SWALI: Yakobo aliposhindana na Malaika alishikwa uvungu wa paja akateguka…Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?
Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Jibu: Uvungu wa paja, ni eneo la juu ya paja ambapo mfupa wa paja umekutana na ule wa kiuno. Kama tunavyosoma hapo Yakobo baada ya kushindana na Yule malaika kwa masaa mengi sana usiku kucha bila kuwa na dalili yoyote ya kumwacha, tunaona biblia inatuambia Yule malaika, alimtengua uvungu wa paja lake.
Kumbuka kutegua/kutengua ni tofauti na kuvunja,..Kitu kikivunjwa maana yake ni kinaharibiwa, kinahitaji kuunganishwa, lakini kikitenguka maana yake ni kinahama eneo lililopo kwa muda tu.. Hivyo kwa namna ya kawaida mwanadamu maeneo yote ambayo mifupa miwili inakutana huwa ni rahisi kutenguka, husani pale anapoanguka sehemu ndefu, au kubanwa au kuvutwa kwa nguvu mahali penye maongeo, kwa mfano goti, au viwiko vya mikono au miguu, vidole, bega au kwenye paja.. Na huwa inaambatana na maumivu makali sana, ambayo maumivu yake yanafanana tu ya yale ya kuvunjika, wakati mwingine yanamfanya mtu asindwe kabisa kutembea kama sio kuchechemea, na mpaka yaishe inaweza kuchukua wiki mbili mpaka tatu au Zaidi.
Sasa Yakobo yeye, alitenguliwa kwenye huu mfupa mkubwa wa paja, ambao ndio mkubwa na maumivu yake ndio makali kushinda yote.
Lakini kwanini Mungu afanye vile, Ni jambo gani tunajifunza hapo?
Baraka za Mungu ni za kuzipigania, na sio hilo tu, bali pia zinaambatana na maumivu.. Ukitaka Mungu akubariki kubali kukutana na mapigano na maumivu fulani, Jina la Israeli halikuja hivi hivi, lilikuwa ni la jasho na maumivu. Vivyo hivyo na sisi, tusikubali kuambiwa njoo, ubarikiwe, na huku, hatutaki kusikia gharama za kubarikiwa, ambazo ni kuishi maisha ya kubarikiwa.
Maisha ya kubarikiwa ni kama haya:
Bwana Yesu alisema Mathayo 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”.
Lakini kama ulichonacho unajilimbikizia wewe tu mwenyewe, Na hapo hapo bado unataka nawe pia ubarikiwe, hilo jambo halipo!. Ipo mifano mingi sana..Ikiwa humtolei Mungu, tena kile kinachokugharimu kabisa, mpaka unaona maumivu rohoni, ni ngumu kubarikiwa na Mungu.
Si wakati wote unahitaji kuomba ili Mungu akuone, unahitaji kufanya zaidi..Pale ulipo unaanza, Mtume Yohana alimwambia Gayo, maneno haya 1Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”.
Utajiuliza huyu Gayo ni nani, kwanini hakumwandikia kila mtu waraka ule wa mafanikio, bali Gayo tu peke yake, Hivyo ukitaka kujua ni kwanini alimwandikia yeye na si wengine, nenda kasome sura ile yote ujue ni mambo mangapi alijitoa kwa Mungu katika kuwahudumia watakatifu na kuwakaribisha wageni wale waliokuwa wanasafiri kuipeleka injili na kuwapatia mahitaji yao, mpaka sifa zake zikavuma katika kanisa lote.. Hapo ndipo Mtume Yohana kwa uongozo wa Roho Mtakatifu akaongozwa kumwandikia maneno yale ya baraka.
Lakini hiyo ilikuwa ni mashindano na maumivu makali ya kuinyima nafsi yake.
Vivyo hivyo na sisi, tukumbuke kuwa Baraka za Mungu zitaambatana na kutenguliwa miguu yetu..Kama tupo tayari kwa hayo basi tuingie mapambano, Na tunaingia mapambanoni, sio kwa maneno bali kwa matendo.
Bwana atubariki sote, katika safari yetu ya imani.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
https://wingulamashahidi.org/ushirikina-na-madhara-yake/
Jabari maana yake ni mtu hodari, asiyeogopa, shujaa.
Isaya 49:24 “Je! Aliye hodari aweza kunyang’anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka?
25 Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye JABARI wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu”.
Unaona, Jabari ni mtu shujaa lakini kibiblia kuna majabari wa aina mbili,
Zaburi 52:1Kwa nini kujisifia uovu, EWE JABARI? Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.
5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
6 Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; 7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. ALIUTUMAINIA WINGI WA MALI ZAKE, NA KUJIFANYA HODARI KWA MADHARA YAKE.
8 Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Waebrania 11:33 “ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,
34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, WALIKUWA HODARI KATIKA VITA, walikimbiza majeshi ya wageni.
35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;
36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.
39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;
40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.
Swali ni Je! Wewe ni Jabari katika nini?
Jibu unalo, lakini ikiwa upo katika ouvu, au mambo ya kidunia, basi Yesu anaweza kukufanya kuwa Jabari lake teule ikiwa tu leo utampokea..Ukipomkea atakusamehe dhambi zako zote, atakufanya kuwa mwana wake,atakuondolea laana zote, atakupa Roho wake Mtakatifu bure, atakupa amani, na kikubwa zaidi atakupa na uzima wa milele .
Unasubiri Nini? Tangu ulipoanza kuitumikia dunia imekupa nini? Hivyo usikawie, ikiwa umedhamiria kwa moyo wako wote, kumkaribisha Yesu katika maisha yako, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Sasa Ikiwa ufuata maaelekezo hayo hapo juu, basi kuanzia sasa wewe ni JABARI la Bwana Yesu. Na utamwona atakavyoanza kutembea na wewe kukutengeneza..
Bwana akubariki.
1Wakorintho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari”.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?
Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?
NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Baradhuli ni nani/ ni nini kama lilivyotumika kwenye biblia?
Kibiblia Baradhuli ni mtu asiyefaa, mpumbavu sana, aliyevuka mipaka
Ipo mistari kadha wa kadha inayoeleza tabia za watu wabaradhuli. Kwa mfano:
Wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji angali wanajua kabisa wanachokifanya ni kinyuma na mapenzi ya Mungu, wanaofanya uchawi, wanaofanya matambiko n.k. Hao ni mabaradhuli kibiblia.
Kumbukumbuku 13:12 Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo Bwana, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa,
13 Kumetoka katikati yako MABARADHULI kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua;
14 ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii; nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano wa haya yafanyika katikati yako;
15 hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga.
Ukisoma kitabu cha Waamuzi utaona Gideoni alikuwa na watoto sabini na wawili, lakini baada ya Gideoni kufa, mtoto wake mmoja aliingiwa na tamaa kutawala sehemu ya Gideoni hivyo akaamua kuwaua ndugu zake wote waliosalia ili yeye afanywe muamuzi badala yake, Ndipo biblia inatuambia alikwenda kuwaajiri watu Mabaradhuli ili kutekeleza adhma yake hiyo ya uuaji,..Hao watu wakashirikiana naye kuwaua ndugu zake wote siku moja juu ya jiwe. (Waamuzi 9:1-5).
Ukisoma tena kitabu cha Waamuzi 19 utamwona Yule mlawi ambaye alikuwa na suria wake, aliyekwenda kufanya ukahaba, kitendo ambacho kilimpelekea amrudishe nyumbani kwa baba yake, hivyo akakaa kule kwa muda wa miezi 4, ndipo baadaye akaghahiri akaamua amfuate surua wake amrudishe kwake, sasa alipokuwa njiani mji mmoja wa ugenini, alikaribishwa na mzee mmoja wa mji ule. Lakini usiku mambo yalibadilika kwani wale watu wa mji ule wa Benyamini, waliizingira nyumba wakataka wapewe hao wageni walale nao..Kama tunavyoijua habari Yule mlawi akaona ni heri amtoe suria wake wamfanye waliyotaka kumfanya..Wakafanya hivyo mpaka asubuhi baadaye Yule Suria akafa..
Waamuzi 19:22 “Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu MABARADHULI wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua”.
Soma sura yote ya 19,20 na 21, upate picha kamili, na nini kiliendelea baada ya pale..
Watu wanaoshikamana na viongozi waasi, au waliokosa heshima katika jamii.
2Nyakati 13:7, Waamuzi 11:3.
Je mpaka sasa mabaradhuli wapo?
Unapaswa ujiulize je! tabia mojawapo ya hizo unazo?
Kumbuka kuwa waovu wote, sehemu yao ni katika lile ziwa la moto. Ikiwa wewe ni muuaji, wewe ni baradhuli, ikiwa wewe ni mchawi(unakwenda kwa waganga) wewe ni baradhuli, n.k.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Lakini tumaini lipo kwa Yesu tu peke yake. Yeye peke yake ndiye anayeweza kuyageuza maisha yako na kukusaheme kabisa kabisa. Na kukufanya kuwa mwana wake.
Je! unahitaji kuokoka leo?
Unahitaji Yesu ayabadilishe maisha yako leo?
Unahitaji kupokea Roho Mtakatifu?
Biblia inasema..
Isaya 1:18 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi”;
Kama ndivyo basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
MWEZI WA ABIBU/NISANI NI MWEZI GANI?
Arabuni maana yake ni nini?
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
Areopago ni nini?
Areopago ni baraza kuu la Waathene au mahali walipokutanika wakuu wa Athene. Kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali ya muhimu,kama vile kusikiliza kesi zinazohusiana na mauaji au dini, au kutoa hukumu, au kuchambua mambo mengine yenye uzito katika jamii.
Eneo hili lilikuwa upande wa kaskazini magharibi mwa mji wa Athene,Ukigiriki, na lilijengwa ya juu ya mwamba mkubwa.
Baraza hili, lilifanana na lile baraza la wayahudi ambalo, wazee pamoja na kuhani mkuu walikuwa wanakutanika kutoa mashahuri juu ya kesi za kidini, kama vile ilivyokuwa wakati wa Bwana Yesu (Mathayo 26:57-68)
Sasa Mtume Paulo alipofika katika mji huu na kuanza kuhubiri, tunaona baada ya habari zake kusikika sana katikati ya jamii ya waethene, walimkamata na kumpeka mbele ya baraza hili kuu (Areopago) ili kumsikiliza vizuri juu ya imani yake.
Tusome:
Matendo 17:16 “Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.
17 Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku.
18 Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.
19 Wakamshika, wakamchukua AREOPAGO, wakisema, Je! Twaweza kujua maana ya elimu hii mpya unayoinena?
20 Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, basi, maana ya mambo haya.
21 Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya.
22 Paulo akasimama katikati ya AREOPAGO, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.
23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua……
32 Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo.
33 Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha.
34 Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, MWAREOPAGO, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao”.
Kama tunavyoona wapo miongoni mwa hao wakuu wa baraza wapo waliodhihaki, na wapo walioamini kama vile huyo Dionisio mwareopago.
Ndio, Hata sasa katika agano jipya ma-areopago yapo mengi, Bwana Yesu alishayazungumzia na kuonya kuwa watakatifu watakutana nayo katika safari zao za Imani, na katika kuhubiri injili.. Lakini Bwana Yesu alitupa kanuni ya kusimamia, akasema hivi;
Mathayo 10:17 “Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.
Hivyo, kama umeokoka,au unahubiri injili na ukajikuta umewekwa katikati ya viongozi wa dini, hupaswi kuogopa Areopago lolote..Kwasababu Bwana ameahidi kuwa na wewe.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.
SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.
JIFUNZE KULIGAWANYA VYEMA NENO LA MUNGU.
Israeli ipo bara gani?
Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe..Ni neema Bwana katujalia kuliona jua tena siku ya leo, karibu tuyatafakari maandiko Pamoja..
Kama tunavyojua tunaishi katika siku za mwisho, na kila dakika inayosogea mbele ndivyo tunavyozidi kuusogelea ule mwisho…Hivyo leo tu tayari tumeshapunguza siku nyingine moja, kati ya zile chache zilizobakia mbele yetu, kuufikia ule mwisho.
