Mavyaa ni nani kibiblia?(Mika 7:6)

Mavyaa ni nani kibiblia?(Mika 7:6)

Mavyaa ni nani?


Neno hilo tunalipata katika mstari huu kwenye biblia;.

Mika 7:6 “Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na MAVYAAYE; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.

7 Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia”.

Mavyaa ni Neno la kiswahili linalomaanisha mama-mkwe, – Yaani mama wa mke/mume wako.

Na kwa upande wa Baba-mkwe ni hivyo hivyo linabadilika na kuwa Bavyaa– Yaani baba wa mke/mume wako.

Hivyo kwenye mstari huo, tunapewa picha ya jinsi audui unavyoanza…Kwamba hauanzii mbali, labda kwa watu wasiotujua hapana, bali uadui wa kwanza sikuzote huanzia kwa watu nyumbani mwetu wenyewe, Lakini uadui hauji hivi hivi bali ni lazima uwe na sababu yake. Na ndio maana mstari ambao Bwana Yesu aliurejea alipokuwa anazungumzia habari za mtu kujikana nafsi yake pale anapotaka  kumfuata yeye, ulikuwa ni huu, na alisema maneno haya:

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.

Hivyo, katika wewe safari yako ya imani, (yaani umeokoka), ni lazima uweke akilini kuwa adui za kwanza kukupinga watakuwa ni watu wa nyumbani mwako, aidha watoto wako, au binti zako, au  mavyaako, au bavyaako, au kaka zako, au wajomba zako au binamu zako n.k. Usitazamie vita vikubwa kutokea mbali.

Kwasababu adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe. Hivyo ukikutana nayo ushingae, songa mbele, ishinde vita, Na Bwana atakuwa pamoja na wewe.

Tazama tafsiri ya maneno mengine ya biblia chini.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments