Neno hori lina maana mbili, maana ya kwanza ni ile inayofahamika na wengi, kuwa eneo la kulishia mifugo.
Biblia inatuambia Bwana Yesu alipozaliwa, alilazwa katika hori la kulia ng’ombe, hivyo maana ya kwanza ya neno hili ndio hiyo.
Luka 2:7 “akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni”.
Maana ya pili ya neno hori ni mkono wa bahari. Yaani eneo la bahari au ziwa lililoingia nchi kavu, tazama picha juu.
Neno hilo utalipata katika vifungu hivi;
Yoshua 15:4 “kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini. 5 Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani; 6 na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni”;
Yoshua 15:4 “kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini.
5 Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;
6 na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni”;
Yoshua 18:19 “kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na matokeo ya mpaka yalikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini”.
Waamuzi 5:17 “Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake”.
Matendo 27:38 “Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini. 39 Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana”.
Matendo 27:38 “Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini.
39 Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana”.
Lakini tukirudi kwenye ile maana ya kwanza.
Ni kwanini Yesu alizaliwa katika hori la kulishia ng’ombe na si kwenye majumba ya kifahari? Ni kwasababu alikuwa ni sadaka iliyoandaliwa kuja kuchinjwa kwa ajili ya upatanisho wa dhambi za watu mbeleni, mfano wa ng’ombe au kondoo, hivyo ilimpasa na yeye azaliwe kule, kama ishara ya utumishi wake duniani.
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. 7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tazama maana za maneno mengine ya biblia.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo:
Baghala ni nini katika maandiko?(2Wafalme 5:16).
Konzi ni nini?(Mhubiri 4:6)
Shokoa ni nini katika biblia?
https://wingulamashahidi.org/2020/09/24/rangi-ya-kaharabu-ni-ipi-kibiblia/https://wingulamashahidi.org/2020/09/24/rangi-ya-kaharabu-ni-ipi-kibiblia/
Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Shalom karibu tuyatafakari maandiko, leo tutaangazia kile kisa cha Yesu na yule mtu aliyekuwa na mapepo kule makaburini. Pengine ulishawahi kuisoma hii habari mara nyingi, lakini naomba tuisome tena kwa mara nyingine, kwasababu Neno la Mungu halina mwisho wa kujifunza (Zab 12:6). Hivyo usomapo zingatia hususani hivyo vipengele vilivyowekwa katika herufi kubwa.
Marko 5 : 1-19 “ 1 Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. 2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. 10 AKAMSIHI SANA ASIWAPELEKE NJE YA NCHI ILE. 11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. 12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. 14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. 15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. 16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. 17 WAKAANZA KUMSIHI AONDOKE MIPAKANI MWAO. 18 Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; 19 lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu”.
Marko 5 : 1-19
“ 1 Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.
2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;
3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;
4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda.
5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.
6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;
7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.
8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.
9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.
10 AKAMSIHI SANA ASIWAPELEKE NJE YA NCHI ILE.
11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.
12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.
13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.
14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.
16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe.
17 WAKAANZA KUMSIHI AONDOKE MIPAKANI MWAO.
18 Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye;
19 lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu”.
Utaona katika habari hiyo, mapepo hayo yalipokutana tu na Yesu, na kuambiwa wamtoke yule mtu, biblia inatuambia yalianza “kumsihi sana Yesu” Yalianza kumlilia na kumwomba kwa nguvu sana na kwa bidii, kwamba Bwana asiyafukuze nje ya nchi ile?.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini hayakutaka kupelekwa nje ya nchi ile?. Sio kwasababu yangeshindwa kuishi, hapana lakini ni kwasababu tayari yalikuwa yameshawezeka mambo yao mengi ya uharibifu katika mji ule, hivyo kuondolewa pale na kwenda kuanzisha uharibifu mwingine ugenini, si jambo dogo itakuwa ni hasara kubwa kwao.
Hiyo inatupa picha kuwa mapepo yamejigawanya kulingana na maeneo ya kijeografia, hivyo yale mapepo yaliyokuwa ndani ya yule mtu, yalijua mchoro mzima wa mji ule, yalijua takribani watu wote waliokuwa katika ule mji, na mipango ya kuwaangamiza.
