Historia ya nyimbo KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili~ Tis So Sweet to Trust in Jesus.
Wimbo huu uliandikwa na mwanamke mkristo wa kiingereza aliyeitwa, Louisa M. Stead, Mnamo mwaka 1882, Ni wimbo unaoeleza furaha mtu anayoweza kuipata katika kumtegemea Kristo, Lakini nyuma ya uandishi wa wimbo huu, imelala historia nzito ya Maisha aliyopitia Louisa M stead,
Ilikiwa ni siku moja Louisa na mumewe Pamoja na mtoto wao wa kike aliyeitwa Lily, walipanga safari ya kwenda matembezi, wakiwa ufukweni mwa kisiwa kimoja ghafla walisikia sauti kama ya mtu inapiga kilele za kuzama, kwenda kukimbia kuangalia wakamwona kijana mmoja, hilo lilimfanya mume wa Louisa, ajaribu kwenda kumwokoa, lakini katika jitihada zake za kufanya hivyo kwa bahati mbaya wote wawili wakazama, wakafa (kijana Pamoja na mume wake), mbele ya macho ya Louisa na binti yake.
Maisha yao baada ya hapo yalianza kuporomoka, Maisha yakawa magumu, Lakini wakagundua kuwa Mungu hakuwaacha katika hali zao, aliwatimizia mahitaji yao, hapo ndipo Louisa na binti yake walijifunza kumtegemea Mungu, na ndipo akauandika wimbo huu;
*****
Baadaye Louisa na binti yake wakasafiri kwenda Afrika kusini kwa kazi ya umishionari.
Lakini ni nini tunajifunza katika wimbo huu na uandishi wake?
Mimi na wewe tunaweza tukawa hatujapitia katika hali ngumu kama aliyopitia yeye, lakini yeye aliyeyapitia amemwona Mungu akimpigania, mpaka anaimba na kusema, “Nimemwona thabiti”..Hiyo ni kuonyesha kuwa hata wewe ukimwamini Yesu na kumtegemea, ..Utamwona thabiti/hakika akiwa na wewe katika maisha yako haijalishi leo unapitia mahali pagumu kiasi gani.
Imba wimbo huu ukikumbuka matendo yote makuu aliyokutendea nyuma. Na hakika utausikia uwepo wake nafsi mwako.
Bwana akubariki.
Tazama chini historia za nyimbo nyingine za Tenzi.
Tafadhali share na wengine.
Mada Nyinginezo:
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
MWAMBA WENYE IMARA
USINIPITE MWOKOZI Lyrics
BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics
CHA KUTUMAINI SINA lyrics
UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate ‘Neno la siku’ kila asubuhi. Na mistari mingine mingi ya faraja ..kwa link hii >>> https://chat.whatsapp.com/GRri9BATojl2FNGbOJpjC6
Mistari ya biblia ya uponyaji.
Inawezekana wewe ni mgonjwa na pengine unapitia katika hali ya kukata tamaa kabisa ya kupona, au unao ugonjwa usioponyeka mfano Ukimwi au Kansa, lakini nataka nikuambie jambo moja, kwa mwanadamu ni kweli haiwezekani lakini kwa Mungu hakuna linaloshindikana,
Hapo kabla nilikuwa ninasikia tu shuhuda za watu wengine kuponywa, nikadhani pengine mimi sistahili, lakini nilipokuwa katika dhambi siku moja Yesu Kristo aliniponya ugonjwa wangu wa sikio uliokuwa unanisumbua kwa muda mrefu, Na hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa kumtazama Kristo kwa sura nyingine, na kuendelea hapo aliniponya mara kadhaa tena katika vipindi tofauti tofauti nilipougua..Kama alinifanyia mimi niliyekuwa na dhambi, atakufanyia na wewe pia.
Kwa maana Yesu mwenye upendo yeye mwenyewe alituambia hivi..
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.
Hivyo nawe pia unapoitafakari mistari hii, nakuombea kwa Mungu ikafanyike Uponyaji mkubwa ndani ya mwili wako na maisha yako kwa ujumla, katika jina la YESU KRISTO.
Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. 2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. 3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.
Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.
Zaburi 30:2 “Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya”.
Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”.
2Wafalme 20:5 “Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana”.
Zaburi 146:8 “Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki”;
3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”.
Yeremia 17:14 “Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu”.
Zaburi 118:17 “Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana”.