Lakini Pamoja na hayo biblia inatuonya kuwa mojawapo ya dalili za kurudi kwa pili kwa Kristo ni kuongezeka kwa MAASI NA MAARIFA. Leo hatutazungumzia sana juu ya kuongezeka kwa maarifa, kama utapenda kufahamu juu ya hilo basi utatutumia ujumbe inbox tukutumie somo lake. Lakini leo tutaangalia juu ya kuongezeka kwa MAASI,(Mathayo 24:12) ambapo tutajifunza kitu cha muhimu sana. Na pia nakushauri kabla ya kusoma somo hili, tenga muda pitia somo fupi lililotangulia kabla ya hili lenye kichwa kinachosema “Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi? Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo?” kwasababu linamahusiano mkubwa sana na hichi tutakachokwenda kujifunza leo.
Ukiyatafakari Maisha ya leo unaweza kusema, ni afadhali na jana na juzi kuliko leo kwa jinsi maasi yanavyozidi kuongezeka…Upendo wa wengi unapoa, mauaji yanaongezeka, chuki zinaongezeka, visasi, ubinafsi, wizi, uasherati na kila aina ya uchafu, unazidi kuongezeka…
Hiyo yote ni ishara ya kurudi kwa pili kwa Kristo, Lakini swali la kujiuliza ni je!.. kwanini ishara ya mabaya ndio iwe dalili ya kurudi kwa Yesu, na si Ishara ya mazuri, yaani kwanini Bwana Yesu asingesema kabla ya kurudi kwake Mema yataongezeka sana?.
Jibu ni kwamba…wakati wa Kristo kurudi, (yaani kipindi kifupi kabla ya kutokea mawinguni) Kiwango cha utakatifu cha watakatifu kitakuwa kipo juu sana.. Na ishara mojawapo ya kuwa kiwango cha utakatifu kimekuwa kikubwa ni kiwango cha maovu kuwa kikubwa.
Ndugu unapoona dhambi zimezidi mipaka, jua kuwa sehemu Fulani mema yamezidi sana… Inaweza isiwe ni watu wengi wanatenda hayo mema, lakini hata kama ni mmoja tu! Basi atakuwa anatenda mema kwa kiwango kikubwa..
Wengi hawalioni hili wakifikiri kwamba kwasababu dhambi ni nyingi katika kipindi hichi basi hakuna kabisa watu wanaompendeza Mungu. Usilisahau hilo siku zote (Maovu kuwa juu ni ishara ya utakatifu pia kuwa juu). Ukiona kuna maasi makubwa sana katika mji fulani jua upande mwingine katika mji huo huo kuna wakamilifu au mkamilifu wa kiwango kikubwa sana.
Wakati Mungu amechukizwa na maasi ya Sodoma na Gomora, wakati huo huo Mungu alikuwa amependezwa sana na mtu mmoja aliyeitwa Ibrahimu, ambaye tunamwita sasa Baba wa Imani, Hivyo Ishara ya maasi kuongezeka Gomora ni ishara ya wema kuongezeka kwa mtu Fulani wa Mungu mahali fulani. Ukiona dunia inazidi kuoza sasa, jua ni ishara kuwa kuna watakatifu mahali Fulani wanazidi kujitakasa sana.
Ukiona sasa hivi kuna wanawake wengi wanaotembea nusu uchi barabarani, na hata wanaingia makanisani wakiwa hivyo… usifikiri ni wote wapo hivyo…Hiyo ni ishara ya kuiogopa sana, kwasababu ni ishara kuwa kuna mwanamke/wanawake mahali Fulani wanaojiheshimu na kujisitiri sana, na kumheshimu Mungu kwa viwango vya kimbinguni..
Unapoona kuna wimbi la manabii wa uongo..ni jambo la kuogopa wala sio la kucheka na kudharau, kwasababu hiyo ni ishara kwamba kuna kuna watumishi wa Mungu wa kweli. Biblia inasema katika siku za mwisho magugu na ngano vyote vitakomaa.. hivyo ukiona shambani magugu yamekomaa jua na ngano pia zimekomaa…Ndio maana mavuno yanakuja.
Hata Maisha ya kawaida yanatufundisha..Ijapokuwa miaka hii watu wanaonekana duniani kuwa dhaifu, na magonjwa kuongezeka na uwezo kupungua…lakini ukifuatilia rekodi, utagundua kuwa bado zinavunjwa kila mwaka.
Mtu mwenye mbio kuliko wote anaishi miaka yetu hii hii ambayo watu wanakula vibaya, watu wana magonjwa sana n.k. kumbe katikati ya kizazi ambacho watu ni wadhaifu watakuwepo watu ambao ni Hodari kuliko wote katika historia?.
Na katika Imani ni hivyo hivyo…Katikati ya maovu ya dunia yaliyokithiri, Bwana anao watu wake walio waaminifu, wakati wa mfalme Ahabu ambapo Yezebeli mke wake aliifanya Israeli kuwa nchi ya kichawi kiasi kwamba manabii wote waliouliwa, lakini mahali Fulani alikuwepo Eliya Mtishbi, na kama hiyo haitoshi walikuwepo pia manabii wengine 7000 ambao hakupigia goti baali katika mji, Bwana aliojisazia.. Hivyo ndugu huu sio wakati wa kusema aaah! dunia imeharibika yote, hivyo na mimi lazima niwe mwovu…au aaah siku hizi hakuna watakatifu hivyo hakuna haja ya mimi pia kujitakasa..n.k Usikubali kuusikiliza huo ni uongo wa shetani ambao upo kama KILEVI, shetani anawalevya watu wote wa ulimwengu, wafikiri kwamba hali inafanana kila mahali na kwa kila mtu.
Likumbuke hili neno.. Mhubiri 7:10 “Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi? Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo”.?
Bwana atusaidie tufumbuke macho..na tuzidi kujitakasa. Maadamu wakati siku ile inakaribia.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAONO YA NABII AMOSI.
Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?