Sasa tukirudi kwenye habari tunaona, kulikuwa na wale watu wanaochunga nguruwe pembezoni wakitazama kila kitu kinachoendelea, wakayasikia kabisa yale mapepo yakimsihi sana Bwana pale, pengine kwa nusu saa, au lisaa hatujui lakini yalikuwa yanamlilia Bwana kweli kweli, Na mwisho wa siku Bwana hakuyaondoa, aliyaacha yaendelee kubaki tu katika ule mji isipokuwa tu yamtoke yule kichaa.
Hivyo wale watu walipoona vile, wakaenda kuitana kule mijini na vijijini, sasa badala wamsihi Yesu aendelee kubaki katika ule mji ili awasaidie kwasababu maadui zao bado wapo mjini, kinyume chake wao ndio wakaanza kumsihi Yesu aondoke mipakani mwao.?
Unaona hilo? Ni sawa na kusema Ondoka Yesu, tuachie mapepo. Cha ajabu nao pia wakaiga mbinu ya mapepo, ya kusihi, wakamsihi Bwana pale pengine kwa dakika kadhaa..Na mwisho wa siku Yesu akawasikia nao pia, akapanda zake chomboni mwake akaondoka, hawakumpa hata nafasi ya kulala siku moja wala kuingia mjini maili moja, alifika pale ufukweni na kugeuza siku hiyo hiyo.
Tunajifunza nini?
Mashetani nayo yanamwomba Mungu, na Mungu anayasikia. Ukitaka kuthibitisha hilo kasome (1Wafalme 22:20-23, na Ayubu 1:9).
Hivyo yanakuwa na kibali maalumu cha kuendelea kubaki mahali fulani, au ndani ya mtu fulani. Sasa kama sisi tutakuwa ni watu wa kuukataa wokovu, ni watu wa kupinga njia za Mungu pale anapotujia kwa lengo la kutuponya roho zetu..Kamwe usitazamie kama utaweza kushindana na majeshi ya mapepo wabaya.
Wale watu waliona jinsi mapepo yale yalivyokuwa mabaya, kwanza yanawafanya watu kuwa vichaa, pili yanafanya kazi ya kuua, ndio maana utaona yalienda kuwauwa wale nguruwe ziwani, kuonyesha kuwa kazi yao kubwa ni uuaji, lakini walimkataa, Sasa kwa kuwa walimkataa Yesu wakamfukuza, yale mapepo pengine yalirudi kazini yakaenda kuwafanya vichaa wengine hata elfu kumi kwa namna ile, na kusababisha vifo vingi.
Hivyo nasi tujue kuwa tusipomsihi Yesu, mapepo yatamsihi kwa niaba yetu, na yatakuwa na haki kabisa ya kukaa ndani yetu, au katika jamii yetu, au koo zetu, kwasababu Yesu hayupo katikati yetu. Tumemfukuza atoke mjini kwetu.
Mpokee Bwana, hii dunia pasipo yeye hakuna ushindi. Shetani kazi yake ni kuharibu (1Petro 5:8-9).
Kama upo bado nje ya Kristo ni vema ukatubu dhambi zako, umrudie yeye leo, Na kama hujabatizwa basi tafuta pia kufanya hivyo mapema sana.
Bwana akubariki.
MAPEPO NI NINI?
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
AKAMSHIKA MKONO YULE KIPOFU, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI.
PALE UNAPOKUWA NA SABABU ZA KUMLAUMU MTU, UFANYE NINI?
MAJINI WAZURI WAPO?
SWALI: Je tunapaswa tushiriki Meza ya Bwana mara ngapi kwa Mwezi, au kwa Mwaka?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Ni neema ya Mungu tumeiona siku mpya ya leo, hivyo nakukaribisha tujifunze Biblia pamoja.
Kutokana na mkanganyiko mkubwa wa kila mmoja kusema ratiba yake, na kuiona kuwa ndio ipo sahihi, imesababisha kuzalika kwa madhehebu mengi, na hivyo kuzidi kuufanya ukristo uwe mgumu kueleweka zaidi kwa wale walio nje. Lakini maandiko yanasema..
2Timotheo 2;19 “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake…”.
