Kutokuihubiri injili, madhara yake ni yapi?
Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe..Karibu tujifunze Biblia mtu wa Mungu…Leo tutajifunza mambo machache muhimu yahusuyo majukumu yetu ya kuihubiri Injili.
Injili maana yake ni “Habari njema”..Habari yoyote au ujumbe wowote unaoupeleka kwa mtu au watu ulio mwema huo tayari ni injili…Zipo Injili za aina nyingi duniani lakini ipo injili moja tu ya wokovu..Au kwa lugha nyingine inaitwa “Injili ya Msalaba”…Injili ya Msalaba inamhusu Yesu Kristo mwana wa Mungu aliyetumwa kuichukua dhambi ya ulimwengu..Hiyo inahusu wokovu wa mwanadamu ambaye alipotea dhambi. Na Kumbuka wanadamu wote walipotea dhambini hivyo injili hii inamuhusu kila mmoja wetu.
Sasa Baada ya Bwana Yesu kuondoka ilikuwa ni sharti injili ihubiriwe ulimwenguni kote kwa kila kiumbe, na kwamba kila mwanadamu lazima aisikie injili hiyo ya wokovu…Na kwa hiari yake mwenyewe achague UZIMA au MAUTI. Kwasababu hiyo basi akawaagiza mitume wake akawaambia..
Marko 13.9 “Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao. 10 NA SHARTI INJILI IHUBIRIWE KWANZA KATIKA MATAIFA YOTE”.
Marko 13.9 “Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.
10 NA SHARTI INJILI IHUBIRIWE KWANZA KATIKA MATAIFA YOTE”.
Hapo anasema ni SHARTI!..Maana yake ni lazima injili ifike kila mahali..Kwa uzima na kifo, hata ikigharimu uhai ni lazima injili iwafikie watu..Hivyo hilo ni jukumu tulilopewa watu wote tuliompokea Kristo..Ni lazima tuihubiri Injili…Na siku zote Mungu anatumia watu kuhubiri Injili, kawachagua watu kusimama madhabahuni kumwakilisha…kamwe hatumii wanyama, wala malaika, wala kiumbe kingine chochote kamchagua mwanadamu tu!!..
Sasa kuna hatari kubwa sana ya kutokuihubiri injili…Kuna hatari kubwa sana ya kutokuitumia karama Mungu aliyokupa katika kuwahubiria wengine..Bwana amekuokoa wewe, ili na wewe ukawe msaada kwa wengine…hajatuokoa ili tu tufurahi sisi wenyewe..Kama tunavyojua wengi wetu hatujampokea Yesu kwa kutokewa na yeye…wengi wetu tumesikia injili ikihubiriwa mahali fulani na mtu Fulani wa Mungu ndipo kwa kupitia hayo mahubiri tukaokoka… Kutokuihubiri injili ni kosa kwa mtu anayeitwa mkristo.
Kadhalika huo ndio utaratibu wa Mungu, Ni lazima tuisikie kutoka kwa mtu fulani wa Mungu…na hivyo na sisi pia lazima tuwahubirie wengine ambao nao watasikia kutoka kwetu, ni kama mnyororo huyu anamzaa huyu katika imani, huyo anamzaa Yule na kuendelea..
Sasa kama umeokolewa na hutaki kuzaa wengine…kuna hatari kubwa sana…Tukirudi kwenye biblia tunamsoma Nabii mmoja aliyeitwa EZEKIELI..Huyu alikuwa ni nabii wa Mungu wa kweli kabisa., ambaye alikuwa miongoni mwa watu wachache waliochukuliwa kwenda Babeli…wakati yupo huko Mungu mwenyewe alimtokea akamwonyesha maono akiwa ameketi katika kiti chake cha Enzi huku maserafi na makerubi wakiwa wamemzunguka pande zote..akasikia sauti ya Mungu mwenyewe..Na Mungu akamtuma aende kuwaambia wana wa Israeli maovu yao na maasi yao na mambo yatakayokuja kuwatokea huko mbeleni wasipotubu.
Lakini yeye alipotoka pale baada ya kuona maono hayo…akaenda kukaa kimya, hakuwaambia watu chochote… sio kwamba alikuwa na dharau hapana! Hakumdharau Mungu…lakini alikuwa anaogopa kuwaambia(Alikuwa na hofu)….alikuwa na uchungu kweli na hasira moyoni, kwa maovu yaliyokuwa yanafanyika katikati ya watu wake lakini alikuwa anajifikiria fikiria namna ya kuwaambia..…akakaa siku saba hawaambii hao watu maono aliyoonyeshwa na Mungu…Baada ya siku saba maono yakamjia tena na kumwonya kwa anachokifanya cha kutowaambia watu maneno ya Mungu..Mungu akamwonya vikali kwa tabia hiyo..
Ezekieli 3:15 “Ndipo nikawafikia watu waliohamishwa, huko Tel-abibu, waliokuwa wakikaa karibu na mto Kebari, nikafika huko walikokuwa wakikaa; nikaketi huko miongoni mwao muda wa siku saba, katika hali ya ushangao mwingi. 16 Hata ikawa, mwisho wa siku saba, neno la Bwana likanijia, kusema, 17 Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu. 18 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. 19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako”.
Ezekieli 3:15 “Ndipo nikawafikia watu waliohamishwa, huko Tel-abibu, waliokuwa wakikaa karibu na mto Kebari, nikafika huko walikokuwa wakikaa; nikaketi huko miongoni mwao muda wa siku saba, katika hali ya ushangao mwingi.
16 Hata ikawa, mwisho wa siku saba, neno la Bwana likanijia, kusema,
17 Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu.
18 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako”.
Umeona?..Ezekieli baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Bwana kwamba “damu ya mtu itakuwa juu yake endapo hatamwambia maneno aliyoambiwa amwambie”..Ndipo akaelewa hakuna suala la mizaha tena kwenye kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu…Tangu wakati huo chochote alichoonyeshwa aliwafikishia wahusika kama kilivyo…Kwasababu alijua atadaiwa damu!. Hakuishi maisha ya kutokuihubiri injili tena.
Ndugu..Kama Bwana anakuonyesha maono ya kuwaonya watu juu ya dhambi zao na wewe huwaambii jifunze kwa Ezekieli hapo juu, kama unafahamu Neno na uwaambii wengine kuna hatari…Ni afadhali uwaambie wakatae kwa mapenzi yao wenyewe wewe utakuwa umenawa mikono..kuliko kutowaambia kabisa…mtu huyo akitoka na kwa bahati mbaya akagongwa na gari na kufa, unadhani wewe utakuwa katika hali gani?.
Kama umefahamu kuwa wazinzi na waasherati watakwenda kuzimu wasipotubu, na wewe mwenyewe sio mwasherati kwanini usiwaambie?…Mwambie ili aokoke, suala la kumbadilisha sio juu yako…wewe kazi yako ni kuhubiri tu injili…Lakini pia kama na wewe binafsi unafanya mambo hayo hayo wanayowafanya hao basi hapo usiwahubirie kwasababu wewe mwenyewe unahitaji wokovu..Na kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake..biblia inasema hivyo.
Hivyo kama ulikuwa uhubiri..anza leo!..Kama ulikuwa unaogopa kuwaambia watu juu ya habari ya siku za mwisho anza kuwaambia..Ezekieli aliogopa kuliko wewe lakini aliposikia suala la damu ya hao watu itatakwa juu yake, aligueka mara moja na wewe hivyo hivyo geuka leo..Na Bwana atakusaidia. Ipo hatari kubwa sana ya kutokuihubiri injili
Na kama hujaokoka kabisa..Tubu leo, mlango wa Neema bado upo wazi.. ila hautakuwa hivi siku zote..Umesoma hapo juu kitu gani kitamtokea mtu Yule atakayekufa katika dhambi zake huku ameonywa na amekataa…
Eze.3:19 “Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye , wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako”.
