Mapepo ni nini?
Mapepo ni Malaika walioasi zamani ambao hawakuilinda enzi yao mbinguni. (Yuda 1:6)
Na shetani mwenyewe akiwa kama pepo mkuu.
Sasa walipoasi ndipo wakatupwa duniani, na hiyo ilikuwa kabla hata ya mwanadamu kuumbwa. Wote walikuwa wameshatupwa huku duniani wakisubiria hukumu yao ya mwisho.
Lakini mwanadamu alipoumbwa, na shetani akafanikiwa kumdanganya pale Edeni ndipo yeye na mapepo yake yote wakapata uhali wa mambo mengi ulimwenguni,
Haya mapepo yakaanza kuwaingia watu jambo ambalo lilikuwa haliwezekani hata kidogo, yakashikilia mambo mengi, na kufanikiwa kuharibu, kwa ufupi yalikuwa na uwezo wa kujiamulia kufanya chochote, yakiongozwa na kiongozi wao mkuu shetani
Mpaka ilipofikia kipindi cha Yesu Kristo kuja duniani, hapo ndipo yalinyang’anywa sehemu kubwa ya mamlaka waliyokuwa nayo, waliyoyaiba kwa Adamu, Yesu ndio akayachukua yakawa ya kwake.
Ufunuo 1:17 “…………Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu”.
Hivyo mapepo yaliyopo duniani leo hii hayana nguvu tena juu ya mtu ikiwa tu, atakuwa ndani ya Kristo basi..Kwasababu yeye ndio aliyepewa mamlaka yote ya mbinguni na duniani kwa sasa (Mathayo 28:28)..
Zamani shetani alikuwa na uwezo hata, wa kuwaendea hata wafu na kuzungumza nao, utaona hilo katika kipindi cha Samweli jinsi Yule mwanamke mchawi alivyompandisha Samweli juu kuzungumza na Mfalme Sauli. Lakini sasahivi wafu wote wanamilikiwa na Yesu Kristo, kiasi kwamba ukifa leo, shetani hawezi kukufikia huko ulipo kwa namna yoyote ile.
Mapepo ni nini
Hivyo fahamu tu, ikiwa upo nje ya Kristo, kwa namna moja au nyingine, mapepo yatakusumbua tu, na lengo lao si lingine zaidi ya kukuua na kukupeleka kuzimu.. Ili kufahamu ubaya wa mapepo, fungua hapa usome >> Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?
Hivyo usijidanganye na kusema mimi siwezi kuwa na mapepo kisa tu hayajawahi kulipuka ndani yangu..Ndugu fahamu kuwa si mapepo yote ni ya kulipuka kama unavyodhani..
Hivyo ikiwa wewe upo nje, kwa namna moja au nyingine ipo roho ya ibilisi imejishikamanisha na wewe hata pasipo wewe kujijua. Njia pekee ya kuyaondoa ndani yako ni kumpa tu YESU KRISTO maisha yako. Ukishamwamini na ukatubu na ukabatizwa, basi maroho hayo yanaondoka ndani yako..Na wakati huo huo ROHO MTAKATIFU anaingia ndani yako. Hapo ndipo utakapojua tofauti yako ya wewe ni jana.
Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”.
Naamini mpaka hapo umeshafahamu kwa ufupi mapepo ni nini.
Usisahau kuwa hizi ni siku za mwisho, Na Yesu yupo mlangoni kurudi, na shetani naye analijua hilo vizuri, hivyo utendaji wake kazi sasa sio kama ule wa zamani, mapepo/majini yanatenda kazi kwa nguvu kuliko pale mwanzo. Hivyo nawe pia unaposikia habari za wokovu usikawie kawie kwasababu, shetani naye yupo karibu yako kuindoa hii mbegu iliyopandwa ndani yako.
Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu’.
Shalom.
Mada Nyinginezo:
MAJESHI YA PEPO WABAYA.
Kuna Malaika wangapi?
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?
JIHADHARI NA UPOTEVU ULIOACHIWA SASA.
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
UHARIBIFU WA MTU.
Ndio kwa kupigwa kwake sisi tumepona!!
Tunao ujasiri wote wa kusema hivyo, kwasababu kuacha kwake enzi na mamlaka mbinguni, kisha kuja kuishi maisha ya taabu na mateso hapa duniani, kuanzia kuzaliwa katika zizi la ng’ombe, Kisha kuishi maisha ya umaskini tangu utoto wake hadi utu uzima,(japokuwa alikuwa ni tajiri)
1Wakorintho 8:9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”.
