Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”.
JIBU: Hapa ni Mungu alikuwa anaonyesha tabia za mtu mwenye haki jinsi zilivyo kwamba huruma zake haziishi tu kwa wanadamu wenzake, bali pia zitadhihirika mpaka na kwa wanyama.
Kama vile Mungu sasa anavyowajali wanyama wake, kiasi kwamba hakuna hata mmoja anayekufa bila ya yeye kujua, na vivyo hivyo na sisi tunapaswa tuwe na tabia hizo, alisema ..
Mathayo 10:29 “Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;”
Sehemu nyingine Bwana Yesu alisema maneno haya;
Luka 14:5 Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?
Akimaanisha kuwa, kumbe watu wengi walikuwa wanainajisi sabato pasipo wao kujua na Mungu asiwahesabie makosa, kwa tendo tu hilo la kuwaokoa wanyama wao.
Utaona pia sehemu nyingine, Balaamu Yule nabii wa uongo alipompigia Yule punda wake, mara tatu, Mungu alichukizwa sana na kitendo kile.. Na ndio maana swali la kwanza aliloulizwa na Yule malaika ni kwanini amempiga Yule punda kiasi kile? (Hesabu 22:32)
Kuonyesha kuwa Mungu hapendezwi na kitendo cha utesaji wanyama.
Hivyo na sisi pia kama tulikuwa na tabia za kuwatesa wanyama, au kutoijali mifugo yetu, kiasi kwamba ukimkuta mbwa unamsindikiza na mawe,tuache hizo tabia, kama wanaishi na sisi pasipo madhara yoyote, hakuna sababu ya kuwapiga piga ovyo, au kuwafuga na kutowahudumia.
Kwasababu kitendo cha kuwatendea mema, biblia inasema kinaongeza pia siku za kuishi duniani soma,
Kumbukumbu 22:6 “Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; 7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.
Kumbukumbu 22:6 “Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda;
7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.
Hiyo ndio maana ya huo mstari ..Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE
USIRUDI NYUMA KWA KUITUMAINIA HAKI YAKO.
SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Tukisoma katika Kitabu cha 1 Wakorintho Sura ile ya Tano, Tunaona Mtume Paulo Akizungumzia Habari Ya kutengwa Kwa Watu wenye kulichafua kanisa la Mungu,… sasa tukija katika Mstari wa 3, alisema hivi..
“ Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha KUMHUKUMU yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo”.
Swali langu ni hili, Katika Huo mstari wa Tatu, naona Mtume Paulo anasema kwamba, mtu wa namna ile, Yaani aliye mzinzi, mlevi N.K.. yeye Amekwisha Kumuhukumu,… Sasa na Tukisoma katika kitabu cha Mathayo, 7:1, Bwana Yesu alituonya Kwamba tusihukumu, kwa maana tukihukumu mtu nasi tutahukimiwa….Sasa hapa imekaaje kaaje?
JIBU: Hukumu Mtume Paulo aliyomaanisha hapo si kuhukumu ile inayozungumziwa katika Mathayo 7..Kwamba msihukumu msije mkahukumiwa,.. Ile inayozungumziwa inakuja pale mtu anapotoa maneno yanatoa hatma ya maisha ya mtu mwingine, kana kwamba ni Mungu , kwamfano,kumwambia mwenzako wewe ni wa motoni tu, hata iweje huwezi kuokoka. Hapo umeshahukumu. Au unapowaona wenye dhambi, kama vile mashoga, na unaanza kusema wale makafiri Mungu hawezi kuwakubali milele, dhambi zao hazifutiki,..Hapo tayari umeshahukumu.
Lakini mtume alichokimaanisha hapo sio hicho, bali alimaanisha hukumu ya ADHABU. Yaani kuadhibiwa kwa huyo mtu.
Na jambo kama hilo Mungu ameliruhusu wakati mwingine katika kanisa kufanyika.. Kwamfano katika habari hiyo ukiendelea kusoma mistari inayofuata utaona, mtume Paulo alisikia wakorintho wamejihusisha na zinaa mbaya, iliyokithiri ambayo haipo hata kwa watu wenye dhambi, yaani mtu anazini na mama yake halafu bado yupo katika kanisa. Sasa kwa kosa kama hilo Paulo akawaambia wakorintho, hata kabla hajafika tayari ameshamuhukumia adhabu mtu kama huyo. Na adhabu yenyewe ni kumkabidhisha shetani amuue, mwili aungamie ili roho ipone siku ile ya hukumu.
