbua na kuzitumia. Na zote hizo ni sharti tuziombe katika jina la Yesu na uweza wa damu yake.Maombi ya namna hii yana nguvu sana, na yatakufanya udumu kwa muda mrefu katika kuomba. Na kufungua vifungo vingi sana katika ulimwengu wa Roho.

Kumbuka pia, vita hivi hatuvielekezi kwa wanadamu, bali kwa Shetani na majeshi yake ya mapepo na kazi zake zote. Kwasababu maandiko yanasema vita vyetu sio juu ya damu na nyama, maana yake ni kwamba sio juu ya wanadamu wenzetu. Bali ni juu ya falme za giza, zikawaachilie mateka, waje kwa Bwana, na sio tuwaue wao pamoja na mateka wao.

Waefeso 6:12  “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 6.13  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.

VITA DHIDI YA MAADUI

NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?

Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)

Rudi nyumbani

Print this post

Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

SWALI: Naomba kufahamu ni hekima gani tunaipata nyuma ya vifungu hivi, vinavyosema “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri”. 


JIBU: Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.  30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;  31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”. 

Swali la kujiuliza ni kwanini wameonekana wana mwendo mzuri na wa kupendeza, jibu ni kwasababu ya tabia yao ya ujasiri na kuamini kuwa wao ni wamiliki.

kwamfano Simba ni mfalme wa pori, kila kitu kilicho mbele yake anakiona ni chakula, hivyo hana uoga na lolote. Anamiliki wanyama wote , hata wale wanaoonekana ni wakubwa na wenye nguvu kuliko yeye. Wote wanamkimbia.

Anamtaja pia jimbi/jogoo, ambaye na yeye ni mfalme wa shamba, usemi wa “kutanua mbawa” umeanzia kwake. Yeye anaamini anaweza kumiliki mitetea yote na kundi lote la kuku. Watafiti wanasema kule kuwika kwa jogoo, sio bila sababu tu. Hapana, bali ni anatuma ujumbe kwa majogoo wengine wasimsogelee kwenye miliki yake na kutafiti kama yupo ambaye anamkaribia, ajiandae kwa mapambano. Tofauti na ndege wengine walio madume, hawana tabia za kujimilikisha kama Jogoo, au kupigana ili kumiliki shamba.

Anamtaja pia Beberu,(Mfalme wa zizi) katika kundi, beberu utamtambua  tu kwa tabia zake, hujiaminisha sana, muda wote hatulii, analimiliki kundi lote kana kwamba yeye ndio mchungaji-msaidizi (Zekaria 10:3). Katika Historia unabii wa  Aleksanda mkuu aliyetawala Ugiriki ya kale, ambaye aliteka ngome nyingi sana, kila alipopatamani alikwenda na akashinda alifananishwa na beberu katika maandiko Kutokana na Tabia zake hizo (Danieli  8:5). Hata sasa mataifa yanayotaka kumiliki mataifa mengine kwasababu ya nguvu zao za kijeshi, au kiuchumi au kisiasi, hujulikana kama mataifa ya kibeberu.

hiyo ni kufuatana na Tabia ya beberu ya kupenda kumiliki zizi.

Lakini wa mwisho anamtaja pia, Mfalme asiyeasika. Ambaye ni mtawala wa Nchi. Kama tunavyojua wafalme ndio viongozi wa taifa, humiliki vyote, na yoyote atakayekatiza mbele yake kujaribu kuuangusha ufalme wake, humuua. Mfalme ni zaidi ya raisi, Wafalme wengi waliteka ngome kwa vita, sio kwa kuchaguliwa, Ujasiri na misimamo yao huwamilikisha.

Ni hekima gani tunaipata?

Hivyo mwandishi wa mithali anajaribu kuonyesha , ujasiri na ushujaa ambao na sisi tunaweza kuupata endapo tutakuwa ndani ya Kristo. Bwana atatufanya tuwe na roho kama za wanyama hawa, mienendo yetu itakuwa bila WOGA sikuzote. Tutaishi kama watu wasio na mashaka kwa lolote. Hatutaogopa wanadamu, wala matatizo, wala wachawi, wala magonjwa, wala shida yoyote. Kwasababu tunajua uwezo wa kuyashinda hayo na kuyamiliki tunao mfano wa Simba na mfalme.