Hakuwa hata na mahali pa kulaza kichwa chake, hata mbweha na ndege walimshinda, hiyo yote ni kwa ajili yangu mimi.
alijaribiwa zaidi yetu sisi, bila kutenda dhambi yoyote, alifunga na kukesha kwa kuomba kwa ajili yangu, na kama hiyo haitoshi, ilimgharimu kuingia matesoni ateswe na ibilisi, atemewe mate, apigwe mijeledi, agongelewe misumari, adhihakiwe, achomwe mkuki, halafu mimi nisiponywe roho yangu hilo litakuwa ni jambo lisiloingia akilini.
Kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Ni haki yako wewe na mimi kuupokea uponyaji wa roho zetu kwanza, na hiyo inakuja kwanza kwa kutubu dhambi zetu , kwa kudhamiria kutubu kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu na tama zake, kisha ndio anakuja ndani yetu na kutuokoa na kufanya makao na sisi. Na baada ya hapo atatuponya na miili yetu pia, kwasababu Kwa kupigwa kwake sisi tumepona, roho zetu na miili yetu pia.
Hivyo kabla sijakwenda kukuombe tatizo lako, Ni vema kwanza ukamkaribisha Bwana Yesu katika maisha yako. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo basi unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Na Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu wako. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako(sawasawa na Matendo 2:38).
Sasa ikiwa wewe Ni mgonjwa, Kumbuka Bwana Yesu haponyi tu roho, anaponya pia miili yetu..mimi ninayekuandikia huu ujumbe ni shahidi alishaniponya mara nyingi, kwa kufuatisha maombi kama haya ninayokuombea vilevile atakuponya na wewe leo. Kwasababu Yesu ni yeye Yule.
Unachopaswa kufanya hapo ulipo..Weka mkono mahali unapoumwa, kisha.
Sema maneno haya kwa sauti.
EWE UGONJWA (UTAJE UGONJWA UNAO KUSUMBUA), MIMI NI MILKI HALALI YA MKUU WA UZIMA YESU KRISTO. NAKUAMURU KWA JINA LA YESU ONDOKA NDANI YANGU KUANZIA HUU WAKATI NA MILELE, KWA KUPIGA KWAKE SISI TUMEPONA. HAKUPIGWA BURE, HAKUDHARAULIWA BURE, HAKUTESWA BURE..BALI HIYO YOTE ILIKUWA NI MIMI NIUPOKEE UPONYAJI KAMILI WA ROHO YANGU NA MWILI WANGU. HIVYO ONDOKA NDANI YANGU SASA KWA JINA LA YESU KRISTO.
EE BWANA YESU, MWOKOZI WANGU, INGIA SASA NDANI YA MWILI WANGU, UNIRUDISHIE AFYA ULIYONIAHIDIA.
ASANTE KWA UPENDO WAKO.
JINA LAKO LIBARIKIWE DAIMA.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha maombi hayo mafupi, basi kuwa na uhakika kuwa Kristo ameshakuponya tayari, ikiwa ulikuwa huwezi kufanya jambo Fulani anza kulifanya, ikiwa ni ugonjwa wa kwenye damu, nenda kapime, ikiwa ni wa viungo vyovyote vile Kristo ameshakuponya.
Hivyo usiache kwenda kushuhudia na kumpa yeye utukufu.
Bwana akubariki sana.
“Ndio Kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Mada Nyinginezo:
YESU MPONYAJI.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.
RABI, UNAKAA WAPI?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Ukisoma kitabu cha Warumi sura ya 9, ya 10, na ya 11..utaona mambo mazito sana mtume Paulo aliyokuwa akiyazungumza juu ya ndugu zake wayahudi. Akieleza jinsi neema ya Mungu ilivyoondolewa kwao, kiasi kwamba hata wangehubiriwa vipi injili wasingeweza kuipokea.
Chukua muda kwa wakati wako, pitia sura hizo kwa utulivu sana, ukisoma juu juu hutaona chochote, lakini ukisoma kwa utulivu huku ukimwomba Roho Mtakatifu akusaidie, nakuambia hutaichezea hata kidogo hii neema tuliyopewa sisi watu wa mataifa.
Mtume Paulo alipewa kulijua hilo mpaka akawa anasema, anayo huzuni nyingi, na maumivu yasiyokoma moyoni mwake kwa ajili ya ndugu zake (yaani wayahudi), maumivu ya kila siku, akijua kuwa wokovu umeondolewa kwao..
Kiasi kwamba alitamani hata kama ingewezekana yeye mwenyewe aupoteze wokovu wake, atengwe na Kristo ili kusudi kwamba ndugu zake wote wapone, basi angefanya hivyo..soma..
Warumi 9:1 “Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu,
2 ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.
