Jina la Bwana wetu Yesu, libarikiwe.
Yapo mambo mengi ambayo yatawafanya wanadamu wengi wasiurithi uzima wa milele siku ile. Wakidhani wapo sawa na Mungu, na kwamba wanampendeza Mungu lakini itakuwa kama jambo la kuwashangaza kwamba wameukosa uzima wa milele. Na hilo si lingine zaidi ya kuukosa utakatifu, biblia inasema katika Waebrania 12:14 kuwa…“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”. Maana yake pasipo huo, haijalishi tunaona maono, haijalishi tunahubiri sana, haijalishi tunatoa sadaka sana, haijalishi tunatoa pepo wengi na kufanya miujiza…bado hatutamwona Mungu.
Fadhili za Mungu huwa zinawalewesha wengi.. Ndugu hata kama utalitukana jina la Mungu leo, hiyo haimfanyi Mungu kukunyima chakula au kutokukupa riziki, hata kama ukiwa mchawi haimfanyi Mungu kutokuangazia jua lake kwasababu fadhili zake ni za milele, na yeye hana upendeleo..anawanyeshea mvua waovu na wema, anawaangazia jua lake waovu na wema.. Hata yule mchawi mwovu kuliko wote anampa uzao, na tena hata katikati ya huo uzao wake wanaweza kutokea watumishi wa Mungu. Lakini pamoja na fadhili zote hizo za Mungu haimaanishi ndio tiketi ya kumwona Mungu siku ile..
Unapoumwa na kumwomba Mungu akuponye, na akakuponya hiyo haimaanishi kwamba ndio upo sawa na Mungu na kwamba hata ukifa leo utaingia mbinguni, Kama ni mtumishi unapomwombea mtu na akapona au unapotoa pepo na likatoka, huo sio uthibitisho kwamba Mungu anapendezwa na wewe…
Vile vile unapopitia shida na ukaona mkono wa Mungu umekuokoa katika hiyo shida…huo sio uthibitisho kwamba Mungu anafurahishwa na wewe ndio maana kakuokoa… anachokufanyia wewe ndicho anachowafanyia mamilioni ya watu duniani kote..na wengine hata sio wakristo anawaokoa kwa ushuhuda mkubwa. Kama unafikiri nakudanganya, tafuta mtu yeyote ambaye sio mkristo kabisa, mtu wa makamo mwulize ni tukio gani ambalo hutalisahau katika maisha yako, ambalo unaamini ni Mungu alikutendea..Utasikia shuhuda atakazokupa!…Hapo ndipo utakapojua kuwa Mungu hanaga upendeleo wa kuwapendelea watu wake tu!..
Hivyo fadhili za Mungu, zisitupumbaze na kujiachia katika dhambi, tukijitumainisha kuwa siku ile tutamwona Mungu…
Hebu yatafakari haya maneno ya Bwana..
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo NITAWAAMBIA DHAHIRI, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Hapo anasema atawaambia “DHAHIRI” yaani maana yake wazi pasipo vificho, kwamba siwajui.
Maana yake ni kwamba kama ukiwa mwasherati kwa siri au kwa wazi, haijalishi unaona malaika kila siku katika ndoto, hautaurithi uzima wa milele, kama unaabudu sanamu kama ni mchawi kama ni mlevi na mambo mengine yote yanayofanana na hayo, basi siku ile hautaurithi uzima wa milele.
Na Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili, hivyo linawahusu watu wote, hata mimi pia linanihusu, kama sitakuwa mtakatifu sitaurithi uzima wa milele, haijalishi nafanya nini sasa.
Ndio maana Mtume Paulo kwa uongozo wa Roho akasema mahali fulani maneno haya…
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATİKA HAYO NAWAAMBİA MAPEMA, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Hapo mstari wa 21, anasema “ANATUAMBIA MAPEMA”..Maana yake ni kwamba siku ile tutakapojikuta tumekataliwa na Kristo kutokana na kuukataa utakatifu…tusije tukasema tulikuwa hatujui!…Ndio maana hapo anatuambia mapema kuwa waasherati, wagomvi, wanaoabudu sanamu n.k hawataurithi uzima wa Milele.