Na wewe leo umesikia injili usipotaka kutubu utakufa katika dhambi zako na madhara ya kufa na dhambi ni ziwa la moto.
kwahiyo pale ulipo mwombe Bwana msamaha, tubia uasherati wako kama ni mwasherati, ulevi wako,uongo wako, rushwa zako, usengenyaji wako,wizi wako, matusi yako… kisha katafute Ubatizo sahihi kama hujabatizwa na Roho Mtakatifu atakutakasa na kukufanya kuwa mkamilifu kama yeye alivyo mkamilifu…
Marko 1:15 “akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili”.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Shalom.
Mada Nyinginezo:
KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?
JE VIBWENGO NI KWELI VIPO?
KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.
UPAKO NI NINI?
Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Kuota unakula chakula maana yake ni nini?
Ninakusalimu katika jina la YESU KRISTO.
Awali ya yote nitoe tahadhari, kuwa kuna wimbi kubwa la mafundisho mengi ya uongo kuhusu ndoto. Hivyo ukikosa uelewa wa tafsiri sahihi kulingana na Mungu anavyozungumzia katika Neno lake..Utajikuta unapoteza kabisa dira ya Maisha yako ya rohoni kiujumla..na kujikuta unaacha kumtazama Mungu na Neno lake na unatazama ndoto unazoziota kila siku.
Kwa ufupi ndoto zimegawanyika katika makundi makuu matatu:
Hizi zikija huwa zinakuja na ujumbe Fulani, au onyo Fulani, au tahadhari Fulani, wala hazikufanya utamani kufanya mabaya, bali zinakufanya ujirekebishe pale ulipokuwa unakosea, , au ukaze mwendo katika safari yako ya kumtafuta Mungu, au kukuhimiza ukatende tendo la haki n.k.
Mfano wa ndoto za namna hii tunaweza kuiona kwa mke wa Pilato. Alipotaka kumzuia mumewe asimlibishe Bwana Yesu,..
Mathayo 27:19 “Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
Na hizi huwa haziji mara kwa mara kama zile ndoto zinazotana na mtu mwenyewe”.
Hizi huwa zinaambatana na vitisho, au tamaa za kutenda dhambi, au mambo maovu, au hofu..Kwamfano utakuta mtu anaota akifanya uzinzi na watu asiowajua au anaowajua, au anaota anafanya matambiko, au anacheza ngoma za kimila n.k. Zote hizo ni ndoto za kutoka kwa yule adui, Na hivyo mtu anaswa azikemee. Au arekebishe mwenendo wake, ni hiyo inakuja kwa kumpa Kristo Maisha yake.
Hapa ndipo asilimia kubwa za ndoto za watu zinapoegemea..
Ndoto za namna hii, kimsingi hazipaswi kuchukuliwa kiuzito kama hizo ndoto za aina mbili tulizozizungumzia hapo juu, kwani hizi zinatengenezwa na ubongo wa mtu tu pale anapokuwa amelala.. hivyo ubongo unatengeneza ndoto kutoka katika kumbukumbuku za matukio yote aliyoyafanya siku za nyuma, au siku za hivi karibuni..
Ndio hapo utakuta mtu labda jana ameona ajali mbaya imetokea, leo usiku akaota ajali nyingi zinatokea tokea..Au jana alikuwa msibani usiku wa leo anaota ndoto ya mtu Fulani kafa na yeye yupo kwenye mazishi..Au jana alikuwa anacheza mpira, leo hii anajiona yupo uwanjani anafunga magoli mengi..Au Maisha yake yote ni ya udereva, usiku anajiona anaendasha magari mengi tofauti tofauti..n.k.
Sasa ndoto za dizaini hii, huwa hazitokani na Mungu au shetani, kwahiyo zinapokujia unachopaswa ni kuzielewa kwanza, kisha kuachana nazo usihangaike hata kutafuta maana zake, kwasababu hazina maana yoyote rohoni..
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi.”
Vilevile aina nyingine ya ndoto zinatokana na ubongo wa mtu, ni ndoto za kula..biblia inasema.
Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani…”
Unaona, kama ulilala jana na njaa ni jambo la kawaida kuota unakula usiku. Mfano kuota unakula nyama, au kuota unakula wali, au kuota unakula samaki..au kuota unakula matunda,.. au kuota unakula karanga,.. au kuota unakula keki,.. au kuota unakula mayai..au kuota unakula hushibi n.k. zote hizo Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa pengine jana usiku ulilala na njaa..Au siku za hizi karibuni ulikuwa unakula aina hiyo ya chakula.
Hivyo ndoto kama hizo zikikujia zipuuzie tu, Endelea na Maisha yako ya kawaida, Jikite Zaidi katika kulitafakari Neno la Mungu kwasababu hilo ndilo linaloweza kukutabiria Maisha yako ya mbeleni ipasavyo.
Ndoto na Maono hazinusi hata chembe kwenye Neno la Mungu, Mungu anazifananisha na kama makapi katika Neno lake..soma
Yeremia 23:28 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana. 29 Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?”
Yeremia 23:28 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana.
29 Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?”
Ikiwa hujaokoka, Mlango wa neema bado upo wazi kwako, japo hautakuwa hivyo daima. Tubu dhambi zako angali muda unao, ukumbuke kuwa tunaishi katika dakika za nyiongeza tu, Kristo yupo mlangoni kurudi kulichukua kanisa lake. Dalili zote zinaonyesha, pengine kizazi chetu hichi kitashuhudia tukio zima la unyakuo wa kanisa.
Hivyo unasubiri nini. Mgeukie Kristo.Naye atakupokea.
Ubarikiwe.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.
KUOTA NYOKA.
NENO LA MUNGU NI UFUNUO MKAMILIFU.
Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
WhatsApp
Nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote;
Kitakachochochea vita kuu mbili kuu ambazo tunazitazamia kuja huko mbeleni..ambayo ya kwanza ni ile vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa katika kitabu cha Ezekieli 38 & 39. Na ya pili ni ile ya Harmagedoni inayozungumziwa katika Ufunuo 16:15 na Ufunuo 19:11-21 ambayo hiyo itakuwa ni Mungu mwenyewe. Ipo nyingine ya Tatu ambayo itakuja kutokea baada ya ile miaka 1000 ya utawala wa Kristo kuisha, ambayo nayo itahusisha Magogu, lakini hiyo hatutaizungumzia leo hapa.
Hiyo ya kwanza inasema mfalme wa kaskazini atashuka akiyangoza baadhi ya mataifa ya kando kando, yatakusanyika lengo lao likiwa ni kuindoa Israeli katika ramani ya dunia..Na kwasasa tunajua mfalme huyo wa Kaskazini atakuwa si mwingine Zaidi ya Taifa la URUSI, (ndio Gogu na Magogu), kwasababu hilo ndilo lipo upande wa kaskazini mwa Israeli, na ndio lenye nguvu kwa ukanda ule wote..Hivyo Siku za usoni, tendo hilo litafanyika, lakini hawatashinda, kwani watauawa kwa mauaji ya halaiki, biblia inasema kutakuwa na mizoga ya miili ya watu itafagiliwa kwa muda wa miezi saba pale Israeli.. na silaha zao watazitumia kama nishati kwa muda wa miaka 7 kwa jinsi zitakavyokuwa nyingi..
Ezekieli 39:12 “Na kwa muda wa miezi saba nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuisafisha nchi. 13 Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU. 14 Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta”
Ezekieli 39:12 “Na kwa muda wa miezi saba nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuisafisha nchi.
13 Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU.
14 Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta”
Na wakati huo ndio utakaokuwa mwisho wa Taifa la Urusi halitakuwepo tena.