Hata sasa, matendo kama haya, yanaendelea katika kanisa la Kristo, leo hii limekuwa ni jambo la kawaida kusikia wachungaji wanazini na washirika wao, wengine wanavuka mipaka hadi na watoto wadogo, utasikia askofu anazini na muumini pamoja na mama yake, jambo ambalo huwezi kuliona hata kwa watu wenye dhambi. Na wenyewe wanaona ni sawa kwasababu hakuna mtu wa kuwakabidhisha kwa shetani.
Paulo anasema, ni heri ukabidhiwe kwa shetani uuawe, walau hasira ya Mungu utapoa juu yako, na siku ile ya hukumu unusurike, kuliko kuendelea kuishi, katika hali hiyo hiyo mpaka kufa kwako, kwani adhabu yako itakuwa kubwa sana siku ile.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana”.
Hivyo hiyo inatukumbusha tuwe makini sana, katika ukristo wetu, vilevile na katika wito wetu.
Shalom.
Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?
KAMA SI YESU, HABARI YETU INGEKUWA IMEISHA ZAMANI SANA.
Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?
JIBU: Kumbuka Mungu ameiandika injili yake katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ni katika kitabu, na sehemu ya pili ni katika moyo wa mwanadamu.
Watu wengi tunadhani, ni mpaka tusikie ndio tutahukumiwa hapana, hiyo ni sehemu ya kwanza, lakini kuna sheria ambayo Mungu tayari kashiweka katika moyo wa kila mwanadamu ajapo hapa duniani, ambayo hiyo inathibitishwa na kutetewa na “dhamiri na mawazo” ya mtu mwenyewe.
Biblia inasema..
Warumi 2:14 “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15 Hao waionyesha KAZI YA TORATI ILIYOANDIKWA MIOYONI MWAO, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;”
Warumi 2:14 “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
15 Hao waionyesha KAZI YA TORATI ILIYOANDIKWA MIOYONI MWAO, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;”
Umeona? Ikiwa na maana kuwa, hata ukienda katika jamii za watu ambao wamejitenga kabisa huko maporini, hawajui chochote kinachoendelea ulimwenguni, kazi yao ni kuwinda na kukusanya tu..bado utawakuta na tabia ambazo zinaendana kabisa na sheria za Mungu, kana kwamba wanaijui torati. Kwamfano utakuta wanapinga vitendo vya uuaji, wizi, au uzinzi n.k.
Mambo kama hayo, hawakuyasoma kwanza kwenye biblia, bali tayari yalishaandikwa mioyoni mwao kana kwamba walikuwa wanaijua biblia. Na ndio katika hayo Mungu atawahukumu. Kwasababu kama tulivyosoma hapo, kwamba kama mtu atafanya yaliyo ndani ya sheria, hata kama hajaisikia, basi tayari anaitenda sheria hiyo ndani ya moyo wake.
Lakini wakati wasasa tunaoishi, injili ya Kristo imeshasambaa ulimwenguni kote, Tumesikia, na bado mioyo yetu inatushuhudia. Haijalishi utaiamini, au huiamini, Hivyo tujue kuwa tusipoitii hatutakuwa na udhuru siku ile ya hukumu.
JE! WATOTO WACHANGA WANAWEZA KUHUKUMIWA NA KUTUPWA MOTONI.
Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
NI LIPI KATI YA MAKUNDI HAYA, WEWE UPO?
Wakati tunaoishi ni wakati ambao kuna machafuko mkubwa sana ya rohoni kuliko hata nyakati nyingine zilizowahi kupita huko nyuma,. Na muasisi wa hayo ni shetani kwasababu anajua katika agano letu jipya kiini cha Kanisa ni ROHO MTAKATIFU. Hivyo anajua akiruhusu Roho wa Mungu peke yake alitawale kanisa, atawakosa watu wengi sana.
Hivyo tangu ule wakati wa mitume, alibadilisha mbinu zake za kivita, akitaka kulishambulia kanisa, haji tena mwilini, bali, ni anakuja na roho za udanganyifu zinazofanana sana na Roho Mtakatifu wa kweli kumbe sio.
Hivyo kuanzia ule wakati alianza kutoa matoleo mengi sana ya roho hizo. Mpaka sasa matoleo aliyonayo ni ya hali ya juu sana, kiasi kwamba usipokuwa makini utaweza ukavamiwa na roho za udanganyifu ukadhani ni Roho Mtakatifu kumbe ni uongo. Tupo katika wakati ambao si wa kiziamini kila roho zinazohubiriwa na watu.
Na ndio maana mitume walituonya na kusema..
1 Yohana 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”.
Sasa ili tuwe salama ni vizuri tukajua tabia za kweli za Roho Mtakatifu zipoje, ili tuwe na amani na tulichokipokea.