Hivyo haijalishi kuna mkorogo mkubwa kiasi gani duniani, lakini walio wa Mungu, hawatapotea kamwe.
Tukirudi katika Maandiko tunasoma mstari ufuatao…
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu”.
Hapo biblia imesema “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu”.. Maana yake wafanye mara kwa mara ndio maana kaongezea neno “kwa ukumbusho wangu”, mbele yake. Sasa katika hali ya kawaida hata nikikupa picha yangu, nikakwambia ichukue hii kwa ukumbusho wangu..haimaanishi kwamba uichukue iangalie mara moja kisha ukaitupe.. la! Bali nimemaanisha uihifadhi, kila unaitazama unikumbuke..na hiyo inaweza kuwa kwa wiki mara moja, au kwa mwezi mara moja..lakini ni ngumu kuwa kwa mwaka mara moja..Kama ukiitazama picha yangu kwa miaka 3 mara moja, ni wazi kuwa mimi sipo moyoni mwako kwa kiwango kikubwa, ndio maana hata hamu ya kunikumbuka huna. Lakini kama nipo moyoni mwako kikweli kweli, ile picha haiwezi kupita siku mbili, au wiki hujaitazama.
Sasa katika kushiriki meza ya Bwana ni hivyo hivyo, Bwana hajaweka kwamba ni mara ngapi kwa wiki, au kwa mwezi au kwa mwaka tunapaswa tuishiriki. Lakini kwa mkristo kweli aliyezaliwa mara ya Pili, ambaye anajua umuhimu wa kuishiriki meza ya Bwana, hawezi kusubiria kulifanya hilo tendo mara moja kwa mwaka, au mara mbili au mara tatu?
Ni sawa na biblia ilivyosema katika Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia”.
Hapo biblia imesema “tusiache kukusanyika” lakini haijasema ni mara ngapi kwa wiki tukusanyike, au mara ngapi kwa mwezi au mwaka. Hivyo kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili, na anayejua umuhimu hasa wa kukusanyika pamoja..haiwezi ikapita wiki bila kuhudhuria kwenye kusanyiko pamoja na wenzake. Kanisa la kwanza walijua umuhimu wa kukusanyika na hivyo wakaona kiwango cha chini cha kukusanyika pamoja angalau kiwe mara moja kwa wiki.Na sisi tunafuata utaratibu huo huo, angalau tukusanyike mara moja kwa wiki, ili kujinoa sisi kwa sisi. Lakini Bwana Yesu hakuwapa masharti wala ratiba ya siku za kukusanyika pamoja.
Kadhalika biblia inasema “ Ombeni bila kukoma (1Wathesalonike 5:17)”. Haijatoa ratiba ya kwamba tuombe mara ngapi kwa wiki, au mwezi au mwaka.. Lakini kwa mtu aliyezaliwa kweli mara ya pili na ambaye Roho Mtakatifu anaugua ndani yake, hawezi kupitisha siku mbili hajaingia kabisa magotini…Lakini yule asiyejua umuhimu wa maombi katika maisha yake, anaweza kupitisha hata mwezi au miezi kadhaa bila kuomba kabisa.
Hivyo hata katika kushiriki meza ya Bwana, kama kweli umezaliwa mara ya pili, na unampenda Bwana, na umepata kujua umuhimu wa kushiriki meza ya Bwana, na jinsi gani tendo hilo lina madhara makubwa sana katika ulimwengu wa roho, huwezi kulifanya kwa mwaka mara moja au mara mbili.
Zipo dini ambazo ibada za kushiriki meza ya Bwana ni mara moja kwa mwaka. Na zinatumia andiko la kwamba Kristo alishiriki na wanafunzi wake mara moja tu, msimu ule wa pasaka. Hivyo na dini hizo zinasema kushiriki meza ya Bwana ni mara moja tu, na tena ni ile siku ya Pasaka.
Ndugu usidanganyike!, Meza ya Bwana tunaweza kushiriki mara kwa mara kwa kadiri tupatavyo nafasi ya kukutanika. Na sio tu meza ya Bwana ndio agizo la msingi.. Yapo na maagizo mengine yaliyo ya muhimu hivyo hivyo, kama KUTAWADHANA MIGUU. Ni lazima sisi kwa sisi tutawadhane miguu mara kwa mara tunapokusanyika pamoja, kama Bwana alivyotupa maagizo hayo. Na pia ni lazima tuwe waombaji wa mara kwa mara, angalau kila siku. Hayo yote ni kwa faida yetu wenyewe.