YONA: Mlango wa 4
UFUNUO: Mlango wa 3 part 3
SWALI: Ibada ni nini, Na je ili ibada ikamilike inapaswa iwe na nini na nini? Na je ni siku gani maalumu ya kufanya ibada?
Ibada ni kitendo chochote kifanywacho kuonyesha unyenyekevu wa hali ya juu, utiifu, heshima, shukrani, na utukufu, aidha kwa Mungu au kitu kingine, na hiyo inaambata na mambo kadha wa kadha, ikiwemo kusifu, kuabudu, kusujudu, kuimba, kufunga, kutoa sadaka, na kushiriki maagano ya imani, Na vilevile kujitoa mwili wako kuvitumikia, hiyo nayo ni ibada kamili.
Kibiblia kuna ibada za aina tatu
Hizi, ni zote tuzifanyazo aidha kanisani au manyumbani kwetu wenyewe, tunapokutana kumwimbia na kumwabudu Mungu, au kumshukuru, au kushiriki meza ya Bwana, hiyo tayari ni ibada kwa Mungu.
Matendo 13:2 “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia”.
Na kama tulivyosema awali hata kujitoa mwili wako kwa ajili ya kutenda matendo yote yampendezayo Mungu ni ibada kamili tayari..
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.
Hizi kwa jina lingine ndio ibada za sanamu. Ambazo biblia imezikemea sehemu nyingi sana katika biblia. Unapokwenda kuisujudia sanamu yoyote ile, iwe na mfano wa mtakatifu Fulani mbinguni, tayari hiyo ni ibada kamili ya sanamu.. Inayomtia Mungu wivu wa kukuangamiza haraka sana.
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
1Wakorintho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu”.
Lakini kama hilo halitoshi, unaweza pengine ukawa husujudii masanamu, lakini mwili wako unafanya maasi, hiyo nayo ni ibada kamili ya sanamu sawasawa na kusujudia vinyago.
Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu”;
Hizi ni ibada ambazo, hazitokani na Mungu wala shetani, bali zinatokana na watu wenyewe, wamejitungia wakidhani kuwa wanamfanyia Mungu, kumbe wanafanya kimakosa..
Wakolosai 2:20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
21 Msishike, msionje, msiguse;
22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, KATIKA NAMNA YA IBADA MLIYOJITUNGIA WENYEWE, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Na zina madhara yake makubwa, kwasababu wakati mwingine zinasababisha hata watu waue watu wengine wakidhani kuwa ndio wanampendeza Mungu, kama tu walivyokuwa wanafanya Warumi na Wayahudi kwenye kanisa la kwanza, na jinsi zinavyofanywa na baadhi dini leo hii duniani kuchinja watu. Zote hizo ni ibada ambazo watu wamejitungua lakini hazitokani na Mungu.
Yohana 16:2 “Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa ANAMTOLEA MUNGU IBADA.
Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa, ibada halisi ni moja tu, nayo ni kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi (YEHOVA), na Kristo wake aliyesulibiwa kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanadamu. Na maagizo pekee ya ibada hiyo halisi yanapatikana katika biblia tu.. Ibada nyingine yoyote tofauti na hiyo, ni machukizo makubwa kwake.
Na pia tunaikamilisha kwa miili yetu kama biblia inavyotufundisha, kwa kuishi maisha yampendezayo Bwana, ndio ibada yenye maana, ikiwa tutakuwa tunahudhuria kanisani kila siku, tunamwabudu Mungu usiku na mchana, tunamtolea matoleo mengi, tunashiriki meza ya Bwana kila wiki halafu matendo yetu, au miili yetu tumeiuza kwa shetani, ibada zetu bado ni batili..Zinakuwa ni ibada za sanamu, au ibada tulizojitungia tu sisi wenyewe.
Lakini kama utayakamilisha yote ya rohoni na mwilini, basi ibada hiyo inafaa sana mbele za Mungu, na inathawabu nyingi sana. Wanaomfanyia Mungu ibada kamili wanakuwa marafiki wa karibu sana Mungu.
Na pia hakuna siku maalumu ya kumfanyia Mungu ibada, kwani ibada yetu halisi ipo rohoni, hivyo wakati wowote na muda wowote uwapo na nafasi inaingia uweponi mwa Mungu, kumsifu, kumshukuru, kumwabudu, kumtolea dhabihu za shukrani n.k.. Lakini pia ipo ibada ya watakatifu wote, ambayo inafanyika kila juma, hivyo ikiwa ni jumapili au Jumamosi, inapaswa ifuatwe. Kama tulivyoambiwa tusiache kukutanika pamoja..
Bwana wetu atusaidie sote, tuweze kuyakamilisha hayo.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
USILETE UJIRA WA KAHABA, NYUMBANI KWA MUNGU.
Nyama zilizosongolewa ni zipi?Je kunywa damu ni dhambi?
JE KUVAA PETE NI DHAMBI?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
CHAPA YA MNYAMA
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.
SWALI: Nini maana ya huu mstari.. Mhubiri 7:10 “Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi? Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo? “
JIBU: Mstari huo kwa lugha ya kueleweka zaidi ni sawa na kusema, “Usiseme mbona siku za kale, au nyakati za zamani zina afadhali kuliko siku hizi au nyakati hizi nilizopo mimi? Kwani kusema hivyo hujatumia hekima kufikiri.”
Msemo huu, ni maarufu hata sasa, tunaona kama wale watu wa zamani walikuwa ni watu wa ki-Mungu sana kushinda sisi, Au Watu wa zamani walikuwa wanaishi kwa raha kuliko watu wa sasahivi..Tukiwa tunafikiri hivyo ni ishara kuwa tumeshindwa kuyatimiza majukumu yetu ya msingi tuliyokabidhiwa sasa na Mungu, kwa kisingizio kuwa majira yamebadilika.
Ukweli ni kwamba hata hao watu wa kale ungewafuata na kuwauliza, nao pia wangekuambia heri watu wa kale kuliko sisi wa kipindi chetu.. Hivyo sisi sote tumepewa nafasi sawa, biblia inaposema hakuna jipya chini ya jua, fahamu kuwa unachokipitia sasa, ndicho walichokipitia watu wa kale, unayoyaona sasa ndiyo waliyoyaona wale, kama maovu yalikuwepo, tena pengine mengi kuliko unayoyaona wewe leo, mpaka wengine wakafikia hatua ya kugharikishwa na wengine kuteketezwa na moto.