Na pia katika Waefeso ni jambo hilo hilo linajirudia…
Waefeso 5:5 “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu”.
Ndugu ni vizuri kuzifurahia fadhili za Mungu, tunapoumwa anatuponya, tunapokuwa katika mashaka anatupa faraja, tunapozungukwa na hatari anatuokoa..ni vizuri kuzifurahia hizo, kwasababu ndio uthibitisho kwamba tunaye Baba mbinguni, lakini hizo zisitupumbaze tukambweteka na kufikiri kuwa ndio tayari anapendezwa na sisi,.. ndio tayari tiketi za kutuingiza mbinguni…hapana! bado kuna jambo lingine la muhimu la kufanya, nalo ni utakatifu.
Hivyo ni lazima tuishi maisha masafi na ya utakatifu na ya toba kila siku. Ili tuwe na uhakika wa kumwona Baba siku ile.
Bwana atubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kama hujaokoka, wokovu unapatikana bure.. Unachopaswa kufanya leo ni kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na Roho Mtakatifu atashuka juu yako, na kukusafisha kabisa na kukupa uwezo wa kushinda dhambi, jambo ambalo kwa nguvu zako mwenyewe huwezi!.Na utapata raha ya wokovu
Maran atha!
Tafadhali unapowashirikisha wengine ujumbe huu usipunguze wala kuongeza chochote, wala usiweke anwani au namba yoyote tofauti na hizi zilizopo hapa,
Na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
JINA LAKE KWA KIEBRANIA NI ABADONI, NA KWA KIYUNANI NI APOLIONI.
Kibiblia via ni viungo vya mwili wa mwanadamu au mnyama,, husasani mikono au miguu.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja Neno hilo;
Ayubu 17: 7 “Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli”.
Ayubu 18:13 “Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake”.
Ayubu 41:12 “Sitanyamaa kusema habari za via vyake, Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri”.
Shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tazama mana ya maneno mengine chini;
Je utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp? basi kama ni hivyo tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya uzima, na leo tena kwa neema za Bwana tutajikumbusha juu ya mambo ya msingi ya kuzingatia siku hizi za mwisho
Tukisoma biblia tunaona Yakobo alikuwa na wana 12, na kila mmoja alikuwa na tabia yake ya kipekee, Yusufu alikuwa na ya kwake, Yuda alikuwa na ya kwake, Benyamini alikuwa na ya kwake, na wengine wote. Vivyo hivyo na uzao wao mbeleni nao pia ukaja kuwa na tabia zao za kipekee kujitofautisha na kabila lingine, kabila la Yuda lilikuwa na tabia yake, kabila la Lawi lilikuwa na ya kwake n.k.
Sasa leo hatutaangalia tabia za makabila yote, lakini tutaangalia tabia la kabila la Isakari, ni nini walikuwa nacho, Biblia inatuambia ilipofika wakati Mfalme Sauli amekufa, na anatafutwa mrithi wa ufalme wake pale Israeli, kulihitajika hekima katika kuchagua, ikumbukwe kuwa hapo kabla kulikuwa na mvutano Fulani wa makabila hayo hususani, lile la Benyamini ambalo mfalme Sauli alitokea huko, lenyewe lilikuwa linataka warithi waendelee kutokea katika uzao wa Sauli kwasababu Sauli alitokea kwenye kabila hilo, wakati makabila mengine yanamtaka Daudi ayamiliki.
Hivyo katika mazingira kama hayo, kulihitajika watu wenye akili ambao wanaweza kutambua majira na nyakati kwa wakati huo, kwamba ni nani anapaswa awe mfalme. Sasa kwa kuwa Israeli ilikuwa inajua wanapofikia saa kama hiyo wamtafute nani na nani, ndipo wote wakawaendea wana wa Isakari, na kuwasikiliza wanasema nini.