Na vita nyingine ni ile ya Harmagedoni, hii itaongozwa na mataifa yatokayo katika mawio ya jua, mataifa ya Mashariki ya mbali, nayo yatakuwa si mengine Zaidi ya korea, Japani, China, Tawani..haya ndio yatakayoingoza vita hiyo, na safari hii haitakuwa mataifa machache tu, hapana bali itakuwa ni mataifa yote duniani yaliyosalia yataungana na hawa viongozi wao kwa ajili ya kuipoteza tena Israeli.
Unaweza ukajiuliza ni kwanini jambo hili litokee tu kwa Israeli?.. Kwani Wana ugomvi gani hasaa mkubwa mpaka ifikie hatua mataifa yote ulimwenguni yanaungana kwenda kukishambulia ki-nchi kidogo kama kile chenye ukubwa usiozidi hata mji wa Daresalaam.
Kama ukifuatilia utagundua Israeli kwasasa hawaingilii siasa zozote…au mambo ya mataifa mengine, kama yanavyofanya sasahivi mataifa makubwa kama vile Marekani, au mataifa ya Ulaya, ambayo hayo kimsingi ndio yangepaswa yawe na sababu za kutosha za kuwa na maadui.
Lakini Israeli, haifanyi chochote lakini inachukiwa,..Watu hawajui kuwa jambo hilo linatoka kwa BWANA. Ikiwa leo hii hata bado neema haijawarudia wayahudi, tayari ni maadui wa mataifa mengi, Fikiria siku ambapo watarudiwa ni nini kitatokea?
Hili shinikizo lilipo sasa litazidi hata Zaidi ya mara mia kwa jinsi siku zinavyozidi kusogea, Mungu atanyanyua visa, mbalimbali ambavyo vitayafanya mataifa yote sasa yawe na kusudi moja la kuingamiza Israeli.. Ni Mungu mwenyewe atayachochea haya mataifa kwa namna isiyo ya kawaida, atayachochoe, kweli kweli mpaka hilo Neno litatimia linalosema…
Zekaria 12:2 “Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu”. 3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.
Zekaria 12:2 “Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu”.
3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.
Unaona, hiyo ndio itakayopelekea sasa mataifa yote duniani kufikia Kiama chao..
Watakusanyika pale Harmagedoni..Sasa kumbuka wakati huo Taifa la Israeli litakuwa litakuwa limeshamwamini Masihi wao Yesu Kristo, hivyo watapaza sauti zao na kumlilia, aje kuwapigania kama alivyowapigania enzi za kale. Wakati huo ambapo mataifa yote sasa yameshaizunguka nchi hiyo ndogo,.. ndipo watakapomwona mwa Adamu akishuka na mawingu kutoka mbinguni kwa nguvu na utukufu mwingi akiwa na majeshi wa watakatifu wake ambao alishawanyakua.
Na hapo ndipo mataifa yote yatakapoomboleza, lakini utakuwa ndio mwisho wao, Bwana atawauwa wote kwa upanga utokao katika kinywa chake..
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana. 17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; 18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. 19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake”.
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake”.
Wakati huo upo karibu sana, leo hii kila mmoja wetu anashuhudia kinachoendelea mashariki ya kati, kama wewe si mfuatiliaje wa taarifa za habari..anza kufuatilia habari hususani za mashariki ya kati… jifunze, au ulizia ufahamu mambo yanayoendelea ulimwenguni.. Idadi ya mataifa yanayoipinga nchi ya Israeli inazidi kuongozeka, dini zinazolichukia taifa la Israeli nazo zinaongezeka.
Hilo lote ni shinikizo kutoka kwa Bwana mwenyewe..Kutuonyesha kuwa mwisho upo karibuni sana..
Na kabla hayo yote hayajatokea Utatangulia unyakuo wa kanisa kwanza..Ambao dalili zote zinaonyesha wakati wowote kuanzia sasa parapanda italia..na wafu wote waliokufa katika Kristo watafufuka na kwenda katika karamu ya mwanakondoo mbinguni..
Ila wale waliobakia mlango wa neema hautakuwa kwao tena, bali kwa wateule wa Mungu wayahudi..Leo hii unasubiri nini usimruhusu Kristo aingie maishani mwako akubalishe, usidanganywe na uvumi kama uvumi wa amani unaouna sasa hivi, huo ni kuwapumbaza watu waone kama tuna mamilioni ya miaka hapa duniani.. biblia inasema…
1Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
1Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
Unaona? Tubu dhambi zote, umgeukie Kristo ndani ya wakati huu mfupi tuliobakiwa nao kabla ya parapanda kulia, tengeneza mambo yako kwasababu injili tuliyonayo sasa si ile tena ya zamani ya kuvutwa kwa maneno laini, tuliyonayo sasa ni ile ya mtakatifu na aendelee kujitakasa na mwenye dhambi aendelee kufanya dhambi..Kwani wakati wa mavuno upo karibu sana…Hivyo maombi yangu ni mimi na wewe tuangukie katika kundi la wanaojitakasa..
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MTINI, WENYE MAJANI.
Vichwa saba vya mnyama wa kwenye Ufunuo 13 na 17, Ni nini?
Je kuzalishwa na mkunga wa kiume ni dhambi?..Je Mungu anaweza kutumia chochote kupitisha uponyaji wake?..Je jina la Yesu Kristo lina nguvu ya kuponya kabisa bila kutegemea daktari?
Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa tatizo lolote au ugonjwa wowote ambao mtu anaweza kuupata..Mungu anauwezo wa kuuondoa pasipo mkono wa mwanadamu yoyote kuhusika…Na hiyo inatokana na Imani mtu aliyonayo kwa Mungu..Ukiamini kwa moyo wako wote, basi yote yanawezekana.
Lakini pamoja na hayo..pia Mungu anaweza kutumia chochote kupitisha uponyaji wake…Anaweza kumtumia mwanadamu, anaweza kutumia chakula au chochote kile.
Mtu anaweza akaugua akala aina fulani ya chakula akapona..sasa kiuhalisia sio chakula kilichomponya bali ni ule uponyaji Mungu aliouweka ndani ya kile chakula ndio uliomfungua…
Kadhalika anaweza kumtumia mwanadamu kumponya mtu…anawapa maarifa fulani wanadamu ambayo kwa hayo mtu anaweza kupata uponyaji kwamfano..Mtu anaweza kuugua ugonjwa fulani..labda uvimbe umeota tumboni…na madaktari wakahusika katika kuuondoa uvimbe ule kwa njia ya OPERATION na mtu akawa mzima kabisa.,Sasa hiyo ni nguvu ya uponyaji Mungu aliyoiweka kwenye maarifa ya wanadamu n.k
Ni wazi kuwa nyakati za zamani sana hakukuwepo kabisa kwa wakunga wa kiume…au kama walikuwepo walikuwa wachache sana..Lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda wanaongezeka sana..Hiyo ni kutokana na matatizo ya wanawake kuongezeka…Magonjwa ya wanawake yanapozidi kuongezeka madaktari nao wanalazimika kuongezeka na idadi kubwa madaktari wanaoongezeka ni wanaume…Hivyo wanaume wengi wanajikita kuingia kusomea mfumo wa kibaolojia wa mwanamke zaidi ya wanawake wenyewe..huku wanawake wakiwa wachache kutokana na sababu mbalimbali.
Kwasababu hiyo basi sio dhambi kuwepo kwa madaktari wa kiume katika kushughulikia matatizo ya wanawake pale wanawake wanapokosekana kwasababu..lengo la wao kuwepo sio kuongeza matatizo bali kupunguza. Hakuna mtu yeyote anayekwenda hospitalini asiyekuwa na tatizo lolote, wote wanaokwenda wanakwenda kutafuta msaada.