Bwana Yesu aliye mfalme wetu, anayemiliki sasa mbinguni na duniani, Simba wa Yuda, aliyashinda na sisi pia tutayashinda endapo tutakuwa ndani yake alisema hivyo.

Yohana 16:33  “…jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

Je! Utapenda kumpa leo Yesu maisha yako? Ili aanze upya na wewe, akupe tumaini jipya la uzima wa milele? Na ujasiri wa kuishi hapa duniani bila woga?

Kama jibu ni ndio basi fuatiliza mwongozo huu, na Leo Leo utaupokea wokovu >> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?

Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67)

Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).

YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.

INAYOENDELEA SASA NI HUDUMA YA RUTHU.

Rudi nyumbani

Print this post

Wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza

SWALI: Naomba kufahamu kwanini mafuta yaliendelea kutumika wakati Yesu tayari alikuwa ameshakuja duniani?

Marko 6:12 “ Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 13  Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza”


JIBU: Ndio, Bwana Yesu alikuwa na kanuni nyingi za kuwaponya watu, kuna wakati alitamka tu na mtu akapokea uponyaje wake, utakumbuka habari ya Yule mtu aliyepooza alimwambia jitwike kitanda chako uende nyumbani(Marko 2:1-9),  vilevile kuna wakati alimgusa kwanza mgonjwa, kisha akaponywa, utamkumbuka Yule mkoma, aliyemfuata na kumpigia magoti kumwomba amponye, maandiko yanasema akamgusa na kusema nataka takasika,(Marko 1:40-42). Vilevile Kuna wakati alitoa tu agizo la kutekelezwa na katikati ya agizo hilo, mtu anapokea uponyaji wake, ile habari ya wale wakoma 10, inatuthibitishia hilo,(Luka 11:17-19) na kuna wakati alitumia visaidizi, kama udongo, mate, kama ishara ya nje, ya mtu Yule kupokea uponyaji wake. Ukisoma habari ya Yule mtu ambaye alikuwa kipofu tangu kuzaliwa utali hakiki hilo nalo (Yohana 9:6).

Na hapa ndivyo ilivyokuwa aliwapa maagizo wanafunzi wake, Pale alipowaita na kuwatuma kwenda kuhubiri injili Ukisoma kuanzia mstari wa 7, Utaona aliwapa maagizo hayo ya kutoa pepo, na bila shaka na ya kuwapaka mafuta wote waliokuwa wagonjwa kwa jina lake.

Lakini hiyo haikuwa staili, kwamba kila mahali watakapokwenda wawe na chupa za mafuta, au maji, au udongo au chochote.

Hata sasa, hatupaswi kudhani Bwana hawezi kutuagiza tutumie kitu chochote cha asili kama ishara ya nje ya kuachilia uponyaji wake. La! Tusifikiri hivyo, Lakini hilo halipaswi lifanyike mara zote, au kama staili, kama inavyofanywa sasa, watu hawahubiri tena Neno la Mungu, kinachopigiwa kampeni ni mafuta na maji ya upako. Lakini mitume hawakufanya hivyo, ukisoma mstari wa 12, hapo anasema “Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu”. Umeona, Walijua jukumu lao kubwa ni kuwahubiria kwanza watu habari za dhambi zao. Na katika huduma hayo mengine yanafuata tena kwa uongozo wa Roho Mtakatifu.

Ni jambo linalosikitisha sasa, Jina la Yesu halitumiwi tena, shetani ameingilia eneo hili na kulivuruga, watu wakidhani hiyo ndio kanuni ya Mungu iliyobora ya watu kupokea uponyaji,  wamemgeuza kama mganga wa kienyeji ambaye yeye kazi yake ni kutoa tu miti-shamba lakini hajali hali ya mtu ya kiroho.

Wengine wanakimbilia lile andiko la Yakobo ambalo linasema,

Yakobo 5:14  “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

15  Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa”

Wanasahau kuwa kilichotangulia ni kuombewa kwanza..kuungamanishwa dhambi zake, kupatanishwa na Mungu, kisha ndio mafuta yafuate, kwa jina(agizo) la Bwana.

Tukikariri kwamba wakati wote tunapaswa tutumie chumvi kisa Elisha aliagizwa atupe chumvi kwenye chemchemi ya maji ili aondoe mapooza(2Wafalme 2:19-22), basi tukariri pia kitendo cha kulala juu ya maiti, kila tunapowaombea wafu ili wafufuke, kwasababu Elisha naye alifanya kitendo kama hicho(2Wafalme 4:32-34). Unaona, tutaonekana ni wachawi.