Kama jina lake lilivyo, “Roho Mtakatifu”, ndicho anachokifanya ndani ya mtu pale anapokuja juu yake rasmi, Atamfanya awe mtakatifu. Kama alivyosema katika 1Wakorintho 3:16, kuwa miili yetu ni lazima iwe mitakatifu kwasababu huyo Roho anayekaa ndani yetu ni Mtakatifu. Hivyo Ni lazima ahakikishe kuwa yale matunda yote ya roho yapo ndani yako sawasawa (Wagalatia 5:22-23)
Hivyo ukiona umepokea Roho, ambayo ndani yako haikupi kiu ya kuwa mtakatifu, yaani kuacha anasa, kuacha uvaaji mbovu, kuacha, miziki ya kidunia, kuacha vimini, na milegezo, kuwa na upendo, na kiasi, basi ujue hiyo sio Roho ya Mungu, haijalishi utanena kwa lugha muda mrefu kiasi gani.. Kimbia hapo, haraka sana.
2) Atakuongoza katika kuijua kweli yote(Yohana 16:13):
Kazi nyingine ya Roho wa kweli wa Mungu, ni kuwa hatakuacha katika hali hiyo hiyo,ya ujinga wa kiroho uliokuwa nao sikuzote, ni lazima akupigishe hatua za kiufahamu mpaka kufikia kusimama imara katika maandiko. Lakini ukiona umeokoka na miaka nenda rudi, hujui chochote kuhusiana na Neno la Mungu, wewe unachojua ni habari za wachawi na mapepo, ujue kuwa Huyo sio Roho Mtakatifu uliyempokea bali ni roho nyingine ya adui ipo ndani yako.
3) Atamshuhudia Kristo ndani yako :
Roho Mtakatifu kazi yake ni kutoa ushuhuda wa Kristo katikati ya kanisa lake, na sio wa mwanadamu yoyote. Ikiwa na maana kiini cha kanisa ulilopo, au huduma, unayoitumikia msingi wa hapo ni lazima awe Bwana Yesu Kristo. Na sio mwanadamu Fulani, au mtakatifu Fulani. Ukiona Kristo hapewi kipaumbele chochote, au anachukuliwa kama mtu wa ziada tu, ujue roho ya mpingakristo ipo hapo.
1Yohana 4:2 “Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani”.
1Yohana 4:2 “Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani”.
4) Ataweka karama au huduma ndani yako (1Wakorintho 12):
Karama hiyo/ huduma hiyo Roho Mtakatifu anaiweka kwa lengo la kulijenga kanisa la Mungu. Haiwezekani, ukawa umeokoka muda mrefu na miaka mingi, na umesema umepokea Roho Mtakatifu lakini kazi yako katika ufalme wa mbinguni haionekani. Wakati mojawapo ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuweka vipawa ndani yetu.
Hivyo kama hutakuwa mchungaji, au nabii, au mwinjilisti, au shemasi, au mwenye karama ya lugha, n.k basi utakuwa ni nyingine yenye faida katika kanisa kama kukirimu, kuimba, kufadhili n.k. Lakini haiwezekani kiungo kikawa hakina kazi kabisa katika mwili wa Kristo, kama mshirika anayekuja na kuondoka, miaka yote, ukiona hivyo ujue kuwa Roho uliyempokea si wa Mungu, bali ni wa adui.
5) Atachochea kuomba ndani yako. (Warumi 8:26)
Maandiko yanasema Roho Mtakatifu anaugua ndani yetu, kwa namna isiyoweza kutamkwa. Ikiwa na maana Mkristo wa kweli aliyepokea Roho, hataona amani kukaa wiki, miezi, miaka bila kuomba. Ile furaha ya wokovu itaondoka tu ndani yake, Hivyo atalazimika, kuwa mwombaji mzuri, kuhudhuria mikesha, na kufunga wakati mwingine.
Lakini ukiona unayo amani, kukaa mwezi mzima bila kuomba, na ndani yako husikii chochote, au mzigo wowote, hapo umepokea Roho nyingine ya adui. Jitathimini tena.
Tabia hizi tano (5), ukiziona ndani yako. Basi ujue Roho uliyempokea ni kweli Roho Mtakatifu, uwe na amani. Lakini kama hivyo vyote havipo ndani yako, Roho uliyepokea ni ya adui ibilisi. Unachopaswa ufanye ni umaanishe kuokoka katika maisha yako.
Maana yake, utubu dhambi zako kweli kweli, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO (Matendo 2:38). Kisha baada ya hapo, Roho wa kweli ataingia ndani yako, kuanza kukupigisha hizo hatua.
Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na tumeaswa sana tuzijaribu hizo roho, usiridhike, na tabia mojawapo tu, jiulize je! Zote hizo zinaonekana ndani yako?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.
