Category Archive Home

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).

Jina la Bwana wetu na Mwokozi wetu, Yesu Kristo libarikiwe…Karibu katika kuyatafakari maandiko, tumekwisha kuvipitia vitabu kadhaa vya Mwanzo, naomba kama hujavipitia na ungependa kuvipitia, basi fungua hapa >> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Leo kwa neema za Bwana tutasonga mbele kitabu kingine kimoja, ambacho ni kitabu cha Zaburi.

Kitabu cha Zaburi ndio kitabu kirefu kuliko vitabu vyote katika biblia, na ndio kitabu ambacho kipo katikati ya Biblia. Sehemu kubwa ya kitabu hichi imeandikwa na Mfalme Daudi, mwana wa Yese.  Lakini sio Milango yote imeandikwa na Daudi, la!..milango mingine imeandikwa na Sulemani, Mfalme Hezekia, Asafu,Musa, Ethani na Hemani.

Kitabu hichi kimeandikwa katika mfumo wa beti za nyimbo. Kwasababu maana tu ya neno lenyewe Zaburi ni “Nyimbo takatifu zilizoimbwa kwa vyombo vya muziki vya nyuzi nyuzi, kama vile santuri, kinubi na zeze”. Kama utapenda kuvijua vyombo hivyo vya nyuzi nyuzi vya muziki kwa urefu utatutumie ujumbe inbox.

Hivyo nyimbo hizi za Zaburi, ziliandikwa si kwa lengo la kuburudisha bali kwa lengo la kumshukuru Mungu, kumtukuza Mungu, kumwomba Mungu, kumsifu Mungu, kuomba ulinzi na haki .

Mfalme Daudi alizitunga nyimbo hizi katika kipindi chote cha maisha yake aliyoishi (yaani miaka 70). Hivyo hakikuandikwa kwa siku moja, au wiki moja. Kila hatua ya maisha Daudi aliyoipitia Roho ya Mungu ilishuka juu yake na kumsukuma kuandika beti za nyimbo hizo, ambazo leo tunazisoma katika biblia.

Sasa swali ni kwanini zimeandikwa katika mfumo wa Nyimbo?

Ikumbukwe kuwa Daudi tangu akiwa mdogo alikuwa na kipaji cha kupiga filimbi na kinubi..Hivyo alijifunza kumwimbia Mungu tangu akiwa mdogo, na kipaji chake hicho Mungu alichompa, kuna kipindi kilivuma mpaka hadi kikamfikia Mfalme Sauli..

1Samweli 16:14 “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua.

15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.

16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona.

17 Basi Sauli akawaambia, VEMA, NITAFUTIENI MTU ALIYE STADI WA KUPIGA KINUBI, MKANILETEE.

18 Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, ALIYE STADI WA KUPIGA KINUBI, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye.

19 Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo……….

23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, NDIPO DAUDI AKAKISHIKA KINUBI, AKAKIPIGA KWA MKONO WAKE, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha”.

Hivyo kipaji hicho cha kupiga vinubi na kuimba, alichokuwa nacho Daudi, aliendelea kukitumia mpaka anaondoka Duniani.

Sasa ni Mazingira gani aliyokuwa mfalme Daudi wakati anaandika hizo Zaburi.

Daudi hakuwa anakaa tu ndani, na ghafla anaanza kujikuta anaandika nyimbo hizo.  Hapana, mfano wa mazingira aliyokuwa anaandika beti hizo, ni wakati labda ametoka vitani na Mungu kampa ushindi dhidi ya maadui zake ambao pengine walikuwa ni hodari kupita wao, hivyo ile furaha anayoipata na huku anaona kama sio Mungu wasingeshinda, ile furaha inamsukuma kuandika nyimbo za kumshukuru Mungu.

Kwamfano hebu tuziangalie beti chache za Daudi katika Zaburi kasha tuzitafute ziliandikwa kipindi gani.

Tuanze na Zaburi ya 105, inasema hivi..

Zaburi 105:1 “Haleluya. Mshukuruni Bwana,liitieni jina ,Wajulisheni watu matendo yake.

2 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote.

3 Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.

4 Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote ”

Je ni kwamba Daudi alikaa tu ndani?..na akachukua tu kalamu na karatasi kuandika ubeti huo?..Jibu ni la!..Ubeti huo uliandikwa kipindi Mfalme Daudi Analitoa sanduku la Agano kwa Obed-odemu kwenda mjini kwake yaani (Yerusalemu).. Hivyo kwa furaha kubwa wakati sanduku la agano linaingia tu mjini mwake, alicheza mpaka nguo zikamtoka, na alilisindikiza Sanduku hilo la agano, kwa nyimbo nyingi za santuri na vinubi…

Tusome…

1Nyakati 15:25 “ Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na maakida wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la agano la Bwana kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;

26 hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Bwana, wakachinja ng’ombe saba, na kondoo waume saba.

