Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?

Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?

SWALI: Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi/manukato (perfumes)?


JIBU: Sio vibaya kujipaka mafuta usoni au mwilini, ili kuondoa ule mpauko wa asili, mafuta hususani yale ya asili ni mazuri kwa ngozi, lakini pia sio amri kwamba lazima tujipake mafuta, hata hivyo ngozi zetu huwa zinatoa zenyewe mafuta yake ya asili.

Lakini yapo mafuta ya kuchubua ngozi, na yenye marashi makali, hayo ni kinyume na maandiko kuyatumia kwasababu lengo lake ni kubadilisha maumbile, ambayo maudhui yake ni Udunia!..Biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na pia miili yetu sio mali yetu wenyewe, ni mali ya Mungu, hivyo hatupaswi kuibadilisha kutoka katika hali yake ya asili na kuifanya tutakavyo sisi (1Wakorintho 6:19).

Sasa unaweza kuuliza ni wapi katika agano jipya tumepewa ruhusa ya kutumia mafuta?

Mathayo 6: 16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

17  Bali wewe ufungapo, JİPAKE MAFUTA KİCHWANİ, UNAWE USO;

18  ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”

Hayo ni maneno yaliyozungumzwa na Bwana Yesu mwenyewe.

Swali lingine ni je! Ni mafuta gani yanayofaa?..Hakuna orodha maalum  ya mafuta yanayofaa, kikubwa mafuta yoyote yale yawe ya kiwandani au ya asili ambayo hayana kemikali nyingi na hayana marashi makali yanafaa kutumika.

Na Marashi ni hivyo hivyo, yapo marashi ya nguo..ambayo lengo lake ni kudhibiti nguo isitoe harufu mbaya aidha ya jasho au ya kitu kingine kisichofaa. (Katika mazingira fulani)

Nayo pia sio vibaya kuyatumia, ilimradi tu yasiwe na maudhui ya kishetani. Marashi yanayotumika mengi siku hizi yana maudhui ya kidunia, marashi mtu anayotumia ambapo mtu aliyesimama mita 2 mbele yake au nyuma yake anasikia harufu yake, tayari lengo la marashi hayo sio kudhibiti harufu bali kuvuta hisia kutoka kwa mwingine…jambo ambalo sio sawa.

Kiwango cha marashi kinapaswa kiwe kidogo sana)..kiasi kwamba mpaka pua ifike karibu na nguo ndipo isikike..(na hiyo ni kama kuna ulazima wa kuyatumia kutokana na mazingira, lakini kama hakuna ulazim hayapaswi kutumika kabisa).

Na zaidi sana, mafuta mengi tunayotumia au sabuni zina kiwango tosha cha marashi ambayo hatuhitaji kuongeza mengine juu yake.

Katika biblia marashi yametafsiriwa sehemu kadha wa kadha kama “Marhamu” au “Manukato”. Unaweza kupitia mistari ifuatayo binafsi (Mathayo 26:7-13, Marko 14:3, Marko 16:1).

Lakini zaidi sana Marashi yetu yanayompendeza Mungu ni Maombi yetu kwake, na utakatifu wetu.

Ufunuo 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa MANUKATO, AMBAYO Nİ MAOMBİ YA WATAKATİFU”.

2Wakorintho 2:14  “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.

15  Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;

16  katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo”

Hivyo tukiwa maridadi wa mwilini, tukanukia vizuri na huku rohoni tunatoa harufu mbaya, hatusali, hatufungi, hatuombi, hatuishi maisha ya kumpendeza yeye..basi mbele za Mungu tunapeleka harufu mbaya.

Lakini tukiwa waombaji, tukimwomba Mungu rehema, na neema..pamoja na tukiwaombea na wengine na kuliombea kanisa, na tukiishi maisha masafi, basi tutakuwa ni lulu mbele za Mungu.

Mungu atasaidie katika hilo.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Jeshi la Mbinguni wana wa Israeli waliloliabudu ni lipi?

SWALI: Ni jeshi gani la Mbinguni ambalo Mungu aliwaacha wana wa Israeli waliabudu katika Matendo 7:42? Je ni Malaika au?


JIBU: Matendo 7: 41  “Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao. 

