SWALI:Bwana Yesu asifiwe naomba kuelewa “Kisima cha joka” na “lango la jaa” vina maana gani kama tunavyosoma katika Nehemia 2:13
JIBU: Nehemia alipopata taarifa juu ya uharibifu wa mji wa Yerusalemu, alifunga na kumwomba Mungu kwa muda mrefu, ili aende kuujenga tena mji huo, ndipo Mungu akasikia maombi yake na kumfungulia mlango wa kwenda Israeli kwa ajili ya kazi hiyo ya ukarabati.
Sasa kama tunavyosoma alipofika,hakusubiri sana, bali aliondoka usiku wa tatu yeye ni baadhi ya watu wachache, ili kuuchunguza kwanza mji, jinsi kuta zake zilivyoharibiwa. Na kati ya sehemu tano (5) alizopita mojawapo ilikuwa ni hapo penye kisima cha joka, na lango la jaa.
Kisima cha joka: Ni kisima kilichokuwa kando ya kuta za mji, kinaaminika, kiliitwa hivyo kutokana na umbile la mdomo wake jinsi ulivyofanana na nyoka., japo wengine wanaamini kuwa hapo kale kilitumiwa na wapagani kwa ajili ya miungu yao ya majini, waliyoitambua kwa jina la joka. Hivyo jina la kisima hicho liliendelea kuwa hilo hadi wakati wa baadaye, Japo hilo halijathibitishwa ni kulingana tu na mapokeo kwasababu biblia haijaeleza sababu ya kuitwa vile.
Lango la Jaa: Jaa kwa jina lingine ni jalala, hivyo, lango hili lilitumika kutolea uchafu wote wa mji (kinyesi). Huko nako Nehemia alifika.
Nehemia 2:11 Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu. 12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe. 13 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya LANGO LA BONDENI, nikashika njia IENDAYO KISIMA CHA JOKA, na LANGO LA JAA; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. 14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama aliyekuwa chini yangu. 15 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo.
Nehemia 2:11 Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu.
12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe.
13 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya LANGO LA BONDENI, nikashika njia IENDAYO KISIMA CHA JOKA, na LANGO LA JAA; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto.
14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama aliyekuwa chini yangu.
15 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo.
Lakini baada ya hayo yote tunaona, Nehemia haraka na mapema alianza ujenzi wa kuta za mji. Na kazi ikaja kukamilika kwa ufasaha wote,licha ya kupitia vipingamizi na vikwazo vingi kutoka kwa maadui zao.
Ni ujumbe gani tunaupata kutoka katika mawazo hayo ya Nehemia?
Ni kwamba hatuwezi kukarabati kitu bila kujua uharibifu wake upo wapi. Ni jinsi gani wakristo, tunapaswa tufumbue macho yetu tuone, uharibifu shetani aliousababisha kwenye kazi ya Mungu, jinsi watoto wanavyoharibiwa, jinsi vijana walivyopotoka kila kukicha, jinsi maasi yanavyoendelea kanisani.., Tukiyaona hayo hapo ndipo wote kwa pamoja tutaona sababu ya kumtumikia Mungu, kwa ushirikiano.
Vinginevyo tutaona kila siku mambo yote ni sawa tu, kama wale watu wa Mji Nehemia alivyowakuta wame RELAX.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Jaa ni nini katika biblia?
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?
Jehanamu ni nini?
UFUNUO: Mlango wa 12
Rudi nyumbani
Print this post
Bwana alisema…
Zaburi 34:8
[8]Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
[8]Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini.
Maana yake ni kuwa Mungu ametoa nafasi kwa kila mtu ambaye yupo mbali na neema kuonja au kujaribu kwanza uzuri ulioko ndani yake kabla hajauingia moja kwa moja..kwamfano kujaribu kungalia kama ndani ya Kristo kuna furaha, au amani, au upendo n.k.
Na pale mtu anapoona kuwa ipo basi anawajibika kumuishia Mungu maisha yake yote, lakini kama hajaiona basi anaruhusiwa kughahiri uamuzi wake..Na Ukweli ni kwamba hakuna aliyemjaribu Kristo akatamani kutoka baada ya hapo.