Sasa ili kufahamu habari yote, unaweza kwenda kusoma 1Nyakati 11-12 yote, hapa tutakiweka kile kifungu tu kinalielezea kabila hili la Isakari,
1Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili NA NDUGU ZAO WOTE WALIKUWA CHINI YA AMRI YAO”.
Unaona, Israeli kabla hawajafanya uamuzi wowote, waliwafuata kwanza hawa wana wa Isakari, ili kuuliza ni nini wanachopaswa wafanye kwa wakati huo, wasije baadaye kuingia matatizoni, walikuwa wapo tayari kujiweka chini ya amri yao, kama maandiko yanavyotuambia, haijalishi watakachoambiwa kitakuwa ni kinyume na matarajio yao..Na hiyo yote ni kwasababu waliwatambua kuwa Mungu aliwapa akili ya kujua nyakati na majira, kuijua torati, na kuisikia sauti ya Mungu inataka nini.
Ulipokuwa unafika wakati kama huo, makabila yote yaliondoa tofauti zao, wakasikilize ni nini Mungu anawaonya kupitia wana wa Isakari. Sio kwamba makabila mengine yalikuwa madhaifu hapana, biblia inasema kabila la Yuda lilishinda zaidi ya yote, na Nyumba ya Yusufu ilikuwa ni kuu. Lakini kuhusu hatma ya maisha yao, ya wakati ule na mbeleni, Isakari walihitajika sana. Na hiyo iliisababishia Israeli, ikae katika Nuru wakati wote.
Vivyo hivyo katika agano jipya, hatupaswi kuishi tu, ilimradi tunaishi, sio kusema nimeokoka tu, sio kusema Bwana atanibariki tu, sio kusema twende kanisani tutimize wajibu kama kawaida, hiyo peke yake haitoshi, tunapaswa tutafute ni nini Mungu anasema juu ya wakati huu na majira haya; Lakini cha kusikitisha ni kuwa Bwana Yesu alisema sisi ndio tulio nyuma kabisa katika kutambua majira tuliyo nayo, na kibaya zaidi, tunafanya hivyo kwa unafiki, na sio kwamba hatufahamu.
Luka 12:54 “Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.
55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.
56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya”?
Unaona? Watu wa kipindi kile kwasababu waliipuuzia kujifunza juu ya nyakati zao na majira yao, walishindwa hata kujua kuwa wanatembea na Mungu mwenyewe duniani katika umbo la kibinadamu, mpaka sisi tunasema laiti tungekuwa kipindi chao tungelala na kutembea na Bwana Yesu wakati wote..
Lakini na wao pia huko walipo leo hii wanatuona sisi wa nyakati hizi za mwisho, ni jinsi gani tupo karibu sana na ule mwisho, wanasema laiti na wao wangekuwepo wakati wetu wangeishi maisha ya kama ya wapitaji tu hapa duniani, kwasababu muda tuliobakiwa nao ni mchache, Yesu yupo mlangoni kurudi na unyakuo ni wakati wowote…
Lakini ni kwanini tunaishi kama tunavyoishi leo hii, ni kwasababu, hatujui majira tuliyopo. Hatujui kuwa tangu kipindi cha Bwana Yesu hadi unyakuo kulitakiwa kupite kipindi cha makanisa saba, na kwamba sita ya kwanza yameshapita, na hili tunaloishi ndilo la mwisho la 7, lijulikanalo kama Laodikia sawasawa na Ufunuo 3:14 na hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili, sisi ndio tutakaoshuhudia tukio zima la Unyakuo. Kwamba lile juma la 70 la Danieli lipo karibuni kuanza kuhesabiwa.
Hatujui kuwa hii neema itakwenda kurudi Israeli siku za hivi karibuni, kama unabii wa biblia inavyotabiri, kwasababu tayari limeshakuwa taifa huru, na hivyo kinachosubiriwa ni unyakuo tu, Mungu akawarudie watu wake kama alivyowaahidi katika siku za mwisho.