SWALI: Tukisoma katika maandiko tunaona sehemu kadha wa kadha likitajwa neno “Torati na manabii”. Sasa hii torati na manabii maana yake ni nini? Kwamfano Mathayo 7:12 inasema
“Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii”.
JIBU: Bwana Yesu aliposema Torati na manabii, alimaanisha Agano la kale, ambalo ndio limeundwa na vitabu vya Musa (Torati), ambavyo ni vitano (5), Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati. Pamoja na vitabu vyote vya manabii, kama vile, Yeremia, Isaya, Danieli, Ezekieli, Hababuki, Amosi, n.k. hapa ikijumuisha pia, vile vingine kama Waamuzi, Zaburi, Ayubu, Wafalme, Mithali, Ruthu n.k. Ambavyo sio moja kwa moja vya manabii, lakini vimebeba nabii za Mungu ndani yake.
Kwahiyo torati na manabii kwa ufupi ni lile agano lote la kale. Hivyo Pale Bwana Yesu alipokuwa anawafundisha juu ya kanuni za kufuata, alirejea biblia yao, akiwaambia kuwa kiini cha biblia hiyo ni UPENDO. Wala hakuna siri nyingine nyuma yake, Torati yote, pamoja manabii wote, walichokuwa wanahubiri ni Upendo, (Ambao umegawanyika, wa Mungu na wanadamu)
Hata sisi wa leo tulio katika agano jipya, tunaposoma biblia yote tujue Ujumbe mkuu tunaoupata katika agano letu ni ule ule UPENDO. Na ndio maana Mtume Paulo alisema.
1Wakorintho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.
1Wakorintho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.
Hivyo na sisi, tunapaswa tuutafute huu, kwa bidii zote, ili tuonekane kuwa wakamilifu mbele za Mungu.
Shalom
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Nini maana ya “Roho za manabii huwatii manabii?
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
JE UPENDO WAKO UMEPOA?
Maswali na Majibu
SWALI: Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wale watu wenye ukoma waende kujionyesha kwa makuhani?, kwanini asiwaponye tu hivyo hivyo na kuwaacha mpaka awaambie waende kwa makuhani.
Luka 17:12 “Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! 14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika”.
Luka 17:12 “Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika”.
JIBU: Kama vile Injili ya Kristo inavyowafikia watu katika namna mbili, wengine kuwaokoa na wengine kama ushuhuda kwao (Mathayo 24:14)
Vivyo hivyo na uponyaji wake alivyouachia, alikusudia uwafikie watu kwa namna mbili. Kuokoa na wakati huo huo kuwa Ushuhuda.Si kila uponyaji au muujiza Yesu aliokuwa anaufanya ulikuwa ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hapana, bali ponyaji nyingine aliziruhusu mahususi kwa lengo la kuwa ushuhuda kwa wengine, ili siku ile ya hukumu wasije wakasema hatukuona, au hatukusikia.
Tunasoma jambo kama hilo katika..
Mathayo 8:1 “Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. 2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika. 4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, IWE USHUHUDA KWAO”.
Mathayo 8:1 “Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.
2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.
4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, IWE USHUHUDA KWAO”.
Ndicho kilichowakuta Makuhani, pamoja na mafarisayo na waandishi. Ni watu ambao walikuwa hawataki kusikia wala kuamini, Hivyo Bwana Yesu, alipowaponya baadhi ya watu hakuwaacha tu hivi hivi waende,kama alivyofanya sehemu nyingine, bali aliwaagiza waende kuwaeleza makuhani miujiza iliyowakuta,. Hivyo walikuwa wanapokea shuhuda nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali walioponywa.. Pengine kwa siku hata watu 100. Na kila walipoulizwa ni nani kawaponya wanasema YESU.
Hivyo hata sasa na sisi, tusifurahie tu miujiza ya Mungu anatuletea miujiza mingi, watu wanaponywa, wanafunguliwa, na huku maisha yetu yapo nje ya Kristo. tusifurahie kwasababu tujue ni hukumu tu tunajiandikia. Na ndio maana Bwana alisema maneno haya sehemu fulani;
Mathayo 11:21 “Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. 22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. 23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. 24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.
Mathayo 11:21 “Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.
22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.
23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.
Hivyo hiyo ndio iliyokuwa sababu kwanini aliwaambia wakajionyeshe kwa makuhani, kwasababu wao ndio waliokuwa hawamwamini wala kuziamini kazi zake.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?
Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda?
MIUJIZA YA KRISTO, HAITEGEMEI KANUNI ZA KIBINADAMU.
WhatsApp
SWALI: Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda na sio kwenye koo nyingine kama vile Yusufu?