42  Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?”

Habari hii inawazungumzia wana wa Israeli wakati wanatoka Misri. Wakiwa jangwani biblia inasema walikuwa wakikengeuka mara kadhaa, walikuwa wakimwacha Mungu na kugeukia kuchonga sanamu, na wakati mwingine kumjaribu Mungu (Kutoka 17:2).

Lakini kuna jambo lingine tunaliona walilokuwa wanalifanya ambalo lilikuwa ni machukizo kwa Mungu, na hilo si lingine zaidi ya KULIABUDU JESHI LA MBINGUNI.

Sasa swali la msingi hapo ni je! Hilo jeshi ni lipi?, ni malaika au ni nini?.

Jibu ni kwamba si Malaika, bali ni miungu ya kipagani. 

Si kila mahali kwenye biblia palipoandikwa neno “mungu” panamaanisha “Mungu wa mbingu na nchi”, vivyo hivyo sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “bwana” panamaanisha “Bwana Mungu wa mbingu na nchi”…hali kadhalika sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “mbingu” au “mbinguni”, panamaanisha “Mbinguni malaika watakatifu walipo”..

Dini karibia zote zinaamini kwamba kuna mbingu..kwamba kuna mahali huko juu ambapo kuna viumbe watakatifu wanaishi,..Na nyingine zinaamini huko mbinguni kuna miungu mingi, kuna jeshi kubwa la miungu, ambayo yote inastahili kuabudiwa. Kwamfano dini ya kihindu tu peke yake ina zaidi ya miungu milioni 330. 

Sasa ikatokea kwa mtu ambaye ni mkristo, ambaye ameshajua ukweli wote kwamba Mungu ni mmoja tu aliyeko mbinguni ambaye anaabudiwa katika roho na kweli.. akaiacha hiyo imani na kisha akaenda kujiunga na imani nyingine(kama hiyo ya kihundu) inayoamini kwamba mbinguni kuna miungu mingi, na akaenda kuiabudu hiyo miungu yao. Hapo ni sawa na kusema “AMEKWENDA KULİSUJUDİA JESHİ LA MBİNGUNİ”..na si mbingu ile ambayo malaika watakatifu wapo bali ni mbingu ya kihindu, ambayo kiuhalisia haipo! ni uongo uliotengenezwa na shetani tu kuwadanganya watu kuwa kuna mbingu yenye miungu mingi!,

Ni agenda ya  shetani na mapepo yake Kutafuta kuabudiwa na kuwapotosha watu wa Mungu. Hiyo idadi yote ya miungu wanayoiabudu ni mapepo yanayojiguza na kuchukua sura ya hivyo wanavyoviabudu. (zingatia: wengi wanaoabudu hiyo miungu, sio watu wabaya na wala si maadui zetu, wengi wao ni watu wazuri, wanafanya hayo kwasababu bado hawajaujua ukweli, au macho ya mioyo yao bado hayajafumbuliwa, kwahiyo wanaabudu vitu wasivyovijua, hivyo ni jukumu letu wewe na mimi kuwapelekea injili na kuwaombea!, ili macho yao yafumbuliwe wapate kuona na kuokolewa Matendo 17:29-31).

Kwahiyo Jeshi la mbinguni linalozungumziwa hapo sio Malaika waliopo mbinguni, bali ni miungu  iliyopo mbinguni huko angani, ambayo kiuhalisia ni shetani na mapepo yake.

Na malkia wa mbinguni aliyezungumziwa pia katika Yeremia 7:18, 44:17-25 sio Bikira Mariamu wala sio Malaika fulani wa kike aliyeko mbinguni bali ni mungu fulani wa kipagani, wanayedai kwamba yupo mbinguni (kwa maelezo marefu utatutumia ujumbe inbox), ambaye ni Pepo!.

Mwisho ni muhimu kuchukua tahadhari!.. pale tunapoonywa mara nyingi!…Hapo kwenye matendo 7:42, biblia inasema “ Basi MUNGU AKAGHAİRİ, AKAWAACHA ili waliabudu jeshi la mbinguni,”. 