3 Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe NIHARIMISHWE NA KUTENGWA NA KRISTO kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili”;
Kauli hiyo si rahisi kuizungumza, lakini kwa huruma ya watu wengine, na huzuni unayoisikia moyoni mwako inakulazimu uitamke, si kwamba unatamani iwe hivyo, lakini kama ingewezekana.. Ni sawa leo umuone mtoto wako mchanga, kapata ajali halafu kakatika mikono, halafu anatapata tapa pale chini kwa maumivu,akilia, ni wazi kuwa utatamani ungeyapitia wewe yale maumivu yake..Kuliko kumuona anaendelea kuteseka katika ile hali.
Ndivyo ilivyokuwa kwa mtume Paulo, alitamani kama ingekuwa inawezekana yeye kuharamishwa, (kufanywa kuwa mwana-haramu,atengwe na Kristo) kusudi kwamba ndugu zake wayahudi waiamini Injili waokolewe.. Lakini ilikuwa haiwezekani.
Ndugu kama hufahamu wakati ule wa kanisa la kwanza ni wayahudi wachache sana, waliiamini Injili, japokuwa ilikuwa ni mamilioni waliokuwa wanaisikia, na ndio maana ukisoma mbele kidogo mtume Paulo anasema.
Warumi 9.27 “..Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa”
Waliokolewa wachache sana, mpaka akasema, kama Mungu asingewaachia mabaki basi wangefananishwa na Sodoma na Gomora,(yaani akiwa na maana asingeokoka myahudi hata mmoja wakati wao)..
Na hiyo yote ilikuwa ni kwasababu waliikataa neema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo, alipokuwa duniani, na kuendelea na njia zao za kumtafuta Mungu, huku wamemweka Kristo pembeni. Ikapelekea mlango wa neema kufungwa juu yao. Na ndio maana utaona haijalishi walikuwa na bidii kiasi gani kwa Mungu lakini hawakuweza kuuona mlango wa neema hata kidogo kwasababu tu walimkataa Kristo (kasome Luka 13:34-35). Mtume Paulo alisema hivyo katika ile sura ya 10
Warumi 10:1 “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa”.
Hilo jambo linaendelea mpaka sasa, takribani miaka 2000 imepita, lakini bado mlango wa neema haujafunuliwa kwao. Na hiyo yote ni ili mimi na wewe (watu wa mataifa), tuipokee neema.
Lakini mwisho kabisa mtume Paulo alipewa siri na Mungu, na siri hiyo aliiweka wazi akataka sisi nasi tuijue (yaani mimi na wewe), kwamba utafika wakati ambao Mungu atawarehemu tena..Na kikisha fika hicho kipindi basi sisi tufahamu Habari yote ndio imeishia hapo, kama mtu yeyote wa mataifa atakuwa hajaingia ndani ya Kristo, ndio basi tena..Soma
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake”.
Jiulize wayahudi kwa miaka 2000 wanautafuta uso wa Mungu lakini hawaupati, unadhani siku hiyo neema ikiondolewa kwetu, sisi tutaipatia wapi? Na dalili zote zinaonyesha wakati wao upo karibuni sana…Tayari taifa hili lilishachipuka tangu mwaka 1948, unadhani ni nini kinachosubiriwa hawa watu Mungu asiwageukie? Usiku na mchana wapo pale kwenye “ukuta wa maombolezo wa Nehemia” wanamlilia Mungu awaokoe (hayo yalikuwa ni majonzi ya mtume Paulo)..Lakini Bwana anakawia kidogo kwa ajili yangu mimi na wewe.
Moja ya hizi siku, Mungu atakisikia kilio chao,.mlango wa neema utafunguliwa kwao, na kwetu utafungwa,. Huo ndio ule wakati wa mwenye nyumba kusimama na kuufunga mlango, na watu watakuwa wakisimama nje na kugonga wafunguliwe lakini Bwana atawaambia siwajui mtokako.(Luka 13:25-28)…Duniani kutakuwa na kilio na kusaga meno.
Hivyo tunaposikia maneno haya, tujitathimini Je! Ni kweli bado tupo ndani ya Kristo? Au tupo vuguvugu. Kama wewe unaisikia injili na bado unasua sua basi uingie sasa kwa nia yote acha kusitasita kwenye mawazo mawili muda unazidi kwenda, kwasababu siku hizi ni za mwisho. Lango hili likishafungwa, halitafunguliwa kamwe.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Msamaria mwema ni mtu wa nanma gani?
Ni kauli ambayo tunaisikia katika jamii yetu mara kwa mara. Na hiyo inatokea pale mtu mfano amekumbana na matatizo au shida Fulani halafu akakutana na mtu asiyemfahamu kisha akamsaidia kutatua tatizo hilo. Sasa mtu kama huyo baadaye akija kuulizwa ilikuwaje ukafanikiwa au ukafanikisha kitu kile katika yale mazingira? ..Ndio hapo utamsikia anasema nilikutana na msamaria mwema akanisaidia…
Lakini baadhi ya watu hawajui chanzo cha msamaria mwema ni nini?..