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?
Ni kwa nini tunasema tunamwabudu MUNGU aliye hai ,Je! wale wanaomwabudu shetani sio mungu wao aliye hai?
UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;
Konzi ni kiasi cha kujaa mkono.
Kama vile ilivyo kiasi cha kujaa ndoo kinavyoitwa debe, vivyo hivyo na kiasi cha kujaa mkono kinaitwa konzi. Tazama picha juu.
Hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo;
Mithali 30:4 “Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua”?
Mhubiri 4:6 “Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo”.
Isaya 40:12 “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani”?
Kutoka 9:8 “Bwana akawaambia Musa na Haruni, Jitwalieni konzi za majivu ya tanuuni, kisha Musa na ayarushe juu kuelekea mbinguni mbele ya Farao”.
Soma pia, Ezekieli 13:19, Walawi 2:2
Lakini biblia inatuambia pia..
Tunapokuwa na kidogo lakini kinatupa amani, ni bora kuliko kuwa na vingi lakini vya malalamiko,manung’uniko, vinyongo, hasira, au wivu.n.k.
Bwana atusaidie.
Tazama tafsiri ya maneno mengine ya biblia chini.
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mavyaa ni nani kibiblia?(Mika 7:6)
SIFONGO NA SIKI NI NINI?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Baghala kwa jina lingine ni nyumbu, lakini sio Yule nyumbu wa porini, bali ni mnyama chotara anayezalishwa kwa kukutanishwa Farasi na Punda. Tazama picha juu.
Utalisoma Neno hilo (Baghala) katika kifungu hichi.
2Wafalme 5:16 “Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. 17 Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa BAGHALA wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana”.
2Wafalme 5:16 “Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
17 Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa BAGHALA wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana”.
Zamani wana wa Israeli walikuwa wanatumia aidha punda au farasi, lakini baadaye tunakuja kuona sehemu nyingi walianza kuwatumia nyumbu katika shughuli zao nyingi, badala ya punda au farasi, kwasababu waligundua ni wavumilivu, na wagumu, na aanabeba mizigo mikubwa zaidi kuliko punda, na wanaishi mara zaidi ya farasi, japo ni wafupi kidogo ya farasi.
Hivyo sehemu zote utakazokutana nazo kwenye biblia zinamzungumzia nyumbu, basi ujue ni mnyama huyu chotara. Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu vinavyomwelezea;
Zaburi 32:9 “Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia”.
Ezra 2:66 “Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano”;
2Samweli 18:9 “Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele”.
1Wafalme 10:25 “Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka”.
Soma pia Nehemia 7:68.
Hivyo kwa kuhitimisha, ni kwamba Baghala ndio huyu nyumbu, tunaliyemsoma. Tofauti na farasi na Punda.
Ubarikiwe.
Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.
Pia ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
Njuga ni nini (Isaya 3:16, Zekaria 14:20)?
USIPIGE MATEKE MCHOKOO!
NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.
Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)
Shalom,
Bwana atusadie ili kila siku tuzidi kuujua uweza wa Mungu,
Kuna wakati Bwana Yesu aliwaambia viongozi wa dini na watu wote kuwa wanapotea kwasababu moja tu, nayo ni kwasababu hawayajui maandiko na uweza wa Mungu (Mt.22:29).
Nasi Bwana atusaidie tusipotee kwa kukosa kuujua uweza wake.
Na moja ya uweza wake ambao pengine hatuujui ni ule uwezo wa kumlipa mtu, kwa kazi asiyostahili, kwasababu tu katia mkono wake shambani mwake..