JIBU: Hatma ya yale makabila 12, na tabia zao tunaona kwa mara ya kwanza zikifunuliwa na Yakobo Baba yao siku ile alipokuwa anakaribia kufa, alipowaita na kuwabariki. ukisoma pale utaona kila mtoto alinenewa habari zake. Kwasasa hatuwezi kuziandika zote hapa lakini kwa muda wako soma Mwanzo 49:1-28. Utaona.
Sasa, kulingana na tabiri zile ni kabila moja la Yuda, ndio lilibeba, vimelea vikuu sana, vimstahili Kristo.
Kwamfano pale makabila hayo yalipofananishwa na Wanyama, utaona Ni Yuda peke yake ndiye aliyefananishwa na SIMBA. Wakati wengine kama vile Naflati lilifananishwa na Ayala, Isakari kama na Punda, Dani kama na nyoka aumaye, Benyamini kama mbwa-mwitu mkali. Yusufu kama mti mchanga uzaao. Lakini Yuda ni kama SIMBA .
Na sikuzote simba anajulikana kama ni mfalme wa pori, tena jasiri.
Mwanzo 49:8 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. 9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? 10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. 11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. 12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa”.
Mwanzo 49:8 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.
9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa”.
Vilevile kama tunavyosoma utabiri wake, utaona anaambiwa, FIMBO YA ENZI, haitaondoka kwake, ikimaanisha kuwa fimbo ya kifalme, itakuwa katika uzao wake daima. Yaani kabila hili la Yuda litakuwa ni kabila la kifalme.
Mambo ambayo yanabeba kabisa tabia zote za masihi atakayekuja. Kwamba ni lazima AWE simba, jasiri, mwenye nguvu, na hodari.. Na ndio maana hatushangai kwanini Bwana Yesu alijiita Simba wa Yuda (Ufunuo 5:5).
Vilevile ni lazima awe Mfalme mkuu sana mwenye nguvu sawasawa na unabii wa (Isaya 9:6). Hivyo kabila lenye enzi za kifalme lilikuwa ni hili na tunathibitisha hilo tangu enzi wa Daudi.
Hivyo hiyo ndio sababu kwanini Bwana Yesu hakutokea kabila lingine lolote Zaidi ya kabila la Yuda, Kwasababu, ilimpasa awe juu ya yote..Lakini kama angetokea kabila ya Yusufu ambalo limetajwa kama kabila lenye mafanikio makubwa, ni wazi kuwa kusingekuwa na vimelea vyovyote vya kifalme kwake.. Jambo ambalo haliwezekani kwa Kristo. Yeye ni lazima awe juu, atawale kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana. Hivyo ni lazima tabia hizo zianze kuonekana tokea mbali sana, kwenye vizazi vya vya nyuma, hadi kumfikia yeye.
Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)
FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
Madhabahuni ni mahali ambapo Mungu amepachagua kukutana na mwanadamu. Hivyo palipo na madhabahu ya Mungu mtu anaweza kuwasilisha dua zake, ibada yake, na shukrani zake, na Mungu akazipokea. Mahali pasipo na madhabahu haiwezekani kukutana na Mungu, na kama ikitokea hivyo basi ujue ni kwa neema zake tu, kakujibu pengine kwasababu hukuujua ukweli. Lakini hakuna njia mtu anaweza kuwasiliana na Mungu pasipo madhabahu.
Sasa tunapozungumzia madhabahu hatumaanishi lile eneo la mbele kanisani linalopambwa, hapana, hicho ni kivuli tu cha madhabahu, madhabahu halisi kwasasa ipo rohoni kule mbinguni, kiti cha enzi cha Mungu kilipo. Na Yesu mwenyewe ndio nyenzo ya kutufikisha hapo, Ikiwa na maana ili uweze kumfikia Mungu ni sharti DAMU ya Yesu ikutangulie kwanza kuzifunika dhambi zako. Hapo ndipo utajua ni kwanini alisema yeye ndio njia kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye.(Yohana 14:6) .Watu wengi wanadhani wanaweza kumkaribia Mungu kwa matendo yao wenyewe au dini zao. Hilo halipo kabisaa.
Sasa turudi kwenye kiini cha somo. Ni nini kinaendelea sasahivi katika madhabahu ya Mungu rohoni. Kama tulivyotangulia kusema madhabahuni ni mahali ambapo watakatifu wanafikisha Maombi yao au haja zao kwa Bwana.
Na ni vizuri kufahamu watakatifu wamegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni watakatifu walio hai duniani, na kundi la pili ni watakatifu waliokufa. Na wote hawa wanawasilisha mahitaji yao mbele ya madhabahu ya Mungu mbinguni. Na leo kwa ufupi tutajifunza ni mahitaji gani wanayawasilisha mbele za Mungu.