Habari yake tunaipata kutoka katika biblia, tusome,
Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?
30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.
31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
33 Lakini, MSAMARIA MMOJA katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo”.
Ni yapi tunajifunza katika Habari ya msamaria mwema?
Sasa ukizingatia hayo, Basi mbele za Mungu utakuwa umekidhi vigezo vya kumpenda jirani yako kama nafsi yako.. Hapo utakuwa umeshida amri ya pili iliyo kuu kuliko zote, kama yule msamaria mwema.
Kumbuka tendo hilo lina thawabu kubwa sana mbele za Mungu.
Hivyo ni wajibu wetu sote, kulikumbuka hilo wakati wote tunapoishi humu duniani, ili na sisi Mungu atuhurumie siku ile tuurithi uzima wa milele..
Mada Nyinginezo:
JIRANI YANGU NI NANI?
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.
MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UNYAKUO.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
Adam na eva akina nani?
Hawa ni wazazi wetu wa kwanza.
Biblia inasema
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.
Lakini kama tunavyojua waliasi, na ndio hapo ikawa chanzo cha matatizo ambayo ndio mpaka leo mimi na wewe yanatuathiri.
Hawa alidanganywa na nyoka kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, Kumbuka “alidanganywa” wala hakushawishiwa, hii ikiwa na maana kuwa hakujua kuwa kitendo anachokwenda kukifanya kingekwenda kuleta madhara yoyote kwa mtu kwa udanganyifu alioambiwa na nyoka, kwasababu alidanganywa kuwa hatakufa, bali kinyume chake atafumbuliwa macho, atakuwa kama Mungu, akijua mema na mabaya.
1Timotheo 2:13 “Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa”.
Lakini siku ile alipojaribu kujitetea kwa kumrushia nyoka mpira, hilo halikusaidia yeye kutoshiriki adhabu.
Vivyo hivyo na sasa, Udanganyifu mwingi umetokea leo hii duniani.. Lakini ni wajibu wako wewe kuujua ukweli na kuushika, kwasababu siku ile hautakuwa na la kujitetea na kusema, mimi mbona sikujua hili, au mimi mbona niliambiwa vinginevyo na watu wanaojiita watumishi wa Mungu.
Kumbuka si watu wote wanaojiita watumishi wa Mungu ni watumishi kweli wa Mungu,, Mtumishi wa Mungu ni lazima akufundishe kweli ya biblia, na kukuongozwa kwa Kristo na sio kwenye mambo ya ulimwengu huu.
Tusidanganywe kama Adam na Eva.
Ndio maana wakati huu wa machafuko mengi ya rohoni, ni vizuri ukawa na Kristo moyoni mwako, na kujifunza Neno la Mungu kwa bidii, ili likae ndani yako ibilisi asikushinde. Kwasababu kama Neno la Mungu halipo ndani yako kwa wingi, kamwe huwezi kuzishinda njama za mwovu,
Utakumbuka kilichomtokea Bwana Yesu kule jangwani, shetani alipomjia na maandiko na yeye alimjibu kimaandiko. Sasa huyo ni mwokozi wa ulimwengu yamemkuta. Itakuwaje mimi na wewe?
Tung’ang’anie NENO LA MUNGU. Maana hilo ndio silaha yetu nyakati hizi za mwisho dhidi ya mwovu shetani, ili tusiwe kama Adam na Eva.
Mada Nyinginezo:
UUMBAJI BORA WA MUNGU, UPO NDANI YA MWANADAMU.
MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.
JINA LA MUNGU NI LIPI?
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
VUKA UJE MAKEDONIA UTUSAIDIE.
UZAO WA NYOKA.
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
Je! biblia inasema nini juu ya wafiraji?
Ufiraji ni Neno linalojumisha kitecho chochote cha kumwingilia mwanadamu mwanzako kimapenzi kinyuma na maumbile.
Na ni dhambi biblia imesema hivyo na kwamba watu wote wanaofanya vitendo kama hivyo hawawezi kuurithi uzima wa milele.
1Wakoritho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala WAFIRAJI, WALA WALAWITI,
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”.
Watu wengi wanajidanganya na kudhani kuwa wakiwaingilia wake zao, maadamu tayari wapo nao katika ndoa, sio dhambi..Ndugu usidanganyike, tendo lolote la kumwingilia mtu mwingine kinyume na maumbile haijalishi ni rafiki, au jirani, au kahaba, au mke, hiyo tayari ni ufiraji.
Vinjari yetu, na chaguzi mbalimbali ili kukidhi kila ladha na bajeti, http://swisswatch.is/ replica watches inapatikana kwa kununua mtandaoni.Na wafiraji wote watahukumiwa.