Embu tafakari ule mfano alioutoa Bwana juu ya yule mtu mwenye nyumba ambaye aliamka asubuhi ili akawaajiri watu wakafanye kazi shambani mwake, pengine saa 12 asubuhi akaenda akakutana na kundi la kwanza akapatana nalo kiasi Fulani cha fedha, biblia inasema akaenda tena saa tatu akukutana na kundi lingine limekaa tu sokoni halina kazi yoyote, nalo pia akaliambia nendeni shambani, akatoka tena sita na saa tisa, akawakuta wengine wapo hawana kazi, akawaambia nao hivyo hivyo nendeni,, na mwisho wa siku, jioni kabisa ile giza linakaribia kuingia akakutana na kundi lingine ambalo kutwa kuchwa limekaa tu, halina kazi yoyote, nalo pia akaliambia nendeni shambani, mkaangalie kazi ya kufanya,
Ni wazi kuwa hili kundi la mwisho halikukutana na kazi yoyote nzito ya kufanya kule shambani, pengine lilikuwa linakufunga funga tu viroba, viwili vitatu, kwani kazi yote ilishamalizwa na wale wengine ambao walikuwepo tangu asubuhi.
Sasa embu tengeneza picha kidogo kwenye kichwa chako, labda wale wa kwanza walipowaona wanakuja waliwacheka au kuwadharau, au kuwahurumia sana? Pengine wakanong’onezana wakisema kama sisi tutalipwa elfu hamsini hamsini, hawa watalipwa sh. Ngapi? kama sio elfu elfu, Lakini matazamio yao yalikuwa tofauti, wakati malipo yalipofika, Mwenye shamba akaja akawalipa wote, fedha sawa sawa, lakini wale wa kwanza wakamlalamikia mwenye shamba wakimwambia mbona umetulipa sawa na hawa, ambao hawajataabika kwa chochote? Lakini Bwana akawaambia maneno haya;
Mathayo 20:13 “Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? 14 Chukua iliyo yako, uende zako; NAPENDA KUMPA HUYU WA MWISHO SAWA NA WEWE. 15 SI HALALI YANGU KUTUMIA VILIVYO VYANGU KAMA NIPENDAVYO? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema”?
Mathayo 20:13 “Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?
14 Chukua iliyo yako, uende zako; NAPENDA KUMPA HUYU WA MWISHO SAWA NA WEWE.
15 SI HALALI YANGU KUTUMIA VILIVYO VYANGU KAMA NIPENDAVYO? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema”?
Unaona? Ameamua kufanya hivyo kwasababu mali ni yake na sio ya yule aliyeajiriwa..Hivyo akitoa vingi au akitoa vichache, hilo ni lake, wewe hupungukiwi kwa chochote maadamu umelipwa kile ulichokubaliana naye. Bwana aliguswa kuona tu walau wamefanya kitu fulani katika shamba lake, haijalishi wamechelewa kiasi gani.
Hata leo hii, tunapaswa tuujue huu uweza wa Mungu, ili tusijione sisi ni wadhaifu kuliko watu mashuhuri waliomtumikia Mungu huko nyuma, au wanaomtumikia sasa, tusijione sisi hatuwezi kulipwa sawa na mitume, tusijione sisi hatuwezi kulipwa sawa na manabii,..Hilo wazo tulifute, Bwana alipatana na mitume wake kuwa katika ulimwengu ujao wataketi katika viti 12 wakihukumu makabila 12 ya Israeli,
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi? 28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.
Hilo ni kweli kabisa lakini hata mimi na wewe Bwana anaweza kutuketisha pamoja nao, tukayahukumu mataifa, na mitume wasiwe na la kumlaumu Bwana. Kwasababu ni haki yake kutumia vilivyo vyake kama apendavyo. Alisema hivyo pia katika ufunuo..
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”
Hivyo ndugu yangu tusipotee kwa kutokujua uweza wa Mungu. Unaweza ukajiona umechelewa, pengine umeshakuwa mzee wa miaka 70, unajiuliza hata nikimtumikia Mungu nitakwenda kupata thawabu gani kule? Wewe itende tu kazi yake, maadamu upo shambani kwa sasa endelea kuifanya kwa uaminifu kwa huu muda mchache uliobakiwa nao..Kwasababu huujui uweza wa Mungu!..Thawabu zinatoka kwake na sio kwa mwanadamu, hivyo ukitumika kwa uaminifu, nani ajuaye utapata kilicho sawa na mitume.