Hatujui kuwa, roho ya mpinga-Kristo inafanya kazi tayari katikati ya madhehebu mengi, na kama hatuna macho ya rohoni, chapa tutaipokea tu pasipo hata sisi wenyewe kujua. Kwa ufupi hakuna dalili ambayo haijatimia inayozungumzia juu ya nyakati hizi za mwisho tukiachilia mbali kuibuka kwa wimbi la makristo na manabii wa uongo, biblia ilizungumzia Tauni(Corona), mafundisho potofu, na kuachiliwa kwa nguvu ya upotovu, ili watu waendelee kuamini uongo wapotee waende kuzimu n.k.
Embu tujitathimini maisha yetu tena, Je! bado tupo katika mstari au tunayumba yumba, Je! tunafahamu majira na nyakati kama wana wa Isakari?, au tupo tu, tunasubiria mambo hayo yatukute kwa ghafla tu,.tubakie kusema laiti tungejua..Bwana atusaidie tusifike huko wakati wa kujua ndio huu. Tunaishi katika saa ya kurudi kwa pili kwa Kristo, muda tuliopewa ni wa nyiongeza tu.
Shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Nyungu ni nini?
Nyungu ni nini kibiblia?(Ayubu 41:20,31, Waamuzi 6:19)
Nyungu ndio Chungu kwa jina lingine, kibiblia kilitumika kuchemshia maji, nyama, nafaka, mboga mboga n..k Unaweza kulisoma Neno hili katika vifungu vifuatavyo;
Hesabu 11:7 “Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola.
8 Watu wakazunguka-zunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga kwa mawe ya kusagia, au kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa NYUNGUNI, na kuandaa mikate; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya mafuta mapya”.
Waamuzi 6:19 “Basi Gideoni akaingia ndani, akaandaa mwana-mbuzi, na mikate isiyotiwa chachu, ya efa ya unga; akaitia ile nyama katika kikapu, AKAUTIA MCHUZI KATIKA NYUNGU, akamletea hapo nje chini ya mwaloni, akampa”.
Ayubu 41:20 “Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake, Kama NYUNGU ikitokota, na manyasi yawakayo”.
Ayubu 41:31 “Yeye huchemsha kilindi MFANO WA NYUNGU; Hufanya bahari kuwa kama mafuta”.
Shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tazama tafsiri ya maneno mengine ya kibiblia chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Kulabu ni nini katika biblia?
Kulabu ni aina ya ndoano, tofauti na ile ya kuvulia samaki hii ni ile inayotumiwa kushikilia vitu, kama vile mapazia, mashuka, nguo n.k., tazama picha juu uone mfano wa kulabu za mapazia,
Na ndio zilikuwa zinatumika katika kushikilia nguo za ua wa hema ya kukutania.
Kutoka 26:37 “Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; KULABU ZAKE ZITAKUWA ZA DHAHABU; nawe utasubu matako ya shaba matano kwa ajili yake”.
Kutoka 27:9 “Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia;
10 na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na matako yake ishirini, matako yake yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha”.
Soma pia Kutoka 27:11,17, 36:36, 38:10,11,12.
Lakini pia Mungu amelitumia Neno hili, kama mfano kwa watu wanaokaidi maagizo yake, kwamba atawatia kulabu/ndoano hiyo puani mwao.
Na kama tunavyojua, wanyama wanaotiwaga kulabu kama hizi puani mwao, huwa wanatii kwa lolote watakaloamrishwa, popote watakapopelekwa watakwenda tu haijalishi ni wakorofi kiasi gani.
2Wafalme 19:27 “Lakini nakujua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako unayonighadhibikia.
28 Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia”.
Maneno haya aliyarudia tena katika Isaya 37:28
Hivyo na Mungu pia anaweza kutitia kulabu na kutulazimisha kwenda mahali ambapo sisi hatutaki, kwa kosa moja tu la kuasi maagizo yake. Mifano kama hiyo tunaiona kwa wafalme wengi wa Israeli wengine walichukuliwa utumwani Babeli, wengine na walichukuliwa na maadui zao. Hivyo na sisi tusipokuwa watiifu kwa Mungu atatutia kulabu.