Zaburi 119:50 “Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, Ya kwamba ahadi yako imenihuisha”.
Mathayo 8:17 “ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu”.
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Mathayo 14:14 “Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao”.
Yeremia 30:17 “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye”.
Isaya 57:18 “Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. 19 Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema Bwana; nami nitamponya”.
1Petro 2:24 “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa”.
Mathayo 9:35 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”.
Yakobo 5:14 “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana”.
Zaburi 6:2 “Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika”.
Mathayo 8:1 “Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. 2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika”.
Mathayo 8:1 “Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.
2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika”.
2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwafuraha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu”.
Zaburi 107:19 “Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao, 21 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.”.
Zaburi 107:19 “Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao,
21 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.”.
Zaburi 103:2 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. 3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote”
Zaburi 103:2 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote”
Kumbukumbu 7:15 “Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao”.
Hosea 14:4 “Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha”.
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa; 3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
Amini!, Endelea kuamini, uponyaji wako hakika umekufukia.
Tafadhali Share, na kwa wengine ujumbe huu wa faraja,.
Pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya biblia kwa njia ya email au kwa Whatsapp tutumie ujumbe kwa namba hii: +255693036618 / +255789001312
YESU MPONYAJI.
Aponywa Ukimwi.
Ameponywa kansa iliyokuwa katika hatua ya Nne.
RABI, UNAKAA WAPI?
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. Na mistari mingine mingi ya faraja ..kwa link hii >> https://chat.whatsapp.com/GRri9BATojl2FNGbOJpjC6
Mistari ya biblia kuhusu upendo.
Upendo ndio nguzo ya kwanza katika Ukristo. Unaweza ukawa na vyote, lakini ukikosa upendo wewe mbele za Mungu si kitu kabisa,
Biblia inazungumza juu ya upendo wa aina 4:
1 Wakorintho 13:1-8 1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
1 Wakorintho 13:1-8
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. (1Yohana 4:8)
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.(1Petro 4:8)
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. 35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (Yohana 13:34-35)
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (Yohana 13:34-35)
Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. (Mithali 10:12)
Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. (1Yohana 4.11)
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.(1Wakoritho 16:14)
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.(Wakolosai 3:18-19)
Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. (Wimbo 3:4)
Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu, Nao wa kuume ungenikumbatia. (Wimbo 8:3)
Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.( Wimbo 8: 6)
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. (Marko 10:6-9)
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. (Marko 10:6-9)
Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.( Luka 6:27-30)
Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.( Luka 6:27-30)
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. (Mathayo 5:43-48)
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. (Mathayo 5:43-48)
Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. (Warumi 12:20-21)
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.(Warumi 12:21)
Upendo huu ndio upendo wa hali ya juu kuliko yote (Agape), upendo wa kujitoa wakfu, usiojali hali, usiojali uzuri au ubaya wa mtu, usio na chembe yoyote ya mapungufu, Upendo wa Mungu.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16)
Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. (1Yohana 4:9-12)
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. (1Yohana 4:9-12)
Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. (1Yohana 4:19)
Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. (Yohana 15:12-13)
Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. (Yohana 15:12-13)
Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; (Kumbukumbu 7:9)
Hivyo mimi na wewe ili Upendo wa namna hii uingie ndani yetu, Ni sharti kwanza tumpende yeye mwenye Upendo huo.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. (1Yohana 4:16)
Hiyo ndilo kusudi la kwanza la sisi kuwepo hapa duniani..Kumpenda Yeye.
Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Marko 12:29-30)
Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Marko 12:29-30)
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?
Je Mungu anawapenda watu wote au ana chuki?
YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.
Je! Ule mwiba uliokuwa katika mwili wa Paulo ulikuwa ni nini?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
Kuota upo kanisani inamaanisha nini kimaandiko?
Hiyo ni ndoto njema itakayo kwa Mungu. Kamwe shetani hawezi kukuotesha ndoto ya namna hiyo..
Kama umeota ndoto hii kuna mawili. La kwanza ikiwa wewe ni mkristo uliyeokoka na umesimama imara, Hapo ni Mungu anakuonyesha kuwa upo katika njia sahihi, hivyo endelea kumtafuta Bwana kwa bidii Zaidi kwasababu Upo uweponi mwake..Daudi alisema..
Zaburi 122:1 “Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana”.
Kwasababu huko ndipo Mungu alipo. Kanisani na nyumbani mwa Bwana, kwahiyo ukiota upo kanisani ni ishara kuwa inaishi kwa Mungu.