Utakumbuka Bwana Yesu alitufundisha kuomba, na katika kuomba kule alisema tutamke neno hili..
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, UFALME WAKO UJE,…
Hii ikiwa na maana kuwa kila mtakatifu aliyepo duniani, kumwomba Mungu ufalme wake uje, ni sehemu ya maisha yake ya kila siku. Hivyo mbele ya madhabahu ya Mungu iliyopo mbinguni, maombi haya yanafikishwa na malaika na kuwekwa mbele ya madhabahu ya Mungu,..Na hivyo Mungu anachofanya ni kuiharakisha ile siku ya kurudi kwake, ifike upesi.
Ufunuo 8:3 “Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi”.
Unaona? Lakini si hilo tu, bado upande wa pili wa watakatifu nao waliokufa katika dhiki, wanayo maombi yao wanayoyapeleka..embu tusome..
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, NIKAONA CHINI YA MADHABAHU ROHO ZAO WALIOCHINJWA KWA AJILI YA NENO LA MUNGU, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, NIKAONA CHINI YA MADHABAHU ROHO ZAO WALIOCHINJWA KWA AJILI YA NENO LA MUNGU, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Unaona, hawa nao wanaonekana wapo chini ya madhabahu, wakiomba.. Hivyo wakati watakatifu wa duniani wanaomba ufalme wake uje..Watakatifu walio ardhini wanaomba mwisho wa waovu ufike.
Walio mbele ya madhabahu wanalia Unyakuo ufike upesi, utawala wa amani wa miaka 1000 uje haraka, karamu ya mwanakondoo ianze upesi.. wakati huo huo waliochini ya madhabahu wanaomba, waovu walipizwe kisasi, wauaji, wafikishwe katika kiama chao, mbingu zikunjwe kunjwe kama ukurusa, mapigo ya vitasa saba yamiminwe juu ya nchi, ili isafishwe, waje wastarehe na Bwana ulimwenguni milele.
Haya ni maombi mazito sana, na yanausumbua moyo wa Mungu, usiku na mchana, vilio vyao na vyetu vinamfikia kila dakika kila sekunde, kutoka huku duniani na kule peponi walipo watakatifu waliokufa.
Na tunasoma majibu Bwana aliyowapa wale waliolala yalikuwa ni haya..”WASTAREHE KIPINDI KIFUPI SANA”.. Kumbe kimebaki kipindi kifupi, majibu ya maombi yote yajibiwe, ndugu yangu, siku isiyokuwa na jina Yesu atarudi, Kama tunavyoona dalili zote, jinsi zinavyotimia kwa kasi sasa, mfano wa gonjwa hili la Corona (Luka 21:11). Hii ni kuonyesha kuwa siku yoyote tutashuhudia tukio la UNYAKUO.
Siku hiyo pengine ni leo usiku, tutashangaa ghafla kundi fulani dogo sana la watu halipo. Ukiona hivyo basi ujue umebaki, na utakachokuwa unasubiria ni kisasi cha Mungu mwenyewe duniani. Ambacho kitatanguliwa kwanza na ile dhiki kuu ya mpinga-kristo (666), ile ambayo Bwana Yesu alisema haijawahi kutokea wala haitakaa itokee . Na baada ya hapo ndipo mapigo ya vitasa saba yafuate (Ufunuo 16), Kisha, ulimwengu wote kumalizwa. Watu watatamani mauti lakini itawakimbia, ni kilio na kusaga meno.
Usifikiri tuna muda mrefu tena kama zamani, injili ya sasa sio ya kubembelezewa wokovu. Ni wewe mwenyewe ushtuke utoke usingizini, utengeneze mambo yako na Mungu wako. Ukipumbazwa na injili za manabii wa uongo, wanaokufundisha, ustarehe hapa duniani, kana kwamba hii dunia ni urithi wako utaishi hapa milele. Jihadhari sana, kwasababu Yesu alishatuonya juu yao kwamba watawadaganya hata yamkini walio wateule(Marko 13:22).
Hivyo tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kugeuka, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi, wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo. Na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu. Hapo ndipo utakuwa umezaliwa mara pili. Na ukiendelea kudumu katika wokovu na utakatifu basi hata Kristo akirudi usiku wa leo, unakwenda naye mbinguni.
Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?
Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?
TUFANANE NA WATAKATIFU WA MAKEDONIA.
Je! Mwandishi wa kitabu cha Warumi alikuwa ni Paulo au Tertio?
Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika (Isaya 6:8)
SWALI: Kwanini Mungu aliufananisha uzuri wa Kaanani na kama nchi ibubujikayo maziwa na asali? Kwanini isiwe kitu kingine chochote, labda dhahabu na nafaka?