Litazame hilo neno kwa makini!..Mungu akaghairi!, akawaacha!! İli waliabudu jeshi la mbinguni…Ni jambo la kuogopesha sana pale Mungu anapoghairi juu yako, na kukuacha uendelee kufanya unayoyafanya!…hilo ni jambo la kuogopesha sana!..Anaabudu masanamu unayodhani ni watakatifu Fulani wa mbinguni, na umeonywa mara nyingi husikii, hapo unamfanya Mungu aghairi juu yako.

Warumi 1:28  “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”

 

2Wathesalonike 2:10  “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo”.

Jiupeshe na ibada za sanamu ni dhambi, jiepushe na mambo yote maovu na mwisho soma neno kwa bidii..

Bwana atubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.

AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neema ya Bwana Yesu Kristo

 2Wakorintho 13:14 “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote”.


Hii ni salamu ya kumalizia ambayo mtume Paulo aliwaandikia wakorintho, na watu wote watakaousoma waraka huo (ikiwemo mimi na wewe).

Maneno haya, yamegusa Nyanja zote tatu za Kusudi la Mungu kwetu sisi wanadamu.

> Paulo anaanza kwa kusema, Neema ya Bwana Yesu Kristo, ikae nasi; Akiwa na maana kuwa mpaka sisi tukamilike, mpaka sisi tushinde, tunaihitaji hii neema ya Yesu Kristo wakati wote itembee na sisi, tukipungukiwa neema, basi ni ngumu kuweza kuushinda ulimwengu. Na neema hii inaanza kutembea juu ya mtu kwa mara ya kwanza pale anapookoka.

> Anasema tena, Pendo la Mungu likae nasi: Ni kwa njia ya upendo Mungu alitukuomboa (Yohana 3:16). Hivyo na sisi tukiukosa Upendo, haijalishi tutakuwa washirika wazuri kiasi gani, haijalishi tutafanya miujiza mingi kiasi gani, tutanena kwa lugha za malaika nyingi kiasi gani, bado sisi tutabakia kuwa si kitu. Hivyo Pendo la Mungu linapokaa ndani yetu basi Mungu anakuwa karibu na sisi. Na pendo la Mungu ndio lile linalozungumziwa katika 1Wakorintho 11:1-8

Na ndio huo Paulo alikuwa analiombea kanisa ukae ndani yao.

> Anamalizia na kusema pia Ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote; Hii ikiwa na maana palipo na Roho Mtakatifu pana ushirika.. Sisi kama wakristo tuliookoka ni jukumu letu kuutunza ushirika wa Roho tukinia mamoja, tukiifanya kazi ya Mungu..

Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.

6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”.

Mambo haya matatu yakienda pamoja na sisi, basi Mungu naye ataenda pamoja na sisi, lakini tukipungukiwa kimoja wapo, aidha neema, au Upendo, au Ushirika, ni ngumu kusimama kama Kanisa.

Hivyo mimi na wewe tujitathmini ni wapi, hatujakamilisha, kisha tukamilishe, Na Bwana atusaidie.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?

UPONYAJI WA ASILI

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

ADAM NA EVA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kibanzi na Boriti ni nini kama tunavyosoma kwenye biblia?

Kibanzi Na Boriti, kwenye biblia vinamaanisha nini?


Boriti ni kipande kikubwa sana cha mbao, kinaweza kikawa ni ki-gogo, au nguzo, au mbao yoyote pana..

Lakini kibanzi, ni kichembe kidogo sana cha mbao, kama mchanga, hata wakati mwingine kufikia kuwa kama vumbi  la mbao ambalo ni ngumu sana kuliona. Hicho ndicho  kibanzi.

Sasa Bwana Yesu alitoa mfano huo, wa picha ili kuweka msisitizo kile alichotaka kukisema, yaani katika hali ya kawaida, kama wewe huwezi kuona nguzo iliyosimama mbele ya macho yako inayokuzuia usione kabisa, utaona vipi vumbi la mbao lililo katika jicho la mwenzako?..Umeona moja kwa moja huo ni unafki..

Vivyo hivyo na sisi kabla hatujawahukumu watu, tuyachunguze maisha yetu Je! hayo wanayoyafanya Je, hayapo ndani yetu na sisi? Kabla hujamwambia Fulani acha usengenyaji, Je! na wewe si msengenyaji? Kama  sivyo basi ni heri ukae tu kimya, kwasababu mistari ya juu yake inasema, kipimo kile kile tuhukumucho ndicho tutakachokuhumiwa na sisi.