Hivyo kuzalishwa na mkunga wa kiume sio dhambi wala kufanyiwa operation na mwanamume sio dhambi..Zipo operation za uzazi, ambazo kizazi kinalazimika kuchanwa kuondolewa ugonjwa usiopaswa kuwemo humo..Na operation kama hizo huwa zinamlazimisha mgonjwa kuvuliwa nguo zote na kuwa kama alivyozaliwa ili matibabu hayo yaweze kufanyika..na madaktari bingwa wanaofanya hizo operation wengi ni wanaume wakiwa pamoja na manesi wa kike…Hivyo kwa mgonjwa wa kike kutibiwa kwa viwango hivyo na daktari wa kiume sio dhambi..wala wa kiume pia kutibiwa kwa viwango hivyo na daktari wa kike ambavyo vitamlazimisha kuwa tupu kabisa mbele ya matatibu sio dhambi…Kwasababu lengo ni kupata matibabu na si kitu kingine.
Na matibabu kama hayo yanafanyika kwa madaktari wa hospitalini tu kwasababu wengi wakiwa katika vyumba vya uchunguzi au operation wanakuwa zaidi ya daktari mmoja tena wa jinsia tofauti, ili kuzuia uzalilishaji na vitu kama hivyo…. na sio kwa waganga wa kienyeji…wala kwa madaktari binafsi wa mitaani ambao wanakuita tu binafsi na kukwambia uvue hichi au kile wakuchunguze..Hao kwa namna yoyote hawapaswi kuruhusiwa kufanya uchunguzi au matibabu ya namna hiyo.
Lakini yote katika yote..Bwana Yesu ndiye mponyaji mkuu..operesheni wakati mwingine zinafeli pamoja na gharama zake zote hizo kubwa…lakini Yesu Kristo hajawahi kushindwa…
Vyakula wakati mwingine vinashindwa kutuponya lakini Yesu Kristo hajawahi kushindwa..Yapo magonjwa ambayo madaktari hawayaelewi chanzo chake lakini Yesu Kristo anayajua.
Madaktari wanatibu kwa gharama kubwa za fedha, na wakati mwingine gharama za kutolewa nguo zote, au nywele zote au kiungo fulani kukatwa ndipo matibabu yaweze kufanyika..lakini Yesu Kristo anafanya bila hayo yote.
Ikiwa unaumwa ugonjwa wowote ule..Nataka na unakaribia kwenda kwenye operesheni…nataka nikuambie Yesu Kristo anaweza kukuponya kabla hujamkaribia huyo daktari..
Weka mkono mahali unapoumwa..kama ni kifuani, kichwani, tumboni..kama ni ugonjwa ambao huelewi chanzo chake weka kichwani…Yesu anajua chanzo chake..
Sasa baada ya kuweka kichwani..unaposoma sala hii ugonjwa wako unakwenda kuhama sasahivi na kutoweka kabisa..Amini tu.
“Bwana Yesu namwombe mtu ambaye simjui ni nani, wala jina lake, wala ugonjwa wake wala mahali alipo, lakini wewe unamjua jina lake, mahali alipo na tatizo alilonalo..namwombea kwa Imani katika jina lako lenye nguvu (Jina la Yesu). Kwamba kila ugonjwa na kila pandikizo lililopandikizwa ndani yake na yule adui likapate kutoweka sasahivi katika JINA LA YESU KRISTO! Amen”.
Ikiwa umeisoma hii sala niliyokuombea…Huo ugonjwa umeshaondoka na kama ugonjwa huo ulivyoondoka ndani yako…Ugonjwa wa rohoni pia unapaswa uondoke pia..Na ugonjwa wa rohoni ni dhambi.
Hizo zinaondoka ndani yako kwa kumkiri sasa Yesu Kristo ambaye amekuponya ugonjwa wako..Na baada ya kumkiri kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako..mwambie akusamehe dhambi zote ulizowahi kuzitenda huko nyuma…na wewe mwenyewe dhamiria kuziacha…kama ulikuwa ni mwasherati..umeona utukufu wa Mungu..hivyo usifanye uasherati tena…vivyo hivyo na dhambi nyingine zote. Usizifanye tena, yasije yakakupata mabaya kuliko hayo uliyokuwa nayo.
Na baada ya kutubu haraka sana nenda katafute ubatizo. Kumbuka ubatizo sahihi ni wa muhimu sana. Na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo.(kulingana na Matendo 2:38). Na Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakuongoza na kukutia katika kweli yote.
Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali share na wengine.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
JE! MUNGU NI NANI?
Biblia ni nini?
kilemba cha neema, Je! Umemvika mwanao ?
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe..Karibu tujikumbushe mambo muhimu katika maisha yetu..Na hayo si mengine zaidi ya maonyo ya Neno la Mungu…Leo kwa Neema za Bwana tutajikumbusha majukumu machache ya wazazi juu ya watoto wetu..
Kutoka 20: 12 “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako”.
Neno hili ni Neno la Mungu kwa watoto wote ambao wanao wazazi…Na hata kama hawana wazazi labda wamefariki au hawaishi nao kwa namna moja au nyingine…Basi nafasi hiyo ya Baba na Mama itachukuliwa na walezi wao…Hao wanasimama kama Baba zao na Mama zao kihalali kabisa mbele za Mungu..hata kama wapo katika vituo vya malezi vya mayatima…hao walezi wao wanachukua nafasi hiyo ya Baba na Mama…wana amri kutoka kwa Mungu kuheshimiwa kama wazazi halisi…Kwasababu kuna Baraka kubwa sana katika kuwaheshimu wazazi na kuwasikiliza..
Kadhalika haijalishi mzazi ni mwovu kiasi gani lakini ni lazima kumheshimu, na kumtii haijalishi yeye hajiheshimu kiasi gani ni wajibu wa kila mtoto kumheshimu mzazi wake..Kwasababu ndio amri ya kwanza yenye ahadi…
Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”
Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”
Kupata heri na kuishi siku nyingi ni vitu viwili tofauti…Unaweza kuishi siku nyingi lakini maisha yasiwe ya heri..Hivyo, vyote viwili vinapaswa viende pamoja…
Sasa Kitu cha Muhimu cha kufahamu kwa mzazi ni kwamba…Hatima ya mtoto, mzazi anaweza kuchangia kwa asilimia kubwa kuitengeneza au kuiharibu…Mzazi anaweza kukazana kweli kumpenda mwanawe, kumlipia karo, kumtafutia shule bora..kumpatia lishe bora, kumlinda..kumhakikishia bima ya afya n.k Lakini kama hatamtengenezea mwanawe mazingira ya kumheshimu au kumtii.. huyo mtoto hawezi kupata heri yoyote huko anakokwenda, wala hawezi kuishi maisha marefu…haijalishi atapatiwa elimu nzuri kiasi gani sasa…au atakuwa na afya nzuri kiasi gani sasa au maarufu kiasi gani…Maisha yake yatakatika katikati na yatakuwa ya tabu.
Hayo ndio mambo ya kwanza ya kuzingatia kabla hata ya kwenda kuangalia ufaulu wake wa darasani…usifurahie anapofaulu sana na huku adabu yake inazidi kwenda chini..furahia pale heshima yake na utii wake unapozidi kupanda kwasababu unajua..hata kama atapepesuka kiafya sasa..hatakufa!..ataishi muda mrefu kwasababu Neno la Mungu linasema hivyo..hata kama hana heri sasa, lakini atakuja kuwa na heri baadaye katika kipindi cha maisha yake yote..
Hivyo kazana kumfundisha awe na tabia ya kukusikiliza…chochote utakachomwambia akutii na afanye kwa kupenda na si kwa kulazimishwa lazimishwa..mfunze tabia nzuri na heshima na utiii kwako na kwa watu wengine, mvishe mavazi ya adabu na mfundishe kuwa mtii….Mjaribu mara kwa mara kuangalia utii wake umefikia wapi ukiona umepungua tafuta namna ya kuurudisha…..mtume dukani mrudishe hata mara mbili au tatu, mpime..ujue kiwango cha utii alichonacho na heshima.