Hivyo kama unaona wengi wao walikuwa karibu na Mungu, basi ni katika shida kama ulizonazo wewe, ni katikati ya maovu kama unayoyapitia wewe. Hivyo kusema heri siku za zamani kuliko hizi, ujue kuwa hutumii hekima kuuliza hivyo.
Ikiwa tunaukataa wokovu sasa au unakataa kuitenda kazi ya Mungu kwa kisingizio kuwa shughuli zinatusonga nyakati hizi zimebadilika, sio kama zamani, tujue kuwa hiyo sio hoja mbele za Mungu.
Ikiwa hatujizuii na mambo ya ulimwenguni, kwa kisingizio kuwa tunaishi katika majira ya dhambi kuliko mengine yote, kisa tunazo Internet, na simu, basi tujue kuwa hizo bado sio hoja mbele za Mungu.
Biblia inasema wapo watakaoshinda ulimwengu vizuri katika siku za mwisho, kuliko hata wale wa kwanza,
Luka 13:29 “Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.
30 Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho”.
Kwahiyo mimi na wewe tusiwe na sababu za kulaumu nyakati na majira tuliyopo..Ni wakati wa kuyafahamu majukumu yetu na kuyatimiza katika huu wakati mfupi tuliobakiwa nao hapa duniani. Ili na sisi tufanye vizuri zaidi kuliko wale, tupokee taji lililo bora. Hivyo tubadilishe hii mitazamo,
Mwisho Bwana atubariki sote, tuliozaliwa nyakati hii ya Laodikia.. Kwasababu tukishinda thawabu yetu ni kuwa kuliko za wengine wote..Kwasababu sisi tumeahidiwa kuketi pamoja na Mfalme mwenyewe (Bwana Yesu Kristo) katika kiti chake cha enzi, katika ufalme wake unaokuja, hakuna kanisa lingine lolote lililoahidiwa thawabu nono kama hii (kasome Ufunuo 3:21-22).. Hivyo Tukaze mwendo tusiikose.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
https://wingulamashahidi.org/sala-ya-baba-yetu-sala-ya-bwana/
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima, karibu tujifunze biblia.
Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo.. Je! Una uhakika wa mambo yatakayokuja ambayo bado hujayaona wala kuyafikia?..Na kama ndio, je kwa kiwango gani?.
Ili Imani yako ionekane kuwa kubwa ni lazima uwe na uwezo wa kuamini vitu visivyoweza kuaminika. Yaani uwe na kila sababu itakayokufanya kuwa na uhakika kwamba jambo Fulani lazima litokee.
Kwamfano ukizungumza na mtu kwenye simu, aliye umbali Fulani akakwambia panda gari (daladala) unifuate mahali nilipo baada ya lisaa limoja…bila shaka kama utakuwa na fedha ya kutosha mfukoni mwako, hutakuwa na wasiwasi wa kufika pale alipo…kwasababu unajua hata Ukikosa daladala utatafuta tax, na hata ukikosa hiyo bado unaweza kupanda pikipiki ukafika pale alipo katika muda ule ule. Hivyo huo uwezo wa kuwa na kila sababu ya kufika pale kwa muda unaotakiwa ndio unaoitwa IMANI (una uhakika wa mambo yatarajiwayo yatafanikiwa asilimia 100).
Lakini kama huna fedha kabisa au unafedha kidogo tu ya daladala, utakuwa na wasiwasi, utasema itakuwaje endapo nikikosa gari? itakuwaje endapo gari nitakalopanda likiharibikia njiani?..si nitachelewa n.k Hivyo unakuwa huna uhakika sana wa mambo yatarajiwayo..Hapo inahesabika kuwa Imani yako ya kufika unakotaka kwenda kwa muda unaotakiwa ni ndogo au huna kabisa.
Sasa tukirudi katika Biblia ni hivyo hivyo..Ili uweze kuhesabika kuwa na Imani kubwa ya kutosha ya kuweza kupata kile unachokihitaji kwa Asilimia zote, ni lazima uwe na Hazina ya kutosha ya UELEWA WA MAANDIKO, ili uweze kukipata kile kitu. Kumbuka hapo ninasema ni UELEWA WA MAANDIKO, na si IDADI YA MAANDIKO. Mtu mwenye idadi kubwa ya maandiko pasipo kuyaelewa huyo ni sawa redio yenye idadi kubwa ya sauti na nyimbo zinazotoka ndani yake, lakini yenyewe haielewi chochote.
Hivyo kinachojalisha kwetu ili tuhesabike kuwa na Imani ya kuweza kupokea jambo lolote lile ni HAZINA YA KUYAELEWA MAANDIKO NA KUYACHAMBUA.
Hebu tujifunze mfano mmoja kwenye biblia ya Mtu aliyekuwa na hazina na uwezo wa kuyaelewa maandiko vyema na kuyagawanya..
Mathayo 15:22 “Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.
Unaweza kuona hapo, anakatishwa tamaa kwa maneno ya YESU, na kama tunavyojua maneno ya Yesu ni Neno la Mungu. Lakini kwa maneno hayo hayo, mwanammke anayafafanua vizuri kwa Bwana, na hatimaye anapata haki yake.. “ni kweli si vyema kutwaa chakula cha watoto kuwatupia mbwa, lakini hata mbwa wanakula makombo yaangukayo chini ya meza za Bwana zao”…Maana yake ni kwamba sistahili kweli kupewa hichi ninachokitafuta, (ni kweli mimi ni kama mbwa).. Lakini kuna vile vidogo vichache vinavyobakigi..ipo neema kidogo inakuwepo kwa Mungu kwa wale wasiomcha yeye…Hiyo ndio ninayoihitaji mimi!..Ni kweli Mungu hasikii maombi ya waovu, lakini bado Mungu huyo huyo anawanyeshea mvua waovu na wema…anawaangazia jua lake wenye haki na wasio haki..