Mathayo 7:1 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Bwana atusaidie sote tuyashinde hayo.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?

UNYAKUO.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Israeli ipo bara gani?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

Rudi Nyumbani:

Print this post

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA (Mwongozo 2026).

Jiunge na channel yetu ya Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. kwa link hii >>> https://chat.whatsapp.com/GWxBOH2GXncIc0pwVIhnch


Mistari ya Biblia ya Faraja

Unaweza ukawa unapitia wakati mgumu, mateso, majaribu, jangwa, au shida. Kama mkristo, imani yako inaweza kujaribiwa. Lakini Biblia peke yake ndiyo inayoweza kukupa faraja ya kweli. Haijalishi maneno elfu kumi ya faraja kutoka kwa wanadamu, Biblia peke yake inaweza kukupa utulivu wa kweli.

Mistari ya Faraja kutoka Biblia

Wafilipi 4:13

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.

Isaya 41:10

“Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.

Isaya 40:31

“Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.

Kumbukumbu 31:6

“Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha”.

Isaya 40:29

“Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo”.

1 Wakorintho 10:13

“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

Kutoka 15:2

“Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza”.

Kumbukumbu 20:4

“Kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi”.

Isaya 12:2

“Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu”.

Mathayo 6:34

“Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.

Zaburi 27:1

“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani”?

Zaburi 31:24

“Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja Bwana”.

Zaburi 73:26

“Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele”.

Zaburi 29:11

“Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani”.

Zaburi 23:4

“Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.

Zaburi 118:14

“Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu”.

Habakuki 3:19

“YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka”.

Yohana 16:33

“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

2 Wathesalonike 3:3

“Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu”.

Luka 1:37

“Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu”.

Yeremia 29:11

“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho”.

Wafilipi 1:6

“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu”.

Zaburi 34:8

“Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini”.

Mathayo 11:28

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.


Jiunge na Forum ya Neno la Mungu

Mada zaidi zinazohusu Faraja:


Uko Tayari Kumfuata Yesu Leo?

Inawezekana hujaokoka, lakini leo hii unataka Yesu asikupite bila kuyaokoa maisha yako. Ikiwa umeamua kumgeukia Mungu kwa moyo wako wote, yeye mwenyewe anasema:

“Kila ajaye kwangu sitamtupa Nje kamwe”.

Leo hii Yesu ataingia ndani ya maisha yako kama umeamua kweli kumfuata. Fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa Sala ya Toba: KUONGOZWA SALA YA TOBA


Bwana akubariki.


Ikiwa unataka, naweza pia kuunda meta description na SEO keywords zinazofaa ili chapisho hiki kionekane vizuri kwenye Google, bila kubadilisha maneno.

Je, nifanye hivyo pia?

 

Mada Nyinginezo:

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Arabuni maana yake ni nini?

Tukiachilia mbali, Eneo linaloitwa Arabuni ambalo limetajwa sana katika biblia,  .

Kama tunavyosoma katika vifungu vifuatavyo..

2Nyakati 9:14 “mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na maliwali wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha”.

 

Isaya 21:13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.

 

Yeremia 25: 13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.

 

Wagalatia 1:17 “wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski”.

 

Wagalatia 4:25 “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto”.

Eneo ambalo walikuwa wanaishi jamii ya watu wa kiarabu.. Au kwa jina lingine linaitwa Arabia.Tazama picha juu.


Lakini Neno hili limetajwa kwa namna nyingine, katika biblia kama tunavyosoma katika vifungu vifuatavyo

2Wakorintho 1:22 “naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu”.

 

2Wakorintho 5:5 “Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho”.

 

Waefeso 1:3 “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.

14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake”.

Sasa Mungu alipotugawia ahadi zake za uzima wa milele na nyinginezo, hakutaka kutupa mikono mitupu tu hivi hivi bila uthibitisho wowote, Hivyo ili kututhibitishia kuwa ahadi zake ni kweli alitupa uhakika huo kwa kutugawia Roho Mtakatifu,  kama garantii au tunaweza kusema, kuponi, ya kuwa ahadi zake tutafikia, au atatutimizia.. Sasa hiyo garantii/kuponi  ndio inayoitwa arabuni.

Ukipokea Roho Mtakatifu basi unayo arabuni ya uzima wa milele, kama alivyowaahidia wale waliomwamini.

Ukipokea Roho Mtakatifu basi una uhakika kuwa wewe ni mbarikiwa wa Mungu, hakuna laana yoyote inayoweza kukaa juu yako.

Ukipokea Roho Mtakatifu basi maombi yako ni hakika kuwa yanasikiwa na kujibiwa mbinguni, sawasawa na ahadi za Yesu kwa wote waliomwamini.

Lakini ukiwa huna Roho Mtakatifu, na unasema umeokoka, bado mbinguni hutaenda..Kama vile maandiko yanavyosema..

Warumi 8:9 “…Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Hivyo kama na wewe unataka upate hii arabuni(garantii) ya urithi wa ahadi za Mungu zote za mwilini na rohoni,, basi ni sharti umpokee Roho Mtakatifu. Na mtu anampokea Roho Mtakatifu kwa kuzaliwa mara ya pili.

Mtu anazaliwaje mara ya pili?

Pale unapotubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, , na baada ya kutubu  ukawa tayari kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, sawasawa na Mdo 2:38, hapo utakuwa tayari umeshazaliwa mara ya pili.

Na moja kuwa moja, kuanzia huo wakati na kuendelea Roho anashuka ndani yako..Na unakuwa tayari umeshapokea garantii hiyo(arabuni) ya kuwa wewe ni mwana wa ahadi… Hivyo kama hutarudi nyuma utaendelea tu kuishi katika maisha matakatifu ya wokovu ya kumpendeza Mungu na kudumu katika ushirika wa Mungu..Ni uhakika kuwa hata ukifa usiku huo huo, wewe ni wa mbinguni tu mrithi wa ahadi zote za Mungu..

Hivyo kama hujaokoka, basi anza sasa kufuata hatua hizo kwa moyo wako wote..Kama unahitaji leo kumpa Yesu maisha yako basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na ikiwa utahitaji kubatizwa usisite kuwasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312: Ubatizo ni bure, na unafanyika pindi tu mtu anapotubu dhambi zake..Hakuna madarasa ya kupitia, wala hakuna kutoa fedha, kwasababu biblia haitufundishi kanuni hizo..

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Yuko azuiaye sasa hata atakapoondolewa! ni nani huyo?

USIFIKIRI FIKIRI.

KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya “Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake?”

SWALI: Biblia inamaanisha nini inaposema “Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”


JIBU: Huu ni msemo ambao umeonekana ukipachikwa katikati ya vifungu kadha wa kadha kwenye biblia..

Kwa mfano utaona.. pale kwenye Kutoka 23:18-19 inasema..

18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Ukisoma tena..Kutoka 34:25-26, utaona inasema hivi..

“25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi.

26 Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya Bwana Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake”.

Ukirudi tena kwenye Kumbukumbu 14:21 nayo pia utaona ikisema.

“Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye”.

Sasa pale anaposema, usimtokose mwana-mbuzi, katika maziwa ya mama yake, anamaanisha kumchemsha mtoto wa mbuzi, kwa maziwa ya mama yake, yaani badala ya kumchemsha kwenye maji, wewe unachukua yale maziwa anayoyanyonya kutoka kwa mama yake na kumchemshia nayo..

Kwa namna ya kawaida ni kitendo kisicho cha kiungwana chenye ukakasi kidogo, hata kwako wewe unayesikia eti?..Utajiuliza ni kwanini ufanye hivyo? Kwani hakuna maji ya kumchemshia, au kitu kingine mpaka utumie maziwa, tena yale yale ya mama yake? Ni sawa na nguruwe aliyezaa mtoto, halafu unampa mtoto wake mwenyewe amle kama chakula chake..sasa hiyo ndio picha iliyopo hapo.

Ni kitendo kinachoonyesha unyama si unyama, ukosefu wa nidhamu..?

Ni utaratibu na mfumo wa kipagani ambao ulikuwa unafanyika na watu wa mataifa wasiomjua Mungu, walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu za kishirikina, ni kama mila zinazoendelea siku hizi, hivyo Mungu aliwaonya wana wa Israeli wasifanye mambo kama hayo, kwasababu ni machukizo mbele zake, ni Utaratibu ambao hauna tofauti na ule wa kuwapitisha watoto kwenye moto, (soma 2Wafalme 21:6, 2Wafalme 16:3).

Hata sasa, wengi wetu tunafanya kafara kama hizo rohoni?.

Tunamtolea Mungu dhabihu zilizochanganyikana na mambo ambayo Mungu ameyakataza, tunafanya mambo kama watu wa mataifa. Tunamsifu Mungu na huku vinywa vyetu vimejaa matusi, na masengenyo, chuki na visasi, tunamtolea Mungu na huku biashara zetu ni haramu, tunahudhuria kanisani lakini tunaendelea kudumisha mila zetu za kishirikina, hali kadhalika tumeokoka lakini heshima kwa mzazi haipo, na heshima kwa Watoto wetu haipo (hiyo yote katika roho ni sawa na kumtokosa mwanambuzi katika maziwa yake) N.k.

Bwana atusaidie, tuzishike amri zake na tumpendeze yeye.

Bwana atuokoe na kutubariki..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

USITUMAINISHWE NA MANENO YA UONGO.

YESU KWETU NI RAFIKI

Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao.

ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

CHOCHOTE UMFANYIACHO KRISTO KINA THAMANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Imani ya mitume ipo katika maandiko?

Imani ya mitume (Apostle’s creed), inapatikana wapi kwenye biblia?


Imani ya mitume ambayo unaisikia mara kwa mara ikikiriwa katika baadhi ya madhehebu hususani Katoliki, Lutherani, na Anglikana, haipo mahali popote katika maandiko, na wala haikuwahi kukikiriwa na mitume wa Kristo sehemu yoyote.

Imani hii, ilikuja kuaandikwa miaka mingi mbeleni(zaidi ya miaka 300),baada ya mitume kuondoka, waliiandika wakizingatia kiini cha wazo kuu la mitume walichokuwa wanaamini  katika maandiko.

Na kimsingi imani hii ipo kimaandiko. Hivyo mtu kuikiri hakuna shida, kwasababu haimpotezi katika misingi ya imani ya biblia.

Inasema hivi.

Namwamini Mungu Baba mwenyezi, muumba wa mbingu na nchi, na Yesu Kristo, mwana wake wa pekee, Bwana wetu.

Aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Akazaliwa na bikira Mariamu. Akateswa zamani za Pontio Pilato. Akasulubiwa. Akafa. Akazikwa.

Akashuka mahali pa wafu. Siku ya tatu akafufuka. Akapaa mbinguni. Ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba mwenyezi. Kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.

Namwamini Roho Mtakatifu, kanisa takatifu lililo moja, ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, ufufuo wa wafu na uzima wa milele.

Amina.

Jambo la kuzingatia ni kuwa, ukiikiri/usipoikiri sio tiketi ya wewe ni mkristo, au utakwenda mbinguni, huu ni utaratibu tu au mapokeo tu ya baadhi ya wakristo. kitachokufa wewe uwe mkristo, ni kuamini, kutubu na kuoshwa dhambi zako kwa damu ya YESU Kristo, kwa njia ya ubatizo( sawasawa na Matendo 2:38).

Na ubatizo sahihi wa kimaandiko ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi,(Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo.

Hivyo kama utahitaji upate ubatizo huu sahihi.  Na Kama utapenda tuwe tunakutumia masomo  ya biblia  kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

 Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?

Je mtu akifa anakuwa hana dhambi tena?

KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?

Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?


JIBU: Biblia imetupa majibu kama ifuatavyo..

Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA.  

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.

Huo ni mstari wa kwanza kabisa unaozungumzia uumbaji wa mwanadamu katika biblia, hakuna mstari mwingine kabla ya huu.. Na unasema Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. (maneno hayo mawili yapo katika umoja.). Na haijasema Mungu alimwumba Mwanaume na wanawake.. wala haijasema Mungu alimuumba mwanamke na wanaume. 