Lakini sio sisi tu tunaonja vya Mungu.. Mungu naye pia anayotabia ya kutuonja sisi auminifu wetu na uelekevu wetu kwake kama tunakidhi kweli vigezo vya yeye kutupa moja kwa moja kile tulichomuomba…au kutukaribia moja kwa moja milele.
Sasa hatua kama hii ukishafikia tambua kuwa unapaswa ung’ang’ane kweli kweli kwasababu huwa hakiwi kipindi cha raha sana.
Tukirudi kwenye biblia…tunaona wana wa Israeli walipotoka Misri, Mungu alikuwa nao karibu katika kiila hatua waliyopiga, walichokitaka walikipata wala hawakuachwa bila majibu..mpaka wanavuka bahari ya shamu wote wakawa wanamwimbia Mungu na kumchezea kwa shangwe kwa jinsi alivyowatendea miujiza mikubwa..Hivyo hilo likamvutia Mungu sana..Mungu akashawishika kushuka atembee nao milele katika furaha na raha..
Lakini kabla ya yeye kufanya vile ilimpasa kwanza AWAONJE..aone kama ni kweli wamekidhi vigezo vya yeye kuwa Mungu wao au la.
Hivyo alichofanya ni kuwaacha siku tatu kwa Kiu kule janwani pindi tu walipovuka bahari ya shamu, jambo ambalo hawajawahi kulipitia kabisa maisha yao yote tangu walipoanza kutembea na Mungu..
Tusome…
Kutoka 15:22-25
[22]Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. [23]Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. [24]Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? [25]Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO.
[22]Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.
[23]Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.
[24]Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?
[25]Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO.
Unaona mstari wa 25 inasema Mungu akawaonja huko.kama kweli walimpenda kutoka moyoni au ni kwa miujiza tu..au kwa mikate tu..au kwa mafanikio tu..
Lakini tunaona wana wa Israeli walinung’unika badala ya kujinyenyekeza..Hivyo Mungu hakuona ukamilifu ndani yao.akajua kumbe walimpendea kwasababu walipata raha tu lakini sio kwasababu ni Mungu wao..Laiti wangejinyenyeza ni wazi kuwa tangu ule wakati na kuendelea wasingekaa kusikia kitu kinachoitwa shida au taabu au masumbufu…
Ndugu yangu..Mungu akidhamiria kushuka kwako moja kwa moja kukaa na wewe au kukupa kitu fulani ulichomuomba ni sharti kwanza AKUONJE..uaminifu wako kama alivyofanya kwa Ibrahimu kumtoa mwanae Isaka..Hiyo ndio kanuni yake ambayo wana wa Israeli walishindwa kuielewa..
Soma pia Kumbukumbu 8:1-3 utaona Bwana akilisisitiza neno hilo hilo..
Hivyo ndugu uliyeokoka..lijue jambo hilo, liweke akiba moyoni mwako. Kabla hujawa rafiki wa Mungu wa milele ni sharti kwanza akuonje..ukikidhi vigezo basi ndio kimekuwa chako milele.
BIRIKA LA SILOAMU.
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
UFUNUO: Mlango wa 14
KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.
JIBU: Saumu ni neno lenye asili ya lugha ya “kiaramu” lenye maana ya “kujizua kufanya jambo/kitu fulani kwa ajili ya ibada”.
Hivyo pale mtu anapoacha kula kwa kipindi fulani, kwa ajili ya sala..Mtu huyo yupo katika saumu.au kwa jina tulilolizoea tunasema yupo katika mfungo.
Neno hilo utalipata katika vifungu hivi kwenye biblia..
Zekaria 8:19
[19]BWANA wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.
Yoeli 1:14
[14]Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,
Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,
Soma pia Yoeli 2:15.utaliona neno hilo.
Saumu ya kweli ni ipi?
Lakini pia tofauti na wengi tunavyodhani..kwamba saumu inayompendeza Mungu ni ile ya chakula tu..ni kweli hiyo anaitazama lakini sio kiini cha saumu anayotaka kuiona ndani ya mtu.. Saumu anayoipokea ni ile ya kufunga vifungo vya uovu na dhambi.