Kilichosababisha Sodoma na Gomora viangamizwe, kilikuwa ni kitendo hichi cha ufiraji,
Yuda 1:7 “Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
8 Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu”.
Hivyo kama wewe ni mmojawapo tubu haraka sana, kwa kuacha kitendo hicho. Mgeukie Yesu Kristo ayaokoe maisha yako. Ikimbie hukumu ya Mungu. Ziwa la moto lipo kweli.
Jiepushe na utazamaji wa picha na video chafu za ngono zinazozagaa mitandaoni, watu wengi wanaingiliwa na hizi roho kwa kuzitazama tu. Utakuta hapo mwanzo, hakuwa hivyo lakini siku alipooanza kuzitazama tu, anaona kama, shinikizo fulani la nguvu linatoka ndani kumuhimiza kufanya hivyo.
Kama na wewe ni mmoja wapo basi, nakushauri, kaa mbali sana na mambo hayo, shetani anafahamu kuwa wakati wake ni mfupi aliobakiwa nao. Hivyo itazame sana mienendo yako.
Mada Nyinginezo:
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
SI KILA KIPENDEZACHO KINATOKA KWA BWANA.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Ulokole/ Walokole wametoka wapi?
JIBU: Kabla ya kwenda kujua maana ya ulokole, ni muhimu kujua kwanza maana ya neno ‘kanisa’..Tafsiri ya kwanza ya kanisa sio “jengo” bali ni “mkusanyiko wa watu waliomwamini Yesu”..Kwahiyo popote palipo na mkusanyiko wa watu waliomwamini Yesu, tayari hilo ni kanisa hata kama hakuna jengo. Soma mistari ifuatayo itakusaidia Matendo 2:47,1Wakorintho 1:2,14:5,14:23,15:9,16:19 n.k
Na kanisa la Kristo ni moja tu duniani kote ambalo linajulikana kama Bibi-arusi wa Kristo…Hilo ndio linajumuisha wakristo wote waliomwamini Yesu na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake (kumbuka hapa hatuzungumzii madhehebu), bali kanisa la Kristo moja ambalo pia sio jengo, bali watu wote duniani waliomwamini Yesu. Na watu hawa ambao ndio kanisa la Kristo, ndio watakaokuja kunyakuliwa siku ya parapanda katika tukio lijulikanalo kama UNYAKUO WA KANISA. Unaitwa unyakuo wa kanisa na si makanisa…kwasababu kanisa la Kristo ni moja tu.
Lakini sasa Kanisa la Kristo ni kweli ni moja lakini lina washirika wengi, na haliwezi lote kukusanyika pamoja na kwa wakati mmoja kufanya ibada, au kumwabudu Mungu, kama ni hivyo basi halina budi kuwepo na makusanyiko tofauti madogo madogo katika kila eneo ili kukamilisha kusudi lile lile la kukusanyika pamoja…Ndio hapo wakristo waliopo Mkoa wa kilimanjaro watakusanyika kivyao, na waliopo Morogoro watakusanyika kivyao huko waliko, n.k..
Lakini kumbuka Imani ni moja, na Kristo ni yule yule anayeabudiwa kote, utendaji kazi unaweza ukawa unatofautiana kulingana na kanisa na kanisa, lakini Imani ni sharti iwe ile ile moja, Bwana mmoja, Roho Mmoja, Ubatizo mmoja sawasawa na (Waefeso 4:3-7), tofauti na hapo hilo ni jambo lingine.
Sasa katika mkoa huo huo wa Morogoro pia sio wakristo wote wapo Morogoro mjini, kuna wengine wapo vijiji vya ndani huko…hao nao hawana budi wakusanyike huko walipo, hakuna sababu ya kusafiri mpaka mjini….na huko vijijini pia kuna uwezekano wa watu wasiwe karibu karibu…hivyo tena yatazaliwa makundi mengine madogo madogo mengi kulingana na mahali, hata inaweza kufikia kanisa likawa na watu watano..lakini yote yenye imani moja. Umbali ndio unaosababisha yajigawanye hivyo.
Sasa haya makanisa mengi madogo madogo ambayo yanakuwa katika eneo husika kwa kiingereza yanajulikana kama LOCAL CHURCHES, (Yaani kanisa la eneo husika aidha mtaa, au kijiji).
Na makanisa haya zamani, kutokana na uchache wa watu yaliyonayo na maeneo yalipo mengi yaliishia kudharaulika… na asilimia kubwa ya washirika wake ni maskini…kwasababu wengi wanaoishi vijijini au katika miji midogo midogo si matajiri kulinganishwa na wale wanaoishi mijini. Hivyo walidharaulika lakini kama biblia inavyosema kuwa..