Ndugu, kuwa makini na staili za kisasa za uponyaji, ni makundi machache sana yanayoongozwa na Bwana kutumia vitu hivi vya asili katika kufanya huduma, na utaona havitumiki mara kwa mara au kila siku bali kwa mwongozo Fulani. Lakini ukiona mahali hapo ndio imekuwa staili, kimbia hapo Mungu hayupo hiyo ni ibada ya sanamu. Wana wa Israeli walimkosea Mungu hivyo hivyo, baada ya kuona Mungu amewaponya kwa kuitazama  ile nyoka ya shaba, Musa aliyoagizwa aiunde kule jangwani,  wao wakadhani Mungu sikuzote yupo katika sanamu ile, matokeo yake ikawa walipofika katika nchi ya ahadi wengine waliendelea kuiunda, wakiitazama ili kutatuliwa matatizo yao, ikawa ni chukizo kubwa sana kwao. Mpaka baadaye sana mfalme Yosia alipokuja kuivunja vunja, ndipo hasira ya Mungu ikaisha.(2Wafalme 18:1-5)

Hivyo usigeuze kitu chochote kuwa sanamu yako, kukitegemea hicho angali maisha yako yapo mbali na dhambi utakumbana na laana badala ya  baraka. Tumepewa jina la YESU hilo ndio mwanzo na mwisho. Vinginevyo vyote tusubiri kwanza uongozo wa Roho Mtakatifu, kama haupo, tuache.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)

NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?

MAOMBI YA KUFUNGULIWA KIUCHUMI.

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?

VITA BADO VINAENDELEA.

Rudi nyumbani

Print this post

Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.

SWALI: Katika Mithali 30:24, tunaona wanatajwa wanyama wanne, wenye akili sana, lakini naomba kufahamu juu ya Yule wanne ambaye ni mjusi, Anaposema “Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme” Maana yake ni nini?


JIBU: Tusome,

Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.  25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.  26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.  27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.  28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”

Mjusi ni kiumbe ambaye ameumbiwa wepesi wa kupanda na kupita karibia sehemu zote zenye upenyo hata ule mdogo sana, uwezo wa mikono yake unamfanya aweze kusimama katika pembe yoyote ile ya ukuta, iwe ni ukuta wa juu, au wa pembeni, au wa chini, kwake vyote ni sawasawa, tofauti na wanyama wengine, ambapo pengine hutegemea kucha zao, ambazo hizo zinawasidia kupanda baadhi ya maeneo tu kama miti.

Na ndio maana utawakuta katika kila nyumba, hawazuiliki, hadi katika majumba ya wafalme biblia inasema hivyo utawakuta, mahali ambapo pana ulinzi, pana uangalizi, lakini wao wanaingia huko bila shida yoyote na kufanya makazi.

Ni kutufundisha nini katika hekima yake?

Ni kwamba, na sisi tunapokuwa ndani ya Kristo tunapewa mikono kama ya mjusi katika roho. Uwezo wa hali ya juu kupanda kila kuta ngumu, Hatuzuiliki kwa kitu chochote, popote tutakapotaka kupafikia tutapafikia, hata katika malango mazito ya ibilisi tutayamiliki.

Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; NA UZAO WAKO UTAMILIKI MLANGO WA ADUI ZAO;  18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”

Je! Unataka uupokee uwezo huo? Kanuni ni moja tu, nayo  ni kumpa Kristo maisha yako, jikane nafsi yako, simama kikamilifu na Bwana, kisha utaona jinsi Mungu anavyokupigania kuangusha kuta na kumshinda ibilisi kiwepesi, ziwe za kimaisha au za kiroho. Kwako hakuna kikwazo kitakachokuwa kigumu kukishinda.

Bwana akubariki.

Je! Utapenda kufahamu hekima iliyo nyuma ya wale watatu waliosalia?

Fungua link hizi>>>

Wibara > Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

Nzige >TUWATAFAKARI NZIGE WA JANGWANI.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Nzige, Parare, madumadu na tunutu ni wadudu gani? (Yoeli 2:25)?

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8)

Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?

Je! Lewiathani ni nani?

Lumbwi ni nini katika biblia?

tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri, ni ipi?

Biblia inasemaje kuhusu Kazi?