Isaya 58:3-8
[3]Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. [4]Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. [5]Je! Kufunga namna hii ni SAUMU niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA? [6]Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? [7]Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? [8]Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
[3]Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
[4]Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
[5]Je! Kufunga namna hii ni SAUMU niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?
[6]Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
[7]Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
[8]Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Umeona? Hivyo na wewe ufungapo basi fahamu kuwa Mungu anatazamia kuona mageuzi makubwa ya maisha yako dhidi ya dhambi na kutenda haki. Usifunge tu kidini ili kutumiza sheria.Funga kwa lengo la kuwa mkamilifu mbele zake.
Vinginevyo unaweza ukafunga hata siku 40 usiku na mchana bila kula, kama Musa na Mungu bado akaona unafanya kazi bure.
Bwana akubariki.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
KWARESMA IPO KIMAANDIKO?
Maana Ya Maneno Katika Biblia.
Mafundisho
Si kila tunayemuhubiria, ni lazima tuone matokeo ya papo kwa papo ya badiliko.. Ni kweli tunatamani iwe hivyo kwa watu wote , na wakati mwingine ukiwa kama muhubiri unaweza kuvunjika moyo, pale ambapo unazunguka kila mahali, mwezi mzima, au mwaka mzima, kuhubiri, halafu hufanikiwi kupata tunda lolote la kudumu, au hata ukiyapata basi ni machache sana, ukilinganisha na nguvu ulizowekeza hapo.
Lakini ukiwa katika hali kama hiyo, jambo ambalo unapaswa usilitoe katika akili yako ni kuwa, mwisho wa mavuno sio siku hiyo unayohubiri, mwisho wa mavuno sio leo uliyopo mkononi mwako. Mwisho wa mavuno utakuwa ni siku ile ya mwisho, Mungu atakapotuma malaika zake, kuyatenganisha magugu na ngano. Na ngano kuziweka ghalani, sio sasa.
Mathayo 13:39b … mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika…. 49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
Mathayo 13:39b … mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika….
49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
Kwahiyo ndugu, huyo mtu unayemshuhudia/ unaowashuhudia, ikiwa hawaonyeshi badiliko leo, bado wewe endelea kuhubiri, kwasababu wakati wa kuhitimisha kila kitu bado. Pengine leo unapanda mbegu, mwingine kesho atatia maji, au wewe unatia maji leo, mwingine atapalilia, au wewe utapalilia mwingine atamalizia kuvuna,.kabla ya mwisho wa mavuno kufika.
Kwahiyo, usivunjwe moyo sana, mwisho wa dunia bado, japo upo karibu sana, hivyo wewe endelea kuingaza nuru ya Kristo katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho, hata kama matunda hutayaona sasa. Mwachie Mungu amalize kazi zake. Kwasababu Biblia inasema..
Mhubiri 11: 4 Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
Songa mbele. Tangaza habari za Kristo.
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.
Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.
UPO UMUHIMU MKUBWA WA KUMTOLEA BWANA!
SWALI: Kwanini katika Mwanzo 5:2 tunasoma Mungu aliwaita Adamu na Hawa jina moja la Adamu..na sio mawili tofauti.?
Mwanzo 5:2
[2]mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
JIBU: Kumbuka siku Mungu alipowaumba wanadamu(mwanamke na mwanamume)..hàkuwaumba wote kwa pamoja..Bali alimuumba ADAMU peke yake..kisha hawa baadaye..ambaye alikuja kuumbwa kutoka katika ubavu wa Adamu.
Hivyo wakati Mungu anatoa majina kwa viumbe vyake Hawa hakuwepo..Jina hilo alikuja kupewa na Adamu mwenyewe baadaye soma..
Mwanzo 3:20
[20]Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
Kwahiyo kwanini Mungu aliwaita jina moja ni kwasababu alipomuona Hawa alimuona Adamu kwasababu ni zao lake..hivyo machoni pake hakuona mwanamke anastahili kuitwa kitu kingine tofauti na jina la Mume wake ..Ni sawa na wewe uone ‘sisimizi’ huwezi wala huioni sababu ya kumuita sisimizi wa kike jina tofauti na yule wa kiume..wote utawaita tu jina moja sisimizi..na ndivyo ilivyokuwa machoni pa Mungu kwa Adamu na Hawa.