Yakobo 2:5 “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao”
Hivyo hao waliodharaulika na kujulikana kama “Local churches”… ndio waliokuwa wa kiroho zaidi..Ishara nyingi na miujiza mingi ilifuatana na haya makanisa madogo madogo, kuliko hayo makubwa, …ndio watu waliokuwa na bidii zaidi ya kumtafuta Mungu, na ndio waliokuwa wanamheshimu zaidi Mungu.
Sasa kutokana na makanisa hayo madogo madogo kufahamika kama local churches…na washirika wao ndio wakajulikana kama “local people”..na kwa lugha yetu hii wakatafsiriwa kama (wa-locally) au WALOKOLE.
Hivyo kama mtu utaitwa mshamba kwa sababu unamwamini Yesu na kuzishika amri zake basi hiyo ni THAWABU. Kuliko kama utaitwa mwenye Elimu na wa-kisasa na huku umemwacha Kristo.
Ufunuo 3:17 “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona”
Usijisifie ukubwa wa kanisa unaloabudu, wala wingi wa watu wa kanisani kwenu…Jisifie Yesu uliye naye maishani mwako hata kama upo kanisa la watu watano..jitathmini je! unazishika amri zake hapo ulipo?, je! unaishi kulingana na neno lake? Kiasi kwamba hata parapanda ikilia utakwenda naye!..Je hapa nilipo nanufaika roho yangu kiasi gani?..kama sinufaiki rohoni ni heri nikatafute wenzangu wenye Imani ya kweli hata kama ni wachache, ninusuru roho yangu..kuliko kuendelea kwenye umati wa watu wengi na kuipoteza nafsi yangu…
Ni heri nijulikane mlokole lakini naenda mbinguni kuliko kukubalika na kila mtu, mwisho wa siku naishia kwenda jehanamu. Na kama pia hapo ulipo penye watu wachache huoni dalili ya kuurithi uzima wa milele ni heri ukaenda kutafuta penye watu wengi ambao wanakwenda mbinguni..Lakini siku zote kumbuka mlango ni mwembamba na njia ile imesonga na ni wachache wanayoiona…na mlango ni mpana wa njia iendayo upotevuni na wengi wanauendea.
Bwana akubariki na Bwana atusaidie.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?
MIHURI SABA
Wafilisti ni watu gani.
YEREMIA
MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.
UNYAKUO.
Yapo maneno ambayo huwezi kuzungumza, isipokuwa kwanza unaelewa vizuri ni nini unazungumza vinginevyo unaweza kujiweka kwenye kitanzi mwenyewe na kuingia matatizoni..
Kuna wakati Bwana aliwaambia wale watu wanaoshindana naye maneno haya…
“Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi..”? (Yohana 8:46)
Maneno haya si mepesi kabisa, Kumbuka juu kidogo tu kwenye sura hiyo hiyo swali la namna hii hii aliwauliza wale watu waliomfumania yule mwanamke katika uzinzi, lakini majibu yake ni kuwa sio tu kutomtupia yule mwanamke mawe, bali pia waliona aibu kuendelea kubaki maeneo yale, kwa mtihani huo mgumu waliopewa.
Yohana 8:7 “Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao;
akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati”.
Unaona? Lakini hapa na yeye pia anajiweka katika hicho kitanzi na kuwauliza watu.. Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?
Jaribu kujiweka wewe katika hiyo nafasi ukiwa kama kijana wa miaka 33 ambaye tayari umeshapitia mambo mengi katika maisha, halafu unasimama katikati ya umati wa watu wanaoshindana na wewe, unawauliza ni nani kati yenu anayenishuhudia kuwa nina dhambi?
Je! Wewe unaweza kusema hayo maneno?(Mimi siwezi)..Ndugu zako wote wamesimama karibu nawe , marafiki zako wote uliowahi kuishi nao na kusoma nao, wote pia wamesimama karibu hapo, majirani zako nao wapo, wafanyakazi wenzako wanasimama hapo vilevile halafu unawauliza wote “Kati yenu ninyi ni nani anayenishuhudia kuwa nina dhambi”..
Ni nani alishawahi kuniona au kusikia nimemsengenya mtu, ni nani nilishawahi kumdanganya au alishawahi kunisikia nadanganya, ni wapi nilishawahi kutamani, ni wapi nilishawahi kumvunjia mtu heshima, au kumwonea wivu, au kumwekea kinyongo, au kuonyesha unafki, kumfokea, kumtukana? ..Kama yupo hapa asimame, au ajitokeze, asimeme wewe siku fulani nilikuona ukikwepa kodi kwenye ile biashara yenu ya useremala…
Lakini wote waliosimama pale, hakuonekana hata mmoja aliyekuwa na la kumshitaki Yesu..sio jambo rahisi kama tunavyofikiri,
Na ndio maana mahali pengine biblia inasema..