Lakini ikiwa umeiota ndoto hii upo kanisani, na huku nyuma unajijua kabisa hauna mahusiano yoyote na Mungu, au hata kanisani huendi, Maisha yako ni ya dhambi..
Basi ujue hiyo ni sauti ya Mungu, anayokuvuta kwake,..Anakuonyesha kuwa hapo ndipo unapopaswa uwepo, hapo ndipo nyumbani kwako.. Wewe sio wa ulimwengu huu.
Hivyo itii sauti ya Mungu, mgeukie yeye, kwasababu huwezi jua ni kwanini afanye hivyo kwako leo… Kumbuka duniani hapa sisi ni wapitaji pengine kesho inayodhani itakuwepo inaweza isiwe yako.
Hivyo fanya uamuzi haraka wa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuucha ulimwengu moja kwa moja, na ukifanya hivyo YESU atakusamehe, Fahamu hiyo ndoto inatoka kwa kwa Mungu kabisa hivyo usiipuuzie. Mungu huwa anazungumza na watu wakati mwingine hata Zaidi ya mara moja.
Ayubu 33: 14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani”;
Ayubu 33: 14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani”;
Pengine Mungu alishazungumza na wewe kwa njia mbalimbali utubu dhambi zako umgeukie. Leo hii usiifanye shingo yako kuwa ngumu.
Kama upo tayari kuokoka na kuanza Maisha mapya na Yesu Kristo basi huo utakuwa ni uamuzi wa busara sana kwako..Unaweza kusema mimi mboni ni muislamu, haijalishi wewe ni nani, Mungu anakuita, kwasababu amekuchagua wewe na anakupenda, na anataka kukuokoa upate uzima wa milele..Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa Sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na hayo mengine yaliyosalia Bwana atakusaidia kuyashinda.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
KUOTA UPO UCHI.
Hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge.(Ufu 21:27)
FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.
Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?
Kuota umechomwa kisu au Kuota umepigwa risasi kuna maanisha nini?
Awali, ni vyema kujua kuwa si kila ndoto aotayo mtu, ina maana katika maisha yake, Hilo ni vizuri ukalifahamu, Ndoto nyingi tunazoziota kila siku zinatokana na shughuli zetu za kila siku (Mhubiri 5:3), au mazingira yanayotuzunguka, au mambo ambayo tunayawaza mara kwa mara, au tulishawahi kuyaona, au kuyapitia sehemu Fulani katika maisha yetu (Isaya 29:8)..
Naweza kusema asilimia 90 ya ndoto tunazoziota kila siku zinaangukia katika kundi hili,.Hapo ndipo watu wengi wanaposhindwa kuelewa, wanataka kila ndoto wapate tafsiri ya rohoni, au maishani, hilo jambo halipo, utaishia kudanganywa, au kujidanganya mwenyewe, Kumbuka kinachoweza kueleza hatma ya maisha yetu kwa ufasaha wote, sio ndoto tunazoziota usingizini, bali Neno la Mungu tunaloliishi kila siku.
Mungu anaziita ndoto kama makapi ukifananisha na Neno lake(Yeremia 23:28-29). Akiwa na maana kuwa mtu Yule anayeishi kwa kulishika Neno lake, Ni bora kama ngano, kuliko yule anayetafuta maana za ndoto zilizofananishwa na makapi.
Ni mara chache, ndoto zinabeba ujumbe, ili kutambua ndoto yako inatoka kwa Mungu au kwa shetani, au kwako mwenyewe, basi fungua hapa usome kwanza>>> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?
KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.
Hivyo ukiwa umeshasoma, na unao uhakika kabisa kuwa ndoto uliyoota, si ya kawaida, imekujia kwa uzito mwingine wa kitofauti, imekushtua sana, imeonekana kama ni jambo la halisi kabisa, basi upo ujumbe wa rohoni.
Sasa kwa namna ya kawaida, ukishaona mpaka mtu amefikia hatua ya kukuchoma kisu, au amekupiga risasi ni wazi kuwa kuna jambo ulilifanya, au unalifanya sasa hivi, ambalo limemchukiza sana, kiasi cha kufikia uamuzi wa kuona kufa kwako ni bora kuliko kuishi.