Lakini Mungu alitaka kutufundisha nini kwa kuwaita vile?
Ikiwa wewe ni mwanamke fahamu kuwa ukishaolewa, Mungu hakuoni tena kama ni mtu tofauti na mumeo. Atakutambua kwa jina lake. Hivyo jifunze kumtii mumeo. Kwasababu yeye ndio kila kitu kwako kwa muda huo.
Vilevile wewe kama mume..mpende mke wako, kwasababu ule ni ubavu wako. Na ndio maana haitwi jina lingine zaidi ya hilo la kwako. Hata kama utajaribu kumuita kwa majina mengine lakini Mungu anamtambua kwa hilo jina lako. Hivyo jifunze kumpenda na kumuhudumia.
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Je Mungu aliumba watu wengine kabla ya Adamu?
JIBU: Andiko ambalo linaonyesha kutengwa kwa mwanamke anapotokwa na damu au anapokuwa katika siku zake ni hili;
Mambo ya Walawi 15:19-33
[19]Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni. [20]Na kitu cho chote akilaliacho katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho akiketia kitakuwa najisi. [21]Mtu ye yote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni. [22]Mtu ye yote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni. [23]Kwamba ni katika kitanda, au cho chote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hata jioni. [24]Na mtu ye yote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi. [25]Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye yu najisi. [26]Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake. [27]Na mtu ye yote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni. [28]Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi. [29]Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania. [30]Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake. [31]Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao. [32]Hii ndiyo sheria ya mwenye kisonono, na ya mtu ambaye shahawa yake yamtoka, akawa na unajisi kwa hiyo; [33]na ya mwanamke ambaye yu katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, kama ni mtu mume, kama ni mtu mke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.
[19]Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni.
[20]Na kitu cho chote akilaliacho katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho akiketia kitakuwa najisi.
[21]Mtu ye yote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
[22]Mtu ye yote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
[23]Kwamba ni katika kitanda, au cho chote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hata jioni.
[24]Na mtu ye yote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.
[25]Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye yu najisi.
[26]Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake.
[27]Na mtu ye yote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
[28]Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.
[29]Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania.
[30]Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
[31]Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao.
[32]Hii ndiyo sheria ya mwenye kisonono, na ya mtu ambaye shahawa yake yamtoka, akawa na unajisi kwa hiyo;
[33]na ya mwanamke ambaye yu katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, kama ni mtu mume, kama ni mtu mke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.
Kumbuka tunapaswa tujue kuwa si kila jambo ambalo lilitendeka agano la kale, linatendeka vilevile hadi wakati wa agano jipya..mambo mengi yalikuwa ni kama kivuli tu kuwasilisha ujumbe wa rohoni kwa agano letu jipya…kwamfano kwenye suala la chakula utaona Bwana alikuja kurekebisha akasema kimwingiacho mtu hakimtii unajisi bali kumtokacho mtu kwasababu kinamtoka moyoni..hivyo chakula kwa namna yoyote hakiwezi kumfanya mtu amkosee Mungu kikilika kwa shukrani..lakini zamani kwamfano wanyama ambao walikuwa hawacheui(yaani hawawezi kurudisha tena chakula wanapokimeza) walijulikana kuwa ni najisi ikifunulia kuwa kwasasa rohoni wapo watu najisi ambao hawana tabia ya kucheua chakula cha kiroho wanacholishwa..yaani hawana muda wa kuyatafakari ya nyuma waliyofundishwa au waliyofanyiwa na Mungu, Au kutendea kazi yale waliofundishwa.
Vivyo hivyo na suala la wanawake katika siku zao kwa kawaida damu kama damu haina shida lakini jiulize kwanini hiyo inayotoka katika viungo vya uzazi ilionekana ina unajisi..Hiyo ni kufunua kuwa uchafu unazoalika kutokana na zinaa ni unajisi mkubwa sana kwa mtu.