Hata na sisi sote pia, kila mmoja wetu, ni kweli kuna mahali amezembea au amechelewa, kuingia shambani mwa Bwana. Amekuwa kama wale wa saa kumi na moja jioni. Sasa huu sio wakati wa kuanza kujilaumu, au kujiona hufai.. Kumbuka hata kama ungekuwa umebakisha wiki moja uondoke duniani, na umeokoka, tafuta kazi ya kufanya ya Bwana, usikae tu hivi hivi, jibidiishe, kwa lolote kwa chochote uhakikishe injili inasonga mbele. Kwasababu hata Bwana hakuwalipa watu ambao hawajafanya chochote.
Na suala la malipo muachie yeye. Ni haki yake kutumia vya kwake kama apendavyo,
Hivyo sisi tuliookoka, tuamke sasa tuanze kwa Bwana kwa hari nyingine mpya. Na wewe ambaye bado upo nje ya Kristo, mlango wa neema upo wazi, lakini hautakuwa hivi sikuzote, njoo kwa Yesu ayabadilishe maisha yako, njoo uokolewe, uoshwe dhambi zako, dunia hii inakwenda kuisha, tunaishi katika dakika za nyiongeza tu. Unyakuo wa kanisa upo karibu, jiulize ukifa leo katika dhambi utaenda kuwa mgeni wa nani huko uendako??
Hivyo tubu, na kama hujabatizwa ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako mapema kabisa, ikiwa utahitaji huduma hiyo unaweza kuwasiliana nasi,. Na baada ya hapo anza kuishi maisha yanayolingana na wokovu.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
TAFUTA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.
JE! KUNA UCHAWI KATIKA KUTENDA WEMA?
NAYE HERI AWAYE YOTE ASIYECHUKIZWA NAMI.
Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema; Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao?
KUOTA UNAJIFUNGUA.
Njuga ni kengele ndogo ndogo zinazofungwa miguuni au mikononi, na wakati mwingine shingoni, wanavishwa watoto, au watu wanapotaka kucheza ngoma, au wanyama, kama vile ngamia, na farasi n.k..tazama picha
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja Neno hilo;
Isaya 3:16 “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao; 17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao”.
Isaya 3:16 “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao”.
Zekaria 14:20 “Siku hiyo katika njuga za farasi yataandikwa maneno haya, WATAKATIFU KWA Bwana; navyo vyombo vilivyomo ndani ya nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya madhabahu”.
Kutoka 28:33 “Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote;
Kutoka 28:34 “njuga ya dhahabu na komamanga, njuga ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote. 35 Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Bwana na hapo atokapo nje, ili kwamba asife. 36 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, MTAKATIFU KWA Bwana”.
Kutoka 28:34 “njuga ya dhahabu na komamanga, njuga ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote. 35 Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Bwana na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
36 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, MTAKATIFU KWA Bwana”.
Soma pia;
Kutoka 38:25-26, Isaya 3:18.
Maana yake rohoni ni ipi?
Njuga zinafanya kazi kuu mbili, ya kwanza ni zinafungwa ili mtu au mnyama asipotee, kwasababu kule anapotembea zile kengele zinalia kumtambulisha yupo wapi. Na pili zinatumika kama zana za muziki, katika tamaduni nyingi watu wanaocheza ngoma walikuwa navaa njuga.
Vivyo hivyo kila mmoja wetu ni lazima awe amevishwa njuga za Bwana, ili tusipotee usoni pa Bwana, na pili ili kumwimbia Mungu sifa, za kweli. Hivyo anakuwa amevikwa njuga hizi, pale anapojazwa Roho Mtakatifu. Swali ni je sisi tumejazwa Roho Mtakatifu?
Tazama tafsiri ya maneno mengine ya ki-biblia chini.
Mjanja ni mtu wa namna gani kwenye biblia?(Mathayo 27:63)
Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?
Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?
Mjanja ni mtu anayetumia njia za kujifanya, ili kuwadanganya au kuwalaghai wengine. (Mtu mdanganyifu).
Makuhani walimwita Bwana wetu kwa jina hilo; walimfananisha na mtu mdanganyifu anayewalaghai watu kwa kujifanya kuwa anaweza kufufuka wakati hawezi, ili watu wamwamini pale wanafunzi wake watakapokuja kuiba maiti yake.