Vivyo hivyo katika ndoto ukiona umepigwa risasi, au umechomwa kisu, au upanga, au mkuki,au kitu chenye ncha kali, hiyo ni ishara kuwa maishani mwako, lipo jambo ambalo unalifanya, halifurahiwi na wengine, aidha ni zuri au baya,
Katika biblia tunasoma habari ya mtu mmoja, aliyeitwa Egloni mfalme wa Boabu, huyu, aliwatumikisha Israeli kwa muda wa miaka 18, na hiyo yote ilikuwa ni kutokana na makosa yao wenyewe(Israeli)..Lakini walipomlilia Mungu, awaokoe kutoka katika utumwa na mateso ya mfalme huyu, Mungu akawasikia ndipo akawapelekea mwokozi aliyeitwa Elihu.
Huyu Elihu alijifanya kama mjumbe, aliyeituwa na Israeli, kumbe hila zake zilikuwa ni kwenda naye katika chumba cha siri, ili wakiwa wao wawili peke yao achomoe upanga wake na kumchoma tumboni, Tusome kidogo..
Waamuzi 3:20 “Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake. 21 Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake; 22 hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma. 23 Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo. 24 Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi. 25 Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa”.
Waamuzi 3:20 “Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake.
21 Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake;
22 hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma.
23 Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo.
24 Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi.
25 Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa”.
Umeona? Sasa huyu Elgoni alichomwa kutokana na makosa yake, lakini, pia wapo wengine waliochomwa kutokana na haki zao, mfano mmojawapo ni Bwana wetu YESU KRISTO..Yeye alichomwa mkuki pale msalabani, sio kwasababu alikuwa mwovu hapana.
Hivyo na wewe jiangalie ni wapi katika maisha yako, pana vita kwa wengine, wewe umesimama, Ikiwa upo ndani ya Kristo basi, ujue maadui wa imani wapo, lakini huna haja ya kuogopa, Kwasababu Mungu atakupigania, kikubwa unachopaswa ufanye ni kuzidi kuwa mwombaji.
Lakini kama upo nje ya Kristo, ukweli ni kwamba, licha tu kuzungukwa na hatari za maadui, lakini, maisha yako ya rohoni yapo hatarini.. Mungu anaweza kweli kukuepusha na hatari za mwilini, lakini zile za rohoni za ibilisi hawezi kukuzuia kutokana na kwamba wewe ni milki ya ibilisi.
Jiulize ukifa leo ghafla katika dhambi utakuwa mgeni wa namna huko uendako?
Hivyo ndugu ikiwa unahitaji kumpa leo YESU maisha yako..Basi uamuzi huo utakuwa ni busara sana kwako, Kama upo tayari kufanya hivyo, moja kwa moja fungua hapa, kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na hayo mengine yaliyosalia Mungu atakujalia rehema zake.
Kwa mafundisho zaidi ya Neno la Mungu.
Whatsapp: +255 789001312
Kuota unafanya Mtihani.
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.
HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?
NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
Kuabudu Sanamu ni nini? Na ibada za sanamu ni zipi?
Kuabudu sanamu: Katika agano la kale ni kitendo chochote cha kwenda kuabudu au kusujudia, au kutumika kitu kingine chochote, tofauti na Mungu mkuu mmoja aliye hai (YEHOVA).
Moja ya amri 10 Mungu alizowapa wana wa Israeli, ilikuwa ni pamoja na kujiepusha na ibada za sanamu za aina yoyote..
Amri ya pili inasema hivi..
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
Hivyo mtu akikigeuza kitu chochote, kuwa mbadala wa Mungu, huko ni sawa na kuabudu sanamu, ukiweka mdoli nyumbani kwako na kwenda kumpigia magoti na kumwomba kana kwamba ni Mungu, ujue hapo unafanya ibada za sanamu..
Ukitengeneza kinyago chenye sura ya mtakatifu Fulani labda Mariamu, au Bwana Yesu akiwa pale msalabani, kisha ukakihusianisha na mambo ya ibada kwa mfano kukisujudia, au kukiabudu, au kuombea dua zako kwa kupitia hicho, tayari hiyo ni ibada za sanamu,
Ukining’iniza picha ukutani ya mtu Fulani maarufu, au mnyama , au kitu Fulani kwa lengo la kukifanya kama kipatanishi chako na Mungu, au kitu chako kinachoweza kukupa bahati Fulani, hiyo tayari ni ibada za sanamu.