Bwana atusaidie tusifikie viwango hivyo.
Shalom.
Mistari mingine inayoelezea Neno hili, ni hii;
Ayubu 41:1 “Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu”?
Ezekieli 19:4 “Mataifa nao wakapata habari zake, akanaswa katika rima lao, wakamchukua kwa kulabu mpaka nchi ya Misri”.
Ezekieli 19:9, 29:4
Amosi 4:2 “Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajilia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana”.
Tazama maana ya maneno mengine chini;
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
SWALI: Naomba kuuliza, huu mstari una maana gani? “..VITU VIWILI visivyoweza kubadilika ambavyo kwa hivyo Mungu hawezi kusema uongo”?! (Waebrania 6:18).
JIBU: Shalom..
Tusome…
Waebrania 6:17 “Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;
18 ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo”
Kama ukianza kusoma kuanzia mstari wa 13 kwa umakini, mpaka mstari wa 18, utajua kuwa Vitu hivyo viwili visivyoweza kubadilika ni AHADI YAKE na KIAPO CHAKE.
Hivyo ndio vitu viwili pekee vya Mungu visivyoweza kubadilisha Neno la Mtu.
Kwa mfano katika Maisha ya kawaida, Mtu akitaka kuthibitisha neno lake Huwa anatoa Ahadi..Kwamfano unaweza kumwambia mtu nitakuja kesho kukutembelea…Na yule mtu ili kupata uhakika zaidi na kwamba hutamdanganya ataweza kukuambia “embu niahidi”..na wewe utamwahidi…Na ili kupata uthitisho ulio mkubwa zaidi anaweza pia kukuambia “hebu Niapie kwamba utakuja”..
Maana yake kwa ahadi uliyomuahidi, na kiapo ulichomwapia…Ni ngumu wewe kuwa umemdanganya! Ni lazima utamtembelea tu kwa vyovyote vile hiyo siku ya kesho, Na hata kama kikitokea kitu ambacho kitazuia safari hiyo, utakapokumbuka kwamba ulishatoa ahadi, na tena ulishaapa, basi unajikuta unatimiza ahadi yako kwa gharama zozote zile.. (Sasa huo ni mfano tu, sisi wakristo haturuhusiwi kuapa).
Vivyo hivyo Mungu, ili kutuhakikishia kuwa Neno lake ni kweli…Neno hilo kaligeuza na kuwa Ahadi, na hajaishia tu kulifanya kuwa ahadi, bali kaenda mbele Zaidi kaliapia…ili kwa vitu hivyo viwili, (Ahadi na kiapo) atuhakikishie sisi Watoto wake kwamba yeye si MWONGO, Maana yake ni lazima atalitimiza tu neno lake alilolitamka kutoka katika kinywa chake.
Ndio maana Mtume Paulo hapo, anachukua mfano wa Ibrahimu, jinsi Mungu alivyolithibitisha Neno lake kwa kumwapia zile ahadi alizompa.
Waebrania 6:13 “Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,
14 akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza”.
Hivyo Neno la Mungu limehakikiwa kwa “ahadi na kiapo”…kwamfano aliposema kwenye Neno lake
Yohana 16:23b “… Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu”.
Hapo mzizi wa hilo neno ni kwamba “tumwombe Baba” basi, lakini Bwana Yesu akituambia tumwombe tu Baba bila kutupa ahadi yoyote, tusingeamini kwamba tutapata majibu..Hivyo ili kulithibitisha hilo neno, akaongezea mbele yake ya kwamba “tukimwomba atatupa”…hilo neno “atatupa” tayari ni Ahadi…. Lakini hajaishia hapo ili kulithibitisha kuwa hajatudanganya akaongezea na kiapo juu yake na kuanza kwa kusema “Amin…Amin nawaambia”..tukimwomba Baba kwa jina lake atatupatia.
Hivyo tunapomwomba Baba popote pale, tufahamu kuwa ni haki yetu kupokea majibu yetu kama tumeomba sawasawa na mapenzi yake…hajatudanganya!, kwasababu katupa ahadi na kiapo..
Unaweza pia kusoma maneno mengine mfano ya hayo, kwa kuongeza maarifa, kasome Yohana 14:12, Luka 18:29-30.
Zaburi 138:2b “….Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote”
Bwana atubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Mount Gerizim and Mount Ebal: Their Meaning and Spiritual Significance
SWALI: Kwanini Musa aliagizwa awaambie wana wa Israeli watengeneze madhabahu kwa mawe yasiyochongwa? Kwanini yawe mawe yasiyochongwa?
JIBU: Tusome vifungu vyenyewe;
Kutoka 20:24 “….. kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
25 Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi”.
Kumbukumbu 27:5 “Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.
6 Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;
7 ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za Bwana, Mungu wako”.
Yoshua 8:30 “Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali.
31 Kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa Bwana, na kuchinja sadaka za amani”.
Shalom,
Madhabahu sikuzote inasimama kama kiunganishi cha kufikisha maombi yetu, dua zetu, sadaka zetu na shukrani zetu kwa Mungu, na pia inasimama kama nyenzo ya sisi kuwasiliana na Mungu. Ni kama tu mnara wa simu, mahali ambapo hapana mnara unaorusha mawimbi ya sauti mbali, kamwe hatuwezi kuwasiliana haijalishi simu zetu zitakuwa za kisasa kiasi gani.
Sasa kwenye agano la kale madhabahu zilikuwa zinatengenezwa kwa kupanga mawe kuanzia chini, mpaka kimo fulani, na kisha juu ya mawe hayo zinapangwa kuni kavu, na juu ya kuni hizo panawekwa sadaka ya kuteketezwa ambayo ilikuwa ni aidha Wanyama au ndege, na sadaka hiyo inachomwa na moshi kupanga juu..
Hivyo katika agano la kale Wana wa Israeli walipewa maagizo kwamba mahali popote atakapopachagua Mungu ili wamjengee madhabahu ya mawe ni sharti kwamba wasitumie ujuzi wao katika kuitengeneza, hii ikiwa na maana kuwa wakikutana na jiwe ambalo limezidi kimo kidogo katika ujenzi wao, walitumie hilo hilo, wasilichonge kulipunguza, wakikutana na lilililopungua vilevile walitumie hilo hilo, wasilichonge wala kulipiga nyundo, vinginevyo madhabahu hiyo itakuwa batili.
Sasa hicho kilikuwa ni kivuli cha jinsi madhabahu halisi ya Mungu itakavyokuja kujengwa katika agano jipya. Mungu aliwapa maagizo hayo kufunua madhabahu halisi ya agano lililo bora itakavyokuja kuwa.
Na YESU KRISTO ndiye madhabahu yetu kwasasa. Yeye ndio kiunganishi chetu sisi na Mungu.
Na tunamuunda kama madhabahu yetu kwa namna mbili;
Namna ya kwanza ni pale tunapokuwa kanisani, tunapokusanyika pamoja sisi tuliookoka, sasa kule kuja pamoja ni sawa na tunavileta viungo vyote sehemu moja na hapo mwili wa Kristo unaumbika, na Kristo mwenyewe anakuwepo, na madhabahu inatokea, Hivyo tunapokutanika ni wajibu wetu kujua kuwa karama zinatolewa na Mungu mwenyewe na si wanadamu..Pale tunapozizuia karama za Roho kujidhihirisha katikati ya viungo vya Kristo (mawe), badala yake tukaweka uongozi ambao tunaouna unafaa mbele ya macho yetu wenyewe na si mbele za Mungu, tunaweka vyeo vya kibinadamu vituongoze, vyeo vya kisiasa n.k…ni sawa na tumechonga mawe hayo wenyewe, na hivyo madhabahu hiyo inakuwa najisi mbele za Mungu. Uweza wa Mungu haushuki mahali hapo.