Na ndio maana biblia inasema na malazi yawe safi.. (Waebrania 13:4)
Tunapaswa tuitunze miili yetu mbali na uasherati
Lakini haimaanishi kuwa ukitokwa na damu, wewe tayari ni najisi hapana kwasababu lile ni tendo linalokuja lenyewe halipangwi na mwanamke. Hivyo halimtoki rohoni mpaka likamtia mtu unajisi..Mungu alitumia mfano ule tu kuonyesha jinsi mambo yatokayo kule yasivyofaa(katika uzinzi)… Kwahiyo mwanamke akitokwa na damu au asipotokwa na damu hakumzuii yeye kumwomba Mungu wake au kumtumikia madhabahuni pake..
Anachopaswa kufanya ni kujiweka tu katika mazingira ya usafi na uangalifu.
Mada nyinginezo:
MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?
KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.
UFUNUO: Mlango wa 17
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Rudi Nyumbani
SWALI: Kwanini wakristo wa kwanza waliposikia kuwa Petro kafunguliwa hawakuamini badala yake walitumia neno “Ni malaika wake”..kwanini wawaze vile au waseme vile?
JIBU: Tusome.
Matendo ya Mitume 12:11-17
[11]Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi. [12]Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. [13]Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza. [14]Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. [15]Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. WAKANENA, NI MALAIKA WAKE. [16]Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. [17]Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
[11]Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.
[12]Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.
[13]Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza.
[14]Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango.
[15]Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. WAKANENA, NI MALAIKA WAKE.
[16]Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu.
[17]Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
Wayahudi tangu zamani hadi sasa wanaamini kuwa kila mtu anaye malaika mlinzi..Na malaika hawa wanaweza kuja katika maumbile tofauti tofauti..wanaweza kuja kwa sura ya mtu mwingine au kwa sura au sauti ya yule mtu anayemlinda.
Vilevile tunaweza kulithibitisha hilo pia katika maneno ya Bwana aliyoyasema katika (Mathayo 18:10) Kwamba wapo malaika wanaosimama kwa ajili ya watu tangu wakiwa wadogo.
Sasa kulingana na hiyo habari ni kuwa Roda aliposikia sauti ya Petro, .hakuhangaika kuhakikisha kwamba yeye anayegonga ni Petro au la! bali aliamini moja kwa moja na kwenda kutoa taarifa ..Lakini alipowapelekea habari wale waliokuwa ndani haikuwa rahisi kwao kuamini moja kwa moja kama yule angeweza kuwa Petro. Kwasababu kutokana na mazingira Petro aliyofungiwa, ni ngumu kutoka kwani alikamatwa kwa amri ya mfalme, na vilevile alikuwa chini askari 16.
Hivyo jambo ambalo wangeweza kudhani ni kuwa malaika wake ndio amekuja kwa maumbile ya Petro au pengine kwa umbile lingine isipokuwa katumia sauti ya Petro labda kuwafariji au kuwapa taarifa juu ya kifo chake.
Lakini walipoona Petro anazidi kugonga mlango wakaenda kumfungulia, wakathibitisha kuwa kumbe alikuwa ni Petro na sio malaika wake.
Ni nini tunaweza kujifunza katika habari hiyo?
Ni karama ya Mungu kuwatuma malaika zake kutuhudumia.Lakini malaika hawa hawamuhudumii kila mtu tu ilimradi hapana bali ni watakatifu tu..ikiwa na maana kama wewe ni mwovu ujue kinachokulinda ni rehema za Mungu tu ili uendelee kuishi, lakini hakuna huduma yoyote unayoweza kupokea kutoka kwa malaika zake. Kinyume chake ni kuwa mapepo ndio walinzi wako.
Na ndio maana huwezi kuishi maisha ya raha au ya amani hata kama unazopesa zote ulimwenguni..ni kwasababu ufalme wa Mungu haupo wala hautembei pamoja na wewe. Ni heri ukatubu leo ukamkabidhi Yesu maisha yako. Naye atakuokoa na kuuleta ufalme wake wa mbinguni kutembea pamoja na wewe. Hapo ndipo utakapoona tofauti yako ya jana ambayo hukuokoka na leo ambayo umeokoka.
Na wokovu unakuja kwanza kwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha na pili ni kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu.
Hivyo kama utapenda kumpokea Kristo leo basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi kwa msaada huo wa kiroho bure. Kumbuka saa ya wokovu ni sasa na wakati uliokubalika ni leo.
+255693036618/ +255789001312
Bwana akubariki
Mada Nyinginezo
HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.
TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.