27 Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

28 Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.

29 Hata ikawa, sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake”.

Sasa tukiendelea mlango wa 16 kuanzia mstari wa 9 ndiyo tunaiona Zaburi hiyo ya 105 ilipotokea.

Tusome..

1Nyakati 16:1 “Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana.

3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.

4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;

5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;

6 nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu.  7 Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze.

8 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake.

9 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote.

10 Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.

11 Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.

12 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;

13 Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

14 Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake.

15 Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.  16 Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka;

17 Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele”

Umeona?..Kwahiyo Zaburi hazikutungwa tu pasipo sababu yoyote, bali zilitungwa kila baada ya tukio fulani la ki-Mungu lililotokea katika maisha ya Daudi. Zaburi zote 150, zilindikwa kwa msukumo wa Roho baada ya tukio fulani la ki-Mungu.

Zaburi nyingine Daudi aliziandika, baada ya kuokoka kimiujiza kwenye mikono ya Sauli aliyekuwa anatafuta kumuua, hivyo akaandika nyimbo hizo kumshukuru Mungu. Na sehemu kubwa ya Zaburi ya Daudi aliandika baada ya kupata ushindi dhidi ya Maadui zake (Yaani mataifa yaliyokuwa yanafanya vita dhidi ya Israeli)

Lakini pamoja na hayo nyimbo hizo za Zaburi, licha tu ni nyimbo katika mfumo wa maombi, shukrani, sifa  n.k. kwa Mungu lakini pia zina unabii ndani yake.

Na unabii wa kwanza na Mkuu ziliobeba ni unabii wa kuja kwa Masihi, yaani Yesu Kristo, na unabii wa Wana wa Israeli kuchukuliwa mateka Babeli.

  • Kitabu cha Zaburi pekee ndio kimetabiri neno la Mwisho la Bwana Yesu pale Kalvari alilosema “Mungu wangu..Mungu wangu mbona umeniacha. Kasome Zaburi 22:1, linganisha na Marko15:34”.
  • Kadhalika kitabu cha Zaburi pekee ndicho kilichotabiri usaliti wa Yuda, hakuna kitabu kingine kilichozungumzia usaliti wa Yuda zaidi ya hichi cha Zaburi..

Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”. Linganisha na maneno ya Bwana Yesu katika Yohana 13:18

Yohana 13:18  “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake”.

  • Pia kitabu hichi ndio kitabu pekee kilichotabiri juu ya mavazi ya Yesu kupigiwa kura na wale askari pale msalabani…

Zaburi 22:18 “Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura”…Linganisha na Mathayo 27:35

  • Kitabu cha Zaburi  pia ndio kitabu pekee kilichotabiri kufufuka kwa Bwana Yesu, na kwamba Kristo hataona uharibifu soma..Matendo 2:27-33. Hakuna kitabu kingine chochote kilichotabiri kufufuka kwa Yesu, hata kitabu cha Isaya hakikutabiri.

Hivyo kitabu hiki kwa sehemu kubwa kimebeba Ufunuo juu ya Yesu..Ndio maana Baada ya Yesu kufufuka alitaja kuwa yote aliyoandikiwa katika Zaburi na torati lazima yatimie..

Luka 24:44  “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi”

Mbali na hayo, Kitabu cha Zaburi kinatufundisha Mambo yafuatayo.

  • Kuomba: Zab. 51 ni mfano wa zaburi inayotufundisha sisi namna ya kuomba na kujisongeza mbele za Mungu kwa unyenyekevu.
  • Kumshukuru Mungu:
  • Kumsifu Mungu; Kwamba tunapaswa tumsifu Mungu sio tu kwa midomo mikavu bali kwa kumwimbia kwa vinanda vya nyuzi kumi, na vinubi na santuri…Kwa nyakati zetu hizi ni kwa kutumia vyombo vyote vya muziki kama guitar,vinanda, matarumbeta, piano n.k. na kwa nguvu sana pamoja na vigelegele vya shange na nderemo.(Soma Zab.33:2, Zab 144:9).
  • Kumtegemea Mungu, na kutohofu chochote: “ Zab. 23:4 Nijapopita kando ya bonde la uvuli wa mauti sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja nami” na “Zab. 27:1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nao

Bwana akubariki.

Usikose mwendelezo wa vitabu vinavyofuata…

Maran atha!

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

UFUNUO: Mlango wa 1

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

NA BAADA YA LILE TONGE, SHETANI AKAMWINGIA.

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

Biblia inaziorodhesha bahari kuu nne, tuzisome;

1 ) Bahari ya shamu: Kwa sasa inajulikana kama bahari nyekundu, (Kwa kiingereza red sea). Hii ni ile bahari ambayo wana wa Israeli waliivuka baada ya Mungu kuipasua pale walipokuwa wanafuatiliwa na maadui zao, ambapo tunaona baadaye walikuja kumezwa na bahari ile.

bahari ya shamu

Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji”.