Ni kweli mimi sio mkamilifu mbele zake, lakini bado wale waovu kuliko mimi anahakikisha wanafikiwa na miale ya jua, anahakikisha upepo mwanana unawaburudisha, anahakikisha wanapata hewa safi ya oksijeni kila dakika..hivyo kwa rehema hizo, ni lazima na mimi na mimi lazima nipone, lazima nibarikiwe na kufanikiwa katika yote..Mungu hana mbaraka mmoja tu!.
Hebu tujifunze Zaidi kisa cha Esau na Yakobo.
Tusome..
Mwanzo 27: 33 “Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.
34 Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
35 Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.
36 Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?
37 Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu?
38 ESAU AKAMWAMBIA BABAYE, UNA MBARAKA MMOJA TU, BABANGU? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.
39 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia,penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu”.
Hebu tafakari Esau, angenyamaza asingelia kuomba na yeye abarikiwe, hebu tafakari angeishia kuondoka kwa majonzi leo hi angeishia kuwa kama Kaini, asingekuwa na baraka yoyote….Lakini japokuwa aliikosa ile Baraka kuu, lakini alilia kwa baba yake..akamwambia baba yake nibariki na mimi, kwani una mbaraka mmoja tu??? Na mwishowe akabarikiwa akaambiwa palipo na manono ya nchi patakuwa mahali pake, ingawa Mungu alimchukia Esau(Warumi 9:13)… lakini bado alimbariki alikuwa na mali nyingi hata Zaidi ya Yakobo kasome (kasome Mwanzo 33:9)
Na sisi ni hivyo hivyo, (simaanishi kuwa tuwe waovu, Mungu atusaidie), nachomaanisha ni kuwa ikiwa wewe ni mkristo hupaswi kukata tamaa hata kama inaonekana mambo yameshashindikana…Tujue tu! Mungu hana mbaraka mmoja tu!, usijiangalie ukamilifu wako!..Esau Mungu alimchukia lakini kwa kupambana akambariki hivyo hivyo…
Ukiona jambo Fulani katika Maisha kama haliwezekani, basi jua huo ndio uthibitisho kwamba linawezekana….kibiblia kutokuwezekana ndio uthibitisho wa kuwezekana kwa jambo. Amini tu! Amini tu.. usiache kumwamini Mungu kamwe.
Mwisho kabisa kama tulivyosema… “kubarikiwa wakati mwingine sio uthibitisho wa kumpendeza Mungu”..Esau hakumpendeza Mungu lakini alibarikiwa, na wengine wengi katika biblia…na hata leo Mungu ni yule yule…anawanyeshea mvua waovu na wema…Kwahiyo kuzimu watakuwepo matajiri sana, na mbingu pia watakuwepo maskini, hivyo lililo la Muhimu sana ni kutafuta kuyatenda mapenzi ya Mungu, ambayo hiyo inakuja kwa kutubu na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa Maisha yako na kutafuta ubatizo sahihi wa kimaandiko (Matendo 2:38), na kupokea Roho Mtakatifu, hilo ndio jambo la muhimu na la kwanza, mengine yatafuata. Lakini kama unahitaji jambo lolote…Mwombe Mungu kwa bidii na kumwamini, utaona majibu…
Bwana anakupenda, Bwana anatupenda, na Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.
HIZI NI NYAKATI ZA KUJIINGIZA KWA NGUVU.
JIFUNZE KULIGAWANYA VYEMA NENO LA MUNGU.
Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Maana yake nini?
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Shalom, kila mahali biblia inatuasa juu ya kujiweka tayari, wakristo wengi tunadhani wokovu ni suala la kuotea tu kwamba nitaokoka au tutaokoka siku yoyote, au baada ya kuokoka leo basi hakuna haja ya kuyakamilisha yale mapungufu niliyonayo..Hatujui kuwa wokovu ni process, ni mchakato endelevu,. ni jambo lenye maandalizi, maana yake ni kuwa mpaka unyakuliwe ni lazima uwe umekidhi vigezo vyote vya kuwa bibi-arusi kamili wa Kristo, na sio suria.
Kama tunavyoijua ile habari ya wanawali 10 katika Mathayo 25. Ni habari ambayo inatupa picha halisi ya kitakachotokea muda mfupi kabla ya Yesu kurudi, ambapo tunaona 5 wao walikuwa werevu na 5 wao walikuwa wapumbavu, Lakini wote hawa walikuwa wanadai wanamngojea Bwana wao aje waende karamuni, mfano tu makundi yaliyochanganyikana ya wakristo leo kanisani, kila mtu anadai anamngojea Bwana, hata Yule mzinzi kanisani naye pia madai yake ni hayo hayo.. Lakini tunasoma wale werevu walikuwa wamejiandaa kwa kila kitu, mpaka na mafuta ya ziada katika chupa zao, lakini wale wengine hiyo kwao haikuwa na umuhimu hata kidogo, japokuwa walijua kuwa taa zao hazitadumu, lakini hawakulizingatia hilo, waliendelea kubahatisha hivyo hivyo tu, wakidhani maadamu wameshafika mahali pa kumsubiria Bwana basi hiyo inatosha..Lakini kilichotokea ni kwamba, ghafla tu usiku wa manane, pakawa na kelele..
Wote wakashtuka kuna nini? Wakaambiwa Bwana wao anakuja,..wale werevu wakawasha taa zao, lakini wale wengine ndio wakaanza mchakato wa kuzichochea taa zao, wakawa wanaona zinazima, wakaanza kuwaomba wenzao wawapunguzie kidogo, Lakini hilo halikuwezekana ikabidi wakajinunulie ya kwao (kwasababu Roho Mtakatifu hatolewi kwa mwanadamu bali kwa Mungu..Na waliporudi wakakuta mlango umeshafungwa..
Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi”.
Ni jambo gani nataka tuone hapo; kabla mlango haujafungwa, palitangulia kwanza na sauti za kelele ili kuwaamsha wote..Yaani maana yake ni kuwa wote walipewa muda mfupi sana wa neema kutengeneza mambo yao kabla Bwana hajawasili.. Lakini muda huo haukuwa si muda wa kwenda tena kununua mafuta, ulikuwa ni muda wa kuwasha tu taa.