Hata ukipanda mti, au Ua fulani, ukiamini kuwa linaweza kukulinda, au kueleza hatma ya maisha yako, tayari hiyo nayo ni ibada za sanamu.
Kumbukumbu 16:21 “Usipande mti uwao wote kuwa Ashera kwako kando ya madhabahu utakayofanya ya Bwana, Mungu wako.”
Na ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu, yanayomtia wivu kiasi cha Mungu kukupatilizia maovu hata ya baba zako, uone ni jinsi gani kitendo hicho kinavyomuudhi Mungu..
Ipo mifano mingi sana katika biblia, ya watu walioadhibiwa kwa makosa kama haya..Kumbuka hili ndilo lililowafanya wana wa Israeli wengi wasiione Kaanani, kadhalika hili ndilo lililochangia wana wa Israeli tena baadaye kuchukuliwa utumwani Babeli.
Hivyo kuhusianisha kitu chochote na Ibada ni hatari sana, Ibada zako zote zinapaswa zimwelekee Mungu peke yake.
JE! KUABUDU SANAMU/IBADA ZA SANAMU KATIKA AGANO JIPYA KUKOJE?.
Tukirudi katika agano jipya, kuabudu sanamu sio tu kwenda kusujudia vinyago tu peke yake n.k., hapana ni Zaidi ya hapo, biblia inasema..
Waefeso 5:5 “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu”.
Unaona, mtu yeyote ambaye ni mchafu, mbele za Mungu ni mwabudu sanamu, Mtu yeyote aliye na tamaa mbele za Mungu huyu naye ni mwabudu sanamu.
Hawa wote biblia inasema hawana urithi katika ufalme wa Mungu.
Hivyo mimi na wewe tunapaswa tujiepushe na Ibada zote mbili, yaani sanamu za nje, Pamoja na zile Sanamu za ndani. Ili Mungu atupokee tukaurithi uzima wa milele aliyotuandalia tumpendao.
Ikiwa hujaokoka na unataka kufanya hivyo leo, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara kwako. Fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba.>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ubarikiwe.
Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?
USIABUDU SANAMU.
CHAPA YA MNYAMA
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
NEEMA YA MZALIWA WA PILI.
HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.
Usinipite mwokozi Lyrics| Swahili, – “Pass me not, O Gentle Savior”
Historia ya nyimbo Usinipite mwokozi.
Wimbo huu uliandikwa mwaka 1868, na mwanamke wa kimarekani aliyeitwa Fanny Crosby. Mwanamke huyu mkristo alizaliwa akiwa mzima lakini wiki 8 baada ya kuzaliwa kwake alipatwa na opofu, ambao ulidumu mpaka kufa kwake, lakini katika maisha yake yote aliyoishi hapa duniani (yaani miaka 94), haikuwa bure kwa Mungu wake, alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8,000..Hivyo hiyo ikamfanya apate umaarufu na kumfanya ajulikane kwa jina la “mtunzi-kipofu-wa-nyimbo-za-tenzi”, na “Malkia wa nyimbo za Injili”.
Lakini siku moja alipokuwa amealikwa kwenda kuzungumza na wafungwa wa mji, na alipokuwa akitembea kule gerezani alimsikia mfungwa mmoja akisema “Bwana mwema usinipite, usinigeuzie mgongo wako,unikumbuke”,
Fanny anasema aliguswa sana na maneno yale, jambo ambalo halikuondoka kwenye kichwa chake mpaka alipofika nyumbani. Na huko ndipo alipoandika beti zote nne za wimbo ujulikanao kama USINIPITE MWOKOZI.
Alipomaliza kuuandika akampa muhusika wa kuweka midundo, na mwaka, 1870 wimbo huo, ulizinduliwa rasmi katika machapisho..
Na kwa kipindi kifupi` sana ukapata umaarufu mkubwa duniani kote.
Jambo hili tunaliona kwa wale kipofu wawili waliomsikia Yesu anapita..
Mathayo 9:27 “Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, UTUREHEMU, MWANA WA DAUDI. 28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate”.
Mathayo 9:27 “Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, UTUREHEMU, MWANA WA DAUDI.
28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate”.
Na itakuwa hivyo na kwako:
Ikiwa wewe umeokoka, na unaona unapita katika hali ngumu, ambayo unaona kwa namna ya kawaida huwezi kutoka, basi wakumbuke watu kama hawa, wakutie nguvu,..Zidi kumwita Yesu, atakuonekania kwa wakati wake. Kwasababu yeye anatupenda na kutujali, na yote yanawezekana kwake.