Na namna ya pili ni tunaijenga sisi wenyewe (binafsi),
Pale tunapokuwa peke yatu aidha nyumbani, au mahali pa utulivu kuwasiliana na Mungu, ni lazima madhabahu iwepo na hiyo si nyingine zaidi ya Yesu Kristo moyoni mwetu, yeye ndiye jiwe ambalo halijatiwa unajisi kwa dhambi yoyote, halijachongwa na mwanadamu yoyote halijachongwa kwa siasa au kitu kingine chochote,
Hivyo ikiwa umempokea Yesu moyoni mwako na umebatizwa na umepokea Roho Mtakatifu, tayari Yesu kashaingia moyoni mwako na kuweka makao, na hivyo madhabahu imeshatokea, basi maombi yako, dua zako, sadaka zako zina uhakika kumfikia Mungu..Lakini ukiyachonga mawe yako mwenyewe, yaani unaenda mbele za Mungu kwa kumuonyesha matendo yako, uungwana wako, uzuri wako, sadaka zako unazozitoa na huku Kristo umemtupa nje, hana nafasi kabisa katika moyo wako, hapo unafanya kazi bure ndugu yangu. Mungu hapokei uso wa mwanadamu yeyote, anapokea uso wa Yesu Kristo tu.
Hivyo ni wajibu wetu kujua kuwa madhabahu sahihi inajengwaje mioyoni mwetu, na katika kanisa.. Tusipende karama za kuchonga, tusijitumaishe na matendo yetu na huku Yesu yupo mbali na sisi.
Kama bado upo katika dhambi ni heri umgeukie yeye leo kwasababu yeye ndiyo jumla ya mambo yote hapa duniani. Bila yeye leo hii dunia ingekuwa imebakia kuwa historia tu, hivyo na wewe usisibiri uwe historia siku za usoni, Mpe Yesu maisha yako leo ayaokoe, upokee uzima wa milele. Usidhani utaweza kushinda haya maisha bila Yesu. Hilo halipo, wala halijawahi kuwepo.
Wokovu unakuja kwa kumwamini Yesu, na kutubu dhambi zako, kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la YESU KRISTO,(Matendo 2:38, Matendo 8:16), Kama hujabatizwa na unahitaji kufanya hivyo, utawasiliana nasi inbox, au tutafute katika namba hii +255789001312 / 0693036618
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Ni uthibitisho upi unaoonyesha kuwa kuna MBINGUNI na KUZIMU?
Nini maana ya neno kuchelea kama tunavyolisoma katika biblia?
Kuchelea ni hofu au wasiwasi, husanani ule unaotokana na kuzuka kwa madhara Fulani.
Kwa mfano tusome mstari huu;
2Wakorintho 11:2 Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
Hapo ni Paulo anaonyesha wasiwasi wake, kwa kanisa la Kristo kudanganywa na ibilisi haraka, na kuuacha unyofu wa moyo. Na ndio maana ukiendelea kusoma mistari inayofuata utaona Paulo, akiwatahadharisha, wasipokee injili nyingine, au Yesu mwingine au roho mwingine ambao wao hawakumuhubiri kwao..Ili wawe salama na uongo wa ibilisi.
2Wakorintho 12:20 “Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong’onezo, na majivuno, na ghasia”;
Vifungu vingine vinavyozungumzia Neno hili, ni kama vifuatavyo;
Matendo 23:9 “Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini?
10 Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome”.
(Hapo ni jemedari alikuwa anaonyesha hofu yake ya kuuliwa kwa Paulo katikati ya baraza lile)
Soma tena;
Matendo 27:29 “Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne za tezi, wakaomba kuche”.
Soma pia Wagalatia 4:11.
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tazama pia maana ya maneno mengine chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Kutahayari maana yake ni kuweka katika aibu, kuaibisha, kuaibishwa, kuaibika.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolieeleza Neno hilo;
2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli”.