Rudi nyumbani

Print this post

BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.(Kutoka 15:3)

SWALI: Naomba kufahamu maana ya huu mstari..Kwanini biblia imtaje Mungu kama mtu, angali maandiko yanasema yeye sio mtu.

Kutoka 15:3

[3]BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.


JIBU: Neno hilo halimaanishi kuwa Mungu ni mtu, Bali biblia hutumia mifano halisi ya kibinadamu kuwasilisha picha Fulani Rohoni..

Kwamfano ukisoma andiko lingine linalopatikana katika Mithali 30:26, utaona mnyama anayeitwa Wibari anatajwa kama mtu..

Mithali 30:26

[26]Wibari ni watu dhaifu;  Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.

Tunafahamu kabisa wanyama hawa wibari(Pimbi) sio watu, isipokuwa kwa wingi wa akili zao, mwandishi anawafananisha na watu, Ni kwasababu gani? Ni Kwasababu ijapokuwa ni waoga, wadhaifu, wanawindwa na kila mnyama mkali..lakini hawajengi nyumba zao katika sehemu dhaifu kama kwenye viota, au kwenye mashimo, au vichaka, ambapo ni rahisi kuvamiwa au kuharibiwa na majanga, Bali wanaweka makazi Yao katika miamba mikubwa iliyojificha sana  Mahali ambapo ni ngumu adui kuwashambulia.. wanafananishwa na watu waliojenga maisha yao juu ya MWAMBA, pekee yaani Yesu Kristo

Mathayo 7:24  “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”

Hivyo tukirudi katika andiko hilo, anaposema “BWANA ni mtu wa vita”. Anajaribu kumfananisha Bwana na shujaa wa kivita, jemedari mwenye uzoefu mkubwa sana katika vita vikali, mfano wa Sauli, au Daudi, ambao walikuwa wanasimama mstari wa mbele katika vita, ili sisi tupate picha jinsi gani Mungu wetu alivyo mkuu sana, pale anapoitwa Bwana wa Majeshi, tumwelewe uweza wake wa kutupigania na kutusaidia kuangusha ngome za ibilisi jinsi ulivyomkubwa haijalishi zimekita mizizi kiasi gani.

Zaburi 24:8 “Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita”

Hivyo mstari huo hakumaanisha kuwa yeye ni mtu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU

Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?

VITA DHIDI YA MAADUI

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.

Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?

Rudi nyumbani

Print this post

Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake;

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali 27:8 “Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake”

JIBU: Hapa Sulemani alikuwa anajaribu kueleza jinsi tabia ya ndege inavyoweza kufananishwa na tabia ya mkristo katika maisha yake hapa duniani. Kwa kawaida ndege anapotoka katika kiota chake, huwa na lengo la aidha kutafuta chakula, au kukiendeleza kiota chake, au kujipumzisha mahali Fulani kwa muda. Hivyo huwa anaenda na kurudi, anaenda na kurudi kwa siku hata mara 10 na zaidi, anaweza kufanya hivyo.

 Lakini wakati huo huo, awapo katika mazingira ya kuzunguka huko na huko, hukutana na hatari nyingi sana. Aidha Maadui au mitego. Hivyo asipokuwa makini anaweza asirudi, kabisa nyumbani kwake.

Hivyo ndivyo alivyo mkristo, ambaye misingi yake ni “biblia na Kanisa”. Ukweli ni kwamba si kila wakati atakuwa katikati ya watakatifu, au atakuwa uweponi akimsifu Mungu na kumwimbia, au akilitafakari Neno la Mungu. Zipo nyakati atatoka kwa muda ataenda kazini, atatoka kwa muda ataenda shambani pengine kujitafutia riziki, ataenda shuleni masomoni na kama si hivyo basi kwa namna moja au nyingine atajihusisha na mambo ya kijamii, kama kutembelea jamaa, na ndugu, majirani n.k.

Sasa awapo katika mazingira haya anafananishwa na ndege atokaye katika kiota chake na kuzunguka huko na huko. Hivyo anapaswa awe na busara kwa sababu huko nje, zipo hatari nyingi sana za yeye kunaswa na adui asipokuwa makini.