2) Bahari kubwa , au bahari ya Wafilisti, (Kutoka 23:31): Kwasasa inajulikana kama habari ya Mediteranea. Ipo upande wa Magharibi wa taifa la Israeli. Hii ndio bahari kubwa kuliko zote zinazoorodheshwa kwenye biblia.

bahari kubwa, ya wafilisti, au mediterenia

Hesabu 34:6 “Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; hii ndiyo mpaka wenu upande wa magharibi”.

Soma pia Yoshua 9:1, 15:47, 23:4, Ezekieli 47:19

3) Bahari ya Galilaya; Au kwa jina lingine Bahari ya Tiberia, au ziwa la Genesareti au Bahari ya Kinerethi Yoshua 12:3, 13:27, 34:11. Hii ndio ile bahari ambayo Bwana Yesu alitembea juu ya maji.

bahari ya galilaya

Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,”

Mathayo 4:18 “Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi”.

4) Bahari ya chumvi: Hii ni habari ndogo sana, ambapo ipo chini ya mto Yordani, maji yake ni ya chumvi nyingi sana, jambo ambalo linaifanya bahari hiyo isiwe na kiumbe wa kuishi ndani yake kama samaki, sehemu nyingine wanaiita ‘bahari mfu’(Dead Sea)

bahari ya chumvi

 Hesabu 34:3 “ndipo upande wenu wa kusini utakuwa tangu bara ya Sini kupita kando ya Edomu, na mpaka wenu wa kusini utakuwa tangu mwisho wa Bahari ya Chumvi kuelekea mashariki”;

 Kumbukumbu 3:17, Yoshua 15:2.

Shalom, tazama maeneo mengine mbalimbali ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)

JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)

Maana ya Neno Sharoni ni “uwanda” au “nchi tambarare”. Katika biblia, tunaona lipo eneo (wilaya) lililojulikana sana na waisraeli kama Sharoni, japokuwa biblia haijatolea maelezo yake mengi, Lakini ni eneo lililokuwa na rubuta nyingi, na lilikuwa lipo karibu na fukwe za ile bahari kubwa(yaani bahari ya Mediterenia), tazama ramani.

Utalisoma Neno hilo kwenye vifungu hivi vya biblia;

1Nyakati 5:16 “Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake”.

1Nyakati 27:29 “na juu ya makundi ya ng’ombe waliolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya makundi waliokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai”;

Isaya 33:9 “Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani”.

Isaya 65:10 “Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta”.

Na katika agano jipya utalisoma katika kifungu hichi;

Matendo 9:35 “Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana”.

UA LA UWANDANI

Lakini tukisoma kitabu cha wimbo ulio bora, tunaona, lipo Ua moja linatajwa kama Ua la Uwandani, au kwa jina lingine Ua la Sharoni (Rose of Sharon). Mwandishi wa kitabu hichi, anajifananisha yeye na Ua hilo ambalo limechipuka katika nchi hiyo ya Sharoni.

Wimbo 2:1 “Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni.

2 Kama nyinyoro kati ya miiba, Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti”.

Na bila shaka Ua hili ni Kristo, yeye ndiye aliyechipuka katika bonde la ulimwengu, na uzuri wake, na mwonekano wake ulikuwa ni tofauti na mwanadamu yoyote ulimwenguni. Yeye ndiye aliye Nuru ya ulimwengu, yeye ndiye aliyeiondoa harufu mbaya ya huu ulimwengu wa dhambi, hata tukapata kibali cha kumkaribia Mungu, yeye ndiye mwokozi wa ulimwengu.

Je! Na wewe umeliona Ua hilo?, Je umempata mwokozi moyoni mwako? Kumbuka hakuna njia nyingine yoyote utakayoweza kumfikia Mungu isipokuwa kwa njia yake yeye. Hakuna mwanadamu yoyote anayeweza kumpendeza Mungu kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa Yesu Kristo peke yake. Ukimkosa Kristo maishani mwako, haijalishi umepata ulimwengu mzima, hesabu kuwa umepoteza kila kitu. Lakini ukimpokea yeye, hata ukikosa vyote hesabu kuwa umevipata vyote.

Uamuzi ni wako,  kumbuka hizi ni siku za mwisho, Lakini ikiwa leo utapenda kuyakabidhi maisha yako kwake, Huo utakuwa ni uamuzi wa busara sana, Basi fungua hapa kwa ajili ya maelekezo ya Toba>>>  SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Uwanda wa dura ni nini?

Konde la Soani ni nini? (Zaburi 78:12,43)

Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)

Jaa ni nini katika biblia?

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

LANGO LIMEBADILIKA.

Ezekieli 44:1 “Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa.

2 Bwana akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa”.

Shalom,

Kwa jinsi tunavyozidi kuishi hapa duniani ndivyo dunia inavyozidi badilika kwa kasi sana mbele ya macho yetu, na haibadiliki kuelekea pazuri, bali inabadilika kuelekea pabaya..Inabadilika kuelekea kwenye maovu mengi zaidi…Maovu ya jana ni heri kuliko ya leo…Na hiyo ndiyo inayopelekea wokovu kuwa mgumu kupatikana mioyoni mwa watu siku baada ya siku.

Ukitazama mistari hiyo, ambayo iliandikwa katika agano lake, na nabii Ezekieli inazungumzia juu ya unabii wa Masihi siku atakapokuja na kuingia hekaluni kupitia lango la mashariki, unabii huo upo mwilini na rohoni, lakini lengo leo sio kuzungumzia habari hizo .. Nachotaka uone ni huyo ujumbe uliopo hapo, kwamba, hilo lango lipo wazi lakini siku moja litafungwa, na likishafungwa kamwe halitakaa lifunguliwe tena daima.. Huo ndio ujumbe, Na wote tunajua kuwa lango hilo ni Neema ya wokovu.

Sasa   tukirudi kipindi cha agano jipya, tunaona  tena Yesu akilitaja lango hilo, lakini safari hii yeye halitaji tena kama “Lango”Kana kwamba ni kubwa sana.. bali analitaja kama mlango, na tena sio mlango tu, bali ni mlango mwembamba sana..tusome..

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango,…..”.

Unaona? Sasa utajiuliza ni nini kimetokea mpaka sio lango tena bali ni mlango?

Ni kwasababu majira yanabadilika, Mlango wa mbinguni tangu zamani, Mungu aliukusudia uwe mpana ili watu wote waingie na ndivyo ulivyo, alikusudia uwe mwepesi kwa watu wote na mataifa yote kuuingia, ni LANGO pana sana. Hilo ndio lengo la Mungu hata sasa, Mungu hawezi kumminya mtu kwa makusudi kwamba akipate kile kitu kwa shida, sasa atufanyie hivyo ili iweje?.

Lakini kutokana na maovu na mambo mengi yaliyopo ulimwenguni sasa imepelekea mlango huu kuwa mwembamba sana, na hyo ni kutokana na kuzuka kwa milango mingine mingi sana ya upotevuni, na watu wamekuwa wakiiangalia kwa hiyo, na kusahau lile lango moja tu la Mungu.

Ndugu yangu, hizi ni nyakati mbaya sana tunazoishi, leo utaudharau wokovu wa Yesu Kristo, lakini alishatabiri kuwa kuna siku ataufunga mlango huu, na siku hiyo utakapofungwa ndipo watu watakapogundua kuwa walikuwa wanapuuzia kitu cha msingi sana, cha uzima wa roho zao.. Ndipo watakapoanza kubisha wafunguliwe, kumbe hawakujua  kuwa lango hilo likishafungwa mara moja, halitafunguliwa tena daima. Kitakachofuata baada ya hapo ni majuto makubwa sana ambayo hayajawahi kutokea duniani kote.

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.

29 Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.”

Hivyo wokovu sio wa kukwepwa, injili si ya kudharauliwa wala kupuuziwa kabisa, huu si wakati wa kumwangalia jirani, au ndugu, au mzazi, katika suala lako la wokovu, Ni wakati wa kumkimbilia Kristo na kumwangalia yeye tu, kwasababu muda uliobakia ni mchache, nani ajuaye lango hilo litafungwa leo usiku, au kesho asubuhi. Jiulize Unyakuo ukipita leo halafu ukabaki, na injili zote hizo ulizosikia, na mafundisho yote hayo uliyofundishwa na kujifunza, utaenda kujibu nini mbele ya kiti cha hukumu.

Usikubali kusongwa na jambo lolote, huu mlango umeshakuwa finyu sana.  Kuiingia sio mrahisi tena kama tunavyodhani, hivyo  ni wakati wa kufanya maamuzi magumu, wa kukubali kujitwika msalaba na kumfuata Yesu, na uwe tayari kwenda kubatizwa na  kupokea Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki sana.

Ikiwa bado hujabatizwa, na utapenda kupata huduma hiyo ya ubatizo, au kumpa Kristo maisha yako, basi wasiliana nasi inbox au kwa namba hizi +255789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?

NI NANI ANAYEUFUNGA MLANGO WA MAARIFA?.

YONA: Mlango 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)

Bisi ni nini?


Kama wengi tunavyofahamu bisi kwa mazingira yetu ni yale mahindi yanayokaangwa na kufutuka na pale yanapobadilika na kuwa na mwonekano mwingine (mweupe mweupe ) huliwa. Kwa wengine wamezoea kuyaita Popcorn lugha ya kigheni. Tazama picha kushoto.

Lakini kwa wayahudi, na jamii nyingi za watu wa mashariki ya kati, bisi zao haziwi kama hizi zetu za mahindi bali zao zinakuwa za ngano, na zinakaangwa vile vile kama zinavyokaangwa za mahindi isipokuwa tu  mwonekano wake haubadilika sana, kama ulivyo  wa mahindi.

Kuona jinsi inavyoandaliwa na mwonekano wake, tazama video hii >>>

https://www.youtube.com/watch?v=5fSY4YCVSoM

bisi za nganoHivyo mahali popote unapokutana na neno hili Bisi kwenye biblia basi ujue ni hii inayotengenezwa kwa ngano, na sio mahindi.

Kwamfano ukisoma biblia, utaona, Mungu anawapa wana wa Israeli maagizo kuwa pindi watakapovuna mavuno yao ya kwanza, wasile kwanza chochote katika walichokivuna, ikiwemo bisi, au masuke, mpaka watakapoleta kwanza kile kinachomstahili Mungu.

Walawi 23:14 “Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote”.

Utalisoma Neno hilo tena katika vifungu hivi;

Ruthu 2:14 “Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza”.

1Samweli 17:17 “Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako;

18 ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao.

1Samweli 25:18 “Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.

19 Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.

Yoshua 5:10 “Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko.

11 Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo”.

Soma pia, 2Samweli 17:28,

Je! Tunapaswa tukumbuke nini, kila tunapolisoma hili Neno?

Ni kwamba hata sisi, kwa kila Mungu anachotubariki, tusifikirie kula kwanza, mpaka tutakapohakikisha fungu la Mungu tumelitenga na kulitoa. Biblia imetumia neno bisi,  kwasababu ni chakula chepesi sana kukipika, ni kitendo cha kuweka kwenye sufuria na kukikaanga na kula, jambo ambalo halihitaji maandalizi mengi kuandaa, tofauti na vyakula vingine vya ngano, hii ikiwa na maana kuwa mtu anaweza kuvuna shamba lake, na hapo hapo akaenda kuchukua ngano hiyo na kukaanga mara moja na kula. Lakini hata hivyo Mungu kakataza. .. Hivyo na sisi, hatupaswi kufikiria kutumia hata  kwa vocha au kwa chipsi kile Mungu anachotubariki, kabla hatujalitenga fungu lake pembeni.

Hivyo ndio Mungu atakavyotubariki.

Shalom.

Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.

Pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Masuke ni nini? (Luka 6:1, Marko 4:28)

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Choyo ni nini kibiblia? (Luka 12:15, Zaburi 10:3)

USITAFUTE KUKANWA NA BWANA SIKU ILE.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

Rudi Nyumbani:

Print this post

Jaa ni nini katika biblia?

“Jaa” ni nini katika biblia?

Jaa ni mahali ambapo uchafu unalundikwa, na uchafu huo unaweza kuwa ni kinyesi cha wanyama (yaani mbolea), au uchafu unaotokana na shughuli za kibinadamu (matakataka). Hivyo Jaa ni kama kifupi cha jalala tu.

Katika biblia tunaona neno hili likitumika..

Zaburi 133: 7 “Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani”.

Maana yake Bwana anaweza kumpandisha mtu kutoka majalalani na kumpandisha juu.

Ezra 6: 11 “Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili”.

Isaya 25: 10 “Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika MAJI YA JAA

Pia unaweza kusoma Danieli 2:5, Danieli 3:39, Maombolezo 4:5 na 1Samweli 2:8.

Katika Agano jipya neno hili limetumika mara moja tu, na Bwana Yesu Kristo katika kitabu cha Luka..

Tusome..

Luka 14:34  “Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?

35  Haiifai nchi WALA JAA; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie”

Kinyesi cha wanyama kikizidi kuharibika kinafaa katika mbolea, watu wanakikusanya na kukifunya mbolea baadaye, hali kadhalika takatata nyingine zote zinavyozidi kuharibika huwa hazikosi matumizi, zinaweza hata kutumika katika kuzalishe gasi ya asili, ambayo itatumika kama nishati..

Lakini chumvi ni kitu cha ajabu, ikishaharibika huwezi kuitumia kwa matumizi yoyote yale, huwezi kuitumia kwenye chakula, wala huwezi kuitumia kama mbolea, wala huwezi kuilundika pamoja na kutengeneza jalala na kuzalisha gesi, …Kwaufupi inakuwa kama mchanga tu..

Sasa Bwana Yesu alitufananisha sisi, tuliompokea yeye na chumvi..

Mathayo 5:13  “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

14  Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima”.

Umeona? Bwana anatuonya, tujihadhari tunavyoenenda katika hii dunia, matendo yetu yasije yakatuharibia sifa zetu moja kwa moja, hata tusifae tena mbele za Mungu na wanadamu.

Kwa urefu juu ya somo hili la chumvi fungua hapa >> NYINYI NI CHUMVI

Je umempokea Yesu?..Kama bado, Kristo yupo mlangoni kurudi kulinyakua kanisa lake, biblia inasema atakuja kama mwivi usiku wa manane, maana yake ni hii, wakati watu na ulimwengu unahisi bado sana, kumbe huo ndio wakati wa kurudi Kristo kulichukua kanisa lake,

Swali ni je!..Bwana Yesu akija leo, una uhakika wa kwenda naye mawinguni?. Kama huna uhakika basi huo ni uthibitisho kwamba hutaenda naye atakapokuja. Hivyo tubu leo kwa dhati na amua kuanza maisha mapya na Kristo, naye atakupokea na kukupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Husuda, faraka na uchafu?

IMANI NI KUWA NA UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO.

IJUE NGUVU YA IMANI.

KILA KIUNGO LAZIMA KISHUGHULIKE.

TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

NYAYO TUNAZOPASWA KUZIFUATA.

Shalom, Jina la Bwana Yesu libarikiwe, karibu tuyatafakari maandiko pamoja..

Ukifika mahali umepotea, na huoni mtu hata mmoja mbele yako wa kukupa msaada, lakini unapotazama chini, unaona nyayo za miguu zinaelekea upande fulani..bila shaka hatua inayofuata ni kuzifuata hizo nyayo, kwasababu unajua mwisho wa hizo nyayo ni kumfikia huyo mtu alipo.

Na Kristo sasa hayupo hapa duniani kwa namna ya mwili, yupo juu mbinguni..lakini katuachia nyayo…ambazo katika hizo tukizifuata tutamfikia yeye na kumwona macho kwa macho.

Sasa nyanyo hizo ni zipi?

Neno la Mungu linasema..

1Petro 2:20  “Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.

21  Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, AKAWAACHIA KIELELEZO, MFUATE NYAYO ZAKE.

22  Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.

23  YEYE ALIPOTUKANWA, HAKURUDISHA MATUKANO; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki”.

Tunapokuwa wapole kama Yesu alivyokuwa hapo tunaziendea nyayo zake, katika hii dunia iliyojaa upotofu, tunapostahimili mabaya, tunapotukanwa haturudishi majibu kama yeye, tunapoudhiwa ni lazima tusamehe..hapo tunazifuata nyanyo zake..na tutakapomaliza mwendo tukiwa tumezifuata nyayo hizo ni lazima tutamfikia hatutapotea.

Lakini sasa kuna nyayo nyingi duniani, kila mtu anatengeneza nyayo zake…mfano wa nyayo potofu ni hizi zinazosema… “mpende akupendaye, asiyekupenda mchukie”.. Hizi ni nyayo ambazo zinaonekana ni za faraja na za kujilinda, lakini ni nyayo potofu, mwisho wake ni upotevuni…Mwisho wake ni ziwa la moto.

Hivyo tusijifanye tunajua kumsahihisha Bwana Yesu Kristo na kufikiri, hakupaswa kuwa mpole vile… Siku zote fahamu kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kuwapoteza maadui zake pale kwa dakika moja tu, wala hakuna mtu ambaye angeweza kumgusa. Lakini hakuutumia huo uwezo kwasababu lengo lake ni hao watu watubu kwa wema wake..

Ndicho kitu Yesu anachotaka kwetu pia, kwamba kwa wema wetu, wengi wavutwe kwake…Lakini kama tukijiona kwamba sisi tuna ufunuo kuliko yeye, kwamba hatupaswi kuwa wapole, na wanyenyekevu, hatupaswi kuwa watu wa kusamehe wanaotuudhi,  hizo njia tunazoziendea tutajikuta kwenye ziwa la moto.

Mathayo 26:51  “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

52  Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.

53  Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?”

Soma tena..

Luka 9:52  “akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.

53  Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.

54  Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?

55  Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]

56  Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”.

Bwana atupe macho ya kuona nyayo zake, na kuzifuatia katika Jina la Yesu.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Neno kuwiwa maana yake ni “kudaiwa”.  Mtu anaposema ninawiwa kiasi fulani cha fedha maana yake ni “anadaiwa kiasi fulani cha fedha”, Au mtu anaposema ninamuwia mtu fedha, maana yake ni “anamdai mtu kiasi fulani cha fedha”. Hivyo kuwiwa/kuwia ni neno la kiswahili cha zamani lenye maana ya kudai au kudaiwa.

Katika biblia tunaona mifano kadhaa ambapo neno hili lilitumika.

Mathayo 18: 22  “Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

23  Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

24  Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.

25  Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni

26  Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

27  Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni”.

Mistari mingine katika biblia yenye neno hilo “kuwiwa” ndani yake ni Luka 16:7 na Warumi 13:8.

Mbali na hilo, Biblia inatufundisha kuwa baada ya kuokoka na sisi pia tunakuwa na deni la kwenda kuwapelekea wengine habari za wokovu. Hivyo tunakuwa TUNAWIWA na watu wa ulimwengu habari za wokovu.

Hivyo hatuna budi kuipeleka injili kwa wengine, ambao wapo nje ya wokovu, kwa karama zetu, kwa  mali zetu na kwa nguvu zetu, kwasababu hilo ni deni kwetu.

Kama Mtume Paulo alivyosema mahali fulani kwamba ANAWIWA na watu wa aina mbali mbali, katika kuwapelekea injili..

Warumi 1:13  “Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.

14  NAWİWA NA WAYUNANİ na wasio Wayunani, NAWİWA na wenye hekima na wasio na hekima.

15  Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi.

16  Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Hivyo pia na sisi baada ya kuokoka ni wajibu wetu, kuipeleka injili kwa watu ambao hawajaokoka, roho zao ni deni kwetu, kwahiyo ni lazima kuwapelekea habari njema za wokovu pasipo kuionea haya injili, kwasababu injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu.

Marko 16: 15  “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16  Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?

Akawaambia Enendeni ulimwenguni mwote,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE.(Marko16:15.) Yesu Anamaanisha nini kusema MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?

EPUKA KUTOA UDHURU.

BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu;?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Hirimu ni nini kibiblia?(Wagalatia 1:14)

Hirimu ni nini?


Hirimu ni mtu aliye katika kundi la umri wako (rika). Kwamfano tukisema, Petro na Yohana ni hirimu moja, tunamaanisha Petro na Yohana ni watu wa umri mmoja.

Lakini kibiblia hirimu linakwenda mbali kidogo  zaidi ya hapo, mahali pengine linamaanisha kijana mdogo.

Kwamfano mistari hii inazungumzia hirimu kama mtu wa umri mmoja naye.

Danieli 1:10 “Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme”.

Hapo ni Yule mwangalizi wa Vijana, towashi akiwaeleza akini Danieli hofu yake juu kukunjamana sura zao, pale vijana wenzao wa rika lao watakapoitwa nyumbani kwa mfalme na kuonekana wananawiri kushinda wao, atauliwa yeye.

Soma tena..

Wagalatia 1:14 “Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.

15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,”

Hapo mtume Paulo anazungumzia jinsi alivyofanya bidii ya kuzishika dini za kiyahudi kuliko hata watu waliokuwa wa rika lake, au umri wake, vijana wenzake.

Lakini katika vifungu hivi, vinalitaja neno hili, vikimaanisha kijana mdogo.

Waamuzi 8:14 Ndipo akamshika mtu mmoja hirimu katika watu wa Sukothi, akamwuliza; naye akamwandikia majina ya hao wakuu wa Sukothi, na wazee wa mji, watu sabini na saba.

Soma pia..Waamuzi 17:7,11, 18:3

Hivyo, ni nini tunaweza kujifunza kutokana na Neno hili?

Hata sisi tupo katika marika, tujiulize katika marika tuliyopo, ni mambo gani ya maana tunafanya kwa Mungu etu. Upo katika rika la miaka 12 angalia kwenye biblia waliokuwa na miaka hiyo walikuwa na bidii gani kwa Mungu. Yesu alipokuwa na umri huo, alikuwa hekaluni akijifunza sheria ya Mungu, je na wewe unafanya hivyo?

Upo katika rika la miaka 30, jiulize katika umri huo, unatenda jambo gani katika ufalme wa mbinguni? Bwana Yesu alipokuwa katika umri huo, alianza kuitenda kazi ya Mungu kwa nguvu akijua kuwa muda wake aliobakiwa nao kuishi duniani ni mchache.. Je, na wewe uliye katika rika hilo unalijua? Hirimu yetu Kristo Yesu alitendaje katika umri huo?

Vivyo hivyo upo katika miaka 40, au 50, au 70  au 80 jiulize ni nini unakiingiza katika ufalme wa mbinguni, Je ni kutwa kuchwa kusumbukia ya ulimwengu? Je, ni elimu tu, Je ni familia tu, au ni nini?. Musa alikuwa na miaka 80 alipoanza kumtumikia Mungu lakini utumishi wake aliuthamini, kana kwamba alikuwa na miaka 20, Je! Na wewe unafanya hivyo?

Kumbuka biblia inasema..

Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.

Heshimu umri wako, tambua ni nini unapaswa ufanye kwa wakati huo.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Choyo ni nini kibiblia? (Luka 12:15, Zaburi 10:3)

Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?

Baadhi ya watu  na misemo ambayo haipo katika biblia.

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?

SWALI: Naomba ufafanuzi kidogo hapa sijaelewa vizuri, kwanini wakati Bwana Yesu anakuja kukamatwa naona kijana waliyemkamata alikuwa na nguo ya kitani ila baadae tunaona anaitupa nguo na kukimbia uchi , Marko 14:51-52

JIBU: Tusome;

Marko 14:50 “Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote.

51 Na kijana mmoja alimfuata, amejitanda mwili wake nguo ya kitani; wakamkamata;

52 naye akaiacha ile nguo ya kitani, akakimbia yu uchi”.

Biblia haielezi huyu kijana alikuwa ni nani, wengine wanasema alikuwa ni Marko mwenyewe aliyeandika kitabu hicho, au mwanafunzi mwengine mbali na wale

12, kwasababu wale walikuwa tayari wameshakimbia, ukisoma mstari wa 51. Lakini kufahamu kama huyu kijana alikuwa ni miongoni mwa wale 12 au wengineo sio la muhimu sana kwenye habari hiyo . La muhimu ni kujua kwanini tukio kama lile lijitokeze.

Kwanini biblia inasema aina ya vazi alilovaa kwamba ni la kitani?. Kwanini aache vazi akimbie na sio kitu kingine? .Tukiweza kuyatafakari maswali hayo tutapata ujumbe mkubwa sana nyuma ya tukio lile.

Kama tukichunguza asili ya vazi hilo, kwa mazingira yaliyokuwa yanaendelea pale tunaweza kusema ni vazi linalomsitiri mtu mwili wote. Kiasi kwamba likivaliwa halihitaji kuvaliwa na kitu kingine ndani. Kiasi kwamba mtu akilivua ni rahisi kubakiwa uchi.

Pili, ni vazi ambalo ni rahisi kuvulika, halihitaji kufungwa au kushikizwa kwa vitu vingi. Na ndio maana utaona kijana huyo alipokamatwa tu na wale askari, ilikuwa ni rahisi kuwaachia lile vazi na kukimbia. Ingekuwa ni vazi lenye vifungo, au mikanda mingi, isingekuwa rahisi kujikwamua kwa wale askari.

Na jambo lingine unaweza kuona pale, ni kuwa wale askari waliona njia pekee ya kumkamata ni kwa kulishika vazi lake, na sio pengine mikono yake au kitu kingine,. Na ndio maana utaona kijana alitumia njia ya kuacha vazi ili akimbie.

Hiyo ni kutufundisha, kuwa lipo vazi la rohoni (Kitani ya rohoni). Ambalo linauwezo wa kuusitiri uchi wote wa mtu wa rohoni, lakini pia ni jepesi sana mtu kulivua. Na ndio Bwana Yesu alisema..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na KUYATUNZA MAVAZI YAKE, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”

Unaona hapo anasema heri “ayatunzaye” mavazi yake. Ni kuonyesha kuwa mavazi hayo yanapaswa yatunzwe sana..kwasababu ni rahisi kuvulika.. Tutaona mbele kidogo mavazi hayo ni nini..

Na adui yetu shetani, anachokiwinda kwetu, sio miili yetu, sio mionekano yetu, si madhehebu yetu, si dini zetu. Bali ni mavazi yetu ya rohoni..Hayo ndiyo anayokimbilia kuyashika, haya ndiyo anayotaka umuachie, kama alivyofanya kwa yule kijana, Na mavazi yenyewe si mengine zaidi ya “matendo yetu ya haki” (yaani, utakatifu). Biblia inasema hivyo katika.

Ufunuo 19:8 “Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; KWA MAANA KITANI NZURI HIYO NI MATENDO YA HAKI YA WATAKATIFU”.

Unaona? Mavazi ya kitani ni matendo ya haki ya watakatifu.  Mpaka hapo utakuwa unapata kufahamu ni picha gani Mungu alikuwa anatuonyesha kwa yaliyokuwa yanaendelea kwa Yule kijana rohoni. Hata sasa ni kawaida watu wanapopitia shida kidogo, au dhiki au wanapokutana na matatizo  kuuacha wokovu, wanaacha utakatifu, wanamwacha Mungu, wanaacha kutenda matendo mema tena, wanamwachia adui vazi lao la thawabu.

Hivyo Neno la Mungu linatufundisha, tukutanapo na udhia wowote, au dhiki, tusiwe wepesi wa kuuacha wokovu wetu na utakatifu wetu.

Swali ni je! VAZI hili unalo? Ikiwa huna

Bwana Yesu anakupa shauri katika Ufunuo 3:18 kuwa ukanunue kwake mavazi hayo meupe uvae ili aibu ya uchi wako isionekane.. Hivyo tubu kama bado hujafanya hivyo, ukabatizwe, upokee Roho Mtakatifu. Ukamilishwe kwa vazi hili

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.

Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?

MAVAZI YAPASAYO.

Nguo za magunia katika biblia ni zipi?

JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?

Rudi Nyumbani:

Print this post