Kutoka 3:8 “nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi”.
JIBU: Mungu aliposema Kaanani ni nchi ibubujikayo maziwa na asali, hakumaanisha kuwa kuna mito ya maziwa, au mabomba ya asali, kila mahali hapana. Bali alitumia lugha hiyo ya picha kuonyesha uzuri wa nchi ile jinsi ulivyo.
Kama tunavyojua maziwa yanatolewa na mifugo, kama ng’ombe,. Na ng’ombe ili atoe maziwa mengi na ya kutosha, anategemea sana mazingira yenye malisho mazuri ya kijani na chemchemi nzuri za maji. Hivyo Hapo ni Mungu alikuwa anawaonyesha wana wa Israeli kuwa nchi waiendeayo si nchi kame, bali ni nchi yenye rutuba nyingi sana, ambayo mboga mboga na malisho mazuri vinastawi, kiasi kwamba tukisema ni maziwa basi mifugo yao itamwaga maziwa mengi sana, hadi yasiwatoshe kwa wingi wa malisho yaliyopo huko.
Vilevile aliposema asali, aliwalenga nyuki. Na nyuki ni wadudu wanaotegemea sana, aina mbalimbali za mimea na maua ili kutengeneza asali yao, Kama tunavyojua mahali ambapo pana jamii chache za miti na mimea, inawachukua muda mrefu sana kuunda asali kidogo, kwani inawagharimu kutembea umbali mrefu sana, kutafuta virutubisho hivyo.
Lakini kama wapo eneo lenye misitu, na jamii tofauti tofauti za miti na mimea, huwa inawachukua muda mfupi sana. Hivyo Mungu aliposema hiyo nchi ibubujikayo asali, alimaanisha kuwa ni nchi yenye aina mbalimbali ya miti ya vyakula na matunda, Kama tukisema ni nyuki watengeneze asali, basi asali itakuwa ni ya kumwagika sana.tofauti na hiyo nchi ya ukame waliyotoka.
Na ndio maana wale wapepelezi waliotumwa na Musa kwenda kuipeleleza Kaanani, aliporudi na kichala kikubwa cha mzabibu na tini na mkomamanga, waliwaambia wana wa Israeli maneno haya;
Hesabu 13:27 “Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake”
Unaona, kwa yale waliyoyakutana nayo huko walithibitisha maneno ya Mungu kuwa ni kweli, kuwa nchi hiyo ni ya maziwa na asali.
Hata sasa, Mungu ana mpango huo kwa watoto wake , kuwafikisha katika nchi hii, lakini ni lazima kwanza, awafundishe kanuni zake, na jinsi ya kuishi ndani yake. Vinginevyo wakiifikia na huku maisha yao bado hajabadilishwa, nchi hiyo itawatapika kama ilivyowatapika wenyeji wa Kaanani. Na kanuni zenyewe ni kuishi sawasawa na amri za Mungu (Neno lake).
Walawi 18:26 “Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ILI KWAMBA HIYO NCHI ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.
Walawi 18:26 “Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28 ILI KWAMBA HIYO NCHI ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.
Lakini tukiishi sawasawa na Neno lake, wakati huo utafika na Bwana atatuingiza katika nchi hiyo kama alivyofanya kwa wana wa Israeli walipozitii amri zake.
Hesabu 14:8 “Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali”.
UNYAKUO.
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
UFUNUO: Mlango wa 18
Kuota upo nchi nyingine.
ESTA: Mlango wa 4
Daudi ni mfalme ambaye alikuwa amezungukwa na mashujaa hodari sana, na mashujaa hao aliowachagua walikuwa wamegawanyika katika makundi makuu matatu, Kundi la kwanza kabisa ambalo lilikuwa ndio la juu kabisa zaidi ya yote liliundwa na maaskari watatu, na lile pili yake liliunda na wawili, na lile la tatu liliundwa na mashujaa 37.
Sasa ukitaka kujua kwa urefu ushujaa wao, na mashujaa wenyewe walikuwa ni wakina nani fungua link hii usome zaidi…
Lakini leo tutaona kwa ufupi, ni nini kilimtokea mmojawapo kati ya wale mashujaa watatu wa kwanza, Na ni ujumbe gani Kristo anataka tuupate kupitia ushujaa wake.
shujaa huyu aliitwa Eleazari, yeye kuna wakati walikutana na jeshi kubwa la wafilisti, wakati huo alikuwa peke yake tu, Israeli yote ilikuwa imeondoka, hata wale mashujaa wenzake hawakuwepo.. Lakini hakuogopa vita bali alinyanyuka na kuushikilia upanga wake mmoja.. akaanza kupigana na wafilisti yeye peke yake kama vile Samsoni, aliushikilia upanga wake kwa nguvu sana kiasi kwamba haikuwa rahisi kuuondoa mkononi mwake.