Ndivyo ilivyo katika siku hizi za mwisho,.Tunapozidi kuukaribia ule mwisho, wakati wa unyakuo, kabla parapanda haijalia, kutatangulia kwanza sauti za kelele, sauti hizo zitakuwa ni mahubiri maalumu ambayo yatahubiriwa katika ulimwengu mzima, hayo ni mahususi kwa ajili ya kuwaweka tayari watakatifu wote waliomwamini Yesu kwa ajili ya tukio la unyakuo ambalo linakwenda kutokea ndani ya kipindi kifupi sana.
Lakini wakati huo ukifika, na wewe ulikuwa hauuthamini wokovu wako, ulikuwa unaishi hoe hae tu, vuguvugu, mguu mmoja nje, mwingine ndani..usidhani siku hiyo itakuwa ni ngumu kuivuka.. Hata iweje, Ni kweli utajua kabisa Unyakuo umefika, na utaanza michakato ya kuyatengeneza mambo yako kwa Mungu, lakini hilo halitakamilika, ghafla tu utashangaa wenzako uliokuwa unashiriki nao kanisani hawapo ndipo utakapokuwa katika kilio cha kusaga meno.
Wokovu ni maandalizi..Kwenda katika unyakuo, ni kukamiliza vigezo vyote, sio kusema tu nimeokoka, halafu basi, wale wanawali wapumbavu nao pia walikuwa wameokoka, lakini kumbuka kwa Mungu hatufiki kwenye muda wenyewe tuliopangiwa, hapana bali tunafikia ndani ya Muda….Kwa mfano mtu akikuambia tuonane saa 8 kamili..na wewe ukafika pale muda huo huo wa saa 8, hapo ni sawa na umefika kwenye muda wenyewe..Lakini ukifika saa 7 na nusu, hapo umefika ndani ya muda, na ndio Mungu anachotaka kwetu.. Kwa Mungu ukifika saa 8 umeshachelewa..
Kwasababu, kabla haujamfikia huwa kunakuwa na maandalizi rasmi. Na ndio maana hata ukisafiri huwa unawekewa kabisa muda wa kuwasili(reporting time) na Muda wa kuondoka(departing time), Kama ukisema mimi nitafika ule muda wa kuondoka..Ujue tayari umeshachelewa, kwasababu zipo hatua za kufuata ambapo mpaka ukamilishe zote, tayari ule muda wa kuondoka utakuwa umeshapita..
Hivyo, katika hichi kipindi cha mwisho, wewe kama mkristo unaishi ukristo wa kubahatisha, ule wa kusema tu mimi nimeokoka, halafu, hakuna mabadiliko katika maisha yako, siku zinakwenda siku zinarudi haujiweki sawa kwa ajili ya kurudi kwa pili kwa Kristo. Ndugu yangu nataka nikuambie, Unyakuo utakupita, mbele ya macho yako hivi hivi ukiona ikiwa wakati huo utakuwa hai. Na kama utakuwa umekufa hutafufuliwa, kuungana na walio hai kwenda mbinguni.
Huu wakati wa mwisho ni wa ajabu kwasababu biblia inatoa maelezo kuwa kutakuwa na makundi mawili ya wakristo wakristo wanaomngojea Bwana, na sio kundi moja kama inavyopaswa iwe, ndio hao wanawali werevu na wapumbavu. Sasa swali la kujiuliza mimi na wewe je! tupo katika kundi lipi?
Sio kila staili unayoiona kwa watu Fulani wanaoitwa wakristo ni ya kuiiga..
Sio kila maisha unayoona anaishi mtu Fulani anayejiita mkristo ni ya kuyaiga.
Sio kila mahubiri na mafundisho ni ya kuyasikiliza, ni lazima uyachuje.
Sio kila sauti inayosema ndani yako ni ya kuifuata.
Huu ni wakati wa kuitengeneza taa yako wewe mwenyewe binafsi, na kuwa na uhakika kuwa hata leo mambo ya kibadilika ghafla ninaweza kwenda kumlaki Bwana mawinguni.
2Wakorintho 13:5 “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa”.
Naamini sisi sote tutaanza kuishi kama wanawali werevu. Na Bwana atusaidie.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. Ni neema za Mungu tumeiona siku nyingine, hivyo nakukaribisha katika kuyatafakari maandiko, ambayo ndio chakula cha roho zetu.
Watu wengi tumekuwa tukitafuta msaada kutoka kwa Mungu wetu, jambo ambalo ni zuri sana, kwasababu hakuna pengine popote ambapo tunaweza kupata msaada, shetani kazi yake ni kutuharibu na si kutupa msaada.
Hivyo basi zipo njia nyingi za kupata msaada kutoka kwa Mungu katika jambo lolote lile unalopitia au unalohitaji.
Njia ya kwanza na ya Muhimu kuliko zote, ni wewe binafsi kupiga magoti na kumwomba Mungu. Kama Maovu na dhambi zote zinazoendelea leo ulimwenguni zinamfikia Mungu, si Zaidi maombi yetu!. Mungu wetu anasikia hata sauti ya mapigo ya mioyo yetu, kila sekunde yanapodunda, hata ile sauti ya jogoo anayewika alfajiri inamfikia, Si zaidi sana maneno yanayotoka katika vinywa vyetu.
Kwahiyo njia ya kwanza na bora ni ile ya kupiga magoti binafsi na kumwomba Mungu hitaji la moyo wako huku ukiamini kwamba anakusikia na atakifanya hicho ulichomwomba kikiwa ni sawasawa na mapenzi yake.
Njia ya Pili, ambayo ndio kiini cha Somo letu, ni ile ya KUWATUMIA WATUMISHI WA MUNGU.
Njia hii sio bora kuliko hiyo ya kwanza lakini ni Njia halali, ambayo imehalalishwa na Mungu mwenyewe. Upatapo shida, au upitiapo jambo lolote..watafute watumishi wa Mungu wa ukweli. Hao Bwana amewapa neema ambayo huwezi kuipata mahali pengine. Watakapokuombea au kukushauri ni rahisi kupata majibu au matokeo yaliyo sahihi kabisa.