Hapo ni Paulo akimwambia Timotheo, ajitahidi kuishi maisha yanayopendeza Mungu, ili asiwe na sababu ya kuona aibu katika kuitenda kazi ya Mungu. Kwamfano kama Timotheo angekuwa ni mlevi, na huku anahubiri injili, asingekuwa na ujasiri wa kuwahubiria walevi, angeona aibu, lakini akijionyesha kwa matendo yake kuwa hanywi pombe, hataona aibu kuwahubiria walevi, hata tahayari.
Vifungu vingine ni kama hivi;
2Wakorintho 7:14 “Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli”.
(Maana yake sikuaibishwa)
2Wathesalonike 3:14 “Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari”;
(Maana yake apate kuona aibu)
Ayubu 11:3 “Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya? Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha”?
(Maana yake atakayekuaibisha)
Soma pia;
Isaya 50:7 “Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya”.
2Wakorintho 7:14, Isaya 44:11.
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali angalia chini maana ya maneno mengine ya ki-biblia.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
SWALI: Sifongo na siki ni nini, alizopewa Bwana Yesu pale Msalabani?
JIBU: Tusome..
Yohana 19: 28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.
30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake”
Sifongo ni kiswahili cha neno la kiingereza “sponge” ambalo sisi tumezoea kujitaja neno hilo kama SPONCHI au SPONJI...Sasa yapo masponchi ya aina nyingi…yaliyozoeleka sana ni yale yaliyotengenezwa na malighafi ya godoro, Mara nyingi yanatumika kwa kuoshea vyombo na matumizi mengine, kwasababu yanakuwa yanauwezo wa kufyoza maji na kutengeneza povu. Enzi za zamani (za Bwana Yesu) yalikuwepo pia masponji, ambayo yalikuwa yanakaribiana sana kufanana na haya ya kwetu ya sasa. (Tazama picha chini, mfano wa sifongo za kale)
Hivyo Sifongo ni sponji. Sasa tukirudi kwenye maandiko tunasoma yule askari, alitwaa hiyo Sifongo na kulitia kwenye SIKI, na lengo la kufanya hivyo ni ili hiyo SIKI ijifyonze kwenye hiyo sifongo.
SASA SIKI NI NINI?
Siki ni kiungo ambacho kinakuwa katika kimiminika, kinachotengenezwa kwa kuchachushwa kama vile zinavyotengenezwa pombe…Na kimiminika hicho kazi yake ni kuongeza ladha kwenye chakula au kukihifadhi chakula kisiharibike…Zipo siki za aina nyingi kulingana na jamii za watu na tamaduni. Huku kwetu Afrika hususani Afrika mashariki, Siki haziwi katika mfumo wa kimiminika kizito sana…lakini nchi nyingine zinatengenezwa viwandani na kuwa kama Maji (mfano wa hizo ni zile vanilla zinazotumika kwenye ice-cream na keki ambazo zinakuwa zinahifadhiwa kwenye kachupa kadogo), na pia maeneo ya Mashariki ya kati, ikiwemo Taifa la Israeli, siki zao zilitengenezwa na Zabibu, hivyo zilikuwa hazina tofauti sana na Divai.
Kwahiyo siki iliyotumika pale msalabani ilikuwa ni kama Divai, lakini si divai kabisa…Na zilitumika katika matumizi ya vyakula. Hivyo wale askari walichovya sifongo kwenye siki na kuiweka kwenye mti, ili ifike juu pale msalabani alipokuwepo Bwana Yesu.(Tazama mfano wa siki ya divai katika picha ya juu kabisa ya somo hilo)
Na kwasababu siki kwaasili ni INA UKALI, inaukakasi na ni chungu na ina tindikali nyingi, kwa ufupi haifai kuwekwa katika kinywa cha mwanadamu kwa ukali wake, walifanya vile ili Mwili wa Bwana Yesu ukaukiwe maji…kwasababu walimsikia akisema Naona kiu.
Sasa ipo siri kubwa sana katika tukio hilo lililotendeka hapo juu msalabani, Kama utapenda kufahamu zaidi siri hiyo basi unaweza kufungua hapa >> YESU ANA KIU NA WEWE
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Mount Gerizim and Mount Ebal: Their Meaning and Spiritual Significance