Lakini kama hujaokoka, basi ni vizuri leo ukamwita kwanza mwokozi akuokoe maisha yako, usiruhusu akupite, anapokwenda kuwapa wengine uzima wa milele, sema na mimi leo nauhitaji huo uzima, hivyo kama upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa, kwa ajili ya Sala ya Toba..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki..
Tazama historia ya nyimbo nyingine za Tenzi chini.
TENZI ZA ROHONI
Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?
MUONEKANO MPYA WA YESU BAADA YA KUFUFUKA.
UNYAKUO.
BWANA MUNGU NASHANGAA KABİSA lyrics ~Swahili (How Great Thou Art).
Toleo la kwanza kabisa la Wimbo huu liliandikwa na mtu mmoja raia wa Sweden, aliyeitwa Carl Boberg wimbo huu aliuandika mnamo mwaka 1885 baada ya kuvutiwa na mazingira aliyopishana nayo alipokuwa akitoka Kanisani yeye na marafiki zake. Anasema muda wa mchana walipokuwa njia hali ya hewa iliwabadilikia ghafla, wakaona wingu la tufani likitokea kwa mbali, na mara hiyo hiyo kukaanza kumulika mianga mingi kama ya radi angani, upepo mzuri ukaanza kuvuma juu ya mashamba yaliyokuwa pembeni, Na kisha manyunyu ya mvua matulivu yakaanza kudondoka juu yao, na baada ya muda kidogo, wingu lile la tufani likapotea, muda huo huo ukatokea upinde mzuri wa mvua angani..
Na alipofika nyumbani na kufungua madirisha atazame nje, aliona ufukwe ya mji wake kama vile kioo, akatazama upande wa pili akasikia ndege wazuri wakitoa milio yao na kwa mbali kegele za kanisa zikilia, Hapo ndipo wimbo huu ulipomjia kichwani kuutunga na kuuandika.
****
Bwana Mungu nashangaa kabisa,
Nikifikiri jinsi ulivyo,
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia,
Viumbavyo kwa uwezo wako.
Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu, Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu.
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Jinsi wewe ulivyo mkuu.
Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba nawasikia,
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia.
Nikikumbuka vile wewe Mungu,
Ulivyompeleka mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno.
Yesu Mwokozi atakaporudi,
Kunichukua kwenda mbinguni,
Nitaimba sifa zako milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.
Tujiulize na sisi tunao utaratibu kwa kukaa chini na kuushangaa utukufu wa Mungu na kumtukuza?..Au kila kitu tunaona ni kawaida tu..Kumbuka Sifa kamili kama hizi mbele za Mungu ni bora kuliko dua na sala tunazompelekea kila siku.
Mungu anataka kuona, na sisi tukiufurahia uumbaji wake, kwa kumwimbia.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
Karibu tuongeze maarifa ya rohoni. Yapo maswali machache ya kujiuliza ambayo yanaendelea katika jamii yetu..maswali hayo ni je! popobawa ni nani? Na je popobawa ni kweli yupo?..
Popobawa kulingana na waathirika wanasema ni viumbe (majini)..yanayowatokea watu usiku na kuwaingilia watu kinyume na maumbile pasipo hiari yao. Viumbe hao wanaonekana wakati wa usiku tu!..na vinawaingilia watu wa jinsia zote, wakiume na wakike pamoja na watoto wadogo.
Sasa kabla ya kujua hawa viumbe (popobawa ni nani)?..Hebu kwanza tujifunze historia ya uumbaji kulingana na biblia.
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye IBILISI NA SHETANI, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”.
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye IBILISI NA SHETANI, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”.
Biblia inasema hapo huyo joka aliyetupwa chini ni shetani/ ibilisi, na hakutupwa peke yake, bali alitupwa pamoja na Malaika zake… Sasa hapo kwenye hilo neno “pamoja na malaika zake” ndio kiini cha somo hili.
Kama tunavyojua katika vita Yule kiongozi wa juu..hana tabia zinazofanana na wanajeshi wake asilimia mia…Ni wazi kuwa kila mwanajeshi anatabia yake na kazi yake maalumu..wapo wanajeshi waangani, wapo wa nchi kavu, wapo wa majini..Na katikati ya hao wanajeshi wapo wakatili sana, na wapo wenye roho ya wastani, na pia wapo wenye tabia mbaya na wapo wenye tabia za wastani…Na wanapopigwa basi wote wanakuwa wameshindwa na wanaonekana waasi…kwasababu wanashirikiana kwa kila kitu.
Kadhalika na malaika wa shetani ni hivyo hivyo, hawa malaika wa shetani baada ya kuasi na kushindwa vita mbinguni waligeuka na kuwa mapepo…sasa sio wote wanatabia zinazofanana..wapo walio wabaya sana, na wapo walio wa wastani..lakini wote ni wabaya tu!..kwasababu wanafanya kazi katika upande wa giza!..lakini wanatofautiana viwango…Na pia wanatofautiana vitu wanavyovipenda..yapo mapepo yanayopenda mazingira ya ulevi, yapo yanayopendelea mazingira ya uuaji na ukatili, yapo yanayopendelea mazingira ya uzinzi na uasherati, yapo yanayopendelea mazingira ya wizi n.k…Kama vile jinsi watu walivyo na tabia tofauti tofauti na haya mapepo ni hivyo hivyo.
Sasa pepo linaloitwa na watu “POPOBAWA” lipo katika hilo kundi la mapepo yanayofanya kazi katika mazingira ya UZINZI na UASHERATI. Kwa ufupi ni mapepo ya “uzinzi”…Lipo kundi moja na hayo mengine wanayoyaita “majini mahaba”..Yote yanafanya kazi moja ambayo ni “kupalilia dhambi ya uasherati duniani”.
Na Mapepo hayo (popobawa na mengineyo) yanaweza kuwatokea watu kwenye ndoto! Au kwa wazi kabisa..Lakini huwa ni nadra sana kutokea kwa wazi, mara nyingi yanawajia watu kwenye ndoto. Kwahiyo hiyo popobawa ni kweli yupo?; Jibu ni ndio yupo!…anaweza kujulikana kwa majina tofauti tofauti kulingana na mahani na mahali…na pia anaweza kuonekana kwa maumbo tofauti tofauti, sio lazima aonekane na mabawa ya popo kama, anavyoshuhudiwa na watu….Ni mapepo yaliyoasi pamoja na shetani mbinguni, hivyo yanaweza kuchukua umbo lolote lile.
Sasa ni kwanini haya maroho (popobawa) yanawatokea watu na kuwafanya hayo yanayofanya?
Jibu ni rahisi sana..ni kutokana na hali za kiroho za watu!.
Mtu yeyote aliye nje ya Kristo ambaye hajaokoka anakuwa ni mlango uliofunguliwa wa kuingiliwa na roho yoyote ya mapepo…Na mapepo hayo yanayomwingilia yanaweza kumfanya chochote yanachokitaka kwa jinsi tabia zao zilivyo…kama ni pepo la uzinzi basi likimwingia litamfanya kuwa mzinzi, na hata linaweza kumtokea na kumwingilia..kama ni pepo la uuaji ni hivyo hivyo.
Hakuna mtu yoyote ambaye ameokoka kikamilifu na akasumbuliwa na hizi roho, hakuna! Kwasababu biblia inasema..Mtu aliye ndani ya Kristo “uhai wake unakuwa umefichwa” (Wakolosai 3:3).
Sasa ni namna gani unaweza kujidhibiti na hizi roho za popobawa na nyinginezo?
Kuna uongo uliozagaa kwamba unaweza kuzidhibiti kwa kuchoma ubani au udi, au kutojiangalia kwenye kioo, au kulala huku umevaa nguo, au kukesha usiku, au kulala na mfupa wa nguruwe!. Ndugu usidanganyike hakuna njia hata mojawapo ya hizo inayowafukuza au kuzidhibiti hizo roho. Dawa ni moja tu!..Ingia ndani ya Yesu UHAI WAKO UFICHWE. (Mwisho wa somo hili nitakufundisha jinsi ya kuingia ndani ya Yesu)!. Ukitumia njia nyingine ndio utayaita zaidi badala ya kuyafukuza.
Pili utafanyaje kama tayari umetembelewa na hizi roho(popobawa) na bado zinakusumbua katika mwili na hata katika ndoto?.
Usiende kutafuta msaada kwa waganga wa kienyeji, wala usiende kutangaza…upo usemi kuwa ukienda kutangaza ndio zitaacha..nataka nikuambie tu hazitaacha!..badala yake ndio zitazidi, pengine utaona unafuu kwa kipindi Fulani lakini bado zipo ndani yako na zitaendelea kukutesa. Suluhisho pekee ni YESU KRISTO.