Ipo mistari mingi kujifunza juu ya neema waliyopewa watumishi wa Mungu, lakini leo napenda tujifunze mistari ifuatayo ili tupate kuelewa Zaidi.
Marko 6:34 “Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa;
36 uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula.
37 Akajibu, akawaambia, WAPENI NINYI CHAKULA. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula?
38 Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili.
39 Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi.
40 Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini.
41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, AKAWAPA WANAFUNZI WAKE WAWAANDIKIE; na wale samaki wawili akawagawia wote.
42 Wakala wote wakashiba.
43 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia.
44 Na walioila ile mikate wapata elfu tano wanaume”.
Katika mistari hiyo kuna mambo kadhaa nataka tujifunze.
Jambo la kwanza Bwana aliwahurumia makutano lakini hakuwapa yeye ile mikate. Badala yake aliwaambia wanafunzi Ndio wawape wao chakula (soma mstari wa 37).
Jambo la Pili, ni kwamba muujiza ule haukufanyika mkononi mwa Bwana, bali mikononi mwa Wanafunzi wake. Utaona kuwa Bwana alishukuru kisha akaimega ile mikate mitano na samaki wawili na kuwapa wanafunzi… Na wala hakuimega mikate elfu tano na kuwapa wanafunzi. Hapana! Maana yake ni kwamba miujiza ilitendeka mikononi mwa wanafunzi na si mkononi mwa Bwana Yesu. Hivyo likatimia neno Bwana alilowaambia “wapeni nyinyi chakula”, na wanafunzi wakawapa chakula.
Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba muujiza ule ulifanywa na Bwana Yesu, kwa kupitia mikono ya mitume wake (watumishi wake). Bwana hakushindwa kufanya yeye, lakini ndivyo ilivyompendeza yeye kuwatumia watumishi wake kutimiza kusudi lake la kuwahudumia watu wake wenye kuhitaji msaada.
Hivyo upatapo tatizo, na hujui pa kuanzia msaada wa kwanza piga magoti mwombe Mungu binafsi, na kama bado unaona una mashaka mashaka, au bado kuna mambo unaona bado hayajakaa sawa..basi watafute watumishi wa Mungu wa kweli…watakusaidia, kwasababu Bwana anafanya kazi kupitia wao. Na Mungu anao watumishi wake karibia kila mahali, kwasababu anajua watu wake wengi wanahitaji msaada.
Kama unahitaji ushauri wa kimaisha, wa kiroho, au una ugonjwa, au jambo lolote lile, mtafute mchungaji wako, au askofu, mweleze usimfiche kwasababu tatizo unalodhani wewe peke yako ndio wa kwanza unalipitia, kumbe hujui kuna wengi waliotangulia kuwa nalo na likatatulika..hivyo usikubali shetani akutengenezee hofu, na kusema haiwezekani..Chukua hatua kawatafute, na jaribu kueleza kwa kina, kama unavyomweleza daktari unapokwenda hospitali..Ukifanya hivyo ni rahisi kupata msaada kwa haraka sawasawa tu na kama Kristo mwenyewe angekuwepo hapo kukuhudumia…
Na pia nakushauri!..Usiende mikono mitupu!..na wala usiende na saikolojia kwamba anahitaji fedha yako..nenda kama vile unaenda kukutana na Kristo, na kwamba huwezi kuondoka bila kuacha chochote cha kumshukuru Mungu. Ukifanya hivyo utaona matokeo makubwa sana.
Na pia kama wewe ni mtumishi wa Mungu wa kweli, utawahurumia wenye matatizo kama hawa wanafunzi walivyofanya, hata kufikia kupeleka hoja zao mbele ya Kristo. Wanafunzi wa Yesu, hawakuona fursa ya fedha bali waliona matatizo ya watu.. Ingawa walijua wale watu walikuwa na fedha zao mifukono mwao, ndio maana walimwambia Bwana awape ruhusua wakajinunulie chakula, hilo neno kujinunulia linaonyesha kabisa kwamba wale watu ingawa walikuwa na matatizo lakini walikuwa na fedha mifukoni mwao!..
Lakini mitume walihurumia matatizo yao na hawakutamani fedha zao. Na nani ajuaye pengine baada ya kupokea ile miujiza ya kula mikate na kushiba, zile fedha walizokuwa nazo walizitoa pale kama sadaka!!!..pengine walitoa kwasababu katika hali ya kawaida hakuna mtu ambaye anaweza kuponywa na kufanyiwa kitu cha kimiujiza na asiguswe kabisa kutoa chochote.
Na pia tunajifunza kitu kingine kuwa wanafunzi waliwaketisha watu kwa SAFU, watu hamsini na sehemu nyingine watu mia. Pengine yalitengwa makundi ya wanawake na wanaume kivyao, hali kadhalika ya wazee kivyao na Watoto kivyao..hawakuchanganywa wote kwa Pamoja.
Hiyo ni kutufundisha watumishi kuwa ni lazima katika kuwahudumia watu Utaratibu uwepo.. Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, mahali pasipo na utaratibu basi Mungu hafanyi kazi. Na utaratibu ni Pamoja na kuwaheshimu watu, kujua jinsi gani ya kushughulika na marika..Huwezi kumhudumia mzee kama unavyomhudumia mtoto, huwezi kuzungumza na mzee kama unavyozungumza na kijana. Hekima na heshima lazima viwepo, ndipo Bwana ataachilia miujiza yake.
1Wakorintho 14: 40 “ Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu”
Hivyo ni kwa njia gani utapata msaada kutoka kwa Mungu? Ni kwa kuwatumia pia watumishi wa Mungu, na sio tu msaada wa kimwili, bali pia msaada wa kiroho ambao ni Neno la Mungu.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
UNAZO KILA SABABU ZA KUMSHUKURU MUNGU
Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Maana yake nini?
Mafuta yanayozungumziwa kwenye Yakobo 5:14, ni mafuta gani?
Nyamafu ni nini?
HUDUMA YA WALE MASHAHIDI WAWILI.
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
Nyamafu ni nini?