Ulokole ni nini? Na kwanini wakristo waliookoka wanaitwa walokole?

Ulokole ni nini? Na kwanini wakristo waliookoka wanaitwa walokole?

Ulokole/ Walokole wametoka wapi?


JIBU: Kabla ya kwenda kujua maana ya ulokole, ni muhimu kujua kwanza maana ya neno ‘kanisa’..Tafsiri ya kwanza ya kanisa sio “jengo” bali ni “mkusanyiko wa watu waliomwamini Yesu”..Kwahiyo popote palipo na mkusanyiko wa watu waliomwamini Yesu, tayari hilo ni kanisa hata kama hakuna jengo. Soma mistari ifuatayo itakusaidia Matendo 2:47,1Wakorintho 1:2,14:5,14:23,15:9,16:19 n.k

Na kanisa la Kristo ni moja tu duniani kote ambalo linajulikana kama Bibi-arusi wa Kristo…Hilo ndio linajumuisha wakristo wote waliomwamini Yesu na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake (kumbuka hapa hatuzungumzii madhehebu), bali kanisa la Kristo moja ambalo pia sio jengo, bali watu wote duniani waliomwamini Yesu. Na watu hawa ambao ndio kanisa la Kristo, ndio watakaokuja kunyakuliwa siku ya parapanda katika tukio lijulikanalo kama UNYAKUO WA KANISA. Unaitwa unyakuo wa kanisa na si makanisa…kwasababu kanisa la Kristo ni moja tu.

Lakini sasa Kanisa la Kristo ni kweli ni moja lakini lina washirika wengi, na haliwezi lote kukusanyika pamoja na kwa wakati mmoja kufanya ibada, au kumwabudu Mungu, kama ni hivyo basi halina budi kuwepo na makusanyiko tofauti madogo madogo katika kila eneo ili kukamilisha kusudi lile lile la kukusanyika pamoja…Ndio hapo wakristo waliopo Mkoa wa kilimanjaro watakusanyika kivyao, na waliopo Morogoro watakusanyika kivyao huko waliko, n.k..

Lakini kumbuka Imani ni moja, na Kristo ni yule yule anayeabudiwa kote, utendaji kazi unaweza ukawa unatofautiana kulingana na kanisa na kanisa, lakini Imani ni sharti iwe ile ile moja, Bwana mmoja, Roho Mmoja, Ubatizo mmoja sawasawa na (Waefeso 4:3-7), tofauti na hapo hilo ni jambo lingine.

Sasa katika mkoa huo huo wa Morogoro pia sio wakristo wote wapo Morogoro mjini, kuna wengine wapo vijiji vya ndani huko…hao nao hawana budi wakusanyike huko walipo, hakuna sababu ya kusafiri mpaka mjini….na huko vijijini pia kuna uwezekano wa watu wasiwe karibu karibu…hivyo tena yatazaliwa makundi mengine madogo madogo mengi kulingana na mahali, hata inaweza kufikia kanisa likawa na watu watano..lakini yote yenye imani moja. Umbali ndio unaosababisha yajigawanye hivyo.

Sasa haya makanisa mengi madogo madogo ambayo yanakuwa katika eneo husika kwa kiingereza yanajulikana kama LOCAL CHURCHES, (Yaani kanisa la eneo husika aidha mtaa, au kijiji).

Na makanisa haya zamani, kutokana na uchache wa watu yaliyonayo na maeneo yalipo mengi yaliishia kudharaulika… na asilimia kubwa ya washirika wake ni maskini…kwasababu wengi wanaoishi vijijini au katika miji midogo midogo si matajiri kulinganishwa na wale wanaoishi mijini. Hivyo walidharaulika lakini kama biblia inavyosema kuwa..

Yakobo 2:5 “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao”

Hivyo hao waliodharaulika na kujulikana kama “Local churches”… ndio waliokuwa wa kiroho zaidi..Ishara nyingi na miujiza mingi ilifuatana na haya makanisa madogo madogo, kuliko hayo makubwa, …ndio watu waliokuwa na bidii zaidi ya kumtafuta Mungu, na ndio waliokuwa wanamheshimu zaidi Mungu.

Sasa kutokana na makanisa hayo madogo madogo kufahamika kama local churches…na washirika wao ndio wakajulikana kama “local people”..na kwa lugha yetu hii wakatafsiriwa kama (wa-locally) au WALOKOLE.

Hivyo kama mtu utaitwa mshamba kwa sababu unamwamini Yesu na kuzishika amri zake basi hiyo ni THAWABU. Kuliko kama utaitwa mwenye Elimu na wa-kisasa na huku umemwacha Kristo.

Ufunuo 3:17 “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona”

Usijisifie ukubwa wa kanisa unaloabudu, wala wingi wa watu wa kanisani kwenu…Jisifie Yesu uliye naye maishani mwako hata kama upo kanisa la watu watano..jitathmini je! unazishika amri zake hapo ulipo?, je! unaishi kulingana na neno lake? Kiasi kwamba hata parapanda ikilia utakwenda naye!..Je hapa nilipo nanufaika roho yangu kiasi gani?..kama sinufaiki rohoni ni heri nikatafute wenzangu wenye Imani ya kweli hata kama ni wachache, ninusuru roho yangu..kuliko kuendelea kwenye umati wa watu wengi na kuipoteza nafsi yangu…

Ni heri nijulikane mlokole lakini naenda mbinguni kuliko kukubalika na kila mtu, mwisho wa siku naishia kwenda jehanamu. Na kama pia hapo ulipo penye watu wachache huoni dalili ya kuurithi uzima wa milele ni heri ukaenda kutafuta penye watu wengi ambao wanakwenda mbinguni..Lakini siku zote kumbuka mlango ni mwembamba na njia ile imesonga na ni wachache wanayoiona…na mlango ni mpana wa njia iendayo upotevuni na wengi wanauendea.

Bwana akubariki na Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

MIHURI SABA

Wafilisti ni watu gani.

YEREMIA

MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Bornface
Bornface
2 years ago

Am the one who need more knowledge of Christ nikuwa mlokole

SSMM1995#
SSMM1995#
2 years ago

Kuwa mlokole huku ukikataa amri za Mungu ni upagani. 1yohana 2:3-4

Lipembe james
Lipembe james
2 years ago

Nimependa sana hiyo moment