Sasa utaingiaje ndani Yesu Kristo! Ili usalimike na hayo mapepo?(popobawa na mengine) pamoja na kuurithi uzima wa milele.
Hapo ulipo piga magoti peke yako!..Sali sala hii kwa imani…Sema..
“Bwana Yesu nakuja mbele zako leo, mimi ni mwenye dhambi, naomba nisamehe dhambi zangu zote, nami nawasamehe wale wote walionikosea…naomba nioshe kwa damu yako iliyomwagika pale msalabani…kuanzia leo nakupokea wewe maishani mwangu.. Nisaidie nisiishi tena katika dhambi, naomba uniponye na roho zote za adui kuanzia leo, roho zote za uasherati, na nyingine zote zinazoninyemelea, zisinifuate tena… katika Jina lako tukufu, jina la Yesu. Amen”
Baada ya kusali sala hii kwa imani, amini kwamba tayari Bwana Yesu kashaingia ndani yako…kuanzia sasa utaanza kuona kuna amani Fulani inaingia ndani yako..Na yale maroho ambayo leo umeyakana kwa kinywa chako tayari hayana mamlaka tena juu yako, wewe ni mshindi…Hivyo usiishi tena katika dhambi, wala usijiuhusishe na mazingira yoyote ambayo maroho hayo yanayapenda…mazingira kama kwenye disko, mazingira ya kutazama picha za ngono mitandaoni..na mengineyo..Kuanzia sasa tafuta kanisa lolote la kiroho lililo karibu nawe..Nenda huko kuanzia leo..Bwana atazungumza na wewe huko huko kupitia watu utakaowakuta huko. Pia anza kusoma kitabu cha Mathayo ili roho yako ianze kujengeka na kukua.
Bwana akubariki sana.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
JINI MAHABA NI NINI?
JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?
JE VIBWENGO NI KWELI VIPO?
MAJINI WAZURI WAPO?
MAJESHI YA PEPO WABAYA.
CHA KUTUMAINI SINA, Swahili Lyrics. (My hope is built on nothing less)
Tenzi hii iliandikwa na mchungaji wa kanisa la kipatisti, aliyeitwa Edward Mote, raia wa nchi ya uingereza, mnamo mwaka 1834, Edward Mote alifanikiwa pia kuandika tenzi nyingine nyingi Zaidi ya 100, lakini iliyopata umaarufu mkubwa ni hii ijulikanayo kama “Cha Kutumaini sina”.
Tenzi hii aliibuni akirejea ule mfano alioutoa Bwana Yesu wa mjenzi mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba imara, Na yule mpumbavu ambaye aliijenga nyumba yake https://www.high-endrolex.com/2juu ya mchanga (Mathayo 7:24-27), Na kuonyesha ni jinsi gani mtu anapaswa aishi kwa kwa kumtegemea Kristo aliye mwamba salama, na ulio imara.
1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”
Na ndio hapo akaundika wimbo huu;
Cha kutumaini sinaIla damu yake Bwana,Sina wema wa kutoshaDhambi zangu kuziosha;
Kwake Yesu nasimama,Ndiye mwamba; ni salamaNdiye mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefuYeye hunipa wokovu;Mawimbi yakinipigaNguvu zake ndiyo nanga.
Damu yake na sadakaNategemea daima,Yote chini yakiisha,Mwokozi atanitosha.
Nikiitwa hukumuni,Rohoni nina amani;Nikivikwa haki yakeSina hofu mbele zake.
Amen hata mimi na wewe, tukiwa ndani ya Kristo, tupo salama wakati wote, lakini tukimkosa yeye ndani yetu, basi hata kuimba kwetu ni bure, tutakuwa tu sawa na yule mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga..
Hivyo ukiwa unahitaji kuokoka ili Yesu leo awe kweli Mwamba ulio salama, basi fungua hapa kwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
MWAMBA WETU.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/2-swali-kwanini-mtu-atoe-pepo-aombee-wagonjwa-wapone-asikie-sauti-ya-mungu-ikimwambia-hiki-na-kile-kuhusu-watu-na-yeye-mwenyewe-kufunua-siri-za-mioyo-yao-aone-maono-na-kutembea-na-malaika-katika/