Lakini kwasababu maadui walikuwa wengi,kuna muda ulifika alilemewa sana, na ile nguvu ya kuendelea kuushikilia upanga ikamwishia, akataka kuuachilia ule upanga kwasababu alichoka sana, lakini biblia inatuambia upanga ule hakuwezi kutoka katika mkono wake, ikiwa na maana ulijiganda kama gundi katika mkono wake. Pale alipojaribu kurusha mkono, upanga haukuchomoka mkononi mwake, bali ulikwenda naye Hivyo akaendelea kupigana na wafilisti mpaka akawamaliza wote. Baadaye Israeli walipokuja kazi yao ikawa ni kuteka nyara tu huko nyuma, kwa kipigo cha jeshi la mtu mmoja.
2Samweli 23:9 “Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; 10 huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu”.
2Samweli 23:9 “Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
10 huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu”.
Hiyo ni kuonyesha jinsi gani, mtu anapotaka kung’ang’ana na kusudi la Mungu, kusudi nalo litang’ang’ana naye, ili kutimiza lile lengo.
Leo hii ukiling’ang’ania kusudi la Bwana kwa moyo wako wote na kwa bidii, lile kusudi nalo litang’ang’ana na wewe tu, hamna namna, kwasababu hiyo ni kanuni ya ki-Mungu, hata kama utafikia wakati umechoka, bado litaendelea kukung’ang’ania tu. Na ndio maana unaona ni kwanini watumishi wa Mungu wa kweli, hawachoki kumtumikia Mungu, japokuwa hawafanyi kazi ya mshahara, sio kwamba hawachoki, au hawapitii magumu, au hawapungukiwi nguvu..wanachoka, lakini wakati wanakaribia kuanguka, lile kusudi la Mungu linang’ang’ana nao, hivyo wanajikuta bado wanaendelea mbele na safari.
Isaya 40:29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.
Isaya 40:29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.
Hata sisi sote, tunapodhamiria kweli kwa mioyo yetu yote, kutembea na Mungu, kamwe Mungu hawezi kutuachia katikati tuaibishwe na shetani, tunakuwa mfano wa Eleazari, nguvu za Mungu zitaambatana na sisi kuhakikisha kuwa lile kusudi la Mungu linatimia kwa gharama zozote zile.
Lakini tukiwa watu vuguvugu, leo tupo na Mungu kesho shetani, hatujajikana nafsi zetu na kusema kuanzia leo mambo ya ulimwengu basi, tunakwenda na Kristo. Kamwe nguvu ya Mungu haiwezi kushikamana na sisi kama alivyokusudia, pale tunapoishiwa nguvu au tunapokumbana na majaribu. Na ndio hapo utaona mkristo anakuwa moto na Mungu siku za mwanzoni mwanzoni, tu ikifika baadaye, anapoa, mpaka anauacha wokovu kabisa..ukimuuliza ni kwanini atasema, hali ya maisha ilikuwa ngumu, mwingine nilipitiwa na ujana, mwingine nilikuwa katika mazingira yasiyo rafiki,..Sasa tatizo halipo kwa Mungu bali kwa huyu mtu.
Kwasababu Mungu akishaianzisha safari ndani ya maisha ya mtu huwa haikatishi katikati, Kwasababu Mungu huwa hashindwi , anaelewa kabisa kuwa yapo majira mbalimbali tutapitia hapa duniani kama wakristo, hivyo anatuhakikishia nguvu ya ziada kutoka kwake, lakini hiyo inakuja endapo tu tutakuwa na nia ile ile ya kutembea naye.
Paulo alisema
Wafilipi 1:6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”
Hivyo ishi maisha ya kumaanisha mbele zake, ishi ndani ya kusudi la Mungu, ili Mungu awe nawe nyakati za taabu. Swali ni Je umemaanisha kweli kumfuata Kristo? Kama bado basi leo ndio wakati wako wa kudhamiria kutoka katika moyo wako kutubu na kuacha dhambi zako zote, Fanya hivyo kisha baada ya hapo nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO ikiwa hukubatizwa hapo kabla, Na Mungu mwenyewe atakupa Roho wake Mtakatifu, akutie nguvu hadi siku ukombozi wako.
Zingatia: Waliokombolewa na Mungu hawashindwi na ulimwengu.
Ikiwa utapenda upate huduma ya ubatizo sahihi, basi utawasiliana na sisi kwa namba hizi 0693036618, tukusaidie.
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.
NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.