Mathayo 27:62 “Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, 63 wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. 64 Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza. 65 Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo. 66 Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi”.
Mathayo 27:62 “Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato,
63 wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.
64 Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.
65 Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.
66 Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi”.
Bwana hakuitwa jina hilo tu, kuna wakati walimwambia ana pepo, wengine wakamwambia amerukwa na akili”.
Hivyo hilo ni jambo la kawaida hata kwa mtakatifu kuzushiwa majina kama hayo. Lakini Bwana alishatupa taarifa hizo mapema, na hiyo ni kututhibitishia kuwa sisi ni wanafunzi wake kweli kweli, alisema;
Yohana 15:20 “Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu”.
Mathayo 10:25 “Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake”?
Tazama tafsiri ya maneno mengine chini.
Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)
Rangi ya kaharabu ni ipi kibiblia(Ezekieli 1:4,27,8:2)?
Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.
Safari ya wana wa Israeli kutoka Misri, kuelekea Kaanani, ni ufunuo kamili wa safari yetu ya Kristo kutuokoa katika dhambi na kutuingiza katika Neema ya wokovu. Musa anafananishwa na Kristo.. Kama vile Musa alivyowaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, kwa ishara na miujiza Mingi aliyokirimiwa na Mungu, ndivyo Kristo alivyodhihirishwa kwetu kutuokoa kutoka dhambini, kwa ishara na miujiza mikubwa kuliko ile ya Musa. Sasa ni kwa namna gani safari ile ya wana wa Israeli imefananishwa na safari yetu ya wokovu, unaweza kusoma binafsi kitabu cha 1Wakorintho 10:1-12.
Lakini kuna kipengele kimoja ningependa tukiangalie katika Wito huo wa kutolewa Misri kupelekwa Kaanani..na hicho tunakisoma katika mstari ufuatao..
Kutoka 8:1 “Bwana akamwambia Musa, Ingia kwa Farao, ukamwambie, Bwana asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili WAPATE KUNITUMIKIA”
Tusome tena;
Kutoka 9:13 “Bwana akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa WAENDE ILI WANITUMIKIE”.
Kupitia mistari hiyo nataka tuona sababu Nyingine ya Mungu kuwatoa wana wa Israeli kwenye utumwa wa Farao ni ipi.
Hapo tunasoma kwamba Bwana aliwatoa ili WAKAMTUMIKIE. Maana yake ni kwamba Wamefunguliwa kwenye utumwa mmoja na kupelekwa kwenye utumwa mwingine. Hawajafunguliwa na kisha kuwekwa huru tu, kutembea tembea huko la!. Bali walifunguliwa kutoka kumtumikia Farao na kupelekwa katika utumwa wa kumtumikia Mungu.
Pia tunasoma maneno hayo hayo katika…
Kutoka 10:3 “Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ILI WANITUMIKIE”.
Ndugu, ni muhimu kulifahamu hili kwasababu pia lengo la Kristo kututoa dhambini ni hilo hilo la sisi kwenda kumtumikia yeye. Anatufungua ile nira ya Adui ambayo ni ngumu, na kutuvisha nira yake iliyo laini..
Ndio Bwana Yesu alisema katika Mathayo 11:28 kwamba “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu”
SASA TUNAMTUMIKIA KWA NAMNA GANI?
Warumi 6:16 “Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. 17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; 18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki”
Warumi 6:16 “Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki”
Unapowahubiria wengine Neno la Mungu, hapo tayari umefanyika kuwa mtumishi wa Mungu..Unakuwa unamtumikia Mungu, na Mungu atakuheshimu..Na kumtumikia Mungu sio tu kuwa mchungaji, au Mhubiri mkubwa, au Nabii au Mtume. Hapana…popote pale ambapo unaweza kufaa katika kulitangaza Neno..Katika nafasi hiyo, tayari unamtumikia Mungu. Hakunaga karama ya Mhubiri Mkubwa, au Nabii Mkuu, au Mchungaji mkuu, au Mwalimu mkuu…kama ni mhubiri ni mhubiri mbele za Kristo wote ni sawa, kama ni mwalimu ni mwalimu mbele za Kristo wote wanaheshimika sawa n.k. Aliye nabii mkuu ni Yesu mwenyewe, aliye Mwalimu Mkuu ni Yesu pekee, aliye Mtume Mkuu ni Yesu pekee..wengine wote haijalishi wingi wa wafuasi walionao…wote mbele ya Kristo wanafanana.