Ni lazima ajiwekee mipaka, si kila biashara afanye, si kila jambo la kidunia analoletewa mbele yake ajihusishe nalo, si kila mazungumzo ayaongee. Bali muda wote awapo nje, atambue kuwa makao yake ni KANISANI awezapo kufanya ibada, na kujumuika na watakatifu wenzake. Muda wote atambue usalama  wake ni katika Neno la Mungu basi. Alale katika hilo na aamke katika hilo.

Akitafutacho huko nje ajue ni kwa lengo la kuendeleza tu kiota chake (kazi ya Mungu), na sio vinginevyo. Mtu huyo akizingatia vigezo hivyo atakuwa salama. Lakini watu wengi wamenaswa na ulimwengu. Hata Kanisani hawaonekani tena baada ya kupata kazi, Upendo wao kwa Mungu umepoa pale walipokutana na marafiki Fulani wapya, muda wa maombi wanakosa kisa wapo buzy na mihangaiko ya maisha. Kauli zao zimebadilika, kwasababu muda mwingi wamekaa na watu wenye mizaha, na matusi, hadi na wao wakajifunza lugha zao.

Biblia inatuambia,

Waefeso 5:15  “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16  mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17  Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

Anasema tena..

Wakolosai 4:5  “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6  Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.

Hivyo tuwapo nje ya uwepo wa Bwana, tujichunge, tujizuie, tuwe na kiasi, tutakuwa salama. Ili tusijikute tunanaswa katika mitego ya ibilisi.(Mithali 1:17,  7:22)

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,

Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)

Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?

Nini maana ya “Atamwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”. (2Wathesalonike 2:8).

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Rudi nyumbani

Print this post

Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali 16:33

[33]Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

JIBU: Kura zilipigwa kwa namna mbalimbali zamani, njia iliyokuwa nyepesi ndio hiyo ambayo kipande cha shuka, au nguo, iliyofumwa vilitumiwa kukusanya kura za watu mbalimbali ambazo ziliandikwa katika vipande vya vibao vidogo vidogo, au mawe kisha hukorogwa, na lile litakalotoka la kwanza au kuchukiliwa humo basi ndio kilichosahihi..

Wengine walitumia makopo, wengine kofia, kisha kuzikoroga kura na ile itakayotoka au kuchaguliwa cha kwanza huko ndio huaminika kuwa chaguo sahihi

Hivyo, zipo nyakati ambazo Mungu aliruhusu baadhi ya mambo yaamuliwe kwa kura kama vile kugawanya nchi n.k.Soma(Hesabu 26:55, Yoshua 18:6-10)Lakini si kila jambo, mengi Mungu alitoa majibu kwa njia ya moja kwa moja, kwa kufunuliwa aidha kwa kupitia manabii au maono au ndoto.

Sasa tukirudi katika mstari huo..

Anaposema..

Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Maana yake ni kuwa Japo kuwa kupiga kura ni tendo linaloonekana la kibinadamu lakini ikiwa linafanyika katika Bwana, majibu ya kweli hutoka kwake.

Yule atakayechaguliwa, au kile kitakachopendekezwa, ndio jibu sahihi kutoka kwa Bwana.

Katika Biblia tunaona mtume Mathiya alichaguliwa kwa kura, lakini kabla ya kupiga kura ile, mitume walimtanguliza kwanza Mungu katika uchaguzi wao,waliomba na kumsihi Bwana aingilie uchaguzi wao..kisha kila mmoja akaandika pendekezo lake na jawabu likatoka na ndio likawa kweli jibu sahihi la Mungu.

Matendo 1:23-26

[23]Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya.

[24]Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,

[25]ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.

[26]Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

Wakati mwingine tunaweza kulaumu, viongozi tuliowachagua, tukasema waliiba kura n.k. lakini kama Mungu asingetaka wawepo pale wasingekuwepo tu, kwasababu yeye ndio anayewamilikisha watawala haijalishi watakuwa ni waovu au wema..

Danieli 2:21

[21]Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;

Hii ni kuonyesha uhuru wa Mungu wa kuchagua, yapo mambo kwetu tutaona kama tumeamua sisi, au yametokea kwa bahati, lakini kumbe ni Mungu kapanga..kwake yeye vitu havitokei kwa bahati, bali vyote chini ya makusudi yake.Mungu ndiye ayaruhusuyo yote..

Utukufu una yeye milele na milele.

Amina.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?

HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.

Ni kura ya aina gani waliipiga wale watu waliosafiri na Yona?

NI WAPI UTAKUTANA NA MALAIKA WA BWANA?

Rudi nyumbani

Print this post