Kwahiyo hakukuwa na mwanaume Zaidi ya Adamu, na wala hakukuwa na mwanamke mwingine Zaidi ya Hawa katika uumbaji.

Jambo linalowachanganya wengi ambalo ndilo limezua swali hili, ni kuhusu mke wa Kaini, kwamba Kaini alitolea wapi mke?

Kwanza kabisa Ni muhimu kufahamu kuwa Adamu na Hawa, walizaa Watoto wengine wengi wakike na wa kiume baada ya Habili na Kaini. Watoto wa Adamu hawakuwa wawili tu, bali wengi.

Mwanzo 5:4 “Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.

Kwahiyo miongoni mwa hao Watoto wa kike aliowazaa Adamu, mmojawao ndio alikuwa mke wa Kaini, na Kaini na mkewe walizaa Watoto, na watoto wao walizaa Watoto, na wajukuu zao pia walizaa..Na wakati huo watu walikuwa na uwezo wa kuishi mamia ya miaka.

Kwahiyo ni uongo kusema kuwa Adamu alikuwa na mke mwingine tofauti na Hawa.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

 

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

SALA YA BABA YETU/SALA YA BWANA.

Sala ya Baba yetu/ Sala ya Bwana.


Sala hii inapatikana katika sehemu kuu mbili kwenye biblia..

  1. Ya kwanza ni Mathayo 6:9-13 Inasema.

“9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.

11 Utupe leo riziki yetu.

12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

 

       2.   Na ya pili ni  Luka 11:1-4

“1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.

2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]

3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.

4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu]”.

Sala hii inachukuliwa kirahisi rahisi na watu wengi, kama ni sala kutamka tu, sekunde nne,,tano umemaliza..

Lakini sivyo ambavyo Bwana Yesu alimaanisha pale.. Kumbuka wanafunzi wake walipomuuliza Bwana tufundishe jinsi ya kusali, walikuwa wanamaanisha kweli kufahamu kwa undani jinsi ya kusali, Walikuwa wanataka kujua siri ya Bwana Yesu kujibiwa maombi yake na Mungu ni nini?, walikuwa wanatamani kujua siri za kufanya maombi yao yawe na nguvu mbele za Mungu..  Walikuwa wanahitaji muongozo sahihi.

Hivyo usifiri waliambiwa watamke maneno yale tu machache ni tayari wameshasali, na sala zako zimeshasikiwa, hapana kama na wewe ulikuwa na mtazamo huo kama mimi..Basi leo ujue jinsi ya kusali mbele za Mungu kama Bwana Yesu alivyotuelekeza/

Ni kwa namna gani tusali sala ya Baba yetu/sala ya Bwana ipasavyo?

Kwa ufupi ni kuwa, maneno yale yalikuwa kama mwongozo tu, kama Ilani, kama ramani ya mtu anaposalia apite wapi na wapi,..Ili maombi ya Mtu yawe yana hoja za nguvu na mashiko, yafuate vigezo vipi na vipi.

Unapoomba sio tu, kuzungumza maneno ilimradi maneno tu, muda uende, fahamu, kanuni za uombaji, na kanuni zenyewe ndio hizo Bwana Yesu alizozihorodhesha hapo. Kipengele kimoja hadi kingine ni eneo la kuomba, kwa mfano anapoanza kwa kusema, Baba yetu uliye mbinguni..Hicho ni kipengele kimojawapo kama utangulizi wa maombi yako yafikije kwa Baba..

Sasa kwasababu somo hili tulishaliandika kwa urefu..Fungua hapa, ili uanze sasa kupitia kipengele kimoja hadi kingine, na mwisho wa somo hilo utakuwa tayari sasa umefudhu kuwa mwombaji mwenye nguvu katika ulimwengu war oho sawasawa na maagizo ya Yesu.

Fungua sasa hapa usome..>>>>>> ZIFAHAMU HOJA SABA ZENYE NGUVU MBELE ZA MUNGU.

Bwana akubariki.

Masomo Mengineyo:

RABI, UNAKAA WAPI?

FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU

https://wingulamashahidi.org/2019/05/13/zifahamu-huduma-kuu-10-za-shetani-duniani/

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post