Rudi Nyumbani:
SWALI: Nini maana ya kuutia moyo ufahamu? Mtu anatiaje moyo wake ufahamu?
Danieli 10:12 “Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako”.
JIBU: Ukisoma kitabu cha Danieli chote utagundua Danieli alikuwa ni mtu ambaye si wa kuchulia mambo juu juu tu..alikuwa ni mtu anayechunguza na kufuatilia mambo baada ya kusikia
Kwa mfano angalia ile ndoto aliyoota Nebukadreza..ndoto ile hakuota Danieli, lakini baadaye alipoona ina maana kubwa alimwomba Mungu ampe kujua zaidi..Na ndio hapo utaona Danieli akifuniliwa kwa undani mkubwa sana mambo yahusianayo na ile ndoto, Juu ya zile Milki nne za ulimwengu. Soma Danieli 2,5,7
Ukisoma tena Danieli sura ya 9 utaona..alipokuwa anasoma vitabu akagundua kuwa kumbe imeshaandikwa na nabii Yeremia kuwa Israeli watakaa Babeli kwa muda wa miaka 70 tu..Hilo jambo lilimshangaza kwasababu hakuwahi kudhani kama Israeli ingekaa utumwani kwa muda mfupi vile. Hivyo hakukaa hivyo hivyo tu..Ndipo akaanza kumlilia Mungu kwa toba..baadaye Mungu akamfunilia jinsi itakavyokuwa mpaka mwisho.
Vivyo hivyo kuna wakati mwingine mbeleni biblia inatuambia Danieli alifunuliwa jambo lingine jipya..japokuwa jambo hilo halijaandikwa katika biblia ni lipi…lakini linaonekana lilikuwa ni la kutisha na ndio maana alisema ni vita vikubwa..Sasa alipofuniliwa kwa muhtasari tu,, kama kawaida yake hakukaa tu hivi hivi..bali aliingia katika maombi ya mfungo na maombolezo kwa muda wa wiki tatu nzima kumsihi Mungu amfunulie..
Tusome..
Danieli 10:1-3,
[1]Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo. [2]Katika siku zile mimi, Danieli, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. [3]Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.
[1]Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
[2]Katika siku zile mimi, Danieli, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.
[3]Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.
Unaona…Sasa tukiendelea kusoma mbeleni ndio tunaona akitokewa na yule malaika. Na kumwambia maneno haya;
Danieli 10:12
[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Kumbe kitendo cha Danieli kuzingatia jumbe alizopewa..mbinguni alikuwa anaonekana kama mtu aliyetia moyo wake ufahamu ili kutaka kujua.
Ni nini tunajifunza kwa Danieli?
Hata sasa, Mungu anatafuta watu kama hawa. Ni mara ngapi watu wanamsikia Mungu akizungumza nao kwa njia mbalimbali hususa kwa Neno lake lakini hawataki kutia mioyo yao ufahamu kusikia?.
Na ndio hapo utashangaa mtu anaona kila kitu ni sawa tu. Hajui kuwa ni Mungu anataka kumpigisha hatua nyingine..lakini yeye anaenda kwa desturi na mazoea ..kila siku kanisani ni kusikia tu Neno basi hatii moyo wake ufahamu wa kutaka kusikia sauti ya Mungu inamwambia nini nyuma yake(Maana yake kuwa hatilii maanani).
Na ndio maana hakuna badiliko lolote la maisha yake.
Mungu huwa anataka tutie mioyo yetu ufahamu kwanza ndipo aseme na sisi zaidi au kutuhudumia, kama alivyokuwa akifanya Danieli.
Shalom
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
TUSIWE WATU WA KUPUNGUKIWA AKILI.
Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?
Shalom nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Leo nataka tujifunze jambo la muhimu sana ambalo Bwana anataka tufahamu tunapokwenda mbele zake hususani katika kumwomba msamaha au rehema..hili ni jambo la muhimu sana..naomba usome hadi mwisho.
Kwa kawaida hakuna mtu asiyemkosea Mungu..hata kama hutamkosea kwa dhambi ya moja kwa moja zipo dhambi nyingine ndogo ndogo ambazo si rahisi kuzitambua kwa haraka..kwamfano unaweza kumkwaza jirani yako kwa kauli fulani.ambayo pengine wewe uliiona ni sawa tu, lakini kumbe hujui tayari ulishatenda dhambi mbele za Mungu, kumfanya mwenzako ajisikie vibaya…na ndio maana maisha ya toba ni ya muhimu sana kwa mkristo yeyote..
Sasa jambo ambalo wengi hatujui ni kuwa msamaha wa Mungu unayo masharti yake..huwa hauji hivi hivi tu kama unavyodhani..Na leo tutaona ni kwanini..
Embu kaa chini uitafakari kwa makini ile sala ya Bwana..ukisoma pale vizuri utaona wanafunzi wake walipomwomba awafundishe kuomba hakusita kuwafundisha, mwanzoni alianza kwa kuwaambia vipengele vya kuombea, bila masharti au vigezo vyovyote ..kwamfano aliposema “utupe leo riziki zetu hakutoa” sababu yake mbele kwanini iwe hivyo..hakusema kwa kuwa na sisi tunawapa wengine riziki zetu..hapana..bali alisema tuombe tu hivyo hivyo na Mungu atatugawia..vilevile aliposema “usitutie majaribu” hakusema kwasababu na sisi hatuwatii watu wengine majaribuni hapana..alisema tuombe tu hivyo hivyo inatosha na yeye mwenyewe atatuepusha na majaribu yote…
Lakini alipofikia kipengele cha Utusamehe makosa yetu..utaona hapo hapo alitoa na sababu ya kwanini sisi tusamehewe..na sababu yenyewe ni kwasababu na sisi tunawasamehe waliotukosea makosa yetu..
Hapo ndipo Mungu anapataka kila mmoja wetu ajue na aliweke hilo akilini kwamba hayo mawili yanakwenda sambamba..hapo hamvumilii mtu yeyote..na ndio maana kayaambatanisha yote mawili kwa pamoja.
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] 14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”.
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”.
Umeona bado huko mwishoni kabisa Kristo analiwekea tena msisitizo neno lile lile alilolisema katika hiyo sala..kwamba Mungu anasamehe tu pale tunaposamehe..ndugu Mungu anaweza kukupa kila kitu unachomwomba hata kama wewe huwapi wengine hivyo vitu…anaweza kukufanyia jambo lolote lile utakalo hata kama huwafanyii wengine hayo..unaweza ukawa mchoyo wa kupindukia na mbinafsi kwelikweli hutaki kuwapa watu vyakula vyako vinaozea huko ghalani..lakini ukamwomba Mungu akupe nafaka nyingi zaidi na akakupa tena tele mpaka ukakosa pa kuweka.
Lakini kwenye suala la kumwomba msamaha kama hutamsamehe ndugu yako aliyekukosea..hutamsamehe mke wako/mume wako aliyekuvunja moyo au kukusaliti ..sahau Mungu kukusamehe na wewe makosa yako..hiyo ondoa akilini kumbuka Mungu yupo makini (STRICT) sana na neno lake…akisema amesema..usijidanganye wala usidanganywe na mtu..huna msamaha wowote wa dhambi zako zote zilizokutangulia wala unazozitenda leo hii..
Ukifa leo ni moja kwa moja kuzimu..hakuna mzaha hapo..Na ndio maana jambo la KUSAMEHE linapaswa liwe ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Haijalishi amekuudhi kiasi gani, amekutukana mara ngapi..kama bado una vinyongo vya tokea mwaka juzi, hutaki kuachilia na bado unaona okay..utakufa vibaya sana Ndugu ukiendelea hivyo, haijalishi utasema umeokoka. Dhambi hii imewashusha wengi kuzimu. Ni wengi kweli kweli kwasababu neno msahama kwao ni gumu lakini bado wanawataka na wenyewe wasamehewe na Mungu.
Bwana atutie nguvu. Tujifunze kusamehe Tutembee katika kanuni zake.Ili tuishi kwa amani hapa duniani, tuikwepe hukumu ya Mungu.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?
NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?
SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.
Kama Mungu ndiye kaumba kila kitu, je ni yeye huyo huyo ndiye aliyeumba dhambi pia?