1Petro 2:22 “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.”
Ni Yesu peke yake, katika ulimwengu mzima, katika vizazi vyote, ambaye tangu amezaliwa mpaka anakufa, hakuwahi kutenda dhambi hata moja, japokuwa alipitia majaribu mazito ya dhambi kuliko hata sisi.
Ndugu yangu Kwa YESU pekee mimi nimetia nanga! Sijui kwako?, kwasababu hakuna mwingine kama yeye, huyu pekee ndio wa kumtumainia, ni huyu pekee ndio wa kumtegemea kutusaidia kushinda huu ulimwengu kama yeye alivyoshinda, ni huyu huyu pekee ndio atakayetuokoa tukimwamini. Mimi na wewe tukimfanya kuwa rafiki wa maisha yetu, jambo la kwanza na la ajabu ni kuwa anatusamehe dhambi zetu zote, halafu anatuhesabia haki bure pasipo matendo yetu kwa neema, kiasi kwamba mbele za Mungu tunaonekana kuwa tumestahili haki yote.
Kisha baada ya hapo anamtuma Roho wake Mtakatifu ndani yetu. Ambaye kazi yake ni kutupa sisi nguvu ya kuishinda dhambi kama yeye alivyoishinda, na kutuongoza katika kuijua kweli yote.
Hivyo kama bado hujaokoka, saa ya wokovu ni sasa, fanya haraka mkaribishe Yesu maishani mwako. Kama umezichoka dhambi kweli, kama hutaki nafsi yako ipotee, basi mkimbilie Yesu haraka maadamu muda upo, Lakini tukikataa kuyasikia maneno yake basi yeye naye atatuacha, na kutuona tu kama sio watu tuliochaguliwa na Baba yake soma..
8:46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu”.
Natumaini wewe leo utayasikia maneno yake.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
RABI, UNAKAA WAPI?
NENO HILI NI GUMU,NI NANI AWEZAYE KULISIKIA?
Yeshuruni ni nani katika biblia?
KUMBUKA, VIVUKO VYA YORDANI VINAKUNGOJA MBELENI.
NA MTU MMOJA AKAVUTA UPINDE KWA KUBAHATISHA, AKAMPIGA MFALME
UNYAKUO.
Ahadi za Mungu ni za kweli kabisa,.. Lakini tatizo kubwa linalotukabili sisi wanadamu ni kutokujua njia Mungu anazozitumia kutimiza ahadi zake.
Na hiyo inawafanya watu wengi waishie kukata tamaa pale anapoona mbona ahadi za Mungu zimechelewa, pengine nimemkosea Mungu, au Hanisikii..
Fahamu kuwa wakati wa Mungu kutimiza ahadi zake, sio lazima uwe ule wakati ulioupanga wewe Tena mara nyingi huwa anauchagua ule wakati ambao haufahau, wakati ambao mambo yote yanaokana yameharibika, mipango imevurugika, umeshachelewa, hapo ndipo Mungu anasimama ili kutimiza ahadi zake kwako.
Na hakupewa tu mtoto basi, bali na mwili wake pia ulirudishwa na kuwa kama wa kijana, yeye pamoja na mke wake Sara.
Lakini Ibrahimu katika kipindi chote hicho hapo katikati hakumkosea Mungu imani na ndio maana akaitwa baba wa Imani, tunasoma hilo katika..
Warumi 4:18 “Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki”.
Na hazikutimia akiwa nyumbani mwa Potifa hapana, bali zilitimia akiwa gerezani, mahali ambapo hapana tumaini lolote, la kuishi. Kwa kipindi karibu cha miaka 2 akiwa kule gerezani, siku moja isiyokuwa na jina Mungu alimtembelea na kumwinua, akatoka na kufanywa kuwa Waziri mkuu na makamu wa Raisi wa taifa kubwa lililokuwa lina nguvu kuliko yote ulimwenguni wakati ule (Misri).
Hivyo zipo ahadi za Mungu nyingi katika biblia ambazo tukianza kuzichambua hapa moja baada ya nyingine hatuwezi kumaliza zote..
Ahadi za Mungu kwa mkristo:
Hiyo ni kutupa tu hamasa mimi na wewe ambao pengine umesubiria ahadi za Mungu kwa muda mrefu sasa na bado hujaona matokeo yoyote. Unachopaswa kufanya ni kusubiri ndugu yangu, huku ukiendelea kumtumikia Mungu kwa moyo ule ule wa kwanza.