Hivyo kwa hitimisho ni muhimu kufahamu tumetolewa dhambini ili tukamtumikie Mungu na si tukajitumike wenyewe au tukautumikie ulimwengu. Ndio maana wana wa Israeli hatua ya kwanza baada ya kutolewa Misri, walipelekwa nyikani kupewa sheria na amri za Mungu..Na walipoingia kaanani Bwana aliwapa jukumu la kuwafundisha wana wao na vizazi vyao vilivyokuja juu ya sheria, amri na hukumu za Mungu. Na sisi wa sasa tunalo jukumu hilo hilo baada ya kuokoka.
Umeokoka, nenda kamtumikie Mungu..kwa kuwafundisha wengine uliyojifunza.
Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”
Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”
Maran atha!
Kutoka 10:1 “BWANA anasema atampa Farao moyo Mgumu, asimtii, je! hapo Bwana Atamhukumu Farao kama mkosaji siku ile?”
Konde la Soani ni nini? (Zaburi 78:12,43)
Bildi ni kitu cha kupimia kina cha maji,Mara nyingi huwa ni kamba ambayo wanaifungia kitu kizito kwenye moja ya ncha zake, kisha wanakishusha kitu hicho kwenye maji, aidha ya mto, au ya ziwa, au ya bahari. na moja kwa moja mpaka kwenye sakafu ya bahari. Kikishafika kule wanapima urefu wa kamba ile na hapo ndipo wanapojua bahari hiyo ina urefu wa kina gani.
Neno hilo utalipata, katika ile habari ya mtume Paulo alipokuwa akisafirishwa kama mfungwa kuelekea Rumi. Kama vile tunavyoijua habari, walipokuwa katikati ya safari yao bahari iliwachafukia sana, mpaka wakakata tamaa ya kuishi, wakakaa siku nyingi bila kuona jua wala nyota. Lakini kama baada ya siku 14 walifika mahali ambapo walihisi kama kuna nchi kavu mbele yao, hivyo ikabidi wajaribu habati yao kwa kupima kina cha maji sehemu mbili tofauti ili waone kama ni kweli kina ndio kinapungua au kinaongezeka..
Hapo ndipo wakatupa bildi hizo kwenye maji, walipotupa ya kwanza ikapima urefu wa “pima” 20, (Pima moja ni sawa na futi 6), hivyo urefu wa kwanza ulikuwa ni futi 120.
Wakaenda mbele kidogo wakatupa bildi nyingine tena, wakapata pima 15 ambazo ni sawasawa na futi 90. Hapo ndipo walipogundua kuwa kina cha bahari kinapungua na kwamba wapo karibu na nchi kavu. Ikawabidi watie nanga, wasisogee popote tena mpaka kukuche.
Matendo 27:27 “Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu. 28 Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano. 29 Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne za tezi, wakaomba kuche.”.
Matendo 27:27 “Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu.
28 Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano.
29 Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne za tezi, wakaomba kuche.”.
Hata sisi wakristo kila mmoja rohoni anapaswa awe na bildi ya kuipima safari yake akiwa hapa duniani.
Ni lazima tupime mienendo yetu, kila wakati, je namna ya maisha tunayoishi leo na jana tofauti yake ni nini?. Ikiwa hali ya maisha tunayoishi leo ndio inatufanya tuende mbali zaidi na Mungu, tupoe kiroho kuliko ilivyokuwa hapo jana..Hapo tunapaswa tuchukue maamuzi ya haraka sana ya kubadili mfumo wa maisha yetu, ili tusiendelee mbele kwenye madhara zaidi. Tukapotea moja kwa moja.
Lakini kama tutaishi maisha ambayo kila siku yanatutupa mbali na Mungu na bado tunaona ni sawa tu, tunaruhusu yaendelee hivyo hivyo , tujue kuwa mwisho wetu utakuwa ni mbaya sana.
Swali ni je mara ya mwisho kuishusha bildi yako ni lini?
Mkomamanga ni nini? Na katika biblia unawakilisha nini?
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.