SWALI: Naomba kufahamu Wagalatia 1:8 ina maana gani? Ni kwa namna gani malaika wa mbinguni wanaweza kutuhubiria sisi?
JIBU: Tusome,
Wagalatia 1:8 “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe”.
Ni vizuri tukafahamu kwanza ni kwanini mtume Paulo alisema kauli kama hiyo. Alisema hivyo kutokana na kuzuka kwa makundi ya watu ambao walianza kuhubiri injili nyingine tofauti na ile waliyokuwa wanaihubiri yenye kiini cha Yesu Kristo, na matokeo yake ikapelekea mpaka imani za watu wengi kupinduliwa, ambao tayari walikuwa wameshaijua njia ya kweli.
Na ndio maana mistari ya juu yake Paulo anasema..
Wagalatia 1:6 “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. 7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo”.
Wagalatia 1:6 “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo”.
Unaona? na jambo la hatari zaidi ni kuwa watu hao waliowafundisha , walikuwa wanasema mambo hayo wamefunuliwa na Mungu mwenyewe, kwa kupitia maono ambayo waliletewa na malaika wa mbinguni.
Utalithibitisha pia hilo katika.
Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, KWA KUNYENYEKEA KWA MAPENZI YAKE MWENYEWE TU, NA KUABUDU MALAIKA, AKIJITIA KATIKA MAONO YAKE NA KUJIVUNA BURE, KWA AKILI ZAKE ZA KIMWILI; 19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu”.
Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, KWA KUNYENYEKEA KWA MAPENZI YAKE MWENYEWE TU, NA KUABUDU MALAIKA, AKIJITIA KATIKA MAONO YAKE NA KUJIVUNA BURE, KWA AKILI ZAKE ZA KIMWILI;
19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu”.
Sasa kwa namna ya kawaida ni rahisi mtu kuamini pale anapoambiwa maono hayo au maagizo hayo, yameletwa na malaika. Ni rahisi kudhani agizo hilo ni la Mungu.
Mpaka baadaye taarifa hizo zikawafikia mitume, ndipo hapo sasa tunaona mtume Paulo, akitoa maneno makali kama hayo, na kusema, “ ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe”.
Yaani akiwa na maana kuwa maono yoyote yanayosadikika yametoka mbinguni aidha kwa mkono wa malaika, au wa nabii au mitume wowote, lakini ni nje na mafundisho ya msingi ya mitume, basi na ALAANIWE.
Lakini kumbuka kauli hiyo haimaanishi kuwa malaika watakatifu wanaweza kuleta maono ambayo hayatokani na Mungu hapana, ni mapepo ndio yanayoweza kufanya hivyo. Isipokuwa tu mtume Paulo hapo alikuwa anaweka msisitizo wa uhakika wa injili yao. Kwamba ni ya kweli na haiwezi kupinduliwa na kiumbe chochote kilicho juu mbinguni au kilicho chini duniani, kwasababu ni injili ya kweli ya Mungu mwenyezi.
Hata sasa, ndugu yangu wapo watu wanaoishi kwa maono na ndoto, wamelitupa kapuni Neno la Mungu, wapo tayari kutii kila wanachoambiwa au kusikia hata kama kinakwenda kinyume na Neno la Mungu. Kipindi hichi roho za udanganyifu zipo nyingi, na ndio maana tumeambiwa tusiziamini kila roho bali tuzipime kama zimetokana na Mungu au la!,(1Yohana 4:1 ). Utasikia mtu anasema Mungu amenifunulia,nikamwoe mke wa fulani au nikaongeze mke wa pili, na yeye bila kutathimini hayo maagizo kama yanaendana na Neno la Mungu, yeye anakwenda kufanya vile. Kumbe hajui kuwa tayari ameshapotea, anaishi katika uzinzi na siku ya mwisho atahukumiwa.
Hivyo tuwe makini sana, suluhisho pekee ni tudumu katika mafundisho ya mitume (Neno la Mungu), ndio tutakuwa salama daima. Usitishwe na maneno ya mtu yeyote anayekuambia malaika kanitokea au nimeonyeshwa maono. Lithibitishe kwanza katika Neno la Mungu. Kama linakinzana litupe kapuni, ishi kwa Neno.
Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? Ina maana gani?
Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)
Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?