Unaweza ukawa ni mtumishi wa Mungu, na umejaribu kuacha kila kitu ili tu uifanye kazi yake..Nataka nikuambie endelea hivyo hivyo, upo wakati utafika ile hadi yake ya kuwa UTAPATA MARA MIA, itatimia juu yako, haijalishi ni miaka miwili tokea sasa, au 5 au 10 au 20, lakini fahamu kuwa ukiendelea kung’ang’ania njia yako bila kuiacha, utavuna ulichopanda.
Mungu atakulipa tu, mema, ukiwa hapa hapa duniani, na vyote ulivyovipoteza utarejeshewa vyote mara mia. (Marko 10:28-30) Hivyo endelea kumtumikia MUNGU.
Vilevile Bwana aliposema, usisimbukie maisha ule nini, unywe nini, avae nini, bali utafute kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine utazidishiwa. Basi fahamu kuwa ukijikita kuutafuta kwanza uso wa Mungu, na kutaka kumjua yeye, ni ahadi yake kuwa hatakuacha ufe njaa, bali atahakikisha kuwa anakuhudumia ili uendelee kuishi,..Kwasababu unautafuta ufalme wake..Hiyo ni kweli kabisa hawezi kudanganya.. Ahadi za Mungu ni thabiti.
Vivyo hivyo na ahadi nyingine yoyote aliyowahi kukuahidia , endelea tu kuingoja, wakati wake utafika tu,. Kikubwa usiuache wokovu wako na utakatifu wako kama wewe umeokoka.
Lakini kama hujaokoka, basi hakuna ahadi yoyote ya Mungu inayoweza kutimia juu yako. Hivyo unachopaswa kufanya ni kumpa Kristo maisha yako ili ayaokoe, kwani hizi ni siku za mwisho na Unyakuo upo karibu,..Moja ya hizi siku mabadiliko makubwa sana yatatokea duniani. Na dhiki kuu itaanza, hivyo mgeukie muumba wako kabla ya hizo za hatari hazijakufikia kwa ghafla.
Bwana akubariki.
Ahadi za Mungu ni Yakini.
Mada Nyinginezo:
KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
UNYAKUO.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Yeremia alikuwa ni nabii aliyezaliwa Israeli (Kwa asili alikuwa ni Myahudi)..na alitokea nyakati za mwisho mwisho kabisa, karibia na wakati wa Israeli kuchukuliwa mateka Babeli. Ni nabii aliyetabiri na kushuhudia kuteketezwa kwa mji wa Yerusalemu na watu kuchinjwa na baadhi kuchukuliwa mateka. Tafsiri ya jina lake ni “Yehova atapandisha au atanyanyua” .Unaweza kutazama tafsiri za baadhi ya majina hapa >>>Maana ya majina na tafsiri zake
Kama jina lake lilivyo, Yeremia alitabiri Israeli kunyanyuliwa tena na Mungu baada ya kushushwa chini..alisema..Bwana atawarudia tena watu wake baada ya kukaa ugenini miaka 70.
Yeremia 25:11 “Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.
12 Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema Bwana, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele”.
Yeremia tofauti na manabii wengine, yeye aliitwa na Mungu katika utumishi akiwa na umri mdogo na ni moja ya manabii waliopitia mateso mengi sana katika huduma zao, lakini Mungu hawaacha!..na Mungu alimtuma kwa mataifa mbali mbali…Manabii wengine wa Israeli kama Samweli, Ezekieli,Musa, Malaki na wengineo hawakutumwa kwa watu wa Mataifa, isipokuwa kwa watu wa jamii yao tu (yaani kwa wasraeli wenzao!). Yeremia na wengine wachache ndio pekee waliotumwa watoke nje ya mipaka ya Israeli kusema na watu wa Mataifa ya mbali.
Yeremia 1:4 “Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. ”
Mungu alimtuma Yeremia kwa mataifa mengi ulimwenguni, kuyatangazia hukumu…kwamba yote yatawekwa chini ya utawala mgumu wa Nebukadneza kama yasipotubu na kuacha njia zao mbaya…na mataifa hayo yote hayakuisikiliza sauti ya Yeremia nabii na yote kuishia kuwekwa chini ya mikono ya Nebukadneza (kasome Yeremia 25:15-28) ikianza na Yuda. (Na Yeremia aliifanya kazi hiyo ya Mungu kwa uaminifu mpaka alipokuwa mzee.)
Kwa maelezo ya urefu kuhusu Nabii huyu, vitabu alivyoandika, na huduma yake ilivyokuwa kwa mapana fungua hapa >> Vitabu vya Biblia (sehemu ya 7)
Wito wa Mungu hauna mipaka, Mungu anaweza kukuita na kukutuma katika umri mdogo kama Yeremia, na vile vile anaweza kukuita na kukutumia katika umri mkubwa, kama Elisha. Kwa wito wowote ule tutakaoitwa na Mungu, tunapaswa tuwe waaminifu.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo: