Je Bwana Yesu alikuwa na mchoro (tattoo) katika paja lake?

Je Bwana Yesu alikuwa na mchoro (tattoo) katika paja lake?

Tusome..

Ufunuo 19:16 “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”

Mstari huu unatumika na wengi wanaohalalisha uchoraji wa tattoo katika miili yao, kuwa hata Bwana Yesu mwenyewe alijichora tattoo katika paja lake.

Je ni kweli hiyo ndio maana ya huo mstari?
Jibu ni la! Katika Maono hayo Yohana aliyoyaona, hakuona nyama ya paja la Bwana Yesu ikiwa limeandikwa hayo maneno, bali alichokiona ni vazi lililofunika paja limeandikwa maneno hayo, BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME.

Kwamfano kuna andiko linasema jifunge upanga pajani mwako..

Zaburi 45:3 “Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako”.

Je kwa mstari kwa huo biblia imemaanisha, kuchua upanga na kuubandika kwenye nyama ya paja?..

Bila shaka haikumaanisha hivyo bali ilimaanisha funga upanga katika ghala iliyopo viununo mwetu.

Au labda mtu akupe maagizo ya kubeba kiroba cha mzigo Begani, je atakuwa anamaanisha uvue nguo ubaki bega wazi ndio ubebe mzigo huo?.

Au mtu akwambie vaa mkanda kiunoni, atakuwa amemaanisha uvue nguo zote halafu ujifunge mkanda kwenye nyama ya kiuno chako? Jibu ni la!..bali amemaanisha katika vazi lililopo kiunoni kama ni suruali au nguo nyingine yoyote, ifungwe kwa mkanda.

Vile vile katika mwonekano mwingine wa Bwana kuna mahali, maandiko yanasema alionekana kafungwa mshipi wa dhahabu “matitini”.

Ufunuo wa Yohana 1:13 “na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini”.

Bila shaka mstari huo haukumaanisha ndani ya kifua cha Bwana kuna mshipi umedungwa wa dhahabu, bali biblia imemaanisha kwenye vazi lake la nje, sehemu ya kifua palikuwa na mshipi (yaani mkanda).

Kadhalika katika mstari huo,wa Ufunuo 19:16, biblia haijamaanisha kuwa kuna maneno yaliyoandikwa kwenye nyama ya paja, bali imemaanisha maneno yaliyoandikwa katika vazi lililofunika paja.

Hakuna mahali popote maandiko yanaagiza wala kutufundisha kujichora tattoo.

Kujichora kwa aina yoyote ile, ikiwemo kupaka hina ni dhambi kibiblia, Na wote wanaojichora hawataurithi uzima wa milele (Kwa maelezo marefu kuhusu kujichora na kujichanja kibiblia unaweza kufungua hapa Kujichota ni dhambi

Je umempokea Yesu?..je umebatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jinala Yesu?, Mambo haya mawili ndio msingi wa wokovu, na kila mtu lazima ayafanye ili awe mkristo.

Bwana atubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp ya kila siku basi jiunge kwa kubofya hapa >>> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JE! WEWE NI MFUNGWA WA BWANA?

NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU.

WAKAMCHA BWANA, NA KUITUMIKIA MIUNGU YAO WENYEWE.

HAPANA MFUPA WAKE UTAKAOVUNJWA.

Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?

USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Friedrich the son of JESUS%
Friedrich the son of JESUS%
2 years ago

Leave your message
Amina! Mungu azidi kukupa ufunuo zaidi!
Good92&peace and joy.