Mpime anapokuwa na wageni na watu wengine anakuwa na tabia gani zisizofaa na zile zinazofaa mpongeze…ukiona kasoro tumia fimbo kidogo, maana biblia inasema ukimpiga hatakufa…Wengi hawatumii fimbo wakidhani wanamharibia ujasiri mtoto, fimbo isiyokuwa na mafunzo sahihi ndiyo inayomharibia ujasiri..lakini fimbo yenye ujumbe wa kujenga ndiyo inayomjenga zaidi mtoto…
Na Mungu alivyowaumba watoto hawana kinyongo ili kwamba waweze kutengenezeka..ukimwadhibu sasahivi baada ya nusu saa mnacheka na kufurahi, ule upumbavu utakuwa umendoka lakini upendo wake kwako bado upo…..ukimwacha sasa bila kumfunza atakapokuwa mtu mzima hali za kuwa na vinyongo na uchungu zitakapomjia itakuwa ni ngumu kumtengeneza….kila utakalomwambia atakuwa anakwambia unamnyanyasa,..mara unaingilia uhuru wake..mara hujali hisia zake, mara wewe ni mkoloni, mara unamwaibisha n.k
Pia katika utoto aliopo, mfundishe biblia..mpe mistari kadhaa ya kuikariri na kuishika kwasababu watoto wengi bado hawajaweza kuipambanua mistari..wape tu waikariri itawasaidia ukubwani..kuliko kukariri nyimbo za kidunia..pia wafundishe nyimbo za kuabudu, na kumsifu Mungu na wafundishe sala za kuomba muda wote na habari za Yesu ambazo ndizo za muhimu kuliko zote..Na wapime je hivyo unavyowafundisha au wanavyofundishwa na wengine wanavizingatia.??
Ukimpima mtoto vizuri na kujua kuwa anakutii na kukuheshimu na anaheshima kubwa ambayo mpaka watu wa nje wanaishuhudia na kusema Yule mtoto anaheshima na adabu…Basi, kuna Baraka ambazo Mungu anaziachia ambazo ulimwengu hauwezi ukaziona..hapo ndipo nyota njema ya mtoto inapoanzia..
Mithali 22: 6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”…
Wengi wanaogopa kuwafundisha wanao adabu na heshima kwasababu wanahisi wakishafikisha umri Fulani labda wa kuvunja ungo au kubalehe watakengeuka..Huo ni uongo wa shetani!!…Watoto wengi wanakengeuka ukubwani kwasababu wazazi wao ambao hapo kwanza walikuwa wanawalea vizuri leo wamekengeuka!..sasa kama mzazi kakengeuka mtoto atasalimikaje?..Mzazi alikuwa anakwenda kanisani na mwombaji sasa hafanyi hivyo tena..mtoto ataendeleaje kwenda kanisani?…Mtoto alikuwa amezoea nyumbani ni mahali pa ibada sasa nyumbani kunapigwa kila siku kwenye TV, nyimbo za kidunia, mtoto ataendeleaje kuwa mtakatifu?….Lakini kama mzazi akibaki vile vile Yule mtoto kamwe hawezi kukengeuka hata atakapokuwa mzee..biblia sio kitabu cha Uongo!… Haiwezi kusema mtoto hataiacha ile njia halafu aje kuiacha!..sasa Mungu atakuwa ni mwongo.
Sasa faida nyingine ya mwisho na kuu ambayo mtoto anaweza kuipata kutoka kwako mzazi kwa kumfanya akutii na hata akusikilize na kukuheshimu katika viwango vya juu ni KUVIKWA KILEMBA CHA NEEMA KICHWANI PAKE?.
Mithali 1: 8 “Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, 9 Kwa maana hayo yatakuwa KILEMBA CHA NEEMA KICHWANI PAKO, Na mikufu shingoni mwako”.
Mithali 1: 8 “Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
9 Kwa maana hayo yatakuwa KILEMBA CHA NEEMA KICHWANI PAKO, Na mikufu shingoni mwako”.
Hii ni Baraka kubwa sana ambayo wazazi wengi hawaijui…Hapa duniani tunaishi kwa Neema,…Hivyo Neema ya Kristo inapokuwa nyingi juu yetu..ndipo tunapokuwa na nafasi zaidi ya kumkaribia Mungu, ndipo tunapokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuwa watumishi wa Mungu…Na utumishi wa Mungu sio tu ule wa kuhubiri madhabahuni hapana! bali hata ule wa Danieli ni utumishi wa Mungu..Pale Mungu anapokuweka katika ngazi Fulani ya juu na huko anakutumia kuwatunza watu wake..Hivyo Neema kama hiyo ni njema kwa mtu yeyote…Mtu anayemtumikia Mungu,.. Mungu atamheshimu biblia inasema hivyo (katika Yohana 12:26).
Sasa ni nani asiyetaka kuheshimiwa na Mungu?..Je! unataka mwanao aheshimiwe na Mungu?…Kwa kuvikwa neema ya kuwa mtumishi wake?…Ni kwa kumfanya akutii na kukuheshimu..huku na wewe ukionyesha kielelezo cha kumcha Mungu maisha yako yote ili usimwangushe..
Kuwa na mtoto ni Baraka!..Hususani kama umemvisha kilemba hicho cha neema….Neno la Mungu linasema wapeni watu vitu nanyi mtapewa kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika ndivyo watu watakavyowapa kifuani mwenu…..Na wewe umempa mwanao hicho kipimo cha Neema ya Mungu juu ya kichwa chake kubwa namna hiyo…Bwana atamtumia huyo huyo kukulipa..kukurudishia kipimo cha kujaa na kushindiliwa nakusukwasukwa hata kumwagika katika siku za mbeleni..Na kwasababu mwanao au wanao watakuwa wanatembea na hiyo NEEMA kubwa sana kichwani mwao basi kila watakalomwomba Mungu, Mungu na kila watakalolifanya litafanikiwa katika maisha yao.
Kama wewe mzazi hujaokoka!..Tambua kuwa huwezi kuwavika wanao KILEMBA HICHO CHA NEEMA vichwani mwao..Wataharibikiwa na kuwa na maisha mabaya..kwasababu maisha yako wewe ni mabaya!..Hivyo ni vizuri leo hii ukamgeukia Kristo akuoshe dhambi zako kweli kweli kwa damu yake..Ili uwe mzazi/mlezi bora…Unachopaswa kufanya ni kutubu kuanzia leo na kumwambia Bwana akusamehe..akusamehe, uasherati wako kama ulikuwa unaufanya..akusamehe kwa kutowajali wanao,..akusamehe kwa kila uchafu uliokuwa unaufanya..na hivyo unamwahidi kwamba utafanya tena..
Baada ya kutubu kabatizwe katika ubatizo sahihi kwaajili ya ondoleo la dhambi (Matendo 2:38)..Kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa mwili wote kwenye maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo. Baada ya kufanya hivyo Roho Ambaye atakuwa ndani yako atakuongoza kufanya mengine yote yaliyosalia na kukupa uelewa wa ajabu wa kuyaelewa maandiko na kukusaidia kushinda dhambi ambazo kwa nguvu zako ulikuwa huwezi.
Kumbuka pia Yesu Kristo atarudi..Biblia inasema “Itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima na kisha tupate hasara za nafsi zetu’’..Hivyo uwe unalitafakari hilo kila siku.
Maran atha!..Shalom.
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.
MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
KIMBIA! KIMBIA! KIMBIA!
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
BONDE LA KUKATA MANENO.
Ulinzi wa daima (eternal security) ni neno la kimaandiko?
JIBU: Ulinzi wa daima, kama inavyojulikana kwa lugha ya kiingereza“eternal security”, linamaana kwamba mtu akishamwamini Kristo akaokoka, basi mtu huyo anakuwa tayari anao ulinzi wa milele wa wokovu wake, na kwamba hawezi kuanguka tena kwenda kuzimu hata iweje, kwani wewe tayari ni milki ya Mungu milele. “Once saved, forever saved”.
Wanaoamini hivyo wanasema, suala la wokovu ni la Mungu mwenyewe, anamwokoa mtu kwa neema na si kwa matendo yake mwenyewe. Na hivyo hata mtu anapochukua uamuzi wa kuupokea wokovu, hata hayo yaliyobakia pia ya kumlinda mtu huyo hadi siku wa mwisho yanakuwa ni ya Mungu..
Ni kweli ulinzi wa daima/milele ni neno la kimaandiko, kwamba ni kweli mtu akishaokolewa, Saa hiyo hiyo Mungu anampa uhakika wa uzima wa milele, anakuwa ametiwa muhuri hadi siku ya ukombozi wake, (Soma Waefeso 4:30, Warumi 8:33-34, Warumi 8:38-39)..Lakini ahadi hiyo ni kama mtu akidumu katika hiyo neema tu!. Ikiwa atafanya hivyo Mungu hawezi kumwacha akaangamia, atamshikilia mkono kila anapokwenda kuhakikisha haanguki.. Lakini kama hatataka yeye mwenyewe kudumu katika neema (Imani) hiyo, wazo hilo ni la uongo.
Ni sawa umemshika mtoto mkono na kumwambia atembee huku umemshika mkono na ukamwakikishia kwamba akiwa katika mikono yako kamwe hataanguka atakuwa salama daima..Lakini Yule mtoto akasikiliza ushauri wa mtu mwingine kwamba anaweza kutembea peke yake hivyo kwa hiyari yake mwenyewe akakataa na kusema sitaki kushikwa na wewe na akatoka mikononi mwako kwa nguvu je! Akianguka atakulaumu..na kumwambia ulimwahidia hataanguka daima atakuwa salama?..Kitu kisichofahamika na wengi ni kwamba Mungu hawezi kuvuka maamuzi yetu..Huwa hatulazimishi kufanya kitu kama sisi wanadamu tunavyolazimishana..
Hivyo tunapookolewa, hatukai tu tukijitumainisha kuwa tumeshashinda vita moja kwa moja, na kwamba tupo mikononi mwa Mungu salama…Tunapaswa tufahamu kuwa ndio kwanza tumeanza vita kwasababu Adui yetu shetani atataka kutufanya tuamue kuiacha imani..
Na ndio maana kuanzia huo wakati (baada ya kuokoka) mambo huwa hayawahi marahisi wakati mwingine tunakumbana na vita na majaribu mengi kutoka kwa adui, na misukosuko mingi ili tu tuiache imani,..Hivyo kama shetani angekuwa anajua kuwa kama mtu ameupata wokovu ndio kaupata milele, basi asingekuwa na haja ya sisi kutufuatilia tuiache Imani baada ya hapo, maana kwake yeye ingekuwa ni kazi bure.,Lakini kinyume chake kila siku anatupiga vita kwasababu anajua kuwa uwezakano wa kukipoteza kile tulichonacho upo!…Anajua pia bado kuna uwezekano wa kuupoteza ulinzi huo wa milele.
Hivyo ikiwa kama tutadumu katika mapenzi ya Mungu basi uhakika wa wokovu huo ni lazima.. Lakini ikiwa hatutailinda neema tuliyopewa kwa bidii, tukawa wazembe, yaani tunaishi tu kama tunavyotaka, uwezekano mkubwa wa kuupoteza wokovu wetu upo.
Mtume Paulo alikuwa ni mtu aliyetokewa na Kristo, aliyejitoa kweli kwa Mungu, aliyehubiri injili kwa mataifa mengi, maelfu au pengine mamilioni ya watu waliokolewa kwa kupitia huduma yake..Lakini kuna wakati alisema..
1Wakorintho 9:26 “Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.
1Wakorintho 9:26 “Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.
Unaona, alishaona kumbe anaweza akawa sio tu mkristo peke yake, bali akawa hata mtumishi wa Mungu aliyeitwa, lakini mwisho wa siku akawa ni mtu wa kukataliwa (akaenda Jehanamu ya moto).
Paulo alisema vile kwa kumaanisha, sio kama kujionyesha kuwa ni yeye ni mnyenyekevu..Aliona uwezekano huo wa kupotea bado upo kwa asilimia kubwa!.
Wapo watumishi leo hii, ni wazinzi, wanadhani bado wanao ulinzi wa daima ndani yao..Wapo wachungaji ni wanywaji pombe na wavutaji sigara, wanadhani bado wanao ulinzi wa daima ndani yao..Kwamba hata wakifa watakwenda mbinguni kwasababu maandiko yanatuambia tunaokolewa kwa neema.
Nataka nikuambie, Hata Yuda, aliyechaguliwa na Kristo, mwenyewe,..Na alianza vizuri lakini hakuilinda neema aliyopewa na mwisho wa siku akaangukia katika mikono ya shetani. Sasa kama Yuda aliyetembea na Yesu miaka 3 na nusu alikengeuka…Mimi na wewe ni nani ambao hata hatujawahi kumwona Yesu tujidanganye kuwa tukishaokolewa tumeokolewa?.
Hivyo usipoithamini neema uliyopewa bure kwa damu ya Yesu Kristo, hujibidiishi kuilinda Imani yako, huko nyuma ulimaanisha kuokoka kweli, lakini leo hii, unakwenda Disko,.. unavaa nguo za uchi uchi, unatazama picha chafu mitandaoni, unasikiliza miziki ya kidunia, unakula rushwa, unakwenda kwa waganga..Nataka nikuambie kwako ulinzi huo wa daima (eternal security) ulishaondoka!!..Na hata ukifa leo hii utakwenda kuzimu na adhabu yako itakuwa kubwa Zaidi ya wale ambao hawakumjua Kristo, Haijalishi wewe ni kiongozi mzuri wa kanisani kiasi gani,..haijalishi umeshahubiri kiasi gani, haijalishi umewaleta wengi kwa Kristo kiasi gani…Usipoyafanya mapenzi ya Mungu, utapotea tu.
Ezekieli 3:20 “Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa;”
2Petro 1:10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”.
Uthamini wokovu wako, ili Mungu apate nafasi ya kukulinda..
CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!
INJILI YA KRISTO HAITANGAZWI KWA HATI MILIKI.
NI KIPI MUNGU ANACHOKITAZAMA ZAIDI, MOYO AU MWILI?
KWANINI AWE PUNDA NA SI MNYAMA MWINGINE?
BIRIKA LA SILOAMU…Bwana Yesu alisema..”Mtu akiona kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.
Shalom, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu ambalo ni mwanga wa njia zetu, na taa iongozayo miguu yetu.
Yohana 9:6 “Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, 7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona”
Yohana 9:6 “Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho,
7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona”
Bwana wetu Yesu angeweza kumponya mtu huyu pasipo hata kumwambia akanawe katika birika la Siloamu.. Tafsiri ya birika ilivyotumika hapo sio birika la kuwekea chai au maji ya moto..hapana! bali birika maana yake ni Bwawa dogo lililotengenezwa kwa kusudi maalumu…ni kama swimming pool kwa lugha ya kiingereza..
Katika Yerusalemu zamani za agano la kale, lilikuwepo birika hilo ambalo lilitengenezwa mara ya kwanza na Mfalme wa Israeli aliyeitwa Hezekia, ukisoma 2Wafalme 20:20 utaliona jambo hilo,..lakini birika hilo lilikuja kubomolewa na Mfalme wa Babeli Nebukadneza, lakini baadaye lilikuja kutengenezwa tena na Nehemia…na likaendelea kuwepo mpaka wakati wa kipindi cha Bwana Yesu…ingawa lilikuja kufanyiwa ukarabati tena na Herode.
Yohana 7: 37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”.
Yohana 7: 37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”.
Yohana 4: 6 “Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. 7 Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. 8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria). 10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa”
Yohana 4: 6 “Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
7 Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.
8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula.
9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria).
10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.
11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.
16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa”
Je umeyapata hayo maji?..Roho Mtakatifu ndiye maji ya Uzima..anakata kiu ya dhambi, kiu ya uasherati, kiu ya rushwa,kiu ya wizi na kila aina ya uchafu, maji hayo yanapatikana bure…
Ufunuo 21: 6 “Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure” Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.
Ufunuo 21: 6 “Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure”
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.
Pengine umesikia habari hizi za maji ya uzima mara nyingi sana zisizohesabika…lakini nataka nikuambie ukiyadharau haya maji leo yanayopatikana bure utayatamani siku ile katika ziwa la moto na utayakosa kama yule Tajiri aliyemwomba Lazaro achovye kidole chake kwenye maji hayo ili auburudishe ulimi wake akakosa…Na ndivyo siku ile utayatamani maji hayo utayakosa…usikazane kutafuta maji ya upako, au kutafuta kuzamishwa kwenye mabwawa yajulikanayo kama mabwawa ya upako..tafuta MAJI YA UZIMA…Bwana atusaidie tuyapate maji haya kwa wingi..ili tuwe na Uzima…Tunamshukuru sana Bwana wetu Yesu Kristo wa kutuletea maji haya ya uzima..jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Maran atha!
UMEPATANISHWA NA MAADUI ZAKO?
KIJITO CHA UTAKASO.
BWANA ANAPOTUKASIRIKIA ANA LENGO ZURI NA SISI NDANI YA MOYO WAKE.
Marko 3:5 “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. 6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”
Marko 3:5 “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
6 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza”
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Neno la Mungu ndio chakula kitupacho uzima wa milele,. hivyo tunapochukua muda kulitafakari kila siku,. basi tunafanya jambo ambalo faida yake hatutaiona hapa peke yake, bali hata miaka miaka trilioni moja mbele.
Leo kwa neema za Mungu tutaangazia jambo moja kwa ufupi juu ya Hasira ya Kristo..Tukiyatafakari hayo maneno hapo juu tunaona kuna wakati Bwana alikwenda kwenye sinagogi na kukutana na mtu ambaye alikuwa na mkono uliopooza…
Lakini alipotaka kumponya, aligundua kuwa Mafarisayo na Maherodi walikuwa wanamzivia ili wamjaribu kama atamponya mkono wake siku ya sabato, ili wapate kumshitaki..Lakini yeye alipogundua hilo akakasirika sana, akatulia kwa muda akiwaangalia wale watu kwa hasira..kuanzia kushoto kwake mpaka kulia kwake, wale waliokuwa mbele yake, hadi wale waliokuwa nyuma yake… wote aliwaangalia kwa makusudi ili wauone uso wa Kristo ulivyojaa hasira..
Ni rahisi kusema huyu mtu kashaanza kutuchukia,. Au huyu mtu anakinyongo Fulani ndani yake kwa ajili yetu, lakini tunasoma biblia inasema, ndani ya moyo wake,. Alikuwa na huzuni kubwa kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao.. Alikuwa anawaonea huruma ndani ya moyo wake, alikuwa anawapenda upeo na hivyo hataki wapotee na ndio maana japokuwa uso wake ulikuwa umejaa hasira nyingi,.. Lakini moyoni mwake alikuwa unadondosha machozi mengi ya huzuni.. Hiyo ndio hasira ya kweli ya ki-Mungu.
Mungu anapokukemea kwa ajili ya dhambi zao, usidhani kuwa Mungu anakuchukia, au anakutesa, au ni mkatili,. uso wa Mungu unapogeuka kwako, usidhani kuwa Mungu hakupendi, lakini badala yake anafanya hivyo kwasababu anataka ugeuke usipotee, moyoni mwake anakuthamini kushinda wewe unavyodhani..(kumbuka tena Bwana anapotukasirikia ana lengo zuri na sisi)
Mungu anapokuambia, uzinzi unaofanya utakupeleka kuzimu, usidhani anakuchukia,. Anapokuambia, rushwa unayokula, ushirikina unaoufanya, matambiko na kafara unazozitoa, moja ya hizi siku utakwenda kuchomwa katika moto usiozimika,. Sio kwamba anakuchukia, anapokuadhibu kwa dhambi zako, na kumwona Mungu kwako kama ni mkatili mwenye uso wa hasira sikuzote kwako..Furahia ni kwasababu anakupenda, na anataka ubadilike..wakati mwingine anakunyang’anya hata baadhi ya vitu ulivyonavyo, au unamwomba hakupi hata kimoja,. Sio kwasababu hakujali, au hakuoni, hapana, Kaonyesha uso wa hasira nyingi kwako kwasababu njia zako ni mbaya..
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
Mungu akikupenda hata acha kuonyesha uso wa hasira kwako, hataacha kukuonya juu ya dhambi zako, kama vile leo hii anavyokuonya.. Anakueleza ukiendelea kuvaa nguo za nusu uchi utaishi jehanamu ya moto,. ukiendelea kutazama pornography utaishi jehanamu ya moto, ukiendelea kwenda disko utakufa siku moja na kushukia kuzimu…kwasababu anasema wote niwapendao! anawakemea.
Hivyo usishupaze shingo yako,. bali utubu leo hii, mgeukie Bwana wako, ili uugeuze uso wake wa hasira na kuwa wa furaha. Unachotakiwa kufanya ni kujisalimisha kwa Bwana, ukiwa na mzigo wa dhambi zako, na kumwambia, nisamehe nimekosa Mungu wangu na leo hii ninataka kuanza upya tena..Ninaacha hiki, ninaacha kile kwa kumaanisha kabisa..
kwa kuanza kujishughulisha na mambo ya Mungu na kukaa mbali na dhambi ulizokuwa unazifanya hapo kabla,. kama ni nguo za kizinzi unazichoma, kama ulikuwa unaishi na mke/mume ambaye si wako unamuacha.. kama ulikuwa unakwenda bar, unaacha, kama ulikuwa unatazama picha chafu mitandaoni unazifuta,.. kama ulikuwa unafanya uasherati na girlfriend au boyfriend hamjaona, unaacha, kisha unaanza kutafuta ndugu wa kikristo na kukaa nao,..
Sasa Mungu akishaiona Imani kama hiyo, na toba yako iliyoambatana na matendo kama hayo,. yeye mwenyewe kuanzia huo wakati anachukua jukumu la kukufanya kuwa mwana wake kweli kweli, atakupa uwezo wa ajabu wa kuweza kuyashinda hata yale ambayo ulikuwa huwezi kuyaacha..Na mwisho wa siku utajikuta umeshaimarika ndani ya Kristo kwa viwango vya juu sana.
Lakini pia kumbuka, mara baada ya kutubu kwako unapaswa ukabatizwe,. na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi (Yohana 3:23), na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38,.Ubatizo sahihi ni muhimu, fanya hivyo na hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili.
Kumbuka anasema wote niwapendao nawakemea au kwa lugha wote niwapendao niwaeleza ukweli..Hivyo umeusikia leo ukweli. Kubali na kugeuka.
Marko 3:5 “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao”
Ubarikiwe. Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Maswali na Majibu
NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
Habari ya UZIMA? Naomba unisaidie tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu Kwa Sisi Tumwaminio/wafuasi wake. Je! Damu ya Yesu inakazi ya Kutulinda sisi au Mali zetu pale tunapoomba kupitia Damu? Ni sahihi kuomba hivyo? Je! Damu ya Yesu inatumikaje Kwa sisi wakristo?
JIBU: Ili kuelewa tofuati ya utendaji kazi wa damu ya YESU na Jina Jina la Yesu, Ni vizuri kwanza tukajifunza katika maisha ya kawaida…Katika maisha ya kawaida mtu anayo DAMU na vilevile analo JINA…Jina la mtu linaelezea utambulisho wa mtu yule, cheo alicho nacho, heshima aliyo nayo, nguvu aliyo nayo na mamlaka aliyonayo.. Kwamfano katika nchi yoyote mtu mwenye jina kubwa na lenye nguvu kuliko wote ni Raisi wa nchi hiyo…
Vilevile katika upande wa pili DAMU ya mtu inaelezea Uzima wa huyo mtu, asili ya mtu huyo, Undugu alionao na wanafamilia wenzake, na inaelezea pia Urithi alionao..yaani watu atakaowarithisha mali zake.
Sasa tukirudi katika mamlaka ya kimbinguni ambayo hiyo ni kuu kuliko ya kiduniani…Tunaye Mfalme mmoja, naye ni Yesu Kristo (Huyo ni Zaidi ya Raisi yeyote wa nchi)…Na huyu analo JINA vilevile na anayo DAMU.
Kama tulivyosema damu inaelezea undugu wa mtu, yaani uana-familia.….na Bwana Yesu pia anao ndugu zake wa damu,..ambao ni wale wote waliozaliwa mara ya pili…Hao wanayo mamlaka ya kumsogelea katika meza yake na kula naye, na kumwomba lolote kwa jina lake na kupewa…Mtoto wa mfalme akiomba apewe jimbo fulani kutoka kwa Baba yake…haitachukua mlolongo mrefu kupewa haja ya moyo wake..mara moja tu baba yake atamwandikia hati ya nakala kwa jina lake na kuipeleka mahali husika kupata anachokihitaji…Na huyo mtoto kwa jina la Baba yake anaweza kupata lolota katika nchi…..Lakini hebu mtu wa kawaida tu amsogelee mfalme wa nchi na kumwomba apewe hicho kipande cha ardhi uone mlolongo wake!…anaweza kufukuzwa au hata asipofukuzwa basi ombi lake linaweza kuchukua muda mrefu sana kujibiwa…
Ni kutokana na kwamba mtoto wa Mfalme anatumia DAMU kupata lolote kwa JINA la Baba yake…wakati wengine wanatumia bahati tu!..kwamba ombi lao likikubaliwa ni kama wamepata bahati tu!..wangeweza kukataliwa…lakini mtoto wa Mfalme anauhakika kwasababu anatumia damu.
Kwahiyo tukirudi kwenye swali: Tofauti kati ya damu ya Yesu na jina la Yesu ni ipi? Tumeshaiona hapo juu na …na je ni sahihi kuomba kutumia damu ya Yesu kutulinda sisi na mali zetu? (damu ya Yesu inatumikaje)
Jibu: Mtu aliyeokoka tayari damu ya Yesu inanena mema juu yake..kama kwa hiyo mifano tuliyoiona hapo juu…Haihitaji kumweleza sana Baba wa mbinguni kwamba unahitaji ulinzi..kitendo tu cha kuwa mwanawe wa damu tayari ni jukumu lake kukulinda wewe na mali zako..na kwa jina lake kupewa chochote katika huu ulimwengu..Tofauti na mtu ambaye hajaokoka…huyo si mwana wa Mungu,..huyo hana uhusiano wowote na damu ya Mungu…Kwahiyo hata akiomba lolote kwa jina la Yesu kwake ni bahati nasibu kupata anachokiomba…
Umefanyika kuwa mwana wa Mungu?..umekuwa damu moja na Mungu?..Kama hujaokoka basi fahamu kuwa ni ngumu wewe kupokea upendeleo wowote kutoka kwa Mungu..Kwasababu Mungu anawaangalia kwanza wanawe kuwapatia mema (Soma Warumi 8:28-29)..na hao ndio atakaowarithisha uzima wa milele…hawezi kuwarithisha watu wasio wanawe…hata wewe mwenyewe ni ngumu kumrithisha mtoto asiye wako mali zako na kuwaacha wanao bila urithi…
Sasa kwanini uwe kama Yatima siku ile?..wakati wenzako wanairithi mbingu…wewe unarithi ziwa la moto kutoka kwa baba yako ibilisi?..mwache shetani aende kuzimu mwenyewe wewe mgeukie Kristo, mwenye urithi udumuo.
Hivyo unachopaswa kufanya ni kutubu kama hujatubu, kama ulikuwa ni mwasherati unatubu kwa kuacha kufanya hivyo, kama ulikuwa unaweka make-up unaacha, kwasababu mabinti wa Mungu waliozaliwa kwa damu ya Mungu hawafanyi hivyo, ..kama ulikuwa unasuguliwa kucha na wanaume saloon, utubu na kuacha,.., kama ulikuwa unavaa vimini, unapamba uso, unavaa surali, unatubu na kuacha kama ulikuwa ni mlevi, mvutaji wa sigara na mfanyaji masturbation na mtazamaji wa picha chafu katika mitandao unatubu na kuacha, kama ulikuwa ni mwizi vivyo hivyo…
Na baada ya kutubu kwa kudhamiria kabisa na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. …utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuhesabika mwana-familia wa familia ya kimbinguni. Na hivyo kuwa mrithi, na ile damu ya thamani isiyoisha muda wa matumizi, damu ya Yesu Kristo itaanza kunena mema juu yako.
Bwana akubariki.
Tafadhali share na wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?
BUSTANI YA NEEMA.
KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.
Je! ni dhambi kuimba wimbo wa Taifa hata kama umetungwa kidunia?.Na je ni dhambi kwa watoto wa kikristo kuimba zile nyimbo za chekechea?
JIBU: Nyimbo karibia zote za kitaifa hazijatungwa kidunia… Nyingi zilitungwa wakati au baada kidogo ya uhuru wa Taifa husika..Zilikuwa ni nyimbo za Kumshukuru Mungu na kulitakia amani, baraka na mafanikio Taifa husika. Hivyo nyimbo nyingi zilitungwa kama sala iliyo katika mfumo wa kama wa wimbo hivi.
Hakuna wimbo wowote wa Taifa lolote duniani..unaiombwa kwa lengo la kunyanyua hisia za uasherati, wala kutukana kama nyimbo zinazotungwa siku hizi, wala kwa lengo la kujiburudisha, wala kutafuta fedha, wala kujulikana…Hata wengi wa watunzi wa nyimbo hizo hazikuwa mali zao wenyewe kwamba wana hati miliki nazo..bali zilikuwa ni mali za Taifa.
Lengo lingine pia la nyimbo hizo, zimetungwa kuinua morali ya kufanya kazi, kuishi kwa umoja, upendo na kuliheshimu Taifa.
Hivyo hakuna ubaya wowote wa kuimba wimbo wa Taifa mahali popote.
Na sio tu nyimbo za Taifa, bali hata nyimbo za Chekechea (Nursery) kwa watoto wa kikristo.
Mtoto wa kikristo si dhambi kushiriki nyimbo za shuleni na watoto wengine..Maadamu nyimbo hizo zimejulikana ni za kimaadili na za kujifunza na zipo katika mtaala wa shule!..Lakini nyingine zozote zilizosalia za kidua ambazo si za kielimu wala si za kiheshima, wala hazipo katika mtaala wowoe wa kishule watoto wa kikristo hawaruhusiwi kushiriki wa vyovyote vile.
Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NYIMBO ZA WOKOVU
Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?
TENZI ZA ROHONI